Search This Blog

JINI ZAITUNI - 1

 





    IMEANDIKWA NA : HUMPH DE THRONE



    *********************************************************************************



    Simulizi : Jini Zaituni

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Ilikuwa ni usiku wa manane usiotulia kwa upepo mkali na mawimbi yanayopiga kwa kasi katika ziwa Tanganyika hali iliyopelekea kukosekana kwa utulivu eneo hilo ambalo lilikuwa ni kama wanafua umeme wa maji ambapo katika ufukwe huo wa ziwa alionekana kijana mmoja ambaye alikuwa na kijibukta kifupi kiasi kwamba mapaja yote yalikua nje huku akiwa kifua wazi na yai mkononi ambalo lilionekana wazi ni la kuku wa kienyeji

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alikuwa anaongea kwa sauti kubwa iliyosikika wazi alichokuwa akisema "nimetaabika sana kila kukicha nikifanya shughuli mbali mbali ambazo hakuna hata moja iliyonifaidisha sikuchoka nikakazana lakini sasa uvumilivu umenishinda ndiyo mana nipo hapa kuomba msaada wenu ninahitaji mtu atayeniongoza na kunisaidia niondokane na huu umaskini uliokithiri"



    Ndipo alipolitupa yai hilo ziwani ambapo upepo mkubwa ulivuma kuzidi ule wa mwanzo ambao safari hii uliambatana na radi zilizomfanya atoke kwa mwendo wa haraka kama anakimbizwa akirudi nyumbani kwake ambapo alikuwa katika chumba kimoja kipana japo ni nyumba ya udongo.



    Alichukua kopo jeupe akatia maji kisha akachukua sabuni inayonukia akaanza kuitikisa kwenye kopo lenye maji mpaka povu likakolea pamoja na pafyumu inayonukia vizuri akapulizia ndani ya povu hilo alipomaliza akaanza kunyunyizia chumbani mwake huku akisema maneno ambayo hayakusikika wazi alichosema baada ya hapo alirudi kulala.



    Adhuhuri kama ilivyoada alikutana na wavuvi wenzake wawili wakawahi kwenda kuangalia mtego wa wavu walioutega jioni ya siku iliyopita walipata samaki kidogo ambao walirudi nao nchi kavu wakawauza na wengine waliosalia kidogo waligawana kwaajili ya mboga ndipo walipoagana na hapo ndipo nilifahamu kijana huyu alikuwa anaitwa Zaka ambaye alikuwa akisimulia kisa chake.



    Siku hiyo ilipita bila majibu yoyote juu ya kile nilichoomba ziwani mwishowe wiki ikakatika bila mafanikio wala dalili yoyote..........



    *******------********-----****



    Katika sehemu moja isiyofahamika majini kulikuwa na kikao kizito cha familia moja ya Mfalme Zutasha kilichojumuisha watu watatu binti wa mfalme na mkewe mpendwa Malkia Suraiya ambao walionekana miili yao bado inadai ujana kulingana na walivyokuwa wanavutia mbele ya mtazamaji yeyote yule am aye angetokea kuwatazama wapenzi hawa walioshibana vilivyo,,walikuwa wamezama katika mazungumzo na binti yao "Mwanangu Zai binadamu si wema kwani wakipata wanachohitaji hasa hujisahau na hata kuvunja masharti uliyompa binti yangu"



    Zai"baba mi nimesha

    sema ninachohitaji ni ruhusa tu toka kwenu ya kwenda kumsaidia huyu kiumbe vile vile ikibidi tuoane kwakuwa nimevutiwa nae sana"



    "Mwanangu mimi mama yako hilo suala nilishawahi liona kabla sidhani kama mtafika mbali mana waliowahi kuolewa na binadamu waliishia kutendwa tu sembuse wewe binti mfalme"



    Zai"mama mimi nataka kwenda hayo mengine nitajua huko huko jinsi ya kuyadhibiti tafadhali naomba mniruhusu"



    "aaah! binti yangu naamini umeshakua ila yakikushinda sisi usituhusishe maana binadamu niwakaidi mno watakupenda leo kesho wanakuchukia na hata kukuteketeza kabisa ,unaruhusiwa kwenda kwa kuwa hatuna njia nyingine ila kukuona ukiwa na furaha wakati wote"



    Zai alicheka sana kwa furaha isiyo na kifani akawakumbatia wazazi wake akiwa mwingi wa tabasamu ambalo lilizidi kumuongezea uzuri usioelezeka kwani vitundu vidogo vilivyotumbukia katika mashavu yake yaliyo jengeka vizuri maarufu kama dimpozi kumfanya mwanaume yeyote yule rijali asitamani kupitwa nae kwani alikuwa na sifa kedekede zisizomalizika kwa maandishi haya hakika ni zaidi ya mrembo.



    *****--------**********

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku hiyo ilikuwa yenye bahati sana kwangu Mimi Zaka kwani sikutegemea na haikuwahi kutokea na haikufutika katika kumbukumbu zangu, tulivua samaki wengi sana ambao tulifanikiwa kupata hela nyingi na kitu nilichokifanya ni kwenda kununua kitanda na godoro siku hiyo hiyo.



    Ilipotimia usiku nililala mapema ili kuondoa uchovu vilevile ilikuwa imepita miaka sijaonja ladha ya kitanda kwani nilikuwa nalala chini kwenye turubai. Nilistuka usiku wa manane upepo mkali ukivuma chumbani kwangu madirisha na milango vyote vikafunguka hofu ikazidi kutanda moyoni mwangu.





    Niliinuka nikauelekea mlango na kuufunga vizuri ili usiweze kufunguka tena kisha nikageuka kurudi kitandani kwa ajili ya kulala. Wakati nikikikaribia kitanda nikapokelewa na ugeni katika pua zangu, harufu nzuri ya marashi ilikuwa imetawala katika chumba changu, kadri dakika zilivyozidi kwenda na harufu hiyo iliongezeka maradufu na kuzifanya pua zangu ziwe na kazi ya kunusa harufu hiyo isiyokera.



    Uoga nao ukazidi kunitawala kwani kila nilipotazama inapotokea harufu hiyo sikuweza kupaona. Nikajaribu kuwaza pengine kuna mtu aliyekatiza nyuma ya dirisha la chumba changu akiwa amepaka marashi hayo lakini nikajikuta nikipingana na wazo hilo kwani haikuwa kawaida kwa watu kukatisha eneo hilo katika usiku kama huo. Nikiwa katika tafakari nzito iliyonichukua dakika kadhaa, ghafla!! nikahisi harufu ile ikipotea taratibu katika pua zangu na baada ya muda ikapotea yote na kuiacha harufu niliyoizoea ya chumba changu. Loooh!! nikahisi pengine nilikuwa na mawenge ya usingizi niliokuwa nao hapo kabla.



    Sikutaka kuendelea kukifikiria kitu nisichokiona nikaamua kujitupa kitandani, usingizi nao haukuwa na hiyana kwani ulinitwaa barabara. Wakati nikiwa katika usingizi mzito nikaanza kuota niko katikati ya ziwa nikiogelea, nilipoibuka kwenye maji macho yangu yakakutana na msichana mrembo ambaye toka nizaliwe mpaka kuwa na akili timamu sikuwahi kuona msichana mzuri anayefanana nae au hata kukaribia nusu ya uzuri wake. Hakika alikuwa ni msichana mrembo haswaa mwenye kila sifa ya kuitwa mrimbwende. Uzuri wake ulitosha kumfanya kila mwanaume rijali akodoe macho kumtazama. Nikabaki nimeduwaa, nisikwepeshe wala kupepesa macho yangu.



    Hata waigizaji mbalimbali wa filamu wa nje za nchi hawakumfikia,hakufanana na watu wa nchi yoyote yani si mwarabu,shombeshombe,mwafrika wala mfilipino kiukweli nilibaki nimeduwaa nisikwepeshe macho na hata kutingisha kope za macho yangu.



    Nikiwa namshangaa yeye alitoa tabasamu pana lilizozidi kunipumbaza, ghafla katika hali nisiyoitarajia akaanza kunita kwa ishara nimfuate kule aliko ikawa kama ninaevutwa na sumaku nikaanza kumfuata taratibu lakini kabla sijafika mbali nilisikia naitwa jina langu.



    Nilistuka na hapo nikagundua nipo kitandani na ile ilikuwa ni ndoto tu kuangalia dirishani kulikuwa na mwangaza kuamanisha kumesha kucha niliinuka nikaenda kufungua mlango nikakutana na lawama za mvuvi mwenzangu Mika "we boya utalalaje mpaka saa hii wewe"



    "Samahani bro unajua uchovu ndiyo unaosababisha hivyo halikuwa lengo langu kuchelewa"



    "Hee!! makubwa ina maana unataka kuniambia miaka yote hii hilo li mwili lako halijazoea tu mikiki ya ziwani"



    "Dah! si kwamba haujazoea ila siku hazifanañi ndo maana nilichoka sana" nilijitahidi sana kumficha kwani hata waswahili husema ndoto uliyoota usimuhadithie mwenzako, ndipo tulipofuatana kuelekea ziwani kwenye mtego wetu.



    Ebooo!! Ilikuwa maajabu kwani siku hizi mbili mfululizo tulipata samaki wengi mno tofauti na kipindi cha nyuma, tulianza safari tukipiga kasia kwa nguvu maana mzigo ulikuwa mzito kwahiyo hata mwendo haukuwa mkubwa kiasi kwamba tungetumia masaa kadhaa kufika ufukweni.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wateja walikuwa wengi wakachukua samaki wote mapema na sisi tulibeba mboga zinazotutosha kwa siku hiyo. Nikiwa narudi nyumbani msichana mmoja mrefu wa wastani alipita jirani yangu akanisabahi alivyopità tu ile harufu nzuri ya marashi ikapenya katika pua zangu.



    Loooh!! Harufu ilikuwa ileile ya usiku uliopita nikashikwa na butwaa nisijue cha kufanya ghafla akageuka na tabasamu nyororo huku akinikonyeza lahaulaa!! Nusura nizimie kwa mstuko nilioupata baada ya kubaini ni yule msichana mrembo wa ndotoni.......





    Hapo nikahisi kuchanganyikiwa kwani nilihisi kabisa ni mauza uza yanayonitokea,yeye aliendelea na safari bila ya kugeuka tena kuniangalia licha ya kwamba nilionesha dhahiri mstuko wangu katika mboni za macho yake, nikajipa ujasiri wa kumfuata mana alikuwa ameniacha kwa umbali mrefu kidogo kutokana na mwendo aliokuwa nao na kabla sijamfikia niliona anakatisha katika kona ya nyumba mojawapo.



    Na Mimi nikaona hiyo ni nafasi ya dhahabu kwani ilikuwa ni nadra sana kupatikana sehemu kama hizo nilianza kutembea kwa kasi nikipiga hatua kubwa kubwa ili nimfikie mapema na kweli sikuchelewa nikawa nimefika lakini yule msichana hakuonekana japo sehemu ile ilikuwa ni ya uwazi na iliyonyooka mpaka barabarani hapo ndiyo nilizidi kuduwaa nikaona nijiongeze nikafuata ule uwazi mpaka barabarani niliangaza angaza kila sehemu lakini sikufanikiwa kumuona.



    Nilianza kurudi nyumbani kwangu nikiwa na mawazo tele juu ya yale yanayonitokea hasa matukio haya mawili nilijiuliza nini hatma yangu au nina dalili za kuchanganyikiwa na maisha lakini jibu lilikuwa hapana, sasa yule ni nani? Lakini sikumuona wa kunijibu.



    Nilifika nyumbani kutokana na uchovu niliingia kupumzika kwanza na baadae ndiyo nianze kazi ya kupika kwani sikutaka kuoa kutokana na ugumu wa maisha nilionao. Nikiwa katika usingizi mzito nilianza kuisikia sauti ikinita sikuweza kufungua kinywa changuo nilihisi ni kizito mno, mbele yangu alikuwa msichana mrembo na ndiko sauti ilipotokea akazidi kunita nami sikusita nikamfuata pale alipo



    Alikuwa akitabasamu kila mara na alikuwa na unywele mrefu ulioishia mabegani ila sura sikuifahamu mpaka pale nilipomsogelea kabisa ndipo nikang'amua kwamba ni msichana wa ndotoni nikaanza kuhisi miguu inakosa mwelekeo wa kusimama ikazidi kulegea cha kushangaza zaidi yeye alizidi kutabasamu huku akinishangaa ninavyohangaika na miguu Yangu.



    Ghafla nikaupata ulimi wangu "we...we... ni....ni.. na..ni na... u..na...ta.....ka ni...ni kwa...ngu?"



    "Zaka usiniogope sina nia mbaya na wewe wala sijaja hapa kukudhuru"



    "Mmmmmh!! Na... Ji....na la...ngu u..me..li...ju...a..je?" Niliuliza kwa uoga huku haja kubwa na ndogo zikitafuta kwa kutokea hasa baada tu ya kulisikia jina langu



    "Nina kufahamu vilivyo lakini haina haja ya wewe kuuliza nimekufahamu aje kwanza samahani kama ntakuwa nimekukwaza kwa jina naitwa Zaituni binti wa mfalme Zutasha niko hapa kukusaidia kutokana na ombi lako"



    Moyo ulinilipuka kwa furaha kuona nimepata msaada japo uoga haukunitoka "Sijui nisemaje lakini nashukuru sana kwa kukubali ombi langu asante sana" huku nikitoa tabasamu la furaha iliyojionyesha wazi wazi



    "Usinishukuru kwa kuwa bado mtihani ni mgumu kwako na inabidi unisikilize kwa makini"



    "Aaaaaah!! Mtihani tena ila mi sijali na haijalishi ni mgumu ama mwepesi Nina uhakika ntaweza kukabiliana nao la msingi nautaka sasa hivi kwani ni mda mrefu nimekuwa nikisubiri kitu kama hiki kitokee" nilisema kwa ujasiri mkubwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/"Kumbe sikutambua kama wewe una ujasiri wa namna hiyo kuukabili huo mtihani usikurupuke nina kupa siku nzima ya Leo ujiandae na kesho ndiyo nitakufuata"



    Sikuwa na neno la kuongeza niliposhuhudia mrembo huyo akitoweka machoni pangu ndipo nikakurupuka kitandani looh!! Ni ndoto tena juu ya msichana yule yule lakini cha ajabu chumba kizima kilikuwa kinanukia marashi mazuri niliyowahi kuyaskia kwa yule msichana hapo hisia zikaniijia ilikuwa kweli nimeongea nae nikaanza kuruka ruka kwa furaha



    Ila ghafla furaha yangu ilizima kama mshumaa gizani nilipokumbuka kuwa nimeambiwa nina mtihani tena nisikurupuke nijiandae dah!! Na akili ikagota kufikiri mawazo yakanitawala nisijue ni mtihani wa aina gani huo........



    Usiku ulifika hata usingizi ulinipaa kabisa nikiwaza na kuwazua kwani hakuna kitu kibaya kama mtihani haikarishi ni mgumu au mwepesi kiasi gani lazima uwe mwingi wa wasi wasi na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwangu kijasho chembamba kilikuwa kinanitoka taratibu nikiwa nasubiri kesho ifike.



    Nilistuka asubuhi na sikujua ni saa ngapi usingizi ulinipitia mpaka mda huo nilipoamka kiukweli sikujisikia kabisa kwenda katika shughuli zangu za kila siku lakini kutokana na shida zilivyonizidi hata ile pesa niliyoipata ilikuwa kama inazipunguza tu kitu ambacho kilizidi kuniumiza kichwa kila siku.



    Tukiwa ufukweni tuliuza samaki kama kawaida sasa tulipogawana mapato yetu kabla hatujaachana hapo kwa mbali nilimuona msichana akiwa amesimama akiangalia upande niliopo tukawa tunatazamana nikaona ananiita nisogee kule aliko akitumia ishara kwa kuwa haikuwa rahisi sauti kufika mahali nilipo.



    Na mimi nilinyoosha kidole kunielekea kifuani nikiashiria ananiita mimi au kuna mwingine na hapo niliona amekubali kwa kichwa kuonyesha mtahiniwa ni mimi mwenyewe, sikusita nikamfuata kule aliko,loooh!! sikudhani kama angekuwa ni yule mwalimu alietakiwa kunipatia mtihani ule niliokuwa naungojea kwa ujasiri ambao nilienda nao na sikutegemea kuufanya mtihani huo katika mazingira kama haya niliyokuwepo



    Nikahisi kibofu kinataka kupasuka kutokana na uoga nikaibana miguu kwa nguvu, nikaanza kuhisi kuna kimiminika kinateremka kwapani duh! Nikajua ni jasho hizo,nikajikaza kisabuni mpaka nilipomfikia alitoa tabasamu lililochanua mithili ya Jua la asubuhi lililoambatana na salamu



    "Habari yako Zaka"



    "Nzuri tu sijui za kwako" niliitika kwa sauti ya kukwaruza iliyochanganyikana na uoga ndani yake



    "Safi tu, tusipoteze mda nimekuja kukutaarifu kuwa ondoa hofu kwanza kwani mtihani wa kwanza unafanyia hapa mingine yote ni nyumbani kwako sijui uko tayari"



    Moyo ulianza kwenda mbio kama Niko vitani tena mbele ya adui nimeshikiwa bastola nikajikakamua kiume kujibu "Sawa niko tayari kuuanza"



    "Vizuri, inatakiwa urudi nyumbani kwako ukaondoe uchafu wote yaani usafishe nyumba yako kisha kama ni mlevi acha kuanzia sasa alafu sihitaji ule nguruwe wala kuiona mifupa yake hivyo tafadhali ukaiondoe na ukimaliza tafuta udi wenye chata ya paka uuwashe, huo ndiyo mtihani wako wa kwanza"



    Nilishusha pumzi kwa nguvu baada ya kuona nimeushinda mtihani huo kwa asilimia hamsini kwani ukiuona mtihani au kumfahamu adui yako ni nusu ya ushindi, wakati huo nilikuwa nimeinamisha kichwa chini upepo ukanipuliza ghafla nilivyoinua kichwa laaah! Yule msichana alikuwa ametoweka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilifika nyumbani nikaanza kusafisha kila sehemu kwa juhudi zote,ila kiukweli toka nilipokata tamaa ya maisha kiliwazo changu ilikuwa ni pombe tu na huyo ndiye alikuwa suluhisho kwa kila jambo linalonitatiza kila nipatapo pesa sikuchoka kumtembelea na hapo nikawa najiuliza nitamuacha kweli huyu rafiki yangu wa kweli, aaaah! Nitajitahidi kumuacha.



    Nilipomaliza kufanya usafi niliwasha udi nikauchomeka ukutani, nikajipumzisha haikupita hata mda mrefu nikasikia naitwa huku nikitikiswa niamke, nikadhani ni ndoto tena lakini wapi nilizidi kutikiswa tena safari hii ilikuwa kwa nguvu tofauti na mwanzo



    Nikaamka haraka na kuudaka mkono uliokuwa una nitikisa loooh!! Nilistuka kushika mkono laini kama ule ambao ulionyesha kila dalili ya kuwa mrembo alieshikwa huwa hagusi kazi yoyote zaidi ya kuupara tu, ilinibidi niuachie haraka nikapokelewa na kicheko kikubwa ila kisichokera



    Alinitazama usoni akizidi kutabasamu hapo nikagundua kuwa ana nyusi nyingi na kope ndefu kama wale wadada wa filamu za kibongo lakini hizi zilionekana za asili, kiini cha jicho lake kilikuwa na weusi mno kiukweli alizidi kuvutia,nikahisi amenistukia ninachowaza kwa jinsi alivyonitazama akiwa amenikazia macho yasiyo na mzaha



    "Zaka kwani hujaona wasichana warembo zaidi yangu?" Lilikuwa ni swali lililoniacha mdomo wazi amejuaje kama nilikuwa nawazia uzuri wake



    "Zaka mbona unajiuliza maswali mengi hivyo kuhusu Mimi" niliongezewa swali lingine zaidi lililonifanya nizidi kushikwa na bumbuwazi kabisaa huku macho yakinitoka pimaaa......





    Lakini yeye hakuonesha wasi wasi ni kama aliongea jambo la kawaida sana ambalo linaeleweka kitu ambacho kilizidi kunishangaza, nilijifikiria kwa mda nikawa sina la kufanya zaidi ya kukubali kuwa nimekamatika haswa



    Kwa kuwa aliona simjibu aliamua kuvunja ukimya "nafahamu kuwa bado unaniogopa,lakini naamini utanizoea tu"



    "Mmmm! Sawa ila unanitisha na maswali yako hayo"



    "Usijali Zaka, nadhani mtihani wa kwanza umeushinda lakini si kwa asilimia zote nikiamaanisha kuwa hiyo itakuwa ni desturi yako kila siku na endapo ukikiuka adhabu yake ni kubwa mno kuliko hata unavyoweza kufikiria"



    "Sawa mi niko tayari kwa lolote suala niondokane na haya maisha magumu"



    "Hilo lisikupe shida kwa kuwa moyo wako umeridhia, sharti la kwanza ili ufanikiwe huna budi kunioa na utakapofanya hivyo utambue sitoweza kukuona na mwanamke mwingine na endapo itatokea atakuwa halali yangu, pia sitaki kutambulishwa kwa yeyote mpaka pale nitakapokwambia ufanye hivyo na baada ya hapo ni ndoa ambayo tutafunga kwetu ujinini na kaa ukijua unakokwenda mi nipo nyuma yako hivyo usije kufikiria kunidanganya, nasubiria jibu kutoka kwako"



    Ukisikia mwanaume analia jua kweli kuna tena akiwa mtu mzima kama mimi ujue yamemfika shingoni yaani naoa jini na sitakiwi kuwa na mahusiano na binadamu loooh!! Ujanja wangu wote mfukoni nikabaki nimejiinamia, kale karoho kakutaka utajiri niliona hakafai ila waswahili walisema "maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge" hapo sikuwa na jipya zaidi ya kukubali tu

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zaituni alifurahi sana akanirukia na hapo ndipo kwa mara ya kwanza nikahisi joto kali limepenya mwilini mwangu na hisia fulani zikaanza kuniijia, yeye hakujali hilo alikuwa akikazana kuhangaika na papi za midomo yangu kutafuta kinywaji kisicho na ladha ilikuwa ni pata shika ndani kwangu.



    Usiku kama wa saa moja nilikuwa nimetulia na mrembo wangu mpaka hapo nilikuwa nimeanza kumzoea, nikaanzisha mbwembwe zangu ukizingatia nilikuwa muongeaji mno. Zaituni alikuwa anakazi ya kucheka siku hiyo kwani nilimchekesha mno kwa vituko vyangu nilivyoonyesha mbele yake.



    Kumbe wakati Zai anacheka sauti ilikuwa inafika mpaka kwa jirani yangu Mama Halima nae alivyommbea akawa amekuja kwangu akanza kunigongea mlango Zai akakaa kimya, nilipofungua mlango mama Halima alinitumbulia macho "enheee! Habari za usiku Zaka"



    "Nzuri tu mama za mida"



    "Safi tu mwanangu, samahani nimesikia kicheko cha mwanamke kinatokea ndani kwako umeoa baba"



    "Hapana mama mimi mbona nipo mwenyewe humu ndani au umehisi vibaya mama yangu"



    "Mmmmh! Kweli baba maana hata nilipokaribia nimeisikia hiyo sauti"



    "Kweli mama yangu nipo mwenyewe"



    "Baba tusifichane baba mi nilitaka nimfahamu tu mkwe wangu"



    "Usijali mama siwezi kukuficha ningemleta nyumb....." Kabla sijamalizia niliisikia sauti kubwa ya Zai akasema mruhusu aingie ndani ajionee,nilistuka nikajua mama Halima amesikia lakini nilipomtazama alionesha hajui kinachoendelea



    "Ingia ndani mama ujihakikishie mwenyewe" nilimwambia lakini moyoni nilikuwa nina hofu sana kuwa sasa akimkuta ndani nitafanyaje si nitaonekana mhuni, nikamzuia kisha nikamuuliza tena



    "Mama unahisi kabisa sauti uliisikia ikitokea humu ndani kwangu"



    "Aaaaaaaah! Mwanangu kwanini nikudanganye tena kicheko chenyewe kilikuwa kinasikika mpaka nyumbani kwangu si ndiyo maana nikakufuata ili nijue umevuta lini hilo jiko na ikibidi nilione mwanangu, kuna ubaya"



    "Hamna ubaya wowote mama nilitaka tu nipate uhakika wa haya unayosema" nikaisikia tena sauti ya Zai sasa hivi ilikuwa ya ukali kidogo "si nimesha kwambia muache aingie ndani huelewi au aya mruhusu aingie"



    Sikuwa na jinsi ilinibidi tu niachie njia apite kuingia ndani kwangu, wakati anaingia Mimi nikabaki mlangoni nikiwa nahisi moyo unaruka kichura chura........



    Mama Halima aliingia kwa pupa macho yake akiyaelekeza kitandani kwangu lakini macho yake hayakudumu kitandani hapo bali aliangaza chumba kizima ni kama anatafuta kitu, Mimi nikashindwa kumuelewa ina maana hajaona kama kuna mtu pale kitandani kwasababu ndipo Zai alikuwepo na alikuwa anatabasamu tu kila mara.



    Baada ya kumaliza kuangaza Mama Halima alirudi nilipokuwa nimesimama akiwa na mshangao na wasi wasi mwingi

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Samahani baba tusameheane kwa hili, nilihisi vibaya tu uniwie radhi kwa kweli"



    "Usijali mama yangu na ndiyo maana nilikuuliza kama una uhakika sauti ilitokea humu, ila ondoa hofu yameshaisha"



    "Kweli baba"



    "Ndiyo mama wala usiwazie vibaya hayo yameisha kabisa"



    "Eeeeh!! Ahsante baba yangu siwezi kurudia tena"



    "Sawa mama usiku mwema" niliamua kukatiza maongezi kwa kumuaga akawa ameenda akiwa amenyong'onyea ni kama mtu aliemwagiwa maji yenye ukoko



    Mama Halima hakufika mbali nikasikia kicheko kikubwa kutoka kwa Zai kilichonistua maana sikuwahi kumsikia mtu yeyote akicheka namna hiyo ndipo nilipomshuhudia mama Halima akitimua mbio bila kujali unene alionao na mara chache akiwa anaanguka anguka kwa kukosa mhimili.



    Nilijua kile kicheko alichocheka Zai labda kilikuwa ni cha kutaka kumuogopesha mama Halima la hasha! Kumbe alikuwa amechukia, nilivyoingia ndani na kufunga mlango Zai alikuwa ananitazama tu na nilipomfikia nilibaini kuwa ana hasira tena alikuwa amekunja ndita kama jogoo waliopo kwenye mpambano.



    Hapo ndipo somo langu la kwanza lilipoanzia nikajifunza kuwa majini huwa na wivu mno endapo tu ikatokea kuna mtu anakufuatilia ama anakupenda ni lazima ampe fundisho au onyo



    "Zaka nafikiri hutambui ni jinsi gani nakupenda na sirika yetu sisi huwa tunawivu sana hasa kwa mtu tunaempenda kama ilivyo Mimi na wewe hivi sasa, Huyu mama Halima huwa anakutaka siku nyingi lakini wewe hufahamu kwasababu ya bize zako ila subiri nitamfundisha adabu"



    "Jamani Zai sasa tunaanza kuishije hivyo kwa visasi, unadhani Mimi nitakuwa na amani kweli siyo vizuri hivyo ujue"



    "Zaka sitaki uniingilie maamuzi yangu au unampenda na wewe eti"



    "Aaaaah! Sasa mama watoto huko unafika mbali eeeeh! Mimi nakupenda wewe tu hao wengine wa nini sasa kwanza jitazame ulivyoumbika mithili ya malaika aliyesahaulika duniani, wewe kwangu ni sawa na mwezi nyakati za giza totoro eeeh! Mama nikikuacha wewe unaevutia kama jua lichomozapo nitampata nani?, achana nao hao watakutia wazimu bure malkia wangu"



    Nilimbembeleza kwa mane no laini mpaka akakubali kumuacha mama Halima, kweli niliamini ule msemo unaosema hakuna msichana mgumu mbele ya uongo na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Zai alitulia kama mtoto mdogo.



    Alianza kunisimulia maisha ya kwao jinsi wanavyoishi na shughuli zao za kila siku kiukweli hayakuwa na utofauti na Maisha yetu japo tulichotofautiana ilikuwa ni chakula tu,Tuliongea mengi kuhusiana na maisha akiwa ananisitiza sana kufuata masharti kwasababu anataka kunifanya mtu mkubwa yaani tajiri asiyeelezeka.



    Nilipitiwa na usingizi wakati wa maongezi, nilianza kuota ndoto nipo sehemu yenye majumba ya kifahari nikiwa na Zai akawa ananionesha mandhari tofauti tofauti na nilimuuliza ni wapi kwani hata katika runinga sijawahi kuona majengo ya namna hiyo ya kipekee tena yenye mapambo rukuki, hakika yalipendeza mpaka nikawa na hamu ya kuishi huko.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alitoa tabasamu murua kabisa likiambatana na jibu kuwa ni nyumbani kwao,niliishiwa pozi sikutegemea hata siku moja kama naweza kuja kufika ujinini kutokana na habari nilizowahi kusikia kuwa ujinini kunatisha na hata watu wa huko nilisikia hawaeleweki japo sikufanikiwa kuwaona lakini mmoja tayari nilikuwa nae ambaye ni Zai mwenyewe.



    Tulisimama mbali kidogo na jumba moja la kifahari kuliko yote akaniambia pale sasa ndiyo kwao kabisa na ndipo mfalme Zutasha anapoishi na malkia wake Suraiya, akazidi kuniambia sipaswi kufika pale mpaka nitakapokuwa naenda kutambulishwa na kufunga ndoa hiyo ndiyo itakuwa tiketi yangu ya kutalii katika jumba hilo la kifahari.



    Tukiwa hapo tunatazama jumba hilo linalopendeza Zai alistuka kama amehisi kitu akaniambia turudi duniani, nilistuka kama nilietoka ndotoni nikamkuta Zai ameweka kidole mdomoni



    "Shhhhhhhhh!!, njoo hapa karibu yangu nikuoneshe"



    Sikuwa mbishi niliinuka kiuchovu mpaka pale alipo

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog