Search This Blog

JINI ZAITUNI - 3

 





    Simulizi : Jini Zaituni

    Sehemu Ya Tatu (3)



    "Sikia Zaka Mimi siwezi nikawa nakutafutia msingi mzuri wa Maisha alafu wewe unawawazia hao rafiki zako ambao hata kula hawakupi angalia usiwe na masikio ya kenge mpaka yavuje damu ndiyo usikie shauri yako."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Jamani Zai yaishe basi sirudii tena kusema hivyo mchumba wangu nitafuata kile unachosema"





    "Kweli bosi hilo nalo neno maana sikufikiria kabisa si unajua mambo mengi bosi wangu."



    "Ooh! Kumbe, lakini haujaniibia ila umenizidishia hizi" nilimpatia zile sarafu akapokea kwa bashasha mno



    "Ahsante sana bosi wangu ubarikiwe si unaelewa wateja ni wengi sasa najisahau kabisa" ndipo na Mimi niliona nimeutua mzigo mahali sahihi kabisa lakini sikufurahishwa na tabia yake ya wizi kwa wateja kama alivyofanya kwangu na ndiyo maana watu wengi hawaendelei kwasababu ya manung'uniko Ya watu juu ya pesa zao walizotafuta kwa jasho alafu wao wanaiba kirahisi kabisa.



    Nilifika nyumbani kwangu nikiwa hoi kama niliyefanya kazi nzito ya kubeba zege. Nilipoingia ndani nilisimama mlangoni macho nikiwa nimeyatoa kama nipo kwenye kiza kinene sikuamini nilichokiona nikaanza kupikinya macho lakini nilichokiona ni kile kile nikaamua kufunga macho ilinione kama hali itabadilika lakini haikuwa hivyo



    Ndani kulikuwa kumeenea vyombo vipya kabisa na chupa kubwa ya chai na vyombo vyangu vya zamani sikuviona mhali nilipovitunza hapo awali,ndani mlikuwa mmependeza yaani mpaka Mimi mwenyewe nikajisikia aibu nilivyo kuwa mchafu hapo awali kwani wakati mwingine nilipitisha hata siku tatu au nne bila kusafisha ndani.



    Cha kwanza nilisogea kwenye chupa ya chai nikaitikisa, ilikuwa imejaa pomoni nikachukua lesi lesi zangu nakuanza kutuliza mashetani ya tumboni mwangu.



    Nilipokuwa nakaribia kumaliza kupata kifungua kinywa nilisikia mlango unabishwa hodi niliporuhusu aingie hakuwa mwingine ila Zai, siku hii alikuwa amependeza mno akiwa katika gauni lililodariziwa safi siyo siri alinivutia kama ndiyo nimemuona siku hii.



    Alinitazama kwa furaha na Mimi sikutaka nijioneshe ushamba wangu niliinuka na kwenda kumkumbatia pale alipo. Joto la wastani lilipenya katika maungio ya mwili wangu nikapata msisimko na hamasa ya kupata ile kitu roho inapenda lakini nilijizuia sana zile hisia zilizoamka mpaka nikafanikiwa kuzituliza.



    Niligundua nimeanza kuwa na hisia nae tena Kali kuliko za awali,alipoinua macho yake yakakutana na yangu ana kwa ana ila Zai aliwahi kuinama halooo! Hapo nikapata somo lingine kuwa hakuna mkate mgumu mbele ya chai.



    Nilimshukuru mno kwa vyombo na shuka ambalo sikuwahi kuliona hata katika matangazo yanayooneshwa ya hoteli nzuri.



    Nilitoka ndani nikaelekea maliwatoni, nilipokuwa humo nilisikia sauti inaniita



    "Zaka, zaka, Zaka " ilikuwa sauti ya mvuvi mwenzangu



    Aliingia ndani baada ya kuona kimya kimezidi,alifungua mlango uliokuwa wazi akajitoma ndani alipoingia akaona mtu amelala kitandani akajua ni Mimi Zaka akawa amesogea mpaka kitandani akaanza kumtikisa hakujua kuwa ni Zai aliyekuwa amelala pale alizidi kumtikisa akiita lakini alistushwa na weupe wa miguu na pingili zilizojaa vyema, aliposogea kuangalia tena alishangaa zaidi kuona nywele zikiwa zimeishia mabegani looh! Alichanganyikiwa akaamua kutoka akijua amemchungulia shemeji yake.



    Nilitoka maliwatoni nikakutana na jamaa yangu huyu aliyekuwa na wasi wasi

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Zaka vipi mbona nimebisha hodi upo kimya"



    "Samahani bro si unaelewa tena nilikuwa katika starehe hivyo siyo rahisi kuitikia." Nilimjibu nikitabasamu



    "Alaaa! Ila ni kweli ile starehe haihitaji bugudha"



    "Kweli kabisa, unaonekana una wasi wasi kulikoni bwana kaka?" Nilimtupia swali la uchokozi nifahamu nini kinamsibu



    "Bwana mdogo ni hatarii si nimeingia kwa pupa ndani nikakutana na mtoto mkali"



    "Mmmh! acha kunitania bro" niliguna na kumuuliza tena ili nipate uhakika kama amemuona Zai



    "Aaaah! Bwana Zaka nitakutaniaje wakati nimemshuhudia kwa macho yangu,hivi ni kweli umeoa?"



    "Bado bwana ni dada mmoja ametoka kwa baba yangu mdogo alifika Leo na ataondoka hii leo"

    Niliamua kumdanganya ili nisiwe nimekiuka masharti niliyopewa hapo mwanzo



    "Sasa Zaka uwe unanitaarifu maana Mimi ni kama ndugu kwako alafu sijamuona sura kama mnafanana"



    "Heee! Kwani alikuwa macho au?" Nilistuka kuona alitaka kumuona mpaka sura



    "Hamna bwana Zaka alikuwa amelala nikajaribu kumuamsha lakini hakuamka"



    "Duh! Amechoka mno na safari maana ilikuwa ndefu mno"



    "Sawa lakini yule mtoto angekuwa wako sijui"



    "Aaaaah! Acha mbwembwe zako bwana ingekuwaje kwani" nilimuuliza nijue amekusudia kusema nini



    "Aiseee! Yuko bomba yaaani kama shombe shombe hivi ila wewe domo zito utawezea wapi watoto wa humu tu wanakutoa nduki"



    "Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Kweli bhana mimi ni bado mmasai sina swaga nitawaweza wapi maji marefu hao" niliongeza utani ili ajue naamanisha kweli lakini ukweli ulibakia moyoni mwangu japo nilitamani kumwambia kuwa yule ni wangu



    "Basi bwana mimi naona nikuache tutaonana baadae japo umetususa kazini"



    "Sijawasusa bro nitakuja maana nimebanwa na wageni tu hawa" alikubali akapanda baiskeli yake akawa ametokomea barabarani



    Nilirudi ndani, nilipoingia Zai hakuwepo niliangaza lakini sikumuona nikawa nimesimama kwa muda nikijiuliza ameenda wapi nikapata wazo la kumuita, niliita sana lakini hakutokea nikaamua kujitupa kitandani.



    Zai alikuwa amesimama pembeni ya barabara kama anasubiria gari apate lifti lakini haikuwa hivyo kwa ambaye angepata fursa ya kumuona alivyojawa na hasira, kwa mbali alionekana yule mvuvi mwenzangu ambaye alikuja nyumbani mda si mrefu alikuwa akielekea upande ule ule aliopo Zai.........



    Alikuwa akiendesha kwa mwendo mkali mno kutokana na mteremko ule, alivyokuwa anazidi kuteremka ghafla upepo ulianza taratibu na hatimaye ukazidi kuwa upepo mkali uliokusanya vumbi na kufanya kama kimbunga, baiskeli ilianza kuyumba kushoto kulia huku yeye akifumba macho kutokana na vumbi hilo japo hakupoteza uelekeo kama Zai alivyotarajia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zai alizidi kujawa na hasira mithili ya mbogo aliyejeruhiwa kwasababu yule rafiki yangu hakupoteza muelekeo kwani alitumia akili nyingi kuliko nguvu, Zai aliamua kusogea kabisa barabarani akiwa anamtazama vizuri yule mvuvi anavyokuja na baiskeli yake kwa kasi na alipomkaribia Zai pale alipo Zai alimpisha kidogo akawa amepita ilihali hakutambua kama kuna mtu eneo hilo tena anaetaka kumfanyia ubaya.



    Zai alipomkwepa yule mvuvi alisimama nyuma kisha akanyoosha mkono wake uliotoa upepo mkali zaidi kuliko wa awali ambao ulimsukuma mvuvi mpaka pembeni ya barabara ambako palionekana kisiki cha mti uliokatwa



    breki nazo zikiwa zinasaliti amri yake nao usukani ukagoma kabisa kukunja kona hakika ule msemo wa "siku ya kufa nyani miti huteleza" ndiyo ulikuwa unaenda kumpata rafiki yangu huyu. Hakuwa na ujanja zaidi ya Kuvamia kile kisiki kwa nguvu,kishindo kikubwa kilisikika pembeni ya barabara hiyo iliyokuwa na watu wachache.



    Zai alisogea pale alipoangukia mvuvi mwenzangu akimsaili kwa macho kama bado ni mzima, alitabasamu baada ya kumsikia akikoroma kwa maumivu aliyopata bila hata ya kufumbua macho. Watu wachache walianza kusogea eneo la tukio Zai hakuona umuhimu wa kujua kinachojiri zaidi ya kutoweka eneo hilo.



    Kila mtu aliongea lake wengine walidai alikuwa amelewa ndiyo maana amepata ajali, wengine walisema ni upepo umemchanganya na wachache walielezea kimbunga kilivyotokea wakihusisha sana na imani za kishirikina.



    Nilikuwa nimepitiwa na usingizi mzito ambao uliisha ghafla baada ya kusikia sauti ya mvumo wa upepo mkali, nilipoamka niangalie kulikoni nilipokelewa na mawimbi ya ziwa hali iliyonifanya nigutuke toka pale nilipo nikasimama wima.



    nikajaribu kuvuta kumbukumbu Mara ya mwisho nilikuwa wapi nikafanikiwa kukumbuka kuwa nilikuwa nimelala ndani, nikajiuliza swali nimefikaje fikaje hapa na kabla sijapata jibu sauti ya Zai ilisikika akicheka mno.



    "Zaka haujaacha tu uoga wako huo?"

    Aliniuliza huku akicheka



    "Yaani kama ningekuwa na moyo mwepesi sasa hivi ningezirai."



    "Kwa hali hiyo uliyonayo ni halali,unatetemeka mpaka meno mwanaume wewe."



    "Kawaida tu, sasa mimi sielewi nimefikaje huku?" Nilimuuliza nikiwa nimemkazia macho



    "Niliona si vyema kukuamsha katika usingizi ule mzito hivyo nikakuchukua tu" alijibu kirahisi mno kuliko hata nilivyofikiria, hakuchukulia uzito wowote jambo hilo



    "Sikia nikwambie Zai haya mambo mengine unayofanya utakuja kuniua bure alafu kwanini usiniamshe taratibu ningekuelewa mbona?"



    "Mmmh! Kwahiyo unataka kuniambia kuwa hujapendezwa na hilo?"



    "Ndiyo kwani wewe unaona ni mazuri haya unayofanya,sijui kama angekuwa binadamu mwenzangu ningempa adhabu gani?" Niliongea kwa jazba na kujiamini mpaka nikaogopa ule ujasiri nilionao



    "Zaka nimeshakuelewa na sitarudia makosa. Nilifanya hayo yote kuonesha ni jinsi gani nakuthamini na kukupenda."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Siku nyingine ujifikirie kabla haujachukua maamuzi" niligeukia pembeni nikampa mgongo na ukimya ukapita kidogo ni kama sehemu hiyo haikuwa na watu



    Nilianza kuisikia sauti ya mtu kama anamafua anavuta kamasi haikuchukua mda kilisikika kilio cha kwikwi hapo nikajua nimmetibua Zai, niligeuza shingo yangu upesi kuelekea kule alipo loooh! Zai alikuwa amelowa kwa machozi afadhali na mfiwa msibani. Nilimuonea huruma kutokana na muonekano alionao japo sikujua machozi yake yaliishia katika gauni lake au la kwani chini hayakuonekana.



    Nilimfuata taratibu mpaka nikamfikia cha kwanza nilitoa kitambaa mfukoni nakufuta machozi yaliyokuwa yakichirizika kama maji bombani huku nikimchombeza taratibu



    "Umechukia nini Zai wangu au nimesema vibaya, na kama ni hivyo kwanini usiniambie mama kuliko kuanza kulia, usinifanyie hivyo mwenzio ni hasira tu mahabuba wangu tafadhali nyamaza nipo hapa kwaajili yako"

    Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kumrudisha katika hali yake ya kawaida



    "Zaka imetosha Mimi naona kabisa hizo ni dalili za kunichoka na unanitesa kisa nakupenda kweli kwanini eeh! Kwanini lakini unanifanyia hivi?"



    "Zai usikasirike mpenzi wangu kwani sikuwa na jinsi vile vile sikuweza kuzidhibiti hasira zangu, nakiri kosa kwako nisamehe."



    "Zaka unafahamu kabisa ninavyokupigania kila kukicha kwasababu ya penzi lako Zaka lakini Leo unaniona sifai kweli ni haki hiyo?" Nilijua kinachofuata atakasirika kabisa alafu nigeuzwe nyama ya buchani nikaona nianze kujihami mapema kabla hayajatokea mengine



    "Zai wewe kwangu ni zaidi ya usingizi na wewe ndiyo kila kitu kwangu ni kheri ni kose vyote lakini si kukupoteza wewe hilo utambue na kosa moja siyo kosa mpenzi wangu ila kurudia kosa" Zai alitoa tabasamu hafifu



    "Huwa unafanya makusudi ili ujue kama Zai huwa analia sasa ipo siku yako wewe nichezee hivyo hi yo."



    Nilicheka kwa kauli aliyoitoa huku nikimpiga busu katika paji la uso kisha nikamkumbatia kabisa



    "Zai wewe ndiyo furaha yangu. Ukicheka nami nitacheka na ukilia nami nitalia vile vile"



    "Nashukuru Zaka kwa kuupokea moyo wangu kwani ni kweli kabisa unastahili kunipa raha niliyoingoja kipindi kirefu mno"



    "Usijali Zai wewe ni wangu tu na hakuna atake tutenganisha" niliongeza maneno huku nikizidi kumkumbatia barabara



    "Zaka haya mazingira umevutiwa nayo"



    "Ndiyo ni mazuri mno tena sana tu" nilisifia eneo lile lilikuwa linapendeza kwa mtazamaji yeyote na tangu niwe mvuvi sikuwahi kufika eneo hilo



    "Zaka nataka utambue kuwa nimekuleta hapa ili ujumuike namimi hii furaha niliyonayo isiyokuwa na kifani"



    "Mmmh! Umefurahishwa na nini Zai wangu?" Nilimuuliza nikiwa namgeukia ili nisikie vyema alichofurahishwa nacho

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hahaaaa! Ni mjinga mmoja hivi amejitia kimbele mbele nimemkomesha"



    "Mmh! Yupi huyo kajipendekeza kwako Zai wangu?" Niliuliza kwa shauku mno nikiwa nataka kujua



    "Si yule rafiki yako aliyekuja Leo."



    Nilibaki hoi, machozi yakaanza kunilenga lenga.....



    "Zai umemfanyia nini mtoto wa watu?"

    Nilimuuliza kwa unyonge

    "Nimempa onyo tu wala hajaumia sana na hivi ninavyoongea atakuwa hospitalini bila kukosea"

    "Alifanya nini mpaka umtendee kitendo cha kinyama namna hiyo?" Nilizidi kumuuliza kwa masikitiko makubwa

    "Amenikosea mno. Yeye si wa kunishika vile tena wakati nimelala nikmsamehe kwa kuwa hakujua wa kunishika ni wewe tu na si mtu nwingine alafu akazidi kunikosea zaidi na kunikasirisha alipoanza kukuuliza maswali ya ovyo ovyo,alikuwa amepitiliza mipaka sasa ikabidi nimfuatilie nimpe haki yake"

    "Zai hayo si maamuzi sahihi tambua ni rafiki yangu wa karibu mno"

    "Kwahiyo kama ni rafiki yako wa karibu amenioa yeye au wewe?"

    "Ni mimi Zai lakini ulivyomfanyia umekosea kabisa kwani haikumstahili atendewe hivyo"

    "Kumbe jibu unalo kuwa wewe ndiye mmiliki halali wa mwili wangu sasa huyo sijui ndiyo rafiki yako mahusiano yetu hayamhusu"

    "Zai tambua kuwa yeye hafahamu kuhusu mahusiano yetu"

    "Vizuri,naona unamtetea sana sasa kesho ni lazima uhame na kama hautafanya ninavyotaka kichwa cha rafiki yako ni halali yangu"

    "Eeeeh! Zai ya nini yote hayo mpenzi wangu?"

    "Nimekwambia nataka jibu moja unahama hapa au hautaki kuhama?"

    Nilibaki kimya nikibishana na ubongo wangu na muafaka nikaona ni heri nihame ili niepushe vifo na ajali za watu ninaowapenda kwani hali ilizidi kuwa mbaya kila kukicha.

    "Nitahama hapa lakini naomba rafiki yangu umuache kama alivyo" nilimjibu nikiwa nimejiinamia kwa uchungu niliokuwa nao

    "Hapo sawa umefanya vyema na huyo rafiki yako sina shida nae tena"

    "Nashukuru Zai kama umeamua kumsamehe"

    "Zaka kwa kuwa muda umekwenda kesho ndipo utahama pia kila kitu ulichonacho kuanzia nguo,vyombo na vingine vidogo vidogo utavikuta huko labda Kama una kitu cha maana sana unaweza kukibeba,nafikiri tumeelewana siyo?"

    Nilikuwa nafikiria masharti yanavyo niandama kila siku inayoitwa Leo mpaka nikawa nayakumbuka Maisha niliyokuwa nayo licha ya kwamba nilikuwa napata shillingi mia mia lakini nilikuwa na uhuru wa kuishi nitakavyo Mimi.

    Nilistuka baada ya kuguswa bega na Zai ndipo nikakumbuka kuwa tulikuwa na maongezi ambayo hayajaisha

    "Zaka nakuuliza umenyamaza kimya maana yake nini na kama kuna kitu kinakusumbua niambie nikusaidie kuliko kunyamaza kimya haisaidii kitu"

    "Umesema kila kitu kitakuwepo huko huko?"

    "Sahihi kabisa na sitaki umuage yeyote kuwa unahama"

    "Kwanini nisiage kwa hawa marafiki ambao nimekuwa nao bega kwa bega miaka nenda rudi."

    "Kwasababu hamna mtu hata mmoja anaeaminika miongoni mwao"

    "Sio kweli Zai mimi na wao tunaaminiana vilivyo kwahiyo lazima niage"

    "Naona umeanza kuwa na jeuri sasa subiri zamu yako wewe nenda ukawaage"

    "Eeeeh! Hapo sawa si kila kitu unaamua wewe tu mengine niachie mimi"

    "Usijali Zaka na Leo silali nyumbani kwako naenda kwetu nitarudi kesho kukuchukua kuelekea makazi mapya"

    "Hilo halina shida"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zai aliondoka akiniacha mpweke mno siku hiyo hata usiku wenyewe niliuona umekuwa mrefu sana kwa upande wangu. Nilikuwa sielewi nini hatima yangu na kwa Mara ya kwanza kabisa nilijutia maamuzi yangu ya kuoa jini kwani ni sawa na kumkumbatia nungu nungu ilihali unatambua ana miba mwili mzima.

    Asubuhi na mapema niliwahi nyumbani kwa Mika ili nimtaarifu kuhusu kuondoka kwangu na sikupanga kabisa kumwambia ukweli kwani ungeniletea matatizo

    "Habari yako bwana Mika"

    "Nzuri tu Zaka sijui ni kwema huko maana umewahi mapema mno na hii sio siku ya kazi.".

    "Nafahamu hilo ila nimepatwa na dharura kidogo napaswa kuelekea mjini."

    "Kuna nini huko mjini maana si kawaida yako kwenda"

    "Ni kweli lakini nimepewa taarifa baba yangu mdogo yu hoi hivyo nahitajika"

    "Zaka mbona sijawahi kukusikia kuwa una ndugu wewe?"

    "Aaaah! Eeeh! Ndiyo ila naomba tuyazungumze nikirudi kutoka huko"

    "Haina shida ni uamuzi wako"

    "Pia umtaarifu Sanga kuwa nimesafiri na naomba unilindie nyumba yangu iwe salama japo sijui nitarudi lini."

    "Sawa ila Sanga alipatwa na ajali ya baiskeli Jana hivi ninavyokwambia alipelekwa hospitali na wasamalia wema."

    "Alipatwa na ajaliiii???" Nilijifanya kushangaa wakati naelewa kinachoendelea.........



    "Ndiyo kwani wewe haujasikia hizi habari?"

    "Hapana sijazisikia na hivi ndiyo nazipata kwako hapa" nilikanusha kabisa ni kama Mimi sio chanzo cha yeye kupata ajali

    "Sawa lakini ndiyo hivyo imeshatokea"

    "Kumbe Mimi nikukimbie bwana Mika na umpe pole sana Sanga ila nitakuja kumpa pole zake zaidi nikirudi" niliamua kuaga ili nisije nikapewa swali ngumu kulijibu ikawa tatizo

    "Sasa mbona hata funguo hauziachi Zaka maana usafi ni lazima bwana"

    "Nilitaka kusahau kabisa si unaelewa nina matatizo sasa kichwa kimejaa mawazo mengi"

    "Aya karibu tena Kijijini kwetu na usisahau zawadi wakati wa kurejea"

    "Hilo tu ondoa shaka bwana Mika"

    Niliondoka haraka haraka mpaka nyumbani kwangu nikaketi nje nikimsubiri Zai, japo nilikuwa katika hali Fulani ya kutopenda kuhama lakini hauwezi kuamini nikikwambia usiku mzima nilikuwa naota tu kuhusu sehemu ninayo hamia ina uzuri kiasi gani na furaha hakuwa mbali kuushambulia moyo wangu.

    Nilimsubiri sana Zai lakini hakuonekana nilipata kazi ya kutazama huku na huko lakini sikumuona nilijaribu hata kusimama na kutembea tembea kushoto kulia nikidhani labda atakuwa ananichungulia au ananiona nilivyo na kihoro cha kuhama.

    Kwa mbali niliona Prado ya rangi bluu ikielekea uelekeo wa nyumbani kwangu ila sikuitilia maanani kwa kuwa ile ilikuwa ni njia tu kama ilivyo kwa njia nyingine zinazokatisha mitaa. Nilisimama kwa muda nikarudi tena kuketi,ile gari ilikuwa imefika usawa wa nyumba yangu ikasogea mpaka uwanjani kwangu ikageuzwa kama inarudi ilikotoka.

    Mimi nilikuwa naishangaa tu na nikawa nimeudhika na dereva kwanini asigeuzie gari yake huko alikotoka ila nyumbani kwangu kwani hajaona viwanja vingine huko, nikawa najiuliza kwani fikra hazikunituma kabisa kutambua yule ni nani.

    Piiiiiii....piiiii.......piiiiii....piiiii zilikuwa ni honi za gari ile zililalamika, hapo nikafahamu huenda naitwa pale nikainuka na kwenda japo akili ilikuwa inagoma na kujiuliza kuwa anataka nini kwangu maana sina rafiki au ndugu ambaye ana uwezo mkubwa wa kumiliki gari namna hii.

    Kioo kilishushwa nilipokaribia na nilipofika kabisa nilizidi kubaki mdomo wazi, lilikuwa ni tabasamu laini kutoka kwa Zai na macho ya kunihadaa

    "Mbona unashangaa hivyo Zaka au huamini kama ni Mimi?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog