Search This Blog

PENZI LA SHETANI - 2

 





    Simulizi : Penzi La Shetani

    Sehemu Ya Pili (2)





    "Mark, kwanza ningependa kujua, baada ya mama kufariki, je kuna mtu yoyote unayeishi nae nyumbani zaidi ya baba?" dokta alimuuliza Mark.

    "Hapana dokta, nimebaki mimi na baba tu na hakuna mtu yoyote tunayeishi nae pale nyumbani."

    "Je huyu uliongozana naye kuja hapa hospitali ni nani?" Aliuliza dokta huku macho yake yakimtazama Sala.

    "Huyu anaitwa Sala, ni rafiki yangu sana na pia sote tunasoma shule moja."

    "Vizuri Mark, lakini kwanini unajua nimekuuliza haya yote?"

    "Hapana dokta bado sijajua sababu." Mark alimjibu dokta.Dokta alishusha pumzi yake kwa nguvu, akamtazama Mark, alimuonea huruma sana Mark na akaona jinsi gani kijana yule alivyokuwa na majukumu mazito ambayo hayakustahili akumbane nayo katika umri wake.

    "Mark, haya unayoyaona mkononi mwangu, ni majibu kuhusiana na ugonjwa unaomsumbua baba yako, mzee Peter.Baada ya kumfanyia vipimo na kumchunguza mwili wake wote, tumegundua mzazi wako amepata ugonjwa wa kupooza na hatakuwa tena na uwezo wa kufanya chochote kile, ili apone ugonjwa huu, inahitajika si chini ya shilingi milioni sabini(70 millions) kwa ajili ya kumsafirisha kwenda nje ya nchi kwa matibabu." Dokta alimtaarifu Mark kuhusiana na ugonjwa wa baba yake.Taarifa ile ya dokta, ilimuhuzunisha na kumnyong'onesha sana Mark, akahisi na sasa anakwenda kumpoteza baba kama alivyompoteza mama yake kutokana na ukosefu wa fedha nyumbani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Dokta, hali yangu kama unavyoiona, maisha yetu yanaenda kwa kutegemea misaada mbalimbali tuipatayo, nitaweza vipi mimi kumuhudumia baba yangu katika hali hii na kuweza kupata fedha zote hizo angali mimi bado ni mwanafunzi?", Ee Mungu uwepo wako uko wapi, kila siku sisi tumekuwa watu wa shida tu, kwanini umekuwa mmbaguzi baba..!!!??" Kwa uchungu mkubwa huku machozi yakimdondoka, Mark alizungumza maneno haya na kumlaumu Mungu, kwanini kila siku yeye amekuwa mtu wa kukumbana na matatizo tu.Kwa upande wake Sala, akawa anajitahidi sana kumtuliza Mark katika wakati ule mgumu aliokuwa nao.Kilio kikubwa cha Mark, kilimgusa na kumuumiza sana dokta na alizidi kumuonea huruma Mark.Dokta akainuka katika kiti chake, akamfuata Mark ili aweze kumtuliza.

    "Mark, usitamke maneno hayo ya kumkufuru Mungu kwakuwa Mungu ni wetu sote.Mitihani kwa mwanadamu ni kitu cha kawaida tu kijana wangu.Katika hili la baba yako, kwa upande wangu nitakusaidia katika jambo moja." Alizungumza dokta na kumueleza Mark.Mark lile kidogo likamfariji moyoni mwake na akawa tayari kuupokea msaada wa dokta yule.



    "Najua kwa hali ya nyumbani mliyokuwa nayo, itakuwa ngumu sana wewe kuweza kumuhuduia mzazi wako katika maradhi haya yamsumbuayo, hivyo mimi nitakusaidia katika hili kijana wangu.Baba yako tutamuweka katika kituo chetu cha wazee wasiojiweza na wenye maradhi mbalimbali na atakuwa chini ya usimamizi wa madaktari.Kama ukitaka kuja kumuona, unaweza kufika hapa hospitali na kwenda kumsalimia." Kwa busara kubwa sana huku akimtuliza kijana mdogo, Mark, dokta alizungumza maneno haya.

    "Nakushukuru sana dokta kwa msaada huo mkubwa ulionipatia, mimi nakuahidi nitajitahidi sana kusoma ili siku moja niweze kupata kazi na kupata fedha za kuweza kumtibu baba yangu." Mark alimshukuru dokta kwa msaada ule alioutoa kwake na kwa uchungu mkubwa akaeleza nia yake ya kutaka kusoma kwa bidii kubwa ili siku moja aweze kupata fedha za kumtibu baba yake, mzee Peter.Baada ya kumaliza kuongea na dokta, dokta akawachukua Mark pamoja na Sala na kuwapeleka mpaka katika kitanda alichokuwa amelazwa mzee Peter.Mzee Peter alifarijika sana kumuona kijana wake Mark mahali pale, alitabasamu na kumfurahia lakini alishindwa kumuongelesaha chochote mtoto wake kwasababu alikuwa hana uwezo wa kuongea tena kutoka na kupooza viungo vyake vyote vya mwilini.Mark akashika mkono wa baba yake na kuweka nadhiri kubwa mbele ya baba ya kuwa, kwa gharama yoyote ile atajitahidi na kuhakikisha siku moja atamuinua baba yake pale kitandani na kumrudisha katika hali yake ya kawaida.Maneno yale ya Mark yalimfanya mzee Peter kudondosha chozi pale kitandani alipolala, Mark pamoja na Sala wakamkumbatia baba na kuchukua baraka zake kisha wakamuaga na kurudi nyumbani.



    Ni siku nyingine asubui na mapema, Mark pamoja na Sala wanawasili shule kwa ajili ya kuendelea na masomo yao kwa mara nyingine baada ya kila kitu kuisha.Wanafunzi wachache walienda kuwapa pole kutokana na matatizo haliyowakuta, lakini wengi wao walichukizwa na kutofurahia kwa kitendo kile cha Mark pamoja na Sala kurudi shule kwa mara nyingine tena.Mark na Sala hawakuyajali yale, zaidi walijikita katika kusoma na kuendelea kujiandaa na mtihani wao wa taifa ambao ulikuwa karibu kufanywa.Mtihani huu waliokuwa wanajiaandaa nao, ulikuwa ni mtihani wa mwisho kwa ajili ya kumaliza elimu yao ya Sekondari kwa kidato cha nne na kuingia kidato cha tano.

    Mark pamoja na Sala, kasi yao katika kusoma ilikuwa kubwa sana na walizidi kuongeza umakini katika maandalizi yao ya mtihani.



    Siku nazo zikazidi kusogea na hatimaye tarehe za kuanza mitihani yao ikawadia.Mark na Sala, kwa pamoja wakasali kabla ya mitihani na kumuomba Mungu, awabariki na kuwaongoza katika mitihani ile muhimu katika kuandaa maisha yao ya baadae.

    Walijitahidi kuifanya mitihani yao kwa umakini tangu mwanzo mpaka walipomaliza na kila mmoja akitarajia kufanya vizuri katika mitihani ile.Baada ya matokeo kurudi, shule ya Sekondari Dakawa ilionekana kufanya vizuri sana na kufanikiwa kufaulisha wanafunzi wengi.Miongoni mwa wanafunzi walionekana kufanya vizuri pale shuleni walikuwa Mark pamoja na Sala.Mark aliona amekamalisha moja ya njozi zake alizokuwa anazoziwaza katika maisha yake na akazidi kujiandaa kwa ajili ya kuendelea na masomo yake akiwa bado chini ya ufadhili wa yule mzungu.

    Baada ya wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa taifa kupangiwa shule kwa ajili ya kuanza elimu ya kidato cha tano na cha sita, Mark pamoja na Sala wakajikuta wakipangiwa katika shule moja.Mark na Sala walilifurahia lile na kufarijika sana maana walishazoeana sana na hakuna hata mmoja aliyetamani kukaa mbali na mwenzake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Katika kipindi chote hiki, Mark hakuchoka kwenda kumtembelea baba yake mzee Peter mahali alipohifadhiwa kwakuwa aliamini mafanikio yake, pia yanatokana na mchango mkubwa kwa baba yake kwa kumuombe na kuzidi kumtakia mema katika masomo yake.

    Baada ya kufanikiwa kufaulu mtihani wake Mark, alihisi sasa anaanza kuuona mwanga wa kuweza kufanikisha malengo yake aliyojiwekea na aliamini ipo siku shida zote azipitiazo zitakwenda kuisha na kubaki kuwa historia katika maisha yake.Mark aliona, elimu ndio tumaini na njia pekee ya kuweza kupita katika kuyakamiliaha malengo yake yote aliyojipangia.



    Baada ya kuanza masomo ya kidato cha tano (Advance level), Mark alipata shida kidogo katika kuyaelewa masomo na kuanza kuiona elimu ngumu, kutokana na ugumu wa masomo aliyokuwa anayosomea.Lakini Mark alichukulia ile ni moja ya changamoto tu katika elimu na haitoweza kumkatisha tamaa katika kuutafuta mwanga wa mafanikio.Huku akiwa pamoja na rafiki yake wa karibu Sala, Mark alizidi kuongeza bidii ya kusoma.



    Kadri siku zilivyozidi kwenda, Mark pamoja na Sala walizidi kuyazoea masomo na kuanza kufanya vizuri.Juhudi yao ilikuwa kubwa na hatimaye walifanikiwa kufaulu katika mitihani yao ya kuhitimu elimu ya kidato cha sita na kufanikiwa kupata nafasi ya kuingia chuo.Faraja ilizidi kuongezeka kwa Mark pamoja na Sala na wakazidi kumshukuru Mungu kwa baraka kubwa anayowajalia katika maisha yao.Umakini ule mkubwa wa Mark katika masomo, ulimfurahisha sana mdhamini wake, akamuita ofisini kwake na kumpa ahadi kubwa ambayo ilimfanya Mark kujiona wa kipekee sana katika dunia hii.





    "Wewe ni kijana mwelevu sana Mark na nashukuru kwasababu haukuwai kuniangusha tangu nikuchukue na kuanza kukusomesha.Pia sambamba na hilo nachukua fursa hii kukupongeza sana kwa kuweza kufaulu mitihani yako na kufanikiwa kuingia chuo, hongera sana kijana wangu." Alizungumza mdhamini wake Mark ambaye alikuwa akijulikana kwa jina la Mr.Harry. Mr Harry alikijiua kiswahili vilivyo ijapokuwa yeye ni raia wa Marekani kwasababu alishakaa sana hapa Tanzania na kufanikiwa kujifunza lugha hii hadhimu hapa Tanzania.

    "Asante sana bosi." Mark alimshukuru mr.Harry kwa pongezi zake.

    "Pamoja na hilo, lipo jambo moja ninalotaka kukufanyia Mark na naomba ulikubali jambo hili."

    "Bila shaka niambie tu bosi" kwa utulivu mkubwa alijibu Mark.

    "Nchini Marekani nina kampuni kubwa ya vinywaji, hivyo nahitaji baada ya wewe kumaliza chuo nikupeleke Marekani ili ukaisimamie kampuni hii." Alizungumza Mr.Harry.

    Jambo hili alilotarifiwa Mark, lilimpa faraja sana moyoni mwake na kuona hii nafasi ya kipekee kwake anayotakiwa aitumie ili aende kukamilisha ndoto zake.Bila kuchelewa Mark, alikubaliana na Mr.Harry katika lile na kumuahidi yupo tayari kwenda Marekani na kuisimamia kampuni ile baada ya kumaliza Chuo. Mr.Harry naye akafurahishwa na lile, akatoa kiasi cha fedha na kumkabidhi Mark kwa ajili ya matumizi na maandalizi ya chuo.



    Siku hii Mark alionekana kuwa na raha sana, muda wote usoni mwake kulionekana kujawa na tabasamu.Baada ya kutoka ofisini kwa mr.Harry, Mark akaona ni heri akaonane na Sala ili aweze kumtaarifu kuhusu aliloambiwa na mdhamini wake mr.Harry.Alifika nyumbani kwa Sala, Sala alifarijika sana baada ya kumuona Mark, akamkaribisha ndani ili aweze kuzungumza nae.

    "Mark, uso wako unaonesha kuna raha kubwa iliyopo ndani yako siku ya leo, embu nishirikishe na mimi, raha hiyo inatokana na nini?" Aliuliza Sala.

    "Hahahaha!, Hakika Sala wewe ni mmbea sana?" Mark aliangua kicheko na kumtania Sala kidogo.

    "Kwanini unasema hivyo Mark?"

    "Yani umeweza kunigundua jinsi nilivyo haraka namna hiyo!"

    "Hapana Mark, tumeshakuwa pamoja kwa muda mrefu sana hivyo nakutambua vilivyo, ukiwa katika hali ya huzuni nafahamu na ukiwa katika hali ya furaha nafahamu pia."

    "Sawa, ila leo nina habari njema sana!"

    "Zipi hizo Mark!? Kwa shauku kubwa ya kutaka kujua, Sala alimuuliza Mark.

    Mark akamsimulia kila kitu Sala juu ya safari yake ya kwenda nchini Marekani baada ya kumaliza chuo na ahadi zote alizohaidiwa na mdhamini wake Mr.Harry.Lakini Mark alipata mshangao sana baada ya kumuona Sala kutoonyesha kulifurahia jambo lile alilomueleza huku akionekana akiwa amebaki kimya bila kuongea chochote.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Mbona unaonekana hujafurahishwa na jambo hili la mimi kwenda nchini Marekani Sala, nini tatizo?" Mark alimuuliza Sala, lakini Sala alibaki kimya na kutomjibu chochote Mark.

    "Tafadhali Sala naomba uniambie, tatizo nini!?" Kwa sauti ya upole Mark akamueleza Sala.Sala akashusha pumzi na kumtazama Mark usoni.

    "Mark, wewe unaenda kuishi mbali uko, unahisi mimi nitabaki na nani hapa na wakati unafahamu kabisa kuwa mimi siwezi kukaa mbali nawe?" Kwa sauti ya unyonge, alizungumza Sala.

    "Yani hili ndilo linalokupa hofu Sala, kama mimi nitaenda kufanya kazi Marekani, nakuahidi lazima nitakuchukua wewe na tutaenda wote." Mark alizungumza na kumueleza Sala.Baada ya Mark kuzungumza maneno haya, moyo wake Sala ulilipuka kwa furaha, akainuka alipokaa na kwenda kumkumbatia Mark.

    "Nakupenda sana Mark na sitamani kukupoteza kabisa katika maisha yangu, naomba usije kujaribu kukaa mbali nami kwasababu moyo wangu utapata maumivu makali sana." Alizungumza Sala.Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Sala kuzungumza maneno kama haya mbele ya Mark, Mark alibaki ameduwa na kupata kigugumizi cha ghafla, akamuangalia Sala na kutaka kumueleza kitu.

    "Sa..sa..saw..sawa Sala!, hata mimi sitamani kukaa mbali nawe lakini naomba nikuombe kitu moja Sala." Alizungumza Mark.

    "Sema tu Mark, mimi nakusikiliza."

    "Naomba kwa sasa Sala, tuzingatie sana katika masomo yetu tunayokwenda kuanza chuoni na baada ya hapo ndipo mambo mengine yafuate." Kwa sauti ya upole, Mark alimueleza Sala.

    "Ondoa hofu kuhusu hilo mimi nitasubiri tu ila naomba uniahidi kitu na wewe pia." Alizungumza Sala.

    "Nikuahidi nini Sala!?"

    "Naomba uniahidi kuwa hautokuja kuwa na mwanamke mwingine zaidi ya mimi." Kwa sauti ya kubembeleza, Sala alimueleza Mark.Mark akashusha pumzi kwa nguvu, akamtazama Sala na kumueleza kitu.

    "Sala, nakuahidi sitokuwa na mwanamke mwingine katika maisha yangu zaidi yako ila naomba kwa sasa tuzingatie sana na kujikita zaidi katika masomo." Mark alizungumza na kumueleza ahadi yake Sala.Sala alifajika sana kwa lile, akaandaa chakula na kula pamoja na Mark.



    Maisha ya chuo hayakuwa magumi sana kwa Mark wala Sala, kwasababu akili yao yote walielekeza katika masomo kama walivyokubaliana awali.Saa, siku na miaka ikasogea, hatimaye Mark pamoja na Sala walikuwa wamebakiza mwaka mmoja kabla ya kuhitimu masomo yao ya chuo, ambapo wote walijikita katika kusomea mambo ya kibiashara.Mark hakuwa na shaka kuhusu ajira kwasababu Mr.Harry alishamuahidi baada ya kumaliza chuo, atamsafirisha na kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kusimamia kampuni yake.Siku moja Mark akiwa na Sala chuoni, huku wakiendelea kujisomea, ghafla Mark akaitwa ofisini kwa mkuu wa chuo.Mark naye bila kuchelewa akatii wito ule.Baada ya Mark kufika ofisini, akashangaa kumuona mkuu wa chuo anatikisa kichwa huku akimuangalia yeye kwa kumuonea huruma sana.Hofu na wasiwasi ikanza kumuingia Mark na kujiuliza maswali mengi ya kwanini mkuu wake yupo katika hali ile baada ya yeye kuingia pale ofisini.





    "Karibu uketi Mark" mkuu wa chuo akamkaribisha Mark katika kiti ili aweze kuketi, naye Mark akaketi na kusalimiana na mkuu.

    "Ndio mkuu, nimeitika wito wako." Alizungumza Mark baada ya kusalimiana na mkuu wa chuo.

    "Nimekuita Mark kwa lengo la kukupa taarifa ambayo tumeipata hivi punde."

    "Ndio mkuu, nakusikiliza"

    "Tumepokea taarifa ya huzuni kidogo na inahusiana na wewe Mark." Alizungumza mkuu wa Chuo.Kauli hii ya mkuu, ilimshtua na kumpa wasiwasi mkubwa Mark kwasababu hakuelewa ni taarifa ipi hiyo ya huzuni inayohusiana na yeye.

    "Mark taarifa tuliyoipokea, inasemekana mdhamini wako Mr.Harry asubui ya leo amepata ajali mbaya sana ya gari wakati akielekea katika majukumu yake ya kikazi.Pia sambasamba na hilo , ajali hii aliyoipata mr.Harry, ilipelekea na umauti kumfika hapo hapo.Hivyo kutokana na hili, sisi hatuna budi ya kukupa pole kwa msiba huu mzito upande wako na pia unahitajika haraka ufike nyumbani kwa Mr.Harry ili nawe ukashiriki katika msiba huu." Mkuu wa chuo alizungumza na kumtaarifu Mark kuhusu msiba wa mdhamini wake.

    Nguvu zote Mark zilimuisha na kulegea mwili mzima baada ya kupokea taarifa hii, machozi yakaanza kumdondoka bila ya yeye mwenyewe kutambua, akahisi kila kitu kilichopo akili mwake kinaenda kufutika kabisa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hapana mkuu, siku ya jana mimi mwenyewe nilionana na kuongea nae mr.Harry na akaniahidi na kuniambia, siku ya leo baada ya kutoka chuo nipitie ofisini kwake kwa ajili ya kuchukua ada na fedha nyingine zilizobaki kwa ajili ya malipo ya chuo, hivyo nina hakika mr.Harry yupo hai au pengine ulinukuu vibaya taarifa hii." Kwa uchungu mkubwa, Mark alizungumza na kumwambia mkuu wake huku akiiamini kuwa mr.Harry bado yupo hai.Mkuu wa shule akasimama na kumfata Mark pale alipokaa, akamshika bega lake na kuongea maneno kwa ajili ya kumtuliza.

    "Najua ni vigumu sana kwa wewe Mark kuamini taarifa hii, lakini huu ndio ukweli wenyewe tulioupata na naomba uwe mvimilivu katika wakati huu mgumu kijana wangu." Yalikuwa maneno ya busara yakitoka katika kinywa cha mkuu wa chuo kwa ajili ya kumfariji na kumtuliza Mark.



    Akiwa amejituliza na kuendelea kupitia na kusoma vitabu mbalimbali Sala huku akiendelea kumsubiri Mark ambaye alikuwa ameelekea ofisini na kumuacha mahali pale baada ya kupokea wito kutoka kwa mkuu wa Chuo, mara anakuja John ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Mark pale chuoni.

    " 'Hallow' mrembo, vipi mbona uko peke yako, rafiki yangu Mark ameenda wap?" John alimuuliza Sala.

    "Mark ametoka kidogo na kuelekea ofisini kidogo maana mkuu wa chuo alimuhitaji" Sala alimjibu John.

    "Sawa Sala, Kama hutojali Sala, naomba nafasi ya kukuuliza Swali moja." Alizungumza John.

    "Unaweza ukauliza tu shem, mimi nakusikiliza."

    "Hivi unafikiri Mark ni mwanaume sahihi upande wako, mimi naona kabisa mtu kama Mark hastahili kabisa kuwa na mtu kama wewe kutokana na hadhi yake aliyonayo." Alizungumza John.Sala alishtuka kidogo baada ya kusikia kauli hii kutoka kwa John, akamgeukia na kumtazama John ili aweze kuongea nae vizuri.

    "Unamaanisha nini kuongea maneno hayo John!?' Kwa mshangao mkubwa, Sala alimuuliza John.

    " Usinifikirie vibaya shem, ila mimi, Mark ni rafiki yangu mkubwa na namtambua vizuri sana tangu tukutane hapa chuo, naomba uwe makini sana Sala katika uteuzi wako."

    "Mbona sikuelewi shemu, nini unachomaanisha!?"

    "Ninachomaanisha Sala, Mark sio mwanaume sahihi kwako na naomba tafuta mwanaume sahihi na anaendana na hadhi yako kama sisi kuliko chokoraa na maskini kama Mark." Yalikuwa maneno ya kashfa sana kwa Mark, aliyazungumza John na kumwambia Sala.Maneno haya yalimuumiza Sala na kumpelekea kuingiwa na hasira mno, uvumilivu ukawa mdogo kwa Sala, akainua mkono wake na kumtandika kibao John katika shavu lake.

    "Hivi wewe unamfahamu Mark kuliko mimi!?, Hivi unafahamu vizuri mimi na Mark tulipotoka!?, Unafahamu mambo mangapi tumepitia mimi na Mark mpaka leo tuko hapa!?, sasa naomba unisikilize John, tena unisikilize kwa umakini sana, ukiendelea kuzungumza maneno yako haya ya kipuuzi nitakuja kukufanya kitu kibaya sana na pia nitamsimulia na kumueleza Mark kila kitu ulichonieleza hapa.

    Baada ya kupigwa kibao kile na Sala, John akaona ni udhaifu na fedhea kubwa kwake kupigwa na mwanamke, naye akathubutu kuinua mkono wake ili aweze kumpiga Sala.Wakati akijiandaa kuchusha mkono wake na kuachia kibao kwenda mwilini kwa Sala, ghafla akasikia sauti ya ukali nyuma yake na ikimtaka kusimamisha jambo lile atakalo kulifanya.Muda wote huo Sala macho yake aliyakuwa ameyafumba ili asiweze kushuhudia kibao kile atakachopigwa na John, lakini baada na yeye kusikia sauti ya kumsimamisha John kumuadhibu yeye, akafumbua macho ili aweze kumtazama mtu aliyekuja kwa ajili ya kumsaidia.John naye akashtuka sana, taratibu akashusha mkono wake chini na kugeuka ili aweze kumtazama mtu aliyemsimamisha yeye kumpiga Sala.Baada ya kugeuka nyuma, John akashindwa kuamini kwa kile alichokiona pale, kwa kasi kubwa, jasho likaanza kumtoka mwilini mwake huku hofu na wasiwasi mkubwa ukamuingia, akasimama ila aweze kuzungumza neno lakini kabla hajaongea lolote akashtukia kofi zito likishuka mwilini mwake na kumpelekea kuanguka chini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Kitendo cha kumgusa na kutaka kumuumiza Sala, hilo ni kosa kubwa Sana kwangu.Tafadhali John, kama unahitaji urafiki wetu usiingie dosari, usije kujaribu kufanya kitendo hiki ambacho ulitaka kukifanya hapa kwa Sala!" Ilikuwa sauti ya Mark iliyoambatana na ghadhabu kubwa mno, akimueleza na kumuonya John kwa yale aliyotaka kuyafanya kwa Sala.Huku aibu kubwa ikiwa imemshika, John akainuka na kusimama.

    "Mark, wewe ni rafiki yangu wa kweli kabisa na katika maisha yangu sijawahi kuwa na rafiki mzuri kama wewe, nakuomba Mark usinifikirie vibaya na mimi siwezi kufanya chochote kibaya kwa binti huyu umpendae." Huku akionekana kuwa mpole sana, John alizungumza na kumueleza Mark.

    "Sawa John, unaweza ukaenda ila naomba uzingatie sana hayo niliyokueleza." Mark aliongea na kumueleza John, kisha John akaondoka na kumuacha Sala na Mark mahali pale.



    Baada ya John kuondoka, ndipo Mark akapata fursa ya kuweza kuzungumza na Sala.

    "Japokuwa John ni rafiki yangu lakini naomba kuwa nae makini sana Sala." Mark alizungumza na kumtaka Sala kuweka umakini dhidi ya rafiki yake John.

    "Sawa, nimekuelewa Mark.Tukiachana na hayo Mark, vipi mkuu alikutia nini ofisini kwake?" Sala alimuuliza Mark, lakini Mark hakumjibu chochote Sala badala yake akainamisha kichwa chake chini na kuwa katika hali ya masikitiko sana.Sala alizidi kupata hofu baada ya kumuona Mark machozi yakimdondoka na akionekana kuwa katika hali ya huzuni sana.

    "Mark, mbona upo katika hali hii, ulipotoka kuna usalama kweli!?" Kwa wasiwasi mkubwa, Sala alimuuliza Mark.

    Mark alishusha pumzi yake kwanguvu, akainua kichwa chake na kumtazana Sala usoni.

    "Ondoa shaka Sala, nitakusimulia kila kitu nilichoelezwa na mkuu." Mark alimtuliza Sala na kuamua kumsimulia kila kitu juu ya alichotaarifiwa na kuelezwa na mkuu wa chuo.

    Baada ya kupata taarifa zile za msiba wa mr.Harry, Sala alimuonea huruma sana Mark kwasababu kila siku katika maisha yake amekuwa ni mtu wa kukumbana na mitihani.

    "Pole sana Mark, najua ni taarifa ambazo zimkushtua mno na kuumiza sana moyo wako ila ni vema ukaenda nyumbani kwa mr.Harry ili ukahakikishe kama haya uliyoambiwa ni ya kweli." Kwa sauti tulivu na ya kubembeleza, Sala alimueleza Mark huku akiendelea kumtuliza ma kumtaka kuwa mvumilivu katika lile.Bila kuchelewa, Mark akaona ni heri asiupuuze ushauri ule aliopewa na Sala, akamuaga Sala na kuondoka pale chuoni kwa ajili ya kwenda kuhakikisha kuwa kama ni kweli mdhamini wake mr.Harry ambaye ni raia wa Marekani amefariki kama alivyotaarifiwa na mkuu wake wa chuo.Baada ya Mark kufika nyumbani kwa Mr.Harry, lile alilokuwa analipinga ndilo alilolikuta pale.Watu wengi walikuwa wamefika na kukusanyika nyumbani kwa mr.Harry huku huzuni kubwa ikiwa imetawala kila mahali.Huku uchungu mkubwa ukiwa umemjaa na kutoamini kwa kile alichokiona pale, taratibu Mark naye akajumuika kwa ajili ya kushiriki katika msiba ule.Ikiwa ni mida ya jioni, moja ya ndugu wa karibu na familia ya mr.Harry akatoka na kutangaza utaratibu wote kuhusu msiba ule.Utaratibu ambao ulikuwa umetangazwa, siku ya kesho maiti itachukuliwa na kusafirishwa nchini Marekani kwa ajili ya maziko.Baada ya kutolewa utaratibu huu, Mark akaona ni heri naye akajumuika kwa kulala palepale msibani.

    Ikiwa ni siku nyingine, maandalizi yote yalikuwa tayari kwa ajili ya kusafirisha mwili wa Mr.Harry, Mark alibaki na huzuni kubwa moyoni mwake na kukata tamaa kabisa ya maisha kwa sababu mr.Harry ndio mtu pekee aliyekuwa anamtegemea katika kukamilisha ndoto zake.Akiwa katika hali hiyo Mark, mara anakuja mtu pale alipokaa na kumpa taarifa kuwa yupo mtu mmoja anahitaji aonane nae pale msibani.



    Akiwa nyumbani Sala, hofu kubwa ilikuwa juu ya Mark ambaye kila alipojaribu kupiga simu yake ilikuwa haipatikani.Wasiwasi mkubwa ulimjaa Sala kwasababu hii haikuwa kawaida ya Mark, kushindwa kuwasiliana nae zaidi ya kupita siku moja.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mark akatoka na kwenda kuonana na mtu yule amwitaye.Alishangaa baada ya kumuona mke wa marehemu mr.Harry ndiye aliyekuwa anahitaji kuoanana nae.Mark akamsalimia mke wa mr.Harry na kusikiliza kwa kile anachotaka kuambiwa.

    "Wewe ndio Mark?" Mke wa mr.Harry alimuuliza Mark kwasababu alikuwa hamtambui, lakini Mark yeye alikuwa akimtambua kupitia mdhamini wake mr.Harry kabla hajapatwa na umauti.

    "Ndio mimi bosi." Alijibu Mark.

    "Je unamfahamu vipi mr.Harry?"

    "Alikiwa mdhamini wangu katika masomo bosi"

    "Sawa Mark, mume wangu alinieleza kila kitu kuhusiana na wewe, ila nilikuuliza ili nipate uhakika kama ndio wewe mwenyewe."

    "Asante bosi, pia nachukua fursa hii kukupa pole kwa kuondokewa na mume wako, mr.Harry."

    "Asante Mark, Nimekuita hapa kwa lengo la kutaka kukueleza jambo moja."

    "Sawa bosi nami nakusikiliza." Alijibu Mark na kuongeza umakini wa kusikiliza ili aweze kusikia anachotaka kuambiwa na mke wa mdhamini wake.

    "Mark, kama unavyoona kuwa kwa sasa mume wangu ameshafariki, hivyo kutokana na hili sisi hatuna budi kuamisha makazi yetu kutoka hapa Tanzania na kurudi nyumbani kwetu Marekani kwasababu tulikuwa tunaishi hapa kwa ajili yake.Pamoja na hilo Mark napenda kukueleza sisi hatutakuwa na uwezo wa kukusimamia wewe tena katika masomo yako, hivyo naomba ujitahidi kutafuta mtu mwingine ili aweze kukuendeleza pale tulipoishia sisi.Naomba usijisikie mnyonge kwa hili Mark na wala lisikuvunje moyo katika masomo yako na zaidi napenda kukuahidi, kama huko niendako mambo yatakaa sawa nitakuita ili uje kusimamia kampuni ambayo marehemu mume wangu alikuahidi kukupa fursa hiyo." Yalikuwa maneno ya mke wa Mr.Harry.Maneno haya yalikuwa mithili ya msumari wa moto ambao ulienda moja kwa moja kuchoma na kuumiza sana moyo wa Mark.Maneno yale aliyoambiwa, yalimnyong'onyesha sana Mark na kuona ndoto zake alizokuwa anaziota sasa zimefikia kikoma kutokana na kupoteza masaada ule aliokuwa anaupata kutoka kwenye familia ya mr.Harry.Hakuwa na jinsi Mark, akamsikiliza mrs.Harry na kumuelewa kwa yale aliyomwambia.



    Ni wiki sasa imepita, Sala akiwa chuoni, mawazo yalikuwa mengi sana juu ya Mark ambaye hakuweza kumuona zaidi ya wiki sasa.Sala alijitahidi kumtafuta Mark kupitia simu yake ya mkononi lakini hakuweza kufanikiwa kumpata kwasababu muda wote, simu yake Mark ilikuwa haipatikani.Pia Sala alijitahidi sana kwenda nyumbani kwa Mark, lakini nako Mark hakuwepo nyumbani zaidi ya wiki na haikujulikana wapi alipo.Huzuni kubwa ilimjaa Sala kwa kushindwa kujua wapi alipo kipenzi cha moyo wake Mark, muda wote Sala, machozi machoni mwake hayakukauka na huzuni kubwa iliendelea kumtawala kila alimpomfikiria na kukumbuka Mark wake.Masomo kwake yalikuwa magumu sana maana muda mwingi alishazoea kusoma akiwa pamoja na Mark.

    "Oooh! Mark mpenzi, kwanini imenifanyia hivi?, ungenipa hata taarifa sehemu ulipo kuliko kiniachia maumivu kama haya.Nitafanya nini miki Mark?, wiki sasa sijakutia machoni na sifahamu kama uko hai au umekufa.Usiendelee kuniacha katika hai hii, tafadhali njoo Mark, njoo Mark mwenzako nipo mpweke sana." Ni baadhi ya maneno na maswali ambayo Sala alikuwa akijiuliza mwenyewe bila kupata majibu.

    Akiwa katika hali hiyo ya huzuni na machungu makubwa Sala, mara anafika John na kumsemesha.

    "Sala, kwanini muda wote unakuwa katika hali hii, amini tu rafiki yangu Mark yupo salama na atarudi tu." Alizungumza John kwa lengo la kumfariji Sala.Sala hakujibu chochote zaidi alibaki kimya na kuendelea kulia tu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sala, umeshalia sana sasa, naomba unyamaze kwasababu naamini Mark yupo na atarudi kwako tena."

    "John, nafahamu Mark ni rafiki yako sana naomba uniambie, kweli hukuwahi kumuona mahali kokote kule." Kwa unyonge na simanzi kubwa ikiwa ndani yake, Sala alimuuliza John ambaye ni rafiki mkubwa wa Mark.

    "Nyamaza Sala, binafsi naumia sana ninapokuona upo katika hali muda wote na ndio maana nilikuonya awali uwe makini sana ili usije kupitia wakati mgumu na kuumiza moyo wako kama hivi." Alizungumza John.

    "John, kwa maneno hayo unayoniambia nina hakika kuna mahali umemuona Mark, naomba uniambie John, Mark yuko wapi?"

    "Lolote lile nitakalokwambia Sala kuhusu Mark nadhani hutoniamini, naomba tuache kama lilivyo ila amini tu Mark atarudi." Yalikuwa maneno ya kimafumbo sana kutoka kwa John ambayo yalizidi kumchanganya Sala.

    "John, kama huwezi kunieleza lolote hapa naomba ondoka na uniache peke yangu kwasababu unaonekana wewe hili halijakugusa kama lilivyo nigusa mimi." Kwa uchungu na hasira kiasi fulani, Sala alimueleza John.

    "Unajua Sala mimi sipendi kuzidi kukuumiza zaidi ya hapa unapoumia, ila kwa kuwa unahitaji nikwambie, basi nami nitakwambia kitu juu ya Mark" Alizungumza John na kumfanya Sala atulie ili aweze kumsikiliza kwa umakini.

    "John, naomba unieleze umemuona Mark na kama umemuona yuko wapi kwa sasa?"

    "Sawa Sala, kwasababu unahitaji nitakwambia.Siku ya jana, majira ya asubui nikiwa nakuja hapa chuo nilimuona Mark akiwa na mwana.....!!?"

    "Sala...!!".

    John aliamua kumueleza Sala juu ya anachokifahamu kuhusu Mark, lakini kabla hajamalizia maelezo yake, mara wakasikia sauti ikiita jina la Sala mahali pale.





    Sala alikuwa wa kwanza kuitambua sauti ile, moyo wake ukafarijika na kulipuka kwa furaha baada ya kusika sauti ile ambayo ilipenya vilivyo masikioni mwake.Baada ya kugeuka na kumtazama mtu amwitaye, hakika alikuwa kipenzi cha moyo wake Mark akiwa amefika mahali pale.Bila kujali chochote, kwa furaha kubwa ya kumuona Mark, Sala alisimama pale alipokaa na kwenda kukumkumbatia Mark.John alibaki amepigwa na butwaa kwa ujio ule wa ghafla wa Mark, huku akionyesha tabasamu la kinafiki naye akainuka na kumkumbatia Mark na kushukuru Mungu kwa kurudi kwake akiwa salama.

    "Mark ulikuwa wapi?, kwanini uliondoka bila kuniaga?, kwanini ulifanifanyia hivi mimi?, ulihisi nitabaki na nani mimi Mark!?", yalikuwa maswali ya mfululizo huku machozi yakimdondoka machoni mwake, Sala alimuuliza Mark.

    " Mark akamkumbatia Sala kwa lengo la kumtuliza kwasababu alitambua jinsi gani anavyoumia moyoni mwake kwa kumkosa yeye zaidi ya wiki sasa.

    "Naomba utulie Sala, usijali Mark wako nipo salama na hakuna tatizo lolote lililonikuta ila kuna mambo kidogo hayakuwa sawa, ngoja nikaonane na mkuu halafu nitakuja kukueleza mengi zaidi." Mark alimtuliza Sala, akamuaga na kuelekea ofisini kwa mkuu wa chuo.

    Mark akaongoza na kufika ofisini kwa mkuu, akasalimiana nae na kukaribiswa aweze kuketi katika kiti cha wageni pale ofisini.Siku hii Mark alishangaa kidogo baada ya kumuona mkuu wake kutoonyesha furaha kwake kama alivyomzoe anapokutana nae.Baada ya kuketi Mark, mkuu wa chuo akafungua droo yake na kutoa bahasha yenye rangi ya kaki na iliyofungwa vizuri na kumkabidhi Mark.

    "Mkuu hii bahasha uliyonipa, inahusiana na nini!?" Kwa mshangao mkubwa, Mark alimuuliza mkuu wake.

    "Mark, ndani ya bahasha hiyo niliyokupa kuna barua ya kukusimamisha chuo.Kutokana na madeni unayodaiwa pamoja na ada ya mwaka huu wa mwisho ambayo bado unadaiwa, uongozi wa chuo umeamua kukusimamisha na kukupa muda wa wiki moja uweze kukamilisha madeni hayo la sivyo tutakufuta kabisa hapa chuoni." Yalikuwa maneno maelezo kutoka kwa mkuu wa chuo akimueleza Mark kuhusu barua ile aliyomkabidhi.Ilikuwa ni taarifa ambayo ilizidi kumnyong'onyesha na kumchanganya sana Mark.Mark aliinuka na kwenda kupiga magoti mbele ya mkuu wake wa chuo, huku kilio kikimtawala, akajitahidi kumuomba na kumlili mkuu wake aweze kumuongezea muda wa kuweza kulipa mdeni yale anayodaiwa, lakini mkuu wa chuo akakataa katu katu na kudai lile limetoka katika bodi ya chuo na haliwezi kutenguliwa.

    Baada ya kulia na kubembeleza sana, Mark akaamua kukubaliana na lile na kutoka nje ya ofisi ya mkuu baada ya kuona mkuu wake kutoonyesha dalili yoyote ya kumsaidia katika lile.Baada ya kutoka kuongea na mkuu wa chuo, Mark akawakatu John pamoja na Sala wakiwa wanamsubili pale nje.Sala alimuangalia sana Mark wakati anasogea pale waliposimama wao, Mark alionekana kuwa mnyonge sana na uso wake ukionyesha yupo kwenye huzuni kubwa sana.

    "Mark, Uso wako unaonesha upo kwenye huzuni kubwa sana tofauti na ulivyokuja awali, nini tatizo? Sala alimuuliza Mark.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Usijali Sala mimi nipo sawa ila kwasasa nahitaji kwenda nyumbani kupumzika kidogo na mengi zaidi nitakutafuta baadae tuongee." Mark alimjibu Sala.

    "Mark, wiki sasa imepita bila ya mimi kuonana na wewe ina maana huna hamu ya kukaa na mimi hata kidogo tuweze kuongea kwa muda huu?"

    "Sala , naelewa yote hayo ila naomba kwa sasa nikapumzike halafu baadae nitakutafuta tuweze kuongea." Mark alimjibu Sala na kuondoka pale chuoni.Kitendo kile kilimuumiza sana Sala, machozi yakawa yanamdondoka na akahisi thamani yake kwa Mark imeshuka na ndio maana Mark anaonekana hamjali wala kumsikiliza kwa kile anachohitaji.

    Baada ya Mark kuondoka, John akawa anajitahidi kumbembeleza na kumnyamazisha Sala.

    "Naomba usilie Sala, kila kitu kitafika mwisho wake usijali." John alimueleza Sala huku akiwa amemkumbatia kwa lengo la kumtuliza.

    "John, thamani yangu imekuwa ndogo sana kwa Mark sijui nini kimempata nashindwa kumuelewa kabisa."

    "Sala, kwasasa si muda wa kuyafikiria maumivu unayoyapata bali ni muda wa kutafuta dawa ili uweze kutuliza maumivu hayo" John aliongea kimafumbo na kumueleza Sala.

    "Unamaanisha nini John kusema hivyo?"

    "Kipo kitu juu ya Mark ambacho bado hujakijua, naomba tukae chini ili nikueleze kitu hicho" John alimueleza Sala na kuketi chini ili amueleze kitu kinachomsumbua Mark.



    Mark alirudi nyumbani huku kichwa chake kikiwa kimejaa msongo mkubwa wa mawazo hasa zaidi kuhusu jinsi ya kupata fedha ambazo zinaweza kumrejesha chuo kwa ajili ya kuendelea na masomo yake.Muda wa wiki moja aliopewa na uongozi wa chuo kuweza kupata fedha hizo ambazo ni zaidi ya millioni ishirini, ulikuwa mdogo sana.Mark akawaza sana, nani anaweza kumpata ili aweze kumsaidia katika tatizo lile.Baada ya kuwaza sana ndipo akapata wazo la kimpigia rafiki yake mmoja aitwaye Nick ambaye alishawahi kusoma nae na kwa sasa Nick alikuwa akifanya kazi katika kampuni moja ya kibiashara baada ya kushindwa kuendelea na masomo kutokana na kufeli kidato cha nne.

    " 'Hallow Nick', Mark naongea, vipi uko poa wewe?"

    "Anhaa!, Mark, mimi ni mzima sijui wewe rafiki?"

    "Namshukuru Mungu mimi ni mzima rafiki yangu Nick.Vipi, leo jioni tunaweza tukakutana?"

    "Sawa, nitakutaarifu baada ya kutoka kazini tukutane 'THE GRAND BAR'."

    "Sawa Nick, usisahau kufanya hivyo"

    "Pamoja kaka" alijibu Nick na kukata simu.Hili kidogo likamfariji Mark kwa kuhisi pengine Nick anaweza kumsaidia kwa chochote katika kulikabili deni lile analodaiwa chuo.



    "Sala sidhani kwa hili nitakalokueleza kuhusu Mark kama utaniamini." John alimueleza Sala.

    "John, wewe niambie tu, nini kilochomsibu Mark mpaka abadilike namna hii." Sala alimueleza John kwa shauku kubwa ya kutaka kujua.

    "Sawa Sala, naomba unisikilize kwa umakini kuhusu ili nitakalokueleza." Alizungumza John na kujiweka tayari kwa ajili ya kumueleza kitu Sala kuhusiana na Mark.



    "Nilishindwa kukueleza hili mapema Sala kwasababu ya kuogopa mimi kuja kuonekana mchonganishi katika mapenzi yenu.Jambo moja tu nahitaji ufahamu Sala, yupo mwanamke mwingine tofauti na wewe ambaye ameuteka moyo wa Mark na ndio maana unamuona Mark, kwasasa amebadilika sana." Aliongea John na kumueleza Sala.

    "What!!!??, " John, naona unarudia ujinga wako kwa mara nyingine tena!, Kwa jinsi Mark anavyonipenda na kunithamini mimi, hawezi kufanya jambo la kipuuzi kama hilo."

    "Sala naomba uliamini hili, unataka nikuthibitishie vipi Sala mpaka uniamini mimi!?, Huo nilikouleza ndio ukweli halisi unaomuhusu Mark" Huku akionyesha kuwa na uchungu mkubwa, alizungumza John.Maneno yale ya John, yalimfanya Sala kupata huzuni na kilio kikubwa kilimtawala huku akishindwa kuamini kabisa kama Mark anaweza kumfanyia kitendo kama kile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog