Simulizi : Baba Wa Kambo
Sehemu Ya Tano (5)
Naam..baada Chongela kuona nyoka wengi wakimfuata kwa kasi,,aliushika vema upanga wake. kisha akasubili nyoka yoyote atakae katiza mbele yake....Kweli punde si punde..nyoka wale walimfikia Chongela..hivyo nae kwa kujiamini aliwakata vichwa mfano wa mtu anavyokata vichwa vya dagaa..Ingawa ilifikia muda Chongela alishiwa nguvu,,wakati huo mbele yake kwa mbali alionekana nyoka mkubwa kuriko wote...nyoka huyo alijiburuza pole pole kumfuata Chongela...hali yakuwa Chongela nae akiwa chini hawezi hata kujinyanyua ili kuyaokoa maisha yake dhidi ya yule nyoka mkubwa wa kutisha alieonekana kujiburuza kumfuata.
Kwa hakika Chongela akiwa pale chini,aliinua uso wake kumtazama yule nyoka...ghafla alijikuta akinyong'onyea zaidi kwani alitamani kumwangamiza ila uwezo huo hakuwa nao kwa sababu alikuwa amechoka sana ...Na hivyo kijana Chongela akawa amekubali matokeo,,ingawa roho ilikuwa ikimuua sana,kwa sababu lengo la kiungia katika msitu ule wa kutisha ni kumtafuta Zimwi ambae alitoweka na mama yake,,pia kumuuwa kabisa kwani alitabiliwa kukiangamiza kijiji cha geza..kijiji ambacho anaishi Chongela.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hivyo wakati Chongela akizidi kulia na moyo wake ..wakati akiwa bado kalala chini...mala ghafla nyuma yake alitokea yule mschana sono...na hivyo sono akiwa katika umbile nusu mtu nusu nyoka..alizipiga hatua kumfuata Chongela..na baada kumfikia,sono alikinga kiganja chake kisha akatema mate kwenye kiganja,,mate hayo ambayo yaligeuka kuwa kidude frani mfano wa almasi kwamaana kilionekana kung'aaa sana...Sono alichuchumaa chini kisha akamlisha Chongela kile kidude ambacho kilifanana na almasi..Hakika Chongela nae baada kukimeza,,alijikuta akiwa upya kabisa..nguvu na hali mpya..hata majeraha mbalimbali aliyokuwa nayo kwa mwili wake nayo yalipotea.
Na hapo ndipo Chongela alipo uchukuwa upanga wake kisha akazipiga hatua kumfuata yule nyoka mkubwa aliekuwa akimnyemelea,,lakini baada Chongela kumfikia yule..ghafla alishtuka baada kumkuta yule nyoka amekafa,na alipotazama pembeni ya yule nyoka..aliziona nyayo za Zimwi...
"Naam kumbe hauko mbali...sasa huu ni wakati wa kukusaka popote pale ulipo" Alisema kijana Chongela huku akiitazama milima ambayo nayo ilionekana kutoa mfuke mkali kwa sababu ya baridi kali iliyokuwemo ndani ya ule msitu.
"Usijali utampata tu...na nakuahidi tutakuwa pamoja katika kulifanya hili jambo" Ghafla ilisikika sauti ya Sono..akiongea hivyo huku mkono wake ukionekana kumshika shika bega Chongela...hivyo Chongela nae baada kuisikia sauti hiyo ya Sono,,alishtuka kwani alijuwa kuwa Sono alisha muuwa miongoni mwa wale nyoka aliowafyka vichwa..Kwahiyo baada Chongela kuisikia kwa mala nyingine tena sauti ile alishtuka kiukweli.
Lakin wakati Chongela alipokuwa yupo katika mishangao kuhusu Sono..punde si punde ilitokea tetemeko kubwa..tetemeko ambalo lilizamisha baadhi ya miti katika ule msitu...wakati hao huo lilitokea shimo kubwa mbele yao Chongela na sono,ambapo katika shimo lile zilisikika ngoma za asiri na nyimbo bila kusahau vigelegele..Chongela alizidi kustaajabu maladufu,woga ulimjia lakini sono alimtoa wasiwasi kwa kumwambia "usiogope hiyo ni moja ya mizimu katika msitu huu..kinacho takiwa wewe ni....." Kabla sono hajamaliza sentensi yake,ghafla ndani ya lile shimo alitokea mtu mmoja ambae alionekana kutisha...Mtu yule alizipiga hatua kuelekea kule walipo Chongela na sono..na mala baada kuwafikia,yule mtu wakutisha aliwazunguka mala tatu kisha akamshika mkono Chongela na kumvuta pembeni ya sono.
"Unaitwa nani.." yule mtu alimuuliza Chongela...lakini Chongela hakujibu...ambapo yule mtu alirudia tena kumuuliza Chongela jina lake..ila mambo yakawa yale yale.
kwa hasira kali yule mtu alitaka kumpiga kofi Chongela.lakini ghafla mkono wake ulidakwa na Mschana sono ambae nae alionekana kubadilika sana licha ya kuwa nusu nyoka nusu binadam,ila kwa wakati ule sono alizidi kuwa nyoka ili aweze kukabiliana na yule mtu endapo kama ataanzisha vurugu..
Hivyo yule alipo dakwa mkono wake..hatimae hasira zilimzidi ambapo kwa kutumia mkono wake wa kushoto alimsukuma sono..nae sono akarushwa umbali mrefu kidogo..lakini cha kushangaza sono kabla hajatua chini..alipaa juu zaidi kisha akatua pale pale alipokuwa amesimama mwanzo..na cheko kubwa lilisikika sono akicheka...na mala baada kumalizika kucheka,,sono kwa kutumia kiganja chake kilichokuwa na magamba ya nyoka alijibu pigo..lakini ghafla yule mtu alijtoa mala tano yaani watu watano wanao fanana..hivyo kazi ikawa ngumu kwa sono kumtambua yupi mtu halili.
Sono aliwatazama wale watu watano kwa umakini..wakati huo Chongela akiwa pembeni akiangalia mchezo mzima jinsi unavyokwenda kwani Chongela kwa wakati ule hakuwa na miujiza yoyote .....na ndio maana ugomvi ule wa sono na yule mtu wa ajabu akuweza kuingilia zaidi yeye alimtamani Zimwi ili ale nae sahani moja mpaka kieleweke.
Sono baada kuona kuwa hamwoni mtu halali ni yupi...hatimae alichuchumaa chini kisha akageuka kuwa nyoka..ambapo kwa kutumia macho yake ya nyoka..aliweza kumtambua mtu halali na wale wingine wanne walikuwa ni vimvuli tu...hivyo sono baada kumtambua mtu halali..kwa kasi ya ajabu alimfuata na kisha kumrukia ambapo alijikunja kwenye mwili wa yule mtu,kisha akamvunja mbavu...lakini cha kushangaza yule mtu hakuvunjika zaidi nae alibadirika kuwa nyoka aina tofauti na jinsi alivyokuwa nyoka sono...na hapo ndipo ilipokuwa ugomvi wa nyoka kwa nyoka.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Na wakati hayo yakiendelea,,upande mwingine nako katika lile shimo lililotokana na tetemeko,walitoka watu wengine wa ajabu ajabu...watu wale baada kuuona ugomvi ule wa nyoka sono na mwenzao...haraka sana walizipiga hatua kuelekea kwenye ule ugomvi..na hapo ndipo Chongela alipojiandaa kikamilifu kukabiliana na wale watu ambao ni mizimu ya mle msitu...lakini kabla wale watu wa ajabu wajamfikia Chongela,,ghafla sauti ya kubwa mfano wa ngurumo ya radi,ilipasa angani jirani kabisa na maeneo walipokuwa wamesimama wao.. Hivyo Chongela baada kuisikia sauti ile alitazama ilikotokea...ambapo wakati muda huo huo anga lilianza kubadilika,,,giza totoro kilionekana..ile hali ya kupatwa kwa jua na mwezi ikawa imeonekana kwa mala nyingine baada ya miaka kadhaa kupita.
Na baada ile hali kutokea,,mbele yake Chongela kwenye kile kiza totoro...alitokea Ajuza akiwa sambamba kabisa na mkongojo wake pamoja na kibuyu kidogo mkononi..Ajuza yule baada kutokea aliinamisha kile kibuyu kwenye kiganja chake..ukatoka unga mweusi ambao aliupuliza moja kwa moja uliekea kule alipokuwa Chongela..na baada kumfikia Chongela,hatimae nae alijisikia kuwa na nguvu za ajabu.....lakini licha ya kujisikia kuwa na nguvu zile za ajabu hakuweza kuingilia Kati ugomvi ule wa nyoka kwa nyoka..zaidi alizipiga hatua kuelekea kule ilipo sikika sauti ya Zimwi .
Baada Chongela kusikia sauti ya Zimwi katika msitu ule wa kutisha...aliamuwa kuelekea kule ambako aliisikia sauti...huku akiacha sono akipigana na yule mtu ambae alionekana si wakawida.
Lakini wakati Chongela alivyozidi kuzipiga hatua kuelekea kule alikoskia sauti ya Zimwi,mala ghafla alisimama baada nafsi kumsuta kwa kitendo kile cha kumwacha sono katika mazingira magumu ya kushambuliwa na wale watu wa ajabu ambao ni moja ya mizimu katika ule msitu.
Hivyo baada nafsi kumsuta...Chongela alibadilisha maamuzi,akawa amerudi kule aliko mwacha sono akipambana na wale mizimu..Na baada kukalibia eneo lile la tukio,Chongela alisimama kwanza akijiuliza "Nitapambana vipi na wale watu,,hali ya kuwa wenzangu nyoka,na mimi sio nyoka??.." Alijiuliza Chongela,wakati huo roho ikimuuma kumwona sono akipambana peke yake....Nakabla hajaamua cha kufanya..mala ghafla ilisikika sauti ya Zimwi kwa mala ya pili..sauti hiyo iliambatana na tetemeko jepesi...Hivyo kitendo kile kilimfanya Chongela kutambaua kuwa shughuli anayokwenda kukutana nayo si ndogo..Na hapo hapo aliamua cha kufanya,ambapo aliondoka zake huku moyoni akijisemea"Sono natamani kukusaidia..lakini uwezo kama wako sina" Alijisemea hivyo Chongela kwa huzuni kabisa,,huku akizidi kuzama ndani ya msitu.
Hakika safari haikuwa nyepesi kwa Chongela,,kwani alitembea sana usiku na mchana kumsaka Zimwi...lakini yote kwa yote hakuweza kufanikiwa ndani ya siku hizo mbili..Hivyo kwa kuwa alikuwa amchoka baada kutembea umbali mrefu,hatimae kwa kutumia upanga wake mdogo,alikata fito kisha akajenga hema ndogo la kupumzikia..huku akitumia kuezekea majani marefu na mapana..
Baada hema kukamilika,,Chongela hakuishia hapo..moja kwa moja Alitafuta mti wa kuweza kumpatia moto...ambapo haikuchukuwa muda mreefu aliupata..alikata kipisi.Na hivyo shunghuli ya kupekecha kipisi cha mti ili utoe moto ilianza..punde si punde moto uliwaka...Baada moto kuwaka,Chongela aliongezea magogo makubwa..magogo ambayo yaliufanya moto kuwa mkali sana... Chongela alirudi ndani ya hema lake kulala,,huku akiuacha moto mkali ukiwaka nje.
Na ilipotimia saa sita usiku..ghafla katika moto ule aliokoka Chongela,alitokea mnyama wa ajabu...manyama huyo sura yake ilifanana na binadam..
Hivyo yule mnyama alitulia kando kidogo ya ule moto...wakati huo huo anga nalo kilionekana kubadilika..dalili ya mvua kunyesha ikaonekana,kweli punde si punde mvua kubwa ilinyesha..kitendo ambacho kilimfanya yule mnyama wa ajabu kukimbilia ndani ya hema alilolala Chongela...Lakini kwa kuwa Chongela alikuwa yupo kwenye usingizi mzito,,hivyo hakuweza kujuwa kama kaingiliwa ndani na mnyama wa ajabu..zaidi alilala fofofo huku yule mnyama nae akiishia kumtazama tu.
Na usubuhi ilipofika,mnyama yule aliondoka zake bila kumdhuru Chongela..ila wakati Chongela alipoamka alishtuka baada kuziona nyayo za yule mnyama wa ajabu..Hivyohharaka sana alianza kuzifatilia ili ajuwe yule mnyama wa aina gani.
Chongela akiwa na silaha zake..alizipiga hatua kuzifuatilia zile nyayo..lakini alipo fika mbali zaidi,ghafla alikutana na madoa ya damu kwenye majani..Chongela hakusita alizidi kuzipiga hatua kusonga mbele zaidi,hatimae alikuta mwili wa yule mnyama ukiwa umeliwa vibaya,huku pembeni kidogo ikionekana nyayo ya Zimwi.
Hivyo wakati Chongela alipokuwa akizitazama zile nyayo za Zimwi..punde si punde angani walionekana ndege wakubwa wakiunyemelea mzoga wa yule mnyama wa ajabu..ambapo Chongela alipo waona aliondoka zake ili wale ndege wasimdhuru.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nam safari sio kifo,,kwani Chongela alizidi kuzama kabisa ndani ya msitu kwa nia ya kumtafuta Zimwi...Zimwi ambae alitokomea na mama yake mzazi.
Hivyo wakati Chongela alipokuwa akiendelea kutembea,mala ghafla kunako mti mkubwa uliokuwa na miba,ulitokea mjusi wenye rangi nyekundu ..cha ajabu mjusi ule ulipasa sauti ukimwita Chongela ambae nae alikuwa bize akiendelea na mawindo ya kumtafuta Zimwi...lakini alipo sikia sauti ikimwita,,haraka sana Chongela aligeuka upande ule ilikosikika sauti..wakati huo ule mjusi nao uliteoemka kwenye ule mti wenye miba kisha ukaelekea mahali alipokuwa Chongela..ila kabla haujamfikia,ghafla ule mjusi uligeuka ukawa kibuyu kidogo..kibuyu ambacho kilionekana kikifuka moshi mweusi mzito.
Sauti nene ilisikika ikisema" Chongela chukuwa hicho kibuyu,kisha kiinamishe kwenye kiganja chako..yatatokea mafuta..mafuta hayo hayo jipake mwili.." Ilisema hivyo ile sauti nene..wakati huo Chongela nae alikuwa makini sana akiisikiliza ile sauti..ambapo baada ile sauti kutoweka,Chongela alikisogelea kile kibuyu akafanya kama alivyo ambiwa kisha akaendelea na safari ya mawindo.
Kwa hakika Chongela alizidi kumsaka Zimwi huku akiwa na shauku ya kumtia machoni ili alipe kisasi...Na hatimae aliifika katika mbuga kubwa mbuga ambayo ilionekana kutawaliwa na wadudu wanyonyao damu..Na ng'ambo ya ile mbuga alionekana Zimwi huku akiwa amezungukwa na jopo la majoka...Hivyo Chongela alishusha pumzi baada kumwona kiumbe kile.wakati huo huo sauti ya ajuza ilisikika ikisema"Chongela kazi kwako huyo ndio Zimwi Alietoweka na mama yako" Ilipotea ile sauti baada kusema maneno yale,na hapo ndipo Chongela alipo jiandaa vizuri kwa ajili ya mapambano..lakini hofu ilimjia baada kufikilia kuwa namna gani atamfuata yule Zimwi..hali yakuwa alikuwa amezingilwa na majoka makubwa pamoja na wadudu wanyonyao damu.
Chongela alitaharuki baada kumwona Zimwi kwa mala yake ya kwanza,,hivyo alijiuliza "Je,nitaweza kupigana na huyu kiumbe wa ajabu...???" Alijiuliza hivyo Chongela huku akijiandaa kujitosa kwenye ile mbuga iliyojaa wadudu wanyonyao damu ili aweze kufika mahali alipokuwa Zimwi.
Hivyo punde si punde Chongela alijitosa,alizipiga hatua kumfuata Zimwi..kwa hakika Chongela alijikuta akishangaa asiamini kama kweli wale wadudu wangemwacha salama,lakini wakati Chongela alipokuwa akishangaa kitendo kile cha wale wadudu kuto kumnyonya damu,ghafla ule mjusi wenye rangi nyekundu ulitokea,mjusi ambao uliweza kumpatia Chongela kibuyu chenye mafuta,mafuta yaliyoweza kumlinda Chongela dhidi ya wale wadudu wabaya.
Naam baada mjusi ule kutokea,punde si punde uligeuka ukawa ajuza,,ambapo ajuza yule alimtazama Chongela ambae nae alikuwa akizidi kuzipiga hatua kumfuata Zimwi.
Hatimae Chongela alifanikiwa kuivuka ile mbuga,,Hakika hakuweza kuamini kama kweli kaivuka salama mbuga ile..ambapo aligeuza shingo yake kutazama alipotoka..Naam alishusha pumzi kisha akasema.."Hakika kama ninetoka mbali,nimeweza kuvuka vigingi vya kila namna...iweje nikuache we mnyama ulielaaniwa??.." Kwisha kusema hivyo,Chongela aliendelea na safari ya kumfuata yule Zimwi,ambae alikuwa mbali kidogo na mbuga ile..
Lakini kabla Chongela hajamfikia yule Zimwi,mala ghafla ilisikika sauti ya mtoto mchanga ikilia,sauti hiyo iliweza kumfanya ashtuke..hivyo haraka sana aliuadaa upanga wake kisha akazipiga hatua kuelekea kule ilipo skika sauti ya mtoto mchanga....Ila kabla Chongela hajafika lile eneo,punde sauti ile ilipotea kisha zikaibuka sauti nyingi mno zote za watoto wachanga wakilia.
Kwa hakika sauti zile ziliweza kumchanganya Chongela..hadi akajikuta anayaziba maskio yake...wakati huo huo mbele alijitokeza nyoka mkubwa..nyoka huyo alijiburuza kumfuata Chongela ambae nae alionekana kuwa bize kuziba maskio yake ili yasiathiliwe na sauti zile za ajabu.
Nyoka yule mkubwa kabisa,alizidi kumsogelea Chongela..na hapo ndipo Chongela alipo achana na jukum la kuziba maskio yake,hivyo haraka kwa kutumia mikono yake miwili..alikamata panga vizuri kisha akamsubili yule nyoka amfikie..
Kweli punde si punde,,yule nyoka alimfikia Chongela...ambapo aliweza kujirusha kutoka chini mpaka kwenye mwili wa Chongela...kwa hiyo kutokana na kasi aliyokuwa nayo yule nyoka..Chongela alishindwa kumpiga panga,,na hivyo nyoka yule akawa amefauru kumkunja mbavu Chongela.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sauti ya maumivu aliitoa Chongela..sauti ambayo iliweza kuskika msitu mzima...ambapo yule Zimwi baada kusikia ile sauti,hima aliifuata...hali ya kuwa Chongela nae huku alizidi kubanwa mbavu zake kiasi kwamba alishindwa hata kupumua,hivyo pole pole aliishiwa nguvu.
Na wakati Chongela alipokuwa katika wakati mgumu..mala ghafla alitokea Ajuza,ambapo ajuza yule baada kumwona Chongela hawezi kujitete kwa yule nyoka..haraka sana alichukua kibuyu chake kidogo kisha akakiinamisha kwenye kiganja chake,,ulitokea unga mweusi kutoka ndani ya kile kibuyu...unga ule aliupuliza juu,na punde likutokea wingu angani...wingu hilo halikuchukuwa muda likadondosha matonya ya mvua..Na wakati huo ikumbukwe kuwa Chongela akinyeshewa na mvua lazima abadilike na kuingia katika umbile la nyoka..kweli matonya yale yalipo mpata Chongela,,pole pole aliingia katika umbile la nyoka,,kitendo kilicho mfanya aweze kujikwamua kutoka kwenye imaya ya yule nyoka.
Lakini ile hali kabla haijamwendea kugeuka kuwa nyoka,,ghafla mvua ilikatika,,hivyo Chongela akawa nusu nyoka nusu binadam..ambapo aliuchukuwa upinde wake kisha akaufyatua kuelekea kwa yule nyoka..ambae nae baada upinde ule kumpata hapo hapo alianguka chini..wakati huo Chongela akizidi kumshambulia kwa kutumia upinde wake ambao ni moja ya siraha alizotembea nazo.
Baada nyoka yule kufa..Zimwi nae alifika mahali alipokuwa Chongela ambae tayali alikuwa katika umbile lake la ajabu..
Hivyo kicheko kikubwa kilisikika kutoka kwa yule Zimwi baada kumwona Chongela..wakati huo jopo la nyoka wadogo wadogo wakiwa nyuma yake.. lakini cha ajabu yule Zimwi aliwameza nyoka wale wote ili apate sumu Kali ambayo itaweza kumwangamiza Chongela.
Hivyo pambano lilianza..Na wakwanza kuanzisha pigano alikuwa ni Chongela .ambapo alirusha upinde wake..lakini mshale ule alio urusha ulifeli baada Zimwi kutokomeza kwa kutumia kiganja chake. ila Chongela hakuweza kutishika na kitendo kile,kwani alizidi kumsogelea zaidi Zimwi,,ambae nae Zimwi kutoka na umbile kubwa alilo kuwa nalo alishindwa kumwona Chongela,,hivyo aliamua kuwatoa nyoka wake ambao muda wote walikuwa kichwani mfano wa nywere.
Hivyo nyoka wale licha ya kumfuata Chongela kwa kasi..Ila waliteketezwa wote..Naam hapo Zimwi sasa akawa ameishiwa nguvu..kwani nyoka wake alio wategemea waliuliwa,,Hivyo akawa anategemea wale alio wameza ambao nao hakuwa na nguvu.
Kwa hakika nafasi ile,,Chongela aliitumiw kwa kumjeruhi Zimwi yule..lakini kabla hajamuua,ghafla alishtuka baada kumwona Zimwi akianguka mwenye,na nyuma alipokuwa amesimama Zimwi lilonekana pango dogo..ndani ya pango lile alionekana mwanamke ambae umri ulikua umekwenda ingawa sio sana.
Chongela alistaajabu baada kumwona yule mwanamke,,lakini kabla hajaelekea kumfuata,akitaka kujuwa kwanza kwanini Zimwi kauwawa bila yeye kumuuwa??hivyo aligeuka nyuma yake..Hakika hakuamini alipo mwona Sono..kumbe Sono ndie aliemuuwa Zimwi kwa kutumia nguvu yake ya giza..Chongela alitabasam baada kumwona Mschana sono kisha akazipiga hatua kuelekea kule alipomwona mwanamke mateka..Na mala baada kumfikia,ghafla ilitokea ajuza..Ajuza yule akitabasam alisema "Chongela huyo ndio mama yako...fanya haraka mchukue ili mtoke kwenye huu msitu..kumbuka msitu huu si wakawaida.."
Chongela baada kuisikia ile sauti,haraka haraka alimfungu minyororo mama yake aliyokuwa amefungwa...ingawa Chongela hakuwa na kumbukumbu ya kuweza kumtambua kama kweli yule ni mama yake.
Lakini yote kwa yote..safari ya kurudi kijijini geza ilianza..ambapo Chongela akiwa sambamba na Sono mschana mwenye jamii ya nyoka bila kumsahau mama Chongela wote kwa pamoja walirudi kijijini..
Na safari haikuchukuwa muda,hatimae wakawa wamekikalibia kijiji cha geza..wakati huo msituni kule walikotoka ulionekana moto mkali ukiteketeza ule msitu...Kwa Hakika furaha isiyokifani ilitawala kwenye moyo wa Chongela,asiamini kama kawza kuweza kukitetea kijiji chake pia kumuuwa yule Zimwi ambae aliweza kuyumbisha kijiji kwa kusababisha majanga mbali mbali.....
Lakin wakati hayo yote akiyawaza Chongela..punde si punde ajuza alitokea tena..Ajuza yule alifanya mambo yake ambayo yaliweza kumfanya Chongela kurudisha katika kumbukumbu zake..Hivyo Chongela akawa ametambua kuwa yule aliemwokoa kutoka kwenye himaya ya Zimwi ni mama yake mzazi..Na yule Zimwi alikuwa ni baba yake wa kambo ambae aligeuka kuwa Zimwi baada kulaaniwa na ajuza.
Kwisha kukumbuka hayo Chongela alifrahi zaidi kumwona mama yake..wakati huo jopo la wanakijiji waliandamana kwenda kumpokea shujaa Chongela.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
BAADA YA WIKI MBILI.
Shujaa Chongela alipewa uchifu bila kujali umri wake...yote heshima ya kile alichokifanya..huku yule chifu wa siku zote umri wake ulikuwa tayali umekwnda hivyo alisubili wa kumkabidhi madaraka nae hakuwa mwingine ni Chongela..akisaidiana na Sono ambae hakichuwa muda walioana wakawa mke na mume...huku neema tele ikizidi kuongezeka katika kijiji cha geza...
Vile vile ile hali ya Chongela kuwa katika umbile mbili tofauti ilipotea..ambapo hakuwa muda sono nae alirudi katika hali ya kuwa binadam wa kawida..Hivyo maisha yakazidi kuwa mazuri kwa chifu Chongela..SHUJAAAAAAAAAA.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment