Simulizi : Niliongea Na Shetani Ili Niwe Tajiri
Sehemu Ya Pili (2)
"hawa ni wachungaji maarufu sana huko duniani wanaolihubiri jina la mkuu
wetu kupitia hizo dini zao. wachache huwafahamu kama wakiwa pamoja nasi
katika ulimwengu huu wa Gamboshi" Nilikuwa nimetumbua macho muda wote.
hakika ilikuwa habari ya kushangaza na kutisha muda wote. Kisha babu
aliendelea kuniambia. "wengi wamepata nguvu ya uponyaji kutoka kwa mkuu
wetu. Unapoponywa na mmoja kati ya wachungaji hawa, lazima wewe uwe mmoja
wa wanachama wa kuleta watu wengine wengi katika ulimwengu wa mkuu wetu."
sasa ndio nikakumbuka mama aliwahi kuniambia mwisho wa dunia yatatokea
mambo mengi ya kutisha na kushangaza. Manabii wengi wa uongo wataponya.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
viwete wakatembea, viziwi wakasikia na mabubu kupiga yowe; nikiona ishara
hizo nisihangaike katika kukimbilia miujiza nisimamie imani yangu. Mwili
wangu ukasisimka hata vinyweleo vikasimama. Nilimgeukia babu na kumuuliza.
"mbona gari imesimama na hawa wanashuka?" babu alinieleza kuwa "hawa ni
wachawi ambao wanaenda kuongezewa vyeo kwa kazi walizofanya bada ya kutumwa
na kuzifanikisha. Hupewa fisi wa kutembelea ama mnyama yeyote. Hongezewa
nguvu pia kwa kujilinda na maadui na nguvu za walokole"
kisha aliendelea kunieleza kuwa, wale wachawi wanaelekea eneo ambalo
kulikuwa na joka kubwa lenye vichwa vitatu. Joka hilo, ni kubwa sana. Joka
linalotowa nguvu hiyo. Vichwa hivyo vina sura za binadamu zinazotisha. Kwa
mtu wa kawaida huwezi kuzitazama zaidi ya sekunde tano bila nguvu za
kichawi, utazimia au kufa kabisa. Babu aliponieleza hayo niliogopa sana.
Siwezi kueleza kiasi nilichoogopa lakini hata wewe nikusimuliaye hadithi
hii, bila shaka unatetemeka. Basi gari lilikuwa linaenda kwa kasi kama
treni ya umeme. Tulipofika eneo Fulani, mimi na babu tulishuka na wale
wachungaji waliendelea na safari.
nilimuuliza tena babu "kumbe kule bado kuna safari nyingine ndefu?"
Alinijibu "kule ndipo mwisho wa safari, kule ndipo alipo mkuu wetu, kule
ndipo nilipokuonesha siku ile ya kwanza na kukuelekeza ile ni sehemu
takatifu sana. Ipo siku utakwenda ukishakuwa na nguvu za kutosha na
kukabidhi madaraka niliyonayo."
lile gari halikuchukuwa muda mrefu likawa limeshapotea machoni pangu. "sasa
mimi nimekuja kufanya nini huku ikiwa mimi bado sijawa mchawi?"
babu alicheka kama kawaida na kuniambia "wewe ni mchawi tayari ila huna
nguvu za kutosha za kukutana na mkuu wetu." Nilijiuliza mara kwa mara huyo
mkuu anayetajwa na babu sana, atakuwa ni nani? lakini sikupata jibu. Katika
kutembea na kuzuru eneo ambalo misukule walikuwa wakifanya kazi kulingana
na kazi zao au vipaji walivyokuwa navyo huko duniani, tuliingia katika
jengo moja ambalo babu aliniambia hiyo ni hospitali ya hapo Gamboshi.
Niliuliza
kwa mshangao "Hospitali? Kwani huku nako watu hupigania uhai?"
babu alinieleza " hiyo ni sehemu ya kubadilishana viungo baina ya misukule
na wachawi ambao huumizwa na nguvu za maombi ya walokole." Babu akanieleza
jambo moja ambalo hata leo silisahau "wachawi hawaogopi biblia wala jina
la huyo aliyekuja akasulubiwa msalabani(yesu) bali kwa hao wanaojifanya
wanaomfuata huyo mtu wao" hapa babu alinieleza kwa maneno ya kashfa sana.
Maneno ambayo yalimdhihaki Mungu. M Sikupenda niyaandike yote. Mara
nikamuona msukule ambaye alikuwa akifanyiwa jambo kama operasheni.
Alitolewa mguu na kubandikwa mtu mmoja aliyekuwa uchi akiugulia maumivu.
Babu alinieleza kuwa yule ni mchawi aliyevunjwa mguu na nguvu za maombi. Babu
akanigeukia na kunieleza "leo tutakuwa na safari ndefu kidogo huku
Gamboshi. Lakini isiyochosha. Leo ni siku ambayo utakabidhiwa utawala wangu
na utakuwa msichana wa kwanza tangu ulimwengu huu ulipoumbwa kwa kushika
nafasi kubwa kama hii. Mkuu wetu amependezwa na mg'ao wa nyota yako hivyo
ameamini akikutumia wewe atapata wafuasi wengi. Hakuna falme itakayoshinda
mara itakapojaribu kujiinua kupigana na wewe. Utakuwa msichana mwenye nguvu
za ajabu na utajiri usioelezeka. Ila kuna masharti utakayopewa ukiyatimiza
hayo utakuwa umenifurahisha sana."
Alinipiga piga mgongoni nikahisi kama nimeshikwa na nyaya za umeme.
Nilitetemeshwa.
Nilimuuliza babu nikiwa na tabasamu "babu sasa kwanini mkuu wenu ameamua
kunichagua mimi ikiwa bado mimi ni binti mdogo? Na nisiye na uwezo wowote
kifedha?"
"swali zuri sana. wakati wote nakueleza kuwa mkuu wetu amependezwa na nyota
yako hiyo ndio sababu iliyomvutia mkuu wetu" aliyameza mate kisha
aliniambia "mkuu wetu ana utajiri mkubwa yeye haihitaji sadaka" kisha babu
alicheka kifedhuli.
niliacha kuuliza maswali na kuendelea kuzuru Gamboshi kama mtalii. Nikaona
kikao kimoja klichohudhuriwa na watu wengi sana, kikiwa kinaongozwa na joka
kubwa yaani joka lile lilikuwa kubwa kupitiliza. Joka lile lilikuwa
likiwatemea wale watu mate yake. Cha ajabu mate yake yalikuwa mengi kila
alipokuwa akiwatemea ikawa kama ilikuwa inanyesha mvua. hivyo kila mmoja
aliye katika kikao kile alilowa chapachapa. babu alinieleza kuhusu joka
lile.
"yule ni mdogo sana kwangu, ni mtu wa heshima sana huko Nigeria yeye
hugawa nguvu na kukubalika pamoja na kufunguka kwa milango yao ya pesa
lakini bado hajafika katika wadhifa wangu yeye hapa ni sawa na waziri mkuu
huko duniani" Nilijiuliza sana moyoni
'sasa babu atakuwa ni nani ikiwa huyu nyoka mkubwa, anayetisha angekuwa yu
chini ya babu?' ilibidi nimuulize "sasa wewe ni nani katika wadhifa wako?"
Babu alicheka, wala hakuniambia wadhifa wake. Ila nilimuuliza tena "kwa
hiyo babu wale ni matajiri wa wapi?" alinijibu kwa majivuni "wale ni
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
matajiri kutoka katika kila pembe ya dunia si wa Nigeria peke yake"
hapo nikawa nimeelewa. Nilimuuliza swali lingine tofauti "hivi babu! yule
mwanamke aliyekuja pale nyumbani siku ya msiba wa mama, akajitambulisha
kuwa alitokea Gamboshi alikuwa ni nani?" hili nalo hakunijibu. Aliita jina
moja nisilolifahamu kwa sauti iliyotetema kama radi. "Consolathaa!" Fumba
na kufumbua mbele yetu akatokea yule mwanamke aliyekuja siku ile nyumbani
kwenye msiba wa mama. Alikuwa ni mchafu na kunuka sana. Alikuwa ni huyo
aliyeitwa na babu kwa jina hilo la Consolatha. Babu akanieleza hadithi fupi
iliyomuhusu Consolatha. "huyu ni mwanangu wa kike wa pekee niliyemzaa
baada ya baba yako kuacha ziwa katika miaka mitatu iliyopita kwenye uzao wa
bibi yako. Mizimu ikapendezwa naye lakini alifanya kosa dogo la kijinga
katika masharti aliyopewa na mkuu"
wakati ambao babu alikuwa akinielezea hayo, Consolatha alikuwa amepiga
magoti akiwa ameinamisha kichwa chini kwa heshima kama akisujudu mbele yetu.
Babu aliendelea kunieleza "yeye aliambiwa ile damu iwatokayo kila mwezi
ahiifadhi katika kikombe na kukiweka kwenye kitanda alaliacho na baada ya
kukata, amletee mkuu wetu na iwe kama kiapo chake kwa kuinywa kikombe
kimoja" babu alikohoa, akameza mate kisha aliendelea
"yeye alishindwa kwa kuona eti ulikuwa ni uchafu" mimi mwenyewe nilikunja
sura kwa kuona ni uchafu niliona kuwa ni jambo ambalo lisingewezekana.
Kunywa uchafu uliotoka mwilini mwangu? Ni heri niukose huo umalkia.
Nilimsalimia shangazi. Baada ya kuniitikia salamu yangu alitoweka. Babu
akaniambia "hata wewe usithubutu kwenda kinyume na masharti ya mkuu.
Utapata shida huku Gamboshi, duniani na popote utakapokuwa unaenda"
niliteteeka kwa uoga sana. Niliitikia tu bila kumaanisha kama nimeelewa
alichoniambia. Akaniambia tena "sasa muda wa kwenda kukuapisha na kukupa
nguvu umefika. Lakini kama haupo tayari kupewa masharti utakayopewa ni heri
usikubali."
hapo ni kawa mzito kukubali. Sikujua niseme lipi kati ya "ndiyo ama hapana"
lakini nilijipa moyo kuwa masharti ambayo ningepewa huenda ningeyaweza. Babu
akaniamuru nivue nguo nilizovaa "vua zote ubaki kama ulivyozaliwa"
Nilikataa.
"usiogope, hutabaki uchi kila mahali utakapokuwa unaenda, kuna nguo ambazo
nitakuvalisha kwa ajili ya utukufu mbele za mkuu" Bado nilikataa. Punde si
punde dakika chache mbele nilijishangaa kuona nimevaa gauni lenye rangi ya
zambarau. Kiunoni mshipi wa rangi ya damu ya mzee pamoja na viatu vya rangi
ya dhahabu. Hakika nilipendeza sana. Nilipendeza kupitiliza. Nywele zangu
zikawa laini kama sufi na ngozi yangu iliteleza kama mtoto mdogo. Ule uzuri
niliokuwa nikisifiwa kule duniani, niliona kama uchafu, huku Gamboshi
ulikuwa maradufu. Nilitamani kujitazama muda wote. Tabasamu likanipoyoka
na kumzawadia babu lile maridhawa. Babu alikuwa akinitazama huku
akitabasamu kiukweli.
aliniambia. "nilikueleza huku hakuna kinachoshindikana" kisha tulipotea na
kutokezea katikati ya kundi kubwa la watu. Wake kwa waume wakiwa wamefurahi
kupita kiasi.
Nilimuuliza babu "Hawa wamefurahi nini?"
Babu alikuwa na furaha sana siku hiyo, alinishika mabegani na kuniambia
"hawa wote wapo eneo hili kushuhudia msichana wa kwanza akikabidhiwa
mamlaka makubwa na mazito ndani ya Gamboshi haijapata kuwahi kutokea tangu
kuumbwa kwa ulimwengu msichana aliyechaguliwa na mkuu mwenyewe wa ulimwengu
huu. hakika ni furaha iliyoje kwa ukoo wangu na watu wote wa Matonde" babu
alicheka sana. Alicheka, akacheka kupitiliza. mimi nilijisikia ufahari
kuona kila mtu akicheza na kunisujudia mbele yangu. Watu walikuwa ni wengi
sana. Wengi walikuwa wamefunika sehemu zao za siri na ngozi ya mnyama. Fisi
na wanyama wengine nao walikuwepo kila nyuso iliyokuwa mahali pale
ilionesha uchangamfu na furaha iliyoje nilicheka usoni na moyoni tabasamu
likachanua hakika. kikaja kiumbe cha ajabu. Kiumbe kilichotetemesha
Gamboshi nzima.
ulikuja upepo ukavuma kwa muda mrefu sana. Kabla ya kusikika kelele za hapa
na pale, kulikuwa na radi iliyopiga na kutoa cheche kutoka kila kona ya
sehemu zote za Gamboshi. Ufinyu wa mwanga haukuwepo tena, kiumbe hicho
kiling'aa sana. Kilikuwa ni kiumbe kirefu na kikubwa sana. Kila kiumbe
hapo Gamboshi kilisujudu mbele ya kiumbe kile, hata babu pia. Mimi
sikufanya chochote kwakuwa nilikuwa nimekalishwa mbele ya kiti pembeni na
ambacho angekaa yeye kiumbe huyo. Alikuwa na macho yaliyong'aa sana. Mfano
wa macho yake yalivyong'aa ni sawa na paka uliyemmulika gizani sehemu za
machoni. Hakuwa na macho mawili, jicho moja tu tena lilining'inia juu ya
paji la uso. Mdomo wake ulikuwa mkubwa sana na kichwa chake kilikuwa kama
ndege aina ya korongo. Wote waliosujudu waliongea vitu ambavyo haikuwa
rahisi mimi kufahamu walizungumza nini. Lakini waliongea lugha ya tofauti
na Kiswahili na wala haikuwa kiingereza. Niliendelea kuwatazama, wakati
kiumbe yule wa ajabu mwenye mwili wa nyoka sehemu ya chini ya kiuno chake
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
baada ya kiwiliwili cha juu , kukaa sehemu aliyoandaliwa. Yeye alivaa joho
la rangi ya dhahabu. Dhahabu iliyong'aa sana. Hata viatu vyake vilikuwa ni
dhahabu tupu. Alikuwa anatoa ala za muziki kila atembeapo. Ala zile
zilipendeza sana kuzisikiliza. Kichwani alikuwa na taji la dhahabu
lililomeremeta sana. Alishika kitabu Fulani kikubwa ambacho sikukifahamu.
Alionesha kuwa na furaha sana. Alipokuwa akinitazama muda wote, alikuwa
akicheka kwa furaha.
aliliita jina langu huku akicheka
"Bella"
kabla sijageuka kukitazama kile kiumbe, eneo lote la Gamboshi likalipuka
kwa makofi yaliyokuwa yakipigwa kila kona ya mkutano huo. Niliogopa sana
kukaa karibu na kile kiumbe. Kikiongea kilikuwa kinatema moto
nikamfananisha na zile katuni za dragoni. Mwili wote ulijaa jasho kwa uoga.
Kile kiumbe kilitamka
"usiogope mwanangu Bella"
kikacheka sana, kisha kiumbe kile kikaendelea kuniambia
"mimi ni mkuu wa wakuu wa ulimwengu huu. Mimi ndiye baba wa wababa wa
vizazi vyako vyote vilivyopita. Mimi ndiye niliyekuandaa wewe kuja kurithi
falme atakayoiacha Babu yako Mzee Matonde, mimi ndiye Lucifer mtakatifu
kuliko wote awaye"
nilshituka kwa mshangao ambao sikutarajia. Sikuzimia kutokana na hali kuwa
mbaya eneo hilo. Macho yangu yalipokuwa yakielekea eneo la usingizi mzito
wa kupoteza fahamu, mimi nilishindwa kuzimia kutokana na uoga.
Nilimkodolea macho.
Sikuamini ambacho kilikuwa kikitokea kwa wakati huo, Niliona kama ndoto.
Kiumbe kile kikabadilika kikawa binadamu aliyevutia sana. Alikuwa ni mzuri
kuliko mvulana mzuri yeyote ambaye uliwahi kumuona duniani.
Hakikutisha tena.
kila kiumbe katika mji wa Gamboshi kilipiga kelele. Yule kiumbe wa ajabu
akafura kwa sifa kwa heshima aliyopewa.
Alisema
"ninao utajiri wa kutosha pamoja na nguvu nyingi. Mimi si mchoyo kwa yeyote
aniombaye. Hutoa vipawa na karama kwa kila mtu anifuataye. Mimi humbariki
kila mmoja lakini kuna adhabu kali kwa yeyote akiukaye maagizo yangu"
nilimuona yue mtu aliyejiita Lucifer, akiwa amefura kwa hasira na uso wake
kujikunja sana. Hakika alikuwa na hasira na ghadhabu sana. Mimi sikuwa
nikimsikiliza kwa umakini ila niliogopa sana kwa kuwa sikuamini kama
nimekaa karibu kabisa na yule wanayemuita shetani. Niliwaza mengi sana.
Nilitetemeka kwa uoga lakini haikusaidia.
labda nikuambie kitu. Huyu kiumbe ndiye yule aliyewahi kuwa mmoja wa
malaika wakuu huko mbinguni. Yeye alikuwa na kazi ya kumsifu na kumuimbia
mungu.
Aliitwa Lucifer.
baada ya kujiona yeye ni mmoja kati ya malaika walioumbwa vizuri kuliko
malaika wote, akapatwa na kiburi. Kiburi cha kutaka kumpindua mungu. Kama
utakumbuka mwanzo wa safari yangu ya huku Gamboshi, nilimuuliza babu kuhusu
ule mji ambao niliuona kwa mbali ukiwa unang'aa na kupendeza. Akaniambia
kuwa ule si mji mzuri kufikiria wala kutamani kuingia. Akasema kuwa kule
ndipo alipokuwepo mkuu wao hapo mwanzo. Basi eneo lile naweza kusema ndio
mbinguni na yeye Lucifer akatupwa ulimwenguni katika ziwa la moto. Kutokana
na adhabu kuwa kali, aliapa kuondoka na kila mwanadamu wa kumdanganya. Ila
kipindi hiki ambacho nilikuwa Gamboshi sikuweza kuwa na ufahamu wa kutosha.
Hivyo niliendelea kukaa nikifurahia utukufu niliopewa. Watu walianguka
miguuni mwangu kwa kusujudu. Nilijisikia ufahari sana. Sikujuwa kuwa
nilifungwa ufahamu wangu.
yule kiumbe wa ajabu akaendelea.
"leo nitakukabidhi utawala wa babu yako. Utawala wa kusimamia Gamboshi na
kushika wadhifa mkubwa Duniani. Utakuwa mtu wa heshima hapa na huko
duniani. Utajiri utakutafuta na si kuutafuta kwa jasho. Mdomo wako utakuwa
Baraka kwa kila ukinenacho na kukitamka. Laana iwe juu ya kila mtu
atakayekulaani"
babu alisogea mbele yangu. Babu alikuwa amevaa joho la rangi ya zambarau
pia, kama gauni langu. Alikuwa amevaa taji kubwa kichwani mwake. Alishika
fimbo mkononi.
yule kiumbe wa ajabu alipomuona babu, alicheka kwa sauti kubwa sana.
hakucheka kwa karaha bali fedheha. Hapa nikagundua mbali ya ubinadamu
halisi hakuna kiume kilichocheka kwa kumaanisha furaha halali. Babu
alilivua taji lake na kunivisha mimi, pamoja na kunikabidhi pete yake.
Fimbo yake pia alinipatia; yule kiumbe wa ajabu akapaza sauti
"nakukabidhi rasmi utawala wa babu yako. Utawala uliotukuka Gamboshi na
ulimwenguni kote. Upate heshima nchini mwako na nje ya nchi. Uwe na utajiri
wa kutosha kwa kutumia pete hiyo. Fimbo hiyo itibu kila ugonjwa
utakaosumbua kila mtu akuombaye msaada, taji hilo uwe malkia wa ulimwengu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mzima lakini hayo yote ni baada ya kutimiza masharti haya nikupayo"
alinyamaza kwa muda kabla hajaendelea. Babu alinitazama kwa jicho la
huzuni. Sikujua ilikuwa hivyo kwanini.
Fimbo hiyo itibu kila ugonjwa
utakaosumbua kila mtu akuombaye msaada, taji hilo uwe
malkia wa ulimwengu mzima lakini hayo yote ni baada ya
kutimiza masharti haya nikupayo"
alinyamaza kwa muda kabla hajaendelea. Babu
alinitazama kwa jicho la huzuni. Sikujua ilikuwa hivyo
kwanini. Mimi nilitabasamu kumpa moyo babu kuwa
ningeyaweza yote ambayo ningeambiwa. Yule kiumbe wa
ajabu, alikohoa kisha alizungumza.
"masharti hayo ni kwamba tunamuhitaji yule mpenzi wako
kama kafara. Ndugu jamaa na raiki zako hapa Gamboshi
wanywe damu yake na kuila nyama yake katika sikukuu
ya kukabidhiwa utawala wako" nilifahamu kuwa huyu
kumbe alikuwa akimaanisha Jordan. Nilinyamaza
kumsikiliza. Aliendelea
" Pia usiongee na mtu yeyote kwa siku nzima mara
utakapoamka leo ukitoka hapa Gamboshi. Usithubutu
kulowa maji kwa muda wa siku tatu ikiwa mvua ama
kuoga kufanya hivyo utatoa utawala wako katika koo
nyingine na adhabu yako itakuwa ni kuongea milele na
kutoa siri zako ovyo kwa yeyote hata usiyemfahamu.
Wewe na maji mtakuwa maadui mpaka unakufa"
sikukubali haraka. Mkutano mzima ulikuwa kimya kusikia
kama ningekubali kufuata masharti ya kiumbe huyo wa
ajabu. nilinyamaza kimya kwa muda. Babu aliuinua uso
wake na kupaza sauti "Bella mjukuu wangu tunasubiri jibu
lako ili tuweze kutawanyika"
niliendelea kunyamaza. "na kama hutajibu leo, usitarajie
kuamka milele siku ya kesho ukitoka hapa Gamboshi"
nikaipata sauti yangu kwa uoga wa kitisho cha kiumbe
huyo wa ajabu nikasema. "nitatimiza kila ninalopaswa
kulitimiza" mkutano mzima ukalipuka kwa shangwe. Kila
mtu alifurahi sana, furaha ikazidi kupitiliza. Babu
alipongezwa kwa kuimaliza kazi, kazi ya kunikabidhi
mikoba. Kazi iliyomchukua muda mrefu kuikamilisha. Kazi
iliyopingwa na mama kwa muda mwingi, sasa ikawa
kama kumsukuma mlevi. Kile kiumbe kikapotea kikiwa na
furaha ya ajabu. Niliwaona wale wachawi wa Gamboshi
wakila na kunywa. Nilipotoka kitini na kwenda kujumuika
nao, nilistaajabu sana. Nilistaajabu kuona wakinywa damu
ya binadamu kwa furaha wakitafuna nyama ya mtu. Babu
alinipongeza kwa kuniambia kuwa "umefanya jambo zuri
sana" alinikabidhi nyama ya mtu ambayo niliikataa.
Sikuwa mzoefu ghafla kiasi hicho kuanza kula nyama ya
binadamu mwenzangu. Ila kutokana na jinsi ilivyochomwa
na babu alivyonilazimisha niinywe, nilijishangaa nikikakata
pande na kulitia mdomoni. Ama kweli ndio maana
tulikatazwa tusimle binadamu mwenzetu. Nyama ilikuwa
ni tamu kupitiliza. Hakuna mnyama yeyote iwe wa
kufugwa ama wa porini, aliupita utamu wa Binadamu. ila
babu alilinisisitiza sana nisifanye kosa katika masharti
niliyopewa
"nitakuwa sina jinsi ya kukusaidia katika hili ukifanya
kosa. Kwa kuwa umekubali mwenyewe" aliniambia
"Hakikisha unatimiza yote uliyoambiwa"
nilimkubalia babu huku moyoni nikiwa na jambo
ninalolifikiria. Mawazo yangu moyoni, hayakuwa juu ya
utawala wala wadhifa niliokabidhiwa. Mawazo yangu
yalikuwa kwa Jordani. Sura ya Jordani ilikuja kwenye akili
yangu na kunipotea kila nikikumbuka sharti nililopewa na
yule kiumbe. Jordan mwanaume niliyempenda kuliko kitu
chochote katika hii dunia. Sikutaka nimpoteze Jordani, si
kwenye kifo hata kwa mwanamke mwingine. Ndio maana
nikachuma bibo kutoka katika mti wa mkorosho
nyumbani, nikajichora jina lake 'JORDANI' kwenye mkono
wangu kwa kutumia utovu wake. Nilimpenda sana Jordan
baada ya mama yangu. Sharti hilo ndio nililiona lingekuwa
gumu kuliko yote niliyopewa hapo Gamboshi. Nikiwa bado
Gamboshi kila mtu alipepesuka kwa ulevi wa furaha.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tulirudi lile eneo ambalo mimi na babu tulibadilishia nguo.
Nilizivua zile nguo abazo zilikuwa maalumu kwa ajili ya
shughuli ile ya kukabidhiwa mamlaka na nguvu, kisha
nikazivaa zile nilizokuja nazo. Babu akanieleza kitu cha
ajabu sana aliniambia
"Bella nimeitumikia Gamboshi kwa muda mrefu sasa.
Inabidi nilipe fadhila kwa kila jambo walilonifanyia nikiwa
duniani. Miaka yangu ya kuishi duniani ilishakwisha muda
mrefu sana, ila niliongezewa muda wa kuwakabidhi wewe,
urithi mamlaka yangu. Sasa ninatakiwa kuja kuishi huku
Gamboshi nikipewa nafasi nyingine baada ya wewe
kuikaimu nafasi yangu. Nitaishi huku Gamboshi mpaka
wakati wangu wa kuishi utakuwa umekwisha kabisa"
nilishangaa sana. Sikujuwa kama kumbe kuna miaka ya
kuishi duniani na miaka ya kuja kuishi huku Gamboshi.
Nilimuuliza babu hii inakuwaje. "sijaelewa kabisa" babu
alinieleza
"kwa sisi huku Gamboshi tunaishi miaka nusu kwa nusu
nikimaanisha kama duniani ulitakiwa kuishi miaka
themanini, utaishi arobaini duniani arobaini huku
Gamboshi. Kwa hivyo wakati mimi naanza kuhiji huku
Gamboshi nilipimwa na kugundulika nina miaka mia na
nne ya kuishi duniani" nilishituka, macho yakanitoka pima.
babu akaendelea
"hivyo ndio maana nimeishi miaka sitini duniani na
iliyobaki yote nitakuja kuishi huku Gamboshi"
hapo nikawa nimemuelewa babu. Tulipomaliza
kubadilisha nguo babu aliniambia kuwa nisimueleze mtu
yeyote, ila siku chache zijazo atalala usingizi wa milele
akiwa kitandani kwake. Hivyo nisishitushwe na hayo
yatakayotukia kwa sababu ni lazima yatukie.
Nilitamani kulia lakini alinieleza "mjukuu wangu mimi na
wewe tutakuwa tunaonana mara kwa mara hivyo
usiogope" nilijipa moyo kwa kutabasamu kinafki. Nilikuwa
nimeshamzoea Babu. Ubaya wake sikuuona tena na
nilimpenda sana. Nilihisi kuupenda uchawi zaidi kwa
kipindi hiko, ila kila nikifikiria kuila nyama ya mwanaume
nimpendaye, niliona ni jambo gumu sana kulitimiza. mimi
na babu tulitoka Gamboshi tukarudi katika ulimwengu wa
kawaida. Babu aliishi magomeni usalama mimi nilielekea
Sinza nyumbani nilipobakia mimi na Mzee Nyegezi baada
ya mama kufariki.
..........................
Nilijikuta nipo kitandani Mzee Nyegezi alikuwa
akiniamsha. Nilipiga ukunga mkubwa sana
"haiwezekaniiiiiiiii!!!" Mzee Nyegezi aliruka pembeni na
kuniacha. Niliendelea
"siwezi kumuua Jordani" nilipoamka kabisa niliuona
mshituko wa dhati wa Mzee Nyegezi.
aliniuliza "una tatizo gani" Nilinyamaza. Nilinyamaza kwa
kuwa nilikumbuka sharti nililopewa Gamboshi. "usiongee
na mtu yeyote mara kutapokucha baada ya kutoka hapa
gamboshi" sauti ya yule kiumbe aliyejitambulisha kama
Lucifer, ilijirudia kichwani mwangu. Mzee nyegezi
hakutoka hata nilipokuwa nimenyamaza muda wote.
Niliushika mdomo wangu wa uoga nikijiuliza kama, Mzee
nyegezi alisikia nilichoropoka, ama hakukitilia maanani.
"Bella una nini? Umeanza kupiga kelele muda mwingi
sana. Tangu usiku mimi sikulala kabisa" Aliposema hivyo
nilijiuliza, hivi mbona Gamboshi nilichukuwa muda mrefu
katika kila jambo lililotokea kule? sasa iweje Mzee
Nyegezi ahesabu kama ilikuwa ni siku moja tu?
nikajisahau nikamuuliza swali.
"kwani nimelala kwa muda gani?"
"sasa hivi ni saa tatu asubuhi na ulilala jana mapema
hata chakula cha usiku hukula"
nikakumbuka hapo hapo kuwa nimeshavunja sharti moja
wapo kati ya yale niliyopewa kule Gamboshi. Nililia sana
hata Mzee Nyegezi asijue nilikuwa nalilia nini. Nilimpiga
kikumbo mzee nyegezi na kuelekea chooni kunawa uso
huku nikiwa nalia. Chooni ndipo nilikutana na babun Babu
alikuwa akilia na yeye pia. Alilia machozi mfano wa damu.
Aliniuliza
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"ina maana mjukuu wangu yote niliyofanya kwako
yamekuwa ni bure kabisa?"
nilikabwa na kitu kooni hata nikashindwa kuongea nililia
kwa uchungu ambao sikuwahi kuupata tangu nijitambue.
Nilimuomba babu msamahan "nisamehe babu. Naomba
uniombee anisamehe mkuu wa Gamboshi" Babu alinivunja
moyo kabisa, aliniambia. "tazama jinsi Gamboshi
ilivyohuzunika, tazama kwa macho yako" kwa kuwa ukuta
wa choo chetu ulikuwa mweupe sana ikawa kama sinema
nilipotazama aliponioneshea kwa kidole. Ilikuwa ni taswira
ya Gamboshi.
Mkuu wa Gamboshi ambaye ni yule Lucifer, alikuwa
amekasirika sana. Babu alinionesha hadi kwenye makazi
yake alipokuwa akiishi yeye lucifer. Kutokana na hasira,
alikuwa akibadilika kila mnyama. Moto ulimtoka mdomoni
kwa hasira iliyomzidi na kushindwa kujizuia kupunguza
hasira zake. Hakika nikagundua nimefanya makosa
makubwa sana.
babu alinieleza "kuanzia sasa umepokonywa utawala na
wadhifa wako wote umevuliwa kutoka Gamboshi.
Hutakuwa na nguvu zozote, bali utakuwa na uwezo kama
wa mchawi yeyote yule." babu alinyamaza kisha
aliniangalia kwa huzuni. Mimi nilikuwa nalia sana, hata
macho yalifumba kwa machozi. babu aliendelea "sijajua
mkuu atakupa adhabu gani ila amekasirika sana sina cha
kukueleza" babu akatoweka kabla sijamueleza chochote.
siku hiyo nikawa nimeianza vibaya. Mzee Nyegezi
hakuthubtu kuniuliza kitu kingine niliporudi chumbani na
kupishana naye kibarazani. Alikuwa akinitazama tu,
alipokuwa akielekea nje. Nilipokuwa chumbani, nilikaa
kimtegomtego, nikimtegea babu nikidhani labda ningesikia
ujio wake. Upepo ungevuma, kama siyo radi ingepiga
baada ya mngurumo wa kutisha. Nilitamani kujua
chochote kutoka Gamboshi. Niliumia sana kuukosa
utawala niliokabidhiwa. Nikamuona mzee Nyegezi ni mtu
mbaya sana kwangu. Nikamchukia kwa kuniamsha
asubuhi na kunifanya nizungumze. Kuzungumza kule
kulinifanya nivunje sharti. Moyo uliniuma kila nilipofikiria
kuona kuwa sharti dogo nililodhani ningeliweza, kumbe
hilo ndio lilikuwa gumu sana kwangu. Niliutamani tena
ukuu na uwezo niliokabidhiwa kutoka katika kiti cha urithi
wa babu. Mawazo yakanisonga, mawazo yakanifanya hata
nisahau kufanya mambo mengine. Kwa sababu ya
mawazo, nilisahau hata kula wala kupika. Kwa sababu ya
mawazo, sikujua nilijilaza kwa muda gani hapo kitandani
kichwa changu kikielea juu ya kidimbwi kidogo cha
machozi. Kwa sababu ya mawazo, mawazo yakawa
mawazo, nikapitiwa tena na usingizi. Niliamka saa nne ya
usiku, tena si kwa kupenda ni Mzee Nyegezi ndiye alikuja
kuniamsha. Alipatwa na wasiwasi jinsi nilivyolala. Nililala
tangu jana mapema, lakini nilichelewa kuamka.
Aliponiamsha saa sita mchana nilimuacha chumbani na
niliporudi chumbani niliendelea kulala mpaka sasa.
alizungumza na mimi kwa upole "Bella kama unaumwa
sema. Kukaa kimya si vizuri" mimi sikumjibu kitu.
Nilimchukia sana Mzee Nyegezi. Nilimuona Mzee Nyegzi
hakuwa akinitakia mema. Alining'ang'ania kunibembeleza
mpaka nilipoamua kuzungumza. "siumwi nipo sawa"
nilimjibu kwa dharau sana. Lakini hakuweka ukali katika
sauti yake. "sasa kwanini unalala lala oyo? Jana umelala
saa moja jioni. Nimekuja kukuamsha leo saa sita mchana,
nashitushwa kukukuta umelala tena. Umekula nini leo?"
niliendelea kumjibu kwa dharau nikibetua midomo yangu
kama shangingi.
"ningesikia njaa ningeamka kupika" aliendelea "najua
unajisikia vibaya kutokana na kifo cha mama yako,
hakuna ambaye hajaguswa nacho. Tafadhali Bella usiwe
mnyonge kiasi hicho nipo hapa kwa ajili yako" alitoa noti
tano za elfu kumi na kunipatia baada ya kunibusu.
Nilimsonya na kujilaza tena kitandani.
nikiwa nimejilaza huko, kile ambacho nilikuwa nikikisubiri
tangu mchana nilikisikia kikinijia. Ilikuwa ni sauti ya
upepo mkali sana. Mngurumo mkubwa wa radi, ulisikika
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kila pande. Tetemeko la ardhi likatokea katika chumba
changu na kukipasua chumba changu katikati. Wakati
hayo yakitokea. Mlango wa chumba changu ukafunguliwa.
Alikuwa Mzee Nyegezi.
aliniambia "pipa halina maji hata kidogo, hakikisha
unayakinga haya ya mvua kisha urudi tena kulala" wakati
akiyaongea hayo, mimi nilikuwa nikipatazama pale
palipopasuka. Kulikuwa vile vile na moshi mzito ulikuwa
ukifuka kutoka katika shimo hilo. Nilikuwa nikimuangalia
Mzee Nyegezi, hakuonesha kama aliona kile ambacho
mimi nilikuwa nikitazama. Niljifanya kumskiliza kwa
makini na kumkubalia alichoniagiza.
Alipoondoka nilijiuliza. Nilijiuliza ina maana hakuona
kilichotokea chumbani kwangu? Chumba changu
kilipasuka na kuweka mfano wa bonde la ufa. Ndani yake
akatokea kiumbe aliyetisha sana. Nilianza kutetemeka
kwa uoga uliopitiliza. Kiumbe huyo alikuwa na uso wa
babu, Mzee Matonde. Babu alikuwa akilia machozi ya
damu. Sikujuwa machozi hayo yalikuwa yakimaanisha
nini. Mara kwa mara babu alikwa akilia hivyo. Alikuwa na
mwili wa mnyama. Babu alikuwa na mwili wa fisi, fisi
mwenye miguu mikubwa sana kama ya tembo. Fisi huyo
hakuwa wa kawaida. Alikuwa na mabawa kama ndege na
meno marefu kama ngiri. Shimoni alipotoka, kulikuwa
kukifuka moshi mzito sana. Moshi huo ulisindikizwa na
harufu kali ya uvundo. Joto la chumbani lilizidi na
kunifanya nihisi kama nipo karibu na moto mkali wa
jikoni. Nilivuja jasho japo sikujua lilikuwa ni jasho la
uwoga ama hili la joto kali.
Kiumbe kile kikapata sauti yake iliyotisha. "mjukuu
wangu" nikajuwa kuwa alikuwa ni babu
"kesho asubuhi utapata habari za msiba wangu. Lakini
hakikisha mwili wangu haufanyiwi maombi wala kuagwa
na watu wengi." nilishitushwa na habari hizo. Japo
nilikwishajua kiumbe yule ni babu, sikuwa na uhuru nafsini
mwangu. Alikuwa akitisha sana. Nilimuuliza
"kwanini hayo?" akaniambia "mimi nitakuwa sijafa ndiyo
sababu ya kukueleza ufanye hayo"
"sasa babu, mimi nitawezaje kuzuia watu wasiuage mwili
wako au wasiuombee?"
Aliniambia "nitakupa uwezo huo wa kuongea chochote
ukakubalika bila kupingwa kwa swali lolote" hiyo
iliniduwaza pia nilikubali bila kumpinga. Nilimuuliza babu
kwa kuropoka "babu"
alikuwa tayari anataka kuondoka, akasimama alipokuwa
akitaka kuingia shimoni alipotokea.
"Nataka kufahamu mkuu anasemaje?" akanijibu
"tutazungumza baada ya msiba wangu"
kisha babu alidumbukia shimoni humo. Mzee Nyegezi
alikuja tena chumbani kwangu
aliniuliza kwa ukali "bella umekuwa na tabia gani sasa
hivi?" nilishitushwa na swali hilo mara tu alipoingia.
"kwanini baba" akanijibu kwa hasira "si nilikueleza uamke
ukinge maji"
nilishangaa sana ile hali. Ni kweli mvua ilikuwa kubwa,
lakini cha kushangaza mara tu babu alipotoweka, mvua
ilikatika. Hata lile joto lililonivujisha jasho jingi, likapotea.
Nilimjibu baba
"si imeshakatika?" akaniamba "sasa nataka kesho uamke
mapema ukakinge kwa mama Tunnu" nilimkubalia na yeye
akaondoka. Nililala kwa usingizi wa mang'amung'amu.
..........
Hata asubuhi ilipofika, bado sikujuwa nililala saa ngapi.
Mzee Nyegezi, alikuja mbio chumbani kwangu "Bella
amka... we Bella.. bella" alikuwa amevaa singlendi na
bukta nyepesi. Niliogopa sana. Nilijifuta uso kutoa
tongotongo kwa kiganja cha mkono.
alikuwa ameshika simu "shangazi yako anataka kuongea
na wewe" Baba alikuwa na wasiwasi sana. Ila niliipokea
simu kutoka kwake na kuongea "shikamoo shangazi"
nilichokisikia kutoka upande wa pili, sikutamani kusikia
mara ya pili. Ilikuwa ni sauti ya shangazi akiwa analia.
Alikuwa analia huku akimtaja babu. Ndipo nilipomuuliza
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"shangazi kuna nini kwani? Babu kafanya nini?" kwa sauti
ya kilio alinijibu "babu yako amekufaaa Bella" shangazi
aliongea kwa huzuni sana "Bella babu yako Mzee Matonde
amekufa kiajabu mwanangu. Mzee Matonde kipenzi
chako. Kwanini sisi. Kwanini Bellaaaa"
simu iliniponyoka na kudondoka chini. Midomo yangu
ilianza kucheza shere kwa kugongona gongona ya juu
ikaipiga ya chini. Nikabubujikwa na machozi. Mzee
Nyegezi alikuwa akinitazama muda wote, sasa
alinisogelea. "pole Bella" aliniambia kwa sauti iliyopwaya.
mimi nililia sana, kwasababu babu Mzee Matonde hakufa.
Ukweli nilioufahamu kuhusu babu, uliniongezea
machungu. Hicho ndicho kilichoniumiza sana.
nikakumbuka babu alivyoniambia jana usiku "kesho
asubuhi utapokea habari za kifo changu. Hakikisha mwili
wangu hauombewi wala haugwi na watu wengi" ilinibidi
nifanye haraka kuelekea alipokuwa akiishi babu, si mbali
sana na nyumbani; Japo ilinilazimu kupanda gari kwanza.
Mzee Nyegezi naye alitoka chumbani na kwenda
kujiandaa aliniambia "nitaelekea kwanza ofisini, kisha
nitakuja baadaye msibani" nikajibu "sawa" nilizivua nguo
zangu nikajitundika taulo langu safi jeupe. Nikachukuwa
sabuni na kwenda kuchota maji kwenye jaba lililopo jikoni.
Nilipomaliza kujipimia maji niliyoona yanatosha, niliinua
ndoo yangu mswaki mdomoni na kuingia bafuni. Nilianza
kwanza kupiga mswaki. baada ya kumaliza kupiga
mswaki, nikalivua taulo langu na kuliweka pembeni.
Nikausahili mwili wangu kwenye kioo kilichopachikwa
ukutani. Hakika niliumbika. Ukubwa ulioanza
kuninyemelea ukanitunisha mapaja yangu na kuwa
mrembo haswa. Nikatabasamu kidogo kisha nikairudia
ndoo yangu ya maji. Nilichota kopo moja la maji ile
kujimwagia tu usoni, nilianza kuwashwa. Sikuanza
kichwani, kwasababu kama ujuavyo wanawake
kujimwagia maji kichwani kwetu ni sumu. Uso ulianza
kuwashwa sana, mara ukafuatia mwili mzima. Niliwashwa
kupitiliza kama nimejimwagia upupu. Nikawa najikuna
hapa, mara pale. Chini ya matiti yangu, mara mgongoni.
Kucha pekee hazikutosha. Nikajipeleka ukutani. Najikuna
lakini wapi. Muwasho ukazidi. Nikaendelea kuwashwa
zaidi. Muda wote huo sikushituka mapema kama nilikuwa
sioni kitu chochote. Sikujuwa kama macho yangu
yalikuwa yamefumba. Sikujuwa kama nilikuwa nikitembea
kwenye giza nene.
Chini ya matiti yangu, mara mgongoni.
Kucha pekee hazikutosha. Nikajipeleka ukutani. Najikuna
lakini wapi. Muwasho ukazidi. Nikaendelea kuwashwa
zaidi. Muda wote huo sikushituka mapema kama nilikuwa
sioni kitu chochote. Sikujuwa kama macho yangu
yalikuwa yamefumba. Sikujuwa kama nilikuwa nikitembea
kwenye giza nene.
"nimekuwa kipofu" nilijiuliza kwa uoga. nikapapasa
ukutani kwa shida na kulitwaa taulo langu. Nikajifunga
mpaka eneo la kifua na kulifanya liwe fupi kidogo. hapo
hapo nikausikia mguso wa mkono ukiugusa mgogo
wangu. Niliuputa ule mkono kwa uoga na kugundua
ulikuwa ni mkono wa mnyama. Mkono ulikuwa na
manyoya manyoya kila sehemu. Nilipiga kelele za kuomba
msaada "baba nakufaaa" sauti yangu haikufika popote
kumbe aikuwa ni babu. Nilimgundua ni yeye baada ya
kunitibu na kupata kuona tena. Alinitibu kwa kunishika
macho yangu huku akiongea maneno Fulani ambayo
sikuyaelewa kwa urahisi. Alikuwa akiyafikicha fikicha
baada ya kupaka mate kiganja chake. baada ya kufumbua
macho, niliona mwanga mkali sana. Kisha ukapotea. babu
aliniuliza. "umefanya nini?"
sikumuelewa babu alimaanisaha nini hivyo ilinibidi
nimuulize. "babu kuna nini?"
babu hakunijibu chochote. Aliniangalia kwa huzuni kisha
linionesha kwa kidole chake katika kioo. Ilikuwa ni taswira
ya Gamboshi. Hapa alinionesha ile siku ambayo nilikuwa
nikikabidhiwa mamlaka yake. Yule kiumbe wa ajabu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alikuwa akinipa masharti ya kuyafuata.
"hakikisha maji hayagusi mwili wako, iwe ya mvua ama
ya bomba. Iwe hivyo kwa muda wa siku tatu" hapo
nikalijua kosa langu. Sikuongea chochote mbele ya babu.
Nilitazama chini kwa aibu. babu aliniuliza tena. "Bella
kama hukuwa tayari, kwanini ulikubali kupewa masharti
haya?" nililia "babu nisamehe" babu alinikatisha kwa sauti
ya ukali "nikusamehe? Nikusamehe vipi?" alikuwa
amekasirika sana. kadiri babu alivyokuwa amekasirika,
ndipo alikuwa akiongezeka urefu. Alikuwa mrefu.
Akaongezeka zaidi. Alikuwa mrefu kupitiliza hata unyayo
wa miguu yake tu, ndiyo iliyobaki bafuni. Vidole vyake
vikagusa bati na kulitoboa kabisa. Kisha alirudi kwa
nguvu za ajabu. Alikuwa akitoa moto alipokuwa akirudi
katika hali yake ya kawaida. Alikua kama yule muhusika
wa kwenye filamu ya ghost rider. akaniambia kwa sauti
iliyotetemeka "umeniuzi sana, umemuuzi mkuu. Siwezi
kusema nimekusamehe ikiwa sio mimi niliyekupa yale
masharti." hapo akaacha kuongea kwanza. Alikohoa,
akakohoa sana kama aliyepaliwa na chakula. Akaniambia
"acha niende. Nimekuja kukuponya upofu ulioupata ili
uende katika msiba wangu ukawaonye wasiuombee mwili
wangu" aliniangalia kwa huzuni kisha aliniambia "Bella
una kazi ngumu na adhabu kali mbele za mkuu" babu
alitoweka kisha akauacha moshi mzito sana bafuni.
Sikuoga tena Nilitoka bafuni na kurudi chumbani. Nilivaa
nguo za kawaida tu ndani kisha nilijitanda kanga mbili za
aina moja. Hatimaye nilitoka kulekea msibani. eneo la
msiba lilifurika watu wengi na kujaa simanzi nzito. Rafiki
zake babu walikuwepo ndugu na wengine ambao
sikuwafahamu, wote walikuwa wana huzuni kubwa. Ndugu
waliponiona walilia kwa sauti ya juu sana. Naweza
kusema kwa upande wa baba yangu mzazi, babu
alinipenda sana mimi kuliko hata watoto wake aliowazaa.
Alinipenda kuliko kitu chochote au mtu yeyote. Hakuna
mtu ambaye alikuwa hajui kwamba babu alikuwa
ananipenda kiasi kile. Tuliingia chumbani ilipo maiti ya
babu ikioshwa.
shangazi mkubwa aliyebaki, akasema "hajafa katika
mapenzi ya mungu. Hapa kuna jambo. Inabidi tumuite
mchungaji kabla hajazikwa" mimi niliogopa sana. Sauti ya
babu ikajirudi kichwani mwangu kama mwangwi.
"hakikisha mwili wangu hauombewi" Nikapata nguvu ya
kuzungumza "hapana shangazi. Huyu asiombewe wala
kuagwa ninaomba iwe hivyo"
sikuwa na hakika kama shangazi angekubali kile
nilichomueleza kwa sababu aliniangalia kwa jicho kali
sana kisha alisema. "Bella!?" alinishangaa kwa tuo. Mimi
macho yalinitoka nisijue nitafanya nini akaendelea.
"kwanini hutaki babu yako asiombewe, wala kuagwa?"
Nilijua ni lazima mtu yeyote angeuliza swali kama hilo.
Mtu yeyote mwenye akili timamu, angeniona kama
niliyeanza kurukwa na akili. Hivyo nikashikwa koo na
kigugumizi cha ghafla. Kigugumizi nisijue nitajibu nini? Si
shangazi pekee aliyeshangazwa na jambo hilo! Hata mimi
pia sikuelewa nilipoambiwa kwa mara ya kwanza. Mimi
pia nilijiuliza sana, kwanini mwili wa babu usiagwe wala
kuombewa?. "mimi sijafa katika mpango sahihi, Hivyo
katika kuagwa huko, kuna watu ambao wanaweza kutoa
siri kuwa mimi sijafa na sipo katika lile jeneza"
nikaikumbuka sauti ya babu. Nilichoambulia kukifahamu
kutoka kwa wachawi, yaani wanapoua mtu kabla siku
zake za kufa hazijafika, basi humchukuwa na kwenda
kumuhifadhi sehemu ambayo humtumikisha kazi nyingi
sana. Kama vile kulima shamba kubwa sana, ambalo
huchosha hata kikundi Kikubwa cha watu lakini msukule
mmoja hulima ndani ya dakika chache. Hubeba mizigo ya
wachawi au kwenda kuleta damu, baada ya kusababisha
ajali katika barabara kuu iendayo mikoani. Na pale katika
jeneza wanaweka mgomba ambao humuwakilisha yule
mtu ambaye amechukuliwa msukule. Watu ambao
hawana uwezo wa kichawi hawawezi kugundua kama ule
ni mgomba. Bali mchawi pekee au mwenye nguvu kweli
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
za kimungu. Wazazi ndugu jamaa na marafiki zake
marehemu, Wanaweza hata kulia kwa kumshika mshika
kwa huzuni, lakini wasione tofauti yeyote na mwili wa
kawaida. Ila kwa babu hakuwa msukule. Babu alikufa ili
kwenda kuitumikia Gamboshi baada ya mkataba
walioafikiana kutimia. Hivyo alikuwa analipa fadhila.
Fadhila ya kipumbavu, fadhila ya kijinga, fadhila ya
kishenzi kutoa uhai wako kwenda kuishi katika mji wa
kichawi Gamboshi.
Nilipokuwa katika kuwaza nisijue nini nimjibu shangazi.
Ghafla mbele yangu nilimuona babu. Babu alikuwa
akitabasamu. Aliniambia "usijali nitakusaidia" Kisha
alipotea.
nilimgeukia shangazi mara baada ya tukio hilo la
kushitukiza. Nikataka nimjibu, akaniambia huku
akitabasamu. "Bella umeanza kuwa na akili sana
mwanangu" alinishika shika kichwani na kutabasamu kwa
raha. Nilijiuliza shangazi alikuwa akimaanisha nini?
Nilibaki katika bumbuwazi ya ajabu, nisijue nini shangazi
alimaanisha. Aliendelea "basi nitapinga mwili wa babu
yako usiagwe wala kuombewa, ila ni ngumu sana
kueleweka kwa watu timamu"
nilishangaa sana. Kukubali huko kwa shangazi. Lilikuwa ni
jambo la haraka, wakati mimi sikujibu chochote!
Kulinifanya nijiulize maswali mengi. 'babu alitumia kinywa
changu kumjibu shangazi, bila mimi kufahamu? Alimfunga
akili shangazi hata asikumbuke kuwa hilo ni jambo la
kushangaza? Mwili usiagwe wala kuombewa? Ni ajabu na
inayoshangaza?'
mshituko wangu haukuwa na madhara yoyote kwa
shangazi. Hakuniuliza jambo lolote, tukatoka chumba cha
kuoshea maiti ya babu. Ndugu waliokuwa wakisubiriwa
kutoka katika kila pande ya visiwa vya ukerewe. Visiwa
ambavyo babu ndipo alipozaliwa, walikwishafika baada ya
siku tano za msiba baadaye. Shangazi aliwaeleza
nilichomueleza. "naona ni vyema tukamsikiliza kama
alivyosema" nilishangazwa na kaka zake babu,
walivyounga mkono hilo jambo. Ila mmoja aliweka
pingamizi. Hapo ndipo palinigusa, nikataka nifahamu. "ila
nyinyi jamani mbona tunataka tuishangaze jamii?"
alikuwa ni shangazi aliyemfuata yule niliyekutana naye
kule Gamboshi, kuzaliwa. Ndugu wa baba niliwafahamu
kutokana na babu kunitambulisha kwa sauti ya kawaida
bila mtu yeyote kusikia. Babu alikuwa eneo hilo la msiba
bila mtu yeyote kumuona. "wewe dada Suzi embu
nyamaza. Wewe ufahamu kuwa Bella ndiye mrithi wa
mizimu ya ukoo wetu?" nilipigwa na butwaa. Hata hawa
walifahamu kuwa mimi tayari nimekwisha zuru
Gamboshi? Yule aliyemnyamazisha shangazi Suzi,
alinigeukia na kuniambia. "mwanangu sawa tumekuelewa.
Usijali kuhusu hilo, tutafuata kila ulichotuelekeza." kikao
cha familia kikavunjwa baada ya lile nililoliongea
kupitishwa bila kupingwa zaidi. Msiba ulienda kimipango
bila kuvunjika hata moja. Babu akazikwa katika makaburi
ya kigogo mburahati.
.........................................
Baada ya msiba, ndugu wa baba ambao hatukuwahi
kuonana kabisa walijitambulisha kwangu na mimi kwao.
Wengi walipendezwa sana kuniona na mimi sikuzificha
hisia zangu kuwa pamoja nao. Nilifurahi sana. Shughuli
nyingine zikaendelea. Siku moja mimi na baba mkubwa
Christopha tulikuwa nje ya nyumba chini ya mti wa
mchikichi tukizungumza.
Baba mkubwa aliniuliza "sasa Bella ilikuwaje ukavunja
masharti?" kikohozi kikavu kikanipitia. Nilikohoa sana
kabla sijamjibu lolote, aliniambia tena."unafahamu sababu
ya kifo cha babu yako?" nilimjibu kwa wasiwasi. Hii
ilitokana na kudhani kuwa huenda kuwa sababu ya kifo
chake ilikuwa ni siri yangu pekee yangu. Nilimwambia
"hapana sifahamu baba" nilinyamaza kidogo kumeza
mate kisha niliongeza "ninachofahamu ni kifo cha ugonjwa
wa ghafla tu. Nadhani inaweza ikawa ni uzee?" nilijitia
kuuliza swali ili nimchimbe alichotaka kunieleza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
aliniamba yote yaliyohusu kifo cha babu yangu. "babu
yako amejitoa kafara baada ya wewe kushindwa
masharti. Kifo chake kimesababishwa na wewe.
Hakustahili kufa, ila wewe" mshangao ulikuwa wazi katika
macho yangu na uso wangu. Midomo yangu ilitetemeka
sana kwa uoga. Nikamuuliza. "nahisi sijakuelewa baba?"
alitabasamu kwa kejeli na kuniambia "ulipopewa masharti
yale matatu na ukashindwa kutimiza, babu yako
aliambiwa kuwa baada ya siku tatu ungekufa, ungekufa
kinyama. Ndipo alipobatilisha adhabu hiyo na kuongea na
mkuu wake na kuomba adhabu hiyo apewe yeye." bado
nilikuwa nikishangaa nisijue chochote anachonieleza kati
ya hivyo. Nilikuwa gizani, hata babu alinificha. Sikujua
sababu ya babu kunificha jambo kama hilo.
baba mkubwa alinieleza jambo lingine "umewahi kujiuliza
kwanini babu yako hutoka machozi ya damu kila
alipokuwa akikutokea?" macho yangu yakapata nuru ya
ajabu na kuwa na shahuku ya kutaka kujua sababu.
Jambo hilo la machozi ya damu lilinichanganya sana.
Nilijibu kwa shahuku ili nifahamu ilikuwa inasababishwa
na nini. "hapana sifahamu. kwanini alikuwa anatoa
machozi ya damu?" akaniambia "inatokana na..."
ghafla sauti yake ikaishia mdomoni kwake. Nadhani hata
masikio yake mwenyewe hayakuisikia sauti yake vyema.
Hili likanishangaza. Nikamuuliza "baba una nini?"
macho yalinitoka kwa uoga. Yeye alikuwa akijitahidi
kupiga kelele lakini sauti haikutoka. Nilitoa mbio
tulipokuwa tumekaa na kwenda kuwaita ndugu zetu
wengine. Walipofika tulipokuwa tumekaa, baba mkubwa
hakuwepo. Nilishituka sana. Shangazi Suzi aliniuliza
"we Bella! Yuko wapi sasa?" kwa kuwa bado sikuelewa
kilichotokea, niliwaeleza kwa kunyoosha kidole. Mara
nikaipata sauti yangu "alikuu..wa alikuwa hapa jamani"
kila mtu alikuwa katika hali ya kutaharuki asijue nini
kimetokea. "kwani mlikuwa mnazungumza nini na nini
kilitokea" Shangazi Suzi aliniuliza "tulikuwa tumekaa hapa
na yeye alikuwa ananieleza sababu ya kifo cha babu"
kabla sijamaliza kuongea, sauti ya babu ikasikika
masikioni mwangu. "usimueleze yeyote kuhusu ulilosikia"
nilipokuwa nikiitafakari ile sauti. Yule shangazi mkubwa,
aliniuliza "bella una nini? Mbona umenyamaza" Nilimjibu
yule shangazi "alikuwa akinieleza jinsi ambavyo babu
alikuwa akinipenda sana. Alinieleza ambavyo baba yangu
mzazi alikuwa ni mtu wa watu na kifo chake kilisikitisha
wengi"
Ilibidi nidanganye. wengine walifahamu hila zangu na
kuondoka nilipo. Mimi mahali pale nikabaki nikiwa na
shangazi mkubwa na Suzi, wakinidadisi hili na lile. Macho
yangu muda mwingi yalikuwa yakiangalia juu ya mchikichi
huenda angekuwa amebebwa na babu, lakini hakuepo.
Nikatazama njia ielekeayo barabarani labda nilidhani
angekuwa akija, napo kukawa patupu. Wote tukaingia
ndani kwa kuwa tayari ilikuwa jioni. tukiwa tunasimuliana
hadithi mbalimbali, tulishituswa na sauti ya uoga aliyoitoa
shangazi Suzi. Shangazi alikuwa ameenda chooni. Hivyo
alitoka mbio mpaka sebuleni tulipo sisi. Alikuwa na jasho
jingi usoni na uoga uliujaza uso wake. "kuna nini?" baba
mdogo Joseph, alimuliza shangazi. Shangazi alikuwa
ametoka chooni, chupi ikiwa chini, sketi akiwa
ameishusha kama kawaida, macho kayatoa pima. Bila
shaka yale maji maji niliyoyaona yakichuruzika miguuni,
ulikuwa ni mkojo uliomtoka ghafla. Wachache tukamcheka
kwa kuwa shangazi huyu, ndiye alionekana kuwa mtundu
katika familia yote ya watoto wa Babu. "nimekutana na
James chooni" alizungumza macho kayatoa isivyo
kawaida. Alikuwa akituangalia sisi kisha akigeuka
akiitazama njia ielekeayo choooni. Wote kwa pamoja
tukaanza kushituka na kukaa kwa uoga. Wachache
tulisimama kama tulikuwa na ujasiri wa kuelekea chooni
vile.
shangazi mkubwa akauvunja ukimya "chooni?" ghafla
kicheko cha baba mkubwa James, kikasikika kikija eneo la
sebuleni. Nilimshuhudia shangazi Suzi akitaka kukimbia,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
lakini kukawa hakuna njia zaidi ya kuelekea popote. Hivyo
akawa akiwasukuma ndugu wengine. Alikuwa baba
mkubwa James mwenyewe. Alikuwa kama vile ambavyo
nilikuwa naye mchana. Alikuwa akitabasamu kama
hakuna lolote lilitokea. Alinitazama kwa furaha na
kuwaangalia wengine zamu kwa zamu. Kila mtu
alishangaa kwa kujiuliza maswali kadha wa kadha.
Maswali ambayo yalijionesha dhahiri juu ya nyuso zao.
Hakuna ambaye alipata ujasiri wa kumsogelea wala
kuongea naye chochote. Ni mimi peke yangu nilitoka
nyuma ya shangazi yule mkubwa na kumfuata baba
mkubwa Nilimuuliza. "baba mkubwa" kabla sijaendelea
kuongea chochote, aliniziba mdomo na kuniambia
ninyamaze. Alikuwa akitabasamu, hakika alitabasamu kwa
furaha. Baba mkubwa, alizungumza sasa "kwanini
mnaniogopa sasa?" nilimsikia yule shangazi mkubwa
akicheka. Naye alitoka alipo na kumsogelea baba
mkubwa. Alimuuliza "hivi wewe James" hawa walipishana
kuzaliwa. Alianza Shangazi kisha Baba mkubwa james.
shangazi akaendelea "huoni hata mdogo wako ametoka
na chupi chooni kwa uoga?" alikuwa akimuoneshea
Shangazi Suzi. Kwa kweli hakuna ambaye alijizuia
kucheka siku hiyo. Tena walicheka kwa nguvu hata
shangazi akaona aibu. Nadhani hata yeye mwenyewe
hakujijua kuwa chupi ipo chini. Aliivaa haraka haraka
kisha shangazi mkubwa aliendelea "ulikuwa wapi?" baba
mkubwa James akacheka, kisha alisema. "nilikuwa
chooni, kwani nimetokea wapi?" nikauliza ghafla
"umewazaje kuongea tena? Kila mtu akashangaa
"kuongea?"walinyamaza kwa pamoja. Nilipowatazama,
shangazi Suzi aliuliza "kwani alikuwa haongei huyu?"
baba mkubwa James alinishika mkono wangu kisha
alinibinya binya ninyamaze kuongea na kuwaeleza "wakati
nipo na Bella pale chini ya mti nilikabwa na tunda ambalo
nilimeza mbegu zake, sasa ndipo alipokuja kuwaita ninyi
na mimi nikawa nimetoka kuelekea chooni" kila mtu
alicheka kwa kuudhika. Shangazi mkubwa akasema.
"wewe James usitufanye sisi wajinga. Ni masaa mawili
yamepita sasa, tangu wakati ambao hujaonekana. chooni
kote tumekutafuta, mpaka chini ya uvungu hukuonekana.
Sasa huko chooni ulienda choo kipi" shangazi aliuliza kwa
ukali kidogo.
Nilipowatazama,
shangazi Suzi aliuliza "kwani alikuwa haongei huyu?"
baba mkubwa James alinishika mkono wangu kisha
alinibinya binya ninyamaze kuongea na kuwaeleza "wakati
nipo na Bella pale chini ya mti nilikabwa na tunda ambalo
nilimeza mbegu zake, sasa ndipo alipokuja kuwaita ninyi
na mimi nikawa nimetoka kuelekea chooni" kila mtu
alicheka kwa kuudhika. Shangazi mkubwa akasema.
"wewe James usitufanye sisi wajinga. Ni masaa mawili
yamepita sasa, tangu wakati ambao hujaonekana. chooni
kote tumekutafuta, mpaka chini ya uvungu hukuonekana.
Sasa huko chooni ulienda choo kipi" shangazi aliuliza kwa
ukali kidogo. Baba mkubwa james bado aliendelea
kucheka na kusema. "ili hali nimeshaoonekana hakuna
sababu ya kuniuliza maswali yasiyo na msingi acheni
nipumzike" aliondoka na kuelekea nje. Alikaa kibarazani
katika kiti kile cha kunesa nesa. Kilikuwa ni kiti cha babu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alinesa kuelekea nyuma kisha alirudi mbele. Alikuwa
ameshaichomoa sigara yake na kuipachika mdomoni.
Alikuwa akiuvuta moshi wake taratibu na kuwa katikati ya
tafakuri nzito. Alikuwa akitazama mawingu na nyota
chache zilizojitutumua angani. Nilimnyatia taratibu mpaka
alipo na kukaa mbele yake. Nilimuuliza. "Unaweza
kunieleza kilichotokea?" alikisimamisha kile kiti kwa
kushusha miguu yake chini na kunishangaa "umefika saa
ngapi hapa?" sikutaka nicheke ndio maana nilicheka kwa
hasira. "sasa baba mkubwa hukutaka niwepo hapa? Au
kuna mtu ulikuwa naye" nilimuuliza nikiwa naangalia huku
na huko kana kwamba nilikuwa nikimtafuta mtu ama kitu.
"hapana Bella sijasikia hata ukija hapa nilipo. Nilikuwa
mbali sana kimawazo" nilimuuliza "huko mbali nataka
nipafahamu baada ya kuniambia ulikuwa wapi baada ya
kupotea pale mtini?" baba mkubwa alicheka na kutingisha
kichwa. Aliniambia
"una msimamo kama baba yako" nilitabasamu tena kwa
kukereka. Nilifahamu baba mkubwa hakuwa tayari
kuzungumza lakini nilikuwa na shahuku pia ya kujua wapi
alipokuwa na walimfanya nini mpaka alishindwa
kuzungumza "baba mkubwa, tulikuwa wawili tu mimi na
wewe. Ulishindwa kuongea nikikuona na si tunda kama
ulivyodanganya. Ukapotea katika mazingira ya
kutatanisha." nilinyamaza kuyaruhusu maneno hayo
niliyoyazungumza yamuingie vizuri. Nilifanikiwa kwa kuwa
nilimuona akitaka kunieleza yote yaliyomkuta. Aliizima
sigara yake huku akinisikiliza kwa umakini. "naomba
unieleze ilikuwaje sikukuta pale na ulienda wapi?"
alinieleza "mwanangu, babu yako hakupendezwa na mimi
kukueleza yale yote niliyokueleza na kuniambia kuwa
endapo nikikueleza pia sitochukuwa muda mrefu nitakufa"
Niliuliza kwa mshangao "utakufa" akanijibu "ndiyo,
nitakufa tena katika kifo cha utatanishi kama nilivyopotea"
alinieleza yote sasa, kama vile hakuogopa kifo
alichoahidiwa.
"babu yako ndiye alinifunga mdomo nisikueleze kuwa kwa
nini huwa analia machozi ya damu. Machozi yale Bella
humaanisha umwagikaji wa damu au kufa kwa mtu ama
watu wengi. Lile hutokea pia kama kuna kitu ambacho
hakipo sawa katika uwezo wake machozi yake ya damu
humaanisha uangamivu" mimi moyo ulikuwa ukinienda
mbio sana. Jasho likanitoka taratibu kana kamba
kulikuwa kuna joto, kumbe wala. Baridi lilipuliza vizuri tu.
Wakati nikiendelea kumsikiliza baba mkubwa. Ghafla
nilimuona akikohoa. Alikohoa sana. Damu zikawa
zinamtoka mdomoni kila akikohoa. Nilipiga kelele za
kuwaita shangazi na baba wadogo. Baba mkubwa James
aliniambia "mwanangu nakufa, nakufa kwa ajili yako"
wakati akiyasema hayo shangazi Suzi alikuwa akisikia
yote. Alikuwa ameshafika na kuniona nikiwa nimemshika
baba mkubwa kichwa. Aliropoka "mchawi mkubwa wewe.
Mchawi kama baba yako. Umemuua kaka yangu?"
nilishituka sana hilo alilolisema shangazi. Nilishindwa cha
kusema kwa kuwa kila mtu alikuwa tayari ameshafika na
kuniona nikiwa nimekishika kichwa cha baba mkubwa,
damu zikimtoka mdomoni. Yule shangazi Suzi alinisogela
akanipiga kikumbo kikubwa pale nilipokuwa nimekaa,
nikiwa nimemshika baba mkubwa, James. Nilianguka
upande wa pili, nikiwatazama wale wengine. Baba
wakubwa kwa wadogo walinitazama kwa hasira na yule
shangazi mkubwa alikuwa akilia. "mkosi gani huu jamani
katika familia yetu?, Dah!" shangazi mkubwa alisema.
mimi machozi yalinitoka nisijue nijitetee vipi. Yule
shangazi mkubwa aliniambia neno lliloniumiza sana nafsi
yangu. "nyamaza mnafki mkubwa wewe, unalia nini
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wakati umemuua baba yako? Tena ondoka hapa
nyumbani hatukutaki tena usije ukatuua na sisi mchawi
mkubwa wewe"
linibidi niondoke nikiwa bado siamini kilichotokea. Ilikuwa
ni saa tano ya usiku nikiwa naelekea nyumbani peke
yangu kutokea Magomeni kwa babu ulipokuwa msiba.
Sasa kukawa na msiba wa pili wa mjomba wangu. Nikiwa
katika kukatiza kichochoro hiki na kile, niliwaona vijana
wakija nilipokuwa nikielekea. Walikuwa wanakuja kwa
mbele yangu. Walikuwa vijana sita niliwahesabu kwa
msaada wa mwanga wa mbalamwezi. Nilijipa ujasiri kuwa
wasingeweza kunifanya chochote. Niliendelea kutembea
kwa mwendo wa kawaida lakini nilikuwa nikitetemeka
sana. Ulkuwa ni usiku na nilikuwa ni msichana, ikawa
hatari zaidi. "vibaka!" Ilikuwa ni sauti ambayo
ilizungumza ndani ya fikra zangu. Walikuwa hawana sura
za kuwaamini hata kidogo. Nilipowasogelea, mmoja
alinitolea tabasamu la kejeli. Wanne wakanipita wawili
wakasimama mbele yangu. "we binti unaenda wapi?"
waliuliza huku wakicheka kibabe. Mimi nilikuwa naogopa
sana hivyo hata sauti yangu ilikuwa ni ya chini. "naenda
nyumbani" mmoja alinicheka kwa nguvu huku akiyashika
matiti yangu.
"nyumbani? umetoka kwa bwana wako huku?" Huyu
akadakia "da! ana kifua kizuri aisee! moyo umenienda
mbio sana" mimi nikamputa mkono yule aliyekuwa
akinishika matiti yangu. Nikaponyokwa na sonyo.
Nikaropoka "sitaki bwanaa!" walicheka kwa pamoja na
wale wengine wanne waliokuwa wamenipita, walirudi pale
tulipo na wale wenzao. Kuna sauti iliyonijia kichwani
haraka "Bella kimbia" nilipopata upenyo nikawachomoka
wale wawili, katikati yao. Nilikimbia kwa kasi ya ajabu.
Kabla hata sijafika, mbali walinikamata. Ilikuwa ni kabla
sijafika kituoni, walikuwa wote sita kwa pamoja. "tena
afadhali umejisogeza mwenyewe huku kwenye giza"
alisema yule mmoja aliyeanza kuniongelesha. Niliwaomba
wasinifanye chochote kibaya, lakini hawakunisikiliza wala
hawakuwa na muda huo. Mmoja wao alinipiga mtama
nikaisalimia ardhi iliyojaa michanga, mawe na vitu
vingine. Walinivutia kwenye kijichaka kidogo ilichopo eneo
hilo. Nikapata wazo la kupiga kelele. Hapo hapo nikapiga
yowe la nguvu. "wananibakaa!!!" yule ambaye tayari
alikuwa akiishughulikia sketi yangu, akanipiga ngumi ya
uso. Maumivu ya ngumi ile, nikayasikilizia kwenye pua na
mdomo wangu. Nikahisi maji maji mazito yakishuka
kutoka katika pua zangu. Nilipojipangusa nikafahamu
"damu" mmoja akasema "na bado ukituzingua tunakuua
nani anatufahamu" "fanyeni faster" ilinibidi niwe mpole
kwa kuwa tayari walikwisha nitolea, visu pamoja na sime
zao walizozihifadhi viunoni mwao. Alianza yule aliyenipiga
ngumi. Alinibaka alivyotaka mpaka alipochoka hakutumia
zana yeyote. Aliingia wa pili, wa tatu mpaka wa nne.
Kutokana na maumivu niliyokuwa nikiyapata, nilizimia.
niliamka baada ya muda kadhaa mbele. Ulikuwa ni usiku
mkubwa sana. Nilikuwa nimechafuka kupita kiasi. Damu
zilikuwa zikinioka sehemu zangu za siri. Nilipotaka
kunyanyuka, nilishindwa kutokana na maumivu. Nilipiga
kelele za kuomba msaada.
"nisaidieni jamani!" nashukuru mungu kuna kaka mmoja
alikuwa ametoka kuchoma maindi barabarani, alikuwa
akipita karibu na eneo hilo. Alikuja mbio. "kuna nini dada?
Kuna nini?"
mimi nilikuwa nikilia nikisikilizia maumivu katika kiuno
changu. "wamenibaka kaka yangu naomba unipeleke
hospitali sina nguvu" yule kaka alinisaidia kuninyanyua
"inabidi twende kwanza polisi kupata pf3 halafu Rb kisha
ndio twende hopitali" kwa kuwa kituo cha polisi cha
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
magomeni hakikuwa mbali, alinikokota kwa miguu mpaka
hapo. Damu zilikuwa zimekuka ila nilikuwa nikisikia
maumivu makali sana. Sikutamani kuendelea kukaa japo
dakika nyingine nyingi zaidi hapo polisi. Waliniuliza
maswali kadhaa nikayajibu kama ilivyokuwa na kuwaeleza
walikuwa ni wangapi kisha tuliruhusiwa twende hospitali.
Yule kijana aliita taksi iliyo nje ya kituo hicho "tupeleke
mwananyamala" dereva taksi alijibu "elfu kumi na tano".
yule kijana aliniingiza ndani ya gari bila kuzungumza naye
chochote. Taksi ilikuwa ikienda kwa mwendo wa kawaida
kwa kuwa usiku ule hakukuwa na magari mengi
barabarani. "kwani sasa hivi saa ngapi?" niliuliza huku
nikigugumia kwa maumivu. Yule kijana alinijibu "Saa nane
usiku sasa hivi" niliendelea kulia kutokana na maumivu
niliyoyapata. Hatimaye tuliingia katika hospitali ya
mwananyamala. Kutokana na uchovu wa hospitali hii,
sikupata msaada wowote wa haraka. Ilikuwa ni yule
kijana ndiye aliyenisaidia mpaka katika chumba cha
daktari alinikokota hivyo hivyo huku aipishana na
wauguzi.
"dokta nina mgonjwa wangu" dokta alikuwa akiniangalia
katika hali ya ukinyaa akauliza "usiku huu imekuwaje tena
na damu hizo mapajani" mi sikujali nikajitupa katika
kitanda kilicho karibu na kiti alichokaa daktari. Yule kaka
akampatia pf3 tuliyo tuliyoandikiwa kule polisi na daktari
kumwambia atoke nje ili aweze kunihudumia. Yule kijana
alitoka nje akiwa ananiambia "usiwe na wasiwasi dada
nipo hapa nje" nilijihisi faraja sana. Yule dakatari alirudi
pale nipo baada ya kuufunga mlango na kuanza kunisaili
kwa maswali. "kumbe yule ni kaka yako?" nikajibu
"hapana ni msamari mwema tu" akaniambia nipanue
miguu. Kutokana na maumivu na hali niliyo nayo
unadhani ningebisha? Basi ndivyo nilivyofanya mwenzenu.
Akiwa anatazama sehemu zangu za siri na msaada wa
tochi yenye mwanga mkali akaniuliza "ulipatwa na nini?"
nikajibu "nimebakwa. Nimebakwa na vijana sita mpaka
nikapoteza fahamu" nilimsikia daktari akisikitika.
Alisimama na kunieleza "hali ya huku chini si nzuri hata
kidogo" nilishituka sana macho yakanitoka, daktari
alikohoa kisha akaniambia
"inaelekea baada ya kukufanyia huu mchezo walikuingiza
vitu vyenye ncha kali na kukutoboa vibaya hivyo
umechanika sana sehemu hizi na pia kizazi chako sina
hakika kama hakijaharibika" alinitazama akiniangalia
akiwa amenishika begani huku akinipiga piga kwa liwazo.
Nililia sana haikuwa habari njema hata kidogo kwangu
kwa wakati huo. Nilisikia uchungu mkubwa sana. Mimi ni
msichana wa miaka kumi na nane tu duniani leo
ninakikosa kizazi changu jamani? Kwanini mimi? Nilijikuta
nikiropoka "dokta kwa hiyo sitozaa?"
dokta alitabasamu kunipooza alielewa machungu na
huzuni niliyojisikia baada ya kupewa taarifa ile. Alinieleza
"hii ni kwa uchunguzi wa macho binti, sijawa na hakika
kama ni kweli au lah lakini kesi kama hizi mara nyingi
matokeo yake ni hayo" nikawa nalia "sasa dokta
utanisaidiaje mwenzio mimi jamani?" nilikuwa nikilia kwa
uoga na uchungu. Niliwachukia wale vijana na kuwaona ni
watu waliotumwa kuaribu maisha yangu na ndoto zangu.
Dokta akaniambia "tutakupeleka sasa sehemu ya
kukufanyia uchunguzi zaidi na kama upo sawa
tutakusafisha tu na kukushona pale ulipochanika" niliitikia
kumuonesha kuwa nimemuelewa. Nilijikokota kutoka
kitandani kisha mimi na daktari tulitoka katika chumba
hicho na kwenda katika chumba cha upasuaji. Nilimkuta
yule kijana amekaa kwenye benchi la mapokezi.
Alipotuona, alisimama "vipi daktari?" akajibiwa "tulia
endelea kusubiri"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
yule kijana aliendelea kukaa pale akisubiri. Daktari aliingia
chumba fulani na kuwaita wauguzi watatu. "nawahitaji
chumba cha upasuaji" nilipofika niliambiwa nilale kama
nilivyolala kule kwa daktari chumba cha mwanzo. Wale
wauguzi walioitwa waliingia na visu mikasi pamba na
madawa madawa. Niliogopa sana. Hali ya hospitali
ilitisha sana. Wale wauguzi walivaa gloves na kuanza kazi
yao wa kuchunguza kizazi changu pamoja na daktari.
Mimi nilichomwa sindano ya ganzi hivyo sikujua nini
kilikuwa kikiendelea huko chini. Zilipotea zaidi ya dakika
arobaini na tano kisha daktari aliibuka na kunieleza "pole
sana kizazi kilikuwa kimesogea ila sasa kipo sawa na pia
tumelazimika kukushona kutokana na ulichanika kwenye
mashavu na pia tutakuapa dawa kwa ajili ya kusafisha
uchafu wote ulioingiziwa japo mara kwa mara tumbo
litakuwa likikusumbua hiyo hali isikutie hofu"
nikajibu kwa kukunyekea "nashukuru sana dokta" yule
daktari alitabasamu tu kisha alinieleza "unapaswa upate
muda wa kupumzika labda kama ni ruhusu utapata
kesho. Leo kuna dripu utatundukiwa kwa ajili ya
kuongezewa damu iliyopotea" nikamuuliza "kwani
mmeshanifanyia vipimo vya damu yangu" "hiyo ndiyo kazi
yetu tumekupima ukimwi upo sawa tumekupima pia na
group yako tumefahamu kuwa wewe ni group AB huna
tatizo hivyo utapata damu hiyo sasa" nikauliza kwa
kudadisi "kwanini labda nisingepewa dawa za kuongeza
damu au nile nini na nini niongeze damu?" akaniibu
kiufasaha "wewe damu yako imepotea kwa wingi saa ndio
maana unajisikia hivyo unavyojisikia hata sisi hatuna
damu ya kutosha ila tunalazimika kuigawa kwa watu
waliopoteza wingi wa damu kama wewe"
moyo wangu ulifarijika sasa. Kitanda changu
kikasukumwa mpaka kwenye wodi nyingine ambapo huko
nilipewa kitanda na kutundukiwa dripu iliyokuwa ikiingia
taratibu katika mishipa yangu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment