Search This Blog

MIMBA YA JINI - 5

 







    Simulizi : Mimba Ya Jini 

    Sehemu Ya Tano (5)







    "Haloo laaziz, vipi mpenzi wangu?"

    "Safi tu."

    "Mbona kama mnyonge?"

    "Bwana huyu msichana ananichanganya sana."

    "Kafanya nini?" Shehna alijifanya kuuliza.
    "Hajafika mpaka saa hizi yaani ofisi chafu."

    "Basi usikonde mpenzi wangu baada ya dakika mbili watakuja wasichana wangu kuja kufanya usafi uwape nafasi tu."

    "Hakuna tabu." 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya muda kidogo wasichana wawili warembo walibisha hodi kwenye geti, Mustafa alipowatazama alijua ndiyo waliotumwa na mpenzi wake Shehna.
    "Asalaam aleykum," wale wasichana waliwasalimia kwa bashasha na sauti tamu.

    "Waleykum salaam, nina imani ninyi ni wageni wangu?" Mustafa aliuliza.

    "Swadakta, hatuna muda tuoneshe hiyo kazi."

    Mustafa aliongozana nao hadi ofisini, baada ya kuwaonesha mmoja alisema:

    "Haya tupishe tufanye usafi."
    "Hakuna tatizo," Mustafa alijibu huku akitoka nje na kuwaacha wale wasichana.

    Baada ya kutoka walipiga makofi, haikuchukua muda waliongezeka wengine ambao walifanya kazi ya usafi kwa muda mfupi. Baada ya usafi wenzao walitoweka na kuwaacha wale wawili. Nao walitoka hadi alipokuwa amekaa Mustafa getini na mlinzi walipokuwa wakizungumza tabia za Sara zilivyobadilika tofauti na zamani.
    Walipofika walimweleza kwa sauti tamu yenye lafudhi ya kimwambao.

    "Bwana sisi tunakukimbia tuna imani utafurahia usafi wetu."

    "Nina waamini, nashukuru sana."

    "Haya si tukukimbie."
    "Haya, msalimieni sana Shehna."

    "Salamu zimefika."

    Wasichana wale walitoka nje ya geti na kutembea kufuata barabara, baada ya kuwa sehemu ambayo walijua Mustafa hawaoni walitoweka ghafla kurudi chini ya bahari.
    Mustafa alirudi ofisini na kuikuta ofisi inapendeza kila kitu kilikuwa kimesafishwa ndani kulikuwa na hewa na harufu nzuri ya manukato. Alikaa kitini na kuanza kazi huku akiamini kama atamuoa Shehna basi ataishi maisha sawa na peponi.

    ***

    Kila usiku Mustafa alifuatwa akiwa ndotoni na kujikuta yupo sehemu nzuri akiwa amelala pembeni ya Shehna aliyekuwa amelala huku tumbo lake likizidi kukua. Lakini alikuwa amevaa gauni jepesi lililoziba tumbo lake. Usiku sana Shehna alizima taa na kuondoa nguo zake na kumruhusu Mustafa alichezee tumbo lake lakini ikiwa gizani.
    Siku zote Mustafa alifurahi kuwa karibu na mpenzi wake na kutamani siku zote awe karibu yake. Tumbo la Shehna halikuwa likimsisimua lakini hakupata nafasi ya kuliona, siku zote alimbembeleza kuliona Shehna alimwambia avute subira. Mustafa alikubaliana na mpenzi wake.Katika siku alizolala alishangaa tumbo la Shehna kuwa kubwa akilala akiwa hana nguo tofauti na akimkuta amevaa nguo. Ile ilimfanya apange kumvizia wakati amelala ili awashe taa aone sababu ya 

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    tumbo lile kuwa kubwa tofauti na matumbo ya kawaida ya wanawake wenye mimba.Wakati huo Sara aliendelea kuteseka na baridi na njaa hakutoka kwenye nyumba ile mbovu mpaka kiza kilipoingia, aliogopa kutoka muda ule kwa kuhofia kupigwa na kuumizwa. Kiza kilipoingia ndipo alipotoka na kurudi nyumbani, lakini alipofika sehemu ya chumba chake ambacho kilikuwa kimefungwa alisikia mtu akisema:

    "Jamani yule mbwa wa asubuhi amerudi tena."
    "Jamani huyu mbwa atakuwa ametumwa tu, tena amesimama kwenye chumba cha Sara."

    "Jamani lazima kutakuwa na tatizo, Sara jana si alilala chumbani kwake ajabu asubuhi tukumuona na kukuta mlango upo wazi na mbwa huyu alitoka ndani. Ajabu tulimfukuza asubuhi usiku amerudi," shoga yake Happy alisema.
    "Sasa na Sara atakuwa wapi?"

    "Hapa ndipo tunachanganyikiwa maana hajaaga kama amepata dharura usiku."

    Sara yote aliyasikia akiwa bado amesimama kwenye mlango wake, lakini alishindwa kuzungumza kwa kuhofia kubweka na kuwatisha kitu kitakachowafanya wamfukuze kwa kumpiga.




    "Hapa ndipo tunachanganyikiwa maana hajaaga kama amepata dharura usiku."

    Sara yote aliyasikia akiwa bado amesimama kwenye mlango wake, lakini alishindwa kuzungumza kwa kuhofia kubweka na kuwatisha, jambo ambalo lingewafanya wamfukuze kwa kumpiga. Akiwa bado amesimama mlangoni alisikia akiitwa jirani yake kwa sauti aje amfukuze.

    "Baba John, yule mbwa wa asubuhi amerudi tena," mama John alimwita mumewe.

    Sara alijua majanga bado yanamuandama, alilia kilio cha kimyakimya kwa kuogopa kutoa sauti kuwatisha. Alijiuliza atajitetea vipi ikiwa hawezi kuzungumza sauti ya kibinadamu. Alimuona jirani yake baba John akitoka ndani na kuuliza:

    "Yupo wapi?"

    "Yule pale kwenye mlango wa Sara."

    "Huyu mbwa anatafuta kufa hapa subiri," alisema kwa sauti ya hasira aliyoisikia Sara.

    Baba John alisogea pembeni na kuchukua gongo ili ampige, Sara alishangaa kusikia sauti iliyokuwa ikimtokea bila kumuona anayezungumza ikisema:

    "Sara ondoka haraka watakuumiza."

    Sara hakuchelewa alitimua mbio, alipoondoa mguu tu gongo lilitua kwenye mlango na kutoa sauti, alisikia sauti ya baba John akisema:

    "Bahati yake lingempata angekufa, ------- kafie mbele kama umetumwa."




    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Jamani huyu ni mchawi, huyu mbwa si bure, iweje ang'ang'anie hapa tena kwenye chumba kimoja cha Sara?" alisema Happy kwa uchungu.

    Sara alitimua mbio mpaka nyumba ya jirani na kutweta huku akijiuliza nini hatima ya maisha yale?Alijiuliza atalala wapi usiku ule wenye baridi, kama angekuwa na uwezo wa kibinadamu basi angechukua kamba na kujinyonga. Njaa na kiu vilimshika, asingeweza kula jalalani au maji machafu. Kwake kilichobadilika kilikuwa umbile tu lakini akili ilikuwa ileile ya kibinadamu.

    Wingu la mvua lilitanda na baridi ilizidi kuwa kali na kumfanya atetemeke, ilionesha mvua kubwa inaweza kuteremka wakati wowote. Aliona sehemu anayoweza kujistiri usiku ule ni mule kwenye jumba bovu lenye harufu kali ya kinyesi.

    Alijiuliza nini hatima yake hata kama usiku ule utapita na atawezaje kulala na njaa na kesho yake aamke?

    Hakuwa na jinsi kwani wingu lilikuwa zito, alikimbilia kwenye jumba lile na kuingia ndani ili mvua isimkute. Alisogea kwa ndani na kutafuta sehemu kavu kisha alijilaza chini, moyoni alijuta kutosikiliza maneno ya Shehna. Kiherehere chake kilimponza na kujiuliza hata kama Shehna ni jini, bado hakumuhusu kwa vile Mustafa hakuwa mumewe, wala ndugu yake na ujio wake pale hakumuathiri chochote.

    Sara alilia sana lakini hakuna aliyesikiliza kilio chake kwa vile kilikuwa cha kujitakia, hakikuwa na pole. Njaa nayo ilizidi kumchonyota kwa vile toka asubuhi hakuwa ameweka kitu chochote tumboni wala kunywa maji. Hakuwa na jinsi, alikubaliana na yaliyokuwa mbele yake na kumuachia Mungu aamue maisha yake.

    Majira ya saa saba usiku, mwanga mkali ulimpiga machoni, alipoangalia vizuri aliwaona wanawake wawili wazuri waliokuwa wamesimama mbele yake na kumwita jina lake.

    "Sara."

    Alishindwa kuitikia kwa kuhofia kubweka, aliwaangalia tu huku akijiuliza wale ni akina nani na wamejuaje yupo pale. Wale wasichana warembo walimwambia atoke ndani, alinyanyuka na kuwafuata. Alishangaa kuwasogelea bila kushtuka, alipowasogelea walimshika kichwani, ghafla Sara alirudi katika umbile la kibinadamu.

    "Sara tumetumwa na Shehna tukuletee chakula."

    "A..asa..sante," Sara alishukuru huku akipiga magoti.

    Alijua baada ya chakula atabakia katika umbile lake la kibinadamu, alitoka nje ya jumba lile na kurudishwa kwenye chumba chake kisha akala chakula kile kitamu na kunywa maji. 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kula na kushiba alielezwa maneno yaliyomnyong'onyesha na kutamani ardhi ipasuke na kummeza.

    "Sara, samahani tutakurudisha katika umbile la adhabu kisha tutakurudisha tulipokutoa."

    "Jamani nisameheni, sirudii tena, nikirudia nifanyeni vyovyote," Sara alipiga magoti kuwaomba msamaha.

    "Sara sisi hatujui sababu ya wewe kugeuzwa mbwa, tumetumwa tukuletee chakula tu, zaidi ya hapo hatuna mamlaka yoyote."

    "Na..naomba unikutanishe na Shehna nimweleze haya."

    "Sara unatuchelewesha," walimshika kichwani mara moja Sara akarudi katika umbile la mbwa. Wale wasichana warembo walitoweka ghafla na kumuacha Sara nje ya jumba bovu walipomtoa na kumrudisha.

    ****

    Mustafa kila alipokuwa kazini, alikuwa na maswali mengi juu ya tumbo la Shehna kuwa kubwa kama puto lililojazwa hewa lakini lilikuwa laini na kupenda kulishika muda wote hata kumfanya kila siku alale kwa muda mchache.









    Kilichomuumiza akili kilikuwa ukubwa wa tumbo kila wakizima taa lakini akiwa na nguo zake za kulalila ilikuwa mimba ya kawaida.

    Alijiuliza kwa nini wakizima taa linakuwa kubwa na kingine kwa nini hataki kumruhusu kulichezea tumbo lile kwenye mwanga! Alipanga siku ile usiku amtegee Shehna amelala awashe taa ili kutaka kujua kwa nini usiku tumbo lake linakuwa kubwa sana. Aliendelea na kazi kama kawaida huku taarifa za Sara zikizidi kumchanganya kutokana na kuelezwa hajulikani halipo wala hakuaga.

    Mazingira ya kutoweka yalikuwa yakilingana na ya mara ya kwanza kitu kilichomfanya ajiulize Sara ana matatizo gani yanayosababisha kutoweka bila taarifa. Alikumbuka maelezo aliyopewa na Sara siku aliyorudi kazini baada ya kupotea kimiujiza alitoka kwenda kununua chakula cha usiku na kujikuta akiwa katika pori la kutisha na baada ya kutembea bila kujua na kutokea Dodoma.

    Kingine kilichomshtua kuambiwa kuna mbwa alikutwa chumbani kwa Sara baada ya kumfukuza alirudi tena usiku na kusimama kwenye mlango uleule. Alijiuliza kipi hasa kimempata Sara na ana siri gani ambayo yeye na majirani zake hawaijui. Alipanga akienda kwa Shehna kumueleza tatizo lile labda angeweza kumsaidia.

    Usiku ulipoingia kama kawaida aliposhtuka usingizini alijikuta yupo pembeni ya mpenzi wake Shehna. Kama kawaida tumbo lilikuwa la kawaida lililokuwa katika nguo nyepesi ya kulalia. Baada ya kuliwazana wote walipitiwa usingizi, Mustafa 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    hakulala sana alishtuka mapema na kutulia kitandani alilichezea tumbo la Shehna ambalo lilikuwa haliishi hamu kwa vile lilimpa raha ya ajabu kila alipolipapasa.

    Alitulia kwa muda kusubiri Shehna usingizi umkolee, baada ya muda alimsikia akikoroma. Alijua usingizi umemkolea. Aliteremka kitandani taratibu na kuelekea kwenye kandili ya dhahabu, aliiwasha huku akitetemeka aliipandisha mwanga ili aone vizuri.

    Baada ya kuwasha taa na kumulika kitandani, alishtuka kuona kiumbe cha ajabu juu ya kitanda. Sura ilikuwa ya mpenzi wake Shehna lakini tumbo lake lilikuwa la ajabu lililokuwa kubwa na pembeni lilikuwa na rangi kama magamba ya nyoka na chini alikuwa na mkia mnene unaoungana na tumbo.

    Mustafa alishtuka sana na kuanza kutetemeka, kingine kilichomshtua kuona kitanda walichokuwa wamelalia kilikuwa juu ya maji katika ya bahari. Mshtuko uliompata ulimfannya aanguke chini na kupoteza fahamu.

    Baridi kali lilimuamsha Shehna usingizini, alipofumbua macho alishtuka kukuta amelala juu ya bahari. Haraka alijirudisha katika umbile la kawaida, palepale usiku mwili wake ulirudi kama kawaida na kuwa chumbani kwake lakini kandili ilikuwa ikiwaka. Alijiuliza nani aliyeiwasha taa ile, alishangaa kujikuta peke yake na kujiuliza Mustafa alikuwa wapi!

    Alipoteremka kitandani alishtuka kumkanyaga mtu, alipoangalia alimuona Mustafa akiwa amelala chini amepoteza fahamu. Alijua tayari siri yake ilikuwa hadharani, alijiuliza atamwambia nini Mustafa amuelewe kuwa yeye ni jini pia alijiuliza akimueleza ukweli atakuwa tayari kuendelea kuwa naye!

    Shehna alianza kulia kitu kilichomshtua mama yake baada ya kudondokewa na machozi. Malkia Bi Zaldau mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu alikwenda katika chumba cha mwanaye. Alipofika alimkuta jasho likimtoka japokuwa kulikuwa na hali ya baridi, alishangaa kumuona Mustafa amelala chini.

    "Vipi?"

    Shehna ilibidi amweleze mama yake kilichotokea aliposhtuka usingizini.






    "Shehna nani kawasha taa?" mama yake alishtuka kuiona hali ile.

    "Sijui mama, labda Mustafa."

    "Ina maana hukumueleza taratibu zetu?"

    "Nilimueleza hata sijui likuwaje mpaka akawasha taa?"

    "Ina maana alifanya kiburi cha kibinadamu?" Bi Zaldau aliuliza kwa hasira.

    "Mama yaani sijui nimechanganyikiwa, jinsi ya kumuamsha na kumuuliza, lakini naogopa kumueleza mimi ni jini."

    "Hivi vitu vyote unavyomfanyia hajashtuka na kukuona kiumbe wa ajabu."

    "Huwa anashtuka lakini akili yake ilionekana ngumu kukubaliana kuwa mimi jini."

    "Akijua jini?"

    "Anaweza kuniacha nami nampenda sana."




    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Basi tumfanye hamnazo."

    "Hapana mama sitaki awe hivyo, ana familia inamtegemea unafikiri akiwa hivyo atafanyaje kazi?, Lazima atafukuzwa."

    "Kila kitu tutaipa familia yake na wewe kuwaeleza masharti ya kukaa naye, hatakiwi kwenda kwa mganga mpaka ujifungue."

    "Mamaa, umesahau mimi sitakiwi kutoka huku kipindi hiki."

    "Mmh! Hapo ndipo penye tatizo."

    "Au nimrudishe kwao."

    "Kumrudisha umechelewa, fanya hivi, mtume jini mmoja akachukue nguo zake kwake kisha tumrudishe ofisini ili akishtuka aamini alikuwa amelala na kuota akiwa ofisini."

    "Labda tufanye hivyo."

    Walimchukua na kumrudishia fahamu kabla hajajitambua walimpuliza na kumfanya apitiwe na usingizi. Waliwatuma vibaraka kwenda kuchukua nguo za Mustafa nyumbani kwake na kuzipeleka haraka kisha walimvisha na kumpeleka ofisini kwake.

    Kama kawaida ulifanyika kwanza usafi kisha walimweka kwenye kiti chake na kumuacha amelalia meza na kuondoka.

    Mlio wa simu ulimshtua Mustafa kwenye usingizi mzito, alijishangaa kulala ofisini kitu ambacho kilikuwa hakijawahi kumtokea hata siku moja.

    Alipiga miayo na kuangalia saa yake, ilimuonesha ni saa tatu asubuhi. Simu iliyokuwa pembeni yake iliendelea kuita, aliichukua na kukuta inatoka kwa mkewe, alipokea mara moja.

    "Haloo mke wangu."

    "Mpenzi, vipi leo?"

    "Kivipi mke wangu?"

    "Imekuwaje leo umeondoka bila kuniaga?"

    Swali hilo lilimchanganya sana Mustafa na kujiuliza aliwezaje kuondoka bila kumuaga mkewe, kila alivyojiuliza alikosa jibu. Ukimya wa kujiuliza maswali ulimfanya mkewe kumuuliza.

    "Mume wangu."

    "Naam."

    "Mbona hunijibu, au ulikuwa na kazi muhimu ofisini?"

    "Ndiyo," Mustafa alikubali ili kuepusha maswali asiyoyaelewa kwa wakati ule.

    "Hata kama hivyo, basi ungenipigia simu kunijulisha maana nimeshtuka kuamka asubuhi bila kukuona kitandani."

    "Yaani simu yako ndiyo iliyonishtua na kuachana na kompyuta toka nilipoingia," alitengeneza uongo unaofanana na kweli japokuwa bado alikuwa hajielewi kwa vile alikuwa hakumbuki kama asubuhi alitokea nyumbani kwake.

    "Pole mume wangu, lakini upo salama?"

    "Asante nipo sawa sijui wewe mpenzi wangu niliyeondoka bila kukuaga."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mi sijambo, hujambo imeongezeka baada ya kuishusha presha yangu."

    "Pole sana mke wangu."

    "Asante, basi nikuache ufanye kazi."

    "Asante mke wangu."

    Baada ya kukata simu alijikuta mtu mwenye mawazo mengi sana baada ya kujikuta amelala ofisini bila kukumbuka alifika pale muda gani mpaka kumfanya alale ofisini tena kwa muda mrefu.

    Alinyanyuka kitini na kujinyoosha mwili uliokuwa umechoka sana.

    Baada ya kujinyoosha na kutengeneza nguo zake vizuri, alitoka nje ili kuzungumza na mlinzi kutaka kujua amefika saa ngapi mpaka kujikuta muda ule amelala. Alikwenda hadi getini, mlinzi alipomuona alimshangaa na kumuuliza kwa sauti ya juu.

    "Bosi leo umelala ofisini?"

    "Kwa nini?"

    "Sijakuona kupita pia macho yamevimba kwa usingizi."

    "John, jana nilipotoka hukuniona?"

    "Nilikuona, ajabu sijakuona kupita kuingia lakini unatokea ndani ya ofisi."

    "Una uhakika hujaniona napita kuingia ofisini?"

    "Sijakuona ndiyo maana nakushangaa."

    "Mmh! Ipo kazi."

    "Kwani vipi, mbona kama huelewi?"

    "John hebu njoo ofisini."

    Mustafa aliongozana na mlinzi hadi ofisini ili wazungumze vizuri kwani muda ule alikuwa hajielewi. Baada ya kufika ofisini, Mustafa alimweleza mlinzi.

    "Kaa chini."

    John alikaa kwenye kiti kumsikiliza bosi wake, Mustafa baada ya kukaa alitulia kwa muda kuvuta kumbukumbu kwa yote yaliyomtokea na kutaka ushauri kwa mlinzi kwani alianza kuchanganyikiwa baada ya baadhi ya mambo kuyaona kama mauzauza. Muda wote John alikuwa ametulia akimuangalia bosi wake aliyekuwa ameinama.

    "John," Mustafa alimwita huku akinyanyua kichwa kumtazama.

    "Naam."

    "Kuna kitu kinanichanganya sana."

    "Kitu gani bosi?"

    "Kuna baadhi ya mambo siyaelewi ni ya ndotoni au kweli?"

    "Mambo gani?"

    "Unamjua yule mwanamke mzuri anayekuja hapa?"

    "Ndiyo."

    "Unamuonaje?"

    "Kivipi?"


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     

    Muda wote John alikuwa ametulia

    akimuangalia bosi wake aliyekuwa

    ameinama.

    “John,” Mustafa alimwita huku akinyanyua

    kichwa kumtazama.

    “Naam.”

    “Kuna kitu kinanichanganya sana.”

    “Kitu gani bosi?”

    “Kuna baadhi ya mambo siyaelewi ni ya

    ndotoni au kweli?”

    “Mambo gani?”

    “Unamjua yule mwanamke mzuri anayekuja

    hapa?”

    “Ndiyo.”

    “Unamuonaje?”

    “Kivipi?”






    SASA ENDELEA...

    “Unamuona yupo kama wanawake wengine?”

    “Ndiyo, kwani vipi?”

    “Ushawahi kuona mwanamke mzuri kama

    yule?”

    “Mmh! Sijawahi wewe umemtoa wapi, kwa

    kweli ni mzuri sana tena sana ajabu kila

    nikimuona mwili unanisisimka na mapigo ya

    moyo hunienda mbio.”

    “Unajua kwa nini?”

    “Hata sijui.”

    “Mimi nawasiwasi na yule mwanamke ni ji....”

    Mustafa alinyamaza ghafla baada ya

    kumuona aliyekaa mbele yake hakuwa mlinzi

    John bali Shehna akiwa anamtazama uso

    wake umejaa machozi ya damu. Alishtuka

    sana mpaka akaanguka chini ya kiti, John

    aliyekuwa amekaa kwenye kiti alishtuka

    kumuona Mustafa akishtuka na kuanguka vile.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alimuokota na kumkalisha chini kisha

    alimnyanyua kumrudisha kwenye kiti, lakini

    ajabu kila alivyoongea sauti haikutoka. John

    alishtuka na kujitahidi kumwita Mustafa

    ambaye alinyanyua mdomo kuzungumza kakini

    sauti haikutoka. Alimpigia simu mkewe

    ambaye naye alifika mara moja. Alishtuka

    kumkuta mumewe kwenye hali.

    “Vipi ilikuwaje?” alimuuliza mlinzi.

    “Tulikuwa tukizungumza ghafla nilimuona

    mwenzangu akishtuka na kuanguka chini.

    Nilipomuinua kila alipotaka kusema sauti

    ilipotea.”

    “Sasa kipi kimempata jamani mume wangu?”

    Husna aliuliza.

    “Hata mi nashangaa, kwa kweli siku ya leo

    simuelewielewi kabisa bosi.”

    “Inawezekana ni malaria tumuwahishe

    hospitali.”

    Mustafa kila alipojaribu kuzungumza sauti

    haikutoka, alikwishajua makosa yake kwa

    kutaka kutoa siri ya Shehna ambaye

    alifahamu kuwa si kiumbe cha kawaida

    kutokana na matukio yaliyokuwa ya kimtokea

    japo awali hakutaka kukubaliana na akili yake

    kuwa Shehna si kiumbe cha kawaida.

    Aliamini yote yaliyotokea haikuwa ndoto bali

    kweli baada ya kuupata ukweli wa wasiwasi

    wake wa tumbo la Shehna. Vyote alivyoviona

    na kujikuta amelala katika ya bahari aliamini

    moja kwa moja mpenzi wake si mtu wa

    kawaida bali jini japokuwa hakuwahi kumuona.

    Alijiuliza nini hatima yake baada ya kutaka

    kuitoa siri ya Shehna ambayo hakutaka

    kiumbe chochote akijue. Aliwasikia

    aliyopanga jinsi ya kumpeleka hospitali,

    aliwakatalia kwa kutikisa kichwa na kuomba

    kurudishwa nyumbani kwa kuwaandikia

    kwenye kalatasi.

    “Sasa mume wangu utaponaje?”


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nirudisheni nyumbani,” aliwaandikia

    kuwasisitiza wasimpeleke hospitali. Lakini

    alipoulizwa anaumwa nini aliwambia hajui ila

    wamrudishe nyumbani. Mkewe alikubaliana na

    mumewe na kumrudisha nyumbani.

    Mustafa alitegemea kupata simu kutokwa

    kwa Shehna naye apate nafasi ya kuomba

    msamaha. Lakini wiki ilikatika bila dalili

    zozote za simu kutoka kwa Shehna, kazini

    hakuweza kwenda kwa wiki nzima ilibidi

    apewe mtu mwingine nafasi ile huku kampuni

    ikijitolea kumtafutia matibabu.

    Hospitali zote alizokwenda halikuonekana na

    tatizo lolote, Mustafa aliogopa kuwaeleza

    sababu ya yeye kuwa vile kwa kuhofia adhabu

    zaidi toka kwa Shehna. Baada ya tiba ya

    hospitali kushindwa, watu walimshauri Husna

    kuangalia upande wa pili labda mumewe

    kachezewa. Mustafa pia hakutaka kwenda

    kwa mganga kwa kuhofia kukatazwa kwa

    mkewe kwenda kwa mganga na Shehna wakati

    wa matatizo. Lakini ilibidi akubali kwa vile

    ndugu zake wasinge muelewa.

    Ilipelekwa kwa mganga mmoja Vingunguti,

    alipofika walisubiri kwa muda ndipo

    walipopata nafasi ya kuonana na mganga.

    Alikuwa mganga kijana lakini alikuwa mtu

    aliyejijengea sifa kutokana na kuwasaidia

    watu matatizo yao. Baada ya kukaa mganga

    alitaka kujua wateja wake wana tatizo gani.

    Husna mkewe alimuhadithia mganga toka siku

    ya kwanza kutokewa na tatizo lile kutokana

    na maelezo ya mlinzi na hatua walizochukua

    mpaka siku ile waliyompeleka mbele yake.

    Baada ya kuwasikiliza alishika mkono wa kulia

    kwenye paji la uso, baada ya muda akitikisa

    kichwa kama amesisimka na kuanza kutua

    mbwewe mfurulizo kisha aliweka mkono

    sikioni kama anasikiliza simu na kuwa kama

    anakubaliana alichokisikia kupitia kiganja

    chake cha mkono na yeye alijibu kwa kusema:


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Eeh... ndiyo... ndiyo...ndiyo...

    sawasawa...sawasawa... hapana...eeh...ndiyo...

    hapana...sawa..sawa nimekuelewa.”

    Baada ya kuzungumza vile kwa zaidi ya robo

    saa alitoa mkono sikioni na kuwatazama

    wateja wake kwa kutembeza macho kwa kila

    mmoja huku macho yake yakionekana

    kumeremeta kama ya simba na kuwatisha

    wateja wake. Wote walikuwa kimya

    wakimsikiliza kwa sauti kama mtu anayevuta

    moshi wa kitu ndani alisema:

    “Tatizo nimeliona, lakini linaonesha mwenyewe

    analijua tatizo.”

    “Kwa hiyo unatusaidia vipi?”

    “Dawa yake hakuna ila naomba wote mtoke

    abakie mgonjwa,” mganga aliomba kuachwa

    peke yake na mgonjwa.

    “Mmh! Kwa hiyo ndiyo atapona?” Husna

    aliuliza.

    “Naomba kwanza mtoke.”

    Walitoka nje na kumuacha Mustafa na

    mganga, baada ya kutoka mganga alitulia kwa

    muda kisha alimwita Mustafa kwa jina lake.

    “Mustafa.”

    “Naam,” sauti ilitoka.

    “Unajua tatizo lako?”

    “Ndiyo.”

    “Kwa nini ulifanya vile?”

    “Nilikuwa na wasiwasi na mpenzi wangu

    kutokana na mimba yake, ndiyo maana

    nilikiuka masharti yake ili nione gizani kuna

    nini.”

    “Unajua kilichompata msaidizi wako?”

    “Sijui.”

    “Ubishi kama wako, sasa hivi ni mbwa.”

    “Mungu wangu!” Mustafa alishtuka na kushika

    mdomo.

    “Baada ya kufanya kosa la kwanza bado

    umeendelea kufanya kosa lingine la kutaka


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kutoa siri ambayo ni yako peke yako hatakiwi

    mtu kujua. Ni kweli mpenzi wako ni jini hilo

    ulitakiwa kulijua mapema na si kwa kuitoa siri

    nje.”

    “Jini?” Mustafa alishtuka.

    “Unashtuka nini wakati matukio yote yalikuwa

    si ya kawaida, kwa vile bado ilibakia siri,

    mpenzi wako kila alipozima taa aligeuka kuwa

    jini kamili na tumbo lile kubwa ni mimba

    yake.”

    “Sasa nitafanyaje?”

    “Kitendo cha Shehna kuja mbele yako wakati

    unataka kutoa siri nje, amesababisha

    maumivu makali ya tumbo sasa hivi yupo hoi.

    Msaada wako ni kuendelea kuwa hivyohivyo ili

    ibakie siri mpaka ajifungue, kama atakufa

    lazima na wewe utakufa kwa vile tayari kuvuli

    chako kimo ndani ya damu yako ambayo wale

    wanao walio tumboni katika ujauzito ile.

    “Hukutakiwa kuuona tumbo akiwa katika

    umbile la kijini, ungeweza kufa muda uleule,

    lakini mapenzi ya jini yule ni makubwa sana.

    Kwa vile bado hukutaka kuelewa ukutaka

    kutoa siri ile hapo ndipo ulipopewa adhabu

    ambayo itaisha mpaka ajifungue.”

    “Lini?”

    “Baada ya miaka miwili.”

    “Miaka miwili niwe hivihivi?” Mustafa

    alishtuka.

     


    Baada ya miezi saba atakapojifungua."

    "Mmh! Miezi saba niwe hivihivi?" Mustafa alishuka.

    "Hiyo ndiyo faida ya kiburi chako na adhabu hiyo ni ndogo kuliko zote ambazo amezitoa mama yake baada ya Shehna kuingilia kati kitendo chako kile kimemuumiza sana mama yake. Bila hivyo ulitaka kugeuzwa hamnazo."

    "Mungu wangu, sasa utanisaidia vipi?"

    "Sina msaada wowote zaidi ya kuitumikia adhabu yako, zaidi ya hapo ukitaka chokochoko utapotea wewe na waliokuzunguka."

    "Siwezi kuonana na Shehna nimuombe msamaha?"


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Yupo katika uangalizi mkali baada ya kutoka ujinini bila idhini ya wazazi wake ili kukuzuia usiitoe siri yake na kumsababishia matatizo makubwa sasa hivi hana kauli, hajiwezi kwa lolote."

    "Kwa hiyo utakuwaje?" Mustafa alishtuka.

    "Adhabu yako ni kuitunza siri hii kwa miezi saba, cha kuomba Shehna apone upesi ili uweze kukupunguzia adhabu au kukuondolea ububu."

    "Kwa hiyo baada ya mazungumzo narudia katika hali ya ububu?"

    "Ndiyo usalama wako."

    "Itanibidi nikubali sina jinsi," Mustafa alikubali kwa shingo upande.

    Baada ya makubaliano aliitwa Husna mke wa Mustafa na mtu aliyemsindikiza ambao waliamini watakuta mabadiliko ya kukuta akizungumza. Lakini ilikuwa tofauti na mawazo yao, Mustafa alikuwa bado yupo katika hali ya ububu.

    "Umefika wapi?" Husna aliuliza.

    "Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu imeonesha ugonjwa huu utatoka taratibu bila kutumia dawa yoyote."

    "Itachukua muda gani?"

    "Sijajua, ila msirogwe kwenda kwa mganga yeyote eti amponye, dawa atakayompa ndiyo itakayomfanya awe bubu milele."

    "Kwa hiyo hata panadol tusimpe akiumwa?" Husna aliuliza.

    "Dawa zote mpeni, ila si za kutibu ugonjwa huu, msikubali kumpeleka kwenye maombi ya aina yoyote au kwa mganga yeyote. Ukifanya hivyo mtanikumbuka."

    "Sawa tunashukuru."

    Baada ya kukubaliana na mganga walimchukua mgonjwa wao ambaye ilikuwa vigumu kuamini anaumwa kwani alikuwa kwenye hali ya kawaida na kurudi naye nyumbani.



    ***

    Siku zilizidi kukatika huku Mustafa akiwa katika hali ya ububu na Sara akiwa katika umbile la mbwa. Mateso makubwa yalikuwa kwa Sara ambaye aliendelea kuishi maisha ya kujificha kukimbia watoto kumpiga mawe na kulala kwenye majumba mabovu.

    Chini ya bahari, Shehna alipata nafuu haraka sana na kuweza kukaa hata kula mwenyewe baada ya kupoteza fahamu kwa miezi mitatu iliyotishia uhai wake. Kukubali kwa Mustafa kuendelea kuwa katika hali ya ububu na kuyakubali maelekezo ya mganga, ile ilimsaidia sana kuwahi kupata nafuu.

    Kama mkewe Mustafa angekuwa mbishi lazima angewapoteza mumewe na


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Shehna pamoja na watoto waliokuwa tumboni. Baada ya kupata nafuu alitaka kujua Mustafa yupo katika hali gani kwani aliamini hasira za mama yake lazima angemfanya kitu kibaya.

    Katika vitu vyote alimkataza mama yake kumuua hata kumpa adhabu kali mpenzi wake.

    "Mama mpenzi wangu yupo katika hali gani?"

    "Nilimgeuza bubu ili asitoe siri mpaka muongee wenyewe na kukubaliana."

    "Nimepona, vipi hali yake kwa sasa?"

    "Bado sijamtoa ububu lakini niliyaangalia maisha yake ya siku zote, ila amenifurahisha kutotafuta dawa kwa ajili ya kutibu ububu. Kitendo kile kimesaidia wewe kupata nafuu upesi."

    "Mustafa ni msikivu sijui kwa nini siku ile hakutaka kunielewa mpaka akawasha taa."

    "Wewe ndiye mwenye makosa, ulitakiwa kujitambulisha mapema kwa vile alikuwa akikupenda sana, angekuelewa."

    "Mama nilihofia kumueleza mimi jini, angenikimbia."

    "Ona sasa alikuwa anatoa siri nje kwa vile alikuwa hakuelewi, kila kitu kingekuwa wazi, ububu na uelewa wake ndiyo nafuu yako, bila hivyo ungekufa, hali ilikuwa mbaya."

    ‘Sasa nifanye nini?"

    "Aletwe leo aambiwe ukweli lazima atakuelewa tu."

    "Sawa mama."

    Malkia Zaldau mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu mama wa Shehna walikubaliana na mwanaye usiku wa siku ile Mustafa apelekwe chini ya bahari.

    ***

    Mustafa alishituka usingizini na kujikuta akiwa pembeni ya Shehna ambaye tumbo lake lilikuwa limeongezeka katika umbile la kibinadamu lililokuwa ndani vazi la kulalia. Shehna alikuwa akimtazama huku macho yakiwa yamejaa machozi na kuongeza uzuri wake.

    "Shehna."

    "A..abeee," aliitikia kwa sauti ya kilio.

    "Nisamehe mpenzi wangu."

    "Huna kosa, nisamehe mimi."

    "Kwa kosa gani mpenzi?"

    "Nimekutia kwenye mateso bila kosa."

    "Shehna huna kosa bali mimi ndiye niliyeshindwa kukusikiliza."

    "Hapana Mustafa mwenye makosa ni mimi kushindwa kukueleza ukweli mapema."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/






    "Shehna nimekuelewa, najua una wasiwasi lakini ulitakiwa kunieleza mapema, nilikuwa na wasiwasi wewe labda nani lakini akili yangu ilikataa."

    "Kwa hiyo umenielewa mimi ni nani?"

    "Ndiyo."

    "Hutaniacha?"

    "Nilikueleza mapema sitakuacha maishani mwangu wewe ni kiumbe muhimu sana. Najuta kutaka kukupoteza wewe, mimi mwenyewe na watoto wetu watarajiwa."

    "Mustafa ukitoka hapa hutaitoa siri hii kwa watu?"

    "Sitatoa, nimejua makosa yangu sitarudia, Shehna wewe ni kiumbe mwenye huruma sana na mapenzi mazito."

    "Kesho utarudi katika hali yako, ukiamka rudi kazini kama kawaida, usihoji kitu chochote ukifika endelea na kazi zako."

    "Sawa nimekuelewa."

    "Mustafa nitafanya kila kitu ili maisha yako yawe juu baada ya kujifungua nitakubadilishia kazi nataka uwe mmoja wa matajiri duniani."

    "Asante mpenzi wangu," Mustafa alimkumbatia Shehna kwa furaha.

    "Naomba usiniogope kwa vile ushanijua."

    "Siwezi, nakupenda Shehna."

    "Baada ya kunipa zawadi ya mtoto baada ya mimi kujifungua mkeo naye atapata mtoto. Nisingempa dawa ya ujauzito mkeo kwa sasa kwa vile nisingeweza kujifungua mpaka ajifungue yeye hivyo ningeteseka kwa uchungu kwa muda mrefu."

    "Nimekuelewa mpenzi."

    Baada ya mazungumzo ya kimabaha walilala kwa Shehna kuzima taa na kuondoa nguo zote kumuachia Mustafa kulichezea tumbo lililokuwa zimezidi kuwa kubwa. Ilikuwa ni siku ya furaha kwake. Alipanga siku nyingine amuombee Sara msamaha ili atolewe kwenye umbile la kimbwa.

    ***


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku ya pili Mustafa aliposhtuka asubuhi alijaribu kumwita mkewe sauti ilitoka.

    "Mke wangu."

    "Ha! Jamani Mungu mkubwa umepona mume wangu?" Husna alikurupuka usingizini baada ya kusikia sauti ya mumewe.

    "Ndiyo."

    "Jamani Mungu mkubwa, siamini kama mume wangu leo ukizungumza sauti inatoka!"

    "Niandalie maji nioge ili niwahi kazini."

    "Unataka kwenda kazini?"

    "Ndiyo."

    "Kwani unajua ulikuwa kwenye hali gani?"

    "Najua, si sauti ilikuwa haitoki sasa naweza kuwasiliana na wateja kama kawaida."

    "Si ungeiangalia hali yako kwa wiki ndipo uende kazini?"

    "Ni kweli, lakini naamini nimepona."

    "Mmh! Haya."

    Mkewe Husna alinyanyuka kitandani na kwenda kumwandalia maji mumewe, baada ya kuoga na kupata kifungua kinywa aliondoka kwenda ofisini. Mlinzi alipomuona alishtuka.

    "Ha! Bosi."

    "Vipi John."

    "Umepona?"

    "Ndiyo, nipo ofisini," Mustafa hakutaka mazungumzo mengi aliingia moja kwa moja ofisini na aliikuta ipo katika hali ya usafi aliouzoea japo hakuwepo kwa muda mrefu. Hakukuwa na mabadiliko yoyote naye hakuhoji kitu kama alivyoelekezwa na mpenzi wake Shehna. Alifanya kazi kama kawaida mpaka jioni na kurudi nyumbani.

    Husna alizidi kumshangaa mumewe na kutaka kujua tatizo lile lilitokana na nini. Baada ya chakula cha usiku wakiwa kitandani alitumia nafasi ile kumuuliza mumewe kilichomsibu.

    "Mume wangu pole kwa matatizo, maana asubuhi sikuweza kuzungumza na wewe baada ya kutoka kuwa na haraka ya kuwahi kazini."

    "Asante."

    "Hivi nini kilichokusibu kupoteza uwezo wa kuzungumza mpaka mganga akasema hutakiwi kutumia dawa yoyote?"

    "Mke wangu tuacheni na hayo."

    "Hapana mume wangu, ni mimi ndiye nilikuwa nateseka kuishi na wewe muda wote ukiwa bubu. Lazima kuna kitu kilichosababisha hali ile, hata mlinzi alishtuka kuona ukibadilika ghafla wakati mlikuwa mkizungumza."

    "Naomba uachane na hayo mke wangu kwa vile nimepona."

    "Kwa nini?"

    "Kuwa mwelewa au unataka nirudi katika hali niliyokuwa nayo?"

    "Hapana."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Basi tuachane na hayo."

    "Nimekuelewa mume wangu."

    Mustafa aligeukia upande wa pili na kuvuta shuka, mkewe naye alijisogeza karibu na mumewe na kumkumbatia kuitafuta siku ya pili.

    ***

    Kama kawaida Mustafa alishtuka na kujikuta akiwa pembeni ya mpenzi wake, uso wa Shehna ulikuwa na tabasamu pana na kuzidi kuongeza uzuri wake. Alimuangalia sana Mustafa kama anataka kusema kitu na kufanya aulize.

    "Vipi mpenzi?"

    "Najua kuna kitu kinakuumiza akili siku nzima."

    "Kitu gani?"

    "Kuhusu Sara."

    "Ni kweli, nilipanga kumuombea msamaha, nina imani wote tumekukosea."

    "Mustafa wewe hujanikosea lakini Sara kanikosea sana kafikia hatua ya kutaka kuniua!" Shehna alisema kwa sauti ya kilio.

    "Adhabu aliyopata nina imani hawezi kurudia tena."

    "Mustafa nitamleta mbele yako aseme siku akirudia sitampa adhabu bali kumuua, nimefanya hivyo kwa ajili ya mapenzi yangu kwako."

    "Nakuahidi kuusemea moyo wake hatarudia tena."

    "Sawa."

    Shehna alinyanyuka na kutoka nje na kupiga makofi, vijakazi na watwana walifika haraka mbele yake kumsikiliza.

    "Naam binti wa mfalme wa bahari ya dhahabu unasemaje?"

    "Kamleteni Sara mbele yangu."

    "Sawa binti mfalme."

    Alitoweka ghafla na kumuacha Shehna akirudi ndani, kabla hajaweka makalio chini Sara alikuwa mbele yake katika umbile la kimbwa. Mustafa alishtuka kumuona mbwa mbele yao.

    "Mustafa usishtuke huyu ndiye Sara."

    "Ha! Usishangae, sijawahi kuona kiumbe mwenye kiburi kama huyu mwanamke."

    Sara yote aliyasikia lakini aliogopa kusema kuomba msamaha kwa kuogopa kubweka na kuwatisha.


     Machozi yalimtoka na kupiga magoti kuomba msamaha kwani mateso aliyopata asingeyasahau mpaka anakufa. Mustafa machozi ya uchungu yalimtoka kumuonea huruma Sara anavyotaabika.Shehna alimshika Sara kichwani, ghafla alirudi katika umbile la kibinadamu. Hakusubiri maelezo, Sara alijitupa chini ya miguu ya Shehna kuomba msamaha."Shehna shoga yangu najua jinsi gani nilivyokukosea, nipo chini ya miguu yako haki ya Mungu, sitarudia tena kukufuatilia wala kufuatilia mambo yasiyonihusu. Nimeamini sisi wanadamu ndiyo wabaya, pamoja na mabaya yote niliyokutendea, hukuniacha nilale na njaa wala nile jalalani.Nakuahidi kama utanibakiza na umbile langu la kibinadamu, nitakuwa kiumbe kipya, sitajiingiza tena katika mambo yasiyonihusu.""Nina imani sasa unanijua, mimi ni nani?" Shehna alimuuliza huku akimtazama kwa jicho kali.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Shehna."

    "Nilipokuja kwako ulinionaje?"
    Sara alishindwa kujibu alibakia kimya, Shehna alimuuliza tena.

    "Ulikwenda kwa waganga ili kuchunguza kama mimi ni nani?"

    "Ji.." hakumalizia, aliogopa kusema.
    "Malizia tu, kwani nilipokuja kwako nilikuambia mimi ni nani?"

    "Jini."

    "Baada ya kunijua?"
    "Shehna, nimekukosea naomba unisamehe sitarudia tena, najutia nafsi yangu," Sara alilia kilio cha majuto.

    "Mustafa elewaneni na Sara ili likitokea, mimi simo tena," Shehna alijitoa kwenye kiburi cha Sara.

    "Sara, ukitoka hapa, ya hapa yaache hapahapa ukiropoka litakalokukuta utalia na nafsi yako."
    "Kaka Mustafa sirudii tena, nimejifunza kiburi si maungwana."

    "Nina imani mmeelewana leo sitazungumza chochote siku ukinitibua, nitakufanya kiumbe cha ajabu, siwezi kukuua tu ila cha moto utakiona."
    "Shehna nakuapia sitathubutu kusema chochote wala kufanya lolote."

    "Kesho utaamka asubuhi nyumbani kwako, majirani wakikuona lazima utakutana na maswali mengi, usiwajibu kitu, oga wahi kazini."

    "Nimekuelewa shoga yangu."
    Shehna alimshika Sara kichwa na kujikuta akipitiwa usingizi mzito, aliwaita wasaizidi wake wamrudishe nyumbani kwake ili asubuhi aamkie kitandani kwake.Baada ya Sara kuondoka, Shehna alimgeukia Mustafa aliyekuwa ametulia akimtazama na kumwambia:

    "Mustafa, kuanzia leo sitaonekana mchana wala kufika kazini kwako."

    "Kwa nini?"
    "Sina tena uhuru wa awali, najiuliza atakaponiona mchana utanionaje au Sara akiniona ofisini atanionaje?"

    "Nina imani kila kitu kimeisha, nimesha kuelewa, siwezi kukushangaa."
    "Kwako, lakini kwangu itachukuwa muda kujionesha wazi kwako."

    "Sasa nikiwa na shida na wewe?"
    "Utaniona mara moja lakini si kama mwanzo."

    "Mmh! Sawa," Mustafa alikubali kwa shingo upande.

    "Mustafa naomba ukubaliane na mimi ili twende sawa."

    "Nimekubali mpenzi."



    ***


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku iliyofuata Sara alishtuka asubuhi na kujikuta kitandani kwake, aliamka na kwenda kuoga. Alipotoka nje, majirani zake walimshangaa na kumuuliza alikuwa wapi. Aliwajibu alikuwa safari ila wangezungumza vizuri jioni akirudi kazini. Alikwenda kazini kama kawaida.
    Akiwa kazini alijawa na mawazo mengi juu ya maswali ya majirani zake, alijiuliza akirudi atawaeleza alikuwa wapi baada ya kuondoka ghafla. Mawazo yalipokuwa mengi, aliamua kwenda kwa bosi wake kuomba ushauri, baada ya kumsikiliza alimwambia:

    "We wanyamazie tu."
    "Wasumbufu sana watataka kunichimba, nitashindwa kuwajibu."

    "Ulikuwa na wazo gani?"

    "Kuhama pale."
    "Hakuna tatizo."

    Mara simu iliita Mustafa alipoangalia alikuta ni Shehna, alisema kwa sauti.

    "Shehna."
    "Anasemaje shoga yangu," Sara alisema kwa tabasamu.

    Alipokea simu:

    "Haloo mpenzi."
    "Nipe Sara." Mustafa alimpa simu Sara.

    "Haloo shoga," Sara alisema baada ya kuchukua simu.

    "Ni hivi, ukitoka hapo usirudi nyumbani, umeshahamishwa."

    "Nimehamishiwa wapi?"
    "Masaki, nyumba inatazamana na duka la jumla, nina imani hayo yatakuwa maisha yako mapya."

    "Asante shoga, ufunguo?"
    "Mustafa atakupeleka sehemu yako mpya."

    "Asante shoga."

    "Haya kwaheri."
    Sara alimpa Mustafa simu, baada ya kupokea alipewa maelekezo na Shehna, baada ya kukata simu alimgeukia Sara na kumueleza.

    "Ukimaliza kazi nitakupeleka."
    "Duh! Siamini nikitoka kazini nakwenda Masaki, siamini nami nimekuwa mtu wa matawi ya juu!" Sara alisema akishika kifua.

    "Hongera, ulitaka kumtibua bure kumbe mambo mazuri yalikuwa yakija."

    "Mbona nimekoma."
    "Nina imani tatizo lako limekwisha, kaendelee na kazi."

    "Sawa bosi," Sara alirudi kuendelea na kazi.
    Muda wa kutoka Mustafa alimpeleka Msaki kwenye nyumba aliyoelekezwa na Shehna. Ilikuwa nyumba nzuri iliyokuwa na kila kitu ndani, hakukuwa na kitu chochote kutoka chumbani kwake zaidi ya vitu vyake vyote muhimu. Sara aliendelea kumshukuru Shehna na kuona kumbe jini ni umbile lakini wapo wenye roho nzuri kushinda hata wanadamu.

    ***


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwezi moja kabla ya kujifungua, Shehna alimweleza Mustafa kuwa muda ule anatakiwa kuwa sehemu maalum ambayo hatakiwi mtu yeyote kuingiza zaidi ya mzazi wake na mkunga tu.
    Pia alimweleza kuonana naye itakuwa baada ya miaka mitatu. Mustafa alikubaliana naye, hakuwa na kipingamizi.



    Muda ulipofika Shehna alijifungua watoto mapacha watatu wa kike wawili na wa kiume mmoja. Ilikuwa ni furaha ilioje kufanikiwa kupata watoto toka kwa mwanadamu. Wakati wa kujifungua mawasiliano kati ya Mustafa na Shehna yalipotea, siku zote Mustafa alikuwa na hamu ya kuonana na Shehna lakini masharti yalimzuia.

    Shehna baada ya matukio yote ya kuhatarisha maisha yake alikatazwa na wazazi wake asionekane mchana katika umbile la kibinadamu kwa muda wa miaka mitano nyongeza ya miaka miwili.

    “Shehna kama mtoto umepata, sasa tulia kama ukiwa na shida na baba wa watoto wako tutamleta hukuhuku akiwa ndotoni baada ya miaka mitatu. Lakini kuonana naye akiwa na akili timamu ni baada ya miaka mitano.”

    “Kwa hiyo nitarudi lini kama zamani?”

    “Baada ya miaka kumi na tano ruksa kurudi t-ena katika umbile lako la kawaida na kutembea mchana kila mtu atakuwa amesahau yote yaliyopita hata watoto kumtembelea baba yao.”

    “Sawa.”

    Kuanzia siku ile Shehna aliendelea kulea wanaye kwa muda wote huo hakuweza kuwasiliana na Mustafa japokuwa alijua mzazi mwenzie alikuwa katika mawazo mazito ya kumtafuta mpenzi wake. Lakini aliheshimu maelekezo ya wazazi wake kwa kuhofia kwenda kinyume na kukutwa na matatizo.

    Wakati Shehna akipewa maelezo na mama yake upande wa pili nyumba ya Mustafa ilikuwa inawaka moto baada ya wazazi wa Mustafa kumjia juu mtoto wao kutokana na siku kukatika bila kupatikana mtoto. Pamoja na kuwasihi wawe wavumilivu kwa vile mtoto ni siri ya Mungu hawakukubaliana naye.

    Walitaka aachane na Husna kwa vile walikuwa wakitaka mjukuu, aliwaeleza mwaka ule ukiisha bila mkewe kushika ujauzito ruksa kuivunja ndoa yao. Wazazi wake walimkubalia na kumweleza mwaka ukikatika bila mtoto watampelekea mke nyumbani kwake.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mustafa aliondoka kwao kichwa kikimuuma na kujiuliza zawadi aliyotaka kupewa na Shehna ya mkewe kushika ujauzito atapewa lini. Upande mwingine alimlaumu mkewe kwa kitendo chake kukiuka masharti ya Shehna muda ule wangekuwa na mtoto. Kibaya zaidi muda ule alikuwa amepoteza mawasiliano.

    Alirudi nyumbani akiwa mnyonge sana, hakujua hatima ya ndoa yake kwa kuona mwaka unaweza kukatika kabla mkewe hajashika ujauzito na kufanya wazazi wake kumletea mke mwingine.

    Usiku wa siku ile alichukuliwa na kupelekwa chini ya bahari, aliposhtuka alijiona yupo pembeni ya Shehna ambaye wakati huo hakuwa na tumbo kubwa. Ile ilimjulisha moja kwa moja tayari Shehna amejifungua.

    “Pole mpenzi wangu.”

    “Sijapoa kwa vile ndoa yangu inavunjika wakati wowote.”

    “Najua ndiyo maana nimekuleta huku kabla muda wake, ilikuwa kazi nzito kuwashawishi wazazi wangu uje huku wakati ni juzi tu nimejifungua. Kwanza napenda kukupa hongera ya kuwa baba wa watoto wangu.

    “Mungu kajalia nimejifungua mapacha watatu wawili wa kike mmoja wa kiume, wa kike ni wazuri kuliko mama yao na wa kiume ni mzuri kama baba yake. Kwa vile muda wangu wa kutoka huku bado. Niliwaomba wazazi wangu uje tujadiliane ili kuiokoa ndoa yako.”

    “Nitashukuru.”

    “Sasa kuna kitu nataka tukifanye iwe siri yetu, kwa sasa itakuwa vigumu kwa mkeo kushika ujauzito mpaka watoto wangu wafikishe mwaka. Kwa muda uliozungumza na wazazi wako lazima utapita na wazazi wako watavunja ndoa, najua na wewe unampenda sana mkeo.”

    “Ni kweli.”

    “Ni hivi nitampatia mkeo mimba tupu ambayo itakuwa ya muda mfupi kuliko mimba zote. Muda ukifika atakwenda kujifungua, kitakachotoka tumboni mwake kitakuwa upepo ambao utafanya wakunga wapitiwe na usingizi mfupi pamoja na mkeo. Sauti ya mtoto ndiyo itakayo washtua wakiamka watakuta mtoto pembeni ya mama yake.”

    “Umesema atakuwa na mimba hewa na tumboni kutatoka hewa mtoto huyo atatoka wapi?”

    “Mustafa nipo kwa ajili yakuokoa ndoa yako, kati ya wanangu nitamtoa mmoja ambaye wakati wamelala ataletwa na kuachwa hapo ili wakishtuka wajue amejifungua.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nina imani baada ya hapo kesi itakuwa imeisha kwa wazazi wako kuamini mkeo siyo mgumba.”

    “Kwa hiyo utamuachia huyo mtoto?”

    “Hapana nitampa kwa miezi mitatu, kisha nitamchukua. Nahofia akianza kukua atakuwa na tabia za ajabu ambazo zitawachanganya hasa mkeo na majirani. Kwako atakuwa mwoga kwa vile ni baba yake lakini kwa mtu mwingine itakuwa vigumu kumsikiliza.”

    “Utamchukua vipi?”

    “Atapotea katika mazingira ya kutatanisha, usishtuke nitakuwa nimemchukua mwenyewe.”

    “Sisi utatuachaje?”

    “Najua mkeo ataumia kupotelewa na mwanaye, mbembeleze kwa vile baada ya muda mfupi atashika mimba ya kweli na kuzaa mtoto wa kwenu asiye na masharti.”

    “Mmh! Sawa.”

    “Mustafa usihuzunike kwa vile sina jinsi lazima nifanye hivyo ili kuokoa ndoa yako, nitakupa dawa utampa kwenye maji akinywa atakuwa na dalili zote za ujauzito. Najua atashtuka mwambie anywe maji glasi moja kuituliza.

    Ujauzito huo utakuwa wa miezi mitano safari hii nendeni hospitali ili wazazi wako wajue ujauzito kumbe ni wa muda mrefu, baada ya miezi miwili atajifungua.”

    “Sawa.”

    Mustafa aliposhtuka akijikuta amelala kitandani kwake akiwa na dawa mkononi. Aliamka na kutulia kitandani kwa muda akikumbuka yote aliyoelezwa na Shehna, hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali ili kuiokoa ndoa yake.

    Asubuhi kabla ya kwenda kazini alimpa mkewe dawa aliyopewa usingizini na Shehna, baada ya mkewe kunywa alimuaga na kwenda kazini. Alipofika kazini kabla ya kuanza kazi mkewe alimpigia simu hali yake ni mbaya kama mtu mwenye ujauzito wa muda mrefu.  




    Alimwambia anywe glasi moja ya maji, mkewe alifanya hivyo, baada ya kunywa hali ilitulia lakini alikuwa amechoka sana, alipanda kitandani kulala. Alipoamka alijishangaa kukuta tumbo limekuwa kama ujauzito wa muda mrefu.Ile hali ilimshtua na kumpigia simu mumewe kumweleza kilichotokea.

    “Usiogope hiyo ni hali ya kawaida huenda ujauzito huo uliingia muda mrefu, dawa niliyokupa imeufukua hivyo usiwe na wasiwasi. Kama vipi nenda hospitali ukapime hali yako.”


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    “Mume wangu hunipendi, tuliambiwa nini na Shehna?”

    “Amesema sasa tunaweza kwenda.”

    “Hapana tafuta ufumbuzi mwingine, sirudii kosa kidogo nife,” Husna aliogopa kurudia kosa.

    “Usiwe na wasi mke wangu, Shehna ameruhusu, basi subiri nije nikupeleke mwenyewe.”

    “Kama hivyo sawa.”

    Mustafa aliacha kazi zake na kurudi nyumbani kumfuata mkewe na kumpeleka hospitali, alipofika nyumbani alishtuka kuona tumbo la mkewe limekuwa kubwa la ujauzito wa muda mrefu.

    Lakini alificha mshtuko wake kwa kuhofia kumshtua mkewe na kuona kitu cha ajabu kimemtokea. Alimchukua na kumpeleka hospitali ambako katika kufanyiwa vipimo ilionesha ujauzito upo sawa.

    Daktari alishangaa kukaa nao zaidi ya miezi mitano bila kufika hospitali, alimuonya asifanye vile tena kukaa na ujauzito kwa muda mrefu vile.

    Baada ya maelekezo waliruhusiwa kurudi nyumbani akiwa amechoka kama ujauzito wote ulipitia hatua zote kufikia hatua ya kumchosha vile.

    Walikubali na mumewe kukaa na siri ya chanzo cha ujauzito ule, ilikuwa tofauti na ujauzito anaoufahamu. Miezi miwili baadaye ujauzito ulipofikisha miezi saba kwa vipimo vya hospitali na maelezo ya Shehna, Husna alishikwa na uchungu mkali na kukimbizwa hospitali.

    Kutokana na muda wa ujauzito ule, wengi waliamini ni maumivu ya tumbo tu, lakini kulionekana dalili zote za kujifungua.

    Baada ya kufikishwa Husna aliendelea kuugungulia huku mkono mmoja umeshika kiuno na mwingine kichwa kutokana na maumivu makali ya uchungu.

    Wauguzi walimkimbiza wodini wakiwa hawana uhakika kama siku ile ndiyo ilikuwa ya kujifungua. Baada ya kumfikisha walimpandisha kitandani huku Husna akiendelea kulalamika katika dalili zote za kujifungua. Ilibidi wampe huduma ya kujifungua, Husna alianza kusukuma mtoto, ghafla ulitoka moshi uliowafanya wote walewe na kusinzia.

    Muda huo Shehna alimtuma jini wa kike kumpeleka mtoto wake wa kiume aliyekuwa akifanana na baba yake na kumweka pembeni ya Husna. Baada ya muda wote walishtushwa na kilio cha mtoto. Mtoto alikuwa amesha katwa kitovu kabisa na kusafishwa.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakuna aliyejua nani kafanya vile, kila mmoja aliamini mwenzake ndiye kafanya. Walimpa hongera mzazi kwa kupata mtoto wa kiume mwenye afya nzuri, hali ya mzazi nayo ilikuwa njema. Alipelekwa wodini kwa huduma zaidi. Baada ya taratibu zote, Husna aliruhusiwa kutoka hospitali na kurudi nyumbani na mwanaye ambaye kila aliyemuona alisema anafanana na baba yake.

    Mustafa alijua kila kitu na kubaki na siri nzito moyoni huku amani akirudi nyumbani kwake kwa familia kufurahi na kusema mpaka wamtishe ndipo atafute mtoto. Japokuwa yule mtoto alikuwa wa kwake lakini hakuwa wa mkewe bali wa jini Shehna.

    Siku nazo zilikatika muda nao ulisogea mtoto wa Shehna kurudi kwa mama yake.

    Miezi mitatu ilipotimu, alitumwa jini kumfuata mtoto, akiwa katika umbile la kibinadamu mwanamke aliyevaa kiheshima. Jini Shaunani alitembea taratibu na kubisha hodi kwenye nyumba ya Mustafa.

    Wakati huo mke wa Mustafa alimkuta amemaliza kumnyonyesha mtoto, alikwenda kufungua mlango na kumuona mwanamke mzuri aliyekuwa akinukia manukato kama anayotumia mumewe.

    “Karibu.”

    “Asante,” mgeni alijibu huku akiingia ndani.

    Alipofika aliketi na kusema:

    “Habari za hapa.”

    “Sultani hajambo?” lilikuwa jina la mtoto ambalo Mustafa aliambiwa ampe mtoto na ndilo lilikuwa jina lake la ujijini.

    “Hajambo.”

    “Hebu nimuone.”

    Husna bila wasi alimkabidhi mtoto jini Shaunani ambaye alikuwa mcheshi sana. Kutokana na ucheshi wake, alimzoea haraka Husna, hakuwa na wasiwasi alimuomba samahani.

    “Samahani mgeni natoa vyombo vya mtoto.”

    “Hakuna tatizo.”

    Husna alirudisha vyombo vya mtoto jikoni na kurudi kumsikiliza mgeni, baada ya kukaa alimkaribisha tena.

    “Karibu mgeni.”

    “Asante,” kabla Husna hajaongeza neno simu iliita na kumshangaza kuitia chumbani wakati alikuwa nayo muda mfupi na hakurudi chumbani.

    “Jamani hii ajabu simu nilikuwa nayo hata sijui niliondoka nayo muda gani kwenda nayo chumbani.”


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Labda umesahau haiwezi kujibeba yenyewe, kasikilize huenda ni shemeji,” jini Shaunani alisema.

    Husna alinyanyuka na kwenda kupokea simu, kitendo cha kuingia chumbani tu. Jini Shaunani alitoweka na mtoto. Husna alipofika chumbani alishangaa kukuta simu haina ‘missed calls’. Alishangaa wakati alisikia simu ikiita kabisa hata mgeni alisikia.

    Alitoka sebuleni alishangaa kukuta sebule tupu, hakuna mgeni wala mtoto wake.

    “Mgeni...mgeni,” aliita kwa sauti.

    Hakukuwa na jibu alitoka nje labda ametoka vilevile hakukuwa na jibu lolote, alijiuliza atakuwa amekwenda wapi.

    Alitoka hadi nyumba ya pili labda wamemuona mtu akiwa na mtoto nao walisema hawajamuona. Alimpigia simu mumewe kumueleza kupotea ghafla kwa mwanaye.

    Taarifa ile haikuwa ngeni kwa Mustafa, alijua mtoto keshachukuliwa na mama yake. Alirudi nyumbani haraka ili kumtuliza mkewe ambaye muda ule alikuwa amepagawa.

    Alipofika alimkuta amepagawa akilia ovyo mikono kichwani. Husna alipomuona mumewe alimkimbilia na kumkumbatia na kuendeleza kilio.

    “Mume wangu mwanangu ameibiwa!”




    Alijitahidi kumbembeleza na kumueleza watamtafuta, walipeleka taarifa polisi na kwenye vyombo vya habari lakini ajabu walipotafuta picha za mtoto hawakuziona. Taarifa ilitawanyika kila kona ambayo siri yake alikuwa akiijua Mustafa. Familia ya mume nayo iliungana na Husna katika tukio lile.

    Japokuwa mtoto alikuwa amepotea lakini hali ya amani ilikuwepo kwenye ndoa na wazazi kuamini mkwe wao siyo mgumba. Walimpa moyo kuwa awe makini na watu wasiojulikana kutokana na tabia za watu kuiba watoto wachanga. Mustafa alitengeneza uongo kwa kumueleza kuwa Shehna amesema asilie kwa vile mtoto wao atarudi na kumfanya aishi kwa matumaini.

    Kupotea kwa mtoto kulifanya wazazi wa Mustafa waendelee kumpa moyo Husna kwa kuhofia kumuumiza kwa kumkumbusha maumivu ya kuibiwa mtoto wake. Baada ya miezi saba kukatika, usiku mmoja Mustafa aliota akizungumza na Shehna akimueleza kuwa ni muda muafaka mkewe kushika ujauzito wa kweli.

    Shehna aliendelea kumueleza mtoto yule atakuwa chini ya ulinzi wa majini mpaka atakapokuwa ndipo atarudishwa chini ya wazazi wake. Lakini wakati huo ndugu zake watakuwa wamekua, wataendelea kumlinda siku zote za uhai wake.

    Baada ya wiki moja akiwa kazini mkewe alimpigia simu kumweleza mumewe hali aliyohisi, Mustafa alijua dalili zile zilikuwa majibu ya ndoto aliyoota, walipokwenda hospitali vipimo vilionesha ujauzito wa mwezi mmoja. Ujauzito ule ulikuja kawaida wa miezi tisa tofauti na mimba ya ajabu iliyotangulia ya miezi miwili tu mtoto 


    kuzaliwa.

    Ujauzito ulikwenda vizuri ulipotimiza miezi tisa alijifungua salama mtoto wa kiume, Husna baada ya kujifungua alimlinda sana mwanaye ili asirudie kosa la awali. Mtoto alikuwa katika malezi mazuri, Mustafa na Sara waliendelea na kazi zao huku Sara akiwa na somo kubwa maishani mwake kuwa mwanadamu anaweza kuwa mbaya kuliko jini pia kutofuatilia lisilokuhusu. Hakuamini kama majini wana roho nzuri siku zote aliamini ni viumbe wabaya kumbe wapo wazuri na wabaya kama wanadamu.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mustafa alisubiri miaka mitatu ili aende kwa Shehna kwa njia ya ndoto kuwaona watoto wake japo wa kiume alimuona.

    Mtoto wao naye alikuwa vizuri bila kujua akiwa mkubwa atakuwa na tabia gani?



    Mwisho
    .
     

0 comments:

Post a Comment

Blog