Search This Blog

VITA YA WACHAWI - 1

 





    IMEANDIKWA NA : ALLY MBETU 



    *********************************************************************************



    Simulizi : Vita Ya Wachawi

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    TUMESHUHUDIA Wachawi wakiwatesa watu wasio na hatia hata kuanzisha vita na waganga wa jadi ambao hujitolea kuwasaidia waliowaroga kuwaondolea mateso mazito kutokana na kutupiwa uchawi ambao huwatesa katika maisha yao yote. Tumeshuhudiwa



    vifo vya ghafla vya watu na baadaye kusikika wameonekana sehemu fulani wakiwa hai au wamegeuzwa msukule.



    Wachawi siku zote wamekuwa na umoja katika mambo yao ikiwa na kujenga chama cha pamoja chenye nguvu huku kila mwanachama akichangia mtu mmoja ambaye huwa kitoweo chao. Pia wamekuwa wakishirikiana katika kumsaidia mwenzao anapoingiliwa na nguvu za kiroho au za dawa za jadi kuhakikisha wanapambana nao mpaka tone la mwisho la damu yao.



    Lakini nao huingia vitani baada ya mmoja kuonekana anajifanya anajua au kuingilia kazi ya mwenzake au mmoja kutaka kumpima mwenzake. Hapo hutokea vita kubwa ambayo hugawa makundi kwa kila moja kusaidia upande wake ndipo panapokuwa hakuna cha kumsalia mtume.



    Mapenzi ya watu wawili yamefanya Vijiji vya Ibungu, Mbako, Kilasilo mpaka Isaki katika Wilaya ya Ileje mkoani Mbeya kuingia katika vita kubwa ya kichawi kwa maeneo hayo kuoneshana ubabe. Hukuwepo malaika wako alikuwepo. TEREMKA NAYO.



    Pamoja na mvua kali ya radi kuendelea kunyesha, Ambakisye na Atuganile hawakutoka porini walijificha chini ya mti kwa vile muafaka ulikuwa bado haujapatikana. Mvua iliendelea kunyesha na radi za kutisha zilipiga, Atuganile aliendelea kulia machozi ambayo hayakuonekana kutokana na kusafishwa na mvua.



    "Ambakisye mpenzi wangu, hebu jifikirie wazazi wangu hawatanielewa kabisa."



    "Atu unajua kabisa tatizo lipo wapi, mimi kama mimi sina uamuzi wowote, nimewaeleza lakini wamekataa."



    "Umewaeleza na hali yangu?"



    "Nimewaeleza lakini wamekataa kwa vile tayari walikuwa wameisha nitafutia mwanamke wa kuoa."



    "Ambakisye nilikueleza mapema kuhusu hili na ulinikubalia lakini leo unanigeuka?"



    "Atu siyo mimi ni wazazi wangu ndiyo walioamua hivyo, siwezi kwenda kinyume nao."



    "Na hii hali nifanyeje?" Atuganile alisema huku akionesha tumbo lake lililokuwa na ujauzito wa miezi mnne wakati huo mvua ilikuwa ikiendelea kuwalowesha chapachapa .



    "Basi tuitoe."



    "Siwezi kuua mwanangu kwa ajili ya ujinga wa wazazi wako, Ambakisye wewe ndiye muamuzi wa mwisho kumbuka nimekataa wanaume wangapi kwa ajili yako hata wazazi



    wangu wanajua wewe ndiye mume wangu, unafikiri watapokeaje taarifa hii. Nimewaficha toka uliponieleza, nimekuwa nalia kila nikiwa peke yangu ili wazazi wangu wasijue kitu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “ Ambakisye wazazi wangu nawajua vizuri, nikiwaeleza wanaweza kukufanya kitu kibaya, hebu kaa na wazazi wako waeleze kuwa mimi ndiye chaguo lako na haupo tayari kumuoa mwanamke mwingine!” “Hawezi kukubali kwa vile tayari wameshapeleka posa, kilichobakia ni ndoa tu.”



    “Amba wazazi wako wasijejilaumu kwa uamuzi wao wa kikatili nikitoka hapa naenda kuwaeleza wazazi wangu, naogopa watakachokifanya kwa vile hawatakubali. Nataka kukuhakikishia hutamuoa huyo mwanamke.” “Sina jinsi kawaeleze litakalotokea watakuwa wamelitaka.”



    Kwa vile muda ulikuwa umekwenda sana, giza nalo lilikuwa limeanza kuingia. Ambakisye na Atuganile ambao walikwenda porini tangu asubuhi ili kulijadili jambo lile ambalo lilimuumiza sana Atuganile.



    *** Miaka mitatu nyuma katika Kijiji cha Ibungu katika Wilaya ya Ileje, Ambakisye na Atuganile walianzisha uhusiano wa kimapenzi ambao ulifahamika kwa familia zote mbili.

    Lakini familia ya mzee Amangise anayotokea Ambakisye ilikuwa na chaguo lao lingine bila kumueleza mtoto wao.

    Ila familia ya mzee Andendekisye anayotoka msichana Atuganile walijua kabisa mtoto wao ataolewa na



    Ambakisye hata waliposikia mtoto wao mjamzito, hawakuwa na wasiwasi zaidi ya kujiandaa kwenda kwenye familia ya mzee Amangise kupanga jinsi ya watoto wao kuoana.

    Atuganile, akiwa na furaha ya kupata ujauzito, alikwenda kwa mpenzi wake kumueleza hali yake ya ujauzito. Mwenzake alipokea taarifa hiyo kwa furaha na kumweleza kuwa atakwenda kuwaeleza wazazi wake ili wapange mipango ya ndoa yao.



    Lakini ilikuwa tofauti kwa wazazi wa Ambakisye baada ya kuwaeleza hali ya mpenzi wake, alishangaa wazazi wake kumueleza habari nyingine kuwa wao tayari wamemchagulia mke ambaye muda huo walikuwa tayari wametoa posa na siku iliyokuwa inafuata ilikuwa ndiyo ya kwenda kujitambulisha.



    Ambakisye alichanganyikiwa kutokana kauli ya wazazi wake na kuwaeleza kuwa mchumba wake tayari ni mjamzito. Lakini walimweleza kuwa hawawezi kubadili uamuzi kwa vile tayari walishatoa posa. “Wazazi wangu mbona mnanifanyia ukatili? Mnajua kabisa Atu ni mpenzi wangu na sasa hivi ana ujauzito wangu. Nitaieleza nini familia yao wakati niliwathibitishia kumuoa binti yao?”



    “Imeanza lini mtoto kujitafutia mwanamke wa kuoa?” Wazazi wake walimuuliza. “Lakini wazazi wangu mnajua kila kitu, kwa nini mmefanya hivyo?” “Tumeshaamua jiandae na kesho asubuhi tuna safari ya Kilasilo ukweni kwenda kujitambulisha.” “Wazazi wangu japokuwa mimi ni mtoto wenu lakini hamkunitendea haki, mlitakiwa kunishirikisha kwanza.”



    “Sisi wazazi ndiyo wenye haki kukutafutia mchumba kutoka katika familia bora si mke bora mke.” “Mmh! Sawa.” Ambakisye hakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana nao kwa shingo upande, lakini alijua ana kazi kubwa ya kumweleza mpenzi wake taarifa ile nzito itakayoujeruhi moyo wake. Siku ya pili alipelekwa Kijiji cha Kilasilo ukweni kutambulishwa kwa wazazi wa mchumba wake, mtoto wa familia ya mzee Ambokile.



    Baada ya kufika huko Ambakisye alikutanishwa na mchumba wake aliyechaguliwa na wazazi wake. Alikuwa ni binti mzuri, lakini hakuwa chaguo lake kwa vile tayari alikuwa na mpango wa kuoana na Atuganile. Siku hiyo ilifanyika sherehe kubwa na kuchinjwa ng’ombe na pombe kunywewa kwa wingi.

    Jioni walirudi kijiji kwao kwa ajili ya maandalizi ya harusi wa mtoto wao, Ambakisye hakulala pamoja na kwamba ulikuwa usiku mnene, alikwenda kwa mpenzi wake kumweleza kilichotokea siku ile. Alikuta familia ya mzee Andendekisye ilishalala.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa vile chumba cha mpenzi wake alikijua alikwenda kugonga. Baada ya muda alisikia sauti ya Atu ikiuliza: “Nani?” “Mimi Amba.” “Ooh! Mpenzi wangu, leo ulienda wapi maana nilikutafuta sana,” Atu alisema huku akifungua mlango na kutoka nje.



    “Nilitoka na wazee kidogo.” “Mmh! Umerudi saa ngapi?” “Hata dakika tano hazijakatika.” “Za huko?” “Nzuri, mbaya.” “Uzuri wake nini na ubaya wake nini?” “Uzuri tumekwanda salama tumerudi salama.” “Ubaya?” Atu alimuuliza huku akimtazama usoni akisaidiwa na mwanga wa mbalamwezi uliokuwa ukiwaka sana. “Ubaya wake, safari niliyopelekwa ilikuwa kwenda kuoneshwa mchumba.”



    “Mchumba! Hapo sijakuelewa unamaanisha nini?” Atu alimsikia lakini hakumuelewa. “Wazazi wangu wamenipeleka Kijiji cha Kilasilo kunitafutia mchumba.”







    “Wewe uliwaambiaje?”

    “Niliwashangaa kwa vile wanajua wewe ni mchumba wangu.”

    “Au hujawaeleza hali yangu?”

    “Niliwaeleza lakini waling’ang’ania uamuzi wao.”

    “Mmh! Amba hili siwezi kuwaeleza mapema wazazi wangu, naomba ukakae tena na wazazi wako uwaeleze mimi na hali hii nitaolewa na nani?”

    “Acha nijaribu lakini nina kazi kubwa.”

    “Jaribu nina imani watakuelewa.”

    “Haya mpenzi wangu usiku mwema.”

    Baada ya Ambakisye kuondoka Atuganile alibakia amesimama mlangoni akiwa haamini taarifa zile, alijiuliza Ambakisye alikuwa akimtania au nini! Baada ya kupigwa sana na baridi alirudi ndani na kujilaza. Bado usingizi ulikuwa mbali kwa mawazo, alitoka nje kwenda kumuuliza Ambakisye alichokisema ni kweli au anamtania.

    Pamoja na hali ya usiku ilikuwa imetulia lakini muda ule ilikuwa ikitisha kutokana na wazazi wa watoto pale kijijini waliwakataza watoto wao kutembea usiku.

    Pamoja na woga wa Atu lakini asingelala mpaka apate ukweli wa maneno ya Ambakisye alichomueleza ni kweli au anamtania. Upepo wa usiku ulivuma kuongeza ukali wa baridi, alitembea huku mapigo ya moyo yakiwa juu. Kila aliposikia sauti tofauti aligeuka kuangalia nyuma huku akiongeza mwendo.

    Alifika nyumbani kwao Ambakisye, alikuta wazazi wake hawajalala lakini wamo ndani kutokana na kusikia wakiongea. Alinyata kusogea katika chumba cha mpenzi wake na kugonga dirisha huku akiita “Amba…Amba.” Ambakisye alishtuka kusikia sauti ya mpenzi wake.

    “Atu!” alishtuka.

    “Abee.”

    “Vipi mbona tena huku?”

    “Amba bado sijaelewa.”

    “Hujaelewa nini mpenzi wangu?”

    “Uliyosema ni kweli au unanitania?”

    “Atu ni kweli kabisa siwezi kukutania.”

    “Mmh! Sawa.”

    Atuganile alisema huku akigeuka kuelekea kwao huku akilia, Ambakisye alitoka na kumfuata kumbembeleza.

    “Atu usilie, si umenipa kazi ya kuzungumza na wazazi wangu basi tusubiri.”

    “Basi naomba asubuhi uzungumze nao ili saa nne nipate jibu.”

    “Sawa.”

    Ambakisye alimsindikiza mpenzi wake mpaka kwao na kurudi kulala.

    ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakukuwa na mabadiliko yoyote toka kwa wazazi wa Ambakisye zaidi ya kusimamia msimamo wao. Atuganile siku ya tatu alimpitia mpenzi wake kwao asubuhi sana na kwenda naye porini ili wakayazungumze kwa kina. Baada ya kufika porini ambako waliingia ndani sana wakiamini watakuwa peke yao.

    Wakiwa katikati ya mazungumzo wingu zito lilianza kutanda kitu kilichofanya Ambakisye amweleze Atuganile warudi kijijini.

    “Atu wingu linaonesha mvua kubwa inashuka tuondoke mpenzi wangu.”

    “Amba kwani mvua ikishuka kuna nini?”

    “Inaweza kuwa kubwa na kutudhuru.”

    “Kifo cha kunyeshewa na mvua si kikubwa kama familia yako ilivyoupasua moyo wangu bila ganzi.”

    “Kwa hiyo?”

    “Hata kama wazazi wako wameamua lakini nataka msimamo wako wewe juu yangu?” Atuganile alimkazia macho Ambakisye.

    “Mimi nakupenda wewe.”

    “Upo tayari kusema hivyo kwa wazazi wako?”

    “Ndiyo.”

    “Huwezi kuamini toka siku ile sijaieleza familia yangu, najua kwa jambo kama hili lazima tutajenga uadui mkubwa ambao unaweza kuleta maafa makubwa,” Atuganile alimtahadharisha Ambakisye.

    “Hata mimi najua, lakini wazazi wangu wanajifanya wameweka pamba masikioni.”

    Mvua ilianza kuteremka na kuwafanya wasogee chini ya mti mkubwa kujikinga japokuwa wasingeizuia kutokana na kasi yale iliyoteremka nayo. Atuganile pamoja na woga wa mvua lakini katika kuyatetea maumivu ya moyo wake hakuogopa kitu. Waliendelea kulowa huku radi na miungurumo mikubwa ikiendelea kulindima angani.

    Kutokana na mvua kuwa kali iliyoambatana na upepo baadhi ya miti ilianza kukatika na kuzidi kuwatia hofu ya kutoka eneo lile salama.

    “Amba, achana na mvua hebu niangalie upande wangu nitasimama wapi, wazazi wangu watapokea vipi habari za kushtua kama hizi?” Atuganile alisema kwa sauti ya kilio.

    “Kwa kweli wazazi wangu hata mimi hawakunitendea haki.”

    “Ambakisye hebu jifikirie mara mbili mpenzi wangu wazazi wangu nawajua mimi naogopa kutokea matatizo mazito hasa kwako mpenzi wangu.”

    “Atu, unajua kabisa tatizo lipo wapi, mimi kama mimi sina uamuzi wowote, nimewaeleza lakini wamekataa.”

    “Umewaeleza na hali niliyonayo kwa sasa?”

    “Nimewaeleza lakini wamekataa kwa vile tayari walikuwa wameishanitafutia mwanamke wa kuoa.”

    “Ambakisye nilikueleza mapema kuhusu hili na ulinihakikishia utanioa lakini leo unanigeuka?”

    “Atu siyo mimi ni wazazi wangu ndiyo walioamua hivyo siwezi kwenda kinyume.”

    “Na hii hali nitafanyaje?” Atuganile alisema huku akionesha tumbo lake lililokuwa na ujauzito wa miezi minne wakati huo mvua ilikuwa ikiendelea kuwalowesha chapachapa .

    “Basi tuitoe.”

    “Siwezi kuua mwanangu kwa ajili ya wazazi wako, Ambakisye wewe ndiye muamuzi wa mwisho kumbuka nimekataa wanaume wangapi kwa ajili yako wazazi wangu wanajua wewe ndiye mume wangu unafikiri watapokeaje taarifa hii. Nimewaficha toka uliponieleza nimekuwa nalia kila nikiwa peke yangu ili wazazi wangu wasijue kitu.





    "Ambakisye wazazi wangu nawajua, nikiwaeleza wanaweza kukufanya kitu kibaya, hebu kaa na wazazi wako waeleze kuwa mimi ndiye chaguo lako."

    "Hawezi kukubali kwa vile tayari wameshapeleka posa, kilichobakia ni ndoa tu."

    "Amba wazazi wako wasije kujilaumu kwa uamuzi wao wa kikatili, nikitoka hapa naenda kuwaeleza wazazi wangu."

    "Sina jinsi, kawaeleze."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa vile muda ulikuwa umekwenda sana, giza nalo lilikuwa limeanza kuingia. Ambakisye na Atuganile walirudi kijijini, wakati huo mvua zilikuwa zimebaki za rasharasha.

    ***

    Atuganile alirudi nyumbani kwao huku macho yamemvimba kwa kilio, alipofika nyumbani alimkuta mama yake yupo nje, baada ya kumsalimia aliingia ndani moja kwa moja chumbani kwake. Mama yake alishtuka na kuacha kazi zake na kumfuata, alipoingia chumbani alishangaa kumkuta mwanaye amekaa chini kichwa amekilaza kitandani mikono kichwani.



    Kitendo kile kilimshtua sana mwanaye, kurudi amelowa, tena akiwa amechelewa bila kujua siku ile alikwenda wapi, japokuwa hawakuwa na wasiwasi kwa kujua yupo na mpenzi wake Ambakisye.

    "Atu," alimwita kwa sauti iliyomshtua mwanaye ambaye alikimbiza mkono kwenye macho kufuta machozi.

    "Abee mama," alijitahidi kuitika vizuri lakini sauti ilionesha alikuwa akilia.

    "Kuna nini mwanangu, kwanza umeondoka alfajiri umerudi umenyeshewa na mvua, umefikia kulia, kuna nini?"

    "Mama, hata sijui nikueleze nini unielewe."

    "Niambie tu mwanangu nitakuelewa tu."



    Atuganile alimueleza mama yake yote aliyoelezwa na mpenzi wake juu ya wazazi wa Ambakisye kumtafutia mtoto wao mchumba mwingine. Kauli ile ilimshtua mama yake na kutaka ufafanuzi zaidi.

    "Wamemtafutia mwanamke mwingine, ulikataa kuolewa?"

    "Hapana, anasema hata yeye alikuwa hajui kitu."

    "Yeye kasemaje?"

    "Japokuwa hakuafiki kitendo cha wazazi wake lakini hawezi kupinga."

    "Na hali hiyo?" Alimuuuliza kuhusu ujauzito.

    "Amenishauri niitoe."

    "Akaja na mahala, usosye ulwanda? Ikulonda mwisukulu gwangu afwe?" (Hana akili, utoe mimba, anataka mkujukuu wangu afe?)

    "Unasema wamesema wazazi wake?"

    "Anatutania."

    "Kweli mama, Jumapili walikwenda kutambulishwa ukweni."

    "Mmh! Sawa, tuachie kazi hiyo naona hawatujui."

    "Lakini mama msimfanye Ambakisye kama John."

    "Wao si wamekuona hufai, basi tutaoneshana kazi."



    (John ni mvulana aliyeanza naye mapenzi, lakini alikwenda jijini Dar na kupata mwanamke mwingine na kumuoa, alipoulizwa alionesha dharau. Haukuchukua mwaka, alipata ajali mbaya akiwa na familia yake iliyochukua maisha yao, ikiwa mkono wa wazazi wa Atuganile.) Mwanzo wa mapenzi kabla ya kumkubali alitaka kuhakikishiwa kuolewa.



    Ambakisye alimhakikishia kumuoa ndipo Atuganile alipomkubali na penzi lao lilijulikana kijijini kwa kila mmoja kuamini wawili hao wataoana. Kukataliwa kwa Atuganile kulimchanganya sana na kuwa na wasiwasi na uamuzi wa familia kwa kuamini maisha na mpenzi wake yatakuwa hatiani.



    Mama Atuganile alikwenda kwa mumewe aliyekuwa akirekebisha banda la nyumba sehemu iliyokuwa ikivuja mchana. Alimuomba waingie ndani, mzee Andendekisye aliingia ndani kumsikiliza mkewe, kwa vile nguo zilikuwa zimelowa maji alisimama wima kumsikiliza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Unasemaje mama Atu?"

    "Leo familia ya Amangise imenikata maini," alisema akishika mkono kiunoni.

    "Kuna nini?"

    Alimueleza yote aliyoelezwa na mwanaye, baada ya kumsikiliza alisema:

    "Aliyesema hayo ni wazazi au Ambakisye?" Alimuuliza mkewe.

    "Ambakisye lakini yamesemwa na wazazi wake."

    "Kwa vile kesho tulipanga kwenda kwao kwa ajili ya kuzungumzia hali ya mwenetu, nina imani kila kitu kitajulikana."

    "Naona wamenisahau, nitaisambaratisha familia yote, nyumba ibakie gofu."

    "Usiwe na haraka ya kufanya lolote, yote tutajua kesho."

    "Yaani nilivyokasirika, Ambakisye jua la kesho asingeliona."

    "Usiwe na pupa, twende kwanza tukawasikilize."

    "Yaani bila wewe sijui ingekuwaje?" Mama Atuganile alisema huku akitweta.



    Mama Atuganile jazba ilikuwa juu, siku zote mumewe alimshusha bila hivyo uamuzi wake huwa mbaya. Hata kifo cha John hakumshirikisha mumewe, alifanya mwenyewe, jibu lilikuwa baada ya tukio ndipo alipoielezea familia yake kuwa yeye ndiye aliyetenda.



    Baada ya kukubaliana, alirudi chumbani kwa binti yake na kumueleza asiwaze sana kwani kesho wanakwenda kusikiliza kauli ya familia ya mzee Amangise.

    ****

    Siku ya pili, mzee Andendekisye na mkewe walikwenda nyumbani kwao Ambakisye, walipofika walipokelewa vizuri. Kama zilivyo mila na desturi, walikaribishwa pombe ya chimpumu kwenye kopo kubwa la plastiki la lita moja.

    "Jamani karibuni sana."

    "Asante."



    Baada ya kunywa kidogo, hawakutaka kupoteza muda, walisema kilichowapeleka pale.

    "Jamani si wakaaji sana, kuna jambo limetuleta," alisema mzee Andendekisye.

    "Ndiyo, jambo gani?" Aliuliza mzee Amangise.

    "Nina imani unajua uhusiano wa vijana wetu wawili, Ambakisye na Atuganile."

    "Ndiyo."

    "Jana usiku kaja binti yetu kutueleza jambo ambalo kwa kweli limetushtua sana."





    "Jambo gani?"

    "Kuwa Ambakisye anataka kuoa mwanamke mwingine."

    "Ni kweli Ambakisye anataka kuoa mwanamke mwingine toka Kijiji cha Kilasilo."

    "Sasa wazazi wenzetu kwa nini mmechukua hatua hiyo wakati mnajua uhusiano wa vijana wetu?" aliuliza mzee Andendekisye kwa sauti ya utulivu.

    "Unajua mzazi humtafutia mtoto wa kiume mwanamke wa kuoa, na si kijana kutafuta mwenyewe. Sisi tuliishamtafutia mtoto wetu mwanamke wa kumuoa muda mrefu ilibakia kujitambulisha tu," alijibu mzee Amanyise.

    "Kama mlijua hivyo kwa nini hukumkataza mwanao asimpotezee muda mtoto wetu?" mama Atuganile alimwuliza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nilijua ni urafiki wa kawaida si wa kuwa mke na mume kwa vile sote tunajua mtoto wa kiume hutafutiwa mchumba na wazazi wake kama wakiwa hai," alijibu mama Ambakisye.

    "Kwa hali ya mtoto wetu itakuwaje?" (akimaanisha ujauzito wa Atuganile)

    "Hilo si juu yetu mwanenu alitakiwa kuwa makini kwa vile hatukuwa na makubaliano ya kumuoa."

    "Kwa hiyo tutamfanyaje na mwanenu ndiyo kisha mharibu mtoto wetu?" mama Atuganile aliuliza.

    "Kwa vile ujauzito ni wetu tutaulea akijifungua tutachukua mtoto."

    "Kwa hiyo mmeamua kumuharibia binti yetu maisha?" mama Atuganile aliuliza huku mumewe akiwa kimya akitafakari majibu ya wazazi wenzao.

    "Tumemuharibia kivipi?" mama Ambakisye aliuliza yakabaki majibizano ya kina mama.

    "Nani atakayemuoa wakati wakijua amezaa na fulani tena wa kijiji hikihiki, lazima watamtia kasoro mtoto wetu kuwa amezalishwa na kutelekezwa na kuolewa binti wa mbali."

    "Sisi hayatuhusu, kama hivyo tuutoe ujauzito kabla haujajulikana."

    "Kweli hamna huruma mnataka kuniulia mjukuu wangu?" mama Atuganile alikuja juu.

    "Si ili mtoto wetu apate mchumba," mama Ambakisye alijibu kwa mkato.

    "Jamani tusije kulaumiana kama mumeamua kumharibia maisha mwanetu."

    "Hilo mnajua nyie mlitakiwa kumkanya mtoto wenu kabla ya ndoa."

    "Mmh! Sawa," mzee Andendekisye alinyanyuka kwa hasira na kumshika mkono mkewe na kuondoka huku akigonga meza iliyokuwa na pombe iliyosababisha kumwagika, hawakugeuka waliondoka huku wakizungumza kwa hasira.

    ***Atuganile aliyekuwa amebakia nyumbani akiwa na shauku ya majibu ya familia ya mpenzi wake kwa wazazi wake. Akiwa amekaa uani aliwaona wazazi wake wakirudi huku mikono ikirushwa juu kuonesha walipotoka hapakuwa na maelewano.

    Moyo ulimuuma alijikuta akiwa na hamu ya kusikiliza kilichojiri walipokwenda. Baba yake alipofika alikaa chini hakuwa na hamu ya kukaa juu ya kigoda na kumuomba binti yake maji ya kunywa huku mkewe akiingia ndani.

    Atuganile alikimbilia maji ndani na kumletea baba yake, baada ya kunywa alishusha pumzi ndefu kitu kilichomfanya binti yake kuuliza:

    "Baba kuna usalama mtokako?"

    "Wao si wanajifanya wajanja sasa hivi sitii neno lolote kwa mama yako nitamuacha afanye anavyotaka. Watakuja hapa wanalia nasi tutawajibu kama walivyotujibu."

    "Lakini baba Ambakisye yeye hana tatizo ila wazazi wake," alimtetea mpenzi wake.

    "Wao si wanafurahi hali uliyonayo basi tutaharibiana tupate hasara wote."

    Atuganile alijua hasira za wazazi wake hasa kama baba yake amekubali kulipa kisasi hakuna msalie mtume. Kwake yeye mpenzi wake Ambakisye alikuwa bado anamuhitaji katika maisha yake hakutaka atendewe lolote baya. Wazo lake lilikuwa kumpoteza mwanamke anayetaka kuolewa ili nafasi yake ibakie palepale.

    Lakini aliogopa kuwaambia wazazi wake kwa kuonekana anataka kumuhukumu asiye husika, alitaka mpango wake aupange kimyakimya na haraka kabla wazazi wake hawajamfanyia kitu kibaya mpenzi wake. Moyo wake ulikuwa kwenye wakati mgumu juu ya uamuzi wa wazazi wake hakujua wanataka kufanya kitu gani hasa waliposema kila mmoja apate hasara.

    Alipanga jioni kwenda kwa bibi Tumwambilile ambaye alikuwa mtu maarufu sana pale kijijini ili amsaidie tatizo lake ikiwezekana azungumze na wazazi wake ili wasimfanye chochote mpenzi wake pia ampe msaada wa kuzuia ndoa ya mpenzi wake na mchumba aliyechaguliwa na wazazi wake.

    Wakati yeye akiwaza hayo wazazi wa mpenzi wake nao walikuwa na mikakati yao, walimwita mtoto wao na kumuweka chini ili wapange mipango baada ya kuona upande wa pili umekuja juu.

    "Mume wangu tuwe makini najua hawawezi kutuelewa, lazima kuna kitu watafanya kulipa kisasi."

    "Mi siwaogopi wakileta mchezo nitafyeka ukoo mzima, wao si wananunua uchawi? Mimi ninao wa kurithi."

    "Unajua nini?"

    "Hata sijui."CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Wao kisingizio kikubwa si ujauzito wa mtoto wao! Basi dawa yao ni kuutoa, ile dawa na kutega itafaa tena tunampa Ambakisye akaitege."

    "Atakubali?"

    "Tutamdanganya atakubali tu kazi hiyo niachie mimi."

    "Hebu kwanza mwite tuzungumze naye."

    "Wee! Ambakisye," mama yake alimwita.

    "Naam mama."

    Ambakisye alikwenda kusimama mbele ya wazazi wake.

    "Unajua wazazi wa mwenzako wameondoka hapa hawapo katika hali nzuri? Kuna dawa tutakupa uende ukaitege mlangoni kwa mpenzi wako."

    "Ili?"

    "Kwa vile wameondoka na hasira wanaweza kuutoa ujauzito wa mpenzi wako."

    "Sasa kama watautoa si ndiyo itakuwa vizuri! Ili tumalize lawama zao."





    "Hapana sisi hatupo tayari kumpoteza mjukuu, tunataka kuhakikisha anazaliwa, we hupendi mtoto?"

    "Napenda, mbona mwanzo ulinishauri nimwambie atoe?"

    "Tulitaka kumpima tujue ana msimamo gani."

    "Sasa kwa nini nisimuoe kabisa."

    "Hebu kwanza fanya hili, mengine tuachie."

    "Sawa wazazi wangu," Ambakisye alikubali akiwa na matumaini ya wazazi wake kubadili uamuzi kwa kujua umuhimu wa yeye kuwa na



    mtoto.

    "Lakini fanya mpenzi wako asijue."

    "Hakuna tatizo."

    Baada ya makubaliano, Ambakisye alijawa na furaha moyoni mwake kuomba mambo kama yanataka kunyooka. Alipanga kwenda usiku



    nyumbani kwa mpenzi wake kuweka ile dawa huku akimpoza kuamini wazazi wake walikuwa na kitu wanataka kukifanya juu yao.

    Jioni ya siku ile, Atuganile aliondoka kwao bila kuaga anakwenda wapi na kwenda kwa Bi Tumwambilile. Alipitia kwenye Klabu ya



    Mwangibile na kununulia Chimpumu lita tano na kumpelekea. Bi Tumwambilile alimpokea.

    "Jamani Atu karibu mke mwenzangu."

    "Asante bibi."

    "Vipi mbona jioni, kwema utokapo?"

    "Kiasi."

    "Kuna nini?"

    "Bibi mbona una haraka hebu kunywa kwanza pombe kidogo nimekuletea ndipo tuongee."

    "Niwekee kwenye kikopo changu kipo juu ya kichanja."

    Atuganile alikwenda kwenye kichanja cha kuaminikia vyombo na kuchukua kikopo cha kunywea pombe na kumwekea kiasi na kumpa.

    "Karibu bibi."

    "Asante," Bi Tumwambilile alipiga funda ndefu kuonesha alikuwa na kiu na kuweka kopo chini kisha alifuta mdomo na kumgeukia

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Atuganile.

    "Mmh! Umenipatia kweli nilikuwa na kiu cha kufa mtu."

    "Nilijua ndiyo maana nilipitia kwa mzee Mwangibile kukuchukulia najua kiu kitaisha." Na kweli, haya niambie mjukuu wangu una



    tatizo gani."

    Kabla ya kumueleza kilichompeleka pale, alimueleza kisa kizima cha yeye kukataliwa na familia ya mzee Amangise wakati akiwa



    mjamzito. Baada ya kumsikiliza, alishusha pumzi ndefu na kubeba kopo lake na kunywa kupiga funda tatu na kuweka chini.

    "Mmh! Sasa kwa nini wamefanya hivyo?"

    "Wanasema wamempatia msichana mwingine kutoka Kijiji cha Kilasilo."

    "Ina maana wasichana wa kijijini kwetu hawafai, mbona wanatutukanisha hivyo?"

    "Yaani bibi hata siwaelewi, kibaya zaidi nina ujauzito wa Ambakisye sasa mimi nitaupeleka wapi?"

    "Ulitaka kuutoa?"

    "Hapana."

    "Kwa hiyo wewe ulikuwa unatakaje?"

    "Kwanza nilikuwa nataka umwambie mama asimfanye kitu chochote mpenzi wangu, pili nilikuwa nataka kumpoteza yule msichana



    anayetaka kuolewa na Ambakisye ili niolewe mimi."

    "Sawa vyote vinawezekana."

    "Kwa hiyo unaniambiaje?"

    "Jibu lako njoo uchukue kesho na jina la huyu mwanamke anayetaka kuolewa."

    "Sawa."

    "Tulichozungumza usimwambie mtu yoyote."

    "Sawa bibi."

    "Nikamwambie mama aje umwambie?"

    "Hapana nitaonana naye tu, hilo lisikukuumize akili."

    "Nitashukuru bibi."

    "Nilitaka kusahau."

    "Nini bibi?"

    "Kuna kitu nataka nikutume."

    "Kitu gani?"

    "Ukiweza nenda Kijiji cha Kilasilo katika mto Kiwila wa sehemu watu wanao chota maji ya kufulia na kuoga ili uchukue maji



    yake na majani ya pembeni uniletee."

    "Sawa bibi nitafanya hivyo."

    Atuganile aliagana na bibi Tumwambilile na kurudi nyumbani, kwa vile ulikuwa muda wa kuandaa chakula cha usiku, alifikia



    jikoni bila kuwaeleza wazazi wake alikuwa amekwenda wapi. Alifanya kazi zake akipanga usiku aende kwa Ambakisye akaulizie



    jina la mwanamke anayetaka kumuoa ili kesho ampelekee bibi Tumwambilile pia kumuomba amsindikize Kijiji cha Kilasilo.

    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Majira ya usiku baada ya chakula cha usiku, wazazi wa Atuganile walikuwa na kikao chao kujadili kulichotokea asubuhi.

    "Kama hutaki nifanye hivyo tufanyeje?" mama Atuganile alimuuliza mumewe baada ya kumkatalia hatua aliyotaka kuichukua kwa



    Ambakisye baada ya kumtia mimba binti yao na kugoma kumuoa.

    "Basi tumfanye asiwe karibu tena na wanawake."

    "Timtie kichaa."

    "Hapana watajua ni sisi."

    "Mbona hiyo adhabu ni ndogo kuliko uliyotaka kuitoa?"

    "Tufanye isiyoendana na tukio la kumtia mimba mtoto wetu."

    "Nilikueleza awe mbali na wanawake kwa kumuua nguvu za kiume."

    "Tutafanyaje bila kumshirikisha Atu ambaye siamini kama atakubali."

    "Tutatengeneza uongo kwamba akifanya hivyo basi mpenzi wake hawezi kumuacha. Kwa vile hatujaonesha kukemea kilichotokea



    itakuwa njia rahisi ya kutimiza dhamira yetu."





    “Basi tufanye hivyo.”

    Walikubaliana kumwita Atuganile na kumweleza kitu cha kumfanyia mpenzi wake kama kuongeza mapenzi kumbe kummaliza. Aliitwa Atuganile aliyekuwa akiosha vyombo.

    “Atu,” mama yake alimwita kwa sauti.

    “Abee mama.”

    “Njoo mara moja.”

    Atuganile aliacha kuosha vyombo na kusuuza mikono yake na kuwafuata wazazi wake waliokuwa wamekaa pembezoni mwa nyumba wakizungumza.

    “Abee,” aliitikia huku akifuta maji kwenye khanga aliyojifunga.

    “Kaa hapo,” alisema baba yake, naye alitii amri na kukaa kitako.

    “Atu,” mama yake alimwita.”

    “Abee mama.”

    “Nina imani umejua kilichotokea wewe na mpenzi wako?”

    “Ndiyo.”

    “Tuna imani unampenda sana Ambakisye?’

    “Ndiyo mama.”

    “Sasa kuna dawa tutakupa ambayo ukikutana na mwenzako kimwili hakikisha unajipaka mkononi na kumpaka sehemu za siri ili asiweze kukuacha.”

    “Jamani Ambakisye hana tatizo bali wazazi wake sasa hiyo dawa ya nini?”

    “Sisi ndiyo tunajua hebu fanya zoezi hilo kisha tuangalie nini kinaendelea.”

    “Sawa wazazi wangu.”

    “Lini unaonana naye?”

    “Hata leo.”

    “Basi subiri,” mama yake alisema huku akinyanyuka kuelekea ndani, baada muda alirudi akiwa na karatasi na kumpa Atuganile.

    “Hakikisha unampaka baada ya tendo na si kabla.”

    “Sawa mama.”

    “Haya malizia kuosha vyombo uwahi kwa mwenzio.”

    “Sawa mama.”

    Atuganile alinyanyuka na kuingia ndani kuweka dawa yake na kurudi kuendelea na kazi ya kuosha vyombo ili baadaye aende kwa mpenzi wake.

    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ambakisye akiwa anajiandaa kutoka kumfuata mpenzi wake alisikia mlango ukigongwa, alipotoka alimuona mpenzi wake mlangoni.

    “Ha! Atu.”

    “Ndiyo mimi mpenzi.”

    “Karibu mpenzi.”

    “Asante,” Atuganile alisema huku akiingia ndani.

    “Yaani ndo nilikuwa najiandaa kuja nawe umetokea.”

    “Leo nimemaliza kazi mapema nikaona nije mwenyewe.”

    “Nimefurahi kusikia hivyo.”

    “Hivi kweli Amba upo tayari kuoa mwanamke mwingine?” Atuganile alimuuliza huku akikaa kitandani.

    “Atu nikueleze mara ngapi mi nakupenda lakini lililoamuliwa na wazazi wangu lipo nje ya uwezo wangu.”

    “Kwa hiyo upo tayari kuoa mwanamke mwingine na kuniacha mimi?”

    “Hata kama nitamuoa mapenzi yangu yote yatakuwa kwako.”

    “Sasa mimi nitaishi hivi mpaka lini?”

    “Kwa kweli huo ni mtihani walionipa wazazi wangu.”

    “Hivi kwa bahati mbaya mchumba wako akifa utakuwa tayari kunioa?”

    “Hilo halina tatizo, wewe ndiye mke wangu mwingine ni kulazimishwa.”

    “Halafu mchumba wako anaitwa nani.”

    “Bupe.”

    “Bupe nani?”

    “Ambokile.”

    “Kwao unapokaa unapajua.”

    “Si nilikuambia Kijiji cha Kilasilo.”

    “Kesho nina safari ya Kilasilo nimetumwa nilitaka unipeleke na baiskeli yetu, lakini nina wasiwasi mchumba wako atakuona ukinisindikiza nami siwezi kwenda peke yangu.”

    “Usiwe na wasiwasi nitakusindikiza tu kwa vile yeye amekukuta kama akisusa si itakuwa nafasi yako.”

    “Nimefurahi kusikia hivyo, kweli unanipenda mpenzi wangu.”

    “Hata wewe unajua.”

    Baada ya mazungumzo ambayo yalitawaliwa na siri nzito mioyoni mwa wapenzi wawili toka katika familia zao. Walizama kwenye mahaba mazito mwisho wa safari Atuganile alimpaka dawa aliyopewa na wazazi wake sehemu za siri bila kujua anamuumiza mpenzi wake.

    Baada ya kustareheshana kama kawaida Ambakisye alimsindikiza mpenzi wake mpaka kwao na yeye kurudi kulala bila kupeleka dawa aliyopewa na wazazi wake akaitege mlangoni kwa mpenzi wake.

    Atuganile aliamini huenda dawa aliyomfanyia mpenzi wake itasaidia Ambakisye asioe.

    Siku ya pili alikutana na wazazi wake na kuwaeleza kila kitu kimekwenda kama walivyomuagiza.

    “Hukukosea?” mama yake alimuuliza.

    “Sikukosea nilikuwa makini sana.”

    “Basi kazi yako umemaliza tuachie sisi.”

    “Sawa mama.”

    Kwa vile asubuhi ile alikuwa na safari ya kwenda Kilasilo alipotumwa na bibi Tumwambilile. Walikubaliana na mpenzi wake wakutane mbele ambako hakuna mtu atajua safari ile wamekwenda pamoja. Atuganile alisubiri wazazi wake waende shamba alichukua baiskeli na kutoka nayo. Kwa vile alikuwa akijua kuendesha alimpitia Ambakisye ili kumjulisha anatangulia.

    Ambakisye alimfuata mbele na kupakizana kwenye baiskeli na kuelekea Kijiji cha Kilasilo, Atuganile alianza kwa kumpakia mpenzi wake alipochoka Ambakisye alichukua baiskeli na kumpakia mpenzi wake mpaka walipofika.

    Walifika Kijiji cha Kilasilo saa sita mchana, kwanza Atuganile aliomba apelekwe Mto Kiwira sehemu ambayo watu wanatumia kwa huduma muhimu za kufua, kuoga na kuosha vyombo.

    Alipofikishwa aliteremka mtoni na kujifanya ananawa na kuchukua maji ya mto na kuweka katika kichupa kidogo na kuchuma majani yaliyoingia mtoni kisha alirudi mjini ambako alimuomba mpenzi wake amsubiri sehemu na yeye kuchukua baiskeli na kwenda mbele na baadaye kurudi kwa mpenzi wake huku akitengeneza uongo.

    “Yaani nimefanya kazi bure,” Atuganile alijifanya kusikitika.

    “Kwa nini?”

    “Wamesema amekwenda Isaki mpakani.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/







    "Basiturudi nyumbani."

    Walikubaliana kurudi nyumbani, walifika nyumbani majira ya saa moja na nusu usiku, baada ya kuagana, Atuganile hakwenda nyumbani kwao, alichepuka na kukimbilia kwa bibi Tumwambilile. Alipofika alimpa mzigo aliotumwa.

    "Bibi mzigo huu hapa."

    "Ulienda na nani?"

    "Na Ambakisye."

    "Ulimwambia unaenda kufanya nini?"

    "Nilimwambia nimetumwa na mama, lakini nilifanya vitu vyangu bila kujua chochote."

    "Jina la mchumba wake?"

    "Bupe Ambokile."

    "Basi mjukuu wangu kapumzike kazi yote niachie mimi ila kitakachotokea ibakie siri yako hata wazazi wako usiwaambie."

    "Siwaambii ndiyo maana nilikuja peke yangu."

    "Basi majibu utayapata kwa siku mbili kuanzia kesho."

    "Nitafurahije bibi, nimeumia sana kumkosa Ambakisye."

    "Najua ndiyo maana kazi yako sikumpa mtu yeyote, nitaifanya mwenyewe."

    "Nakuamini bibi, nitakupa zawadi nzuri."

    "We iandae tu."

    Atuganile aliagana na Bibi Tumwambilile na kurudi nyumbani ambako aliwakuta wazazi wake waliotaka kujua alikuwa wapi siku nzima.

    Alidanganya alimsindikiza mpenzi wake Ambakisye Kijiji cha Mbako.

    "Njiani hamkufanya chochote?"

    "Hatukufanya chochote, tumekwenda na kurudi."

    "Mmh! Sawa, lakini kwa nini hukuaga?"

    "Niliogopa mnaweza kunikatalia nami sitaki kumuudhi mpenzi wangu, nina imani dawa niliyompaka itafanya kazi. Nimefurahi wazazi wangu kuupigania moyo wangu. Maana nilikuwa najiuliza uso wangu nitauweka wapi."

    "Usiwe na wasi kila kitu kitaenda vizuri."

    Baada ya kula alijipumzisha kumsubiri mpenzi wake kwa vile alikuwa amechoka sana kwa ajili ya kuendesha baiskeli masafa marefu huku amempakia mtu.

    ***

    Usiku wa saa tatu, kama kawaida Ambakisye alitoka nyumbani kwao kumfuata mpenzi wake. Kabla hajatoka, alikumbuka dawa aliyopewa na wazazi wake ya kwenda kuitega mlangoni kwa mpenzi wake ambayo jana yake aliisahau akiamini kufanya vile ni kuzuia ujauzito ambao wazazi wake walitaka kuutoa.

    Baada ya kuichukua dawa, alikwenda mpaka kwenye chumba anacholala mpenzi wake, kabla ya kumgongea aliinyunyizia kukata mlango ili akitoka airuke.

    Aliifanya kwa umakini mkubwa huku akiangalia nyumba ya wazazi wake waliokuwa wamelala, baada ya kulifanya zoezi aligonga dirisha la mpenzi wake ambaye muda huo alikuwa amepitiwa na usingizi kutoka na uchovu wa safari.

    "Atu..Atu," alimwita kwa sauti ya juu kidogo.

    "Mmh!"

    "Mi Amba."

    "Ooh! Mpenzi."

    "Eeh! Nimefika."

    "Nakuja."

    Atuganile aliamka na kujifunga upande wa kanga kwa vile alilala na gauni akimsumbiri mpenzi wake na kutoka nje. Kutoka na maelezo aliyopewa Ambakisye na wazazi wake kuwa lazima aruke ile dawa, alisimama mbele kidogo ya mlango.

    Baada ya Atuganile kufungua mlango, alimfuata mpenzi wake aliposimama na kuruka dawa aliyotegewa bila kujua huku Ambakisye akifurahi kumuokoa mwanaye aliye tumboni bila kujua alikuwa akimuua.

    Baada ya kutoka ndani kabla hajamkumbatia mpenzi wake alisikia kitu kikimkata ghafla chini ya kitovu na kupiga kelele ya maumivu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mama nakufa," alisema huku akiinama akiwa ameshika tumbo.

    "Nini mpenzi wangu?" Ambakisye alishtuka.

    "Nimesikia kitu kikinikata chini ya kitovu," alisema kwa sauti ya maumivu.

    "Mmh! Nini tena?" Ambakisye alimshika mpenzi wake aliyekuwa ameinama bado ameshika tumbo.

    "Usiwe na wasi mpenzi ni mshtuko tu," Atuganile alisema huku akinyanyuka baada ya maumivu kukata ghafla.

    "Vipi?"

    "Nipo sawa, tunaweza kwenda."

    Waliurudisha mlango na kuondoka kuelekea kwa mpenzi wake, walipofika kama kawaida waliingia chumbani kwao. Baada ya mazunguzo walijiandaa kwa ajili ya kustarehe.

    Kila Atuganile alivyomuandaa mwenzake kama kawaida alishangaa mpenzi wake kuwa baridi.

    "Mmh! Amba vipi leo?"

    "Hata mimi nashangaa."

    Atuganile hakukata tamaa, aliendelea kumuandaa mpenzi wake mpaka jasho likamtoka japokuwa kulikuwa na hali ya baridi. Lakini ilikuwa hali ileile maiki kuendelea kutotoa sauti na sinyaa kitu kilichowashtua wote.

    "Amba umekuwaje leo mpenzi?"

    "Yaani leo nashangaa toka nizaliwe sijawahi kutokewa na hali hii."

    "Sasa hii ni nini?"

    "Labda uchovu wa safari," Ambakisye alijitetea.

    "Si kweli mbona uliniambia kuna siku ulikwenda na baba yako Isaki na wewe ndiye uliendesha kwenda na kurudi lakini jioni tulipokutana ulikuwa kwenye hali ya kawaida?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog