Search This Blog

NILIVYOTESWA NA UCHAWI WA SUMBAWANGA - 5

 







    Simulizi : Nilivyoteswa Na Uchawi Wa Sumbawanga

    Sehemu Ya Tano (5)



    MAMBA WA AJABU

    Nilivutwa mpaka nikaanza kuona nagusa mchanga. Hii inamaanisha kina cha maji kilipungua. Sikuwa na shaka, niliona kawaida. Yaani kwa kifupi naweza kusema kuwa akili yangu ilishindwa kutafsiri chochote.

    Nikiwa kama mtu aliyelala akiwa anapiga mbizi, nilivutwa mpaka mchangani. Ilikuwa usiku na mbalamwezi ilikuwa inawaka sana angani na kufanya eneo lile lifunikwe na mwanga wa kutosha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikiwa nchi kavu, nilimuona mwanaume mmoja ambaye tulipokutanisha macho alitabasamu. Alikuwa amekaa chini ya mti, kwahiyo alisimama. Kwa jinsi alivyokuwa anaonesha furaha mbele yangu, hakuwa mtu wa shari.



    "Helena, Helena, mama yako leo atafurahi sana. Hatimaye umerejea, ha ha haaa!" Yule mtu ambaye sikumfananisha na yeyote kwa sura yake, alicheka baada ya kutamka maneno hayo. Alivaa nguo chakavu na miguuni alikuwa peku."Tumehangaika sana lakini leo umerudi. Balinaba alaaniwe, Mungu atakulipia kisasi. Tumeambiwa malipo ni duniani," yule mtu alizungumza akiendelea kupiga hatua kunifuata.



    Kwa maneno hayo, nami nikaanza kupata mshawasha wa kumuona mama. Nilishaamini kwa wakati huo kwamba nimeokoka, hivyo nilichosubiri ni kuwa katika dunia huru, isiyo na maudhi ya namna yoyote ile.



    Mungu hakupanga niokoke wakati huo jamani! Yule mtu akiwa amebakiza hatua kama tatu hivi anifikie, ghafla nyuma yake alitokea mamba mkubwa mno. Yule mtu naye akageuka kuangalia nyuma kwa sababu alipopita vichakani, nyasi zilitikisika.



    Mbio za yule mamba ni vurugu tupu, ile anageuka kumuangalia, hapo naye akapata upenyo wa kumvuka kwa kasi akafika ananipiga kikumbo nikarudi kwenye maji. Kufumba na kufumbua akanifuata na kunibana kwenye mdomo wake.



    Safari nyingine ikaanza. Tulisafiri kwenye maji ambayo sikujua kama ni ya mto, ziwa au bahari. Tulitokeza nchi kavu halafu yule mamba akaanza kunisafirisha kwa mwendo kasi hadi tukafika makaburini.



    Yalikuwa makaburi mengi, alinibwaga chini halafu akaanza kuondoka. Sekunde 10 nyingi nikawa nimezungukwa na kundi kubwa la watu, wanawake kwa wanaume wenye umri mkubwa. Ni wachawi ila walinifanyia udhalilishaji mkubwa sana.



    Nilikuwa uchi, kwahiyo walipofika walianza kuuchezea mwili wangu kadiri walivyotaka. Nilijaribu kuwakemea lakini ikawa ngumu kuwarudisha nyuma. Wingi wao na nguvu yao, vilifanya iwe mtihani mkubwa.



    Mwingine alinishika titi moja na kumuacha mwenzake aendelee na lingine. kuna aliyepeleka mkono wake kwenye kitovu. ila aliyeniudhi zaidi ni yule mwenye mkono mkavu, wenye kukwaruza ambaye alipeka vidole vyake katika eneo nyeti.



    Aliingiza kwa ndani vidole vyake viwili na kunifanya nichubuke mno. Maumivu yalikuwa makali kupita mfano. Lakini yote yakawa tisa, mwisho walinigeuza na mwanaume mmoja alielekea kutaka kuniingilia.



    Mapigo ya moyo yaliongeza kasi, nilimuangalia maumbile yake makubwa nikahisi mwisho kabisa ningepoteza maisha, ukizingatia tayari nilikwishachubuliwa na kuachiwa majeraha na yule mwenye mkono kama dodoki.



    Alikuja huku akiwa anatabasamu, alionesha furaha ya ajabu ilhali kwangu ni maumivu. Bakora yake kubwa, ndefu na nene kama mwichi wa kinu kidogo, ilikuwa wima. Nilihisi kuchanganyikiwa, nikaanza kupiga kelele.



    Umbile langu dogo, ukijumlisha na ukavu wake, kwahiyo ile fimbo yake ikawa haiwezi kupita. Iligoma lakini mwenyewe akawa analazimisha hivyo kuongeza maumivu.



    Kuona hivyo nilipiga sana kelele, ghafla nikashtuka na kujikuta nimelala peke yangu juu ya kaburi. Nikashindwa kupata picha yenye maelezo ya kina. Nimeshtuka na kujikuta nipo kaburini, wakati hata yule mamba alinipeleka makaburini.



    Sura ya makaburi niliyoona baada ya yule mamba kunifikisha ndiyo ile ile ambayo niliiona wakati huo. "Hii ni ndoto gani ambayo kila kitu kinajionesha ni kile kile?" Nilijiuliza swali hilo lakini sikupata jipu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliposimama ili nijiondoe kwenye lile kaburi, mara nilisikia sauti za watoto wakilia. Nilikaza macho kuangalia sauti zilipotokea, kwanza nikaona bundi mkubwa amenitolea macho, halafu nikaona vichwa vya watoto vikiwa vimetenganishwa na viwiliwili vyao. Mungu wangu!




    Kusema ukweli kila tukio halikuwa ndoto. Huwezi kuota upo kwenye mazingira ya daladala halafu ushtuke usingizini ujikute hapo hapo. Kuna kitu zaidi, na hicho si kingine bali ni hila za wachawi waliokuwa na uchu wa kuniangamiza.



    Bado nikajiuliza sababu ya mimi kutaka kukutana na yule mwanaume wa chini ya mti kisha yule mamba kuniwahi ni kunirejesha majini. Mpaka hapo sikujua kama yale maji yalikuwa ni ya ziwa, mto au bahari.



    Nakuwa ngumu kujua kwa sababu Sumbawanga ipo Rukwa, ina ziwa Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa, pia kuna maporomoko. Hivyo, sikujua pale ambapo mamba alinichukua ilikuwa kwenye aina gani ya maji ukizingatia wachawi wana uwezo mkubwa.



    Unaweza kudhani upo Sumbawanga, kumbe siku nyingi ulihamishiwa Tanga na pale ni katika Bahari ya Hindi. Wachawi wana nguvu nyingi na mamba yule hakuwa mnyama wa kawaida, isipokuwa ni wa kichawi ambaye hutumwa kutimiza kazi fulani fulani.



    Niliposimama nilipepesuka na kurudi juu ya kaburi. Ikafuatia hali ya upepo mkali uliovuma kutoka mbali. Mwanzoni nilisikia sauti lakini muda ulivyosogea nikaona kasi yake imefika jirani na sauti ikawa jirani zaidi.



    Ule upepo ulivuma na lindi kubwa la watu, mmoja baada ya mwingine alichomoza kwenye miti, kutahamaki kundi kubwa likawa mbele yangu. Hawakuvutia kwa muonekano wao lakini waliniudhi na kunitisha kwa kile walichokifanya.



    Baada ya kukusanyika mbele yangu walianza kuimba nyimbo za kushangaza. Zilikuwa kelele masikioni mwangu. Walicheza kwa mitindo ya ajabu ambayo sijapata kuona sehemu yoyote kwa mazingira ya kawaida.



    Siku hiyo nilishuhudia kwamba kumbe mchawi akishika mbegu tatu za mti wa zambarau anaweza kupaa mita zaidi ya 20 halafu akaganda hewani kwa zaidi ya dakika tano kabla ya kurudi chini lakini hawezi kwenda sehemu yoyote.



    Nilishuhudia pia kwamba kumbe mchawi akijipaka mchanga kidogo kutoka kwenye kaburi la mtoto, halafu akaficha mbegu ya ubuyu chini ya ulimi, hupotea na hawezi kuonekana kwenye macho ya kawaida mpaka atakapoamua kuondoa mbegu hiyo.



    Kitu kingine nilichokiona siku hiyo ni kwamba kumbe nyoka wa kawaida, hawezi kufanya chochote kwa wachawi. Ila nyoka ambaye ametengenezwa kichawi anaweza kutumika kumshambulia mchawi mwingine kutokana na maelekezo aliyopewa.



    Nililigundua hilo kwa sababu eneo lile lilikuwa na nyoka wengi na wote walitawanyika baada ya ujio wa wale wachawi. Hata wale waliokuwa wamejificha kwenye mashimo, walitoka na kukimbia mbalia na pale.



    Walikuwa wengi mno!

    Lile kundi la wachawi wakati l,ikiendelea kucheza na kuimba mbele yangu, lingine lilitokea kwa nyuma likiwa limeshika kuni na sufuria kubwa. Hatua hiyo ilifurahiwa na wengi kwa sababu shangwe ziliongezeka.



    Kilichokera zaidi ni kuona wanatenga vichwa vitatu vya watu na kuvifanya ni mafiga. Wakaweka zile kuni, moto ukawashwa halafu vile vichwa vya watoto vikatumbukizwa. Yakaitwa mafuta, nikangoja kuona lakini ikwa balaa lingine.



    Lililetwa dumu la ujazo wa lita 20, nilipoona wekundu nikadhani ni mafuta ya mawese, yale yanayotengenezwa kutokana na mbegu za michikichi lakini haikuwa hivyo. Nilishtushwa mno, yalinuka vibaya, hayakuwa mafuta ya kawaida.



    Ilikuwa ni damu ya binadamu. Wakati inaungua ilitoa harufu kali ambayo ilinipa shida. Nilijizuia sana ili nisitapike. Wale wachawi walishangilia kila hatua. Walifurahi kwa jinsi vile vichwa vya watoto vilivyoungua, wao walidai wanavikaanga.



    Walipojiridhisha kwamba vimeiva, bila kuhofu moto, waliingiza mikono na kutoa. Kila aliyetoa kichwa kimoja, aliongozana na mwingine kwenda kugawana. Ikawa mgao ni huo kwamba kichwa kimoja watu wawili. Mgao uliendelea mpaka vikaisha.



    Wapo waliokosa. Kelele za kulaumiana zikaanza. Vurugu zikatawala na kidogo watwangane. Mmoja wa wale wachawi ambaye naye alikosa, akionekana ndiye mkubwa wao aliwanyamizisha. Wote wakatulia kumsikiliza ingawa hasira kali ilisomeka kwenye nyuso zao.



    Aliwaambia waache kupigana, halafu yeye akashinga fimbo yake akapiga kwenye kaburi la kwanza ikatokea maiti ikiwa imezungushiwa sanda. Akachagua kaburi lingine, alikuwa anaangalia wale ambao hawakuwa na muda mrefu tangu walipozikwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zilipatikana maiti tatu, akaagiza ziingizwe kwenye sufuria. Mungu wangu! Ilikuwa inatisha mno kuangalia, kwani haraka haraka wale wachawi waliwavua zile sanda, halafu wawili walimshika kwa mbele, wengine wawili nyuma katikati ikaachwa nafasi.




    Waliponiachia nilitaka kutema lakini pale pale, mmoja wa wale wachawi aligeuka chatu mkubwa. Nikaambiwa nikitema tu, yule chatu atanimeza. Nikatakiwa kuchagua mawili, kutafuna na kumeza ile nyama ya mtu au nimezwe na chatu.



    Nilichelewa kidogo kufanya uamuzi, papo hapo yule chatu alinivamia, akanizunguka mwilini mwangu kisha akaanza kunibana mbavu. Nilijisikia naanza kuishiwa na pumzi, nikawa naona giza lakini baada ya muda aliniachia, hivyo nikahisi nafuu.



    Mmoja wa wale wachawi ambaye alikuwa kiherehere kweli, aliniuliza tena kama nitatafuna na kumeza au nitaendelea kukaidi. Kwa wakati huo akili yangu ilikuwa imechanganyikiwa, hivyo sijui ilitokea nini, nikajikuta tu nimetema ile nyama. Kusema ukweli sikupanga kutema licha ya kwamba sikutaka kula nyama ya binadamu mwenzangu.



    Kumbe kutema ile nyama ilikuwa ni kosa kubwa kuliko hata kumcharaza makofi hakimu mahakamani. Wale wachawi walinishambulia kila mtu kwa staili yake, mwingine alikoa konzi, yule alinipiga ngumi, mwingine kiwiko, kuna aliyenitemea mate.



    Hata hivyo, aliyenikera zaidi ni mama mmoja. Tena namjua, nyumba yake ipo mtaa wa tatu kutoka pale nyumbani kwetu. Nazungumzia kwa baba na mama yangu. Sina maana ya kwa mzee Balinaba, aliyelazimisha penzi langu, matokeo yake akaamua kunitesa kwa wachawi wenzake.



    Yule mama aliona wote waliokuwa wananiadhibu wanacheza, kwa hiyo alichokifanya alikuja akanikalia, akaanza kunisugua usoni kwa makalio yake ambayo hakuwa ameyavalisha nguo halafu akanipumulia ushuzi ambao ulininukia vibaya sana.



    Wachawi ni wadhalilishaji mno. Fikiria mtu kupumulia ushuzi wake usoni kwako, tena akiwa hajavaa nguo. Iliniuma sana lakini nilijisikia zaidi kinyaa nilipomtafakari kwa jinsi alivyo mchafu, akiwa amejipakaa masizi usoni, pia makalio yake yalikuwa na chale mbili kubwa.



    Mchana alionekana ni mwanamke mstaarabu tena alipenda sana kujitokeza kwenye shughuli za kijamii kwenye kitongoji chetu. Iwe misiba na hata harusi lakini usiku ni shetani mkubwa. Hajiheshimu na ni katili kwa namna nyingi na hathamini haki za binadamu wengine.



    Wale wachawi wakiwa wanaendelea kunishambulia, ilitolewa sauti kwamba niachiwe ili chatu aniadhibu.

    Wakatawanyika, moja kwa moja yule chatu akanivaa kwa mara nyingine, safari hii akiwa na kasi kubwa kuliko mwanzo. Alianza kunikaba kwa nguvu kubwa.



    Macho yakaishiwa nuru, pumzi ikawa haitoki na kwa hapo nikahisi sasa nakufa. Kwa mbali nikasikia sauti, nikaifananisha. Nikajitahidi kufumbua macho, alikuwa ni mama akiwa anatabasamu kwa uso usio na shaka. Alikuwa ameshika kisu kirefu, akaniambia imebaki siku moja nitakuwa huru.



    Sikutaka kuona kama kauli yake ina nguvu kutokana na ukweli kwamba pale nilipokuwa ni sawa na nusu mfu kutokana na jinsi yule chatu alivyonikabili. Pale pale mama alinirushia kile kisu, kikanichoma usoni. Niliogopa kwa kudhani kwamba kinakuja kunimaliza.



    Haikuwa hivyo, kilikuwa kisu chenye ukombozi. Baada ya kunichoma, mwili mzima ulitokeza vitu mfano wa miba lakini imara kama misumari. Vilimchoma yule chatu ambaye kwa haraka alijikunjua kwenye mwili wangu na kujitupa pembeni. Kumbe chatu analia sana akiumizwa!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipiga kelele kwa sauti kubwa sana halafu akawa anatweta pembeni. Kumbe kila kilichotokea pale wale wachawi hawakukiona. Hawakumuona mama na hawakujua nini ambacho kimempata yule chatu. Walibaki kushangaa, yaani wao wenyewe waliona miujiza.



    Yule mchawi aliyenitolea hewa chafu usoni, alisogea kwangu kuona kama nina kitu. Alipoona kawaida, alihamia kwa chatu. Akataka kumchunguza. Akawa amefanya kosa kubwa. Yule chatu alimvaa kwa kasi ya ajabu, akamzungusha mzima mzima, akambana mbavu, alipolainika alimmeza.



    Nilitegemea wale wachawi wangeumizwa na ile hali. Siku hiyo niligundua kwamba kumbe wachawi kwa wachawi huwa hawaoneani huruma. Yule mwenzao alipokuwa anamezwa, wao walishangilia kwa nguvu sana. Walicheka kwa kujipongeza kama vile wamepata ushindi mkubwa.



    Baadaye niligundua kuwa kumbe ule kwa taratibu za wachawi ni ushindi mkubwa. Yaani mwenzao kamezwa kama kafara, kwa hiyo wao wangeweza kuendelea na shughuli zao huku wakimtumia yule chatu, vinginevyo ingekuwa tabu na angevuruga mipango mingi ya wachawi.



    Chatu alipomaliza kummeza yule mwanamke mchawi, wachawi wengine walifika pale wakambeba kwa upole. Wakaondoka naye na sikujua wamekwenda wapi. Lilibaki kundi la wachawi wachache ambao walininyanyua tukaongozana kwenye uwanja mkubwa.



    Tulikuta kuna nyungo nyingi na kila ungo ulikuwa na tunguri pamoja na bundi mmoja. Tuliondoka hapo wote kwa kutumia ungo. Mimi nilipanda na babu mmoja ambaye alikuwa mgeni machoni mwangu na sijawahi kumuona popote katika dunia hii, zaidi ya siku hiyo katika mazingira ya uchawi.



    Tulipaa angani kwa muda mfupi mno. Haikuwa zaidi ya sekunde 20 tukawa tumefika kwenye nyumba ya yule mama. Wachawi wote wakatua na papo hapo waligeuka paka kisha walianza kulia kwa sauti kubwa. Kumbe hapo ndiyo walikuwa wanaomboleza.




    Binafsi nilibaki nashangaa. Nikawa sijui vizuri kila kilichoendelea. Ile staili yao ya kuomboleza ilinishangaza na zaidi iliniacha hoi kutokana na vibweka vya ajabu vilivyofanywa na wale paka watu'.

    Niliona kila kitu, ingawa nilishindwa kujua kikamilifu kama mtu angetokea hapo angeweza kuniona. Binafsi macho yangu yalikuwa na udadisi mwingi. Kusema kweli nimeona mengi.



    Wale paka walifanya fujo nyingi, siku hiyo nikapata elimu nyingine kuwa wakati mwingine paka wakilia sana kwenye nyumba na ikabainika kutokea msiba, maana yake aliyekufa aliwahusu.



    Nifafanue kitu hapa kuwa mtu aliyekufa anaweza kuwa anawahusu kwa maana wao wachawi ndiyo wamemuua, hivyo wanapojigeuza paka wanalia, wewe unaweza kudhani wanalia kumbe pale wanacheka, wanashangilia nyama.



    Inawezekana pia aliyekufa alikuwa msumbufu, kwa maana aliwaumiza kichwa siku nyingi kuweza kumuondoa duniani, kwahiyo hushangilia sana kama kielelezo cha kufanikiwa baada ya kusumbuka muda mrefu.



    Lingine ambalo ningependa nilitoe hapa ni kuwa mtu ambaye amewasumbua wachawi kwa muda mrefu, huwa haliwi nyama, badala yake hupelekwa kwenye shughuli za uzalishaji ambapo hufanyishwa kazi kama msukule.



    Hata hivyo, endapo mtu huyo aliyechukuliwa msukule atakuwa mbishi, amri hutolewa ya kuuzwa kwenye himaya ya wachawi wengine na ikiwa huko nako ataendelea kusumbua, atauzwa kwingine mpaka atapotea.



    Hii ina maana kuwa mtu anaweza kuchukuliwa msukule Sumbawanga, baada ya muda akauzwa Tanga au Zanzibar, lakini inawezekana akapelekwa Congo Brazzaville mpaka Nigeria kutokana na mawasiliano.



    Unajua inauma sana. Mtu nyumbani kwao ni Sumbawanga lakini wachawi wanamchukua msukule na matokeo yake anaenda kutumikishwa Ghana kwa wachawi ambao hawamjui, kwahiyo wanamtesa wanavyotaka.



    Msukule huyo anaweza kuteswa, akifanyishwa kazi kwenye mashamba, mifugo, viwanda, maduka na shughuli nyingine za uzalishaji kwa miaka mingi kabla ya kufa ambapo baadaye hurudishwa kwenye kaburi lake la asili.



    Kwa ufafanuzi ni kuwa mtu anapochukuliwa msukule, ndugu zake huchimba kaburi na kuzika kitu ambacho wao hudhani ni mtu. Pale huwa hazikwi mtu, isipokuwa ni mgomba, gogo la mti wa mjorowe au mpapai.



    Kwa maana hiyo, yule msukule anapofariki dunia, hurejeshwa kuzikwa kwenye lile kaburi ambalo alichimbiwa na ndugu zake. Na msukule anapouzwa kutoka eneo moja kwenda lingine, sharti la kwanza kwa yule anayeuziwa ni kujua kaburi lake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kingine ni kuwa elimu yangu ndogo ilinipa mwanga wa kujua kuwa msukule ni lazima azikwe kwenye kaburi lake, pia nikapata kufahamu kwamba siku zote mtu akishageuzwa msukule huwa haliwi nyama.



    Hivyo basi, siku hiyo walikuwa wanaomboleza kifo cha mwenzao ambaye walimtoa kafara kwa chatu aliyetaka kunimeza mimi, lakini mama akaniokoa kwa njia ambayo sikuielewa. Na wala sikufahamu alifikaje pale.



    Nilishangaa kusikia sauti za watu wakilia ndani ya nyumba, hapa ina maana kuwa tayari walikwishapata fahamu kwamba yule mchawi alifariki dunia. Kadiri muda ulivyosogea ndivyo sauti za vilio zilivyopaa.



    Yule mkuu wa wachawi aliyenishika mkono, yeye niliendelea kumuona katika umbile lake la binadamu. Tulisimama kwenye moja ya pembe za nyumba, mara tukatokeza chumbani.



    Hapo niliona mauzauza mengine. Niliona mtu kama yule mwanamke mchawi aliyemezwa na chatu. Umbo na sura ni vile vile. Nikashangaa sana kwa sababu nilishuhudia kwa macho yangu akimezwa na chatu.



    Yule mkuu wa wachawi, aligusa kitanda kile ambacho amelala, yule mtu akapotea na badala yake kukawa na shina la mpapai. Ajabu ni kuwa watu ambao baadaye niligundua ni wanaye hawakutambua na wakawa wanamlilia sana.

    Hawakuniona wala hawakumuona yule mkuu wa wachawi. Baadaye kulipokucha, misukule wengi waliletwa na kuwekwa kwenye paa la nyumba lakini hawakuonekana. Nilishangaa kuona lile shina la mpapai linachukuliwa na kwenda kuoshwa.



    Niliona wanavyohangaika, kusema ukweli niliwahurumia kwa maana binadamu wanasumbua kweli. Wao wanahangaika kumuosha kwa kudhani ni mtu kumbe ni shina la mpapai. Niliona mengi siku hiyo.




    Kila kitu kiliendelea kufanywa kama ilivyo kwenye shughuli yoyote ya mazishi. Nami niliendelea kufuatilia, kimsingi nilijifunza kitu kikubwa sana kupitia msiba huo hususan yale mambo ya kichawi ambayo hutekelezwa pasipo binadamu wa kawaida kuona.



    Mazishi yalifanyika majira ya saa 10 alasiri, lakini kabla ya kufika muda huo kulitokea jambo zito. Ilikuwa mishale ya saa 8 mchana. Kuna dada mmoja alikuwa na maruhani, kwahiyo yalipanda akawa anapiga kelele kuwa eneo hilo kuna vitu vya ajabu.



    Kufumba na kufumbua ile misukule ikaondolewa haraka na wachawi wote wakatoweka. Tulibaki mimi na yule mkuu wa wachawi ambaye alikwenda katikati ya nyumba na kumkalia mtoto mdogo mwenye umri wa miaka minne.



    Yule mtoto alilia sana lakini ikachukuliwa kuwa kilichomliza ni zile kelele za yule dada aliyepandisha maruhani. Alipotulia na maruhani yake, yule mkuu wa wachawi naye aliondoka kwa yule mtoto, hivyo naye akanyamaza. Utulivu ukarejea.



    Kufuatia purukushani za dada mwenye maruhani, angalau idadi ya wachawi na misukule ikapungua, walikuja wachache msibani na kukaa kwa kuibia, halafu wakawa wanabadilishana. Niliendendelea kuwa shuhuda wa mambo hayo yote.



    Kitu kikubwa ni kuwa endapo msibani anatokea mtoto analia sana wakati ambao mtu mwingine kapandisha maruhani, hapo haraka sana inatakiwa kila mmoja kwa imani yake ya dini amkumbuke Mungu kwa maombi yenye nguvu ili kukimbiza ushirikina uliopo.



    Mtu kupandisha maruhani na mtoto au watoto kulia kwa sauti ya juu msibani ni dalili za kuwepo kwa wachawi, mchawi au mazingira ya uchawi katika eneo husika, kwahiyo ni vyema kumtumia Mungu kusafisha kila uchafu unaokuwepo.



    Tukio lingine la kukumbuka usiku huo ni namna wachawi walivyobadili chakula cha watu usiku. Hili lilifanyika kwa wanaume, walikwepa kwa wanawake kwasababu ya yule dada aliyepandisha maruhani alikuwepo, hivyo bila shaka wangefika huko yangeamka tena.



    Wachawi walikuwa wakitembelea makundi ya watu ambao waligawanywa kwenye makundi ya watu watatu kwa kila sahani moja, wakawa wanachukua mboga ambayo ni mchicha na kuweka majani ya maboga mabichi lakini kwa sababu ya kuzingirwa kichawi hawakubaini.



    Walikula pasipo kushtukia chochote. Roho iliniuma nilipowaona wachawi wanachukua mboga ile na kujitenga pembeni na kula wao. Kusema ukweli walifanya hivyo kwasababu ya roho yao mbaya, hakuna lolote ambalo walivuna, kwani kuchemsha mchicha kuna ugumu gani?



    MAMA ALIVYONIOKOA

    Wakati wa kula, mimi nilipewa sahani yangu yenye ugali na mchicha. Yaani wakati watu wa kawaida wakigombea ugali kidogo, watatu kwa sahani moja pamoja na mboga ya majani ya maboga mabichi ambayo walikula wakidhani ni mchicha ulioiva, mimi nilitengewa peke yangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ugali ulitoka jikoni nikapewa, lakini mboga ilichanganywa kwenye kundi moja. Njaa nilikuwa nayo, kwahiyo nilikula kikamilifu mpaka nikashiba. Baada ya kuona tumbo limejaa, nikaanza kutafakari wema wa yule mkuu wa wachawi.



    Tangu kuokoka kule makaburini kumezwa na chatu, aligeuka mtu mwema kwangu, ingawa sikuwa na uhakika kama wema huo ungeendelea hata baada ya kumalizika msiba huo au ni wa kipindi kifupi na baada ya hapo mateso yangerudi tena.



    Nikiwa natafakari hayo, eneo la msibani lilizungukwa na upepo mkali. Mwanga mkali ukawa unatoka angani na kufunika kila kona kiasi kwamba kila aliyeona alidhani mvua kubwa ingefuatia.



    Waliokuwa wamejiandaa kulala barabarani pale msibani, walianza kutafuta sehemu ya kujihifadhi ndani. Ghafla wale wachawi walianza kutawanyika kila mmoja na upande wake.



    Misukule walibaki pale pale msibani. Kikundi cha watu watatu wenye tunguri, wakiwa wamevaa kaniki walitinga kwenye eneo hilo. Sura zao ziliashiria hawakuwa na muda wa kupoteza.



    Nikiwa nawashangaa nilisikia naguswa begani. Alikuwa ni mama. Akaniamuru niwafuate wale watu, nikatii. Mmoja alinishika mkono, wengine wawili wakaenda kuwakusanya wale misukule. Haikuwa kazi rahisi, yalifuatia mapambano makali mno.



    Wachawi hawakutaka kabisa ile misukule iondoke, wakati wale watu ambao kwa wakati huo sikujua wanahusika vipi, nao walilazimisha kuwachukua. Siku hiyo nilishuhudia vita kali mno, kweli ulimwengu wa giza una mambo mengi.




    Mapambano kati ya wachawi na wale watu ambao mama aliniamuru niwafuate, yalidumu kwa dakika takriban 20. Ajabu ni kuwa wengine waliokuwepo pale msibani hawakuona chochote. Kwa wakati huo nilibaki nimeshikwa huku nikishangaa kwa kile kitu.



    Yalikuwa ni mapambano makali. Kwa wakati huo nilijiuliza wale ni watu wa aina gani kwa sababu walionekana wana nguvu nyingi. Walikuwa wachache lakini waliwamudu wale wachawi. Nilishangaa sana kwasababu kabla ya hapo niliamini wachawi wana nguvu nyingi.



    Mwisho wa mapambano hayo, wale watu watatu walishinda. Mchawi mmoja baada ya mwingine waliondoka kwa zamu. Mkuu wao alisimama mbali na akawa anatazama kwa jicho kali. Hakuna aliyejali. Safari ya kuondoka ilianza.



    Kufumba na kufumbua tulifika nyumbani. Ilikuwa furaha ya usiku kwa usiku. Mama alinikumbatia lakini sikuweza kuonana na ndugu yeyote baada ya wale watu nilioongozana nao kudai mambo hayajatulia, hivyo ilitakiwa wakaniwekee ulinzi zaidi.



    Wale watu walitumia dakika zisizozidi 10 kuweka ulinzi wa nyumba kwa maana ya zindiko. Baada ya kuhakikisha kila kitu kipo sawa, safari ya kuondoka ilianza. Mama aliahidi kunifuata siku mbili baadaye.



    Siku hiyo sikujua pale ni wapi lakini kesho yake nilibaini kwamba ni moja ya vijiji katika Wilaya ya Mpanda. Nilijua kutokana na mazungumzo ya wale watu na wakazi wengine wa nyumba tuliyofikia.



    KUMBE NI WAGANGA KUTOKA KONGO

    Swali la wale ni akina nani lilinisumbua kwa muda mrefu. Nikawa nahitaji kujua wamehusika vipi na matatizo yangu. Siku tatu baadaye mama alipokuja kuniona, aliniambia wale ni waganga kutoka Kongo, Brazzaville.



    Aliniambia kuwa baada ya kuhangaika kwa muda mrefu, hasa baba alipofariki dunia, alitafuta njia tofauti za kuniokoa ndipo aliposhauriwa kuhusu watu hao wa Kongo ambao wana nguvu kubwa ya kupambana na wachawi.



    "Mwanangu nilijionea. Wana nguvu kubwa," mama alinisimulia. "Siku mbili tu za mwanzo nilijionea namna wanavyofanya kazi. Nilikuwa nimekupoteza, nikaweza kukuona kupitia chungu chao. Ni waganga wenye nguvu kubwa.



    "Nakuomba sana ukipona kabisa tutoe sadaka kumshukuru Mungu kwa miujiza aliyokutendea. Walitaka kukuua"



    "Hapa imefanyika kazi ya siku 170 mpaka ukaokolewa. Na kilichopo ni kwamba ukishafanikiwa kupona kabisa, utakwenda Tabora kwa shangazi yako mwenye jina kama lako la Helena, amelia kwa muda mrefu mpaka machozi yamekauka.



    "Kwahiyo mwanangu usione hivi, nimehangaika sana. Nimebakiwa na mashamba mawili, matatu nimeuza ili kupata nauli ya kufika Kongo na kuwaleta waganga hao mpaka Sumbawanga. Nakuomba sana, ukipona kabisa tutoe sadaka kumshukuru Mungu kwa miujiza aliyokutendea. Walitaka kukuua."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilitumia dawa kwa wiki nzima. Zilikuwepo za kunywa. Usiku nilioga dawa na ilikuwa ni kawaida kwa wale waganga kuvaa mavazi meupe kisha wakawa wanaimba nyimbo mbalimbali kwa lugha yao.



    Nilikuja kuambiwa baadaye kuwa ile ni njia yao ya kupambana na wachawi. Wale misukule ambao waliwachukua kule walipokuja kuniokoa, taratibu nao wakawa wanarejea kwenye hali ya kawaida, tatizo walikosa ndimi kwahiyo wakawa hawawezi kuzungumza.



    Mwezi mmoja walipona kabisa, wakawa wanarudishwa kwa ndugu zao kwa siri kubwa. Nami nilipelekwa Tabora kwa shangazi Helena, wajina wangu. Maisha yalibadilika kabisa, afya ikarejea ila umri wangu umekwenda.



    Mpaka sasa naisha Tabora, natamani siku moja niwe na mume wangu, nizae japo mtoto mmoja ambaye jina lake nitampa Ushindi'. Kitu kinachonisumbua ni umri wangu kwa maaana umekwenda. Hivi sasa nina umri wa miaka 43.



    KIFO CHA MZEE BALINABA

    Wiki tatu tangu maisha yangu yahamie Tabora, nilipokea taarifa kuwa mzee Balinaba anaumwa. Kwa kukumbushia, mzee Balinaba ndiye aliyenisababishia matatizo yote kutokana na tamaa yake ya kimapenzi kwangu na akanioa kwa nguvu.



    Baadaye kwa hisia kuwa namgeuka, alianza kunitesa mpaka maisha yangu yakabadilika kwa kiwango cha kutisha. Ndugu yangu, acha leo nijione mshindi na namshukuru Mungu na mama yangu kwa kunipigania.



    Nilikuwa kama mnyama, nimekula vitu vya ajabu. Nimefanya mapenzi na wanyama mbalimbali mpaka misukule. Leo hii nipo salama, kweli Mungu ni bingwa wa kila kitu na nitaendelea kulitaja jina lake kila siku na kila nukta.



    Mwezi mmoja baadaye, niliambiwa mzee Balinaba amekufa. Nasikia Sumbawanga ilikuwa sherehe badala ya vilio. Nami sikuona ajabu kwa maana watu wengi walimchukia kwa kitendo alichonifanyia pamoja na watu wengine.







    ''Mwisho.''


           

0 comments:

Post a Comment

Blog