Simulizi : Niliongea Na Shetani Ili Niwe Tajiri
Sehemu Ya Tano (5)
Niliingia ndani baada ya kuutokomeza muda wa
zaidi ya dakika thelathini hapo nje. Nilipoingia ndani,
niliwakuta wote wakikoroma kwa pamoja. Walilala ovyo
hakika walikuwa wamechoka.
Mimi nilijiandaa kufanya usafi
japo nilikuwa mgeni, nilitaka niwaridhishe wasije
kuendelea kunighasi niingie katika kazi hiyo ya kuuza
mwili wangu. Nilifanya kazi kwa bidii nilifua nguo zao zote
na kuosha vyombo na kufagia uwanja. Nilichukuwa muda
mrefu pia kuchota maji kutoka umbali mrefu. Nilipomaliza
niliwakuta tayari Caro Prisca na zamda wamekwishaamka
na wamekaa kibarazani wakicheza karata. Zamda
aliponiona aliniambia
"mdogo wangu unaonyesha wewe ni mchapakazi sana?"
sikumjibu lolote nilinyamaza kimya kisha nikaingia ndani.
Nilipotoka tena ndani nikitaka kujumuika nao, prisca
akaropoka
"acha upuuzi wewe unakaa umeshapika?"
nilijinyanyua bila hiyana nikaenda kuandaa chakula. Kwa
kuwa sikuwa na hela niliwaomba hela ya kwenda gengeni
kununua viungo vya mboga.
"nani akupe hela? Wote si wanawake humu ndani? Kuna
bwanako humu? Nenda kanunue hivyo viungo kwa hela
yako hatuuzi mwili kulisha watoto yatima sisi"
maneno ya caro yalinichoma sana, ila sikuwa na jinsi
nilienda kuchukua senti iliyobaki kwenye akiba yangu na
kununua viungo na vipaja vya kuku vilivyouzwa kwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mafungu. Siku hiyo tulikula tukashiba. Hakuna ambaye
alithubutu kunikaripia wala kunigombeza usiku ulipotimu
kila mmoja alishika njia yake kwa wakati wake wakiniacha
mimi nimelala. Asubuhi ikawa vile vile wamerudi wakiwa
wamelewa na kama kawaida ya prisca alirudi na maneno
yake ya maudhi. Ikawa vile kwa muda wiki nzima mimi
ndiye nilitoa pesa yangu iliyobaki kutoka shule
nilipofukuzwa na kuwalisha wao, hiyo iliokana na kuogopa
kushinda njaa ama kufukuzwa kwa sababu ya kukataa
kujiuza yaani kufanya biashara ya uchangudoa. Ni katika
siku hizo pia nilijitahidi kutafuta kazi mbali mbali sehemu
mbalimbali lakini ni nani angenipokea ikiwa sikuwa hata
na cheti cha form four? Ni nani alikuwa anahitaji mtu
ambaye alikuwa hajui hata chuo ina rangi gani? Ni hapo
ndipo nilipokata tamaa ya maisha na kuona nimepewa
adhabu kubwa sana nisiyoweza kuistahimili. Nilimlilia
sana mama yangu usiku na mchana na kumuuliza mungu
kwa nini amemchukua wakati nikiwa bado namuhitaji
mama. Wakati ambao alikuwa na umuhimu mkubwa
katika maisha yangu. Mtu pekee aliyekuwa na uchungu na
mimi. Mtu pekee niliyefahamu kuwa alikuwa ananipenda
na kunihangaikia ili niwe na maisha mazuri. Ni hapo chozi
likanitoka nikiwa nje ya chumba cha zamda nikiwaza
mengi. Ni siku hiyo ndiyo nilimuahidi zamda kuwa
nitaianza kazi hiyo. Kazi ya kuuza mwili wangu. Zamda
alifurahi sana. Alifurahi huku akiniambia kuwa
"utapata wanaume wengi sana mdogo wangu hadi
naogopa utanipora mzungu wangu"
alisema huku akicheka, mimi moyoni nikilia. Nikalitoa
tabasamu la hudhuni nikiwa nalia ndani kwa ndani.
Nilirudi ndani nikamkuta Zamda ndiyo anajiandaa.
Alishangaa kunikuta bado nipo ndani ya midabwada
yangu isiyotamanisha kuitazama
"we bella ha!"
alikuwa amesimamisha zoezi la kuivaa ile pensi iliyokuwa
imembana haswa. Kisha alikuwa ananishangaa mimi
niliyekuwa namshangaa yeye.
"mbona bado umevaa hiyo matambara yako? Si nimekupa
nguo wewe uvae?"
nguo alizonipa zilikuwa bado kitandani nimeziweka.
Nilipoziangalia, nilishindwa kulizuia chozi lililoniponyoka.
"unalia nini sasa?"
nikamjibu "zamda sijajua itakuwaje siku ya kwanza katika
hii biashara mimi si mwenyeji zamda naumia moyo
wangu unaniuma"
alinicheka kwa dharau kisha aliniuliza
"hivi kuna mtu ni mwenyeji katika kila jambo? Acha
upumbavu au unapenda unavyotukanwa tukanwa na
prisca? Unajua ni kiasi gani wanaudhika kukuona
ukiwategemea humu ndani? Nimeshachoka kukutetea mtu
hubebeki"
alikuwa anaivaa nguo yake kwa ghadhabu. Na mimi
ikanilazimu nivae nguo hiyo kwa juu nikajitupia khanga
zangu. Moja nilijifunga kwa chini ya pili nikajitupia kifuani.
Niliumia sana. Nilianza kujiona ni msichana mchafu
asiyefaa katika jamii. Lakini kutokana na shida
inayonikabili, ilinipasa kufanya hivyo. Niliingia barabarani
kule maeneo ya ubalozi wa ufaransa ndiyo ilikuwa windo
letu. Tulipoona kulipooza mimi na zamda tulihama kijiwe
tukaelekea maeneo ya jolly club huko tulikuwa tumekaa
barabarani tukisimamisha kila gari la kifahari lililokuwa
likitupita. Mimi sikuwa mzoefu na wala moyo
haukunisukuma kufanya hayo. Nilikaa chini huku baridi la
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
usiku likinipiga. Nilikuwa nalia sana, nililia kupita kiasi.
Nasukuru mungu siku hii hakukuwa na wateja kabisa
hivyo mimi sikupata mtu wala zamda hakupata mtu.
Zamda alinieleza kuwa siku ya jumanne mara nyingi huwa
mbaya katika vijiwe vyote anavyoibukaga. Mimi kwangu
ikawa afadhali sikuona kama hiyo ilikuwa ni mbaya au
nuksi kwangu. Siku ikapita vizuri. Kutokana na tabia
yangu ya kukataa wateja waliokuwa wananihitaji, Zamda
alikerwa nayo. Yeye akaniambia wazi.
"sikia bella, mimi siwezi nikawa nakuhudumia bure
unakula na kulala bure. Naomba uchukuwe ustaarabu
wako"
alikuwa hana mzaha kwa kile ambacho alikizungumza.
Mimi nilianza kuogopa. Nilfikiria ni wapi nitaenda endapo
kama zamda pia naye amenichoka? Niliamua kukubali.
Nikamuahidi zamda
"nitafanya na nitaleta pesa nyumbani Zamda naomba
unisamehe"
alitabasamu baada ya kuridhishwa na jibu langu. Kisha
tukaingia kazini.niliingia kazini kwa mara ya kwanza
nikalala na wanaumewawili. Moyo wangu uliniuma sana
siku hii lakini sikuwa na jinsi. Nikawa changudoa mpya.
Wanaume wale waligundua mimi si mzoefu kutokana na
ugeni wangu katika mambo ya kitandani. Hata katika
kuwavalisha zana sikufanya kama wengine waliozoea.
Waliponiingilia nilikuwa nalia machozi yakinishuka. Sikulia
kwa sababu nilisikia raha au nilifurahia tendo hilo ila nililia
kwa uchungu. Uchungu wa kuwa changudoa bila kupenda.
Nilirudi nyumbani na noti mbili za shilingi elfu kumi ikawa
sawa kwao wakatabasamu na prisca ndiye aliniambia
"utazoea tu dogo usilie kama una mama vile"
caro akampokea
"ndiyo hivyo bella cha msingi jitahidi tu utundu usije
ukakimbiwa bila kuachiwa chochote maana wateja wetu
wengine ni wehu"
kisha siku hii pia nilijaribu pombe. Sikuijaribu tu niijue ina
ladha gani kwa kuwa nilifahamu ilikuwa ni chungu kama
silki. Lakini nilijaribu nikidhani ni njia sahihi ya kukata
mawazo niliyo nayo. Jinamizi la mawazo lililonikaba na
hatia ya mimi kutembea na wanaume nisiowafahamu hata
kwa majini. Hakika nilijihisi fedheha. Aibu na
kudharirishwa sana ila glass ya kwanza ya pombe ile aina
ya value brandy niliyoichanganya pamoja na maji ya uhai
ilitosha kuuteka ufahamu wangu. Nilianza kuwa
mchangamfu na muongeaji sana. Wote kwa pamoja
tukawa tupo bwi mimi na wenzangu. Tulirudi nyumbani
tukiwa tunapepesuka. Tulikokotana mpaka eneo la
barabara baada ya kuiacha bar ya Q bar maeneo ya
masaki tulimoenda kupata kilaji. Tukakutana na bajaji
kadhaa pale katika kituo cha macho. Ikatupeleka mpaka
katika geto letu la mwananyamala. Sikukumbuka ni nani
alikuwa na akili kidogo kati yetu aliyemlpa yule dereva wa
bajaji pesa yake na kutufungulia sisi kuingia chumbani.
Ninachokumbuka ni mimi nilijikuta nikiwa juu ya godoro
asubuhi iliyoanza kupitisha jua lake kali chumbani humo
huku nikimtusi Caro kwa kunipandishia miguu nadomo
lake lililotoa harufu kali ya pombe na kukoroma kwa hali
ya juu katika sikio langu. Nilimsukumuzia upande wapil
akakutana na uso wa zamda wakakumbatiana baada ya
zamda kujizaba kibao kumpiga mbu aliyekuwa
amemng'ata na hapo ndipo nilimtazama Caro kwa hali ya
uvivu nilishitushwa kumkuta yeye alilikataa godoro na
kwenda kulala chini kabisa akiibusu sakafu. Nilijinyanyua
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
taratibu lakini kichwa kikakataa. Kilikuwa kikiniuma kupita
kiasi. Nikaijutia pombe niliyoinywa kwa furaha jana usiku.
Niliamka nikaenda kupigwa mswaki na kuuweka mwili
sawa na kuanza kuandaa chai ya chapati za maji yaani
na mayai pia. Hapo mmoja baada ya mwingine wakawa
wanaamka wakiwa na uchovu mwingi. Zamda ndiye
alikuwa wa kwanza kunyanyua chapati moja kuitia
mdomoni
"mnhh mwanamke wewe ni mjuzi haswa wa jiko"
akaimeza moja ya ile chapati niliyoitia iliki inukie
akaendelea kunipa sifa zangu
"yaani ningekuwa na kaka ningekupa hata usipate hizi
shida zote. Mtoto tashtiti wewe"
nilimuangalia kisha nikaangua kicheko jinsi
alivyonitingishia sehemu zake za nyuma. Hakika zamda
alikuwa amebarukiwa mzigo mkubwa sana sehemu zake
za huku nyuma na juu ya kiuno alikatika ki kike. Unywele
uliomdondoka mpaka mgongoni nikajiuliza kimoyo moyo
"mungu jakunyima nini wewe dada mpaka ujiuze mwili
wako ulivyo wa thamanu hivyo?"
nikajisonyea taratibu nikimuangalia alipokuwa akijitingisha
huku akiingia ndani. Mimi niliugeuza geuza mkaa na
kuendelea kumwaga unga wa ngano uliojaa mayai na maji
kidogo na iliki nyingi kikaangoni.
Pishi lilipokuwa tayari nikalitupa juu ya sahani nikaliweka
kati gombania goli ya mikono ikawa imeanza. Kila mtu
alikuwa akiguna alipokuwa akishushia na maziwa ambayo
sikuacha kuweka kila kiungo. Kama mdalasini, tangawizi
na iriki. Hakika chai ikawa imekolea. Furaha ikawa kubwa
ndani ya geto hili la machangudoa wenzangu. Ila kipindi
hiki chote hakuna ambaye alifahamu upande wangu wa
pili. Upande ambao ulinifanya kuikosa shule na kumkosa
mwanaume wa maisha yangu, Jordan. Kila nilipokuwa
nikimkumbuka yeye machozi yaliniponyoka. Hakika nilihisi
huzuni sana kumkosa Jordan. Si Caro wala Prisca
ambaye hakunipenda tena ndani ya ile nyumba. Siku za
usoni nikawa mzoefu na mtundu kazini. Kutokana na pesa
nilizokuwa nazipata, nikaongeza nakshi katika vifaa
vyangu vya kazi. Nikwa na maana kuwa kiuno changu
nikakipamba na mkufu wa dhahabu. Nikaingia unyagoni
nikafunzwa jinsi ya kumkatikia mwanaume. Zamda
alinieleza
"bibi wewe mwibie kihisia akuongeze mkwanja"
alikuwa akisema hayo huku akikatika. Nakiri kusema
zamda alifuzu chuo cha mapenzi. Sikupata picha
wanaume ambao anakutana nao yeye katika shughuli zetu
za uchangudoa. Ila nilipomuuliza hakuwa tayari kunijibu.
Mahudhurio mazuri kazini yakazidi kuleta manufaa zaidi
katika kazi na maendeleo katika chumba chetu. Chumbani
kwetu kukawa na vitu vingi vya kifahari. Ni hapo ndipo
tukapatwa na wazo la kuhama katika chumba kimoja na
kutafuta vyumba viwili yaani sebule na chumba.
Tulipokipata, tukanunua sofa set, runinga ya kupachika
ukutani, friji na zuria la manyoya ikaipamba sebule yetu
iliyoibeba meza kubwa ya duara. Chumba kikapuliziwa air
fresh pakanukia vizuri na kubeba kitanda cha kifahari
nilichopata kukiona kwenye tamthilia mbalimbali
walizoigizia katika vyumba vya mahotel. Nilijihisi raha siku
zote na kuifurahia kazi yangu. Siku nyingine nililazimika
kuwawekea madawa wale ambao nilifahamu kuwa
walikuwa na pesa za kutosha ili niwaibie wakiwa
usingizini. Nilifanikiwa kwa kuwapagawisha kwa viuno
vyangu. Uzuri ule niliokuwa naukataa zamani sasa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nikajitamani mwenyewe nilipojitazama kwenye kioo.
Ikafika ile siku ambayo nilipatwa na mshituko mkubwa
sana moyoni yaani ni mshituko wa ajabu. Mimi nilikuwa
pale pale kwa siku zote ambapo huwa nakaa nikitege
mingo zangu yaani wateja. Ndipo likatoke gari ya kifahari.
Siwezi kukambuka ilikuwa ni gari ya aina gani kwa
sababu mimi si mjuzi mzuri wa magari. Sikupata shida
kulikimbilia kwa kuwa lilinifuata mpaka pale nilipo
likiwaacha wenzangu watatu pale mwanzo. Lilipopiga
breki mbele yangu kioo cha mbele kilifunguliwa na
kukutana na kijana ambaye alikuwa anaonesha fedha
kwake haikuwa tatizo. Alinipatia shilngi elfu hamsini bila
kuongea naye chochote kisha aliniambia ingia ndani ya
gari. Kwa kuwa nilihitaji pesa niliingia bila wasiwasi.
Humo ndani ya gari nikakutana tena na watu watatu..
Watu hao sikuweza kuwafahamu wala kuona nyuso zao
kutokana na giza zito lililopo ndani ya ile gari. Gari hilo
likaanza kutembea kwa mwendo wa kawaida huku wale
vijana wa kule nyuma wakiwa wameniweka katikati yao
wakianza kunichezea chezea kila sehemu yangu ya mwili.
Kwa kuwa tayari walikwisha nilipa, mimi niliwaachia
wafanye wanachotaka. Walinishika sana mpaka pale
waliponihitaji tukiwa humo humo ndani ya gari nikahisi
kuifahamu sauti ya mmoja wa watu hao. Yeye alikuwa
akilazimisha sana kuanza yeye.
"niacheni nianze bwana masela mimi ndiye nimetoa pesa
nyingi"
alikuwa akikoroma. Sauti hiyo ikawa inaniadhibu
ikaniadhibu sana. Nikajiuliza wapi nimeiskia? Wale watu
wakaanza kuniingilia mmoja baada ya mwingine wakiwa
wamevaa zana zao. Walipomaliza wakanishusha pale pale
waliponichukua na mmoja kati ya wale watu alishuka na
mimi kwa nia ya kuongea. Alpokuwa akishuka mimi
sikujuwa lengo lake. Ula nilifahamu kuna uwezekano labda
huduma yangu ilimpagawisha. Tulipofika eneo lenye
mwanga ni hapo nilipoanza kuukosa mhimili wa
kusimama na kutaka kuzimia. Lakini nilijitahidia hilo
lisitokee. Aliyekuwa amesimama mbele yangu hakuwa
mwingine bali ni Jordan. Jordan mpenzi wangu alikuwa
amesimama mbele yangu naye akiwa ameshitushwa sana
Nilimuita huku midomo ikiwa inatetemeka
"jordan"
hata maneno nayo hayakusikika sawia. Naye aliniita kama
alikuwa akijifunza kuzungumza.
"bella? Ni wewe tulikuwa ndani ya lile gari"
alikuwa kama amewehuka akaniuliza tena
"unafanya nini hapa?"
nilimjibu kwa ujasiri huku machozi yakinitoka
"jordan mimi ni changudoa sasa"
"Bella? Ni wewe tulikuwa ndani ya lile gari"
alikuwa kama amewehuka akaniuliza tena
"unafanya nini hapa?"
nilimjibu kwa ujasiri huku machozi yakinitoka
"jordan mimi ni changudoa sasa"
Nilipouinua uso wangu jordan alikuwa akimalizia
kuufunga mlango wa gari na lilipotiwa ufunguo gari
likachomoka kwa mwendo wa kasi. Siku hii nilikosa raha
sana sikuamini kama Jordan pia alikuwa akifanya upuuzi
wa namna ile. Alikosa mwanamke wa kutembea naye
hata aanze kutafuta machangudoa? Nikaishusha thamani
nikamuona jordan alikuwa ni mwanaume mchamu
aliyepitiliza. Amewamaliza wale wanafunzi wa pale
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
shuleni na sasa ameamua kuja na huko kwa
machangudoa? Niliumia sana. Nikajilaumu kwa nini
nililaghaika ni ile shilingi lakimoja waliyonipatia? Kwanini
sikutaka kuwashwa kwa taa za ndani ya ile gari ili
nisikubali kufanya mapenzi na jordan? Si kwamba
sikuwahi kufanya mapenzi na jordan ila iliniuma yeye
kufahamu pia nimejiingiza katika uchangudoa. Hapo moyo
wangu ukaniambia kuwa jordan si wangu tena. Yaani
mimi na jordani ni watu wawili tofauti wanaoishi katika
maisha mawili tofauti hakika nisingeweza kuwa na jordan
tena. Iliniuma nikalia machozi yakanikauka. Ukawa msiba
ulionizika mwenyewe. Nikajipa moyo lakini bado uchungu
ulining'ang'ania. Kumpoteza jordan kukawa ni sawa na
kumpoteza mama yangu. Nakumbuka siku hii nililewa
kupita kiasi.nilikunywa sana kupita kiasi. Nililewa hata
sikujitambua. Niwale wasichana wa geto la kina sandra
ndiyo waliompa taarifazamda kuwa sijitambui. Siku ya pili
nilijikuta kitandani nikiwa nyaka nyaka lakini pochi yangu
ilikuwa salama. Zamda alikuwa akinitazama jinsi
nilivyokuwa najigeuza geuza pale kitandani nilipoamka
akaniuliza
"vipi mwenzangu? Wamekuweza jana?"
kwa kuwa nilikuwa nina pombe nyingi kichwani bado,
nikamjibu kilevi levi.
"anhaa! Achana na mimi"
baada ya muda waliniletea supu iliyojazwa ndimu na pili
pili nyingi. Niliinywa haraka haraka kutokana na njaa kali
iliyoniyafuna. Kisha nilitapika sana siku hii. Baada ta
kupata nafuu niliwaelezea kila jambo lililotokea mpaka
nikakutana na jordan. Caro alicheka sana prisca akadakia
huku naye akiwa anapasuka mbavu kwa kucheka. Alisema
"wewe bella hayo ni mambo ya kawaida kazini, wengine
tuliwahi kukutana na wajomba zetu tukaliana buyu hivyo
hayo mambo ni ya kawaida sana kazini chukulia poa
halafu ngoma isambe"
siku za usoni nikawa sawa na mawazo ya jordan
yakaniisha. Ni hapo ndio nikauona mwezi huu ulikuwa ni
mwezi mbaya zaidi kwangu. Kwa kuwa likatokea jambo
baya zaidi ambalo sikuwahi kudani kama lingewahi
kunitokea nikiwa kazini. Ni jambo nililoapa nitaacha kazi
hii ya uchangudoa. Ni siku hiyo ndipo niliutafuta mzimu
wa babu ulipo na kumuomba nafasi yake ya mimi
kuongea na mkuu wa nitimize sharti lolote analotaka ili
niwe tajiri. Sasa nikautamani utajiri kwa nguvu zote.
Yaani sikuona pibgamizi lolote la mimi kutimiza sharti
lolote ili mradi tu niwe tajiri. Ni siku hiyo nilipokutana na
mzungu mmoja aliyekuja akiwa ndani ya gari nyeupe aina
ya discovery. Alikuwa akivuta sigara zao zile kubwa
walizoziita siga. Alivutiwa na mimi kama ilivyo kawaida
ya wanaume wenye macho ya tamaa ya mwanamke
mwenye mvuto. Uso wake ulipambwa na tabasamu lauchu
huku akilamba lamba midomo yake. . Alishusha kioo cha
gari yake nikapulizwa na kiyoyozi cha ndani ya gari hiyo
kisha aliniambia.
"nitakupa shilingi laki tano"
nilishituka sana kwanza nilishituka kiasi hicho ca pesa na
pili nilishitushwa jinsi alivyoongea kiswahili fasaha. Lakini
tamaa haikunikaa mbali na moyo wangu. Nilitabasamu
lakibi nikijitia kuwa na wasiwasi nilimuuliza
"kwanini kiasi kikubwa hivyo?"
"wewe ni binti mrembo sana hivyo sipo peke yangu
nitakuwa na mwenzangu ambaye anatusubiri nyumbani."
hapo nikawa nimemuelewa nikaingia ndani ya gari kisha
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
safari ya kuelekea kwake ikaanza. Zile fedha alinikabidhi
shilingi laki mbili kwanza na nyingine kuniahidi kuwa
atanilipa nikishafika hapo kwake.
Nyumba yake ilikuwa ni ya kifahari sana. Nakumbuka
hakuwa na shida ya mlinzi amfungulie geti japo alikuwepo
askari wa kumlinda. Alilifungua geti kwa remot baada ya
kubonyeza tarakimu kadhaa ambazo sikujisumbua
kuzinakili kichwani. Gari likaingizwa sehemu ya parking.
Mimi na yule mzungu tulishuka baada ya kuja
kunifungulia mlango akakikamata kiuno changu. Nilikuwa
nashangaa jisni ya utajiri wa huyu mzee kweli alishindwa
kuwa na mke huyu? Iweje apende kuja kuchukuwa
machangudoa na kuwalipa kiasi kikubwa namna ile? Basi
nilifahamu jibu fika ningelipata ndani ya nyumba hiyo.
Sebule ya kifahari ikatupokea kwa makochi ya thamani.
Runinga pana yenye ukubwa zaidi ya nchi 42 ilipachikwa
ukutani ni zile zinazoitwa plasma. Jokofu lenye milango
miwili lililofunguka kama kabati la nguo. Hakika nilijihisi
kusimama katika moja ya sebule za ghali duniani ambazo
niliwahi kuingia na ambazo sijawahi. Nilikuwa nikiangaza
huku na huko nikitazama ufahari wa mzee huyu wa
kizungu. Alipoona nikitazama kila kona ya nyumba yake
bila kuchoka. Alikohoa kuupata uwepo wangu, kisha
aliniambia
"karibu kochini ili niweze kumuita ndugu yangu basi
tuanze biashara yetu"
mimi nilitabasamu huku macho bado yakiwa katika kila
kona nikitazama hiki na kile. Nilikaa lakini bado macho
yangu hayakuridhika kutazama nilichokuwa nakiona mbele
yangu. Nikiwa nimekaa, yule mzungu alikuja na mbwa wa
kizungu. Yale majibwa makubwa yenye mashavu
yaliyoshuka. Huyu alikuwa mnene sana na mwenye afya.
Huwa wanaitwa bull dog. Moyo wangu haukushituka
sana. Nilisimama na kuanza kumchezea chezea yule
mbwa bila uoga. Mimi nilikuwa mpenzi mkubwa wa mbwa
hivyo nilimshika mshika yule mbwa manyoya yake
yaliyonivutia. Nilipoona yule mzungu naye amekaa,
nikamuuliza
"yuko wapi rafiki yako? Muda unakwenda ninahitaji
kuondoka?"
yule mzungu akatabasamu. Kwa kuwasikumuelewa
niliendelea kusubiri nifahamu atajibu nini. Aliniambia
"nadhani damu zenu zimependana. Wengi humuogopa
bobby lakini wewe hukuwa na haja ya kukuelekeza nini
cha kumfanyia"
nikawa bado sijamuelewa nikawa katika kumshangaa.
Nikamuuliza
"sijaelewa. Rafiki yako yuko wapi?"
nilimuona akinyanyuka kwa hasira akija kiti cha jirani na
nilipokaa mimi. Aliniambia kwa hasiara kidogo
"wewe malaya. Huyu ndiye rafiki yangu. Anaitwa bobby ni
mbwa anayejua zaidi ya binadamu hivyo hutajisikia
vibaya. Nahitaji ufanye naye mpaka aakaporidhika"
nilihisi sikusikia sawia alichoongea. Nilimuuliza ili nipate
hakika
"huyu ndiye rafiki yako uliyeniambia!!?"
akatingisha kichwa huku tabasamu likiwa usoni mwake.
Tabasamu lililoanza kunikera. Nilipomtazama yule mbwa
alikuwa akitoa ulimi wake kwa uchu. Sehemu zake za siri
zikawa zimeanza kusimama. Jasho likanitoka nikawa
nikimuangalia mbwa na yule mzee kwa zamu. Sikuamini
kama leo nilikuwa natakiwa nilale na mbwa yaani mimi
nitembee na mnyama? Niliona kitu ambacho
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hakikuwezekana hata chembe. Niliutazma mkoba wangu
ulio na pesa zote ulikuwa karibu. Nikatazama umbaii wa
mlango ulipo na nilipokaa,nikapima hazikuzidi hatua kumi
kwa kukimbia. Chozi likaanza kunitoka ilipomuona yule
mbwa akianza kunisogelea akinilamba lamba mapaja
yangu. Nakumbuka nilichomoka kama mshale kwenye kile
kiti ila nilifanya kosa dogo. Wakati nikikimbia niliuweka
mguu wangu sambamba na mdomo wa yule mbwa.
Hakuaacha kunipitishia meno yake na kuniparua kwa
makucha yake. Yule mzungu alikuwa akicheka sana huku
akimuambia vitu fulani yule mbwa ambavyo sikuvielewa.
Nilianguka bila kukosa mhimili mzuri. Yule mbwa akawa
ameshalipata titi langu na kucha zake zikiwa zipo juu ya
kifua changu. Aliichana sehemu kubwa ya titi langu la
kushoto lakini ikawa sawa na kunipa nguvu ya kumpiga
ngumi moja nikausikia mlio mmoja tu aliutoa kwa
uchungu na kumuona akiwa ameanguka mbali kidogo na
mimi. Nilianza tena harakati za kukimbia nje kuokoa
maisha yangu. Yule mzungu hakunipata hata alipojaribu
kunikimbiza. Nilikuwa tayari nimeshafika nje ya geti
baada ya kumpita yule mlinzi wake aliyekuwa akikoroma.
Ilikuwa yapata saa kumi alfajiri. Nilirudi hadi lile eneo
ambalo alinitoa yule mzungu.
Kutokana na titi langu moja kuwa wazi na nguo zangu
kuchanika nilishindwa kurudi nyumbani moja kwa moja.
Nilirudi eneo lile ili niweze kupata msaada wowote kwa
wenzangu. Nilipofika sikukuta mtu, nilimkuta kaka mmoja
ambaye alikuwa akifungua duka lake eneo hilo.
Nilimuomba hifadhi kwa kumueleza kila kitu bila kumficha
chochote akaniweka ndani ya kiduka chake kidogodogo
kisha nilimpatia shilingi elfu ishirini ili aweze kuninunulia
doti za kanga. Alikubwali kwenda kunitafutia. Nashukuru
alirudi akanipatia khanga hizo ambapo damu zilikuwa
zimeanza kukauka juu ya titi langu. Nikajifunika moja juu
na nyingine chini hakuna ambaye angefahamu kama ndani
nilikuwa uchi kabisa. Nilikuwa nikilia njia nzima. Wengi
walizani kuwa nilifiwa kutokana na uvaaji ule wa khnga
na jinsi nilivyokuwa rafu. Mmoja wa watu waliopishana na
mimi alinipa pole mwingine alisikitika
"masikini inawezekana amefiwa na mtu wake wa karibu"
ilikuwa tayari asubuhi mpaka niliofika katika geto letu.
Nilianza upya kulia baada ya kuwakuta wote wapo.
Niliwahadithia kila kitu na kuwaonesha majeraha ya
mbwa aliyening'ata. Waliniapa pole na kuanza taratibu za
hospitali. Mimi moyoni nikaapa siwezi kuwa changudoa
tena. Niliichukia kazi ile nikaichukia zaidi. Niliumia sana
kwa yaliyonikuta. Baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali
tulirudi nyumbani nikiwa nimeambiwa na daktari nipate
muda mwingi wa kupumzika.hiyo ikawa tiketi ya kuaga
biashara hiyo. Usiku ulipofika wenzangu waliniaga na
kuniambia kuwa kama nikipata nafuu nisiache kwenda au
hata kama nilihisi hali ilikuwa ni mbaya zaidi niwataarifu
wao watakuja kunitazama. Niliwaitikia kwa kichwa
nikiwaigizia kua nimezidiwa. Baada ya kuniacha na mimi
nikapitiwa usingizi. Katikati ya usingizi nilisikia sauti za
ajabu zikizungumza ndani ya hiko chumba nilicholala.
Niliamka nikiwa nimelowa sana jasho. Nilipoitazama feni,
ilikuwa ikifanya kazi yake kama kawaida. Nikajiuliza
"sasa hili joto linatoka wapi?" nikajifuta hilo na kujilaza
tena juu ya mto. Nikiwa hata kabla sijafunga macho
yangu nilisikia kelele za bati lililopasuka na mwanga mkali
mweupe kupenya ndani. Ilikuwa ni hali iliyotisha lakini
miujiza ya namna hiyo ikawa ni kawaida kwangu. Kiumbe
cha ajabu kikawa kimeshuka mfano wa ndege aina ya tai
kikanikwapua kutoka kitandani kwangu nilipolala na
kuanza kupaa na mimi kunipeleka nisipopajua. Hatimaye
kiumbe kile kilicho na umbo kama la ndege huyo
kikanitupa chini ya mti mkubwa aina ya mbuyu yaani
ulikuwa mkubwa sana huku moto ulikuwa umewashwa na
watu kadhaa wakiuzunguka moto huo. Niliwasikia
wakiimba nyimbo mbalimbali nisizozijua wala kufahamu
zilikuwa ni za lugha gani. Ule mti ukapasuka katikati na
kutoka kiumbe kingine cha ajabu yaani lilikuwa ni joka
lililotisha na kuwameza kila mmoja aliyekuwa katika eneo
hilo. Lilinimeza na mimi pia. Sikuhisi madhara yeyote
nilipokuwa ndani ya tumbo la huyu nyoka. Ila nilihisi
tulikuwa tunashuka kwa kasi sana yani kasi iliyonifanya
nihisi huenda ningeuacha mwili wangu na roho pekee
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ndiyo ingedondoka huko nilipokuwa nikielekea. Wale
wengine walikuwa uchi wakishangilia tukio hilo. Sikuweza
kumtambua hata mmoja ila nilikuwa nikisubiri kutazama
kitakachotokea. Moyo haukuwa na uoga sana kwa kuwa
nilishi tu ni lazima ilikuwa ni safari nyingine ya Gamboshi.
Lakini nilipata sana shida kila nilipojiuliza binafsi kwanini
babu hakuwa tayari kunisaidia nilipokuwa katika tatizo
kama la kung'atwa na mbu? Safari ikaishia katika kijiji
nilichokitarajia, Gamboshi. Nilipoangaza huku na huko
nikahisi kugongwa bega. Nilipogeuka alikuwa ni babu.
Alinikumbatia na kunipa pole. Kisha alinieleza
"usiku ule ule hakuweza kuliona japo jua la asubuhi"
babu alimuongelea yule mzungu aliyetaka nitembee na
mbwa wake
"mlinzi wake alistaajabu kumuona yule mbwa akimtafuna
mpaka mifupa huku kichwa pekee kikiwa kimelalia damu
yake nzito iliyoanza kuganda"
nikatamanu kuona hiko ambacho baba alikuwa
akinihadithia japo nilitabasamu kwa raha. Babu
akaniambia
"safari hii ni ya kukupa tena nafasi yako uliyopokonywa
baada ya kushindwa masharti na kukupeleka kwa mkuu
mwenyewe na umueleze shida zako"
Nikamuuliza swali babu
"shida zangu? Nimueleze nini babu?"
babu alinicheka akaniuliza
"ina maana wewe huna shida? Huna chochote unachotaka
kuomba mbele za mkuu?"
Nikamuuliza swali babu
"shida zangu? Nimueleze nini babu?"
babu alinicheka akaniuliza
"ina maana wewe huna shida? Huna chochote unachotaka
kuomba mbele za mkuu?"
Kiukweli si kwamba sikuwa na shida au sikumuelewa babu
alichonieleza ila ni jinsi ambavyo nilikuwa nahitaji mambo
mengi na makubwa nikahisi nitapewa masharti mengine
ambayo nitayashindwa kabisa kuyatekeleza. Nilimjibu
"nahitaji utajiri babu nataka niishi maisha mazuri nikiwa
na familia yangu"
"hayo ndiyo yakumueleza mkuu sasa"
tulipotea pale tulipokuwa kisha tukatokezea sehemu
ambayo sikuwahi kuingia tangu nianze safari zangu za
huku Gamboshi. Mahali hapa palikuwa ni pazuri sana.
Kulikuwa na watu wengi wakicheza ngoma na kuimba
nyimbo mbalimbali. Babu aliniambia kuwa.
"mkuu wetu ni mkuu sana. Hupenda kuabudiwa na
heshima hivyo hata ukiwa unazungumza naye hakikisha
kichwa chako kinasujudu mbele zake"
niliitikia kwa kutingisha kichwa huku nikiendelea kutazama
wale watu walivyokuwa wakicheza. Nyimbo zile
zilionekana kuwafurahisha sana jinsi walivyokuwa
wakiendana na midundo ya ngoma ilivyo kuwa ikipigwa.
Nilianza kutabasamu kidogo kidogo kutokana na mimi pia
nilianza kuvutiwa na ngoma hizo. Baada ya muda kidogo
watu wote wakainama zaidi hata babu pia alipoinama
alipiga kelele na mimi niiname pamoja naye. Niliinama pia
huku nisijue nini kinaendelea. Nilimtazama babu
nikimuuliza nini kinatokea
"mkuu ndiyo anakuja" Alininong'oneza. Baada ya muda nilisikia kicheko kikali
kutoka ule upande wa kaskazini yaani mbele nilipokuwa
nikiatazama. Sikuinua kichwa changu. Wakati hu uo
nikasikia sauti y a mkuu ikiita jina langu kwa sauti ya juu
"bella mwanangu karibu tena Gamboshi"
babu alinionesha ishara ya kusimama. Nilisimama
nikainamisha kichwa mbele zake
"ahsante mkuu"
nilimjibu kwa sauti ya juu iliyomfikia kutokana na eneo hili
lilirudisa sauti na kutengeneza mwangwi uliokera. Yule
mkuu alikua ni kile kiumbe cha ajabu kilichonipatiamashar-
ti niliyoyashindwa kipindi kile. Fumba na kufumbua
nilijikuta pembeni yake akichezeachezea nywele zangu.
Alikuwa anavuja damu na macho yake yaliudhi sana. Vile
vinanda vilikuwa vikitoa ala nzuri ya mziki kila alipokuwa
akicheka. Yule kiumbe aliniambia
"unataka nini kwangu? Sema nini nikufanyie?"
nilihisi furaha ya ajabu moyoni mwangu na wepesi kiasi
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
fulani. Nilipoipata sauti yangu nilimuambia
"nahitaji maisha mazuri na niwe mwenye mamlaka yaani
utajiri wa kuogopwa na kila mtu hata wale viongozi wa
serikalini"
yule kiumbe kikacheka mpaka kikatoa ceche za moto na
kusema
"inawezekana"
neno hilo likajirudia mara nyingi nyingi. Kisha aliniambia
tena
"sharti letu kubwa tunaitaka roho ya jordan. Pia usizae
mpaka utakapofikisha miaka 30 na usiwe mwenye
kumueleza mtu kila kitu usiyemjua"
nilitabasamu na kumjibu harakaharaka
"usijali mkuu nitatekeleza kila unaloniambia. Kama ni roho
ya Jordan hata sasa nitakuletea kama utahitaji"
alicheka sana yule kiumbe aliyetisha na kuniambia tena
"nenda nenda nenda utajiri upo nyuma yako ukikufuata.
Utakuwa tajiri mwenye viwanda vingi ndani na nje ya
nchi. Bidhaa zako zitapendwa na kugombewa kama
njugu. Ni utajiri utakaowashangaza wengi lakini
usimueleze yeyote na kumwambia chochote yeyote.
Nimekubariki wewe na uzao wako endapo utafuata
masharti hayo" kisha nilitoweka eneo hilo la gamboshi na
kujikuta nikiwa tena kitandani. Nilipowasha taa na
kutazama ilikuwa ni saa ngapi
"saa tisa?"
nikajilaza tena nikiwa nina mipango mipya ya kuitafuta
roho ya Jordan. Hii ilikuwa ni usiku wa siku ya pili.
Kutokana na kila mtu kuwa mzoefu, mimi niliwaaga
wenzangu kuwa naenda kijiwe kingine kutafuta wateja.
Walinikubalia bila kujua hila zangu. Wao waliniacha mimi
bado nikiendelea kujivuta vuta.
Nilikuwa nina uhakika kuwa wakati huu ni wakati ambao
kule shuleni ni lazima wangekuwa wameshalala. Niliwaza
jinsi nitakavyoitoa roho ya Jordani. Mwanaume ambaye
nilimpenda kuliko mwanaume yeyote katika hii dunia. Ila
sasa sikuona uchungu tena wa kuitoa roho yake.
Nilijaribu kuitafuta huruma lakini ilikuwa mbali na roho
yangu. Sikujuwa sababu ya kumchukia Jordan lakini
nilichojua sikumpenda tena wala sikuwa na huruma juu ya
kifo chake. Nilishuka mpaka juu ya bati la bweni ambalo
alikuwa akilala Jordani. Nakumbuka nilipata uwezo wa
kulipasua bati na kuingia mpaka alipo yeye. Alikuwa
akikoroma kwenye usingizi mzito uliomdondosha udenda..
Nilimnakuwa na kuanza kupae naye. Nilikuwa nimeota
mbawa na kugeuka kiumbe cha ajabu. Nilielekea mpaka
ulipo ule mbuyu ambao ulinidumbukiza mpaka ilipo
Gamboshi. Kama siku ile ya mwisho ndivyo ambavyo ule
mbuyu ulipasuka. Nikiwa bado nimembeba Jordan
sikumuona kama ni mzito tena. Ulembuyu ulipasuka na
lile joka likatokeza mbele yetu likanimeza mimi pamoja na
Jordan. Lilitumeza na kudumbukia mpaka Gamboshi.
Umati mkubwa ulikuwa ukitusubiri kwa hamu huku ngoma
mbalimbali zikiwa zinapigwa. Waliponiona watu wale
nikiwa na Jordan umati ule wote uliripuka kwa furaha ya
ajabu wakiwa wanapiga nduru na vifijo vigele gele vikiwa
juu. Nilielekezwa sehemu ya kumlaza Jordan mimi nikiwa
nimerudi katika hali yangu ya kawaida. Yule mkuu wa
Gamboshi alikuja kujumuika nami pale nilipokuwa
nimemlaza Jordan akiwemo na babu yangu. Kisha babu
ndiye alinipa kisu, akaniambia
"tunauhitaji moyo wa Jordan"
nikakipokea kile kisu. Mikono ikawa inanitetemeka.
Sikufahamu sababu ya mikono kunitetemeka ila nilijua ni
uoga uoga wa kuitoa roho ya binadamu? Nilishatoa za
wangapi? Nikauinua mkono ulioshikilia kisu na
kukichomeka upande wa moyo ulipo. Nilikipasua kifua
chake kwa kisu kilichopenya sawia kwenye moyo wake.
Jordan aliamka na kuanza kutapa tapa huku macho
kayatoa pima. Baada ya tukio hilo umati ule ulilipuka tena
kwa furaha na mkuu naye aliongeza shangwe hizo kwa
kicheko chake kilichokera. Nikaunyofoa moyo wake
uliokuwa ukidunda dunda na kumkabidhi babu. Kile
kiumbe kilizungumza
"umeweza bella umewezaa"
alikuwa ni mwenye furaha sana. Kisha mimi nikatoweka
na kujikuta juu ya kitanda changu. Sikulala siku hii,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nikikumbuka vile ambavyo niliutoa uhai wa jordan.
Nikiyakumbuka macho ya Jordan yaliyokuwa
yakinitazama kwa huruma. Nilitamani kulia lakini machozi
hayakunitoka. Ni hapo nilipoamua kuwasha taa ili niweze
kutoka nje nikakutana na begi lilotuna pembezoni mwa
kitanda nilichokaa. Nikavuta kumbukumbu kama niliwahi
kuliona humo ndani hapo kabla,
"hapana sijawahi kuliona"
nlipotaka kulisogelea nikaiangalia saa kutazama ilikuwa ni
saa ngapi. Ilikuwa yapta saa 8 usiku. Nikajiuliza.
Inawezekana kati ya Caro Prisca ama Zamda ni nani
alikuja na mgeni ambaye sijamuona? Nilipotaka
kulifungua niliusikia upepo uliovuma kwa nguvu sana
kisha nikaisikia sauti ikiniongelesha. Ilikuwa ni sauti ya
babu akiniamba
"huo ndiyo utajiri wako bella"
alijitokeza mzima mzima mbele yangu na kuniambia
"umemfurahisha sana mkuu wetu kwa kafara
uliyoifanikisha mbele yetu kuitoa roho ya mpeniz wako
umeuonesha ujasiri wa hali ya juu kama ambao ulinfanya
akuchague wewe. Utakuwa tajiri usiyefilisika katika
maisha yako na ukoo wako unachopaswa kuzingatia ni
kufuata masharti mkuu aliyokupa ndio kitu muhimu na
cha kuzingatia"
katika begi lile kulikuwako na pesa nyingi sana.
Maburunguta ya pesa zakigeni yaani dola mia mia.
Kuanzia siku hiyo maisha yangu yakabadilika. Sikuwa
changudo tena na wala sikuwa na maisha ya kutanga
tanga tena. Kila mtu akanijua na kunizungumzia kati ya
mmoja wa matajiri wa kutetemekewa ndani ya tanzania
na nje furaha yangu ikawa imetimia ya KUONGEA NA
SHETANI MPAKA KUUPATA UTAJIRI sifikiri kuyavunja
masharti wala kukiuka agano nililoweka mbele ya mkuu.
Nitawapeleka mamia Gamboshi na kuwaangamiza wale
waliokuwa wakimpinga mkuu wa Gamboshi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment