Simulizi : Baba Wa Kambo
Sehemu Ya Pili (2)
Basi upande mwingine nako alionekana mama chongela kwa mbali akiwa katika msitu mnene tulivu,huku mkono wake wa kulia ukiwa umeziba jicho lake alilotobolewa.Hivyo mama chongela alizidi kuambaa ndani ya ule msitu na alipo fika mbali kabisa hatimae alikutana na wamasai wakiwa na mifugo yao,baada kuwaona wale wamasai aliwasalim kisha"mmeniona bibi yoyote akipita hapa?
Aliuza hivyo mama chongela,lakini wale masai waliishia kumshangaa anacho kiuliza mama chongela na mwisho waliachia cheko kubwa huku wakigongeana fimbo..ajabu punde si punde wakapotea na mifugo yao kitendo ambacho kilimwacha mdomo wazi mama chongela kumbe wale walikua si wamasai bali ni katika ya mizim ya miaka mingi ambayo ilikua ikiishi ndani ya ule msitu.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hivyo mama chongela aliamua kuendelea na safari yake huku kwa mbali ikishuka mvua kubwa na radi na radi ambazo ziliweza kupasua baadhi ya miti ndani ya ule msitu,lakini mama chongela hakujali licha ya kutokea hayo mambo.Zaidi alizidi kuambaa na njia akielekea kwa yule bibi kizee ambae alimpatia mtoto kwa njia dawa za kienyeji ingawa alimpamasharti kadhaa kua mtoto wake asinyeshewe na mvua.Kweli hatimae alikiona kibanda cha yule bibi kikifuka moshi,hakika alifrahi sana ndani ya nafsi yake akiamini kua huwenda akarudishiwa mwanae chongela ambae kageuka kichuguu baada kunyeshewa na mvua kubwa iliyokuta njiani akitoka kijiji jirani baada kutumwa dawa na baba yake wakambo.
Basi mama chongela kwa unyenyekevu wa hali ya juu alisogelea kile kibanda cha yule ajuza,kweli alimkuta akiota moto ndani,hivyo alimsalim lakini yule ajuza hakuitikia zaidi alianza kufuko huku akitoa miguu yake juu ya mafiga kumfuata mama chongela mahali alipokua amesimama.
"Nilikwambia nini kuhusu chongela??
Aliongea hivyo kwa hasira yule ajuza akimwambia mama chongela huku meno mawili ya mbele yakiwa yamebadilika kua kama ya nyoka.
Kiukweli ile hali ilimfanya mama chongela kuogopa lakini alijikaza kisabuni kwa sababu alikua bado anania ya kumrudisha mwanae katika uhai wake baada kugeuka kichuguu.
Hivyo basi wakati yule ajuza alipokua akiendela kumuuliza maswali kadha wa kadha mama chongela,huku nako upande wa pili hali ilikua mbaya kwa aliyekua baba wakambo chongela maana kadli radi na ngurumo zilivyokua zikirindima angani,nae alikua akipata maumivu makali mwilini mwake.
Basi mama chongela alizidi kumwomba yule ajuza amrudishie mwanae,kiukweli yule ajuza nae mwishowe alikubali na akafanya hivyo kwq kumkabidhi mama chongela jungu kuu ambalo ndani yake lilikua na nyoka huku juu likiwa limefunikwa kwa kitambaa cheusi.
"uneweza kuondoka ila usirudie kosa,na endapo ukirudia kosa basi kitakacho kukuta usilaumu pia hakikisha hicho chungu kisidondoke chini,we nenda nacho moja kwa moja mpaka kwenye kile kichuguu kisha kwa kutumia ule udongo kifunike hiki chungu"
Kwisha kunena hayo,ghafla ulitokea umeme wa radi ukawa umempoteza yule ajuza,wakati huo mama chongela nae akijipanga kurudi kijijini kwake hali yakua mvua kubwa ya mawe ikiwa bado inaendelea kunyeshe....Lakini cha ajabu mama chongela hakujali hilo,kwa kutumia khanga yake licha ya kua kukuu alikifunika kile chungu kisha akaendelea na safari.
Hakika mama chongela wakati alipokua njiani,alikutana na vikwazo vingi lakini hakuthubutu kudondosha chungu kile alichopewa na yule ajuza wa ajabu...Zaidi aliendela kuambaa ambaa na njia katikati msitu uliojaa kila aina ya mauzauza,mpaka mwishowe akafanikiwa kuingia kijijini kwao wakati huo giza lilikua limesha Ingia.
Hivyo basi mama chongela baada kufika nyumbani kwake,kitu cha kwanza alichokifanya ni kukifukia kile chungu katika udongo wa kichuguu kwa kutumia jembe,ambapo kile kishindo cha jembe kiliweza kumshtua mume wake alikua ndani amelala,hivyo bila kuchelewa nae alitoka nje kuangalia ni kitu gani kinacho endelea pembezoni mwa nyumba yake wakati huo mama chongela akiwa ameshamaliza kila kitu.
Basi baada baba yake wa kambo chongela kumwona mkewe kwa mala nyingine,alifrahi sana huku akimwomba msamaha kwa yote aliyomfanyia...Lakini mama chongela yeye
hakuonyesha furaha kutoka moyoni mwake bali alionyesha furaha ya usoni tu...huku akijiuliza"leo hii nimeonekana mke mwema baada mwanangu chongela kupotea?.. kwa hiyo chongela ndio kikwanzo??..Ee mungu nisaidie"
Alijiuliza hivyo mama chongela na mwishowe alimaliza kwa dua,,pasipo kujua kua mume wake ameshapata laana kutoka kwa yule ajuza ambae anampatia mtoto.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Naam. ilipo timia saa tano na dakika hamsini na saba usiku,zikiwa zimebaki dakika tatu pekee ili itimie saa sita muda ambao baba yake wakambo chongela anatarajia kugeuka zimwi,ghafla ulivuma upepo mkali kijijjni kwo...upepo ambao uliweza kuezua baadhi ya paa za nyumba zilizokua zimejengwa kwa manyasi...na punde si punde mama chongela alibanwa na haja ndogo,ambapo aliamka mwenyewe kisha akaelekea chooni kujisaidia wakati huo huo saa sita kamili ndio ikawa imetimia.
Kwa hakika yule mume wa mama chongela alionekana kua tofauti sana,jitu kubwa lenye milaba minne huku kichwa chake kikionekana kujaaa vichwa nyoka pia mkia nao ukiwa unawaka moto muda wote.
Basi baba yake wakambo chongela akiwa katika hali ile,hatimae alitoka ndani wakati huo nae mama chongela akiwa ametoka chooni kujisaidia na hivyo akawa amemwona ingawa hakuweza kumtambua zaidi alijua kua huwenda moja ya wanyama waishio mstuni...Lakini alipo ingia ndani nakisha kukuta kitanda kitupu kiukweli alistaajabu huku machale yakimcheza wakati tayali mume wake ambae kageuka zimwi ameshaondoka pale nje.
Naam.Basi masaa yalidi kwenda huku mama chongela akiwa tongo macho kwa kukosa amani ya kusinzia licha kuulazimisha usingizi,lakini nafsi bado ilimsuta kitendo ambacho kilimfanya kuhisi kua huwenda kutatokea tatizo.
Ila mwishowe hadi anasinzia hakuna kibaya chochote kilichozuka,mpaka asubuhi alipo amka na kujikuta bado yupo peke yake ndani.
Na wakati mama chongela alipoku akifungua mlango,kwa mbali alisikia mbiyu ya kijiji ambayo ilikua inahusu uvamizi wa mifugo uliofanyika kijiji usiku .
Hivyo taarifa hiyo iliweza kumshtua mama chongela japo hakua na mfugo hata mmoja ,na hapo ndipo alipo amua kufungua mlango wa nyumba yake ili aweze kusikia vizuri...Lakini cha ajabu aliziona nyayo za mnyama ambae hakumfaham kando kidogo na mlango wa nyumba yake,,kiukweli hofu kwa mala nyingine ilimjaa mama chongela huku akihisi kitu kwa mume wake.
"mh huyu ni mnyama gani,mbona nyayo zake sijawahi kuziona tangu nizaliwe" Alijisemea hivyo mama chongela,akiwa anazifatilia ziliko elekea.Lakini alipo fika mbali kidogo na nyumba yake,hakuziona tena zile nyayo zaidi aliona mburuzo mkubwa wa nyoka,aliogopa akawa amerudi nyumbani hima.
Basi baada mama chongela kufika nyumbani kwake,moja kwa moja alielekea mpaka kwenye kile kichuguu alichofukia chungu ambacho alicho kabiziwa na yule bibi kizee ili kumrudisha chongela katika uhai wake kama awali baada kugeuka kichuguu.
Ila kwa bahati mbaya mama chongela hakuona kitu chochote kunako kile kichuguu,kiukweli aliuzunika sana akiamini kua safari hiyo huwenda yule bibi kizee kamdanganya lakini yote kwa yote alivuta subira ingawa alikua tayali amesha anza kupoteza imani ya kurudi kwa mwanae chongela.
Wakati huo ile mbiyu ya kijiji nayo ilikua ikiendelea kupasa kila kona ya kijiji,ambapo ili walazim baadhi ya wanakijiji waliokua wamedamkia mashambani kurudi hima kijijini kwao ili kuskiliza kipi kimetokea au kipi kinacho tarajia kutokea..maana wahenga walisha sema LAMGAMBO LIKILIA UJUE KUNAJAMBO.
Naam.Basi baada ya nusu saa wanakijiji walikua tayali wamekusanyika kwa chifu(mtemi)kumsikiliza wakati huo chifu nae akionekana akitoka ndani ya nyumba yake iliyokua ya majani juu na chini...wanakijiji wote kimya baada kumwona chifu akijikongoja na bakora yake mkononi huku nyuma yake akionekana mfuasi wake akiwa amebeba kiti cha kukalia chifu.
Chifu alikohoa kwanza,huku akiwatazama wanakijiji wake walitii mbiyu yake pia pole pole akiketi kwemye kiti chake.
"Habali zenu" Chifu aliwasalim wanakijiji,nao wakaitikia kwa adabu na taadhima,ambapo baada chifu kuitikiwa na wanakijiji wake aliongeza kwa kusema.
"kwanza kabla sijaendelea na mada nyingine,ningependa kuuliza swali,nalo hilo swali lijibiwe na mtu mmoja"Akakohoa kwanza,kisha akanywa kidogo pombe yake ya kienyeji iliyokua kwenye kibuyu pembeni yake.
"naam sasa swali lenyewe ni hili hapa..hivi mnajua jana usiku tulivamiwa na kitu gani?"
Chifu aliwauliza wanakijiji wake,ambapo nao walikua wakitazamana.
Lakini mala ghafla kwenye ule mkutano alitokea mama chongela,hivyo kabla hajakaa sawa aliulizwa swali na mtu aliekua pembeni yake swali lile lile alilo uliza chifu...Kwahiyo kwa kua mama chongela alikua ameziona nyayo za mnyama ambae hakumtambua malangoni kwake,haraka sana alinyoosha mkono kutaka kumjibu chifu swali lake.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"eenhe mama emnu tuambie"
Chifu alimruhusu mama chongela kujibu swali lake.
"ndugu chifu najua swali lako ni ngum sana kulijibu,lakini kwa maelezo zaidi nendeni nyumbani kwangu mtapata majibu sahihi"
Aliongea hivyo mama chongela huku akitetemeka,na punde si punde chifu aliwaamuru vijakazi wake kwenda haraka nyumbani kwa mama chongela ambapo waliweza kuzishuhudia nyayo za mnyama wa ajabu ambae mala ya mwisho kutoke ni miaka milioni kadhaa iliyopita.
Hivyo basi baada wale vijakazi wa chifu kupata data kamili walitaka kuondoka lakini walisita baada kusikia sauti ya mtu akikohoa ndani ya nyumba ya mama chongela.."shiiii tulia bwana usikurupuke"
Mmoja kati ya wale vijakazi wa chifu alimnyamanzisha mwenzake ambae alionekana kutaka kumwita kwa amri yule mtu aliekohoa ndani ya nyumba aliyokua anaishi mama chongela.
Basi wakati wale vijakazi walipotaka kufungua mlango wa nyumba,mala ghafla ulifunguliwa nae hakua mwingine ni baba yake wakambo chongela alionekana kua na maskio tofauti pia hata macho yake yalikua si ya kibinadam.ZIMWI.
Waliogopa wale vijakazi,bila kuchelewa walikimbia mpaka mkutanoni ambapo waliweza kutoa taarifa kamali juu ya kile walichokion.
Na hivyo chifu aliwaita vijakazi wengine ambao walikua wakihesabu idadi ya wanyama waliokufa kwa kujeruhiwa na mnyama wa ajabu ambao hawakujua.
"naaam chifu"Vijakazi walitii amri kwa chifu wao.
"naam niniii?chuku silaha na mbwa nendeni mkamtafute huyo mnyama kwa kufata nyayo zake mahali alipopita,pia na mwambieni huyo mwanaume mlie mwona akiwa na maskio ya ajabu aje hime kwa chifu"
Chifu aliongea kwa ukali,wakati huo polepole anga likionekana kubadirika kua giza hali ya kuwa saa sita mchana..Vile vile nyumbani kwa mama chongela kwenye kile kichuguu alichofukia chungu ambacho alipewa na yule ajuza,ghafla alionekana nyoka ambae kadli muda ulivyozidi kwenda nae yule nyoka alikua akibadilika kuingia katika umbile la binadam.
Wakati kunako kichuguu akionekana nyoka ambae alikua akibadilika pole pole kuingia kwenye umbile la binadam,muda huo huo walitokea vijakazi wa chifu wakiwa na kundi kubwa la mbwa pamoja na siraha mbalimbali..
"yuko wapi yule mzee"
Alihoji mmoja kati ya wale vijakazi,ambae alikua akiulizia mahali alipo baba yake wa kambo chongela.
"sijui labda tuzunguke nyuma ya nyumba"
"ok tunazunguka wawili wengine mbaki hapa hapa mpaka pale mtakapo sikia mayowe,sasa??"
"sawa mkuu"
Walikubaliana hivyo wale vijakazi,nia na madhumuni kumpata baba yake wa kambo chongela ili wamwambie kua anahitaji kwa chifu.
Wale vijakazi wawili waliojiteua walizunguka nyuma ya nyumba wakiwa sambamba kabisa na mbwa,na hivyo punde si punde mbwa mmoja alionekana kuambaa na njia kuelekea polini kumbe tayali alikua ameshanasa harufu frani ya mnyama,basi nao wale vijakazi baada kugundua hilo,walimfatilia yule mbwa ghafla wakawa wameshtuka baada kuona nyayo za mnyama ambae hata wao hawakuweza kumtambua.
Haraka sana bila kupoteza wakati waliwaita wenzao,wakaungana pamoja na safari ikawa imeanza rasmi kumtafuta huyo mnyama ambae hakuweza kutambulka vilevle alikua amefanya balaa la kutafuna mifugo ndani ya hicho kijiji cha geza ambacho ndicho alichokua akiishi chongela.
Hivyo basi harakati ziliendelea mbwa wakiwa mstari wa mbele,lakini punde si punde ilisikika sauti ya mbwa ambapo alilia mala moja tu wakati huo anga nalo likizidi kubadilika licha ya kua mchana kweupe jua kali,lakini giza lilianza kujongea kiendo ambacho kiliwafanya vijakazi wa chifu kuingiwa na hofu kubwa...na hapo ndipo walipoamua kujikusanya kwa pamoja huku wakipiga mirunzi ya kuwaitwa mbwa.
"jamani hili sasa limeshakua balaa"
Aliongea hivyo kiongozi wa kikosi.
"haswaa hata mimi ninahofu huko tuendako,maana kama mlivyoona tayali tumempoteza mbwa mmoja ambae ndio jasiri kuliko wengine je,tunajua kilicho muua?
Mwingine kati ya wale vijakazi aliongeza kwa kusema hivyo,huku akimaliza kwa swali ambalo liliwafanya wote kutazamana.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Basi hatimae kimya kilitawala kidogo,wengine wakionekana kusokota sigara aina ya tumbaku vile vile wengine macho yao yalikua yakiangalia juu wakistaajabu jinsi jua na mwezi vinavyo ingiliana kwenye njia(kupatwa kwa jua)
"jamani angalieni jua na mwezi vinagombana"
Aliongea mmoja kati ya wale vijakazi,ambapo alikatazwa na mkuu wa kikosi kutazama pindi ambapo jua na mwezi vinapo patwa.akimwaminisha kwamba ni vibaya kwqni huwenda akageuka kua mbwa mwitu.
Hivyo baada mkuu wa kikosi kwisha kusema hayo hatimae giza nene lilitanda angani,mchana ukawa giza huku kwa mbali ndani ya msitu ikisikika sauti ya ajabu ambayo ilizidi kuwatia hofu wale vijakazi wa chifu.
Kiukweli hofu ilizidi kuwajaa,huku mkuu wa kikosi akishindwa kutoa uamzi sahihi kama kuendelea na mawindo au laa...Maana laiti kama ataamulu kurudisha jeshi kijijini basi adhabu ni mmoja tu kutoka kwa chifu kuua kwa sababu chifu wa hicho kijiji alikua hapendi kushindwa au vijana wake washindwe.
Ama hakika jasho lilimtoka mkuu wa kikosi,akiwatazama wenzake kwa mwanga hafifu ambao ulianza kuonekana baada jua na mwezi kuachana polepole.
Naam.basi wakati mkuu wa kikosi akiwa bado haelewi kipi cha kufanya,huku kijijini nako alionekana mama chongela akikimbia hima kuelekea nyumbani kwake baada kutoka kwenye mkutano wa kijiji.
Hivyo kabla hajaingia ndani alielekea kule kwenye kichuguu ambako ndiko alikokua kakifukia chungu alichopewa na ajuza..Kwa hakika mama chongela alifrahi sana baada kumwona mwanae chongela juu ya kile kichuguu..lakini kabla hajambeba kuondoka nae,ghafla ilisikika sauti ikimwambia mama chongela kua amchunge chongela asinyeshewe na mvua au kulowanishwa na maji yoyote yale...Ili uhai wa chongela uwe mrefu kinyume na hapo chongela atapotea na baadae kusababisha maafa kwenye kijiji.
Kweli mama chongela alitii kwa kutikisa kichwa huku akiachia tabasam pana,ila ghafla tabasam ilipotea baada kumwangalia mwanae na kugundua kua chongela ni nusu mtu nusu nyoka.
Hakika hofu ilimjaa mama chongela,ila alitulizwa na ajuza aliyemtokea na kumwambia kua"huyo ndio mkombozi wenu katika kijiji chenu mtunze awaokoe"
Baada kusema hivyo,yule ajuza alinyoosha kiganja chake kisha akamwonyesha mama chongela jinsi mume wake alivyolaaniwa mpaka kugeuka zimwi.
Kiuweli mapenzi yana nguvu,kwani licha mama chongela kunyanyaswa na mume wake kuhusu chongela,ila bado alimlilia mume wake ambae kageuzwa zimwi...Lakini wakati mama chongela alipokua akiendelea kulia,mala ghafla.
____
Akawa amepasa sauti kali iliyoambatana na mwangwi ikisema.."Kaa kimya kabla sijabadilisha uamzi wangu"
Naam! kutokana na ile sauti kumtisha mama chongela,hatimae alinyamanza kimya huku akimtazama mwanae chongela ambae kwa mbali alionekana na mwili gamba la nyoka.
"Ondoka mahali hapa,pia usipuuzie masharti niliyokwambia kuhusu kumtunza chongela"
Ajuza aliongea hivyo kwa msisitizo,wakati huo giza limeshapotea...na mwanga nao ukawa umeangaza kijiji kizima.
Baada mwanga kumlika kila kona kijiji kizima,hatimae yule kiongozi wa kikosi aliamulu vijana kuendelea na mawindo ya kumuwinda yule mnyama ambae hakuwahi tokea tangu karne ya ya sita..lakini mwishowe waliambulia patupu kwa maana hawakuweza kumwona zaidi walikuta nyayo tu....Kwahiyo baada kumkosa waliamua kurudi kijijini wakiwa mikono mitupu,huku mbwa wao mahili wakiwa wameshampoteza..kitendo ambacho kilimuudhi chifu,hivyo akawa ameamulu auwawe aliekua kiongozi wa kikosi....Kweli bila huruma alifungwa kamba ya katani,kisha akapelekwa kwenye mti mkubwa kuliko yote pembezoni kidogo ya kijiji,mti uliokua umefungwa kitambaa chekundu..na hapo ndipo alipo chinjwa kama mbuzi mbele ya umati wa wanakijijji huku familia yake ikishudia jinsi mzee wao anavyo angamizwa na chifu kikatili.
Hakika ulikua msiba mkubwa kwa familia husika,wanakijiji hakuwa wakilidhika na huku ya chifu wao ila ndio hivyo hakuwa na amri ya kumng'oa madarakani...
Naam!!Basi baada siku kadhaa kupita,hatimae chifu,aliteua kiongozi mwingine wa msafara nia na madhumuni ni kumwangamiza yule mnyama ambae hakuweza kujilikana...pasipo kujua kua yule ni baba yake wakambo chongela ambae alilaaniwa akageuka zimwi ambae ndio aliesababisha maafa kwa wanyama wa kufunmgwa.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
BAADA MIAKA MITATU
Mama chongela akiwa na mwanae nje akimsimulia hadithi za zamani baada kumaliza chakula cha usiku,mala ghafla kwa mbali katika mbalamwezi hafifu alionekana mume wake akipiga hatua kuja mahali alipokua amekaa mama chongela na mwanae, Kwa hakika ni furaha isiyo kifani iliyomjia mama chongela kwani ndani ya miaka mitatu alikua hajamtia machoni mume wake zaidi ya kuambiwa kua mume wake kageuza zimwi...
Lakini wakati baba yake wakambo chongela alipozidi kusongea nyumbani kwake,pembezoni ya nyumba alikuwepo mbwa koko mbwa mwemba ambae mbavu zake zilikua zikihesabika,lakini cha ajabu licha ya yule mbwa kuonekana mchovu ila alibweka kwa sauti kali iliyowafanya mbwa wengine waishio kijijini kuanza kubweka.
"Embutoa kelele zako hapa"..Aliongea mama chongela akimfukuza yule mbwa koko huku akimwandalia chakula mume wake ambae alikua amepotezana ndani ya miaka mitatu...Na kilichokuja kustajabisha ni ile tabia kupotea ya kumchukukia chongela,kwani siku hiyo alionekana kuongea kwa upole na mtoto chongela wakati huo kelele za mbwa zikiendelea kuskika kijiji kizima.Kuonyesha kua kijijini si salama.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment