Search This Blog

JINI WA KUZIMU - 3

 





    Simulizi : Jini Wa Kuzimu

    Simulizi : Safari Ya Kuzimu

    Sehemu Ya Tatu (3)



    ILIPOISHIA JANA....

    Alipokuwa akiendelea kushangaa ile damu, alishitukia anapigwa makofi na mtu ambaye hakumuona. Watu walikuja na kumzunguuka wakimshangaa akilia kwa uchungu ambao wao hawakujua umesababishwa na nini. Hapakuwepo na hata mmoja ambaye aliiona ile damu iliyokuwa ikitoka kwenye kile kisiki. Walishangaa kuona mikono ya Yasini ikikakamaa na kupinda. Sauti ilikata na kudondoka chini kama gunia la chumvi.

    SASA ENDELEA.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wenzake walimbeba na kumkimbiza katika zahanati ya shule.

    Daktari alitoa huduma zote lakini Yasini hakupata ahueni zaidi ya kuongezeka kwa maumivu. Ingawa alikuwa na fahamu zake lakini hakuweza kutoa kauli yoyote wala kujisogeza. Daktari alivyoona mambo ni magumu walimhamishia hospitali ya Teule. Hata walivyofika huko mambo bado yalikuwa ni magumu. Yasini hakupata ahuweni yoyote. Mikono ilizidi kupinda na kusababisha maumivu makali mwilini.

    Akiwa kwenye kitanda cha hospitali alimuona Husna akimsogelea huku akiwa amekasirika mithili ya nyati aliyemuona binadamu kwa mara ya kwanza. Alimtazama Yasini kwa sekunde kadhaa kisha akasonya.

    “ naona sasa umeanza kuwa na kiburi, si ndio?” Husna alihoji, lakini Yasini hakuwa na uwezo wa kujibu chochote kutokana na ile hali aliyokuwanayo. Alimsogelea na kumshika kichwani. Baada ya kitendo kile Yasini alikuwa na uwezo wa kuzungumza ingawa hali yake ilikuwa bado si nzuri.

    “Yasini, leo ni lini ?”

    “jumanne”

    “nilikwambia nini?”

    “nisifanye kazi siku ya jumanne”

    “na umefanya nini?”

    “samahani Husna, nilikuwa namsaidia yule mgonjwa”

    “ Wewe na yeye nani ni mgojwa?”

    “naomba unisamehe Husna, sitorudia Tena”

    “umenifadhaisha sana Yasini. Siwezi kukusamehe”

    “no! Husna usifanye hivyo nateseka sana mwenzio”

    “najua unateseka, na hata mimi nataka uteseke hivyohivyo ili uwe na adabu”

    “sitarudia tena naomba unisamehe Husna”

    “ok, hilo ni onyo. Endapo ukirudia kitakachokupata tusijekutafutana”Aliongea Husna na kutoweka katika yale maeneo ya hospitali.

    Baada ya dakika kama mbili tangu Husna kutoweka, Yasini alirudi katika hali yake ya kawaida. Wakati daktari ana kuja kumtazama alishangaa kumkuta amekaa kitako kwenye kitanda. Alivuta pumzi na kuzitoa kwa nguvu. Kisha akasema.

    “Allahu akbaru….. vpi kijana unaendeleaje”

    “niko safi Dr. Mimi siumwi”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ nimekuja kukupa dawa naomba unywe ili tuongee”

    “dawa za nini wakati nimekwambia siumwi”

    “sikiliza kijana, umeletwa hapa hujitambui. Sasa ukisema huumwi unakosea”

    “dokta, nilikuwa naumwa lakini sasa nimepona”

    “huwezi kupona bila dawa. Kijana”

    “dawa mlizonipa ndizo zimenisaidia”

    “ok. Ngoja nikachukue vipimo. Ili nijue nini cha kufanya”

    Daktari alitoka na kwenda kuchukua vipimo, lakini aliporejea Yasini alikuwa amekwishatoroka maeneo yale. Daktari alitoka nje na kuanganza kila upande lakini hakumuona. Alikata tamaa na kurudi kutoa huduma kwa wagonjwa wengine.

    Pigo alilolipata Yasini lilimfanya kuwa makini siku za jumanne. Siku hiyo hakufanya kitu kingine chochote ambacho kingemtoa jasho zaidi ya kwenda darasani na kula tu. Baadhi ya wanafunzi walianza kumchukulia kijana yule kuwa ni mshirikina. Wengine walikuwa wakimuogopa, na wengine walimuonea huruma wakidai kuwa alikuwa amerogwa kwasababu alikuwa anapendwa sana na watu. Hata hivyo yeye mwenyewe hakujali maneno ya watu, alifanya kile alichotakiwa kukifanya.

    Wanafunzi pamoja na walimu wote walimzoea Yasini. Waliamini kuwa alikuwa na matatizo ambayo yangemkuta endapo tu angejaribu kufanya kazi siku za jumanne. Hivyo siku hiyo hakuna mtu aliyeonekana kumsumbua kwa lolote. Yeye mwenyewe alijisikia faraja sana kwa jambo lile kueleweka kwa kila mtu na hata wale waliomtenga wakiamini kuwa alikuwa ni mchawi. Lakini nani aliyemwambia asifanye kazi siku ile ilikuwa ni siri yake.

    * * *

    Yasini alifanikiwa kumaliza masomo yake na kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne. Siku alipokuwa anaondoka shule mwalimu mkuu alimkabidhi kiasi cha shilingi laki tatu na nusu (350,000/=) pesa ambazo zilibaki katika zile alizopewa na wadhamini kwaajili ya matumizi.Yasini alichukua pikipiki iliyompeleka hadi kijijinikwao Mkanyageni. Alipofika maeneo ya nyumbani kwao alishangaa sana, alikuta bwawa kubwa limeenea kwenye eneo lililokuwa na nyumba yao. Hakuweza kuelewa yale maji yalikotokea wapi hadi kuweza kufunika nyumba nyingi kiasi kile. Aliweka begi lake chini na mikono akaibandika kichwani. Hakuelewa kama wazazi wake walikuwa hai au wamefariki kutokana na yale maji. Alikuwa hajui aanzie wapi ama afanye nini. Mara aligutushwa na sauti ya mtu ikimsalimia,

    “hujambo mjukuu wangu?” ilikuwa ni sauti ya ajuza.

    “sijambo bibi, shikamoo”

    “marahaba mjukuu wangu, unasubiri nini hapa?”

    “bibi mimi ninatoka shule. Nimefika hapa nimekuta nyumba yetu imemezwa na maji”

    “mjukuu wangu hapa plikuwa na mwamba, ndani ya huo mwamba kulikua na maji, na kwenye hayo maji kulikuwa na nyoka mkubwa. Sasa mwamba umepasuka na kusababisha hili bwawa. Watu wengi wamekufa, na kupoteza mali zao nyingi.”

    “unamaanisha hata wazazi wangu wamefariki?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “baba yako anaitwa nani?”

    “mzee Shabani”

    “familia ya mzee Shabani ilinusurika”

    “kwahiyo wako wapi kwa sasa?”

    “wanaishi Muheza.”

    “unaweza kufahamu ni maeneo gani pale muheza?”

    “inasemekana anakaa Kimara”

    “ahsante sana bibi”

    “ondoka haraka hapa sio mahali pazuri. Pamekuwa ni makazi ya majini na mashetani”

    Aliongea ajuza yule na kuondoka. Yasini alichukua begi lake na kuelekea kituo cha basi ambako alipanda basi hadi muheza. Alipoteremka Kimara aliongoza mojamkwa moja hadi kwenye nyumba iliyokuwa karibu na kituo cha basi. Lengo lake ni kuulizia mahali anapoishi wazazi wake. Mlango wa ile nyumba ulipofunguliwa alikutana na sura ya mama yake. Bila kuuliza alimrukia na kumkumbatia. Kila mmoja alikuwa na furaha ya kuonana na mwenzie baada ya muda mrefu kupita pasipo kuonana.

    “mama ni wewe?” yasini alihoji kama vile hakuamini macho yake.

    “ni mimi mwanangu, karibu sana” alisema mama Jumbe na kuchukua begi la Yasini na kuliingiza ndani. Yasini alipofika sebleni alijikuta akishangaa na kuzunguusha shingo kama pia. Hakuweza kuamini kama pale ni nyumbani kwao au wamehifadhiwa kwa muda. Kulikuwa na mazingira tofauti na alivyoyaacha kule nyumbani kwao mkanyageni siku alipokuwa anakwenda shule. Sebule ilikuwa imeenea na kukamilika kila kitu kilicho stahili kuwa katika sebule ya watu wenye maisha mazuri.

    Mama Jumbe alirejea na kukaa na mwanae wakitakiana habari. Yasini alimtazama mama yake usoni kwa sekunde kadhaa kisha akavunja ukimya,

    “mama”

    “mwanagu”

    “imekuwaje?”

    “mwanangu yaliyotukuta ni makubwa….. siku moja sote tulikuwa tumetoka. Tuliporudi tukakuta maji yamejaa kwenye mtaa wetu,nyumba yetu ilikuwa imezama kiasi cha kuonekana bati tu”.

    “kwahiyo watu walikufa?”

    “watu wengi walipoteza maisha. Waliopona ni wachache mno”. Mama Jumbe aliongea maneno hayo huku akibubujikwa na machozi.

    “basi usilie mama. Enhe ikawaje?”

    “baba yako alikwenda kuomba msaada kwa rafiki yake waliokuwa wakifanya nae kazi, kwa bahati yule mhindi alikuwa anarudi kwao India, hivyo akatuachia nyumba yake na kila kitu unachokiona. Yeye amesema hatorudi tena Tanzania” alizungumza mama Jumbe.

    Yasini alpotaka kujua alipo baba yake pamoja na kaka yake Jumbe. Alipata habari za kufurahisha ambazo hakuweza kuamini. Mzee shabani alikuwa amepata kazi kwenye mamlaka ya usindikaji magunia. Kumbe suala hilo nalo pia lilichangia kubadilisha maisha ya pale nyumbani. Jambo jengine lililomfurahisha Yasini ni kusikia kuwa kaka yake Jumbe naye alikua akisomea ufundi makanika.

    * * *

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Matokeo ya mtihani wa Yasini hayakuwa mazuri sana, hivyo hakuweza kuendelea na masomo ya kidato cha tano. Alichukua mafunzo ya udereva ambayo mwisho wa siku alikabidhiwa TAX na mzee Mwaifurile ambaye alikuwa akiishi jirani na wao. Mzee huyo alihitaji kuletewa shilingi elfu ishirini tu kwa siku. Yasini aliweza kupeleka kiasi hicho cha pesa kutokana na wateja kuwa wengi. Kwa siku aliweza kukusanya zaidi ya shilingi elfu hamsini.

    Ilikuwa ni mida ya saa mbili asubuhi. Kama kawaida ya Yasini aliwasha gari kuelekea kwenye kituo cha basi ambako ndiko kulikokuwa na kijiwe chake. Alipofika maeneo ya Msangazi kwa mbali alimuona msichana amesimama barabarani kama vile alikuwa akisubiri usafiri. Alikuwa ni msichana mrembo sana na aliyevalia mavazi yaliyomfanya apendeze zaidi. Yasini alipomuona alisimamisha gari pasipo kusimamishwa. Alipomtazama vizuri alibaini kuwa alikuwa anamfahamu. Hakuwa mwengine bali ni Husna....



    “vipi Husna unakwenda wapi?”

    “nilikuwa naelekea nyumbani kwenu”

    “twende basi”

    “Mimi ninashida na wewe, tayayari tumeshaonana. Nyumbani kwenu kwa nini tena?”

    “haya niambie ulikuwa unasemaje?”

    “nataka unipeleke mjini”

    “pesa yako tu, hata kama ukitaka mbinguni nitakupeleka”

    “usijali we twende tu”

    Walianza safari ya kuelekea Tanga mjini. Yasini alikanyaga mafuta na kumfanya atambae kama nyoka juu ya barabara ya lami, breki ya kwanza ilikuwa Pongwe kwenye kituo cha mafuta. Yasini aliteremka na kuongeza damu kwenye usafiri wake. Alirudi na kujiweka kwenye usukani. Alimtazama Husna kupitia pembe ya jicho lake la kushoto. Kama jicho lingekuwa linatoboa basi sikuhiyo jicho la Yasini lingemtoboa Husna.

    Alipokuwa akiendelea na safari, alitafakari mambo mengi sana.kiukweli nikwamba alivutiwa sana na urembo wa Husna, lakini kila alipokumbuka vituko vya mama huyo alijikuta akikata tamaa ya kufungua ukurasa wa mapenzi. Alivunja ukimya na kuamua kuzungumza,

    “hivi Husna wazazi wako bado wanaishi Mkurumuzi?”

    “vipi unataka kuja kunitolea posa nini?”

    “ah! Kwani kuna ubayagani nikifahamu unapoishi?

    “ok. mimi naishi kwa shangazi yangu KIDUTANI. wazazi wangu wamehamia Zanzibar”

    “mambo si hayo bwana” Yasini alisema na kukanyaga mafuta.

    Kwenye mida ya saa tatu asubuhi walikuwa wamekwishaingia Tanga mjini. Walipinda kushoto na kukamata barabara iendayo Bombo. Baada ya dakika kadhaa walikuwa nje ya hoteli ya IN BAY THE SEA HOTEL. Ni hoteli iliyokuwa ufukweni mwa bahari. Yasini alipaki gari na kuhoji kabla Husna hajateremka

    “kwahiyo mama nikufuate saa ngapi?”

    “acha masihara Yasini, hembu ambatana na mimi bwanaaa”

    Waliteremka na kwenda kukaa kwenye kibanda kimoja kilichokuwepo ufukweni. Mhudumu alipowafuata waliagiza juisi. Walipokuwa pale ufukweni Yasini alijikuta akichanganyikiwa kila alipomtazama Husna. Mara alikumbuka vituko alivyomfanyiwa kipindi alipokuwa mwanafunzi, lakini aliamua kupotezea na kujifanya kama hakumbuki kitu chochote. potelea mbali…. nzi kufia kwenye kidonda si haramu. Hiyo ndiyo kauli aliyoitamka moyoni mwake, akaamua kujitosa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “unajua Husna ni bahati sana kutolewa out na mrembo kama wewe” alisema Yasini na kumeza mate.

    “wacha utani Yasini…. Inamaana huwaoni warembo hadi hilo jina uniite mimi?”

    “sawa, lakini moyo wangu umekuchagua wewe”

    “umenichagua kivipi, mbona sikuelewi”

    “nakupenda Husna, natamani tuoane”

    “wacha utani bwana”

    “sio utani Husna. Yaliyomo yamo”

    Husna alihema kwa nguvu, na kuinamisha kichwa chini kwa sekunde kadhaa. Alipoinua shingo alimuomba Yasini afumbe macho. Alifungua pochi yake na kutoa ua jekundu. Alimkabidhi Yasini mkononi kisha akamuamuru afumbue macho. Yasini hakuweza kuamini kilichokuwepo mbele yake. Sasa alianza GBkupata hisia kuwa kumbe hata Husna alikuwa anamkubali. Wote kwa pamoja walijikuta wakielea kwenye kisiwa cha mahaba.

    Ilipofika mida ya saa kumi jioni walianza safari ya kurudi Muheza. Walipofika Mkanyageni Yasini alipinda kulia na kukamata barabara iendayo Kidutani. walipofika maeneo ya ziwani, Husna alimuomba Yasni amshushe maeneo yaleyale. Kwakweli sehemu ile ilikuwa inatisha mno. Kulikuwa ni porini na kunazizima mno kwa upweke....





    Yasni alimsihi kumpeleka hadi nyumbani kwao lakini hakukubaliana na swala lile. Alidai kuwa shangazi yake alikuwa ni mkali mno, hivyo akimuona anarudishwa kwa Tax atamfokea. Yasini alisimamisha gari maeneo yale ya ziwani na kumshusha Husna, kisha yeye aligeuza na kuelekea Muheza.

    * * *

    Ndani ya miezi sita tangu Yasini na Husna kuanzisha uhusiano wa kimapenzi, Kila mmoja alikuwa amekolea kwa mwenzake. Mapenzi yao yalikuwa yamepamba moto. Hawakuona sababu ya kuchelewa hivyo wakaamua kuvishana pete ya uchumba ili wapate kufunga ndoa mapema iwezekanavyo.

    Siku moja Yasini alipotoka kazini, aliitwa na baba yake Mzee Shabani kwaajili ya maongezi. Mzee shabani alimueleza Yasini kuwa amempatia mchumba ambaye alimuona kuwa anafaa kuolewa na kijana wake. Yasini alimwambia baba yake kuwa tayari alikuwa na mchumba wake ambaye alipanga kufunga nae ndoa. Mzee shabani alionekana kutofurahishwa na habari za Yasini. Hivyo alimlazimisha kufanya kile ambacho yeye kama baba yake anakitaka. Yasini nae alionekana kushikilia msimamo wake wa kumuoa Husna.

    Mwisho mzee Shabani alitaka kujua asili ya huyo msichana ambaye anaonekana kumzuzua kijana wake. Alipoambiwa kuwa asili ya Husna ni Zanzibar, hasira zilimzidi. Hakutaka kabisa kijana wake kwenda kuoa visiwani akiamini kuwa maadili yao yalikuwa hayaendani. Mbaya zaidi Yasini alishindwa kueleza historia ya mchumbawake kwa mzee Shabani. Hivyo mzee Shabani alitoa angalizo kwa kijana wake kuwa endapo ataendelea kung’ang’ania suala la kumuoa Husna na kumkataa Nyamizi litakalomkuta asije kulalamika. Hadi wanamaliza kikao Yasini alikuwa hakufikia muafaka na wazazi wake, hivyo alipewa muda wa kufikiria kwa makini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilipita wiki moja tangu Yasini alipopewa muda wa kujifikiria ili aweze kufanya maamuzi yaliyo sahihi. Suala hilo lilikuwa likimchanganya sana, asjue aamue lipi. Akiwa kijiweni akisubiria wateja, alijipumzisha ndani ya gari huku akiwaza na kuwazua hatma ya mapenzi yake yeye na Husna. Mara alisikia sauti ya Husna ikimuongelesha.

    “baba, ukilala na biashara nayo hulala”

    “ahaa, bibie huyo, karibu”

    “vipi mbona umelala?”

    “ah, uchovu tu”

    “amka basi nimekuja na habari njema” alisema Husna huku akiingia ndani ya gari. Yasini naye alijiinua na kujilaza mapajani mwa Husna na kumuangalia usoni. Husna alimwambia Yasini kuwa wazazi wake wanataka wamuone. Taarifa ile ilmshtusha kidogo Yasini na kujikuta amepigwa na butwaa kwa sekunde kadhaa. Husna aliigundua ile hali ya mpenzi wake, lakini alipotaka kujua kilichokuwa kikiendelea, Yasini alimficha na kujifanya yupo kawaida.

    Hata hivyo Yasini aliiona ile ni nafasi pekee ya kuwathibitishia wazai wake kuwa alikuwa akimpenda sana Husna kuliko yule msichana waliyekuwa wakimtaka wao. Yasini alimuomba waende nyumbani kwao kwanza kabla ya kwenda kwa wazazi wa Husna. Kwakuwa kila mmoja alikuwa na hamu ya kuishi na mwenzie kama mke na mume, Husna alikubali kwenda nyumbani kwa wazazi wa wasini siku ileile waliyokutana.

    Yasini na Husna walifika nyumbani kwa mzee Shabani, lakini mapokezi waliyoyapata yalikuwa ni ya kukatisha tamaa. Mzee Shabani alimtimua Husna mithili ya paka mwizi. Mama jumbe na Yasini walijaribu kumsihi lakini Hakutaka kusikiliza la mtu. Husna alijikuta akibubujikwa na machozi na kulia kama mtoto. Yasini alimchukua na kuondoka nae bila kuzungumza kitu.

    Walipofika njiani Husna alitaka kujua kama Yasini alikuwa na msimamo wa kumuoa yeye au Nyamizi msichana ambaye amechaguliwa na wazazi wake. Yasini alimhakikishia kuwa alikuwa tayari kutengwa na familia yake lakini sio kumuacha Husna na kumuoa mwanamke mwengine. Lakini Husna alimuomba akubaliane na wazazi wake,, jambo ambalo hakutaka kulisikia hata kidogo.

    Husna alimuhakikishia Yasini kuwa angefanya juu chini ilimradi afunge ndoa na yeye, lakini ili waweze kufanikiwa ni lizima kwanza Yasini akubaliane na mawazo ya wazazi wake. Lakini yasini hakukubali kumuunga mkono kwa maneno hayo. Akasema kuwa alikuwa tayari kupoteza hata maisha kuliko kumuoa mtu ambaye hakuwa chaguo lake.

    “kukubaliana na mawazo ya baba yako haimaanishi kwamba ndo utamuoa. Ila hiyo ndiyo njia pekee itakayoweza kutusaidia” alisema Husna

    “kivipi?”

    “hilo niachie mimi, chamsingi ni wewe kukubali maneno ya wazazi wako. Nakuahidi nitafanya juu chini kuhakikisha kuwa humuoi mtu mwingine yeyote zaidi ya mimi”

    “sikuelewi Husna”

    “Yasini inamaana umenisahau? Hembu kumbuka miaka michache iliyopita”

    “sawa, mimi nimekuelewa lakini usije ukaniangusha mpenzi”

    “mimi ndio Husna bwana, hakuna linalonishinda hapa duniani. Au we unanionaje?”

    “nakuaminia mpenzi”. Baada ya maongezi hayo machache walikumbatiana na kila mmoja akiwa na matumaini ya kuishi na mwenzake kwa ghalama yoyote.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    * * *

    Maandalizi ya harusi ya Yasini na Nyamizi yalifanyika haraka iwezekanavyo. Ilibidi harusi ile kufungwa haraka ilivyowezekana ili kumuwahi Yasini asije kubadilisha wazo la kumuoa binti huyo. Wazazi wa pande zote mbili walionekana kuzama kwenye dimbwi la furaha na shamrashamra za vijana wao kufunga ndoa.

    Tangu Yasini alipoachana na Husna siku ambayo mzee Shabani alivyowatimua nyumbani kwake hadi siku ya ndoa ya Yasini na Nyamizi walikuwa hawajawahi kuonana tena. Yasini alianza kupoteza matumaini ya kuwa na Husna. Hakuelewa ni kwanini Husna alimshawishi kufunga ndoa na Nyamizi msichana ambaye hakuwa amempenda hata kidogo. Usaliti wa Husna ulianza kumuumiza Yasini. Alijikuta akijilaumu kukubaliana na mawazo yake. Hata hivyo aliendelea kujipa moyo.

    Zilikuwa zimebakia dakika chache tu za Yasini na Nyamizi kuwa mke na mume. Shekhe alikuwa amekwishafika tayari kwa kufungisha ndoa.kila mtu alijaribu kuonesha furaha yake. Aliyekuwa na huzuni ni Yasini pekeyake. Shekhe alikunja goti huku ameshikilia kitabu chake tayari kwa kufungisha ndoa. Mzee Angumbisye pamoja na Yasini nao walikunja goti moja huku wamepeana mkono. Watu walitulia kimya wakimsikiliza Shekhe aliyekuwa akifungisha ndoa…





    Kelele za mtu aliyekuwa akilia kwa sauti zilisikika kutokea ndani. Kelele hizo hazikuwa za mtu mwingine bali ni Nyamizi. Alilia huku akiwapiga ngumi watu waliojaribu kumsogelea. Maneno aliyokuwa akiropoka hakuna aliyemuelewa.Baada ya dakika kadhaa alianza kuvua nguo na kutaka kukimbia. Kwa bahati nzuri walitokea wanaume kadhaa na kumuangusha chini walifanikiwa kumfunga kamba za miguu na mikono. Wakampakia kwenye gari na kumkimbiza Hospitali.

    Kwa takribani wiki nzima Nyamizi alitibiwa lakini hakuwa amepata ahuweni hata kidogo. Kila kulipokucha hali yake ilizidi kuwa mbaya.Mzee Angumbisye alikuwa amechanganyikiwa kutokana na hali ya binti yake. Hakujua la kufanya juu ya hali ile. Alikata tamaa kabisa ya kumuona tena mtotowake katika hali ya kawaida. Kila alipokaa alijikuta machozi yakimtiririka mithili ya maji ya bomba.

    Mzee kasiani alitoa wazo la kumpeleka Nyamizi kwa waganga wa kienyeji. Alisema kuwa Pangani kulikuwa na mganga hodari asiyeshindwa na kitu. Kwakuwa hali ya Nyamizi haikuwa nzuri watu wote walikubaliana kumpeleka mototo wao huko Pangani pengine kungeweza kuwa na uzima. Hawakutaka kuchelewa, siku hiyohiyo walimtoa Hospitali na kumsafirisha hadi pangani kwa Dr. Kisonoko

    “karibuni sana” ilikuwa ni sauti ya Dr. kisonoko

    “ahsante mtaalamu” mzee Kasiani alijibu

    “nimewaona tokea mlipokuwa nyumbani. Tatizo lenu ni kubwa sana….. tena sana” Dr. Kisonoko aliongea huku akiunguruma kama samba.

    “mtoto wenu anaitwa Nyamizi, au sio?” mganga alihoji

    “tawile mganga”

    “binti yenu ana Jini la kipemba, Lakini hapa mmefika mimi ndio Dr. Kisonoko. Nitamchoma moto huyo Jini huku mkishuhudia”

    “tawile mganga”

    “mtakaa hapa siku saba, tukiendelea kumpatia tiba Binti yenu. Sawaaaaa” Dr. Kisonoko aliongea na kuunguruma tena.

    # * # * #

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nyumbani kwa mzee Shabani nako mambo yalianza kuwa magumu. Yasini hakuwa sawa kiafya, alikuwa hajijui wala hajitambui. Muda wote mate yalikuwa yakimtoka kutokana na mdomo wake kukataa kufumba. Pamoja na kumpeleka hospitali lakini hali yake haikubadilika na kurejea ya awali. Alikuwa chizi si chizi, mzima si mzima, mzimu si mzimu, yaani alionekana mtu wa ajabu. Mama Jumbe alikuwa akilia kila alipomtazama mtoto wake huyo ambaye alikuwa ni kipenzi cha moyo wake.

    Mzee Shabani akiwa usingizini alioteshwa kuwa kulikuwa na mganga wa jadi ambaye ndiye pekee mwenye uwezo wa kumtibu kijana wao. Mganga huyo alikuwa akipatikana Bagamoyo. Aliambiwa kuwa mganga huyo alikuwa akiitwa Dr. Ngoma. Pamoja na maelezo yote hayo alionywa kumpeleka kijana wake Pangani kwa mganga Kisonoko, na kama angefanya hivyo basi angempoteza kabisa.

    Kulipokucha Mzee Shabani alimueleza mkewake juu ya ile ndoto aliyoiota. Mkewake alimshauri wafanye hivyo kwani pengine hao walikuwa ni malaika wa Mungu ndio wamemuotesha. Walijipanga na kuanza safari ya kuelekea bagamoyo kumtafuta huyo mganga aliyefahamika kwa jina la Dr.Ngoma ili aweze kumpatia tiba kijana wao.

    Kama Mzee Shabani alivyooteshwa kwenye ndoto, ni kweli yule mganga aliuwepo Bagamoyo. Hawakupata shida sana kipata nyumba ya mganga huyo kutokana na umaarufu aliokuwa nao pale mjini. Walipouliza tu walipelekwa hadi kwa mganga. Walimkuta akiwa ameketi kwenye kibanda kilichokuwa kimejengwa kwa matope.

    “Ehee, habari za boma wandugu?” Dr. Ngoma aliwasabahi

    “sio nzuri mtaalamu” mama jumbe alijibu kwa sauti ya upole na yenye huruma.

    Dr, Ngoma alichukua kipande cha kioo kilichokuwa kimefungwafungwa kwa vitambaa vyilivyokuwa na rangi tatu, ambazo ni nyeusi, nyeupe, na nyekendu. Akachukua kibuyu kikubwa kilichokuwa kimefungwafungwa shanga nyingi shingoni. Alimimina vitu vyeusi vilivyofanana na mkaa uliopondwapondw

    a. Alipakaza unga ule kwenye kioo na kuanza kukichungua huku akikigeuzageuza.

    “mnh. Kazi ipo” mganaga Ngoma alijisemesha na kuendelea kukichunguli kile kioo kwa umakini mkubwa.

    “wakuru, kuna uwezekano wa kijana wenu kupona”

    “tutashukuru baba” alisema mama Jumbe

    “lakini……”

    “lakini nini mganga?”

    “pia kuna uwezekano wakijana wenu kuto kupona” mganga alisema kwa sauti yake nzito......



    “Mungu wangu! Tusaidie mtaalamu” mama jumbe alisema

    “ninaweza kuwasaidia, lakini masharti ni magumu mno”

    “masharti gani mtaalamu? We twambie tupo tayari kwa lolote” alisema mzee Shabani kwa kujiamini.

    “Mpo tayari?” mganga alihoji.

    “ilimradi kijana wetu arudi katika hali yake ya kawaida” mzee Shabani alijibu

    “kama kweli mtamudu masharti,basi kijana wenu atakuwa ameshapona. Lakini vinginevyo mtampoteza kabisaaa” alisema mganga Ngoma maneno ambayo yalizidi kuwachanganya mzee Shabani na mkewake. Mganga Ngoma alichukua chungu kikubwa kilichokuwa kimefungwa matambaa meupe na mekundu huku kikiwa kimeviriringishwa shanga za rangi nyingi. Baada ya kufungua mfuniko wa kile chungu, moshi mweusi ulianza kufoka kutokea ndani ya chungu na sauti nzito, nene na yenye kukwaruza ilisikika kutokea humo.

    # * # * #

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa upande wa Dr. Kisonoko nako mambo yalikuwa moto. zilikuwa zimepita siku tatu tu tangu Nyamizi alivyopelekwa pale kwa mganga. Kutokana na tiba alizokuwa akipata haliyake ilikuwa inaridhisha kiasi. Hakuwa anapiga tena mayowe na kutaka kukimbia. Tunaweza kusema kuwa alikuwa amepona kabisa ukilinganisha na siku alivyopelekwa. Hivyo kilichokuwa kikisubiriwa ni kumalizia matibabu yake ndani ya siku saba walizokuwa wamepewa na Mganga. Siku hiyo ndiyo siku ambayo Dr.Kisonoko alipanga kwenda kumuangamiza Jini aliyekuwa akimsumbua Nyamizi, huku watu wote wakishuhudia kifo cha adui yao.

    Safari ya kwenda kisiwani kupambana na jini ilianza. Wote walitoka ndani kinyumenyume. Nyamizi alikuwa amebeba ungo uliokuwa na mkate, ndizi, tende, halua, wali, bisi, karanga, vitumbua, pamoja na vipande vya nyama ya kondoo iliyochomwa. Walipofika nje walikamata njia ya kuelekea baharini. Mbele alitangulia mfuasi mmoja wa mganga, akafuatiwa na Nyamizi, mama Jumbe, na mzee Angubisye. Nyuma ya mzee Angumbisye walifuata wafuasi watatu, na mwisho kabisa alimalizia Dr. Kisonoko.

    Hawakupata tabu kufika baharini kwasababu mbaramwezi ilikuwa ikiwaka sana. Kwa bahati walikuta ngarawa za wavuvi ufukweni. Wakachukua tatu ambazo moja alipanda mfuasi mmoja wa mganga, mzee Angumbisye, pamoja na mama Jumbe. Ngarawa nyingine walipanda wafuasi wawili wa mganga, na ile ya tatu walipanda Dr.ngoma, Nyamizi, na mfuasi mmoja wa mganga. Walipiga makasia kuelekea kwenye kisiwa cha Njuguni.

    Kulikuwa kumebakia kama kilometa tatu tu kukifikia kisiwani. Kisiwa kilikuwa kikionekana kimetulia mno, na hapakuwepo na dalili yoyote ya kuwepo kwa binadamu maeneo yale. Kila walivyosonga mbele hali ya hewa ilibadilika. Bahari ilianza kuchafuka kutokana na mawimbi makubwa yaliyosukumwa na upepo mkali. Ngarawa zilisukumwa huku na kule mara zilipopigwa na mawimbi. Dr. kisonoko alishika pembe la mnyama mkono mmoja na mkono mwingine alikamatia kibuyu. Alianza kuongea kwa sauti huku akifokeana na mtu ambaye hakuna aliyemuona wala kumsikia. Kila alivyozidi kufoka ndivyo upepo nao ulivyozidi kuvuma kwa kishindo.

    Wimbi kubwa lilikuja na kuifunika ngarawa ya Dr. kisonoko. Hali ilipotulia walishituka sana baada ya kuiona ile ngarawa ikielea tupu. Walipigwa na bumbuazi wasiamini kilichokuwa kikiendelea mbele ya macho yao. Mara waliuona mwili wa mganga ukiwa umekatwa vipande viwili ukielea juu ya maji huku damu zimetapakaa maeneo yale. Alitokea samaki mkubwa na kuchukua kipande kimoja cha ule mwili. Baada ya sekunde kadhaa yule samaki alirudia kile kipande kilichobaki na kutoweka nacho.

    Mzee Angumbisye na mkewake walikuwa wamechanganyikiwa wasijue mtoto wao alikuwa wapi. Lakini kwa asilimia kubwa waliamini kuwa binti yao alikuwa ameshapoteza maisha. Msaidizi mmoja wa mganga alitoa ushauri wa kurudi nchi kavu, lakini mzee Angumbisye alipinga wazo lile.

    “wewe unawazimu?..... tuondoke pasipokujua hatma ya mtoto wangu?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “lakini mzee hali yenyewe ndio kama unavyoiona, tukiendelea kubaki hapa hata sisi tunaweza kupoteza maisha”

    “potelea mbali, mbona mtoto wangu amekufa”

    “sawa mzee. Sisi ngoja tuondoke” alisema mfuasi wa mganga na kuanza kupiga makasia kurejea ufukweni. Mzee Angumbisye alijikuta roho inamuuma sana. Wakati wote huo mama Jumbe alikuwa amepoteza fahamu. Lakini walipofika ufukweni fahamu zilikuwa zimekwisha kumrejea. Vilio na huzuni vilikuwa vimewatawala Mzee Angu na mkewake. Walianza safari kuelekea kwa nyumbani kwa mganga ambako wangechukua usafiri wao na kurejea Muheza.

    Mama Nyamizi aliingia ndani ya gari huku akilia kwa kwikwi. Alijikuta akiujutia uamuzi wao wa kumpeleka binti yao kwa mganga wa kienyeji. Mzee Angu naye alikuwa akifungua mlango wa gari akahisi mkono wa mtu ukimgusa begani. Alipogeuka alipigwa na butwaa baada ya kumuona Dr,Kisonoko amesimama nyuma yake. Akajikuta akitetemeka kwa woga na wasiwasi wa hali ya juu…



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog