Simulizi : Padri Mla Nyama Za Watu
Sehemu Ya Tano (5)
Walitembea, kila mmoja hatua kama mbili, wakaanguka.
Tulijua nini kinakwenda kuwapata, hivyo tuliwaruhusu kichawi kurudi walikotumwa huku sisi tukiandaa namna ya kukabiliana na makombora ya wenzetu kwani tulijua kitendo
tulichowafanyia ni kama tulichokoza nyuki.
Katika vita kama ile, huwa inategemea na uwezo na uzoefu wa kila mchawi, welevu wale ni muda wa kukaa katika kazi ya uchawi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mimi nilijiamini sana si kwa muda mrefu wa kukaa katika kazi ya uchawi, bali kwa ushupavu na uhodari wa kufanya uchawi, ndiyo maana wengi walikuwa wakiniogopa kwa ajili hiyo. Ni
muda mchache sana nimejiingiza katika uchawi lakini tayari nilikuwa kiongozi mkubwa tu na kuweza kupambana na maangamizi.
Tukiwa kwenye eneo letu husika, mimi nilisimama katikati, nikaamuru painuliwe ili nisimame juu kabisa niweze kuongea na kila mchawi.
Wachawi wawili walisogea, wakachota mchanga wa pale niliposimama wakaurusha juu, wakati ukirudi chini wakawa wanaupuliza na ndivyo pale niliposimama palivyokuwa panainuka juu na
kusababisha kichuguu kirefu kidogo huku nikiwa nimesimama juu yake.
Nilipokuwa naanza kuwahutubia nilichotaka, upepo mkali sana ulivuma toka pande zote, yaani mashariki, magharibi, kusini na kaskazini.
Mshtuko zaidi ulitupata pale tulipobaini kwamba, upepo huo uliambatana na joto kali sana, mfanowe hakuna, tena linalounguza.
“Uwiii,”
“Jamani.”
“Mamaweee.”
“Ooo.”
“He!
“Haaa!”
“Jamani tunakufa.”
“Ohooo!”
Hiyo ilikuwa misemo ya baadhi ya wachawi walipokumbwa na ule upepo wenye joto kali sana.
Nilijua tuko katikati ya mapambano makali sana, hakuna kingine zaidi ya kuhakikisha ushindi bado unakuwa wa kwetu licha ya kuvamiwa.
Sauti za magari kama yale mabasi zilisikika, ikawa kama zinapita toka upande mmoja, kwenda pande nyingine huku sauti za abiria zikiwa zinasikika vyema kama vile kila mmoja alikuwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akiongea na abiria na mwenzake.
Nilinyoosha mkono juu ili kuuzuia ule upepo lakini hali ndiyo kwanza ikazidi kuwa mbaya.
Ilifika mahali niliamini kuwa, mwelekeo wa upepo ule ni mbaya kiasi kwamba, lazima mmoja au zaidi yetu wafe ili kutuliza ghasia ile.
Ndipo nilipoamua kukemea kwa sauti kama vile wachungaji wanavyotoa mapepo, lakini pia haikusaidia.
Mchawi mmoja, mwanamke akaanguka chini kama aliyepigwa ngwara na mtu, damu zikamtoka kinywani huku akilia sana na kusema anakufa kwa sababu mbele yake anaona moto mkubwa.
Picha niliyoipata kichwani ni kwamba, mchezo ule hakuwa wa wale wachawi, bali mkono wa Mungu uliingilia kati kwa kutenda maajabu yake huku akionesha ukuu na uwezo.
Ni kweli, yule mwanamke aliyeanguka alinyoosha miguu, akakata roho, lakini tukiwa tunaendelea kufikiria hali ya mwenzetu na umauti wake, ghafla mwingine alianguka chini, huyu ni
mwanaume.
Kishindo cha uangukaji ni kile kile kama cha yule wa awali. Sikuona sababu ya kuwaacha wengine eneo lile. Ilibidi niwaamuru kila mchawi akimbilie kwake na kuhusu wale tuwaache, mambo
mengine yatajulikana kesho yake kama kutakucha salama.
Kweli, wachawi wote wakachangukana kila mmoja na njia yake. Mimi pia nilishika njia yangu mpaka kwenye makazi yangu ya kitumishi, nikaingia chumbani japo kwa njia ya kichawi, nikaoga
ili kulala.
Usingizi haukuchelewa kunipata, lakini nikiwa usingizini niliota ndoto hii:
Eti nilikuwa ndani ya kanisa siku ya ibada ya Jumapili, kiongozi mkuu wa kanisa ambaye anaishi makao makuu alifika ghafla, bila taarifa ya awali kwamba angekuja.
Waumini wakasimama, wakamsalimia huku ibada ikiendelea kwani mimi sikutaka kuacha. Alinyoosha mkono kwangu na kusema:
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Naomba simamisha ibada mara moja.”
Nilisimamisha, nikabaki nimeduwaa nikimkodolea macho ya mshangao.
Akaja hadi madhabahuni, akasimama sambamba na mimi akawageukia waumini.
“Nimekuwa nikisikia mengi sana kuhusu huyu padri. Na kila nilichosika nilikifanyia uchunguzi na kugundua ni kweli. Kwa hiyo sasa, kuanzia leo namsimamisha na kwamba, si mtumishi tena
wa kanisa hili.”
Nilishtuka kutoka usingizini na kukaa huku nikihema sana.
Siku ya ibada Jumapili ilifika nikiwa sina raha, sina amani wala sijisikii kuendesha ibada.
Lakini kwa vile nilikuwa sina mtu wa kusimama badala yangu, nilioga, nikavaa mavazi ya utumishi na kwenda ibadani.
Nakumbuka ilikuwa kwenye kipindi cha nyimbo wakati wa kutoa sadaka, nikiwa nimekaa kwenye kiti na huku kidogo nikiwa na amani kwani baada ya sadaka ibada huwa haichelewi kwisha,
kwa hiyo ndoto yangu ingekuwa ni upuuzi mtupu na si tukio la kweli, nikasikia mlio wa gari likisimama nje.
Waumini wote waligeuka kuangalia mlango mkubwa kama vile kuna mtu walijua anakuja.
Na mimi macho yangu yakiwa mlangoni, ghafla aliingia mkuu wa kanisa letu akiwa ameongozana na watu wengine wawili.
Nilisimama, yeye akaja mbele, wale watu wawili wakakaa kwenye dawati kama waumini wengine.
Nilinyoosha mkono kumpa yule mkuu kama salama, akakataa.
“Sitaki mkono wako, naomba simamisha ibada mara moja.”
Nilisimamisha, nikabaki nimeduwaa nikimkodolea macho ya mshangao.
Akaja hadi madhabahuni, akasimama sambamba na mimi akawageukia waumini.
“Nimekuwa nikisikia mengi sana kuhusu huyu padri. Na kila nilichosika nilikifanyia uchunguzi na kugundua ni kweli. Kwa hiyo sasa, kuanzia leo namsimamisha na kwamba, si mtumishi tena
wa kanisa hili.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilijisikia miguu ikikosa nguvu, nikaanguka. Nilipokuja kuzinduka, nilikuwa hospitalini, pembeni yangu alikuwepo dada yangu kwa mama na baba mmoja, alinipa pole kwa yote.
“Dada,” nilianza kusema.
“Nakusikia kaka.”
“Yaliyotokea yote ni uwezo wa Mungu, ametaka kuniambia kuwa, yeye hachezewi wala hajaribiwi, ni kweli Mungu hataki mtu vuguvugu, kwa hiyo namkiri kwa mara ya tena kwamba yeye
ndiye Muumba wa mbingu na nchini.”
“Ni kweli kaka, lakini we unadhani kwanini umesimamishwa utumishi wa Mungu?”
“Dada, kumbe hufahamu? Da! Nilimtumikia shetani.”
“Kwa njia gani kaka?”
“Njia ya kishetani.”
“Ipi hiyo kaka?”
“Nilikuwa shetani mimi mwenyewe.”“Kaka mimi sijakuelewa.”
“Nilikuwa mchawi dada
“Ha! Kaka.”
“Nimeamua kutubu dada ndiyo maana nimekwambia, naacha kuanzia sasa.
Dada alilia sana, na mimi nikajisikia vibaya, nilinyoosha miguu na mikono…
Padri Akataa roho!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
''Mwisho.''
0 comments:
Post a Comment