Search This Blog

UCHAWI WA MAMA MKWE - 1

 







    IMEANDIKWA NA : GLOBAL PUBLISHERS





    *********************************************************************************







    SIMULIZI : UCHAWI WA MAMA MKWE 

    Sehemu ya Kwanza (1)



    HAIKUWA rahisi kwa mume wangu kuamini kuwa mama yake ni mchawi tena ana uchawi wa kutisha. Ni mwanamke ambaye alikuwa akiwanga usiku kila chumba katika nyumba yetu iliyokuwa Metropol jijini Arusha.Nilikuwa naogopa kumuambia mume wangu kuhusu uchawi wa mama mkwe na tabia yake ya kutusotea usiku tukiwa tumelala.

    Siku moja alikuja chumbani kwangu na kunishusha chini akidhani kuwa amenipumbaza kwa dawa zake alizomwaga lakini nilikuwa na akili timamu. Nilichukia sana baada ya kuona anataka kumfanyia kitu mbaya mume wangu ambaye ni mwanaye wa kumzaa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kunishusha juu ya kitanda na kunilaza kwenye zulia chumbani kwetu, mama mkwe alianza kumtambuka mume wangu akiwa kitandani, kisha kumvua bukta yake. Nilijisemea, “Nijifanye nimezinduka?”



    Kutokana na kumuangalia mama mkwe wangu alivyokuwa akimfanyia mume wangu, moyo wangu ulikuwa ukidunda kama vile nimetoka kufanya pushap hamsini dakika chache.

    Japoku kulikuwa na giza lakini mwanga wa ‘taa za ulinzi’, zilizokuwa zikiwaka nje, ziliniwezesha nione kila kitu alichokifanya mama mkwe dhidi ya mume wangu.




    Ni ajabu sana kuona mama mtu mzima akihangaika na mwanaye aliyemzaa na akawa anatembea naye huku nikimuona.



    Uvumilivu uliniishia nikajifanya nanyoosha miguu huku nikikohoa. Haraka sana kama vile paka anavyomkamata panya, bi mkubwa yule aliruka kitandani na kusimama huku akiniangalia, nikajifanya sijazinduka usingizini.

    Alitoka mbio na kwenda chumbani kwake huku akiniacha nikiwa bado chini kwenye zulia na mume wangu alikuwa yupo kitandani lakini alikuwa hajui lolote linaloendelea maana alikuwa hajitambui.

    Sikujua nini alimfanyia mpaka akawa kama aliyezimia. Niliinuka pale chini na kuketi kitandani.

    Ghafla mama mkwe akaingia tena chumbani humo huku akiwa na tunguri ndogo ambayo ilikuwa na shanga kibao kuzunguka mdomo wake na ilikuwa imepakwa mafuta.

    Baada ya kuniona nikiwa nimekaa kitandani alipigwa na butwaa akashindwa kurudi nyuma kwa sababu aliingia akiwa na spidi kali.

    “Mama kwa nini umeingia chumbani kwetu? Kuna nini?” Nilimuuliza.

    Mama alipata kigugumizi cha miguu maana alishindwa kurudi alipotoka au kuingia ndani kabisa akawa kama bonge la chumvi lililoganda.

    Akawa ananiangalia bila kusema chochote. Niliinuka na kuwasha taa, baada ya kuwasha taa ndipo alipoanza kutetemeka kama vile anaugua malaria kali.

    “Mama umefuata nini humu chumbani kwetu?”

    “Nime….nime…..”

    “Mbona mikononi una tunguri ni ya nini? Mama kumbe wewe ni mchawi? Unaturoga?”

    “Sikiliza wewe mama Nachope… sitaki kusikia unasema jambo hili kwa mtu yeyote, umenielewa?” alifoka mama mkwe.

    “Lakini mama kwa nini unatufanyia hivi, ina maana umeshindwa kwenda kwenye nyumba nyingine ukafanya upuuzi huu. Huyu ni mwanao, kwa nini umemvua bukta?” nilisema huku nikitetemeka kutokana na hasira.

    “Narudia tena, sitaki kabisa kusikia hili jambo kwa mtu yeyote, ikivuja tu nakuumiza, nakuambia kweli,” alisema mama mkwe huku akionekana kujawa na hasira.

    Wakati anasema hayo nilijitahidi kumuamsha mume wangu lakini alikuwa hajui kinachoendelea. Nilijitahidi kumtikisa lakini akawa haamki wala kusema lolote alibaki kukoroma.

    Niliamua kumvalisha bukta yake huku mama yake akiangalia. Nilipandwa na hasira nikatamani nimrukie mama mkwe wangu lakini niliona uhai wa mume wangu ni muhimu zaidi, hivyo nikawa najitahidi kumtingisha huku nikimuita jina.

    “Usijifanye kuwa na hasira nakuambia kitu kimoja. Sema hapa kwamba hutasema siri hii kwa watu la sivyo nitamuacha mumeo akiwa katika hali hiyo, tuone utaringia nini.”


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maneno hayo yalinifanya niamini kwamba mchawi huwa hana huruma. Kama mwanaye wa kumzaa anathubutu kusema atamuacha akiwa amezimia namna hii, je ningekuwa mimi si angeniacha nife kabisa?

    “Mama tafadhali, mrudishie akili yake mume wangu.” Nilimsihi lakini yeye akawa hajali na badala yake alikuwa akisema kwa kunong’ona maneno ambayo sikuwa nafahamu maana yake kwa sababu hayakuwa ya Kiswahili.

    Wakati akifanya hivyo ghafla giza lilitanda chumbani. Sikujua nani alizima taa, awali nilidhani Tanesco wamezima taa lakini niliamini ni mazingaombwe ya yule mama mkwe kwa sababu mwanga wa taa za nyumba ya jirani ulikuwa ukiingia katika nyumba yetu.

    Kufumba na kufumbua nikaona mbele yangu limesimama kundi la watu waliokuwa wamevaa nguo nyeusi yaani kaniki. Kila mmoja akiwa amepaka rangi nyeusi usoni na katika mikono yao walikuwa wameshika usinga.

    Niliishiwa nguvu na kujikuta nikiwa nimeketi kitandani kando yangu akiwa mume wangu ambaye alikuwa haelewi kinachoendelea.




    Mama mkwe baada ya kuwaona watu wale ambao sikujua waliingilia wapi kwa kuwa milango na madirisha ilikuwa imefungwa, walianza kuimba polepole huku wakicheza.

    Nilimwagiwa na mama mkwe unga fulani ulionifanya niishiwe nguvu na kujikuta nikimdondokea mume wangu ambaye alikuwa amelala fofofo.

    Japokuwa nguvu ziliisha lakini ubongo wangu ulikuwa ukijua kila kilichokuwa kinaendelea pale. Nilifumba mambo kwa hofu kwamba nikiwaangalia wanaweza kuniangamiza kabisa au kunipa dawa zaidi ambazo zitaniumiza.

    Nilitamani mume wangu naye apate fahamu ili ajionee mauzauza haya anayofanya mama yake na washirika wake kwa mambo ya ulozi.

    Mzee mmoja ambaye sikuwa namjua jina nilimsikia akimuuliza mama mkwe.

    "Tuambie, umetuitia nini?" Mama mkwe nilihisi alihama pale alipokuwa amesimama na sasa alikuwa karibu kabisa na pale tulipolala mimi na mume wangu kwa sababu nilihisi alikuwa akinipaka kitu mkononi. Akajibu.

    "Huyu ni mkwe wangu. Amenigundua leo kuwa mimi ni mchawi, nikaona ni vema niwaiteni wenzangu mnishauri nifanye nini?"

    Baada ya kusikia kilichowafanya wale wachawi waje pale, moyo wangu ulienda mbio nikajua kuwa siku ya mwisho wa maisha yangu imefika.

    "Unataka tukuchagulie sisi cha kumfanya mkweo?" Mchawi mwingine aliuliza, nadhani alikuwa wa kike kutokana na sauti yake kuwa nyororo utadhani ni mwimbaji wa taarab.

    "Hapana kwani kuomba ushauri kuna ubaya? Mimi nilijua kuwa mtapita hapa kunipitia nikaona ni vema niwaombe muingie humu ndani mnishauri."

    "Sasa mbona unampaka dawa, ni ya nini?" Alidakia mwingine.

    "Ahaa hii dawa ni ya kumfanya asizinduke sasa hivi mpaka tumalize mazungumzo yetu. Asijue mnashauri nini."

    "Kwani mkweo anaitwa nani?"

    "Jina lake ni Naomi Pirikisha, ni mkazi wa Ndanda ndiyo kwao," mama mkwe aliwajibu nikaona kama hivyo ndivyo basi wanataka kunimaliza.

    "Je unataka huyu Naomi Pirikisha tumfanye zezeta?"

    "Hapana. Kwa jinsi mwanangu anavyompenda, atapata shida sana kwani hatamuacha, atakuwa akimhudumia, sasa kwa kuwa huyu atakuwa hana akili, hatateseka, mwanangu ndiye atapata mateso."

    "Sasa ni juu yako kuamua utamfanya nini mkweo kwa sababu kila tunachokuambia unajiwa na huruma, sasa uamuzi ni wako."

    "Sawa niachieni nitajua la kifanya," alisema mama mkwe.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***

    Nilishitukia asubuhi naitwa jina na mume wangu.

    "Baby Naomi, mbona leo umechelewa kuamka?" amka basi," alisema mume wangu huku akinitikisa mguu.

    Moyo wangu ulienda mbio baada ya kutikiswa mguu nilidhani bado ni usiku na nilikuwa natikiswa na wale wachawi walioalikwa na mama mkwe.

    Nilipofumbua macho nilimuona mume wangu akiwa amesimama nyuma ya miguu yangu huku akiwa amefunga taulo kiunoni na mdomoni alikuwa na mswaki.

    Nahisi ndiyo maana sikuweza kumtambua sauti wakati ananiita nikiwa usingizini kwa sababu mswaki ulimfanya asitoe sauti niliyoizoea.

    Nilifikicha macho ili nimuone vizuri na kwa kuwa ndani ya chumba chetu cha kulala kuna saa niliiangalia na kuona kuwa ilikuwa saa 12.30 asubuhi na kweli muda huo mimi huwa nimeshaoga na kuanza kazi ndogondogo hapa nyumbani kwangu.

    Niliamka na kuketi kitandani lakini ghafla nikakumbuka sakata la wachawi wa usiku na nikaanza kutokwa na machozi.

    "Kwa nini unalia mke wangu?"

    "Ni ;" nilishindwa kujieleza kwa sababu nilifikiri sana na kujiambia kimoyomoyo kuwa nikisema mama mkwe alikuja chumbani usiku akafanya yale yasiyofaa kwa mume wangu na mimi pia sijui kama mwenzangu atanielewa.

    Nilitafakari sana juu ya hilo, hivyo nikashindwa pa kuanzia badala yake machozi yakawa yanatiririka bila kujua niseme nini kwa mume wangu. 




    Nilikuwa na maswali ya kujiuliza kwamba je nikimuambia mume wangu kuwa mama yake ni mchawi atakubaliana nami? Nikajiuliza pia kuwa nikimfahamisha kuwa usiku alimvua bukta nami kunilaza chini ya zulia na akamfanyia mambo mabaya atanielewa?



    Maswali hayo nilishindwa kujijibu nikabaki natokwa na machozi. "Naomi nieleze, umepatwa na nini?" Mume wangu alizidi kudadisi. "Naomba niache kwa muda, nitakuambia," nilimjibu lakini hakuona kuwa ni haki abaki na maswali mengi kichwani mwake bila kujua nini kinaniliza.



    Alinibembeleza nimueleze kinachoniliza lakini sikutaka kupasua jipu wakati ule hasa ikizingatiwa kuwa mama yake ambaye nimetokea kumchukia ghafla baada ya kumbamba akiwa chumbani kwetu. Nilimuambia mume wangu kuwa aende kazini na akirudi jioni nitampa kisa kizito.



    "Kisa kizito?Sitaweza kufanya kazi bila kuniambia. Kama kuna jambo limekukwaza tafadhali sana niambie wala usiwe na mashaka juu yangu kwa sababu lako ni langu na langu ni lako. Niambie umekwazwa na nini?"

    " Mume wangu tafadhali sana niamini, kinachonikwaza wala hakihusiani na wewe ni matatizo yangu tu ya maisha haya tuliyonayo." "Matatizo ya maisha ndiyo yakufanye uahirishe kuniambia linalokukwaza sasa mpaka jioni nitakaporudi kazini? Hapana, utakuwa hunitendei haki.



    " Baada ya kufikiria sana niliamua kumueleza mume wangu uongo ili tu kumfanya aende kazini. "Sikiliza mume wangu.

    Mimi huwa nasikia moyo ukinienda mbio sana nahisi nina tatizo la moyo na ndiyo maana nalia. Nawaza kama moyo wangu ni mkubwa si ndiyo mwisho wa maisha yangu na kukuachia watoto wadogo?" "Mke wangu kama hilo ndilo tatizo ulipaswa kuniambia mapema, kwani umeanza kupata tatizo hilo lini?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ni usiku. Nilijaribu kukuamsha lakini ukawa huamki, hapo ndipo nilipoanza kulia." "Nakuapia kwa jina la Mungu, sikujua kabisa kama uliniamsha. Kweli unaweza kuniamsha nikaacha kuamka tena usiku? Hakuna asiyejua kuwa usiku una mambo. Tafadhali sana mke wangu nisamehe sikufanya kusudi."

    "Nimekusamehe mume wangu." "Kama hivyo ndivyo, basi ngoja nipige simu ofisini kuomba ruhusa kisha nikupeleke hospitali." "Unaona? Ndiyo maana nilikuwa sitaki kukueleza, nilijua utakatisha safari yako ya kwenda ofisini. Nenda ofisini na mimi nitakwenda mwenyewe hospitali."



    "Itakuwa ni kichekesho. Mtu ambaye usiku hakulala kwa maumivu ya kitu nyeti, moyo, aende hospitali peke yake? Nitaonekana mpumbavu mbele ya jamii. Jiandae twende sote hospitali." Kabla ya kuondoka na kwenda kwenye tiba hospitalini niliingia bafuni kuoga.



    Wakati naingia nilimkuta mama mkwe akiwa amesimama kwenye mlango wa kuingilia bafuni. Alikuwa ananitazama wakati namkaribia pale aliposimama. Nilitegemea angenipisha ili nipite badala yake akawa bado amesimama mlangoni huku mikono yake ikiwa imeshika upande mmoja mmoja wa mlango.



    Nilisimama ili kuona kama atanipisha badala yake akanisogelea na kuanza kuninong'oneza. "Ukimuambia mumeo kilichotokea usiku nakuua, umesikia?" " Kwa nini uniue?" "Kwa sababu ile ni siri ya wachawi. Thubutu kumuambia uone kitakachokupata.



    Usione nipo hivi, nimechukia sana kuona unafahamu siri yetu rejareja, jaribu kumuambia mumeo uone. Umesikia?" Sikumjibu neno badala yake nilikuwa namuangalia kwa kumshangaa mama kwa kuendekeza uchawi.

    Akaendelea. "Nilikuwa nakusikiliza kwa makini sana ulipokuwa chumbani na mume wangu lakini nilifurahi kuona kuwa hukumuambia mumeo ambaye ni mwanangu yale mambo ya usiku. Endelea kuficha siri." 




    "UNAJUA mume wangu kichwa ambacho kimeniuma asubuhi kilikuwa cha ajabu sana. Nilikuwa nahisi kama kuna mtu ana nyundo ananigonga kichwani, nikajikuta nikilia," nilimdanganya.



    "Pole sana, unajua wakati mwingine uwe unajikaza kulialia namna ile kama mwenzako ana presha anaweza kuanguka, ukampoteza."

    "Pole sana, sikuwa na nia ya kukushitua ni maumivu tu ya mwili yalinifanya niwe vile."



    Kimya kilipita huku wote tukiwa kitandani na baada ya dakika kama kumi na tano hivi nilimsikia mume wangu akikoroma.

    Niliinuka kitandani hadi kwenye mlango na kuhakikisha kuwa umefungwa kwa ufunguo. Nilifanya hivyo ili kudhibiti wale waliokuja jana usiku bila taarifa.



    Mimi nilichelewa sana kupata usingizi kutokana na kuwaza hili na lile kuhusiana na tabia mbaya ya uchawi ya mama mkwe.

    Hata hivyo, usingizi hauna adabu, nilijishitukia nikiwa nimelala fofofo na baada ya hapo sikujua kilichoendelea hadi saa tisa usiku niliposhituka baada ya kuona mtu kanishika kichwani.



    Nilipofumbua macho nilimuona mama mkwe akiwa chumbani kwetu akiwa mbele yangu. Nilitamani kupiga yowe lakini nilishindwa. Ni kwamba mwili ulikuwa unataka kufanya hivyo lakini nikawa sina nguvu hata ile ya kujitikisa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipigwa na butwaa na kujiuliza maswali mengi bila majibu. Huyu mama kaingiaje? Mbona mlango nilikuwa nimefunga kwa funguo?'

    Yeye alikuwa akiniangalia huku akiwa ameweka kidole kimoja mdomoni ishara ya kuniambia kuwa nisiseme kitu nibaki nimetulia. Lakini haraka sana nilifumba mambo na akawa ananipigapiga kofi kwenye mashavu yangu ili kuthibitisha kama nimelala kweli usingizi au nilikuwa macho.



    Niliamua kujifanya nimelala usingizi ili nione alichotaka kufanya. Alipanda kitandani na akawa anatutambuka mmoja baada ya mwingine. Kati ya mimi na mume wangu, alitutenganisha kwa kuweka nafasi katikati yetu kwa kuwa kitanda chetu kilikuwa kipana sana cha sita kwa sita.



    Baadaye alipuliza tunguri yake na mara nje nikasikia upepo mkali ukivuma lakini ukaishia juu ya mabati ya nyumba yetu. Nilikosa amani kabisa. Nilifumba macho kwa nguvu sana kwa sababu mama mkwe alikuwa anashuka kitandani kupitia kichwani kwetu.



    Nilimsikia akiimba nyimbo ambazo sikujua maana yake kwa sababu hazikuwa nyimbo za Kiswahili nadhani zilikuwa ni za kijini au kichawi. Kwa kuwa chumbani kulikuwa na mwanga hafifu kutokana na ukweli kwamba nilikuwa nimezima hata ile taa ya mwanga mdogo, sikujua kuwa mama mkwe alikuja chumbani mwetu akiwa na kijimfuko.



    Nilikiona hicho kijimfuko baada ya yeye kuchuka chini na kukiinua na akawa anachakuachakua ndani. Alitoa kitu kirefu kama mkia wa taa, sikujua anataka kuufanyia nini na mwanga wa taa za nje ulinisaidia kuona kila alichokuwa akikifanya.

    Nilihisi kuwa inawezekana ule siyo mkia wa taa bali ni kamba na hakuna ajabu kama ataamua kuitumia kuninyonga nayo.



    Nilikuwa na hofu hiyo kwa sababu aliahidi mchana mara mbili kuwa kama mambo yake ya uchawi nitamjulisha mume wangu ambaye ndiye mwanaye, ataniua na mwili wangu kuufanya nyama ambayo ataila!



    Mbaya zaidi ni kwamba sikuwa na uwezo wa kupiga yowe au kutumia nguvu ili asinifunge shingoni na kitu kile kama mkia wa taa. Hata hivyo, tofauti na mawazo yangu, aliinua ule mkia na kunitandika nao makalioni pwaa. Dakika hiyohiyo nikawa nakosa nguvu hata ya kufumbua macho.

    Niliyalazimisha kuona nikafanikiwa japokuwa yalikuwa yamefunguka kidogo sana kutokana na kichapo cha mkia ule.



    Je, huo ndiyo mwisho wa mama Ajigale? Fuatilia simulizi hii ya kusisimua Kesho.....  




    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog