Simulizi : Baba Wa Kambo
Sehemu Ya Tatu (3)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Naam! Baada baba yake wakambo chongela kumaliza kula chakula,aliinuka kisha akaenda kulala pamoja na mkewe,ila ilipo karibia kutimia saa saa sita kamili usiku,mala ghafla ulivuma upepo mkali,na punde si punde ilisikika sauti ya yule ajuza ikimwita mama chongela..."mama chongela..mama chongelaaaaaa"
Iliskika kwa sauti ya kizee kabisa...wakati huo mama chongela akiwa katika njonzi ya kutisha iliyoweza kumtoa usingizini hivyo akawa amekutana na hiyo sauti ya ajuza alie mpatia mtoto.
Hivyo basi baada mama chongela kusikia ile sauti,aliinuka kutoka kitandani kisha akafunua pazia ya dirisha akatazama nje ghafla akamwona yule ajuza akizidi kupasa sauti kumwita....Kwahiyo baada mama chongela kugundua kua anaitwa,hima alitoka ndani akaenda kumsikiliza "Mama chongela mamaaaa..toka na mwanao ondoka nae mbali kabisaa"
Aliongea yule ajuza akimwambia mama chongela,wakati huo ikiwa ibaki dakika moja pekee kutimia saa sita usiku muda ambao baba yake wakambo chongela huwa anageuka kua zimwi kwa mala nyingine.
Kweli haraka sana mama chongela alizama ndani kisha akatoweka na mtoto mbali kidogo na kijiji,huku mume wake akiwa bado kalala kitandani hatambui chochote...Lakini punde si punde alikurupuka kutoka kitandani ghafla akaanza kuunguruma mithili ya simba aliebanwa na mtego,muda huo huo mkia ukaonekana nyuma yake huku kichwani nywere ni vitoto vya nyoka pia hata mdomo nao ulionekana kutisha,,hakika ni zaidi ya laaana.
Hivyo baada ngurumo kali ya yule zimwi kusikika kijijini,hima vijakazi wa chifu walijikusanya wakiongozwa na jopo la mbwa moja kwa moja mpaka nyumbani kwa akina chongela,bila kukawia wakawa wameizunguka nyumba huku wakiwa wamesha jiandaa kwa lolote,kilichobaki ni zimwi ajitokeze ili waweze kumshambulia...
Huku nako hali ya hewa ikionekana kubadilika,radi na ngurumo za mvua zikilindima kila mala angani...na hivyo ukawa mtihani kwa mama chongela ambae alikua amejificha mbali na kijiji..Hali ya kua chogela hatakiwi kunyeshewa na mvua.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
______
Hakika mapigo ya moyo yalimwenda mbio mama Chongela akiamini kua tayali kwa mala nyingine anamkosa mwanae...wakati huo wale vijakazi wa chifu walikua tayali wamesha izunguka nyumba ya akina Chongela hivyo walingoja amri kutoka kwa mkuu wa kikosi ili waanze kuishambulia,lakini kabla hawajafanya jambo lolote ghafla alitokea baba yake wa kambo chongela akiwa katika hali ya Zimwi...hivyo bila kupoteza wakati aliweza kuwateketeza wale vijakazi wa chifu pamoja na mbwa wao huku akitoa nguromo kali mfano wa simba aliyenaswa na mtego,kitendo ambacho kiliwafanya baadhi ya wanakijiji walioisilia ile sauti kubana milango ya nyumba zao kwa kuongeza komeo ya pili..
Hakika vurumai iliendelea,huku mvua nayo iliyoambatana na radi pia ngurumo ikiendelea kunyesha,ndivyo hivyo vijakazi wa chifu nao walizidi kuwawa vibaya na yule aliekua baba yake wa kambo chongela kabla ya kulaaniwa kugeuka zimwi.
Naam!Basi baada vurumai kuisha,ghafla kimya kilitawala tayali zimwi alikua ameshamaliza kazi yake..Wakati huo mvua kubwa zaidi ikiendelea kunyesha,kwa hakika mama chongela akiwa na mwanae Chongela polini alipokua amejificha ili kuokoa maisha yake pamoja na mwanae dhidi ya yule zimwi..Aliweza kujisogeza mpaka mahali palipokua na mti mkubwa wenye majani mengi mapana japo sio sana kisha akaketi huku akiwa ememkumbatia mwananae ili asizuruke na matonya ya mvua..lakini alishindikana kwa sababu majani ya ule mti yaliweza kudondosha matonya na baadhi yakawa yanamdondokea Chongela ila mama Chongela hakuonyesha wasiwasi wowote zaidi aliyafuta huku akiomba dua mvua iweze kukatika.
Kweli mwisho mvua ilkatika,na hapo tayali ilikua imeshatimia saa tisa usiku...Hivyo mama chongela aliamua kujilaza pale pale chini ya ule mti uliomstili akingoja asubuhi ifike ndipo arudi kijijini kwao...Lakini wakati mama Chongela alipokua katika usingizi mzito ulioambatana na ndoto za kutisha kuhusu mambo yajayo mbeleni kijijini kwao,mala ghafla alimtokea binadam ambae alikua na jicho moja huku mikono yake ikiwa na vidole vitatu pia ngozi yake ikiwa na mwonekano kama wa nyoka aina ya cobra.
Hivyo yule binadam wa ajabu alivuta hatua kuelekea mahali alipokua amelala mama Chongela pamoja na mwanae,kisha akapasa sauti "Mama chongela,mama chongela...nini umefanya kwa chongela??
Aliongea hivyo yule binadam wa ajabu,sauti ambayo ilipenya kunako maskio ya mama chongela..naam!Haraka sana alishtuka kutoka usingizi kisha akatazama huku na kule bila mafanikio ya kumwona mtu alie mwita,hivyo alipuuzia akijua kua huwenda ni ndoto aliyoota.Akarudia tena kulala.
Basi baada mama Chongea kurudia tena kulala,hivyo hivyo yule binadam wa ajabu alimtokea tena mama chongela,akamwambia maneno yale yale aliyo mwambia awali.....Na hapo ndipo mama chongela alipokosa amani kwani hata usingizi aliokua nao ulitoweka.
Hivyo aliinuka kisha akakaa kitako akiyatafakali yale maneno aliyo yasikia...huku macho yake yakimtazama Chongela aliekua bado kalala.
Basi akiwa bado hajapata jawabu la fikra zake,,hatimae sauti ya jogoo kutoka kijijini iliskika,hivyo mama chongela alimwamsha mwanae kisha mwendo wa kobe alijirudisha kijijini,ambapo aliweza kupigwa na butwaa baada kukuta maafa makubwa yakiwa yametokea kijijini kwao.....Kwa hakika ulikua msiba mkubwa mno kwa chifu kuwapoteza vijana wake wote,pia hata wale wanafamilia husika nao walilia na kuomboleza kwa kuwapoteza walezi au wazazi wao.
Naam!Basi hatimae siku zilikwenda ,wanakijiji wa geza nao wakijaribu kuyasahau yote yaliyopita...Wakati huo chongela akiendelea kukua....Lakini ilitokea siku moja ambayo kila mwanakijiji alipokua amesha yasahau yote ya nyuma,mala ghafla angani walionekana nzige wengi ambapo moja kwa moja walitua kwenye mazao ya wanakijiji cha nzega,kisha kuyateketeza kwa kuyala..Hivyo katika hou msim ukawa msim wa njaa kali haijawahi tokea.
Kiukweli Chifu wa kijiji alistaajabu akijiuliza sababu ni nini inayo sababisha matukio hayo...Hatimae alipata taarifa kwamba kijiji jirani kuna mganga wa kienyeji ambae anaweza kugundua sababu ya matatizo mbalimbali...Hima chifu alimtuma kijana mmoja shupavu mwenye mbio kama farasi ili akamwite huyo mtaalam.
Kweli ndani ya masaa kadhaa yule kijana alilejea kwa chifu akiwa na mganga wa kienyeji ambae alionekana akiwa vifaa vyake maalum.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Basi mganga yule wa jadi,alitoa heshima yake kwa chifu..Kwisha kufanya hivyo ndipo Chifu alipomwelezea juu ya mambo yanayotokea kila kukicha kijijini kwake.... Hivyo yule mganga wa jadi alitikisa manyanga yake huku akipandisha mizim yake,na punde si punde alipata jibu ambapo moja kwa moja alimpelekea chifu.
"Chifu...katika kijiji chako unaishi na mtoto ambae si wa kawaida... kwahiyo fanya msako huyu mtoto aondolewe kwenye kijiji chako"
Ni jibu ambalo mganga yule wa jadi alilitoa huku akitetemeka,kwani alijua tayali kalizio balaa...kweli kabla Chifu hajamuuliza jina la huyo mtoto ambae ndio chanzo cha matatizo,mala ghafla angani lilitanda wingu la kawaida kisha manyunyu ya mvua yalianza kudondoka...na punde si punde ilitokea radi ambayo liweza kumuunguza yule mganga mbele ya Chifu.
Kwa hakika Chifu alizidi kuchanganyikiwa asijue kipi cha kufanya,na kesho yake ilipo fika haraka sana alipiga mbiyu iliyoweza kuwakusanya wanakijiji wote katika kijijicha nzeg.Hapo ndipo aliwaeleza wanakijiji wake juu ya mambo yanayotokea kadri siku zinavyokwenda,pia alienda mbali zaidi kwa kutaka kila mwanamke aliekua na mtoto ambeleke mbele yake ili aweze kumchunguza akiamini kua watoto wa ajabu ajabu huwa wanakasoro inayojitokeza.
Hivyo wale wanawake wa kijiji cha geza,waliharakisha kuwapeleka watoto wao mbele ya Chifu,huku wakiwapanga kwa mstari..Lakini ilikua tofauti kwa mama Chongela ambae mwanae alionekana kua mchanganyiko wa ngozi,yani ngozi ya binadam na ya nyoka.
Basi mama Chongela alibana katikati ya umati wa watu,kwani alihofia kufanyiwa kitu kibaya na Chifu endapo kama atamgundua Chongela kuwa sio binadam wa kawaida...Lakini wakati mama Chongela alipokua amebana kwenye umati wa wanakijiji,ghafla ilisikika sauti ya mtoto Chongela,kitendo ambacho kilimfanya Chifu kustisha kuwakagua wale watoto waliokuwa mbele yake,haraka sana aligeukia kwenye ule umati wa watu kulikotokea sauti matoto.
Hakika Chifu aling'aka huku akihoji..."Je tunataniani au?
Alihoji Chifu huku akionekana kukaghazibika,wakati huo Chongela bado akiendelea kuongea...Hivyo lile swali la Chifu liliweza kuwafanya wanakijiji waliokuwepo kwenye ule mkutano kuanza kumgeukia Mama chongela ambae nae alionekana kumkumbatia mwanae kisha kutoweka nae pale mkutanoni.
"Mkamateni,mnashangaaa niniiiii"
Amri ilitoka kwa Chifu akiitoa kwa hasira,hivyo vijana waliokuwepo pale walimkimbilia Mama Chongela ambapo nae alikua ameshafika mbali kidogo.....Naam!Basi baada hilo tukio kutokea hatimae Chifu alivunja mkutano,kwani alijua kuwa mwenye mtoto ambae anasababisha matatizo ni mama Chongela.
Hakika mbio nyingi mama Chongela alizokimbia,na kila alipo tazama nyuma aliwaona vijana wa kijiji cha nzega wakimfuata hivyo ndivyo alivyo zidi kukaza mwendo,lakini mwishowe alichoka hatimae akawa ameshindwa kuendelea na Safari....Kwa hakika baada Mama Chongela kushindwa kuendelea na safari ya kumwokoa mwanae kutia mikononi mwa Chifu,aliketi chini ya mti mkubwa huku akihema kwa nguvu...Alimtazama mwanae mala mbili mbili..Asiamini kuwa kwa mala nyingine anampoteza mwanae..Naam!Chozi la uchungu lilimtoka Mama Chongela wakati huo wale vijana wakimkalibia zaidi.
Na punde si punde walimfikia ambapo hata wao walistaajabu baada kumwona Chongela jinsi alivyokua ameumbika...Hivyo haraka walimchukua kisha wakaondoka nae wakimwacha mama Chongela akipiga kelele pale chini ya mti,kwani alishindwa kuwafuata kwa sababu alikua amechoka,na kibaya zaidi upande wa jicho lake moja ambalo lilitobolewa na mume wake ambae ndio aliekua baba yake wakambo Chongela kabla ya kulaniwa kugeuka zimwi,lilikua likimuuma maumivu ambayo yalisambaa mpaka kwenye jicho lake pili hivyo akawa ameshindwa kuona chochote.
Hivyo basi Chongela alilia huku akimtaja mama yake,ambavyo ndivyo ilivyokua kwa mama Chongelea ambae nae alimlilia mwanae...Lakini wale vijana hawakujali zaidi walitaka kutimiza matakwa ya Chifu,istoshe walidiliki kumpiga makofi Chongela ili akae kimya kuondoa fujo.....Ila wale vijana kabla hawajamfkisha Chongela kijijini kwa Chifu..Mala ghafla anga lilirudia kubadika,hivyo giza polepole likaanza kutokea na hatimae jua na mwezi vikaingiliana kwenye njia,kitendo ambacho kilizua taharuki kwa wale vijana waliokua wamembeba Chongela kumpeleka kwa chifu...Na punde si punde sauti ya kutisha ilisikika kutoka milimani sauti ambayo ilifanana na sauti ya Simba,nayo haikua sauti ya kitu kingine bali ilikua sauti ya ZIMWI ambae hapo awali kabla ya laana alikua baba yake wakambo Chongela ...Hakika hapo ndipo woga ulipozidi mala dufu kwa wale vijana,hivyo wakawa wanatazamana hawajui nini hicho kilicho sikika milimani...Na walipokuwa bado wapo kwenye mishangao,mala ghafla alitokea yule ajuza ambaae ndio alie mlaani baba yake wa kambo Chongela,ajuza ambae alitokea akiwa na mkongojo wake mkononi huku akionekana kua na hasira.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
_
Ajuza alieonekana kuwa na hasira kali alipasa sauti akisema"Mnampeleka wapi huyo mtoto?..
Alihoji hivyo yule Ajuza kwa sauti kali ambayo iliweza kusababisha mwangwi milimani..Kitendo ambacho kiliwaogopesha wale vijakazi wachifu,hivyo bila kuchelewa walimshusha chini Chongela.Wakati huo ile hali ya kupatwa kwa jua na mwezi ikiwa bado inaendelea..na punde si punde nyota ziliandama angani kama inavyokua usiku.
Basi baada hali ile kutokea.....Kijijini kwa Chifu nako aliingia mgeni ambae aliitwa Mzee sule,nae huyo mzee alikua ni mmoja ya waganga wa kienyeji maarufu katika kijiji cha mhonza,kijiji ambacho kilikua kimetawaliwa na mizim jamii ya Ikwete mizim mikali yenye uwezo wa kila aina katika ulimwengu.
Hakika baada yule mzee kuingia kwenye kile kijiji cha geza,kijiji kilichokuwa kinakumbwa na kila aina ya majanga..Kiukweli baadhi ya wanakijiji walio mjuwa Mzee sule,walifrahi baada kumwona kijijini kwao kwani waliamini kuwa huwenda Mzee sule akalitatua tatizo la njaa pia kumpoteza yule Zimwi ambae hapo awali kabla ya laana alikua baba yake wakambo chongela.
Hivyo basi,katika giza nene Mzee sule aliitazama saaa yake ya mkononi aina ya Disco..saa ambayo alipewa na mmoja ya wazungu hapo zamani aliemtibia baada kugongwa na nyoka wakati walipokua wakitafuta mahali yalipo madini...Maana kwa kipindi kile mtu kumiliki saa ilikua ni nadra.
"Saa saba mchana??...Au saa yangu imepotea majira!!"
Alijisemea hivyo Mzee sule,huku akipiga hatua kuelekea kwa Chifu ili apate malazi yaani sehem ya kulala...Punde si punde alikalibia ambapo alilakiwa na sauti za mbwa aliokua amewafuga chifu,kitendo ambacho kilimtoa Chifu ndani baada kuskia mbwa wake wakibweka..haraka sana alichukua upinde akidhania kuwa tayali kavamiwa na Zimwi..
"Mwakyila...mwakyila"
Mzee sule alisema maneno hayo kuashilia kuwa amani ipo kabla Chifu hajaachia upinde wake,na hivyo Chifu baada kuyaskia maneno hayo hatimae alishusha chini upinde huku akimkalibisha Sule nyumbani kwake..Wakati huo huo mwanga wa jua uliokuwa hafifu mfano wa mwanga unaopenya kwenye kioo cheusi,ulionekana kuashilia kwamba jua tayali jua na mwezi vinaachana,lakini kasoro sehem mmoja tu ndio iliyoonekana kua na giza kubwa nayo sio sehem nyingine ni mahali walipokuwa wamesimama vijakazi wa chifu wasijue cha kufanya baada kutokewa na ajuza.
Maongezi kadha kati ya Chifu na Mzee sule yaliendelea huku wakinywa pombe ya kienyeji ndani ya nyumba,ila yalifikia tamati mala baada anga kupambazuka...wakati huo baadhi ya wanakijiji wakionekana kujazana nyumbani kwa Chifu wakimtaka Chifu azungumze na Mzee sule kuhusu majanga yanayo kikumba kijiji chao.
Lakini kabla chifu hajatoa tamko..Mzee sule aliwatangazia wale wanakijiji waliokuwepo pale "Nipo tayali kuwasaidia kwani hili tatizo dogo sana kwangu"
Naam!kwa sauti ya kishujaa mkono ukiwa juu,Mzee sule aliongea maneno hayo..na hapo ndipo kelele za Shangwe na vifijo vilipo lindima kwa furaha kutoka kwa wale wanakijiji kwani walikua wamechoshwa na matukio ya ajabu ajabu yaliyokuwa yakitokea kila kikicha.
Basi baada Mzee sule kuonyesha moyo wa ushirikiano kwa wanakijiji cha geza,mala ghafla kilitokea kimbunga kikubwa kilicho weza kuezua baadhi ya nyumba pale kijijini geza...Na kibaya zaidi kile kimbunga kilisunguka huku kikijisogeza nyumbani kwa Chifu...Hivyo wanakijiji wote waliokuwepo pale walikimbilia ndani ya nyumba ya Chifu kwa kuhofia kile kimbunga hatari kilichokuwa kikisogea nyumbani kwa Chifu.
Kwa sauti ya wasiwasi Mzee Sule alimuuliza Chifu "Chifu unaungo ndani?...Na kama upo basi tuma mtu aniletee sasa hivi kabla hiki kimbunga hakijafika mahali hapa maana hii hatari"
Aliuliza hivyo Mzee sule,wakati huo akifungua zipu ya mkoba mdogo aliokuwa nao muda wote begani.....Punde si punde alichomoa hirizi kubwa na mfupa mkavu wa mjusi..wakati huo tayali ameushikilia ungo aliohitaji..Hivyo moja kwa moja Mzee sule alipiga hatua kukifuata kile kimbunga..Alipo kifikia alitupia ile hirizi yake pamoja na mfupa mkavu wa mjusi kwenye kile kimbunga kisha akafunika na ungo.Lakini wakati Mzee sule alipokuwa bado kakifunika kile kimbunga kwa kutumia nyongo,mala alitokea yule Ajuza ambae hapo awali aliwatokea wale vijana waliotumwa na Chifu kumkamata mama Chongela. .Hivyo basi baada Mzee Sule kumwona yule ajuza,faster aliuachia ule ungo ili amthibiti yule ajuza waajabu ajabu wakati huo pale ulipokua ungo ghafla..
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ghafla ungo ulijifunua..akatokea Nyoka mkubwa aina ya chatu..Kitendo ambacho kiliwafanya wanakijiji wote waliokuwa majumbani kukimbilia kwa chifu kuangalia hilo tukio,hata wale waliokuwa mashambani nao waliahilisha kazi zao..hima waliungana na wenzao kushuhudia balaa lilokuwa likiendelea pale kwa Chifu kati ya Mzee sule pamoja na Ajuza.
Hivyo Nyoka yule ambae alionekana kajikunja,alijikunjua akajiburuza mpaka mahali alipokuwa amesimama Ajuza..Baada kumfikia,moja kwa moja alijiviringa kwenye kiuno cha yule ajuza kisha akazitoa nje ndimi zake huku akimtazama Mzee sule ambae nae alikuwa tayali kajiandaa kwa mapigano dhidi ya yule ajuza wa ajabu...
Wakati huo akiivua saa yake aina ya Disco ambayo alikuwa ameiva..punde tu akawa tayali kwa niaba ya kupigano..Lakini kabla halijafanyika jambo lolote,ghafla alionekana mama chongela akiwa na mwanae..Sauti kubwa ilipasa kutoka mdomoni kwa Chongela akimzuia yule ajuza asifanye jambo lolote ..Baada hiyo sauti kuskika ndipo wanakijiji cha geza waliokusanyika pale kwenye tukio,hatimae walitupia macho yao kule ambako iliko tokea sauti..walipigwa na butwaa wasiamini kama ni Mtoto chongela ambae alitoa sauti ya kumzuia yule Ajuza asipigane na Mzee sule,wakati Chifu nae akijiuliza kua ni kitu gani kilicho wakuta wale vijana aliowatuma wakamkamate Chongela ambae alikuwa ametimka na mama yake.
Wakati chifu alipokua akiendelea kujiuliza huku akikuna kidevu chake,Chongela alitimua mbio mpaka kwa yule ajuza ambapo moja kwa moja alikumbatia miguu yake huku akimtazama usoni,nae Ajuza baada kumwona Chongela anamtazama usoni kwa uso wa huzuni..Aliamini kabisa kua chongela hataki yeye afanye kitu kibaya juu ya yule Mzee sule ambae alijitoa muhanga kupigana nae.
Basi baada yule ajuza kuligundua hilo suala..hatimae alizituliza hasira zake..kisha akamwita Mama chongela ambae nae alikuwa kajitenga kando na wale wanakijiji,kwani alikuwa na haibu baada kugundulika kuwa anamtoto wa ajabu...Hivyo mama chongela alitii wito wa yule ajuza,akiwa na wasiwasi alichuchumaa chini ili kusikiliza alichotaka kusema ajuza.
"Mama chongela.."
"Abee bibi.."
"Unakumbuka nilicho sema kuhusu mwanao Chongela?.."
"Ndio bibi...ila....."
"Mmmh..sio ila..sihitaji maelezo yako..Kumbuka wakati ulipojificha polini kumkwepa Mumeo alie badilka kuwa Zimwi saa sita ya usiku,ilinyesha mvua..ukawa umekimbilia chini ya mti kujinginga na ile mvua ili mwanao asinyeshewe lakini mwishowe ule mti ulidondosha tonya la mvua ambalo lilimpata chongela..°°Alikohoa kwanza ajuza kisha akamaliza kwa kusema "Kilicho baki sasa mama Chongela ni kuwa makini na Meno makali ya nyoka aliyonayo mwanao Chongela...Kwa sababu lile tonya la Mvua lilimsababishia matatizoo"
Alimaliza kwa kusema hivyo Ajuza....Kwa hakika Mama chongela alilia sana baada kuyaskia hayo maneno ya Ajuza aliempatia mtoto ambae ni Chongela..Wakati huo wanakijiji wqkizidi kutaharuki baada kumwona mama Chongela akilia pasipo wao kujuwa chochote...
Basi Mama chongela hatimae aliinuka huku moyoni akiwa hana furaha,kisha akamchukuwa mwanae ambae nae muda wote alikuwa kang'ang'ania miguu ya ajuza..Hivyo Mama chongela kama mzazi,ilimlazim amlazimishe Chongela amwachie Ajuza ili aondoke zake....Lakini kabla Chongela hajamwachia yule bibi,ghafla Mzee sule alinyoosha mkono wake wa kushoto juu..punde si punde katika kiganja chake ulionekana upanga mkubwa kiasi,upanga ambao ulikuwa na nembo ya rupia huku ukimelemeta kiasi kwamba binadam wa kawaida huwezi kuutazama mala mbili.
Hivyo baada Mzee sule kulikamata vizuri lile panga...alipiga hatua kwenda kwa yule ajuza ili akammalize kwa kutumia panga lile la kichawi huku baadhi ya minong'ono ya kumsifia mzee sule ikisikika kutoka kwa wanakijiji waliokuwa wakishudia lile tukio...Ila kabla Mzee sule hajamfikia Ajuza..Tetemeko kubwa lilitokea kisha Mshindo mkali ulioambatana na sauti ya kutisha ilisikika kutoka nje kidogo ya kijiji cha geza...Ghafla alitokea yule zimwi ambae hapo awali kabla ya laana aliyopewa na Ajuza wa Ajabu...alikuwa ni Baba yake wa kambo Chongela..kiukweli wanakijiji walishtuka baada kumwona yule kiumbe,hata chifu nae alijikuta akikimbilia ndani kwa woga..wakati huo Mzee sule kwa kutaka kulinda heshima yake..alistisha uamuzi wa kwenda kumshambulia Ajuza,na hivyo akawa amehamia kwa Zimwi ili amwangamize na baada ya hapo amalizane na Ajuza ambae ni bibi kizee aliyekumbwa na mizim hapo zamani baada kukataa kuiridhi enzi za ubinti wake.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hofu kubwa ilitanda moyoni kwa Mzee sule..mala tu alipo mtazama yule Zimwi aliekuwa mbele yake..wakati huo wanakijiji wa geza walikuwa wamekusanyika kuangalia mchezo mzima.
Hivyo Mzee sule alinyoosha kwa mala nyingine mkono wake juu,punde si punde lilitokea panga lingine..hatimae akawa na mapanga mawili mkononi mwake...Huku upande wa Zimwi nako lilionekana kujianda haswa kwa mapigano,ambapo lilidindisha nywere zake ambazo zilikuwa ni nyoka wadogo..haraka sana likaanza kuwachomo kwa kasi kumfuata Mzee sule..hivyo kwa kua Mzee sule nae alikuwa si haba,hatimae aliweza kuwamudu kwa kuwakata vichwa wale nyoka ambao kimsingi walikuwa na sum kali isiyokuwa na tiba.
Kelele nyingi kutoka kwa wanakijiji ziliskika wakimshangilia mzee sule,huku baadhi yao wakithubutu kusema.."Huyu ndio mzee sule bwanaa...wengine wazugaji tu..."
Mwingine mwanakijiji akadakia,akianza na cheko "Kwanza mimi nilivyo mwona tu kaingia kijijini kwetu,nikajuwa kabisa matatizo yote yamekwisha..."
Mwingine akaongeza kwa kusema"Huyu babu we acha tu mwisho wa matatizo..tazama sasa jinsi anavyolitesa hilo limnyama lenye umbile kubwa kama..."..Huyo mwanakijiji wa tatu kabla hajamalizia sentensi yake,alikatishwa na sauti kubwa aliyopasa yule Zimwi baada Mzee sule kufanikiwa kupiga kwa kutumia upanga wake ambao nao ulikuwa wa kichawi...Hakika hapo ndipo mayowe na milunzi ilipo zidi kutawala kutoka kwa wale wanakijiji....Kumbe wakati Mzee sule alipokuwa akimpiga jinsi atavyo yule Zimwi...Ajuza alikuwa amemfyonza nguvu zimwi ili sule afanikiwe jambo lake,na ndio maana mwishowe yule ajuza alimpoteza zimwi kimazingara ambapo alimkwapua na mama Chongela..akawa ameondoka nae huku zikidondoka khanga chini..
Hivyo wanakijiji pamoja nae Mzee sule walishangaa baada kuona kile kitendo...wakati huo yule ajuza ngozi yake ikibadilika kutoka hali ya ubinadam,na kuingia katika umbile la nyoka.
Mzee sule alishusha pumzi,akitafalali kama atamuweza yule ajuza au la!...Lakini mwishowe alipiga moyo konde kwani hakutaka kuharibu wasifu wake ndani ya kile kijiji pia vijiji vingine ambavyo alikuwa akifahamika..Akiwa na mapanga yake mawili mkononi..mapanga ya kichawi,Mzee sule alipiga hatua kumfuata yule ajuza akiwa na lengo la kumfyaka kichwa..lakini kabla hajamfikia,ghafla angani lilitanda wingu ndogo ambalo ndani ya sekunde chache lilidondosha manyunyu...punde si punde katika lile wingu ilotokea radi ambayo ilimuunguza Mzee sule,akawa amekufa huku akiwa amesimama..Mwili wake ukionekana kuwa mweusi mfano wa nyama iliyoungua..
Kiukweli wanakijiji wale waliokuwa wakimshangilia Mzee sule,,walipigwa na butwa akiwemo na Chifu,wasiamini kama kweli sule kafariki..
Baada kufanya hayo,Ajuza alimgeukia chongela ambae alikuwa akimlilia mama yake aliekwapuliwa na zimwi...kisha akamgusa kichawani...Hatimae chongela alikaa kimyaa..Na hapo ndipo ajuza alipo potea..huku akiacha sauti ikisema.."Sishindwi kumfanyia ubaya kwa yule atakae jaribu kumdhuru chongela...Chifu,chifu,chifu..Mtunze huyo mtoto atakuwa Msaada siku za usoni"...Alimaliza kwa kusema hivyo ile sauti ya ajuza ambayo ilikuwa ikijirudia malambili mbili...wakati huo chongela akaziokota nguo za mama yake ambazo zilidondoka baada kukwapuliwana Zimwi ambae alitokomea nae.
Hivyo basi baada ya hilo tukio kupita...Hakika maisha ya tabu alikuwa akiishi Chongela bila ya kuwa na mama,kwani kwa jinsi alivyokuwa ameumbika alitengwa na wanakijiji...hivyo Chongela akawa anaishi kama chokolaa.
Lakini siku moja alijitokeza mama Mjane ambae alijitolea kumsaidia chongela pasipo kujali umbile lake...Mama huyo nae alijikuta akichukiwa na wanakijiji hivyo akawa ametimuliwa kijijini...Ingawa kutimuliwa kwake kwa yule mjane ambae aliamua kuondoka na chongela hukukuweza kusaidia kitu,zaidi majanga juu ya majanga yalizidi kuongezeka maludufu katika kile kijiji cha geza.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
---BAADA MIAKA KUMI NA TANO----
Hatimae yule mama mjane ambae alijitolea kuishi na Chongela,alifariki dunia baada kugongwa na nyoka mwenye sumu kali wakati alipokuwa porini kutafuta kuni...Wakati huo Chongela alikuwa ameshakuwa mkubwa kijana ambae anajitambua..Na hivyo kazi yake rasmi ilikuwa ni uwindaji.
Siku moja wakati chongela alipokuwa kwenye msitu mnene akiwinda wanyama kwa niaba ya kitoweo,ghafla alishtuka baada kuziona nyayo za mnyama ambae hakuwahi mwona hadharani..hivyo alijiuliza "mnyama gani huyu?? .." wakati huo alipokuwa akijiuliza,pole pole alipiga hatua kuzifatilia zile nyayo..Na alipo fika mbali zaidi aliiona cheni chini na kando ya ile cheni lilionekana fuvu la binadam..
Kiukweli chongela alizidi kustaajabu huku akiupeleka mkono wake kuishika ile cheni...na baada kuishika ghafla...
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment