Search This Blog

VITA YA WACHAWI - 3

 





    Simulizi : Vita Ya Wachawi

    Sehemu Ya Tatu (3)





    ILIPOISHIA:

    "Najuta mpenzi wangu kukubali kitu nisichokijua," Atuganile alisema huku akilia kilio cha majuto.

    Ambakisye alimbembeleza mpenzi wake na kumuomba waendelee na safari yao ya kwenda kumuona bibi Tumwambilile.

    SASA ENDELEA...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walikubaliana kuondoka kwenda kwa bibi kwa kupitia kilabuni kwa Mwangibile kununua chimpumu ya lita mbili na kwenda nayo.

    Walikwenda hadi kwa bibi Tumwambilile, walipofika walikuta hakuna mtu ila mlango upo wazi na katikati ya mlango kulikuwa na paka mweusi.

    Kwa vile Atuganile alikuwa amepazoea pale, walipofika alimwita kwa sauti ya juu huku akiingia ndani na kumuacha Ambakisye nje.

    "Bibiiii Tumwa."

    Alimpita yule paka mweusi mlangoni na kuingia mpaka ndani na kuendelea kuita mpaka chumbani lakini hakukuwa na jibu la mtu, ilibidi atoke nje alipokuwa amesimama mpenzi wake na kumuita kwa sauti ya kukata tamaa.

    "Mmh! Hayupo."

    "Sasa atakuwa amekwenda wapi?"

    "Hata najua, lakini mlango upo wazi inaonesha hayupo mbali."

    "Basi tumsubiri."

    "Mmh! Labda yupo nyuma ya nyumba."

    "Kamuangalie."

    Atuganile alizunguka nyuma ya nyumba ya bibi Tumwambilile lakini vilevile hakumuona, alirudi na kumueleza mpenzi wake.

    "Hata nyuma ya nyumba hayupo."

    "Basi tumsubiri lazima atakuwa karibu."

    Walisogea pembeni kwenye gogo na kukaa kumsubiri bibi Tumwambilile, paka aliyekuwa mlangoni alitoka alipokuwa amesimama na kuzunguka nyuma ya nyumba.

    Baada ya dakika moja alitokea bibi Tumwambilile nyuma ya nyumba akiwa amejifunga kaniki nyeusi mabega nje.

    "Wajukuu zangu karibuni."

    Kwanza walishtuka kwa vile muda mfupi hakukuwa na mtu, kisha waliitikia kwa pamoja.

    "Asante bibi shikamoo."

    "Marahaba, karibuni wapenzi."

    "Asante."

    "Nakuja," alisema huku akiingia ndani.

    Baada ya kuingia ndani walijikuta wakitazamana na kila mmoja alinyanyua mabega juu. Baada ya muda alitoka bibi Tumwambilile akiwa amebadili nguo na kujifunga kitenge na kingine kujitanda juu. Alikaa kwenye kizingiti cha nyumba yake na kuwafanya Atuganile na mpenzi wake wasogee kwa kubeba kipande cha gogo cha kukalia.

    "Karibuni wapenzi leo naona mpo pamoja," bibi alisema huku akiachia tabasamu la kizee.

    "Asante bibi," waliitikia kwa pamoja.

    "Leo jua litawaka usiku Ambakisye kuja kwangu."

    "Hapana bibi, huwa napita lakini sikuoni.

    "Mmh! Kuna kipi kimewaleta jioni?"

    "Bibi kama tulivyozungumza nimeona leo nije na mwenzangu."

    "Tulizungumza nini?"

    "Kuhusu matatizo yetu."

    "Kwani nilikuambiaje?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ulisema nisiyachimbue sana kwa vile tumeshapona."

    "Kipi kimebadilika?"

    "Hali ya mwenzangu ndiyo bado inatuchanganya."

    "Nilikuambia nini kuhusu tatizo lake?"

    "Ile dawa niliyopewa na mama hakutumia alisema mpaka azungumze na baba yake, jioni tulipokutana alinieleza walienda kwa Mwakasanga," Atuganile alijisahau kuwa alimwambia mpenzi wake kapewa na bibi Tumwambilile.

    "Yule mganga?" bibi Tumwambilile aliuliza.

    "Ndiyo."

    "Ehe."

    "Basi kule sijui walielezwa nini na kupewa dawa nyingine ambayo kaanza kuitumia leo, kaambiwa baada ya siku tatu arudi kujua anaendeleaje. Ameniomba nije kwako ili utusaidie tujue tatizo lipo wapi."

    "Sasa mbona unamuongelea kama yeye hana mdomo," bibi Tumwambilile alimgeukia Atuganile aliyeongea kwa niaba ya mpenzi wake.

    "Amba hebu mwambie bibi ili atusaidie."

    "Bibi nafikiri hakuna nitakachosema tofauti na aliyoyasema mpenzi wangu. Ni kweli bibi hali yangu ni mbaya na inaonekana kabisa matatizo yetu wazazi wetu wanahusika kwa asilimia kubwa kwa kutupa dawa kwa kutudanganya matokeo yake imekuwa madhara kwetu.

    "Bibi nina imani wewe ni msaada mkubwa kwetu hebu tupe ukweli wa tatizo hili, japo hupendi tuchimbue lakini mambo mengi yapo wazi kwa vile kuna siri kubwa kwa wazazi wetu."

    "Kwani mlipokwenda kwa Mwakasanga alisemaje?"

    "Alimwambia baba kuwa alipiga naye kapigwa."

    "Alipiga nini na kapigwa nini?"

    "Inaonekana kutoka kwa ujauzito wa Atu, ulitoka katika familia yangu na mimi ndiye niliyemuua mwanangu bila kujua. Na hii hali niliyonayo inatoka katika familia ya mpenzi wangu naye aliniuliza bila kujua kama hali hii itanitokea. Pia alimuuliza kama ilikuwa wanalipa kisasi alijibiwa kuwa upande wa pili ndiyo wanajiandaa kulipa kisasi sasa sijui kisasi cha nini na kisasi gani.

    Alimwambia kuwa vita ya familia mbili haitapata mshindi zaidi ya kubakisha magofu, suluhu ni familia mbili kukaa chini kumaliza tofauti zake. Kwa hiyo bibi naomba msaada wako."

    "Msaada upi?"

    "Kwanza kupata ukweli ya ninayowaza juu ya wazazi wetu, kipi kilipigwa toka pande zote. Na mwisho naomba kama yote ninayo yawaza yapo sawa basi wewe ndiyo usimame katikati kuiokoa vita ambayo naamini haina mshindi zaidi ya kufa wote."





    “Atuganile leo umetukosea heshima kutuita wachawi,” mama yake alikuja juu.

    “Mama ninyi wachawi tena wabaya na mnajipanga kumuadhibu mpenzi wangu kosa lake nini?

    SASA ENDELEA...



    Nawaambia tumechoka kugeuzwa nyika kuumizwa kwa vita ya mafahari. Na pia nakuhakikishia Amba akifa mniue na mimi la sivyo watakufa wengi.”

    “Unataka kutuua wazazi wako?” baba yake aliuliza.

    “Muueni mpenzi wangu tumechoka kugeuzwa daraja la chuki zenu, hata kama nisingeolewa na Ambakisye kulikuwa na haja gani ya kumroga?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Atu, leo upo sawa au umekunywa pombe?” mama yake alishangazwa na ujasiri wa mwanaye.

    “Kwani kuna neno gani hamkunielewa nimeliongea kilevi?”

    “Nani kakuambia uongo huo?” mama yake aliuliza.

    “Wazazi wangu nawaheshimu sana lakini kwa hili siwezi kukaa kimya kwa vile vita ya kichawi haina mshindi zaidi ya kubakia magofu tu. Kama mmechoka kuishi tuacheni sisi bado wadogo tuna hamu ya maisha. Kwani kila anayekupiga lazima umlipize ninyi si Wakiristo? Yesu aliwafundisha nini, ukipigwa shavu moja geuza na la pili, mbona hamfuati kila kitu lazima mlipe kisasi?”

    Kauli ile iliwafanya wazazi wake wabaki kimya na kushangaa ujasiri wa mtoto wao na kujiuliza kautoa wapi pia aliyosema yote yalikuwa kweli. Ilibidi wawe wapole na mzee Andendekisye alimfuata mwanaye aliyekuwa akilia kwa uchungu na kumbembeleza.

    “Basi mwanangu uliyosema tumekusikia na kutafanya kama unavyotaka, tulifanya vile kwa uchungu. Tusamehe sana hatukuwa na nia mbaya nawe ila kwa watu walio tudharau.”

    “Baba naomba myamalize kwa vile vita yetu tunayeumia ni sisi watoto.”

    “Sawa mama basi kapumzike kila kitu tutafanya kama unavyotaka.”

    Atuganile huku akiendelea kulia aliondoka mbele ya wazazi wake huku moyo wake ukiwa mweupe huku akijiuliza mpenzi wake naye atazungumza nini na wazazi wake na watamuelewa vipi. Aliomba nao wawe tayari kukubali kosa na kujirudi ili tatizo liishe.

    ***

    Ambakisye naye baada ya chakula cha usiku, aliwaita wazazi wake ambao walishangaa wito ule ulionesha una jambo zito moyoni mwake. Baada ya wote kukaa alianza kuzungumza.

    “Wazazi wangu.”

    “Ndiyo mzee.”

    “Wazazi wangu toka nilipotoka tumboni kwa tumbo la mama yangu sijawahi kuwavunjia heshima.”

    “Ni kweli, leo baba unataka kutuvunjia heshima?” mama yake alitania.

    “Hapana na sitawahi ila nilitaka kuwauliza jambo moja.”

    “Jambo gani?”

    “Kuhusu ugomvi wenu na familia ya mzee Andendekisye nini hatima yake?”

    “Mpaka atakapopatikana mshindi,” mzee Amangise alijibu kwa mkato.

    “Sasa hii vita nani anayeumia kati yenu na sisi watoto?”

    “Hiyo si juu yako, wewe ni mtoto sisi wazazi wako tunajua tunachokifanya.”

    “Kwa hiyo mlipomuua mwanangu mlijua mnachokifanya, halafu kibaya mkanituma kumuua mwanangu bila kujua. Hivi ninyi ni wazazi wangu kweli mnaidhuru damu yangu? Nilitegemea ninyi ndiye wa kulea wanangu, kwa bahati mbaya kama Mungu akinichukua lakini kumbe ndiye maadui zangu wakubwa.

    Sasa nimefahamu ule moto uliosemwa unataka kuwaka na kuunguza kila kitu, cheche ni ninyi wazazi wangu, na bado mnataka kuendeleza vita ya nini ina faida gani kwenu. Basi tumieni miili yenu kuliko kutumia miili yetu katika mateso,” Ambakisye aliwapa makavu laivu wazazi wake.

    “Ambakisye wewe mtoto mdogo hujui kitu, mchumba wako kauawa na familia ya mpenzi wako unaona kitu cha kawaida. Mimi ndiye Amangise Mwanambo huwa sirudi nyuma mtu akinianza lazima nimalize.” Mzee Amangise alijitapa.

    “Mmh! Sasa nasema hivi chochote kitakacho mtokea mpenzi wangu au familia yao hakikisheni na mimi mnaniua kama si hivyo mimi ndiye nitakuwa adui yenu namba moja.”

    “Acha vitisho vya kitoto, wewe mtoto utabakia kuwa mtoto.”

    “Mimi si mtoto, hata haya matatizo yangu chanzo ni wewe kwa nini hawakukupiga wewe wananiumiza mimi kwa kiburi chako?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “He! Amba una tatizo gani?”mama mtu alishtuka kauli za mwanaye.

    “Mimi sasa hivi sina tofauti na mwanamke,” Ambakisye alisema kwa uchungu huku akilia.

    ”He! Umefanya nini?” mama yake alishtuka.

    “Sehemu zangu zimekufa na yote sababu yenu.”

    “Mungu wangu! Imeanza lini?”

    “Siku ambayo wazazi wangu mlishiriki kumuua mwanangu.”

    “Mmh!” maneno yalikuwa mazito.

    “Wazazi wangu siamini, tena leo baba kaambiwa kuwa chanzo ni cheche na suluhu ni kuelewana na si nguvu za kichawi.”

    “Unamuamini vipi mganga?” baba yake aliingilia kati.

    “Basi naomba kuanzia leo mnitoe kwenye familia yenu nitahangaika kivyangu. Nina imani kwa nguvu za Mungu nitapona na nguvu zenu za kichawi zitashindwa. Kuanzia leo ukitaka kupigana na familia ya mzee Andendekisye tafuta ugomvi mwingine si kuhusu mimi.

    Naomba nikinyanyua mguu wangu hapa nifuteni katika akili zenu, mkiweza kuniroga nirogeni nife lakini Mungu ataniongoza siku zote haki ya mtu haipotei.

    “Pia nakuombeni nikifa msije kunizika hata kama nitaoza au nikiliwa na wadudu,” baada ya kusema vile aligeuka na kuelekea chumbani kwake na kuwaacha wazazi wake wakiwa wamepigwa bumbuwazi.

    “Baba Amba umemsikia mwanao?”

    “Mmh! Alipofikia sehemu inatisha, au amekunywa?”

    “Kwani aliyosema kuna la uongo?”

    Wakiwa katikati ya mazungumzo Ambakisye alitoka na begi lake, hali ile ilimfanya mama yake kukimbia mbio na kwenda kujitupa mbele ya mwanaye.“Amba mwanangu unataka kufanya nini, kwa nini

    unachukua uamuzi mkubwa kama huo?”

    “Nina imani mnaye mtoto mwingine naomba niwaache na maisha yenu nikifa Mungu atanisitiri.”

    “Hapana baba usiondoke linazungumzika.”

    “Kwani nikiondoka kuna mtakachopungukiwa, kama mateso ya vita yenu napata mimi, heri niondoke ili nife na Mungu wangu.”

    “Ambakisye mwanangu ni hasira tu baba, nimekusikia mwanangu nipo tayari kuyafanya yote. Usiondoke tupo chini ya miguu yako,” mzee Amangise naye aliungana na mkewe kumuomba mtoto wao asiondoke.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Watu waliumia kutokana na tabia za Bupe kila mvulana alipenda awe mkewe, wengi waliamini mchezo ule umefanywa palepale kijijini kwa wivu wa kuolewa yeye na kuwaacha wasichana wengine. Kilasilo kila mtu alisema lake lakini mzee Ambokile alijua kila kitu.

    SASA ENDELEA...



    Kutokana na mwili kutoka kwenye maji hawakutaka kuuweka sana, walipanga mazishi yake siku ya pili asubuhi. Siku ya pili yalifanyika mazishi yaliyohudhuriwa na umati wa watu ambao waliguswa na msiba ule ambao nguvu za giza zilitawala na kutishia ndoa za wasichana wa Kilasilo ambao walikuwa mbioni kuolewa kwa kuamini nao watakufa kama Bupe.

    Baada ya mazishi, jioni mganga alikuwa na mazungumzo na familia ya mzee Ambokile juu ya tukio lile.

    "Jamani nimejitahidi kadri ya uwezo wangu, lakini nilikuwa napambana na jeshi la watu wengi. Bila hilo ningeweza kumtoa hai. Sasa baada ya tukio hilo kama wazazi mlikuwa mnasemaje?"

    "Tunakusikiliza wewe."

    "Mnamuachia Mungu au na nyinyi mnataka kurudisha kombora lilipotoka?"

    "Kwa vile wamemkata binti yangu hivihivi na mimi nataka aliyefanya hivi basi naye akatike kama mwanangu," alisema mama Bupe kwa uchungu.

    "Basi kazi hiyo kwangu ndogo sana," alisema mganga Msioka.

    "Unasema wameshiriki zaidi ya mtu mmoja wote utawafyeka?"

    "Kila aliyehusika hatabaki hai hata awe nani kwa dawa nitakayoifanya utaniambia, hata uwe ukoo mzima utapukutika ila kwa aliyehusika tu."

    "Majibu lini?"

    "Narudi leo Malawi, leo usiku silali nitakesha na kazi hiyo, asubuhi nalituma kombora, mpaka jioni mtasikia majibu ya kazi mliyonituma, kwa vile sehemu yenyewe mbali unaweza kwenda kusikilizia kumetokea nini."

    "Tutashukuru maana wametuchukulia jicho letu, kama ikiwezekana fagia ukoo mzima."

    "Ninyi si mmenipa kazi, basi kaeni kimya muuone moto wangu, mimi ndiye Msioka," mganga alijitapa.

    Baada ya makubaliano, mganga Msioka aliondoka kurudi Malawi ili kurudisha kombora kwa mtu aliyeshiriki kumuua Bupe.

    KIJIJINI IBUNGU

    Siku iliyofuta taarifa zilifika kijijini Ibungu juu ya msiba wa mchumba wa Ambakisye aliyetolewa na mganga toka Malawi akiwa amefariki na mazishi kufanyika haraka siku iliyofuata kutokana na kuogopa mwili kuharibika.

    Taarifa ile ilikuwa kama shubiri kwa mzee Amangise baada ya kusikia mazingira ya kifo cha mkwewe mtarajiwa, aliamini kabisa waliofanya hivyo ni familia ya mpenzi wa mwanaye.

    Lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kuzipokea habari zile na kuziacha kama zilivyo kutokana na maneno mazito aliyoyatoa mwanaye juu ya familia ya mpenzi wake kama kingewatokea chochote basi yeye angechukua uamuzi mzito juu ya familia yake.

    Taarifa za kuonekana kwa Bupe akiwa amekufa zilimfikia Ambakisye ambaye alifurahia moyoni kwa kujua ndoa na Atuganile ipo karibu hasa baada ya familia yake kuonesha kubadilika na uamuzi wao mzito juu ya wazazi wenzao.

    Alitoka na furaha hadi kwa mpenzi, Atuganile alipomuona alijawa na shauku ya kutaka kujua jana yake mpenzi wake kazungumza nini na wazazi wake.

    "Karibu mpenzi wangu, yaani uso wako unaonesha kuna dalili njema."

    "Ni kweli, hebu nipe kwanza kwenu ilikuwaje ili nami nikujuze yaliyojiri."

    Atuganile alimweleza mpenzi wake jinsi alivyowachachafya wazazi wake mpaka wakabadili uamuzi na kufuata anachokitaka yeye.

    Ambakisye naye alimueleza mtiti aliouanzisha kwao baada ya mpenzi wake kumsikiliza alimuuliza.

    "Sasa Amba kama baba yako angeendelea kusimamia msimamo wake ungeondoka kweli?"

    "Nilikuwa sitanii ningejua mbele ya safari lakini si kukaa nyumba ya wauaji wale."

    "Sasa tutafanyaje ili familia zikae pamoja na kumaliza tatizo?"

    "Si bibi Tumwambilile alisema atakaa nao kwa vile kazi kubwa tumemaliza itakuwa rahisi kulizungumza."

    "Na kweli, unaonaje twende tukamwambie sasa hivi?"

    "Poa, tena nina habari njema mpenzi wangu."

    "Habari gani tena mpenzi?" Atuganile alishtuka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Bupe kapatikana..."

    "Sasa hizo ndizo habari njema, yaani kumbe unanidanganya unanipenda kumbe mawazo yako yapo kwa Bupe?" Atuganile alimkata kauli mpenzi wake na kuliza wivu.

    "Atu, mbona unanikata kauli kabla sijamaliza sentesi yangu."

    "Kuna nini zaidi ya kunirusha roho, jana nimewakosea adabu wazazi wangu kwa ajili yako, kumbe kuna mtu unayempenda."

    "Atu, tutakorofishana naomba uniache nimalize ninachotaka kukueleza."

    "Haya sema."

    "Bupe kapatikana juzi mtoni akiwa amekufa na kazikwa jana."

    "Muongo unataka kuniongopee."

    "Atu mpenzi wangu kipi utakachoniamini, kweli taarifa imefika nyumbani nasikia ametolewa ndani ya maji akiwa amenyolewa upande mmoja. Tena nasikia baba yake kasafiri mpaka Malawi kumfuata mganga kwani wa pale Kilasilo walichemka."

    "Mmh! Unajua siamini."

    "Ndiyo maana nikakuambia habari njema, sasa hivi ndoa nyeupe baada ya kuwatolea uvivu wazazi wetu."

    Atuganile alifurahi kwa kurukaruka na kumkumbatia mpenzi wake baada ya kujua aliyekuwa akimpa presha amekufa.

    "Sasa hivi nina uhakika wa kuitwa Mrs Amba," Atuganile alijishebedua.

    "Basi tuwahi kwa bibi Tumwambilile."

    Walikubaliana kwenda kwa bibi Tumwambilile kumwambia walipofikia na wazazi wao. Walikwenda taratibu huku wakizungumza:

    "Mmh! Bado siamini kama utanioa."

    "Kipi kitakachofanya nisikuoe ikiwa yule msichana amekufa."

    Wakiwa wameacha barabara kuu na kuingia yenye majani ili kupita njia ya mkato, ghafla mbele yao alitokea nyoka mweusi walishtuka na kutaka kumkwepa kwa kuruka nyuma lakini nyoka yule aliruka na kutaka kumuuma Atuganile. Kwa vile alikuwa amemuelekea alijitahidi kumkwepa na kurudi nyuma lakini kwa bahati mbaya alijikwaa na kuanguka chini.

    Nyoka yule alimgonga mguuni, alikuwa tofauti na nyoka wengine baada ya kumgonga Atuganile wakati akipiga kelele za kuomba msaada kwa maajabu yule nyoka, aliingia mdomoni na kuishia wote ndani ya mwili. Muda uleule Atuganile alibadilika rangi na kuwa mweusi, Ambakisye alichanganyikiwa na kushindwa kumsaidia mpenzi wake.





    Alitoka mbio hadi kwa bibi Tumwambilile kuomba msaada, alipofika alikuta nyumba ipo kimya ila mlango ukiwa wazi, alimwita kwa sauti lakini hakukuwa na jibu lolote.

    Aliingia ndani na kushtushwa na mkoromo mzito, aliposogea alishtuka kuona aliyelala pale chini kumbe ni bibi Tumwambilile bila nguo yoyote huku ndani kukiwa na harufu kali ya kinyesi, hali ile ilimtisha sana.

    Alimsogelea akitetemeka huku ameziba pua kutokana na harufu kali, alijaribu kumwita hakukuwa na jibu lolote zaidi ya kuzidi kukoroma, baada ya muda alimsikia akivuta mkoromo mrefu na kutulia. Hali ile ilizidi kumchanganya Ambakisye aliyetoka mbio kurudi kwa mpenzi wake.

    Alipofika alishangaa kukuta akiwa bado yupo palepale amelala chini mdomo ukiwa wazi, alipomsogelea karibu huku akitetemeka alishtuka kuona kitu mdomoni kwa mpenzi wake. Alipoangalia vizuri alikiona kichwa cha nyoka kikichungulia kuonesha yule nyoka alitaka kutoka.

    Ghafla yule nyoka alitoka mdomoni kwa Atuganile na kutoweka bila kujua amekwenda wapi. Akiwa bado anatetemeka alimsogelea mpenzi wake aliyekuwa bado amelala chini ametulia kama amekufa kwa vile alikuwa hajigeuzi.

    Kwenye jeraha la kuumwa na nyoka palianza kutoa funza kama kidonda cha muda mrefu, Ambakisye alizidi kuchanganyikiwa na kuanza kulia kwa sauti iliyofanya wapita njia kumfuata na kutaka kujua alitokewa na nini. Walipofika walishtuka kumuona Atuganile akiwa amelala huku mwili wake ukiwa mweusi kama kapakwa mkaa.

    "Kafanya nini?"

    "Tulikuwa tunapita ghafla katokea nyoka wa ajabu na kumgonga kisha kutoweka katika mazingira ya kutatanisha."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mmh! Watu wamesha anza, jamani watu wa kijiji hiki hawamuogopi Mungu kila kukicha kurogana?" alisema mama mmoja kwa uchungu.

    "Mmh! Tumuwahishe kwao, hali ya Atu inatisha," mwingine alitoa wazo.

    Walimbeba na kumpeleka kwao akiwa amepoteza fahamu, wazazi wake walishtuka kuwaona watu wamembeba Atuganile juujuu.

    "Vipi jamani kulikoni?" mama Atuganile aliuliza kwa hofu.

    "Amegongwa na nyoka."

    "Nyoka?"

    "Ndiyo tena nyoka mwenyewe wa mauzauza baada ya kumgonga amepotea."

    Wazazi wa Atuganile walichanganyikiwa, walipomuangalia mtoto wao alikuwa na kila dalili za mfu, hakuwa na dalili za kupumua huku kidonda chake kikitoa harufu kali ya kuoza na wadudu kuendelea kutoka. Kilichowashangaza, mwili ule ulianza kuvimba na kuwa kama papai lililoiva.

    "Amba, mwanangu umemfanyaje?" mama Atu alimuuliza Ambakisye huku akilia.

    "Tulikuwa tunakwenda kwa bibi Tumwambilile akatokea nyoka ambaye alimgonga na baadaye kuingia mdomoni."

    "Mungu wangu! Yaani nyoka kaingia mdomoni kwa mwanangu?" mama Atuganile alisema kwa sauti ya kilio.

    "Lakini alitoka ."

    "Mungu wangu! baba yako amemuua mwanangu," walipeleka tuhuma moja kwa moja katika familia ya mzee Amanyisye.

    "Mume wangu wahi kwa bibi hali ni mbaya."

    Ambakisye alishindwa kuwaeleza alichokikuta kwa bibi kwa kuogopa kuongezewa tuhuma kwa kuonekana tatizo alilomkuta nalo bibi Tumwambilile familia yao inahusika. Alikaa kimya ili kusubiri jibu atakalorudi nalo baba Atuganile.

    Mzee Andendekisye alikimbilia kwa bibi Tumwambile kumweleza tatizo lililomtokea mwanaye. Alipofika mlangoni alishtuka kukutana na nyoka mkubwa, alisita kuingia mara yule nyoka alitoka na kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

    Kwa vile alikuwa akijua michezo ya bibi hakushtuka sana na kuingia ndani huku akiita. Nyumba ilikuwa kimya kama hakuna mtu, aliingia ndani huku akiita jina la bibi,akakutana na harufu kali ya kinyesi. Alitoka nje kutokana na harufu ile kuwa kali, alizuguka nyuma ya nyumba labda atamkuta lakini hakukuwa na jibu.

    Alitaka kuondoka kurudi nyumbani lakini moyo ulisita, aliamua kuingia ndani ili ajue kama amelala ili amuamshe kwa vile asingerudi bila kumuona. Pamoja na harufu kali aliingia ndani alipokaribia mlango wa chumbani alimuona mtu amelala chini akiwa hana nguo mwilini. Alishtuka sana na kumsogelea huku harufu ya kinyesi ikiwa kali. Alimwita kwa sauti ya chini labda ataamka pale chini alikuwa amejitapakaza kinyesi.

    Alijipa moyo na kumgeuza ili amuondoe kwenye kinyesi kile na kumfanyia usafi, kwa vile alikuwa amelala kifudifudi alimgeuza na kushtuka kumuona hana jicho moja, sehemu ya jicho ilikuwa ikivuja damu na kuonesha bibi Tumwambilile alikuwa amekufa kifo kibaya sana.

    Alitoka mbio kwa hofu na kujikuta akijikwaa na kuanguka kwenye vumbi na mwili wote kujaa vumbi kama alikuwa akiogelea kwenye vumbi. Alirudi nyumbani mbio kama mtu anayefukuzwa na simba, mke wake na watu waliokuwepo walishtuka na kumuuliza:

    "Vipi mbona hivyo?"

    "Wametumaliza."

    "Una maanisha nini?"

    "Tegemeo letu wamelimaliza."

    "Una maanisha nini hebu kuwa muwazi."

    "Bi...bi...bi...a...a...me...ku.."

    "Amefanya nini?"

    "Amekufa kwa...kwa...kutolewa roho kikatili."

    "Mungu wangu nisaidie mimi! Jamani kijijini kwetu kumeingia nini?" jirani mmoja alisema kwa uchungu huku mikono ikiwa kichwani.

    "Yaani kama mwanangu akifa aliyekula mbuzi wangu atanilipia ng'ombe kumi," mzee Andendesye alisema kwa uchungu.

    "Sasa mume wangu tutafanyaje?"

    "Labda tumfuate Kigugu nasikia na yeye ni mtaalamu wa mambo haya."

    "Nina wasiwasi na mwanangu maana sioni dalili zozote za kuwepo mtu hapa," mama alisema kwa kukata tamaa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Usiseme hivyo jirani.”

    Mzee Andendekisye alikwenda kwa mganga Kigugu kumchukua ili aje amtibu mwanaye.

    Japo sehemu alipo mganga ilitakiwa baiskeli lakini aliona anachelewa na kuamua kwenda kwa miguu huku akikimbia. Mazingira yale yalimchanganya Ambakisye na kuona heri aondoke na kwenda kuwaeleza familia yake kuwa wamefanikiwa kwa walichokifanya juu ya mpenzi wake.

    Alikwenda nyumbani kwao na hasira kwa baba yake na kuapa kufanya kitu ambacho kitakuwa historia kijijini alikuwa tayari kunyongwa kama mpenzi wake atakufa. Alipofika nyumbani kwao hakukuwa na mtu aliamua kuwafuata shamba ili wamueleze jana walizunguza nini na leo yake wamefanya nini. Aliamini kabisa kuwa baba yake ndiye alifanya vile baada ya kifo cha Bupe na kuanza kummaliza bibi Tumwambilile kwa vile ndiyo kimbilio lao.

    Alitembea njia nzima huku akilia kwa uchungu na kuichukia familia yake na kujuta kuzaliwa kwenye familia ya viumbe wakatili kama wake.

    Mzee Andendeksye pamoja na umri wake mkubwa hakutulia mpaka alipofika nyumbani kwa mganga huku akitweta. Kutokana na kukimbilia umbali mrefu bila kupumzika, aliposimama alianza kusikia vichomi vikali na kizunguzungu. Wasaidizi wa mganga walipojua amechoka kwa vile alikuwa akitweta sana na jasho kumtoka kama maji, walimuacha apumzike kwa muda ili wamuulize.

    Kutokana kupatwa na kizunguzungu kikali alianguka chini na kipoteza fahamu, waliingia kazini kumpa huduma ya kurudisha hali yake ya kawaida. Baada ya kupata huduma alipumzika dakika kumi ndipo alipoweza kuzungumza na kuomba kukutana na mganga Kagugu.

    Aliingizwa katika chumba cha mganga na kukaa kwenye mkeka.

    “Ndiyo mzee wangu unaonekana una jambo zito,” mganga alianza kwa kuuliza.

    “Ni kweli hali ya mwanangu ni mbaya sana.”

    “Amefanya nini?”

    “Ameumwa na nyoka wa mazingara.”

    Baada ya kusema vile, mganga alisimama na kutoka nje na kwenda kuangalia jua kwa muda na kurudi ndani.

    “Ni kweli kapigwa.”

    “Na nani?”

    “Hiki ni kisasi.”

    “Cha nani?”

    “Uchawi umetoka mbali ulivyotumwa ndivyo ulivyorudi.”

    “Unamaanisha nini?”

    “Aliyepigwa karudisha.”

    “Nimeishamjua,” Mzee Andendekisye alijua ni baba Ambakisye ndiye aliyefanya vile baada ya kumpiga mwanaye.

    “Sasa mganga utanisaidia nini?”

    Mganga alinyanyuka na kutoka tena nje na kuangalia jua kwa muda mrefu kuliko mwanzo na kurudi tena ndani.

    Baada ya kukaa kwenye kiti chake alitulia kwa muda na kusema:

    “Hamna kitu,” alisema huku akitikisa kichwa kuonesha anakataa.

    “Hamna kitu kivipi wakati unasema amepigwa?” mzee Andendekisye alimshangaa mganga.

    “Kwa sasa sina msaada wowote kwa vile waliopiga wamemaliza kazi.”

    “Unamaanisha nini?”

    “Mtoto wako hana uhai.”

    “Nimekusikia lakini sijakuelewa.”

    “Nimeangalia jua na kukutana na kiza cha kutisha, ukiona jua kali lakini limetandwa na kiza kizito inaonesha hakuna kitu.”

    “Mganga mbona unanizungusha hivyo, hicho kiza umekiona peke yako?”

    “Ndiyo maana umekuja hapa ungekuwa na uwezo wa kuona wala usingesumbuka kuja hapa.”

    “Basi naomba unifahamishe hakuna kitu gani?”

    “Mwanao amefariki.”

    “Etiii?” mzee Andendekisye alisema macho yamemtoka pima.

    “Ukweli ndiyo huo yule nyoka aliyetumwa ndiye aliyemmaliza, inaonesha amekufa kipindi, hesabu zinaonesha saa moja iliyopita.”

    “A..a..sante,” alisema huku akinyanyuka na kutoka nje bila kuaga na kurudi nyumbani akilia kama mtoto mdogo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipofika nyumbani mkewe alikuwa bado ameupakata mwili wa mwanaye, alipoingia eneo la nyumbani kwake aliangua kilio na kumfanya mke wake ampokee kwa kilio.

    “Mume wangu unalia nini?” alimuuliza kwa sauti ya kilio.

    “Amangise kaniulia mwanangu...Amangise kaniulia mwanangu.”

    “U..u...na..maanishaaa Atu amefariki?”

    “Ndiyo mke wangu, Amangise kaniweza kuchukua jicho langu.”

    Taarifa ile iliwashtua watu wengi na kufanya vilio vitawale kwa majirani hasa mashoga wa Atuganile. Walimchukua na kumpeleka kwenye hospitali ya wilaya ambako vipimo vilithibitisha Atuganile amefariki dunia.

    Mwili alihifadhiwa kwenye chumba cha maiti na kuanza matayarisho ya msiba na taarifa zile kusambaa kila kona ya mji wa Ibungu.

    Wakati huo Ambakisye bila kujua nini kinaendelea nyuma alikwenda hadi shamba walipokuwa wakilima wazazi wake. Alipofika aliangua kilio kitu kilichowashtua wazazi wake na kuhoji kulikoni hali ile kutokea.

    “We Amba kuna nini?”

    “Jamani wazazi wangu mmenifanyia ukatili gani?”

    “Ukatili! Wa nini tena?” walishtuka wote.

    “Jana tumezungumza nini na leo mmenifanyia nini?”

    “Amba mbona hatukuelewi una maanisha nini?” wote waliacha kulima na kumsogelea mtoto wao aliyekuwa akilia.

    “Baba umemfanya nini Atuganile?” alimuuliza baba yake.

    “Mimiiii!” baba mtu alishtuka.

    “Wazazi wangu kwa nini mmenigeuka, kwani umenitendea unyama huu?”

    “Unyama upi huo mwanangu?”

    “Mpaka mmetimiza azma yenu ya kumuumiza mpenzi wangu.”

    “Kwani amefanya nini?”

    “Mnajua mnajua wazazi wangu... niliwaeleza jana kuwa kama vita yenu kwa nini msipigane wenyewe kuliko kutugeuza ngao katika mapigano yenu.”

    “Hebu tufafanulie Atuganile amefanya nini?” mama yake alimuuliza.



    Atuganile ameumwa na nyoka kisha kamuingia tumboni."

    "Mungu wangu! Unasema kweli?" mama yake alishtuka.

    "Mama unaweza kuwa hujui lakini baba anajua kila kitu," Ambakisye alimshutumu baba yake.

    "Ambakisye nakuapia kwa jina la Mungu kuwa sihusiki na kitu chochote kuhusu mpenzi wako, tuliongea jana yalitosha kukuelewa na kuwa radhi umuoe Atuganile."

    "Hapana, baba aliapa kutenda na ametenda," Ambakisye aliendelea kumshutumu baba yake.

    "Najua huwezi kuamini lakini nakuapia kuwa sijatenda, nenda popote hutakuta ukweli mimi baba yako nimeshiriki."

    "Mmh! Sasa yupo kwenye hali gani?" mama yake aliyekuwa bado kapigwa na bumbuwazi aliuliza.

    "Mama nikiambiwa Atu amekufa siwezi kushangaa."

    "Baba Amba hebu kuwa muwazi ni kweli Atu umemtenda?"

    "Siwezi kumtenda mke wangu, kama nilivyo usafi moyo jana, japokuwa nilikuwa na hasira, lakini niliuapia moyo wangu kutoshiriki kwenye jambo lolote la kumchukiza Mungu na hivi nilikuwa mbioni kuokoka.

    Kusema nilishiriki kweli moyo unaniuma sana, Mungu ndiye anayejua nani katenda pia namuomba kwa kila aliyetenda amhukumu na hukumu yake asichukue muda mrefu kabla jua halijazama basi awe ametoweka katika sura ya dunia," mzee Amangakisye alisema kwa uchungu mkubwa.

    "Sasa nani katenda unyama ule?" Ambakisye aliuliza.

    "Mwanangu dunia hii kuna maadui wengi tunaweza kufikiri sisi ndiyo tulikuwa tunagombana tu kumbe kuna adui wa pembeni aliyeingiza mkono wake."

    "Hivi nimekimbia kwao baada ya mzee Andendekisye na mkewe kukushutumu kuwa umemuua mtoto wao."

    "Wamethibitishaje?"

    "Mimi nitajuaje, waliniambia kuwa wewe umemuua na kuapa kama umekula mbuzi wao lazima utalipa ng'ombe. Huoni hapo ile kauli ya kubakia magofu itatimia ninaamini lazima wataanza na mimi," Ambakisye alijitetea baada ya kuona akitoka mpenzi wake atakayefuata ni yeye.

    "Najua lazima watajua ni sisi kwa vile nao walikuwa wanataka kushindana na sisi."

    "Sasa mume wangu tuwahi kumsaidia mtoto kwani bila hivyo kuna baya linaweza kumpata."

    "Hilo ndilo linalonila akili, inatakiwa kesho nisafiri naye kwa ajili ya kumkinga."

    "Fanya hivyo mume wangu."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zoezi la kulima halikuendelea tena na waliamua kurudi nyumbani, wakiwa njiani walikutana na taarifa ya kifo cha Atuganile. Habari zile zilimshtua sana Ambakisye ambaye alianguka chini na kupoteza fahamu. Wazazi wake waliingia kazi ya kumsaidia kumpa huduma ya kwanza hata alipoamka hakuwa na uwezo wa kutembea, alisaidiwa na baba yake kupelekwa nyumbani.

    Ambakisye alikuwa na maumivu makali moyoni kwa kumpoteza kipenzi chake, mwanamke wa ndoto yake. Alitembea njia nzima akilia kwa sauti huku wazazi wake wakimbembeleza mpaka walipofika nyumbani. Taarifa zilizagaa kijijini kuwa mzee Amangise ndiye aliyemloga Atuganile ili asiolewe na mwanaye.

    Mzee Amangise aliamini hakuna atakayeamini kuwa yeye hausiki na kifo cha Atuganile, kutokana na taarifa ile kusambaa, alijua lazima kuna bomu zito litatua nyumbani kwake hasa kwa kuanza kwa mwanaye, Ambakisye.

    Alipanga kesho yake alfajiri aondoke ili kuvuka boda kwenda Malawi kwa ajili ya kujilinda ikiwezekana wawahi kabla hawajawahiwa. Safari yao walipanga kuondoka kabla hakujakucha ili mpaka saa nne wawe wamevuka boda na kufika kwa mtaalamu.

    Wakati wao wakiwaza hivyo mzee Andendekisye alipanga kutozika haraka mpaka asafiri kwenda kupata ukweli kama kweli mwanaye amekufa basi alipue bomu hukohuko ili akirudi kumzika mwanaye na jirani yake naye anamzika wa kwake.

    Yeye alipanga kuondoka usiku uleule akatafute kitu cha kumtia adabu mzee Amangise baada ya kuamini ndiye mhusika mkuu.

    ***

    Kijijini Kilasilo siku ya pili mzee Ambokile alimtuma kijana mmoja kwenda kijiji cha Ibungu kusikia kuna taarifa gani. Kijana aliyetumwa alipanda baiskeli mpaka kijiji cha Ibungu na kukuta taarifa za msiba wa watu wawili mmoja msichana na bibi wa kijiji ambao wote walikufa katika mazingira ya kutatanisha.

    Baada ya kuzipata taarifa zile alirudi Kilasilo kurudisha taarifa ya Ibungu, habari zile zilimfurahisha sana mzee Ambokile na mkewe kwa kuamini aliyemuua mwanaye naye kamfuata, watakutana kwa Mungu na kumueleza kwa nini walimuua bila kosa.

    Wakati mzee Ambokile akifurahia kulipa kisasi, mzee Amangise alikuwa anajiandaa na safari ya kwenda Malawi kumuwahi adui yake.

    Usiku wa siku ile jirani yake aliondoka kuvuka boda kwenda kutafuta tatizo la mwanaye ili awahi kurudi siku ya pili yake jioni ili siku ya tatu kama amekufa kweli wafanye mazishi.

    ***

    Mzee Andendekisye alivuka boda saa sita usiku na kupanda land rover old model mpaka mji wa Matipa jirani na msitu mkubwa wa Matipa. Alifika saa nane za usiku. Usiku uleule alikutana na mtaalamu wake Maemba. Baada ya kumweleza tatizo lililomkuta na kutaka kupata ukweli.

    "Kwanza pole, najua umesafiri umbali mrefu kutaka kujua binti yako ana matatizo gani?"

    "Ni kweli."

    "Ukweli ulioelezwa kwenu ndiyo huohuo."

    "Upi?"

    "Juu ya mwanao."

    "Ni kweli amekufa au kiini macho?"

    "Ni kweli amekufa."

    "Sasa nataka kwanza huyu kijana aitwaye Ambakisye Amangise jua la leo jioni asilione."

    "Hakuna tatizo."

    "Baada ya kumkata kijana huyo kisha familia yake aondoke mmojammoja."

    "Kazi hiyo ndogo."

    Baada ya kukubaliana mganga alisema kazi ile inafanyika usiku uleule na yeye alitakiwa kurudi kuendelea na mazishi lakini kesho yake mpaka jua linazama ataipata taarifa ya kifo cha mtu.

    Mganga aliingia kazini kuandaa kombora litakalo msambaratisha Ambakisye ambaye alfajiri ya siku ile angekuwa akivuka boda naye kwenda kufanya mambo yake.

    Baada ya mganga kukamilisha kazi yake iliyochukua saa tatu, mpaka anamalizia kulikuwa kumekucha.

    Waliagana na mzee Andendekisye aliyetakiwa kurudi kule baada ya mazishi kwani aliamini adui yake naye lazima atahangaika japokuwa Maemba aliamini kwa kinga ndogo aliyompa itamuwezesha kurudi salama baada ya mazishi ya binti yake.

    Mzee Andendekisye aliondoka Matipa alfajiri na kufika mpakani saa moja asubuhi alivuka na kwenda kuchukua baiskeli yake alipoiacha na kurudi kijijini kwake kuendelea na maandalizi ya mazishi ya mwanaye kipenzi. Wakati akirudi jirani yake Amangise alikuwa safarini kuelekea kwa jamaa yake ambaye alisoma na kuingia kwenye utaalamu wa miti shamba Ligula.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walitoka vizuri na mwanaye kwa kupakiana kwenye baiskeli na kuelekea boda ili wavuke kwenda Karonga ili wakamzime mzee Andendekisye kabla hajawazima. Kama kawaida Ambakisye ndiye alikuwa akimuendesha baba yake.



    Baada ya mwendo wa saa mbili Ambakisye alisimamisha baiskeli na kufanya baba yake kumuuliza.

    “Vipi umechoka nikusaidie.”

    “Hapana baba kichwa kimenishika ghafla.”

    “Mmh! Mbona unanitisha,”

    Mara Ambakisye alishika kichwa na kuanza kupiga kelele za maumivu.

    “Baba kichwa, nakufa mimi kichwa kinapasuka kinapasuka….Mungu wangu nakufa..baba nakufa kichwa kinapasuka,” Ambakisye alisema huku ameshikilia kichwa kama kinataka kutoka.

    “Ni nini mwanangu?” baba yake alishtuka.“Baba nina wasiwasi na familia ya kina Atuganile wamelipa kisasi, kama ni wao naamini siponi,” Ambakisye alisema kwa shida.

    “Hapana utapona tu mwanangu, mbona mimi sijafanya lolote kwa kifo cha mpenzi wako kisasi hicho kitokane na nini? Wacha niendeshe mimi nikuwahishe kwa mganga,”

    “Baba…niagie kwa mama nakufa bila kumuaga,” Ambakisye alisema kwa sauti ya kukata tamaa.

    “Huwezi kufa mwanangu,” mzee Amangise alisema huku akimshika mwanaye aliyetaka kuanguka na kumdaka na na kumkalisha kwenye miguu yake.

    “Ba..ba..ba..” Ambakisye alimwita baba yake kwa shida kwa sauti ya chini.

    “Na..na..am mwanangu,” baba yake aliitikia huku hofu kubwa ikiwa imemtawala.

    “U..u..naona ubishi wako?”

    “Mbona mwanangu nilikubaliana na wewe.”

    “Alichelewa tayari cheche imeisha unguza msitu na moto hakuna wa kuuzima.”

    “La..la..kini..”

    “ Ba..ba, suluhu ya hili ka..ka..ma ..Mu..mungu watanichukua usilipe kisasi, ukilipa patabakia ma..ma..ma..go..fu..”

    Ambakisye hakumalizia, ghafla alibadilika na damu zilianza kumtoa mdomoni, puani, masikioni na machoni huku macho yakiongezeka ukubwa. Taratibu alifumba macho na kutulia.

    “Amba..Ambakisye…Ambaaaa,” alimtikisa kwa nguvu lakini hakukuwa na jibu lolote. Alimshika mapigo ya moyo yalikuwa yametulia, mzee mzima aliangua kilio kumlilia mwanaye ambaye alijua amechelewa kumpeleka kwenye kinga .

    Wapita njia walishtuka kumkuta mtu wanayemfahamu kampakatia mtu huku akilia.

    “Vipi mzee Amangise?”

    “Jamani mwanangu,” alijibu kwa sauti ya kilio.

    “Ha! Ni Ambakisye! Amefanya nini?” walishtuka kumuona ni mtu wanayemjua katika hali ile.

    “Jamani mwanangu ameniacha ghafla.”

    “Mungu wangu, alikuwa akiumwa?”

    “Wala, tulikuwa na safari ya kuelekea Kilasilo lakini ghafla kichwa kimemuuma hata dakika kumi hazikuchukua amefariki dunia.”

    Mzee Amangise aliangua kilio kama mzazi wa kike akimlilia mwanaye, walimsaidia kuurudisha mwili wa Ambakisye kijijini. Watu wote njiani walishtuka kuwaona walivyobebwa Ambakisye kwenye baiskeli huku baba yake akilia kilio cha chini chini.

    “Jamani kuna nini?”

    “Nimemkuta mzee Amangise akilia huku amemkumbatia mwanaye kwa kweli mpaka sasa hatujajua nini kimemsibu.”

    “Eti mzee wangu kuna nini?”

    “Wa..wa…,” alishindwa kuzungumza kwani doge la uchungu lilimkaba kooni.

    Walimsaidia kuufikisha mwili wa Ambakisye ambaye hakuwa na uhai wakati huo, ujaji ule ulimshtua mama Ambakisye aliyekuwa akifanya usafi uani. Alitulia akiwa amepigwa na butwaa na kujikuta vitu alivyoshikilia mkononi vikimdondoka na kuanguka chini.

    Aliyekuwa ameshikiliwa kwenye baiskeli alikuwa mwanaye Ambakisye, walipofika waliuteremsha mwili wa mwanaye na kuingiza ndani.

    “Kafanya nini?” mama Ambakisye aliuliza huku akisogea alipokuwa mumewe ameinama huku akilia kilio cha sauti ya chini.

    “Vipi mume wangu Amba kafanya nini?” alimuuliza kwa sauti ya juu.

    “Wametuwahi.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wametuwahi nini mume wangu?”

    “Inaonekana walitangulia kabla hatajafika.”

    “Una maanisha Amba anaumwa?”

    “Ha..ha..p..”

    “Hapana nini mume wangu, kwani kafanya nini?” mama Ambakisye alimuuliza mumewe akiwa amemkwida shati na kumtikisa kwa nguvu.

    “A..a..me..ku..ku..u.”

    Kauli ile ilimfanya mama Ambakisye amuachie mumewe taratibu na kuteremka chini na kujitupa kama mzigo akiwa amepoteza fahamu baada ya kupata mshtuko kutokana na taarifa ile. Wakati huo wajirani walikuwa wamefika kutokana na kelele za mama Ambakisye kabla ya kupoteza fahamu.

    “Jamani kuna nini?”

    “Ambakisye amefariki ghafla,” alijibu mmoja wa watu walioleta mwili wa Ambakisye.

    “Wewee!” msichana mmoja alishtuka na kuweka mikono kichwani.

    “Kweli Ambakisye hatunaye.”

    “Mungu wangu mambo gani haya, mpenzi wake si amefariki juzi tu,” mwanamke mmoja alisema huku ameshika mdomo.

    Kina mama walimpa huduma ya kwanza mwanamke mwenzao huku wazee wa eneo lile wakimchukua mzee Amangise na kukaa naye pembeni kutaka kujua tatizo, pia wafanye nini baada ya kutokea kitu kama kile kwa ghafla.

    “Vipi mzee mwenzetu kulikoni?”

    Aliwaelezea hali iliyomtokea Ambakisye ghafla, aliongeza uongo walikuwa wakienda kuhani kwa mchumba wa mwanaye aliyefariki katika mazingira ya kutatanisha.

    “Sasa hii itakuwa nini, juzi mtoto wa Andendekisye, Atuganile na bibi Tumwambilile wamefariki katika mazingira hayahaya







    Wapo waliosema hizo ndizo dalili za maisha anayokwenda kuishi kwa vile ubaya ndiyo uliomzunguka kuliko mema katika maisha yake. Kwa hiyo picha ya maisha ya kuzimu ilijionesha mapema. Wakiwa wanasubiri vijana wamalizie kuchimba, ghafla walisika sauti ya kushtusha.

    “Jamani chini tunapochimba kunatoka maji.”

    “Maji?” Watu walishtuka, “ Tena yanatoka kwa wingi kama kumepasua bomba.”

    SASA ENDELEA...



    “Makubwa, tokea lini maeneo haya yakawa na chemchem, mbona leo mauzauza kwenye kaburi la bibi?”

    “Sasa tutafanyaje tumzike hivyohivyo au tuchimbe lingine?”

    “Tukichimba lingine yanaweza kutokea hayahaya.”

    “Hapana tuchimbe kaburi lingine hatuwezi kumzika binadamu mwenzetu kwenye maji, bado thamani yake ni kubwa kwetu. Huyu alikuwa bibi wa kijiji nani ambaye alikwenda kwake hakupata msaada japo kuna maneno ya kijinga juu yake. Lakini lazima tumpe heshima yake,” alisema mzee Mwangibile aliyekuwa mzee wa kijiji.

    Vijana kwa shingo upande waliingia tena kwenye kazi ya kuchimba kaburi la tatu, muda nao ulikuwa unakatika, kigiza nacho kilianza kuingia. Lakini watu waliendelea kuwepo makaburini mpaka wamzike bibi. Shughuli ya kuchimba iliendelea kwa dakika ishirini kaburi lilikuwa tayari.

    Ajabu lilikuwa katika hali ya kawaida tofauti na yaliyotangulia na kumfanya mzee Mwangibile kuuliza.

    “Sasa kipo wapi mbona kaburi limeisha vizuri?”

    “Mzee usiseme hivyo, subiri tuzike kwanza.”

    “Hakuna kitu kitakacho tokea.”

    Baada kumaliza kuchimba waliochaguliwa mwanzo waliingia tena kaburini ili kupokea mwili wa bibi Tumwambilile. Wakati wakijiandaa kuupokea mara walishtuka kusikia vitu vikiwatembea miguuni, walipoangalia waliona lundo la siafu ambao walianza kuwapandia miguuni na kufanya watoke huku wakijikung’uta.

    Baada ya kutoka ndani ya kaburi waliangalia tena na kukuta siafu wamejazana na kuzidi kuwashtua watu na kujiuliza hali ile inatokana na nini.

    Mmoja alitoa wazo waitwe wataalamu wa asili waangalie tatizo ni nini.

    Bahati mganga Kagugu alikuwa amefika muda mfupi, alisogea kwenye makaburi yote na kuyatizama kwa muda na kuchukua mchanga uliochimbwa na kuutupia ndani ya kaburi kisha alisema:

    “Zikeni kaburi lolote hakuna kitu.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwa nini unasema hakuna kitu wakati kila kaburi lina mauzauza yake?”

    “Nimesema zikeni hakuna kitu chochote, yote yale ni kiini macho tu hakuna nyoka, maji wala siafu.”

    Walibeba mwili wa bibi Tumwambilile na kuuzika bila tatizo lolote na kurudi nyumbani wakati giza lilikuwa limeshaingia.

    Njiani kila mtu alisema yake huku wengine wakijiuliza kama ni kiini macho kimeonekana kwa ajili gani. Tukio lile lilikuwa gumzo kijijini pale na kushangaza wiki ile kuwa ya mauzauza huku wengine wakijiuliza nini kitatokea kwenye mazishi ya Atuganile na kisha Ambakisye.

    Siku ya pili kulikuwa na mazishi ya Atuganile, kama kawaida wanakijiji walikusanyika nyumbani kwa Andendekisye kwa ajili ya mazishi. Wakati watu wakiwa msibani mzee Andendekisye alisema kwa sauti kuwa hataki kumuona Amangise kwenye msiba wa mwanaye na akimuona atamkata mapanga.

    Hakuna aliyemsemesha kitu kwa vile waliogopa kuingia kwenye ugomvi usiowahusu.

    Muda ulipotimu ilifanyika ibada ya kumsalia maiti iliyoongozwa na Padri Thomas Mayunga iliyochukua zaidi ya saa nzima na zoezi la kuuaga mwili wa marehemu lilianza. Zoezi la kuaga lilipoisha, watu waliuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika makaburi ya Wakristo.

    Walipoufisha mwili makaburini ilifanyika ibada nyingine ya kulibariki kaburi na zoezi la kuteremsha jeneza kaburini lilianza kwa watu kuingiza jeneza kwa kamba. Jeneza baada ya kuteremshwa kaburini na kutolewa kamba, ilifanyika misa ya mwisho kabla ya kuzika.

    Padri alifungua kitabu cha sala kusoma ibada ya wafu kisha alichukua udongo na kuutupia kwenye jeneza na kusema:

    “Ulitoka mavumbini na mavumbini utarudi.”

    Kisha alichukua chetezo chenye uvumba na kupitisha kaburini alipomaliza alichukua maji ya baraka na kuanza kunyunyizia kwenye jeneza (sanduku) huku watu wakiwa wametulia kusikiliza ibada ile.

    “Ulibatizwa kwa maji...”

    Wakati akinyunyiza maji, ghafla walisikia mtikisiko ndani ya jeneza kama kuna kitu kilicho hai, hali iliyomfanya padri asite kuendelea na ibada na kusababisha watu kusogea kaburini wengine wakiamini Atuganile amefufuka.

    Hakuna aliyeweza kuingia kaburini, wote walibakia kimya wakiendelea kusikiliza vurugu zilizokuwa ndani ya jeneza ambazo zilikuwa kubwa.

    Wakati watu wakiwa katika wasiwasi, ghafla jeneza lilipasuka na kutokea bonge la mamba likiwa na pande la nyama mdomoni na kufanya watu wote wapige kelele za woga na kutimua mbio. Yule mamba hakushtuka alimalizia kukimeza kipande cha nyama kilichokuwa mdomoni na kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.

    Ndani ya jeneza kulikuwa kumejaa damu lakini mwili wa Atuganile haukuonekana, ilionekana kama yule mamba ndiye aliyemla.

    Lakini walijiuliza ameingia muda gani na kuweza kumtafuna kwa muda mfupi wakati wakiaga mwili wa marehemu hawakuona kitu chochote?

    Watu wote makaburini walipagawa na kuzidi kuona maajabu kwa wiki nzima toka vifo vyao mpaka mazishi yao. Baada ya muda hali ilitulia huku kila mmoja akiogopa kusogea kaburini kutokana ha hali iliyojitokeza. Wakati wa tukio la kupasuka jeneza, mganga Kagugu alipatwa na mshtuko wa ghafla na kuanguka chini na kupoteza fahamu.

    Alirudiwa na fahamu baada ya tukio kutulia alipoombwa kwenda kwenye kaburi akaangalie kumetokea nini, alikataa kwa kuhofia maisha yake. Ilionekana uchawi uliotumika pale ulikuwa mkubwa kuliko uwezo wa nguvu zake za kiganga.

    Mzee Andendekisye na mkewe walipagawa na kumshtumu moja kwa moja kwa sauti kuwa Amangise baba wa Ambakisye ndiye aliyefanya vile na kuapa kula naye sahani moja.

    Alijikuta akisema kwa sauti na kujisahau kuwa yupo mbele za watu.

    “Wewe si umefanya hivi basi moto utakuwakia, nimeanza na mtoto, sasa nafagia ukoo mzima.”



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog