Simulizi : Niliongea Na Shetani Ili Niwe Tajiri
Sehemu Ya Nne (4)
"amediriki kunywa pombe ikiwa hairuhusiwi kuwa mlevi
katika ukoo wetu. Sikumuadhibu mimi ila ameadhibiwa na
kiongozi mkuu atupaye nguvu sisi mizimu ya koo zenu.
Mkuu huyo amemuadhibu kwa kitendo cha kutaka
kumbaka binti malkia wa Gamboshi"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
babu alinitazama akitabasamu. Mimi nikawa sijaelewa
nikamuuliza babu
"kwani yule kiumbe alimaanisha nini?"
babu sasa akacheka zaidi akaniambia
"ni nani basi aliyekutoa katika kiti cha umalkia wa
Gamboshi?"
he! hapo nikashituka zaidi.
"babu ina maana mimi bado nina nafasi Gamboshi?
Kwanini basi napata amteso ya kuhangaika huku na
huko?"
"siku utakapotimiza masharti ya mkuu"
neno lile likawa sawa na kuniaga. Babu alipotea na mimi
niliamka. Nilipoamka nilijikuta katikatia ya watu wengi
wamenizinguka wakinishangaa. Nikawauliza kwa
mshangao pia
"kuna nini?"
mmoja kati ya wale alikuwa mmama aliyekuwa
ananifahamu. Alikuwa ni jirani akasema
"bella unaumwa?"
"hapana kuna nini kwani?"
"ulikuwa unaweweseka umetokwa na jasho jingi pamoja
na kuwa na joto kali sana. Tumejaribu kukuita muda
mrefu lakini hukuamka"
Nilijichekelesha kuwapoteza lengo. Na wakapotezeka
kweli, wakaendelea na shughuli zao. Msiba uliisha na
matanga tukaanua. Upweke ukamtawala mama yake na
schola. Upweke uliomkosesha raha, hata mimi na schola
hatukuweza kumpa tulizo la nafsi kama tulikuwa tukijaribu
kufanya. Nachoshukuru mungu, nilifanikiwa kuianza shule
nikiwa mwanafunzi wa bweni kwa msaada wa mama
schola. Nilijiapia ntasoma, nikauahidi moyo wangu
ntasoma kupitiliza. Uchungu wa shule nilionao niliuweka
kwenye masomo peke yake. Nilihudhuria kwa mara
nyngine tena masomo darasani nikiwa nina furaha tele.
Furaha ya kumuona tena Jordan na furaha ya kuwa
katika sare pamoja na wenzangu. Nlitumia muda wangu
mwingi kumsikiliza mwalimu na kujisomea pale
nilipoupata muda. Niliutumia ule muda wa prepo vizuri ili
niweze kuelewa pale nilipokuwa sipaelewei. Nakumbuka
siku moja nikiwa prepo majira ya saa mbili usiku. Mimi
nilikuwa peke yangu na meza nyingine walikuwa
wanafunzi kadhaa. Wavivu wachache wakaondoka kulala
baada ya nusu saa kupita. Mimi na kikundi cha rafiki
yangu Hilda ndio tulioendelea kukomaa zaidi. Punde
nikasikia nikiitwa.
"bella"
nilipotazama sauti iliyotoka upande wa dirishani,
sikumuona mtu. Mara ya pili ikaita upande wa kulia.
"bella"
nilipogeuka nako kukawa kama awali pale dirishani.
Nilipokuwa nikijiuliza ni nani. Bla kujua.ghafla nilisikia
kicheko kikilipuka kwa nguvu mbele ya ubao. Niliyaelekeza
macho yangu kule niliposikia kicheko kile. Alikuwa ni
babu. Nikawatzama wakina hilda kama walikuwa
wamemuona. Lakini wao walikuwa wanaendelea na
shughuli zao. Waliendelea kuinamia madaftari yao huku
sehemu yote ikiwa kimya kabisa. Nilipokuwa nikimtazama
babu, akili yangu ikahama. Nakiri akili yangu ilihama
kutokana na mawazo yangu ya kibinadamu hayakuwepo
tena. Akili ikachotwa nikafanya kile alichokuwa
akinielekeza babu kule ubaoni aliposimama. Babu aliniita
kwa kidole chake na mimi nilinyanyuka na kumfuata pale
alipo. Niliwapita wakina hilda. Nakumbuka nilimsikia hilda
akiniita
"bella"
sikuitika kwa kuwa sikujitambua zaidi ya kusikia na kuona
tu. Akaniuliza bila kujali kama niliitika au lah!
"leo umechemka mama uanenda kulala"
pia akaambulia patupu. Nilipofika eneo la ubaoni tu na
kumpa mkono babu, tukapotea. Tulipotea na babu katika
mazingira ya kushangaza wala sikujuwa nini kikundi cha
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hilda cha kujisomea wangenchukulia vipi. Mimi na babu
tulielekea Gamboshi. Tulipofika huko nikiwa bado
sijitambui, babu alinilaza kitandani kama vile vitanda vya
hospitali. Na kuchukuwa beseni la maji mengi lakini
yalikuwa meusi sana na kipande cha khanga aina ya
kaniki. Alianza kunikamulia mahi yale machoni mwangu
na kunilazimsha nipanue mdomo wangu. Nilipopanua
akaniambia niyanywe yale maji machafu nikatii. Kisha
alikuwa akiongea maneno ambayo sikuaelewa kabisa
wala sikujuwa ilikuwa ni lugha ya wapi. Kila
nilichofanyiwa sikuweza kuzuia kutokana sikuwa na nguvu
za kutosha wala kutambua kitu gani nilikuwa nafanyiwa.
Baada ya kunimalizia hayo babu aliniamsha.
"bella amka"
japo nilikuwa macho nikiona kila kitu lakini nilijikuta
nikihisi nimetoka katika usingizi mzito sana. Nilikumbuka
kila kitu. Na nilipoamka nilijikuta nipo ndani ya darasa lile
lile la prepo lakini sasa hakukuwa na mtu hata mmoja.
Wakina hilda na wenzake walikwishaenda kulala. Babu
aliniambia
"bella"
nilishangaa tena kumuona amekaa pembeni yangu baada
ya kuniona nikianza kufunua daftari na kutaka kuanza
kusoma. Aliniambia
"huu si muda wa kusoma, unapaswa ukalale"
alikohoa kidogo kisha akameza mate
"huna sababu ya kusoma kwa kuwa nimekupa nguvu ya
kutosha . Nguvu ya kufanya miujiza mikubwa sana hapa
shuleni. Hakuna anayeweza kushindana na wewe tena
katika masomo. Utakuwa kichwa hata usipogusa daftari
kwa muda mrefu cha msingi cha kuzingatia usije ni hili
sharti lingine ninalokupa utakuwa ukiamka usiku na kuiba
akili za wenzio kila siku usiku wa manane na usimwambie
mtu yeyote kuwa wewe huwezi kusoma lakini utafaulu tu
yaani wewe ni genious usijisifie hata siku moja kuna
ambao wataharibu akili yako pia"
aliniambi hayo na kutoweka. Niliyakusanya madaftari
yangu na kurudi bwenini. Nilipokuwa nikipata karibu na
mlinzi, alikurupuka kutoka katika usingizi mzito. Nilicheka
kumkuta amesinzia.
"ulizani bosi nini?"
nikaendlea kucheka
"majura bwana!"
yeye hakucheka wala kutabasamu. Aliniangalia kwa
makini na kuiangalia saa yake. Mimi pia nikakosa pozi
nikawa namuagalia. Nikamuuliza
"vipi?"
alitingisha kichwa kwa kusikitika kisha aliniuliza kwa
kutoamini
"hivi unajua sasa hivi saa ngapi?"
nilibetua midomo yangu kumwambia kuwa nilikuwa
sifahamu. Akaniambia kwa manjonjo
" sasa ni saa kumi kasoro alfajiri"
alikohoa kidogo na kuniambia
"kusoma gani huku sasa bella? Nilikujwa kukuomba
nizime jenereta lakini ukanisihi kuwa unataka kusoma
kweli ndiyo mpaka saa kumi?"
aliniuliza ten akiipiga piga saa yake akiwa ananiangalia
kwa mshangao. Nilimjibu kivivu
"niache bwana mi nikalale Majura tutazungumza kesho"
aliniangalia akisikitika nilipokuwa nikiondoka. Akawa kama
anajiambia mwenyewe
"yaani kama watoto wangu wangekuwa na uchungu wa
kusoma kama wewe? Leo nisingekuwa mfungua geti mimi
hapa leo"
kisha akcheka kicheko cha kuudhika akasema kwa nguvu
kidogo, huku sauti yake ikinisindikiza kushuka ngazi.
"haya bella na mungu akulinde ufanikishe ndoto zako"
Niliingia bwenini na kuwaamsha wawili watatu ambao
walikuwa bado hawajazama moja kwa moja usingizini.
Walishitushwa sana kuniona nikiwa na madaftari usiku
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
huo nikitoka prepo.
"he makubwa watoto mliotumwa na kijiji mna kazi kweli"
huyu alikuwa na mdomo sana nikamsonyo nikampita hilda
aliyekuwa akijigeuza geuza kitandani kwake chini juu
akiwa amelala Schola.
"bella"
aliniita kama hakuamini kuniona mimi nkiwa ndiyo nakaa
kwenye kitanda changu cha chini jirani yake. Aliamka
akakaa kitako. Aliniuliza
"tangu muda ule umeenda chooni mpaka sasa ulikuwa
prepo?"
kiukweli alishangaa sana alishangaa kwa kuwa hakikuwa
kitu cha kawaida. Mimi nilimpa tabasamu tu kisha nilivua
shamba dress zangu na kulala. Sikuchukua walao zaidi ya
robo saa nikatekwa na usingizi. Usingizi wa leo ukawa
mtamu mtamu zaidi. Nililala bila ndoto yeyote mbaya.
Nikalala zaidi kwa kuwa babu hakuja kunitembelea tena
usiku huu. Nilalala kwa amani mpaka kengele ya asubuhi
ilipopiga kuitwa paredi. Kengele hiyo ilinikuta nikiwa
nimeshamaliza kujiandaa nimeshavaa sare zangu nikilekee
paredi.
....
Usiku wa siku ya pili nikawa siendi tena prepo kama ilivyo
kawaida yangu wakina hilda wakaniita tuongozane lakini
mimi sikuwa tayar kwenda tena
"bella jamani mbona hatukuelewi?"
"nyie nendeni tu jamani mi sijisikii poa"
niliwajibu nikijichekelesha kisha wakaondoka. Ila hilda
hakuridhika kuniacha mimi nikilala bwenini kwa kuwa
alifahamu uchungu wangu wa kusoma. Nikajisemea
"laiti angejua asingenionea huruma"
mtu kama mimi sasa sikupaswa kuonewa huruma tena.
Nilikuwa nimeuvaa umalkia nje ndani nikiwa ni kiumbe
kinachotisha. Kiumbe kisicho na huruma. Kiumbe
kinachosubiri kuchukuwa matilio ya wenzangu yote
waliyoyasoma niyahamishie jwangu kiuchawi. Nakumbuka
babu alinipa dawa ya kufanya haya yote yatimie. Aliipa
kinyesi cha ndama yaani ng'ombe mtoto kisha
akakichanganya na mchanga wa kaburi. Babu aliniambia
"mchanga wa makaburini una nguvu sana katika kazi zetu
za kichawi"
kisha alinielekeza jinsi ya kuichanganya dawa hiyo.
"ichanganye na mafuta ya mgando kisha ipake kwenye
makalio yako na paji la uso hii itakusaidia wakati ukiwa
uchi kabisa unaweza kumsotea makalio yako juu ya
kichwa cha muhusika ambaye umepanga kumuibia
masomo yake kichwani kwake ukishafanya hivyo msonye
sana yaani sonyo kubwa kisha asubuhi uanpoamka
usimuangalie usoni hata akikusalimia angalia chini na
uepuke sana kukutanisha macho ya mtu mwingine na
yako iwe unamfahamu au humfahamu"
nilipokumbuka maelekezo ya babu, nilitabasamu
"kazi rahisi sana"
nilijisemea kimoyomoyo. Nikapitiwa na usingizi wa
mang'amang'amu mpaka maira fulai niliposikia kelele za
wanafunzi wakirudi kutoka prepo. Niliamka bila kufungua
macho. Nikamsikia schola na hilda wakizungumza
"masikini kabella ketu kamelala"
alikuwa hilda, schola akajibu
"muacheni dada yangu jamani apumzike si mnakumbuka
aliwahi kusoma hadi sa kumi ya alfajiri!?"
wakacheka kwa pamoja kisha kila mmoja nikamsikia
akipanda kitandani wake kulala. Sikusubiri muda upite
sana wauzoe usingizi. Ilinibidi wakati huo huo niipulize ile
dawa ya usingizi. Ile dawa iliyoitwa mpiyuru. Mti mmoja
ambao sikujua jina lake vizuri ulichomwa na kukaushwa
juani majivu yake kisha ikalowekwa na unga unga fulani
mweupe ndani ya damu ya mtoto mchanga. Vitu hivyo
vyote vikawekwa kwenye jua kali kali sana yaani kisha
vikawekwa juua ya dari kwa siku saba ikawa dawa kamili.
Dawa iliyotimia kwa kunuia maneno ambayo ulikuwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ukitaka. Dawa hii kama ungekuwa ukitaka watu hawa
walale muda wako wote mpaka utakapomaliza shughuli
basi wangetii. Kamakumvuta aliye mbali au hata kuvuta
mvuto na bahati ya kitu chochote katika maisha yako
kienda sawa dawa hii hutimiza. Ina nguvu ya kutosha.
Basi mimi niliipuliza dawa ile niliyoichota kidogo kutoka
katika kikopo nilichopewa na babu kule Gamboshi.dawa
ilikuwa imejaa mimi nikaiweka kwenye karatasi na kuanza
kuipulizia darasa zima. Wote wakakoroma hata ambaye
alikuwa analala kimya kimya. Nilisaula nguo zangu na
kubaki uchi wa kuzaliwa yaani sikuwa na nguo yeyote
mwilini mwangu. Nilimfuata Hindu. Huyu msichana
alikuwa na akili sana darasani. Nilimkalia kwa juu na
kuanza kujisugua sugua makalio yangu niliyojipaka ile
dawa kisha nikamsonya na kumfuata schola, naye
nilijisugua sugua juu ya kichwa chake mpaka nilipomaliza
kunuia yote niliyokuwa nikiyataka kutoka kwake na
kumaliza nusu bweni zima. Wengine ambao hata mimi
niliwapita sikuwa na haja nao. Nilirudi kulala baada ya
kuanza kuona kunakaribia kukuchwa. Sikutaka mtu
anikute nikiwa katika hali ile.
....
Hali ile ikaendelea bila kuonesha madhara yeyote kwangu
yaani kushitukiwa lakini kwa wahusika walipata tabu
sana. Tabu ya kujaribu kukumbuka sana kila mara
walipokuwa wakikutana na maswali kadhaa ambayo jana
waliyasoma usiku na leo walikutana nayo darasani lakini
majibu yalikuwa yanakuja na kupotea. Mimi nilikuwa
nikiwacheka kichinichini pale niliokuwa nikikaa na
mwalimu kunipongeza kuwa nimejibu sahihi. Wale ambao
walikuwa wakienda kusoma prepo wakaanza kuona uvivu.
Walichoshwa kuona walikuwa wakifanya juhudi nyingi
katika kusoma lakini walikuwa wakisahau yote mara tu
walipokuwa wakigusa vitanda vyao. Ni hapo mmoja
mmoja alianza kumuuliza mwenzake.
"yaani mwenzenu inanishangaza yaani mi nasoma usiku
lakini asubuhi nikiamka kila kitu nimesahau ni nini siku
hizi?"
mwingine aliitikia vivyo hivyo na kuonekana hali hiyo
iliwakatisha tamaa. Lakini sasa wakaniona mimi ni kama
kimbilio lao wale walioniona sasa nimekuwa mzembe
kutosoma kwangu kabisa prepo. Schola alikuwa mmoja
wao kuniuliza ile na lile ambalo hakulielewa.
"hivi bianka siku hizi umebadilika sana"
nilishangaa kubadilikaje? Yeye akanijibu
"yaani huingii prepo kabisa lakini unatukimbiza sana
aisee"
alikuwa akitabasamu na kutamani kujua siri yangu.
Akaniuliza
"embu nipe mbibu mpya shosti uliyoigundua maana hata
sielewi siku hizi nna nini mwenzio"
mimi nilicheka tu kumpoteza maboya kisha nilimwambia
bila kuwa na ukweli wowote katika yote niliyomueleza
"msikilize sana mwalimu. Labda huwa unasoma kitu
ambacho mwalimu hajakizungumzia"
nilimuona yeye akiridhika na kuahidi atasoma kile
ambacho mwalimu amemuelekeza darasani kuachana na
vitabu vya nyambari nyangwine.
Babu alikuja kunipongeza sana kwa kazi jinsi ambavy
nilikuwa nikiitekeleza. Sikuchoka na niliifanya kwa bidii.
Niliwachosha wanafunzi wasiipende shule, nikawachosha
walimu wacukie kufundisha. Sikuishia tu katika bweni
langu. Nilienda katika mabweni tofauti tofauti na
kuwachezea wanafunzi wengine. Wengi walianza
kulalamika kuwa wanachoka sana siku hizi. Walipiga
mihayo wakiwa darasani na wengine waliombea mwalimu
amalize haraka waende kulala.
Babu alikuja kunipongeza sana kwa kazi jinsi ambavy
nilikuwa nikiitekeleza. Sikuchoka na niliifanya kwa bidii.
Niliwachosha wanafunzi wasiipende shule, nikawachosha
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
walimu wacukie kufundisha. Sikuishia tu katika bweni
langu. Nilienda katika mabweni tofauti tofauti na
kuwachezea wanafunzi wengine. Wengi walianza
kulalamika kuwa wanachoka sana siku hizi. Walipiga
mihayo wakiwa darasani na wengine waliombea mwalimu
amalize haraka waende kulala. Jordan sikuwahi
kumchezea wala kumfanyia chochote nilimpenda sana
jordan nilimpenda kwa moyo wangu wote. Nilidirika
kujichora jina lake kwene mkono wangu kwa kutumia
utovu wa korosho. Sikujali maumivu ila nilifanya kwa
watu niwepandao. Mama yanagu pamoja na jordan
wangu. Nilijisikia fahari sana kuwaonesha kila mtu ni kiasi
gani nampenda Jordan. Nikavunja agano nililopewa kule
Gamboshi. Pete niliyopewa na mkuu wa Gamboshi
nikampa Jordan aivae kama urembo kwa kuwa aliipenda.
Ilikuwa ni pete ya dhahabu. Pete nzuri yenye urembo wa
kila aina. Siku moja babu alinifuata na kunieleza kuwa
kesho jumapili inabidi niende mjini na schola. Na
nitakutana na mchungaji fulani ambaye ni mtu wao na
kuna jambo atakaloniambia nilitekeleze. Nilikubwali.
Alinisisitiza nitumie mbinu zote mpaka nihakikishe
nimeenda na schola. Nikamwambia
"usiwe na shida babu ni lazima akubali"
pale shuleni kumbe kuna watu ambao walishaanza
minong'ono. Walikuwa wakinijadili chinichini kuwa mimi ni
mchawi. Sikujua walihisi vipi ila hili swala lilianzia ofisini
kwa walimu. Ile pete ambayo nilimpa Jordan
walikwishaivaa rafiki zake wote. Wa mwisho kuivaa
alikuwa ni Kelvin. Aliitwa ofisini na mwalimu wa nidhamu
na kuulizwa
"hiyo pete umeipata wapi?"
kelvin alikuwa ni kijana mtundu na uoga ulikaa pembeni
naye hivyo alijibu haraka kwa kutumia uongo alioufikiria
haraka haraka.
"ni ya kwangu mwalimu"
mwalimu yule wa kike alitabasamu na kumwambia kelvin
"hiyo pete si ya kwako. Mumeshaivaa kundi lenu wote na
wewe ni wa mwisho imetoka kwa jordan aliyepewa na
mpenzi wake bianka. Nimeongopa?"
kelvin alishituka sana aliyatoa macho yake kutokana na
bumbuzwazi iliyomkumba ghafla asijue mwalimu alijuaje.
Asijue kuwa mama yake na shola alikwisha kuja hapo
shuleni na kutoa malalamiko kunihusu mimi. Siku kadhaa
nyuma niliwahi kumfuata kimazingira mama schola na
kumueleza
"naomba usisali muda wasiku kumuombea schola"
nilimaanisha kweli. Sikupenda anaposali. Alikuwa
akiharubu kazi zangu na kunufanya nisitishe kuwafanyia
wengine. Mama yake aliwaomba walimu wanitzame kwa
makini kwakuwa nilikuwa nina ishara zote za kichawi.
Habari hivyo ikasambaa kutoka katika ofisi za walimu na
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
minong'ono kuwafikia wanafuni kutoka katika kinywa cha
kelvin. Jordan alifahamu kuwa mimi naitwa mchawi naye
akaniogopa sana ila ni mtu mmoja tu ambaye hakunijua
mimi vizuri hakunijua upade wangu wa pili mimi ni nani.
Yaani mimi ni mtu wa aina gani ndani ya moyo wangu.
Aliupenda umalaika nilio nao nje lakini aliti angefahamu
kuwa mimi ni mtu wa aina gani ndani asingethubutu kuwa
karibu na mimi. Huyu alikuwa ni schola sikuwa na nia ya
kumdhuru, ila babu na uongozi mzima wa gamboshi;
ulivutiwa naye. Ulinishauri nikae aye karibu kwa ukaribu
sana.
Jumapili hii nikamtafuta schola sikumuona, nilimuulizia
kwa kila mtu; hakuna ambaye alikuwa na jibu. Nilipochoka
kumtafuta, nilimuona kwa mbali maeneo ya getini.
Alikuwa na tabasamu mdomoni mwake, mkononi akiwa
ameibeba biblia. Alikuwa amependeza sana. Sikumsubiri
anifikie pale nilipo nilimfuata mpaka hapo. Alionesha
kushangaa kitendo cha mimi kumkimbilia isivyo kawaida.
"bella!?"
aliniita baada ya kusimama. Mimi nilisimama pia
nikaanza kutembea mwendo wa kawaida mpaka
nilipomfikia. Nikamwambia jambo lililosindikizwa na
tabasamu pana.
"schola mama, naomba unisindikize kwa mtu mmoja hivi"
alionesha kushangaa. Alishangazwa na kitu ambacho
mimi sikukifahamu ila aliniuliza
"hivi bella huoni kuwa nimetoka kanisani jamani?"
"sikia rafiki yangu hii ni emergency naomba unisaidie
mwenzio"
nilimlainisha schola akaingia mkenge. Alirudi bwenini na
kuitupa biblia yake juu ya kitanda, tukatoka vile vile
alivyoingia. Hakubadilisha chochote. Tulielekea mjini kwa
kumpa kitu kidogo yule mlinzi rafiki yangu. Tulitoka na
kuelekea kwa mzee mmoja aliyeitwa shekhe Majid.
Shekhe huyu alikuwa anasomea watu kisomo cha kuwatoa
watu majini na kuwatoa watu katika matatizo
yanayowasibu. Babu alinielekeza kuwa Majid hakuwa
hivyo kama vile wengi ambavyo walimfahamu. Majid
alikuwa ni jini kamili. Jini lililovaa mwili wa binadamu na
kusambaza ubaya juu ya watu wema. Alikuwa akiroga na
kuwafanyia mabaya. Huyu alikuwa ni jini aliyetengenezwa
na moto. Huyu ni jini mbaya sana. Alikuwa akiishi katika
mbuyu ambao watu wa kawaida walikuwa wakiona kama
sehemu nzuri na ya kawaida. Tulipofika maeneo ya
mwananyamala kisiwani, huko kwa Majid, schola alianza
kuingiwa na wasiwasi. Aliniuliza
"huku tunaenda wapi bella jamni mbona vichochoroni
sana?"
nilimzawadia tabasamu pana, na kumwambia kwa asijali.
Nilimuonesha nyumba moja ya kifahari iliyo pembezoni
mwa makaburi. Schola akanisimamisha
"we bella! Nyumba yenyewe ndiyo ile?"
alikuwa akiuliza kwa mshangao uliomsawajisha uso wake
"ndiyo schola yule ni rafiki wa babu yangu na ana jambo
muhimu la kuniambia. Kwanini umeniuliza hivyo?"
"yaani ile nyumba sijuhi kwanini"
alipatwa na kigugumizi cha ghafla. Alikuwa akitetemeka
sana. Kisha aliendelea
"hapana bella ile sio sehemu nzuri nimepatwa na
msisimko mkubwa nilipoiona ile nyumba na haswa
uliponieleza kuwa ndiyo sehemu ambayo tulikuwa
tunaenda nywele zangu zimenisisimka sana"
nilicheka kisha nikamueleza kuwa asipatwe na wasiwasi.
Majid ni mtu mzuri na asiwe na wasiwasi naye. Nilimsifia
kuwa majid alikuwa ni mpole na mwenye upendo wa
kushangaza. Nilimpa hadithi za uongo za kutunga
kumuhusu majid. Nilijifanya kumfahamu fika majid kumbe
nilikuwa simfahamu hata anafananaje. Kwa mwendo wa
taratibu huku bado uoga ukimtawala. Nilimpa tu moyo
mpaka tulipoifikia nyumba ya majid. Nyumba hii babu
alinielekeza kabla sijaifikia hivyo haikunipa shida kupajua
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wapi. Babu alinieleza kuwa majid alikuwa anafahamu kila
kitu kuhusu ujio wangu na Schola. Babu alinieleza kuwa
walikuwanahitaji kivuli cha schola kivuli kilicho na nguvu,
nguvu ya kuwaharibia kazi zao. Yaani kazi yao ikiharibika
na mimi nisingefanikiwa chochote katika mambo yangu ya
kichawi. Mimi sikuwa tayari kupoteza nguvu zangu kwa
ajili ya kujilinda. Nilikuwa tayari kutoa kumtoa kafara
kulinda nguvu zangu zisipotee. Tukaugonga mlango sauti
ya mwanaumeikatupokea bila kuchelewa. Alikuja kufungua
mzee mmoja mfupi mwenye upara lakini ndevu nyingi
zilitawala kidevu chake. Alikuwa na asili ya kiarabu.
Alitabasamu kutuona. Mimi nilipomtazama hakuwa na
kiwiliwili cha binadamu chini yaani kuanzia kiunoni mpaka
kushuka miguuni, alikuwa ni moto tu. Kwa mtu mwenye
macho ya kawaida usingeweza kuona kile ambacho
nilikiona. Aliniita jina langu
"bella umekuwa mama"
nilikuwa katika mshangao lajini sikutaka schola afahamu
chochote. Alitukaribisha ndani huku Majid akiwa na furaha
sana ya kuniona. Tulipofika sebuleni ndipo kila kitu cha
ajabu bila kutarajia kikatokea. Niliiona miale fulani
iliyofanana na utandu wa buibui. Ulimvaa schola na yeye
kujigawa mara mbili. Yaani schola sasa walikuwa wawili.
Yule niliyekuja naye nilikuwa naye akishangaa mazingira
ya sebule ya majid. Lakini yule aliyemtoka schola
ninayemfahamu alikuwa akilia akielekea katika chumba
ambacho majid aliingia. Nllijiuliza maswali mengi sana
lakini sikupata jibu sahihi. Majid alitoka akiwa
amepambwa na tabsamu lisilo na raha yeyote. Alikuwa
amebeba jag lililobeba maji ya matunda. Alituambia kwa
ukarimu
"karibuni jamani. Msiishangae sebule yangu haina viti
kama mlivyozoea"
alipotusogelea aliliweka lile jag katia stuli iliyoa na vitairi
na kuisukuma kidogo na kutuelekeza pa kukaa
"hii mito ndiyo kama makochi yangu karibuni jamani"
nilimuona schola akitabasamu na yeye ndiye alikuwa wa
kwanza kukaa. Aliniita
"bella kaa basi"
majid naye alitabasamu na kuniambia
"mtazame mwenzako ameshakaa. Embu nawewe ukae
basi tuzungumze"
sikukaa kwa sabbu eti sikuyazoea mazingira ya aina ile.
Nilichoshangaa uoga wa ghafla uliomtoka schola
alipazoea hapo na kuwa kama mwenyeji nilipokaa majid
alianza kuzungumza
"karibu bella"
"asante anko huyu hapa ni rafiki yangu anaitwa schola"
alimgeukia schola na kufanya kitendo cha kushangaza.
Aliutoa ulimi wake na kumtoa kitu mfano wa moshi mzito
mweusi ulimtoka mdomoni mwake schola. Nilikuwa
nikistaajabu sana linalotokea. Schola hakuonesha
wasiwasi wowote wale kufahamu kile alichokuwa
akifanyiwa. Nilimtazama majid kwa makini kisha wote
walitoleana tabasamu. Tabasamu la heri ya kujuana.
Walishikana mikono na hapo ndipo schola akamsalimia
majid kwa mara ya kwanza. Tuliongea mengi na hadthi
zisizo za kweli kuhusu mambo mbali mbali kumpoteza
schola. Baada ya muda kwenda mimi na schola tuliaga
na kuondoka. Majid alinishukuru akanishukuru sana. Kisha
tulirudi shule. Tulipofika shule kama kawaida yangu mimi
nililala nikamuacha schola yeye aeleke kusoma. Huko
ndipo schola naye akawa anasikiliza hadithi zilizotapakaa
shuleni hapo. Kwa bahati nzuri waliokuwa wakihadithia
kunihusu mimi ni mchawi walikuwa hawanifahamu. Hivyo
wakahadithia kinadharia jinsi nilivyo
"tena anakaa katika bweni lenu kabisa, humfahamu
jamani?"
alikuwa akimwambia schola. Schola bado akawa
hajanijua mpaka pale mmoja aliposema kitu
kilichomshitua
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"tena leo mwalimu karim ametuambia kuwa alimuona
akiwa na msichana mwingine maeneo ya mwananyamala
kisiwani mwalimu karin alivyokuwa mbea jamani
aliwafuatilia mpaka huko"
schola alishitushwa sana baada ya kusikia hilo jambo.
Alianza kutetemeka na kusikiliza kwa makini.
"basi yule mwalimu akawa anatuambia kuwa walipokuwa
wanaenda ni maeneo ya makaburini chini ya mbuyu
mmoja mkubwa"
schola alibwatuka
"mbuyu?"
wote walimtazama schola kwa mshangao. Schola alikuwa
analia. Hapo ndipo schola alisema
"jamani huyu aliyekuwa na huyo dada ni mimi jamani
nakufa mie jamani mungu wangu bella mchawi bella wee
unaniua"
walimbembeleza na kushauriana kwa pamoja kwenda
kumuamsha matroni kumueleza swala hilo. Kutokana na
usiku ulikuwa mkubwa. Matroni hakuwa na la wa
kuwajibu. Aliwashauri waende kulala na kesho asubuhi
atazungumza na walimu na kujua nini watanifanya. Mimi
sikutishwa kwa kuwa niliwasikia kila kitu walichokuwa
wakizungumza. Nilikuwa pale tu wakati wote nilioufahamu
kuna watu walianza kunifuatilia. Kuna watu walikuwa na
nia mbaya na mimi. Nilijinyanyua kutoka kitandani na
kuliacha gogo la kuwapumbaza wengine kama mimi
nilikuwa nimelala bado. Nilikuwa nikisikia kila kimoja
walichokuwa wakizungumza na matron matilda na
walichoelezwa na matroni. Waliporudi mabwenini mimi
nilirudi kulala pia. Sikumfanya chochote yule matroni kwa
kuwa nilimuona hana hatia nilirudi kulala nikisubiri hiyo
kesho itakuwaje. Nilitaka nifahamu nini wataongea na hao
walimu kunihusu mimi.
Asubuhi tuliamka kama kawaida, paredi tukajumuika
pamoja wanafunzi wote. Kisha ule wakati wa kila mtu
aliutamani ukafika. Nilipoingia darasani, kila mtu
alinikwepa. Yaani walinikwepa kama waliniona
nimejimyea. Sikujjali kwa kuwa kila nilichokifanya ni kwa
ajili yangu na niliona fahari kufanya hivyo nilichojali ni
furaha ya Jordan yaani nilijisikia raha sana nikimuona
Jordan akitabasamu mbele yangu na kuniambia lile neno
Nakupenda kutoka kinywani mwake. Hakika nilimpenda
sana Jordan. Nilimpenda kupita kiasi na nilitambua hilo.
Nikawa nimekaa kwenye kiti changu darasa zima likiwa
kimya. Ni sauti za watu wachache walikuwa wakikohoa
na wengine wakinong'ona. Ni wawili watatu ambao
walinitupia jicho la wizi wizi. Mimi niliwatazama pia huku
nikitabasamu tu bila kuwaonesha kuwa nilikuwa
nikiwaangalia. Nilipotazama pale ambapo schola alikuwa
anakaa siku zote, hakuwepo. Nikaangaza angaza kila
sehemu ya darasa, sikumuona pia. Nikahisi huenda bado
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hakuwa ameamka. Lakini mbona nilimuona paredi?
Nikaamua nimpotezee nikiendelea kufunua dftari
nikipitisha pitisha macho nikijifanya nasoma. Haukupita
muda mrefu aliingia schola na mwalimu wa zamu wiki
hiyo alikuwa ni mwalimu karim. Yule ambaye niliwasikia
wanafunzi wakisema kuwa alituona mimi na schola
tukienda kwa majid. Schola alipoingia alitazama moja kwa
moja pale kwangu nilipokaa. Nilipoiona sua ya schola
nilishitushwa. Ulikuwa ni uso uliovimba na alikuwa akilia.
Ulivimba kutokana na kulia kwa muda mrefu sana. Schola
hakuja kukaa, alisimama pale mbele mpaka alipoingia
mwalimu Karim na Bushiri. Walikuwa wamebeba fimbo.
Nikafahamu fika wote walikuja kwangu baada ya kikao
cha kunijadili kuhusu tuhuma zinazendelea kunihusu mimi.
Mwalimu bushiri ndiye aliongea. Huku mwalimu karim
akiniangalia mara moja moja
"wanafunzi hamjambo"
wote kwa pamoja tukamsalimia. Kisha tulikaa chini baada
ya kusimama kwa heshima. Aliirekebisha sauti yake
baada ya kikohozi kifupi kumpitia, kisha aliendelea
"sasa wanafunzi labda tuwaulize ni wangapi
wamekwishawahi vaa pete ya aina hii?"
aliitoa ile pete niliyopewa na babbu na mimi nilimpitia
Jordan. Mimi nikamtazama jordan, mwalimu karim na
schola wakanitazama mimi. Jordan alikuwa ameshituka
sana na yeye akanitazama mimi.’
Walikuwa wamebeba fimbo.
Nikafahamu fika wote walikuja kwangu baada ya kikao
cha kunijadili kuhusu tuhuma zinazendelea kunihusu mimi.
Mwalimu bushiri ndiye aliongea. Huku mwalimu karim
akiniangalia mara moja moja
"wanafunzi hamjambo"
wote kwa pamoja tukamsalimia. Kisha tulikaa chini baada
ya kusimama kwa heshima. Aliirekebisha sauti yake
baada ya kikohozi kifupi kumpitia, kisha aliendelea
"sasa wanafunzi labda tuwaulize ni wangapi
wamekwishawahi vaa pete ya aina hii?"
aliitoa ile pete niliyopewa na babbu na mimi nilimpitia
Jordan. Mimi nikamtazama jordan, mwalimu karim na
schola wakanitazama mimi. Jordan alikuwa ameshituka
sana na yeye akanitazama mimi. Bushiri akarudia tena
"nauliza kwa ulinzi wenu mathubutu ni nani ambaye
ameshaivaa hii pete?"
walinyoosha mikono yao wavulana wawili akiwemo Kelvin
wakiongozwa na Jordan wangu, jumla waki watatu.
Bushiri akatabasamu kifedhuli kisha aliniita mimi Bella
simama na kila kitu chako. Nilikusanya madaftari yangu
niliyoyafungua na kuyaibeba nikawa nimesimama. Bushiri
akaniambia kwa sauti aliyoitia ukali kidogo
"njoo huku"
nikaenda mpaka pale mbele walipokuwa wamesimama.
Tukawa tumetoka. Nyuma tukaacha mzozo mkubwa,
yaani minong'ono ilianza kwa sauti ya chini hatimaye
darasa likageuka soko la kariakoo. Nikawa naelekea
ofisini kwa walimu wote wanapokaa. Nilipofika huko
nilikuta kuna kikao kikubwa cha siri. Walikuwa wavulana
wengine wanne ambao walikwisha vaa pete ile. Mama
yake na schola alikuwa amekaa mbele akiwahadithia
jambo. Jambo la kushangaza na jambo lililowavutia kila
mmoja aliyekuwa eneo hilo waliponiona naongozana na
schola pamoja na walimu na wale wakina Jordan,
walinyamaza kuongea. Nilimsalimia mama yake schola
hakuitika. Nikawa nimeelekezwa pa kukaa kisha nikawa
nawatazama kila mmoja aliye katika kikao hiko kwa
awamu. Mama yake na schola alikuwa amefura kwa
hasira akinitazama kwa chuki. Kifua chake kilipanda na
kushuka kana kwamba alitamani kunimeza muda wowote
kama angekuwa na uwezo huo. Mwalimu mkuu ndiye
alianza kunisemesha.
"wanakuita nani hapa shule?"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alianza kuniuliza kwa kejeli, tabasamu liloudhi likiuharibu
uso wake. Na mimi nikatabsamu vivyo hivyo nikamjibu
jibu la kipumbavu kama alivyotaka.
"jina langu ni Bella"
akacheka kidogo kisha akaipaza sauti yake kwa hali ya
kukereka
"bianka"
akayatoa macho yake kama aliyejaribu kunitisha lakini
uoga ulikuwa mbali na moyo wangu mimi pia nilimkazia
macho. Akaniuliza
"hii pete ni ya nini? Na ilikuwaje ikaingia shuleni na
unafahamu haturuhusu vitu kama hivi hapa?"
aliitoa ile pete akaitupa juu ya meza kwa dharau.
Niliitazama ile pete bila kujibu chochote. Niliitazama zaidi
ya dakika ishirini. Mkuu wa shule alisimama akawa
anazungukazunguka nyuma ya viti vya walimu wengine na
waliojumuika katika kikao hicho. Alizungumza.
9aomba utujuze hii pete ina lengo gani hapa shuleni?"
alikuja nyuma yangu na kuniinamia kwenye sikio langu na
kuniuliza
"pete ile ndiyo urithi wa kichawi au ya kumroga
aliyeivaa?"
akatabasamu na kucheka kimaudhi. Kisha alinigeukia na
kunitoa katika lile nililokuwa naliwaza kwa kugonga meza
kwa nguvu na kuniambia.
"hii pete ni yako na siku zote ulikuwa unaivaa huna
sababu ya kuitazama kama ndiyo leo mara ya kwanza
umeiona. Naomba utujuze hii pete ni ya nini?"
nikapata la kumjibu. Niliuinua uso wangu na kumwambia
"ni ya urembo wa kawaida tu"
alinitazama kwa muda akawa amesimama
kuzungukazunguka alikokuwa anakufanya na kuniambia.
"pete ya kawaida? Urembo? Na kwanini basi waivae
wavulana na si wasichana wenzio?"
"niliyempa nafikiri ndiye ana jibu hilo"
nikawa nimemtazama Jordan aliyekuwa amenuna mithili
ya kutaaka kupasuka. Mwalimu mkuu na wengine nao
walimgeukia Jordan. Mkuu hapa akawa amelegeza ukali
akawa aamuuliza Jordan kwa sauti ya upole.
"jordan embu tujuzue imkuwaje umegewa ete
usiyeifahamu? Pete ya maajabu isiyovutia kwa lolote.."
hasira zikanipanda, zilinipanda toka ndani. Yaani nilisikia
kitu cha ajabu kikilpuka ndani ya moyo wangu na kutaka
kumfanyia mwalimu mkuu lakini nikajizuia. Kisha nikawa
namsikiliza alikuwa akiendelea
"ukaichukua wewe ukaivaa ikaanza kutembea kwa
wengine na ni wavulana wenzio tu na si wasichana?"
jordana akawa anatokwa na jasho jingi hata nikaanza
kumuonea huruma. Ule upendo nilio nao juu yake
ukanitafuna moyo wangu nikajihisi kumtupia mpira mpenzi
wangu asiye na hatia. Nikiwa nimeyatoa macho kutoka
kwake nikaiangalia meza ndipo Jordan akaipata sauti
yake.
"ni mimi ndiye niliiomba kutoka kwa Bianka"
akawa ananiangalia kwa jicho la chuki huku akimjibu
mwalimu mkuu swali. Akawa anaendelea
"lakini siku aliyonipa, hazikupita siku kadhaa ikapotea
katika mazingura ya kushangaza pale nilipoihifadhi. Lakini
cha kushangaza mara ya mwisho nilimkuta nayo Kelvin"
hapo ndipo akanyamaza na kumwangalia mwalimu mkuu
aliyenyamaza kimya muda wote na kumwambia
"mimi sifahamu chochote zaidi ya haya niliyokueleza
mkuu"
mkuu aliitikia kwa kuonesha kumuelewa. Kisha mkuu
alituambia wote kwa pamoja baada ya kurudi katika kiti
chake kilichokuwa kikitazamana na changumimi ila kwa
umbali mrefu sana kutokana na meza iliyo katikati yetu.
Akasema.
"nina kila sabbu ya kuwaruhusu wote muende darasani
lakini hapa abaki schola na bella peke yake"
kila mmoja ainyanyuka akawa anaelekea darasani. Mimi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nikawa naichezea chezea mikono yangu mara nishike
daftari mara vidole sikujua kitu gani sahihi cha kufanya.
Mkuu akasema
"bella nimesikitika sana kwa hali iliyopo kwako sasa"
mimi nikawa namtazama tu tena kwa makini.
"nilipopata taarifa umefiwa na mama yako nilisikitika sana
nikadhani huenda ungeanza kuwa na uchungu wa kusoma
kwa bidii"
akameza funda la mate kisha aliendelea.
"lakini haikuwa kama nilivyotarajia. Wewe umekuwa na
sifa mbaya zaidi kuliko mwanafunzi yeyote shuleni. Wewe
umekuwa na mambi ya ajabu ajabu"
mkuu wakati anasema hayo alitokea yule mlinzi Majura.
Nilishangaa sana kumuona kati ya watu wanaohusika
katika kikao hicho. Mwalimu alimgeukia majura na
kumueleza
"embu Majura kabla hatujachukua muda wako mwingi
naomba utujuze chochote kuhusu rafiki yako Bella"
nilipomtazama Majura, nikaiona sura ya usaliti na kicheko
cha kebehi. Nikamchukia Majura na kumuona kama adui
yangu mpya. Nikaitamani nguvu yangu mbaya niweze
kumsambaratisha Majura. Nikamtazama kwa dharau
nikamsonya. Yeye akacheka kidogo kisha akaanza
kuzungumza.
"mwalimu ninachoweza kusema huyu si mwanafunzi"
macho ya kila mmoja katika kikao hicho yakang'aa kwa
kustaajabu. Yeye akaendelea kuzungumza
"hapo kabla naanza kumjua bianka kabla ya kumjua bella,
nilimuona ni msichana mzuri tu mwenye utii wake kwa
kila mtu. Lakini baada ya muda ndipo nilianza kuona
vituko"
mwalimu Bushiri akakohoa kidogo nilipomtazama naye
alinitazama. Nikaona hana la maana huku nikiendelea
kumsikiliza Majura
"mimi nimechanjwa chale"
alianza kuonesha chale zake mikononi na kila sehemu ya
mwili wake kwa kutuonesha zile za mgongoni na kila
sehemu.
"hizi chale hunisaidia mimi kuona wacawi na kila kitu
wanachokifanya. Siku moja bella akiwa na wenzake huko
darasa la kule juu wanajisomea alitoweka ghafla bila
wenzake kuonesha jambo lolote la kushangaza lilotokea.
Lakini pale alipokuwa amekaa bella, aliuacha mgomba
uliyomuwakilisha. Hivyo kama hukuwa na ile dawa ya
kukufanya kuona wachawi basi usingeweza kutambua
kama yule si bella"
kila mtu alikuwa anashangazwa na hadithi hizo za
majura. Japo ilikuwa ni kweli mimi nilikaa kimya.
"bella alikuja akachukuliwa na babu mmoja mzee sana na
anayeonesha ni ana nguvu nyingi sana za kichawi.
Alimchukua bella mpaka sehemu ambayo mimi
sikufahamu walielekea wapi lakini baada ya muda mimi
nikapitiwa na usingizi. Hivyo sikutambua kuwa bella
alirudi muda gami kwa kuwa ilikuwa yapata majira ya saa
kumi kasorobo alfajiri ndipo bella alirudi akiwa anaelekea
darasani. Mimi sikuonesha hali ya kujua chochote kwa
kuwa bella hakugundua kuwa mimi nilkuwa nawaona"
kila mmoja akawa amenikazia macho akinitazama kwa
kutokuamini kile ambacho alikuwa akikisikia. Majura
akanyamazishwa na kkohozi cha mwalimu mkuu
aliyemtaka asimame kisha akamruhusu kuondoka. Mimi
nilibaki nimeshika kichwa nikajuwa kila kitu kimeharibika.
Mwalimu mkuu akaanza kuzungumza
"sasa kutokana na join instruction yetu haituruhusu kuwa
na mtu mwenye vitendo vya kichawi hivyo tumevumilia
mambo mengi sana ambayo tumekuwa tukiyasikia kutoka
kwa watu waliokushuhudia kabisa na sio kukuonea.
Mfano mwalimu Bushiri kukuona ukienda maeneo ya
makaburini ukiwa na mwanafunzi mwenzio Schola
mkiingia ndani ya mbuyu pamoja na kumtokea mama
yake na schola usiku wa manane ukimtisha kumuua
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
endapo akiendelea kumuombea mtoto wake ulinzi sasa
basi tunakufuta shule kuanzia leo hatukuitaji tena"
machozi yalinitoka ghafla na kitu cha uchungu kikapiga
ndani ya moyo wangu hakika nililia kwa uchungu sana. Ni
kweli niliadhibiwa kwa jambo la kweli lakini iliniuma
kuachishwa shule. Ningeenda wapi? Ningekuwa mgeni wa
nani mimi? Sina baba wala mama? Sina pa kwenda.
Mama schola asingeniruhusu hata chembe hata
ningemlamba miguu yake kwa ulimi wangu. Nimeumbuka
mimi nitaenda wapi mimi? Mwalimu mkuu akanigukuza
ofisini hapo na kuniambia nirudi bwenini kujiandaa ili
niweze kutoka eneo hilo la shule. Yaani sikuhitajika
kabisa. Nililia bila mtu yeyote kunionea hutuma wala
kunitazama nilitoka nikiwa nimeshikwa na aibu
nikimtazama kila mmoja wao wakiwa wananitazama kwa
hasira
Nilitoka nikaelekea bwenini nikachukua kila kilichokuwa
changu. Nilipokuwa napita kurudi ofisini kwa ajili ya
kuchukua barua yangu ya kufukuzwa shule, kila
mwanafunzi alinyanyuka kutokea madirisha ya darasani
akawa anazomea. Jina kubwa waliloniita ni
"mchawi huyoo.. Mchawi huyo..."
iliniuma sana. Lakini sikuwa na jinsi nilizidi kulia.
Nilikutana na Jordan nilimsimamisha ili nizungumze naye
alinikimbia kama kinyaa. Niliumia sana. Niliumia Jordan
kunikwepa na kuiona mimi ni mbaya kwake. Sawa mimi
nilikuwa mchawi mbona hakuwa akijua siku zote hizo
ubaya wangu hakuwahi kuuona lakini nilikuwa mzuri na
aliniambia mimi ni msichana mzuri kuliko wote duniani,
kwanini leo anione mimi ni mbaya? Jamani Jordan
wangu? Ina maana hanitak tena? Mapenzi yangu na yake
ndiyo yamekufa? Vipi ningemuangamiza yule christina
aliyezini naye chooni na mimi nikiwashuhudia bila wao
kuniona? Ni mara ngapi jordan alikuwa akisaliti penzi
langu lakini mimi nilizidi kumpenda? Ina maana upendo
wangu wote bella mimi umekuwa bure? Nilikuwa
nikijiuliza hayo nikimtazama Jordan aliyekuwa akitembea
haraka haraka kuelekea darasani. Mimi machozi
yalinitoka kila nikimuangalia. Leo nimebaki peke yangu.
Peke yangu bila mama na baba. Kila mtu alinipiga teke
nilipokuwa nikimuomba msaada. Uchawi wangu
ukaniponza. Lakinisipo tayari kuuacha. Nikaanza
kutembea kuelekea ofisini kwa mkuu wa shule. Nilimkuta
mama yake na schola. Alikuwa akilia sana mbele za mkuu
wa shule
"mtoto wangu mimi sijuhi hata wamemfanyaje jamani..
Upole wangu na huruma ndiyo imeniponza"
nilimsikia yote aliyokuwa akizungumza nikajisikia vibaya
sana. Alinyamaza aliponiona mimi akawa anafuta
machozi yake na kuvuta kamasi jepesi lililokuwa linamtoka
kila wakati
"shika hii barua kaa ukifahamu kuwa usije kufikiria
utaenda shule yeyote ukapata shule iliyokuvumilia zaidi ya
hii. Nakuombea maisha mema huko uendako na cha
msingi uache hizo tabia za kichawi."
alinipatia barua yangu. Nikaipokea kisha nilitoka humo
ofisini. Mama schola alikuwa akinisindikiza kwa macho
yaliyojaa machozi. Mimi nilitoka mpaka getini kwa
Majura. Majura sikumkuta. Niliondoka zangu popote pale
ambapo pangenipokea. Sikujua wapi naelekea wala vipi
ningeishi. Nikahisi babu amenidhulumu. Ameidhulumu
sana nafsi yangu. Mateso haya ninayoyapata ni yeye
anayasababisha. Kwanini anaruhusu watu kufahamu vitu
vyangu? Yeye si ana nguvu? Kwanini hakujitokeza katikati
ya kikao kile na kunitetea mimi kwa kuwapumbaza wote?
Jamani dunia imenielemea. Nitaenda wapi sasa? Nilikaa
kwa muda mrefu kituoni mpaka nilipopata akili ya kwenda
kwa majid kule mwananyamala kisiwani. Nikachukuwa
gari mpaka magomeni mikumi kisha nikaunganisha
mpaka mwananyamala kisiwani. Nilivipita vile vichochoro
tulivyopita mara ya kwanza nikiwa na schola kisha
nikaibukia katika kichochoro cha mwisho kilichounganisha
njia ielekeayo kwa majid nilipakumbuka vizuri. Lakini
kilichonishangaza nilipofika katika ule uwanja ambao
ulitakiwa niuvuke nifike kwa majid nilikuta makaburi
matupu. Na nilipotazama mbele zaidi nilipozani labda
ningeiona nyumba ya majid nikaambulia kuuona mbuyu
mmoja mkubwa. Nikahisi labda nimepotea au nimeanza
kuwehuka mama mmoja alipopita eneo hilo nikamuuliza
"samahani kwa usumbufu mama ati aya makaburi
yamejengwa lini hapa"
alinicheka sana yule mama alinicheka mpaka nikaona
machozi yakimtoka akaniambia.\
"dada yangu hii ni sehemu ya makaburi miaka yote
napafahamu hapa ni makaburini mimi nimezaliwa
nimeyakuta na hata mengine yameanza kupotea lakini hili
ni eneo la makaburi"
nikaanza kuchukia kutokana na junicheka huko lakini
haikunizuia kumuuliza
"sawa lakini kwanini unacheka?"
alinyamaza kisha akanijibu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"si wewe tu hii sehemu inaonesha ina mauza uza ya peke
yake kwa sababu wengi huja hapa na kubaki
wakishangaa. Wanashangaa na kutuuliza sisi wenyeji "hivi
hapa haya makaburi yamekuja lini?" sasa ndio hapo pa
kujiuliza makaburi yanabebwa na kuletwa sehemu moja
na nyingine?"
aliendelea kucheka huku akijipiga piga mapajani baada ya
kupiga magoti chini. Nikamuuliza swali lingine
"unamfahamu Majid?"
nilimuona kushituka sana. Alishitua haswa na kuyatoa
macho kwa mshangao. Aliniuliza kwa kubwatuka huku
akiwa amesimama wima
"unamfahamu Majid?"
nilimuona kushituka sana. Alishitua haswa na kuyatoa
macho kwa mshangao. Aliniuliza kwa kubwatuka huku
akiwa amesimama wima
"shekhe majid?"
niliitikia kwa kumtingishia kichwa kuonesha ndiye
niliyemmanisha. Kitu cha kushangaza alianza kulia. Alilia
haswa tena alilia kupitiliza kama mtoto mdogo kamasi
jepesi likamtoka na nilipombembeleza kwa muda mrefu
alinieleza
"huyo si binadamu dada yangu"
mimi nikajitia kushituka nikauliza kwa mshangao
"si binadamu!? Umejuaje?"
kutokana na kilio ilinipa shida kumuelewa kiufasaha
alichokuwa akizungumza. Ilimbidi nimkatishe kwanza
alichokuwa akiongea ndipo nilimuomba arudie alichokuwa
akiongea nimuelewe zaidi. Aliniambia
"huyo ni jini aliyekuwa akimlinda mjomba wangu. Ni jini
aliyetengenezwa kwa moto ni mweye nguvu sana.
Alisababisha matatizo makubwa sana nyumbani. Ni jina
aliyenunuliwa mascut lakini mjomba alipovunja masharti
alimnyonya damu mjomba pamoja na kumuweka ukilema
wa maisha bonamu yangu alitoroka katika chmba
alichomowekwa na kuanza kuzagaa mitaani"
alizidi kulia akalia sana. Mimi nilimpooza baada ya
kunyamaza tena aliniuliza
"wewe umemfahamu vipi Majid?"
na mimi nikamueleza kila lililonikuta. Nilimueleza kuanzia
mwanzo wa kuingia Gamboshi mpaka nilipofukuzwa
shule. Ni siku hiyo ndiyo niliamua nije kumtafuta majid ili
niweze kupata nguvu ya utajiri na mvuto wa biashara.
Niliona jambo la kufanya na la kunipatia pesa kwa haraka
ni kutumia nguvu hizo za kichawi kupata pesa. Sikujua ni
biashara gani nitafanya ila sikuumiza sana kichwa
kuchagua aina ya biashara. Hiyo ni kutokana na elimu
yangu ndogo kunituma nifikirie kuwa hata mfanyakazi wa
ndani lakini kwa kutumia nguvu za kichawi niwe na mvuto
wa kupata mshahara mkubwa. Ndipo hapo yule msichana
aliyejitambulisha kwa jina la zamda akaniuliza
"una sehemu ya kukaa sasa?"
nilipata shida kumjibu moja kwa moja lakini ilibidi nimjibu
ili nisikose sehemu kama alikuwa na nia ya kunisaidia.
"sina sehemu yeyote ya kukaa zamda naomba unisaidie
dada yangu"
alinikaribisha nyumbani kwake. Chumba kimoja kisicho na
kitanda bali godoro kubwa la sita kwa sita likiwa
limetandazwa chini kuonesha kuwa hiyo ndiyo ilikuwa
sehemu yake ya kulaza mbavu zake. Nilipokuwa
nikishangaa chumba hicho ni hapo aliponieleza kuwa
"hatupo peke yetu sehemu hii kuna wenzangu wawili
ambao wameelekea kazini mimi natokaga saa nne"
nilijiuliza kazi gani ya jioni? Kazi ya usiku asubuhi
mahesabu ndiyo hii? Nikahisi nilikuwa nikizungumza na
dada poa dada anayeuza mwili wake kujipatia kipato.
Nikaanza kuingiwa na uoga nikatetemeka. Zamda
aliniambia
"usiogope utakaa hapa kwa muda na utazoea tu ata
wewe mwenyewe utatamani kazi yetu. Inalipa sana"
alinieleza uzuri wa kazi yao.
"yaani kwa siku unalala na wanaume hata kumi kila
mmoja anaklipa buku kumi na kondomu wale wanaopenda
kavu kavu unawachomoa hata 50"
macho yakanitoka pima nisiamini kile ninachokisikia.
Ilikuwa ni sauti ya zamda iliyokuwa ikitoka bila mzaa na
uso wake ukiwa umepambwa kwa tabasamu pana.
Aliyakatisha maongezi na kulirudia jiko lake na kuanza
kupika. Lilikuwa ni pishi la wali wa nazi na samaki.
"dada yangu hii ni sehemu ya makaburi miaka yote
napafahamu hapa ni makaburini mimi nimezaliwa
nimeyakuta na hata mengine yameanza kupotea lakini hili
ni eneo la makaburi"
nikaanza kuchukia kutokana na junicheka huko lakini
haikunizuia kumuuliza
"sawa lakini kwanini unacheka?"
alinyamaza kisha akanijibu
"si wewe tu hii sehemu inaonesha ina mauza uza ya peke
yake kwa sababu wengi huja hapa na kubaki
wakishangaa. Wanashangaa na kutuuliza sisi wenyeji "hivi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hapa haya makaburi yamekuja lini?" sasa ndio hapo pa
kujiuliza makaburi yanabebwa na kuletwa sehemu moja
na nyingine?"
aliendelea kucheka huku akijipiga piga mapajani baada ya
kupiga magoti chini. Nikamuuliza swali lingine
"unamfahamu Majid?"
nilimuona kushituka sana. Alishitua haswa na kuyatoa
macho kwa mshangao. Aliniuliza kwa kubwatuka huku
akiwa amesimama wima
"shekhe majid?"
niliitikia kwa kumtingishia kichwa kuonesha ndiye
niliyemmanisha. Kitu cha kushangaza alianza kulia. Alilia
haswa tena alilia kupitiliza kama mtoto mdogo kamasi
jepesi likamtoka na nilipombembeleza kwa muda mrefu
alinieleza
"huyo si binadamu dada yangu"
mimi nikajitia kushituka nikauliza kwa mshangao
"si binadamu!? Umejuaje?"
kutokana na kilio ilinipa shida kumuelewa kiufasaha
alichokuwa akizungumza. Ilimbidi nimkatishe kwanza
alichokuwa akiongea ndipo nilimuomba arudie alichokuwa
akiongea nimuelewe zaidi. Aliniambia
"huyo ni jini aliyekuwa akimlinda mjomba wangu. Ni jini
aliyetengenezwa kwa moto ni mweye nguvu sana.
Alisababisha matatizo makubwa sana nyumbani. Ni jina
aliyenunuliwa mascut lakini mjomba alipovunja masharti
alimnyonya damu mjomba pamoja na kumuweka ukilema
wa maisha bonamu yangu alitoroka katika chmba
alichomowekwa na kuanza kuzagaa mitaani"
alizidi kulia akalia sana. Mimi nilimpooza baada ya
kunyamaza tena aliniuliza
"wewe umemfahamu vipi Majid?"
na mimi nikamueleza kila lililonikuta. Nilimueleza kuanzia
mwanzo wa kuingia Gamboshi mpaka nilipofukuzwa
shule. Ni siku hiyo ndiyo niliamua nije kumtafuta Majid ili
niweze kupata nguvu ya utajiri na mvuto wa biashara.
Niliona jambo la kufanya na la kunipatia pesa kwa haraka
ni kutumia nguvu hizo za kichawi kupata pesa. Sikujua ni
biashara gani nitafanya ila sikuumiza sana kichwa
kuchagua aina ya biashara. Hiyo ni kutokana na elimu
yangu ndogo kunituma nifikirie kuwa hata mfanyakazi wa
ndani lakini kwa kutumia nguvu za kichawi niwe na mvuto
wa kupata mshahara mkubwa. Ndipo hapo yule msichana
aliyejitambulisha kwa jina la Zamda akaniuliza
"una sehemu ya kukaa sasa?"
nilipata shida kumjibu moja kwa moja, lakini ilibidi nimjibu
ili nisikose sehemu kama alikuwa na nia ya kunisaidia.
"sina sehemu yeyote ya kukaa Zamda naomba unisaidie
dada yangu"
Alinikaribisha nyumbani kwake. Chumba kimoja kisicho na
kitanda. Lilikuwepo godoro kubwa la sita kwa sita likiwa
limetandazwa chini kuonesha kuwa hiyo ndiyo ilikuwa
sehemu ya kulaza mbavu zake. Nilipokuwa nikishangaa
chumba hicho, ni hapo aliponieleza kuwa
"hatupo peke yetu sehemu hii kuna wenzangu wawili
ambao wameelekea kazini mimi natokaga saa nne"
Nilijiuliza kazi gani ya jioni? Kazi ya usiku, asubuhi
mahesabu; ndiyo hii? Nikahisi nilikuwa nikizungumza na
dada poa. Dada anayeuza mwili wake kujipatia kipato.
Nikaanza kuingiwa na uoga, nikatetemeka. Zamda
aliniambia
"usiogope utakaa hapa kwa muda na utazoea tu hata
wewe mwenyewe utatamani kazi yetu. Inalipa sana"
alinieleza uzuri wa kazi yao.
"yaani kwa siku unalala na wanaume hata kumi kila
mmoja anakulipa buku kumi na kondomu wale
wanaopenda kavu kavu unawachomoa hata 50"
macho yakanitoka pima nisiamini kile ninachokisikia.
Ilikuwa ni sauti ya Zamda iliyokuwa ikitoka bila mzaa na
uso wake ukiwa umepambwa kwa tabasamu pana.
Aliyakatisha maongezi na kulirudia jiko lake na kuanza
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/---
kupika. Lilikuwa ni pishi la wali wa nazi na samaki.
Mimi sikuona cha kumsaidia, hivyo niliendelea kutalii
ndani ya hiko chumba kwa macho. Dakika chache
baadaye nikiwa bado nimezubaa, waliingia wasichana
wawili. Hawakuwa bado wamefikia umri wa kuitwa
wanawake kwa kuwa hawakufika huko. Walikuwa
wamevaa vivazi vilivyoacha maungo yao wazi kwa
asilimia kubwa. Niliwatazama kwa aibu kidogo sikutarajia
kama kuna binadamu mwenye uwezo wa kutembea
barabarani namna ile. Wale wasichana walishituka sana
kuniona. Wote walikuwa weupe lakini mmoja alionekana
kuwa mweupe zaidi kutokana na kujikoboa. Niliwasalimu
nao walinisalimu huku wakiwa wamezubaa kwa
kunishangaa. Mmoja alikuwa anavuta sigara mwingine
akiwa na chupa ya wine. Zamda aliwauliza
"hoya mbona mmerudi mapema leo? Tusizinguane mjue"
Wale mabinti walicheka kilevi levi huku wakiwa
wameshajitupa kitandani. Mmoja wao ndiye aliipata sauti
yake
"leo tumepata lizungu hilo, lina mihela kibao. kila mmoja
kamganjia laki mbili mbili"
wakawa wanachomoa noti za elfu kumi kumi. Nyuso zao
zikiwa zimepambwa na tabasamu pana sana. Zamda naye
alionekana kuchanganyikiwa kupita kiasi. Aliwarukia
wenzake na kuanza kushangilia kwa pamoja. Mimi
sikuelewa kilichoendelea hivyo nikatulizana katika kochi,
nikiwatazama tuli.
Baada ya muda kidogo chakula kikapakuliwa tukala.
Wakati huo wa chakula mabinti wale waliolewa chakari,
ndipo walipaza sauti zao
"we zamda"
zamda alimgeukia yule aliyezungumza
"hivi mbona haututambulishi huyu ni nani?"
zamda alinigeukia mimi na kutabasamu, kisha kicheko
kidogo kikampitia. Alisema
"huyu ni mdogo wangu tutakuwa naye hapa geto"
alinigeukia mimi na kuniambia
"Bella hawa ndiyo wafanyakazi wenzangu na ndio
tutakuwa nao hapa siku zote hii ni hali ya kawaida tu
isikushangaze"
mimi nilisikitika tu, huku kicheko kisicho na ladha ya
kicheko kikinipitia. Wakati ambao mimi naenda kulala
zamda alitoka akiwa amevaa baibui na kujifunika kama
ninja. Lakini nilishangazwa na alichovaa ndani. Kilikuwa
ni kituko na kitu cha kushangaza. Alivaa kipensi cha jeanz
na kitopu kilichoziba matiti yake tu. Aliondoka na wale
mabinti alionitambulisha kwao kuwa ni Caro na Prisca.
Pombe zilikuwa zimewaisha kidogo, hiyo ilikuwa yapata
saa 7 usiku. Nililala zangu lakini kwa uoga kidogo.
Nilikuwa muoga kutokana na ugeni nilionao katika hicho
chumba. Akili yangu ilianza kutafakari kuhusu kulala
nyumba moja na wasichana waliokuwa wakiuza miili yao.
Hiyo ilinitisha sana. Nikajisikia vibaya na kuapa kuwa
sitoingia katika kazi hiyo hata kama nina shida kiasi gani.
Nikiwa katika kuwaza huko, sikujua usingizi ulinipitia saa
ngapi. Nilishitushwa na mlango uliogongwa kwa ghadhabu
na sauti ya kilevi zile za Caro na Prisca ndio zilipiga
kelele sana. Yeye Zamda aliniita jina langu kabisa
"bella fungua bwana"
nilijinyanyua kivivu na kwenda kuwafungulia, huku
nikipikicha macho yangu nikiwa nimenuna. Nilipotupia
jicho saa iliyopachikwa ukutani, katika chumba hicho;
ilikuwa imetimu saa 12 asubuhi. Wote walikuwa
wamelewa chakari. Zamda alikuwa anapepesuka sana.
Caro hakujiweza kabisa, Prisca ndiye akaropoka uozo
ulioniudhi
"halafu Zamda sisi hatulei watoto yatima humu ndani.
Sisi tukauze miili yetu, yeye alale asubiri kupakua tu.
Hapa kama vipi mimi nahamia geto la kina Sandra, sitaki
unafki mimi mtoto mzuri kabisa huyu"
alinishika matiti yangu akiyabinya binya. Nilimputa mkono
wake na kutoka nje. Nilikuwa nikilia. Sikutaka kuwa
changudoa sikutaka niuze mwili wangu. Hivyo nikiwa nje
zamda alinifuata. Alinishika bega langu kwa upole na
kunipa moyo
"Bella mdogo wangu sisi haya ndiyo maisha yetu hapa
geto. Mimi mwenyewe nilipotoka kijijini nililelewa na
mama mmoja huko kinondoni, yeye ndiye aliyeniingiza
katika hii biashara. Nilikuwa nikifanya kazi za ndani
kwake kumbe yule mama alikuwa anauza mabinti.
Sikupenda kama wewe, lakini hivi sasa nimezoea. Na
wewe utazoea tu mdogo wangu"
nilimuangalia kama nilikuwa nikitazama kinyesi kilichotoa
harufu iliyokera. Nilimjibu kwa hasira
"siwezi.. Siwezi kuwa changudoa zamda"
alinicheka kwa sauti ya kilevi. Kisha alinyanyuka kwa
kutumia muhimili wa bega langu kujinyanyua. Akaniambia,
huku akipepesuka pepesuka.
"sina lingine la kuzungumza, umetaka sawa hujataka
sawa. Lakini kama hauhitaji, unaweza kuchukuwa njia
zako"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alimaanisha. yaani alichoongea kilikuwa ni kile ambacho
kilimtoka ndani ya moyo wake. Nilijishika kichwa nikiwaza
sana. Sikujuwa nitaishi vipi baada ya kutoka hapa kwa
zamda. Nililaani kila maisha niliyoyapitia baada ya mama
kufariki. Niliyachukia maisha ya Gamboshi. Nikamchukia
babu kunipeleka huko. Yeye ndiye alinisababisha mimi
kuwa mnyama na ubinadamu unikae pembeni. Niliikosa
shule, na nikawapoteza wale waliojitolea kunisaidia
kuyasongesha maisha yangu kwenda sehemu fulani.
Machozi yakanitoka. Yakaniponyoka kwa uchungu nikiwa
hapo nje. Niliingia ndani baada ya kuutokomeza muda wa
zaidi ya dakika thelathini hapo nje. Nilipoingia ndani,
niliwakuta wote wakikoroma kwa pamoja. Walilala ovyo
hakika walikua wamechoka.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment