IMEANDIKWA NA : STALLONE JOYFULLY
*********************************************************************************
Simulizi : Niliongea Na Shetani Ili Niwe Tajiri
Sehemu Ya Kwanza (1)
wazazi waliniita Bella, shuleni nikajiita Bianka. Nilitunukiwa tunu ya urembo, yaani urembo haswa. Hapo mwanzo nilikuwa nikichukia macho ya wavulana waliokuwa wakinitazama kwa uchu. Ndio, nilifahamu ulikuwa ni uchu, kwa kuwa sikuwa najitambua wala
kupevuka bado. Kioo changu mwenyewe pia sikukiamini kila nilipojitazama. Ni wachache walionifuata na kuniambia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Bella wewe ni mrembo uliyependelewa"
hiyo ndio sababu ya kushinda kwenye kioo na kuutazama
huo uzuri. Muda mwingine nilikaa nikijiuliza "inawezekana
wanataka kunichezea? Huo uzuri uko wapi sasa?"
nilicheka kidogo nikajigeuza geuza, nisione jinamizi lolote
lililofanana na kitu kinachoitwa uzuri.
Nikakiacha kioo na kukirudia kitabu changu. Ndipo
nilisikia sauti ya mama, akiniita kutoka nyuma ya mlango
wa chumbani nilioufunga. Kumbe mama alikwisha gonga
sana mlango ila mimi sikusikia. Kitabu kilichoitwa KIVULI
CHEUSI kiliuteka ufahamu wangu. Nilipenda sana simulizi
za huyu kijana mwenye njaa, hata anaandika vitu
vinavyogusa na kusisimua, Stallone joyfully. Niliendelea
kusoma kitabu nikidhani huenda labda akiwa ananihitaji
sana ataendelea kuniita mara ya pili. Aliita mara ya tatu
ndipo na mimi nikaupata ulimi wangu.
"bee mama"
Nilinyanyuka na kwenda kuufungua mlango.
Nilipoufungua, na kuutoa uso wangu. Nilikutana na uso
wa mama ulioghafirika. Mama aliniangalia kwa dharau
kabla ya kusonya. Sikujali kwa kuwa nilikwishamzoea.
Mama yangu, alikuwa ni mama mwenye mashushu na
ngebe za hapa na pale. Kwa mtu usiye mzoea utashangaa
na roho yako. Aliingia ndani moja kwa moja na kwenda
kukaa kwenye kitanda changu. Kama kawaida yake
alianza kuniambia.
"mwanamke mchafu wewe!" Nilicheka tu sikuongea
chochote. Nilipokuwa nafunga mlango nikimfuata alipo,
aliniambia. "yaani embu tazama kitanda kilivyo" aliinua
ipod yangu, akakiinua kitabu nilichokuwa nasoma
akairudia sauti yake "..yaani hata hakieleweki"
Niliendelea kunyamaza nikitabasamu. Nilijua tu kuna
jambo analotaka kunieleza, hivyo sikuwa na haraka
niliendelea kumsubiri. Alianza.
"mwanangu umekuwa"
alikuwa akinisahili kuanzia juu mpaka chini, akanifanya na
mimi nianze kujitazama.
"miaka kumi na sita si midogo haswa uzuri ulio nao"
nilishituka niliposikia neno hilo kutoka kwa mama, pia
sikujibu kitu. Kisha aliendelea "mwanangu kuna jambo la
muhimu nataka kukueleza ili ulifahamu kabla sijafa"
"kufa!?" niliropoka kimoyomoyo. kiukweli mama
alinichanganya sana, sikujuwa alikuwa na maana gani.
Sikuweza kuongea chochote kwa kuwa sikuwa na lolote la
kumwambia au kumuuliza. Nilihisi machozi yalitaka
kunitoka. Lakini sikujuwa sababu ya mimi kutaka kulia.
Nilimpenda sana mama yangu. "Ndiyo", nilikuwa na baba
ila mama yangu ndiye alikuwa rafiki yangu wa karibu.
Baba hakunijali kama alivyonijali mama. Nilikaa
nikimsikiliza kwa makini alichotaka kuniambia. Aliniambia
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"mwanangu, usikubali hata siku moja kuwa mchawi. Babu
yako alinilazimisha kunirithisha mikoba yake, nikakataa.
Amedai kuwa mizimu imekupenda. Yupo katika harakati
za kuniua kwa sababu ya kumpinga wewe kuwa mchawi"
Niliumizwa sana na taarifa hiyo. Mama alikuwa akiongea
huku machozi yakimtoka.
Nilimbembeleza mama huku nikimuhakikishia kuwa siwezi
kuwa mchawi.
Mama aliniambia.
"mwanangu muheshimu sana huyu mzee unayeishi naye"
nikamuuliza "mzee? Mzee yupi!?"
Sikuweza kutambua kama alikuwa akimzungumzia baba.
Aliniambia
"Mzee Nyegezi, si baba yako, Bella. Ni mwanaume
aliyeyaokoa maisha yangu baada ya mume wangu wa
kwanza kutolewa kafara na babu yako"
Nililia sana. Nililia kwa uchungu kwa sababu sikujua
kama, babu yangu angekuwa na roho ya kinyama kiasi
kile. Amuuwe mwanaye kwa sababu ya uchawi? Kafara?
Kwa faida gani? Unyama ulioje? Nilimchukia babu kwa
kuninyima haki ya kumjua baba yangu na mimi kulelewa
na baba wa kambo.
Mama aliniambia
"mwanangu, mzee Nyegezi atakulea vyema kama baba
yako mzazi. Nina uhakika sina siku saba zaidi duniani,
lakini nitakapokufa usisahau kusoma kwa bidii na
usikubali kuwa mchawi" Mama alinyanyuka na kuondoka.
Nilichokuwa nikisoma kikatumbukia nyongo hata wimbo
wa Ben Paul haukuwa mtamu kama nilivyokuwa
nikiupenda siku zote. Niliitupa ipod yangu mbali na
nilipolala, nikapitiwa na usingizi ulioletwa na kulia sana
.............................
Niliamshwa na upepo mkali uliovuma chumbani kwangu.
Upepo niliodhani huenda ungeezua hata paa la nyumba
yetu. Muda mwingine nilihisi kitanda nilichokilalia, kama
kilikuwa kinabebwa. lakini hiyo ilitokana na nguvu ya
upepo. Nilipotaka kupiga kelele za kuomba msaada,
nilijifahamu kuwa napiga kelele kwa sauti ya juu, lakini
sauti yangu mwenyewe sikuisikia. Jasho jingi likanitoka.
Macho yakanitoka pima kwa uoga. Ile hali ilipotulia,
nilitaka kunyanyuka; lakini sikuweza kusogeza hata
kidole. Nikasikia sauti ya kicheko, kikicheka kwa dharau.
Kicheko kilikuwa ni kicheko cha sauti ya juu sana.
Nikaangalia mlangoni labda alikuwa ni mama, lakini
hakukuwa na mtu. Machozi yalinitoka kwa uoga. Sauti ile
ikacheka zaidi na kujirudia rudia kama mwangwi katika
chumba changu. Hatimaye nikauona moshi mweusi
ukitanda kutoka katika paa na kushuka mpaka usawa wa
kitanda. Mbele yangu akasimama mwanaume ambaye
sikumfahamu kabisa. Alikuwa amejifunga sanda nyeupe
na kuonekana macho na pua. Puani aliwekwa pamba,
mdomo ulikuwa hauonekani. Aliongea na mimi kwa sauti
iliyokuwa ikijirudia rudia.
"Bella lazima urithi lazima urithi mikoba"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kisha alisonya, sonyo lililonifanya nipige kelele kwa nguvu
mpaka niliamka. Kumbe nilikuwa nimelala. Nilijikuta
nikiwa mapajani kwa mama akinifuta jasho lililolowesha
gauni yake aliyovaa. Aliniuliza "babu yako alikuwa
anasemaje"
nilishituka, kwa kuwa nilijua fika nilikuwa ndotoni. Sasa
mama alijuaje? Nilihisi huenda mama alimuona babu.
Nikamuuliza "mama umejuaje kama ni babu na mimi
nilikuwa naota?"
mama alinicheka kama niliyekuwa nikichekesha.
Aliniangalia baada ya kusikitika na kuniambia.
"mwanangu nafahamu yote"
"unafahamu!?" nilishangaa
"ndiyo" akanijibu
"unafahamu nini?" nilimuuliza huku nikiwa ninakaa kitako
kumsikiliza.
Aliniambia kuwa alipokuja kuniamsha ili nikale chakula
cha usiku, aliniona nikiweweseka. Akaja na kukipakata
kichwa changu huku akiniombea. Ndipo akaisikia sauti ya
babu ikiniambia "lazima niirithi mikoba" Aliisikia sauti ya
babu katika ulimwengu wa roho. Nililia sana, huku
nikimwambia mama kuwa sitaki kuwa mchawi. Mama
alitabasamu na kuniambia
"nakuombea Bella msimamo wako uwe hivyo hivyo"
tulienda sebuleni kupata chakula cha usiku, kabla ya
kulala tena mpaka kesho siku nyingine mpya. Baada ya
kumaliza kula, nilimuomba mama aniombee kabla ya
kwenda kulala. Tuliomba kwa muda mrefu sana. Mama
alivunja nguvu za giza zote na uchawi wa babu yangu.
Wakati nikiwa nimefumba macho, nilishituka kuhisi mama
amenyamza ghafla. Nilipofungua jicho langu moja kwa
kuibia, nilimuona mama kaanguka chini. Niliogopa. Mama
alikuwa anatoa mapovu mdomoni na akigalagala pale
chini kama mwenye degedege. Nilimuita baba, Mzee
Nyegezi. Alikuja na tukasaidiana kumpeleka hospitali.
Ulikuwa ni usiku mkubwa, hivyo ilikuwa rahisi kwetu
kufika mapema na kupewa matibabu haraka. Baada ya
daktari kumchukua na kuanza kumshughulikia mama,
zilipita dakika 30 mpaka alipotoka.
"anaendeleaje!" baba alimuuliza
"nifuateni ofisini" Tulimfuata ofisini huku tukiwa na
asilimia chache za mama kuwa mzima. Niliogopa sana.
Tukiwa katika chumba cha daktari. Mimi jasho jingi
lilikuwa likinitoka. Kiukweli sikuwa tayari kupokea habari
za msiba wa mama. Baada ya daktari kumaliza kuandika
vitu fulani katika kadi kadhaa zilizotapakaa katika meza
yake, aliinua uso wake baada ya kikohozi kifupi kumpitia.
"poleni sana" alisema
mapigo ya moyo yalinilipuka na kwenda kasi sana.
Yalienda mara tatu zaidi ya kasi ya kawaida. Nilihisi
machozi yakianza kustahimili uvumilivu wake na kutaka
kuniponyoka. Daktari aliendelea "ndugu yenu, amepatwa
na homa kali sana lakini ni mzima. Tumemuwekea dripu
ya dawa hivyo kesho asubuhi muje kumtazama
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
anaendeleaje. ila kama mngechelewa? Angekuwa katika
hali mbaya zaidi ama mngempoteza kabisa" daktari
akaturuhusu kuondoka. Kiukweli niliona kama muujiza
mama kupona. Moyo wangu ukiwa na amani sasa na
furaha. Tulikuwa njiani tukirudi nyumbani mimi na baba
ndipo tulimuona mtu kasimama kando ya barabara.
Alitupungia mkono. Baba alisimamisha gari na kumpa lift
yule mtu. Baada ya kuingia ndani ya gari, alitusalimu.
Baba aliendelea kuendesha gari kwa mwendo wa
kawaida. Yule mtu tuliyempakia alikuwa mwanaume.
Alikuwa muongeaji sana. Muongeaji mzuri aliyeleta
mazungumzo ya hapa na pale
"poleni na mgonjwa" Ghafla alituambia. Nilishituka sana.
Nilishituka kwa kuwa hakuna ambaye alimwambia wapi
tumetoka. Mimi sikuzungumza chochote, lakini kwa
mshituko mkubwa, baba alisimamisha gari ghafla na
kumuuliza
"wewe umejuaje?" yule mtu tuliyempakia alijichekelesha
bila sababu na kutuambia.
"sikiliza mzee Nyegezi" moyo ukanilipuka kama ulitaka
kunyofoka kifuani. "amelijuaje pia jina la baba?" likawa
swali kichwani kwangu; lililokosa majibu. Nilibaki
nikimsikiliza. Baba naye alimsikiliza macho yakimtoka
kwa bumbuwazi.
"nafahamu kila kitu kuhusu mama yake Bella" alinyamaza
huku akiniangalia mimi siti za nyuma nilipokuwa nimekaa.
"ubishi wake unamponza ubishi utampokonya maisha
yake anayoyaringia ubishi unaweza kumletea matatizo
makubwa katika kizazi chake na Bella" moyo wangu
ulinienda mbio sana mwili ulininyong'onyea nikapoteza
nguvu. Nilifikiri sana mtu huyu wa ajabu, alitujua vipi na
kufahamu fika siri za familia yetu. Kicheko kikamlipuka na
kurudia rudia kama mwangwi, kisha alisonya kabla ya
kutoweka na kutuachia moshi mzito mweusi ndani ya
gari. Sikujuwa nilifikaje nje ya gari, wala sikukumbuka
kilichotokea. Nilijikuta katikati ya barabara nikikimbia
kuliko kawaida. Mara chache nilistahimili kujikwaa
nilipokuwa nikifanya uzembe wa kutazama nyuma, ndipo
nilimuona baba naye akinijia mbio. Aliniita baada ya
pumzi kumuishia akiwa amechoka hoi. Nilisimama na
kurudi alipo
"baba gari tumeiacha wapi..." sikujuwa tulikimbia umbali
gani hivyo hata gari sikuiona. Baba alikuwa amechoka
haswa, ilimbidi akae chini.
"gari.. Gari ipo... ipo.. Kule" alikuwa amegeuka na
kunionyesha tulipokuwa tumetoka, ndipo gari ilikuwepo.
Baba akanishauri tupumzike kwanza. Baada ya dakika
chache tulirudi nyuma lilipo gari. Milango ilikuwa wazi na
taa zikimulika huku likiwa limewashwa "hukuzima?"
nilimuuliza. "wewe unajitambua ulitoka vipi"
Tulicheka kwa pamoja na kuingia ndani ya gari,
tukaondoka kurudi nyumbani. Safari ilikuwa fupi tuliongea
mengi ya hapa na pale tukicheka pamoja. Nilipokuwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nikiingia chumbani kwangu, baada ya kufika nyumbani;
baba alinishika mkono na kuniambia.
"Hivi bella unafahamu wewe ni binti mrembo sana?"
Baba alinishangaza sana. Sawa nilishaambiwa hata na
mama, nilianza kuuhisi urembo wangu pale nilipokuwa
nikicheka mbele ya kioo na pia rafiki zangu walinihusudu
sana na kutamani wangekuwa kama mimi. Iweje baba
anishike matiti yangu na kunitomasa kiuno changu? Hapo
ndipo nilipoipata ile nguvu ya kuuputa mkono wake na
kuutoa kiunoni mwangu.
"baba nakuheshimu kama baba yangu"
neno hilo likaniponyoka. Nilishuhudia mshangao wa
kuigiza katika uso wa Mzee Nyegezi. Sikujali niligeuka na
kutaka kuingia zangu chumbani. Alinishika tena mkono na
kuniambia
"hivi kama mama yako ameshakuambia, mimi si baba
yako mzazi; huoni kama hakuna kinachotuzuia sisi kuwa
wapenzi?" Alikuwa akicheka cheka kicheko kilichouudhi.
Alinisogelea na kuanza kunitomasa tomasa na mdomo
wake kuanza kuunganisha na papi zangu akiwa na nia ya
kutaka tubadilishane mate. Nilirudi nyuma baada ya
kumzaba kibao na kumuacha akiugulia maumivu na mimi
niliingia ndani haraka. Niliufunga mlango kwa ufunguo
nikimuacha nje akiropoka ropoka "mshenzi wewe huna
adabu nimekulea mimi siku zote leo unanivunjia adabu
mimi? Unanipiga kibao? Nitakuonesha mwanaizaya wewe"
alipotelea chumbani kwake huku akiendelea kubwatuka
"Baba nakuheshimu kama baba yangu"
neno hilo likaniponyoka. Nilishuhudia mshangao wa
kuigiza katika uso wa Mzee Nyegezi. Sikujali niligeuka na
kutaka kuingia zangu chumbani. Alinishika tena mkono na
kuniambia
"hivi kama mama yako ameshakuambia, mimi si baba
yako mzazi; huoni kama hakuna kinachotuzuia sisi kuwa
wapenzi?" Alikuwa akicheka cheka kicheko kilichouudhi.
Alinisogelea na kuanza kunitomasa tomasa na mdomo
wake kuanza kuunganisha na papi zangu akiwa na nia ya
kutaka tubadilishane mate. Nilirudi nyuma baada ya
kumzaba kibao na kumuacha akiugulia maumivu na mimi
niliingia ndani haraka. Niliufunga mlango kwa ufunguo
nikimuacha nje akiropoka ropoka "mshenzi wewe huna
adabu nimekulea mimi siku zote leo unanivunjia adabu
mimi? Unanipiga kibao? Nitakuonesha mwanaizaya wewe"
alipotelea chumbani kwake huku akiendelea kubwatuka
___________
Niliamka asubuhi na mapema kwenda hospitali. Sikuona
umuhimu tena wa kumsubiri baba ikiwa ameanza
kunivunjia heshima. Amenivunjia heshima ya kunitaka
kimapenzi. Nilipanda daladala, kwa mwendo mrefu
ulioongezwa na msongamano, lakini nilifika. Mama
alikuwa ameamka, amekaa katika kitanda alicholazwa.
Baada ya salamu aliniuliza kiuchovu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"baba yako yuko wapi!?" sikumjibu. Sikujuwa cha kumjibu,
kwa kuwa sikutaka mama atambue yaliyotokea jana
usiku. Nilimpa uji niliotayarisha asubuhi. Aliunywa vibakuli
viwili na kutosheka. Aliniuliza tena. "ina maana baba yako
hajui kuwa nipo hospitali?"
nilimjibu "atakuja baadaye mama. Huenda yupo njiani"
mama akaniuliza tena "babu yako jana ulimuona tena?"
Nilimuhadithia yote kuanzia yule mtu aliyepewa lift na
baba na yote yaliyotokea na kutuambia kuhusu yeye
kukataa mimi kurithi mikoba ya babu. Mama naye
akaniambia
"jana usiku hospitali nzima iliona cha moto. Hapa
yenyewe leo nimelazimika kupewa discharge kutokana na
mauzauza yaliyokuwa yanatokea jana, yaani ni makubwa"
mama akaanza kunihadithia "Mwanangu jana wakati babu
yako anakuja alianza kuja katika umbile la mnyama" Mimi
mwili ulinisisimka na vinyweleo kunisimama. Ni nani
ambaye asingeogopa kusikia binadamu kawa paka?
Binadamu kuwa mnyama? Ni jambo la kushangaza.
Mama aliendelea "muuguzi mmoja aliyekuwa
akinihudumia alimpiga teke yule paka mwenye rangi ya
kijivu. Mimi sikuwa na habari kama yule alikuwa babu
yako. Alipomaliza kunifunga dripu ghafla alianza
kulalamika maumivu ya mguu. mguu ukazaa kichwa.
kichwa kichwa, kikazaa mauti ya ghafla" mama
alinyamaza kuruhusu pumzi ya kumeza mate. Mimi
nikabwatuka
"akafa? Mbona ghafla? Ilikuwaje?" mama alicheka
akaniambia
"mwanangu uchawi upo na una nguvu sana usipokuwa
mcha mungu. Nakumbuka yule muuguzi niliyemtambua
kwa jina la Rebecca wakati anampiga teke yule paka
aliropoka jambo" mimi nilikosa ustahimilivu, nikaropoka
tena "alisema nini?"
mama alitabasamu tena na kuniambia "usiwe na haraka
Bella ni hivi alisema 'hawa paka wengine ni wanga' Mimi
sikutilia maanani kwa kuwa nilimchukulia yule paka kama
mtu wa kawaida. Mara nilishangaa hospitali nzima ilijaa
paka wa kila aina. Madaktari na wagonjwa wenye nafuu
walijaribu kuwafukuza, lakini hawakufanikiwa. Paka hao
walikwishawauwa wagonjwa wawili na daktari mmoja.
Wale waliokuwa wanapambana na wale paka walikimbia
hovyo na wengine kuvunjika miguu. Kuna wengine
walionusuru roho zao. Lakini kati ya wale paka alijitokeza
paka wa kijivu yule aliyemuuwa muuguzi Rebecca na
kusimama karibu na kitanda changu" mimi macho
yakanitoka pima, nikamuuliza mama "sasa ulifanyaje"
mama aliendelea "nywele zilinisimama kama nimepigwa
na shoti ya umeme basi yule paka alijigeuza na kuwa
katika umbile la binadamu mbele yangu. niliogopa sana.
nilimsihi kwa machozi tele asinidhuru wala kuitoa roho
yangu. alikuwa ni babu yako Mzee Matonde. alicheka
sana na kuniambia, 'sijaja Kuitoa roho yako wala
kukudhuru. hili ni onyo la mwisho acha kumkataza Bella
kuirithi mikoba yangu'. kisha alinikumbusha ni jinsi gani
alivyoila nyama ya mwanaye wa kiume ambaye ni baba
yako. Pia kilikuwa ni kifo cha ghafla cha kuanguka bafuni.
Baba yako aliumia mguu tu. Mguu ukaoza ukaanza kutoa
harufu kali ya uvundo uliokera. Tukaliuza shamba la
mihogo, alipe pesa ya kitanda cha hospitali, pesa
hazikutosha. Akanishauri na kuniambia nisiliuze lile la
michikichi na fenesi kwa kuwa alishajua.
"umejua?" nilimuuliza mume wangu "umejua nini?" "baba
anataka kuniua"alipumzika baada ya kumeza donge zito
la uchungu. Chozi likamponyoka, likanyang'anya furaha
yake "najua atamsumbua mwanangu Bella lakini
nakuomba sana usiache kumuongoza mtoto wetu katika
maombi" mume wangu hakusubiri hata nimfute chozi kwa
kiganja changu wala hata hakutaka kuniaga, aliondoka
kimya kimya. Ukimya ulioniumiza na kunifanya nilie sana
na kusimama na msimamo wa kukataa kurithi mikoba ya
babu yako. Mzee Matonde alikuja siku moja nikiwa Eda
aliniambia kuwa 'nyama ya Jose tamu sana' nililia kwa
uchungu lakini sikuwa na la kumjibu. Alitokomea
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alikokujua akicheka kifedhuli. Baada ya miaka mingi ndiyo
akarudi tena, aliniambia asingeshindwa kuitafuna mifupa
yangu kama nitaingilia harakati zake kama nilivyoingilia
kwa baba yako na kumsababishia kifo mume wangu.
Wakati Mzee Matonde anajaribu kunitisha, wale paka
waliyekuja na babu yako walitokezea na maiti za watoto
wadogo ambao walizaliwa kabla ya siku zao. sikujua nia
na madhumuni ya kuzichukua maiti zile. Babu yako alirudi
katika umbile la paka na kutoweka machoni mwangu
katika hali ya kufumba na kufumbua" wakati mama
anamaliza kunihadithia yaliyotukia jana, baba aliingia
akiwa na tabasamu la kuudhi. Mimi sikumjali akili yangu
ikawa imezama katika hadithi hiyo ya kusisimua hadithi
iliyonitingisha moyo wangu na kuanza kuogopa.
"Bella kumbe upo huku"
"niliamua kuwahi kumletea mama uji" nilimjibu kwa
karaha, kisha nilitoka nje. Baada ya muda mfupi naye
alitoka na kunieleza
"nimefurahi kwa kuwa, umenionesha umeanza kukuwa.
Hukumueleza kabisa kuhusu yaliyotokea jana? inabidi
nikupatie zawadi" sikumjibu. Japo yeye alicheka, mimi
nilinuna. Alielekea ofisini kwa daktari kulipia gharama za
matibabu ya mama, kisha tuliruhusiwa kurudi nyumbani.
mama alitakiwa apate muda mwingi wa mapumziko na
azimalize dawa zake za kunywa zitakazomsaidia
kuongeza damu, kutokana na upungufu wa damu alio
nao. Tulirudi nyumbani nikiwa na furaha ya mama kupata
nafuu. Mama alionekana akiwa na huzuni, mzee nyegezi
akiwa amepambwa na tabasamu la kishetani usoni
mwake.
Siku zikapita mpaka afya ya mama ilipotengemaa. Mimi
sikuona mauzauza yoyote tangu siku ile, mpaka leo siku
ya nane. Nilimuuliza mama "mama au babu kaamua
kutusamehe"
"we Bella omba Mungu tu mwanangu" mama aliamua
kunijibu kiuchovu. Nilicheka kicheko kisicho na ladha ya
kicheko. Nilimwambia tena mama "ameshindwa bwana na
madude yake. Mbona haji tena?" Mama akanikatiza "Bella
hufahamu wanapanga nini juu yetu.... Funga mdomo
wako" Nilinyamaza huku nikiwa na hakika babu hatokuja
tena. Hali ilikuwa shwari na siku saba alizozisema mama,
kuwa anaweza asifike basi zilipita. Nilifurahishwa na hali
hiyo na tuliishi kwa amani. Amani ya kutosumbuliwa na
babu lakini usisahau, Mzee Nyegezi hakuacha
kunisumbua. Alipopata upenyo wa kumtoroka mama
chumbani alinijia chumbani kwangu na kunitomasa
tomasa kimahaba. Nilipomtishia kupiga kelele, alikurupuka
kutoka chumbani kwangu na kurudi chumbani kwao. Siku
moja alipokuja chumbani kwangu mauzauza yakaibuka
tena haya yalichachamaa zaidi.
Baba aliingia kwa mwendo wake ule ule wa kuninyatia.
Hakutumia muda mwingi wala umbali mrefu kunifikia.
Alizipiga zile hatua ndefu ndefu zisizotoa sauti. Mimi
nilikuwa nimelala fofofo, hivyo sikusikia. Alipotaka kuitoa
khanga mwilini mwangu, nami nilishituka. Nilimuona baba
akiwa uchi wa mnyama. Alikuwa anatabasamu, tabasamu
la dharau. Nilipotaka kupiga kelele yeye alicheka kwa
nguvu alininong'oneza jambo
"mama yako ameifakamia wine niliyoweka madawa ya
kulevya. Utadhani hakuwahi kunywa wine tangu
amezaliwa?" alinicheka kwa kejeli. kisha aliongeza sauti
ya kicheko huku akibinya binya matiti yangu. wakati
akiendelea na mchezo huo mchafu ndipo niliusikia upepo
mkali uliovuma kwa nguvu. ulikuwa ni upepo mkali sana.
sauti ya kicheko cha dhihaka kikasikika kati kati ya
kicheko hicho. nilifahamu alikuwa ni babu. baba
alijidumbukiza ndani ya shuka kuificha aibu yake. alikuwa
anatetemeka sana. mimi nilijibanza ukutani pia nikiogopa
ile hali. mara mbele yetu akatokea joka kubwa lenye
vichwa viwili. alikuwa ni nyoka mwenye mabawa. siwezi
kusimulia kwa urahisi ni kiasi gani niliogopa lakini
nilishangaa kumuona Mzee Nyegezi amepoteza fahamu.
yule nyoka alizungumza
"nitakulinda siku zote. popote uendapo"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nilishajikojolea kwa uoga. Nilitetemeka haswa. yule nyoka
aliufahamu uwoga wangu aliniambia
"usiogope. mkuu wa ulimwengu huu amekuchagua"
kisha kama alivyokuja, aliondoka vile vile. Upepo wa kisuli
suli uliingia chumbani kwangu na kulimeza lile joka. Mimi
pia nilizimia kanga ikiwa mbali nami. Nguo ya ndani
ilisitiri maungo yangu huku mkono wa baba ukiwa kifuani
kwangu.
.........
sikumbuki nilipoteza fahamu kwa muda gani, ila
nilishituka kipindi ambacho kulikuwa kumeshakuchwa.
Baba bado alikuwa amelala pembeni yangu. Nilikuwa
nikiugulia maumivu ya kichwa. Maumivu ambayo,
yaliyogonga kama niliyetaka kuzimia tena au nilipigwa na
kitu kizito. Nilikumbuka usiku uliotisha. Usiku wa joka
kubwa lenye mabawa. Upepo wa kisuli suli ukalibeba lile
joka na kupotelea hewani. Hakika ilikuwa ni hali ya
kumfanya yeyote kuzimia. Ndiyo hapo niliona kitu cha
kushangaza mbele yangu. Mwili wa mama ukiwa
umekumbatia sakafu. Mama alikuwa amedondoka karibu
na mlango wa chumbani kwangu. Akiwa ameyalalia
mapovu yaliyomtoka mdomoni. Kiukweli nilishituka sana.
Sikujua nianze vipi kumsaidia mama ikiwa Mzee Nyegezi
naye alikuwa hajiwezi. Nilitoka nje, nikarudi ndani.
Nilipanda kitandani mara nikashuka. Nilimuita mama
lakini hakusikia. Nilimuinamia kwenye kifua chake na
kuyasikiliza mapigo yake ya moyo niliyasikia yakidunda
kwa mbali sana. Nikapata uhakika kuwa bado alikuwa
hai. Nilivaa nguo zangu haraka haraka. Nikafungua droo
katika kabati yangu kutazama kiasi cha pesa nilichokuwa
nacho. "shilingi elfu thelathini' zinatosha," nilijiambia.
Nilitoka mpaka eneo la hifadhi ya barabara, nilienda
kuchukua tax. Tax haikuchelewa, tulirudi nyumbani na
yule mzee ambaye alikuwa dereva, ndiye alinisaidia
kumbeba mama na kumuingiza ndani ya gari. Nilikuwa
nimechanganyikiwa sana. Nilichanganyikiwa baada ya
kufahamu kuwa, mama alipata mshituko wa kutuona mimi
na Mzee Nyegezi, tukiwa tumelala pamoja. Mzee Nyegezi
alikuwa kama alivyozaliwa, mimi nikiwa sina chochote
kifuani na nguo ya ndani pekee ilihifadhi maungo yangu.
Sikutaka niwe sababu ya kifo cha mama yangu. Sikutaka
kumuumiza mama. Wala sikutaka mama atoe chozi kwa
sababu yangu. Nilidondosha chozi nilipokuwa katika
kuwaza.
Yule dereva aliniuliza. "binti kuna nini?"
"acha tu mzee, naomba unipeleke lugalo"
"itakuwa elfu kumi"
"nimekuambia nipeleke Lugalo hospitali" Nilimjibu kwa
karaha. Sikujali kuhusu pesa, nilijali mama afike mapema
hospitali; apate matibabu. Nilikuwa nikimpepea mama
aliyelalia mapaja yangu, huku nikilia kwa uchungu. Nililia
huku nikimlaani mzee Nyegezi kwa tamaa zake. Mwendo
wa tax ulikuwa ukiridhisha. Mzee yule aliikimbiza tax
huku akipiga honi za hapa na pale. Japo alikuwa
akiendesha kwa kasi kama uwajuavyo madereva tax,
hakuacha kunisumbua kuniuliza hili na lile. Aliniuliza "na
Yule mwanaume aliyelala uchi pale kitandani ni nani?"
nilitamani nimtukane, ila nilimuheshimu. Sikumjibu kitu
niliendelea kuomba Mungu mama awe mzima. Foleni
ilimpisha na yeye kupita bila matatizo. Punde si punde
tulifika eneo la hospitali. Machela ikakimbizwa na
kumbeba mama. Mimi nilimlipa Yule babu na kumfuata
mama alipokuwa akipelekwa. Nilipofika katika wodi flani
ambayo sikuitambua kwa haraka nilisimamishwa.
"tafadhali naomba usubiri hapo nje" Muuguzi mmoja
alisema na mama kuingizwa sehemu fulani hivi na
kufunika pazia la kijani. Nilibaki nikiwa nimesimama.
Nilizunguka kila sehemu. Kulia nilitaka, maombi nikaona
yalichelewa. Kila muuguzi alipotoka katika chumba
alichoingizwa mama, mimi nilitoka mbio kumfuata.
"naomba unijuze hali ya mama"
"tafadhali kuwa na amani, amepata mshituko wa kawaida
yupo sawa" nilikaa kwenye benchi iliyopo katika baraza la
hospitali. Daktari aliyekuwa akimuhudumia mama, alitoka
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akaniambia "wewe ndiye mwenye mgonjwa hapa?"
"ndiyo"
"nifuate ofisini" Nilimfuata ofisini nikiwa katika hali ya
uoga sana. Sikujuwa nini alikuwa anaenda kuniambia,
lakini sikupenda kupokea jibu lolote baya. Nilipoingia
baada ya kukaa, aliniambia. "ilikuwaje huyu mama
akafikia katika hali hii?"
"nahisi alipoteza fahamu baada ya kupata mshituko,
Daktari"
"hilo ndiyo jambo baya lililomkuta" Nilishituka sana
daktari aliposema hivyo. Nilianza kulia sikujua daktari
alimaanisha nini. Yeye alininyamazisha na kunieleza yote
sasa.
"sasa unalia nini? Nimeshakueleza tatizo kwani?"
Alinyamaza akavuta pumzi baada ya kumeza mate na
kuniambia. "huyu mwanamke hana tatizo lolote la
kimuonekano, ila ubongo wake umecheza na kusababisha
kumpotezea kumbukumbu mara kwa mara hivyo watu wa
karibu inabidi muizuie hali ya yeye kudondoka dondoka
kila mara"
"sawa dokta, ninaweza kumuona?"
"bila shaka"
Nilienda katika chumba ambacho daktari alinielekeza.
Chumba ambacho mama alikuwa amewekwa kama
mapumziko. Nilipomtazama mama, machozi yalikuwa
yakinitoka tu bila sababu. Nilijisikia vibaya sana kwa hali
aliyotukuta nayo na Mzee Nyegezi. Nilimsalimu na
alionesha kunikumbuka. "marahaba Bella"
Lakini hakuwa amechangamka wala hakuwa na furaha.
Niliona chozi likimponyoka na kushuka mpaka kwenye
mashavu yake. Nilmsogelea na kumwambia "mama
naomba nikueleze" akaniambia "huna haja ya kunieleza
lolote Bella inatosha"
"mama sivyo kama unavyofikiria mama" Nilimsihi
anisikilize, nilimuhadithia kila jambo lilivyokuwa mpaka
mimi na Mzee Nyegezi kuwa katika hali aliyotukuta nayo
asubuhi. Aliniambia "kwanini hukunieleza mapema?"
"niliogopa wewe ungegombana na baba"
mama hakuongea chochote mimi nilitoka katika kile
chumba na kwenda kwa daktari. Nililipa kila gharama za
uuguzi wa mama yangu na kuambiwa kuwa nimuache
kwanza mpaka mchana ndiyo nitaweza kuondoka naye.
Mama alitundukiwa dripu ya maji. Mimi nilirudi nyumbani.
Sikumkuta mzee Nyegezi katika chumba changu tena.
Nikatoka na kwenda jikoni. Ndipo nikasikia hatua za mtu
akinyata niliposimama, akaniziba mdomo.
"mama sivyo kama unavyofikiria mama" Nilimsihi anisikilize, nilimuhadithia
kila jambo lilivyokuwa mpaka mimi na Mzee Nyegezi kuwa katika hali
aliyotukuta nayo asubuhi. Aliniambia "kwanini hukunieleza mapema?"
"niliogopa wewe ungegombana na baba"
mama hakuongea chochote mimi nilitoka katika kile chumba na kwenda kwa
daktari. Nililipa kila gharama za uuguzi wa mama yangu na kuambiwa kuwa
nimuache kwanza mpaka mchana ndiyo nitaweza kuondoka naye. Mama
alitundukiwa dripu ya maji. Mimi nilirudi nyumbani. Sikumkuta mzee Nyegezi
katika chumba changu tena. Nikatoka na kwenda jikoni. Ndipo nikasikia hatua
za mtu akinyata niliposimama, akaniziba mdomo.
****
Nilijitahidi kujinasua, lakini mikono ya mwanaume huyo ilinishinda nguvu.
Ilikuwa imejaa misuli, hakika alikuwa na nguvu za kutosha. Punde si punde
nilianza kulegea. Macho yakakosa nguvu nikawa nimepoteza fahamu. Nilipoamka
nilijikuta nina hali ya tofauti hali ya utatanishi juu ya mapaja yangu.
"damu" damu zilikuwa zimetapaaka kwenye mapaja yangu na kiuno kilivuta
haswa. Kengele ya hatari ikagonga kichani kwangu. "bikra yangu" imetoka?
Nilijiuliza kwa huzuni. Bikra yangu imetoka bila kuridhika kuitoa kwa yule
ampendaye. Nilishamuahidi mpenzi wangu Jordan kuwa, yeye ndiye atakuwa wa
kwanza kuuona usichana wangu. Sasa sikuwa nao tena. Atanielewa vipi
nikimueleza ukweli kuwa nimebakwa? "mama!"
Nikakumbuka nilimuacha mama hospitali. Nilimuacha ikiwa nilimuahidi
nitarudi kumletea chakula baada ya dripu aliyotundukiwa kwisha. Sasa
atakuwa ametoka? Alisharudi nyumbani? aliniona mimi nikiwa katika hali hii?
Nikajinyanyua tena kwa hasira. Maumivu makali yakazidi katika nyonga zangu
na kunifanya nitembee kama binti niliyekeketwa. Miguu yangu ilikuwa kama
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
gulubaja na nililazimika kujipinda kidogo nikidhani huenda maumivu
yatapungua. Nilioga na kubadilisha nguo zangu na kutoka. Sebuleni
nikakutana na Mzee Nyegezi. Mzee Nyegezi alikuwa akitabasamu kinafki.
Tabasamu la kishetani. Sikushitukia chochote kutoka katika tabasamu hilo.
Nikataka kumpita bila kumsalimia. Mwendo wangu ukaniadhiri. Nilikuwa
nikichechemea kutokana na maumivu. Mzee Nyegezi akaniuliza. "Bella vipi?
Umeumia?"
"nimejikata kucha vibaya kidole kinaniuma" Nilimjibu huku nikianza tena
kupiga hatua kuelekea nje. Aliniambia "hali hiyo utaizoea Bella" alikohoa
kidogo. Kikohozi alichokisindikiza na kicheko cha kinafki na kuniambia
"usipokuwa mbishi na kunipa bila utata" Moyo wangu ulilipuka kutokana na
hicho alichosema. 'hali hiyo utaizoea Bella' sauti yake ikajirudiarudia
kichwani mwangu na kujenga kitu kama mwangwi. 'usipokuwa mbishi' Nikaupata
ulimi wangu. "hali? Hali ipi?" Alicheka kifedhuli. Akacheka kwa sauti ya
juu hata nikajisikia vibaya. Nikawa nimeshagundua nini kinaendelea na ni
nani amenifanyia mchezo ule mbaya. Kitendo cha kinyama. Kufanya mapenzi na
mimi bila ridhaa yangu. Ndipo akaanza kuniambia. "wewe ni binti mtamu sana.
Niruhusu niwe wako, usinikatalie. siku nyingine nikatumia nguvu kama leo
nikakusababishia maumivu zaidi"
"ahsante sana shetani mkubwa wewe"
"hata wewe na familia yako yote ni mashetani ndio maana mnashriki katika
njama za kula nyama za watu" alicheka, kisha aliniuliza. "hivi mama yako
yuko wapi? Sijamuona tangu asubuhi?" nilimjibu "ameshajua yote
unayonifanyia na amekukuta chumbani kwangu asubuhi ukiwa uchi. Umesababisha
mama yangu akapoteza fahamu na sasa yupo hospitali unataka kuniulia mama
yangu" nilitoka nje nikiwa nalia. Nilimuacha Mzee Nyegezi akiwa anashangaa
aamini alichosikia.
nilirudi hospitali na kumkuta mama naye akijiandaa kutoka. Tulikaa tena kwa
dakika chache zaidi mpaka alipomaliza kula. Aliniuliza "Bella, mbona
umechelewa kurudi?"
"mama nilipatwa na matatizo nikiwa narudi nyumbani"mama alidakia kwa
mshangao "babu yako amekuja tena?"
"hapana mama, nitakuhadithia yote" tuliondoka baada ya kuruhusiwa na
daktari aliyekuwa akimuhudumia mama. Tulipofika nyumbani sikumuhadithia
lolote.
.......
Nakumbuka ilikuwa ni usiku tukiwa mezani tunakula. Mzee Nyegezi
hakuthubutu kuinua sura yake wala mimi sikuthubutu kumtazama mama. Kuna
wakati nilikuwa nikimuibia mama kwa jicho la wizi wizi. Ni wakati huo ambao
pia nilimkuta yeye akitutazama mimi na Mzee Nyegezi. Niliyarudisha macho
yangu chini tena, kwa aibu wala sikuendelea kumtazama. Mama akakiacha
chakula na kwenda kwenye makochi kutazama video. Chakula alichokipenda, leo
alikigusa kwa kijiko kimoja tu. Mara nyingi alipendelea kutazama kwaya na
kusikiliza mahubiri. Mahubiri ambayo aliinunua cd yake kanisani. Huko nako
hakutumia muda mwingi kumaliza kile alichokuwa anakiangalia. Alirudi kwenye
meza ya chakula tulipo mimi na Mzee Nyegezi. Mimi nilikuwa nimeshamaliza
chakula changu. Nikawa nataka kuinuka, nilipomuona mama akirudi niliendelea
kukaa kwanza kwa muda. Sikujua kwanini moyo ulinienda mbio na uoga
ukaendelea kunitafuna.
"Nyegezi kwanini unanitenda hivi" Mama alimuuliza Mzee nyegezi macho yake
yakiwa yamefumba kwa lita za machozi. Mzee Nyegezi alijitutumua kiume
kupotezea mada aliyotaka kuianzisha mama. Hakufanikiwa.
Mama aliendelea kubwatuka kwa kilio chenye kwikwi na hasira ikaikamata koo
yake. Sasa akawa anaongea kama vile alianza kujifunza kuongea.
"Nyegezi, umekosa nini kwangu? Kwanini unathubutu kutaka kutembea na
mwanangu? Au kwasababu si wako?" mimi nafsi moja ndani yangu ikanisuta,
'kwanini hujamueleza mama kuwa ameshakubaka?' nilijaribu kupoteza sauti
hiyo. Lakini ilikuwa king'ang'anizi kichwani mwangu. Ilirudi ikarudi
ikaendelea kurudi zaidi. Ikanikera moyo. Nikataka kusimama mama akaniambia
"Bella kaa chini" Nilikaa
"Nyegezi sikutegemea kama wewe ungebadilika hivi." Mama alinigeukia mimi na
kuniambia
"Bella hata leo nikifa naomba usikae hapa tena. Nenda popote unapopafahamu,
nenda popote pale lakini siyo na huyu mwanaizaya" Nilimuitikia mama kwa
kumaanisha nimemuelewa alichoniambia.
Baada ya muda kwenda na usiku kuzidi kuwa mkubwa, wote tuliiacha runinga na
kwenda kulala. Mama aliingia chumbani kwangu ili tuweze kusali kabla ya
kulala. Hiyo ilikuwa ni lazima ili kuilinda nyumba yetu na mzimu wa babu
ambao hutusumbua kila mara. Nakumbuka siku hii tuliomba kwa muda mrefu sana
na mimi niliomba pia na mama huku nikibubujikwa na machozi. Ndipo hapo
likatokea jambo baya kati kati yetu mimi na mama. Chumba kilianza
kutetemeka kama vile nje kulikuwa na trekta linalolima. Alikuja fisi mkubwa
sana. Kama kisingekuwako kitanda na sisi kukikalia, basi angekuwa amekimeza
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
chumba chote. Yule fisi alikuja kama Yule nyoka mwenye mabawa alivyoondoka.
Ulianza upepo wa kisuli suli, kisha kati kati yake akatokea fisi huyo. Yeye
alikuwa na ukubwa kama wa farasi na meno kama ya ngiri. Miguu yake ilikuwa
ni minene kama tembo. Niliweza kugundua na kusema alikuwa ni fisi kwa kuwa
alikuwa na umbo la fisi. Hakuwa fisi wa kawaida alitisha sana. Cha ajabu,
fisi huyu alizungumza lugha ambayo mimi na mama hatukuielewa. Kisha
katikati yetu, Yule fisi alijigeuza maumbo mbalimbali ya wanyama na mwisho
kuwa binadamu kabisa. Alikuwa ni babu. Alicheka kwa sauti kuu na
iliyotetemeka. Kabla hajasonya alitoa kisu kilichong'aa sana. Lakini
kilikuwa kinavuja damu. Alitoa na bakuli kubwa katika moja ya mifuko yake.
Vitu hivi vyote vilikaa katka mfuko wa suruali yake lakini sikutambua
kutokana na ukubwa wa vitu hivi ilkuwaje vilienea na kukaa bila shida. Muda
wote mimi nilikuwa nikikemea chini kwa chini. Mama alikuwa anatetemeka kwa
uoga kupitiliza. Babu aliendelea kucheka alicheka sana. Kisha aituambia.
"msiogope"
alimsogelea mama mpaka karibu na uso wake akamwambia "nilikuahidi
ukiendelea kumpingia Bella urithi wake, roho yako ni halali yangu" Mama
alitetemeka sana. Sikuwahi kumuona mama akilia kwa uchungu namna ile.
Nilimsihi babu asimuuwe mama, lakini sikufanikiwa. Nilimsikia mama akikemea
kwa sauti ya chini chini huku akinena kwa lugha ya roho mtakatifu(ile lugha
ambayo huongea walokole)
"Bella, wewe ni lazima uwe, hata kwa kuangamiza dunia nzima. Mkuu wetu
ameipenda roho yako ya kishujaa na ujasiri. Sina jinsi ya kutekeleza
ninaloagizwa"
"mkuu?" Niliuliza kwa mshituko. Kwa nguvu alizo nazo babu, nilitegemea
kusikia yeye ndiye shetani mwenyewe. Alikuwa na mambo makubwa ya kuogofya.
Iweje yeye awe kibaraka wa huyo mkuu anayemtaja? Kama yeye yupo hivi? Huyo
mkuu wao ana nguvu za kiasi gani sasa? nahisi babu aliyajua mawazo yangu.
Akacheka sana kisha aliniambia. "utamuona"
sauti yake ilijirudia rudia huku akiwa anacheka kwa sauti ya juu sana.
Kicheko chake kilinifanya nihisi hata majirani ni lazima wangeamka. Aliendelea
kuniambia "mkuu wetu, ni mkuu wa huu ulimwengu wote. Ana nguvu nyingi sana.
Atakupa wewe endapo utakubali uwe mrithi wangu, usisahau kuwa mali na vitu
vyote ni vyake hivyo utakuwa tajiri zaidi ya tajiri yeyote unayemfahamu
hapa duniani"
mama aliniambia "usikubali Bella, hata nikifa leo naomba usije kukubali
kuwa mchawi"
"mama siwezi kuwa mchawi kama nilivyokuahidi" mimi na mama wote tulikuwa
tunalia sana. Lakini kitu cha kushangaza hatukuweza kusimama wala
kusogeleana japo kuwa tulikaa katika kitanda kimoja. Nilijihisi nikiwa
mzito sana. Sikuweza kunyanyua japo kidole wala mkono kumgusa mama.
Kilichoweza kusogea katika mwili wangu ni jasho jingi lililokuwa likinitoka
mfululizo pamoja na mkojo uliotoka bila mpangilio kwa uoga. Moyo wangu
ulipiga mara nne zaidi ya mapigo yake ya kawaida. Ulipeleka damu kwa kasi
katika kila kiungo cha mwili wangu na kunifanya nihisi kizunguzungu na
mwili kukosa nguvu. Babu alikiinua kile kisu juu na kuongea maneno fulani
ambayo mimi na mama hatukuyaelewa. Katika kuzubaa huko, kisu kile kilipita
katika shingo ya mama na damu nyingi kurukia kwenye bakuli alilolishika
babu. Babu alikinyofoa kichwa cha mama, na kuanza kukitafuna. Sura ya babu
ilianza kubadilika na kuwa ya paka. Macho yake yaling'aa na kutoa mwanga
mkali kama wa jua. Kiwiliwili cha mama kilikuwa kinarukaruka huku na kule
pale kitandani tulipokaa mpaka damu ilipokatika yote na kuchuruzikia kwenye
lile bakuli ambalo alilishika babu. Mimi nilizimia. Nikiwa katika usingizi
mzito wa kuzimia, nilikuwa nikitumbukia katika shimo moja refu sana.
Lilikuwa ni refu kupita kiasi. Siwezi kusema urefu halisi wa lile shimo,
lakini lilikuwa ni refu kupitiliza. Ndani ya shimo hilo lililo na giza
nene, Kulikuwa na hewa nzito na iliyoogopesha kila nilipokuwa nazidi
kutumbukia.
*******
Sikuweza kuona chochote mbele wala chini nilipokuwa nikidondoka kwa mwendo
wa kasi. Ulikuwa ni mwendo ambao sijawahi kudhani kama ningeweza kudumbukia
katika katika shimo kama lile ikiwa mwili bado haujaiacha roho. Nilipofika
mwisho sikuanguka wala sikuumia.
Kumbe tulikuwa na babu pamoja na mama.
Nilishituka kumuona mama akiwa mzima, lakini hakuwa na uwezo wa
kuzungumza. Hakuwa na uwezo wa kuzungumza, kwa kuwa nilimuita hakuitika
wala kuniambia chochote. Alibaki akinitazama kwa hudhuni. Alipojitahidi
kuniongelesha niliona ulimi wake ukiwa umekatwa na kubaki kipande. Babu
aliniambia "hapa panaitwa Gamboshi, nitakutembeza kila sehemu uweze kuona
wabishi waliokuwa wakijaribu kukatisha mipango yetu duniani"
"umemfanya nini mama na mbona haongei"
wakati huo wote mama alikuwa akinitazama machozi yakimtoka. Hakuwa na
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
tofauti na wale mazezeta ninaowafahamu. Babu alicheka kwa kejeli kisha
alikuwa akiongea huku akimtazama mama "huu ndiyo mshahara wa kukwamisha
harakati za mkuu wetu. Huyu si mama yako tena, sasa hivi ni msukule.
Atakuwa huku kwa muda mpaka siku yake ya kufa itakapofika"
niliwahi kusikia kuhusu misukule, lakini nilichofahamu mimi kuhusu watu
waliogeuzwa misukule nilidhani huenda ni wale walioishi katika maisha
ambayo hayakumpendeza mungu. nilijiuliza sana iweje wawe na nguvu ya
kumgeuza mama msukule? Wakati hadi wakati mama anakufa alikuwa akinena kwa
lugha ya kimbinguni, lugha inayonenwa na watakatifu tu?
wakati nikiwaza hayo, ghafla niliona kama sinema mbele yangu. Niliyaona
maisha ya mama yote upande wa pili mbali na ulokole ambao nilikuwa
nikiufahamu. Wakati mama akiwa duniani baada ya mume wake wa kwanza Joseph
ambaye ni baba yangu mzazi kufariki, aliishi katika mazingira magumu sana
kabla hajaolewa na mume wake huyu wa pili, Mzee Nyegezi. Aliwahi kushauriwa
na rafiki yake waenda kwa mganga apate mume tajiri ambaye atamuowa. Mama
alikubali. Masharti ya mganga yalikuwa ni vichekesho vitupu. Mganga yule
mbilikimo, alimtaka mama wafanye naye mapenzi, kwa madai kuwa hiyo ni njia
ya kumtumbukizia dawa katika mwili wake kupitia njia ya kujamiana. Mama
hakukubali.
Wa pili alikuwa ni yule mjukuu wa babu kutoka kigoma. Yeye alimshauri alale
na maiti mbili usiku wa manane katika makaburi ya kisutu. Mama alikataa
pia. Rafiki yake akawa amemchoka. "rafiki yangu mimi siwezi nikawa napoteza
muda wangu kila siku halafu wewe unakataa masharti unayopewa"
"sio hivyo rafiki yangu. yaani kweli unanishauri nilale na maiti jamani?"
"maiti si alikuwa binadamu kama wewe tu? Embu usiniangushe bwana. Siku moja
tu haidhuru jambo" nilisikitika sana picha ambayo ilioneshwa mbele yangu.
Mama alilala na maiti zote zilizofukuliwa kichawi katika makaburi yale yale
ya kisutu. Kisha baada ya kupata mume tajiri halafu kutokana na kushindwa
masharti ya mganga ya kuendelea kulala na maiti kila mwisho wa mwaka, ndipo
alipoamua kuokoka. Mama aliokoka akiwa na mume wake huyo huyo aliyempata
kupitia kwa mganga kwa masharti ya kulala na maiti mbili.
Chozi likaniponyoka. Ndipo nikaoneshwa saa chache kabla mama hajauwawa
kichawi na babu, alikuwa na hasira juu ya Mzee nyegezi. Alikuwa na chuki
ambayo alishindwa kumsamehe Mzee Nyegezi. Nikaogopa sana kufahamu kumbe
hasira na kutomsamehe mwingine kunaweza kusababisha mimi nishindwe kwenda
mbinguni. Nilimuonea huruma mama kila nilipomtazama. Babu alikuwa
akitutembeza katika mitaa ya sehemu hiyo ambayo alinitambulisha kama ni
Gamboshi. Ilikuwa ni mitaa ya kawaida kama mitaa ya duniani. Nilisema hivyo
kwa sababu hapa kulifanana kabisa na ulimwengu Fulani wa siri. Ulimwengu
ambao kulikuwa na viumbe vingine vyenye sura za binadamu lakini walipaa
kama ndege. NIlimuona kiumbe kimoja kilichonguzwa Vibaya na moto. Sura yake
ilikuwa imeharibiwa vibaya na kuwa iliyotisha. Nilimuuliza babu "huyu mbona
yupo hivi?"
Babu aliniambia "walokole duniani huwaharibu sana watu wetu huku Gamboshi
kwa maombi ya wanayoyamba" kisha aliniinamia na kunionesha mtu fulani
aliyekuwa mbele yetu, amevaa kaniki huku akipepeta unga katika ungo mkubwa
sana. "unamuona yule?"
Nilishituka sana. Alikuwa ni kijana fulani ambaye nilimfahamu kwa jina la
Fikiri. Alikufa miaka miwili iliyopita. Tulikuwa tukiishi naye mtaani. Yeye
alikuwa akiuza maji kwa kupitisha katika madumu kila nyumba. Watu wengi
walinunua maji yake na kuwa maarufu sana. Hata kifo chake kilihudhuriwa na
watu wengi sana. Lakini wengi walinong'ona msibani kuwa hakikuwa kifo cha
kawaida.
"alikuwa akicheza tu mpira akaanguka ghafla"
"itakuwa bibi yake. Maana inasemekana yeye ndiye mchawi maarufu"
rafiki zake Fikiri walifikiria hivyo na kunong'ona kwa nguvu kutokana na
jazba iliyojaza mioyo yao. Nilimuuliza babu. "fikiri alifanya nini?"
babu aliniambia "yeye hakuwa na tatizo. Ila alitolewa kafara na bibi yake."
bibi yake alikuwa mchawi na alilazimika kumtoa yeye Fikiri kwa sababu zamu
yake ya kutoa damu na nyama ilifika. Babu alinieleza kuwa hapo kuna kambi
nyingi za wachawi na wa kila aina. Lakini Gamboshi ndiyo kilikuwa kijiji
ambacho mkuu wao alikuwa akiishi. Nguvu zote za wachawi zilitoka katika
kijiji hiki. Ilikuwa ni kijiji cha wachapakazi na watu walikuwa busy kuliko
kawaida. Nilibahatika kuwaona watu wengi niliowafahmu huko duniani.
Babu akaniuliza Swali "je upo tayari kuurithi ufalme wangu mara
nitakapokufa?"
aliniambia huku akiwa na anatokwa na machozi ya damu. Sikuelewa hali hiyo
ilimaanisha nini ila nilishindwa kukubali haraka haraka. Lakini pia
sikupenda kufa mapema kama alivyokufa mama. Nilitambua fika ule ndio
ulikuwa mwisho wa kuonana na mama yangu. Mama aliondoka katikati yetu na
kuvalishwa kaniki nyeusi kama walizovaa wengine wengi katika kjiji
hicho. Baada
ya kutafakari sana kwa dakika chache baadaye nilimjibu babu. "babu naogopa
kuwa mchawi" Nilijibu kiuwoga. Nilijibu nikiwa namaanisha kweli ninaogopa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kuwa mchawi. Tuliendelea kutembea katika mitaa mbalimbali ya kijiji hiko
cha wachawi.
Babu alitabasamu na kunigeukia "mjukuu wangu uchawi hauna madhara yoyote"
"babu hauna madhara?" Niliuliza kwa mshituko. Babu alicheka na kunijibu
kifupi
aliniambia huku akiwa na anatokwa na machozi ya damu. Sikuelewa hali hiyo
ilimaanisha nini ila nilishindwa kukubali haraka haraka. Lakini pia
sikupenda kufa mapema kama alivyokufa mama. Nilitambua fika ule ndio
ulikuwa mwisho wa kuonana na mama yangu. Mama aliondoka katikati yetu na
kuvalishwa kaniki nyeusi kama walizovaa wengine wengi katika kjiji
hicho. Baada
ya kutafakari sana kwa dakika chache baadaye nilimjibu babu. "babu naogopa
kuwa mchawi" Nilijibu kiuwoga. Nilijibu nikiwa namaanisha kweli ninaogopa
kuwa mchawi. Tuliendelea kutembea katika mitaa mbalimbali ya kijiji hiko
cha wachawi.
Babu alitabasamu na kunigeukia "mjukuu wangu uchawi hauna madhara yoyote"
"babu hauna madhara?" Niliuliza kwa mshituko. Babu alicheka na kunijibu
kifupi
"ndiyo, hauna madhara yoyote"
"babu mimi siwezi kula nyama ya mtu, kunywa damu ya binadamu wala mnyama,
siwezi kuua. Babu sitaki kuwa mchawi"
babu alizungumza na mimi kwa upendo hata nikajisikia faraja
"mjukuu wangu, nafasi niliyo nayo ni kuwaadhibu wale wanaokiuka masharti ya
mkuu wa ulimwengu huu hivyo wewe nawe utakuwa vivyo hivyo kama utakubali
kurithi nafasi yangu"
nilimuomba babu anipe muda nitafakari jambo hilo kwa muda. Babu alinipa
masaa machache hivyo alidai kuwa angelifuata jibu lake usiku. Tulipokuwa
tukiendelea kutembea tembea, nilishituka kumuona mtu ninayemfahamu kabisa.
Alikuwa ni mtu mmoja maarufu huko duniani. Alikuwa ni mwanasiasa
aliyeogopwa sana na vyama pinzani, pamoja na chama chake. Nilisikitika
kumuona akiwa pale. Amechoka, amekuwa mweusi tofauti na alivyokuwa kule
duniani. Nilipotaka kuzungumza naye, babu alinizuia.
"hapana Bella, wewe bado hujawa na nguvu za kuweza kuzungumza na misukule"
nikamuuliza babu "kwani huyu amefanya nini mpaka yupo mahali hapa?"
"yeye alitolewa kafara na mume wake, mume wake ni mfanyabiashara maarufu
lakini yupo katika chama kimoja maarufu kinachotoa kafara na kumwaga damu
kwa sababu ya utajiri"
nilitetemeka sana niliposikia hivyo. Baada ya muda, nikatamani kuzunguka
zunguka tu mule katika kile kjiji cha Gamboshi ili niweze kuwaona watu
mbalimbali ambao ninawafahamu.
Tulipita katika kijiji duni ambacho niliwaacha wale misukule sasa tukaingia
katika sehemu yenye uafadhali wa maisha katika shemu hiyo ya Gamboshi.
Babu alinieleza "kule tulipopita mwanzo, ndipo wanapoishi misukule. Lakini
huku ndipo ilipo ngome yangu na wachawi wengine wakubwa huko duniani."
mbele ya majumba mbalimbali ya kifahari. Yaliyojengwa kiufahari. Niliuona
mji Fulani ulikuwa uking'aa sana. Ulikuwa ni mji uliokuwa ukiwaka taa
zilizotowa mwanga mkali hata kufanya niuone mji ule ukipendeza sana.
Nikamuuliza babu "kule ni wapi na kuna nini?" Babu hakunijibu kitu na
kunieleza ile si sehemu nzuri kuifikiria wala kutamani kwenda. Alinieleza,
miaka mingi sana iliyopita ufalme wa falme ile ilijaribu kutaka kupindua
tawala ya mkuu wao na kushindwa. hivyo ilijitenga nao na kuwa maadui
wakubwa baada ya urafiki uliokithiri na kujikita katika ndani ya mishipa
yao ya damu kabisa, kupoteza mvuto. Sikutaka kuendelea kuuliza zaidi lakini
nilihisi jambo kuhusu mji ule niliouona. Mji ule na hapa Gamboshi tulipo,
kuliteganishwa na shimo moja refu liliokuwa likitokota uji mzito wa moto.
Tofauti ya mji ule na huu wa ngome ya babu ilipo. Japokuwa mji ule
ulipendeza na uling'aa sana lakini huu wa babu ulififia na kuwa kama wenye
giza Fulani lisiloeleweka. Babu alinitoa hapo na kunionesha sehemu ambayo
mkuu wao alikuwa akiishi. Alinieleza "mjukuu wangu, sehemu hii ni takatifu
sana. Watu wote maarufu uwajuao huko duniani, huja mahali hapa kumuomba
mkuu wetu utajiri na kusafisha nyota zao ili waweze kukubalika zaidi na
zaidi."
"ninaweza kumuona?"
niliuliza
"hapana, bado hujafikia viwango vya kukanyaga sehemu ile" tuliondoka mahali
hiyo na kurudi kule kwa awali. Kule kulipochosha. Kule niliposhuhudia
misukule ikifanya kazi kwa bidii. Kule ambapo naamini ningemuona tena mama
na nimuage kuwa ipo siku nitarudi kuja kumtoa. Nilimuuliza babu "hivi hawa
hufanya kazi kwa muda gani" Babu alicheka sana na kunieleza kuwa "hawana
mapumziko, hufanya kazi usiku na mchana na hupumzika mara moja tu kwa siku"
alinyamaza baada ya kumeza mate kasha aliendelea kunieleza "wakati ambao
umepangwa wa wao kula tu"
"na huwa wanakula nini?" akanijibu "unga na funza, ndio chakula chao kikuu"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nilishangaa sana, ghafla machozi yalinitoka. Nilihuzunika kwa kuwa
nilifahamu mama yangu naye alikwisha kuwa msukule. Hivyo chakula chake
nacho kingekuwa ni hicho hicho. Nilimlaumu babu kwanini alimuuwa mama
yangu. Nililia kwa uchungu huku nikikimbia kusikojulikana. Nilikuwa sijuhi
wapi naenda ila nilipishana na misukule na vile viumbe vilivyopaa kama
ndege lakini wakiwa na maumbo ya binadamu. Ghafla Mbele yangu nilikutana
babu akinicheka kwa sauti ya juu sana. Aliniambia "Bella huku huna pa
kunikimbia" nilimjibu "babu nakuchukia, nakuchukia kuliko navyomchukia
shetani"
ghafla babu alinipiga kibao kilichonifanya nipoteze fahamu. Fahamu
iliyonitoa katika ulimwengu wa Gamboshi na kunirudisha duniani. Nilijikuta
nikiwa katikati ya watu wengi. Watu waliokuwa wakilia wakinamama
wamejifunga kanga zao. Wengine wakinipepea huku wakilia kwa uchungu
wakiliita jina la mama yangu.
niliposhituka nilipiga chafya mara tatu mfululizo. Watu walijawa na
mshituko. Niliwaona wengi wakiwa na maswali mengi sana juu ya kifo cha
mama. Mimi pia nilianza kulia kwa uchungu. Nilifahamu fika sitoweza kumuona
tena mama yangu katika ulimwengu huu wa kawaida. Watu walinibembeleza
lakini niliona kama walikuwa wakiniongezea uchungu zaidi. Walimuita Mzee
Nyegezi. Mzee Nyegezi alikuwa akizungumza na askari polisi waliofika eneo
la nyumbani kwetu. Watu walikuwa wamejaa sana. Hakika kifo cha mama
kilishitua wengi. Mzee Nyegezi na wale askari, walisubiri ninyamaze kulia
kisha waniulize maswali kadhaa. "pole sana binti" Alizungumza askari mmoja
aliyevalia sare zake.
"salama" kwikwi ilinibana, lakini nilijibu hivyo hivyo. Wakati huo huo
ambao askari wakiendelea kuzungumza, ghafla niliisikia sauti ya babu yangu
ikizungumza na nafsi yangu
"usiwaeleze chochote askari kuhusu kifo cha mama yako, wajibu hufahamu kitu"
nilipopata kigugumizi cha kujibu kutokana na sauti niliyoisikia, macho
yangu yakapata mshangao zaidi nilipomuona babu mbele yangu. Alikuwa kwenye
msiba huo kama waombolezaji wengine wa kawaida. "unaweza kutueleza
chochote ulichokiona?"
askari mmoja akalirudia Swali aliloliuliza zaidi ya mara tatu. Sikulisikia
kutokana na uwoga na nilijifanya sikuliskia kwa kuwa jibu walilotaka sikuwa
tayari kuwajibu.
walinipa muda wa kupumzika zaidi. Huku nikisikia kuwa, mwili wa mama upo
hospitali kwa ajili ya uchunguzi. Bado nilikuwa katika woga zaidi. Watu
mbalimbali waliingia katika chumba nilichomo kunipa pole. Nilimuona Jordan
mpenzi wangu. Nilimuona Bertha rafiki yangu na wanafunzi wenzangu wa
shuleni. Dakika chache baadae aliingia mwanamke fulani mwenye mwili mpana
na uso wa mviringo. Uwazi Fulani katikati ya meno yake ukamfanya awe na
mwanya hata akapendezesha kwa jino la dhahabu. Alijitanda kanga juu, chini
akakivaa kitenge kutoka kongo.
sikuwahi kumuona hata siku moja. Aliniambia "pole sana Bella" Nilikuwa
nikimtazama kwa makini bila kukumbuka ni wapi niliwahi kumuona. Nilimjibu
"asante, sijuhi niliwahi kukuona wapi?" akanijibu. "Gamboshi," hapo hapo
nilipoteza fahamu na kuisalimia sakafu kwa kuibusu. Dakika chache baadaye
niliamka kutoka usingizini. Nilijikuta katikati ya kundi kubwa la watu
wakinisikitikia. Kila mmoja alisema lake
"kufiwa na mama si kitu cha mchezo"
"tena kuna tetesi alikuwa naye" mwingine alisema "mama yake amekufa kifo
cha kinyama sana" Nikaanza tena kulia kwa uchungu. Nililia sana kwa sababu
nilifahamu fika chanzo na sababu ya kufa kwa mama yangu ni kuzuia harakati
za babu mimi kuwa mchawi. Nikiwa katika kulia huko sikujua nilipata hisia
gani hata zikanigusa nitazame nyuma ya mlango wa chumba nilichomo.
Nilimuona mama akiwa hana uwezo wowote wa kuongea.
Nilizidi kulia. Mbele yangu akatokea babu na kunieleza kuwa. "sasa umeweza
kuwa mchawi" Nilishituka sana. Sikujuwa ilikuwaje nikawa mchawi bila
kukubali mwenyewe na ilikuwa saa ngapi nikawa mchawi. Babu aliongea na
mimi bila mtu yeyote kufahamu kama nilikuwa nikizungumza na babu
"uliniambia nikupe jibu jioni kama nimekubali, imekuwaje uniambie nimekuwa
mchawi sasa?" Alicheka sana kisha aliniambia
"mjukuu wangu unatamani utajiri na nyota yako inawaka sana"
"hujajibu swali langu babu"
"ipo siku utanielewa acha tuyamalize haya ya msiba kwanza"
alipotaka kutoweka mbele yangu nilizishangaa nguvu nilizonazo. Niliweza
kumzuia.
"mama anafanya nini hapa?"
nilimuuliza huku nikiangalia eneo la mlangoni. Babu naye aligeuka kuangalia
alipo mama. Alinigeukia huku akitabasamu kifedhuli na kuniambia
"atakaa pale mpaka mtakapomsalia katika mazishi yake. Ule mwili ambao
wameenda kuufanyia uchunguzi si mwili bali ni mgomba. Usiogope, hana uwezo
wa kufanya lolote pale na hakuna anayemuona"
nilisonya kwa hasira na babu alitoweka hapo hapo. Nilisonya kiasi kwamba,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-
hata waombolezaji wengine walishituka. Mama mmoja aliniuliza "kuna nini
Bella?"
nilitingisha kichwa nikikataa kuwa hakuna kilichotokea. Nikatoka nje,
nilishangaa kumkuta babu akiwa pale pale nilipomuona mchana akiwa na wale
askari pamoja na Mzee Nyegezi. Mzee Nyegezi naye alinifuata na
kuniuliza "unajisikiaje
sasa Bella" nilimjibu tu, ilimradi
"vizuri" akaniuliza "Nyama ya mama yako ni tamu?" alikuwa akinichekea kwa
kunikejeli. Akaamsha hasira zangu. Nilimuangalia Mzee Nyegezi kwa jicho la
chuki hata nikamuona akianza kutokwa na jasho jingi sana. Nilijihisi nikiwa
na nguvu za ajabu, nguvu za kumuadhibu yeyote kwa kumtazama tu. Ilikuwa
inashangaza.
Muda wote huo babu alikuwa akinitazama. Alikuwa akitabasamu kwa raha sana.
Nilimuona Mzee Nyegezi akilalamika. "Bella unaniunguza na macho yako". Nikampa
onyo
"ole wako umueleze yeyote kuhusu msiba wa mama"
"nisamehe Bella usiniadhibu sintomueleza yeyote"
taratibu za mazishi ziliendeshwa na famila ya mama mkubwa. Ndugu na
marafiki wa mama walijumuika pamoja kumsindikiza mama katika safari yake ya
mwisho. Watu walikuwa ni wengi sana. Siwezi kusema kuwa nilihesabu idadi
yao, kwasababu nisingeweza. Misa takatifu ya kumuombea mama, ilifanyika
katika kanisa la katoliki mule mule ndani ya hospitali ya muhimbili.
Nilishituka kumuona yule mama aliyenitokea mule chumbani kichawi, akiwa
kwenye madhabahu huku akitoa maelekezo
"mwili wa mama yake Bella hautafunuliwa kutoka katika jeneza lake kutokana
na wingi wa watu pamoja na kifo alichokufa. Hivyo tumeamua kuweka picha tu
ambayo mtapita mkitoa heshima zenu za mwisho kwa kupita njia hii na
kuelekea nje ambapo kuna magari ya kuwapeleka makaburini." Nilimgeukia Mzee
Nyegezi aliye pembeni yangu, nikamuuliza
"hivi huyu mama ni nani?"
"nimetambulishwa na babu yako kuwa ni ndugu wa mama yako"
"na babu si ni baba wa baba yangu? Imekuwaje yeye afahamu ndugu wa mama
yangu?"
"sifahamu Bella naomba uniache kidogo"
tulienda kuaga kwa taratibu tulizoelekezwa na yule mama. Nilijaribu
kumtafuta, lakini sikumuona tena eneo hilo la msiba. Mpaka tulipoingizwa
kwenye magari ya kuelekea makaburini kuuzika mwili wa mama.
Baada ya mazishi tulirudi nyumbani. Baada ya siku chache baadaye, msiba
ulipomalizika maisha yalikuwa shwari wala babu na yule mama wa maajabu
hawakutokea tena. Siku moja nikiwa shuleni pamoja na rafiki zangu, alikuja
Berther na kunieleza kuwa "kuna mtu kule nje anakuita" nikamuuliza
"mwanamke mwanaume?"
"mmama mmoja hivi, ila niliwahi kumuona msibani kwenu"
mimi nilitoka mbio mpaka getini kumtazama huyo mama. Mawazo yalijua fika ni
yule mjumbe wa wachawi kutoka Gamboshi. Alifuata nini kwangu? alitaka nini?
Nilipofika getini, sikukuta mtu. Nilipotaka kugeuza na kurudi ndani.
Nilimuona babu amesimama pembeni ya ukuta wa shule akicheka "vipi mbona una
wasiwasi?" aliniuliza ghafla. "babu yule mwanamke ni nani?" nilifahamu
fika anafahamu ninachozungumzia. Alicheka bila kunipa jibu lolote.
Nikamuuliza tena "umekuja kufanya nini hapa?" alinijibu "nataka ukadhuru
Gamboshi mara ya mwisho kabla hujarithi kiti changu" moyo wangu ukaanza
kwenda mbio sana. Ghafla mbele yetu tuliposimama, lilikuja gari la maajabu
na ndani yake abiria walikuwa uchi wa mnyama. Nikisema gari la maajabu,
namaanisha gari lile lilipita eneo la shule bila hata kufunguliwa geti na
wala hakukuwa na barabara eneo hilo. Tulielekea gamboshi. Tulipoingia ndani
ya lile gari la kichawi, sikuwa muoga tena. Niliwaona watu walio nadhifu
kimavazi kuonesha walikuwa na uafadhali wa kifedha. Watu hao walijitundika
ndani ya suti nyeusi mikononi walizibeba biblia. Nikajinong'oneza
"wachungaji?" nilishituka sana. Ilibidi, nimuulize babu. "hawa si watumishi
wa mungu?" Babu alinipiga kibao kikali sana na kunikataza kwa kuniambia
kuwa, jina hilo halikuruhusiwa kutajwa eneo lile. Kisha aliniambia kuwa
"hawa si watumishi wa huyo anayedhaniwa kuwa aliwaumba binadamu"
nilimeza mate nikiugulia maumivu huku nikiwaangalia wale watu waliokuwa
kimya muda wote. "sasa huku Gamboshi, wanaenda kufanya nini?"
Babu alicheka kicheko kisicho na ladha ya kuitwa kicheko. Kisha aliniambia
kuwa
"hawa ni wachungaji maarufu sana huko duniani wanaolihubiri jina la mkuu
wetu kupitia hizo dini zao. wachache huwafahamu kama wakiwa pamoja nasi
katika ulimwengu huu wa Gamboshi" Nilikuwa nimetumbua macho muda wote.
hakika ilikuwa habari ya kushangaza na kutisha muda wote. Kisha babu
aliendelea kuniambia. "wengi wamepata nguvu ya uponyaji kutoka kwa mkuu
wetu. Unapoponywa na mmoja kati ya wachungaji hawa, lazima wewe uwe mmoja
wa wanachama wa kuleta watu wengine wengi katika ulimwengu wa mkuu wetu."
sasa ndio nikakumbuka mama aliwahi kuniambia mwisho wa dunia yatatokea
mambo mengi ya kutisha na kushangaza. Manabii wengi wa uongo wataponya.
viwete wakatembea, viziwi wakasikia na mabubu kupiga yowe; nikiona ishara
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hizo nisihangaike katika kukimbilia miujiza nisimamie imani yangu. Mwili
wangu ukasisimka hata vinyweleo vikasimama. Nilimgeukia babu na kumuuliza.
"mbona gari imesimama na hawa wanashuka?" babu alinieleza kuwa "hawa ni
wachawi ambao wanaenda kuongezewa vyeo kwa kazi walizofanya bada ya kutumwa
na kuzifanikisha. Hupewa fisi wa kutembelea ama mnyama yeyote. Hongezewa
nguvu pia kwa kujilinda na maadui na nguvu za walokole"
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment