Search This Blog

UCHAWI WA KURITHI - 2

 





    Simulizi : Uchawi Wa Kurithi

    Sehemu Ya Pili (2)



    Wakiwa pale njiani, kukatokea kimbunga cha ajabu na kuwasomba mama Yusuphu na mama Huruma. Ilikuwa ni tukio la kushtukiza sana na hakuna aliyejiandaa nalo kwakweli.

    Wakabebwa juu juu na kile kimbunga na Wakaenda kutupwa mtoni, na walipozinduka hapo walikuwa ni watu wasiojielewa. Na ndio hapo wakaanza uchizi wa kuokota makopo na kufanya mambo yote wafanyayo machizi.

    Nyuta alipopata habari hiyo akajipongeza sana, kwani kwake ilikuwa ni habari ya ushindi.

    Nina alipoona kimya cha muda, akaanza kumtafuta mama yake. Akamtafuta sana bila mafanikio yoyote, uoga ukamtanda na hofu ikamshika. Ni hapo alipoamua moja, kuikimbia nyumba yao.

    Akaamua kwenda kuishi nyumbani kwa dada yao mkubwa aliyeitwa Yusta. Akamueleza matukio yote yaliyotukia kabla na baada ya msiba wa Solo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    NINA: Dada hali ni mbaya, mambo ya ajabu yanatokea nyumbani na hata mama amepotea.

    YUSTA: Sasa Nina jamani, unawezaje kuikimbia nyumba yetu jamani?

    NINA: Dada, siwezi kabisa. Mimba yangu imetoka katika hali ya kutatanisha na mchumba aliyepanga kunioa ameghairi yani kila siku matukio halafu niendelee kukaa nyumbani?? Siwezi dada.

    YUSTA: Kwahiyo unadhani hili ni suluhisho la wewe kukimbilia kwangu?

    NINA: Dada, nitaenda kuishi popote ila nyumbani sirudi.

    YUSTA: Hebu acha ujinga wako, mimi nitaenda kumtafuta mama. Haya na huyo mtoto wa kaka umekuja nae kwa ruhusa ya nani?

    NINA: Dada hakuna wa kumuachia, na siwezi kumpeleka kwa mama yake wakati najua ataangamia. Huyu mtoto nitaishi nae popote na nitakula nae chochote.

    YUSTA: Unamaanisha wifi Nyuta ndio mbaya?

    NINA: Nahisi hivyo dada, maana mambo anayoyafanya ni ya ajabu sana.

    YUSTA: Yani Nina umekimbia wakati mbaya ushamjua? Mie nitamfata kumpa maneno yake.

    NINA: Dada usithubutu, Nyuta anaonekana ni mtu hatari sana.

    YUSTA: Usinitishe bhana, nitamfata tu.

    Nyuta akiwa amekaa na Yusuphu nje ya nyumba wanayoishi, wakamuona Kuna mgeni anakuja. Nyuta akaanza kumuuliza Yusuphu.

    NYUTA: Nani yule anakuja?

    YUSUPHU: Namuona kama dada yangu Yusta.

    NYUTA: Anataka nini?

    YUSUPHU: Labda anakuja kutusalimia.

    Yusta akawa amewafikia kabisa, hata angekuwa mtu wa aina gani lazima angeweka shaka kwa Nyuta. Yani mgeni amefika, hata kumkaribisa hakuna. Alichofanya ni kuinuka na kuanza kuongea nae kama kuna shari vile.

    NYUTA: Unataka nini?

    YUSTA: Kheee, wifi hata salamu??

    NYUTA: Kwani nikikusalimia utanenepa au utakonda?

    Yusta alipatwa na wakati mgumu sana kwani alishindwa kumuelewa kaka yake aliyekuwa kama hamuoni vile, yani Yusuphu nae alikuwa kama vile hakuna mgeni aliyefika.

    Yusta akaamua kumfata pale chini alipokaa,

    YUSTA: Kaka, inamaana hunioni au ni nini?

    YUSUPHU: Nakuona ila nakushangaa unagombana nini na wifi yako?

    NYUTA: (Akadakia), wewe Yusta hujaja kwa kheri. Sasa kwavile umekuja kwa shari na shari yako utaipata.

    YUSTA: Usinibabaishe bhana, kwanza wewe mwanamke ni mwanga.

    NYUTA: Nani mwanga? (huku hasira zikimpanda).

    YUSTA: Wewe apo ni mwanga.

    NYUTA: Mimi mwanga eeh!! Ngoja utauona uwanga wangu sasa hivi.

    Baada ya kuimaliza hiyo kauli, Yusta akashtukia amepatwa na tumbo la gafla akawa anagalagala chini na hakuna anayemsaidia, hata kaka yake Yusuphu alikuwa akimuangalia tu dada yake anavyohangaika.

    Yusta akateseka sana na lile tumbo, baada ya muda kidogo likatulia. Nyuta akamfata Yusta na kumwambia,

    NYUTA: Umeuona uwanga wangu sasa?

    Yusta akawa analia tu na kujilaumu kwanini ameenda.

    NYUTA: Kilichokuleta ndio kinachokutesa, eeh mdogo wako kaenda wapi na mwanangu?

    YUSTA: Hilo sio tatizo ila unanitesha bila hatia.

    NYUTA: Asilimia kubwa ya wanaoteseka hawana hatia kama hujui.

    Yusta akazidi kulia tu pale huku akimsihi Nyuta aache kumtesa.

    NYUTA: Chagua moja, nikutumie kwenye mambo yangu au nifanye nitakacho juu yako?

    YUSTA: Nitumie kwenye mambo yako.

    Yusta alikuwa akilia na Nyuta alikuwa akicheka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    Nyuta akafanya dawa na kumuingiza Yusta ndani kwake kimazingara.

    Nina akiwa nyumbani kwa Yusta, akaona kimya kimezidi na mwenye nyumba harudi. Hapo hata hakutaka kujiuliza zaidi, alichoamua ni kumchukua tena mtoto Mussa na kutokomea nae kwenye vijiji vya mbali.

    Ni huko alipoenda kumlea na kumkuza Mussa akiwa kama mwanae.

    Nyuta akawa anamtumia Yusta katika mambo mbalimbali, alimfanya Yusta kuwa msukule mwenye uwezo wa kuongea na kufanya mengine ila alimnyima tu uwezo wa kutoroka kwenye himaya hiyo ya misukule.

    Nyuta akazidi kumtuliza Yusuphu na madawa aliyokuwa akimfanyia.

    Yusuphu hakuwa na kauli yoyote kwa Nyuta.

    Mtaa wanaoishi ukawa na mashaka na Nyuta kwani mambo mengi ya ajabu yalikuwa yakiwapata na ni mtu mmoja tu ambaye alikuwa hashtushwi na jambo lolote, nae ni Nyuta.

    Nyuta alifuga misukule, anaposhindwa kuilisha huwa anaifungulia inaenda kuparamia mashamba ya watu na kula mahindi.

    Mwanadamu akishakuwa msukule ile akili ya binadamu wa kawaida inapotea huwa anafanya mambo ya tofauti kabisa.

    Basi ndio hiyo misukule, kwa kawaida hawaonekani labda mtu awe amepakwa dawa.

    Nyuta alijisikia amani kabisa kuishi na misukule ila roho ilimuuma juu ya mwanae Mussa kwani hakuweza kabisa, kufahamu alipo.

    Makombola yake yakahamia kwa mama yake wa kambo, Nyuta bila huruma aliua wadogo zake wawili hadi akagombana na baba yake kwani Kisu alielewa kama mchezo ule unafanywa na binti yake mwenyewe Nyuta. Yule mama nae akashindwa kuvumilia kuishi na kisu kwa mauzauza kwahiyo akaamua kuikimbia nyumba. Na huo kwa Nyuta ni ushindi mkubwa sana.

    Nyuta akafanikiwa kupata watoto wawili, wakike akamuita Huruma jina la mama yake na wakiume akamuita Kisu jina la baba yake. Watoto hawa aliwafuzu vilivyo kiuchawi, watoto hao wakawa wanaogopewa mtaa mzima, watoto hao ndio waliokuwa wanaenda kuwaua watoto wa wanawake wanaoenda kujifungua.

    Nyuta akapatwa na furaha kubwa kwa kuongeza jeshi lake la uchawi ila uchungu bado ulimpata kwa Mussa kwani angekuwa jeshi kubwa zaidi ukizingatia, alikuwa ndio mtoto wa kwanza.

    Uchawi wa hao watoto ulikuwa ni hatari, waliloga na kuchawika kila mahari.

    Kila jambo na wakati wake, Yusuphu akiwa kazungukwa na wachawi tupu ndani na mtu wa kawaida akiwa peke yake sasa akaweza kugundua tofauti yake na wao. Akaweza kufunguka macho na kuona, akagundua wazi kuwa hakumpenda Nyuta hata akawa anajishangaa aliwezaje kumuoa na kuishi nae mwanamke ambaye hakumpenda.

    Yusuphu akafunguka ufahamu, akaona pale hapamfai. Wakati akitafakari hayo, akaiona sura ya Maria ikumuangalia kwa upole, akatamani amvute Maria ili awe nae. Alikuwa Maria yule yule aliyemjua ila pale alikuwa kabadilika na kupauka sana.



    Maria aliyemuona Yusuphu alikuwa ni maria yule yule mchumba wake wa kipindi kile ila alikuwa amepauka sana, Yusuphu akajawa na moyo wa huruma, akainuka na kumsogelea ili amkumbatie, ile anataka kumkumbatia tu Maria akatoweka. Kitendo hicho kilimshtua sana Yusuphu, akawaza mambo mengi sana.

    Yusuphu alijiona wazi kutokumpenda Nyuta na alizidi kujishangaa kuwa ilikuwaje hadi akamuoa huyo Nyuta.

    Baada ya kutafakari kwa muda, Yusuphu akaona kuwa pale hapamfai, akaanza kufikiria mambo mengi ndugu zake, mama yake na hata mtoto wake Mussa, hakujua walipo sasa. Akaamua kufanya mpango wa kumtoroka Nyuta, hakutaka kumuaga kwakweli. Alitaka afanye mambo kimya kimya.

    Akili ya Yusuphu ikafanya kazi haraka, ingawa aliwapenda pia wale watoto wake wengine ila hakutaka awashirikishe kwenye mpango wake kwani aliwaona hao watoto wakiwa na dalili zote za tabia za mama yao, walikuwa na roho za kikatili na kinyama.

    Mpango wake ulipokamilika, akaamua kuondoka kimya kimya bila ya kumuaga mtu yoyote.

    Yusuphu akaamua kukimbilia mbali na kwenda kuanzisha maisha yake peke yake. Hakutaka tena kuishi utumwani tena ni vitu hata visivyoeleweka ndani.

    Nyuta na wanae waliporudi nyumbani hawakumkuta Yusuphu, ikabidi Nyuta amuulize yule msukule aliyemuweka kama msaidizi wake ambaye ni Yusta kwani alimfanya kuwa kama mlinzi wake, naye akajibu kuwa hajui, Nyuta akachukia sana.

    Akawageukia wanae na kuwaambia,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    NYUTA: Baba yenu hanijui vizuri naona, ila namwacha tu sina shida naye mie.

    HURUMA: Ila baba kafanya vibaya, yani hata kutuaga dah!!

    NYUTA: Msijali wanangu.

    Nyuta alikuwa na chuki za waziwazi, na bila huruma akawa anawatokomeza hadi jirani zake na kuwafanya misukule.

    Nyuta alijisikia furaha kujaza misukule ndani na wala hakuona kama ni tatizo kwa yeye kuwafanya vile wanadamu wenzie.

    Misukule hiyo iliishi kama wanyama tu wasio na akili yoyote. Ilifanya mambo ambayo mwanadamu na akili zake hawezi kuyafanya kabisa.

    Ingawa watoto hawa wa Nyuta walikuwa na roho mbaya sana ila hata wao hawakujua sababu ya mama yao kufuga misukule mingi kiasi kile.

    Kutokana na roho mbaya aliyokuwa nayo Nyuta ilimfanya mtaa mzima umchukie. Hakuna aliyempenda Nyuta hata mmoja, kila mtu alimchukia Nyuta. Hakuwa na rafiki wala wale majirani wa ukaribu nae, hakuna aliyependezwa na vitendo vya ushirikina alivyovifanya Nyuta.

    Baada ya kuona jamii iliyomzunguka karibia yote imemtenga, Nyuta akaanza kujifanya kuwa anabadilika, akaanza kujifanya ni mcha Mungu na mwana maombi.

    Akaona hiyo haifai, akaamua kuhama na mtaa.

    Akatafuta nyumba sehemu nyingine na kwenda kuishi na wanae, kwahiyo kama kawaida nyumba ile akaiacha kuwa nyumba ya misukule.

    Mtaa aliohamia Nyuta, wengi hawakuzijua tabia zake za ushirikina, wengi walimuita mwana maombi au mcha Mungu.

    Nyuta alijifanya kubadilika na wengi wakamuamini kwa staili hiyo.

    Hadi majirani aliokuwa anakaa nao mtaa mmoja mwanzo wakawa wanamshangaa.

    JIRANI: Halafu mitaa mingine ni wazushi sana, yani mimi zamani nilikuwa nakuogopa kweli.

    NYUTA: Ndio wanadamu walivyo ndugu yangu, hawana jema hata kidogo.

    JIRANI: Nafurahi sasa tumekuwa majirani wema.

    Nyuta alifurahi moyoni, na kujisemea kuwa kwa sasa atafanya mambo kimyakimya ili wanaomzunguka wasimuwekee mashaka tena.

    Mussa akakua na kuwa kijana mkubwa, akapata mchumba aliyeitwa Mariam, akaamua kumchumbia ili amuoe. Shangazi yake ambaye ni Nina akampa baraka zote za kumuoa binti yule. Na hakika akamuoa kwani ndiye aliyemchagua.

    Wakiwa ndani ya ndoa, Mussa akatamani kuwaona wazazi wake. Alijua kuwa wanaishi pamoja kumbe baba yake alishatoroka kitambo sana.

    Nina bila kinyongo akamuelekeza Mussa wanapoishi wazazi wake.

    Mussa akapanga safari na mkewe Mariam aliyekuwa na ujauzito wa miezi mitatu, shida yao ilikuwa ni kupata baraka zao.

    Wakiwa njiani kuelekea kwa wazazi wao, wakajishangaa miyoyo yao ikiwa mizito sana ila wakajipa imani tu.

    Wakauliza kwa watu, wakaonyeshwa nyumba waliyoelekezwa. Walikutana na kijana mmoja aliyeitwa Moze, yeye ndiye aliwaelekeza hadi kwenye ile nyumba aliyokuwa akiishi Nyuta.

    MOZE: Nyumba yenyewe ile pale ila kuna wakati tunapenda kuiita nyumba ya maajabu.

    MUSSA: Kwanini?

    MOZE: Wenyewe humo wamehama ila ukiwa karibu na nyumba hiyo unahisi kabisa kuwa kuna watu wapo ndani.

    MUSSA: Kivipi? Na wenyewe wamehamia wapi?

    MOZE: Walipohamia sijui ila hapo kwenye nyumba hiyo ni noma, mara nyingine ukipita kama unaitwa vile ila ukigeuka nyuma hakuna mtu.

    MUSSA: Mbona unatutisha wewe? Unauhakika ndio hiyo nyumba aliyokuwa akiishi mtu aliyeitwa Nyuta?

    MOZE: Nina uhakika, na mara nyingine huwa anakuja kuicheki.

    MARIUM: (Huku akijivutavuta), ila Mussa mie nimechoka kwakweli. Tujaribu kupumzika kidogo, halafu tutafute watu watuelekeze huko kwingine.

    Kwavile ile nyumba ilikuwa na ubalaza mzuri wa kupumzikia, Mussa akamvuta Mariam hadi kwenye kile kibaraza wakakaa hapo na Moze akawaaga kwa kuwaambia kuwa anaenda kuwaulizia kwa watu wengine ili wawaelekeze alipo hamia Nyuta kwa sasa.

    Mariam na Mussa wakiwa pale kibarazani, mara Mariam akaanza kupatwa na maumivu ya tumbo, akaanza kuhangaika na kugalagala pale kibarazani.

    Akawa akilalamika tumbo na huku akitapika damu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Marium alizidiwa sana na maumivu ya tumbo yaliyomfanya agalegale na kutapika damu, Mussa alihisi kuchanganyikiwa kwani hakujua cha kufanya muda huo na mke wake.

    Akiwa anawaza hiki na kile mara Moze akawa amerudi mahali pale, hata yeye alishangazwa na hali ya Marium,

    MOZE: Si niliwaambia!! Hapa pabaya ila nyie ubishi wenu tu.

    YUSUPHU: Acha maneno basi, cha msingi tuelekeze hospitali tuweze kwenda kutibiwa.

    MOZE: Mambo kama hayo si ya hospitali kaka, cha msingi nishaelekezwa anapoishi bi mkubwa wako, twendeni niwapeleke huko na yeye ndio atawapeleka hospitali.

    YUSUPHU: Kwani wewe kutupeleka hospitali kuna nini?

    MOZE: Hospitali ziko mbali bhana kaka mkubwa.

    Yusuphu akambeba Marium mgongoni kwani alishindwa hata kutembea.

    Safari ikaanza ya kuelekea kwa Nyuta.

    Wakiwa njiani wakakutana na mwanamke mmoja ambaye Mussa aliweza kumtambua kwa haraka kuwa anaitwa Fatuma, hata walipotambuana Fatuma akamshangaa Mussa kuweza kumtambua yeye wakati aliondoka akiwa mdogo sana.

    Baada ya kumueleza Fatuma tatizo lililomkumba Marium, Fatuma hakuafikiana kuhusu swala la kumpeleka kwa Nyuta badala yake akaamua awapeleke kwa mganga wa jadi.

    Kufika huko mganga yule akawaambia kuwa Mariam amekutana na upepo mbaya na ilikuwa bado kidogo angepoteza ule ujauzito wake.

    Yule mganga akawapa mitishamba ya kwenda kutumia, na hapo Mussa akaghairi kwenda kwa wazazi wake na kupanga kwenda siku nyingine.

    Mussa akaenda kumueleza shangazi yake Nina kuhusu lile tukio la mkewe.

    NINA: Ila Mussa usipende sana kwenda kule.

    MUSSA: Kwanini shangazi wakati kule ni kwa wazazi wangu?

    NINA: Hakuna sababu ila ule mtaa sio mzuri kabisa mwanangu.

    MUSSA: Sawa shangazi, lakini mimi nikienda kule itakuwa ni kwaajili ya kuwasalimia tu na si mambo ya mtaa wao.

    Nina hakutaka kumuweka wazi Mussa kuwa mama yake ni mchawi kwani anajua wazi kuwa Mussa hawezi kuamini hiyo kauli.

    Mussa akaendelea kuishi na mkewe huko mjini huku akipanga siku ya kwenda kuwasalimia wazazi wake.

    Katika pitapita za hapa na pale, Nina akabahatika kukutana na kaka yake kipenzi Yusuphu na alifurahi sana kukutana nae na wakaongea mambo mengi hadi ya kuhusu mtoto Mussa.

    Yusuphu alifurahi sana alipoambiwa kuwa sasa Mussa ameoa na ana watoto, hiyo ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa Yusuphu.

    Nina akapanga siku ya kumpeleka kaka yake huko kwa Yusuphu.

    Na siku ilipowadia akampeleka huko.

    Yusuphu alifurahi sana kumuona mwanae na wajukuu zake.

    Na yeye akamsisitiza mwanae Mussa kuwa asipende kwenda kumsalimia mama yake, kwavile walikuwa hawamuelezi kikamilifu Mussa aliona kama wanampigia kelele na akajisemea kuwa lazima aende kumsalimia mama yake.

    Ingawa Nyuta alikuwa akijifanya kuwa kabadilika ila kuna mtu aliyemfanya Nyuta awe na chuki nae, mtu huyo ni yule Fatuma. Nyuta alijikuta akimchukia Fatuma na kumlaumu kuwa amemuingilia mambo yake mengi sana haswa lile la kwenda kumtoa uchawi na sasa ni hili la kuikimbiza mimba ya Marium ambayo ingekuwa ni halali yake. Alikuwa akijisemea, "yule alikuwa mtoto wa kwanza yani ni halali yangu kabisa."

    Yani Nyuta aliyajua yote yaliyotendeka pale kwake wakati yupo Mussa na mkewe.

    Nyuta akapanga mkakati wa kumkomesha Fatuma.

    Siku moja binti wa Fatuma aliyeitwa Husna akiwa anatoka kuchota maji na ndoo yake kichwani, akafika mahali ikawa kama mtu kamsukuma basi ile ndoo ikaanguka na kupasuka.

    Husna akarudi kwao mbio huku analia, Fatuma akamuhoji na kujua kuwa Husna amepasua ndoo, wazo lililomjia Fatuma kichwani ni kuwa Husna alikuwa anacheza njiani ndiomana kapasua ndoo.

    Fatuma bila kufikiria mara mbili akachukua kiboko na kumshika Husna ili amcharaze asije akarudia siku nyingine.

    Fimbo mbili tu ziliweza kuzima sauti ya Husna, kwani Husna alianguka chini na kufa hapo hapo. Kwakweli Fatuma alihisi kupagawa na hakuamini macho yake kama imetokea vile ilivyotokea, alishangaa sana hakujua kama kuna wakati unapomuadhibu mtoto na mtu mbaya anapitia hapo.

    Fatuma alijutia kitendo chake cha kumcharaza mwanae hadi kufa.

    Fatuma alikosa raha, alitamani siku zirudishwe nyuma ili matukio yaweze kubadilika lakini ndio ilikuwa hivyo kwamba Husna ameshakufa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Fatuma alilia sana tena aliomboleza kupita kawaida, alikuwa na mtu mwenye majonzi muda wote.

    Baada ya mazishi, Fatuma alizidi kujipa lawama juu ya kifo cha binti yake, hakuamini kwamba kupasuka kwa ndoo moja ndio kumemsababishia mwanae hadi amekufa.

    Fatuma alijipa lawama zote, hakutamani kuishi tena na bila kufikiri akakoroga sumu na kunywa ili ajiue.



    Fatuma akajipa lawama zote na bila kufikiri zaidi akakoroga sumu akanywa ili afe na kuikimbia fadhaa ya moyo wake.

    Taarifa zikatapakaa kuwa Fatuma kajiua kwa kunywa sumu. Nyuta akajipongeza sana kwa kazi aliyofanya, akajiona kuwa yupo juu sana, akajisikia raha na amani kwa matukio hayo.

    Watu katika jamii ile hawakudhani kama yale matukio yamefanywa kichawi, wakati uchawi ndio uliocheza katika matukio yale ya Fatuma na mwanae.

    Nyuta akazidi kujiona mshindi, ingawa alikosa kuonana na mwanae Mussa ila akajipa matumaini kuwa kuna muda lazima Mussa atarudi tena kumuona mama yake tu.

    Pale kijijini napo hawakumuelewa Nyuta kabisa kwani mambo mengi aliyafanya kwa tofauti, kuna kipindi akawa anawapa magonjwa watu wa pale mtaani halafu anajifanya kuwa anawaombea wanapona kwahiyo kuna baadhi yao wakaanza kuiamini ile janja ya Nyuta.

    Jirani mmoja wa Nyuta alikuwa na mashaka na Nyuta hakuweza kumuamini Nyuta hata kidogo, jirani huyo alikuwa ni mama wa watoto wawili mapacha, watu walipenda sana kumuita mama Doto kwakuwa mwanae Doto ndiye aliyezoeleka sana mahali hapo na hata hivyo Kulwa alikuwa ameshakufa tena na yeye aliuliwa na michezo michafu ya Nyuta.

    Mama Doto aliwahi kugombana na Nyuta kuhusu mipaka ya shamba na vilevile waliwahi kugombana kuhusu watoto pindi Huruma na Kulwa walipopigana na hiyo ndio ikawa sababu pia ya Kulwa kutoweshwa kichawi na hakuna aliyejua alipo Kulwa kabisa ndiomana wakasema kuwa alishakufa.

    Mama Doto alikuwa ni mwanamke mbabe wa maneno asiye na mume, ila mpinzani wake alikuwa ni mwanamke shujaa wa uchawi naye hana mume.

    Imani ya mama Doto kwa Nyuta ilikuwa ndogo sana, na mama Doto aliweza kuwaambia watu wengi kuwa Nyuta ni mchawi.

    Nyuta alipanga namna ya kufunga mdomo wa mama Doto dhidi yake.

    Siku hiyo Doto na mama yake wakiwa wanatoka kwenye safari zao, mama Doto akamwambia mwanae kuwa yeye anapita gengeni mara moja kwahiyo Doto atafute mahali amsubiri.

    Doto akiwa hajui hili wala lile akasimama chini ya mti wa mwembe kumngoja mama yake.

    Mara akili ikamtuma kuwa aangalie juu ya mti, naye akainua macho yake juu lahaula akamuona nyoka juu ya mti, haikuchukua hata sekunde yule nyoka akamtemea mate Doto machoni, Doto akaanza kupiga makelele kwani macho yalikuwa yanamuwasha sana, mama yake naye aliporudi akastaajabu watu wamemzungukia mwanae ikabidi wamsaidie Doto kwa kumpa huduma ya kwanza, walimuosha uso.

    Haikusaidia chochote, Doto akapelekwa hospitali nao wakafanya vile wanavyojua wao, mwisho wa siku Doto akarudishwa nyumbani akiwa na hali mbaya sana kwani macho yalivimba na hakuweza kuona tena.

    Kila siku Doto akawa analia tu, hakuona raha ya maisha kabisa.

    Mama Doto akawa anahangaika na mwanae huku na kule.

    Mama Doto akaenda kumtafutia dawa mwanae, hakuwa na kimbilio akaamua kwenya kwa Nyuta. Nyuta akamcheka sana mama Doto.

    NYUTA: Wapi ubabe wako wa maneno?

    MAMA DOTO: Nisaidie jirani, nakuomba Nyuta.

    NYUTA: Ooh Nyuta mchawi, sijui nini na nini, vipi unataka dawa kwa mchawi?

    MAMA DOTO: Naomba tusahau yaliyopita, nisamehe jirani.

    NYUTA: Nadhani unataka kumjua jirani yako wewe?

    MAMA DOTO: Kivipi?

    NYUTA: Nenda kwako utamkuta.

    Mama Doto akiwa haelewi chochote na wala haelewi kuhusu huyo jirani aliyeambiwa ametangulia ni nani.

    Mama Doto akafika kwake mara gafla akapatwa na baridi kali, kizunguzungu kikamshika na kumuangusha chini.

    Aliposhtuka pale alijikuta ametutumkwa na vipele mwili mzima yani utadhani ni mtu mwenye ukimwi, kwakweli mama Doto alijishangaa sana kwani kilikuwa kitendo cha muda mfupi.

    Baada ya hapo, siku zinazofuata mtaa mzima wakatangaza kuwa mama Doto ni muathirika, wengi wakamtenga. Mama Doto na mwanae Doto hawakuwa na msaada kabisa, mwisho wa siku walikutwa wote wawili wakiwa wamekufa mule ndani ya nyumba yao.

    Huo ukawa mwisho wa mama Doto mbabe.

    Nyuta akajisifu sana kama kawaida yake.

    Mussa na familia yake yani mkewe na watoto wakapanga waende kumtembelea Nyuta.

    Na safari ikaiva na ikawa tayari kabisa.

    Siku ikafika nao wakajiandaa vizuri kwenda huko kwa Nyuta, wakiwa wameshafika karibia na kwa Nyuta mara watoto wao wote wakapatwa na ugonjwa wa kutapika na kuharisha kwa muda huo huo wakawa kama wagonjawa wa kipindupindu.



    Mussa na familia yake wakiwa wanaenda kwa Nyuta, njiani watoto wao wote watatu wakapatwa na ugonjwa wa kuharisha na kutapika wakawa kama wagonjwa wa kipindupindu .

    Mussa na mkewe wakawa wanashangaa na bila ya kuelewa chochote wakabaki wanajiuliza tu kuwa mbona wakiwa wanaenda kule ndio wanakutana na maswaibu ya ajabu ajabu.

    Wakiwa bado wanayatafakari yale, mara akatokea Kisu mtoto wa mwisho wa Nyuta, akawa kama anawashangaa mahali pale.

    KISU: Tatizo ni nini hapa?

    MUSSA: Wanangu hapo kama uwaonavyo wamezidiwa.

    KISU: Dah! Poleni ila msijari twendeni kwa mama yangu huwa anaombea wagonjwa na wanapona.

    Mussa na familia yake wakaanza kumfata Kisu anapowapeleka.

    Walipofika, Mussa akashangaa kuwa huyo mtu anayeitwa mama na Kisu ndio huyohuyo mama yake na yeye, akafurahi sana na kujitambulisha kwao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nyuta akampokea mwanae na familia yake, kutokana na wale watoto kuwa wagonjwa, Nyuta akaingia nao kwenye chumba chake cha maombi baada ya muda mfupi akatoka nao wakiwa wazima kabisa.

    Mussa alifurahi sana na alifurahia zaidi kugundua kuwa mama yake ni mwanamaombi, akawa anajisemea kimoyomoyo

    "mi nilijua tu kuwa wanamsingizia mama yangu kuhusu huo uchawi."

    Mussa akatambulishwa kwa wadogo zake nao wakafurahi sana kumfahamu kaka yao.

    Wakakaa vizuri sana ila Nyuta alijikuta akimchukia sana Marium ila hakutaka kuweka hisia wazi hadi wagundue kuwa anamchukia.

    NYUTA: Hivi ulijisikiaje kuishi na mwanaume ambaye hata huijui familia yake?

    MARIUM: Kwakweli sikujisikia vizuri ila shangazi yake nilimfahamu kabla.

    NYUTA: Shangazi na wazazi nani zaidi?

    MARIUM: Wazazi ni zaidi mama.

    NYUTA: Yani wewe unazaa watoto kimya kimya, hujui kama kila ukoo unatamaduni zake katika kulea mtoto?

    MARIUM: Mama nisamehe kwa hilo ila mimi nilikuwa sijui.

    NYUTA: Si unaona hapo umezaa watoto watatu hakuna hata mtoto mmoja aliyefanyiwa mila na hakuna hata uliyemrithisha jina, hata sijui hayo majina uliyowapa umeyatoa wapi!

    MARIUM: Mama mbona ni majina ya kawaida tu.

    NYUTA: Ila si utamaduni huo. Maana kati ya watoto watatu hakuna hata mmoja mwenye jina langu!

    MARIUM: Mama tusamehe tu.

    Yaani Nyuta alijikuta tu akimchukia Marium labda sababu jina lake limefanana na Maria yule aliyetaka kuolewa na Yusuphu mwanzoni.

    Katika wale wajukuu zake watatu, Nyuta alivutiwa sana na yule mjukuu wake mdogo kabisa aliyeitwa Pendo.

    Nyuta alipendezwa na ujanja alionao Pendo ila alikigundua kitu kimoja kwa Pendo kuwa ni mdadisi. Alipojaribu kuongea nae ndipo alipogundua udadisi alionao Pendo.

    PENDO: Bibi mbona wakati tunakuja kwako, tulipokaribia tu ndio tukaanza kuumwa?

    NYUTA: Kwasababu ugonjwa hauna hodi, popote pale unaweza kukupata mjukuu wangu.

    PENDO: Na mbona wewe ulipotuombea tu tukapona?

    NYUTA: Kwasababu nimepewa kipawa cha kuombea na kuponya.

    PENDO: Umepewa na nani?

    NYUTA: Nimepewa na mwenyezi Mungu.

    PENDO: Na mbona ukaenda tukuombea kwenye chumba cha peke yako?

    NYUTA: (Alijihisi kuchukizwa na maswali ya mtoto huyu), kwani tatizo ni nini?? Mwisho wa maswali.

    Nyuta akajiuliza mambo mengi kuhusu huyu binti, na pia akaamua kumfatilia ajue udadisi wake unakwamia sehemu gani.

    Bibi huyu hakuwa na shaka yoyote kwa Abra na Amina ingawa kati ya watoto wa Mussa alimtamani sana huyu Abra na kujisemea moyoni kuwa mtoto huyo alikuwa halali yake toka yupo tumboni ila kutokana na kiherehere cha Fatuma kikamfanya amkose mtoto huyo kwa kipindi kile ila kwa hapo alijileta mwenyewe.

    Nyuta hakutaka kuwashtukiza wajukuu zake.

    Akamuangalia Amina, alionekana ni binti mwenye uoga mwingi na mwenye Huruma, akajua kwamba akimuingiza kwenye uchawi atampa shida kama binti yake aliyenae ndani ambaye ana Huruma kama jina lake.

    Akaona tayari ameshakuwa na tatizo kwa kuwa na yule binti Huruma hadi huwa anashindwa kumwambia mipango yake mingine, na kama akimuingiza Amina ndani yake litakuwa tatizo zaidi. Akawaza sana kuhusu mjukuu atakayerithi mikoba yake kati ya wale watatu Abra, Amina na Pendo.

    Nyuta hakuacha kumpa lawama Marium.

    NYUTA: Na mbona umekuwa na watoto wachache sana, yani watatu tu?

    MARIUM: Mama maisha yanabadilika, watoto wanatakiwa wapate elimu ndiomana tunakuwa na wachache tunaoweza kuwatunza.

    NYUTA: Mbona mimi nina wachache na hawajasoma, inamaana siwezi kuwatunza?

    MARIUM: Hapana mama sina maana hiyo.

    Nyuta alipanga vitu vingi sana vya kumfanyia Marium.

    Na bado alipanga kitu cha kufanya kwa mtoto Pendo ili kupima kikomo cha udadisi wake.

    Walikaa pale kwa Nyuta ndani ya wiki moja na safari ya kurudi mjini ikafatia. Nyuta alitaka kujua mengi kuhusu maisha anayoishi mwanae kwa sasa kwahiyo akawapa kijana Kisu aambatane nao hadi mjini.

    Hawakujua kuwa Kisu anaenda kuchora vizuri mazingira wanayoishi, walichojua ni kwamba wanaenda nae tu kumbe kisu alikuwa na kazi ya ziada kule nyumbani kwa Mussa na familia yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walipofika walikuta hali shwari kabisa kama walivyopaacha na wakaingia kuanza maisha huku Kisu akiwa pamoja nao.

    Marium alikuwa ni mfanya biashara wa mifugo mzuri sana, alikuwa akifuga ng'ombe, kuku na mbuzi.

    Kwahiyo Kisu alipofika mjini alifurahi sana kufanya kazi ya kuhudumia mifugo hiyo.

    Siku moja Marium alipoamka asubuhi ili akawahudumie kuku wake hao wa mayai, alikuta kuku wote wamekufa mule bandani.

    Hakuwa na mtu wa kumuuliza kwani ni yeye mwenyewe aliwahudumia usiku wa jana yake.

    Akaenda kumuamsha Kisu na wakasaidiana kwenda kuwasomba wale kuku na kuwazika, huzuni ilimtanda sana Marium hakutegemea hasara kubwa kiasi hicho, maskini Marium hakujua kama mtu mbaya anaye ndani ya nyumba yake.

    Akiwa anatafakari juu ya kuku wake hao, akamsikia kijana wa ng'ombe akimuita, muda huo Kisu hakuwepo nyumbani.

    Marium kufika kwa kijana wa ng'ombe naye akastaajabu kwa alichokiona kwa ng'ombe wake.



    Marium kufika kwa yule kijana wa ng'ombe wake naye akastaajabu alichokiona.

    Akakuta ng'ombe wale wakikamuliwa badala ya kutoka maziwa inatoka damu. Ni kitu cha kushangaza kwa ng'ombe anayekamuliwa kila siku kutoa damu badala ya maziwa.

    Ikabidi Marium atafute daktari wa mifugo.

    Daktari wa kwanza hadi wa mwisho wote wakashindwa kugundua matatizo ya ng'ombe wale, wakawapa dawa za kila aina ila tatizo bado liliendelea na ubaya zaidi hata walipokuwa wakijisaidia ng'ombe walikuwa wakipiga kelele kama wamekabwa. Mwisho wa siku ng'ombe wale ambao walikuwa watatu wa maziwa wakafa na kuacha ndama mmoja kwani ndama wengine alishawauza ili kupata namna ya kuwatibu ng'ombe hao.

    Marium alihuzunika sana, aliona sasa umaskini unanukia, alikosa raha na furaha. Tegemeo lake likabaki kwenye mbuzi.

    Baada ya kama wiki kupita, Marium akakuta mbuzi wake wamebabuka ngozi. Akaanza kujiuliza ni ugonjwa gani umeipata mifugo yake napo hakupata jibu. Kuuliza watu wakamwambia labda mbuzi wake wamekula majani ya sumu. Kwakweli Marium alishindwa kujielewa kabisa, na mbuzi hao hawakuchukua muda wakafa, yule ndama nae wakamkuta chini amekufa. Marium akaona haya sasa majanga.

    Pesa akaishiwa akawa na hali ngumu sana akawa anakopa vyakula madukani, watoto nao wakarudishwa nyumbani sababu ya ada. Marium alihisi kuchanganyikiwa bila ya kujua adui mkubwa ni yule shemeji yake Kisu.

    Hali ya maisha ilivyozidi kuwa mbaya Kisu akawaaga kuwa anaenda kuishi maisha yake mwenyewe.

    Kisu alishapapenda mjini, aliona raha kuwa mjini kuliko kule kijijini.

    Alijitengenezea chuma ulete yani hirizi iliyomnufaisha yeye na kuwaumiza wengine, hirizi iliyongoja wengine wafanye kazi ila pesa apate yeye, hiziri hiyo inamaana kuwa mtu mwingine anahangaika kusaka pesa ile yeye anakaa na pesa inakuja yenyewe toka kwa huyo aliyeisaka. Alijisikia fahari sana kuwa mchawi, aliona mambo yake yakimnyookea kwa wepesi na bila ya kutumia jasho.

    Akatafuta nyumba mjini hapo na kuanza maisha yake.

    Hakukuwa na mwanamke aliyeonekana kuvutiwa na Kisu, ila kutokana na uchawi aliorithi toka kwa mama yake, Kisu aliweza kumvuta mwanamke yeyote amtakaye.

    Mussa alipoona hali ya maisha nyumbani kwake inazidi kuwa mbaya, akaamua kufunga safari na kwenda kwa mama yake ili kupata ushauri.

    Alipofika akamkuta mama yake, na wakaongea mengi ikiwemo na lile la familia yake na hali ya uchumi nyumbani kwake kwasasa.

    NYUTA: Tatizo watoto wetu huwa mnajiamulia kuoa tu bila kujaribu kushirikisha wazazi wenu wote wawili haswaa mama.

    MUSSA: Ila mama sidhani kama kuna tatizo kwa mke wangu.

    NYUTA: Tatizo lipo mwanangu, mkeo ana mkosi wengine wanaita gundu hata hakufai.

    MUSSA: Mama, nimeishi na Mariam kwa muda mrefu sasa na yeye ni kila kitu kwenye maisha yangu nashindwa kukuelewa huo mkosi unakuwa vipi?

    NYUTA: Tatizo umetawaliwa na mapenzi, na umejikuta ukimuamini huyo Marium kupitiliza ila kwa kifupi hakufai.

    MUSSA: Mama nishauri jinsi ya kupambana na haya maisha ila si kuhusu Marium mama, nampenda sana naye ananipenda pia.

    NYUTA: Huwezi kunielewa hadi pale maisha yatakapokushinda, hapo ndio utaelewa kuwa huyo unayesema ni kila kitu kwenye maisha yako hakufai. Unashindwa hata kuthamini mawazo ya mama yako sababu ya mwanamke!!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MUSSA: Sio kiivyo mama.

    NYUTA: Ila Marium hakufai, utakumbuka maneno haya siku moja. Mtu mzima dawa.

    Mussa hakuelewa kabisa ushauri anaopewa na mama yake ikabidi afunge safari hadi kwa baba yake na kumweleza yote yaliyojiri.

    YUSUPHU: Mussa mwanangu maisha yako yapo mikononi mwangu, shika kile unachoshikilia na amini kile unachoamini, ukitetereka kidogo tu basi yule adui atakushambulia kwa haraka sana.

    MUSSA: Baba mbona nashindwa kukuelewa hapo?

    YUSUPHU: Jaribu kuelewa kile unachoelewa, fanya maamuzi sahihi kulingana na moyo wako unavyokutuma.

    MUSSA: Baba unaongea kwa mafumbo sana hata nashindwa nianzie wapi kutafakari.

    YUSUPHU: Mambo mengine hata ukiyaweka wazi ni kazi bure kwani unaweza usiaminike ndiomana nakwambia kwa mafumbo ili akili kichwani mwako ikae sawa.

    Siku zote Yusuphu hakuweza kusahau vibweka alivyoona akiwa kwa Nyuta hali hiyo imemfanya kugundua vitu vingi afanyavyo Nyuta ila vilevile alishindwa kuweka wazi mambo hayo.

    Maisha kwa Marium na familia yake yakawa magumu sana, ndipo hapo walipogombana na familia ya mama John baada ya kukopakopa sana.

    MAMA JOHN: Mmezidi sasa, natamani niwachore nembo mgongoni kila mtu awajue kama nyie ni ombaomba.

    MARIUM: Usinitusi hivyo, sikupanga hali hii initokee.

    MAMA JOHN: Nenda mwanakwenda usinijazie nzi hapa loh!! Maskini wee, nenda zako wewe.

    Marium hakuwa na amani pale mtaani alijikuta akigombana sana na hao watu kulingana na kubadilika kwa hali yake ya maisha.

    Kitu kilichomuuma sana ni watoto wake ambao hawakuweza tena kwenda shule zaidi ya kukaa nyumbani kwani hakukuwa na pesa ya kuwalipia ada.

    MUSSA: Maisha haya hadi lini mke wangu?

    MARIUM: Hata sijui mume wangu.

    MUSSA: Kazi nimefukuzwa na biashara nazo zimekufa, na wewe kazi huna tena. Hivi itakuwaje kwa watoto wetu?

    MARIUM: Sijui ila tunahitaji mtu wa kutushauri kwa karibu sana.

    MUSSA: Kweli kabisa Marium.

    Maisha yakazidi kuwa magumu, hawakuwa na la kufanya na pia hawakujua wafanye kitu gani.

    Wakiwa wamelala usiku wa manane, wakasikia mtu anagonga mlango. Kila mmoja akajiuliza ni nani anayegonga mlango usiku ule wakati wote wapo ndani wamelala.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog