Search This Blog

PENZI LA SHETANI - 4

 





    Simulizi : Penzi La Shetani

    Sehemu Ya Nne (4)





    Siku tatu zilipita bila ya Mark kuweza kuwasilianana na Jane wala kumuona binti yule, Mark, tayari alishakata tamaa na kuhisi ile haikuwa bahati yake ya kuweza kuwa karibu na Jane, hivyo Mark akaona ni heri akajikita zaidi katika majukumu yake ya kikazi kuliko kupoteza muda wake mwingi, kukifikiria kitu ambacho hana matumaini nacho.

    Ikiwa mida ya jioni, Mark akiwa ofisini huku akiendelea na majukumu yake mapya ya kikazi, mara simu yake ya mkononi inaita.Mark akachukua simu yake na kutazama namba ya mpigaji wa simu ile, alishangaa kuona namba ile ilikuwa ngeni kwake, tena isiyoanza na kodi ya +225 ambayo hutumika katika namba za mitandao yote nchini Tanzania.Mark akapokea simu ile na kuweka sikioni ili aweze kuongea na mpigaji.

    "Hallow!"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "'Hallooooow!", naongea na Mark?"

    "Ndio, Mark hapa,nani mwenzangu na unapiga simu kutokea wapi!?" Aliuliza Mark na aliweza kugundua mpigaji wa simu ile alikuwa msichana kupitia sauti yake aliyoisikia.

    "Hahahahahah!, Oooh, asante Mark"

    "Mh! Mbona umefurahi mno, halafu bado mimi sijakutambua vizuri, naomba ujitambulishe ili niweze kukufahamu kwanza" Alizidi kuuliza Mark.

    "Naitwa Jane, kama unanikumbuka ni dada ambaye tulikutana THE GRAND BAR iliyopo maneo ya pale Bima hapo Moro." Alikuwa ni Jane, akajitambulisha kwa Mark ili aweze kumfahamu.Moyo wake Mark kafarijika na kulipuka kwa furaha baada ya kugundua mpigaji wa simu ile alkuwa ni Jane.

    "Oooh!, Jane! Uko wapi!?, mbona nimekutafuta sana kwenye simu yako sikuweza kukupata!?, vipi kuna tatizo lolote lililokusibu Jane!?" Huku akiwa na furaha kubwa, Mark alimuuliza Jane kwa mfululizo.

    "Naomba unisamehe kwa usumbufu Mark, nilisafiri kikazi, ila usiku wa leo majira ya saa saba natarajia kuwasili Tanzania na ndege hivyo kama una nafasi, naomba uje kunipokea katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere." Jane alimuleza Mark.

    "Sawa Jane, ondoa shaka, nitakuja kukupokea" Alizungumza Mark na kukubaliana na ombi la Jane.

    Mark alifarijika sana baada ya kusikia jambo lile kutoka kwa Jane, alitazama saa yake na ilikuwa saa kumi jioni, alihisi muda huu unamtosha kwa yeye kuweza kusafiri kutoka Morogoro na kwenda Dar es salaam.Akaenda ofisi kuu na kuomba udhuru wa siku mbili, baada ya kuaga ofisini, Mark akaenda nyumbani na kujiandaa kwa ajili ya safari yake.



    Maisha ya furaha na upendo yakapata kurejea tena katika mapenzi yao, John kujitahidi na kuzidi kumuonesha Sala kwa jinsi gani amebadilika na kuwa mtu mwema kwake.

    "Asante sana John kwa kunifanya nami nikawa muda wote kuwa mwenye furaha, nakupenda sana na sihitaji kukaa nawe mbali hata kidogo" Alizungumza Sala na kumueleza John, wakiwa katika moja ya matembezi yao ya pamoja.

    "Asante Sala, yani mimi ndio sijiwezi kabisa kwako."

    "Nashukuru sana mpenzi wangu, natumaini utakuwa mume bora kwangu." Sala alimueleza John.Wakiwa katika mazungumzo hayo, ghafla John akagusia jambo moja na kumueleza Sala ambalo lilimfanya Sala kushtuka kidogo na kujiuliza, kwanini John amezungumza vile.



    "Kama hutojali, naomba unisaidie kitu kimoja kwa ajili ya kuandaa maisha bora katika familia tunayoenda kuianzisha." John alimueleza Sala.

    "Jambo gani hilo mpenzi wangu!?"

    "Unaonaje kampuni hii iliyoachiwa na baba, tukaijumuisha ndani ya kampuni yetu ili tuweze kukuza kiwango cha biashara na jina la kampuni yetu." John alimueleza Sala na kumuomba kuichukua kampuni ya kibiashara ambayo awali ilikuwa ikimilikiwa na baba yake Sala na baada ya kifo cha baba, kampuni ikawa chini ya mikono ya Sala.Sala alifikiri sana ombi hili la John, lakini kutokana na upendo mkubwa uliopo baina yao na maneno mazuri ya John ambayo yaliendelea kumshawishi Sala vilivyo kuweza kukubaliana na ombi lile, mwisho Sala akaridhia na kukubaliana na ombi la John.John alifurahi sana, akamkumbatia Sala na kumshukuru kwa kumkubalia ombi lake.

    "Nashukuru sana Sala, hakika najivunia sana kupata mwanamke mwelevu kama wewe"

    "Ondoa shaka John, nafanya yote haya kwasababu ya imani kubwa niliyokuwa nayo kwako, naomba jitahidi sana kuwa makini na kampuni hii ambayo niliachiwa na marehemu baba yangu kwasababu hii ndio nguzo yangu pekee ninayoitegemea katika maisha yangu." Kwa msisitizo, Sala alizungumza na kumueleza John.

    Siku hii John alikuwa na furaha mno, japokuwa aliomba kampuni ile kwa wema lakini kichwani mwake alikuwa na malengo tofauti na alihitaji kufanya kitu tofauti kwa Sala.Katika kudhihirisha furaha aliyokuwa nayo siku hii, John akamchukua Sala na kumpeleka katika hoteli kubwa na yenye hadhi ya kimataifa kwa ajili ya kupata chakula cha jioni kwa pamoja.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yakiwa majira ya usiku wa saa mbili, Mark akawasili katika jiji Dar es salaam kwa ajili ya kumpoke Jane ambaye anayetarajia kuingia Tanzania usiku huu. Kwakuwa hakuwa na mahali au sehemu anayoifahamu hapa Dar es salaam ambayo anaweza kufikia, Mark akaamua kwenda kukodi chumba katika hoteli moja, iliyojulikana kwa jina la THE DREAMS EXECUTIVE HOTEL, kwa ajili ya mapumziko kabla ya kwenda kumpokea Jane ambaye anatarajia kuwasili Tanzani majira ya saa saba usiku.THE DREAMS EXECUTIVE HOTEL, hii ni hoteli kubwa sana na yenye hadhi ya nyota tano na ambayo ilikuwa inafikiwa na wageni wengi kutoka nchi mbalimbali na wengine wakifika katika hoteli hii kwa ajili ya kupata vyakula bora vilivyokuwa vinapatikana mahali hapa.Baada ya kupata chumba kwa ajili ya mapumziko, Mark akaamua kwenda hadi sehemu wanapouza chakula pale hotelini ili aweze kupata chakula cha jioni kabla ya kuanza safari ya kuelekea uwanja wa ndege muda utakapofika.



    Katika siku hii, John naye aliamua kumchukua mpenzi wake Sala na kumleta katika hoteli hii ambayo amefikia Mark bila ya wao kutambua, kwa ajili kupata chakula cha jioni na kuendelea kuyafurahi mapenzi yao kwa pamoja.Wakiwa mezani, mazungumzo mbalimbali yaliendelea baina yao.

    "Umeionaje sehemu hii Sala!?"

    "Hakika ni nzuri na inapendeza mno mpenzi wangu, asante kwa kunijali."

    "Hii ni sehemu mahususi ambayo watu huja na watu wao maalumu kwa ajili ya kupata chakula cha jioni na kuendeleza furaha yao."

    "Asante John, ila nina ombi moja kwako"

    "Bila shaka niambie tu mke wangu mtarajiwa"

    "Naomba kabla ya mwaka huu haujaisha, tufunge ndoa maana nina hamu sana, kidoleni mwangu nami kukawa na pete ya ndoa."

    "Ni wazo zuri sana Sala, lakini kwasasa bado mapema, acha kwanza tutengeneze maisha kabla ya kulitimiza ilo mpenzi wangu."

    "Hapana John!, naomba tulitimize hili ndani ya mwaka huu ili tuwe huru katika mapenzi yetu, tafadhali John kubaliana na ombi langu mpenzi wangu...."

    "Sawa, kwakuwa umelihitaji hilo na mimi sipendi kukuona ukiteseka, basi tutalikamilisha hilo mapema iwezekanavyo ndani ya mwaka huu." John alizungumza na kukubaliana na ombi la Sala, lakini moyoni mwake alikuwa na adhimio tofauti katika lile.



    Sehemu ambayo alikuwa amekaa John pamoja na Sala, haikuwa mbali sana na eneo ambalo alikuwa amejituliza Mark, lakini kutokana na mwanga hafifu uliokuwepo mahali pale, hakuna aliyeweza kutambua uwepo wa mwenzie katika sehemu ile.

    Mark aliendelea kupata msosi wake, huku akiwaza na kujiuliza maswali mengi kichwani mwake na kushindwa kuelewa kwanini anayafanya yale yote kwa ajili ya binti yule.

    "Mbona najihisi kuwa mtumwa ghafla!?,

    Yanawezekanaje yote haya kuyafanya mimi!?,

    Hakika Jane atakuwa ni mwanamke wa muhimu sana katika maisha yangu, haitajiki kumpoteza hata kidogo mwanamke huyu, lazima nimueleza kitu ili aweze kutambua fikra zangu mapema, nashukuru sana Mungu kwa jicho lako kumtazama mnyonge ambaye ameteseka kwa muda mrefu sana" yalikuwa mawazo ya Mark huku akijikuta muda wote akisikia raha isiyo na mfano ndani ya moyo wake.Akatazama saa yake, tayari ilashatimia mida ya saa tano na nusu usiku, akaona huu ni muda muafaka wa yeye kuanza safari ya kuelekea uwanja wa ndege wa Julias Nyerere kwa ajili ya kumpokea binti ambaye alijikuta, ghafla ameingia moyoni mwake na kuanza kumpenda.Baada ya kufanya malipo ya chakula na akianza kutoka pale hotelini, mara akasikia sauti ikimuita jina lake, Mark alishtuka kidogo maana katika safari yake ya kuja Dar es salaam hakuna mtu alimfahamisha, akageuka nyuma ili aweze kumtambua mtu aliyemuita.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mark!!!?"

    "Nick.!!.!.." Mark alishangaa baada ya kumuona Nick mahali pale na ndiye mtu aliyekuwa anamuita.

    "Kweli wewe ni Mark!?"

    "Yah, ndio mimi Mark, habari ya siku nyingi Nick!?"

    "Hapana Mark!, mbona mimi niliambiw.....!!". Nick alitaka kuzungumza kitu, lakini mara machozi yakaanza kumdondoka na kushindwa kuendelea kuongea.Mark alibaki kwenye mshangao mkubwa na kushindwa kuelewa kwanini Nick amebadilika ghafla na kuanza kulia baada ya kuonana na yeye.

    " Nick!, tatizo nini kwani rafiki yangu!?, mbona unaniacha njiapanda, ni kitu gani hicho ulichoambiwa mpaka kikupelekee kudondosha chozi!?" Kwa mshangao mkubwa, Mak alimuuliza Nick.

    "Mark naomba tuketi, ili niweze kukusimulia kitu kidogo"

    "Sawa Nick, ila naomba tutumie muda mfupi maana kuna mtu naenda kumpokea uwanja wa ndege usiku huu." Mark akamueleza Nick na wakatafuta sehemu ambayo haikuwa na watu, wakaketi ili waweze kuongea vizuri.

    "Hapa tunaweza kuongea vizuri Nick, unaweza ukaendelea sasa"

    "Siku moja wakati niko katika mizunguko yangu, nilikutana na Sala akiwa ameambatana na kijana mmoja ambaye alijitambulisha kwangu kwa jina la John.Nilipomuuliza Sala kuhusana na wewe ulipo maana siku nyingi sijakuona, jibu ambalo alinipa Sala, hakika liliniumiza na kunifanya kuwa na simanzi kubwa sana moyoni mwangu..."

    "Alikupa jibu gani Sala!?" Aliuliza Mark kwa shauku kubwa ya kutaka kujua.

    "Sala alinieleza kuwa tayari wewe ilishafariki katika dunia hii na katika kunithibitishia hilo, yule John aliongezea kuwa ulikufa kwa kupigwa risasi baada ya kujiingiza katika magenge ya kijambazi.Niliumia sana rafiki yangu baada ya kuambiwa taarifa hizi, kwasababu nilihisi katika kifo chako, nami nahusika kwa namna moja au nyingine kwakuwa nilishindwa kukusaidia kipindi kile ulipokuja kuniomba msaada."

    "Unahakika Nick, hivyo ndivyo alivyokwambia Sala!?"

    "Ndio Mark na ndio maana nimeshangaa sana kukuona wewe hapa tena ukiwa bado upo hai." Alizungumza Nick kwa msisitizo na kumueleza Mark.Maneno haya ya Nick, yalimuumiza sana Mark, aliona Sala pamoja na John ni zaidi ya mashetani kwake kwasababu pamoja na mambo yote yale waliyomfanyia lakini bado wakadiriki kusambaza habari za uongo juu yake.

    "Nick, siku yoyote nitakayokutana na John au Sala, nahidi nitafanya kitu juu yao, nimeshateseka na kuumia sana kwasababu yao lakini sasa naona imeshafika kikomo." Huku akionekana kupandwa na hasira kwa kiasi fulani na kwa uchungu mkubwa, Mark alimueleza Nick.

    "Embu naomba uniambie Mark, imekuwaje mpaka Sala amebadilika na kufikia hatua hii na ni kitu gani kilichotokea baina yenu!?"

    "Nick, ni stori ndefu sana ila kwasasa nina haraka kidogo ya kwenda uwanja wa ndege kwa ajili ya kumpokea mgeni wangu, mengi zaidi nitafuta kesho tuweze kuongea vizuri kabla sijaondoka na kurudi katika makazi yangu mkoani Morogoro." Mark akamueleza Nick, kisha Mark akatoka na kuondoka, akimuacha Nick akiendelea kupata chakula pale hotelini.



    Mark aliwasili uwanja wa ndege, na kumsubiri Jane ambaye alibakisha dakika kumi ili ndege aliyopanda iweze kuwasili. Baada ya muda kupita kidogo, Mark akiwa mapokezi, kwa mbali akamuona Jane pamoja na abiria wengine wakiwa wanasogea upande wa mapokezi baada ya kushuka kwenye ndege.Moyo wake ulifarijika sana Mark, mwendo wa madaha na umbo zuri aliojaliwa Jane, ilizidi kumchanganya Mark.Ilikuwa ngumu Mark kuzizuia hisia zake kwa binti yule, akatoka na kumkimbilia Jane na kumkumbatia kwa lengo la kumpokea na kumkaribisha Tanzania.

    "Karibu sana Jane, nimefarijika sana baada ya kukuona kwa mara nyingine tena."

    "Asante Mark na pia nashukuru sana kwa kuja kunipokea." Jane alimshukuru Mark kisha wakaanza safari ya kuelekea katika hoteli ambayo alifikia Mark, ili waweze kupata mapumziko.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kupata chakula cha jioni, John pamoja Sala, taratibu nao wakaanza safari ya kurejea nyumbani.Wakiwa karibu na kutoka pale hotelini, wakashangaa kumuona Nick akija upande wao huku uso wake ukionyesha kuwa katika hali ya hasira mno.John na Sala walibaki wameshangaa sana, wakasimama ili waweze kuzungumza na Nick.



    Nick alifika karibu na mahali walipo John na Sala, akawasalimi na kuzungumza nao.

    "Mbona uso wako unaonesha leo hauko sawa Nick, vipi kuna tatizo!?" sala alimuuliza Nick.

    "Hapana mimi nipo sawa Sala, ila siku ya leo nina furaha iliyochanganyika na hasira kidogo"

    "Unamaanisha nini kusema hivyo Nick!?"

    "Furaha yangu leo ni pale nilipofanikiwa kukiepuka kikombe cha dhambi ambacho mwanzoni nilihisi kimeniangukia, na hasira yangu inakuja baada ya kuwaona mashetani ambao walijaribu kuniweka katika hali ya wasiwasi mkubwa kwa kipindi chote hiki."

    "Bado sijakuelewa Nick, unamaanisha nini kuzungumza maneno hayo!?"

    "Hahahahaha.! usijali Sala, mtaelewa tu muda ukifika." John aliangua kicheko cha dharau, kisha akaondoka na kuwaacha John pamoja na Sala, wakiwa katika mshangao mkubwa na wakijiuliza maswali mengi ambayo walishindwa kupata majibu yake.

    "John, hivi kuna chochote ilichokielewa kuhusu alichozungumza huyu mpuuzi" Sala alimuulza John.

    "Nahisi atakuwa amechanganyikiwa ndio maana alikuwa anajiropokea tu.Mimi naomba usiyaweke akilini mpenzi wangu kwasababu yatakuumiza kichwa, ngoja nichukue usafiri hapa tuweze kurudi nyumbani." Alizungumza John na kumueleza Sala.Katika maneno ambayo alizungumza John, kwa kiasi fulani Sala akawa ameelewa kitu japokuwa alikuwa hana uhakika nacho, hii ikamfanya kuwa na hofu kidogo na kukosa amani katika moyo wake.John akatoka na kuchukua usafiri, kisha wakatoka pale hotelini na kurudi nyumbani.



    Ilikuwa siku njema sana kwa Mark, akiwa pamoja na Jane wakawasili THE DREAMS EXECUTIVE HOTEL baada ya kutoka uwanja wa ndege.Baada ya kufika hotelini, Mark akamuongoza Jane hadi sehemu ya chakula ili naye aweze kupata chakula cha usiku, baada ya kutoka safari ndefu.Meza ambayo Jane na Mark walienda kukaa, ndio meza ambayo walikuwa wamekaa John pamoja Sala muda si mrefu walipokuja kupata chakula pale hotelini.Katika kiti ambacho Mark alikwenda kukaa, aliweza kuokota kadi ya biashara ambayo ilikuwa imeandikwa jina la kampuni ambayo alikuwa akiifahamu sana.Mark akachukua kadi ile na kuweka mfukoni mwake.

    Wakiwa mezani, Jane akiendelea kupata chakula, stori mbalimbali waliendelea kuzungumza.

    "Umeionaje sehemu hii Jane?"

    "Hii ni sehemu nzuri sana, imetulia, chakula chake ni kizuri, hakika ni sehemu ambayo inavutia mno na hongera kwa kuchagua sehemu nzuri kama hii."

    "Asante Jane, nimefanya yote haya kwa ajili yako."

    "Nashukuru sana Mark kwa kampani yako kubwa unayonipa, umekuwa mwema kwangu kila wakati" Huku akiwaa anatabasamu Jane alimueleza Mark.Tabasamu lake na uzuri aliobarikiwa binti huyu, vilizidi kumchanganya Mark na akijikuta muda wote anatamani kumuuangalia Jane na kuzidi kumpenda moyoni mwake.

    "Jane, naweza kukuomba kitu?"

    "Bila shaka, unaweza kuzungumza Mark"

    "Kama una nafasi, naomba siku ya kesho tuendelee kukaa hapa Dar es salaam ili tuweze kutembea pamoja na kuufahamu vizuri mji huu."

    "Kwasasa nipo likizo Mark, hata ungesema mwezi tukae hapa, mimi ningekaa tu" Alizungumza Jane na kumjibu Mark.Jibu hili lilimpa furaha sana Mark na akiamini, ndani siku hii aliyoiomba, anaweza kuitumia vizuri na kumueleza Jane yaliyopo moyoni mwake.

    Wakaendelea kuzungumza Mengi, na kila mmoja akapata nafasi ya kumfahamu mwenzake vizuri, mwisho baada ya maongezi marefu, wakatoka na kurudi vyumbani kwa ajili ya kjpumzika huku kila mmoja akiwa amechukua chumba chake pale hotelini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ikiwa siku ya pili, Sala akamkabidhi John rasmi kampuni yake ili aweze kuisimamia na kuiongoza yeye kama walivyokubaliana.Moyoni mwake John alifurahi sana, na akiamini sasa anaenda kukamilisha malengo yake aliyoyapanga.

    "John, nimekukabidhi kampuni hii kwasababu nakuamini na nakupenda sana, naomba kuwa makini sana na kampuni "

    "Ondoa shaka Sala, nakupenda mno na nafanya yote haya kwasababu nahitaji kukupatia furaha siku zote."

    "Asante John, nashukuru sana kwa kunijali, nakuhitaji na sitamani kukupoteza kabisa." Alizungumza Sala na kumueleza John.Moyoni mwake Sala aliamini kabisa John ndiye mwanaume pekee ambaye anaweza kukumkabidhi maisha yake na ndio maana hata John alipomuomba kampuni, hakuhitaji kufikiri wala kuumiza sana kichwa katika kukubaliana na ombi lake la kumkabidhi kampuni.



    Siku hii pia, baada ya kupata chai kwa pamoja, Jane na Mark wakatoka kwa ajili ya matembezi ili waweze kuzungumza na kufanya mambo mengi wakiwa pamoja.Walitembelea sehemu nyingi katika mji wa Dar es salaam, furaha muda wote ilikuwa imetawala katika matembezi yao, ilipofika mida ya jioni, wakajisogeza katika fukwe moja ya bahari ili waweze kuzungumza mengi na kumalizia furaha zao.Hii ndio nafasi pekee ambayo Mark alihisi anaweza akaitumia vizuri na kueleza hisia zake kwa mtu ampendaye.



    Katika maisha yangu, leo ni siku ambayo sitoweza kuisahau kabisa." Alizungumza Mark na kumueleza Jane.

    "Kwanini unazungumza hivyo Mark!?"

    "Muda mrefu umepita, sijawahi kupata furaha kama hii ya leo, hakika wewe ni mwanamke wa tofauti sana Jane."

    "Hapana Mark, furaha au huzuni mtu hujitengenezea mwenyewe ila hata wewe uko tofauti sana na vile nilivyokudhania awali"

    "Jane, naweza kukuuliza kitu!?"

    "Niulize tu Mark, maana wewe kwa maswali, hauna tofauti na mwandishi wa habari." Alitania Jane na wote kujikuta wakiangua kicheko kutoka na utani mwingi uliokiwepo katika mazungumzo yao.

    "Je ulishawahi kuwa na mpenzi na kama ulikuwanae, mahusiano yenu yalikuwaje? Aliuliza Mark.

    "Mh! ni swali gumu sana kwangu Mark, ila kwa kifupi, neno mapenzi ni geni kwangu na sijawahi kuwa na mtu anayeitwa mpenzi." Alijibu Jane. Baada kupokea jibu hili, Mark akajikuta akipata furaha na kufarijika sana moyoni mwake.

    "Je wewe Mark, umeshawahi kuwa na mpenzi" Aliuliza Jane

    "Ndio, ila hatukukaa sana tulitengana"

    "Ikawaje mpaka mkatengana!?"

    "Mh!, ni stori ndefu kidogo, ila nitakusumulia kwa ufupi jinsi ilivyokuwa" Alizungumza Mark.Mark akaamua kumsimulia kila kitu Jane, jinsi mahusiano yake ya kimapenzi na Sala yalivyokuwa bila kusahau shida pamoja na misukosuko yote aliyopitia.Simulizi ile ya Mark ikamgusa sana Jane, akijikuta machozi yakimdondoka bila ya yeye mwenyewe kutambua, aliona jinsi gani Mark alivyoweza kupitia wakati mgumu, alimuonea huruma sana Mark kwa taabu zote zile alizopitia katika maisha yake, akajisogeza karibu na Mark na kumlaza kifuani mwake kwa lengo la kumtuliza na kumfariji maana baada ya kumaliza simulizi yake, kilio tu kilikuwa kimemtawala Mark na kusikia uchungu mkubwa kila anapokumbuka mambo yale yaliyomkuta.

    "Pole sana Mark, naomba unisamehe kwa kukuuliza swali hili, maana sikutarajia kama ulipitia mambo mazito kama hayo" Alizungumza Jane huku akiendelea kumtuliza Mark.

    "Usijali Jane, ila kisasi changu ni kikubwa kwao na sitoweza kuwasamehe kabisa watu hawa" kwa uchungu mkubwa Mark alizungumza.

    "Haina haja ya kuweka kisasi moyoni mwako Mark na wala usimfikirie John wala Sala kwasababu utazidi kujiumiza tu, cha umuhimu kwasasa unapaswa kuangalia maisha yako." Kwa sauti ya upole na taratibu sana na ambayo iliweza kupenya vilivyo katika masikio ya Mark, Jane alimueleza Mark.

    "Naomba tuachane na hayo Jane na turudi katika furaha zetu.Mwisho wa wiki hii, kuna rafiki yangu mmoja pale ofisini anatarajia kufunga ndoa, hivyo kama hutojali naomba tuambatane pamoja siku hiyo na kuhudhuria harusi hii." Mark alimueleza Jane.

    "Ondoa shaka Mark, tutaenda wote siku hiyo"

    "Asante sana Jane, umekuwa mfariji kwangu kwa kila gumu nilipitialo.Ooh! Kwasasa muda umeenda sana naomba turudi hotelini ili tukajiandae na safari yetu." Mark alimshukuru Jane kwa kampani yake kubwa anayompa, kisha wakasimama na kwenda kujiandaa na safari yao ya kurudi mjini Morogoro katika mida ile ya jioni.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mapenzi yao yalizidi kuchanua, kila alipomtazama John, Sala alijiona mwenye bahati kubwa sana kwa kuweza kumpata mwanaume anayemjali na kumuonesha upendo wa kweli kama afanyavyo John.

    "Nakupenda sana John na naomba baada ya kuisha harusi ya mdogo wako na sisi utakuwa wakati wetu mzuri wa kufunga pingu za maisha." Alizungumza Sala na kumueleza John.

    "Hata mimi nakupenda sana mpenzi wangu na nahitaji tutakapoenda kwenye harusi hii ya mdogo wangu, nataka upendeze zaidi ya watu wote watakaofika ukumbini"

    "Ikiwezekana nimshinde hata bibi harusi wenu"

    "Haswaaaaa.., hivyo ndivyo ninavyotaka." Yalikuwa ni maongezi yaliyojawa na utani mwingi baina ya Sala pamoja na John na kuendelea kujiandaa na safari yao ya kwenda kuhudhuria katika harusi ya ndugu yake na John.



    Ilikuwa siku nzuri na ya furaha sana, ndani ya kanisa kuu hapa mjini Morogoro, Charles sambamba na mpenzi wake anayeitwa Pendo, walikuwa wakifunga pingu za maisha na kuwa mke na mume.Baada ya ndoa kufungwa kanisani, wageni mbalimbali pamoja na maharusi, walijikusanya pamoja katika ukumbi mkubwa na wenye hadhi ya juu sana kwa ajili ya kuendeleza shamrashamra na kusherekea siku hii ya muhimu sana kwao.

    Sherehe ikiwa inaendelea, sasa ilikuwa zamu ya maharusi kuweza kuwatabulisha watu wao wa karibu.Alianza Pendo kuwatambulisha ndugu, marafiki pamoja na jamaa zake na baada ya kumaliza, akamkabidhi kipaza sauti mumewe ili naye aweze kufanya utambulisho.Charles alikamata kipaza sauti na kuanza utambulisho.

    "Napenda kuwatambulisha wazazi wangu, naomba msimame muweze kupunga mkono" Alizungumza Charles na kuwatambulisha wazazi wake.

    "Pia napenda kutambua uwepo wa kaka yangu ambaye amefunga safari kutoka Dar es salaam mpaka hapa Morogoro, Kaka John pamoja ubavu wako naomba msimame" Charles alimtambulisha kaka yake, John akiwa ameambatana na Sala wakasimama na kupunga mkono.Baada ya hapo akawatambulisha marafiki zake pamoja na baadhi ya ndugu zake waliokuwepo pale ukumbini.

    "Mwisho kabisa, napenda kumtambulisha mtu wa muhimu sana kwangu, Japokuwa ni mkubwa wangu wa kazi pale ofisini lakini naweza nikasema mtu huyu ni zaidi ya ndugu au rafiki kwangu na ambaye amenipa msaada mkubwa mpaka mimi kuweza kufanikisha tukio hili siku ya leo, napenda kumkaribisha aweze kuingia ukumbini." Alizungumza Charles na Kumkaribisha ukumbini mtu huyu wa mwisho kwake kumtambulisha.Watu wote wakageuka nyuma ili waweze kumshuhudia mtu huyo, kwenye sakafu kukiwa na kumetandikwa kapeti jekundu(red carpet) na mwimbo wa taratibu uliendelea kuchombeza pale ukumbini kwa ajili ya kusindikiza ukaribisho ule.





    Akiwa kwenye suti ya rangi nyeupe na iliyokuwa nadhifu mno huku akiwa akiwa ameambatana na Jane aliyependeza vilivyo na gauni lake lenye kumeremeta la rangi ya bluu, kwa mwendo wa taratibu, Mark anaingia ukumbini huku wakishangiliwa na ukumbi mzima kutokana na jinsi walivyopendeza.

    Hili lilikuwa pigo la kwanza kwa Sala pamoja na John, walishindwa kuamini kwa walichokiona pale, Hofu kubwa ikamjaa Sala na kuhisi baridi mwili mzima ambalo alishindwa kufahamu lilipotokea.Kwa upande wa John yeye alihisi kama yupo ndotoni na kushindwa kuamini kama mtu amuonaye pale ni Mark, katika kukwepa aibu ile na ili wasionekane kwa Mark , John akamshika Sala mkono na kutoka nje ya ukumbi kupitia mlango wa pili tofauti na ule wanaoingilia Mark pamoja na Jane.Baada ya kufika nje, John na Sala hawakuona sababu ya kuendelea kubaki katika eneo lile la ukumbi waliingia kwenye gari yao na kuondoka.

    Baada ya kuwasili katika ukumbi, Mark akakabidhiwa kipaza sauti na kuongea machache kisha wakaenda kukaa katika sehemu yao waliyoelekezwa.Sherehe ilizidi kuendelea lakini Charles moyoni mwake alijisikia vibaya kwa kitendo kile cha kaka yake kutoka ukumbini na kuondoka, akajitahidi kuficha huzuni yake na kuendelea na sherehe.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kutoka ukumbini, John na Sala hawakuona sababu ya kuendelea kubaki katika mji wa Morogoro, wakaamua kufunga safari ya kurudi Dar es salaam usiku ule.Wakiwa kwenye gari, ukimya ulitawala, kila mmoja akitafakari kwa alichokiona pale ukumbini.Baada ya ukimya wa muda mrefu, Sala akaanzisha mazungumzo.

    "Siwezi kuamini kabisa John kwa nilichokiona pale, kweli yule ni Mark!?"

    "Sala, sina haja ya kueleza kitu hapo maana yote unayafahamu"

    "Inawezekanaje John!, Inawezekanaje yule akawa Mark!?" kwa sauti kubwa, alilalamika Sala.John alifunga breki ya ghafla na kumgeukia Sala.

    "Nyamaza Sala..!!?, sihitaji kelele wala maswali kwasasa, kwasababu wewe ulikuwa unaufahamu ukweli wote ila ukanificha"

    "Ukweli..!!?, ukweli upi huo John, mbona unanishangaza." Alizungumza Sala na kustajabu kwa tuhuma zile anazopewa.Waliendelea na safari huku wakiendelea kubishana na John akizidi kumtuhumu Sala na kumuhisi pengine alikuwa akifahamu ukweli juu ya uwepo wa Mark.



    Ikiwa ni mida ya saa saba usiku, baada ya sherehe kuisha pale ukumbini, Mark akamchukua Jane ili waweze kurudi nyumbani.

    "Asante sana Jane kwa kukubali kuongozana nami kuja katika sherehe hii"

    "Usijali Mark, kwako nimekuwa mdhaifu mpaka najishangaa"

    "Kwanini Jane!?"

    "Mark!, usiku umeshakuwa mkubwa sasa, endesha gari nirudi nyumbani, nahitaji kwenda kupumzika sasa." Alizungumza Jane na taratibu Mark akaanza kuendesha gari kwa ajili ya kurudi nyumbani.Wakiwa ndani ya gari mazungumzo kati yao, yalizidi kuendelea.

    "Jane naweza kukuomba kitu!? Aliuliza Mark.

    " Bila shaka Mark, zungumza tu"

    "Usiku ni mkubwa sasa na kule unapokaa ni mbali, unaonaje ulale hapa kwangu karibu halafu kesho ndio uende nyumbani"

    "Mh!, Mark nahofia sana kulala nje ya nyumbani, maana sijawahi kufanya hivyo hata siku moja"

    "Jane, nyumba yangu ina vyumba vya kutosha, hivyo huna sababu ya kuhangaika usiku huu, pumzika kwangu hapa halafu kukishapambazuka utarudi nyumbani" Kwa sauti ya taratibu na ya kubembeleza, Mark alimueleza Jane na mwisho Jane akamuelewa Mark na kukubaliana ombi lake.

    Walifika nyumbani, Mark akamkaribisha Jane nyumbani kwake na kumuonesha chumba ambacho anaweza akakitumia kujipumzisha usiku ule.Kila alipozidi kumuangalia Jane, Mark alizidi kuchanganyikiwa kutokana na umbo zuri alilobarikiwa mrembo yule, akiwa kitandani kwake, alishindwa kabisa kupata usingizi, akatoka kitandani na kwenda kukaa sebuleni na kutazama runinga.Akiwa amejituliza pale Sebuleni, mara Jane naye anatokea na kusogea pale alipo.

    "Jane!, bado haujalala!?" Mark alimuuliza Jane.

    "Nahisi kutopata usingizi kabisa Mark, ndio maana nikaona bora nije kijiunga nawe hapa"

    "Sa..sa.Sawa karibu uketi" Huku akiwa na kigugumizi cha ghafla, Mark akamkaribisha Jane ili aweze kuketi.Jane akasogea na kwenda kukaa katika kochi alilokaa Mark.Wakiwa wanaendelea kuangali runinga, muda wote ukimya ulitawala na kila mmoja akimuangalia mwenzake kwa macho ya kuibia.Hisia kali zilimshika Mark na kushindwa kujizuia kabisa, mwisho macho yao yakagongana na kubaki wakitazamana, Mark alipomuangalia Jane, macho yake yaliyojaa huba yalitosha kujieleza anachohitaji na taratibu akajisogeza karibu na Jane na kukutanisha ndimi zao, wakaendelea kubadilisha mate huku kila mmoja akiwa na hisia kali juu ya mwenzake.Wakiwa katika tendo hilo, ghafla Jane akajito mikononi mwa Mark na kusimama, machozi yakaanza kumtoka, bila kuongea chochote akatoka mbio na kurudi chumbani kwake.Mark alibaki katika mshangao na kushindwa kuelewa kwanini imekua vile.Alijilaumu na kujiona mkosefu mbele ya Jane kwa tendo lile alilolifanya.Alitamani akamuombe msamaha Jane, lakini alihisi pengine angemsumbua kwa wakati ule, akarudi chumbani na kusubiri kupambazuke ili aweze kuzungumza nae na kumuomba msamaha.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Asubui na mapema Mark akaamka na kujiandaa kwa ajili ya kwenda kazini, kabla ya kuondoka nyumbani akahitaji kuzungumza na Jane ili aweze kumuomba msamaha kwa lile walilolifanya usiku.Akasogea hadi katika chumba alichokuwemo Jane, akabisha hodi lakini kulionekana kuwa kimya.Akibisha hodi tena, lakini ukimya ulitawala.Baada ya kubisha hodi mara nyingi bila kujibwa chochote, Mark akapata wasiwasi na kuingiwa na hofu kuhusiana na Jane, akafungua mlango haraka na kuingia ndani.



    Yakiwa majira ya asubui, hasira ilikuwa kubwa kwa John na kuendelea kumtuhumu Sala kuwa alikiwa akitambu mahali alipo Mark.

    "John, naomba unielewe mpenzi wangu, tangu Mark aondoke kipindi kile, mimi sikuwahi kuwasiliana nae wala kufahamu mahali alipo." Kwa unyonge mkubwa alizungumza Sala.

    "Siwezi kukuamini kabisa Sala kwa hili ulilolifanya"

    "John naomba unielewe ili niweze kukueleza taarifa hii njema kwetu ninayohitaji kukuambia." Alizungumza Sala kwa sauti ya upole.

    "Unaweza ukazungumza tu" Alijibu John kimkato

    "John naomba sahau yote hayo kuhusiana na Mark na tuangalie maisha yetu kwasasa na zaidi ninachotaka kukueleza, unaenda kuitwa baba sasa mpenzi wangu maana mimi tayari ni mjamzito hapa." Alizungumza Sala na kumtaarifu John.Taarifa hizi zilimshtua sana John, taratibu uso wake uliokunjamana kwa hasira, ukaanza kunyooka na kuonekana kulifurahia lile.Moyoni mwake alifurahi sana Sala na kumshukuru John kwa kumuelewa, lakini ghafla akshtukia kofi zito likitua shavuni mwake na kupelekea kuanguka hadi chini.



    "Shetani mkubwa wee!, yote uliyofanya umeona haitoshi, ukaamua kumbebea na mimba huyo Mark wako..!?" Alizungumza John na kufoka kwa hasira.

    "John, kwanini unanibebesha mzigo wa dhambi ambao mimi sijaufanya, hii mimba ni ya kwako na sivyo unavyofikiria wewe." Kwa uchungu mkubwa alizungumza Sala.

    "Labda niseme neno moja tu ili unielewe Sala, kuanzia sasa mimi sikuhitaji nyumbani kwangu na uende ukatafute baba wa uyo mtoto ili mkalee." Yalikuwa maneno mazito kutoka katika kinywa cha John ambayo yalimuumiza vilivyo Sala

    "Hapana John usiniadhibu namna hiyo, mimi siwezi kufanya chochote bila ya wewe"

    "Hahahahaha!, unanifurahisha sana Sala, eti adhabu.!, adhabu ipi hiyo unayozungumzia kama adhabu ulishaikubali mwenyewe tangu awali kwa kukubali kudanganywa na kumuacha mwanaume aliyekupenda kweli"

    "Unamaanisha nini John!?, ina maana yote yale yalikuwa ni uongo!?" Aliuliza Sala kwa mshangao.John aliendelea kumcheka Sala kwa dharau huku akitikisa kichwa chake, akimaanisha kumsikitikia Sala.

    "Wewe ni mwanamke mpumbavu sana Sala, Mark alikupenda sana wewe ukamkataa, lakini mimi nilipenda mali zako ukanikubali, nashukuru kwa burudani zote ulizonipa na sasa unaweza ukaenda" aliongea John na kuendelea kumdhihaki Sala.Yalikuwa ni maneno mithili ya msumari wa moto ambayo yalienda kuchoma vilivyo moyo wa Sala, baada ya kupita muda mrefu, leo ndio anafahamu alifanya ukatili mkubwa kwa nafsi ya mtu aliyekuwa na mapenzi ya kweli kwake na kumkaribisha nyoka aliyejivisha ngozi ya chui katika moyo wake.Kilio cha masikitiko na majuto kiliendelea kumtawala na kujilaumu sana kwa kufanya kwake vitu bila kuwaza wala kufikiria.

    John akamuinua Sala pale chini alipokaa, alimkokota kama mzigo na kumsukuma nje ya nyumba, kisha akafunga milango ya nyumba na kuingia kwenye gari na kuondoka huku akimuacha Sala akiwa nje ya geti na kuendelea kulia.Sala aliitazama nyumba ile ambayo aliirithi baada ya wazazi wake kufariki, gari, kampuni, vyote tayari alishavikabidhi chini ya umiliki wa John, nafsi yake ilizidi kujuta na kuumia sana.Huku akiwa tayari ameshabeba mimba ya John, alishindwa kujua wapi atakapoenda na kupata hifadhi ya kuishi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Baada ya kuingia ndani, Mark alikuta chumba kikiwa tupu na bila ya Jane kuwepo ndani yake.Aliinua simu yake ya mkononi ili aweze kumpigia, lakini simu ya Jane ilikuwa inaita bila kupokelewa.Moyoni mwake huzuni ikamjaa Mark na kujutia sana kwa kile alichokifanya kwasababu aliona anaenda kumpoteza mrembo yule ambaye tayari alishampenda na kumuingiza moyoni mwake.Alitoka nyumbani na kuelekea ofisini japokuwa alikuwa hayupo katika hali nzuri kabisa siku hii.

    Alifika ofisini Mark na kuingia katika ofisi yake ili aweze kuendelea na majukumu yake ya kikazi.Akiwa ofisini, akashangaa kuona wafanyakazi wenzake wakija ofisini kwake na kumletea maua mengi huku wakimpa pongezi nyingi sana.Baada ya wafanyakazi kumpongeza, mwisho anaingia David, ambaye ni rafiki yake wa karibu sana pale ofisini huku mkononi mwake akiwa amekamata shampeni au mvinyo na keki kubwa iliyopambwa kwa maandishi mazuri.Baada ya kuvuta kumbukumbu zake vizuri Mark, akakumbuka siku hii ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa(Birthday).Mark alifarijika sana na kuwashukuru wafanyakazi wenzake kwa kupongezi zao japo yeye alipitiwa kabisa kama siku hii ilikuwa ya kumbukumbu ya kuja kwake duniani.Pamoja na yote hayo lakini kuna swali moja alikuwa akijiuliza kichwani mwake.

    "Asanteni sana kwa kunifanyania kitu kama hiki katika siku yangu hii, hakika moyoni mwangu nimefarijika sana japo nilipitiwa kabisa kama leo ni siku ya muhimu sana kwangu" Mark aliwashukuru wafanyakazi wenzake kwa zawadi na maandalizi yote waliyomfanyia katika siku yake hii ya kuzaliwa.

    "Lakini ningependa kufahamu kitu kimoja, hakuna mtu hapa ofisini niliyewahi kumwambia tarehe yangu ya kuzaliwa, Je mmewezaje kuifahamu!?" Mark aliwauliza wafanyakazi wenzake.

    "Mark, yupo mtu muhimu sana kwako aliyetuambia hili na yeye ndiye amefanya maandalizi yote haya" Alizungumza David na kumueleza Mark.

    "Nani huyo!?nahitaji kumuona sasa hivi"Aliuliza Mark kwa shauku kubwa ya kutaka kumfahamu mtu huyo, lakini kabla hajajibiwa chochote kile, mara simu yake inaingia meseji, akachukua simu yake na kufungua meseji ile ili aweze kuisoma.

    "'Hellow mpendwa wangu Mark, napenda kukutakia heri ya kuzaliwa kwako siku ya leo, pia naomba sahau yote yaliyopita na naomba leo baada ya kutoka kazini tukutane katika hoteli ya SUN DREAM kuna zawadi nzuri nimeiandaa kwa ajili yako.'" Ulikuwa ni ujumbe mfupi ambao Mark aliusoma.

    Baada ya kusoma ujumbe huu, moyoni mwake alifurahi sana maana alifahamu ni meseji ambayo ilitumwa na Jane, alisogea katikati ya wafanyakazi wenzake na kuanza kucheza kwa furaha huku wenzake wakimsindikiza kwa kumuimbia nyimbo mbalimbali za kumtakia heri na mafanikio katika siku yake ya kuzaliwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog