IMEANDIKWA NA : ALEXIS WAMILLAZO
********************************************************************************
Simulizi : Baba Wa Kambo
Sehemu Ya Kwanza (1)
Katika mvua kubwa iliyoambatana na ngurumo kubwa pia radi,,,kwa mbali alionekana chongela akiwa katika mavazi yake ya shule,,mavazi ambayo yalikua kukuu pia mfuko wake wa madaftari nao ukiwa na mikanda ya kamba za migomba.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Basi chongela alitembea harakaharaka ili awahi nyumbani,,Hivyo harakaharaka ikawa mwendo hatimae chongela alifika nyumbani kwao,ambapo alitaharuki baada kumkuta mama yake akiwa ameshikata tama huku machozi yakimtoka mashavuni mwake ...Lakini chongela licha ya kuona hali ile hakuweza kuhoji chochote,bali alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwake kubadilisha nguo zake za shule na kisha kuzianika kwenye fito nyembamba iliyokua imetundikwa chumbani kwake kwa niaba ya kuwekea nguo.
Na baada ya hapo alivaa nguo zake za kushindia ambazo nazo zilikua na viraka kila upande,,kisha akatoka chumbani akaelekea sebleni alipokua amekaa mama yake ambae alikua akitokwa na machozi.
"mama kuna nini mbona unalia"..Chongela alimuuliza mama yake kwa sauti ya upole huku akimfuta machozi kwenye paji la uso wa mama yake..Lakini mama chongela hakumjibu mwanae bali aliishia kumtazama tu huku machozi yakizidi kumtoka..kitendo ambacho kilimfanya chongelea nae kuangua kilio wakati huo akizidi kumbembeleza mama yake.."mama nyamanza mi sina njaa..mamaaaa nyamanza basi"
Chongelea alisikika akisema hivyo,kwani alijua huwenda mama yake anafikilia jinsi yeye atakavyopata kula...
Basi wakati kilio cha mama na mwana kikiendelea ndani,mala ghafla alikuja baba yake wa kambo chongela ambae ndie aliemuoa mama chongela.."kwahiyo nyumba yangu mmegeuza zahati au"..Aliongea hivyo kwa sauti kali baba yake wa kambo chongela,huku akiweka jembe na panga chini maana alikua ametoka shamba.
Hivyo mama chongela baada kusikia sauti ya mume wake,alifuta machozi yake kisha akamnyamanzisha na mwanae,,akakaa kimya.
Nam.baada kimya kutawala ndani,ndipo baba yake wa kambo chongela alipo ingia chumbani kwake halafu akamwita mkewe..Nae mama chongole haraka alitii wito wa mume wake.
"mama chongela kwanini unakiburi sana mke wangu"..Alihoji hivyo yule baba yake wakambo chongela,lakini mama chongela hakujibu chote zaidi aliishia kuinamisha uso wake chini akionekana kulitafakali swali alilokua ameuliza na mume wake.
"hujaelewa nilicho kuuliza"
Aliongeza kwa kusema hivyo baba wa kambo baada kuona hajibiwi swali alilouliza.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Basi mama chongela nae ndipo aliposhusha pumzi kisha akasema"najua kua hutaki kuishi na mwanangu,ila kumbuka wakati unachumbia nilikwambia kua nina mtoto..nawe ukasema hilo sio tatizo,sasa nashangaa leo hii unanigeuka hivyo unadhani nitampeleka wapi mwanangu"..Alijibu hivyo mama chongela kwa sauti ya huruma huku akijifuta machozi na khanga yake aliyokua amejifunga kifuani.
Lakini licha ya mama chongela kutia huruma,ila mume wake hakujali zaidi thamani ya chozi lake,,bali alizidi kukandamiza kwa kusema"nimekuoa wewe ili tujenge familia na sio nimekuoa ili tumlee huyo chokolaa lako"
Hakika yalikua maneno mabaya sana,maneno ambayo mume wake mama chongela alithubutu kuongea wakati huo chongela akiwa sebleni akisikia yote yaliyokua yakiongeleka chumbani kwa mama yake...Kiukweli chongela aliumia sana moyoni huku akijiuliza maswali juu ya yule baba yake wa kambo,kwa sababu siku zote alijua kua yule ndio baba yake mzazi kama alivyokua ameambiwa na mama yake hapo awali.
Basi siku hiyo chongela alishinda mnyonge kwani yale maneno ya baba yake wa kambo yalimkwanza sana moyoni mwake,,na hata usiku ulipoingia chongela alikataa kula kitendo ambacho kilimfanya pia mama yake kusisia chakula.
Hivyo licha ya mama na mwana kukataa kula chakula,ila ilikua tofauti kwa baba yake wakambo chongela kwani alikula bila wasiwasi huku akitoa maneno ya mabaya kwa chongola..lakini chongela hakujibu kitu chochote bali alifkilia kupanga siku ambayo atakaa kumuuliza mama yake wapi alipo baba yake halali.
Basi,siku zilikwenda chongela akiwa bado anaishi katika mazingira magumu kutoka kwa yule baba yake wa kambo,,,kwa maana yule baba yake wa kambo hakuweza kumjali kwa mavazi hata malazi...Nae chongela alipo jaribu kumuuliza mama yake wapi alipo baba yake,cha ajabu mama chongela hukuweza kumjibu mwanae zaidi ya kuishia kusikitika kuashilia kua kuna kitu nyuma ya panzia mpaka kupatikana kwa mtoto chongela mtoto ambae alikua na ulemavu kidogo wa ubongo pia ukimtazama kwa umakini baadhi ya sehem ya mwili wake ilifanana na ngozi ya nyoka...pia kadli alivyozidi kuku, chongela alionekana kupendelea sana kucheza na wadudu,kitu ambacho baba yake wa kambo alikua hakipendi hivyo akawa amezidi kumuwekea uhasama wa kumchukia..ambapo chongela alikosa raha mda wote.
Basi usiku mmoja wa mbalamwezi mama chongela akiwa na mwanae nje akimsimlia hadithi za kale,,wakati huo baba mwenye nyumba akiwa bado hajalejea nyumbani..Ndipo mama chongela alipo pata nafasi ya kumuhusia mwanae kwa kumwambia kua asipende kutembea wakati mvua ikinyesha maana itamletea tatizo...Hivyo chongela nae baada kusikia maneno yale ya mama yake ndipo alipo muuliza"kwanini mama"...Ila kabla mama chongela hajamjibu mwanae,mala ghafla zilisikika nyimbo za hapa na pale,,,nae hakua mwingine ni baba yake wakambo chongelea ambae alionekana kulewa kupita kipimo.
Hivyo basi baada mama chongela kumwona mume wake kwa mbali akiwa amelewa,,,haraka sana alimpeleka mwanae ndani kisha akatoka nje kumpokea mfuko ambao alikua nao mume wake mkononi.....Lakini licha ya mama chongela kuonyesha heshima kwa mume wake,ila yeye hakujali hilo...zaidi aliamwambia mkewe kua endapo kama atamkuta chongela ndani ya nyumba yake,basi atamkata kata mapanga,maneno ambayo aliongea baba yake wakambo chongela huku akiyumba yumba.
Mama chongela alishtuka baada kusikia mume wake ametoa ile kauli,hivyo haraka sana alikimbia ndani kumficha mwanae chini ya kitanda ili asijeruhiwe na baba yake wa kambo.
Na baada kufanya vile,alitoka nje ambapo alimkuta mume wake akinoa upanga kwenye jiwe lilokua jirani na nyumba yake..
"mala nyingi huwa nasema nimekuoa wewe na sio mwanao ila wewe hunielewi,sasa ngoja nikuonyeshe"
Aliongea hivyo yule baba yake wakambo chongela huku akipitisha kidole kwenye makali ya panga ili kujua kama limeshakua kali...Na baada kuona panga lake limekua kali,ndipo alipo nyanyuka kisha akaelekea ndani kwa nia moja tu ya kumchinja chongela.
Kiukweli usiku ule mama chongela alishindwa kuita majiran maana ulikua usiku wa pata saa nne,ampapo kijiji kizima kilikua kimya...Hivyo mama chongela alibaki akiwa ameshika kichwa huku akiomba mungu mwanae asifurukute uvunguni.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Basi baba yake wa kambo chongela aliweza kumtafuta chongela nyumba nzima,lakini hakuweza kumaona,,,na baada kumkosa alimwita mke wake kwa sauti kali,sauti ambayo iliweza kumtia hofu mama chongela..ila alijipa moyo kua endapo kama mume wake atamwanzishia vurugu basi atajitahidi kujitetea,,wazo ambalo
wishowe aliliona halina maana kwa sababu alihofia kufkuza na mume wake..nao ndio utakua mwanzo wa kuteseka na mwanae chongela ambae hatakiwi kunyeshewa na mvua.
Basi mama chingola aliweza kutii wito wa mume wake,,hivo haraka sana aliingia mpaka chumbani na kabla hajakaa sawa ghafla alipigwa kofi la shavuni..kofi ambalo liliambatana na swali"yuko wapi chokolaa wako?"
Lakini mama chongela hakuweza kumjibu swali lake wala kumludishia kofi alilopigwa,ingawa uwezo huo wa kumludishia alikua nao kwa sababu mume wake alikua amelewa sana siku hiyo.
"narudia tena,chokola wako yuko wapi"
Mama chongelea alizidi kuuliza kwa msisitizo,wakati huo chongela akiwa uvunguni akiskiliza kilio alichokua akiitoa mama yake...hakika machozi yalimtoka chongela,alitamani kujipeleka mwenyewe kwenye mikono ya baba yake wa kambo,,ili mama yake awe huru.
Hivyo basi mama chongela baada kuona kibano kinazidi,,,kiukweli alijaribu kujitetea mwishowe akafaulu kuponyoka katika mikono ya mume wake...kwahiyo bila kukawia alikimbilia chumbani kwa mwanae,akamchomoa uvunguni kisha akatoweka ndani akimwamcha mume wake akijinyanyua nyanyua wakati huo akiwa chini.
Nam.Baada mama chongela kutoroa ndani na mwanae,,kiukweli hakuwaza kwenda mbali sana kwani alihofia kushambuliwa na wanyama wakali ambao hupendelea kutembea tembea saa za usiku kijijini kwao...Hivo mama chongela akiwa amembeba mwanae mgongoni na kitenge kilichokua kina viraka vilivyo shonwa kwa sindani ya mkono,,Hatimae aliweza kujibinza kwenye moja shamba la migomba pale kijijini kwo,ili apate kupumzika na mwanae...wakati huo anga nalo likijidhatiti vizuli ili mvua inyeshe maana ulukua msim wa masika.
Kiukweli mama chongela baada kuona hali ile ya mawingu mazito na radi nyingi angani,hakika machozi yalimtoka huku akimtazama mwanae,,amempakata..Alijiuliza ni jinsi gani ataweza kuokoa maisha ya mwanae ambae hatikiwi kunyeshewa na mvua..
Hivyo wakati akiendelea kujiuliza bila kupata jibu,mala ghafla alisikia sauti ya mvua kwa mbali,,,mvua ambayo ilionekana nyingi ikija maeneo aliyokua amejibanza mama chongela na mwanae ambae hatakiwi kunyeshewa na mvua.
Basi mama chongela baada kuona mvua kubwa ikinyesha kuja maahali alipokua,hatimae alimficha mwanae katika ya migomba minne iliyokua imeota kwa pamoja kisha akachuma na majani mawili akayaweka juu ya mwanae alipokua amemuhifadhi.
Hivyo mvua kubwa aliendelea kunyesha usiku ule huku radi mbalimbali zikkmulika kila pande,wakati huo mama chongela akinyeshewa huku akiomba dua mwanae asidondokewe na toni la mvua ...
Na baada kupita masaa mawili,mvua ilikatika na ndipo sauti mbali mbali za fisi zilianza kusikaka..ambapo mama chongela aliamua kumchukua mwanae kisha akajisogeza jirani kidogo na kijiji.
Kweli mpaka anakikalibia kijiji,tayali palikua pamekucha..ambapo mama chongela aliamua kupita kwa mwenyekiti wa kijiji ilikumweleza hali halisi jinsi anavyoishi na mume wake.
Hivyo mwenyekiti wa kijiji nae baada kuguswa na hilo tukio,,aliamua kumtuma kijumbe ili akamwite mume wake mama chongela tena mwenyekiti alionekana kumsisitiza mjumbe amuwahi kabla hajaelekea shamba.
Kweli punde si punde yule mjumbe alirudi na baba yake wakambo chongela,ambapo nae alishtuka baada kumwona mama chongela pale kwa mwenyekiti wa kijiji....
Basi baada mume wa mama chongela kufika kwa mwenyekiti,alitoa salam kama ilivyo ada..na baada ya salam ndipo mwenyekiti alipo muasa baba yake wakambo chongela kua ajaribu kua sambamba na mkewe bila ugomvi wowote.
Kwa upole zaidi,mume wa,mama chongela nae baada kusikia mwenyekiti akimwambia hivyo ndipo nae alipo mjibu kua hana tatizo na mke wake maisha yanaenda sawa sawaia....Aliongea hivyo baba yake wakambo chongela huku akimtazama mkewe kwa jicho la husda.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"sawa kama hakuna tatizo mnaweza kwenda na amani itawale katikati yenu huu msim wa masika pambaneni na jembe na sio nyinyi kwa nyinyi"
Mwenyekit wa kijiji aliwaambia hivyo mama chongela na mume wake..Ambapo nao waliitikia kisha wakanyanyuka na kuondoka.
Lakini wakati mama chongela akiwa njiani na mume wake wakielekea nyumbani baada kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji,,hatimae baba yake wakambo chongela aliamwambia mama chongela kua kamzalilisha kwa mwenyekiti hivyo asubili kipigo.
Kiukweli mama chongela aliumia sana moyoni mwake,lakini ndio hivyo ilimbidi avumilie kwa sababu kijijini kwao aliko zaliwa ni mbali pia njiani kuna wanyama wakali na mauzauza mbalimbali ya mizim toka enzi kabla ya wakoroni..kwahiyo aliogopa kurudi kwao kwa kohofia kumpoteza mwanae njiani.
Hivyo basi baada kufika nyumbani,ndipo baba yake wa kambo chongela alipo amua kumfungia ndani mke wake kisha kumcharaza fimbo..huku akimkashifu kua yeye ni tasa(hazai)
"miaka mingi nimeishi na wewe sioni dalili ya kupata mtoto zaidi ya kunitangaza vibaya kwa mwenyekiti sasa leo utanitambua mimi ni nani"
Aliongea hivyo baba yake wa kambo chongela,huku akimpiga fimbo mkewe...wakati huo chongela akiwa amefjngiwa mlango nje.
Hakika mama chongela alilia sana kwa sauti kubwa,sauti aliyowafanya baadhi ya wapita njia kukatiza nyumbani kwa kinachongela kuja kushuhudia kilichokua kikiendela...
Hivyo nae baba yake wakambo chongela baada kuhisi kua nje kuna umati wa watu...hatimae alitoka ndani na upanga kuwafukuza wale watu waliokua wamekusanyika nje ya nyumba yake,,kweli wale watu nao baada kumwona baba yake wakambo chongela kashika panga,,walisambalatika kwa kuogoa kujeruhiwa.
Na yote hayo yule baba wa kambo aliyafanya huku chongela akimtazama machozi nayo yakimtoka,,hakika chongela alitamani kumwombea msamaha mama yake lakini aliogopa kwa jinsi baba yake alivyokua amefyum.
Hivyo basi baada baba yake wakambo chongela kuwafukuza wale watu waliokua wamekusanyika nyumbani kwake,,hatimae alirudi tena kwa mama chongela ambapo baada kumfikia,,,bila huruma alimtoboa jicho moja huku akisema"hii ndio fundisho kwako na chokolaa wako"..Hakika mama chongela alilalama sana huku maji ya jicho yakimtilika,,wakati huo chongela akiwa nje akiishia kusikia tu kilio cha mama yake pasipo kujua kilichomkuta...lakini mwishowe sauti ya mama chongela ilikata ghafla.
Nam.baada baba yake wakambo chongela kwisha kumfanyia unyama wa kumtoboa jicho moja mama chongela,,hatimae alifungua mlango ambapo alimkuta chongela akiwa amejikunyata pembezini mwa nyumba kama kifaranga cha kuku kilicho nyeshewa.
Basi baba yule baba wakambo,aliweza kumwambia chongela kua aende kijiji jirani akachume dawa kwenye mti aina mtunduli,huku akiamini kua kutokana na umri aliokua nao chongela hatoweza kuujua huo mti zaidi atachelewa tu..na kuchelewa kwake chongela kutamfanya yeye aweze kumzika mama chongela bila mtu yoyote kujua..maana baba yake wakambo chongela liamini kua ameua baada kuona mama chongela akiwa kimya bila kutikisika wa kupumua.
Kweli chongela alihahaa sana bila mafanikio,na mwishowe aliamua kurudi nyumbani baada kuukosa huo mti..lakini wakati chongela alipo kua njia akirudi nyumba,mala ghafla anga lilianza kubadilika ikionyesha kua mda wowote mvua itanyesha maana ulikua msim wa masika...Hivyo basi baada chongela kuona hali ile ndipo alipo kumbuka maneno ya mama yake aliyomwambia kua asitembee kwenye mvua kubwa...Na baada kukumbuka maneno hayo,chongela alitimua mbio ili asinyeshewe ila mbio zake hazikumsaidia kwani alipo karibia nyumbani tu ghafla chongela aligeuka kichuguu,,,na juu ya kile kichuguu alionekana nyoka mkubwa kiasi ambae alikua akitoa ndimi nje mda wote wakati huo mvua ya mawe ikiendelea kunyesha huku kwa mbali akionekana bibi kizee akiwa na mkongojo wake akipiga hatua kuelekea kwenye kile kichuguu.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati hayo yote yakiendelea,ndani nako baba yake wa kambo chongela alikua akichimba kaburi ndani ili amzike kimya kimya mama chongela.
Lakini bahati nzuli wakati akikazana kuchimba kaburi,mala ghafla mama chongela alikohoa kunyesha kua bado yupo hai na sio kafariki kama mume wake alivyodhani.
Hivyo basi kitendendo kile cha mama chongela kukohoa,kilimfanya baba yake wakambo chongela kuahilisha kuendelea kuchimba kaburi ila aliweka meza juu ya ile kaburi huku moyoni akijisemea kua"ipo siku hili kaburi litamfukia mtu tu"
Baada kunena hayo maneno,alitoka ndani na panga pia jembe kisha akaelekea shamba wakati huo mvua ilikua imekatika.Huku akimwacha mke wake akiwa chini jicho lake likizidi kutoa maji na dam kwa wingi,lakini hivyo hivyo licha ya mama chongela kuhisi maumivu makali ya jicho lake alilotobolewa na mume wake,ila alihitaji kujua mwanae kipenzi wapi alipo.Aliita "chongela chongelaa chongelaa"Lakini hakuweza kusikia mwanae akiitika kitendo ambacho kilimfanya awe na wasiwasi mkubwa ila hakuchoka kuita aliendelea kuita,lakini hivyo hivyo chongela hakuitika.
Basi mama chongela baada kuona kimya,aliinuka kutoka pale chini alipokua amezimia muda wote,kisha akaelekea nje kumwangalia mwanae huku mkono wake wa kulia ukiwa umeziba jicho lake lilokua likivuja maji na dam muda wote.
Hivyo baada mama chongela kufungua mlango wa nyumba yake mlango ambao ulikua wa matete,hakika hakuamini kile alicho kiona mbele yake.kikweli alilia kama mtoto mdogo huku akipiga hatua kuelekea kwenye kile kichuguu ambacho.Na baada kukifikia kile kichuguu,hivyo hivyo alizidi kulia mikono yake ukipapasa kile kichuguu,na mdomo wake ukimtaja mwanae chongela.
Lakini kilio cha mama chongela hakikusaidia kitu kwani licha ya kulia sana ila chongela hakulejea.
Hivyo basi huku nako upande wa pili baba yake wa kambo chongela akiwa shamba akiendelea na kazi,mala ghafla yule bibi kizee ambae mwanzo alionekana akipiga hatua kuelekea kwenye kile kichuguu ambacho mwanzo kilikua chongela,alimtokea baba yake wa kambo chongela.
Kiukweli baba yake wa kambo chongela alishtuka baada kumwona yule ajuza, alirudi kinyume huku akipanga njinsi ya kumkimbia yule ajuza ambae alionekana kutisha maana macho yake yalikua kama ya nyoka pia ngozi yake ambayo ilionekana kukunjamaa nayo kwa mbali ilifanana na gamba la nyoka.
Basi wakati baba yake wa kambo chongela alipokua akipanga mipango ya kumkimbia yule ajuza,ghafla alijukuta miguu yake ikiwa imefungwa na kamba ya za katani huku nako anga likizidi kubadilika ambapo punde si punde giza la kawaida lilionekana licha ya kua saa sita mchana huku jua na mwezi yakiambatana pamoja,hivyo ikawa kupatwa kwa jua na mwezi.
Naam.Hali ile iliendelea kiujumla kijiji kizima cha geza,kijiji ambacho ndicho alichokua akiishi baba yake wa kambo chongela pamoja na familia yake..Hivyo hali hiyo ya kupatwa kwa jua iliwafanya baadhi ya wanakijiji kutoka mashambani kurudi majumbani pia wengine kufungulia mifugo ili iingie kwenye mazizi yao.
Wakati huo kule shambani baba yake wakambo chongela alikua akiendelea kuhaha jinsi ya kumkimbia yule bibi kizee,Hivyo alikua akijaribu kuzikata zile kamba kwa kutumia kisu chake kidogo alichokua nacho,lakini hazikukatika. Na wakati akifanya hayo,yule ajuza alikua akizidi kumtazama huku mkononi mwake akiwa ameshika kibuyu kidogo ambacho kilikua cha zamani sana..kwahiyo yule ajuza(Bibi kizee) baada kuona baba yake wa kambo chongela ambae alikua kikwanzo kwa chongela anataka kumkimbia,ndipo alipo dumbukiza mkono wake kwenye kile kibuyu chake kisha akatoa unga frani mweusi,na bila kuchelewa akamwagia yule baba yake wakambo chongela ambapo nae baada ule unga kumpata aliwashwa sana mwili mzima huku akipiga mayowe..na punde si punde aligeuka kua zimwi.
Naam.na hayo ndio yakawa maisha mapya ya baba yake wakambo chongela ambea alikua akimyanyasa atakavyo mama chongela na chongela wake,ingawa licha ya huyo baba kua hivyo ila ni pindi ifikapo mwezi mwandamo na katikatika ya siku yani saa sita usiku ndipo anapogeuka kua zimwi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakika ilikua ni laana kubwa aliyo ipata baba yake wakambo chongela,huku ile hali ya kupatwa kwa jua ilikua imeshapotea na maisha yakawa yanaendelea ingawa baadhi ya wazee wa kijiji walikua wakizidi kupiga lamli ili kujua ile hali ya giza kutokea mchana ilimanisha nini,pasipo kujua kua mda ule kuna mtu alikua akipewa laana.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment