Search This Blog

UCHAWI WA KURITHI - 1

 



    IMEANDIKWA NA : ATUGANILE MWAKALILE





    *********************************************************************************





    Simulizi : Uchawi Wa Kurithi

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Huruma alikuwa ni binti aliyeishi na wazazi wake, katika maisha yake ya huku na kule akaanzisha mahusiano na kijana Kisu.

    Wakawa katika mahusiano, mwisho wa siku Huruma akapata ujauzito.

    Kwao wakamwambia apeleke mwanaume aliyempa ile mimba. Kisu akaambiwa akagoma, ikabidi Huruma aende mwenyewe kukaa kwa kisu.

    Siku zikasonga na kupita, na ile mimba ikazidi kukua na kukua, miezi ya kujifungua ikapitiliza na uoga ukamjaa Huruma kuwa mbona hajifungui, akataka kwenda hospital kujua sababu mumewe akamkataza.

    Ikabidi awataarifu kwao, nao wakamuhurumia kwakweli ikabidi wakamchukue na kumpeleka hospital.

    Huruma akafanyiwa operesheni na kujifungua mtoto wa kike.

    Mumewe alipoenda ilionyesha wazi hakufurahishwa na kitendo cha Huruma kufanyiwa operesheni, ila akajigeresha na kumpa pole. Kutoka pale wazazi wa huruma wakamchukua na kumrudisha nyumbani, wakamkanya kuhusu swala la kurudi kwa Kisu. Ila ni kama walipiga kelele tu kwani mtoto wao alishapenda.

    Mtoto wa Huruma alipofikisha miezi sita na kuonekana mwenye afya kabisa, Huruma akatoroka kwao na kurudi tena kwa Kisu, hakujali kutokuwajua ndugu zake na Kisu alichojali ni mapenzi yake.

    Baada ya kufika kwa Kisu, Kisu alifurahi sana na kumwambia,

    KISU: Nilijua tu kama utarudi Huruma.

    HURUMA: Ulijuaje?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    KISU: Aaah wewe, mi siwezi kukimbiwa na mwanamke wewe.

    HURUMA: Hamna Kisu, kwasababu tu nakupenda.

    KISU: Lazima unipende wewe, mimi ndio Kisu bhana. Haya na mwanangu mmempa jina gani?

    HURUMA: Nimemuita Faraja.

    KISU: Hapana hilo jina haliwezi kukubalika kwetu.

    HURUMA: Kwani linatatizo gani?

    KISU: Kwetu mtoto wa kwanza huwa anapewa jina na wazazi.

    HURUMA: Mmh!! Basi waambie wazazi wako watutajie jina la kumpa.

    KISU: Kwetu hakuna ni lazima aonekane mtoto mwenyewe na hapo ndipo hupewa jina.

    HURUMA: Sasa itakuwaje?

    KISU: Itabidi twende kwetu.

    Huruma akajipanga kwa safari asiyojua watakapoelekea kwani hakumjua hata ndugu mmoja wa Kisu.

    Safari ikapangwa na siku ya siku wakaondoka.

    Huku nyuma wazazi wa Huruma walifanikiwa kufika nyumbani kwa Kisu lakini hawakumkuta binti yao.

    Kwahiyo wakangoja siku atakayorudi ili waende tena.

    Huruma na mumewe wakatumia siku mbili kufika kwenye kijiji cha mumewe.

    Walipofika tu wakapokelewa mtoto, Huruma akajua ndio utaratibu wao.

    Kisu akaitwa na mama yake.

    MAMA KISU: Mwanangu nadhani unatambua kwamba mtoto wa kwanza ni halali ya wazazi?

    KISU: Ndio natambua mama.

    MAMA KISU: Na mbona ajifungulie hospitali?

    KISU: Nilimkataza ila ni ubishi wa huyo mwanamke mama.

    MAMA KISU: Na pia si unatambua kama mwanamke aliyejifungulia hospitali mtoto wa kwanza ni halali ya yetu?

    KISU: Naelewa mama ndiomana nikamleta.

    MAMA KISU: Basi sawa mwanangu.

    Huruma alishangaa yuko pale ila mtoto wake harudishwi hata kunyonya, zikapita siku tatu bila ya kumuona mwanae. Ikabidi aulize, akamuuliza wifi yake.

    HURUMA: Eti wifi mwanangu yuko wapi?

    WIFI: Pole sana wifi, nadhani umekuja sehemu ambayo huitambui vizuri.

    HURUMA: Kivipi?

    WIFI: Kwa kawaida ya huku mtoto wa kwanza ni halali ya wazazi, na mara nyingi huuwawa.

    HURUMA: Heeeee!! Inamaana mwanangu amekufa?

    WIFI: Mwanao hajafa, amekuwa ni mtoto pekee mwenye bahati ili atakapotoka hapo hutaweza tena kuishi nae.

    HURUMA: Kivipi?

    WIFI: Ningekuwa mimi ni wewe ningejiondokea, huku si pazuri wifi utakufa.

    Kusikia hivyo Huruma alijihisi kutetemeka.

    HURUMA: Niambie namna ya kuondoka.

    WIFI: Wewe ondoka tu, kwanza muda wako umeisha.

    HURUMA: Kivipi?

    WIFI: Angalia kule uone.

    Huruma akatetemeka sana, ni kundi kubwa la watu likawa linakuja.

    Huruma akabaki kutetemeka na kuhamaki tu.

    WIFI: Usiwe mjinga wewe, kutetemeka hakuwezi kukuokoa chukua maamuzi ya haraka sasa.

    HURUMA: Nitafanyaje?

    WIFI: Zunguka chukua chungu jifanye waenda kisimani ila wakikukuta njiani usijionyeshe kutetemeka hivyo.

    Huruma hata hakujielewa alijikuta tumbo likimuunguruma tu, hata hakujua ni wapi atakapotokea.

    Akajitahidi na kuinuka ili aweze kutoka, kabla hajafika popote lile kundi lilishamsogele.

    Wakafika na kumbeba juu juu akapiga kelele zisizokuwa na maana kwao, akajikuta kelele zake zikiishia kwenye pipa linalochemka maji, alitumbukizwa humo na kutokota kama nyama na huo ukawa mwisho wa Huruma.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kuchemka vya kutosha wakamtoa na kumgawa vipande vipande, na kila mmoja alijinyakulia kipande kimoja.

    Wifi yake na Huruma, roho ilimuuma sana kwani Huruma hakuweza kuikimbia adhabu ile.

    Baada ya kumaliza kuila ile nyama, ikabidi wamuite huyo wifi ambaye ndio akawa shangazi wa mtoto.

    Wakamwomba atoe jina kwaajili ya yule mtoto.

    Shangazi akabeba mtoto na kumuinua juu na kusema,

    "Huyu mtoto ataitwa Nyuta".

    Wakafurahi sana kwani wao huwa wanapenda majina ya kujiropokea tu kwa mtoto wa kwanza.

    Hakuna aliyejua maana ya yule kumuita mtoto Nyuta, maana yake alibakiwa nayo moyoni mwake.

    Mtoto yule akakabidhiwa yeye amlee na kumfundisha vitu mbalimbali.

    Maana ya jina Nyuta aliijua yeye na nafsi yake na maana hiyo alihakikisha itakuwa kama alivyotaka yeye.

    Alimuita vile akimaanisha nyufa au ufa, yaani kitu kinachotaka kubomoka au kinachoweza kubomoka wakati wowote.

    Nyuta alipendwa sana na bibi yake, alifundishwa mambo mengi ya huko.

    Alipokuwa na umri wa miaka mitano, aliweza kusafirishwa kichawi na kupelekwa kwa mashetani, kitendo kilichofanya aonekane amekufa kwa maisha halisi.

    Wakamuweka na kumfungia kwenye chumba cha peke yake, alikaa siku tano bila kula wala kunywa akiwa amekufa kichawi.

    Siku ya tano alipozinduka alikuwa ni mtoto mwenye sauti ya kusikilizwa kuliko watoto wengine wote, wakamtoa kwenye kundi la watoto na kuwa kwenye kundi la watu wazima wenye uwezo mkubwa. Hapo kijijini akafahamika sana.

    Alipofikisha miaka kumi, Kisu akaenda kijijini kwao na kumchukua Nyuta ili aende nae mjini akawapooze wazazi wa Huruma kuwa ingawa mtoto wao amekufa ila wanaemjukuu mwenye mfano wa mama yake na kweli kabisa Nyuta alifanana sana na mama yake aliyekuwa marehemu kwa muda huo.

    Akaondoka na baba yake na kwenda nae mjini.

    Kufika huko akamkuta baba yake ana mke na watoto wawili,

    kwakweli Nyuta aliumbiwa roho mbaya.

    Shangazi yake alishamwambia kisa kizima cha kuuwawa kwa mama yake, kisa hicho kikamfanya Nyuta azidi kuwa na roho mbaya, aliwaona watu wote si kitu mbele yake.

    Baba yake akampeleka Nyuta nyumbani kwa wazazi wa Huruma, ingawa waliumia kwa kifo cha mtoto wao ila wakafarijika japo kumuona mjukuu wao.

    Siku zikaenda, mule ndani hawakumuelewa Nyuta ni mtu wa aina gani, alikuwa akifanya mambo ya ajabu ajabu.

    Nyuta aliweza kuwatengenezea watu magonjwa kiuchawi, kuna waliojikuta wanaumwa na wakakosa kuhudumiwa hadi kufa.

    Alipofikisha miaka kumi na tano alikuwa ni binti aliyeiva vizuri kwenye uchawi, wakaamua wampe uongozi kwenye chama cha wachawi, yeye akawa ni mwenyekiti wao.

    Katika majaribio yake ya kumaliza watu na kuwatunza misukule, alianza na mtoto wa kwanza wa baba yake kwa mama wa kambo, na mtoto huyo akamtunza msukule kwenye nyumba ya bibi yake mzaa mama.

    Wakawa wanamshangaa Nyuta kwani hakuwa binti mwenye huruma hata kidogo, kwa sura alifanana na mama yake ila roho ilikuwa ni yake peke yake.

    Jaribio la pili la kuweka msukule alilifanya kwa mama yake mdogo ambaye alikuwa ni mdogo wa Huruma.

    Kama kuzaa hapa kwakweli Huruma alizaa shetani.

    Nyuta alikuwa na uwezo wa kujiacha ndani na kusafiri kichawi hadi kwa bibi yake wa kwenye kile kijiji.

    Aliweza kufanya mauaji ya kichawi popote pale na ikawa ni ngumu kumgundua kama ni yeye ndiye anayefanya mambo ya ajabu.

    Alipofikisha miaka kumi na nane, kuna kijana akatokea naye akampenda sana ila kijana huyo akaonyesha kutokumpenda Nyuta.

    Akaamua kusafiri kichawi na kwenda kuomba ushauri kwa bibi yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nyuta akaenda kijijini kwa bibi yake ili akapate ushauri kuhusu kijana anayempenda.

    BIBI: Hata usijari mjukuu wangu huyo kijana atakupenda.

    NYUTA: Nataka anipende tena anipende sana.

    BIBI: Kuna dawa tutafanya, nakwambia atakuona wewe tu kuwa ni mwanamke mzuri dunia nzima na atakupenda sana.

    NYUTA: Nakukubali sana bibi yangu.

    Basi Nyuta na bibi yake wakafanya dawa ya kumvutia kijana huyo aliyejulikana kwa jina la Yusuphu.

    Pia alipata dawa ya kumvutia mwanaume yeyote aliyemtaka mbele yake. Ila akataka kuanza na huyu Yusuphu, mwanaume aliyempenda ila alionyesha kumpenda mwanamke mwingine aliyeitwa Maria.

    Kesho yake Nyuta akaipaka ile dawa usoni na mikononi, akaenda kukatisha maeneo ambayo Yusuphu hupenda kuonekana.

    Na kweli Yusuphu alipomuona Nyuta ikawa kama vile chuma kimeona sumaku maana kinavutwa tu, akajikuta akimfata nyuma nyuma huku akimuita.

    YUSUPHU: mrembo, mrembo.

    NYUTA: (akasimama na kumuuliza), Inamaana leo jina langu hulijui au?

    YUSUPHU: Hapana Nyuta leo umependeza sana hadi nimechanganyikiwa.

    NYUTA: (Huku akicheka, na kutaka kujaribu kama dawa yake imefanya kazi vizuri), sasa nilichopendeza ni kitu gani?

    YUSUPHU: Umependeza sana Nyuta, naapa sijawahi kumuona mwanamke mrembo kama wewe.

    NYUTA: (Akacheka tena), kwahiyo leo nimekuwa ni mrembo kushinda yule mwanamke uliyepanga kumtolea posa?

    YUSUPHU: Yule hakufikii hata kidogo, na kuanzia leo naghairi kumtolea posa nakutaka wewe Nyuta.

    NYUTA: (Akafurahi sana moyoni na kujipongeza kwa ushindi wa dawa yake), kwahiyo humtaki kabisa leo unanitaka mimi?

    YUSUPHU: Ndio Nyuta nakuhitaji wewe.

    NYUTA: Ila siku za nyuma si uliniponda sana wewe?

    YUSUPHU: Tuache yaliyopita Nyuta, na kuanzia leo naenda kuachana na yule mwanamke.

    Nyuta akaondoka pale akiwa na ushindi mkubwa moyoni mwake.

    Akaanza kuitumia ile dawa kwa wanaume mbali mbali ili kusambaratisha mapenzi yao na wanawake wengine kwani mwanamke aliyeonekana akawa ni yeye tu kwenye mtaa wote.

    Nyuta akaitumia dawa ile ile kusambaratisha ndoa ya mama yake mdogo iliyokuwa iko njiani, kwani alimvuta baba yake mdogo na kujikuta anapendwa yeye.

    Bibi yake mzaa mama alichukizwa sana kwa vitendo vya Nyuta kwani mtaa mzima kilio kilikuwa juu yake kuwa Nyuta anaharibu mapenzi ya watu, anavunja ndoa za watu.

    Mama yake mdogo aitwae Rehema akaamua kumuomba mama yao ili wamrudishe Nyuta kwa baba yake.

    REHEMA: Mama huyu mjukuu wako hafai kabisa, mtaa mzima wanalia juu yake. Ona alivyosambaratisha penzi la mdogo wangu! Mama tumrudishe kwa baba yake kwani hata mimi nimeanza kuwa na wasiwasi na ndoa yangu.

    MAMA HURUMA: Mwanangu, hata mimi namshangaa huyu mjukuu kwakweli kwanza ana vitabia vya ajabu ajabu sijawahi kuona. Hata huwa simuelewi jamani. Kwanza najiuliza hao wanaume wanamgombea kwa lipi? Anawagonganisha hata watano ila bado wote wanamgombea yeye, hapa kuna namna mwanangu.

    Mara Nyuta mwenyewe akawafatia,

    NYUTA: Sipendi kujadiliwa, tena nawaambia kuwa sipendi. Kama mnajifanya mnajua sana kujadili watu endeleeni kunijadili. Hapa ni nyumbani kwao na mama yangu kwahiyo siondoki hadi pale nitakapoolewa.

    Ikabidi mama Huruma na mwanae Rehema wakae kimya.

    Wazazi wa Yusuphu wakaanza kupatwa na mashaka juu ya kijana wao.

    MAMA: Jamani Yusuphu mwanangu, majuzi tu hapa ulituambia tujiandae tukatoe posa kwakina Maria uoe, vipi leo hutaki hata kumuona?

    YUSUPHU: Simpendi Maria mama.

    MAMA: Heeee, mwanangu hapa sio bure jamani. Yaani wewe ulivyokuwa unampenda Maria leo unasema humpendi??

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    YUSUPHU: Nielewe mama, mimi nampenda Nyuta na huyo ndiye nitamtolea posa.

    MAMA: Hapana mwanangu, bora hata ungemtaja mwanamke mwingine, huyo Nyuta kila siku anavuruga ndoa za watu na sisi hatumtaki.

    YUSUPHU: Mkimtaka nitamuoa na msipomtaka nitamuoa tu.

    MAMA: Hapa tunamtaka Maria tu na wala si mwingine.

    Yusuphu akaamua kumueleza Nyuta kuhusu msimamo wa wazazi wake kuwa wanamtaka Maria ambaye ndiye mwanamke aliyetangaza kumtolea posa.

    Nyuta akawaza upesi upesi na kujisemea kuwa Maria hawezi kukwamisha hata kidogo.

    Siku hiyo Maria akiwa anatoka sokoni, njiani akiwa anatembea akaona kitu kinang'aa sana mfano wa dhahabu au almasi kipo mbele yake, na kilizidi kung'aa kila alipokikaribia. Alipokifikia akainama ili akiokote ni hapo hapo akaanguka pale njiani na kupoteza fahamu, watu wakamuokota na kumrudisha kwao. Alipozinduka hakuweza kuongea tena, alitamani kusema chochote lakini alishindwa alijikuta akilia tu.

    Baada ya siku chache Maria akafa, kila mtu alisikitika sana kwani Maria alikuwa binti pekee mpole na mcheshi pale mtaani.

    Ila haikuchukua muda Maria kuzikwa na kusahaulika kabisa kama kulikuwa na mtu kama huyo duniani.

    Nyuta akawa mtu wa tofauti sana, baada ya Maria kufa Yusuphu akaenda na kutangaza nia ya kumposa Nyuta.

    Kwakweli bibi yake na mama yake mdogo walikuwa na maswali mengi sana ya kujiuliza,

    REHEMA: Mama bado nina mashaka na huyu Nyuta.

    MAMA HURUMA: Hata mimi mwanangu.

    REHEMA: Mama unajua huwa namuona Maria mara kwa mara ndotoni akiniomba nimsaidie?

    MAMA HURUMA: Wee Rehema mwanangu, Maria huyo si alishakufa?

    REHEMA: Ila mimi nina mashaka na kifo chake mama.

    MAMA HURUMA: Sasa utafanyaje mwanangu?

    REHEMA: Kwanza kifo cha yule mdogo wangu kilinipa mashaka sana, na sasa ni kifo cha Maria. Mama, lazima niende kwa mganga nikaague nini tatizo.

    Nyuta hakupendezewa na maongezi ya bibi yake na mama mdogo wake huyo.

    Siku moja Rehema akiwa anafua ili ajiandae kwenda kwa mganga, akashangaa kichwa kikianza kumuuma na mbele yake alimuona Nyuta akicheka sana, Rehema akajikuta akianguka chini. Wakaja majirani na kumsaidia, Rehema hakuweza kufanya chochote na baada ya siku mbili akafa.

    Nyuta wala hakuonekana kushtushwa na kifo hicho cha msingi na muhimu kwake ni kuwa hataki mtu amfatilie tu.

    Nyuta akawa ndio yule sasa wa kutoa misukule hakuwa na tatizo kuua mtu aliona ni kawaida kabisa.

    Nyuta alipoona wazazi wa Yusuphu wanakawia kumtolea posa ikabidi afanye dawa ya kuwavutia na wao. Baada ya muda mfupi Yusuphu na familia yake wakaenda kumtolea posa Nyuta, kwahiyo baba yake na Nyuta akawakubalia mtoto wao amuoe binti yake.

    Siku ya harusi ya Nyuta na Yusuphu lilitokea tukio la kustaajabisha sana, kila mtu aliyehudhuria alikuwa akishangaa tukio lile.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku ya harusi ya Nyuta na Yusuphu, likatokea tukio ambalo lilistaajabisha sana, kila mmoja alikuwa akishangaa.

    Alitokea kunguru aliyekuwa ni mweupe kote, kila mmoja wa hapo alishangaa kwani kwa kule kwao hawakuzoea kumuona kunguru mweupe.

    Kunguru yule alikuwa amefungwa kitambaa chekundu shingoni, Nyuta alionyesha kuchukizwa sana na tukio lile ambalo hakuritarajia na akajua tu lazima kuna mtu anafatilia mambo yake.

    Nyuta akafanya kitu cha kushtukiza sana kwani alitoweka pale ndani na kuacha mwili wake ukiwa kama mtu aliyezimia, kitendo hicho kikafanya wote waliokuwepo kwenye sherehe ile waache kushughulika na yule kunguru wa ajabu na kuanza kushughulika na Nyuta waliyedhani amezimia.

    Ikawa kufumba na kufumbua, yule kunguru akatoweka.

    Nyuta alipofika kwenye dawa zake akagundua ni baba mdogo wa Yusuphu ndie ambaye alikuwa akimfatilia.

    Akafanya dawa zake na yeye ili amuhadhirishe baba mdogo huyo.

    Baba mdogo wa Yusuphu alienda kwa mganga baada ya kupatwa na mashaka ya ndoa ya Yusuphu na Nyuta, alitaka kujua ni kwanini Yusuphu alichukua uamuzi wa gafla na kumuacha Maria. Ndipo huko alipopewa dawa na kuifanya wakati wa harusi hiyo, kwani aliambia akifanya hiyo dawa, mtu mbaya atajitokeza mwenyewe.

    Bila ya kujua kama mtu mbaya anayemtafiti ni zaidi ya mbaya kama anavyofikiri. Ni zaidi ya katili, ni zaidi ya ubaya wote aujuao yeye.

    Akiwa kwenye shughuli hiyo ndipo akafanya hiyo dawa na kutokea kunguru mweupe, hata yeye mwenyewe hakudhania kama itakuwa kama ilivyokuwa.

    Wakiwa wanahangaika na cha kufanya ili wamzindue Nyuta mara akazinduka mwenyewe na kujifanya hakuna anachoelewa.

    Akainuka pale alipokuwa na kumfata baba mdogo wa Yusuphu, akamshika bega na yule baba akajikuta amepoteza uelekeo kabisa.

    Mara akaondoka eneo lile, hakuna aliyejua alipoelekea na shughuli ya ndoa ikaendelea.

    Baada ya ndoa, Yusuphu na mkewe ikawabidi waende kwenye nyumba waliyoandaliwa ilikuwa ni nyumbani kwakina Yusuphu.

    Nyuta hakutaka kuelekea hapo ila kwakuwa walimlazimisha ikabidi aende kuishi alipoambiwa. Nia yake kubwa ni kuishi kwenye nyumba ya bibi yake mzaa mama ambako ametunza misukule yake.

    Ingawa alikubali kuishi kwakina Yusuphu, ila chumba alichokuwa anaishi kwa bibi yake alikifunga kabisa na hakutaka mtu yoyote aingie zaidi yake.

    Hata hivyo baada ya harusi ikasemekana kuwa baba mdogo wa Yusuphu amepotea, na baada ya siku mbili wakakuta amejinyonga.

    Hakuna aliyejua chanzo cha kujinyonga kwa baba huyo, kila mtu akasema sababu anayoijua yeye ila siri kamili ilibaki kwa Nyuta.

    Baada ya kifo hicho Nyuta akajisifu kwa uwezo alionao wa kumfanya mtu ajulikane amejiua mwenyewe.

    Akajisikia raha na ushindi mkubwa moyoni mwake.

    YUSUPHU: Mbona hata hujaonyesha kushtuka na kifo cha bamdogo?

    NYUTA: Nishtuke nini sasa?? Duniani wote tunapita.

    YUSUPHU: Ila inategemea tunapitaje, kifo cha bamdogo ni cha kushangaza.

    NYUTA: Cha ajabu ni nini kwa mtu aliyeamua kujiua?? Itakuwa maisha yamemshinda maana kila siku watu wanaimba wimbo wa maisha magumu.

    YUSUPHU: Mbona wewe Nyuta ni mtu wa ajabu sana?

    NYUTA: Uajabu wangu ni nini? Ulitaka nilie na kujigalagaza kwa mtu aliyejiua? Kwanza amekufa kidhambi.

    YUSUPHU: Kidhambi?

    NYUTA: Ndio kidhambi, si amejiua mwenyewe!! Yule ni moja kwa moja kwenye moto, hata ninawashangaa mnavyokazana alazwe pema peponi.

    Mdogo wake na Yusuphu ambaye aliitwa Nina aliwasikia wakiongea na kuamua kudakia,

    NINA: Wifi mbona una roho ngumu hivyo? Mmh kama mchawi.

    NYUTA: Hivi Nina, mchawi ukimuona utamjua?

    NINA: Hapana.

    NYUTA: Basi chunga kauli yako.

    NINA: Nilikuwa natania tu wifi yangu, ila ulinishangaza ambavyo hujashtushwa na kifo cha bamdogo.

    NYUTA: Sitaki kutenda dhambi ya kusikitika kwa mtu aliyejiua, maana ni yeye aliyejichagulia kifo.

    NINA: Mmmh!!

    Yusuphu akajihisi ni mtu wa ajabu sana kuishi na Nyuta, kwani alikuwa ni mwanamke asiyeeleweka hata kidogo.

    Yusuphu akajikuta akitamani kujua kwanini baba mdogo wake alijiua ila hakuweza kupata sababu na wala hakujua ni kwanini.

    Siku moja Nyuta na Nina walienda sokoni, kufika njiani.

    NINA: (Huku akimuonyeshea mahali Nyuta), pale ndipo alipoanguka wifi yangu Maria. Na hakuchukua siku nyingi akafa.

    NYUTA: Ulisikitika sana eeh!

    NINA: Ndio nilisikitika kwani nilimpenda sana.

    NYUTA: Mimi je hunipendi?

    NINA: Nakupenda wifi yangu.

    NYUTA: Ila sio kama ulivyompenda Maria?

    NINA: Hapana nakupenda wifi.

    NYUTA: Sawa nikajua hunipendi.

    Nina nae akaanza kuonyesha uoga kwakuwa na huyu wifi yake, alijikuta na uoga uliopitiliza kila alipoongea nae.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara kuna mtu akaja kuwataarifu kuwa mama mdogo wa Nyuta ni mjamzito.

    Nina akashtushwa gafla na kauli aliyoitoa Nyuta,

    "tuone kama atajifungua huyo mtoto"

    Na baada ya wiki wakapata taarifa kuwa mimba ya huyo mamdogo wa Nyuta imetoka.

    Hapo ndipo Nyuta akazidi kujipongeza kwa kazi anayofanya, alijiona kuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana wa kiuchawi.

    Nyuta akapata ujauzito na ujauzito huo akaunenea kuwa lazima mtoto atakayemzaa amuweke kwenye uchawi.

    Mawazo yake makubwa yalikuwa ni kwenye uchawi tu na kutunza misukule.

    Pale kwa bibi yake mzaa mama wakajawa na mashaka na chumba alichofunga Nyuta na kuwakataza watu kuingia kwenye chumba hicho.

    Yule mamdogo wake aliyemtoa mimba kichawi, akataka kujua ni kitu gani ambacho Nyuta ameweka humo ndani na kwanini awakataze kuingia.

    Ni hapo alipoenda kutafuta fundi wa kuvunja mlango huo.

    Wakiwa katika harakati hiyo, mara ikatokea kama tetemeko pale walipokuwa.





    Mama mdogo wa Nyuta aliyejulikana kwa jina la Sifa, akiwa pale mlangoni na fundi wake kukatokea tetemeko kitu kilichofanya wasiweze tena kuvunja ule mlango, kwani baada ya hapo fundi akagoma kuendelea na ile kazi na kujiondokea.

    Mamdogo huyo akachukia sana, akaamua kumfata mama yake.

    SIFA: Mama sielewi kabisa, kwanini inakuwa hivi?

    MAMA: Hata mimi sielewi mwanangu.

    SIFA: Hivi mama huyu Nyuta ndio yule Faraja aliyezaliwa na dada Huruma kweli?

    MAMA: Mwanangu, mimi na wewe tupo gizani kabisa. Mimi kama mzazi nina uchungu sana kwani mwanangu Huruma amefia ugenini nimeletewa taarifa tu na kupewa mjukuu, kukaa kidogo mwanangu mwingine akafa. Na hivi karibuni mwanangu Rehema nae kafa, yani mimi nipo nipo tu maana hapa nimebakiwa na wewe na wale kaka zako wawili tu basi. Familia inakwisha hii mwanangu.

    SIFA: Kweli mama familia inaisha, yatupasa tufungue macho tuone. Nilikuwa napendana sana na mume wangu ila gafla kaniacha. Mama ninamashaka sana na huyu mtoto wa dada.

    MAMA: Mwanangu, huyo ni damu yenu kwahiyo hakuna cha kufanya Sifa.

    SIFA: Mama nitajua cha kufanya, lazima nimchunguze ili nijue kisa mkasa.

    Sifa akajiwekea nia ya kumchunguza Nyuta ili ajue mienendo yake. Bila ya kutambua kama Nyuta hachunguziki kirahisi kama anavyofikiri.

    Sifa akawa na harakati za kumchunguza Nyuta, nae Nyuta hakumtaka Sifa kwenye misukule yake kwa wakati huo kwani Sifa alikuwa ni mwanamke mzembe, ila akampa ugonjwa wa kupooza.

    Sifa alijikuta gafla hawezi kusogea hadi asogezwe, alikuwa hawezi kufanya chochote bila kufanyiwa. Na hapo Nyuta akazidi kujipongeza kwa ushindi.

    Familia ya Yusuphu nayo ikawa inaweka mashaka kwa Nyuta.

    Siku moja mama Yusuphu akamuuliza mwanae,

    MAMA YUSUPHU: Mwanangu, unamuonaje mkeo?

    YUSUPHU: Mbona yupo kawaida tu mama.

    MAMA YUSUPHU: Ila mimi namuona kama tofauti?

    YUSUPHU: Itakuwa sababu ya mimba tu ila yupo kawaida.

    MAMA YUSUPHU: Hivi huwa humkumbuki Maria kabisa mwanangu?

    YUSUPHU: Huwa namkumbuka mama ila ndo hivyo Maria alishakufa.

    MAMA YUSUPHU: Kwakweli kama familia tungefurahi sana kama ungemuoa Maria.

    YUSUPHU: Hata mimi ningefurahi mama, mara nyingine najishangaa kuwa ilikuwaje hadi nikamchukia Maria. Ila Maria ndio alikuwa nimpendae kwakweli.

    MAMA YUSUPHU: sote tunatambua hilo mwanangu ila ndio basi tena.

    Ujauzito wa Nyuta ukazidi kukua huku Yusuphu nae akijishangaa maana mara nyingine anakuwa na mashaka na mkewe ila mara nyingine anamuona ni wa kawaida.

    Upendo wa Yusuphu kwa Nyuta ukaanza kupungua, Nyuta kuona vile ikabidi afanye dawa upesi.

    Siku hiyo Yusuphu akiwa kalala, Nxuta akaenda na kumpaka dawa iliyomfanya Yusuphu asijitambue kwa muda huo. Halafu akapaa nae hadi kule kwa bibi yake kijijini, kufika kule Yusuphu akafanyiwa kila aina ya dawa bila kujijua, nyingine alinyweshwa na nyingine akapakwa, halafu akarudi nae hadi wanapoishi.

    Ila dawa nyingine alitakiwa amuwekee kwenye maji ya kuoga na kwenye chakula muda akiwa na ufahamu wake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yusuphu alipozinduka pale hakujua ni kitu gani kimeendelea, alikuta tu mkewe amemuandalia maji akaoge, na yeye bila kujua kilichomo akaoga na aliporudi akapewa chakula akala, hapo dawa ya Nyuta ikawa imekamilika.

    Hakuna tena aliyeongea kitu kuhusu Nyuta Yusuphu akaelewa hakuna kabisa, Yusuphu hakuweza kumuelewa mtu yeyote yule zaidi ya Nyuta tu.

    Siku ikafika, uchungu ukampata Nyuta nae akaenda kujifungua. Hatimaye mchawi ameshajifungua ili kuendelezaa kazi ya uchawi na kuongeza idadi yao.

    Akajifungua mtoto mzuri wa kiume, mtoto aliyemnenea kuwa lazima amrithishe uchawi.

    Mtoto wake akapendwa sana, baba yake na Yusuphu akatoa jina la mtoto huyo na Yusuphu nae akalikubali kwa kishindo, walikubaliana kuwa mtoto huyo aitwe Mussa, jina la bamdogo wa Yusuphu aliyekufa ili iwe kama kumbukumbu kwani alipotea siku ya ndoa ya Yusuphu na Nyuta. Kwakweli Nyuta alichukizwa sana na jina hilo, hakupendezewa mwanae aitwe Mussa hakupendezewa kabisa.

    Akawaza kuwa pengine dawa aliyomfanyia Yusuphu haikufanya kazi vilivyo, ila hata yeye mwenyewe alipoulizwa kuwa kwanini analikataa jina hilo la Mussa hakuwa na sababu, na pia walipomwambia apendekeze jina analotaka yeye bado hakuona jina la kumfaa mwanae kwani yeye alitaka yule bibi wa kijijini ndio ampe jina yule mtoto.

    Mussa alipofikisha miezi mitatu, yule bibi wa kijijini wa Nyuta akaja mjini kuwasalimia.

    Alifikia kwa mwanae Kisu na kesho yake wakampeleka kwa mjukuu wake Nyuta.

    Alipofika alimshika mtoto na kumuangalia sana halafu akawaambia kuwa yule mtoto anapaswa kuitwa jina la babu yake yaani baba yake na Nyuta, alitaka yule mtoto aitwe Kisu.

    Mama Yusuphu akakataa kabisa akasema jina hilo hilo la Mussa limemtosha mtoto na limempendeza, yule bibi akachukia sana hakupendezewa kabisa na itikadi za wale watu ila mwisho wa siku akakubaliana nao ili kuepusha marumbano.

    Alimshika sana yule mtoto na akapata muda wa kumchora alama za uchawi ili mchawi yoyote akimuona yule mtoto ajue kabisa ni mwenzake.

    Baada ya siku mbili yule bibi akaaga na kuondoka.

    Ikawa ni tatizo kwenye nyumba yakina Yusuphu kwani yule mtoto alikuwa akilia sana usiku na hata mchana mara nyingine alikuwa analia sana, mtoto kula kwa pinde. Hataki kitu ni kulia tu kumbe analia kwa kazi ya uchawi aliyopewa, hata watoto nao hukosa raha kwa kazi hiyo sema huwapa uzoefu na ndio wakikua wanakuwa moto wa kuotea mbali kama alivyo Nyuta aliyepoteza fahamu siku tano kiuchawi.

    Mama Yusuphu akapatwa na mashaka sana kuhusu mjukuu wake, hakujua ni nini kimempata mtoto huyo aliye mzuri na wa kupendeza.

    Hata mwili wa mtoto yule ulianza kunyorodoka hakuwa kama watoto wengine.

    Mtoto yule alipofikisha miaka miwili, alikuwa ni mtoto wa ajabu sana. Alikuwa akifanya mambo ya ajabu mambo ya kushinda umri wake, mara nyingine ukimuangalia anakuwa kama mtu mzima kwani sura imekomaa kumbe imekomazwa kwa uchawi aliopewa.

    Bibi yake akazidi kupatwa na mashaka. Akaamua kutafuta watu wa karibu ili apate ushauri ila napo ikawa kama inashindikana.

    Siku moja mama Yusuphu akatoka na mjukuu wake kwenda kumsalimia rafiki yake, kufika huko kwa rafiki yake huyo aliyeitwa Fatuma.

    Fatuma akashtuka sana alipomuona Mussa. Akaamua kuzungumza kikubwa na mama Yusuphu,

    FATUMA: Ndugu yangu, huyu mjukuu wako si mzima.

    MAMA YUSUPHU: Ana tatizo gani kwani?

    FATUMA: Ana alama za uchawi.

    MAMA YUSUPHU: Kivipi na umezionea wapi?

    FATUMA: Huwezi kuona kama wewe si mchawi.

    MAMA YUSUPHU: Kwa maana hiyo wewe ni mchawi ndomana umeziona?

    FATUMA: Hapana mimi si mchawi ila nilichanjwa dawa ya kuweza kuwagundua wachawi.

    MAMA YUSUPHU: Kwamaana hiyo mjukuu wangu ni mchawi?

    FATUMA: ndio ni mchawi ndomana anazo hizo alama.

    MAMA YUSUPHU: Kwetu hakuna mchawi, sasa nani kampa uchawi? Na tutamtoaje?

    FATUMA: Kutakuwa na mtu wenu wa karibu tu ndio kampa uchawi. Huyu ni mtoto mdogo kumtoa sio tatizo, nitakupeleka kwa mtaalam ataenda kumtoa.

    MAMA YUSUPHU: Twende sasa Fatuma, sitaki mjukuu wangu apotee.

    Wakaianza safari ya kwenda kwa mganga wa kienyeji ili wakamtoe Mussa uchawi, walipofika kwa huyo mtaalamu kwanza alishtuka sana na kuwaambia.

    MTAALAM: Kazi mliyoniletea ni kubwa sana, kwani huyu mtoto ameandaliwa kuwa kiongozi mkubwa wa wachawi hapo badae.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    FATUMA: Tafadhari baba tusaidie.

    MTAALAM: Nitawasaidia ila mkae mkijua kwamba mnaniingiza kwenye matatizo.

    Mganga yule akaanza kwa kumfuta Mussa alama za kichawi.

    Wakati akiendelea mara wingu zito likatanda eneo lile na kuwafanya wote walio kwenye kibanda cha mganga kuanza kuogopa.



    Baada ya mganga yule kumfuta Mussa alama za kichawi, wingu zito likatanda pale kwenye kibanda cha mganga na kuwafanya wote washangae, mara mvua kubwa ikaanza kunyesha huku maradi yakipiga kama vile yanapasua anga.

    Mganga akamgeukia Fatuma na kumwambia.

    MTAALAM: Umeona ilivyokuwa ni kazi ngumu?

    FATUMA: (Huku akitetemeka), nimeona. Sasa itakuwaje?

    MTAALAM: Itabidi tusaidiane kuita mizimu ili ije kutusaidia.

    FATUMA: Wewe tuambie tu cha kufanya, sie tutafanya.

    MTAALAM: Itabidi tuimbe nyimbo za kuwaita, maana huyu mtoto ni hatari.

    Mama Yusuphu alikuwa akishangaa tu, hata asijielewe kabisa kwa mambo yaliyokuwa yakiendelea.

    Wakaambiwa waanze kuimba nyimbo za kuita mizimu, waliimba sana na mvua nayo ikawa inakakazana kunyesha.

    Likapiga radi moja lililofanya wote wanyamaze ilikuwa kama dunia imepasuka, wote wakawa wakitetemeka, mara mti wa nje ya kibanda hicho ukaanza kuwaka moto, kila mmoja alistaajabu kwani moto uliwaka na mvua nayo ikazidi kunyesha.

    Zikatoka cheche kama mbili kwenye ule mti, na zikaangukia mlangoni kwenye kile kibanda cha mganga, mara zile cheche zikabadilika na kuwa joka kubwa mithili ya chatu. Kwakweli mama Yusuphu alistaajabu sana, lile joka likaenda moja kwa moja kwa mtoto Mussa na kumviringisha hadi juu. Wote mule ndani mwa kibanda wakawa wanashangaa sana na kutetemeka.

    Baada ya muda kidogo, lile joka likajitoa kwa mtoto Mussa na kuanza kumlambalamba, halafu likatema chini vitu viwili vigumu vyenye mng'ao kama wa almasi.

    Lile joka likaanza kujisogeza na kurudi mlangoni kufika pale likageuka zile cheche mara zikapotea. Wote wakawa wanashangaa sana, na mara gafla ile mvua ikakatika na kukawa kweupe kabisa kama vile mvua haijanyesha.

    Yule mganga na watu wake mule ndani wakiwa kama hawaelewi yaliyotokea.

    MTAALAM: Fatuma, umeelewa nini hapa?

    FATUMA: Sielewi chochote naona mauzauza tu.

    MTAALAM: Ni bora mizimu imekuja kutusaidia maana hali ilikuwa ni mbaya.

    FATUMA: Kwahiyo tungekufa humu?

    MTAALAM: Ndio tungekufa, yatupasa tuishukuru sana mizimu.

    Yule mganga akachukua vile vilivyotemwa na Joka, akavitwanga na kumchanja mtoto Mussa na kumpaka.

    MTAALAM: Inawapasa kuwa makini sana maana adui anawazunguka.

    MAMA YUSUPHU: Mtaje basi ni nani?

    MTAALAM: Mama, hata mimi najipenda pia. Sitaki mapambano hapa kwangu, cha msingi muwe makini tu.

    FATUMA: Vipi kuhusu huyu mtoto sasa?

    MTAALAM: Huyu mtoto tumefanikiwa kumtoa uchawi ila cha msingi ni kuwa makini maana adui amechukia sana.

    MAMA YUSUPHU: Ila tungemjua ingekuwa rahisi kujiepusha nae.

    MTAALAM: Mtamjua tu wenyewe huko, mimi vitu vingine sihusiki.

    Baada ya yote Fatuma, mama Yusuphu na Mussa wakaanza safari ya kurudi.

    Wakiwa njiani Mussa akawa anamshikilia bibi yake kwa nguvu huku akidai kuwa afichwe kuna watu wanamtisha. Fatuma na mama Yusuphu hawakuelewa chochote ila hata wao walipatwa na uoga.

    FATUMA: Unadhani ni nani anatenda haya?

    MAMA YUSUPHU: Kwakweli sijui chochote ndugu yangu.

    FATUMA: Mmh kazi ipo jamani.

    MAMA YUSUPHU: Tena kazi kubwa ndugu yangu.

    Walipofika njiani wakaagana na mama Yusuphu akarudi nyumbani kwake bila ya kujua kuwa mtu mbaya wanae ndani.

    Nyuta alichukizwa sana na kitendo alichofanya mkwe wake.

    Mussa na bibi yake wakiwa wanaingia ndani, wakamkuta Nyuta amekaa mlangoni tena amejawa na hasira kupita maelezo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    NYUTA: (Akiuliza kwa ukali), mlikuwa wapi?

    MAMA YUSUPHU: Kheee wee mtoto, hata salamu?

    NYUTA: Mtoto ni yule anayenyonya na sio mimi.

    MAMA YUSUPHU: Mbona una kauli chafu sana wee binti?

    NYUTA: Kauli chafu?? Zisafishe basi ziwe safi.

    MAMA YUSUPHU: kuwa na adabu wewe, Mimi ni mkweo ni sawa kabisa na mamako mzazi.

    NYUTA: Sina mama mie.

    MAMA YUSUPHU: Kwahiyo umezaliwa na kibwengo?

    NYUTA: Nadhani hunijui vizuri wewe mmama, ila utanifahamu hivi karibuni.

    Mama Yusuphu alibaki akimshangaa Nyuta na kauli zake, mara Nyuta akamvuta mtoto Mussa na kuanza kumpiga, tena alimpiga kama vile sio mtoto mdogo, ikabidi mama Yusuphu aingilie kati. Ikawa kama vile mama yusuphu kanunua ugomvi kwani likazuka bonge la varangati hadi watoto wa mama Yusuphu ikabidi waingilie kati na kila mmoja hakuelewa Nyuta alikuwa amechukizwa na kitu gani.

    Mara Nyuta akaingia chumbani na kujifungia, hakutoka kabisa siku nzima na hakuongea na mtu yeyote.

    Kesho yake akatoka na kumfata mama mkwe wake.

    NYUTA: Mama samahani kwa yote yaliyotokea jana.

    MAMA YUSUPHU: Kama umetambua kosa haina tatizo mwanangu.

    NYUTA: Sawa mama, si unajua nilimkumbuka mwanangu.

    MAMA YUSUPHU: Sawa usijari.

    Ingawa mama Yusuphu, aliitikia lakini hakufurahishwa kabisa na tabia iliyoonyeshwa na Nyuta.

    Nyuta akabadilika na kuwa mtu mpole na mzuri mule ndani.

    Mtoto mmoja wapo wa mama Yusuphu hakufurahishwa kabisa na kitendo cha mama yake kumsamehe Nyuta kwani aliona kuwa Nyuta alichofanya siku ya jana yake hakikuwa sahihi kabisa.

    Mtoto huyu akawa anamchunguza Nyuta mambo anayoyafanya na kujiuliza kuwa kwanini anajihamini sana.

    Hakuna mtu aliyejua Nyuta ana mpango gani kwenye akili yake.

    Kumbe Nyuta akili yake ilikuwa inapambana na mtu yule aitwaye Fatuma kwani ndio chanzo cha mwanae kwenda kupelekwa kwa mganga na kutolewa uchawi.

    Alitamani amjue Fatuma kwa undani zaidi.

    Akajaribu kupeleleza, akajua taarifa fupi za kumuhusu Fatuma, akatamani Fatuma awe ni mmoja wapo wa misukule wake kwani alimuona ni mwanamke mwenye nguvu ila pia alitamani amuingize kwenye uchawi ili awe msaidizi wake.

    Ila pia Nyuta alikuwa anachukizwa na tabia za kaka mmoja wa Yusuphu, tabia ya kumfatilia mambo yake. Kwahiyo akapanga kumkomesha mkaka huyo aliyeitwa Solo.

    Siku moja akiwa kwenye mazungumzo na huyo Solo.

    SOLO: Hivi wewe Nyuta unajiamini na nini? Hivi kweli wewe ni wa kupigana na mama yetu?

    NYUTA: Hivi na wewe unajiamini nini kunifatilia mimi?

    SOLO: Sikia wewe, mi huwa sigombani na wanawake wewe!

    NYUTA: mimi ndio huwa sigombani na wanaume wala wanawake, kwahiyo kazi ni kwako.

    SOLO: Yani wewe mwanamke wewe, hata sijui kwanini Yusuphu alikuoa wewe.

    Nyuta akawa kimya na wala Solo hakujua Nyuta alikuwa na maana gani.

    Safari hii Nyuta akaamua kufanya mambo kwa kujikamilisha kabisa ila hata kama wakiamua kwenda kwa waganga wao wazidi kukosa majibu kuwa yeye ndiye muhusika wa majanga yote.

    Kutokana na hasira ambayo Nyuta alikuwa nayo akaamua kwenda kummaliza kabisa yule mamake mdogo aitwae Sifa, aliyempa ugonjwa wa kupooza.

    Ikawa kama mshtukizo kwani Sifa alianza kutapika damu, mamake alihangaika nae huku na kule ila mwisho wa siku akafa. Kwakweli yule mama yao hakuona furaha ya kuendelea kuishi kwenye nyumba yake kwani watoto wake walizidi kupukutika.

    Baada ya msiba bibi huyo akafunga nyumba na kwenda kuishi kwa ndugu zake, na hiyo ikawa ni furaha kwa Nyuta kwani aliifanya nyumba ile kama danguro lake la kuwekea misukule.

    Wiki moja baada ya kifo cha Sifa, ikaelekea zamu ya Solo, akiwa amelala usiku akamuona mtu kama Nyuta akija mbele yake na kumkaba, alihangaika na kufurukuta lakini hakupata msaada, mara akahisi kuna wadudu wanamng'atang'ata sehemu za siri. Akapiga kelele ikashindikana.

    Kesho yake, wakamkuta Solo akiwa chumbani amejifia, hakuna aliyeelewa kitu kilichomuua Solo. Kila mtu alishangazwa na kifo chake, na ubaya zaidi wakakuta anavuja damu sehemu za siri, kumuangalia wakakuta kuwa sehemu za siri za Solo zimenyofolewa, kila mtu alishtuka tena walishtuka sana kwa kifo kile cha ajabu.

    Hawakuelewa ni kitu gani kinachoweza kunyofoa sehemu za siri.

    Yote hayo yalimfanya Nyuta abaki na ushindi moyoni mwake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mama Yusuphu akaumia sana kumpoteza mtoto wake Solo, hakuna aliyetegemea kuwa Solo amekufa kwa namna ile.

    Wakiwa katika msiba ule, mara gafla likatokea joka kubwa lenye vichwa viwili. Hakuna aliyejua joka lile limetokea wapi na linaelekea wapi ila lilikuwa na macho makali yanayowaka kama taa.



    Lile joka la ajabu lenye vichwa viwili likawa kinawasogelea Mussa na bibi yake, wote wa pale hawakuelewa kwa haraka kuwa lile joka linamaanisha nini.

    Ila watu wakaanza kupiga kelele kuwa "nyoka nyoka"

    mara lile joka likatoweka na hakuna aliyejua limeelekea wapi, ila wakashangaa Nyuta akitoka ndani na kuhamisha vitu vyake, yaani akawa anahama. Watu wakamshangaa anahama vipi wakati pale kuna msiba, ikabidi Nina amfate na kumuuliza.

    NINA: Wifi, mbona unafanya vitu vya ajabu?

    NYUTA: (Akijibu kwa ukali), vitu gani?

    NINA: Utahama vipi wakati kuna msiba?

    NYUTA: Nami nikuulize swali?

    NINA: Niulize.

    NYUTA: Aliyekufa ni ndugu yenu au ndugu yangu?

    NINA: (akawaza kuwa akimwambia ni ndugu yake atamjibu inakuuma nini kama nimeamua kuacha msiba wa ndugu yangu na akisema ni ndugu yao atamwambia kuwa msiba haumuhusu), Swali gani hilo wifi?

    NYUTA: Kama umeshindwa kunijibu hilo swali basi usiniulize chochote.

    Nyuta akazidi kuhamisha vitu vyake, hadi wanaenda kuzika Nyuta hakuwa kwenye nyumba hiyo.

    Kila mtu alistaajabu mambo aliyoyafanya Nyuta kwenye msiba wa shemeji yake.

    Lile joka likawa kama ndio limemfukuza Nyuta mahali pale.

    Wakiwa ndani baada ya matanga kuisha Nina akawa anaongea na mama yake.

    NINA: Unajua mama toka kaka Yusuphu kamuoa huyu Nyuta, familia yetu imekuwa ikipatwa na mabalaa.

    MAMA YUSUPHU: Tena na maajabu pia, kwanza unamkumbuka yule kunguru mweupe kwenye ndoa yao?

    NINA: Nakumbuka mama, na je lile joka kwenye msiba wa kaka?

    MAMA YUSUPHU: Mwanangu hadi sasa sielewi ila nahisi kuna nguvu za giza hapa.

    NINA: Kweli mama tutafute namna ya kutatua tatizo.

    MAMA YUSUPHU: Mwanangu natamani kwenda kwa mganga nikajue tatizo ila mabalaa yaliyotupata mmh!!

    NINA: Mlienda kufanya nini mama?

    Ikabidi mama Yusuphu amueleze binti yake Nina hali halisi ilivyokuwa.

    NINA: Makubwa hayo mama, sasa unahisi Mussa alipewa uchawi na nani?

    MAMA YUSUPHU: Sijui chochote mwanangu.

    NINA: Mama nina mashaka na wifi Nyuta inawezekana ni mchawi.

    MAMA YUSUPHU: Heeee mwanangu kama ni hivyo basi tumekwisha.

    Nyuta akiwa kwenye nyumba ya bibi yake mzaa mama kwasasa, alijisikia amani sana ingawa alikuwa akiishi mwenyewe. Maana bibi yake alifunga nyumba na kuondoka, hivyo Nyuta akaenda alipohamia bibi yake na kuchukua funguo na kurudi kuishi yeye.

    Alijiona kuwa atakuwa huru zaidi na mumewe aliyekuwa anapelekeshwa kama boya. Kwakweli Yusuphu hakujielewa kabisa kwa kipindi hiko, alijikuta tu akitenda vitu tofauti. Ingawa kwao walisema sana kuwa amerogwa ila ikawa kama wanapiga kelele tu.

    Nyuta alikuwa akijipongeza kwa ushindi na ni hapo alipojigundua kuwa ni mjamzito tena, akawa anawaza sasa jinsi gani amrithishe huyo ambaye bado hajazaliwa.

    Yusuphu alikuwa ni mtu pekee anayemtetea Nyuta, madawa aliyopewa yalifanya amuone Nyuta kuwa ni mtu mzuri sana.

    Hata Yusuphu akienda kwao lazima amtetee Nyuta hata pale alipokosea.

    MAMA YUSUPHU: Hivi kitendo cha mkeo kuhama wakati wa msiba umekiona sawa kabisa?

    YUSUPHU: Mama, Nyuta ni mjamzito kwa sasa ndiomana anafanya mambo ya ajabu.

    MAMA YUSUPHU: Hivi umesikia ujauzito ndo unamfanya mtu kufanya kama alivyofanya Nyuta? Kwakweli namchukia mkeo, kwanza anatuongezea wachawi tu duniani.

    YUSUPHU: Mama, Nyuta si mchawi ila hamumuelewi tu.

    MAMA YUSUPHU: Najua wewe umeshatekwa kwahiyo hapa ni kama nampigia mbuzi gitaa. Najua upo gizani mwanangu ila ipo siku utapata mwanga.

    YUSUPHU: Aah mama na wewe maneno yako!!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MAMA YUSUPHU: Hunielewi baba, ila mkeo hafai.

    Nyuta akiwa na mimba ya miezi sita akaamua kusafiri kichawi ili akawasiliane na bibi yake kuhusu mtoto wake wa tumboni.

    BIBI: Hukuwa makini mjukuu wangu, na lile jina walilompa mtoto limeharibu mambo yote.

    NYUTA: Sasa itakuwaje na huyu?

    BIBI: Ungechelewa ningekufata, huyo inabidi tumchukue kabla hajazaliwa kwahiyo ijulikane kuwa mimba imetoka.

    NYUTA: (Na yeye akaingiwa na huruma), bibi inamaana mwanangu hatayaonja kabisa maisha ya duniani?

    BIBI: Itabidi iwe hivyo mjukuu wangu, ona wa kwanza tumemkosa. Na huyu tukimkosa wenzetu watachukia sana.

    NYUTA: Jamani bibi, nihurumie huyu japo akae duniani. Mwingine ndio tumfanyie hivyo bibi.

    BIBI: Nyuta, nakujua wewe ni shupavu sana. Usitake kumlilia mtoto aliye tumboni ambaye hata sura yake huijui.

    Wachawi wana vyama vyao na kila chama kinakuwa na masharti yake na kawaida ya wachawi ni roho mbaya ndiomana mtu akionyesha roho mbaya kupitiliza huwa mara nyingi tunawafananisha na wachawi.

    Nyuta akarudi huku amesononeka sana, kesho yake walipoamka hadi Yusuphu alimshangaa Nyuta hali aliyokuwa nayo.

    YUSUPHU: Vipi mke wangu?

    NYUTA: Hamna kitu nipo salama kabisa.

    YUSUPHU: Unaonekana huna raha jamani Nyuta.

    NYUTA: Najua ningejifungua mtoto wa kike, tena ningeona raha sana kumpa jina la mama yangu Huruma.

    YUSUPHU: Kwani tatizo liko wapi jamani? Utajifungua tu mke wangu si bado muda.

    Nyuta mwenye roho ngumu kama jiwe akajikuta akilengwalengwa na machozi.

    Ile mimba ya Nyuta ilipofika miezi saba, bibi yake akawa ameshafanya mambo yake. Nyuta akaumwa na tumbo sana na mwisho wa siku walipompeleka hospitali ikajulikana mimba imetoka ila hata madokta walishangaa kwani mimba ya miezi saba ni mtoto kabisa aliyekamili ila Nyuta alitoa mapande ya damu kama vile ana mimba ya miezi miwili au mitatu.

    Baada ya hapo, Nyuta alijikuta akiwa na hasira na chuki za wazi wazi.

    Kila amuonapo mama mjamzito anajikuta akimchukia na kvamani kumfanyia jambo baya.

    YUSUPHU: Pole mke wangu, haikuwa ridhiki yetu.

    NYUTA: Nimeumia sana ila nitajua cha kufanya.

    Yusuphu hakuwa akiyaelewa maneno ya Nyuta kwani siku zote aliongea kama mtu mwenye kisasi na watu fulani.

    Akiwa bado na machungu yake akagundua kuwa mdogo wake Yusuphu yaani yule Nina ni mjamzito, akaona kuwa ile itakuwa sehemu moja wapo ya kupunguza machungu yake.

    Nyuta akaamua kwenda kuwatembelea mama mkwe wake na Nina, akaongea mambo mengi na Nina bila ya Nina kuelewa kuwa wifi yake huyo ana lengo gani na yeye.

    Mimba ya Nina ikiwa na miezi minne, akiwa amelala alijihisi kama mtu anamkata tumboni kwa mkasi au kisu. Alipatwa na maumivu makubwa sana, damu zikaanza kumtoka.

    Mwisho wa siku akaambiwa kuwa mimba imetoka.

    Nina akaumia sana moyoni na wala hakuelewa kwanini mimba yake imetoka.

    Nyuta akajipa ushindi moyoni kwani hawakujua kama ni yeye amefanya vile, wakaanza kuhisi kuwa kuna watu wanaofatilia familia yake, mama Yusuphu akawaza sana kuwa mkwe wake mimba imetoka tena ya kutatanisha, na sasa ni binti yake Nina. Akajihisi vibaya mama huyu bila kujua kuwa mbaya yupo nae karibu.

    Mama Yusuphu akajitoa muhanga na kuanza kutafiti juu ya mtu anayeifatilia familia yake, kuna siku akakutana na bibi wa Nyuta mzaa mama ambaye ndio mama Huruma. Akaamua kumsimulia yote yanayowapata.

    MAMA HURUMA: pole mwenzangu ila mwenzio nimekimbia na nyumba nimemuacha akae mwenyewe huyo Nyuta.

    MAMA YUSUPHU: Hivi yule mjukuu wako ana nini jamani? Maana tangu ameingia kwenye familia yangu mambo yote yameharibika.

    MAMA HURUMA: Kwakweli sijui, yaani yule mjukuu ni wangu ila mara nyingine nilitamani kumfukuza kwani ameleta mkosi mtupu kwenye familia yangu.

    MAMA YUSUPHU: Hata mimi kwangu amekuwa ni mkosi mkubwa kabisa.

    Wakati wakiendelea kuzungumza hayo wakiwa pale njiani wamesimama, kikaja kimbunga cha ajabu na kuwasomba.





    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog