Search This Blog

JINI ZAITUNI - 5

 





    Simulizi : Jini Zaituni

    Sehemu Ya Tano (5)



    Tulifika mpaka mgahawani na kupata chakula ambacho tulitumia muda mrefu kukimaliza,kwa muonekano tulifanana na wapenzi walioshibana lakini haikuwa hivyo kwani hakuna aliyemtamkia mwenzie kuwa anampenda.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Haikuwa kawaida Silvana kupitia kazini kwangu baada ya kazi hiyo ilikuwa mara ya kwanza ambayo siwezi kuisahau kamwe kwani ilikuwa ya kihistoria maishani mwangu.



    Alikuja Silvana akaomba nipitie kwake tupate chakula cha jioni moyo ulikuwa unasita mno kwenda lakini nilijishangaa mwenyewe nilivyokubali kiulaini kama mbuzi anayeenda kuchinjwa machinjioni,tulifika nyumbani kwake ilikuwa ni nyumba nzuri na ya kisasa tena kubwa cha kustaajabisha Silvana alikuwa akiishi mwenyewe.



    Nilisubiri chakula kiandaliwe na masaa yakizidi kuyoyoma mpaka giza lilipoingia sikuwa na wasi wasi maana nilijua nitawahi kurudi nyumbani. Nilipata chakula cha mrembo yule Silvana huku tukizungumza mambo mbalimbali ambayo hayakuhusiana na mapenzi.



    Nilipomaliza kula Silvana alinishauri nikaoge,nilikataa kata kata lakini haikusaidia kitu kwani huyu mrembo ni kama alikuwa na asali mdomoni mwake nilimsikiliza alichotaka bila kipingamizi.



    Nikiwa bafuni alinifuata akiwa na taulo tu liliomsitiri,sielewi siku hiyo nilipewa nini maana nilitimiza haja zake zote za kimwili nikiwa katika sintofahamu. Tulimaliza mambo yetu tukarudi chumbani kwake lakini mchezo ule wa bafuni haukukoma uliendelea tena safari hii ulikuwa na mashambulizi makubwa.



    Nililala fofofo nikiwa nimesahau kabisa kuwa Zai ananisubiri nyumbani na sikumtaarifu chochote tangu nimetoka kazini. Nilishtuka baada ya kuona mwanga mkali umetawala chumba kizima,ilikuwa ni cheni ile cheni niliyozoea kuiona shingoni mwa Silvana ndiyo hiyo hiyo iliyokuwa inawaka kwa mwanga mkali.



    Nikiwa katika mshangao ule Silvana alikuja akitokea chum a kingine akiwa uchi wa mnyama akaanza kuniambia maneno ambayo sikuyaelewa anaamanisha nini.



    "Zaka pole kwa kuingia katika himaya yangu,nafahamu kabisa kuwa hujui lolote kuhusiana na Mimi lakini nitakusimulia kidogo kabla ya saa sita kamili ninapokutoa kafara"



    "Kwa miaka mingi iliyopita niliamua kuutafuta utajiri na haikuwa rahisi kama unavyodhani,nilipiga moyo konde nikaamua kwenda Kongo huko nilipata utajiri niliokuwa nina utafuta kwa muda mrefu lakini kwa sharti la kutoa kafara baada ya miaka mitano kwa kijana ambaye ananyota ya utajiri." Niliduwaa nikijiuliza inahusiana vipi na mimi ila sikupata jibu yeye aliendelea



    "Nilikupenda kweli lakini kwa bahati mbaya huu ndiyo mwaka ninaotakiwa kutoa kafara nyingine na hakuna mwingine wa kumtoa kafara ni wewe kwa kuwa una hiyo nyota hivyo sinabudi kutimiza hili ndiyo maana nikafanya hayo yote ili kuutimiza upendo wangu kwako japo ninaumia,zimebaki sekunde chache kwahiyo jiandae na uwasalimie huko kuzimu unakokwenda."



    Nilitamani kulia lakini haikuwezekana nikaamua kuinuka kitandani kwa hasira nikamvamie Silvana lakini nilikuwa nimechelewa kwani nilipoinuka tu nilishuhudia ile cheni ikigeuka kuwa chatu mkubwa anayetisha



    Nilikaa chini bila kupenda jasho lilikuwa linanitiririka sio makwapani wala kwenye suruali kote huko nilisikia kumelowana chepechepe huku lile joka likiwa linatambaa taratibu kunifuata na Silvana akiwa ananipa tabasamu la kifedhuli...........



    Siku zote riziki ni popote na unachopata hata kama ni kidogo ndicho ulichopangiwa tafadhali usipite njia ya mkato kwani foleni ya mafanikio bado inakusubiri hata kama utapitia magumu mangapi ila bado ulichoandikiwa ndiyo utakachopata.





    Nilikaa chini bila kupenda jasho lilikuwa linanitiririka sio makwapani wala kwenye suruali kote huko nilisikia kumelowana chepechepe huku lile joka likiwa linatambaa taratibu kunifuata na Silvana akiwa ananipa tabasamu la kifedhuli...........



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikuwa na ujanja wowote wa kufanya ili niokoke katika hatari hiyo iliyo karibu yangu.Joka lile lilizidi kunifuata taratibu likiwa linaonekana lina uchu wa kunifanya kitoweo chake cha siku hiyo.



    Nilianza kurudi nyuma nikiwa natetemka mno hasa meno yangu yaliyokuwa na kazi ya kugongana ovyo ovyo bila mpangilio,nilipata wazo la kumuita mkombozi wangu ambaye niliamini ndiye tegemeo langu la mwisho la kuninusuru mahali hapo.



    Nilianza kumuita Zai lakini sauti haikutoka nikajaribu mara kadhaa lakini hali haikubadilika basi sikuwa na haja ya kuendelea kuita,wakati huo Silvana alikuwa akicheka kwa nguvu mno baada ya kuona sauti yangu haifiki popote zaidi ya kuishia kooni mwangu.



    Niliona kifo kikiwa jirani yangu kinapiga hodi nikajilaumu sana kwa ujinga niliofanya nikajiona ni mkosefu ambaye hakuhitaji hata kusamehewa,nikakumbuka masharti ya Zai nikifikiria huenda siku zingerudi nyuma ili nikwepe mahusiano na Silvana



    Ila tayari nilikuwa nimechelewa kufanya hivyo na hapo ninge..... akawa ndiye mfariji wangu,sikujiuliza mara mbili nilianza kutubu makosa niliyonayo kwa Israeli huyu aliyekuwa akinisogelea bila huruma huku nikiamini siku ya kufa nyani miti yote huteleza na hiyo ndiyo ilikuwa siku yangu.



    Nilirudi nyuma nikiambatanisha na sala zisizokuwa na imani hata chembe kwa kile ninachoomba mpaka nikaufikia mwisho wa kitanda ikiwa ni ukutani kabisa,Joka likiwa linakuja taratibu na safari hii lilikuwa likitambaa kitandani kwa nyodo zote ni kama simba aliyeona windo lake katika kichaka.



    Nilikaa tayari kunyakuliwa na malaika mtoa roho nae hakungoja hata sekunde alinifikia nilipo. Nilifumba macho baada ya kuona joka limenyanyua kichwa juu kujiandaa kushuka katika kichwa changu huku lilitanua domo kubwa na kujiweka sawa kama linalongojea amri.



    Wakati nimefumba macho nikisubiri kumezwa nilisikia kishindo ukutani kikitokea ukutani ni kama tetemeko la ardhi lililoitikisa nyumba imara namna ile nikafumbua macho upesi kutazama kishindo kilipotokea tobaaaaa!! Sikuamini nilichokiona nikijua nimuujiza umenitokea kwani lile joka na ukubwa wake wote lilikuwa likivuja damu kila sehemu ya mwili wake.



    Niligeuka tena nimtazame Silvana loooh!! Nilikutana na sura ya kutisha ikiwa inapambana vikali na Silvana kumbe hata Silvana hakuwa haba kwani aliuhimili ule mpambano vilivyo kwa kutumia kila staili ya uchawi aliokuwa akiufahamu.



    Walipambana sana Mimi nikiwa mtazamaji japo sikuwa sawa kutokana na woga ulionitawala nilikuwa nimeloa mkojo suruali yote ukijumlisha na jasho lilivyokolea mwilini nikawa kama mtu aliyenyeshewa na mvua.



    Hatimaye Silvana alikabwa kooni na kuning'inizwa juu akawa anatapa tapa huku na huko akiirusha miguu kwa nguvu mpaka pale alipotulia kabisa ndipo alitupwa chini na jitu lile la kutisha. Silvana alipotupwa chini lile jitu lilitoa msonyo mkali kisha likanigeukia Mimi.



    Sikuwa na lakufanya zaidi ya haja kubwa kufuatia nilipoishuhudia ile sura inavyotisha meno yakiwa yametokeza kwa nje na mikono ikiwa na kucha ndefu zilizojaa damu. Nilikuwa nikitetemeka tu hata ile harufu niliyochafua mazingira sikuisikia kabisa.



    Jitu lile la kutisha lilisogea mpaka karibia na kitanda kisha likaanza kurudi katika umbo dogo tena umbo la kibinadamu,umbo ambalo limezoeleka kwa kila binadamu japo kwangu umbo hilo lilifanana kabisa na umbo la Zai.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Macho yalinitoka pima kuona kiumbe kile cha ajabu na kinachotisha ni Zai kipenzi changu ambaye kwa muda huo sikutakiwa kumuita mpenzi kutokana na usaliti nilioufanya hapo awali.



    Niliinamisha kichwa kwa huzuni kuu nikijiuliza kifo ninachostahili kupewa kama mkosaji ukilinganisha na vifo nilivyo vishuhudia nikiamini kuwa kifo changu kitakuwa cha uchungu kuliko watu wote waliowahi kufa.



    Zai alirudi katika umbo lake kamili tena akiwa anatabasamu kama kawaida yake pindi anapo nitazama,nilizidi kuinama machozi yakaanza kudondoka nikiwa na uchungu kwa kile nilichokianzisha na Leo ndicho kinanimaliza.



    "Hatimaye nimefanikiwa kukupata tena mpenzi wangu Zaka" ni maneno ya Zai yaliyofungua ubongo wangu na kuuchoma vilivyo moyo wangu,sikujibu lolote zaidi ya kubaki tuli kama maji ya mtungini.



    "Nimehangaika mno kukutafuta lakini sikufanikiwa na nilipokata tamaa ya kukupata ndipo nikaisikia sauti yako ikiomba msaada ikiwa kwa mbali sana na hapo ndiyo nikatambua ulipo" aliongeza Zai ndipo na Mimi nilinyanyua kichwa nikimtazama usoni



    "Nimetambua yote sasa kuwa hili si kosa lako kwani huyu msichana alikufunguka wewe na Mimi pia ili ukawa haujielewi japo hata Mimi sikutambua chochote kinachoendelea kati yenu" nilishangazwa na maneno hayo kwani nilijua mwenye makosa ni Mimi kumbe la hasha! Si Mimi ila Silvana



    "Pole sana mpenzi wangu kwani hiyo ni mitihani ya Maisha hasa katika mahusiano ya watu wawili hakukosi vita,visa,chuki,usaliti na mengine mengi ila kuwa imara katika mapenzi yenu ndiyo ushindi wa hayo yote hivyo hauna sababu ya kujilaumu ukidhani wewe ni mwenye makosa" Alizidi kuongea maneno mazito yaliyonigusa mno



    "Tafadhali Zaka bado nina kuhitaji katika maisha yangu nakuomba urudishe amani uliyokuwa nayo mwanzo"



    Nilianza kushawishika na maneno yake na ni kweli Zai nilitokea kumpenda mno kwa kipindi chote nilichomzoea hivyo haikuwa rahisi kwa msichana yeyote kubadili nafasi yake moyoni mwangu lakini nilikosa amani kutokana na lile umbo na sura ya kutisha aliyoionesha pale alipokuwa akipambana na Silvana japo yote aliyafanya kwasababu ya kuniokoa.



    "Zaka nitazame ninavyoumia kwaajili yako,ninavyopambana kwaajili yako,ninavyojitoa kwako,ninavyokupenda mwenzako,tafadhali usiniache mpweke,nakuomba unifute machozi,uniliwaze chumbani,nyumbani na kila niendako Zaka tafadhali nakuomba." Alizidi kuongea Zai lakini sikuwa na ham ya kumtazama tena nilikuwa nimejiinamia



    "Zaka lile ni umbo langu halisi hasa nikiwa na hasira sana lakini nakuahidi kama utakubali kuendelea kuwa na Mimi hata sikumoja siwezi kubadilika namna ile mbele yako"



    Nilishindwa la kufanya kwasababu nikimkatalia ninaweza kuurudia ufukara na nikikubali nitaendelea kuwa tajiri lakini hata moyo wangu ulikiri kumpenda Zai lakini niliona aibu kusimama kutokana na uchafuzi niliofanya katika suruali yangu.



    Zai alikuwa mwanamke wa kipekeee ambaye hakujali hali niliyonayo ila ndiyo kwanza alinishika mkono kunitoa kitandani mpaka nikasimama Kisha akanikumbatia kwa nguvu sana huku machozi yakimtoka



    Nilishindwa kuvumilia harufu ile japo mwenzangu hakujali kabisa akazidi kunikumbatia huku akisema kwa msisitizo neno"NAKUPENDA SANA ZAKA"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilijisikia furaha sana na mwenye bahati kupindukia niliposikia akinitamkia hivyo nami nikarudisha"NAKUPENDA PIA ZAITUNI" kitendo kilichosababisha nikumbatiwe zaidi na zaidi.



    Nyumba ya Silvana iliwashwa moto na Zai kisha tukapotea kwa namna ya ajabu ikiwa ni mara yangu ya kwanza kupotea sehemu moja ndani ya dakika na kutokea sehemu nyingine ambayo ilikuwa ni nyumbani kwetu yaani Mimi na Zai.



    Asubuhi militia taarifa ya kutokwenda kazini ili niifurahie siku hiyo na kipenzi changu Zai kwani bila yeye nisingeiona siku hiyo.



    "Zai mpenzi nina habari nzuri sana kwako Leo hii,unaweza kuotea tafadhali?"



    "Mmmh! Aaah! Ndiyo nahisi unataka kunivisha Pete ya uchumba"



    "Ha! Ha! Ha! Ha! Umejaribu kidogo sasa hakuna nafasi ya kurudia ila naomba unipe mji nitakaoupenda ili nikuambie ni habari gani hiyo."



    "Ooooh! Sawa mimi napendelea uende ujinini ukaione nyumba ya mfalme"



    "Nitaenda kipenzi changu,jibu ni kwamba niko tayari kukuoa kuanzia sasa uwe mke wangu wa ndoa"



    "Weeeeeee!! Usiniambie Zaka wangu" aliinuka kutoka kwenye sofa akija kwangu na Mimi niliinuka haraka Zai akawa amenirukia kwa furaha isiyo na kifani akinishushia mabusu mfululizo,nikapata wasaa wa kupata kile kinywaji chenye ladha adimu wenzetu wanaita "denda".........



    Usiishi kwa kukariri kama unavyoishi siku zote bali jaribu kuangalia ni mtindo upi wa Maisha utakufaa na utaendana na dhamira yako ya kweli uliyonayo. Ishi kwa malengo kwani malengo hutimiza ndoto ya mda mrefu,Jifikirie mara mbili kisha chukua hatua.





    Ukweli ulibaki pale pale kwamba huenda nikimuoa kabisa Zai basi majaribu yatapungua na inawezekana ulinzi ukaongezeka mara dufu nikaishi kwa amani kipindi chote cha Maisha yangu.



    Zai alitosheka na kinywaji kile adimu,tulienda kutembea ufukweni ikiwa ni mara yangu ya pili kwenda na Zai japo mwanzo nilienda bila kupenda lakini safari hii niliridhia kabisa kwenda nae.Ilikuwa ni kama tumeonana mara ya kwanza katika mapenzi yetu kwa jinsi muonekano wetu ulivyokuwa.



    Hata wewe mpenzi msomaji ukitaka mapenzi yenu yadumu jitahidi kuwa mbunifu katika mapenzi sio kila siku unaenda na mtindo ule ule hakika penzi lenu litakuwa halina mashiko nikiwa na maana litadumaa na hatimaye mnaanza kuchepuka ili kupata ladha tofauti za mapenzi tofauti na yale uliyoyazoea.



    Nilijitahidi sana kumuonyesha Zai upendo nilionao kwake ijapokuwa yeye alikuwa jini lakini hakukosa dhaifu za mwili wake katika mapenzi,ilikuwa ni siku njema kwangu na yenye mvuto wa hali ya juu kwani Zai alifanya kila aina ya miujiza ilimradi nifurahi nikiwa na yeye.



    Alikuwa akibadilisha miguu yake anakua kama nguva huku akiruka kama samaki kutoka ndani ya maji kiukweli alikuwa akinishangaza kwa uwezo wa ajabu aliokuwa nao. Tulikaa sana ufukweni hapo tukifurahia uwepo wa kila mmoja katika Maisha ya mwenzake.



    Usiku wa saa moja tulikuwa nyumbani tunapata chakula huku Zai akiwa anasisitiza kuwa ni lazima aende kuwataarifu wazazi wake kabla hatujaenda na aliniambia kwamba inatakiwa kila kitu tumalize siku hiyo ili siku inayofuata iwe ni sherehe tu kule ujinini na baada ya hapo tutarudi duniani kufanya sherehe nyingine.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zai alikuja usiku wa saa sita akiwa amependeza vilivyo katika gauni moja ndefu lililochora vyema umbo lake linalofanania na wagombea umiss.Alivutia mno ukichangia na uzuri aliokuwa nao kwani kila sekunde alionekana uzuri wake unaongezeka hakika jini ni jini tu na hapo ndipo niliamini kwasababu hata gauni lake halikuwa na rangi moja bali zilibadilika badilika kila baada ya sekunde kadhaa.



    Alikuja na nguo kama za mfalme Fulani ambazo duniani hazipatikani kabisa na zilikuwa katika mtindo wa joho refu ambalo halikunichosha kulitazama. Wanasema mgema akisifiwa hali wali mkavu ila kwa Mimi nilianza kujisifia kabla ya kusifiwa na Zai nilivyokuwa nimeng'aa na kama ingetokea mashindano ya mavazi basi ningeibuka mshindi siku hiyo.



    Safari ilianza ya kwenda ujinini ambayo haikuchukua muda mrefu tukawa tumefika,zulia lilikuwa limetandikwa ni kama anayesubiriwa ni Raisi,watu walikuwa wamejaa mno milio ya kila aina za vigeregere ikisikika mbele yetu kukiwa na viti viwili vikubwa vilivyopambwa vizuri huku pembeni kukiwa na mtu mzima wa makamo pamoja na mke wake hapo nikatambua kuwa ni wazazi wa Zai kutokana na kila mmoja kufanana na mtoto wao.



    Nilikaribishwa niketi Zai akiwa si muongeaji kama nilivyomzoea,baba yake alisimama na kuunyamazisha umati ule wa watu



    "Daliiim! Daliiim!" Nilimsikia akisema kwa sauti na umati ukiitikia



    "Zumbweeee! Mfalme Zultasha"



    "Leo ni siku njema katika falme yetu na yenye furaha hasa katika familia hii kwani Zai ametuletea familia mpya" alitulia akiutazama ule umati kwa muda na kuendelea



    "Haikutegemewa katika milki hii msichana yeyote kuolewa na binadamu wakiwa na maelewano mazuri kama ilivyotokea kwa binti yangu,tena hii itakuwa ni historia katika vizazi hadi vizazi"



    "Nampongeza tena na tena na ninafikiri wrote mnazifahamu mila zetu endapo binadamu ataoa kwetu au kuolewa"



    "Ndiyooo" watu walijibu kwa shangwe isiyoelezeka,nikajua wakati wa mtihani umefika.



    "Ni lazima apewe mtihani ila kwasababu binti yangu alimpatia mitihani mingine akafuzu atapunguziwa mtihani huo na kupewa wa kawaida ndipo tuendelee na sherehe ikiwa tu ataushinda mtihani huo."



    Nilianza kutetemeka lakini Zai akaninong'oneza kuwa mtihani aliuandaa yeye kwahiyo ni mwepesi nisihofu kabisa.



    Niliinuliwa na watwana wawili nikapelekwa katika chumba kimoja nikaambiwa mtihani umeanza na nilipofumba macho na kufumbua nilijikuta nipo jangwani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilitazama kushoto na kulia sikuambulia chochote niliporudisha macho mbele nilishangaa kuona mifupa mingi ya binadamu na kwa mbali alionekana mtu akiwa anakuja upande niliopo.



    Nilitazama kwa makini mpaka aliponikaribia loooh! Kumbe lilikuwa ni fuvu limeshika panga,nilianza kutimua mbio lakini nilikuwa pale pale kila nilijaribu kukimbia nakuwa pale pale nilipo.



    Niliamua kusimama nipambane kiume,lile fuvu lilipofika likauweka upanga sawa kuanza mapambano lakini kabla hatujaanza kufuana niliisikia sauti ya Zai ikiniambia mtihani wako ni kuchukua hilo panga.



    Nilikaa tayari kupambana lile fuvu likarusha mkono wenye panga kichwani kwangu nikatua chini,likarusha tena nikapita kwa chini ndipo lilipogeuka kwa kasi likiwa linazungusha mkono wenye panga usawa wa tumbo langu



    Sikufanya ajizi niliudaka ule mkono na lile panga nikatumia nguvu zangu zote za kupiga kasia mpaka ule mkono wa lile fuvu ukavunjika nikastukia nipo katika kile chumba na panga mkononi likiwa linang'aa sana.



    Watwana walinichukua juu juu na panga langu hadi kwenye ule umati,watu walishangilia mno huku Zai akifurahi sana kwa ushindi nilioupata tena wa bila jasho.



    Zililetwa Pete tukavishana na ikiwa ndiyo Mara ya kwanza kufungwa ndoa ya kihistoria kati ya binti mfalme na binadamu wa kawaida.



    Mama yake Zai alinipongeza sana huku akinipa usia kuwa nisimuumize mwanae kama wanavyofanya wanaume wengine na binadamu wengi wanaojisahau wajibu wao katika nyumba na katika mapenzi pia kama mke na Mme.



    Zai aliagiza mama Rehema aletwe katika sherehe ili aishuhudie ndoa yetu,nikaamini ule msemo unaosema muombee adui yako aishi miaka mingi ili ashuhudie mafanikio yako pale unapofanikiwa na ndivyo alivyofanya Zai hakumuua mama Rehema ili baadae aone tunavyofunga ndoa.



    Tulikaa siku tatu tukiwa tunasheherekea usiku kucha mpaka pale tulipopewa ruhusa ya kurudi duniani kuendelea na Maisha yetu ya kila siku. Nilipewa zawadi lukuki ambazo hata kuzibeba ilikuwa shida mpaka tukasaidiwa na watwana katika jumba la mfalme.



    Mama Rehema aliachiwa na sisi tulirudi nyumbani na kuanza kuandaa sherehe kubwa. Walihudhuria watu wengi mno wakiwemo wafanyakazi was kampuni yetu,ndugu na marafiki zao



    Ni sherehe ambayo ilichukua mamia ya watu japo hawakujua kinachoendelea kati ya Mimi na Zai. Mpaka sasa ninaishi na Zai vizuri na tunategemea kupata mtoto wa kwanza hivi karibuni



    Japokuwa nina muamini Zai lakini naogopa kukutana na majaribu mengine yatakayo hatarisha maisha yangu na kunifanya niishi kama digidigi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog