Search This Blog

JINI ZAITUNI - 2

 





    Simulizi : Jini Zaituni

    Sehemu Ya Pili (2)



    "Shhhhhhhhh!!, njoo hapa karibu yangu nikuoneshe"



    Sikuwa mbishi niliinuka kiuchovu mpaka pale alipo

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Sogeza uso wako hapa" nilisogeza pale alipo akapitisha kiganja cha mkono wake usoni kwangu



    "Aya hebu angalia kule" alinionyesha ukutani ila nikaona kama maajabu kwani palionekana uwazi ulioonesha mpaka nje kama vile hamna ukuta na hapo ndipo palinishangaza zaidi, nilipotazama vizuri nilishuhudia wachawi wanne wawili niliwafahamu alikuwa mama Halima na mzee mmoja jirani yangu, walikuwa wanawanga uwanjani kwangu wakiwa uchi wa mnyama.......





    Sikuamini kama mama Halima anaweza kuwa na roho ya namna ile na sikufikiri hata siku moja kuwa anaweza kunitendea kitendo kama kile,niliduwaa kwanza mwili nao ukiishiwa nguvu na akili ikiwa imechoka kabisa kwa kitendo kile nilichoshuhudia



    Niliwahi kuona tu katika maonyesho mbalimbali lakini siyo ana kwa ana kama ilivyonitokea kwa kweli nilihisi hasira zikipanda mpaka nikaanza kupumua kwa kasi ila nilistushwa na sauti ya Zai kabla sijachukua uamuzi wa kufanya



    "We Zaka sasa nini hivyo unataka kufanya na jazba zako hizo"



    "Nataka nikamuoneshe kwamba Mimi huwa sichezewi kirahisi rahisi namna hiyo"



    "Mmmh! Makubwa, we sikuzote ulikuwa wapi uwaoneshe huo ubabe wako etii leo kisa umeniona basi ujifanye baunsa"



    "Zai bhana maneno gani sasa hayo mimi nataka nikuoneshe kwamba kweli upo na kidume"



    "Ila siyo kwa mtindo huo Zaka ukijitokeza tu utakuwa halali yao siku ya leo, wale si wakawaida kama wewe"



    " Ina maana huu mchezo mchafu alikuwa ananifanyia kila siku au ameanza Leo"



    "Zaka huu mchezo hajaanza leo wala Jana kwani alipotambua kuwa akikwambia anakupenda huwezi kukubali sasa akaamua atumie hii mbinu na hapo unavyomuona ilikuwa imebaki siku chache akumiliki kwa njia yoyote ile bila kujali ina hatari kiasi gani."



    "Hapana,haiwezekani anifanyie hivi mtoto wa mwenzie,nakuomba basi ufanye kitu maana siwezi kuvumilia haya ninayotendewa na huyu mama"



    "Hayo ndiyo maneno sasa niliyokuwa nayangoja haswaaa kwasababu sikutaka kukwambia alipoingia humu ndani na kutoka nilitambua undani wake na Nilitulia kimya tu nikijua utasema nimemsingizia, sasa subiri ujionee ninachoenda kukifanya kwake"



    Zai alitoweka mbele yangu nikastuka kidogo kwa kuwa tayari nilikuwa nimeshaanza kumzoea haikunipa tabu sana kuona akifanya vile,nilipotazama kule alipo mama Halima na wenzake kulikuwa na upepo uliochanganyikana na kimbunga kikali,wote waliziba macho na hapo ndipo walifanya kosa la milenia,nilimshuhudia Zai akiwaadhibu kwa makofi makali wale watatu kasoro mama Halima ambaye hakujua kinachoendelea zaidi ya kusikia milio kama ya risasi na yowe za maumivu kutoka kwa wenzake hali iliyompelekea kufunguka kwa bomba lake lililomwaga maji kupunguza vumbi ardhini lisitimke.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa ni vichekesho kwa wachawi kama hawa wanaoonekana wamebobea kuambulia kipigo pasipo kutambua kinapotoka,Mimi nikiwa nimeshikilia mbavu zangu kwa maumivu ya cheko, baada ya mda wachawi wale watatu walikuwa hoi hawajitambui ndipo Zai alijitokeza wazi kwa mama Halima ambaye alizidi kutetemeka kama mgonjwa mwenye malaria Kali.



    Zai alianza kuzungumza kwa dharau "Mama Halima unayemfuata fuata Mme wangu sasa nadhani umegundua ulichokuwa unakichunguza si ndiyo?"



    "Hapana dada yangu nisamehe nimekosa" alizungumza kama mtoto mdogo anaetaka kuchapwa akisahau kuwa anaezungumza nae ana umri kama wa mwanae



    "Ha!ha!ha!ha!ha!ha! Unadhani nitakusamehe kirahisi hivyo, nafahamu kama nyie binadamu hata uonywe mara mia utarudia tu makosa yale yale"



    "Kweli dada yangu Mimi sidanganyi tena na apa kwa jina la mama yangu mzazi sirudiii dada"



    Nilishangaa kuona Zai ameanza kuingiwa na roho ya huruma kumbe hata majini yana huruma mmmh! Nilistaajabu maana huwa nasikia majini hawasamehi na wala hawana hata chembe ya huruma,sijui Zai ilikuwaje akawa na roho hiyo, nilizidi kufuatilia maongezi yao nijue wataishia wapi



    "Mama Halima nimekusamehe ila nitakupa adhabu ndogo ambayo itakuwa kama msamaha wako"



    "Ahsante dada yangu nashukuru kwa msamaha wako"



    "Chagua kati ya kuwa sakafu ya maliwatoni kwetu ili kila mtu akiingia basi akukanyage au nikugeuze majani machungu kuliko yote yaliyowahi kuonekana duniani na hayatachumwa mpaka pale nitakabobadilisha maamuzi"



    "Dada nimeshaapa kuwa sitorudia kamwe sasa na hizi adhabu jamani"



    "Wewe usitake nikasirike ohooo!"



    "Basi dada ni bora niwe hayo majani kwani sitokuwa na mateso mengi"



    "Hili litakuwa onyo kwa watu wengine wenye jeuri kama wewe na wenzako na ukumbuke wadudu watakuwa wakikuadhibu kila siku" Zai alimsogelea mama Halima akamgusa paji la uso na hapo sikumuona tena mama Halima



    Alirudi kwa wale wachawi waliobakia akawanyooshea mkono wakatoweka na Zai akifuatia, Nilipogeuka Zai alikuwa ubavuni kwangu akawa ameniegemea lakini macho yake yalikuwa yaking'aa na kunifanya nimuogope, Sikuwa na usingizi pia kwa yale matukio niliyo yashuhudia mda mfupi uliopita yalizidi kunitahadharisha kuwa Zai si mtu wa mchezo nikikosea tu masharti ndiyo kwa heri.



    Nikiwa katika dimbwi la mawazo nikiwaza na kuwazua jinsi ya kukwepa vishawishi vitakavyo sababisha niondolewe katika orodha ya viumbe hai hapo baadae na Zai, Kumbe Zai alikuwa akiniita bila majibu mpaka aliponizaba ka kibao ka uchokozi akawa amenitoa katika dimbwi hilo zito



    "Kulikoni kipenzi cha moyo wangu maana tunastuana"



    "Yote unayowaza unaweza kufanikisha endapo tu utakuwa mtiifu kwangu"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Dah! tatizo lako ndiyo hilo ninachowaza wewe tayari umeshakijua"



    "Usijali wa ndani wangu ila tu usijaribu kuwazia vibaya kwani nitakuwa nimefahamu nini kinachoendelea"



    "Haina shida we ni wangu tu na sitokusaliti mpaka mwisho"



    "Nashukuru Zaka kwa kunijali ila naomba kesho asubuhi utengeneze sanduku kubwa analoweza kuenea mtoto mdogo na ikifika saa sita mchana uende ziwani uingie mpaka maji ya magotini utakachokiona uchukue maelekezo mengine nitakupatia ukifanikisha hilo"......



    Nilibaki nikimtazama usoni nisijue ni kipi nimuulize kwasababu maelezo yake yalikuwa yanajitosheleza. Mda huo huo jogoo nazo zilianza kuwika kuashiria kumekucha Zai aliniaga kuwa anaenda kwao atarudi mda wa kunielekeza nini nifanye baada ya zoezi nililoachiwa, sikupinga na nikaamua kuanza kufanya maandalizi ya kukabiliana na hilo jambo nililoambiwa.



    Ilipotimia saa moja asubuhi kukiwa kumepambazuka kabisa nilitahamaki kuona wavuvi wenzangu hawajanipitia kama ilivyo siku nyingine hii ilinipa mshangao mkubwa kwa kuwa haikuwahi kupita hata siku moja hawajahudhuria katika mchakato wa kuitafuta riziki ya siku hiyo isipokuwa tu endapo mmoja wapo awe mgonjwa au amepatwa na dharura. nilianza kuelekea kwa fundi seremala niliefahamiana vilivyo ili anitengenezee sanduku.



    Ilikuwa ni ajabu pale nilipofika kwa fundi alikuwa akicheka Cheka tu kila anaponitazama nikashindwa kuelewa ana matatizo gani maana furaha niliyomkuta nayo si ya kawaida nikahisi huenda ameanza kuwa taahira au chizi, nilipogusia kuhusu kutengenezewa sanduku aliongeza umakini kwangu kuliko wateja wengine akaanza kulishughulikia kitu ambacho kilisababisha minong'ono ya chini chini na baadae ikawa kelele.



    Fundi hakujali hilo yeye alikazana kulihangaikia sanduku langu jambo ambalo wateja wake hawakulipenda kwani wengi wao walisema ameanza kuridhika na wengine wakidai anafukuza wateja kwahiyo tabia yake mpya ya kuhudumia wateja wanaochelewa na kuacha waliowahi



    Baada ya malumbano ya mda alipita mzee mmoja wa makamo akatusalimu, tuliitikia kwa pamoja yeye alijibu lakini hakuondoka alibaki amesimama kama anaetaka kuzungumza kitu



    "Ndugu zangu mna habari juu ya tukio lililotokea alfajiri ya Leo?"



    "Hatufahamu mzee kwani kuna lipi limetokea?" Alijibu mmoja kwa niaba yetu



    "Mmmmh! Sasa nyie mnaishi kijiji gani maana hichi kijiji ni kidogo mno kiasi kwamba taarifa inasambaa haraka mno."



    "Sasa mzee mimi naona unatukashifu badala ya kutujuza si ndiyo?" Alifoka kijana mwingine kati yetu



    "Kijana usiwe mkali kwa wakubwa wako utalaaniwa buree"



    "We mzee mwanga nini mbona umeanza kutukoroga kama hutaki kusema si uende tu watu tuna mihasira yetu hapa tusije tukazimalizia kwako"



    "Basi vijana kuweni wapole ni hivi mwenyekiti wa kijiji aliitwa ile alfajiri kuna miili ya wachawi ilikutwa karibia na nyumba ya Mama Halima ndani ya lile shimo lililowahi kutumika kutengenezea tofali shule kipindi cha songambele"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Weeeeeee! Hayo unayosema ni ya kweli au" nilistukia nimeropoka bila ya kujielewa



    "Kwanini ni wadanganye vijana wangu tena kinachoshangaza ni ile miili kuwa na alama za viganja kifuani,mashavuni na mgongoni"



    "Mmmmmh!" Tuliguna kwa pamoja, yule mzee aliendelea



    "Na kinachotutia wasi wasi ni yule kiongozi wa dini hapa kijijini nae ni mmojawapo kati ya hao walio okotwa na ni yeye pekee ndiye amefahamika na uongozi wa kijiji wengine wawili hawajulikani wanatokea wapi"



    "Mzee taarifa hizo ni za kusikitisha sana kwa wanandugu na ni za furaha kwetu kwasababu hao wamekuwa wakirudisha sana maendeleo yetu nyuma na laiti kama amgefahamika aliefanya hilo tukio hakika ningempatia zawadi kubwa" aliongea mama mmoja mtu mzima



    "Jamani hayo mengine mnayofikiria haya nihusu suala nimefikisha ujumbe wacha niende zangu" aliongea yule mzee huku akiondoka



    "Loooh! Kweli we mzee kijana ni mcharuko una maneno kama nini na sipatii picha enzi za ujana wako ulikuaje?" Aliongea kwa utani yule mama wa makamo



    "Haaaa! Kaulize mabinti wenzio nilikuwa sikamatiki mie" alijibu Mzee yule akiwa anatokomea kusiko julikana.



    Nilikuwa nafuatilia maongezi yao kwa makini mno pia nilituliza mwili wangu uliokuwa umeanza kutetemeka kama simu ya Nokia ili nisionyeshe kama nafahamu lolote kuhusu tukio lile kwani ningeibeba kesi nisiyoitarajia.



    Baada ya fundi kumaliza kunitengenezea sanduku niliaga fundi peke yake ndiye alijibu akiwa anacheka cheka kama awali kasoro wale wateja ambao walikaa kimya licha ya kwamba nilitoa sauti kubwa. Sikuwajali nikaondoka eneo hilo bila wasi wasi wowote mpaka nyumbani kwangu,kwa kuwa muda ulikuwa ni saa nne niliamua kwenda mgahawani kupata chochote.



    Nikiwa tayari nimejaza tumbo langu vyema niliamua kupitia kwa mwenyekiti wa kijiji ili nihakikishe yaliyosemwa na yule mzee, nilichukua dakika kadhaa mpaka kufika kwake, nilikaribishwa na umati wa watu waliokuwa eneo hilo wakishangaa na Mimi niliamua kujipenyeza katikati mpaka walipolazwa marehemu waliokuwa wameharibika vibaya miili yao iliyopambwa na alama za vidole.



    Saa sita mchana ilinikuta ziwani, nikajitoma ndani ya maji nikiwa natembea taratibu tena kwa uangalifu mkubwa kichwani nilikuwa na mawazo mawili kama sijakutana na mamba basi nikuua mtu akakae kwenye lile sanduku, nilizidi kusonga mbele kwa umakini wa hali ya juu kama jasusi katika misheni tata,nilipofika maji ya magoti mwili ulinisisimka na nywele zikasimama moyo nao haukuchelewa ukaanza kupiga kwa kasi nikawa na hofu kuu.



    Nilianza kusikia sauti za watu zikilalamika kwa maumivu zikiwa zinaomba msaada siyo watoto,wanawake wala wanaume wote walilalamika ni kama Mimi ndiye nimewaweka hapo. Nilianza kutazama kushoto na kulia sauti zinakotokea sikuambulia kitu nikaamua kujikaza nikaanza kusogea mbele taratibu, moyo ulipiga"paaaaaaah" nilipotazama ndani ya maji zilionekana sura za watu walioonyesha wapo katika maumivu makali yasiyoelezeka

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikaanza kujiuliza ndiyo hiki nilichokifuata au ni mtihani wa kuvuka,ikabidi nitulie kwanza ili nikubaliane na baraza la wa shauri kichwani mwangu, kumbukumbu zikanirejea kuwa Zai alisema nitakachokikuta nichukue sasa utata ukawa hapo hata kama ni wewe mpenzi msomaji unaweza kuchukua sura za watu tena zinazolalamika kwa maumivu makali? Siyo rahisi nikaona haina haja ya kufanya hivyo bora niondoke eneo hilo lakini wazo likaja kuwa kama mama Halima alipewa adhabu ile Mimi je?



    Ikabidi niuvae ujasiri wa kiume liwalo na liwe nikageuka kuzitazama zile sura kisha nikafumba macho na kupeleka mkono kwa kasi kama nanyakua kitu, nilipofikisha mkono ndani ya maji ulisikika mlio wa maji yakiruka na sauti zikatulia kimya......





    Nikafumbua macho haraka nitazame nilichoshika lahaulaa! Kiganja kilikuwa kitupu nikaingiwa na wasi wasi kwani hata ndani ya maji sura zile hazikuonekana nikajua tayari nimefeli mtihani huo nikaanza kuhisi maini yanakatika tumboni haja kubwa nayo ikipiga hodi kila nilipofikiria shughuli ya Zai.



    Nilikata tamaa kabisa nilijikuta nikisali kimoyo moyo ili jua la kesho nilione japo sikuwa nakumbuka Mara ya mwisho lini kusali kama hivi, nilitamani kulia ikashindikana nayo taswira ya Zai akiwa amechukia ikawa inajijenga kichwani mwangu kiukweli sikuwa hata na chembe ya tumaini la kuokolewa kwenye hii kadhia.



    Niliamua nianze kuondoka lakini nilipogeuka tu mwanga ulipiga katika paji la uso ulikuwa kama wa kumulikwa na kioo hivi nikapeleka macho haraka upande huo laaaaah! Niliona sarafu inaelea ikiwa inang'aa na upya wake, niliichukua kwa kusita sita kwasababu haiwezekani sarafu uiweke ndani ya maji ielee haiwezi kutokea hicho kitu isipokuwa tu kwa nadra kama ilivyo kwangu.



    Nilipofika ufukweni kuna mvuvi mmoja alikuwa akitabasamu huku akiniangalia usoni na Mimi kwa aibu niliinamisha uso wangu nikihisi labda alikuwa akifuatilia ninachofanya nilipokaribia kumvuka aliuliza



    "We Zaka siku hizi umekuwa kipofu"



    "Mmmh!" Niliguna huku nainua kichwa kumtazama akazidi kutabasamu



    "Mi nahisi hauko sawa bwana Zaka mana vitu unavyofanya vinaashiria kabisa hauna siku nyingi utaanza kuokota makopo"



    Hapo nikastuka kidogo kuwa ina maana alikuwa ananitazama ninachofanya, niliendelea kutafakari juu yake



    "Bwana Zaka naongea na wewe maana usiposema matatizo yako kwa sisi ndugu zako nani utakae mwambia akakusaidia kuwa muwazi bwana"



    "Hapana, bro Mimi nilikuwa tu nachezea maji wala sina matatizo kabisa"



    "Etiii! Ila inawezekana ikawa kweli kwasababu huwa haufichi endapo ukipatwa na matatizo lakini ukumbuke kuwa mficha maradhi kifo kitamuumbua hivyo kuwa makini"



    "Sawa bro usiwe na wasi wasi na Mimi Niko sawa kabisa"



    "Haina tabu ila angalia bwana Zaka isiwe masharti ya mganga nikawa nimekuharibia dawa"



    "Usijali bro ni kawaida tu" niliondoka nikiwa najiuliza ingekuwaje kama ningejikanyaga katika maelezo niliyoyatoa duh! Ni hatari juu ya hatari na je siku wakigundua itakuwaje?, yote hayo ni maswali nilikuwa nikijiuliza njiani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipofika nyumbani nilifungua mlango pua zangu zikapokelewa na harufu ya manukato adimu, nyumba nzima ilikuwa imesafishwa vyema kuliko hata ambavyo huwa nasafisha, nilishangaa kumuona Zai amejipumzisha kitandani na hata sikupata jibu ameingiaje kwani funguo nilikuwa nazo mimi.



    Katika siku zote nilizowahi kuwa na Zai sikuwahi kupata mda wa kumsaili alivyo dah! mate ya uchu yalikuwa yameanza kunitoka kwa jinsi alivyokuwa amenona kwa umbo matata lenye ushawishi wa hali ya juu na kifua kilichojaa vyema kikiwa na chuchu zilizosimama kama miiba wale wenzangu na Mimi huziita maua saa sita.



    Nilijua kabisa huu ndiyo mwanzo wa kujilia vinono kwa msichana mrembo namna hiyo basi nikajisogeza taratibu mpaka alipo nikajiweka sawa kwanza nikawa nashusha mkono taratibu walau nimpapase lakini uoga ulichukua nafasi yake,kila nilipotaka kumshika nilirudisha mkono kisha nikaanza tena ikawa kama kamchezo



    Wakati naendelea na kupigania kumshika Zai niliona ameanza kutabasamu sasa hapo nikaahirisha zoezi hilo kisha nikajiuliza anaota nini huyu mbona anatabasamu, nikapeleka mkono kifuani kwake safari hii nilidhamiria kweli kumshika nilipokaribia kifuani nilidakwa mkono



    "Mmmh! Zaka siyo mda wake huu jamani"



    "Aaaah! Nilitaka kutoa mdudu alikuwa anatembea kifuani kwako" nilidanganya kutokana na aibu za kugundulika hila zangu lakini Zai aliangua kicheko cha nguvu mpaka nikabaki namtazama kwa kuibia ibia



    "Zaka! Umeanza lini kuongopea watu ha!ha!ha!ha!ha!ha!" Alizidi kucheka akiwa ameshangazwa na uongo wangu mtakatifu



    "Sikia Zaka wangu endapo ukikamilisha kila kitu kuanzia sasa nitakupa Mara moja tu mpaka tukifunga ndoa ndiyo utakuwa huru wakati wote"



    "Dah! Kweli umenikamata mpaka hapo sina ujanja japo nilikuwa nimesahau kama wewe si binadamu"



    "Usijali pia hongera kwa kufanikisha zoezi dogo lililokutoa jasho, unaweza kunipatia ulichokipata?"



    "Kwanini hapana ni hii hapa" nilimkabidhi sarafu ile iliyokuwa ya zamani mno lakini ni mpya kama imetengenezwa Jana



    "Sasa hii sarafu inatakiwa uiweke katika sanduku lile ila kabla ya kuiweka itabidi uchukue noti ya shilingi mia tano uichanganye baada ya hapo utasubiri hii siku ipite kesho ndipo utaitoa hiyo noti ya shilingi mia tano ambayo utafanyia manunuzi yoyote yale haijalishi ni bei kubwa kiasi gani utapewa na pesa inayobaki ila kumbuka sharti lake ni moja tu hauruhusiwi kutumia hela za sarafu ikibidi muachie huyo muuzaji nadhani umenielewa"



    "Nimekuelewa mrembo lakini swali lipo hapa je nikinunua hivyo vitu hiyo shilingi mia tano si itabaki huko?"



    "Ooooh! Kweli Zaka swali zuri ni hivi hiyo mia tano itarudishwa kwako kupitia ile baki utakayolipwa pia kitu kingine ukumbuke ukishapewa hiyo pesa inayobaki kama chenchi ndizo zitakuwa za matumizi mpaka zitakapoisha ndipo unaruhusiwa kutumia hiyo noti ya shilingi mia tano"



    "Nimekuelewa kipenzi changu"



    "Zaka nina ombi lingine kwako"



    "Lipi tena hilo mahabuba au ndiyo mtihani tena?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mmh! Inategemeana kwani umemaliza mitihani yote?"



    "Sijui wewe mwalimu wangu maana haukusema ni mitihani mingapi mpaka nifuzu"



    "Acha uoga Zaka kumbuka wewe ni mtoto wa kiume unatakiwa kujikaza"



    "Hapana Zai hata kama Mimi ni mtoto wa kiume lakini mitihani yako ni afadhali uwe unamkimbia chui porini kuliko kukutana na wewe" nilikuwa namtania tania Zai wangu aliyekuwa hachoki kucheka kila ninapomtania........





    Alinitazama kwa mda mrefu kisha akakohoa kidogo kusafisha koo,nikajiweka tayari kumsikiliza



    "Zaka nafahamu kuwa itakuwa ni vigumu sana kukubaliana na hili ninalotaka kusema lakini kwanza unatakiwa ufikirie kwa kina ndipo utaelewa nina malengo gani kwako." Alitulia kidogo akanitazama tena



    "Naomba hiyo kazi yako ya uvuvi ustaafu na wala sitaki kuona mpenzi wangu unafanya kazi ngumu vilevile naomba nikuhamishe hapa kwako kwani tayari nimesha kuandalia makazi sijui unasemaje Mme wangu mtarajiwa."



    Nilianza kubabaika nijibu lipi kati ya hayo kwasababu ya furaha isiyoelezeka,mate yakawa na kazi ya kuteremka kooni bila mpangilio mpaka nikapaliwa,Zai alizidi kutabasamu akiwa ananiangalia,ilipita kimya kirefu ndipo nilipata la kusema baada ya kichwa changu kurudisha mtandao uliokuwa unayumba yumba



    "Aaaah! Nakubaliana na wewe suala hilo la kuacha hii kazi maana hata Mimi nilishaichoka ila swali liko hapa baada ya kuacha hiyo kazi nitafanya ipi sasa maana sina uzoefu na kazi yoyote ile isipokuwa huu uvuvi"

    Niliongea kwa hisia utadhani naigiza sinema ya majonzi



    "Zaka ondoa hofu utafanya kazi ya maana tena pasipo kutumia nguvu kubwa zaidi ya akili ya ziada na utambue kuwa unapofanya hiyo kazi Mimi nipo nyuma yako kwahiyo hamna kitakachoharibika"



    "Sawa tupo pamoja na vipi kuhusiana na hili suala la kuhama tunahamia wapi?"



    "Aaaah!! Zaka mbona hujiamini we mwanaume unanishangaza au unadhani naenda kukuuza?"



    "Hapana sijafikiria hivyo ila nilitaka nifahamu daraja nililopanda kama ni refu au la maana naogopa nisihamishiwe mitaa wanayoishi vigogo ikawa kazi"



    "Ha!ha!ha!ha! Umenifurahisha mno kuliko siku zote yaani umejaribu kuendana na hisia zangu, jibu ndiyo hilo hilo utahamia sehemu wanayoishi watu wenye hadhi juu"



    Nilichekecha ubongo kuhusu mafanikio yangu ya ghafla nikaona si vyema kwani kitumbua kitakuwa kimeingia mchanga jamaa zangu watakuwa na wasiwasi juu yangu kuwa labda nimetoa kafara au tayari nimejichanganya.



    "Kiukweli Zai sikatai kufanikiwa kwa haraka namna hii ila hawa jamaa zangu watanifikiria vibaya kwani hata uwe mvuvi wa miaka nenda rudi si rahisi kupata mafanikio makubwa kiasi hicho tena kwa ghafla mno."



    "Haaa! Hivi wewe una mawazo kweli kichwani mwako,siku zote ukitaka kufanikiwa usiangalie maneno ya watu na hata vidole vyao pia mafanikio hayawezi kupatikana pasipo fitina Zaka."



    "Ni kama nakuelewa vile lakini nina hofu juu ya hilo" nilionesha wazi kuwa sijaridhika kuhamia huko



    "Zaka nyie binadamu ni vigeu geu sana hasa katika masuala ya pesa sasa ni onyo hili nakupatia endapo utahama hapa sitaki kusikia habari za rafiki zako tena na ujiandae kupata marafiki wapya upo hapo?"



    "Mimi nimeongea tu mamaa kwanini tufike kote huko ukikasirika wewe mi nitakuwa katika taswira ipi?, eeh! Furaha yako wewe ndiyo furaha yangu nakuomba upunguze hasira zako kwani haya ni mazungumzo ya kawaida tu ili tufikie muafaka tafadhali." Niliongea kwa kumbembeleza mno nilipomuona ameanza kunikaripia na kunipa amri zisizoeleweka



    "Sikia Zaka Mimi siwezi nikawa nakutafutia msingi mzuri wa Maisha alafu wewe unawawazia hao rafiki zako ambao hata kula hawakupi angalia usiwe na masikio ya kenge mpaka yavuje damu ndiyo usikie shauri yako."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Jamani Zai yaishe basi sirudii tena kusema hivyo mchumba wangu nitafuata kile unachosema"



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog