Search This Blog

PENZI LA SHETANI - 3

 





    Simulizi : Penzi La Shetani

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ikiwa mida ya jioni, Nick huku akiwa ameambatana na mpenzi wake, anawasili THE GRAND BAR na kumkuta Mark akiwa amfika kitambo kidogo na kumsubiri.Kwa furaha kubwa, Mark akainuka pale alipokaa na kumkumbatia rafiki ya Nick ambaye wakipotezana muda mrefu, wakasalimiana na kuketi.

    "Naona mkubwa mambo yako sio mabaya, unazidi kunawiri tu.." Mark alimtania Nick kidogo na kupelekea wote kuangua kicheko.

    "Hamna rafiki yangu Mark, Mungu tu anamimina neema zake.Mark, naomba umfahamu shemeji yako huyu, anaitwa Angel." Alizungumza Nick na kumtambulisha mpenzi wake aitwaye Angel kwa rafiki yake Mark.

    "Nashukuru kumfahamu, ila hongera sana kaka naona umepata kifaa cha ukweli tena jina lake lenye kufanana na jina la Marehemu mama yangu."

    "Hahahahaha!, Mark unanifurahisha kweli, unataka kuniambia huyu anaweza kushindana na Sala"

    "Weeeee, Sala wangu ni dhahabu ile ambayo ni nadra sana kupatikana hapa duniani." yalikuwa maneno ya kutaniana kati ya Mark pamoja na rafiki yake Nick na kujikuta wote wakiangua kicheko mara kwa mara na kuyafurahia mazungumzo yale.

    "Ok Mark, nimeitikia wito wako, ulikuwa una shida gani rafiki?" Nick aluzungumza na kumuuliza Mark.Mark akashusha pumzi yake kwa nguvu na kumsimulia Nick juu ya yale yote yaliyotokea katika maisha ya kusoma kwake mpaka kufa kwa mdhamini wake mr.Harry.Mambo aliyoyasimulia Mark, yalimgusa Nick na kumuonea huruma sana rafiki yake.

    "Pole sana Mark kwa matatizo yote hayo yaliyokusibu, sasa je inahitajika shilingi ngapi ili uweze kurejea chuo kuendelea na masomo?"

    "Inahitajika milioni ishirini na tano ili niweze kurejea chuoni na ndio maana nimekuja kwako ili uweze kunisaidia katika hili." Kwa uchungu mkubwa, Mark alimueleza rafiki yake Nick.



    Akiwa amejituliza nyumbani huku mawazo yakiwa mengi kuhusiana na Mark na akiambatanisha na maneno aliyoelezwa na John kuwa Mark ana mwanamke mwingine ampendaye, Sala alizidi kuchanganyikiwa na kuwa katika hali ya huzuni muda wote.Mawazo yakizidi kuwa mengi juu ya hayo, mara simu yake ya mkononi Sala, inaingia meseji, Sala akaifungua meseji ile ili aweze kuisoma.

    "Hlw Sala, naomba fanya haraka njoo hapa THE GRAND BAR kuna kitu muhimu juu ya Mark.

    'By handsome John' ", Ilikuwa meseji ambayo ilitumwa na John ambayo aliisoma Sala.

    Meseji hii ya John, ilimshtua sana Sala, bila kuchelewa akajiandaa haraka kwa ajili ya kuelekea THE GRAND BAR ili akafahamu kitu hicho muhimu kinachohusiana na mpenzi wake Mark.



    " Napenda kukupa pole sana rafiki yangu Mark, hakika upo katika kipindi kigumu sana na kiukweli kwasasa mimi sina uwezi wa kukusaidia chochote kile kwasababu hali yangu ya kiuchumi sio nzuri kabisa." Alizungumza Nick na kumueleza Mark.Maneno haya ya Nick yalimfanya Mark kukata tamaa kabisa.

    "Oooh Nick!, wewe ndiye ninayekutegemea kuweza kunisaididia chochote katika hili, fanya kitu kaka ili unikomboe ndugu yako." Huku machozi yakichirizika mashavuni mwake na kwa uchungu mkubwa, Mark alizidi kumuomba rafiki yake Nick.hali ile aliyokuwa nayo Mark, ilmgusa na kumuumiza sana Nick na akaona jinsi gani Mark anavyootabika katika lile.

    "Ngoja nijaribu kitu kimoja, subiri kidogo nakuja." Alizungumza Nick na kutoka nje ya bar na kumuacha Mark pamoja na Angel pale mezani.Angel aliendelea kujitahidi kumtuliza Mark ambaye kwa muda huo alikuwa akilia sana pale alipokaa, akamtaka anyamaze na kumueleza maneno ya kumtia moyo na kumfariji katika lile.Ilikuwa ngumu sana Mark kukizuia kilio kile kutokana na uchungu mkubwa alionao.Angel akainuka alipokaa na kusogea karibu zaidi na alipokaa Mark, akamshika bega na kuendelea kumtuliza na kumueleza maneno ya kumpa faraja.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati hayo yakiendelea, mara Sala naye anawasili THE GRAND BAR, akamkuta John akiwa anamsubiri.John alitabasamu baada ya kumuona Sala.

    "John, embu nieleze ulichoniitia usiku huu, ni kitu gani hicho chenye umuhimu kinachomuhusu Mark!?" Kwa shauku kubwa ya kutaka kujua, Sala alimuuliza John.

    "Hahahaha!, Sala usiwe na haraka, naamini kwasasa utakiamini kile nilichokuwa nakwambia"

    "John, sikuja kupoteza muda hapa, kama bado unaendeleza ujinga wako, mimi naondoka zangu" Alizungumza Sala na kutaka kuondoka.

    "Subiri kidogo Sala, embu geuka pembeni na uangalie katika meza ile ya rangi nyeupe." John alizungumza na kumuonesha Sala meza aliyokuwa amekaa Sala pamoja na Angel ambaye ni mpenzi wa Nick.

    "What!!????, Mark..!!" Sala alishtuka sana kwa kile alichokiona pale.



    Sala akashindwa kuamini kabisa kama Mark wake anaweza kuyafanya yale anayoyashuhudia pale, alihisi kama yupo ndotoni.Uvumilivu ukawa mdogo kwa Sala, huku hasira ikiwa imemjaa, taratibu akaanza kupiga hatua na kuanza kusogea karibu na meza ile.Lile lilimshtua kidogo John, akatoka na kumuwahi Sala kwa lengo la kwenda kumzuia kabla hajafika kwenye meza.

    "Unataka kufanya nini Sala?, unafikiri ukishaenda pale nini kitatokea?, mimi nilihitaji kuthibitisha ukweli wangu kwako, tayari umeshathibitisha kile nilichokueleza na sasa naomba urudi nyumbani ukapumzike." Alizungumza John huku akiwa amemzuia njia Sala ya kusogea mahali alipokaa Mark.

    "John, siwezi kuamini kama Mark amekuwa mkatili namna hii kwangu, naomba unipishe nikazungumze nae na ikibidi nim....", Alizungumza Sala, lakini alishindwa kuendelea kuongea kutokana uchungu mkubwa kumjaa na kuanza kulia.John akamchukua Sala na kutoka nae nje, akampakiza kwenye gari yake na kumrudisha nyumbani.



    " Haina haja ya kuhuzunika sana shem, natumaini Mungu ataonesha njia katika hili" yalikuwa maneno ya Angel, akimueleza Mark kwa ajili ya kumpa matumaini.Baada ya muda, Nick naye akarejea na kujumuika tena kwenye meza.

    "Nambie Nick, kuna lolote ulilofanikiwa?" Mark alimuuliza Nick.

    "Nasikitika Mark, hata kwa mtu ambaye nilijaribu kwenda kuwasilina nae na kudhani pengine angetupa msaada wowote katika hili, nako imekuwa ngumu kusaidiwa." Alizungumza Nick na kumueleza Mark.Maneno haya ya Nick yalizidi kumkatisha tamaa Mark.

    "Lakini Mark, ningependa kukushauri kitu kimoja rafiki yangu"

    "Kipi hicho tena Nick maana naona kama nimeshapoteza dira katika maisha yangu."

    "Embu naomba fikiria kufanya jambo lingine tofauti na kusoma kwasababu naamini zipo njia nyingi za kufanikiwa kimaisha tofauti na kusoma." Alizungumza Nick na kumueleza Mark.

    "Unafikiri naweza nikafanya nini Nick bila ya kusoma mimi?"

    "Mark, nitakutafuta siku nyingine ili tuongee vizuri, kwasasa naomba niwahi kwasababu kuna mahali kidogo naelekea na shemeji yako." Alizungumza Nick, kisha wakaagana na Mark na kuondoka.



    " Ee Mungu, kosa gani nililotenda mbele yako mbona unaniadhibu namna hii mimi mja wako?, Au pengine mimi sikustahili kuwepo katika dunia hii, kwanini baba usinichukue ili nami nikaungane na mama yangu huko alipo?" Yalikuwa maneno ya masikitiko kutoka kinywani kwa Mark huku macho yake akiwa ameyaelekeza kutazama katika anga.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kutoka kuonana na Nick, Mark akaona ni heri apitie kwenda kuonana na kipenzi cha moyo wake Sala, kabla ya kwenda nyumbani.Mark alifika na kumkuta Sala nyumbani, lakini alishangaa sana kumuona Sala akiwa yuko tofauti sana siku hii.Alimsalimia lakini Sala hakujibu salamu yake badala yake akasonya.

    "Sala, mbona nakusalimia lakini hujibu salamu yangu, vipi kuna tatizo kwani!?' Aliuliza Mark.

    " Shetani mkubwa weeee, tena kahaba wa kiume mwenye laana kutoka kwa wazazi wako, unafikiri kuna siri tena, kila kitu kiko wazi sasa" yalikuwa maneno mazito sana kutoka kinywani kwa Sala ambayo yalimshangaza na kumstaajabisha sana Mark.

    "Sala!,Sala.!?, nini tatizo mbona unanitamkia maneno mazito kama hayo."

    " unafiikiri mimi naweza nikaongozana na wewe tena Mark, mwanakulaaniwa wewe, naomba kuanzia sasa tusijuane na iwe mwanzo na mwisho kufika hapa nyumbani kwangu, shwetani mkubwa wee" Kwa ujasiri mkubwa, Sala alimueleza Mark.

    "Sala, naomba utulie kwanza na unipe nafasi ya kukueleza matatizo yaliyonisibu, mbona unanihukumu namna hiyo!?"

    "Yule uliyekuwa nae, anatosha kuyatambua matatizo yako, Mark naomba toka nje ya nyumba yangu na uondoke sasa." Alizungumza Sala, huku akimsukuma Mark kutoka nje.

    "Lakini Sala nini kimekupata, mbona nashindwa kukuelewa."

    "Mark nimesema sikuhitaji, tokaaaa..!!" Kwa sauti ya ukali alizungumza Sala na kumsukuma kwa nguvu Mark mpaka nje.Katika msukumo ule wa Sala, ulimpelekea Mark kudondoka na kupigiza kichwa chake chini vibaya, taratibu fahamu zikaanza kumpotea pale chini alipolala, na mwisho akapoteza fahamu jumla.Sala aliingiwa wasiwasi kidogo, alihisi pengine ameshau, alijaribu kumuita na kumuamsha Mark lakini Mark alionekana kuwa kimya.



    Baada ya masaa mawili, taratibu Mark fahamu zikaanza kumrejea na kufanikiwa kuweza kufumbua macho yake.Baada ya kufumbua macho, Mark akayaona mazingira ya tofuti sana, bendeji kubwa ikiwa imezungushwa kichwani mwake, huku akiwa amelala kitandani na dripu ya maji ikiwa imeunganishwa mwilini mwake, Mark alizidi kushangaa na kujiuliza aliwezaji kufika mahali pale.Akiwa katika hali hiyo, mara anaingia dokta na kusogea karibu na kitanda alicholala na kumsemesha.

    "Kwasasa unajionaje kijana?" Aliuliza dokta.

    "Samahani dokta, nimewezaje mimi kufika hapa!?" Aliuliza Mark.

    "Uliletwa hapa ukiwa umepoteza fahama baada ya kuanguka chini, lakini usijali maana hali yako itakuwa sawa muda si mrefu kwasababu aliwaishwa hapa hospitali" Alizungumza dokta.Baada ya dokta kuongea maneno hayo ndipo Mark naye kumbukumbu zikapata kumrejea na kumkumbuka Sala.

    "Vipi kuhusu Sala!?, tafadhali dokta naomba unieleze, yuko wapi Sala mbona simuoni mahali hapa.!?" Aliuliza Mark huku hofu kubwa ikiwa imemjaa juu ya Sala.Kabla dokta hajajibu chochote, ghafla Sala naye akawa anaingia mahali pale huku mkononi mwake akiwa amefungwa pingu na akiwa ameambatana na maaskari.Mark alshtuka sana na kuzidi kupata hofu baada ya kumuona Sala akiwa katika hali ile.Maaskari walifika karibu na kitanda na kuhitaji kuzungumza na Mark.

    "Sisi ni maafisa wa jeshi la polisi, nahitaji kupata maelezo kutoka kwako Mark kuhusu tukio zima lilivyotokea." Alizungumza askari mmoja.Mark aliinua macho yake na kumtazama Sala, aliona jinsi gana alivyokuwa mnyonge na kuwa katika hali ya huzuni sana.

    "Ililkuwa ni ajali tu, kwa bahati mbaya niliteleza na kupigiza kichwa changu chini lakini binti huyu mliyemkamata hausiki kwa lolote." Yalikuwa maelezo kutoka kwa Mark na kumueleza askari yule.Maelezo aliyoyatoa Mark, yalimshangaza sana Sala na kutoamini kama Mark ametoa maelezo kama yale kwa maofisa wale wa polisi.

    "Una uhakika kijana na unachosema!?"

    "Nina uhakika muheshimiwa." Kwa msisitizo mkubwa Mark alijibu na kupewa karatasi ili aweze kuthibitisha kwa maandishi kile alichokisema.Baada ya Mark kutoa uthibitisho ule, Sala akafunguliwa pingu na kuachiwa, kisha maafisa wale wa jeshi la polisi wakatoka na kuondoka.



    Baada ya muda kidogo, Mark akaweza kuruhusiwa ili aweze kurudu nyumbani.Akiwa anatoka nje ya hospitali, Mark akashangaa kumkuta Sala nje ya hospitali akiwa anamsubiri.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    " Sala, usiku umeshakuwa mkubwa sasa, kwanini bado upo hapa hospitali!?" Mark alimuuliza Sala.

    "Kusubiri kwangu kote huku, nilikuwa nakusubiri wewe Mark kwasababu kuna kitu nahitaji kukueleza"

    "Sawa, unaweza ukazungumza mimi nakusikiliza Sala." Alijibu Mark.

    "Haijalishi hata kama umenisaidia kunitoa mikononi mwa maaskari, ila kwasasa sitahitaji kuongozana nawe tena wala kushirikiana na chochote kile." Sala alizungumza na kuonesha msimamo wake.Mark alitabasamu na kumtazama Sala usoni.

    "Ondoa shaka Sala, sihitaji uzidi kuumia na kuendelea kulia tena kwa ajili yangu, nakuahidi kwa sasa nitakaa mbali nawe na wala sitokusumbua tena na nakutakia maisha mema sana" huku moyoni mwake kukiwa na maumivu makubwa, Mark alimueleza Sala na taratibu akageuka na kuanza kuondoka.Sala naye kwa kiasi fulani aliumia sana moyoni mwake na kutoamini kama ule ndio ulikuwa mwisho wao kati yake na Mark, lakini mwisho akaona ni bora ikawa hivi kuliko kuendelea kuutesa moyo wake.

    Mark alirudi nyumbani huku akiumia sana moyoni mwake kwa yale yaliyotokea kati yake na binti yule ambaye alitokea kumpenda sana katika maisha yake.Mambo mengi alizidi kuyakumbuka aliyoyafanya akiwa pamoja na Sala, Mark alishindwa kuamini kama uhusiano wao umevunjika mithili ya jani kudondoka mtini, alizidi kuiona dunia chungu na kujiona ni mtu asiyekuwa na thamani yoyote ya kuishi, Kilio pekee ndio kilikuwa kama kinanda chake alichokiona kinachoweza kumtuliza na kupunguza machungu na maumivu yale makali anayoyapata.Akiwa katika hali hiyo ya huzuni na majonzi sana Mark, ghafla simu yake inaingia meseji kutoka hospitali ambayo alikuwa analelewa baba yake mzee Peter katika kituo maalumu kwa muda mrefu sasa.

    "Mark, tunaomba asubui ya kesho ufike hapa hospitali kuna taarifa muhimu uje kuzichukua zinazohusiana na baba." Ulikuwa ujumbe mfupi ambao ulitumwa kwenye simu ya Mark.

    Yakiwa majira ya asubui, Mark akawasili hospitilani kwa ajili ya kuonana na dokta kama alivyopata maelekezo kupitia ujumbe aliotumiwa.

    "Karibu Mark na pia asante kwa kufika hapa." Dokta alimkaribisha Mark.

    "Asante dokta, nimeitika wito wako"

    "Mark nimekuita hapa, kwa ajili ya kukupa taarifa ambazo nilishindwa kukueleza kwenye simu" Alizungumza dokta na kumueleza Mark.



    Akiwa chuoni Sala, bado fikra zake zilikuwa ngumu sana kumsahau Mark, kila alichokifanya kilikuwa kinamkumbusha alipokuwa karibu na Mark.Akiwa katika hali hiyo Sala, mara anatokea john na kujisogeza pale alipokaa.

    "Sala!, Sala!, Sala....!"

    "Mh!,ndio...ndio...ndio Mark!"

    "No, mimi ni John Sala, nimeita jina lako zaidi ya mara tatu, lakini inaonekana uko mbali sana kimawazo, nini tatizo!?" John alimuuliza Sala.

    "Hapana John, unajua jana Mark amefanya jambo ambalo limenishangaza sana."

    "Jambo gani hilo Sala!?" Aliuliza John.

    "Baada ya mimi kukamatwa na maaskari, alipokwenda kuulizwa Mark pale hospitalini alipolazwa kama mimi nahusika katika kuumia kwake, lakini yeye alikanusha na kueleza uongo kwa maaskari mbele yangu." Huku machozi yakimdondoka, Sala alizungumza na kumeleza John.

    "Haina haja ya wewe kulia wala kuhuzunika Sala na usifikiri kuwa Mark amefanya vile kwasababu anakupenda, mimi namjua Mark vizuri na amefanya hivyo kuficha aibu yake kwako kwa mambo aliyokufanyia." Alizungumza John na kumkumbatia Sala kwa lengo la kumtuliza na kumtaka aachane na mawazo yote anayofikiri kuhusiana na Mark.



    "Mark, napenda kukutaarifu kuwa, usiku wa leo tumempoteza mzee Peter kutokana na maradhi ambayo yamemsumbua kwa muda mrefu sasa." Dokta alimtaarifu Mark kuhusiana na kifo cha baba yake mzee Peter.Hili lilikuwa ni pigo lingine kwa Mark, akaona kama ni ndoto kwa lile alilolisikia kutoka kwa dokta, lakini ndio ulikuwa ukweli halisi kuwa tayari ameshampoteza baba yake katika dunia hii.Huzuni ikawa juu ya huzuni kwa Mark, lakini alikuwa hana jinsi zaidi ua kukubaliana na lile lilitokea zaidi ni kufanya maandalizi tu kwa ajili ya kumpumzisha marehemu baba yake.

    Baada ya kupumzisha mwili wa marehemu baba yake, Mark hakuona sababu ya kuendelea kuishi katika mji huu tena maana aliona mkononi mwake tayari ameshapoteza kila kitu kilichokuwa chenye umuhimu kwake, hivyo Mark akaamua kufunga safari na kwenda kuanzisha maisha yake upya katika mji mwingine.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Taarifa za kuondoka kwa Mark, zilimuumiza na kumsikitisha sana Sala kwasababu hakutegemea kama Mark angeweza kuchukua maamuzi kama yale.

    "John, kwanini Mark ameondoka hata bila kuniaga?,Je vipi kuhusu chuo au amechukua na uamisho pia!?, sikutarajia kama angekuja kubadilika na kuja kuwa mtu mmbaya namna hii." Sala alimueleza John, ambapo kwa wakati huo walikua mapumziko kidogo pale chuoni.

    "Mark ni mtu wa ajabu sana Sala na hii yote inatokana kwasababu ulishindwa kumtambua mapema, lakini ondoa hofu hata kama yeye ameondoka hakuna chochote kilichoharibika kwakuwa mimi nipo hapa." Kwa sauti ya taratibu, alizungumza John.

    Ilikuwa ngumu kidogo kwa Sala kumsahau Mark mapema, lakini kutokana na uwepo wa John na mabaya yote ya Mark aliyokuwa akielezwa na John, kadri siku zilivyozidi kusogea taratibu Mark akaanza kusahaulika katika fikra za Sala.







    Muda mrefu ulipita tangu Mark aamue kuama katika mji wa Dar es salaam na kwenda kuanzisha maisha yake upya katika mji wa Morogoro.Baada ya kufika katika mkoa wa Morogoro, Mark alijitahidi kuangaika sana kutafuta ajira sehemu mbalimbali na mwisho alifanikiwa kuajiriwa katika kampuni moja ya mawasiliano na akiajiliwa katika kitengo cha masoko na mawasiliano.Japo mshahara ulikuwa mdogo sana kutokana na elimu aliyokuwa nayo, lakini Mark hakusita kumshukuru Mungu hata kwa kile alichomjalia akiamini ipo siku itafika nae atakuja kukamilisha ndoto zake.Juhudi yake katika kazi ilikuwa kubwa sana na tangu Mark ajiiriwe katika kampuni ile, Jina la kampuni lilizidi kukua kwasababu ya ufanisi mkubwa aliokuwa nao Mark. Mabosi pamoja na baadhi ya wafanyakazi walimsifu sana Mark kwa utendaji wake mzuri wa kazi na kujitahidi kuleta mabadiliko makubwa ndani ya kampuni.Pamoja na yote hayo, kama waswahili wanavyosema kuwa 'mti wenye matunda ndio hupigwa mawe', licha ya Mark kuonesha uwezo wake mkubwa katika kazi na kujizolea sifa nyingi kwenye kampuni, lakini baadhi ya wafanyakazi walichukizwa sana na lile na kujaribu kuandaa mipango kwa ajili ya kuweza kumuangusha pale ofisini kwasababu Mark alikuwa ni mmoja ya watu wanaoziba mianya yao ya kujipatia pesa.Changamoto zilikuwa nyingi sana kwa Mark hasa zaidi pale ofisini, lakini Mark hakuyajali yale zaidi aliendelea kufanya kazi zake kwa juhudi kubwa na kuchukulia yale yote anayokutana nayo ni moja ya sehemu ya maisha ambayo binadamu yeyote anaweza kukutana nazo.

    Mara nyingi ifikapo mida ya jioni na baada ya kumaliza mihangaiko ya siku nzima, Mark pamoja na baadhi ya rafiki zake hupendelea kutafuta sehemu moja na kupumzisha akili yao kwa kupiga stori nyingi huku wakipooza makoo yao kwa vinywaji mbalimbali.

    Ikiwa jioni moja, Mark akiwa pamoja na marafiki zake ambao wanafanya kazi ofisi moja, David na Charles, waliendelea kupiga stori nyingi na kupata vinywaji kwa pamoja katika bar ya THE GARDEN BAR iliyopo maeneo ya Bima.

    "Siku zote kila tunapokutana mahali hapa, stori zetu zimekuwa zinahusiana zaidi na majukumu yetu ya kikazi, embu leo marafiki tubadilishe kidogo na mzungumzo yetu yawe zaidi ya kimaisha" Alizungumza David na kuwaeleza marafiki zake.

    "Kabisa David, sambamba na hilo pia napenda kuwakaribisha katika harusi yangu ambayo natarajia kufunga ndoa wiki ijayo." Alizungumza Charles ambaye kwa kiasi fulani bado alikuwa mgeni katika kazi kwasababu alikuwa bado hajamaliza hata mwezi tangu kuajiliwa kwake pale ofisini.

    "Ooh!, hongera sana rafiki na pia karibu sana katika timu yetu ya wanandoa.Mark timu yako ya ukapela inazidi kupukutika tu na mwisho unabaki peke yako sasa."

    "Hapana David, mwaka huu hautaisha bila ya mimi kufunga ndoa na ikishindikana kabisa nitakuja kuomba mke hata kwenu" Alizungumza Mark na kupelekea wote kuangua kicheko.

    Yalikuwa ni mazungumzo yaliyojaa utani na mzaha sana baina ya marafiki hawa watatu na mara kwa mara wote walikuwa wakiangua kicheko na kuendelea kuyafurahia mazungumzo yale.



    *****************************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "John, ni muda mrefu sasa umepita tangu tuwe pamoja lakini bado hujanieleza hatma ya mapenzi yetu.kidoleni mwangu nami natamani kuwa na pete ya ndoa, kama hutojali John naomba unioe mapema iwezekanavyo." Alizungumza Sala na kumueleza John ambaye kwa sasa tayari walishafungua ukurasa wa mapenzi baina yao.

    "Salama!Salama!Sala...!!, Ondoa hofu mpenzi wangu Sala, ndoa tutafunga tu lakini subiri kidogo kuna mambo niyakamilishe kwanza." Alizungumza John.

    "John, unanipenda mimi!?"

    "Hilo sio swali bali ndio jibu lake mpenzi wangu Sala"

    "Basi naomba tufunge ndoa haraka iwezekanavyo" Huku akionekana kuwa na hasira kiasi fulani, Sala alizungumza na kumueleza John.John hakujibu wala kuzungumza chochote, almtazama Sala huku akionekana kukasirishwa sana na suala lile alilozungumza Salama au Sala, John akasimama na kuondoka.Sala alijitahidi kumuita John, lakini John hakuitika wala kumpa jibu lolote Sala na badala yake akaamua kuwasha gari na kuondoka.Jambo lile lilipelekea kumpa wasiwasi mkubwa Sala na kuzidi kujiuliza, kwanini kila anampogusia John kuhusu swala la ndoa yao anakuwa mkali na kuwa katika hali hasira sana.



    ****************************



    Baada ya kuzungumza na kupiga stori nyingi sana, usiku nao ulizidi kuingia, David pamoja na Charles waliagana na Mark na kuondoka.Mark, yeye halikuwa haishi mbali na THE GARDEN BAR, hivyo muda mwingi hupenda kuutumia akiwa mahali pale na kuendelea kutafakari mambo mengi yanayohusiana na maisha yake.Kitendo cha marafiki zake kuzungumzia suala la ndoa, lilimfanya Mark siku hii kumkumbuka sana Sala.Mark alitamani sana siku moja baada ya kumulaza masomo yao chuo, Sala aweze kuja kuwa mke wake ili waweze kuanzisha familia yao pamoja, lakini kwasasa yote yalikuwa yamebaki kama ndoto tu kwake na kujiona mtu aliyepoteza sana katika suala la mapenzi.Alikumbuka mambo mengi sana Mark aliyoyafanya akiwa pamoja na Sala, kama vile tabu, shida na matatizo mbalimbali waliyopitia kwa pamoja yeye na Sala tangu angali wakiwa wadogo, uchungu mkubwa ulizidi kumjaa Mark.Moyoni mwake Mark alizidi kuumia na kuhuzunika sana huku akijiuliza, kwanini Sala alimkatili namna ile na kumfanya awe na kidonda kikubwa moyoni mwake ambacho kimekuwa kigumu kupona na kumfanya awe na maumivu makali sana kila anapomkumbuka.

    Kumbukumbu hizi za kumkumbuka Sala, zilimfanya Mark kudondosha chozi na kujutia sana kwanini aliamua kumuingiza moyoni mwake mwanamke ambaye alishindwa kutambua thamani yake na upendo mkubwa aliokuwa akimuonesha.Akiwa katika hali hiyo ya huzuni huku kilio cha uchungu kikiwa kimemtawala Mark, mara anatokea mtu nyuma yake na kumshika bega lake la mkono wa kushoto huku akimbembeleza na kumtaka anyamaze.





    "Pole sana kaka, naona upo kwenye maumivu makali ambayo imekuwa vigumu kuyazuia." yalikuwa maneno kutoka kwa mtu yule akimueleza Mark pale alipokaa.Sauti hii iliweza kupenya vilivyo katika masikio ya Mark, Mark akageuka ili aweze kumtambua mtu aliyezungumza maneno haya, akastaajabu kumuona mdada ambaye alikuwa mrembo mno, sura yake ya mviringo na mwenye umbo zuri sana la kuvtia akimbembeleza na kumtaka anyamaze.Mark alibaki ameduwaa na kushangaa sana.

    "Mbona unanishaangaa sana!, vipi naweza nikajiunga katika meza yako!?"

    "Ka..ka!.karibu, unaweza ukakaa tu" Huku akiwa na kigugumizi cha ghafla, Mark akamkaribisha aweze kuketi mrembo yule.

    "Ningependa tufahimiane, mimi naitwa Jane, sijui mwenzangu unaitwa nani?" Alijitambulisha jina lake yule dada na kumuuliza Mark.

    "Naitwa Mark na pia karibu sana."

    "Asante Mark, niliona mpweke sana pale nilipokaa, hivyo nikaona naweza nikajiunga nawe hapa angalau niweze kupata mtu wa kupiga nae stori."

    "Ooh!, Hata mimi nashukuru kwa kupata mtu wakuweza kubadilishana nae mawazo." Alizungumza Mark na kumkaribisha Jane mahali pale.

    "muda mwingi wakati nimekaa katika meza yangu, nilikuwa nakutazama na nikakuona uko katika hali ya huzuni na mawazo sana mpaka nikahisi moyo wangu kuumia sana, inaelekea kuna jambo zito sana limekusibu" Alizungumza Jane na kumueleza Mark.Mark alimtazama sana Jane, hakika alikuwa binti mrembo na mwenye kupendeza sana, Mark akatabasamu kwa ajili ya kuficha hali aliyokuwa nayo.

    "Hapana Jane, labda ulikuwa unaangalia vibaya, mimi niko poa kabisa ila nilikosa kampani tu maana rafiki zangu niliokuwa nao wameshaondoka."

    "Mh!, yan mkaka mzuri namna hiyo halafu unakuwa muongo, kama uko sawa mbona macho yako yalikuwa yakidondosha machozi."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Hahahaha!, unanifurahisha sana Jane, hivi unafikiri kila chozi linalodondoka huwa la huzuni?" Mark alifurahi na kumuuliza Jane.

    "Mh!, sina uhakika katika hilo, maana siwezi kutofautisha kati ya chozi la furaha na huzuni, labda nifungue hapo kidogo" Kwa sauti ya taratibu, Jane akamueleza Mark.

    "Hapo pana ugumu kidogo Jane, lakini ningependa kukutambua zaidi, mimi naishi hapa Morogoro na ni mfanyakazi katika kampuni moja ya mawasiliano."

    "Oooh, mimi ni mgeni katika mji huu, nimefurahi kukutana na wewe Mark hakika ni kijana mwelevu sana." Alizungumza Jane huku mcho yake yakiwa yanamtazama Mark.Licha ya uzuri aliokuwa pia Jane alikuwa binti mcheshi sana.Mark alizidi kumtazama Jane, hakika moyoni mwake akahisi kufarijika sana kutokana na uchangamfu mkubwa alikowa nao mrembo yule, kwa muda mfupi tu walioweza kukaa pamoja, Mark akajikuta akisahau shida, matatizo pamoja na mawazo yake yote yaliyokuwa yanamsumbua kwa wakati ule na kujiona yupo katika dunia nyingine kabisa.

    Mark alitumia muda mwingi sana kukaa pamoja na Jane, huku wakendelea kubadilishana mawazo na kupata kinywaji pamoja japo ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kukutana.

    "Jane, kwasasa umeshakuwa usiku mkubwa, sasa nahitaji kwenda kupumzika maana nikichelewa ofisini kesho nitakuja kupigwa na bosi."

    "Hahahahaha!, 'Mark, your so funny...!!', nakushukuru sana Mark kwa kampani yako kubwa uliyonipa usiku huu, nimejikuta moyo wangu ukifarijika sana baada ya kukutana na wewe, nina imani nimepata mwemyeji bora sana.

    "Ondoa shaka Jane, nami nimefurahi sana kukutana na malaika kama wewe, maana umenifanya siku ya leo kujihisi niko tofauti sana." Mark alizungumza na kutania kidogo na kepelekea wote kuangua kicheko.Wakapeana mawasiliano, kisha Mark akamuaga Jane na kuondoka.



    Wakati mgumu sana alikuwa na Sala, hususani kuhusu mpenzi wake John.John alionekana kubadilika sana, ulevi na dharau kubwa ilimjaa na kushindwa kumthamini kabisa Sala.

    Ikiwa mida ya saa sita usiku, Sala alishindwa kulala kabisa kutokana na mawazo mengi aliyokuwa nayo juu ya mpenzi wake john ambaye mpaka muda huo alikuwa bado hajarudi nyumbani.Akiwa yupo katika msongo mkubwa wa mawazo, mara John nae anawasili nyumbani huku akionekana akiwa amelewa mno.Sala aliumia sana na kushindwa kuelewa kwanini John wake amebadikika kupita kiasi.

    "John, kwanini unanifanyia hivi?, mbona kila siku umekuwa mtu kunitesa na kuniumiza sana moyoni mwangu!?, embu nieleze, kosa gani nimetenda kwako mpaka kufikia kunipa adhabu zote hizi!?", kwa uchungu mkubwa, Sala alimueleza John.John hakuzungumza wala kumjibu chochote kile, badala yake akaanza kumpiga na kumuadhibu vikali Sala bila ya sababu yoyote ile.Yote haya John aliyafanya kutokana na kadri pombe ilivyokuwa inamtuma kufanya.

    Kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa Sala, moyo wake ulikuwa hauna amani kabisa na kujikuta muda wote yupo kwenye dimbwi la mawazo na maumivu makali sana.Alijikuta akikumbuka mengi sana yaliyomtokea katika maisha yake, Sla alizidi kumuomba Mungu, ili aweze kumsaidia katika tabu zote zile azipatazo na kumsaidia John wake.





    Akiwa ofisini Mark, muda mwingi fikra zake zilikuwa zikumuwaza Jane na akijikuta akipoteza umakini kabisa katika kazi zake.Akainua simu yake ya mkononi na kutafuta namba ya mrembo yule, ili angalau aweze kusikia hata sauti yake na moyo wake upate kufarijika, lakini namba yake ilikuwa haipatikani.Mark alijaribu tena na zaidi kupiga namba ile, lakini bado simu ya Jane ilikuwa haipatikani.Akahisi pengine amekosea kuiandika namba ile, lakini alipohakikisha kupitia kadi ya mawasiliano aliyopewa na Jane, namba ile ilikuwa ipo sawa.Hofu na wasiwasi mkubwa ukaanza kumjaa Mark, mpaka mwenyewe akaanza kujishangaa na kujiuliza sana, kwanini anakuwa na hofu na wasiwasi mkubwa kwa binti ambaye alikutana nae mara moja.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kila alichokuwa akikifanya pale ofisini, kilikuwa hakiendi sawa maana fikra zake zote zilikuwa juu ya Jane.Hofu ikazidi kumjaa Mark na kuendelea kujiuliza maswali mengi kuhusiana na mrembo yule.

    "Mbona hapatakani, atakuwa amepata tatizo nini?, au pengine alikosea kunipa namba?,Hapana mrembo kama yule hawezi kuniongopea, kwa gharama yoyote ile lazima nimtafute popote kule alipo." Baadhi ya maswali ambayo aliendelea kujiuliza Mark na kujipa matumaini ya kuonana na Jane kwa mara nyingine.

    Mida ya jioni ilipowadia, kama ilivyo kawaida yao, baada ya kumaliza majukumu yao ya kikazi, Mark pamoja na rafiki zake wakafika THE GARDEN BAR kwa ajili ya kuzungumza mambo yao na kupooza makoo yao kwa vinywaji mbalimbali vipatikanavyo katika baa ile.Siku hii Mark alionekana kuwa tofauti sana mpaka baadhi ya rafiki zake wakamshangaa, muda wote Mark alikuwa akimuwaza Jane huku akiangaza huku na kule pale baa, akihisi pengine ataweza kumuona Jane mahali pale.

    "Mark!Mark!Mark...!!?" Aliita David.

    "Nam!,ndi..o..!, Ndio Charles!" Alijibu Mark

    "No, mimi ni David, mbona leo upo tofauti sana Mark, vipi kuna lolote linalokusumbua!?" aliuliza David

    "Hapana David, mimi niko sawa tu rafiki yangu, hakuna jambo lolote linalonisumbua." Alijibu Mark huku akikamata kinywaji chake na kuendelea kunywa.

    "Sawa Mark, ila kama kuna lolote unaweza kutushirikisha maana sisi ni zaidi ya ndugu kwako"

    "Msijali marafiki zangu, mimi nipo sawa kama kuna lolote linalonisumbua, lazima ningewaeleza tu"

    "Poa, ila sisi sio wakaaji sana hapa, maana nampeleka Charles kwenda kununua suti yake ya harusi."

    "Sawa, mimi bado nipo kidogo, mpaka mida mida hivi, nami niweze kujisogeza nyumbani."

    "Poa, kesho tutawasiliana" alijibu David, kisha wakaagana na Mark na kuondoka yeye pamoja na Charles.

    Baada ya kuondoka David na Charles, Mark akainua simu yake kwa mara nyingine na kujaribu kumtafuta Jane kama anaweza kumpata, lakini bado simu ya Jane ilikuwa haipatikani.Mark aliendelea kukaa na kusubiri kwa muda mrefu kama anaweza akamuoa Jane, lakini Jane hakuonekana kuwepo wala kufika mahali pale.Baada ya kusubiri kwa kitambo sana bila mafanikio, taratibu Mark akaanza safari na kurejea nyumbani kwa ajili ya kupumzika huku moyo wake ukiumia sana kwa kushindwa kuonana na mrembo yule.



    " Najutia sana kwa kukuingiza katika tabu na shida zote hizi uzipatazo, naomba unisamehe, unisamehe sana Sala ili nami nipate nafasi ya kuponyesha majeraha yako ambayo yamekupa maumivu makali na kukutesa kwa muda mrefu sasa" Huku akiwa amepiga magoti mbele ya Sala, John alizumgumza maneno haya na kumuomba msamaha mpenzi wake kwa mambo yote mabaya aliyomfanyia.Sala alibaki ameshangaa na kushindwa kuamini kama ni kweli John amepata kujirudi na kutambua makosa yake.John aliendelea kulia na kuzidi kumuomba msamaha Sala kwa yale yote ambayo alipata kumtendeea.Huruma ikamuingia Sala, na akaona jinsi gani John anavyopata kujutia makosa yake, akamuinua pale chini na kumkumbatia.

    "Siku zote nilikuwa nasali, ili John wangu apate kurudi kama zamani, nashukuru sana John kwa kulitambua hili." Alizungumza Sala na kumueleza John.



    Mawazi yalikuwa mengi sana kwa Mark, hususani akiwaza ni wapi ataweza kukutana na kuonana na Jane kwa mara nyingine.Moyo wake ulizidi kuteseka kwa kukosa kumuona Jane.

    Ikiwa ni siku ya pili, majira ya asubui na mapema, Mark akawasili ofisini kwa ajili ya kuendelea na majukumu yake ya kikazi, lakini kabla hajaanza kufanya chochote kile, mara anapokea simu na kuhitajika ofisi kuu.Bila kuchelewa Mark akainuka na kwenda kuusikiliza wito ule.Baada ya kufika ofisi kuu, Mark akasalimiana na bosi wake na kukaribishwa aweze kuketi, Mark akaketi na kusikiliza alichoitiwa na bosi wake.Baada ya kusalimiana, bosi akatoa bahasha na kumkabidhi Mark.Mark alshtuka na kupata hofu, na kushindwa kuelewa bahasha ile aliyopewa na bosi wake ilikuwa inahusiana na kitu gani.





    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kutokana na utendaji wako mzuri wa kazi uliokuwa nao tangu ujiunge na kampuni yetu, Kampuni imeamua kukupandisha cheo na sasa utakuwa meneja katika kitengo chako cha masoko na mawasiliano." Alizungumza bosi na kumtaarifu Mark.Taarifa hii ilimfurahisha na kumpa faraja sana Mark, alishindwa kuamini kama ameweza kuaminika na kukakibidhiwa cheo kikubwa kama kile kwa muda mfupi alikaa tangu aweze kujiunga na kampuni ile.Alimshukuru bosi wake na kumuahidi atakuwa mwadilifu kwa nafasi ile aliyopewa na atajitahidi kwa nguvu zake zote ili aweze kuisaidia kampuni kusonga mbele zaidi ya pale.

    Alirudi ofisini Mark huku moyoni mwake akiwa na furaha mno, baadhi ya wafanyakazi wakiwemo rafiki zake wa karibu pale ofisini, Charles na David, walikuja kumpongeza na kumtakia mafanikio mema katika majukumu yake mapya aliyokabidhiwa.

    "Hongera sana rafiki yangu kwa nafasi hiyo kubwa uliyokabidhiwa, naamini moja ya ndoto zako ulizokuwa unatueleza, sasa unaenda kuzikamilisha." Alizungumza David na kumpongeza Mark.

    "Asanteni nyote marafiki, yote haya naamini yametokana na ushirikiano mkubwa uliyopo kati yetu, hivyo naomba tuzidi kuwa na umoja na mshikamano zaidi ya hapa ili kampuni yetu izidi kuendelea." Mark aliwashukuru wote kwa pongezi zao.

    "Kuna kitu kimoja sasa kilichobaki kwako Mark" Aliuliza Charles.

    "Kitu gani tena Charles!?"

    "Kwa nafasi uliuokuwa nayo hiyo ni lazima uwe na ubavu wa pili ili uweze kufanikiwa zaidi."

    "Hahahaha!, nimeshakuelewa Charles, ondoa shaka, baada ya wewe kumaliza na mimi nitafuata." Mark alifurahi maana alishatambua anachokimaanisha Charles.

    Alizidi kupokea pongezi nyingi Mark, kutoka kwa watu mbalimbali pale ofisini maana taarifa ile ya yeye kupandishwa cheo, tayari ilishawafikia karibu wafanyakazi wote wa kampuni.

    Japokuwa ile ilikuwa habari njema na iliyoweza kumpa faraja kiasi fulani ndani ya moyo wake, lakini Mark bado fikra zake ziliendelea kumuwaza Jane, muda wote simu yake ilikuwa karibu nae na akiendelea kusubiri kama anaweza kupigiwa na mrembo yule ambaye ametokea kuziteka fahamu zake ghafla mpaka kushindwa kujielewa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog