Search This Blog

PENZI LA SHETANI - 5

 





    Simulizi : Penzi La Shetani

    Sehemu Ya Tano (5)





    Hali ilikuwa ngumu sana kwa Sala, likiwa jua kali la saa saba na akiwa hajaingiza chochote tumboni tangu asubui, alijitahidi kuhangaika huku na kule kwa ajili ya kutafuta msaada lakini jitihada zake ziligonga mwamba kwa kila mahali alipoenda kuomba msaada.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ee Mungu, kwanini umenipa adhabu yote hii!?, kwanini hukunifungua tangu awali na kuniacha kufanya ubaya kwa mtu ambaye alionyesha upendo wa dhati kwangu tangu udogo wake.Nitafanya nini sasa, kila kitu nilichokuwa nakitegemea hakipo mikononi mwangu tena." Akiwa amejipumzisha chini ya mti baada ya kuzunguka sana, huku machozi yakimtoka, Sala aliendelea kusikitika na kujuta na nafsi yake.





    Baada ya kufikiri sana, Sala akamkumbuka rafiki yake mmoja aitwaye Suzy, ambaye walisoma wote katika chuo kimoja lakini wakiwa mwaka wa pili wa chuo Suzy aliamua kuachana na chuo na kufanya mambo mengine tofauti na elimu.Sala akaona ni heri akaenda kumuona Suzy, moyoni mwake akihisi pengine anaweza kumpa msaada wowote na kupata hifadhi ya sehemu ya kukaa.Alipofika nyumbani kwa Suzy, Suzy alimkaribishwa kwa furaha Sala maana ni siku nyingi walikuwa hawajaonana.

    "Karibu sana shost yangu, muda mrefu umepita hatujaonana tangu nilipokuacha chuo."

    "Kabisa Suzy, hakika nilikukumbuka sana"

    "Unishindi mimi Sala, yani niliwakumbuka sana wewe na Mark, kijana mpole, mstaarabu na anayejua kumpeti vilivyo mpenzi wake, nilitamani hata ungekuja nae hapa Mark ili niwape hongera zenu.lakini Sala, Mark yeye yuko poa?" Yalikuwa maneno machungu sana kutoka kwa Suzy na ambayo yalimpelekea Sala kudondosha machozi na kuzidi kuumia.

    "Heee!?, mbona unalia shoga, vipi kuna tatizo!?" Aliuliza Suzy kwa mshangao.Suzy alisogea karibu na Sala na kuanza kumtuliza huku akimtaka anyamaze japo alikuwa haelewi sababu iliuomfanya Sala kuangusha kilio.Alijitahidi kumtuliza na mwisho Sala akanyamaza.

    "Embu nieleze shoga, kilio hiki kinatokana na nini!?" Aliuliza Suzy.

    "Ni stori ndefu sana Suzy, unavyoniona hapa sina mahali pa kwenda kukaa ndio maana nimekutafuta wewe rafiki yangu ili unipe hifadhi" Alizungumza Sala kwa upole.

    "Huna mahali pa kukaa!?, mbona unanishangaza Sala!" Aliuliza Suzy kwa mshangao.

    Sala akaamua kumsimulia stori yote Suzy na kumuelezea kila kitu kuhusiana na kilichotokea katika mahusiano yake na Mark.Suzy alimsikitikia sana Sala, akaona jinsi gani John alivyo mkatili na kudhulumu penzi la watu, akamfuta machozi rafiki yake na kumtuliza.

    "Usijali Sala, mimi sina mume wa mtoto ninayeishi nae hapa, tutakaa wote na tutayajenga yetu pamoja"

    "Asante sana Suzy, hakika sitasosahau fadhila yako hii kubwa unayonifanyia siku ya leo"

    "Ondoa shaka Sala, mimi siwezi kukutupa wewe" Suzy alimueleza Sala na kumkaribisha nyumbani kwake ili waweze kuishi wote.Sala alimshukuru sana Suzy, kwa wema wake ule liomtendea na alishukuru kwa kuweza kupata hifadhi ya kuishi pale kwake.



    Ilikuwa jioni ya fahari sana kwa Mark, baada ya kumaliza majukumu yake ya kazi, moja kwa moja akaenda hadi maeneo ya Chamwino katika hoteli kubwa ya SUN DREAM kama alivyoelekezwa na Jane.Akamkuta Jane akiwa anamsubiri huku akiwa amependeza na gauni yake ya rangi nyeupe na iliyojaa vimeremeto kila mahali.Baada ya Mark kuwasili, Jane akainuka na kwenda kukumkumbatia Mark na kumkaribisha mahali pale.Waliagiza vinywaji na kuendelea na mazungumzo yao.

    "Hongera sana Mark kwa siku yako hii ya leo" Jane alimpongeza Mark.

    "Asante sana Jane, hakika umeifanya siku yangu ya leo kuwa yenye nuru sana"

    "Usijali Mark, napenda sana furaha yako" Alizungumza Jane na kumfanya Mark kuzidi kuwa na furaha.

    "Asante Jane, ila nina ombi moja kwako"

    "Lipi hilo tena Mark"

    "Naomba msamaha kwa kile kilichotokea jana pale nyumbani, nahisi nilikufanya uwe katika huzuni sana"

    "Hapana Mark!, mimi ndio napaswa kukuomba msamaha wewe maana nilikuweka katika wasiwasi sana." Alizungumza Jane na kumueleza Sala.

    Walizidi kuzungumza mengi na kufurahia pamoja katika siku hii muhimu kwa Mark.Kila alipomtazama Jane, moyo wake Mark ulizidi kufarijika na kujiona mwenye bahati sana kwa kuwa karibu na mrembo yule.

    "Enhee!, Nimekumbuka kitu Jane" Alizingumza Mark

    "Kitu gani hiko Mark"

    "Uliniambia leo umeandaa zawadi maalumu kwa ajili yangu, iko wapi mbona na hujanipa hadi sasa?"

    "Mark, embu punguza haraka, jambo zuri linaenda taratibu, ngoja tumalize hapa ili nikakupe zawadi yako" Alizingumza Sala na wote wakijikuta wakitabasamu na kuangua kicheko mara kwa mara na kuendelea kuyafurahia maongezi yao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ikiwa mida ya usiku wa saa tatu, Suzy alimuaga Sala na kumwambia anenda katika majukumu yake ya kikazi.

    "Shost, mimi naenda viwanja, baadae kidogo naweza kuja na mgeni hapa nyumbani" Alizungumza Suzy huku akiwa amevalia kimini na kumuaga Sala.

    "Viwanja!, viwanja gani tena usiku wote huu na mgeni gani utakayekuja nae!?" Aliuliza Sala kwa mshangao.

    "Ondoa shaka Sala, wewe ukimaliza kazi zako ingia katika chumba kile nilichokuonyesha ukapumzike, haya mengine yananihusu mimi." Alizungumza Suzy na kuondoka.Sala alibaki katika mshangao mkubwa na kujiuliza sana ni kazi ipi anayoenda kuifanya Suzy usiku wote.





    Furaha, tabasamu na vicheko, muda wote vilitawala huku kila mmoja akijikuta akisahau shida zote na kujihisi yupo katika dunia ya tofauti kabisa.Kila alipomtazama Jane, moyo wake ulizidi kufarijika Mark na kuona baada ya mateso, shida na taabu zote alizopitia, sasa na yeye amepata sehemu ya kuweza kupumzisha moyo wake na kutua mizigo yote ambayo alishaibeba kwa muda mrefu sana.

    "Asante Jane, wewe ni mwanamke pekee uliyeweza kunifanya mtu na kunipa furaha kama hii ambayo niliikosa kwa muda mrefu."alizungumza Mark na kumueleza Jane.

    "Hapana Mark, mimi siwezi kukupa furaha wewe!"

    "Kwanini Jane!?, kwangu wewe ndio thamani yangu pekee ninayoina sasa na umenifanya mimi kusahau shida na machungu yote niliyopitia"

    "Kwangu mimi naamini, furaha ya mtu ipo mikononi mwake mwenyewe na wala hawezi kuipata kutoka kwa mtu mwengine." Kwa sauti ya taratibu, alizungumza Jane.

    "Mark, naweza kukuliza swali?"

    "Bila shaka, uliza tu Jane"

    "kati mtu aliyeamua kujitoa nafsi yake kwa ajili ya kumlinda mtu ampendae na mtu aliyeamua kuilinda nafsi yake na kumtoa mtu ampendae kwa ajili ya kutimiza wajibu wake, Je yupi anastahili sifa kati yao?" Jane alimuuliza Mark, Mark alitafakari kidogo na kupata jibu la kuweza kumjibu Jane.

    "Kwangu mimi nadhani, mtu ambaye anastahili sifa ni yule aliyekubali kuitoa nafasi yake kwa ajili ya kumlinda mtu ampendae kwasababu anatambua nini maana ya upendo wa dhati"

    "Asante Mark, hakika wewe ni mwelevu mno na una weledi mkubwa katika kujibu maswali yako na sasa nahitaji kukupa ile zawadi niliyokuahidi" Alizungumza Jane, kisha akasimama pale alipokaa na kusogea mpaka sehemu aliyokaa Mark, bila kujali uwepo wa watu mahali pale akasogeza mdomo wake karibu na mdomo wa Mark, Wakagusanisha ndimi zao na kubadilishana mate.

    Ilikuwa ni zawadi kubwa sana kwa Mark ambayo hakutegeme kama angeipata ghafla namna ile, alimshukuru sana Jane kwa kutambua thamani yake na kumfanya ajione mtu mpya kabisa.Baada ya furaha zote kuisha, Mark akamchukua Jane na kumpeleka hadi sehemu anapoishi, kisha na yeye akarejea nyumbani kwa ajili ya kupumzika.



    Ikiwa mida ya usiku wa saa saba hivi, Sala akiwa amejipumzisha katika chumba chake, alianza kusikia maumivu makali ya tumbo na kumpelekea kukosa kabisa usingizi.Akiwa katika hali hiyo ya kuumwa tumbo mara mlango wa chumba chake ulibishwa hodi na Suzy ambaye alikuwa ametoka katika shughuli zake, huku akiwa bado na maumivu makali ya tumbo, Sala alijitahidi kuinuka pale kitandani alipolala na kwenda kufungua mlango ili aweze kwenda kuzungumza na Suzy.

    "Vipi shost, mbona umeshika tumbo huku umenikunjia sura!?" Suzy alimuuliza Sala.

    "Tumbo langu linaniuma sana mpaka nashindwa kuelewa linatokana na nini" alijibu Sala huku akiendele kuugulia maumivu yale ya tumbo.

    "Pole shoga yangu, tumbo kuuma kwa mwanamke ni kawaida na ukizingatia mimba yako hiyo bado ni changa, ila mimi nimekuja hapa nina shida moja nahitaji unisaidie."

    "Shida gani hiyo!?" Aliuliza Sala.

    "Leo kidogo nimekuja na wageni wengi hapa nyumbani, hivyo mimi siwezi kuwamudu wote kwahiyo naomba uwachukue wawili ili uweze kuwahudumia" alizungumza Suzy na kumfanya Sala abaki kati mshangao.

    "Mbona sielewi Suzy!?, wageni hao ni kina nani na mimi nitawapa huduma gani usiku wote huu!?" Aliuliza Sala.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mhhh! Shost, mbona unataka kuniangusha na kujifanya uelewi, kuna vidume viwili naomba vije kwako kupata huduma ili tusipoteze mzigo wa leo."

    "Hapana Suzy.!!?, unamaanisha nini.!!!, mimi sitoweza hiyo kazi na sijawahi kuifanya tangu kuzaliwa kwangu na licha ya hivyo huoni hali niliyokuwa nayo hii!?" Alizungumza Sala na kushtuka sana kwa lile analotaka kulifanya Suzy kwake.

    "We chizi nini!, unafikiri hapo ulipolala pamejileta penyewe, changamka mama hapa mjini na kama hutaki ondoka nyumbani kwangu sasa hivi!" Huku akiwa amekasirika, alifoka Suzy.

    Sala alibaki katika kilio tu huku akishindwa lipi afanye kwa wakati ule.Aliona dunia yote imemuelemea yeye na kuzidi kuelemewana mizigo mizito kama ile.Akiwa hajafanya chaguzi wala uamuzi wowote katika lile aliloelezwa, Suzy akamsukuma Sala chumbani kwanguvu na kuufunga mlango, kisha akawaleta wanaume wawili na kuwaingiza chumbani alimokuwamo Sala.Kelele za uchungu ndizo zilizosikika mle ndani, Baada ya saa moja kupita, wanaume wale wawili wakatoka chumbani na kumaliza mahitaji yao, huku jasho zikiwa zinawatiriririka mwilini, wakalipa fedha kwa Suzy na kuondoka.Sala alijikuta akikosa nguvu kabisa na kulegea mwili mzima baada ya shughuli ile nzito, kilio cha uchungu muda wote kilikuwa kimemtawala huku moyoni mwake akilaani sana kwa lile lililotokea.Suzy alimpongeza sana Sala kwa kazi nzuri aliyofanya, alimtaka aweze kupumzika ili apunguze maumivu yale anayoyasikia.



    Baada ya kila kitu kuisha, siku ya pili Mark alifika ofisini na kuendelea na majukumu yake ya kikazi kama ilivyo kawaida yake.Akiwa anaendelea na shughuli zake, mara simu yake ya mkononi inaiita na baada ya kuitazama ilikuwa namba ngeni katika simu yake.Akaipokea na kuweka sikioni ili aweze kuzungumza na mpigaji wa simu ile, kitu ambacho alikisikia, kilimfanya Mark kushtuka sana na kubaki katika mshangao mkubwa huku akijiuliza maswali mengi sana kichwani mwake.





    "Hallow, Naongea na Mark peter"

    "Ndio!, sijui naongea na nani mwenzangu"

    "Mimi ni Mzee Alfred, Je unanikumbuka kijana?" yalikuwa ni maongezi ambayo Mark alikuwa akiongea na mpigaji wa simu ile.

    Baada ya kusikia jina la Mzee Alfred, Mark alishtuka sana,maana baba yake alishawahi kumwambia mzee huyu ni mtu muhimu sana kwake na anatakiwa amtafute ili aweze kumpa siri kubwa inayohususiana na familia yake.Kipindi kirefu Mark alijitahidi kumtafuta mzee Alfred lakini alishindwa kumpata wala kufahamu mahali alipo hivyo baada ya kupigiwa simu ile ndio maana alishtuka sana.Mark alizungumza na mzee Alfred na mwisho wakakubaliana wakutane katika mji wa Dar es salaam, ambapo ndipo yalipo makazi ya mzee Alfred ili akaelezwe siri kubwa ambayo mpaka sasa Mark alikuwa bado haifahamu.

    Kabla ya kuanza safari ya kwenda Dar es salaam, Mark akaona ni vyema aweze kumtafuta Jane ili aweze kuzungumza nae na kumuaga pia.Mida ya Jioni ilipowadia, akatoka na Jane na kutafuta sehemu iliyotulia ili wazungumze.

    "kama nilivyokueleza awali Jane, siku ya kesho mimi naelekea Dar es salaam"

    "Ni jambo la lazima sana Mark mpaka uende haraka namna hiyo?" Aliuliza Jane na kumfanya Mark atabasamu kidogo.

    "Ondoa shaka Jane, najua kinachokusumbua ila nakuahidi nitarudi mapema iwezekanavyo"

    "Sawa Mark nakuombea safari njema lakini nami nina jambo moja la muhimu nahitaji kukueleza baada ya kurudi safari yako"

    "Mh!, kwanini usinieleze sasa hivi!?"

    "Hapana Mark, ukirudi ndipo nitakueleza." Alizungumza Jane na kumuahidi Mark atamueleza jambo atakaporudi safari yake ya Dar es salaam.Waliendelea kupiga stori nyingi na Mark akatumia nafasi hii kumuaga vizuri Jane na mwisho kila mmoja akarudi nyumbani kupumzika.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hali ilikuwa mbaya sana kwa Sala, hakuona sababu ya kuendelea kuishi nyumbani kwa Suzy kutokana na yale aliyomtendea, taratibu akaanza safari pasipo kujua wapi anaelekea.Akiwa anatembea barabara huku msongo mkubwa wa mawazo ukiwa umemsonga kichwani mwake, mara akapushwa na gari na kudondoka pembezoni kidogo mwa barabara.Dereva wa gari ile alisimamisha gari, na kurudi mpaka sehemu aliyokuwa ameanguka Sala.

    "Sala..!!!?"

    "Nick!!, kumbe ni wewe Nick...!!" Sala alishangaa kumuona Nick na ndiye mtu aliyempushi na gari.

    "Sala!, imekuwaje uko hivi na unafanya nini hapa!?" Nick alimuuliza Sala.Sala hakuwa na jibu lolote kwa wakati ule ambalo anaweza akamjibu Nick zaidi alibaki kulia tu.Japokuwa ni mtu ambaye alikuwa akimchukia sana kwa yale aliyoyafanya, lakini Nick alimuonea huruma sana Sala kwa hali ile aliyomuona nayo, akamchukua Sala na kumuingiza katika gari yake na kuondoka nae ili aweze kwenda kuzungumza nae vizuri.

    Nick akatafuta sehemu ili waweze kupata chakula na kumuuliza vizuri Sala yale yaliyomsibu mpaka amkute katika hali kama ile.Wakafika hotelini, kila mmoja akaagiza chakula anachokihitaji na kuanza mazungumzo.

    "Embu nieleza Sala, imekuwaje upo katoka hali kama hii !?" Aliuliza Nick.

    " Naomba unisamehe sana Nick kwa yale yote yaliotokea awali, sikutarajia kama ingekuwa hivi."

    "Sahau yote kuhusu yaliyopita kwasababu mimi nilishakusamehe muda mrefu sana, ila nashindwa kuelewa kwanini sasa upo kwenye hali hiyo"

    "Ni stori ndefu sana Nick, ila nitakueleza kwa kifupi jinsi ilivyokuwa" Alizungumza Sala na kuamua kumsimulia Nick mpaka yeye kufikia kupoteza mali zake kwa mwanaume ambaye alitokea kumuamini sana na kumpa nafasi kubwa moyoni mwake.Machozi yalizidi kumdondoka kila alipomkumbuka John pamoja na mikasa yote ile aliyoipitia, uchungu mkubwa ulimjaa Sala na kupata hasira kwa yale yote yaliyotokea.



    "Pole sana Sala kwa mikasa yote hiyo uliyoipitia"Nick alimpa pole Sala na kumtuliza.

    "Asante Nick, ila kuna jambo moja nahitaji unisaidie"

    "Lipi hilo tena Sala!?"

    "Nahitaji kuonana na Mark."

    "Mark.!!!?" Aliuliza Nick kwa mshangao.



    Ikiwa ni siku ya pili, Mark akasafiri na kufika hadi mahali anapoishi mzee Alfred.Mzee Alfred alimkaribisha Mark kwa furaha na kumpa pole kwa safari ndefu aliyotoka.

    "Karibu sana Mark, hakika sasa umekuwa mkubwa tofauti na kipindi kile nikivyokuona." alizungumza mzee Alfred.

    "Asante mzee, hata mimi nashukuru sana kwa kufanikiwa kukuona"

    "Hakika nina dhambi kubwa sana juu yako kwa kukuacha katika wakati mgumu kwa kipindi chote hiki." Alizungumza mzee Alfred na kumshangaza Mark kidogo.

    "Unamaanisha nini kusema hivyo!?" Aliuliza Mark kwa mshangao.

    Mzee Alfred hakuwa na jibu la kumueleza Mark, badala yake akatoa bahasha kubwa na kuiweka mezani.

    "Ni kitu gani hicho mzee Alfred?" Aliuliza Mark.

    "Ndani ya bahasha hiyo kuna karatasi muhimu na hati halisi zinazothibitisha umiliki wa mali zenu ambazo alidhurumiwa baba yako.?

    Mark alishtuka sana kwa yale aliyoambiwa na mzee Alfred na akapata kuelewa kwanini baba yake kabla ya kifo chake, alimsisitiza amtafute mzee huyu.Alishangaa sana utajiri mkubwa ambao alikuwa akiumiliki baba yake, kampuni, nyumba ya kifahari pamoja na mali nyinginezo nyingi ambazo alifanyiwa hila na kudhurumiwa.Mshangao ulikuwa mkubwa kwake zaidi baada ya kuambiwa mtu ambaye alifanya yote hayo kwa baba yake, alikuwa anaitwa Mathias Leonard ambaye kwasasa ni marehemu na ndiye baba yake mzazi na Sala.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " una hakika na hilo mzee Alfred!, huyu mtu ndiye aliyefanya familia yangu kuishi katika tabu?"

    "Kabisa Mark ila baba yako hakuhitaji kukueleza hilo mapema kwasababu alihitaji usome, lakini kwasasa tumia hati hizo nikizokukabidhi ili urejeshe mali zako." Alizungumza mzee Alfred na kumsisitiza Mark aweze kupambana ili aweze kurejesha mali zake ambazo alizulumiwa baba yake.Mark aliumia sana kutokana na maisha ya tabu na dhiki ambayo familia yake waliishi kumbe walikuwa na utajiri mkubwa kama ule.Mark akaamua kujiapiza, kwa gharama yoyote ile atapambana na kurejesha haki ya familia yake mikononi mwake bila kutambua kuwa mali hizo zote kwasasa zinamilikiwa na mtu mwingine tofauti na familia ya Mathias.



    Baada ya kubembelezwa na kuombwa sana, mwisho Nick akakubali kumsaidia Sala ili aweze kukutana na Mark, akainua simu yake ya mkononi na kumpigia Mark, alizungumza na Mark na kuomba nafasi ya kukuonana nae.

    "Amesemaje Mark!?" Sala alimuuliza Nick kwa shauku kubwa ya kutaka kujua.

    "Una bahati sana Sala, Mark yupo Dar es salaam na amekubali jioni ya leo tuonane."

    "Asante sana Nick, naomba jitahidi kunisaidia katika hili"

    "Usijali Sala, Mark ni mwelewa sana na naamini atakusamehe tu" alizungumza Nick na kuzidi kumpa matumaini Sala.



    Baada ya kupata kila kitu na kuwa na uthibitisho wote, Mark akaamua kwenda sehemu za kisheria ili kusaidiwa kurejesha haki ya familia yake.Hasira ambayo ilikuwa juu yake Mark ilikuwa kubwa mno, hasa akifikiria vifo vya wazazi wake vilitokana na maisha magumu na ya kimaskini sana ambayo walikuwa wanaishi.Mark hakuhitaji kutoa msamaha katika lile japokuwa alikuwa akifahamu mmiliki wa mali zile ni Sala.Taratibu zote zilikaa sawa na ikapangwa siku ya pili, mmiliki wa mali zile kwasasa akamatwe na aweze kutoa maelezo juu ya uhalali wake katika umiliki wa mali zile.



    Ilipofika mida ya jioni, Mark akakutana na Nick kama walivyokubaliana, ili aweze kufahamu kitu cha muhimu ambacho Nick alimwambia anahitaji kumuonesha.Wakasalimiana kwa furaha na kuanza mazungumzo yao.

    "Umeahamisha makazi katika mji wa Dar es salaam!?"

    "Hapana Nick ila kuna mambo kidogo nimekuja kuyaweka sawa."

    "Oooh!, basi sawa hata hivyo umekuja muda muafaka"

    "Kwanini unasema hivyo kaka!?"

    "Mh!, we acha tu unaweza ukazani ni filamu ila kumbe ni hali halisi."

    "Unamanisha nini Nick kusema hayo"

    "Ni kuhusiana na Sala"

    "Sala!!, Sala yupi huyo!?" Aliuliza Mark kwa mshtuko.

    "Ni Sala wako huyo Mark, Sala ana matatizo makubwa kwasasa na msaada pekee uliobaki ni wewe Mark"

    "Mimi!?, Kivipi Nick"

    "Ngoja nikuelezee kidogo" alizungumza Nick na kumueleza Mark juu yaliyomkuta Sala.

    Yalikuwa ni mambo mazito ambayo Mark alipata kuyasikia, alishindwa kuamini kama kweli John ameweza kumgeuka Sala na kumdhurumu mali zote na kuzichukua yeye.

    "Ni kitu kigumu sana kwangu kuyamini hayo unayonieleza, inawezekana pengine Sala alikudanganya"

    "Hapana Mark!, niliyokueleza, yote ya ukweli na Sala anahitaji sana msamaha wako"

    "Nadhani unaelewa kwangu mimi ni ngumu sana kumsamehe Sala kwa yale aliyonifanyia na wala sitamani kabisa kuonana nae."

    " Mark, tazama jicho lako la huruma limuangaze binti huyu, nafahamu amekupa maumivu makali sana lakini huna budi ukatumia busara ya kumsamehe maana tayari dunia imeshamfunza." Alizungumza Nick na kuzidi kumuomba Mark aweze kutoa msamaha wake kwa Sala.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakiwa katika maongezi hayo, Sala hakuwa mbali na maeneo yale, Nick akampa ishara na kumtaka ajisogeze pale walipo wao.Taratibu Sala akasogea hadi aliposimama Mark, kilio cha uchungu kilimtawala huku nafsi yake ikiendelea kujuta kila alipomtazama Mark kwa yale aliyomtendea.

    "Mark, tazama chozi la majuto jinsi linavyomdondoka mwanamke huyu, hakuna kigumu kisichowezeka kusameheka, kunjua nafsi yako rafiki yangu na upate kumsamehe binti huyu" alizungumza Nick, lakini Mark alibaki kuwa kimya tu.

    "Natambua moyo wako unasononeka sana kila unitazanapo, kweli mimi ni mkosefu na mtu nisiyestahili msamaha wako lakini nakiri makosa yangu kwako Mark, nisamehe ili nami nipate amani ya moyo" Alizungumza Sala na kuzidi kumuomba Mark aweze kumsamehe.



    Maneno matamu yaliopangika vizuri na ambayo yaliweza kupenya vilivyo katika masikio ya Mark, taratibu yakaanza kulegeza moyo wa Mark na huruma kumuingia kila alipomtazama Sala na hali aliyokuwa nayo.Akasogea karibu zaidi na alipo Sala, akainua mkono wake na kufuta chozi ambalo lilikuwa linatiririka katika uso wa Sala.

    "Kilio chako kimekuwa ni kama kengelea ambayo imenikumbusha wapi tulipotoka, hustahili kudondosha chozi lako tena kwasababu umetambua wapi ulipoteleza, nimekusamehe Sala."

    "Asante Mark, nashukuru sana kwa msamaha wako"

    "Ila kuna kazi moja naomba tushirikiane kuimaliza"

    Mark alimsamehe Sala na kumuomba msaada katika kulimaliza jukumu ambalo lipo mbele yake.



    Siku ya pili ikawadia, John akafikishwa katika vyombo vya sheria ili aweze kuhojiwa juu ya umiliki wa mali zakee, hisia zake zilimtuma aliyefanya yale atakuwa ni Sala lakini alipata mshangao na kustuka baada ya kufahamu aliye nyuma ya lile ni Mark na ndiye mtu aliyepeleka kesi mahakamani akidai kuwa amedhurumiwa mali zake.





    Kesi ilikuwa nzito sana huku John kwa upande wake akijitahidi kujitetea kuwa mali zile ni za kwake na alikabidhiwa na baba yake.Katika kulithibitisha lile, John alitoa nyaraka ambazo zinaonyesha uhalali wa umiliki wa mali zile.Nyaraka hizi John alizifoji akiamini zinaweza kumsaidia katika kushinda kesi ile.Pia akatengeneza baadhi ya mashahidi wake wa uongo na kuja kuthibitisha mbele ya mahakama kuwa mali zile ni za John na wao walikuwepo wakati anakabidhiwa na baba yake.

    Kwa upande wa Mark, yeye alitoa nyaraka halisi ambazo zilikuwa zinaonyesha mmiliki wa mali zile alikuwa ni baba yake mzazi kabla ya kudhurumiwa na Mathias.Katika kulithibitisha lile, Mark akamkaribisha shahidi wake wa kwanza ambaye alikuwa ni Sala.Sala alithibitisha kuwa mali zile ni za Mark na yeye alizichukua kutoka kwa baba yake pasipo kujua si mmiliki halali wa mali zile.Baada ya Sala Mark akamkaribisha shahidi wake wa pili ambaye alikuwa mzee Alfred, mzee Alfred naye alithibitisha anachokifahama na mwisho Mark akachukua nyaraka zake na kukabidhi mbele ya mahakama.

    Baada ya mahakama kupitia vizuri juu ya nani mmiliki halali wa mali zile, mwisho wakatoa maamuzi ya kuwa mwenye uhalali wa kuchukua mali zile ni Mark kwasababu baba yake ndiye aliyekuwa mmiliki halali kutokana na uthibitisho uliokuwepo.John akapewa hukumu ya kifungo cha maisha jela kwa kosa la kudhurumu mali za watu na kosa lingine la kushiriki katika mauaji wakati anaandaa ushahidi wake.



    Lilikuwa jambo la furaha sana kwa Mark kwa kuweza kushinda kesi ile na kuipata haki ya familia yake.Kampuni, nyumba na miradi mbalimbali vyote vilirudi mkononi mwake na kuwa chini yake.Katika kulisherekea lile, Mark akamchukua Sala na kutafuta sehemu nzuri ili waweze kukaa na kufurahia pamoja na kupongezana kwa kazi nzuri waliyoifanya mpaka kuishinda kesi ile.

    "Hongera sana Mark na pia napenda kuomba radhi kwa niaba ya familia yangu kwa ubaya wote ule waliotenda katika familia yako."

    "Ondoa shaka Sala, mimi kwa sasa naangalia yajayo na siyo mambo ambayo yalishapita."

    "Asante Mark kama umeweza kulitambua hilo na kuisamehe familia yangu." Alijibu Sala na kumshukuru Mark.Ukimya kidogo ulitawala huku kila mmoja akiwa ameshiwa cha kuzungumza, mwisho Sala akaamua kuvunja ukimya na kuanzisha mazungumzo kwa mara nyingine.

    "Naweza kukueleza kitu Mark!?" Aliuliza Sala.

    "Nieleze tu Sala"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mimi na wewe ni watu ambao tumepitia na kufanya mambo mengi tukiwa pamoja, hivi unaonaje kama tukaweza kurudisha mahusiano yetu ya kipindi kile" Aliongea Sala na kumueleza Mark.

    "Ni jambo gumu sana kwangu kuweza kulikubali hilo Sala!?"

    "Kwanini Mark!?"

    "Kwasababu ndani ya moyo wangu yupo mtu mwingine ambaye nimempa nafasi kubwa sana"

    "Hapana Mark, kwani wewe umesahau tulipotoka!?"

    "Mapenzi ni sawa na upofu ambapo wapo watu na wengine kuyangia, hilo ni jambo ambalo halitowozekana kabisa kutokea upande wangu, zaidi ninachoweza kukusaidia ni kukukabidhi mali zote hizi alozokuwa amezichukua John mikononi mwako, Natumaini huu utakuwa msaada tosha ambao utakusaidia kuweza kuyaendesha maisha yako." Alizungumza Mark na kueleza msimamo wake mbele ya Sala.



    Kitendo cha Sala kugusia masuala ya kimapenzi, kilimfanya Mark kumkumbuka sana Jane, akainua simu yake na kujaribu kumtafuta kupitia simu yake ya mkononia, lakini namba ya Jane ilikuwa haipatikani.Mawazo yalikuwa mengi sana kwa Mark kwa kushindwa kufahamu ni kipi kilichomsibu Jane mpaka ashindwe kumpata katika simu yake tangu afike katika mji wa Dar es salaam. Hali ile aliyokuwa nayo Mark, ikamfanya Sala kuhisi kitu kuigundua.



    "Mark!, Mark!, Mark...!?" Sala alimuita Mark zaidi ya mara tatu.

    "M..m!..ndio Sala"

    "Uso wako mbona unaonesha upo katika dimbwi zito la mawazo, nini tatizo!?"

    "Hakuna tatizo Sala ila kwasasa nahitaji kwenda kupumzika"

    "Mark ila naomba jitahidi kuliweka akilini hili nililokueleza, nakuhitaji sana" alizungumza Sala na kumuomba Mark abadilishe msimamo wake.

    Wakati Sala akiendelea kuomba nafasi nyingine kwa Mark, Mark alistuka na kushangaa baada ya kutupa macho yake mbele, alimuona Jane akiwasili eneo lile.Maswali mengi alijiuliza Mark, Jane amewezaje kufika pale alipo wao na lini amekuja katika jji la Dar es salaam, huku wasiwasi pamoja na hofu vikaanza kumuingia Mark akidhani pengine Jane anaweza kuhisi kitu tofauti kati yake na Sala.Jambo ambalo lilizidi kumshangaza Mark, Jane alionekana akitabasamu tena akija upande walipo wao.Licha ya yote hayo, Mark akashindwa kuficha hisia zake kwa jane, mbele ya Sala akasimama ili aweze kumkumbatia na kumkaribisha eneo lile.Sala akibaki katika mshangao na kujiuliza ni kipi Mark anachotaka kukifanya.

    Mark akasogea karibu zaidi ili aweze kumpokea Jane, lakini wakati anataka kumkumbatia akashangaa akipokea na kuadhibiwa kibao cha uso na Jane.







    "We kaka vipi, unanifahamu mimi!?"

    "Maswali gani hayo unaniuliza Jane!?"

    "Jane!, nani amekwambia mimi naitwa Jane!?"

    "Kwani hunitambui mimi Jane!, na umekuja lini hapa Dar es salaam"

    "Samahani kaka, jina langu naitwa Scola na sio hilo Jane, naomba jiheshimu na ujichunge sana" Alijibu yule dada na kuondoka.Sura, umbo na hata tembea yake dada yule, halikuwa hana utofauti kabisa na Jane.Hii ilimfanya Mark kushindwa kuamini kabisa kama yule sio Jane wake, akamkimbilia na kumfuata tena ili aweze kumuuliza vizuri, lakini dada yule aliendelea kusisitiza kuwa yeye haitwi Jane bali jina lake ni Scola.Sala akasimama na kumfata Mark ili aweze kumtuliza na kumuelewesha.

    "Mark, tafadhali jaribu kuwa muelewa, inawezekana huyu siye mtu huyo unayemdhania pengine amefanana nae tu."

    "Hapana Sala!, nina uhakika kabisa yule ni Jane, ila nashindwa kuelewa kwanini ananigeuka!?" Alizungumza Mark kwa uchungu mkubwa huku machozi yakimdondoka.Chozi la Mark pia lilikuwa ni kama kisu cha moto ambacho kilienda kumchoma na kumpa maumivu makali moyoni mwake, alijisikia vibaya sana Sala, aliona jinsi gani Mark anampenda Jane mpaka kufikia hata ya kudiriki kudondosha chozi kwa ajili yake. Mawazo yalikuwa mengi sana kwa Mark, akatoka na kumuacha Sala mahali pale na kwenda hadi katika fukwe moja ya bahari ili aweze kutuliza kichwa chake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akiwa katika ufukwe, huku akiangalia kupwa na kujaa kwa maji, Mark aliendelea kujiuliza maswali mengi sana huku nafsi yake ikiumia kwa kudhani pengine Jane ameamua kumsaliti ndio maana alikataa kujitambulisha kwake mbele ya Sala. Akiwa katika hali hiyo ya kujiuliza maswali mengi na yasiyo na majibu, mara Jane anafika mahali pale.Akili yake Mark moja kwa moja ikamtuma kuwa amuonaye pale ndiye Jane na akihisi pengine amekuja kumuomba msamaha kwa lile alilolifanga alimkaribisha na kuketi ili waweze kuongea.

    "Kwanini uliamua kunifanyia vile Jane!?" Mark alimuuliza Jane.

    "Hapana Mark, yule uliyemuona pale sio Jane, bali ni muhusika halisi." Alizungumza Jane na kumshangaza Mark kidogo.

    "Unamaanisha nini Jane, mbona unazidi kunichanganya!?"

    "Mark, yule uliyemuona mwanzo ndiye Jane halisi ila mimi nilivaa uhusika wake ili nitimeze jukumu nililopewa"

    "Jukumu..!!!, jukumu gani hilo Jane!?" aliuliza Mark kwa mshangao kidogo.

    "Mark, hakika nimeamini mapenzi ni sawa na mawimbi mazito ya bahari ambapo mwenye ufundi wa kuogelea huweza kuyamudu na asiye na ufundi hujikuta akizama katika mawimbi yale na kushindwa kutimiza majumu yake.Mark, Mimi sio binadamu halisi na wala makazi yangi sio hapa duniani bali nilikuja hapa duniani kwa ajili ya kutafuta sadaka." alizungumza Jane na kumfanya Mark ashtuke kidogo.

    "Mimi ni jini Mark na nilikuja hapa ili nitafute mtu wa kumtoa sadaka, lakini kwasababu yako umenifanya kutambua thamani ya nafsi ya mtu ambayo ingenililia kipindi chote cha maisha yangu, sasa narudi nyumbani kulitimiza jukumu hili mwenyewe na nakutakia maisha mema na natumaini utampata mtu wa ukweli kabisa atakayekupenda, kwaheri Mark ila nitakukumbuka daima" Alizungumza kwa uchungu Jane sana huku machozi yakimtiririka machoni mwake.

    "Hapana!, Hapana Jane unaniongepea!, mimi nitakupenda kwa vyovyote vile, tafadhali usifanye hivyo....!!" Mark alizidi kulalamika na kutoamini kabisa yale aliyoelezwa, lakini ule ndio ulikuwa ukweli halisi, Jane hakuwa binadamu kama watu wengine bali ni mtu wa dunia nyingine kabisa.



    Usingizi mzito bila kutambua wapi ulipotokea ukamchukua Mark pale alipoka na kulala zaidi ya nusu saa na alipokuja kuzinduka hakuweza kumuona Jane mahali pale, alijitahidi kuhangaika kumtafuta huku na kule pale ufukweni huku akililita jina lake, lakini tayari Jane alikuwa tayari ameshaondoka na kurudi katika makazi yake halisi.

    Huzuni ilikuwa imemtawala sana Mark, maana kwa kipindi kirefu alijitahidi sana kumtafuta Jane lakini akashindwa kufanikiwa kumpata wala kufahamu mahali alipo.Mwisho akaamua kukubaliana na hali halisi iliyotokea japokuwa ilikuwa ngumu sana kuweza kumsahau binti yule katika kumbukumbu zake.Mark hakuona sababu ya kuendelelea kuishi Tanzania kwasababu kitendo cha kumpoteza Jane, moyoni mwake lilikuwa pigo kubwa sana hivyo akaamua kwenda kuanzisha maisha yake katika nchi nyingine kabisa ili aweze kusahau yale yote yaliotokea katika maisha yake.



    Siku, miezi na sasa takribani miaka mitano ilipita, Sala tayari alikuwa ameshajifungua mtoto wa kiume na kwasasa mtoto yule alikuwa na umri wa miaka minne na alimpa jina la Mark.Maisha yake aliweza kuyamudu kupitia mali ambazo aliachiwa na Mark pia mkononi mwake tayari alishavishwa pete ya ndoa.

    Siku moja Sala akiwa nyumbani, mara analetewa bahasha na kupewa maelezo kuwa aliyetuma bahasha ile anaishi London nchini Uingereza.Baada ya kufungua ile bahasha, Sala akakuta paspoti tatu za kusafiria na kukuta kadi ya mwaliko wa ndoa.

    Mark alikuwa anajiandaa kufunga ndoa na binti mmoja ambaye ni maarufu sana duniani kwa kazi ya uwanamitindo na jina lake aliitwa Scola Darmian na ndiye binti ambaye alitokea kufanana sana na Jane.



    Sala akafurahi sana baada ya kupata taarifa ile, akaongozana na familia yake yote na kuelekea nchini Uingereza kwa ajili ya kuhudhuria katika ndoa ile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MWISHO



    Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa ambao tuliweza kuambatana pamoja katika kuifatilia simulizi hii.Napenda kujua kipi kimekugusa na kujifunza kupitia simulizi hii, pia unaweza ukacha maoni na ushauri wako hasa zaidi katika mapungufu uliyaona ili niweze kufanya maboresho katika simulizi zinozofata.



0 comments:

Post a Comment

Blog