Search This Blog

NILIONGEA NA SHETANI ILI NIWE TAJIRI - 3

 





    Simulizi : Niliongea Na Shetani Ili Niwe Tajiri

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Kitanda changu

    kikasukumwa mpaka kwenye wodi nyingine ambapo huko

    nilipewa kitanda na kutundukiwa dripu iliyokuwa ikiingia

    taratibu katika mishipa yangu

    ..........

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Daktari alimruhusu yule kijana kwenda kupumzika ila aje

    kuniona kesho asubuhi. Nilipokuwa hospitali nikawa

    nawaza mengi. Nilijiuliza jinsi dunia ilivyonipiga kofi kwa

    dakika chache tu baada ya matukio ya ajabu kunitokea

    kwa muda mfupi. Niliona sistahili kuishi. Kwanini niishi na

    Mzee nyegezi ikiwa tayari alishanifanyia kitendo kibaya?

    Ndio maana sijaona umuhimu wa kumueleza tukio hili

    lililonikuta. Sikuona umuhimu wa kuishi kama ikiwa

    nimeonekana mimi ni muuaji wa baba mkubwa. Kwanini

    niishi kama mama yangu ambaye nilimuona kama ndiye

    ndugu yangu rafiki yangu na mama yangu hayupo tena

    duniani? Maisha niliyaona yalikuwa na kisasi na mimi

    kisasi cha kunipa adhabu kutokana na kushindwa

    kutimiza masharti ya mkuu wa Gamboshi. Machozi

    yakalowesha mashavu yangu na kunifanya nijihisi udhaifu.

    Usingizi ukanipitia jirani na asubuhi kabisa. Mguso wa

    muuguzi ndio uliniamsha. "nafikira sasa una nguvu"

    alikuwa akitabasamu: na mimi nilitabasamu kwa amani

    "ndiyo dada" aliichomoa ile sindano iliyokuwa ikipitisha

    damu katika mishipa yangu kisha nilimuuliza "eti! Yule

    kaka wa jana usiku amekuja?" nilimuona akitafakari

    kidogo kama akijaribu kukumbuka kitu. Aliniuliza "yule

    ambaye tulimuacha kwenye benchi wakati wewe

    unaingizwa humu kwenye upasuaji?" nikajibu "ndiyo"

    akaniambia "anha yule ni kijana wa ajabu sana, alienda

    nyumbani saa ile saa kumi na mbili amekuja hapa"

    nilihisi furaha ya ajabu sana. Sikujuwa kama kungetokea

    mvulana ambaye angenisaidia kama yeye. Baada ya

    kumaliza kutoa kila kitu, alipotaka kuondoka,

    nilimsimamisha. Nilimuuliza yule tena "sasa yuko wapi?"

    akaniambia "amekusubiri sana uamke ila aliona

    umechelewa. Alituambia tu kuwa ukiamka tukukabidhi uji

    ambao alituachia na kisha kila kitu ameshalipia hivyo

    katupa namba ya simu ambayo unaweza kuwasiliana

    naye baada ya kutoka hapa na.." yule daktari aliyenitibu

    jana usiku akawa ameingia "na amekuachia pesa za

    matumizi ya leo kama kuna lolote litatokea kwa dharula"

    alimgeukia yule muuguzi na kumwambia "nenda kamletee

    vile vitu vipo kwenye kapu" daktari alinifuata kitandani

    kwangu na kuniuliza "unaendeleaje?" nikamjbu "najisikia

    vizuri dokta. Nashukuru sana kwa huduma niliyopata

    nahisi kama ya upendeleo kwangu katika hospitali hii"

    akanijibu "hii ni kawaida yetu usijali" alinyanyuka na

    kuondoka. Niliunywa uji nikashiba haswa. Nilijisikia nina

    nguvu sasa. Baada ya kumaliza mambo yote pale

    hospitali, nilipewa ruhusu ya kutoka. Nilichukua zile pesa

    pamoja na kila kitu nikarudi nyumbani. Nilirudi kwa Mzee

    Nyegezi. Nilimkuta sebuleni pamoja na binti mdogo. Kwa

    kadirio la haraka haraka binti yule hakufikisha miaka

    ishirini na nne. Mkono wa Mzee Nyegezi ulikuwa

    ukipapasa mwili yule binti, kuanzia kifuani mpaka kiunoni.

    Nilipigwa na bumbuwazi nikasimama ghfla nilipowaona.

    "ulikuwa wapi muuaji malaya mkubwa wewe?" 'muuaji?

    Mimi muuaji?' sauti yangu nikaisikia rohoni ikijiuliza kwa

    uchungu. Chozi likaniponyoka Niliingia chumbani kwangu

    bila kumjibu chochote. Nilikuwa nikilia kwa uchungu sana.

    Sikujua kama Mzee Nyegezi angekuwa na roho ya ajabu

    kiasi kile. Roho ya kinyama na ya usaliti. Roho iliyokosa

    aibu. Nakumbuka aliwahi kunibaka, ila si kuendelea

    kuwabaka wengine wasio na hatia. Yule msichana alikuwa

    mdogo sana kwa mama yangu . Yule msichana hakuwa

    mkubwa kiasi cha kushikwa shikwa maungo yake na mzee

    aina ya Mzee Nyegezi. Maisha yakaendelea kwa

    kuzisukumiza kwa machozi. Nilikuwa nikilia mara kwa

    mara. Nilihuzunishwa na maisha jinsi yalivyonibadilikia.

    Hatia ya kusingiziwa kuwa nimemuua baba yangu

    mkubwa ikaendelea kunitafuna. Moyo ukaninyongolota

    machozi yakanibubujika. Nilijiuliza kwanini mimi? Kwanini

    maisha yamenisaliti? Mzee Nyegezi naye aliishi na mimi

    kama mtu baki ambaye hakuwahi kumfahamu. Ikanibidi

    nianze boarding. Kwakuwa pale shuleni kulikuwa kuna

    aina mbili kutwa na kulala pale, hivyo sikupata tabu ya

    kutafuta shule nyingine. Japo Mzee Nyegezi alikuwa

    akinichukia lakini alinilipia ada hiyo kwa masimango na

    maneno ya kashfa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "najua unataka boarding ili ukawauwe vizuri na wenzako

    na huo ufuska wako usiulete tena nyumbani kwangu

    umalizapo hiyo kidato cha nne chako sihitaji kukuona tena

    nyumbani kwangu ujue utakapoenda kukaa" sikujua kama

    nilimsikia sahihi ilikuwa ni siku ambayo ndiyo alinikabidhi

    pesa ya kwenda kulipia shule. Na siku hiyo ndipo

    nikamkumbuka yule mchoma maindi. Hivyo sikupenda

    niende shule bila kuonana na yule kaka na kumshukuru

    kwa msaada alionipatia siku ile ya matatizo yangu.

    Sikukitupa kile kipande cha karatasi, hivyo nilichukua simu

    niliyo nayo na kunakili zile namba na kumpigia. Simu iliita

    bila kupokelewa. Niliipiga tena ikaita muda mrefu vile vile

    tena bila kupokelewa. Sikuona tena sababu ya

    kumsumbua nikajiandaa. Nikaandaa nguo zangu za shule

    vitabu na madaftari yangu yote. Sauti ya Mzee Nyegezi

    ilipojirudia tena kichwani mwangu, chozi likanidondoka

    tena. Furaha ya kwenda shule ikanipotea nikajiuliza

    nitaenda wapi kama sintokuwa na pa kukaa nikimaliza

    shule? Maisha hakika yamenichapa fimbo. "adhabu ya

    kutofuata masharti" hapana! Sauti hii si sauti ambayo

    huniambia moyoni hii ni sauti ya tofauti. Sauti

    iliyoniambia kwa kunikebehi. Sauti ambayo ilizungumzwa

    na mtu mwingine ambaye sikumuona mtu ambaye

    alionekana kuyasoma mawazo yangu. Nikanyong'onyea

    nisijue cha kumjibu. Mara nyingi imekuwa kawaida kulala

    na njaa. Sikushangaa yule mwanamke mpya wa baba

    kutokuja kuniamsha kuja kula chakula cha usiku japo

    huniamsha asubuhi nikaoshe vyombo. Ingawa chakula

    hicho nilikipika mwenyewe lakini nilisimamiwa eti

    nisiwawekee sumu. Na asubuhi ya siku hii nilikuja

    kuamshwa na yule mwanamke wa baba aliyeitwa Irene.

    Aliniamsha nikaoshe vyombo na kufanya usafi "we malaya

    usiye na kwenu unalala mpaka sasa hivi hapa kwa baba

    yako?" nilidhani labda hakuzungumza na mimi. Niliamka

    nikiwa nimetawaliwa na usingizi, niliuinua uso wangu na

    kumtazama, kisha nikajifunika tena na shuka. "mimi

    nakuamsha wewe unalala mbwa wewe?" nilimsikia

    akiufungua mlango neno lingine likimfuata kwa nyuma

    "subiri nikuoneshe" hapo nikawa nimefahamu ni mimi

    nikawa nipo macho nikiwaza kwanini ananichukia? Kosa

    gani nimemfanyia mimi? Mbona sijawahi kumsumbua kwa

    lolote. Nikiwa katika kuwaza huko nilishtushwa na maji ya

    baridi, yaani baridi iliyopitiliza. Alinimwagia mgongoni na

    kitanda changu kutotamanika tena kulalia. Kililowa chapa

    chapa. Ilinibidi niamke nikamuulize "hivi irene

    nimekukosea nini mimi!" akacheka kwa kebehi, huku

    akiniiga kwa kubana pua "hivi irene nimekukosea nini

    mimi" alinizaba kibao kilichosindikizwa na sonyo. Kisha

    alinivuta kwa nguvu nikajogonga ukutani hakujali lolote

    alilonifanyia Aliniambia "ninachotaka ufanye usafi malaya

    wewe unalala tu hapa kwenu?" nililia sana. Nakumbuka

    sikuu hi ndiyo niliakiwa niwe nimeripoti shuleni mapema

    saa 2 asubuhi. Ila kwa kuwa bado ni saa kumi asubuhi,

    nilijua nitawahi tu. nikaosha vyombo vyote. Vilikuwa

    nivingi hata vikanishangaza. "watu wawili tu wametumia

    vyombo vyote hivi?" nikamezea. Nilipomaliza kuosha

    vyombo, nikafagia uwanja wote ulioizunguka nyumba.

    Nilipomaliza ilikuwa tayari jua limeanza kuchomoza,

    nikajua tayari nimemaliza kile walichokuwa wakihitaji.

    Kumbe! Nikaletewa lundo la nguo la kufua. Lilikuwa ni

    lundo kubwa sana. Zilikuwa ni nguo zilizonichosha hata

    kuzitazama. Nilimwambia irene kwa sauti iliyokata tamaa.

    "irene leo ninatakiwa niwahi shule tafadhali nionee

    huruma irene" bila kujua sikutaka kulia mbele yake, lakini

    chozi likanisaliti tena. Irene hakuwa hata na chembe ya

    huruma wala kujiuliza mara mbili alichonijibu ndicho

    alitaka nifanye

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "sina muda wa kujibizana na wewe, ufue hizo nguo ndio

    nikupe hizi pesa zako za ada sasa sijuhi huko shuleni

    wanahitaji hayo macho yako yaliyolowa kila mara? Hivi ni

    nani kwani asiyelia?" aliniongelea kwa kebehi kiasi cha

    kunifanya nizidi kulia. Aliniiga nilivyokuwa ikiongea naye

    akijifanya kama analia "eti! Irene nionee huruma leo

    natakiwa niwahi shuleni" alinitemea mate juu ya paji la

    uso wangu. Kisha aliondoka huku akizungumza "maliza

    hizo nguo ndio upate hizi ela za kulipa hiyo ada huko

    shuleni. Nikaisikia ile sauti tena, niliyoisikia kule chumbani

    "madhara ya kuvunja masharti" nililia tena, nikalia sana.

    Nikaliendea pipa nikipanga nifue haraka haraka ili saa

    mbii isiishe nikiwa ndani ya hiyo nyumba. "mtume!? Maji

    hakuna" pipa lilikuwa jeupe. Ilinibidi nichote maji ya kufua.

    Na maji yalikuwa ya tabu sana. Yalitoka nyumba moja tu.

    Nilichukua ndoo na kwenda bombani kwa mama Tunnu.

    Nilipofika, geti likawa limefungwa. Niligonga, nikagonga

    mlinzi akaamka.

    "unataka nini?" kwa kuwa ilikuwa ni asubuhi sana hata

    midomo yangu ilipata shida kueleza nilikuwa nataka

    kuchota maji. Nilikuwa nikilia. "wewe Bella unataka nini?"

    yule mlinzi alinifahamu. Nilimueleza "nataka kuchota maji

    Gabu" aliitwa Gabriel ila kutokana na uvivu wa kuliita jina

    lote akafupishwa tukamzoea kwa jina la gabu. Gabu

    alicheka sana kana kwamba niliongea kinachochekesha.

    "wewe Bella, tangu lini ukachota maji saa moja asubuhi

    hapa kwetu?" nilinyamaza kwa kuwa sikua na jibu. "au

    umesahau kuwa hapa mwanzo wa kuchota maji ni saa

    tatu asubuhi?" kutokana ukweli alioniambia nilimuomba

    Gabu na kumsihi anisaidie walau ndoo moja. Alikataa

    kata kata hata yeye mwenyewe aliwaogopa sana mabosi

    zake. Niliondoka nikiwa sijafanikiwa kupata maji. Kichwani

    nikajiuliza 'itakuwaje na saa mbili ndio natakiwa shuleni?'

    basi nikakata tamaa. Nikasubiri litakalokuwa na liwe.

    Nilirudi nyumbani nikiwa na ndoo tupu machozi

    hayakunikauka. Niliyafikiria maisha yalivyonitupa mkono

    ghafla. Kila kitu kwangu kikawa kibaya kila nilichokigusa

    kikageuka laana. Kila nilipokanyaga, nilipaona kama

    kuzimu. Maisha yakawa machungu, machungu yaliyonitoa

    machozi kila nilipokuwa nikiyafikiria. Nilirudi nyumbani,

    nikamuona Irene kashika kiuno; kasimama mlangoni.

    Aliongea kwa ngebe akiutingisha mwili wake wote.

    "nilikuwa nakuja kukufuatilia malaya wewe, una nia ya

    kufua saa ngapi?"

    nilinyamaza sikumjibu kitu. Nilijiuliza sana umalaya

    wangu ni upi? Sikupata jibu kwanini niliitwa hivi.

    Alichukua ndoo ya maji yaliyopo jikoni, maji machafu

    akanimwagia.

    "mimi naongea peke yangu, mbwa wewe?" Alipoona

    simjibu chochote aliingia ndani. Mimi bado nilikuwa

    nimesimama pale pale machozi yakiwa yananilenga lenga,

    moyo ukinienda mbio kwa hasira. Aliporudi, Alinitupia zile

    pesa alizozichukua sehemu niliyozihifadhi, lakini zilikuwa

    pungufu. Aliniambia "hakuna wa kumchuna mume wangu

    hapa. Hiyo ni hela ya ada na nauli, inatosha sana" nikiwa

    nimeinama kuziokota pesa hizo. Aliniambia tena kwa

    kashfa.

    "leo ndio siku yako ya mwisho humu ndani. Ukumbuke

    hivyo" alinyamaza akiwa anapiga hatua kuingia ndani

    ghafla alisimama akanigeukia. Aliniambia kwa nyodo na

    kujiamini.

    " kuwa makini usidhani hatutajua ukiiba. Usije kujaribu

    kuiba chochote ukidhani kwamba ntakuachia" akanisonya

    kisha aliingia ndani kwa gambo. Nilipoziokota nikaingia

    chumbani na kumtafuta yule kaka aliyenisaidia. Uzuri

    nilikuta naye alinitafuta, nikampigia simu

    "halo" sauti yake ilipokoroma tu baada ya kuipokea,

    nilianza kulia. Nililia kwa sauti ya uchungu sana. Na

    kwikwi ikiongeza huzuni hiyo. Nikashindwa kuongea, hali

    iliyonifanya nikate simu. Simu yangu ikaita, sikuipokea.

    Mara ya pili nilipoipokea nikaiweka sikioni, yule kaka

    alikoroma tena "wewe nani unapiga simu unalia?" aliuliza,

    nikamjibu "samahani kaka yangu naitwa Bella" nikavuta

    kamasi jepesi kumuachia nafasi ya kuzungumza. "Bella!?

    Bella gani?" nikajibu kwa kujiamini "najua hunifahamu kwa

    jina ila unanifahamu kwa sura. Mimi ni yule binti

    uliyenisaidia juzi usiku wa manane pale magomeni

    ukanipeleka hospitali ya mwananyamala" akanijibu

    "samahani dada mimi sio mwenye simu ila unayemtafuta

    hayupo tena duniani" nilihamaki kwa mshituko. Sidhani

    kama nilisikia sahihi au masikio yangu yalianza

    kunidanganya. Nilipojaribu kuuliza nini kimetokea? Simu

    tayari ilikuwa imeshakatwa. Nikiwa bado nashangaa, simu

    yangu iliita upande wa ujumbe mfupi. Ulikuwa umetoka

    kwenye namba ya yule kaka aliyenisaidia. "msiba upo

    nyumbani kwa mjomba wake kigogo mburahati, amekufa

    jana usiku akiwa amelala chumbani kwake, bado

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    haijajulikana chanzo" nikiwa nasoma ujumbe huo macho

    yangu yakafumba kwa machozi. Nililiaa nikalia sana.

    Nikiwa katika kulia nikasikia sauti ya upepo mkali

    uliovuma ghafla. Kikaja kimbunga mfano wa upepo wa

    kisuli suli. Kati kati ya vumbi hilo lililozunguka zunguka,

    kikasikika kicheko kikubwa sana. Baada ya muda mrefu

    wa kutona kitu kama hicho kupita, nikamuona babu

    yangu. Alikuwa katika sura ya ujana na tabasamu pana

    usoni mwake. Aliniambia "Bella! Bado unayo nafasi ya

    kusamehewa. Lakini ukiendelea kung'ang'ania roho ya

    Jordani mpenzi wako, basi kila atakayejaribu kuwaza

    kukusaidia roho yake itakuwa halali yetu" akacheka tena

    kilikuwa ni kicheko cha dharau sana. Alipopotea na

    maneno yake. Maneno hayo ya babu ndiyo yakanipa

    mwanga. "inawezekana hata huyu muuza maindi kamuua

    yeye?" hapo hapo mapigo ya moyo yakaanza kunienda

    mbio na kujiuliza ni nafasi ipi ya kuirekebisha ikiwa tayari

    nimeshakosea? Nilikuwa tayari nimeshakauka ule uchafu

    niliomwagiwa na Irene na muda ulikuwa umeshakwenda

    sana. Nilipotoka nje sikumkuta Irene popote nilipomnyatia

    kumtafuta. Nilienda kuchota maji haraka haraka kisha

    nilioga kwenye bafu la nje na kuvaa nguo zangu safi.

    Nikachukua mkoba wangu wa nguo na madaftari yangu

    nikaondoka kwenda kwa rafiki yangu. Sikutaka Mzee

    Nyegezi wala Irene wanikute tena pale. Nilielekea maeneo

    ya kigogo mbuyuni alipokuwa akiishi schola. Nilijua

    nitamueleza nini na atanielewa. Safari ilianza nikiwa sitoi

    tena machozi. Ndani ya daladala msongamano ukiwa ni

    mdogo tofauti na kawaida. Nilifika kwa schola aliyekuwa

    akiishi na wazazi wake. Kwa bahati mbaya sikumkuta

    schola. Mama yake aliniambia "schola ameenda shule,

    nashangaa sana kukuona hapa?" nikamjibu kwa huzuni

    "mama ni hadithi ndefu ila kuna sehemu naenda nitarudi

    hapa naomba niweke begi langu"

    akaniambia "haya weka huko kwa mwenzako" hivyo

    kwakuwa mama yake schola alinifahamu, aliniruhusu

    kuingia chumbani kwa schola bila matatizo. Nikaliweka

    begi langu na kutoka mbio.



    Nilifika kwa schola aliyekuwa

    akiishi na wazazi wake. Kwa bahati mbaya sikumkuta

    schola. Mama yake aliniambia "schola ameenda shule,

    nashangaa sana kukuona hapa?" nikamjibu kwa huzuni

    "mama ni hadithi ndefu ila kuna sehemu naenda nitarudi

    hapa naomba niweke begi langu"

    akaniambia "haya weka huko kwa mwenzako" hivyo

    kwakuwa mama yake schola alinifahamu, aliniruhusu

    kuingia chumbani kwa schola bila matatizo. Nikaliweka

    begi langu na kutoka mbio. Akili yangu yote ilikuwa

    inawaza kuelekea ,kkwa muda mrefu. Na kivest cheupe

    cha matobo matobo kilichopoteza rangi yake ya asili.

    "huyu mzee ni mganga na kuna kijana wake amefariki

    jana usiku huko magomeni sijuhi"

    nikawa namtazama huyu kijana, sasa kwa hofu. sikujua

    kwa nini nilihofu, lakini hofu ilikuwa wazi usoni mwangu.

    Yule kijana aliendelea

    "sasa inasemekana yule kijana kuna dada ambaye

    alimsaidia usiku wa juzi na yule dada ana makosa

    aliyoyafanya huko kwa wachawi wenzie sijuhi"

    nilihisi mkojo ukitaka kunitoka. Nilitamani nikimbie lakini

    kuna sauti ambayo ilinipa nguvu ya kutamani kuendelea

    kusikiliza na kufuatilia kila kilichokuwa kinaendelea.

    "sasa mzee manyota, jana usiku alipigana sana na huyo

    nyoka aliyeuchukua uhai wa kijana wake. Hilo joka

    linasemekana limetokea chini ya ardhi lina kichwa cha

    binadamu mwenye nywele nyeupe kama mvi au bati. Hizo

    nywele unaambiwa zinang'aa sana"

    yule kijana aliendelea kunisimulia kwa hali ya kusisimua

    sana. Akidhani kuwa aliniogopesha akaongeza hata na

    chumvi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "unaambiwa hapa kote kulikuwa kama mchana nay eye

    akiwa kama amelibeba jua"

    Akaongezea huku kimeza mate na kujilamba papi zake.

    Laiti kama angejua hayo yote mimi niliwahi kuyashudia

    kwa macho yangu angenisimulia kwa kawaida. Basi

    aliendelea

    "yule nyoka akautafuna mkono wa yule babu"

    nikaropoka

    "hivyo hana mkono sasa?"

    "ndiyo si unaona jinsi watu walivyojaa?"

    niliuangalia umati mkubwa wa watu kweli ulikuwa ni

    mkubwa. Aliendelea

    "basi kila mtu ana hamu ya kuliona tena hilo joka

    lililoacha gamba lake na kuondoka. Yule mzee manyota

    hana nguvu ya kumuokoa kijana wake, ila anadai huyo

    binti akimpata lazima atakiona cha moto"

    yaani alikuwa akizungumza kwa hamu zote huku machozi

    ya msisimko yakimtoka. Mimi nikanyong'onyea. Nikaisikia

    sauti ya babu ikiniambia.

    "hazifikii nguvu zako hawezi kukudhuru"

    nilimwambia yule kijana twende.

    Niliposogea eneo lile, nilisikia kelele za mtu anayepiga

    kelele kwa sauti ya juu sana. Yule kijana licha ya

    kumpatia elfu mbili yake, lakini naye alikuwa na hamu ya

    kujua nini kitatokea pale kwa yule babu. Aliniambia kwa

    shahuku.

    "huyu Mzee Manyota ni kiboko"

    mimi sikumjibu kitu. Kutokana na wingi wa watu, nilipata

    shida kumuona huyo Mzee mwenyewe. Nilibaki tu kusikia

    sauti yake akiongea sana kama mtu aliyewehuka. Yule

    mzee naweza kusema alikuwa na nguvu sana, kwani

    alianza kuhisi uwepo wangu mahali pale. Aliongea kwa

    sauti kubwa kila mtu alikuwa kimya akimsikiliza.

    "amekuja, amejileta mwenyewe"

    mimi sikugundua chochote. Nikawa bado nakazana

    kutaka kufahamu ni nani huyo aliyejileta mwenyewe.

    Nikawa najinyanyua na kusimamia vidole, nikabahatika

    kuambulia kuona umati mkubwa wa watu. Nilipokuwa

    katika kuhangaika huko, ndipo nikamshuhudia yule Mzee

    Manyota. Alikuwa ni mfupi kiasi mwenye mwili mpana na

    tumbo kubwa. Hakikufaa kuitwa kitambi ila ni tumbo

    lililotisha. Alikuwa na kipara ila kidevu kilichotawaliwa na

    ndevu nyingi. Aliuvaa msuli wake na kuufungia chini ya

    tumbo lake kubwa hakuvaa chochote juu kwa maana si

    shati wala singlend iliyomsitiri kifua chake kisicho na

    mvuto. Kifua kilichosahau makali ya wembe na kugeuza

    msitu wa nywele nyingi chafu juu ya kifua chake. Alikuwa

    akizunguka kitu fulani kama mwili wa binadamu. Nikahisi

    atakuwa marehemu mchoma maindi. Akawa anaendelea

    kumzunguka yule mtu pale chini huku akimtemea maji

    aliyokuwa akiyanywa na akiongea maneno fulani ambayo

    yalikuwa ni ngumu kuyaelewa. Nilimgeukia yule kijana

    nikamuuliza.

    "hivi huyu aliyekufa unamfahamu jina lake?"

    yule kijana niliyeongozana naye, alionesha kutomfahamu.

    Ndipo kuna jamaa aliyesimama pembeni yetu akatuinamia

    kwa kutunong'oneza.

    "nimesikia kuwa anaitwa Malick, alikuwa anakaa huko

    Magomeni"

    nikiwa bado nahangaika kumtazama huyo Mzee Manyota,

    nikapigwa na butwaa ghafla moyo ukanienda mbio jasho

    likanitoa kwa wingi. Viungo vyangu vililegea kupita kiasi.

    Nilikuwa nimegongana macho kwa maho na Mzee

    Manyota. Macho ya Mzee Manyota yaling'aa sana kama

    ya paka. Alikuwa akiongea vitu fulani kwa kumung'unya

    sauti, lakini mimi niliweza kumsikia vizuri. Nilimsikia

    alikuwa akiombea nipoteze maisha pale pale au nigande

    nisipate nafasi ya kutoroka. Hakuweza kufanikiwa

    kunigandisha wala kunipokonya uhai wangu. Nilipotaka

    kukimbia. Nilikutana na kundi kubwa la watu wenye

    mikuki mishale na mapanga. Kundi hilo kubwa la watu,

    lilikuwa uchi. Watu hao walikuwa ni weusi sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walitumia ngozi ya mnyama kuziba sehemu zao za siri.

    Waliuwa wakinifuta mimi kwa hasira. Nyuso zao

    zilionekana zimedhamiria kuniangamiza. Nilipogeuka

    nyuma nilimuona yule Mzee Manyota naye akinijia kwa

    kasi akiwa anapaa juu ya vichwa vya umati wa watu.

    Hapo nilihisi kuwa ndio ulikuwa mwisho wangu. Watu

    waliojaa eneo lile waliendelea kushangaa mbele kama

    kulikuwa hakuna kinachoendelea. Nikafahamu hivi vilikuwa

    ni vita vya mtu mwenye macho ya kawaida asingeweza

    kuona mambo haya. Ilibidi uwe mchawi uliyekubuhu na

    mwenye nguvu za kutosha. Nilimgeukia yule kijana na

    kmuuliza

    "unawaona hawa watu wanaokuja na mapanga?"

    nadhani alinishangaa kuliko kawaida. Alinicheka kisha

    aliniambia kabla ya kuendelea kushangaa kule mbele.

    "watu wataendelea kuja kwa sababu kila mtu

    anamfahamu Mzee Manyota"

    nilijua hakuona umati mkubwa wa watu uliokuwa ukizidi

    kusogea. Watu hao walikuwa wakiongezeka urefu na

    kupishana na watu barabrani kupita chini ya mapaja yao

    ili wasiguswe. Ndiyo maana mtu wa kawaida unaweza

    ukapita sehemu siku nyingine ukashangaa eneo hilo lina

    joto sana. Kaa ukifahamu kuwa umepita chini ya mapaja

    ya wachawi. Nikawa bado nawatazama. Nikajihisi na

    mimi nimeanza kubadilika. Niliongezeka ukubwa nikawa

    mrefu sana mrefu kupita kawaida yaani nikayashika hata

    mawingu. Niliporudi tena chini nikarudi kwa kasi lakini

    katika umbo la nyoka. Nilibadilika na kuwa nyoka aina ya

    kobra. Wale waliokuwa wanakuja walisimama ghafla. Na

    Mzee manyota naye hivyo hivyo. Katikati ya wale watu na

    mimi nilipo kukatokea shimo kubwa sana. Shimo

    lilotenganisha pande mbili yaani kama bonde la ufa. Kati

    ya wale wachawi kama angekuwa ni kiburi angetumbukia

    na asingewahi kuja kufikiria kutoka kamwe. Na hata mtu

    ambaye hakuwa mchawi kama alikuwa na nia a kuja

    kwenye umati ule, niliwashuhudia wakigeuza njia na

    kurudi walipotaka bila kufika au kupita eneo lile. Kuna

    ambao walikuwa wanataka kuondoka nao walisita na

    walirudi katikati ya umati ule. Nikatamka kwa sauti ya

    hasira

    "hamniwezi!!!"

    moto ukawa unatoka mdomoni mwangu. Moto ule

    ukawaunguza lile jeshi lote la wachawi na kutumbukia

    ndani ya lile shimo. Hakuna aliyesalia kati yao. Nikajiona

    nimeshinda na nikamgeukia Mzee Manyota baada ya

    shimo lile kuwameza jeshi lake.

    Nilipomgeukia, nilimuona akiwa amejawa hofu kubwa

    usoni mwake. Nilitabasamu kifedhuli na alipotaka kurusha

    shambulizi kwangu nilizuia kwa kutuma mkia wagu.

    Alirusha moto nikauzuia akarusha mshale wa kichawi

    nikauzuia. Vita ikapamba moto. Nilipoona ameishiwa

    mbinu mpya mimi nikamchapa na mkia uliomdondosha

    chini kwa kishindo kikubwa. kishindo kilichosababisha

    watu kudhani ni mngurumo wa radi ambayo ilitaka kuleta

    mvua, kumbe sivyo. Nilipomsubiri anyanyuke. Alinyanyuka

    akiwa na hasira. Aliongezeka urefu wake na kunirushia

    moto, moto uliowafanya watu kuona ni radi.

    Walikimbizana huku na huko kuokoa maisha yao. Mimi

    niliuzia moto ule na kuurusha wa kwangu uliomchakaza

    kisawa sawa. Mzee Manyota alidondoka chini na

    kupoteza fahamu. Ilinyesha mvua kubwa sana. Mvua

    ilyowafanya watu wakimbie katika vibanda vya jirani

    kujificha wasilowe. Mtu mmoja alipiga kelele

    "mzee manyota jamani"

    kila mtu alikmbia eneo alilopo kushuhudia nini kimempata.

    Hawakjali tena ukubwa wa mvua wala kulowa.

    Walipomnyanyua kumkalisha hakuwa na nguvu tena.

    Nilimsikia mmoja akisema "inawezekana ile adi jaman

    ndiyo imempiga!" mwingine yeye alisema

    "au wachawi wenzake wamemzidi nguvu mbona

    haikuonekana radi eneo hili?"

    nilipojichunguza mimi nilijiona nikiwa sehemu nimejificha

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mvua. Kwenye kibanda Fulani cha mama nisiyemfahamu

    lakini ni maarufu sana eneo hilo. Inawezkana umarufu

    wake ulikuwa ni kutokana na uuzaji wake wa chakula au

    unene uliomzidi. Mzee Manyota akaipata sauti yake

    akazungumza kwa sauti ya chini sana "nakufa" wale

    walio karbu yake kumsaidia ndiyo wakatuzindua tulio

    mbali kwa shangwe "Mzee Manyota kapatikana leo" watu

    walishangilia sana kwa tukio hilo. Hatimaye Mzee

    manyota akalala usingizi wa milele. Giza zio likampokea

    na umauti ukamkaribisha kuzimu. Hadithi za mzee

    manyota zikafutika ikabaki historia. Walimzika Mzee

    mayota katikati ya makaburi mengi yaliyopo kigogo

    Luangwa. Kaburi lake likachimbwa tofauti sana na

    makaburi ya kawaida yaani lilichimbwa urefu wa futi nane

    zaidi. Nilipouliza sababu yakumfanyia hivyo. Vijana

    waliokuwa na furaha sana walinijibu kwa cheko la raha.

    "da huyu mzee naweza kurudi katutesa sana" mimi

    nliondoka zangu baada ya yote yaliyotukia eneo hilo.

    Nilirudi nyumbani kwa kina schola ikiwa na wasiwasi wa

    kuwa nimechelewa. Nilipofika nyumbani anapoishi schola

    na wazazi wake. nilikuta mlango umefungwa na taa

    zimeshazimwa. moyo ulinienda mbio wapi nitalala?

    niliogopa kugonga kwa kuwa sikujua sheria zanyumba hii

    mapema. lakini pia nilifahamu kuwa haikuwa tabia nzuri

    kurudi usiku wa giza zito kwa mtoto wa kike kwa familia

    yeyote yenye maadili.

    "sasa Nitalala wapi?" ni maswali yaliyosumbua akili

    yangu. nilipotaka kugonga nikarudi tena nyuma nkihofia.

    moyo ulizidi kuniendambio zaidi na zaidi. nlipokuwa

    nimezubaa je hapo, niliisikia sauti kutokandani ya nyumba

    aliyokuwa akiishi schola. ilikuwa ni ya kiume

    "wee ni nani?" iliuliza kwa mamlaka, sauti hiyo haikuwa

    ngeni kwangu. alikuwa ni mzee Ngwere bab yake na

    Schola. niliitika kwa sauti ya chini sana sauti ya hofu.

    "mimi baba" Mzee Ngwere aliniigiza kwa kubana pua.

    "mimi baba!" kisha aliweka ukali "pumbavu sma wewe

    nani sina mtoto kahaba anayetembea usiku wa manane"

    baba yake Schola alikuwa ni mkali kupitiliza hivyo kufanya

    wengi kumogopa. nilipkuwa nimesimama nilihisi mkojo

    ukinitoka na machozi yaklowesha mashavu yangu. ndipo

    hapo nikakumbuka kuwa kilichoniliza ni kuitwa kahaba.

    nililichukia hili jina kulik jina lolote. ni jina lililodhalilisha

    wasichana vya kutosha. ni jina la kifedhuli kuita msichana

    asiye heshimika mbele ya jamii. msichana mchafu. nikalia

    zaidi hata uchungu ukanishika. nilipokuwa bado

    nimesimama pale pale, nilimsikia mama yake schola

    akizungumza kwa sauti ya chini sana. saui ya usingizi.

    "inawezekana ni shoga yake schola bwana acha

    kupigizana naye kelele" nilipojitahidi kusikiliza nikaambulia

    ukimya uliotanda ghafla humo ndani. mara nikasikia

    mlango uliofumguliza na schola alisimama mbele yangu.

    alikuwa na khanga moja peke yake aliyojifunga lubega.

    alikuwa akifikicha macho yake kuutoa usingizi. "ingia

    ndani" aliongea taratibu kwa kubughuziwa. alionesha

    hivyo kwa kuukunja mdomo wake na kuuvimbisha kwa

    mbele. nilifunika kombe mwanaharamu apite. tukaingia

    ndani nikijitahidi kumchangamkia Schola. lakini yeye

    hakonesha lolote juu ya furaha. "tulale bwana

    utanihadithia yote kesho" mimi nikajsemea moyoni

    'sidhani kama kesho nitakuwepo hapa tena' usiku

    ukaniteka usingizini kama ulivyofanya kwa wengine.

    schola akakoroma mimi nikakoroma zaidi kwa uchovu. ni

    vibao alivyopigwa mapajani schola ndivyo viliniamsha na

    mimi pia "mnalala hadi sasa hivi watoto wa kike leo

    wikiend amkeni mfanye usafi"

    ni mimi ndiye nilianza kuamka hivyo mama alipotoka

    nilimuamsha schola kuwa tuamke tufanye usafi.

    nilipokuwa nikitoka chumbani kuelekea nje. kwenye korido

    lililounganisha vyumba, nilikutana na Mzee Ngwere.

    Aliniambia "wewe bado upo?" nilimsalimia "shikamoo

    baba" akaniambia "baba yako nani? baba yako ni yule

    asiye na aibu kwenda kutembea na watoto wadogo"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alinyamaza akawa anachukua hatu kutoka nje. Nilifahamu

    kuwa maeneno hayo yalikuwa yakimuhusu mzee nyegezi.

    Mimi nilisimama nikimtazama. Alinigeukia na kuniambia

    "nikirudi sihitaji kukukuta nyumbani kwangu" haya yote

    Schola alikuwa akiyasikia. Niliendelea kuzubaa kwa muda

    nisijue cha kufanya. Ndipo nilimuona Schola nae akitoka

    nyuma ya mlango, akiwa na uso wa huzuni. Nilipomuona

    schola, donge la uchungu likanikaba. Machozi yalipochoka

    kutulizana kwenye macho yangu, yakataka kudondoka.

    Nilijikaza Schola asinione kuwa nadeka. Alinikumbatia

    kwa liwazo, baada ya kuniona nikilengwa na machozi.

    Sikuyazuia tena. Nililia, nikalia kwa sauti ya juu zaidi.

    Schola akachukuwa jukumu la kunibembeleza "usijali

    Bianka(jina ambalo walinizoea wakati nikiwa shule)

    nyamaza" nikamwambia "Schola sina pa kwenda rafiki

    yangu, sina ndugu wala mtu wa kumkimbilia" kilio

    kikanikaba koo, nikashindwa kuzungumza zaidi; nikabaki

    nikigugumia kwa maumivu. Mama yake Schola naye

    alitoka chumbani kwake, na kutufuata sebuleni tulipokuwa

    mimi na Schola. Tulikuwa kwenye makochi yao sebuleni

    hapo, nikimuhadithia Schola kila lililotokea nyumbani kwa

    Mzee Nyegezi. Sikuthubutu kumueleza yeyote kuhusu

    safari yangu ya Gamboshi. Niliogopa kuogopwa na watu.

    Mama yake Schola alikuwa akinisikiliza kwa umakini.

    Mashavu ya Schola yalikuwa chapa chapa kwa machozi.

    Mama yake Schola aliropokan "kumbe yule mzee hana

    aibu? Yaani alikutenda hayo ikiwa bado mama yako yu

    hai?" ndipo wote mimi na Schola tulishituka kumuona

    mama yake Schola akiwa eneo hilo. Hatukujua ni muda

    gani alikuwa akitusikiliza. Wala hatukusikia ujio wake.

    Nilisimama kwa uoga.



    Sikuthubutu kumueleza yeyote kuhusu

    safari yangu ya Gamboshi. Niliogopa kuogopwa na watu.

    Mama yake Schola alikuwa akinisikiliza kwa umakini.

    Mashavu ya Schola yalikuwa chapa chapa kwa machozi.

    Mama yake Schola aliropokan "kumbe yule mzee hana

    aibu? Yaani alikutenda hayo ikiwa bado mama yako yu

    hai?" ndipo wote mimi na Schola tulishituka kumuona

    mama yake Schola akiwa eneo hilo. Hatukujua ni muda

    gani alikuwa akitusikiliza. Wala hatukusikia ujio wake.

    Nilisimama kwa uoga. "shikamoo mama" mama yake

    alitabasamu kwa huzuni. Tabasamu la kuniridhisha

    nisiogope. Akaniambia "marahaba mwanangu. Usiogope,

    nilikuwa nikiyasikia yote uliyokuwa ukimwambia Schola

    nimesikitika sana ulioyapitia. Mimi si kama Mzee Ngwere.

    Nadhani unamfahamu baba yenu alivyo mkali? mimi

    nitakusaidia" 'msaada' macho yangu yalitoka pima. Moyo

    ukanilipuka kwa furaha. Sikujuwa kama masikio yangu

    yalikuwa sahihi na kilichoongelewa. Mama yake Schola

    alijumuika nasi katika yale makochi na kujibweteka katika

    moja wapo lililowazi. Ilikuwa karibu nami. kisha alikuwa

    akiongea kwa kututazama kwa awamu. "inabidi Bella

    uokoke ili uachane na haya mambo ya kutanga tanga

    huku na huko kusiko na mpango. Wewe bado binti mdogo

    sana. Vipi kuhusu shule?"

    hapo ndipo nilipokuwa napataka. Sikuhitaji maswala ya

    uokovu kwa sababu nguvu nilizo nazo zilinilinda na kifo.

    Sikuhitaji wokovu ungenikimbizia nguvu nilizopewa kutoka

    Gamboshi. Nilijibu haraka haraka kuhusu shule.

    "Nashukuru mungu Mzee Nyegezi alinipatia pesa ya

    kutosha lakini msichana wake yule Irene.." kabla

    sijaendelea chochote mama yake Schola akadakia. "ptuu

    mbaka sia" alitemea mate ndani ya blazia aliyoivaa, kisha

    aliongea neno la kichaga na kuendelea kuzungumza

    "umenikumbusha huyo mtoto jamani amekuwaje siku

    hizi?" nikamuuliza "kwani unamfahamu mama?" alimjibu

    "wewe kwani humfahamu yule?" aliijibu kwa ushabiki

    kidogo akautia na umbea wa kiuanamke. Kisha

    alimuangalia Schola kama alikuwa akimkumbusha jambo.

    Sasa akawa anazungumza kwa sauti ya chini kidogo.

    "yule binti si ndiyo yule aliyefiwa na wazazi wake na

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ugonjwa wa ukimwi? Na yeye aliupata baada ya wazazi

    wake kutotambua kuwa wana ugonjwa huo hivyo

    walimuambukiza na mtoto wao?" schola akaonekana

    kukumbuka jambo naye akadakia "we mama kwani huyo

    Irene ndiyo yule wa mzee Chanduku?" macho ya mama

    yake na Schola yakang'ara kwa furaha na kitabasamu

    chepesi kikapitia papi zake akajibu kwa shahuku na

    mbwembwe zote "ndiyo huyo" alicheka kidogo akaendelea

    "ningeshangaa ungesema humfaamu" kisha alinigeukia na

    kuniuliza tena "enhee ikawaje? Hivyo hakukurudishia pesa

    zako?" chozi likaniponyoka. nikahisi midomo yangu

    ikiropoka kitu ambacho sikukitarajia. Nakiri ilikuwa mara

    ya kwanza kwangu kudanganya. Lakini nilikuwa na

    sababu za kumdanganya mama Schola. "hakuniachia hata

    sumni" aliniambia "basi usilie mama ukilia kwani ndio

    mwisho wa tatizo?"

    nilipanga kumdanganya hivyo, ili pesa niliyobaki nayo

    inisaidie nikiwa shuleni na nikitoka shule nipate kidogo ya

    kunisaidia kuendesha maisha yangu. Mama yake schola

    alinieleza

    "Bella nitakupatia kesho fedha za ada na matumizi kidogo

    shuleni ninachokuomba usome kwa bidii na uzingatie

    masomo ukiwa unamtegemea mungu yeye ndiye msaada

    wako peke yake" niliitikia kwa furaha tukakivunja kikao

    hicho. Mimi na Schola tukaendelea na shughuli za hapo

    nyumbani, huku mama yake Schola akituaga kuwa

    anaelekea kazini kwake. Tuliandaa kila kitu, tulipomaliza

    mimi nililala. Nilijifunga upande wa khanga pamoja na

    maungo yangu ya ndani nikiyahifadhi katika skintyt tu

    peke yake. Ilikuwa ni khanga nyepesi sana. Khanga

    iliyoonyesha maungo yangu ya ndani jinsi nilivyoumbika.

    Schola aliniaga kuwa anaenda kumpelekea mama yake

    chakula kazini. Mimi kwa kuwa nilichoka sana nilimuomba

    nipumzike. Nilikuwa nasikia kizunguzungu cha ajabu.

    Nikalala fofofo. nkiwa usingizini, nilisikia mikono

    iliyopembua khanga yangu niliyoivaa na kuibakisha skin

    tyt. Bumbuwazi ilinifanya nisizungumze chochote zaidi ya

    kusubiri kutazama kile ambacho kilikuwa kinaenda

    kutokea. Jasho lilinitiririka mapigo ya moyo yakanienda

    mbio. Nilipokuwa bado nikatafakari nikiwa nimejifanya

    kulala, harufu ya pombe ikapenya katika pua zangu.

    Harufu ya pombe kali iliyoletwa na mdomo uliokuwa

    ukigusa papi zangu. Mikono migumu iliyokuwa ikitekenya

    matiti yangu na kifua kilichokuwa kimebebwa na kifua

    changu. Vilikuwa sambamba kusuhulikia mwili wangu.

    Nilipofungua macho sikuamini nilichokiona. Mapigo ya

    moyo yalizidi kunienda kasi zaidi na zaidi. mtu ambaye

    alikuwa juu ya kifua changu si mwingine bali ni Mzee

    Ngwere. Aliponiona nimeshituka, alitabasamu kifedhuli.

    Tabasamu la kishetani. Akaniambia

    "hii ndio kodi yako"

    akacheka akiwa anaendelea kutalii mikono yake juu ya

    kifua changu.

    "unaonaje nikaonja ladha yako binti yangu mrembo?"

    nilihisi kuishiwa nguvu nisijue cha kufanya. Ghafla nilihisi

    nguvu za ajabu zikinijia nguvu za kumuangamiza. Nguvu

    za kuitoa roho yake zikinisukuma kufanya jambo ambalo

    sikutaka kulifanya. Lakini ilinibidi. Nikageuka paka akiwa

    anawaza kuitoa skini tyt yangu. Nilijigeuza paka wa kijivu

    lakini sikuwa paka wa kawaida. Mzee Ngwere nafikiri

    pombe zilimuisha, akawa haamini kinachotokea. Alipiga

    kelele

    "nisamehe Bella, nisamehe mwanangu"

    alikwishajigonga ukutani, akaisalimia sakafu baada ya

    kuanguka kutoka katika kianda. Aliendelea kuhaha

    "usiniue Bella nitakpa chochote unachokitaka"

    Nikiwa katika umbo lile lile la paka. Mlangoni nilipokuwa

    nimejibanza nikitaka kuita roho ya Mzee Ngwere kwa

    hasira niliona kivul cha mtu akichungulia. Mzee Ngwere

    alikuwa tayari ameshavua suruali yake akiwa amebaki na

    nguo yake ya ndani pekee.

    Mzee Ngwere aliendelea kunisihi nisimdhuru. Mimi pia

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    sikutaka kumfanya chochote ili yule mwenye kuchungulia

    ajitokeze hapo alipojificha. Nilikuwa nikimtisha Mzee

    Ngwere kwa kuyageuza geuza macho yangu na kuwa

    yanayotisha. Niliipinda shingo kwenda juu ikageuka

    nyuma ikaangalia chini mbwembwe zote zilikuwa ni

    kumtisha Mzee Ngwere.

    Akaropoka nilichokuwa nikikitaka.

    "sintofanya tena nilichodhamiria kukifanya kwako Bella, si

    kwako wala kwa mwingine. Sintokubaka Bella"

    alikuwa akilia kama mtoto mdogo. shati kalivua, kitambi

    kimemsimama.

    "Naomba unisamehe bella ninakuruhusu ukae hapa kwa

    kipindi chote unachokitaka"

    nikayayuka pale nilipokuwa kama paka na kuwa eneo hilo

    hilo bila kuonwa na mtu mwenye macho ya kawaida asiye

    na nguvu za kichawi asingeweza kuniona. Yule aliyekuwa

    anasikiliza yote ambayo alikuwa akiyazungumza Mzee

    Ngwere, alikuwa ni schola. Aliingia chumbani akiwa na

    mshangao mkubwa usoni mwake. Alinipita mimi

    nilipokuwa nimesimama. Hakuniona kwa sababu mimi

    nilimuoneshea kidole kidogo cha mwisho na hiyo ilikuwa

    ni njia ya kumfanya asiye na nguvu za kichawi akupite

    wala asihisi kuwa eneo hilo kulikuwa na mtu. Schola

    alimuuliza baba yaje

    "baba niliyoyasikia yote ni kweli ama?"

    mzee ngwere hakuamini kama nilikuwa nimetoweka.

    Nilimuona akimuoneshea mimi nilipokuwa nimejigeuza

    kama paka eneo ambalo nilikuwa nimekaa.

    "bella.. Bella"

    alikuwa amechanganyikiwa. Schola alitoa kicheko cha

    kuudhika

    "ndiyo Bella wewe umembaka"

    nadhani hata mzee ngwere mwenyewe pia akujielewa

    kama ni yeye ndiye aliropoka yale yote ambayo

    ameyaropoka. Alianza kulia kwa majuto. Alilia kwa

    uchungu sana. Akamsihi schola asimueleze mama yake.

    Kilikuwa ni kitendo cha aibu. Kitendo cha kumuaibisha

    yeye pamoja na familia nzima. Akamwambia schola zaidi.

    "mlete rafiki yako muishi naye hapa nyumbani. Muishi

    kama ndugu"

    alivaa shati na suruali yake kisha alitoka kitandani.

    Aliposimama alimfuaa schola akamwambia

    "mwanangu! Bella ni mchawi kaa makini naye na

    ninakuomba usimuleze mama yako kuhusu hili

    uliloshuhudia"

    schola hakujibu kitu ila alimuangalia kama kinyaa.

    Alipofunga mlango mzee ngwere, nyuma akasindikizwa na

    sonyo alilolitoa Schola.

    "hadi naona aibu"

    schola alijishika kichwa chake kama kilikuwa kinataka

    kunyofoka. Alizama kwenye tafakuri nzito. Alikuwa

    amekaa kitandani kajiinamia. Mimi nilitoka mule chumbani

    kupitia ukutani. Wachawi hupita katika pembe za kuta zile

    nne na huwezeshwa na kivuli chao. Nilipita na kuelekea

    chumbani kwa mzee ngwere. Nilipita ukutani na kumkuta

    akiwa amejilaza. Alishitushwa sana na kuniona pale.

    Alipotaka kupiga kelele, nilimnyamazisha. Nilimwambiwa

    kwa sauti ya chini sana

    "ole wako upige kelele" alikuwa ameyatumbua macho

    yake akitazama mlango. Mlango alikuwa ameufunga tena

    kwa ufunguo kwa ndani. Nikajua anajiuliza nimepita vipi.

    Nikaupata ulimi wangu. "habari ya uchawi ife mdomoni

    mwako. Siku utakayojitia kuropoka mimi ni mchawi kwa

    mtu mwingine! Damu yako na nyama vitakuwa halali ya

    mizimu ya babu wa kale" nilijaribu kumtisha bila kujua

    kama nilikuwa sahihi au lah! Niliingia chooni na kuoga

    kisha nilirudi chumbani alipokuwa salome. Nilimkuta

    salome vile vile kajiinamia. Alishituka sana kuniona.

    Aliniuliza kwa mshangao. "ulikuwa bafuni muda wote?"

    nilitabasamu kidogo kisha nilimjibu kwa kujiamini. "ndiyo

    nilikuwa uwani nafua nilipomaliza nikaona vyema nuoge

    kabisa" hakuonesha kujali sana kisha alinieleza kuwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alimkuta baba yake, Mzee Ngwere akiwa kama

    amewehuka. "amewehuka kivipi?" nilimuuliza nikijifanya

    sina ninachokijua. schola alionekana kuchanganyikiwa

    sana na tabia ya baba yake. Alinieleza ilivyokuwa

    "imenishangaza sana kumkuta akitaja taja jina lako.

    Alikuwa amevua nguo zote. Imenishangaza sana Bella"

    mimi nilitabasamu tu bila kumjibu chochote. Nilimshauri

    schola asijiumize akili yake kwa ajili ya baba yake.

    Nilimsihi apumzike. "kwani wewe bella hukuwa humu

    chumbani?"

    nilishituka sana. Nilishituka kuhisi au kuna tatizo

    nililifanya? Au kuna makosa niliyafanya katika kumzuia

    asinione? Nilikosea wapi wakati kila nilichoelekezwa kule

    Gamboshi nilifanya sahihi? Schola akanishitua nikiwa

    katika mawazo.

    "bella nakuuliza? Baba hajakufanyia jambo lolote baya

    kama hilo?"

    sikumjibu haraka ila nikamtupia lile tabasamu mwanana

    kumlagaia tuupoteze uelekeo wa upepo wa mazungumzo

    hayo. Nikamtupia swali

    "ni kawaida ya mzee Ngwere kunywa pombe zake. Leo

    hajaelwa?"

    nikayaona macho ya schola yakikumbuka jambo.

    "Inawezekana mzee amelewa?" alitulia kidogo kisha

    akauinua uso wake na kuniuliza

    "lakini pombe gani awe uchi ndani ya chumba changu

    akikutaja wewe na mimi nilikuacha ukiwa umelala?"

    hapo nikaona kizungumkuti kipya kimeanza kuleta uzito

    wa kuishi ndani a nyumba hii kwa amani. Sikupata la

    kumjibu.

    Tulikaa katika kile chumba mpaka jua lilipo poteza nguvu

    yake. Jioni ikawa jirani kuukaribisha usiku. Ndipo wote

    tulishituka yaani mimi na Schola tulishituka tulichokuwa

    tunakisikia. Ni vishindo vya mtu akipigana. Ngumi

    zilizokuwa zikirushwa ukutani na kutoa kishindo kizito

    kilichotufanya tuangalieni kwa mshangao.

    "nini hicho?"

    schola alikuwa wa kwanza kuuliza ni nini kilichokuwa

    kinatukia. Sauti za mtu akiuguliza maumivu na vicheko

    vya ajabu vikatawala ndani ya ile nyumba. Mimi niliogopa

    schola akaogopa zaidi. Alinisogelea kana kwamba mimi

    nilikuwa na chochote cha kumsaidia schola. Hata mimi

    niliogopa sana. Kuna wakati ambao kuta pia zilitingishika

    kutokana na vishindo vile tulivyokuwa tunavisikia. Schola

    akasema

    "baba yupo chumbani"

    mimi pia macho yalinitoka pima nikajikuta nikiropoka

    pamoja naye.

    "twende tukamtazame"

    utata ukaja ni nani wa kuanza kutoka? Mimi niliogopa

    lakini sikuwa muoga sana kuliko schola. Schola yeye

    aliogopa sana kwa kua hakujuwa chochote kuhusu

    uchawi. Hata kama alikuwa akiujuwa, alikuwa akiusikia tu

    kama si kuusoma kwenye vitabu. Mimi niliujua uchawi

    kwa kuwa mimi mwenyewe nilijithibitishia mimi ni mchawi

    niliyekubuhu. Nilimshinda Mzee Manyota nikamshusha

    nyota zake, kwanini nisijue nini kilichomkuta Mzee

    Ngwere? Hivyo mimi nikawa wa kwanza kutoka.

    Wakwanza kuongoza mpaka katika chumba cha wazazi

    wa schola. Mwendo ulikuwa wa kunyata schola alinishika

    nyuma kana kwamba alikuwa akiogopa sana. Alikuwa

    akitetemeka kupita kiasi. Mimi niliogopa lakini si

    kupitiliza. Niliufungua mlango taratibu, taratibu sana.

    Nilipoufungua mlango nikapigwa na butwaa. Butwaa ya

    kuuona mwili wa mzee ngwere ukiwa umeibusu ardhi

    chini ya kidimbwi kidogo cha damu. Sikuufungua moja

    kwa moja mlango, hivyo schola hakuweza kuona mwili wa

    baba yake. Mwili ulioharibika vibaya na kutapakaa damu

    kila sehemu yake. Akika alikuwa amepata adhabu kali

    sana. Aliikumbatia sakafu kwa heshima na kuogelea

    katika dimbwi la mate damu nzito iliyoanza kuganda.

    Nilihisi kutapika. Nilipokuwa katika hali ya kuduwaa,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    schola alitamani kuona nilichokuwa nikikitazama.

    "kuna nini bella mbona hunipishi?"

    ndipo niligundua kuwa nilimziba kuingia ndani bila

    kutambua kuwa nimemzuia asiingie. Akanipiga kikumbo

    nikapoteza muhimili wa kuendelea kusimama

    nikaikumbatia sakafu pia nikiwa namtazama marehemu

    Mzee Ngwere. 'ndiyo' sikuhitaji ushahidi wa daktari

    kunithibitishia mzee ngwere alikuwa hai. Nilihisi baridi

    lijinipiga na uoga kukithiri. Sikutamani kuona misiba ikizidi

    kunifuatilia. Sikutamani kuona mimi nikiwa chanzo cha

    watu kufa sikutamani, sikutaka kabisa. Nikiwa katika

    kuduwaa huko bila kukumbuka kama nilikuwa

    nimeongozana na schola ndipo nikashitushwa na

    kishindo. Kishindo kilikuwa kizito kama gunia lililoponyoka

    mikononi mwa wabebaji. Alikuwa ni schola. Naye

    aliisalimu ardhi kwa mshituko na kuuangukia mwili wa

    baba yake. Ilikuwa salama yake kuuangukia mwili wa

    Mzee Ngware. Kama isingekuwa hivyo basi angemsalimia

    baba yake huko aendapo kwa kuwa angepasuka kichwa

    pale pale na kuwa amiti ya pili ndani ya ile nyumba



    Mzee Ngwere. 'ndiyo' sikuhitaji ushahidi wa daktari

    kunithibitishia mzee ngwere alikuwa hai. Nilihisi baridi

    lijinipiga na uoga kukithiri. Sikutamani kuona misiba ikizidi

    kunifuatilia. Sikutamani kuona mimi nikiwa chanzo cha

    watu kufa sikutamani, sikutaka kabisa. Nikiwa katika

    kuduwaa huko bila kukumbuka kama nilikuwa

    nimeongozana na schola ndipo nikashitushwa na

    kishindo. Kishindo kilikuwa kizito kama gunia lililoponyoka

    mikononi mwa wabebaji. Alikuwa ni schola. Naye

    aliisalimu ardhi kwa mshituko na kuuangukia mwili wa

    baba yake. Ilikuwa salama yake kuuangukia mwili wa

    Mzee Ngware. Kama isingekuwa hivyo basi angemsalimia

    baba yake huko aendapo kwa kuwa angepasuka kichwa

    pale pale na kuwa maiti ya pili ndani ya ile nyumba.

    Nilichanganyikiwa sana na kuhisi kichwa kikizidiwa

    usingizi na mimi nikapokelewa na usingizi mzito usingizi

    nilioukataa sasa ukawa usingizi kabisa. Nikapoteza

    fahamu. Nilipozinduka nilijikuta kati kati ya watu wengi

    sana. Yaani kilikuwa ni kikundi cha watu wengi sura zao

    zilitisha sana. Usoni walijichora chora kama lile kabila la

    kusini linalojichora usoni kama kuenzi utamaduni wao.

    Mapigo ya moyo yalinienda mbio nikawa nikiwatazama

    kwa zamu. Sikubahatika kumfahamu hata mmoja.

    Nilitumia muda mwingi kuwatazama nikafahamu kuwa

    walikuwa wakicheza huku wakisujudu. Nilianza kusikia

    harufu mbaya kama ile ya Gamboshi. Nilipowatazama

    kwa makini nilifahamu watu hawa walikuwa uchi.

    Niliwasihi waniachie ila kila nilipojaribu kuzungumza wao

    waliongeza kasi ya kucheza. Walicheza kitu ambacho

    sikukifahamu wala sikusikia aina ya mziki au ngoma

    waliyokuwa wakicheza. Ndipo baada ya muda kupita

    nilimuona babu akinijia. Babu alikuwa aktika hali ya

    ujana. Kijana mwenye nguvu haswa

    "bella mjukuu wangu"

    alikuwa akitabasamu na alionesha hekima na busara sana

    katika sura yake. Nilimuangalia kwa huzuni naye akaweka

    sura ya hutuma akaniambia.

    "pole sana kwa yote yanayotokea lakini huna budi kupitia

    hayo ili ukumbuke kuwa makini katika kutimiza masharti

    uanyopewa"

    alicheka mpaka akakaukiwa. Mimi machozi yalinitoka

    nililia kwa uchungu kila nikikumbuka mateso nayoyapitia.

    Lakini kilichonishangaza muda huo wote sikuweza

    kunyanyua kiungo chochote cha mwili wangu.

    Klichonishangaza ni kuwa nilikuwa nimelala tu muda wote

    na kufunikwa na shuka la ajabu. Shuka la funza. Funza

    wengi waliokuwa wakinitambaa na kujenga umbile la

    shuka. Nililia sana nikamuomba babu anisamehe.

    "babu naomba unisamehe nimejifunza babu, nateseka

    sana"

    babu alicheka sana kisha alitoweka. Alitoweka yeye

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    pamoja na wale wengine ambao walikuwa wakicheza.

    Ghfla nikazinduka katika usingizi. Usingizi mzito ambao

    nilijishitukia kuona nilikuwa nikilia. Nilijikuta nikiwa

    hospitali nikiwa nimesimamiwa na daktari pamoja na

    mama yake schola. Nikiwa bado nawatazama sijuhi nini

    kinaendelea, mama yake schola aliniuliza

    "bella kuna nini jamani?" alikuwa amekabwa na kilio huku

    akipiga piga miguu yake chini. Alitumia upande wake wa

    khanga kuziba mdomo kana kwamba mdomo ulikuwa

    ukitoa machozi yaliyolowesha uso wake mzima. Akalirudia

    lile lile swali

    "kuna nini kimetokea jamani? Niambie bella niambieee"

    kilio kikamuangusha chini kwa uchungu akawa anagala

    gala kama kuku anayetaka kukata roho. Wauguzi

    walimnyanyua na kumfunika khanga iliyoanza kuiacha

    kiuno chake kisha wakamtoa nje ya wodi. Mimi nikiwa

    bado katika kuduwaa huko nikaipata sauti yangu

    "schola"

    nilimtazama daktari aliyeniuliza kama vile hakusikia kuna

    kitu nilichozungumza

    "unasema"

    nikarudia tena kuita vile vile kwa sauti iliyokwaruza

    "schola"

    nikiwa bado ntafuta swali sahihi ninalotaka kuuliza.

    Daktari akawa amenielewa nini nilikuwa nataka kuuliza

    akaniambia

    "yule mwenzio mliyeletwa naye jana pamoja na ile maiti

    ya yule baba?"

    alikuwa kama ananiuliza

    nikatingisha kichwa kama vile nilikuwa nakubali,

    kumaanisha alipatia alichouliza kilikuwa ni sahihi na

    nilichotaka kufahamu

    "yeye hadi sasa hajapata nafuu"

    alinyamaza kidogo kisha alikohoa kusuuza koho.

    Alipomaliza kuishughulikia dripu aliyonitundukia, aliniuliza

    "kwani nini kimetokea jamani?"

    sikuwa na nguvu ya kumjibu chochote nikawa

    nikimtazama tu bila kumpa jibu lolote. Akanieleza

    "yaani hapo ulipokuwa umelala ulikuwa unaweweseka

    sana ulikuwa ukirusha miguu kama ulikuwa unakata roho

    ndiyo tukamuita huyu mama aje akutazame ila yeye

    mwenyewe kumbe yupo kwenye kitendawili"

    nikiwa bado namtazama yule daktari yeye aliendelea

    kubwabwaja

    "namuonea hutuma sana mama wa watu yaani

    kachanganyikiwa kupita kiasi sijuhi hata kama amekula"

    alipoona simpi ushirikiano wowote, alitoka zake kimya

    kimya.

    ......................................

    Siku ilikatika baada ya schola kuzinduka. Alikuwa kama

    mwehu aliyewehuka. Alichokumbuka cha kwanza kukitaja

    ni jina langu.

    "bella"

    ikashangaza akili yake ilivyofanya kazi upesi

    akamkumbuka na baba yake.

    "baba"

    alipoita baba ikawa sawa na kusugua kidonda kwa

    msumari wa moto katika moyo wa mama yake. Mama

    yake Schola alianza kilio. Kilio kilicholeta huzuni kwa kila

    mtu.

    Kwakuwa schola hakujua sababu ya mama yake kulia

    naye akaunganisha kulia. Kilio kikawa juu ya kilio. kila

    mtu akalia. Walilia huku wakibembelezana wasilie zaidi.

    Dakika chache baadaye walinyamaza wote kwa pamoja.

    Mimi nikaruhusiwa kutoka kitandani baada ya kuonekana

    nilikuwa nina nguvu za kutosha. Ndugu na jamaa wa

    mama yake na schola, walikuja kumpa pole. Pole ya

    kufiwa na mume na matatizo yaliyomkuta nyumbani

    kwake. Mmoja wa marafiki zake akamuuliza.

    "shoga kwani nini haswa mbona sikuelewi?"

    "mama jabu!"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    uchungu ukamkamata, lakini akaendelea

    "ndugu yangu naona mauza mauza, hadi sasa sielewi nini

    kimetokea"

    mama schola akaangua kilio. Mimi nilikuwa na jukumu la

    kumpooza schola aliyekuwa akilia kwa uchungu. Hospitali

    ikawa kama eneo la msibani. Ikabidi tuondolewe baada ya

    schola naye kuonekana alikuwa amepata nafuu.

    "nashukuru sana dokta"

    ni mimi pekee ndiye nilikuwa na nguvu ya kuzungumza.

    Tuliondoka mpaka nyumbani kwa kina schola maeneo ya

    kigogo mbuyuni. Tulikuta tayari wameshaweka maturubai

    ya msiba. Si schola wala mama yake, hawakushikika kwa

    vilio. Walijidondosha ardhi ikawapokea. Waligala gala

    kama walikuwa wanawashwa na michanga. Jua kali lakini

    hawakulijali. Kilikuwa ni kilio huku wakilitaja jina Mzee

    Ngwere. Ni hapo schola akaropoka bila kujitambua

    "baba pombe ndio zimekuuwa baba yangu, sijuhi ni nini

    kilikuadhibu chumbani kwako baba yangu jamani baba

    wewe baba wewe..."

    nilipokuwa nikisikiliza huku nikijitia kumbembeleza,

    nilijaribu kumpooza asije kuropoka yote, yote

    yaliyomuhusu baba yake kumkuta chumbani kwangu

    akiwa uchi akiniomba msamaha. Akinisihi nisimzuru au

    kumfanyia lolote baya. Si unajua tena waswahili? Licha ya

    mimi tulikuwa wote chumbani na schola lakini watu

    wangefanya mambo yakawa makubwa. Ingewezekana

    hata wangebumburuwa siri za uchawi wangu. Ndio hapo

    wangenitambua. Ningewamaliza wote. Kwani nilishindwa

    nini? Hakuna kilichokuwa kikiniogopesha zaidi ya nguvu

    zangu mwenyewe. Niliamini nilikuwa na nguvu za kutosha

    kufanya chochote na kwa mamlaka niliyopewa kutoka

    Gamboshi. Watu wakazidi kuongezeka na kuamsha kilio

    cha schola na mamaye kama vile hawakuwa

    wakitabasamu muda mchache uliopita ndugu wa mume

    wakawa wamefika msibani na wale wa mke, mama yake

    schola. Kwa kuwa ndugu wa mume ndio ndugu wa

    marehemu hivyo wao ndiyo walikuwa wakisikilizwa

    kuhusu msiba na ratiba zake zote. Yaani wapi maiti

    yatazikiwa na kila kitu kwa ujumla. Baadaye jioni baada

    ya kukivunja kikao cha wanafamilia, walikuja kutueleza

    walichopanga.

    "kutokana na kifo chake kuwa cha utata huyu ndugu yetu

    hatazikwa hapa mpaka maiti yake ionwe na wazee wa

    koo zetu"

    mama yake schola alipinga

    "jamani hakuna kifo ambacho ni cha utata hii yote ni

    mipango ya mungu msijaribu kutaka kuingilia kati kazi ya

    mungu mwacheni mume wangu apumzike jamani"

    mimi nilifurahi kuuona msimamo wa mama schola

    nikaunga hoja kwa kutingisha kichwa kuwa nimekubaliana

    na usemi wake.

    "hapana ni lazima hiki tulichokisema kitimie na

    tumeshaeleza nyumbani kuwa maiti tunaipeleka huko"

    moyo wangu ukajikunja nikamuangalia yule muongeaji

    kwa hasira. Nilipotaka kufanya jambo kisiri siri,

    alinigeukia na kunitazama kwa macho makali. Akamuuliza

    mama yake schola

    "na huyu ni nani katika familia yako"

    mama schola alijibu kivivu bila kujali kile alichojibu.

    "mtoto wa mdogo wangu bwana"

    yule aliyeuliza alitabasamu na nilipoyatazama macho yake

    yaling'aa kama paka. Nikawatazama watu wengine kama

    waliona kile ambacho mimi nilikiona, lakini niliona hakuna

    ambaye alishitushwa na kuona chochote. Kila mtu

    aliendelea na shughuli zake. Mimi nikasonya. Nikawa

    nimemjua kuwa yule pia ni mchawi mwenzangu. Akatoka

    kuwafuata wenzake nje.

    Kisha familia ikakubaliana kuwa msiba uhamishiwe huko

    kijijini kwao. Mzee Ngwere alikuwa ni mmwera wa lindi

    wilaya ya ruhangwa. Wengi tulibaki kuhani msiba lakini

    schola na mama yake walienda pamoja msibani. Walienda

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kuwasikiliza wazee wa ukoo wanasemaje kuhusu kifo cha

    Mzee Ngwere. Mimi nilianza kushikwa na uoga nisijue

    kuwa kama kuna uwezekano wa kujulikana au lah!

    Walipofika huko, walitujulisha wote tukafurahi. Sasa

    mchakato ulipoanza wa kumtafuta mchawi nani, ndipo

    kikatokea kile kitu cha ajabu. Nililala usingizi mzito sana,

    usingizi ambao sikuwahi kulala tangu nizaliwe. Lakini

    mimi sikuwa tena katika mwili wangu. Niliutazama ule

    mwili nikaona lilikuwa ni gogo tu limelala pale. Pembeni

    yangu akawa amesimama babu yangu Mzee Matonde.

    Alinieleza

    "mjuukuu wangu yule mzee amekufa kutokana na adhabu

    aliyopewa na mkuu mwenyewe, nataka twende pamoja

    huko katika huo msiba ukashuhudie jinsi ambavyo mkuu

    wetu ana nguvu na watakachosema hao wazee wao wa

    ukoo"

    kufumba na kufumbua, mimi na babu tulikuwa mbele ya

    nyumba fulani ya udongo. Kuliwekwa turubai kama pale

    kigogo mbuyuni na kulikuwa na watu wachache

    waliouzunguka moto. Mimi na babu tulikaa mbali kidogo

    lakini tulikuwa kama tuna mashine ya x-ray machoni

    mwetu. Tuliweza kuona kila kitu kilichokuwa kikiendelea

    mule ndani. Ndani ya ile nyumba ya udongo. Kulikuwa na

    wazee kumi na sita. Walikuwa ni wazee haswaa. Asilimia

    kubwa walikuwa ni wafupi na waliopoteza nguvu zao.

    Hakukuwa na mwanamke hata mmoja. Walikuwa

    wamemuweka Mzee Ngwere katikati yao wakiongea

    maneno ya ajabu ajabu. Maneno ambayo yalikuwa ni

    vigumu kuelewa. Nikahisi huenda walikuwa wakiongea

    lugha yao kama si kuongea lugha ya kichawi. Kati kati

    yao kukafuka moshi mzito mweusi. Kikatokea kiumbe cha

    ajabu. Kiumbe kilichotisha kiumbe hiki, kilikuwa kimevaa

    kaniki nyeusi na yeye kuwa mweusi zaidi. Alikuwa na

    mapembe. Alicheka kwa kicheko kikubwa sana.

    Nilipowatazama wale waliokuwa pale nje niliona walikuwa

    hawashitushwi na kicheko hicho. Pale nje nilimuona

    schola amejikunyata ndani ya blanket zito na mama yake

    akiwa anapikicha pikicha mikono yale karibu na moto

    kutafuta joto. Mimi niliogopa sana. Babu akaniambia

    "usiogope, tazama kwa macho yako na usikilize kwa

    makini"

    yule kiumbe nilipomtazama vizuri alikuwa na kichwa cha

    mbuzi, mbuzi mweusi sana. Aliendelea kucheka huku wale

    wazee wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini

    wakisujudu. Kicheko kilipomkatika alianza kuzungumza

    "kijana wetu amevunja miiko muda mrefu ya ukoo"

    wale wazee wakaitikia kwa pamoja

    "ndiyo mkuu"

    yule kiumbe ambaye alikuwa ametawaliwa na moshi kama

    kaa la moto. Moshi mzito mweusi aliendelea.

    "sasa sina cha kuwasaidia zaidi ya kuwaambia mumzike

    tu"

    mmoja kati ya wale wazee, vile vile kama alivyoinamisha

    kichwa alimuuliza mkuu bila kuinuo uso wake

    "mkuu tafadhali tunaomba tufahamu sababu ya kifo

    chake"

    yule kiumbe wa ajabu alicheka sana. Babu akniambia kwa

    sauti ya chini

    "ule ndio mzimu wa ukoo wao"

    yule kiumbe akazungumza

    "amediriki kunywa pombe ikiwa hairuhusiwi kuwa mlevi

    katika ukoo wetu. Sikumuadhibu mimi ila ameadhibiwa na

    kiongozi mkuu atupaye nguvu sisi mizimu ya koo zenu.

    Mkuu huyo amemuadhibu kwa kitendo cha kutaka

    kumbaka binti malkia wa Gamboshi"

    babu alinitazama akitabasamu. Mimi nikawa sijaelewa

    nikamuuliza babu

    "kwani yule kiumbe alimaanisha nini?"

    babu sasa akacheka zaidi akaniambia

    "ni nani basi aliyekutoa katika kiti cha umalkia wa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gamboshi?"

    he! hapo nikashituka zaidi.

    "babu ina maana mimi bado nina nafasi Gamboshi?

    Kwanini basi napata amteso ya kuhangaika huku na

    huko?"

    "siku utakapotimiza masharti ya mkuu"

    neno lile likawa sawa na kuniaga. Babu alipotea na mimi

    niliamka. Nilipoamka nilijikuta katikatia ya watu wengi

    wamenizinguka wakinishangaa.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog