Sehemu ya
Pili (2)
Niliyalazimisha macho kuona na
nikafanikiwa japokuwa yalikuwa yamefunguka kidogo sana kutokana na kichapo cha
mkia ule. Niliamini kuwa ule mkia ulikuwa na nguvu ya kumdhoofisha
mtu.
Hata hivyo, mume wangu yeye hakumchapa hali iliyonipa wasiwasi zaidi na kujiuliza kwamba au kuna jambo la ziada juu ya bakora niliyochapwa?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alichukua unga fulani ambao sikujua ni wa nini na kumnyunyizia mume wangu sehemu zake nyeti kisha kuvua bukta yake ambayo alikuwa akiitumia kulalia.
Aliniinua mimi na kuniweka chini ya kapeti mlemle kwenye chumba chetu cha kulala.

Nilikuwa natamani kupiga yowe lakini mdomo
ulikuwa haufunguki na nilikuwa najaribu kujiinua pia nikawa nashindwa kufanya
hivyo.
Baada ya sekunde kama kumi hivi nilimuona mama mkwe akipuliza vitu, sikujua ni vitu gani lakini nilihisi alikuwa akifanya vile ili kutufanya mimi na mume wangu tuzidi kupoteza fahamu kwa sababu yeye alikuwa amefunika pua kwa kitambaa cheusi.
Hata hivyo, baada ya dakika mbili mama mkwe alikaa kitandani akawa anasema maneno ambayo sikuyaelewa maana yake kwa sababu hayakuwa ya Kiswahili wala lugha yao.
Nilishitukia chumba kinakuwa na mwanga kama vile amewasha taa ya umeme. Akili yangu ilikuwa sawasawa tatizo lilikuwa nguvu za kuzungumza nilikuwa sina.
Baada ya mwanga kuwepo mle chumbani nilishuhudia mlango ukifunguka na kundi la wachawi wakaingia chumbani, wote walikuwa wamevaa kaniki (nguo nyeusi).
Sikuweza kuwahesabu kutokana na woga. Lakini mara baada ya kuingia ndani ya chumba chetu walianza kucheza ngoma ya kichawi huku wakiimba polepole sana.
Walimbeba mume wangu na kumshusha kwenye kitanda, akavaa bukta yake wakatoka naye nje akiwa hajitambui.
Sikujua huko nje walikwenda kumfanya nini lakini walichukua muda mrefu kurudi. Wakati wachawi hao wanaondoka, mbele yao alikuwa ni mkwe wangu aliyekuwa na usinga (mkia wa mnyama nyumbu au twiga na kukaushwa).
Alikuwa akiupunga mkia huo huku wachawi wenzake wakipiga manyanga ( kifaa kilichotiwa kokoto au mbegu ambacho hutumika kama ala ya muziki kwa kuwa kinatoa sauti).
Kwa kuwa nilikuwa nimefumba macho na kuangalia kwa chati sana, nilijaribu kuyafungua lakini nikagundua kuwa mle ndani alikuwepo mchawi mmoja aliyeachwa amekaa kitandani.
Nilihisi kuwa yule alikaa kunilinda mimi ili kuhakikisha kuwa siamki na kukuta mume wangu hayupo kitandani kwetu.
Lakini mchawi yule siyo kwamba aliacha anakula raha tu, hapana kuna manuizo alikuwa akiyafanya huku akifukiza uvumba kwenye chombo alichokuja nacho.
Ajabu ni kuwa chombo kile alikiweka juu ya kitanda chetu, shuka zilikuwa haziungui lakini moshi ulikuwa ukifuka chumba kizima.
Nilielewa kuwa alikuwa anakifukiza kwa ajili ya mimi niliyekuwepo kwa sababu wakati anafanya hivyo alikuwa akilitaja jina langu mara kwa mara kwamba nisizinduke.
"Moshi eneo ndani ya chumba hiki na mfanye Mei au mama Ajigale asizinduke," alikuwa akisema hivyo na kukifunika chombo kile kwa kiganja kisha anapofunua moshi mwingi kutoka na kujaza chumba.
Alikuwa akiinama mara kwa mara na kunikagua kuona kama nilikuwa nina uwezo wa kufumbua macho au la, kila aliponiita nilifumba macho.
Kuna wakati alichukua mkono wake mmoja na mwingine akashika sura yangu kisha kufungua jicho langu moja, nami nilijilegeza.
"Duh jicho jeupeee kama aliyekufa," alisema polepole nami sikumuuliza alikuwa na maana gani.
Baadaye alichukua mafuta ambayo sijui ni ya nini na kunipaka kwenye paji la uso huku akisema maneno ambayo sikuyaelewa maana yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alijaribu kuinua mguu mmoja akauachia ukapiga juu ya zulia na akafanya hivyo kwa mguu wa pili. Nilijifanya sijui chochote kwani nilijua kama angegundua nilikuwa namuona angewaambia wenzake kisha ningeuawa na kuliwa chama yangu kama mama mkwe alivyonitishia zaidi ya mara mbili nikiwa na akili timamu.
Mchawi yule baadaye aliamua kujilaza kitandani kwetu huku akiendelea kuimba wimbo wake wa kichawichawi lakini akaacha kufukiza ule moshi.Baada ya dakika kama kumi hivi mimi nikiwa bado chini nimelala kwenye kapeti, mchawi yule nilimsikia akikoroma.Nilishangaa sana mchawi kuja kwenye chumba cha watu na kuanza kukoroma kama vile alikuwa kwake. Mawazo yangu yakaenda kwa mume wangu kwamba amepelekwa wapi?Nilijaribu kuinuka pale nilipokuwa nimelazwa, nikashindwa. Na yule mchawi aliyeachwa anilinde akawa anaendelea kukoroma juu ya kitanda chetu.]Dakika kumi baadaye nilisikia kishindo nje ya nyumba. Nilijua kuwa lile kundi la wachawi walioondoka na mama mkwe wangu lilikuwa linarudi.Moyo ulinienda mbio mithili ya mtu aliyemaliza kukimbia mbio fupi za mita mia moja. Niliona mlango wa chumba chetu ukifunguliwa.Niliminya macho kujifanya nimelala fofofo.Lakini niliyaachia kidogo ili kuona kama mume wangu amerudishwa au amekwenda kuliwa nyama na wachawi wale.Nilifarijika baada ya kuona kundi lile la watu hao wabaya wakiwa wamembeba kama walivyokuwa wameondoka naye.Walipomfikisha kitandani walishangaa kukuta mwenzao waliyemuacha akikoroma."Huyu mjinga kweli kweli. Tulimuacha amlinde mke wa baba Ajigale yeye akaamua kulala," alisema mama mkwe wangu."Muamshe. Muamshe kwa kumchapa na mkia wa taa," aliamuru mtu ambaye sikumjua kwa jina.Mchawi mwingine alichukua mkia wa taa na kumchapa yule mchawi aliyekuwa akikoroma kwenye kitanda chetu. Hakushituka na wote mle ndani wakashituka."Huyu inawezekana alikuwa akimfukizia moshi huyu mke wa baba Ajigale ili asizinduke na matokeo yake naye fukizo limemkolea." "Ni kweli kabisa. Lete ugoro," alisema yule kiongozi wa wachawi.Nilisikia kifuniko kikifunguliwa na baadaye alinusishwa yule mchawi aliyekuwa akikoroma."Chaa, chaa, chaa," alipiga chafya.Baadaye aliketi kitandani na kuulizwa kulikoni alilala kitandani wakati aliachiwa kazi ya kunilinda!"Huyu mama Ajigale alitaka kuzinduka. Nikaamua kuchukua dawa ya mafusho nikawa namfukizia moshi. Nilisahahu kujifunga kitambaa chenye dawa ya kuzuia mimi kuleweshwa, nikalewa.Ndivyo ilivyokuwa," alijitetea."Lakini huyu mama Ajigale hakujua lolote?""Hakujua, nilipoona anajitingisha tu, nikamuwahi na mafusho.""Umefanya kazi nzuri," alisifiwa.Baadaye walimtoa pale kitandani na kumlaza mume wangu. Baada ya hapo walininyanyua pale chini ya zulia jekundu chumbani kwetu na kunilaza kando ya mume wangu.Sikuthubutu kuonesha kuwa najitambua badala yake nilijitahidi kujilegeza kana kwamba nilipoteza fahamu kabisa."Isije ikawa ule moshi wa mafusho ulizidi. Tunaweza kumuacha akapata fahamu kesho saa tisa mchana, tutakuwa tumefanya kitu kibaya sana," mmoja wa wachawi alishauri.Yule mkubwa wao akasema ni vema na mimi ninusishwe ugoro na kazi hiyo akapewa mama mkwe wangu kwa kuwa analala nyumba hiyo hiyo tofauti ni vyumba tu.Walikubaliana. Kilifunguliwa kichupa chenye ugoro na kupewa mama mkwe."Sisi tunatoka. Utamnusisha mkweo baadaye na akianza kupiga chafya tu, toka atazinduka kivyake vyake," alisema yule mtu ambaye mimi namuita ni kiongozi wa wachawi."Sawa," akaitikia mama mkwe.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Giza nene lilitanda na baadaye mwanga ukaja kwa mbali na nikamuona mama mkwe akininusisha ule ugoro. Nilitamani nikatae lakini nguvu zilikuwa zimeniishia kabisa nikawa nashindwa kunyanyua mkono ili kupokea ule ugoro.Alininusisha nikaanza kupiga chafya, haraka sana mama mkwe akakimbia kuelekea chumbani kwake.Nilijaribu kuinua mkono, ukainuka, nikajaribu kuketi pale kitandani, nikafanikiwa. Niligeuza shingo kumuangalia mume wangu na hasa nilimuangalia kifuani kama bado alipumua au walimleta pale akiwa maiti.Niligundua kuwa bado anapumua kwa sababu kifua chake kilikuwa kikitanuka na kushuka alipokuwa anavuta hewa."Baba Ajigale, baba Ajigale," nilimuita lakini hakuitika.Niliwaza kwamba nimuendee mama mkwe nikamshurutishe aje amzindue?Nilipata akili haraka sana kwamba nikifanya hivyo mama mkwe atagundua kuwa nilikuwa naona kila kitu ambacho walikuwa wakikifanya na wachawi wenzake.Akili ikaniambia nizidi kumnusisha ugoro uliokuwa juu ya godoro japokuwa ulikuwa kiduchu' lakini nilijitahidi kuokoteza.Baada ya kazi hiyo nilimnusisha tena akapiga chafya na kufumbua macho. Nilimuita, "Baba Ajigale." Akawa ananitazama bila kusema chochote.Nilifungua mlango na kwenda jikoni kwenye friji, nilichukua soda na kurudi chumbani kwetu, wakati narudi mama mkwe naye akawa karibu kabisa na mlango wa chumba chetu.Alikunja vidole vya mkono wake na kuachia kimoja akawa ananipa ishara kuwa nifunge mdomo wangu.Nami sikumchelewesha nikamuambia kwa kunong'ona kuwa nimemnusisha ugoro nitamuambia kuwa umenipa wewe. Nikazama chumbani.Nilipoingia chumbani, nilimuinua na kumketisha mume wangu kisha nikaanza kumnywesha ile soda.Alikunywa kana kwamba alikuwa ametembea kwenye jua kali sana na alikuwa na kiu. Nilichukua shuka na kumfutafuta pua ambayo ilikuwa na chembechembe za ugoro. Alipiga chafya tena."Najisikia mchovu sana, kwani nilikuwa nafanya nini mpaka ukaamua kuninywesha soda?" aliuliza."Nimekuona unakosa nguvu, kila nikikuita huitiki , nikahisi kuwa inawezekana una sukari kidogo mwilini," nilimdanganya."Sawa, lakini mbona kuna harufu ya ugoro puani kwangu, kulikoni."Kabla sijajibu swali hilo moyo ulipiga paa kwa sababu niliona nikimtajia sababu na aliyeleta ugoro kuwa ni mama yake na wachawi wenzake itakuwa balaa.Nilifikiri sana, lakini sikupata jibu la haraka."Mbona hunijibu, imekuwaje kuna ugoro na kwa nini nimenusishwa?"Nilijua kuwa mama mkwe kutokana na tabia yake ya kubana' nyuma ya mlango wetu alikuwa anasikiliza mazungumzo yetu, hivyo nilipaza sauti ili asikie kule alipo:"Ugoro nilikwenda kumuomba mama mkwe ambaye alinipa nikunusishe, alisema mtu akikosa nguvu akinusa ugoro anapiga chafya, kitendo ambacho kinachangamsha mapafu na kuyafanya yafanye kazi sawasawa, hivyo mtu kupata nguvu,"nilisema huku nikionesha kutokuwa na wasiwasi na maelezo yangu."Hebu nenda kaniletee maziwa yangu kwenye friji, au umekunywa?""Hapana, bado yapo.""Hebu nenda kaniletee.""Sawa."Ile nafungua mlango tu, nikakutana na mama mkwe akiwa pembeni ya mlango. Akanong'ona, "Gonga."Alisema neno hilo huku akitoa tabasamu pana lililomuonesha mapengo yake ya meno ya mbele.Nilitamani nicheke na hasira zote zilinitoka kutokana na mama mkwe huyo kunipa mkono wake na kunitaka nigonge kufurahishwa na nilivyomdanganya mume wangu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Nilikwenda kwenye friji na kuchukua maziwa fresh yaliyokuwa yamekuwa baridi sana. Nilidhani ameondoka pale karibu na mlango wa chumbani kwetu.Ajabu ni kwamba bado alikuwa amesimama palepale huku akitabasamu utafikiri alikuwa ****.***Kulikuwa kumepambazuka na majogoo yalikuwa yanawika kuashiria kuwa jua lipo mbioni kuchomoza. Niliinuka na kwenda bafuni kujisaidia na nilipotoka huko nilikwenda moja kwa moja kwenye meza ya chakula kumuandalia kifungua kinywa mume wangu kabla hajaenda kazini.Naye alikwenda kuoga na akaingia chumbani kwetu. Mama mkwe hakuwa ameamka bila shaka kutokana na kazi nyingi za kichawi za usiku alizokuwa amezifanya.Mume wangu alifika mezani na kukuta chai ipo tayari pamoja na mayai ya kuchemsha mawili na kipande cha mkate mweusi ambao anapenda kula.Mume wangu baada ya kunywa chai alifika mezani hapo mtoto wetu Ajigale naye akapata kifungua kinywa baadaye alilalamika kuwa hali yake siyo nzuri."Umesema hali yako siyo nzuri, kwani unajisikiaje?""Ni kama vile usiku kucha nilikuwa nalima au kufanya mazoezi ya nguvu. Mwili wote unauma, sijui hii hali imenitokea kwa sababu gani?""Lakini"Lakini nini? Bila shaka homa ya malaria inakunyemelea mwanangu," alidakia mama mkwe huku akinitupia jicho nami nikagundua kuwa bila shaka alidhani nitatoa siri ya walichokifanya usiku na wachawi wenzake."Malaria? Dozi nimemaliza wiki moja tu iliyopita?""Baba Ajigale, malaria huwa inajirudia na ndiyo maana madaktari hushauri kuwa ukimaliza dozi, rudi baada ya wiki moja kucheki tena damu.""Mwili wote unauma, ni lazima itakuwa ni malaria," alisisitiza mume wangu.Baada ya kumaliza kupata kifungua kinywa akiwa na mtoto wetu, mume wangu aliomba apewe maji ambayo alisema atakunywa njiani."Nitakwenda kwanza shuleni kumuacha Ajigale kisha nitapitia ofisini ndipo niende hospitali kupima."Alichukua begi lake na kwenda kwenye banda la gari akifuatana na mtoto Ajigale, muda mchache baadaye nikasikia mungurumo wa gari, nikaenda dirishani na kumuona akitoka kwa mwendo wa pole baada ya kufunguliwa geti na mtumishi wetu wa kiume.Mama mkwe alipoona Ajigale na baba yake wameondoka alinijia nilipokuwa nimesimama huku akiwa ameshika mikono yake kiunoni, akaja karibu kabisa na uso wangu."Pale nilikukatiza kwa hasira. Ulitaka kumuambia mambo yangu ya kichawi ya usiku mumeo siyo?" alifoka mama mkwe huku akiwa na ndita usoni."Hapana mama, mimi nilitaka nimshauri kwenda kupima damu hospitali.""Muongo mkubwa wewe, nakuambia kwa mara nyingine, ukitoa siri yangu nakufanya supu siku hiyohiyo wala sikutishi na kama unaona natania jaribu.""Mama kwani ningetaka kumuambia mume wangu ningeshindwa? Sitaki tabia yako ya kunifokea kila siku kama mtoto mdogo," nami nilijitutumua kumpima kisha nilimeza mate na kukaa kimyaa baada ya kuona amepandisha hasira japokuwa sikuona kosa langu lakini nilijua kuwa alikuwa akijihami ili siri yake nisiitoe kwa mume wangu.Tuliachana, yeye akaenda chumbani kwake nami nikaenda jikoni kufanya shughuli zangu za mapishi nikisaidiwa na msichana wa kazi."Mama kwani vipi? Mbona naona siku hizi hamuelewani na bibi?" aliniuliza msichana wa kazi."Shiiiiiiiii," nilimuambia huku nikiwa nimeweka vidole vyangu viwili kwenye mdomo wangu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/* * *Ni saa kumi jioni alikuja jirani yangu, mama Kibela na kutokana na mvua badala ya kukaa kwenye kibaraza tuliamua kukaa sebuleni kuzungumza. "Mama Ajigale nimekuja kukuambia jambo," alisema."Jambo gani?""Ni siri na nakuambia kwa sababu nakupenda. Unajua hapa kwako kuna wachawi wanakuja kila siku usiku?"Baada ya swali hilo moyo ulinipiga paa' na mara moja mama mkwe akatoka chumbani kwake na kujifanya kama anatoka nje kwenye kibaraza.Nilijua kuwa naye moyo wake umempasuka kama ulivyopasuka wangu kwani alijua kuwa jambo lile nalijua mimi tu."Ehee, umejuaje kuwa kuna wachawi wanakuja hapa kwangu?""Sikiliza. Msiishi kitoto, hapa kwenu nimekuwa nikishuhudia wachawi wakija usiku na mara nyingine wanawachukua na kutokomea nanyi.""Kweli mama Kibela?""Niongope jambo zito kama hilo? Ninachokisema ni kweli na niamini.Huwa wanatoka mbali kwa sababu huwa wanakuja na nyungo, ina maana wanasafiri na wakifika mmoja wenu anachukuliwa na kuwekwa katika chombo kisha huruka naye na kutoweka."Wakati anasema hayo mama mkwe alikuwa nje, macho yetu yaligongana akawa amekunja uso kwa hasira. Ni wazi kwamba kutokana na kukunja uso alikuwa anasikia yale aliyokuwa akinisimulia jirani yangu.Alinieleza mengi sana na akasema yeye huwa anawaona wachawi kutokana na dawa alizopewa na babu yake.Sikutaka kumdadisi kutokana na mama mkwe kuniangalia sana tena kama nilivyosema hapo juu, kunitupia jicho kali.Nilijaribu kutumbukiza maneno mengine ili tuachane na topiki' hiyo lakini mwenzangu akawa anaendelea kusimulia."Mama Ajigale haya ninayokuambia siyo masihara maana naona kama unadharau. Wachawi wale wanapofika huwa naona wanatoka na mtu humu ndani usiku. Kama Siyo wewe basi ni mumeo au mama mkwe wako. Lakini anakuwa hajitambui kwa sababu anabebwa kama maiti inavyotolewa ndani au mgonjwa mahututi.""Habari hiyo naomba tuiache, inanitisha," nilisema huku nikimtupia mama mkwe jicho kiwogawoga."Sawa tuyaache. Lakini akifika mumeo muambie na kama atataka ushauri zaidi aje anione.""Sawa," niliitikia, mama mkwe akasonya."Hee, mbona mama mkwe wako kasonya?" aliuliza kwa sauti ya chini."Achana naye. Tangu asubuhi ana mambo anadai hatujamtimizia," nami niliamua kumdanganya yule jirani yangu."Mnafanya vibaya. Wazee kama hawa hamtakiwi kuwasononesha kwa kuwanyima wanachokitaka, mtimizieni, kwani alitaka nini?""Wazee huwajui? Alikuwa akitaka apelekwe kwao lakini mwanaye amemkatalia. Ni hilo tu," nilizidi kumdanyanga lakini yote hayo tulikuwa tukiyasema polepole.Kitendo cha kunong'onezana kilimshitua mama mkwe akaamua kuingia sebuleni na kukaa katika sofa lililokuwa kwenye kona.Sikupenda kabisa macho yetu kugongana licha ya kuniangalia kwa macho ya kutisha. Tulianza kuongelea saluni gani nzuri ili kubadili mazungumzo lakini kwa sauti ya chini."Unamuogopa mama mkwe, wewe sema tu kwa sauti. Unataka nikupeleke saluni gani?"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/"Mama nilitaka nimchukue mkweo anipeleke saluni ambayo amesuka nywele zake. Nimezipenda sana."Mama mkwe alimuangalia kwa jicho baya na hakujibu chochote."Mh, mwaya, naona mama mkwe wako hataki utoke," alisema jirani yangu huku akimuangalia mama aliyekuwa bize kusuka mkeka wake ambao ulikuwa chini ya sofa wakati akiwa nje."Tunaongea tu. Nikuletee chai au soda ama maziwa?" nilimuuliza mgeni wangu."Niletee maziwa." Niliondoka na kwenda kumchukulia shoga yangu maziwa ambayo yalikuwa kwenye themosi."Lakini tusikae humu shoga bora tukae hapo nje kwenye kibaraza. Tuongee huku tukipunga upepo," alisema yule shoga yangu, hivyo kikao tukakihamisha na kwenda kukaa nje.Kwa mara nyingine nilimtupia jicho mama mkwe, akawa anatikisa kichwa, nilijua kuwa alikuwa anadhani tuliamua kumkimbia baada ya yeye kukaa kwenye sofa pale sebuleni.Mazungumzo yetu pale nje yalikuwa ni kuhusu saluni na mavazi huku kila mmoja akimsifu fundi wake wa nguo.Mazungumzo hayo nadhani yalimfurahisha mama mkwe kwa sababu ile stori ya wachawi tuliiacha kabisa.Baada ya mazungumzo marefu shoga yangu huyo aliaga akasema anakwenda kwake kuandaa chakula cha jioni."Si unajua mimi sina msichana wa kazi?""Haya shoga. Nitakupigia simu kesho kukueleza saa ngapi nikupeleke kule saluni.""Usikose.Si unajua Jumamosi mimi nina harusi ya wifi yangu? Leo Ijumaa, kesho inatakiwa twende asubuhi ili jioni tujiandae kwa sherehe ya ndoa.""Sawa."Wakati namtoa kwenye geti mume wangu naye akawa anaingia na gari lake akiwa na mtoto wetu Ajigale."Shemeji vipi, mimi naingia na wewe unatoka, au unanikimbia?" Je, baada ya kuulizwa hivyo alijibuje? Fuatilia simulizi hii ya kusisimua leo usiku.... ITAENDELEA

0 comments:
Post a Comment