Search This Blog

JINI WA KUZIMU - 4

 





    Simulizi : Jini Wa Kuzimu

    Simulizi : Safari Ya Kuzimu

    Sehemu Ya Nne (4)





    Mama Nyamizi aliingia ndani ya gari huku
    akilia kwa kwikwi. Alijikuta akiujutia uamuzi
    wao wa kumpeleka binti yao kwa mganga wa
    kienyeji. Mzee Angu naye alikuwa akifungua
    mlango wa gari akahisi mkono wa mtu
    ukimgusa begani. Alipogeuka alipigwa na
    butwaa baada ya kumuona Dr,Kisonoko
    amesimama nyuma yake. Akajikuta
    akitetemeka kwa woga na wasiwasi wa hali ya

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    juu.
    SASA ENDELEA......
    Alijikaza kiume na kutoa kauli.
    “wewe ni nani?”
    “we una onaje?”
    “mganga amekwisha kufa. Tena nimeshuhudia
    kwa macho yangu” alisema mzee Angumbisye
    huku akiwa na wasiwasi.
    “mimi ni Dr. kisonoko”
    “sawa. Kama wewe ni Dr.kisonoko, niambie
    binti yangu yuko wapi?”
    “unataka kujua alipo mtoto wako sio?”
    “ndio”
    “nifuate ndani” alisema mganga huku
    akielekea ndani. Mzee Angumbisye alipumua
    kwa nguvu huku akitafakari cha kufanya.
    Alipiga moyo konde na kumfuata mganga.
    Alipofika ndani mganga alimtaka aje na mke
    wake. Mama nyamizi hakuwa anajua nje ya
    gari kulikuwa kunaendelea nini.
    Alichokifahamu yeye kwa wakati ule kilikuwa
    ni kutoa machozi tu. Mzee Angu alimchukua
    mke wake na kuingia nae ndani kwa mganga.
    Mama Nyamizi alipokutana na sura ya
    mganga alidondoka na kupoteza fahamu.
    # * # * #
    Kwa upande wa Mganga Ngoma moshi
    uliendelea kufuka kwenye kile chungu. Ile
    sauti iliyokuwa ikikwaruza ilisika ikiongea
    “kijana wenu anamchumba anaitwa Husna. Au
    sio?”
    “ni kweli, lakini sisi hatumkubali” Alisema
    mzee Shabani.
    “kwanini?”
    “kwasababu yupo mchumba ambaye
    tumemtafutia sisi na tunamfahamu kiundani
    kuliko huyo Husna”
    “sasa basi, ili kijana wenu apone ni lazima

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    mkubali amuoe Husna”
    “inamana hakuna njia nyingine mbadala?”
    “hiyo ni amri. Vinginevyo mnaweza
    kumchukua kijana wenu na kuondoka nae”
    “sawa mkuu tumekubali” mzee Shabani na
    mkewake walijikuta wakijibu kwa pamoja.
    “mmekubali?’
    “ndio”
    “basi kazi imekwisha. Hivyo inabidi
    tumsafirishe kijana wenu leo hii akaonane na
    wazazi wa huyo binti”.
    “sasa itawezekanaje, wakati hali yake ndiyo
    kama unavyoiona?”
    “hilo sio tatizo. Akishaondoka tu haliyake
    itakuwa nzuri, na atafika huko akiwa bukheri
    wa afya”.
    “sasa wazazi wa huyo binti wanaishi wapi?
    “KUZIMU”
    “kuzimu….! Unamaana gani mganga?”. alihoji
    mzee Shabani kwa mshangao.
    “namaanisha kuzimu sehemu wanayoishi
    mizimu na wafu”
    “haiwezekani. Kijana wangu hawezi kuoa mfu”
    “Husna sio mfu”
    “kumbe ni nani?”
    “Husna ni Jini”
    “kwahiyo kijana wangu amuoe jini?
    haiwezekani”
    “unamtaka kijana wako au humtaki?”
    “namtaka na nampenda, ndiomana sitaki aoe
    jini”
    Mzee Shabani aliendelea kuwa na msimamo,
    lakini mganga naye alijitahidi kutumia
    maneno ya kumlainisha. Alimueleza kuwa
    majini sio viumbe wabaya kwa binadamu.
    Isipokuwa watu wanashindwa kutofautisha
    kati ya majini na mashetani. Mashetani ndio
    viumbe wabaya na walioahidiwa moto na
    Mwenyezi Mungu siku ya hukumu. Lakini
    majini ni viumbe kama walivyo binadamu. Upo
    uwezekano wa kuishi pamoja pasipo kuona
    tofauti yoyote. Aliwaambia kuwa hata Yasini
    angewezaweza kumuoa Husna na kusiwe na
    tatizo lolote. Akamalizia kuwa endapo
    wangepingana na maamuzi hayo kijana wao
    angepoteza maisha.
    “mnakubali kumpoteza kijana wenu kizembe
    zembe?” Dr. Ngoma alihoji
    “hapana mtaalamu”
    “kwahiyo mnasemaje?”
    “hatuna jinsi. Tumekubali”
    “kazi imekwisha. Sasa tumuandae kijana kwa
    SAFARI YA KUZIMU”
    “kwahiyo atakwenda na usafiri gani?”
    “tunakwenda naye hadi mzimuni, hapo ndipo
    safari yake itakapoanzia” Mganga alifafanua.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Baada ya maongezi hayo ule moshi wa
    kwenye chungu uliongezeka na kusababisha
    kiza kinene kutanda mle chumbani. Hakuna
    hata mmoja aliyeweza kumuona mwenzake
    kutokana na kiza kilichokuwa kimetanda.
    Baada ya muda kidogo moshi ule unapungua
    na kiza taratiibu kinaanza kutoweka. Nuru ya
    jua inaangaza na watu wanaonana. Mazingira
    waliyokuwepo ni tofauti nay ale ya nyumbani
    kwa mganga. Walikuwa katikati ya msitu
    mnene wameketi chini ya mti mkubwa
    uliokuwa umefungwa vitambaa vyekundu
    kwenye shina.
    Dr. alifunika kile chungu kasha akaingiza
    mkono kwenye kikapu na kutoa kibuyu kidogo
    ambacho alianza kukipuliza. Kibuyu kile
    kilitoa sauti mithili ya firimbi. watu wote
    walikuwa kimya wakimuangalia mganga.
    Upepo mkali ulianza kuvuma na kuyumbisha
    miti huku na kule. Alitokea nyoka mkubwa
    sana aliyejiburuza kuelekea pale walipokuwa
    wamekaa. Mgongoni mwa nyoka kulikuwa na
    mtu amekaa mithili ya mwendesha farasi. Mtu
    Yule alikuwa ni mwanamke mweupe mno,
    nyelezake nyeupe zilining’inia hadi kwenye
    mabega, mikononi alikuwa na kucha ndefu
    kuliko kawaida, macho yake makubwa
    yaling’aa kama macho yap aka. Kiunoni
    alikuwa amejifunga shuka jekundu
    lililoburuzika hadi chini kiasi cha kutoruhusu
    miguu kuonekana.
    Nyoka aliyekuwa amembeba mtu Yule
    alisimama hatua chache kutokea pale
    walipokuwa wamekaa. Yule mtu mweupe
    aliteremka na kuwasogelea taratibu. Mganga
    na wafuasi wake walipiga magoti na
    kuinamisha vichwa vyao chini. Mtu mweupe
    alifika na kuwashika vichwa mmoja badala ya
    mwingine. alipomaliza alikwenda kwa Yasini
    na kumpaka vitu vyeusi usoni. Akafungua
    kibuyu cha mganga Ngoma na kutoa dawa
    ambazo aliwapaka mzee Shabani na
    mkewake. Dwa ile ilisemekana kuwa ilikuwa ni
    ya kuwaondoa hali ya woga.
    Baada ya hatua za shughuli za hapa na pale
    walitokea watu wafupi na weusi wengi mno.
    Watu wale walikuwa wamebeba jeneza.
    Walikwenda hadi pale chini ya mti na
    kumbeba Yasini na kumtumbukiza ndani ya
    Jeneza. Mtu mweupe alitangulia mbele na
    watu wote wakaanza kumfuata. Walifika
    sehemu iliyokuwa na shimo kama la kuzikia.
    Walitumbukiza jeneza lile na kuanza kulifukia.
    Baada ya dakika kadhaa Yasini alikuwa
    amekwishazikwa akiwa hai…
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Baada ya mazishi ya Yasini watu wote
    walirejea pale chini ya mti mkubwa isipokuwa
    wale watu wafupi walipotea palepale
    walipomaliza kufukia kaburi. Mtu mweupe
    aliwaambia kuwa walitakiwa warudi pale siku
    ya saba ili kuja kumpokea kijana wao akiwa
    mzima wa afya. Baada ya maneno yale
    alianza kuzungumza na mganga Ngoma kwa
    lugha ya kiganga kasha mtu Yule alipanda
    kwenye nyoka wake na kutoweka kwa mwendo
    wa kasi mno. Mganga alifunua chungu chake
    nacho kama kawaida kilianza kutoa moshi
    mzito uliosababisha kiza kinene.
    #*#*#
    Kwa upande wa Dr. Kisonoko Mama nyamizi
    fahamu zilimrejea. Alipofumbua macho
    alikutana uso kwa uso na Dr. Kisonoko.
    Hakuweza kuamini kilichokuwa kikiendelea
    mle ndani, mambo yote yaliyotokea aliyaona
    ni kama ndoto. Alichokuwa akikiamini ni kuwa
    binti yake pamoja na Mganga wamekufa
    kwenye maji na kuliwa na samaki wa baharini.
    Akajikuta akimuogopa na kumkumbatia mume
    wake kwa wasiwasi. Hata hivyo mganga
    alijitahidi kuwatoa hofu.
    “Hamna sababu ya kuniogopa mimi ni Dr.
    kisonoko yuleyule mnayemfahamu” alisema
    mganga.
    “Na yule aliyekufa kule baharini ni nani?”
    mzee Angumbisye alihoji.
    “ni mimi…. Lakini sikuwa nimekufa. Samaki
    aliyekula mwili wangu alikuwa ni mzimu
    ambao ndio uliniokoa na kunirudisha
    nyumbani”.
    ”kwahiyo binti yetu ndio amekwishakufa?”
    “hapana binti yenu yupo hai”
    “yuko wapi?”
    “Kwa bahati mbaya amechukuliwa na jini
    ambaye tulipanga kwenda kumuangamiza”
    “kwahiyo unampango gani?”
    “ondoeni wasiwasi. Mimi ndio Dr. Kisonoko
    hakuna linalonishinda kirahisi kama hili”
    “wacha masihara Dr. bado tunamhitaji binti
    yetu”
    “kwahiyo hamniamini au?”
    “Tunakuamini, lakini hatukuelewi”
    “najua mtanielewa. Ila tunajiandaa sasahivi
    kuelekea GAMBUSHI, huko tutaweza kufika
    kuzimu ambako Nyamizi amefichwa”. Yale
    maneno hayakuingia kabisa akilini mwa mzee
    Angumbisye. Aliyaona ni kama mchezo wa
    kuigiza. Hata hivyo alijipa moyo na
    kukubaliana na mganga kwasababu
    alimshuhudia akiliwa na samaki lakini
    anamuona mbele ya macho yake. Kwahiyo
    alitegemea muujiza mwengine ungetokea kwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    mtoto wake.
    Saa kumi na mbili asubuhi walikuwa ndani ya
    basi la AIR BUS lililokuwa likielekea mjini
    Shinyanga. Kwenye mida ya saa tano usiku
    walikuwa wamekwishaingia Shinyanga mjini.
    Safari ilikuwa ndefu sana kutokana na basi
    kubata hitilafu njiani. Walilazimika kulala
    kwenye hoteli moja maarufu mjini pale
    liyokuwa ikifahamika kama STAFF IN HOTELL
    hadi kesho yake ndipo waendelee na safari.
    Waliamka saa kumi na moja asubuhi na
    kujiandaa kwa safari ya kuelekea Gambushi
    kijiji kilichosifika kwa uchawi. Lakini
    walipotoka nje hawakuamini kilichokuwa
    kikiendelea. Walikuwa wamesimama nje ya
    hoteli moja iliyokuwepo Raskazoni mjini
    Tanga maarufu kama MKONGE HOTEL.
    “Shit…” alitamka mzee Angumbisye na
    kuelekea mapokezi. Alimkuta dada akiendelea
    na shughuli zake za kikazi akamsemesha,
    “samahani binti”
    “bila ya samahani mzee wangu”
    “hivi hii ni hotel gani na ipo mkoa gani?”
    “ni MKONGE HOTELL na hapa ni mkoani
    Tanga” msichana yula alijibu huku akuwa
    ndani ya mshangao. Maneno yale
    yalimchanganya sana mzee Angumbisye.
    Alipumua kwa nguvu huku akikuna kichwa
    asijue ni kitu gani kilikuwa kikiendelea. Aliinua
    macho na kumtazama yule dada ambaye
    alionekana bado akimshangaa.
    “kwani vipi mzee” msichana yule alihoji
    “ah….aa..h…usijali” alijibu na kuondoka
    kuelekea walipo wenzake.
    Alipofika nje aliwakuta wenzake nao bado
    wakiwa katika hali ya mshangao. Mzee
    Angumbisye aliwagutusha kwa kuwasemesha.
    “vipi Mganga ni kitu gani kinaendelea hapa?”
    “mambo ndio kama unavyoyaona” mganga
    alijibu.
    “sasa tunafanyaje?” mama Nyamizi alidakia
    “mambo ni magumu.. inabidi turudi Pangani
    tukajipange upya” mganga alijibu kwa ufupi.
    Mzee angumbisye na mkewake hawakuwa na
    la kusema kwasababu maji wamekwisha
    yavulia nguo hivyo hawana budi kuyaoga.
    Walikuwa tayari kufanya jambo lolote ambalo
    lingekuwa ni chanzo cho kupatikana kwa binti
    yao. Waliamini kuwa uwongo wa mganga ni
    nafuu kwa mgonjwa.
    Walichukua kibasi kilichowapeleka hadi stendi
    ya mabasi ambako waliingia kwenye basi la
    Rahaleo iliyokuwa ikielekea pangani. Dr.
    kisonoko alikuwa amekaa siti moja na mzee
    wa makamo. Kabla basi halijaanza safari yule
    mzee alimsemesha Dr.Kisonoko.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-
    “ kijana poleni sana kwa safari” maneno yale
    yalionekana kumkera mganga kisonoko, hivyo
    aliamua kugeuzia shingo dirishani na
    kumpuuza.
    “kijana najua upo katika wakati mgumu na
    mimi nimekuja kukusaidia” alisema yule
    kikongwe na kumfanya Dr. kisonoko kushtuka
    na kugeuza shingo kumtazama kwa makini.
    Na kujikuta akimhoji.
    “kwani wewe ni nani?”
    “mimi ni mwanakijiji wa Gambushi. Wakuu
    wamechukizwa na ujio wako na wageni pasipo
    kuwafahamisha” alisema maneno hayo na
    kukohoa kisha akameza mate na kuendelea
    kuongea.
    “hivyo basi ili wewe na wageni wako muweze
    kuingia pale inabidi mtoe kafara la kondoo
    watatu. Tena shughuli zote za kutoa kafara
    zifanyike pale hotelini mlipolala jana”
    alimaliza yule kikongwe na kushika fimbo
    yake kutaka kuondoka.
    “sasa mzee…..” Dr. alitaka kuongea kitu lakini
    alichelewa kwani yule kikongwe alitoweka
    ghafla. Akawaambia wenzake wateremke na
    kurejea hotelini walikolala. Suala lile
    lilimchukiza sana mzee Angumbisye na kutaka
    kuongea kitu kwa hasira lakini mkewake
    alimtuliza.
    Dr. aliwatuma vijana wake kwenye soko la
    Tangamano kwenda kununua kondoo wa
    kafara. Akaingia chumbani kwake kwaajili ya
    maandalizi ya kutoa kafara, lakini alichokiona
    baada ya kufungua mkoba wake wa uganga
    alitamani kufa. Vibuyu vyake vyote vya
    uganga vilikuwa vimebadilika na kuwa vifuu
    vya nazi……


    Alipokuwa akiendelea kushangaa akahisi mtu
    anamshika kwenye bega. Alipogeuka alimkuta
    yule kikongwe wa kwenye basi amesimama
    nyuma yake. Safari hii alionekana amekasirika
    sana.
    “hadi sasa mizimu imekasirika kwa kutakaka
    kupeleka binadamu wa kawaida katika himaya
    ya GAMBUSHI. Unafahamu wazi wanaofika
    kule ni wafu, wachawi,na mizimu. Au hijui
    hilo?” alihoji yule mzee kwa hasira.
    “najua babu, lakini hawa watu wana matatizo
    na huko ndiko pekee kwenye msaada” alijibu
    Dr kisonoko kwa upole.
    “sawa lakini tatizo lako ni kutokutoa taarifa
    kwa wazee”
    “basi mzee naomba msaada wako”
    “nitakusaidia. Ila kwa masharti”
    “sawa mzee wangu”
    “utakapomaliza kutoa kafara, utatangulia

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    wewe kwenda Gambusi, na wengine watakuja
    nyumayako” alizungumza yule mzee na kutoa
    kicheko kwa sauti.
    “lakini babu, zana zangu zimebadilika na
    kuwa vifuu vya nazi”
    “hilo sio tatizo. mabo yatakuwa mazuri.
    Nakutakia kazi njema” alisema mzee na
    kutoweka machoni kwa mganga. Mganga
    alipumua kwa nguvu mithili ya mtu aliyetoka
    kubeba mzigo mzito. Aliusogelea mkoba wake
    na kuufungua. Hakuyaamini macho yake,
    vibuyu vyake vilikuwa vimerudi katika hali ya
    kawaida. Alijawa na furaha isiyo kifani. Mara
    alisikia mlango unagongwa. Akafungua na
    kuwakuta vijana wake mlangoni. Walimueleza
    kuwa tayari wamekwisha leta kondoo.
    Dr aliwaita mzee Angumbisye pamoja na
    mkewake ambao muda wote huo walikuwa nje
    wakitafakari mambo yanayowatokea.
    Walipofika Dr. kisonoko alianza manjonjo yake
    ya kiganga. Aliwasha udi na kuzungumza
    maneno ya kiganga. Baada ya muda mfupi
    hali ya hewa nje ilianza kubadilika. Wingu
    nene lilitanda, radi ikiambatana na ngurumo
    zilimulika, upepo mkali ulivuma. Kutokana na
    hali hiyo watu wote waliokuwa wamepanga
    hotelini pale walijifungia vyumbani mwao.
    Hapakuwepo na hata mtu mmoja
    aliyeonekana nje ya jengo lile. Dr. kisonoko
    aliitumia nafasi ile kutoa kafara.
    Walikwenda ufukweni mwa bahari na
    kuchimba shimo lenye urefu wa kama futi
    tano. Waliwavisha wale kondoo vitambaa
    vichwani. Mmoja alifungwa kitambaa cheupe,
    wa pili kitambaa cheusi, na wa tatu kitambaa
    chekundu. Wakawatumbukiza ndani ya lile. Dr
    kisonoko alivua nguo zote na kubaki kama
    alivyozaliwa kisha akaingia kwenye shimo na
    kuwashika vichwani wale kondoo. Alianza
    kutabana kwa lugha ya kiganga. Hali ya hewa
    nayo ilizidi kuwa mbaya, mawingu yalizidi
    kuwa meusi. Ilikuwa ni saa tano asubuhi lakini
    kiza kilifanya kuonekane kama saa nane za
    usiku. Mwanga wa radi ndio uliwasaidia
    kuona walichokuwa wakikifanya.
    @*@*@
    Yasini alifumbua macho na kukumbana na
    giza nene. Hakuelewa alikuwa wapi na nini
    kilikuwa kinaendelea. Alitulia kama dakika
    tatu akijaribu kutafakari alipokuwa lakini
    hakupata jibu. Akaamua kusimaa lakini
    alishindwa kwasababu alijigonga na
    kurudisha kichwa chake. Alinyoosha mkono
    wake wa kulia lakini hakufanikiwa kwani
    alijigonga. Mkono wa kushoto nao ulikuwa
    vilevile. Hapo ndipo alipogundua kuwa alikuwa
    amelala ndani ya kitu kilichofanana na boksi.
    Alijaribu kuvuta kumbukumbu jinsi alivyoingia
    ndani ya lile boksi lakini kumbukumbu

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    hazikuja. Akanyoosha mikono yake na
    kusukuma kwa nguvu upande wa juu ya lile
    boksi, mara mwanga mkali ukampiga
    machoni. Mfuniko wa lile boksi ulifunuka
    hivyo alitoka haraka sana na kusimama
    pembeni.Loo! kumbe alikuwa amelala ndani
    ya jeneza. Macho yalimtoka mithili ya chura
    mzee. Pumzi zikamjaa na kuanza kupumua
    kwa harakaharaka.
    Sauti kali za paka zilizotokea nyuma yake
    zilimshitua na kumfanya ageuke. Walikuwa ni
    paka wengi weusi waliokuwa na macho makali
    kama tochi ya muwindaji. Wote walikuwa
    wakimkodolea macho yasini. Walinyamaza
    ghafla baada ya Yasini kuwageukia. Alitokea
    paka mmoja ambaye yeye pekeyake ndiye
    aliyekuwa na rangi nyeupe. Alitembea
    kuelekea pale alipokuwa amesimama. Yasini
    alivyogeuka nyuma lile jeneza halikuwepo.
    Hakutaka kuwaza mara mbili, alitimua mbio
    ns wale paka nao walimuunganishia na
    kumfukuza. Kila alivyojitahidi kuongeza
    mwendo paka nao waliongeza. Yasini akaona
    huo ndio ulikuwa mwisho wa maisha yake.
    Hakuweza kuamini macho yake baada ya
    kugeuka nyuma kuwaangalia wale paka.
    Hapakuwepo na hata paka mmoja. Alishindwa
    kuelewa jinsi paka wale walivyokuwa na spidi
    kushindwa kumfikia. Alipohakikisha kuwa
    amewapoteza kabisa alipunguza mwendo.
    Alikuwa amechoka sana. Akakutana na
    msichana mmoja aliyekuwa akitembea
    mwendo wa kukazana, akamuomba msada.
    “naomba unisaidie dada” aliongea Yasini
    huku akihema mfurulizo
    “vipi unatatizo gani kaka?”
    “paka”
    “Paka!... wana nini?”
    “wananikimbiza”
    “wewe ni mgeni hapa?”
    “mgeni! Kwani hapa ni wapi?” baada ya
    Yasini kuhoji swali hili, yule dada alianza
    kucheka
    kicheko cha kebehi. Alifungua pochi yake na
    kutoa kitu kama sarafu na kumkabidhi Yasini.
    “Chukua hii”
    “nini?”
    “chukua itakulinda” Yasini alinyoosha mkono
    kutaka kuchukua lakini kwa bahati mbaya
    ilidondoka chini. Wakati yasini anainama
    kutaka kuokota ile sarafu alijikuta akitamani
    kuzimia. Miguu ya yule msichana ilikuwa ni
    kwato za ng’ombe. Yasini alipoiona hali ile
    aliiacha ile pete na kutimua mbio akimuacha
    yule dada akicheka kwa sauti. Alipoona
    amtefika mbali na hakukuwa na mtu
    aliyemfuata akasimama huku akihema mara
    mbilimbili. Hakuweza kuamini kama
    amefanikiwa kumtoka yule mtu aliyekuwa na
    kwato miguuni.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/--
    Kitu kilichokuwa kikizidi kumchanganya ni
    kuwa hakuwa anajua pale alipo ni wapi.
    Mandhali yale hakuwa anayafahamu kabisa.
    Hivyo alijikuta akikosa muelekeo maalum.
    Hakuwa anajua anakoelekea wala anakotokea.
    Kwa bahati nzuri alitokea mtu na baiskeli.
    Ikambidi kuomba lifti kuelekea kule yule mtu
    alikokuwa anaelekea pengine angeweza
    kupata msaada. Yule mwendesha baiskeli
    alimpakia Yasini bila hiyana wala kinyongo.
    Yasini alitulia kwenye baiskeli utadhani
    alikuwa ana fahamu alipokuwa akielekea.
    Hakuona sababu ya kuvumilia hivyo ilimbidi
    kuhoji.
    “samahani ndugu naomba kuuliza?”
    “bila samahani kijana uliza tu”
    “hivi hapa ni wapi?”
    “kwani we umefikaje hapa?”
    “kwakweli sifahamu. Nimejikuta tu niko hapa
    na kukumbana na vituko mbalimbali. Hivi
    ninavyokwambia nimekutana na mtu ana
    kwato miguuni”
    “kwato?”
    “ndiyo, tena kwato za ng’ombe”
    “kama hizi” yule mtu aliinua miguu yake na
    kumuonesha Yasini miguu yake iliyokuwa na
    Kwato.
    kama yule msichana aliyekuwa
    anamzungumzia. Yasini hakusubiri kitu bali
    aliruka kutoka kwenye baiskeli na kutimua
    mbio. Alijiona ni mtu mwenye mkosi siku hiyo.
    Alitamani kupata msaada lakini hapakuwepo
    na mtu wa kumsaidia. Hakuwa na imani tena
    na mtu yeyote yule. Aliendelea kukimbia bila
    kujua alikokuwa anaelekea.
    Kwa bahati aliuona msikiti na watu wakiwa
    wanajitoharisha kwa kuswali. Alifika pale na
    kusimama huku akihema kama mbwa
    aliyeokoka mikononi mwa chatu. Kila mtu
    alikuwa bize kujiandaa na swala. Akawaona
    hao ndio watu pekee wa kumsaidia. Hivyo
    naye alinawa na kuingia msikitini. Baada ya
    ibada alisimama na kutoa salamu kisha
    akaongea kwa sauti.
    maneno yaliwafanya waumini wote kutulia na
    kumsikiliza kwa makini.
    “kwajina ninaitwa Yasini Shabani. Nimefika
    katika kijiji hiki pasipo kujitambua. Pili
    nimekuwa nikikumbana na mambo ya kutisha
    sana” alisema Yasini
    “mambogani ambayo anakutisha wewe?”
    alihoji mmoja wa waumini wale
    “kwakweli yanatisha mno. Naogopa hata
    kuyasimulia”
    “sasa tutakusaidiaje?”
    “hadi sasa nimeshakutana na watu wawili
    wenye kwato za ng’ombe miguuni”
    “kamahizi” wale waumini waliinua miguu yao
    iliyokuwa na kwato na kumuonesha Yasini.
    Alipotaka kukimbia mlango ulijifunga na wale
    waumini wakaanza kucheka kwa dharau.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Yasini alibaki amesimama akitetemeka kwa
    woga. Ghafla waumini waligeuka paka weusi.
    Akawakumbuka wale paka aliowakimbia muda
    mfupi uliopita. Mara yule paka mweupe
    alijitokeza na kumsogelea tena. Aliongezeka
    ukubwa kila alipopiga hatua. Hadi
    alipomkaribia Yasini alikuwa na ukubwa wa
    mbuzi lakini kichwa chake kilikuwa cha
    binadamu. Hakuwa na la kufanya zaidi ya
    kusubiria kifo. Aliwakumbuka sana wazazi
    wake, akatamani wangeshuhudia kifo chake
    lakini haikuwa hivyo alikuwa anakufa
    pekeyake. Yule paka mtu alianza kucheka kwa
    dharau kisha akamsemesha yasini.
    “unajifanya unajua kukimbia sio?..... kimbia
    sasa” alizungumza yule paka mtu...


    “siwezi kuwakimbia kwasababu siwaogopi.
    Ninamuogopa Mungu pekeyake” Yasini alijibu
    kwa
    jazba akiamini kuwa hata kama akiwa mpole
    hawezi kupona, ni lazima angekufa tu. Majibu
    ya Yasini yalimchukiza sana Paka mtu.
    “unajifanya unakiburi sio?”
    “sijui”
    “sasa subiri.....utakiona chamoto” wakati
    Yasini akisubiri hiko chamoto alichoahidiwa
    na Paka mtu, radi ilipiga na kumfanya Yasini
    kufumba macho. Alipofumbua hakuyaamini
    macho yake. Alikuwa amesimama nje ya ule
    msikiti na wale paka wote wakiwa pembeni
    wamekufa. Lakini yule paka mwenye kichwa
    cha binadamu alionekana yupo hai ingawa
    haliyake ilikuwa mbaya sana huku damu
    nyingi zilikuwa zimejaa mwilini mwake.
    Alijitutumua na kutoa kauli kwa Yasini.
    “bahati yako” baada ya maneno hayo yeye
    pamoja na wale wenzie waliokuwa wamelala
    pale chini wakatoweka. Yasini alibaki
    ameduwaa asijue nini kinaendelea maeneo
    yale. Hakuwa anajua baada ya pale
    angeelekea wapi.
    Alikuja njiwa mweupe na kutua begani mwa
    Yasini. Alipogeuza shingo kumtazama yule
    njiwa alikimbia. Alimtazama alivyokuwa
    akipaa hadi alipotua kwenye tawi la mti mrefu
    uliokuwa jirani na pale alipokuwa
    amesimama. Alishusha macho yake na
    kuangalia pande zote kuhakikisha usalama
    wake kisha akayarudisha juu ya mti
    kumuangalia tena yule njiwa. Alimuona
    msichana amesimama kwenye lile tawi
    alilokuwa ametua njiwa. Moyo ukampasuka na
    kuhisi kuwa tayari kituko kingine kilikuwa
    kikimkaribia. Lakini alipomtazama vizuri
    alibaini kuwa alikuwa ni Husna. Matumaini ya
    kuendelea kuishi yalimrejea tena kwani alijua
    jinsi Husna alivyokuwa na uwezo wa
    kupambana na vituko kama vile. Akanyoosha
    mkono na kumuita aje kumpa msaada.
    “Husna njoo mpenzi nahitaji msaada wako”
    alisema Yasini huku ameinua mkono kumtaka
    Husna ateremke. Husna aliinua mikono yake
    na kupaa hadi pale alipokuwa amesimama
    Yasini.
    “pole sana Yasini nimesikia kilio chako, upo
    salama sasa hakuna tena kitakachokusumb
    ua” alisema maneno hayo Husna huku
    amemshika Yasini mabegani.
    “samahani sana kwa kuchelewa kukupokea.
    Nilipata dharura” alisema Husna
    “kwani vipi Husna mbona sielewi
    kinachoendelea?”
    “usijali, najua huu mji huufahamu kwasababu
    hujawahi kufika. Sasa inabidi nikufahamishe
    upo
    wapi na umekuja kufanya nini” aliongea
    Husna huku akiwa bado amemshika Yasini
    mabegani. Yasini alimtazama Husna usoni na
    kisha akameza funda la mate. Alikuwa na
    hamu kubwa ya kutaka kujua kilichokuwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    kikiendelea. Husna alivuta pumzi na kuzutoa
    nje kwa nguvu.
    @*@*@
    Dr.Kisonoko alibaki ndani ya shimo kwa
    takribani nusu saa. Wakati huo maji nayo
    yalikuwa yameshaanza kuingia kutokana na
    chemchem za maji ya bahari. Alitoka na
    kuwataka vijana wake kufukia shimo
    lililokuwa na kondoo ndani yake. Vijana
    walifanya kama walivyoagizwa. Kondoo
    walikuwa wakilia sana wakitamani msaada
    likini hakuna aliyewajali. Baada ya dakika
    kadhaa walikuwa wamekwisha maliza.
    Walirudi ndani na kuelekea moja kwa moja
    chumbani kwa mganga, Dr. aliwaamuru mzee
    Angu na mkewake wakae chini na kunyoosha
    miguu. Alitoa nyembe na kuanza kuwachanja
    chale katika sehemu mbalimbali za miili yao.
    Alichukua dawa kutoka kwenye moja ya
    vibuyu vyake na kuwapaka kwenye majeraha
    aliyochanja kwa nyembe. Alifungua kibuyu
    kingine na kutoa asali iliyokuwa
    imechanganywa na dawa zake kisha
    akawarambisha wote pamoja na wasaidizi
    wake. Alikamata pembe kubwa la mnyama na
    kumuwekea mzee Angumbisye miguuni na
    kichwani akamuwekea kibuyu kikubwa
    kilichokuwa kimevishwa ngozi ya myama na
    kuzungushiwa shanga. Alianza kugongagonga
    mfuniko wa kibuyu kile huku akiongea
    maneno ya kiganga. Alipomaliza alihamia kwa
    mama Nyamizi na kufanya kama alivyofanya
    kwa mzee Angumbisye.
    Hali ya hewa huko nje tayari ilikuwa shwari
    kabisa. Radi na upepo vilikoma, na kiza pia
    kilikuwa kimetoweka. Dr.Kisonoko aliwataka
    mzee Angu na mkewake wakajiandae kwa
    safari ya kuelekea GAMBUSHI. Mganga
    akawaambia kuwa kuanzi saa ile
    hawakutakiwa kuonesha mshangao kwa
    chochote ambacho wangekiona. Na endapo
    wangevunja sharti basi wasingefanikiwa
    katika safari yao.
    Kila mmoja akilini mwake aliamini kuwa wapo
    mjini Tanga, hivyo safari yao ingeanzia
    kwenye stendi ya mkoa wa Tanga na kuelekea
    mjini Shinyanga kwa mara ya pili. Kitu cha
    kustaajabisha ni pale walipofika nje, walikuwa
    kwenye ile hoteli ya STAFF INN HOTELL ya
    mjini Shinyanga ambayo walifikia siku
    iliyopita. Kama maagizo ya mganga, hakuna
    aliyeonesha wazi kuwa hali ile imemshangaza.
    Wakaelekea kwenye kituo cha daladala
    zilizokuwa zikielekea Mchangani. Kama
    yalivyokuwa maagizo ya kikongwe, Dr.
    kisonoko alitangulia na basi la kwanza,
    wakafuatia wafuasi wake, na basi la mwisho
    walipakia mzee Angumbisye na mkewake.
    Mzee Angu na mkewake walipofika Mchangani
    walichukua vijana wawili ambao waliwapeleka
    kwa baiskeli kutokana na kukosekana kwa
    usafiri wa magari kuelekea kwenye kijiji cha
    Gambushi. Wale vijana waliwapeleka lakini
    walipofika kwenye eneo lililofahamika kama
    kikomo, wakagoma kuendelea na safari.
    Wakasema kuwa huko mbele hakukuwa mahali
    salama, kwani ni watu wachache sana ambao
    wakienda huko hurudi, wengi wao hupotelea
    hukohuko.
    Mzee Angu na mkewake walianza kupiga
    mwendo kwa miguu. Walitembea sana lakini
    hawakuona dalili yoyote ya kufika. Ilipotimia
    mida ya saa tatu usiku walikuwa wamefika
    sehemu moja iliyokuwa na mbuga. Kwakuwa
    hakukuwa na mti ambao wangepanda na
    kulala kwa usalama wakatafuta kichaka na
    kujilaza hapo huku kila mmoja akionekana
    amechoka kupita kawaida.
    Kwambali waliona kama taa za gari lilikuwa
    likielekea kule walikokuwa wao. Walishituka
    na kusimama kuhakikisha kama kweli lilikuwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    ni gari au ni macho ya mnyama. Hata hivyo
    mgurumo uliashiria wazi kuwa lilikuwa ni gari.
    Walijificha huku wakiliangalia kwa makini,
    lakini lilipofika karibu wakabaini kuwa lilikuwa
    ni basi la abiria. Hivyo walijitokeza na
    kulisimamisha. Lile basi liliposimama taa za
    ndani ziliwashwa. Hapo watu wengi waliokaa
    kama abiria walionekana vizuri jambo ambalo
    lilizidi kuwatia nguvu na kuwatoa wasiwasi
    mzee Angumbisye na mkewake mama
    Nyamizi.
    “vipi jamani mnakwenda?” ilikuwa ni sauti ya
    kijana mmoja aliyekuwa amesimama mlangoni
    kama utingo.
    “mnaelekea wapi?” mzee Angumbisye alihoji
    “Gambushi”
    “Ndio tunakwenda” alijibu mzee Angumbisye
    na kuingia kwenye basi pamoja na mke
    wake. Walipofika ndani ya basi kulikuwa
    kumebaki viti viwili tu ambavyo havikuwa
    pamoja. Kimoja kilikuwa mbele na kingine
    kilikuwa nyuma. Mzee Angu aliketi na mtu
    mmoja ambaye alikuwa ni mzee sana, wakati
    mama Nyamizi naye alikuwa amekaa na
    mwanamke ajuza. Mzee Angu alimsalimia yule
    babu kikongwe lakini hakuitikiwa. Vivyo hivyo
    kwa mama Nyamizi naye alimsalimia yule
    Ajuza lakini naye hakuitika salamu yake.
    Gari ilipoanza safari, taa za ndani zikazimwa.
    Ndani ya gari kulikuwa kimya mno.
    Hapakuwepo na mtu hata mmoja
    aliyezungumza na mwenzie. Mama Nyamizi
    na mumewake hakuna aliyepata usingizi kati
    yao. Wote walizama kwenye dimbwi la
    mawazo juu ya mtoto wao na jinsi
    atakavyookolewa kutoka kwenye mikono ya
    huyo jini hatari.
    Gari liliendelea kuchanja mbuga kwa mwendo
    wa kawaida. Ilikamata njia iliyokuwa na
    mitimiti na kuiacha mbuga. Kila waliposonga
    mbele miti iliongezeka na hatimaye wakajikuta
    wamo kwenye msitu mnene. Dereva wa gari
    alisimamisha na kuwa sha taa za ndani. Sauti
    ya utingo ilisikika ikiwataka abiria
    wakachimbe dawa. Mzee angu alipomtazama
    vizuri yule mzee aliyekaanae hakuweza
    kuamini. Alikuwa amekaa siti moja na fisi.
    Aliinuka na kujifanya anakwenda kujisaidia
    lakini alipofika kwenye siti aliyokuwa ameketi
    mke wake akazidi kuchanganyikiwa. Mkewake
    alikuwa amesinzia huku naye akiwa ameketi
    na fisi. Alitaka kumuamsha lkini yule fisi
    alimtazama usoni na kufunua mdomo wake
    kama vile anataka kumng’ata……


    Aliamua kuteremka na kumuacha mkewake amekaa na yule fisi. Alitamani asirudi ndani yagari lakini alipomkumbuka mkewake alijikuta mwenyewe anaingia.

    Mzee Angu alitupa macho kwa mkewake na kumkuta bado amesinzia, lakini yule fisi hakuwepo bali alikuwa amekaa yule mwanamke mzee. Ajuza yule alimtazama mzee angu usoni kwa macho makali kisha akamsonya. Aliporudi kwenye siti yake alimkuta yule mzee naye amebadilika na kuwa binadamu. Aliketi lakini akili haikumtulia kabisa. Mawazo yake yote yalikuwa kwa mkewake ambaye muda wote alikuwa amelala fofofo. Akili ilimtuma kumchukua mkewake na kuteremka nae. Hivyo akajikuta anapaza sauti.

    “kondaaaa?” dereva aliposikia sauti ya mzee Angumbisye aliwasha taa za ndani.

    “tushushe hapo hapo tumefika” abiria wote waligeuza shingo na kumtazama kisha kwa pamoja

    wakaguna. Mzee Angu hakujali miguno yao, alikwenda mojakwamoja hadi kwenye kiti alichokaa mkewake na kumkuta ameamka. Gari liliegeshwa chini ya mti mmoja mkubwa.

    “vipi baba Nyamizi inamana tumefika?” alihoji mama nyamizi

    “ndio”

    “lakini mbona hapa ni porini?”

    “Wacha ubishi mkewangu. Tuteremke” alisisitiza mzee Angu na kumshika mkono mkewake.

    “unadai shilingi ngapi?” alihoji mzee Angu mara baada ya kufika nje. Hata hivyo utingo wa gari

    hakujibu kitu zaidi ya kuingia kwenye gari na kuwatimulia vumbi pale chini. Mzee Angu alipumua kwa nguvu kwani hakuamini kama amefanikiwa kuwatoka wale fisi watu ndani ya gari. Lakini lile gari lilipoondoka tu ule msitu nao ukatoweka na kujikuta wamesimama palepale mbugani walipopandia gari. Hali ile iliwafanya washangae na kusahau masharti ya mganga Kisonoko. Walikuwa wamekwishachoshwa na vituko vya hapa na pale. Wakatafuta sehemu na kujilaza pale mbugani na kausingizi kakawapitia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sauti za paka ziliwagutusha kutoka usingizini. Walipoinua macho wakajikuta wamezunguukwa na kundi kubwa la paka. Paka wale walikuwa weusi na macho yao yalikuwa yanang’aa mno. Mama nyamizi akamkumbatia mumewake kwa woga. Wale paka walianza kuwazunguuka huku wakilia kwa sauti za watoto wachanga. Mara wakaungana na kutokea paka mmoja mkubwa sana. Paka yule alikuwa anatisha kuliko mnyama yoyote mkali. Alikuwa akiunguruma kwa sauti kali na nzito. Mwisho alitoa kicheko na kutoweka kwenye mazingira yale.

    Ilipofika asubuhi mama Nyamizi alimsihi mumewake warudi mjini Tanga lakini mzee yule hakuwa tayari, hivyo waliendelea na safari yao kuelekea GAMBUSHI. Waliiacha mbuga na kuingia kwenye msitu wenye miti mirefu na mikubwa. Kwa mbali waliwaona wanawake watatu wakitembea tembea mle msituni. Wanawake wale walikuwa wamejifunga kaniki tumboni na matiti yao yalikuwa wazi. Mzee Angumbisye na mkewake wakaongeza mwendo hadi walipowafikia wale wanawake.

    “ habari zenu kina mama” mzee angu aliwasalimia.

    “salama baba shikamoo”

    “marahaba”

    “mnatafuta nini kwenye msitu hatari kama huu” alihoji msichana mmoja

    “tunakwenda Gambushi”

    “Gambushi…?”

    “ndio”

    “mnakwenda kutafuta nini kwenye kijiji cha kutisha na chenye hatari?”

    “tumeongozana na mganga wetu. Lakini yeye ametangulia”

    “anaitwa nani huyo mganga wenu?”

    “ Dr. kisonoko”

    “Dr Kisonoko!... yule mganga wa Pangani?”

    “ndiye huyohuyo” mzee Angu alijibu na kuwafanya wale wanawake watazamane kwa mshangao.

    “Dr. Kisonoko pamoja na wafuasi wake wote watatu wamefariki” aliongea msichana mmoja kwa

    sauti iliyojaa masikitiko.

    “wamekufa!...?” mama Nyamizi na mumewake walihamaki.

    “ndio wamefarik, tena usiku wa kuamkia leo”

    “mungu wangu…!” mama Nyamizi alidondoka chini na kupoteza fahamu

    “kwani mna matatizo gani?”

    “tumempoteza mtoto wetu. Mganga amesema huku ndiko tunaweza kumpata kiurahisi”

    “Hakuna jambo kama hilo wazee wangu. Dr. Kisonoko hana uwezo wa kwenda kuzimu na kurudi. Alikuwa analazimisha tu, na hilo ndilo lililompoteza”.

    “ninyi hayo yote mmeyajuaje?”

    “sisi tunaishi huko”

    “sasa humu msituni mnatafuta nini”

    “tumetoroka”

    ‘kwanini?”

    “sisi ni misukule”

    “ina maana huko Gambushi wanaishi wachawi?”

    “maswali yako ni mengi mno mzee na hayana msingi. Mnachotakiwa kukijua ni namna ya kuondoka maeneo haya” alidakia mwanamke mmoja aliyeonesha kukerwa na maswali ya Mzee Angumbisye.

    “sawa tunahitaji msaada wenu”

    “hakuna wa kutatua tatizo lenu zaidi ya Mwenyezu Mungu. Rudini Nyumbani na mtafute viongozi wa dini watawasaidia” alisema yule mwanamke.

    Wakati huo mama Nyamizi alikuwa amekwishazinduka na kurejewa na fahamu hivyo aliweza kuyasikia kwa makini maneno ya wale wanawake.

    “tutawapa dawa itakayowafikisha muendako kwa usalamat” aliongea yule mama na kufungua fundo lililokuwa kwenye nchaa ya kaniki yake. Alitoa ungaunga mweusi na kumkabidhi mzee Angumbisye. Mtajipaka dawa hii usoni huku mkitaja jina la sehemu mnakokwenda. Adui akitaka kuwadhuru hataweza kuwaona hivyo mtafika kwa usalama.

    “tunaweza kujipaka sasahivi?” alihoji mzee Angumbisye.

    “ndio, fanyeni hivyo sasahivi” alisema yule mwanamke kwa msisitizo. Mzee Angu na mkewake walijipaka ile dawa usoni, lakini walipomaliza walishangaa kuona wale wanawake wakiangua kicheko huku wakigongeana mikono kuashilia hali ya ushindi.....

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Kitendo kile kiliwatia mashaka sana mzee angu na kewake, wakahisi wamenaswa na mtego wa watu wa Gambushi.

    “mnaweza kujaribu kwenda juu ya ule mti” mwanamke mwengine aliwaambia.

    Kwa wasiwasi mzee Angumbisye alimshika mkewake mkono na kutamka kama walivyoelekezwa na punde wakajikuta wapo juu ya ule mti mrefu. Walipokuwa kwenye ule mti waliweza kuona kila upande wa msitu. Kwa mbali waliweza kukiona kijiji cha Gambushi. Kulikuwa na watu wengi na wote walionekana kushughulika. Hapakuwepo na hata mmoja aliyekuwa amekaa kizembe. Pia kuna watu walikuwa wakicheza ngoma huku wakiwa uchi. Mzee Angu aliamuru warudi pale walipokuwa wale wanawake.

    “hiyo dawa ni kiboko” alisema mwanamke mmoja

    “mmeipata wapi?” alihoji mzee Angumbisye.

    “Ilidondoshwa na wachawi” mwanamke mmoja alijibu.

    Mara wakasikia sauti ya kitu kikivuma mle msituni. Kila sekunde ilipopotea ile sauti iliongezeka na kuelekea pale walipokuwa wamesimama. Wote watanao wakapaa hadi pale kwenye ule mti mkubwa. Waliweza kuona kundi kubwa la wachawi waliokuwa uchi likipaa kwa nyungo kuelekea kule msituni. Walifika kwa mwendo wa kasi na kutua pale walipokuwa wamesimama mwanzo kina mzee Angumbisye na wanawake.

    Wachawi wale walitoka kwenye nyungo zao na kuonekana kama vile wanatafuta kitu. Walizunguka kila upande lakini walionekana kukosa walichokuwa wakikitafuta. Mchawi moja alisimama na kuangalia juu ya ule mti mrefu waliokuwa wamekaa wakina mzee Angumbisye na wale wanawake watatu. Alitazama kwa muda mrefu na kutingisha kichwa kama vile kuna kitu amekiona. Akapanda ungo wake na kupaa kuelekea juu ya ule mti.

    “mungu wangu tumekwisha!” alihamaki mzee Angumbisye

    “shiiiii!!” mwanamke mmoja akamnyamazisha.

    Mzee Angumbisye alipomtazama mchawi yule alibaini kuwa tayari amewaona. Mchawi yule alifika na kutua kwenye lilelile tawi walilokuwa wamesimama. Taratiibu akaanza kuwasogelea. Mwanamke mmoja akawaonya mzee Angumbisye na mkewake wasizungumze wala kutikisika. Mchawi alifika na kumshika mzee Angumbisye begani na kumuegemea kama vile ameegemea tawi la mti.mzee Angumbisye alipomtazama kwa makini akabaini kuwa anamfahamu vizuri sana yule mchawi. Walikuwa wanaishi naye mtaa mmoja Muheza.

    Yule mchawi alipuliza firimbi na mara wale wachawi wengine nao wakaanza kupaa kuelekea kule kwenye ule mti. Walifika na kuuzunguka mti ule mara kadhaa kabla ya kutua kwenye matawi. Walikuwa ni wengi mno kiasi cha kuonekana kama ndenge aina ya kwereakwerea. Mama nyamizi alikuwa amemkumbatia mama mmoja kati ya wale wanawake watatu. Alikuwa akitetemeka na kijasho chembamba kikimvuja. Alianza kuujutia uamuzi wao wa kumpeleka binti yao kwa mganga wa kienyeji. Wale wachawi walikuwa wanamtishia mno, kila alipomtazama yule aliyemuegemea mumewake alizidi kuchanganyikiwa.

    @*@*@

    Yasini alimeza funda la mate na kumtazama Husna usoni. Alikuwa na hamu kubwa ya kutaka kufahamu kilichokuwa kikiendelea. Husna nae alivuta pumzi kwa nguvu na kuzitoa

    “Yasini hapa ulipo ni KUZIMU”

    “kuzimu!.. sasa mimi nafanya nini hapa Kuzimu?”

    “umekuja kwa lengo la kuwaona wazazi wangu”

    “inamaana wazazi wako wanaishi kuzimu?”

    “ndio”

    “kwanini?”

    “ndiko kwetu”. Husna alijibu na kumfnya Yasini kubaki ameduwaa.

    Aliinua macho yake na kumtazama tena Husna kwa makini. Kiukweli ni kwamba alikuwa akimpenda sana lakini matendo yake ndiyo yaliyokuwa yakimchanganya. Hata hivyo alikumbuka kuwa yaleyale matendo ya ajabu ya Husna ndiyo yaliyomfanya amalize elimu yake ya sekondari. Hivyo hakuona sababu ya kumchukia binti yule.

    Husna alimshika Yasini mkono wa kushoto na kuanza kupaa nae angani kama tai huku Husna akiwa amenyoosha mkono wake wa kushoto juu. Baada ya dakika kadhaa alinyoosha mkono kuelekea chini na kusababisha waanze kutua. Walitua nje ya nyumba kubwa sana iliyokuwa na geti jeusi. Walipofika tu geti lilifunguliwa na msichana.

    “karibu Yasini. Hapa ndipo ninapoishi” alisema Husna.

    “ahsante sana” Yasini aliitikia na kuingia ndani. Lakini alipomtazama kwa makini yule msichana aliyewafungulia geti, akabaini kuwa alikuwa akimfahamu vizuri sana. Alisimama na kutaka mkumsemesha lakini Husna alimkatisha na kumvuta mkono kuelekea ndani. Walifika na kuketi sebuleni. Pale alipokuwa amekaa Yasini, aliweza kuona milango ya vyumba vyote vya ile nyumba.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yule msichana aliyefungua geti alifika na vinywaji na kuwakaribisha Husna na Yasini. Yasini alikuwa akimtazama sana yule binti. Alionekana amechoka sana kutokana na kazi ngumu alizokuwa akizifanya. Yasini akataka kuuliza kitu lakini Husna aliweka kidole mdomoni kumuonya asiongee kitu. Yule msichana akatoka nje na kuwaacha Husna na Yasini pale sebleni. Lakini baada ya dakika kadhaa alirejea tena.

    “dada maji ya kuoga tayari” sauti ya yule binti ilisikika na kumfanya yasini kuzidi kuwa na uhakika wa kumfahamu.

    “twende tukakoge mpenzi” alisema Husna na kumshika mkono Yasini kuelekea bafuni. Baada ya kumaliza, Husna alimtia yasini mgongoni na kumpeleka chumbani ambapo alifika na kumuweka kitandani. Baada ya kumfuta maji, alifungua kabati na kutoa shati na suruali. Kama mtoto mdogo Yasini alivishwa zile nguo.

    “Husna hao wazazi wako wakowapi?” Yasini alihoji huku akimtazama Husna ambaye alikuwa akichana nywele....



    Huasna aligeuka na kuketi pale kitandani na yasini.

    “Sikiliza mpenzi, wazazi wangu wanaishi kwenye nyumba nyingine mbali na hapa”

    “inamaana hapa unaishi pekeyako?”

    “ndiyo, hii ni nyumba yangu, lakini tukifunga ndoa tutakwenda kuishi pamoja Duniani” Yasini alitulia na kutazama huku na kule mle chumbani. Hakuweza kuamini kama Husna angeweza kumiliki nyumba ya kifahari kama ile. Ghafla akapata wazo la kuuliza juu ya yule msichana aliyekuwa akiwahudumia tangu wamefika.

    “hivi huyu msichana anayetuhudumia ni nani?”

    “wacha maswali ya mtego bwanaaa. Inamana humjui Nyamizi wewe?”

    “Nyamizi!.... sasa hapa anafanya nini?”

    “ni kijakazi wangu”

    “kwanini sasa unafanya vitu vya kinyama kama hivi?”

    “Wamenianza, namimi nimewamaliza”

    “inamaana hukuwa na njia nyingine ya kufanya hadi umeamua hivi”

    “vipi, unampenda sana mchumbaako?” Husna alihoji kwa hasira kidogo

    “hata kama, lakini huu sio ubinadamu”

    “sikiliza Yasini. Hawa walitaka kuniua lakini nimewawahi. Hii ni adhabu ndogo sana niliyowachagulia”

    “inamaana sio suala la kutaka kuolewa na mimi?”

    “hilo lilikwisha malizika. Lakini wakajipendekeza kwangu”

    “wako wangapi?”

    “wako wawili lakini mwenzie yupo kwa wazazi wangu anawatumikia huko”

    “na yeye ni nani?”

    “yeye ni msaidizi wa mganga aliyetaka kuniua”

    Husna alimueleza Yasini kuwa kichaa alichokipata Nyamizi siku ya harusi kilikuwa kimesababishwa na yeye. Alisema kuwa baada ya kumsababishia yale wazazi wake wakampeleka kwa mganga wa kienyeji. Mganga alipomaliza kumponya, akataka kuja kupambana naye, lakini Husna alipata taarifa zile kupita kwa wazazi wake ambao walikuwa na uwezo kuliko yeye. Husna aliwafuata na kuanza kupambananao lakini kwa bahati mbaya mganga alifanikiwa kukimbia na kuwaacha wenzake. Hapo ndipo alipoamua kumchukua Nyamizi pamoja na msaidizi mmoja wa mganga na kuwapeleka Kuzimu kuwa vijakazi.

    “kwahiyo nilipoingia hapa hakunifahamu?”

    “kwanini asikufahamu wakti wewe ni mumewake. Ameniogopa mimi lakini angekusemesha”

    “kwanini anakuogopa?”

    “kwasababu ni adui yake”

    “inaonekana unamtesa sana?”

    “zaidi ya sana. Tena anastaili kifo na sio hii niliyompa”

    “mnh!”

    “vipi mbona unagumia?”

    “ah! Hamna kitu”.

    walibaki chumbani hadi mida ya saa mbili za usiku ndipo walipotoka na kukuta Nyamizi amekwishaandaa chakula cha usiku.

    “Karibu chakula mpenzi wangu”

    “ahsante sana mkewangu” alijibu Yasini na kufanya wote kutabasamu. Walikula huku wakiongea hili na lile. Walipomaliza hawakutaka kupoteza muda, walirudi chumbani kujipumnzisha.

    “Husna” Yasini aliita

    “sema mpenzi”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “unaweza kunipa siri ya maisha yako?”

    “siri gani?”

    “najua wewe sio binadamu wa kawaida. Nataka kujua ni kwanini upo tofauti”

    “mbona una haraka sana. Mimi nipo na utanijua tu”

    “naomba nikujue sasahivi” alisema Yasini.

    Husna alimtazama yasini kwa kitambo kisha akaanza kumwagika. Alimueleza kuwa yeye ni binadamu wa kawaida kama walivyo binadamu wengine. Alisema yeye ni mtoto wa mwisho katika familia yenye watoto watatu. Kipindi mama yake anaujauzito wake, baba yake alimtishia kumuua yeye na mtoto endapo angemzalia mtoto wa kike. Kwa bahati mbaya ama nzuri mama yake alijifungua mtoto wa kike. Alipoona vile alimchukua mtoto na kwenda kumficha kwenye msitu mmoja uliofahamika kama msitu wa Mauaji ulioko kwenye kijiji cha Mkanyageni. Mtoto yule aliokotwa na majini ambao walikwenda naye kuzimu na kumlea. Mtoto huyoakapewa jina la Husna.

    “na huyo Husna ndio mimi”

    “kwahiyo unawafahamu wazazi wako?”

    “hapana, hadi leo sijawajua. Na ndiomaana huwa napenda sana kuja duniani”

    “na kule Kidutani ulikuwa unafuata nini?”

    “kule ni kama njia. Kupitia kwenye lile bwawa ni rahisi sana kufika Duniani na kurudi Kuzimu”

    “sasa umepata wapi uwezo wa kufanya mambo yasiyo ya kawaida kwa binadamu?” Yasini alihoji.

    Husna badala ya kujibu swali, aliinua mkono wake wa kushoto na kumuonesha yasini vidole vyake. Kwenye kidole cha kati kulikuwa na pete ya Shaba. Yasini aliikumbuka ile pete kipindi yupo mwanafunzi na jinsi ilivyomsaidia kumaliza masomo yake.

    “hii pete nimepewa na majini walionilea. Ninaweza kufanya jambo lolote kwa kuiamrisha”

    “pole sana Husna. Lakini wasamehe wazazi wako”

    “nimeshawasamehe na ndiomana nawatafuta nikaishi nao duniani” aliongea Husna na kujikuta akilia kwa kwikwi. Yasini alimbembeleza na kumtaka alale apumzishe mawazo. Hadi kufikia saa tano usiku wote walikuwa wamekwishalala fofofo.

    Yasini alishituliwa na ubaridi mkali uliokuwa ukitembea mwilini mwake. Alipoinua macho alimkuta mtu mnene aliyekuwa anawakawaka mwilini mwake. Mtu yule alisogea nyuma hatua kadhaa baada ya kubaini kuwa Yasini ameamka. Mtu yule alikuwa akitoa nje ulimi wake mrefu ambao ulikuwa ukiwaka moto. Macho yake matatu yaliyokuwa yakiwaka kama tochi hayakufumba hata kwa sekunde moja. Yasini alitaka kumuamsha Husna lakini akabaini kuwa alikuwa pekeyake, Husna hakuwepo kitandani.......

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog