Search This Blog

PADRI MLA NYAMA ZA WATU - 3

 





    Simulizi : Padri Mla Nyama Za Watu

    Sehemu Ya Tatu (3)



    “Safari ilianza kwa mke na mume kuelekea hospitali huku sisi tukiwa tumeshafika kwa njia zetu za kichawi.

    Manesi walimpokea vizuri sana mgonjwa huyo huku wakimwambia mumewe kuwa, amefanya vizuri kumwahisha hospitali kwa sababu hali yake ni mbaya zaidi.

    “Lakini atapona?”

    “Atapona tu, usiwe na wasiwasi.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nesi mmoja aliposema hivyo, mimi nilimfuata yule mgonjwa na kumwekea tena mkono kichwani nikamgandamiza naye akaanza kulia kwa sauti huku akishika tumbo lake.

    “Mama nakufa, mume wangu nakufa,” alilalamika.

    Manesi walikimbia huku na kule wakimtafutia dawa za kumpa.

    Ilifika wakati nikawaita wachawi wenzangu waliokuwa wamesimama nyuma yangu, wakasogea, nikawaambia wakinge mikono kwa yule mwanamke, wakafanya hivyo, kitoto kikatoka kikiwa katika hali ya umauti.

    Tuliondoka mpaka kwenye uwanja wa nyumba yake, pale tukaweka mduara na kukiweka kile kichanga chini.



    Tulikimwagia mchanga mpaka kikawa hakionekani kisha ule mchanga tukauchota kidogo na kuutia kwenye kitambaa cheusi, mmoja wa wachawi akakichukua kuutunza kwa ajili ya matumizi mengine.

    Usiku huo huo, tulikwenda kwa mwanamke mwingine ambaye naye ni miongoni mwa wambeya wa kanisani kwa kupita mitaani na kusambaza habari kuwa, mimi ni mchawi wa kutupwa.

    Tulimkuta amelala hoi, huyu mwanamke hakuwa na mume, tulimchukua juu juu akiwa bado amelala hadi nje kwake, tukamtafutia fagio ili afagie uwanja usiku huo huo.



    Alikuwa akifagia huku tunampiga kwa fimbo na kuumia, tulifanya hivyo mpaka akaanguka chini na kupoteza fahamu, tukamchukua mpaka kitandani kwake, sisi tukaondoka zetu.

    Kwa vile kule hospitali kulikuwa na wanawake wengine waliokuwa wajawazito wakisubiri kujifungua, niliamuru turudi ili kufanya uharibifu wetu ambao ungewaweka pabaya wajawazito wote walikwenda kujifungua kwenye hospitali ile.



    Tulifikia mapokezi ambapo mjamzito mmoja alikuwa bado hajapewa kitanda, tulimzunguka na kuanza kumng’ong’a huku tukimgusagusa usoni na kichwani bila mwenyewe kujua kama kuna wachawi, ila akawa anapepea mikono karibu na uso wake akiamini anaguswa na mbu au wadudu wa usiku.

    Baada ya dakika kama tatu, niliamuru wachawi kusimama kisha nikamfuata na kumshika tumbo kwa kulipapasa, pale pale akaanza kujinyoganyonga, ndugu zake wakamzunguka na kumuuliza kama anajisikia vibaya tena.

    “Eee,” alijibu kwa uvivu na kuchoka sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndugu mmoja akaenda mbio kwa manesi huku wengine wakiwalaani kwamba, toka wamempeleka mgonjwa wao pale hakuna kitu kilichofanyika zaidi ya kuendelea kupeana habari za filamu za Kinaijeria.

    Mara, nesi mmoja akaja akiwa ameongozana na yule ndugu aliyewafuata, wakamchukua yule mgonjwa kwenye kitanda, lakini wakati wanakwenda mimi nikamtoa yule mama mjamzito na kubakisha kitenge chake, lakini manesi na ndugu waliendelea kujua wanamburuza yule mwanamke mjamzito.

    Mimi nilipokelewa na wachawi wenzangu huku tukiendelea kuliminyaminya tumbo lake. Tulifanya vile ili tumbo likae vibaya na kushindwa kuzaa sawasawa hivyo apigwe kisu cha upasuaji.



    Walipofika kwenye mlango wa wadi ya kuzalia, nilimrudisha kitandani, wakaingia naye maana hali yake ilikuwa mbaya sana.

    Lakini wachawi wote tukazama ndani ya ile wadi ambako kulikuwa na wajawazito wengine watatu, jumla wakawa wanne na yule tuliyekwenda naye sisi.

    Wachawi wote tukasimama pembeni na kuanza kucheza ngoma za kichawi lakini kwa kuimba nyimbo bila kuwepo kwa ngoma.

    Muda si mrefu, wakaingia wachawi wa kundi jingine, wakaungana na sisi, tukawa wengi sana mpaka manesi wakaanza kulalamika kuwa, ndani mle kuna joto AC hazifanyi kazi sawasawa.



    “Hizi AC yaani zimekufa nguvu kabisa siku hizi,” alisema nesi mmoja akiziangalia kwa macho.

    Ikawa kila mchawi anatoka kwa zamu yake na kwenda kumdandia tumboni mjamzito mmoja, kisha anarudi, anatoka mwingine.

    Kichawi, kwa kufanya hivyo pekee kunafanya tumbo la mjamzito kukaa vibaya hivyo si rahisi kuzaa salama mpango ambao sisi tulikuwa tunautaka.

    Mjamzito mmoja akapiga kelele akisema anahisi kama amewekewa jiko la mkaa lenye moto kwenye tumbo lake. Akalia sana.

    “Sasa unalia nini?” Nesi alimuuliza.



    “Kwani sisi ndiyo tuliokupa hiyo mimba, starehe yako mwenyewe unatupigia kelele sisi,” alisema nesi mwingine.

    Sisi wachawi tuliendelea na zoezi letu huku tukipongezana kwamba kazi inakwenda vizuri, mpaka saa kumi alfajiri wajawazito wote walikuwa wamepasuliwa na kutolewa watoto, kitoto kimoja kikafa kwani tulikiziba pumzi.



    ***

    Ilikuwa Jumapili iliyofuata, tukiwa ndani ya ibada kanisani, mimi nimesimama madhabahuni, akasimama mzeee mmoja bila kuruhusiwa wala kunyoosha kidole.

    Nilitupia jicho baya sana, kwani nilihisi ana kitu kuhusu mimi tu. Sikumwambia kitu, ila yeye akasema:

    “Padri ninataka kusema kitu mbele ya waumini wenzangu, mbele ya kanisa na mbele ya Mungu muumba wa mbingu na nchi.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Moyoni nilitamani sana yule mzee atokee ili akabiliane na zile tuhuma zile ambazo mimi zilinifika shingoni na niliingiwa na kinyongo na kazi ile ya kichawi ambapo awali niliambiwa hakuna ambaye angeweza kutuona wakati tukiwa kwenye matukio yetu.

    “Eee Bwana niepushe na aibu hii, sirudii tena mimi, nimeshajirekebisha,” nilisali kimoyomoyo peke yangu pale mbele ya madhabahu. Nikajikuta nakohoa pia bila sababu.

    Ghafla mzee mwingine akanyoosha kidole, wakawa wawili sasa. Lakini pia wakati yule akiendelea kuongea na vile vidole viwili vikiwa juu, mke wa yule mzee aliyekuwa akiongea naye akanyoosha kidole



    “Mbaya zaidi, watu waliotuingilia kutufanyia hivyo huwezi kuamini ukiambiwa, hii ni aibu kwa kanisa na pia ni kufa kiroho. Mungu hawezi kuuvumilia ubaya huu.”

    Wakati anazidi kubomoa, mimi haja ndogo ilinibana, nikawa navumilia tu.

    Nilitamani ardhi ipasuke, mimi niingie ndani mwake na nisionekane tena maishani mwangu. Mwili ulinitetemeka, akili ikanipotea, nikawa sijui niamue nini.

    “Hali ikiwa hivi kuna siku humu huku kanisani watu watashikania mapanga kutoana damu, hakiyanani vile.”

    Yule mzee alipomaliza kusema hayo, akaa ghafla kama vile alishikwa na kukalishwa kwa nguvu.

    Nikataka kusema muda umekwisha, lakini mzee mmoja kati ya wale walionyoosha vidole alisimama hata bila kuruhisiwa, alipoona mwenzake amekaa tu.

    “Nashukuru sana na mimi kwa kupata muda huu. Zamani uchawi hapa kanisani ulikuwa ni msemo tu, si kitu ambacho kinatingisha, lakini mimi nina habari kwamba, sasa uchawi umo ndani kabisa ya hili kanisa, tena washiriki ukitajiwa majina unaweza kubisha hadi unaanguka chini.

    “Mimi kama nitapata baraka za waumini wenzangu niko tayari nitaje majina, lakini nilindwe.”

    Nilimwangalia vizuri yule mzee nikamwona kama ametumwa, kwani wakati anaongea, hakuwa ananiangalia mimi, wala mtu mwingine, alaiinama tu huku akibwabwaja.

    “Sema.”

    “Wataje.”

    “Waweke wazi bwana.”

    “Tutajie.”

    “Tuambie.”

    Hayo yalikuwa maneno ya waumini wa kanisa lile ambayo yalinichanganya kabisa. Baadhi ya waumini wakawa wanainama kunong’onezana huku wakiniangalia kwa kuniibiaibia.

    “Niwataje?” Yule mzee aliuliza tena kwa sauti ya juu.

    “Watajeeee.”

    Wakati huo, yule mzee mwingie na yule mke wa yule wa kwanza, vidole vyao vilikuwa bado juu wakiomba nafasi ya wao kuongea.

    “Eti niwataje?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Inaonekana aliniuliza mimi kwani aliniangalia. Na hapo ndipo nilipojua kuwa, hata mimi niko ndani ya tuhuma za kutajwa kwani kama nisingekuwemo, yule muumini angeniuliza hivi, ‘eti mtumishi wa Mungu niwataje?’ sasa hakusema mtumishi kwa sababu alishajua sina cha utumishi wala uchungaji.



    “Nalinda heshima ya kanisa, siwataji, ila nawataka waache mara moja tabia hiyo,” alimaliza yule mzee na kukaa.

    Ghafla tena akasimama mzee mwingine hiku akiendelea kunyoosha kile kidole chake.

    Jamani muda naona umetuishia, siwezi kuruhusu mambo hayo, ila nitaunda kamati ya kushughulikia, matokeo yatatangazwa humu humu kanisani.



    “Lini?” Waumini walihoji kwa pamoja.

    “Eee, Jumapili ijayo.”

    “Tuhakikishie.”

    “Ha! Niwahakikishie kwani mimi ndiye mchawi?” Nilijibu kwa jabza sasa.



    “Mh!”

    “Mh!”

    “Mh!”

    Waumini waligunia chini kwa chini. Sasa sikujua waliguna kwa sababu ya majibu yangu au kwa sababu walishajua mimi ni mchawi. Hiyo iliniuma sana, lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kusema hivyo.



    Kilichonishangaza zaidi hata wale wazee wenye hekima zao katika kanisa hakuna aliyetoa sauti kuongea kitu kwa kunitetea wala kutengeneza amani.

    Nilimaliza ibada, watu wakatoka nje mmoja baada ya mwingine. Lakini kule nje wakasimama katika makundi makundi isivyo kawaida.



    Halafu wakawa wanaonekana wakiongea kwa tahadhari sana, kwani kila mara walionekana kuangalia mlango wa kuingilia kanisani na wa ofisini kwangu.

    Na mimi nilitoka nje na kuiacha ofisi tupu, nikasimama ili kuangalia nini kinaendelea kwa waumini wangu, lakini nao wakaanza kutimka mmoja mmoja.



    Hoja kwamba walinigundua mimi ilipata nguvu baada ya baadhi ya waumini kunipita tu wakati wanaondoka wakati su jambo la kawaida kwao.

    “Mama,” nilimwita muumini mmoja, akasimama. Mimi ndiyo nikamfuata aliposimamia.

    “Mama kwani kuna nini leo?” Nilimuuliza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hujui?”

    “Sijui kitu.”

    “He he! Uchawi kanisani,” alisema.

    “Sasa mbona watu wananitenga?” Nilimuuliza, lakini badala ya kunijibu akaondoka zake haraka.



    Ghafla nikasikia mlango wa ofisini kwangu ukigongwa kwa nguvu kama kuna mtu ndani, nikaenda haraka.

    Kufika nikamkuta yule mzee tuliyekwenda kuwanga naye usiku nyumbani kwa wale waumini.

    “Umefanya nini sasa? Ona yaliyokupata.” Aliniiliza kwa hasira sana.





    “Kwani kosa langu ni nini?” Nilimuuliza na mimi nikiamini sikuwa na hatia, bali yeye ndiye aliniingiza mkenge.

    “Wewe umekwenda kanisani bila kumwomba mkuu kwa sala.”

    “Mkuu gani?”



    “Kwani mkuu wako kwa sasa ni nani?”

    “SI Mungu!”

    “Ha ha ha ha! Siyo Mungu, Mungu yupi kwanza, yule wako wa zamani?”



    “Hata sasa.”

    “Amekwambia nani, hujui kama umeshasajiliwa kwa mkuu wa giza? Kuanzia siku ile pale wewe ni wa mkuu wa giza kama sisi.”



    “Oke, turudi kwenye msingi wa maongezi, kosa langu ni lipi?”

    “Kosa nimeshakwambia, leo kanisani kila mtu amekushangaa wewe kwa jinsi ulivyokuwa umevaa nguo za kulalia madhabahuni, lakini wewe mwenyewe ulidhani umevaa joho.”



    Moyo ulinilipuka lip. Nikashangaa sana huku nikijiuliza maswali mengi na kuvuta picha ya jinsi nilivyoonekana.



    Lakini mpaka hapo, nilipojiangalia mwenyewe nilikuwa nimevaa joho la utumishi, sasa hizo nguo za kulalia ni zipi!

    “Mbona nimevaa inavyotakiwa?” Nilimuuliza.

    “Ndivyo unavyojidanganya?”



    “Kh! Si hivi, kwani we hunioni?”

    Yule mzee alicheka, akaangalia chini kisha akatembeza mkono wake chini kama anafuta, ukawa na vumbi kisha akanipaka lile vumbi usoni kwangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pale pale nilipojiangalia, kweli nilionekana nimevaa pajama ya kulalia, ya chini na ya juu.



    Nilishtuka zaidi, mwili ukaingiwa na ganzi na kuanza kuhisi mshangao niliousababisha kwa waumini wangu, nikaanza kupitia maongezi ya wale waumini waliosimama kuongea wakisema hivi:

    “Mbaya zaidi, watu waliotuingilia kutufanyia hivyo huwezi kuamini ukiambiwa, hii ni aibu kwa kanisa na pia ni kufa kiroho. Mungu hawezi kuuvumilia ubaya huu.”



    “Hali ikiwa hivi kuna siku humu humu kanisani watu watashika mapanga kutoana damu, hakiyanani vile.”

    (Mzee mwingine anasimama).



    “Nashukuru sana na mimi kwa kupata muda huu. Zamani uchawi hapa kanisani ulikuwa ni msemo tu, si kitu ambacho kinatingisha, lakini mimi nina habari kwamba, sasa uchawi umo ndani kabisa ya hili kanisa, tena washiriki ukitajiwa majina unaweza kubisha hadi unaanguka chini.



    “Mimi kama nitapata baraka za waumini wenzangu niko tayari nitaje majina, lakini nilindwe.”

    “Sema.”

    “Wataje.”



    “Waweke wazi bwana.”

    “Tutajie.”

    “Tuambie.”



    “Niwataje?”

    “Watajeeee.”

    “Eti niwataje?”



    “Nalinda heshima ya kanisa, siwataji, ila nawataka waache mara moja tabia hiyo.”

    “Niachieni mimi, nitalifanyia kazi na matokeo yatatangazwa humu kanisani.”



    “Lini?”

    “Eee, Jumapili ijayo.”

    “Tuhakikishie.”



    “Ha! Niwahakikishie kwani mimi ndiye mchawi?” (Waumini wanaguna).

    “Mh!”

    “Mh!”

    “Mh!”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    (Anamwita muumini mmoja nje).

    “Mama kwani kuna nini leo?”

    “Hujui?”

    “Sijui kitu.”



    “He he! Uchawi kanisani.”

    “Sasa mbona watu wananitenga?”

    (Yule mama anaondoka haraka).



    “Oooph! Kweli nitakuwa nimeumbuka sana, sasa?” Nilimuuliza yule mzee baada ya kuwaza hayo yote yalivyokuwa kwenye ibada.

    “Hakuna cha sasa, hapa kampeni moja tu, kuhakikisha wale wote waliosimama kuuliza maswali wanakufa.”



    “Mh! Kwa njia gani. Halafu na wewe una makosa, kwanini usije kunishtua pale madhabahuni kuwa nimevaa pajama?” Nilimwambia na kumuuliza yule mzee.



    “Nilijitahidi lakini kukufikia pale mbele ikawa kazi. Unajua makanisa karibu yote yana nguvu ya Mungu mbele, huwezi kufika kirahisi. Mimi nilisimama kushoto kwako nikawa nakuangalia.”



    Tukiwa tunaongea hayo, mara mama mmoja akasimama mbele yetu, ni muumini wa kanisani lakini sikujua kama ni mchawi.

    “Leo padri umechemsha sana,” alisema akiwa amesimama mbele yetu huku akihema kwa nguvu.



    Tulimwaangalia kwa umakini sana huku tukionesha uso wa mshangao.



    “Kwani unajua chochote?” Nilimuuliza.

    “Kuhusu nini?” Naye aliuliza.

    “Kwani umesemaje wewe?”



    “Nimesema leo umechemsha sana madhabahuni kwako.”

    “Ndiyo maana nimekuuliza kwani unajua chochote?”

    “Najua, si nimekuona. Unakujaje kwenye madhabahu ya Bwana ukiwa umevaa pajama?”



    Mwili wote ulikufa ganzi tena, nikahisi roho inataka kumrudia aliyeiumba, mwili kwenda mavumbini.

    “Kwani unadhani mimi sijui kitu kuhusu wewe kujiunga na Mungu wa giza, najua.”



    Niliendelea kumkodolea macho ya mshangao.

    Yule mzee alimwangalia sana, akamuuliza.

    “Wewe upo kwenye kambi ya mzee Masomo?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo,” alijibu yule mwanamke lakini akionekana kama hana habari sana na yule mzee kuliko mimi. Akaniuliza.

    “Ni kwanini umeamua kumtumikia Mungu wa upepo?”

    “Sijamtumikia mimi,” nilimjibu kwa hasira.



    Wote, yaani yule mwanamke na yule mzee wakacheka.

    “Umechelewa sana, kama unataka kufa endeelea kusema hivyo,” yule mzee aliniambia kwa sauti ya kukazia, nikaogopa mwenyewe.



    Yule mwanamke akasimama sawasawa kisha akainama kidogo aliponyanyua shingo, akasema:

    “Padri mimi nimekuja na ujumbe wako, naamini utaupokea na utaufanyia kazi haraka sana, naomba uupokee.”



    “Ujumbe gani na umetoka kwa nani?” Nilimuuliza nikimwangalia kuuona huo ujumbe wenyewe, kama ni barua au maneno tu



    “Ni maneno tu Padri,” alisema huku yule mzee akimkazia macho.

    “Una maanisha nini?”

    “Kwani hujui?”

    “Ningejua nisingekuuliza.”

    “Ulikujaje kanisani vile?”

    “Hilo ndilo tunalolizungumza hapa.”

    “Hapa hatuzungumzi, ni kuachana na huyu, sisi tukutane usiku kwa ajili ya kupanga mikakati mizito mizito ya kuua wale wote walijidai ni vinara kwa kusimama na kusema sema ovyo,” alisema yule mzee.

    Tulikubaliana kuwa hivyo, wote tukatoweka, kwa ahadi ya kukutana usiku ili kupanga hiyo mikakati mizito ya kuua.



    ***

    Ilikuwa ni usiku wa saa sita, nikiwa nimemaliza kusali kwa Mungu wangu, sasa nausaka usingizi mwingine wa awamu ya pili.

    Nilipokuwa naanza kusinziasinzia tu, nikasikia kishindo tii!

    Nikashtuka na kuangalia mle chumbani, nikaona miguu ya watu karibia kumi, lakini niliona kuanzia miguuni hadi kwenye magoti, lakini kwa upande wa nyuma.



    Hii miguu ilikuwa minene, na ilitembea kwa mwendo wa pole kutoka pale iliposimama kuelekea ukutani.

    Halafu ghafla nikawa naona ile miguu inaongezeka katika kuonekana kwake, yaani inaonekana zaidi ya magotini na kuelekea juu hadi kwenye mapaja.

    Nikasikia sauti nzito:

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sisi ni wenzako, tumekuja, amka.”

    Niliamka polepole kitandani mpaka nikakaa, nikaangalia kulia na kushoto, wote wakajionesha moja kwa moja. Wengine niliwafahamu, wengine sikuwafahamu.

    “Simama,” yule mzee wangu alisema akiniangalia na tena akawa ananyoosha mkono kuelekea kwangu kama vile alikuwa akitaka na mimi nimpe mkono wangu ili anishike.

    Nilinyoosha mkono, nikamshika, naye akanishika, nikasimama lakini mwili ukiwa mzito sana.



    Nilipoweza kusimama vizuri mwenyewe, mwanamke mmoja akanirushia nguo nyeusi, ikanivaa mwilini, watu wakapiga makofi chumbani kwangu, nikashangaa sana kwani sikuona ni jambo la kawaida watu wengi kuwemo ndani ya chumba changu na kupiga makofi na kelele za vifijo kwa wingi.

    Yule mzee akasema wote tushikane, yaani kila mmoja aliposimama amshike mwenzake mkono, wote tukafanya hivyo, tukashikana mikono.



    Kufumba na kufumbua tukawa kwenye mti mmoja mkubwa sana, chini palikuwa na moto mkubwa uliokuwa unawaka kwa kasi huku waliouzunguka moto ule wakiwa wanacheza ngoma ya kienyeji.

    Kufika kwetu kukasababisha wasitishe ngoma na kuungana na sisi, wote tukasimama mstari mmoja.

    Tukiwa mstarini, mzee mmoja akasimama mbele na kusema kuwa, mkutano ule ulikuwa ni maalum kwa ajili ya kunisimika mimi kuwa kiongozi wa kundi mojawapo la wachawi akidai naweza.

    Nilinyoosha mkono ili kupinga, lakini wachawi wote walikataa wakisema aliyoyaongea bosi wao ni ya kweli kabisa.

    Basi, nilipitishwa mbele huku nikiwa sijui itakuwaje na wachawi wengine walinisindikiza huku wakipiga makofi kwa furaha ya mimi kusimikwa.



    “Haya, piga magoti hapa,” yule mzee aliniamuru.

    Nilipiga magoti kwa unyenyekevu wa hali ya juu huku nikishikanisha mikono kama ninavyokuwaga mbele za Mungu wangu.

    Yule mzee alinishika kichwa, pale pale mwili wote ukabadilika, nikajiona shujaa, jasiri, sina woga na wala siogopi kitu cha kufikiria au kuonekana.

    Kisha akaanza kusema maneno ya kilugha na sijui alikuwa akitumia lugha gani.



    Alitumia muda wa kama dakika tano kusema kilugha alipokuja kubadilisha, akasema Kiswahili na pale pale nikahisi nipo usingizini, nikaota ndoto.

    Nilikuwa nikipita kwenye kundi la watu nikiwa uchi wa mnyama, lakini watu walikuwa hawanioni kama napita na nikaelekea kwenye ukingo wa barabara huku nikiwa nawashika vichwa watu niliokuwa nawapita.



    Hakuna aliyejua hata kwa dalili kama kuna mchawi anapita katikati yao, hivyo nikajiona ni jasiri na mjanja kuliko wajanja wengine wote wa dunia hii ya mambo na vituko.

    Niliposhtuka kutoka katika ndoto hii, nilijiona nipo bado chini na wachawi wenzangu wakiniangalia kwa macho ya ushindi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilisimama haraka, nikasema:

    “Si muda wa kupoteza huu, wako wanaojifanya wanajua, lazima wakatoke uhai.”

    “Ndiyo,” wachawi wakaitikia.



    “Na sasa kila wote mjipange vikundi vitano, vya watu wanne wanne na kwenda kukabiliana na uovu huu, mume makini sana,” nilisema.

    “Sawa, tutakuwa makini,” walisema kwa pamoja.

    Nilipomaliza kusema, niliwachagua wachawi watatu na mimi wa nne, wengine wakachaguana hivyo hivyo, safari ya kwenda kuvamia nyumba za wale watu waliojifanya wana maswali mengi kanisani ilianza pale pale huku mimi nikiwa jasiri kabisa, siogopi mtu wala sihofii maisha yangu ya baadaye.

    “Mtakuwa mnanifuata mimi ninavyofanya, sawa jamani?” Niliwaambia watu wangu huku tukisonga mbele.

    “Sawa mkuu.”



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog