Search This Blog

PADRI MLA NYAMA ZA WATU - 4

 





    Simulizi : Padri Mla Nyama Za Watu

    Sehemu Ya Nne (4)



    “Nilitembea kukanyaga ardhi huku wachawi wakinifuata kwa nyuma, kila nilipotoa mguu, nyuma yangu alikanyaga mtu.



    Tuliingia kwenye nyumba moja ya miongoni mwa wale watu waliosimama kuuliza kule kanisani.

    Wote tulifikia sebuleni, nikasimama na kuinua mikono huku nikisema kila jicho la mtu aliye ndani ya nyumba hii lisituone, hata kama lina nguvu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipomaliza, nilitangulia mbele, nikasimama kwenye mlango wa chumba, lakini hatukujua ni cha nani.

    Nilichofanya, niliufanya mkono kwa ishara kama nafungua pazia la dirisha ili mwanga upite, pale pale tukaona ndani ya chumba, walilala watu watatu kwenye kitanda kimoja kidogo, lakini



    tukajua ni watoto.



    Mimi nikageukia mlango mwingine ambao nao ulikuwa umefungwa, nikafanya vile vile kama mwanzo, mlango na ukuta vikayeyuka, chumba kikawa wazi.



    Kitandani walilala watu wawili, tukajua ni mke na mume. Nikiwa kama kiongozi wa msafara, sikutaka tuingie ndani, nilinyoosha mkono, nikafanya ishara kama ya kuwaita waje pale mlangoni



    tuliposimama sisi wachawi.

    Nilikuwa nachezesha kiganja kwa staili ya kuita, nachezesha, nachezesha, mpaka wakainuka kitandani na kukaa. Walifanya hivyo kwa pamoja, yaani mke na mume.



    Walitutumbulia macho, nikajua wanatuangalia sisi, wakakaza macho sana kwetu, lakini hakuna aliyeonekana kututambua. Nikazidi kuwaita kwa kutumia ile ishara ya mikono.



    Taratibu walianza kutoka pale kitandani huku wakiziacha shuka zao mpaka waliposimama wima wakasita kutembea. Ilibidi nitumie tena njia ile ile ya kuwaita kwa ishara ya kiganja cha



    mkono, wakaanza kutembea kuja mpaka mlangoni.



    Mambo hayo yalikuwa yakifanyika kwa mwendo wa pole pole sana mpaka wakatufikia, na mimi nikageuka, wachawi wenzangu nao waligeuka, wote tukaanza kutembea kwenda nje ya nyumba



    hiyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ulikuwa uwazi mkubwa nje, ni eneo ambalo unaweza kujenga nyumba hata mbili. Nilisimama na kuwaambia wenzangu watengeneze mduara, wakatii.



    Mduara ule uliwaweka kati wale watu wa familia tuliowatoa ndani kwao. Wakiwa kati, niliinama na kuchota mchanga, nikawarushia, ukawamwagikia, wale watu wakawa wadogo kama mpira,



    nilikuwa wa kwanza kuwafuata na kuwapiga teke kama mpira, wachawi nao wakaja na kuanza kuwacheza kama mpira. Ikawa vurugu ndogo pale nje, huyu anapiga, yule anadaka, yule



    anaurusha.



    Tulifanya hivyo mpaka kunakaribia kucha, kama kwenye saa tisa na nusu usiku, nikasitisha. Nilichota mchanga na kuwamwagia tena, wakarudi katika hali zao za kawaida.



    Nilitangulia ndani, wakafuata wale wana familia, baadaye wakaja na wachawi wenzangu.

    Tuliwaingiza hadi chumbani kwao, sisi tukasimama pale mlangoni, wao wakaenda mpaka kitandani, wakapanda na kulala tena kwa kujifunika gubiwgubi.



    ***

    Asubuhi, kwenye saa tatu nilitoka kwenda mjini, njiani nilisimamishwa na mwanamke mmoja, akanisalimia vizuri sana.

    “Padri, umesikia uchawi unavyoshika kasi kwenye eneo lako?” Yule mwanamke aliniambia, nikajifanya kushangaa, lakini nilishangaa kweli, maana sikujua alikuwa na maana gani.



    “Imekuwaje tena?” Nilimuuliza nikimkazia macho.

    Aliniuliza kama namfahamu mzee…(jina).



    “Ndiyo namfahamu, kafanyaje?”

    “Basi, wachawi wamewaingilia usiku wamewachukua na kwenda kuwalimisha usiku kucha, wameamka asubuhi wakiwa wamechoka sana, wamechafuka pia.”



    Nilijifanya kushtuka na kwamba siyajui hayo huku ukweli ni kwamba, kila kitu alichokiaongea mimi ndiye nilikuwa kinara ingawa si kweli kwamba tuliwalimisha.



    “Sasa waliwatambua?”

    “Hapana, mchawi unaweza kumtambua?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kweli huwezi.”

    “Eee, mchawi hata akiwa baba yako au mama yako, anaweza kukuingilia na usimjue, labda kama una malaika wakali,” alisema.



    Tuliagana, akaendelea na safari yake na mimi na safari yangu.



    Ilikuwa Jumapili iliyofuata, tukiwa ndani ya ibada kanisani, mimi nimesimama madhabahuni, akasimama mzeee mmoja bila kuruhusiwa wala kunyoosha kidole.

    Nilimtupia jicho baya sana, kwani nilihisi ana kitu kuhusu mimi tu. Sikumwambia kitu, ila yeye akasema:

    “Padri ninataka kusema kitu mbele ya waumini wenzangu, mbele ya kanisa na mbele ya Mungu muumba wa mbingu na nchi.”



    “Ghafla mzee mwingine akasimama na kumpinga yule mtu.

    “Hili ni kanisa, siyo jumba la siasa, kama kuna mtu anataka kuongea lazima kuwe na utaratibu maalum, toka zamani watu wanapotaka kuongea kanisani kunatangazwa, lakini siku za hivi



    karibuni kumezuka tabia, watu wanaongea wanavyojisikia.”

    Kundi kubwa la watu, wake kwa waume wakasimama na kumpinga huyu ambaye kwa upande mwingine nilimchukulia kama mtetezi wangu.

    “Mwache aseme kwanza tujue ni nini ndipo utaratibu ufuatwe,” mzee mmoja kati ya lile kundi lililosimama alikuja juu.



    Kundi jingine lilisimama na kusema.

    “Hatutaki watu wenye majungu kanisani, ala! Kama kuongea si kuna vikao na utaratibu wake?”

    Ikawa vurugu ndani ya kanisa tena ibadani, makundi mawili yakawa yanapingana huku wengine wakitishia kupigana na kutoana macho.

    Niliamua kufumbua kinywa na kusema:

    “Mimi nadhani kila mtu ana uhuru wa kusema, lakini kwa utaratibu.”

    Kauli hiyo ikawa kama nimechochea mambo. Mzee mmoja, hata sikumtarajia alitoka kwenye fomu na kuanza kuja mbele huku akisema:



    “Halafu wewe ndiyo tulikuwa tunakutafuta sana.”

    Lakini wakati anafika kwenye korido, kuna watu walitokea na kumkamata na kumtoa nje ya kanisa.

    Kifupi, nilijua hali ya hewa katika kanisa langu iliharibika na uwezekano wa kuuawa ulikuwa mkubwa, kisa najua ni uchawi tu.

    Ili kukwepa kasheshe nilikimbia na kuiacha madhabahu, lakini waumini waliendelea kuchafuana kwa maneno ya vijembe vya kila aina.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Nilifikiria kuwaita askari, lakini nikaona itakuwa vurugu kubwa zaidi kwani watu wenyewe walionekana kuwa na jazba.

    Nilikuwa kwenye chumba kimoja pembeni ya kanisa, mzee mmoja akanifuata:

    “Mtumishi twende ukamalizie ibada, waasi wote wamedhibitiwa,” aliniambia kwa sauti nzito iliyonifanya niogope kidogo.

    “Unadhani kuna amani tena?” Nilimuuliza.

    “Imejaa tele.”

    “Wale wenye fujo wametoka?”



    “Hawajatoka, lakini wametulia na kukubali kufuata utaratibu wa kanisa katika kuongea,” aliniambia.

    Nilimkubalia kwa kumtaka atangulie mimi nafuata nyuma.

    “Sawa mtumishi, njoo mimi nitakulinda kwa kila sababu.”

    Alipotoka tu, nyuma nilipiga magoti na kumwambia Mungu.

    “Ukanilinde bwana, watu wabaya wanaisaka roho yangu, lakini wewe bwana utanipigania sawasawa na maandiko yako.”

    Nilipomaliza, nilisimama na kusogea ukutani, nikanyoosha mikono juu na kusema:



    “Mzimu wa roho mbaya uwapige wote waliojikusanya kinyume na mimi. Nguvu za kichawi kuanzia sasa ziwe mbele yangu, moto ukawake kwa wale watu.”

    Nilipomaliza, nilitoka kurudi kanisani, kabla sijaingia kwa mlango wa pembeni, nikanyanyua mguu mmoja wa kushoto juu sana na kuupiga chini puu kisha nikafuta mikono kama vile



    nilishika vumbi.

    Niliingia ndani kanisani nikiwa si mimi, kwani nguvu na ujasiri niliokuwa nao naamini kila muumini alinishangaa sana.

    “Hili ni kanisa, kila mmoja anapaswa kuthamini uongozi wangu ili naye aheshimiwe na Mungu. Wale wote…”



    Nilipofika hapo nilisita si kwa kuogopa kusema bali kwa kuwafanya wote wawe tayari kunisikiliza ingawa walikuwa wakinisikiliza sana, nikaendelea.

    “Wale waliosimama na kuunga mkono yule mzee aliyesema anataka kusema kitu wasimame.”

    Walisimama waumini kama kumi na tisa hivi nilivyowahesabu kwa haraka haraka.

    “Natangaza kuwafungia ekaristi kuanzia leo mpaka nitakapoamua, kuhusu kuwepo kanisani ni uamuzi wenu, mkija sawa, msipokuja sawa. Kaeni.”



    Nilipomaliza kusema hayo nilisoma baraka za mwisho za ibada ili watu watawanyike.

    Nilikwenda ofisini kwangu, nikiwa nimeshavua kanzu ya utumishi.

    Kule ndani ofisini nilijifungia kwa ndani kisha nikavua nguo na kubaki kama nilivyozaliwa, nikasema maneno fulani, ghafla nikageuka, nikawa sionekani tena katika mwili.

    Nilitoka nikiwa wa mnyama hadi nje. Waumini wengi bado walikuwa nje ya kanisa wakiongea katika vikundi vikundi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilitembea kwa kurukaruka hadi pale walipo, nikatupa macho huku na kule nikimtafuta yule mzee wa kwanza kusimama kanisani na kusema anataka kuongea, hakuwepo.



    Nikamsaka yule mzee aliyetoka kwenye kiti ili aje mbele akisema mimi ndiye haswa niliyekuwa nikitafutwa, alikuwa amesimama na wanawake wawili wakiongea. Lakini mwanamke mmoja



    katika wale ni mchawi kwenye genge letu, akashtuka kuniona nikiwa uchi.

    Hapa nataka kusema, mchawi anaweza kuona wachawi wenzake hata kama yeye hayuko kichawi endapo tu atakuwa alijiandaa wakati anatoka nyumbani kwake kwa kupaka kidogo usoni unga



    fulani.

    Nilimnyooshea mkono kumpa ishara ya kukaa kimya, naye akatii hivyo. Nilimsogelea yule mzee na kumpiga konzi katikati ya kichwa, akaanguka chini.



    Waumini walikimbilia eneo la tukio lakini wale wanawake, mmoja akitawanyika kwa wasiwasi, mwenzake, yule mchawi mwenzangu alisimama pembeni kwa kujifanyisha tu.

    “Jamani siyo tumempoteza huyu?” Yule mwanamke mchawi alihoji.

    “Hapana, tumuwahishe hospitali,” alisema mzee mmoja.

    Lakini wazee wengine walishauri asiwahishwe hospitali kwani huenda ni mshtuko tu wa mambo yaliyotokea kanisani kwa kusimamishwa kushiriki ekaristi.



    Wenzangu pale pale alipiga mguu chini akageuka, akawa haonekani wazi, akaja kujiunga na mimi tukawa wachawi wawili.

    Shughuli ilikuwa pale mzee mmoja aliposhauri aitwe padri kwa ajili ya kumwombea mzee yule aliyeanguka.

    “Jamani, kwanini tusimwite padri aje kumwombea?”

    Wengine wote waliunga mkono, hata yule mwanamke aliyekimbia ambaye sasa alirudi.

    “Kwani yuko wapi padri?” Mzee mmoja alihoji.

    “Ofisini kwake,” karibu wote walisema maana wakati nakwenda ofisini waliniona.



    “Wazee wawili walitoka mbio kwenda ofisini kwangu kwa lengo la kuniita nikamwombee yule mzee aliyepiga mwereka kwa konzi langu.

    Yule mwanamke mchawi mwenzangu, alinifinya mguuni kwa kutumia mguu wake, nikamwelewa, nilipiga mguu mmoja chini, nikaamuru niwe ofisini kwangu muda ule ule, nikawa.

    Nilijirudisha katika ulimwengu wa kawaida, nikiwa na mavazi yangu ya kawaida, tena katika utu wema na unyenyekevu.

    “Ngo ngo ngo,” mlango uligongwa kwa ustaarabu.

    “…kwani we bwana ndiyo unanijua nilivyo, wema wako kwangu ni mkubwa sana, umenilinda, umeniongoza, naomba uendelee ee bwana, nikiikabidhi siku nzima mikononi mwako…”nilijifanya

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    niko katikati ya maombi…



    “Ngo ngo,” waligonga tena mlango, safari hii si sana. Inaonekana hata wao waliamini niko kwenye maombi, lakini kwa sababu ya dharura ya mtu kudondoka ghafla ndiyo maana hawakuwa na



    sababu ya kuacha kunigongea mlango, nikafungua.

    “Karibuni sana wazee wangu.”

    “Asante, tuna tatizo pale, mwenzetu kaanguka,” alisema mmoja wao huku wengine wakigeuka kuangalia eneo la tukio.

    “Nani?”

    Walimtaja jina, na mimi nikaangalia kulekule ili kuwa sambamba nao.

    “Tatizo nini?” Nilihoji nikishangaa sana.



    “Kaanguka tu, sijui ule mshtuko wa kanisani!”

    Tulitoka wote, kufika pale nikamwekea mkono wa kulia kichwani, nikaomba kimoyomoyo, lakini sikuomba kwa Mungu, niliomba kwa mkuu wa wachawi, kwamba amwamshe yule mzee na



    ajifunze kwa tabia yake ya kimbelembele si nzuri.

    Ghafla alipiga chafya, akafumbua macho na kuangaza huku na kule…

    “He! Vipi?” Eti aliuliza yule mzee.

    “Umekuwa mzima tena mzee, lakini acha kimbelembele chako mzee wangu,” nilimwambia bila aibu, wenzake walishtuka na kuniangalia kwa mshangao mkubwa.



    “Mnashangaa nini, kwani uongo?”

    Walibaki wameduwaa, nyuso zao zikiwa na maswali mengi, lakini hakukuwa na mjibuji.

    Nilitembea kuelekea ofisini, nikaifunga na kurudi kwenye makazi yangu lakini kwa mbali nilianza kuhisi kosa nililolifanya mbele ya waumini wangu.

    Nilijua pale niliwachefua hata wale waliokuwa upande wangu…

    “Umekuwa mzima tena mzee, lakini acha kimbelembele chako mzee wangu.”

    Hayo maneno niliyomwambia yule mzee yalikuwa yakijirudia kichwani kwangu kila baada ya sekunde kadhaa. Nilijisikia vibaya sana.



    “Sasa kama wewe uliyesema unajisikia vibaya, je uliyemwambia? Je, waliosikia?” Sauti iliuliza kichwani kwangu, nikashtuka sana…

    “Aaa, Mungu wangu nisamehe sana,” nilisema nikainamisha kichwa.

    “Unaonekana kuwa katikati, huku kwetu ukiwa hivyo unaweza kupewa adhabu nzito sana,” sauti nene sana iliniambia nikiwa nimekaa kwenye kiti, nikashtuka na kuangaza macho kila mahali,

    hakukuwa na mtu mwingine zaidi yangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kufumba na kufumbua, watu watatu, wanawake wawili, wote wakiwa wamevaa kaniki kwa kujiviringisha kiunoni walisimama mbele yangu, mwanaume akasema:

    “Kuna ahadi ilitolewa na mkubwa wa wachawi kulipa deni la damu kwa wakuu wa uchawi wa nchi jirani, hali ni mbaya sana, wakuu wa wachawi wa nchi jirani wanataka damu yao kwa sababu kwenye stoo yao ya damu hakuna kitu, wanashindwa kuendesha ‘ndege’ zao kwa sababu hiyo.”

    Niliwajua, ni wachawi kwenye kundi ambalo naliongoza.



    “Kwa hiyo?” Niliwauliza.

    “Mkuu wa wachawi wa hapa ametutuma kwako, anasema hauko sawa, ndiyo maana ameshindwa kukwambia wewe mwenyewe, ila amesema damu hii inatakiwa mpaka leo jioni iwe tayari kwani wao wana kikao chao usiku, lazima ataulizwa.”

    Ni kweli sikuwa sawa, na nilijua ile sauti iliyojiuliza na kunionya ilikuwa ya huyo mkubwa wa wachawi wote….

    “Nyiye mliotumwa kwangu mmejipangaje?”

    “Hakuna njia nyingine zaidi ya kupata damu mapema.”

    “Kwa njia gani?”

    “Ni ajali tu.”



    “Mnaweza kutekeleza hilo bila mimi?”

    “Ni vyema mkuu na wewe ukawepo,” walijibu.

    Niliingia chumbani, nikafanyafanya ‘mambo’ yangu, kisha nikatoka na kwenda kusimama wote sebuleni waliponikuta, tukashikana mikono wote, tukainamisha vichwa, tukapotea.

    Tulikwenda kuibukia kwenye barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi, kwenye mteremko mmoja mkubwa, tukasimama katikati ya barabara huku kila mmoja akitumia mguu mmoja, wa pili tuliukunja.

    Mara likatokea basi dogo likiwa na abiria ndani, dereva alikuwa kasi, tukarukaruka kwa kutumia mguu mmoja mmoja, huku tukipunga mikono hewani kama vile tulikuwa tunamtahadharisha dereva asimame asije akatugonga, naye akashtuka sana, akapeleka gari kwenye mtaro pembeni ya barabara, likaanguka.



    Wale wanawake tayari walikuwa na vifaa vya kukingia damu, abiria waliojeruhiwa na kutokwa damu nyingi tulikinga vyombo na kuchukua damu zao huku tukilia kichawi, kama wanyama wa porini.

    Wengine walikatika mikono, wengine miguu, wengine usoni, damu zilikuwa nyingi sana. Hapa nataka kusema kwamba, mara nyingi gari likipata ajali abiria wanaokufa, wengi ni wale ambao damu zao zinakingiwa vyombo na wachawi kwa lengo la kujaza stoo zao za damu, hasa kulipa madeni kwenye makundi ya nje ambapo wachawi hudai sana.

    Lakini pia nataka kusema kuwa, si gari huwa linaanguka, yapo mengine yanashindikana kutokana na nguvu ya abiria walipo ndani.



    “Mfano, kwenye gari kuna watu ni waombaji sana mbele ya Mungu, pia ni wasafi kiroho, basi mara nyingi ni vigumu sana kupindua gari walilopanda kwa sababu nguvu ya Mungu inakuwa inawashikilia katika mhimili wao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini inapotokea gari zima hakuna mwombwaji na wote ni wachafu, ni rahisi sana kulipindua kwa sababu kunakuwa hakuna wa kuwakinga kutokana na kukosa nguvu ya kiroho.

    Kinachotokea baada ya ajali, ni kukusanya damu za watu na kuzitia kwenye kitu ambacho kitaweza kukusanya damu nyingi kwa muda mrefu na kwa wingi.



    Hilo lilifanikiwa kwetu, tulichukua damu nyingi sana na kupeleka kwenye stoo yetu ambapo kuna wachawi walishaandaliwa kwa ajili ya kupeleka sehemu kulipa deni.

    Lakini wakati tunakwenda katika eneo la ajali, niliwaambia watu waachane na tabia ya kuua watoto katika ajali hizo. Yaani kufanya juu chini kuhakikisha watoto wanakuwa salama salmini.

    Hilo lilifanikiwa baada ya kumchagua mchawi mmoja ambaye kazi yake kubwa ilikuwa ni kupaa angani kila ajali inapotokea na kupanua mikono ili kumfanya pepo wa kuua kujua nini kinatakiwa kufanywa kwa wakati ule.



    Kwa hiyo pepo huyo anaposhuka, anakuwa anaangalia waliokingiwa mikono ni akina nani, ndipo anapochagua wa kuua kwa ajali ile.

    Ndiyo maana katika ajali nyingi, utasikia wakisema mtoto mmoja tu ndiye aliyesalimika katika ajali, ujue kuna wachawi ambao walikuwa wakifanya kazi ya kukinga mtoto au watoto ili wasife kwa ajali ile.

    Ukikuta ajali inaua mpaka watoto wadogo tambua kuwa, wachawi wanadaiwa damu nyingi sana kwa hiyo wanajikuta hawana uwezo wa kulipa na waliokopwa wanawakomalia damu yao, ndiyo maana inafika mahali wanaua tu hata bila kujali, hasa kama kwenye gari hilo hakuna mtu mwenye usafi.



    Lakini pia ieleweke kwamba, kuna magari yana kinga ya kichawi, haya ni vigumu sana kuyaangusha kwa sababu ya nguvu yake, lakini sasa kinachofanyika, mara nyingi utasikia dereva na kondakta wake wamekufa katika ajali hiyo.

    Hizi zote ni dalili ambazo nazisema ili ijulikane nini hutokea mpaka ajali zinakuwa nyingi. Mara nyingi mwezi Disemba ndiyo huwa wa wachawi kulipana damu, kwa hiyo ndiyo maana ajali zinakuwa nyingi sana wakati huo kuliko wakati mwingine wowote ule.

    Usiku ulipoingia, wachawi na damu zetu tulizipeleka kwa wachawi waliotumwa kuja kukabidhiwa damu ile. Lakini ilionekana haitoshi na wao wajumbe waliotumwa walikuwa hawakubali kuipokea katika upungufu ule kwani walikotoka waliambiwa endapo wangekwenda bila damu wangeuawa wao.



    Ilibidi tukae kikao cha dharura kwa ajili ya kuangalia ni jinsi gani damu itapatikana usiku huo na wajumbe wakaondoka na damu yao.

    Mzee mmoja alisema kwa usiku huo ni lazima kutembelea barabara ya Morogoro ambayo ina magari mengi nyakati za usiku. Hii barabara ni kuanzia Chalinze hadi makutano ya Samora.

    Tuliwaacha wale wajumbe na wachawi wenzetu wawili, tukatoka wachawi hamsini na tano, hao mpaka eneo la Mlandizi. Pale tulipiga kambi, ilikuwa usiku wa saa sita na nusu, tukasimama katikati ya barabara.



    Lakini wasiwasi wetu ulikuwa kwamba, ni magari mangapi ambayo yangepata ajali ili kupata damu ya kutosheleza deni.

    Ghafla lilitokea lori moja likiwa katika mwendo wa kasi sana, tukasimama katikati ya barabara, lakini kwa mbali sana tukaona basi, nikawaamuru watoke pembeni ili tusubiri basi, lakini lile lori lilipopita tu na lile basi likapotea ghafla kwenye upeo wa macho yetu.

    Tulibaki tumeshangaa, kwani sisi ni wachawi wakubwa, sasa mbona kuna mambo ya kichawi zaidi yetu?

    “Hii ni nini?” Mzee mmoja aliuliza.



    “Kuna kitu,” nilijibu nikiangalia angani.

    Ghafla mmoja wa wale wachawi wawili tuliowaacha kule na wajumbe alikuja kwa kutumia usafiri wa ungo, akatua mbele yetu.

    “Nimekuja kuwapa taarifa, wale wadeni wetu si watu wazuri,” alisema.

    “Kivipi?”

    “Kwa sababu mmoja kaondoka, nikamsikia akisema anawafuata kuwajaribu.”

    “Mh!” Wote tuliguna.

    Tukagundua kuwa, kumbe ule mchezo wa basi na lori ulifanywa na wao, tulikasirika sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa natangaza vita na wenzetu,” nilisema.

    Wachawi walishangilia, lakini hakuna hata mmoja aliyesema ni nini tutafanya ili kupigana vita hivyo.

    “Sasa nani watawashughulikia?” Niliuliza.

    Hakuna aliyenyoosha mkono, hii ilinifanya niamini kuwa, hakuna mchawi aliyekuwa na uwezo wa kupambana na wajumbe wale.

    “Mimi mwenyewe nitasimamia mapambano,” nilisema kwa hasira sasa.

    Tukiwa bado pale pembeni ya barabara, mara lilitokea basi jingine, wachawi wakafurahia na kutaka kwenda kusimama barabarani, lakini niliwakatalia na kuwaambia nitawafafanulia sababu.



    Lilipopita, ndipo nikawaambia kuwa, hakuna basi linalopita muda ule hata siku moja, kama ni kuchelewa, basi ingekuwa basi moja na si zaidi ya hapo.

    Wakati nasema, lile basi kwa mbele lilionekana kukata kona kuingia porini, likapotelea huko huku nyasi sikionekana kulala kuashiria kuwa, zilikuwa zikikanyagwa.



    Mara likatokea basi jingine, safari hii hili lilikuwa likipiga honi mfululizo huku kukisikika kelele kubwa kutoka kwa abiria walioko ndani ya basi.

    Niliwaamuru wachawi nusu wavuke barabara haraka, wengine wabaki na mimi. Kwa maana kwamba, basi litapita katikati yetu.

    Ikawa hivyo, lilikuja na kupita katikati, lakini kabla halijatumaliza, lililipuka!





    “Puuu!”

    Wengi walishtuka sana kwa mshtuko, lakini akili zilipokaa sawa wote wakashangilia…

    “Haya turudini kule,” niliwaamuru huku nikijua tutakuta kitu gani.

    Sisi ni wachawi, kutembea kwetu si kwa kibinadamu, ni suala la kufumba na kufumbua tu tayari tulirudi kwenye kilinge chetu.

    Tulimkuta mchawi mmoja, kwani mmoja alitufuata sisi kule kutupa taarifa.



    Tulimkuta peke yake bila wajumbe wale waliofuata nyama, tulipomuuliza wako wapi, akageuka kuangalia pembeni.

    Watu wawili walikuwa wamelala kwa kujikunja kama vile walikuwa wanasikia baridi sana.

    “Vipi tena?” Nilimuuliza yule mchawi mwenzetu.

    “Sijui, mimi nimeona ghafla wanaanguka hapa, niliposhtuka wakapaa na kutua pale. Lakini sijui chochote kile.”

    “Waliondoka muda gani?”

    “Muda uleule mlipoondoka nyinyi kwenda kuongeza damu, halafu alipoondoka mwenzangu muda kidogo ndo wakatua.”

    Tulikwenda kuwaangalia, kila mmoja mwili uliungua moto, hakuna hata mmoja aliyekuwa na nafuu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walikuwa wakilia huku wakitetemeka kama vile walikuwa wakisikia baridi kali wakati wa majira ya mvua.

    Nilinyoosha mkono na kuwashika wote kwa mpigo:

    “Mmetumwa kumbe?” Niliwauliza kwa sauti ya ujasiri.

    “Ndiyo.”

    “Kufanyaje?”

    “Kuchukua deni la damu.”

    “Sasa kwanini mliingia mambo mengine?”

    “Tuliambiwa tuwapime ili kujua uwezo wenu.”

    “Mlitumwa na nani?”

    “Mkubwa wetu.”



    “Kwani sisi tuna uadui na nyinyi?”

    “Hata sisi wenyewe tulikuwa tunashangaa sana wakati tunapewa maagizo haya.”

    “Simameni,” niliwaamuru, wakasimama wote.

    Kusema ule ukweli walikuwa wameungua sana, licha ya kusimama lakini kwa hali ya kawaida, hakuna hata mmoja aliyetakiwa kusimama, na kama ingekuwa ni binadamu nje ya uchawi, wangekuwa wameshapoteza uhai wao.

    “Tembeeni.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog