Search This Blog

JINI ZAITUNI - 4

 





    Simulizi : Jini Zaituni

    Sehemu Ya Nne (4)



    Kioo kilishushwa nilipokaribia na nilipofika kabisa nilizidi kubaki mdomo wazi, lilikuwa ni tabasamu laini kutoka kwa Zai na macho ya kunihadaa

    "Mbona unashangaa hivyo Zaka au huamini kama ni Mimi?"



    "Siyo kwamba hayawezi kuisha la hasha! Ila nahisi unayapenda haya Maisha au unataka nikuache kwenye jumba lako hili la udongo etii?" Yaani sikuwahi kufikiria kwamba siku moja nitakutana na mrembo mbishi namna hii loooh! Nilijuta kufahamiana nae japo nilivumilia tu 
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    "Sijui nikuhakikishiaje kuwa nimeyachoka maisha haya lakini kuomba kwangu msaada ni kithibitisho tosha kuwa sihitaji kuishi hivi kwahiyo usichukie kwasababu sisi binadamu si wakamilifu katika kila jambo tunalolifanya" 


    "Yameshaisha Zaka lakini usiwe unanikasirisha hivyo ili uone sirika yangu huwa sirudi nyuma nikishatoa maamuzi hivyo chunga" nilishusha pumzi kusikia yameisha lakini akili ikanituma niwe mpole ili nifanikiwe la sivyo nitajutia milele nafasi adimu niliyoipoteza 


    Siku hiyo nililala nikiwa na amani tele nikiwa na hamu ya kutumia ile shilingi mia tano niliyopewa kama kianzio.Asubuhi na mapema niliamka nikiwa peke yangu ndani kwa kuwa kulikuwa bado hakujapambazuka vizuri nilitulia ndani nikiwa bado nina shauku ya kutaka kujaribu ile hela.


    Nilipiga hesabu ni wapi niende kujaribia hela yangu baada ya kuitoa katika sanduku kama nilivyoelekezwa, wazo langu likatua kwenye mikate ile mikubwa huwa naisikia tu kwa wateja wetu wanaiita lesi lesi ambazo zitakuwa kitulizo cha njaa niliyonayo.


    Nilifanikiwa kufika katika duka moja kubwa la mtaani kwetu nikaulizia mikate ile, Nilipopewa nikaanza kujishauri. Nikastukia nimeropoka 


    "Samahani bosi unanidai shillingi hapa"


    "Jumla ya vitu vyote ni shillingi elfu sita tu bosi wangu"


    "Anhaaaa! Ok, aaaah! Sawa, sasa kwani na hizo dawa za mbu bei gani?"


    "Shillingi elfu tano tu bosi wangu nikupatie?"


    "Hapana ila na viberiti bei gani bwana?"


    "Ni shillingi mia mia tu bosi ila dazani utanipa mia tano tu."


    "Sawa, alafu siku hizi mnauza na redio humu etii?"


    "Bosi wangu acha masihala bhana wakati unaona kabisa hili duka ni la vyakula sasa iweje niuze redio ama runinga?" Niliuliza maswali ambayo hata mtoto mdogo angeulizwa angetoa majibu kwa kuliangalia tu hilo duka lenye bidhaa mbali mbali hasa vyakula hiyo yote kwasababu ya kuogopa kutoa ile hela yangu.


    "Eeeeh! Aaah! Kweli nimejisahau tu bosi wangu samahani kwa hilo" nilianza kuomba samahani nikiwa bado na maswali kichwani nitaanzaje kumpa hii mia tano kwa vitu vyote vile.


    Nilibaki nimeduwaa wateja wakizidi kuja na kutoka mpaka nikaulizwa tena 


    "Bosi bado hujalipia unasubiri nini au kuna kitu kingine nikuongeze?"


    "Ha...pa...na, ila kuna kitu kimoja nahisi nimesahau sasa najiuliza lakini sikumbuki" niliongea kwa kigugumizi uongo unaofanana na ukweli


    Nilijiwazia peke yangu sikuwa na lakufanya nikaitoa ile mia tano nikamkabidhi muujazi, Alianza kutabasamu kwa muda kisha akaangua kicheko huku akiangalia ile hela.........


    "Aaaah! bro unatisha siku hizi na misimbazi yako yaani toka wiki iliyopita ulipovuna mapesa mpaka Leo hii bado unatanua tu si mchezo aiseee! 
    "Kawaida mbona bosi sema tu najibana sana ndo mana siishiwi mapema." Moyo wangu ulitulia baada ya muujazi kuniambia ni elfu kumi hapo nikapata na amani kidogo
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Nilipewa sarafu na noti kama chenchi nilipotaka kuziweka mfukoni niliisikia sauti ikijirudia kichwani nwangu ikisema"Zaka haupaswi kutumia hizo sarafu mpe huyo au fanya kama umeangusha uziache."


    Mmmmh! Niliguna peke yangu mpaka muuzaji akaniangalia "vipi bosi mbona unaguna peke yako kulikoni au nimekuzidishia chenchi?"


    "Hapana ila mbona wewe unawaza kuzidishia watu ila hauwazi kuwa labda umemuibia mteja chenchi yake?"
    "Si.. Si.. Kwa..mba....si..a..mi..ni..i..la....." Nilikatakata maneno ni kama nina kigugumizi kwa mshangao ulionipata hadi nikashindwa kuendelea kuongea
    "Heheheeeeee!! Hilo lako babu weee kumbe ujanja wote huo ila kitu kidogo kinakubabaisha hivyo" niliambulia kicheko cha Zai kama unavyoelewa wanawake kwa utani wao. Ikabidi nijikakamue kuongea ili nisionekane mwoga mbele yake japo ulikuwa ni udhaifu wangu kwake toka mwanzo
    "Aaaah! Mrembo ni mstuko tu sikutarajia kama utanifanyia sapraiz kubwa kiasi hiki sikutegemea kiukweli" nilianza kutoa hotuba kwa Zai kama mtu vile huku moyo ukijitahidi kutaka kutokea kwa nje
    "Aiseee! Lazima ustuke maana nimekuja kivingine kabisa tofauti na ulivyodhania"
    "Ni kama ulikuwepo maana Mimi nimezoea kuona umeshafika kama si nyuma yangu basi ni karibu yangu"
    "Ni kweli ila kwa sasa hivi itabidi uzoee hali zote"
    "Sawa lakini hii ya Leo ni mpya kabisaaa"
    "Usijali Zaka wangu huu ni nwanzo tu na kama ni mziki basi ndiyo unatungwa hivi"
    "Nashukuru kipenzi changu kwa kuniingiza katika ulimwengu mpya"
    "Aaaah! Zaka si wakati wake kwani bado mapema mno kufanya hivyo hata hivyo nipo kwaajili yako tu"
    "Mimi sina neno zaidi ya kusikiliza na kufuata kile unachosema"
    "Ooooh! Kama ni hivyo basi tuanze safari au hujajikamilisha?"
    "Nipo tayari toka jana wangu ni wewe tu na amri yako jemedari wangu" niliongea kwa utani zaidi nikiongeza vionjo kadhaa kwani mrembo yeyote au hata mpenzi wako kama hamna utani basi hilo penzi litadumaa miaka yote haliwezi kukua na hiyo itasababisha kuchokana na mwisho wa siku mtaachana kabisa.
    "Zunguka mlango ule tuondoke" lakini sikufanya hivyo bali nilisogea katika mlango wa dereva nikaufungua kisha nikamkaribisha malkia wa moyo wangu aingie ndani na alipofanya hivyo nami bila ya kuchelewa nilizunguka mlango unaofuata na safari ikaanzia hapo.
    Gari yetu ilisimama nje ya geti kubwa katika jumba moja la kifahari ambalo kwa kulitazama tu utajua kuwa mmiliki ni mtu mwenye pesa sana. Zai alitoa kiongozi cha geti hilo na kubofya na Mara moja nikaona geti lile likifunguka taratibu na kuacha uwazi wa kutuwezesha kuingia ndani, Roho yangu ilitamani kujua vilivyomo humo ndani pia nilitamani sana kujua tumefikia kwa nani?
    Vinyweleo vilinisimama baada ya gari kupaki nikaambiwa nishuke,nilipokanyaga chini palipotengenezwa vizuri nikagundua kuwa sikuwa na hadhi ya kuwa humo ndani hali iliyopelekea joto la mwili wangu kuanza kupanda.
    Nilijiuliza mengi hasa hili kwamba watu waliomo humo ndani watanionaje muonekano wangu maana nilionekana wazi ni wa shambani huko kwani yeye Zai alikuwa amependeza kama mwanamitindo fulani ambaye ni wa daraja la juu mno
    Zai alikuja kunishika mkononi akiwa mwingi wa tabasamu lililozidi kumpendezesha haswa
    "Zaka karibu na ujisikie upo nyumbani kwako"
    "Mmmh! Mbona unasema nijisikie nipo nyumbani kwangu kwani humo ndani hakuna watu?" Nilimuuliza swali lililoutesa ubongo wangu kwa kitambo kifupi toka niingie humo ndani
    "Swali nzuri, hapa ni makazi yako mapya na ndiyo Maisha yako mapya kwa ujumla pia humu ndani utaishi wewe na mimi tu hakuna mtu mwingine"
    "Unasema kweli Zai?" Niliuliza bila kujiamini
    "Hakika ni kweli ninayo yasema."
    Moyo ulilipuka kwa furaha iliyochanganyikana na machozi, sikuficha hisia zangu nilimkumbatia Zai kwa nguvu huku kilio kikiongezeka Zai akawa ananipiga piga mgongoni kunituliza, nilimuachia nikapiga magoti chini nikimshukuru hata muumba kwa kunifikisha pale nikazidi kulia nikiwa nainuka nilipokuwa nikamkumbatia tena Zai.
    Tuliingia mpaka ndani nikaonyeshwa mazingira yalivyo nikiwa natembezwa kila chumba na baada ya hapo niliruhusiwa kuoga japo siku hiyo ilikuwa ya tofauti kwangu Zai alikuja bafuni kunisugua sugua kitu ambacho sikuwahi kufanyiwa hapo kabla.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Baada ya kuoga nilikuta nguo nadhifu zilizoendana na watu wazito(wenye pesa zao) nikazivaa na kuongozwa moja kwa moja na Zai sehemu ya kulia chakula. Nilishangazwa na vyakula vile ambavyo sikujua vimepikwa saa ngapi na Zai na aliandaa saa ngapi maana nilikuwa nae karibia mda wote.
    Siku hiyo ilikuwa ya vichekesho na vituko sana kwa Zai kila aliponiangalia kwani sikuwahi kutumia uma wala visu kukata na kula sasa ikanibidi kutumia mikono na zile juisi zilipata kazi siku hiyo maana nilimaliza jagi nzima hata vile vyakula nilikula karibia vyote mpaka nikahisi kuvimbiwa.
    Zai hakuwa na neno zaidi ya kucheka ninavyofanya maajabu yangu.......


    Nilipomaliza kula loooh! Nilikuwa nimeongezeka uzito kwani sikuweza kuinuka kirahisi na hapo ndipo aibu zilinishika baada ya kuangalia mezani palivyo chafuliwa kwa fujo zangu.
    Zai alikuwa ananiangalia tu hakuwa akishughulika na chochote zaidi ya kucheka na kutabasamu kwa vitimbi nilivyoonyesha siku hiyo, aliamua kuinuka akanifuata nilipo akaanza kuninawisha mikono japo mimi sikuwa na muangalia kutokana na aibu kuu niliyoionesha kwake tena ingekuwa afadhali kama ni mwanaume nwenzio lakini kwa mwanamke ni aibu isiyoelezeka.
    Tuliingia chumbani kupumzika Zai akiwa amevaa nguo laini za kulalia ambazo zinaonyesha umbo lake halisi,nikawa na kazi ya kumtazama jinsi alivyopendelewa katika uumbaji. Hakika nilitamani kuweka historia siku ile ya kufungulia nyumba ya gharama namna ile na pamoja na kupata penzi la Zai kwa siku moja.
    Lakini haikuwezekana kutokana na umahiri niliouonesha mezani mpaka nikawa najilaumu kwanini nilikula kwa papara vile bila kufikiria,sikuwa na jinsi niliamua kuutafuta usingizi japo tumbo lilikuwa linauma kutokana na mzigo mzito kulielemea.
    Asubuhi ya siku hiyo niliamshwa na Zai jambo ambalo sikulizoea hapo kabla,alinibusu katika paji la uso
    "Umeamkaje mpenzi wangu" alinisabahi baada ya kunibusu
    "Salama tu mama watoto sijui wewe u hali gani?"
    "Mimi ni mzima wa afya kabisa pole na uchovu"
    "Mmmh! Uchovu upi tena mbona sikufanya kazi yoyote"
    "Aiseee! Kweli nimeamini wewe ni msahaulifu kwani ulivyolala uliota nini?"
    "Mmmm! Aaaah! Ni ndoto ya kawaida tu"
    "Zaka acha kudanganya,uliota nini Jana?" Aliweka mkazo lakini si kwamba nilishindwa kumwambia ila aibu zilinitawala mno
    "Ile ndoto Zai ni kama ndoto nyingine tu hivyo usiwe na wasi wasi" nilizidi kujitetea
    "Hivi Zaka jamani usiponiambia mimi mkeo mtarajiwa utamwambia nani sasa kama hilo jambo ndogo tu unashindwa kusema"
    "Ni kweli ni jambo ndogo kwako lakini kwangu ni kubwa"
    "Basi na mimi siondoki mpaka uniambie uliota nini mpendwa" nilikuwa nimekamatika kwasababu mimi naelewa kuwa waswahili wanasema ndoto uliyoota usimuhadithie mwenzio ila Zai alikuwa ameniganda kama nini?
    "Zai sikiliza kwa makini Mimi niliota nipo katika kitanda kimoja cha kifahari japo hata chumba kilikuwa cha ghali mno na sikuwa peke yangu bali na wewe hapo,ila kilicho nishangaza tulikuwa katika mechi na nadhani ilikuwa fainali maana mchuano ulikuwa si wa kitoto kama zilivyo mechi nyingine. Hiyo ndoto ndiyo niliyoota"
    "Ha! Ha! Ha! Ha!" Zai alikuwa ananicheka
    "Sasa unacheka nini? au ni mazuri hayo kwasababu ndoto hata haichekeshi" nilianza kukasirika baada ya kuona Zai ananicheka
    "Haichekeshi ila umenifurahisha ulivyokuwa unaficha ficha ni kama vitu vya ajabu"
    "Ina maana Zai wewe unaona ni kitu cha kawaida hicho tena unavyoniona hapa nina mchoko hata sijiwezi ni kama ile mechi ilikuwa ya ukweli" nilizidi kumsisitiza Zai kuhusu hiyo ndoto kwani yeye aliichukulia ya kawaida mno
    "Pole kipenzi changu kwa ndoto uliyoota na ni kweli kabisa siyo ya kawaida"
    "Nimeshapoa japo bado nina mchoko"
    "Sawa lakini nilikuuliza nikiwa na kusudio langu maalumu"
    "Lipi tena mbona unaanza kunitisha" nilistuka kusikia alikuwa na lengo lake kuniuliza niliota nini?
    "Umeuliza vyema,ile ndoto uliyoiota haikuwa ndoto kama ulivyofikiria wewe bali ni ukweli mtupu ila nilifanya vile kwasababu sikupenda haya mazingira tufanyie kitu kama kile." Alijieleza kwa upana ili nimuelewe lakini mimi niliona wazi kuwa anatania

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    "Zai acha utani mbona mimi nilikuwa nimelala na kama ingekuwa tumefanya kweli si ningekuwa katika ufahamu wa kawaida kuwa nilifanya hicho kitendo"
    "Mimi naona hatuaminiani ila vithibitisho ni viwili kwanza angalia kama umevaa chochote mwilini mwako." Nilijichungulia haraka ili nihakikishe anachosema
    "Ni kweli sijavaa chochote" nilimjibu kwa wasi wasi nikimuangalia usoni
    "Je, unakumbuka kama jana ulilala na nguo au mtupu?"
    "Nililala na nguo" nilimjibu upesi upesi
    "Vizuri,kithibitisho cha pili ni huo mwili wako unajisikiaje hapo ulipo?"
    "Ni mchovu mno kama nilietoka kutumika mda si mrefu sana" nilimjibu nikiwa nimeinamisha kichwa kwa aibu
    "Safi,kwahiyo umeamini nilichosema hapo mwanzo?"
    "Ndiyo,nimeamini na sina kipingamizi chochote" nilimjibu huku nikijaribu kumtazama usoni ambapo tulikutanisha macho ana kwa ana ila yeye aliyashusha macho yake chini kwa haraka
    "Zaka nilikuahidi kuwa kama utatimiza masharti yote nitakupa zawadi ya mwili wangu mara moja tu na ndivyo nilivyofanya ile jana na hutonigusa tena mpaka tuoane" aliniambia akiwa ameinamisha kichwa vile vile safari hii akiwa ananionea aibu mimi jambo lililofanya nitoe tabasamu la kuibia ibia
    "Nimekuelewa Zai sasa ni wewe tu kuniambia ni lini unaenda kunitambulisha ili nikuoe" niliongea hivyo kwasababu ile mechi ya jana yake ilikuwa adimu sasa Mimi nilitaka walau niirudie japo nilijiuliza kwa mfumo upi na jibu likawa ni kuoa tu
    "Zaka wangu kunioa si rahisi kama unavyofikiri kwani bado una mitihani mingi mbele yako"
    "Mmmh! Ina maana mitihani haijaisha tu!" nilimuuliza kwa mshangao
    "Ulifikiri umemaliza ile ilikuwa ya kwangu tu sijajua kama nyumbani watakuachia au la"
    Nilibakia mdomo wazi maana Mimi nilijua kuwa nimeukata sasa kusikia mitihani bado akili ikaanza kuvurugika kwasababu kama mitihani ya Zai ilinitoa jasho itakuwaje hiyo mitihani ya wazazi wake.
    "Zaka hayo mawazo yako yatakupa presha bure,si nimeshakwambia kuna walakini kati ya kupewa au kutopewa mitihani kwahiyo kuwa mpole" alinipa moyo kwasababu alijua ninachokiwaza
    "Kama watasamehe kunipa mitihani nitakuwa na amani tele"
    "Nitajaribu kuwaambia wakuache"
    "Nitashukuru sana mpenzi"
    "Zaka kifungua kinywa kipo tayari mezani hivyo inatakiwa ukaoge kisha uungane nami kupata chai na baada ya hapo nikakukabidhi ofisi yako na kukutambulisha kwa wafanyakazi wako kama bosi mpya"
    "Heeee! Ina maana kila kitu tayari imebaki ni mimi tu?" Niliuliza kwa mshangao maana sikutarajia kama nitaanza kazi mapema kiasi hicho
    "Ndiyo nataka uwe mzoefu mapema na kazi yako ndiyo maana nimewahi kukuandalia mapema hiyo kazi"
    Nilimkimbilia pale alipo nikamkumbatia huku nikitoa mabusu mfululizo mpaka Zai akanitoa kwa nguvu
    "Hebu wahi ukaoge bwana tunachelewa"
    "Nitaenda ila hautaki hata nikushukuru kidogo"
    "Kwani wewe Zaka uliwahi kusikia wapi kuna shukrani za aina hiyo"
    "Niliwahi kushuhudia kwenye runninga wapenzi wanavyopeana pongezi za kipekee kama nilivyofanya Mimi" nilimtania Zai wangu kwa mbwembwe
    "Mmmh! Aya baba watoto endelea kuiga siku moja yatakutokea puani"
    "Sawa nitakazana ili ufurahi mama watoto"
    Niliingia bafuni kuoga na baada ya dakika kadhaa nilikuwa nimeungana na Zai mezani kupata kifungua kinywa cha siku hiyo,kiukweli yale mapishi hayakuwa ya kawaida kwani ladha yake sikuwahi kuisikia na hata kuisimulia sidhani kama itaeleweka kwasababu ile chai ilikuwa imepikwa ikapikika ni kama sio ya dunia hii........
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Nilijitahidi sana nisifanye kituko kama cha jana hivyo nikawa nakula taratibu mno tena kwa umakini wa hali ya juu,Nilimsifia sana Zai kutokana na ufundi wake wa kupika mapocho pocho ambayo hata kama angekuwa ni mgonjwa asiye na hamu ya kula lazima angekula chakula kile kwa jinsi kinavyovutia kwa nje.
    Tulifika katika jengo moja kubwa na kujitoma ndani ikiwa ni sehemu yenye mandhari nzuri kiofisi na inayovutia kwa mteja yeyote anayetaka kuhudumiwa mahali hapo. Wafanyakazi walikuwa wawili sehemu ya mapokezi wote wakiwa wa kike na wenye mvuto japo hawakumfikia mrembo wangu Zai.
    Kila mtu alikuwa bize na majukumu yake ila walipotuona waliacha shughuli zao na kutukaribisha kwa nyuso za furaha mno,Zai alinitambulisha kama bosi mpya kwao,wao hawaku shangazwa na ujio wangu kwani taarifa walikuwa nayo na pia sikufanana na yule Zaka wa zamani maana nilikuwa nanukia pesa kwa mavazi na hata mvuto niliokuwa nao.
    Nilipelekwa mpaka katika ofisi yangu na kukabidhiwa majukumu yangu kama bosi wa kampuni ya usafirishaji wa bidhaa na vitu mbalimbali hasa nje ya nchi. Nilianza kazi siku hiyo kupitia maelekezo kadhaa kutoka kwa Zai na nilishangazwa na uwezo niliokuwa nao wa kutimiza majukumu yangu na kutambua baadhi ya vitu ikiwa ni siku yangu ya kwanza kabisa kuanza kazi hiyo.
    Nilikuwa najiandaa kutoka ofisini kwaajili ya kwenda kupata chakula cha mchana lakini kabla sijafanya hivyo nilipata mgeni,ni kawa sina budi kumruhusu aonane na Mimi kwani huyo ndiye mteja wa kwanza kutaka kuonana na Mimi tofauti na wengine waliomaliza shida zao mapokezi.
    Aliingia msichana mmoja mrembo mno mpaka mwili wangu ulisisimka,macho yakizidi kung'ang'ania kumtazama,fikra nazo zikamsujudu kwa urembo aliokuwa nao,ni kama mioyo yetu ilikuwa na uvutano au mawasiliano kwasababu Mimi nilivyokuwa namtazama yeye ndiyo kwanza aliacha mdomo wazi kwa mshangao licha ya hivyo vyote lakini hakuthubutu kuongea japo hatukufahamiana na ni Mara ya kwanza kuonana.
    Sikuwa na ujanja siku hiyo mbele ya mrembo kama yule hasa pale ambapo macho yangu yalitua kifuani kwa binti yule na kukumbana na cheni moja nzuri ya dhahabu iliyomkaa vyema,niliamua kuvunja ukimya kwa kumkaribisha aketi nae bila kusita aliitikia wito huo na kuanza maongezi
    "Habari yako dada?" Nilianzisha maongezi hayo kwa salamu
    "Safi,pole na kazi"
    "Sijapoa bado mpaka nitakapomaliza majukumu ya Leo" tulicheka kwa pamoja ni kama marafiki wa mda mrefu
    "Nafikiri wewe ndiye mhusika mkuu katika hii kampuni ya usafirishaji"
    "Haswaaa ndiyo Mimi sijui nikusaidie nini mrembo" nilimuuliza nikiwa hata jina sijamfahamu
    "Sawa,kwa jina naitwa Silvana ni mmoja kati ya wahusika wa kusambaza bidhaa mbalimbali nchini hivyo nimefika hapa kwaajili ya kuomba kusaini mkataba wa kusafirishiwa bidhaa toka nje ya nchi kuja humu nchini"
    "Haina tatizo unaweza kufika pale mapokezi utapewa mkataba uusome kama unakubaliana nao basi utakamilisha kila kitu huko"
    "Ahsante na nikutakie kazi njema" alinipa mkono kisha akaanza kuondoka mimi nikiwa namsindikiza kwa macho lakini ghafla alisita kuendelea akanigeukia
    "Samahani kama nitakuudhi,ningependa kufahamu jina lako"
    "Bila samahani Silvana nilisahau hapo awali kujitambulisha,niite Zaka itapendeza zaidi"
    "Una jina nzuri,pia nina ombi lingine kama hautojali"
    "Bila shaka unaweza kuendelea" nilijua naumbuka kama litakuwa swali kuhusu kampuni yetu hivyo nilajiandaa kuruka swali kama litanishinda
    "Naomba unipatie mawasiliano yako tafadhali"
    "Mmmh! Sawa" niliguna kwa mshangao maana isingekuwa rahisi yeye kuchukua namba yangu badala ya namba ya kampuni kitu ambacho kiliniongezea maswali lukuki kuhusu yeye.
    Silvana aliniaga huku akilifinya jicho moja kama wanavyosema wenzetu "kukonyeza" akizidi kutabasamu na Mimi nikafanya vivyo hivyo japo sikuwa nawaza sana kuhusu yeye au urembo wake.
    Nilienda kupata chakula cha mchana kisha nikarudi ofisini mwangu kuendelea na majukumu mpaka ilipohitimu saa kumi jioni ndipo nilifunga ofisi yangu nikiwaacha wafanyakazi wa mapokezi
    nilipofika nje nilishangaa kumuona Zai akiwa ameegemea gari yake akinisubiri sikushangazwa sana na ujio wake kwani nilifahamu wazi ni jinsi gani anavyonipenda lakini nilistaajabishwa na uangaliaje wake ni kama mtu ambaye ndiyo Kwanzaa tumeonana siku hiyo.
    Nilianza kujistukia kuwa labda amenigundua nilichofanyiwa ofisini Leo na Silvana nikazidi kusonga mbele kwa uoga na nilipomkaribia alitabasamu

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    "Umebadilika sana Zaka si yule aliyekuwa mvuvi kwa muonekano ulionao"
    "Mmmh!! Ninaonekanaje kwani mbona Mimi naona sina tofauti yoyote na hapo awali" niliongea nikiwa najitazama vizuri huku nikijigeuza kama mgombea umisi.
    "Zaka sasa hivi wewe niwa tofauti kwanza una mvuto kwa kila mtu anayekutazama na pili ni mtanashati wa nguvu ambaye mda si mrefu utaanza kusifika kila kona"
    "Inawezekana unayoyasema ila sina uhakika nayo" niliongea nikionesha mashaka kuhusu suala hilo
    "Zaka nikuambie mara ngapi kuwa kwangu umefika hivyo amna linaloshindikana mpenzi wangu bado hauniamini tu"
    "Nakuamini kwa vyote hivyo huna budi kujiuliza kama nakuamini kipenzi cha moyo wangu" niliongea kwa msisitizo baada ya kubaini kuwa hajatambua chochote kuhusu Silvana.....
    Tukutane tena Alhamisi pia ahsanteni wote mlionipa pole kutokana na afya yangu kwa sasa Mungu awabariki kwa mioyo mliyonayo.


    "Nakuamini kwa vyote hivyo huna budi kujiuliza kama nakuamini kipenzi cha moyo wangu" niliongea kwa msisitizo baada ya kubaini kuwa hajatambua chochote kuhusu Silvana.....


    Tulipanda katika usafiri aliokuja nao Zai,sikuwa najua kutumia vyombo vya moto kama gari na pikipiki hii ilinifanya niwe mtazamaji kwa dereva wangu Zai jinsi anavyoumiliki usukani vilivyo.


    Zai alitambua umuhimu wa mimi kufahamu kuendesha gari ili niendane na maisha hayo pia kupunguza ghasia za hapa na pale endapo mpenzi wangu huyu atakuwa ametingwa kwa namna moja ama nyingine.


    Nilimshangaa Zai kwani hakupitia nyumbani kama ilivyokuwa safari yetu baada ya kutoka kazini ila alienda moja kwa moja katika uwanja wa mpira kwaajili ya kunielekeza jinsi ya kuendesha gari.


    Nilifurahi sana kwasababu sikuweza kumwambia anifundishe kutokana na aibu niliyonayo pia nilikuwa ni mzito sana wa kusema jambo na mara nyingi huwa nahangaika nianzie wapi kusema kinachonisibu


    Mazoezi yalianza nikiwa najifunza taratibu na kwa vitendo zaidi na kwa bahati nzuri nilipata mwalimu muelewa sana kwani alinifundisha kwa vigezo maalumu na wala hakuwa mwepesi wa hasira,hii ilinifanya Mimi nielewe mapema mno kuliko hata alivyotarajia.


    Zilipita siku kadhaa Silvana akiwa anawasiliana na Mimi Mara kwa Mara mpaka ikafikia wakati tunatoka nae kula chakula cha mchana na mda mwingine huniomba nikapate kifungua kinywa nyumbani kwake lakini nilimkatalia kata kata ijapokuwa sikumwambia kama tayari nimeshaoa.


    Utajiri wangu ulizidi maradufu huku sifa na kufahamika vikiwa mbele kutokana na ukarimu,utanashati pia fedha nilizokuwa nazimiliki kupitia kampuni yangu ambayo hakuna hata mmoja aliyejua ni nani anayefanikisha hayo yote.


    Waswahili walisema pesa ni sabuni ya roho sio uongo kabisa kwani walitokea wadada warembo kupita maelezo wakinitaka niwe nao kimapenzi lakini niligoma kabisa kwasababu sikuwahi kuwaona kipindi cha nyuma ambacho nilikuwa hohehahe tena masikini wa kutupwa.


    Hata ofisini kwangu wafanyakazi niliokuwa nao walithubutu hata kuvaa nusu utupu ilimradi bosi wao niwaone lakini hauwezi kuamini machoni nilikuwa na pazia ambalo ni jeusi tii na nzito kiasi kwamba sikuona hayo yote wanayoyafanya mbele yangu. Ndipo niliamini Kuwa Zai ameniteka vilivyo na wala sikuwa na ujanja mbele yake.


    Nakumbuka siku moja nikiwa ofisini alikuja msichana mmoja mzuri wa wastani akiwa amevalia koti moja refu na la kisasa,nilimkaribisha kama mteja wangu lakini kadri sekunde zilivyozidi kuyoyoma ndivyo alivyozidi kurembua macho yakiwa yamemregea,ghafla akainuka kwenye kiti na kulitupa koti chini 
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Yalabiii!! Sikutegemea tukio kama hilo kutokea ofisini kwangu nikabaki nimekodoa macho bila hata kupepesa kope zangu,Yule msichana hakuishia hapo alikuja kukaa mezani akiwa na chupi tu na sindiria vilivyositiri nyeti zake hakika Mimi Zaka nilijuta kufahamika.


    Nikiwa katika sintofahamu ya nini nifanye nilighutuka baada ya kumuona yule msichana akiwa ameshazunguka upande ule nilipo lahaulaaa!! Kama ni upele ulikuwa umemfika mkunaji aliyebobea lakini kwangu ilikuwa kama sinema lililopambwa vizuri mbele yangu.


    Katika Maisha niliyowahi kuishi hata haya mapya ya kiutajiri sikuzoea starehe wala kuona vitu vya ovyo kama hiki kilichonitokea,yule mdada alifika mpaka nilipokaa akageuza kiti na kunikalia miguuni loooh!! Alipofanya vile nilijihisi kupaa kutokana na kutopata vitu hivyo kwa siku nyingi,


    Hali yangu ikiwa tete mda huo yule mdada alitumia udhaifu huo kwa haraka akailegeza tai na kuanza kufungua vifungo vyangu taratibu,nikiwa namtazama bila kufanya lolote la kunisaidia katika sakata hilo.


    Alifungua vifungo vyote nakuanza kunishika shika kifua akaona bado haitoshi akahamia kwenye zipu ya suruali yangu,baada ya kusikia zipu inafunguka ndipo akili ikanirudia sawia nilipiga yowe la hatariii kumuita Zai 


    "Zaiiiiiiiii....... Zaiiiiii......Zai......." sikumalizia kuita radi ilipiga katika pembe moja wapo ndani ya ofisi yule mdada akaniachia kutokana na kupagawa akiangalia kule ambako radi imetokea akiwa anapumua kwa kasi 


    Moshi mzito ulitanda ofisini kisha ukaanza kupungua hapo ndipo nilishuhudia Zai akiwa anatisha mno macho yake yakiwa mekundu kama nyanya zilizoiva kupita kiasi,akiwa amekunja sura akimuangalia yule mdada 


    Mimi nilikuwa natetemeka mno ni kama nimewekewa mtetemo wa simu ya nokia,ganzi mwili mzima huku nikiwa nashangaa Zai alivyokuwa kiumbe wa ajabu anaetisha mno ambaye sijapata kumuona hapo kabla.


    "A...a...a..na..ta...ka...Ku..ni...ba....ka" niliropoka bila kukusudia


    Zai hakusema neno zaidi ya kumkazia macho yule mdada,akatoka katika ile kona na kumfuata na kabla hajamfikia nilisikia kelele za mjeredi zikitokea kule aliko yule mdada huku akitoa kelele za maumivu makali na alama za mistari zikiwa zinapita kila sehemu ni kama mtu anayechorwa chata.


    Zai hakuwa na huruma nae hata chembe alichokifanya ni kumsogelea yule mdada na fimbo zikakoma hapo hapo,alimshika usoni kwa makucha yake akiwa anamfinya finya huku damu nyingi zikiwa zinamwagika,yule mdada akiwa anapiga kelele za kuomba msamaha.


    Zilipita kama dakika mbili akiwa anamfinya kisha akatumbukiza mkono mwingine kifuani na alipoutoa nilishuhudia akiwa ameshika kitu kinadunda dunda kwa ufahamu wa kawaida niktambua ni moyo ule.


    Nikiwa katika tukio la kusikitisha kama lile nikiwa naushuhudia ukatili wa Zai kwa macho yangu mawili kiukweli nilitokea kumuogopa sana Zai huku nikijiapiza kutovunja masharti mpaka kufa.


    Zai hakujali kama nipo pale alikula ule moyo mbele yangu kisha akatoweka na yule msichana,Nilikurupuka pale nilipo na kukimbilia katika mlango,nilipotoka nikakutana na wafanyakazi wakinitazama kwa hofu wakiniuliza kulikoni huko nilikotoka nakumbuka niliwajibu kuwa "hamjasikia kelele yoyote ile" wao wakajibu hakuna aliyesikia 


    "Msichana aliyetoka humu ofisini kwangu amepita hapa?" Niliwauliza nikiwa bado na kiwewe


    "Hapana bosi hakuna msichana aliyepita hapa,kwani ulikuwa na mtu ofisini?" Nilitupiwa swali lililozidi kuuchanganya ubongo wangu
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/--
    "Swali gani hilo mnaloniuliza kwani nyie si mmemruhusu dada mmoja hivi anione ofisini?" Na Mimi niliuliza swali ikawa ni swali kwa swali


    "Hapana bosi hatujaruhusu mdada yeyote yule kuingia ofisini kwako" jibu hilo lilinifanya nichanganyikiwe zaidi


    "Ooooh!! Sawa sawa Mimi naenda kupumzika hivi sasa kwahiyo mambo yote simamieni sijisikii vizuri kabisa" niliamua kuondoka kutokana na kuzidi kuvurugwa na majibu yao............


    Nilichukua usafiri wangu nikielekea nyumbani kwangu nikiwa siamini kile kilichotokea ofisini muda mfupi uliopita,nikiwa njiani nilikumbuka kelele za maumivu alizokuwa akipiga yule msichana nilishindwa kuvumilia chozi likinidondoka taratibu kwani lile tukio lilinitisha mno.


    Nilifika nyumbani nikapaki gari yangu na kuanza kuelekea ndani lakini kabla sijaufikia mlango ulifunguliwa na Zai akiwa katika tabasamu pana hali iliyodhihirisha ni mwenye furaha isiyo na kifani,nilisimama nikiwa namtazama usoni nakujiuliza maswali kuwa kwanini anafurahi wakati tukio lililotokea ofisini ni kubwa kuliko matukio mengine yaliyowahi kunitokea hapo nyuma.


    Sikutabasamu wala kuongea kutokana na msongo wa mawazo ulioletwa ghafla na matukio ya ajabu ajabu,mpaka nafika nyumbani pale nilikuwa sijielewi kama ni Mimi ndiye niliyaona Yale aliyofanya Zai au niliota na ukizingatia maelezo ya wafanyakazi wangu ndiyo yalizidi kunichanganya zaidi.


    Zai alikuwa ametanua mikono anikumbatie lakini Mimi sikuliona hilo kutokana na kuchanganyikiwa nilazidi kusimama nikimtazama lakini mawazo hayakuwa hapo nilipo nilikuwa mbali mno 


    "Zaka mpenzi wangu ina maana hautaki nikukumbatie jamani eeeeh!" Alikuwa ananisemesha lakini bado nilisikia huku vikatokea kule 


    "Zaka...Zaka....Zaka....weee Zaka si nina kuita Mimi" nilishtuka kusikia sauti ya ukali ya Zai nikama nimepigwa shoti ya umeme 


    "Hivi Zaka una mawazo gani mpenzi wangu mpaka unakuwa hivyo hata kunikumbatia hautaki au nimefanya vibaya kuja kukupokea hapa nje?"


    Aliniuliza maswali mfululizo na halo ndipo akili yangu ikazinduka nikakumbuka alichokifanya looooh!! Niliogopa hata kumsogelea pale alipo nikaanza kutetemeka upya nilipoikumbuka ile sura yake ilivyokuwa inatisha 


    "Zaka tafadhali njoo usiogope ni hasira ndiyo zilisababisha nikafanya vile njoo mpenzi wangu njoo" alianza kuniita akiwa ananibembeleza lakini sikuthubutu kunyanyua kiatu changu kusogea pale alipo 


    Aliniangalia kwa huruma papo hapo nikaanza kumfuata na kumkumbatia sikutambua amenifanyia kitu gani mpaka nikakubali kumsogelea kirahisi namna ile,Ilipita siku hiyo na asubuhi iliyofuata sikutamani kwenda kazini tena hivyo nikaomba wafanyakazi wangu wanisaidie shughuli mbali mbali mpaka pale nitakapojisikia kwenda.


    Nilikaa nyumbani siku mbili nikiwa na Zai na uoga ule ulinitoka kabisa kwani sikukumbuka lile tukio mara kwa mara na kila nilipolikumbuka na kutaka kumuuliza Zai nilisahau nakuanzisha mada nyingine tofauti.


    Ndani ya hizo siku mbili Silvana alikuwa ananijulia hali kila mara jambo ambalo lilizidi kuniweka matatani hasa nikimfikiria Zai japo yeye hakuonesha kujali hata kama nawasiliana nae nikiwa nae pamoja tukifurahia penzi letu.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Siku hiyo nilienda ofisini kama kawaida na utendaji wangu wa kazi haukushuka kiwango ila ulizidi kuwa bora zaidi,mchana nilitoka na Silvana kupata chakula cha mchana kisha kila mtu anarudi kazini kwake kuendelea na majukumu,nilishangazwa sana na Zai kwani alionekana kutokujua kabisa jambo hili na wala hakulitilia shaka.


    Siku zilizidi kusonga huku mahusiano kati yangu na Silvana yakishamiri vilivyo ikafikia wakati hata chai ya Zai sikuinywa nikiwa natoa sababu za kuwahi vikao na mengine mengi.Hakika niliona mabadiliko yangu waziwazi na kila nilipojaribu kujirekebisha na kujizuia nisiwe na Silvana haikuwezekana kabisa kumbe sikujua kilichopo mbele yangu mpaka nikawa vile.


    Zai hakuonesha tofauti siku zote hizo nilizoanzisha visababu vya ovyo ovyo bali alizidisha upendo kuliko ule wa awali mpaka nikawa najihisi vibaya lakini ningefanyaje wakati njia ya kujinasua sikuiona ikanibidi niwe nalia kimoyo moyo kusogeza hukumu yangu.


    Asubuhi moja nikiwa ofisini kwangu alikuja Silvana akiniomba niende nae mgahawani ili tupate chochote kuridhisha matumbo yetu nilimkubalia huku nikiwa nimeacha kazi nyingi ambazo toka niwe karibu na Silvana nilikuwa mvivu wa kupindukia katika utendaji wangu wa kazi,


    Tulifika mpaka mgahawani na kupata chakula ambacho tulitumia muda mrefu kukimaliza,kwa muonekano tulifanana na wapenzi walioshibana lakini haikuwa hivyo kwani hakuna aliyemtamkia mwenzie kuwa anampenda.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog