Search This Blog

VITA YA WACHAWI - 2

 





    Simulizi : Vita Ya Wachawi

    Sehemu Ya Pili (2)





    ILIPOISHIA:

    Atuganile hakukata tamaa, aliendelea kumuandaa mpenzi wake mpaka jasho likamtoka japokuwa kulikuwa na hali ya baridi. Lakini

    ilikuwa hali ileile sehemu kuendelea kusinyaa badala ya kunyanyuka kitu kilichowashtua wote.

    “Amba umekuwaje leo mpenzi?”

    “Yaani leo nashangaa toka nizaliwe sijawahi kutokewa na hali hii.”

    “Sasa hii ni nini?”

    “Labda uchovu wa Safari,” Ambakisye alijitetea.

    “Si kweli mbona uliniambia kuna siku ulikwenda na baba yako Isaki na wewe ndiye uliendesha kwenda na kurudi lakini jioni

    tulipokutana ulikuwa kwenye hali ya kawaida.”

    SASA ENDELEA…

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa hii sijui nini?” Ambakisye alishangaa.

    “Kwanza mbona sehemu zako zimezidi kusinyaa.”

    “Mmh! Hili litakuwa tatizo,” Ambakisye aliingiwa wasiwasi.

    “Sasa tutafanyaje?”

    “Acha nikusindikize kwenu ili niangalie hali hii mpaka kesho.”

    “Mmh! Sawa,” Atuganile alikubali kwa shingo upande.

    Walikubaliana kusindikizana baada ya kila mmoja kuvaa nguo zake, walikwenda hadi nyumbani kwa Atuganile na kuagana kwa shingo

    upande. Ambakisye alirudi nyumbani na kuingia chumbani kwake, hakuamini hali iliyomtokea, alisogeza taa kujiangalia.

    Maumbile yake yalikuwa madogo tofauti na umbile lake halisi la kuzaliwa.

    Hakutaka kuwa na haraka, alilala ili kesho ajitazame hali yake, kama itaendelea kuwa vile basi angemueleza baba yake. Upande

    wa pili, Atuganile alishtushwa sana na hali ya mpenzi wake Ambakisye, akawa na wasiwasi na dawa aliyopewa na wazazi wake

    ampake sehemu za siri huenda ndiyo iliyokuwa imemfanya awe vile.

    Alipanga asubuhi kumuuliza mama yake hali iliyomtokea mpenzi wake, ili amsaidie kwani aliogopa kama ile hali itaendelea

    lazima mapenzi yao yataingia dosari. Baada ya kuwaza sana alipitiwa na usingizi. Usiku wa manane tumbo lilianza kumsokota na

    kufanya asikie maumivu makali.

    Baada ya kuvumilia labda ile hali itapoa lakini kila dakika maumivu yalizidi, ilibidi anyanyuke ili akafie kwa wazazi wake.

    Aliponyanyuka damu nzito nyeusi zilianza kutoka sehemu za siri. Alitembea kwa kupepesuka huku akijitahidi kuwaita wazazi wake

    kwa sauti ya juu.

    “Mamaaa nakufa….Nakufa mie jamani.”

    Sauti ile iliwaamsha wazazi wake ambao walitoka mbio nje walishtuka kumuona Atuganile ameanguka karibu na mlango wao.

    “Mungu wangu mwanangu,” mama Atuganile alisema kwa sauti huku akimkimbilia mwanaye aliyekuwa amekata kauli wakati huo.

    Walimnyanyua na kumuingiza ndani na kumlaza kwenye mkeka, walishangaa kuona amejaa damu nyeusi miguuni. Wakati huo Atuganile

    alikuwa amepoteza fahamu kitu kilichoongeza taharuki kwa wazazi wake.

    “Mmh! Hii nini?” Mzee Andendekisye alichanganyikiwa.

    “Mume wangu tuwe makini la sivyo tutampoteza mtoto hivihivi .”

    Walianza kazi ya kuhakikisha wanaokoa uhai wa Atuganile aliyekuwa bado amepoteza fahamu huku akionesha amepoteza damu nyingi.

    Walijitahidi kumrudisha katika hali yake ya kawaida, ilionekana kama inashindikana kwani hakukuwa na dalili zozote za

    Atuganile kuamka.

    “Mume wangu hii hali inatisha.”

    “Tufanyeje?” mzee Andendekisye alichanganyikiwa kwa hali ya mwanaye.

    “Hebu kimbia haraka kwa bibi Tumwambilile,” ilibidi atafute msaada baada ya wao kuchemsha.

    Mzee Andendekisye alitoka mbio kwenda kwa bibi Tumwambilile japokuwa usiku ulikuwa mzito uliokuwa na kiza cha kutisha kutokana na kutokuwa na mwezi angani. Alipofika aligonga mlango wa bibi Tumwambilile.

    “Nani tena usiku huu?” bibi aliuliza.

    “Mimi Andendekisye.”

    “Baba Atu?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo bibi.”

    “Vipi mbona usiku?”

    “Mjukuu wako anakufa huko.”

    “Kafanya nini?”

    “Tumesikia usiku huu akituita akisema anakufa alipotoka tulimkuta ameanguka chini huku akitoka damu nzito nyeusi katikati ya miguu akiwa tayari kapoteza fahamu.”

    “Mmh! Isiwe ametoa mimba?” bibi aliuliza.

    “Hatujui kwa vile toka tulipomkuta ameanguka haongei na pumzi zake zipo mbali.”

    “Mmh! Hebu subiri.”

    Bibi Tumwambilile alirudi ndani na kutoka baada muda na kusema:

    “Mmh! Wajanja wamewawahi.”

    “Una maana gani? Ina maana Atu ndiyo amekufa?” mzee Andendekisye alishtuka.

    “Sina maana hiyo kuna kitu mtoto wenu alitegewa na kuruka ndicho kilichosababisha tatizo lile.”

    “Tatizo gani?”

    “Ujauzito umetoka?”

    “Kautoa nani?”

    “Kwanza twende tukamhudumie mtoto.”

    Waliongozana usiku ule kuelekea nyumbani, uani kwake bibi Tumwambilile alichuma majani mabichi na kwenda nayo. Walipofika walimkuta mama Atuganile bado amemuinamia mwanaye huku akilia.

    Bibi Tumwambilile alipofika pale alimkemea kwa kitendo cha kumlilia mwanaye aliye hai.

    “Unalia nini wakati wewe ndiye bingwa wa kuwalipua watu, leo umewahiwa badala ya kupambana unalia, kweli vita ikitokea utaiweza?” bibi Tumwambilile alimuuliza akiwa amemkazia macho.

    “Hapana Tumwambilile, sijui mwanangu amepatwa na nini, kila tulivyojitahidi kumrudisha katika hali yake ya kawaida ilishindikana,” mama alisema kwa sauti ya kilio.

    “Siku zote nilikueleza ukijua kupiga ujue na kupigwa, hivyo ujue kukwepa na kujikinga. Umewahiwa unatakiwa kujua utafanyaje kumuokoa mtoto na si kulia.”

    “Mpaka nalia uwezo wangu umefikia mwisho.”

    “Basi tuache maneno tumsaidie mtoto, lete maji kwenye beseni.”

    Walifanya vile mara moja na kumletea maji kwenye beseni , bibi Tumwambilile alimuomba mzee Andendekisye aondoke kwa vile ilitakiwa kufanyika kazi ya wanawake.

    Baada ya kuondoka walimvua Atuganile nguo zote na kumlaza chali kwenye mkeka.

    Walichukua majani mabichi na kuyaweka kwenye maji na kuyachikicha mpaka maji yote yakabadilika rangi na kuwa ya kijani.

    “Msugue sehemu zake mpaka ndani,” bibi Tumwambilile alimuelekeza mama Atuganile. Naye alifanya kama alivyoelekezwa baada ya zoezi lile, alielezwa aendelee kumsugua mwili wote na kufanya hivyo kisha walimwosha maji yaliyobakia. Pamoja na zoezi lile

    kufanyika hakukuwa na mabadiliko yoyote kwa Atuganile alikuwa amelala vilevile hali iliyozidi kumtisha mama yake.

    “Tumwambilile mbona hakuna mabadiliko yoyote?”

    “Kwani nimemaliza kazi yangu, mama Atu unataka kuniudhi,” bibi Tumwambilile alikuja juu.

    “Basi bibi nisamehe nimechanganyikiwa mwenzio.”

    “Wewe ulipotoa uhai wa mtoto wa mwenzio hukuchanganyikiwa lakini ugonjwa wa mwanao ukuchanganye.”

    “Bibi eeh! Si nimekubali nimekosa.”

    Bibi Tumwambilile hakusema kitu alichukua kichupa kidogo alichokuja nacho na kukiweka puani kwa Atuganile kwa muda kisha alikitoa. Walitulia kwa muda ghafla Atuganile alipiga chafya mfululizo na kutulia akiwa bado amejilaza chini.

    “Atu,” bibi Tumwambilile alimwita.

    “Abee,” aliitikia.

    “Vipi?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mmh!”

    Alifumbua macho na kushtuka kumuona bibi Tumwambilile na mama yake wakiwa wamesimama pembeni yake kingine kilichomshtua ubaridi wa usiku ule.

    “Jamani kwani vipi?” alisema huku akikaa na kujishangaa kukaa kwenye mkeka akiwa hana nguo mwilini huku sehemu ya mwili wake zikiwa na vipande vya majani mabichi.

    “Unajisikiaje?” bibi Tumwambilile alimuuliza huku mama yake akiwa kimya kuogopa kumuudhi bibi.

    “Kwani kuna nini?” bado Atuganilie hakuelewa kumemtokea nini.

    “Kwani nini kimekutokea?”

    Atuganile alitulia na kukumbuka kilichomtokea wakati amelala, alikumbuka tatizo lilivyoanza wakati alipofuatwa na Ambakisye.

    Lakini hakutaka kusema chanzo bali tatizo lilivyompata usiku kwa kuhofia kuingiza imani za kishirikina kutoka kwa wazazi wa mpenzi wake na kuleta mzozo wa familia mbili wakati wazazi wake waliisha mhakikishia Ambakisye hawezi kuoa mwanamke mwingine.





    Baada ya kumsikiliza walimpa dawa ya kunywa ya majani mabichi yaliyofikichwa kwenye maji. Yalikuwa mengi ambayo alielezwa anywe ili kuondoa sumu iliyoingia mwilini na kusafishwa sehemu zake ambazo zilikuwa na sumu.

    Baada ya kunywa maji ya dawa jagi zima, Atuganile alianza kutapika na kuharisha kwa wakati mmoja.

    Walimsaidia kumshika mpaka alipomaliza walimuongeza na kufanya aende haja ndogo kwa muda mrefu kisha alipewa dawa ya unga na kunywa kwenye maji ya moto na kupumzishwa ili wajue kesho wafanye nini na kuangalia afya yake japo bibi Tumwambilile alisema ataamka hajambo kabisa.

    Baada ya zoezi lile kwenda vizuri walimshukuru bibi Tumwambilile kisha mzee Andendekisye alimsindikiza mpaka kwake kisha alirudi nyumbani salama. Alimkuta mkewe akimsubiri, baada ya kuingia ndani na kufunga mlango mkewe alimwambia:

    “Mume wangu hii vita, siwezi kukubali mtu amchezee mwanangu nitaununua uchawi kwa gharama yoyote nitaufuata hata Ulaya ikiwezekana.

    Najua hii ni familia ya Amangise ndiyo waliofanya kazi hii ili wapate cha kusema baada ya kumharibu mwanetu. Nakwambia atakufa mtu nitahakikisha nawashikisha adabu,” alisema kwa hasira.

    “Lakini mbona Tumwambilile amekataa kumtaja aliyefanya vile.”

    “Hata asipomtaja waliofanya vile ni familia ya Amangise tu,” Mama Atuganile alisema.

    “Inawezekana wamelipiza kisasi baada ya kumuumiza mtoto wao.”

    “Walitakiwa kuja tuzungumze ili tulimalize kwa sharti la kumuoa Atu na siyo kuniulia mjukuu wangu.”

    “Na kweli, mtoto wao anaweza kupona lakini hawezi kumrudisha mtoto tumboni.”

    “Yaani sikubali damu ya mjukuu wangu ipotee bure nitaipigania kwa gharama yoyote, tena kuna dawa nitampa Atu akampake yule mshenzi ili sehemu zake za siri zioze kabisa asiweze kutibika popote,” mama Atuganile alisema kwa hasira.

    “Kama ni hivyo basi tukio hili tufanye siri yetu Atu asijue kitu ili tuwatie adabu.”

    “Hilo ndilo umesema neno.”

    Baada ya makubaliano walipanda kitandani kulala.



    KATIKA KIJIJI CHA KILASILO

    Bupe mchumba wa Ambakisye aliyechaguliwa na wazazi wake, akiwa nyumbani peke yake baada ya wazazi wake kwenda shambani, alijikuta akiwa na hamu ya kwenda mtoni kuchota maji kitu alichokatazwa na wazazi wake.

    Toka alipochumbiwa na kulipiwa mahari, wazazi wake walimkataza kutoka eneo la nyumbani kwa muda wote mpaka siku ya harusi ambayo haikuwa muda mrefu.

    Siku hiyo alijikuta moyo wake ukimsukasuka kutaka kwenda kuchota maji, alisubiri wazazi wake wamekwenda shamba, alitoka hadi nyumba ya pili na kumwambia shoga yake Pendo, mtoto wa mzee Mwakasanga kuwa waende mtoni wakachote maji.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walikubaliana na kuchukua ndoo kuelekea mtoni, walipofika waliwakuta wanawake wengi, kinamama na wasichana waliokuwa wakifua na wengine wakichota maji.

    Bupe na Pendo walikunja nguo zao na kuingia ndani ya maji kuchota maji. Wakiwa wanachota maji ghafla watu wakapiga kelele baada ya kumuona mamba akielea juu ya maji akielekea walipokuwa wakichota maji.

    “Jamani mambaaa!” mtu mmoja alipaza sauti.

    Walipogeuka walimuona na kila aliyekuwa ndani ya maji alitaharuki kwa kutupa ndoo na kutoka mbio nje japokuwa maji yalikuwa mazito.

    Ajabu yule mamba aliwaacha watu wote waliokuwa karibu na kumfuata Bupe aliyekuwa akikimbilia nje na kumpiga na mkia uliomfanya aanguke ndani ya maji.

    Alimfuata na kumlalia juu na kumzamisha chini kisha aliondoka naye, hali ile iliacha taharuki kwa watu wote waliokuwa pale mtoni na kushangaa ujaji wa mamba yule ambaye alionesha kumchagua mtu na kuwaacha wote waliokuwa nyuma yake.

    “Jamani hivi hali hii itaisha lini mnataka tuishi wapi? Porini wanyama wakali mjini watu wenye roho mbaya!” alisema mwanamke mmoja aliyekuwa ameshikilia mikono kichwani kwa sauti ya kilio.

    “Huyu mamba si bure mkono wa mtu tokea lini eneo hili likatokea mamba?” mwanamke mwingine alihoji.

    “Jamani watu wana roho mbaya yaani Bupe kutaka kuolewa watu hawajafurahi mpaka wanamtumia mamba?” mwingine aliyekuwa akimfahamu alisema huku amejishika kifuani kwa hofu ya tukio.

    “Lakini jamani huu uchawi si wa maeneo yetu lazima mfanyaji amesafiri,” mwingine alichangia.

    “Huu uchawi wa Malawi tu ndiyo wenye tabia ya kutumiana mamba,” mwingine aliunga mkono kauli ya mwenzake.

    Wakati huo Pendo shoga yake alikuwa ameangua kilio kwa sauti ya juu kumlilia shoga yake mpaka akapoteza fahamu, kwa vile ndiye aliyefuatana naye mtoni. Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza alielezea alivyofuatwa na Bupe kwenda naye mtoni.

    “Wazazi wake wapo wapi?” mama mmoja aliuliza.

    “Wameenda shamba.”

    “Si nilisikia anataka kuolewa?” mmoja aliuliza.

    “Ndiyo,” alijibu dada aliyemfahamu Bupe.

    “Sasa ilikuwaje aje kuchota maji badala ya kukaa ndani?”

    “Alikatazwa na wazazi wake asiende kuchota maji wala kutoka eneo la kwao, lakini leo nilishangaa kanifuata na kuniomba nije naye kisimani ndiyo yakatokea haya,” Pendo alipofikia hapo aliangua kilio upya kwa kujitupa chini na kuwapa watu kazi ya kumbembeleza.

    Kila mmoja alisema lake, mwenye jicho la tatu alijua ule ni mchezo umechezwa kwa kutumia uchawi wa mamba ambao ulitumika sana Malawi. Ilibidi taarifa zipelekwe kwa wazazi wa Bupe waliokuwa shamba. Mama Bupe alipatwa na mshtuko uliofanya apoteze fahamu baada ya kuzipata taarifa za mwanaye Bupe na kufanya watu waliopeleka taarifa wapate kazi ya kumbeba kumkimbiza hospitali.



    Taarifa za Bupe kuchukuliwa na mamba zilizagaa kijijini haraka kama moto kwenye majani makavu. Kwa vile upoteaji wake ulikuwa wa utata watu walimshauri mzee Andendekisye aende upande wa pili (Tiba asili). Alielekezwa Kijiji cha Kanjumjumere ambako kulikuwa na mganga aliyekuwa maarufu eneo lile aliyetambulika kwa jina la Mpalapala (aliyeshindikana).

    Siku ya pili walifunga safari na wenyeji wa eneo lile, baada ya kufika walikwenda kwa mganga (Mpalapala) aliyekuwa na nyumba ya majani iliyozungukwa na zingine ndogo. Walipokelewa na kukutana naye. Baada ya kukutana na mganga Mpalapala kuangalia ramli yake alisema:

    “Hili tukio siyo la kawaida, mamba aliyemchukua mtoto wenu si wa kawaida ila wa kichawi. Mpaka sasa mtoto wenu bado amefichwa pembeni ya mto. Wanasikilizia mpaka kesho kama hakutafanyika kitu chochote cha kumrudisha basi wataondoka naye.”

    Kama kuna uwezekano wa tiba ifanyike usiku wa leo ili kumrudisha zaidi ya hapo tutamkosa kabisa au kuokota maiti yake pembezoni mwa mto. Kwa vile kazi ni nzito inatakiwa apatikane mbuzi mweupe asiye na doa ambaye tutamchinja na kumwaga damu yake kwenye maji ili kuweka mwanga wa kumpata alipofichwa.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kama hatutapata mbuzi mweupe?” mtu aliyempeleka mzee Andendekisye kwa mganga aliuliza.

    “Mbuzi yoyote anafaa lakini mweupe atasaidia kuondoa kiza. Mbuzi mweusi au mwekundu hafai kwani ataongeza giza ila mwenye rangi mbili nyeusi na weupe au wa kijivu wanaweza kusaidia lakini itabidi ifanyike kazi ya ziada.”

    “Umesema usiku, je tunaweza kuondoka sasa hivi ili tuwahi muda?” mzee Andendekisye aliuliza.

    “Hakuna tatizo cha muhimu ni huyo mbuzi mweupe.”

    “Tutajitahidi apatikane.”

    Waliondoka Kijiji cha Kanjumjumere na kurudi Kilasilo na kufika saa nne usiku, mara moja ulianza msako wa kutafuta mbuzi mweupe. Walikwenda kwa mzee Mwangibile aliyekuwa na mbuzi na kubahatika kupata mbuzi mweupe lakini mwenye baka jeusi mgongoni.

    Mganga alisema atafaa, majira ya saa sita usiku waliongozana hadi mto Kiwira, ambako ndipo alipokamatwa Bupe na mamba. Walipofika eneo lile mbuzi alichinjwa na damu yake kumwagwa mtoni kisha alichovya usinga wake kwenye damu ya mbuzi iliyochanganywa na dawa na kuanza kurusha ndani ya maji huku mganga akiliita jina la Bupe kwa sauti kubwa.

    “Bupeee….Bupeee….Bupeee.”

    Aliendelea kufanya vile huku akitembea kwenye maji na kusogea sehemu aliyoamini ndipo alipofichwa. Aliendelea kumwita huku akiendelea kuzunguka ndani ya maji, ghafla wote walishtuka baada ya kutokea mamba ambaye alimkamata mganga na kuzama naye chini ya maji na kufanya waliongozana naye kutimua mbio.

    Wasaidizi wa mganga walirudi eneo lile ambalo lilikuwa tulivu bila kuonesha kuna tukio lolote lililotokea. Walijiuliza alikokuwepo, waliita jina lake lakini hali ya ukimya ilitawala.

    Hali ile ilizidi kumtisha mzee Andendekisye na kujiuliza kama mganga naye kachukuliwa itakuwaje.

    Kwa vile ulikuwa usiku mkubwa walirudi nyumbani kulala kwa ajili ya kumtafuta siku iliyofuata. Wasaidizi wa mganga walipanga kuamka alfajiri kwenda kuangalia mtoni.

    Mzee Andendekisye na mkewe walikosa usingizi kwa tatizo lile zito ambalo hawakujua hatima ya mtoto wao kwa vile mganga alisema usiku wa siku ile ukipita hawatampata tena na kama watampata hatakuwa hai.

    “Mume wangu tumewakosea nini walimwengu, kibaya zaidi muoaji anatoka mbali,” mama Bupe alilalamika.

    “Labda vijana wa hapa, si ulisema mtoto wa Mwandambo alikuwa akitaka kumuoa na kumkatalia huenda ndiye aliyefanya mchezo huo,” mzee Andendekisye alisema.

    “Mmh! Yule mtoto mbona alishakwenda Mwanza kwa mjomba wake muda,” mama Bupe alimtetea.

    “Sasa atakuwa amefanya nani?”

    “Mtaalamu amepotea sijui itakuwaje?”

    “Hebu ngoja alfajiri tukienda mtoni tutapata jibu labda ndiyo amekwenda kumsaka,” alijipa moyo.

    Usiku wa siku ile mzee Andendekisye alikesha macho na saa kumi na nusu aliwaamsha wasaidizi wa mganga na kuelekea mtoni.

    Waliongozana hadi mtoni walipofika walipigwa na butwaa baada ya kumkuta mganga akielea pembeni ya mto akiwa amekufa. Kilichowashtua kumkuta akiwa hana nguo huku baadhi ya sehemu zake za mwili zikiwa zimechukuliwa. Sehemu za siri, kucha, ulimi na kunyolewa pembeni ya kichwa.

    Hali ilizidi kutisha, lilikuwa jambo la ajabu kutokea sehemu ile kwa mganga kuchukuliwa kichawi na kukatwa sehemu za mwili kisha kuonekana akielea pembeni ya mto. Kilichowashangaza zaidi, mwili wa mganga uliwahi kuonekana wakati wa mtoto wao Bupe haukuonekana wakati mamba aliyemchukua ni yuleyule.

    Ilibidi mwili wa mganga uchukuliwe na kusafirishwa kwenda kijijini kwake Kanjumjumere kwa ajili ya maziko na kumuacha mzee Andendekisye asijue la kufanya juu ya kutoweka kwa binti yao kwani mganga aliwaambia kama ungepita usiku bila Bupe kupatika angepatikana akiwa maiti.

    Aliamini kwa kauli ya mganga mtoto wao asingepatikana tena.

    Lakini majirani walimpa moyo kuwa asikate tamaa, wengine walimshauri avuke boda kuingia Malawi ambako kulisifika kwa uchawi na waganga.

    Wengi waliamini uchawi ule mtu aliufuata Malawi. Alielekezwa kijiji kinachosifika kwa uchawi na waganga cha Mwakawenge katika mji wa Chitipa. Mzee Andendekisye alipanga kwenda Malawi kufuatilia kupotea kwa mwanaye. ***

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Atuganile aliamka siku ya pili akiwa mzima wa afya njema lakini ujauzito hakuwa nao, wazazi wake walimuweka chini ili kutaka kujua kipi kilimsibu na alikwenda wapi.

    “Atu.”

    “Abee baba.”

    “Jana ulikula nini kwa kina Ambakisye?”

    “Sikula kitu.”

    “Usifiche kwa vile mchezo waliokufanyia ni mbaya sana, bila bi Tumwambilile tungekupoteza.”

    “Kama ni wao wamepata faida gani?”

    “Ndiyo maana tunataka kukupa dawa ili ukampake mpenzi wako kabla ya kukutana naye ili kuhakikisha unashika ujauzito haraka.”

    “Mama haraka ya nini kushika ujauzito kama imetoka kwa bahati mbaya niacheni nipumzike japo moyo unaniuma kumpoteza mwanangu.”

    “Kwa hiyo humpendi Amba?”

    “Nampenda, lakini kuna kitu kimenishtua jana.”

    “Kitu gani?”

    “Siwezi kukisema mbele ya baba,” Atuganile alisema kwa aibu.

    Ilibidi baba yake aondoke ili kumwacha azungumze na mama yake, baada ya kutoka mama yake alitaka kujua kilichomshtua mwanaye.

    “Ehe, niambie mwanangu, kipi kimekushtua?”

    Alimueleza hali iliyomtokea mpenzi wake jana yake walipokutana faragha.

    “Mama hali ile haijawahi kutokea hata siku moja nina wasiwasi na dawa mliyoniambia nikampake.”

    “Si dawa niliyokupa labda ana tatizo lingine,” mama yake alijitetea.

    “Hapana mama dawa uliyonipa jana ndiyo iliyosababisha yote yale.”

    “Sasa mimi nifanye hivyo ili iweje, shida yangu nataka kuhakikisha unaolewa naye.”

    “Mmh! Sawa.”

    “Sawa nini?”

    “Nimekubali, lakini nitampakaje bila yeye kujua kwa ajili ya nini?”

    “Inatakiwa umpake kwa siri asijue.”

    “Hapo ndipo penye tatizo, angekuwa mzima ningeweza kafanya zoezi hilo bila tatizo.”

    “Kuna dawa ya kunywa nitakupa ukampe kisha tuangalie ili ufanye zoezi lako.”

    “Kama hivyo nitakuwa sawa.”



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Atuganile alimkubalia mama yake huku akipanga kwenda kwa bibi Tumwambilile kumweleza hali ya mpenzi wake pia tatizo la kupoteza ujauzito limetokana na nini.

    Mama yake alimpa dawa ya kunywa kwa siku tatu kwenye maji ya vuguvugu. Baada ya kuchukua dawa aliiweka ndani na kupanga kumpelekea akitoka kwa bibi.

    Aliachana na wazazi wake na kwenda kufanya shughuli za usafi kisha aliondoka bila kuaga. Alikwenda mpaka kwa bibi Tumwambilile, alizunguka na kutokea nyuma ya nyumba uani. Lakini alishangaa kukuta pako kimya, ilibidi aite kwa sauti.

    “Bibiiii….Bibiiii.”

    Lakini hakukuwa na jibu, aliamua kuingia ndani huku akimwita kwa sauti.

    “Bibiii….Bibiiiii Tumwaa.”

    “A..a..be,” ilisikika sauti ya chini ikitokea chumbani.

    Atuganile alishtuka na kwenda chumbani kwa bibi Tumwambilile, alikuta amelala kitandani.

    “Vipi bibi unaumwa?” Atuganile alishtuka.

    “Kiasi, afadhali umekuja maana leo asingekuja mtu kwangu ningekufa.”

    “Kwa nini bibi?”

    “Kwanza kafunue kwenye mtungi wangu sebuleni kuna kifurushi cheusi, fungua toa dawa kidogo nichanganyie na maji uninyweshe,” Bibi Tumwambilile alisema akiwa bado amelala kitandani.

    Atuganile alifanya kama alivyoelekezwa na bibi Tumwambilile, alikwenda kwenye mtungi mkubwa uliokuwa nyuma ya mlango wa kuingilia na kufunua ungo uliokuwa juu yake. Alipotaka kuingiza mkono alishtuka kuona kuna joka kubwa limo mule, alishtuka na kupiga kelele.

    “Mamaaa! Nakufa!” Atuganile alipiga kelele za woga zilizomfanya bibi Tumwambilile kuuliza kwa sauti ya shida.

    “Nini mjukuu wangu?”

    “Bibi joka!”

    “Hebu njoo.”

    Atuganile alikwenda chumbani kwa bibi akitweta kwa hofu huku akitetemeka.

    “Unasema umeona nini?”

    “Joka kubwa bibi”

    “Pole mjukuu wangu.”

    “A..a..sante.”

    “Mbona hakuna kitu kwenye chungu ni wasiwasi wako, hebu rudi ukaangalie hakuna joka.”

    “Hapana bibi siendi kuna joka litaning’ata.”

    “Yule ni mlinzi, nilisahau kukujulisha ila sasa hayupo kanichukulie dawa nitakufa mjukuu wangu.”

    “Mmh! Sawa bibi kwa vile wewe ni mtu wangu muhimu, la sivyo nisingekwenda.”

    “Sawa mjukuu wangu.”

    Atuganile alirudi kwenye mtungi mkubwa ambao wakati huo ulikuwa wazi, alisogelea kwa tahadhari kubwa. Alichungulia kabla ya kuingiza mkono ili kuona kama kweli hakuna lile joka kubwa. Lakini ajabu hakukuwa na joka zaidi ya tunguli.

    Aliingiza mkono na kutoa kifurushi cheusi na kukifungua na kukuta dawa ya rangi ya njano. Alichukua bakuli na kuweka ile dawa kwenye maji na kumpelekea bibi Tumwambilile.

    Kabla ya kumpa alimkalisha kitandani na kumsaidia kumnyesha kwani hata nguvu za kushika bakuli hakuwa nazo. Alimnywesha yote kisha alimrudisha kitandani ili asubiri atamwambia nini.

    “Bibi nifanye kitu gani tena?”

    “Zunguka nyuma ya nyumba kuna mti mmoja mfupi una majani mapana, chuma matatu kisha yaweke kwenye maji ya kuoga kisha njoo unisaidie kunitoa nje ili nikaoge.”

    Atuganile alifanya kama alivyoelekezwa, akaenda nyuma ya nyumba na kuchuma majani matatu na kuyaweka katika beseni la maji na kupeleka bafuni ambako alimuwekea na kigoda cha kukalia.

    Alimfuata ndani na kumsaidia kumshika mkono mpaka nje na kumpeleka bafuni, alimkalisha kwenye kigoda na kuanza kumuosha huku akimsugua yale majani kila kona ya mwili.

    Baada ya zoezi lile, bibi Tumwambilile alimuomba Atuganile atoke nje, alitoka na kwenda kukaa kwenye gogo lililokuwa uani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alijikuta akijiuliza kuhusu lile joka ambalo bibi alisema ni mlinzi. Alijiuliza bila ruhusa yake lingemfanya nini.

    “Atu,” sauti ya bibi ilimshtua.

    “A..a..bee bibi,” Atu aliitikia huku akishangaa kumuona bibi Tumwambilile akitokea ndani akiwa amejifunga kaniki wakati alimuacha bafuni na hakumuona kupita kwenda ndani.

    Alitaka kumuuliza lakini aliachana nayo na kufuata yake.

    “Njoo ndani.”

    Atu alinyanyuka na kuingia ndani, waliingia chumbani na kumwambia akae kwenye kitanda, naye alikaa pembeni yake.

    “Atu mjukuu wangu nashukuru kwa kuja kunisaidia bila hivyo ningekufa.”

    “Pole bibi ugonjwa umekuanza saa ngapi wakati uliondoka salama?”

    “Jana nilikuwa na vita nzito, bila ujuzi wa ziada nilikuwa nakufa, kwanza nilitaka kukujulisha ile kazi yako jana ilikamilika.”

    “Usiniambie!” Atuganile alishtuka kwa furaha.

    “Sasa hivi Kilasilo ni vilio, yule msichana kapotea katika mazingira tata na akionekana atakuwa marehemu.”

    “Duh! Bibi asante,” Atuganile alimshukuru bibi Tumwambilile kwa kuondoa kizingiti cha ndoa yake na Ambakisye.

    “Ila jana kuna mganga alitaka kumtoa kabla hajatoka uhai, hali ilianza kuwa mbaya kwa kunivuta na nguvu zake. Lakini washirika walinisaidia na kuweza kunivuta kisha tulimuangamiza.”

    “Kivipi?”

    “Tulituma mamba aliyemkamata na kumzamisha, alipotoka alikuwa marehemu.”

    “Mmh! Kwa hiyo vita ni kali?”

    “Tena kubwa, lakini wala isikuogopeshe nimeisha izoea nilijisahau kidogo ndiyo maana aliniwahi. Mpaka narudi hali ilikuwa mbaya, ugumu wangu ndiyo ulionifikisha asubuhi bila hivyo nilikuwa nakufa najiona.”

    “Pole bibi, sasa utafanyeje wakija tena?”

    “Kuanzia sasa hivi najipanga, sikai kizembe tena.”

    “Sasa bibi kuna kitu kimenileta.”

    “Kitu gani?”

    “Nina imani unajua kilichonipata jana?”

    “Ndiyo.”

    “Eti nani aliyefanya vile?”

    “Kwa vile umepona achana nayo.”

    “Bibi niambie eti wazazi wa Ambakisye wanahusika?”

    “Mjukuu wangu ukifukua jalala lazima utakutana na uvundo, nisikilize mimi achana nayo.”

    “Kingine bibi majuzi nilipewa dawa na mama nikampake mpenzi wangu...

    Itaendelea wiki ijayo.

    ili asiniache, lakini ajabu jana nilipokutana naye hakuwa na nguvu za kiume kilichonitisha zaidi sehemu zake za siri zilizidi kusinyaa. Nimemwambia mama labda sababu ni ile dawa lakini alikataa ila amesema atanipa dawa ya kunywa nimpelekee mpenzi wangu anywe kwa siku tatu kisha atanipa dawa nikampake.

    “Bibi hebu nieleze tatizo la mpenzi wangu linatokana na nini?”

    Bibi Tumwambilile alitulia kwa muda kisha alichukua ugoro na kunusa kisha alipiga chafya na kusema:

    “Mjukuu siku zote chanzo cha moto mkubwa cheche.”

    “Una maanisha nini?”

    “Dawa ya kunywa mpelekee mpenzi wako, ila ya kumpaka usimpake.”

    “Ina nini?”

    “La muhimu kufuata niliyokueleza mengine achana nayo, dawa yoyote utakayopewa na mama yako juu ya Ambakisye usiitumie bila kuniambia.”

    “Sawa bibi.”

    “Hebu nenda kwa mzee Mwangibile kaniletee chimpumu nizimue kwani nilikuwanakufa.”

    Atuganile alipitia kikopo cha lita moja na kuelekea kwenye kilabu cha Mwangibile kununua chimpumu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Atuganile alipitia kikopo cha lita moja na kuelekea kwenye klabu cha Mwangibile kununua chimpumu. Baada ya kununua, alimpelekea kisha aliondoka kurudi nyumbani ili baadaye aende kwa mpenzi wake kumpelekea dawa.

    Siku ya pili, Ambakisye aliamka asubuhi kama kawaida na kujiangalia kutokana na mabadiko wakati akitaka kufanya mapenzi na mpenzi wake usiku. Aligundua mabadiliko sehemu zake za siri kutokana na maiki kuwa dolo kitu ambacho si cha kawaida kwani lazima aamke na kujikuta amesisimkwa sehemu zake.

    Hali ile ilimshtua sana na kumfanya ajiulize inatokana na nini, hali ile ilimtisha na kutaka kwenda kumueleza baba yake. Lakini alitaka kwanza aiache siku ile ipite ili ajiangalizie jioni akikutana tena na mpenzi wake. Akiwa bado hajapata jibu alisikia hodi. Ilikuwa sauti ya mpenzi wake Atuganile, alimkaribisha:

    "Karibu pita ndani."

    Baada ya kuingia ndani alimsalimia mpenzi wake.

    "Vipi mpenzi unaendeleaje?"

    "Mpaka sasa sijielewi maana nimeamka asubuhi mtalimbo umekuwa dolo."

    "Inaweza kuwa tatizo kubwa?"

    "Ndiyo wasiwasi wangu mkubwa."

    "Hebu nione."

    Ambakisye alimuonesha rafiki yake sehemu zake nyeti ambazo zilionesha kunywea.

    "Mmh! Sasa tatizo nini?"

    "Hata najua! Sasa nijaribu tena ili nione." Walikubaliana kujaribu asubuhi ile hali ilikuwa ileile mtalimbo uliendelea kulala dolo.

    "Amba una nini mpenzi wangu?"

    "Najua yaani sijui nani kanifanya hii, lazima utakuwa mkono wa mtu."

    "Ambakisye au yule mwanamke ana mpenzi wake ndiye aliyekufanya."

    "Sasa anifanye hivi kwa kosa gani? Si angewafanyia waliomnyang'anya mke!"

    "Amba kuna dawa nimekuletea ili ujaribu kutumia."

    "Dawa ya nini?"

    "Ya kurudisha nguvu za kiume."

    "Umetoa wapi."

    "Kwa..kwa…"

    Alihofia kusema kapewa na mama yake kuhofia kukataliwa, ilibidi aseme uongo.

    "Ni..nimepewa na bibi Tumwambilile."

    "Halafu umejuana naye vipi yule bibi nasikia wanasema kigagula (mchawi)?"

    "Mimi nitajuaje ikiwa hajaniroga."

    "Nasikia wanasema anatisha."

    "Kama angekuwa mchawi jana angenisaidia."

    "Kakusaidia nini?"

    "Basi jana nilipotoka hapa usiku tumbo liliniuma, maumivu niliyosikia nilimuona mtoa roho kanisimamia mbele yangu. Nilijitahidi kwenda kwa wazazi ilishindikana na nilitokwa na damu nyingi kisha nilianguka na kupoteza fahamu."

    "Mungu wangu unasema umetoa damu nyingi?"

    "Ndiyo mpenzi wangu."

    "Mmh! Mwanangu ana usalama?"

    "Autoe wapi, bibi Tumwambilile alifuatwa na kuja kunusuru roho yangu."

    "Kwa hili familia yako inahusika."

    "Ihusike nini?"

    "Kutoka kwa ujauzito wa mwanangu."

    "Utaionea lakini hata wao wamesikitika sana."

    Wakiwa katikati ya mazungumzo walisikia sauti ya juu ikimwita Ambakisye.

    "Ambakisye."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Naam mama."

    "Njoo mara moja."

    Alitoka nje na kwenda kwa wazazi wake, alipofika alishtuka kuwaona katika sura za huzuni. Pia walikuwepo wageni ambao aliwafahamu ni ndugu wa mchumba wake Bupe.

    "Naam mama, ooh! Wageni karibuni, za Kilasilo?"

    "Nzu..nzuri," walijibu kwa kigugumizi.

    "Mke wangu Bupe hajambo?"

    Swali lile lilikuwa kama kaa la moto mdomoni, walishindwa kulijibu moja kwa moja na kubaki wakitazamana. Hali ile ilifanya baba yake aingilie kati na kusema:

    "Hebu kaa kwanza tuzugumze kilichotokea."

    "Sawa," alijibu na kusima ili asikie alichoitiwa.

    Baada ya ukimya mfupi kila mmoja akiwa ameinamisha kichwa chini, mzee Andendekisye alisema kwa sauti ya upole:

    "Kuna taarifa tata zimefika toka kwa mchumba wako kuwa ametoweka katika mazingira ya kutatanisha."

    "Mkisema mazingira ya kutatanisha mnamaanisha nini?"

    Alielezewa yaliyotokea Kilasilo yaliyomhusu mpenzi wake kuchukuliwa kichawi na mamba ambaye alimchagua yeye peke yake katika kundi la watu."

    "Mungu wangu, ina maana ule mto una mamba?"

    "Hauna, juzi ilikuwa ajabu ya mwaka, kibaya kingine mganga aliyesema atamrudisha alishikwa na mamba na kuzamishwa ndani ya maji na kuokotwa siku iliyofuata akiwa amekufa na kunyofolewa baadhi ya sehemu za mwili.""Mmh! Kazi ipo, nani aliyefanya hivyo?"





    “Hajajua, ila nitaingia kazini kuangalia nani kafanya vile, nikimjua nitakachomfanya Mungu anajua,” alijiapiza mzee Amanyisye.

    “Kwa hiyo nini kinaendelea?”

    “Baba amesafiri leo kwenda Malawi kutafuta tiba kwa vile wanasema uchawi ule unatumika sana huko,” alisema mmoja wa vijana waliokuja kuleta taarifa za kupotea kwa Bupe mchumba wa Ambakisye.

    “Nami nitamtafuta aliyefanya vile nikimjua nitamaliza familia nzima,” alizidi kujiapiza mzee Amanyisye.

    “Sawa nimesikia,” alisema Ambakisye kwa unyonge huku moyoni akifurahi kupotea kwa yule msichana lakini hakupenda afe.

    “Kuna kauli iliyotukatisha tamaa, mganga aliyekufa maji alisema kuwa siku ya jana ikipita hatutampata tena na tukimpata atakuwa ameishakufa,” alisema kaka yake huku akitokwa machozi ya uchungu.

    “Wee waache si wameanza sisi tutamaliza,” mzee Amanyisye aliendelea kujitapa kwa hasira.

    Baada ya vijana walioleta taarifa za kupotea Bupe kuondoka, wazazi wa Ambakisye walikaa kikao cha faragha kulijadili lililotokea.

    “Mke wangu mi nina wasiwasi na familia ya Andendekisye!”

    “Hata mimi nilikuwa na wazo hilo, inawezekana kabisa kitendo cha Amba kumpatia ujauzito mtoto wao ndicho kilichosababisha wafanye hivyo,” mkewe aliunga mkono wazo la mumewe.

    “Na ile dawa tuliyompa aitege aliitega kweli?”

    “Hata mimi nashangaa leo siku ya ngapi hatujapata majibu.”

    “Hebu mwite.”

    Mama Ambakisye alimwita mwanaye kwa sauti ya juu.

    “Ambaaa!”

    “Naam mama.”

    “Hebu njoo.”

    Ambakisye aliyekuwa akimpa taarifa Atuganile aliyejifanya kushituka alimuacha na kwenda kumsikiliza mama yake.

    “Mpenzi nakuja.”

    “Dah! Pole sana nenda ukawasikilize.”

    Atuganile alikuwa na hamu ya kujua familia ya mpenzi wake itapokea vipi kupotea kwa mchumba wa mtoto wao katika mazingira ya kutatanisha. Ambakisye alikwenda hadi kwa wazazi wake, alipofika alisimama mbele yao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Naam.”

    “Eti ile dawa ulimtegea Atu?”

    “Ndiyo jana, halafu kitu cha ajabu alipotoka na kuruka ile dawa alipiga kelele na kuinama chini akishika mikono chini ya kitovu. Usiku alipolala kwao ile hali ilijirudia tena safari ile ilisababisha atokwe damu nyingi na kusababisha kupoteza ujauzito wake,” Ambakisye alisema kwa masikitiko.

    “Mmh!” waliguna wote.

    “Sasa mbona haikusaidia kitu?”

    “Tulikuambia wale si watu wema lazima wameutoa kwa hasira kabla ya kuitega ile dawa,” walitengeneza uongo.

    “Ila hata mimi sikubali aliyemuua mwanangu naye nitamsafiria Malawi, haiwezekani waniulie mwanangu asiye na hatia.”

    “Ambakisye usirogwe kushiriki uchawi, wewe bado kijana mdogo kazi hiyo tuachie sisi wazazi ndiyo tunaweza kukabiliana nao,” mzee Amanyisye aliwahi kumzima mwanaye kwa kujua bomu limetegewa ndani mwao.

    “Mmh! Sawa lakini ungeniacha tu.”

    “Vita ya kichawi inataka uzoefu, ukienda kichwakichwa utapotea. Sasa hivi uchawi wa bure. Kwa vile nimeahidi kupambana nao basi niachie mimi kazi hiyo.”

    “Sawa baba.”

    “Basi kaendelee na kazi yako.”

    Ambakisye aliondoka na kuwaacha wazazi wake wakiendelea kuteta, alirudi hadi chumbani kwake na kupokewa na Atuganile aliyekuwa na hamu ya kujua mpenzi wake aliitiwa nini kwani hata uso wake ulijaa simanzi.

    “Amba kuna nini, mbona hivyo?”

    “Mchumba niliyetaka kumuoa kachukuliwa na mamba katika mazingira ya kutatanisha,” alimweleza mengine japo mwanzo hakumwambia.

    “Mungu wangu pole sana,” Atuganile alijifanya kushtuka.

    “Si bure lazima kuna mkono wa mtu.”

    “Lakini mpenzi usisikitike sana mimi mpenzi wako wa damu si nipo?”

    “Sawa, lakini huoni kama wanaweza kutufikiria vibaya labda tumepanga kumpoteza ili tuendelee kuwa pamoja. Japo tuko pamoja lazima kipindi hicho uhusiano wetu usiwe wa wazi sana kuonana kwetu iwe usiku tu.”

    “Sawa, lakini sikubali utafutiwe mwanamke mwingine kama amepotea au amekufa nasubiri ndoa yangu.”

    “Hakuna tatizo, kama hivyo sitakubali kuchaguliwa tena mwanamke,” Ambakisye alimuhakikishia mpenzi wake.

    “Nimefurahi kusikia hivyo, basi naomba utumie hii dawa ili tujue tatizo nini.”

    “Mmh! Sawa, lakini lazima nizungumze na baba ili nijue ataniambiaje.”

    “Amba kwa nini usitumie tu ili tujue kitakuwa nini kuliko kuwapa presha wazazi wako?”

    “Hapana lazima nimwambie baba kwa vile ni mtu wangu wa karibu ili nijue atanisaidia vipi kabla ya kutumia dawa.”

    “Bibi Tumwambilile tatizo lako aliliona na kusema ukitumia dawa hii ndani ya siku tatu kila kitu kitaenda vizuri.”

    “Sawa, lakini hili ni jambo zito kwa vile toka nizaliwe halijawahi kunitokea, jana nilijua ni uchovu wa safari lakini leo imenijulisha kuwa hili ni tatizo.”

    “Kwa hiyo dawa hii niirudishe?”

    “Hapana, niachie ila lazima nimwambie kwanza baba nisije sema hali imekuwa mbaya.”

    “Mmh! Sawa.”

    “Atu kuna kitu gani kati yetu?”

    “Kipi?”

    “Kwa nini matatizo yametutokea kwa siku moja, huoni hapo kuna mchezo fulani tuliochezewa?”

    “Mmh! Kweli kabisa mpenzi wangu siku uliposhindwa kufanya kazi usiku wake ndipo niliharibu ujauzito wangu.”

    “Unafikiri ni kwa amri ya Mungu?”

    “Hapana lazima kuna mkono wa mtu.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hujamuuliza bibi Tumwambilile tatizo lako linatokana na nini?”

    “Aliniambia nikifukua sana uchafu nitakutana na uvundo na chanzo cha moto mkubwa ni cheche.”

    “Alimaanisha nini?”

    “Nilimuuliza, aliniambia kwa vile nimepona haina haja ya kuchimba sana.”

    “Na mimi?”

    “Kaniambia utumie dawa hii utapona kabisa.”

    “Sasa fanya hivi nitakupitia kwenu ili twende tukamchimbe bibi Tumwambilile, nina senti kidogo najua atakubali kutueleza.”

    “Sawa, basi mi nitakusubiri, muda mzuri jioni nitakuwa nimemaliza kazi.”





    “Poa.”

    Walikubalia amweleze baba yake ili wajue atamsaidia vipi pia ampitie jioni waende kwa bibi Tumwambilile wakajue matatizo yao yanatokana na nini. Kwa vile Atuganile hakutaka wazazi wa mpenzi wake wamuone alitokea dirishani na kwenda kumsubiri Ambakisye kwa mbele.

    Baadaye Ambakisye alitoka na kumfuata njiani na kumsindikiza lakini mama ya Ambakisye aliwaona kwa mbali wakisindikizana na kumwambia mumewe.

    “Baba Amba.”

    “Unasemaje?”

    “Umemuona mwanao kumbe alikuwa na mwanamke wake.”

    “Kapitia wapi?”

    “Hata najua.”

    “Umewaona wapi?”

    “Si walee,” alimuonesha Ambakisye aliyekuwa akimsindikiza mpenzi wake kwa mbali.

    “Mmh! Kazi ipo ndiyo maana hakushtuka sana tulipompa taarifa ya kupotea kwa mpenzi wake.”

    “Nina wasiwasi hata mwanetu anahusika na mpango huu, yaani hakutoa hata chozi ndiyo kwanza yupo na mpenzi wake.”

    “Kule kuonesha ameumizwa na tukio lile na kufikia hatua ya kutaka kupambana, kumbe muongo mkubwa.”

    “Kama ni hivyo basi vita yetu itakuwa ngumu.”

    “Wee fuatilia kwa mtu wako ili tujue tatizo lipo wapi?”

    “Lazima nifanye hivyo.”

    “Kabla ya kulipua hakikisha Amba hahusiki tusijelia mikono kichwani.”

    “Lazima nifanye hivyo.”

    Wakati huo Ambakisye alikuwa akirudi kutoka kumsindikiza mpenzi wake. Alipofika karibu, wazazi wake walibadilisha mada ili asijue walikuwa wakizungumza nini.

    “Baba,” Ambakisye alimwita baba yake.

    “Unasemaje?”

    “Samahani njoo chumbani kwangu mara moja.”

    Baba yake bila kusema kitu alinyanyuka na kumfuata mwanaye chumbani, walipoingia Ambakisye alimueleza baba yake tatizo lililojitokea jana usiku na muda mfupi. Baba yake alishtuka kidogo na kumuuliza:

    “Hali kama hii imewahi kutokea mara ngapi?”

    “Ndiyo mara ya kwanza kibaya hata sehemu za siri zinasinyaa.”

    “Eti?” baba yake alishtuka.

    “Ndiyo baba hali hii imenitisha, kitu cha ajabu imejitokeza kwa wakati mmoja usiku wa jana ilianza kwangu kisha mwenzangu kutoka ujauzito kitu ambacho kinanitisha.”

    “Inawezekana kabisa familia ya mpenzi wako inahusika.”

    “Baba hebu kwanza angalia tatizo langu mbona mnapenda kuwashutumu kila kitu?” Ambakisye alisema kwa jazba kidogo.

    “Hebu teremsha nguo zako nione.”

    Ambakisye aliteremsha kaptura aliyokuwa amevaa na nguo ya ndani na kumuonesha baba yake ambaye alishtuka kuona mambo yapo vile.

    “He! Hili ni tatizo.”

    “Vaa twende mtoni.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ambakisye alivaa nguo zake na kwenda mtoni ambako watu walikuwa wakitumia kuoga. Kauli ya baba yake ilimfanya kujiuliza amegundua nini mpaka kumweleza waende mtoni, hakujua wanakwenda kufanya nini. Njiani mzee Amangise alichuma majani na kuendelea na safari yao.

    Walipofika mtoni walitafuta sehemu iliyokuwa imejificha, baada ya kufika sehemu hiyo ambayo ilikuwa na miti mingi, alimwambia mwanaye atoe nguo zote kama anataka kuoga.

    Ambakisye alifanya kama alivyoelezwa na baba yake, alitoa nguo zote na kusubiri kuona baba yake anataka kufanya nini.

    Mzee Amangise alichukua majani mabichi aliyochuma njiani na kuyafikicha kisha aliyazungusha sehemu za siri za mwanaye na kumwambia aingie ndani ya maji.

    Baada ya kuingia ndani ya maji, baba yake aliangalia sehemu za siri za mwanaye. Hali aliyoiona ilimshtua sana na kumuuliza mwanaye akiwa bado yumo ndani ya maji.

    “Amba hali hii imekuanza lini?”

    “Baba si nimekuambia jana usiku.”

    “Hapana ugonjwa huu huwa wa kuzaliwa si wa kuugua ukubwani kama ungeugua ukubwani kwa dawa niliyokufunga ingeonesha ni tatizo la kutibika, lakini kwa hali hii inaonesha kabisa hata tufanye nini huwezi kupona.”

    “Baba kwani naumwa ugonjwa gani?”Ambakisye alishtuka.

    “Ugonjwa wa kukosa nguvu za kiume wa kuzaliwa.”

    “Hapana baba, siwezi kuugua ugonjwa huo kwa vile ni jana usiku tu wala sina muda mrefu.”

    “Hebu toka ndani ya maji.”

    Ambakisye alitoka ndani ya maji na kuvaa nguo zake, alijikuta akikosa raha kwa maneno ya baba yake. Ilibidi apate ukweli wa tatizo lake kwa kumuuliza baba yake.

    “Baba una maanisha ugonjwa huu hauponi?”

    “Watu wanaokuwa hivyo huwa hawaponi, huu ni wa kuzaliwa nao kwako nashangaa kusema ni jana na kuwa katika hali hii. Mmh! Nimeishajua, naona sasa wananichezea baada ya kumchukua kichawi mchumba wako sasa wamekugeukia mwenyewe.”

    “Kina nani?”

    “Kwani waliondoka siku ya kikao wakisema tutawaona wao kina nani?”

    “Una maanisha familia ya kina Atu?”

    “Ndiyo, walisema watakukomoa naona wametimiza azma yao.”

    “Huenda basi nao wamelipa kisasi cha Atuganile kutolewa ujauzito.”

    “Wala hiyo siyo sababu hebu tupitie kwa Mwakasanga tukaangalie tatizo nini.”

    Walikubaliana kupitia kwa Mwakasanga mtaalamu wa tiba za jadi, walipofika waliingia ndani ili wamweleze tatizo lao.

    “Karibuni, naona leo baba na mwanaye mmenitembelea?”

    “Ndiyo ndugu yangu.”

    “Mbona nyuso zenu zinaonesha kuna tatizo?”“Ni kweli.”





    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kusema vile Mwakasanga aliangalia juu akiwa ameshika mkono kidevuni kwa muda na kucheka kidogo kisha aliuliza:

    "Mmh! Mlikuwa mnasemaje?"

    "Nina imani umeona kila kitu."

    "Ndiyo, mlikuwa mnatakaje?"

    "Umsaidie mwanangu pia kumjua aliyefanya hivi."

    "Waswahili wana usemi wao kuwa moto mkubwa ulianza cheche."

    "Unamaanisha nini?"

    "Unajua vizuri kwa hiyo vita mnayoitafuta haitakuwa na mshindi zaidi ya kubakisha magofu ya miji yenu."

    "Vita na nani?"

    "Mzee Amanyisye we' mtu mzima unajua ulichokifanya na ndicho ulichofanyiwa."

    "Kwa maana hiyo wamelipa kisasi?"

    "Walaa hawajalipa ila wanajipanga kulipa kisasi ila kilichotokea ulipiga wakapiga kila aliyepiga amefanikiwa kutimiza alichokikusudia bila waliotumwa kujua wanaharibu."

    "Nimekuelewa, sasa utanisaidia vipi?"

    "Wewe ndiye mwenye uwezo wa kumaliza tatizo kwa kwenda kwa mwenzio ili muombane samahani bila hivyo nakuapia hakuna mshindi. Mnaweza kuona mlifanya kidogo ndicho kilichompoteza mchumba wa mwanao. Kama nilivyokwisha kusema mwanzo wa moto mkubwa ni cheche na ninavyokwambia tayari moto umeishaanza kuchoma pori sijui nani atapona."

    "Sasa utanisaidiaje?"

    "Unatakiwa kwanza usafishwe kwa vile sasa hivi umechafuka kila nitakachokufanyia hakitakusaidia. Siku zote nguo nyeupe inataka mwili msafi."

    "Mmh! Sawa, na huyu?"

    "Nitakupa dawa atumie kwa siku tatu ikishindikana itabidi nimtibu kichawi."

    "Sawa."

    Walikubaliana kupanga siku ya mzee Amanyisye kupelekwa mzimuni kutubu aliyoyafanya ili aweze kupewa tiba. Ambakisye alipewa dawa ya unga ya kunywa na kuelezwa atumie kwa siku tatu kisha arudi. Alichukua dawa na kuondoka na baba yake aliyeamini amemjua mbaya wake hivyo ni kuingia vitani kuwasambaratisha.

    Wakiwa njiani wanarudi nyumbani, Ambakisye alikuwa na mawazo mengi juu ya kauli za mganga zilizoonesha familia zote mbili zilipigana makombora, moja akiwa amelibeba yeye bila kujua ambalo liliwalipua wenyewe. Alipanga akitoka hapo akambane Atuganile amweleze alipewa nini na wazazi wake kumpelekea bila yeye kujua.

    Pia hakutaka kukaa kimya alimgeukia baba yake na kumuuliza:

    "Baba kumbe dawa uliyonipa ndiyo iliyotoa ujauzito wa mpenzi wangu?"

    "Nani kakwambia?"

    "Si Mwakasanga amesema."

    "Ulimsikia amesema mimi nilikupa dawa ya kutoa ujauzito?" mzee Amanyisye alikuwa mkali kidogo.

    "Hata ukisema kwa ukali baba mmenikosea, hivi nisipopona nitakufa mgumba wakati tayari nilikuwa na mtoto wangu?" Ambakisye alimuuliza baba yake kwa uchungu.

    "Ambakisye aliyozungumza mganga ni mengine kabisa hayahusiani na matatizo yenu," baba yake alipinda ukweli.

    "Sawa ukweli utajulikana tu muda si mrefu."

    "Nimekukataza kujishughulisha na mambo ya waganga unaweza kuambiwa adui ni baba au mama yako ili tu kutugombanisha."

    "Sawa baba nimekuelewa," Ambakisye alikubali shingo upande.

    Walipofika nyumbani baba yake alimhimiza kunywa dawa aliyopewa na mganga na kumuomba tatizo lake liwe siri yao mpaka walimalize pia hata mpenzi wake asimweleze kinachoendelea upande wao. Ambakisye alimkubalia lakini kichwani alikuwa anawaza tofauti.

    Baada ya kunywa dawa aliachana na baba yake na kujipumzisha kusubiri jioni atakapokwenda na mpenzi wake kwa bibi Tumwambilile. Alijilaza kitandani lakini mawazo yake yalikuwa mbali kuhusiana na tatizo lake pia kutoka ujauzito wa mpenzi wake.

    Aliamini cheche za moto zilizoteketeza msitu zilizosemwa na mganga ni baba yake.

    Lakini aliamini yote atayajua akienda kwa bibi Tumwambilile kwa kumbana na kumuahidi zawadi nzuri.

    ****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jioni kama walivyokubaliana na mpenzi wake alimpitia kwao na kwenda kumsubiri kwa mbele. Kwa vile macho ya Atuganile muda wote yalikuwa barabarani alipomuona mpenzi wake akipita alimuacha apite kisha alimfuata kwa kumziba machoni kwa kutokea nyuma yake.

    Ambakisye alimvutia kwa mbele ya kumkumbatia, kila mmoja alionesha furaha kwa mwenzake kutokana na kushibana mioyoni mwao.

    "Za muda?" Atuganile alimuuliza mpenzi wake.

    "Mmh! Kiasi namshukuru Mungu."

    "Vipi, baba alisemaje?"

    "Mmh! Alishtuka sana, alinipeleka mpaka mtoni kunipima kwani hakuamini kusikia tatizo langu lilianza jana usiku. Amesema tatizo lile ni la kuzaliwa nalo anashangaa mimi kulipata jana."

    "Kwa hiyo amesema tatizo lako linapona?"

    "Ndiyo nimeanza kutumia dawa leo."

    "Mungu atakusaidia mpenzi wangu."

    "Asante, Eti Atu, wazazi wako walikupa nini uniletee bila wewe kujua madhara yake?"

    "Kitu gani?" Atuganile alishtushwa na swali la mpenzi wake.

    "Sasa mimi nitajuaje ukiwa ulikibeba wewe."

    "Mmh! Kwani ndiyo sababu ya tatizo lako?" Atuganile alishangaa swali la mpenzi wake ambalo lilimtisha na kuamini kama atajulikana yeye ndiye anayehusika hivyo lazima penzi lao lingevunjika.

    "Ndiyo," alijibu kwa kutojiamini huku vidole vikiwa mdomoni.

    "Basi ndiyo iliyonimaliza."



    "Mungu wangu! Basi watakuwa wamenidanganya."

    "Kina nani?"

    "Wazazi wangu."

    "Wamekudanganya kivipi?"

    "Waliniambia ni dawa ya kufanya usiniache, kama ni kweli naomba usiniache mpenzi wangu."

    Kauli ya Atuganile ilirudi katika agizo alilopewa Ambakisye na wazazi wake ambalo halikuwa tofauti. Kutumia uongo kama ule alimuua mwanaye bila kujua basi ndivyo ulivyoumizwa na yeye. Kwa hiyo hakuona sababu ya kulaumu kwa vile alifanya bila kufahamu.

    "Atu, siwezi kukulaumu najua tatizo lipo wapi," Ambakisye alimtoa hofu mpenzi wake.

    "Najuta mpenzi wangu kukubali kitu nisichokijua," Atuganile alisema huku akilia kilio cha majuto.

    Ambakisye alimbembeleza mpenzi wake na kumuomba waendelee na safari yao ya kwenda kumuona bibi Tumwambilile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog