Search This Blog

MIMBA YA JINI - 4

 







    Simulizi : Mimba Ya Jini 

    Sehemu Ya Nne (4)





    Ofisini walibakia Mustafa na Sara aliyekuwa amesimama.

    "Kaa," Mustafa alimwambia Sara.

    Sara alikaa kwenye kiti, Mustafa aliendelea kusimama.

    "Sara," alimwita."

    "Abee."
    "Una tatizo gani?"

    Sara ilibidi amueleze mkasa mzima kuanzia siku aliyotoka kwenda kununua nyama ya nguruwe. Lakini alificha kufuata nyama ya nguruwe na kusema alifuata chakula cha usiku na yaliyomtokea na vituko vilivyokuwa vikimtokea toka siku aliyofika nyumbani na ofisini.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sara mbona unafanya utani."
    "Kweli bosi, siwezi kusema uongo."

    "Kwa hiyo hata hapa ilitokea?"

    "Kule ilikuwa tisa kumi hapa mpaka sauti katoa."

    "Mmh! Itakuwa nini? Hebu ngoja," Mustafa alisema huku akielekea mlangoni na kuufungua kisha aliita.

    "Shehna njoo."
    "Vipi mmemalizana?"

    "Hebu njoo mara moja."

    Shehna aliingia ofisini na kusimama pembeni ya Mustafa ili kusikiliza alichoitiwa.

    "Unasemaje?"

    Alimweleza yote yaliyomtokea Sara, baada ya kumsikiliza alisema.
    "Mmh! Pole, lakini maji aliyokunywa yatamsaidia haitamtokea hali ile tena."

    "Kwa hiyo aendelee na kazi au akapumzike?"

    "Mwache akapumzike ili kesho aanze kazi vizuri."

    Mustafa alimpa ruhusa Sara akapumzike ili kesho aende kazini, Sara alishukuru na kuondoka na kutaka kutoka lakini alikumbuka alichafua chini kwa haja ndogo baada kumtoka bila kujijua kutokana na hofu ya maruweruwe.
    Alikwenda msalani kuchukua Mop kwa ajili ya kufanya usafi, alipoingia Shehna alimuwahi na kumwambia.

    "Shoga kapumzike nitakusaidia mimi."

    "Acha tu dada."
    "Hapana kapumzike."

    Sara alikubaliana kumpa Mop Shehna na kuondoka kuelekea nyumbani, lakini Shehna alimwambia Mustafa.

    "Mustafa mpeleke Sara, ukirudi utakuta nimemaliza kufanya usafi."

    "Sawa."
    Mustafa alitoka kumpeleka Sara nyumbani na kumpa nafasi Shehna kufanya usafi. Baada ya kuondoka tu Shehna aliwaita vijakazi wake ambao walianza mara moja kazi ya usafi.

    Mustafa alimpeleka Sara mpaka nyumbani na kumuacha kisha alirudi nyumbani na kumkuta Shehna kaisha maliza kazi ya usafi. Baada ya kuachwa Sara aliingia chumbani kwake na kujikuta akianguka kilio kutokana na matukio yaliyokuwa yakimuandama kila kukicha.
    Katikati ya kilio aliisikia tena sauti aliyoisikia wakati alipomuona nguruwe ofisini kwa bosi wake.

    "Kulia siyo dawa zaidi kuacha kuyafuata mambo yasiyo kuhusu la sivyo utageuka nguruwe kabisa."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sauti ile ilimfanya anyamaze na kujiuliza kitu gani ambacho amekuwa akikifuatilia zaidi ya kutaka kumjua Shehna ambaye kwa jinsi alivyomuona na upole wake aliamini si jini bali kiumbe cha kawaida tena mwenye upendo tofauti na alivyomfikiria. Hakuamini mwanamke mrembo kukubali kusafisha haja yake ndogo.
    Lakini alimuhakikishia hali ya kumtisha haitamrudia tena, haikuwa kama alivyomwambia na kusikia sauti ile. Akiwa hajapata jibu simu yake iliita, namba ilikuwa ngeni. Alipokea na kuzungumza.

    "Haloo."

    "Sara umefika salama?" sauti haikuwa ngeni lakini hakuwa na uhakika nayo ilibidi aulize.

    "Nani?"
    "Mi shogayo Shehna."

    "Aah! Dada nimefika salama."

    "Ile hali haijatokea?"

    "Ndi..ndiyo."
    "Mbona kama una wasiwasi?"

    "Ni kweli kuna sauti naisika kwa mara ya pili lakini siielewi."

    "Inasemaje?"






    “Inasema niache kufuatilia mambo yasiyonihusu la sivyo nitageuzwa nguruwe kabisa.”

    “Kwani unafuatilia nini?” Shehna alijifanya kuuliza.

    Swali lile lilikuwa gumu kwa vile asingeweza kumueleza anamfuatilia yeye, alibidi adanganye kwa kusema:

    “Dada wee nimfuatilie nani?”

    “Haiwezekani sauti hiyo kutokea mara ya pili, kama kuna kitu unakifuatilia achana nacho kwa vile kila kitu cha ajabu kikikutokea kina sababu.”

    “Nimekusikia dada yangu.”

    “Hebu acha kufuatilia hicho ulichotaka kukifuatilia tuone nini kitatokea.”

    “Sawa dada.”

    “Basi mdogo wangu oga kisha kunywa maji ya baridi ulale.”

    “Nitafanya hivyo dada.”

    Sara alikwenda kuoga kisha alikunywa maji ya baridi na kujikuta akipitiwa na usingizi mzito.

    ***


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sara aliamka siku ya pili bila kutokewa na mauzauza yoyote, alikwenda hadi kazini kama kawaida na kukuta ofisi haijafanyiwa usafi. Aliingia katika kazi ya kufanya usafi kama kawaida yake na kusubiri muda wa bosi wake kufika. Baada ya muda Mustafa aliwasilili na kupokewa na Sara.

    Kama kawaida alichukua vitu vya bosi na kwenda kuviweka ofisini, Mustafa alipoingia ofisini alishangaa kukuta ofisi chafu. Hata hali ya hewa haikuwa kama ile aliyoizoea wakati wa Shehna akifanya usafi. Alitoka hadi kwa Sara na kumuita.

    “Sara njoo mara moja.”

    Sara alinyanyuka na kwenda kwa bosi wake kumsikiliza alijua anaitiwa kazi ya siku ile. Alipofika alikutana na swali lililomshtua.

    “Sara kazi imekushinda?”

    “Kwa nini bosi?”

    “Mbona ofisi inanuka kama zizi la ng’ombe.”

    “Bosi mbona mi sisikii harufu yoyote mbaya?”

    “Ina maana husikii harufu mbaya ya ofisi?”

    “Bosi kipi kimeongozeka, nimefagia na kufuta kama siku zote sasa hiyo harufu kama zizi imetoka wapi?”

    “Sara kazi imekushinda heri usingerudi ofisi yangu ikaendelea kusafishwa na Shehna, unakuwa kama upo bustanini lakini kurudi kwako hakuna ulichokifanya zaidi ya kuongeza uchafu.”

    “Bosi mbona sikuelewi hiyo harufu kama beberu ipo wapi?”

    Ghafla ndani ya ofisi ilisikia harufu nzuri ya manukato aliyoizoea, alimwambia Sara aondoke.

    “Sara kaendelee na kazi.”

    “Asante bosi.”

    Sara alitoka na kwenda kuendelea na kazi, wakati akifanya kazi alijikuta mtu mwenye mawazo mengi juu ya tukio la muda mfupi uliopita la bosi wake kumgeuka kuwa hajafanya usafi na kusema ofisi inanuka kama zizi. Kilichomshangaza kingine kilikuwa harufu nzuri ya manukato iliyoingia ghafla ofisini ambayo hakujua yametoka wapi.

    Hakutaka kusema kitu aliendelea na kazi na kupanga akitoka kazini jioni lazima aende kwa mganga wake ili amuangalizie kinachomtokea ni nini kwa vile haikuwa hali ya kawaida kwa mtukio yote.

    Wakati akiwaza vile alishtuliwa na sauti ya Shehna.

    “Shoga za kazi?”


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ooh! Dada karibu,” alisema huku akionesha kushtuka.

    Shehna alikuwa amevaa dela zuri lililonakshiwa na nyuzi za hariri, alikuwa amenawiri na kupendeza alionekana mwanamke mrembo zaidi ya siku zote.

    “Asante.”

    “Da Shehna hongera umependeza sana.”

    “Nashukuru.”

    “Karibu dada a’ngu.”






    "Nimekaribia, vipi umeamkaje?"

    "Namshukuru Mungu leo nimeamka salama."

    "Vipi ile hali ilitokea tena?"

    "Kwa kweli mpaka nakuja kazini nashukuru hali ile wala sauti haijanitokea tena."

    "Kama nilivyokueleza, zingatia uliyoambiwa na ile sauti yana sababu, utashangaa mambo yako yatakwenda vizuri."
    "Asante dada kwa msaada wako pia nitazingatia ushauri wako."

    "Vipi bosi yupo?"

    "Yupo pita."

    "Hapana muulize kwanza."

    Sara alinyanyua simu na kumpigia Mustafa aliyemwambia amruhusu aingie.

    "Dada pita."
    "Asante."

    Shehna aliingia ndani ya ofisi alikutanisha macho na Mustafa aliyekuwa akiangalia mlangoni.

    "Wawooo mpenzi."

    Mustafa alijikuta akitoka kwenye kiti chake na kwenda kumpokea kwa kumkumbatia kisha alimchumu.

    "Asante mpenzi," Shehna alishukuru baada ya kubusiwa kwenye shavu.
    Waliachana kwa kila mmoja kukaa sehemu yake, Shehna alionekana mwenye furaha usoni mwake tofauti na siku zote. Alimuangalia Mustafa usoni alitaka kusema neno lakini aliishia kutabasamu na kufanya uzuri wake uongezeke.

    "Vipi mpenzi?" Mustafa alimuuliza huku naye akijenga tabasamu mwanana lililokuwa likimpa uhuru Shehna kuzungumza.
    "Mmh! Mustafa nashukuru sana."

    "Kwa kipi?"

    ;Kwa vyote, lakini kimoja ndicho nimefurahi sana tena sana sipati kusema."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Vipi hivyo na kipi kimekufurahisha sana?"

    "Nikwambie?" Shehna alimuuliza Mustafa huku akimtazama kwa jicho la aibu.
    "Niambie mpenzi," alitoa tabasamu la kumruhusu aseme kilichokuwa moyoni mwake.

    "Kwanza nashukuru kwa kunipa nafasi moyoni mwako, pili kunivumilia kwa usumbufu wangu, tatu kunipa penzi ambalo sijawahi kupata katika maisha yangu yote na kubwa zaidi nimekuja kukueleza sasa hivi mimi ni mjamzito."

    "Wewe!" Mustafa alishtuka.
    "Kweli kabisa, unakumbuka jana ilikuwa siku ya ngapi mimi kulala kwako?"

    "Mmh! Hata sikumbuki."

    "Muone!" Shehna alisema huku akimshika kidevu Mustafa.

    "Jana mpenzi ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya kukutana kimwili, mpaka juzi bado sikuona mabadiliko. Nilichanganyikiwa mtoto wa kike, lakini penzi ulilonipa jana lilikuwa tamu ajabu kidogo nife kwa raha kumbe watoto walikuwa wanaingia."
    "Kweli?"

    "Kweli kabisa nami si muda mrefu nitaitwa mama."

    "Hongera!" Mustafa alisema huku akizunguka meza na kumkumbatia.

    "Hongera wewe kunipatia nilichokitafuta kwa muda mrefu."

    "Basi tuongere wote."
    "Mustafa mpenzi, kuanzia leo hatutaonana mchana kwa vile sipendi kutembea na tumbo."

    "Mbona bado sana?"

    "Siwezi kutembea, familia yetu ikibeba ujauzito husumbuka sana."

    "Sawa mpenzi, lakini nyumbani si utakuja?"

    "Hapana ila nitawatuma watu wakufuate usiku siku mojamoja na alfajiri watakurudisha."

    "Hakuna tatizo."
    "Ila mpenzi kwa mwezi mzima hatutaonana nakwenda nyumbani mara moja kufanya mambo ya kimila baada ya kupata ujauzito."

    "Mmh! Mpenzi nitateseka, nimekuzoea sana."
    "Usiwe na wasiwasi nitakuwa nawe karibu muda wote."

    "Tutakuwa pamoja kivipi wakati hautakuwepo kwa mwezi mzima?"

    "Kila siku nitakuwa katika ndoto zako na ukiamka wala hutakuwa na majonzi, usiku utakuwa kama mchana tena upo na mimi."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Sawa," Mustafa hakutaka kubishana na Shehna kwa kuamini kabisa alikuwa akipewa moyo kwa kujua siku zote furaha ya ndotoni ni maumivu ya asubuhi.

    "Nilitaka kusahau, sasa hivi ruksa kukutana kimwili na mkeo."

    "Hata bila ya dawa?"

    "Yaleyale mafuta mtajipaka sehemu za siri kabla ya kukutana, ila lazima mkutane mara mbili kwa wiki, Jumatatu na Ijumaa."

    "Kwa nini tukutane siku hizo?"

    "Ndizo siku zenye nyota ya mtoto zaidi ya hapo mtakuwa mnatenga maji kwenye kinu."

    "Basi tunaweza kukutana siku zote ila Jumatatu na Ijumaa ndiyo muhimu."

    "Mustafa hiyo unapanga wewe, hii ni dozi ya kutafuta mtoto mkienda kinyume na hapo mtoto mtamsikia kwa kilio, akilia nyumba ya jirani."

    "Nimekuelewa mpenzi."

    "Najua sasa hivi huna matatizo ya fedha, kama utakuwa na shida amka usiku, washa udi utaweza kuniona ndotoni na kunieleza matatizo yako, kama ni fedha kabla ya kuondoka washa udi acha ufunguo mnapouacha ili niweze kukuletea hela."

    "Shehna hivi wewe ni nani hasa?"

    "Kivipi?"

    "Bado nipo njia panda, wewe ni mganga au ji.., hapana sivyo ila naomba uniweke wazi maana mpaka sasa nipo njia panda," Mustafa alimuuliza huku amemkazia macho.

    "Mustafa kipi kimekufanya unitilie shaka hivyo mpenzi wangu?" Shehna alimuuliza Mustafa huku machozi yakimtoka, kitu kilichomfanya Mustafa ajutie swali lake.

    "Basi samahani mpenzi kama swali langu nimekukwaza."

    "Mustafa mpenzi kipi nimekufanyia kibaya mpaka unifikirie hivyo au umenichoka mpenzi wangu?

    Mapenzi yote ninayokupa unayaona bureee?" Shehna aliendelea kulia huku machozi yakimtoka kama maji.

    Mustafa alijikuta akijilaumu kwa swali lake ambalo liliharibu furaha yake ya siku ile.

    Alijutia nafsi yake kwa swali la kipumbavu lakini aliendelea kumbembeleza Shehna amsamehe kwa swali lake lile.

    "Shehna mpenzi nisamehe kwa swali langu la kipuuzi."

    "Mustafa mpenzi nikujali vipi? Siku zote nimekuwa nikikujali mbona sijawahi kukuuliza swali kama hilo? 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Au wema wangu wa kujitolea kwako ndiyo umeniponza?" Shehna alilia mpaka akawa mwekundu.

    Mustafa alichanganyikiwa na kujikuta akitoka kwenye kiti chake na kwenda kupiga magoti mbele ya Shehna na kuanza kulia huku akiomba msamaha kwa kuamini Shehna ni mtu muhimu sana katika maisha yake kutokana na kumsaidia vitu vingi.

    Kilio cha Mustafa kuomba msamaha kilimshtua Shehna ambaye siku zote hakupenda kumuona Mustafa akitoa machozi mbele yake.

    Alimshika na kumnyanyua na kutazamana kila mmoja, macho yake yakiwa yamejaa machozi.

    Machozi ya Shehna yalimfanya aongezeke uzuri maradufu na kuzidi kuutesa moyo wa Mustafa, kumpoteza kiumbe mzuri kama yule.

    "Mustafa," Shehna alimwita kwa sauti ya kinanda.

    "Naam."

    "Nisamehe mpenzi," Shehna alisema huku akimfuta machozi kwa mtandio.

    "Shehna huna kosa, mwenye makosa ni mimi niliyetoa machozi yako."

    "Hapana Mustafa nakupenda sana, nimeumizwa na machozi yako, narudia tena naomba unisamehe."

    "Nimekusamehe japo sioni kosa lako, naomba na mimi unisamehe."

    "Nimekusamehe mpenzi wangu nami nashukuru kwa kunisamehe."

    Walikumbatiana kila mmoja akirudisha furaha yake. Baada ya utulivu wa muda, Shehna alimuomba Mustafa atoke nje mara moja. Alimruhusu hakuchelewa alirudi baada ya dakika mbili akiwa na vinywaji mkononi. Aliviweka juu ya meza na kwenda kwenye friji ndogo na kutoa glasi mbili.




    Alimimina kinywaji kile kwenye glasi na kumpa Mustafa.

    "Karibu mpenzi."

    "Asante," Mustafa alisema huku akikipokea.

    Alikunywa funda mbili na kumumunya midomo kisha alisema:

    "Aaah! Mpenzi kinywaji kitamu sana umepata wapi?"

    "Nilituma mtu nyumbani alete wakati nakuja kukuaga."

    "Ni kitamu hakika sijawahi kukinywa toka nitoke tumboni kwa mama yangu."

    "Utazidi kuvipata maadamu tuko pamoja utakula vitamu zaidi ya hiki. Hii chupa utakuwa ukichukua glasi moja kila siku. Mpaka narudi nitakuta hujamaliza."

    "Shehna wewe ni mtu muhimu sana katika maisha yangu, nitakupenda, nitakutunza na kukuheshimu siku zote za maisha yangu."

    "Mustafa mpenzi mimi si mkaaji, nilikuja kukujulisha habari za ujauzito wangu na kukuaga."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sawa mpenzi nimekuelewa nami nitafuata yote uliyonielekeza bila kufanya makosa."

    "Nitafurahi, kumbuka nakupenda sana Mustafa."

    "Najua."

    "Naomba usinisaliti."

    "Nakuahidi sitafanya hivyo labda nife."

    Walikumbatiana kwa muda kila mtu aliyasikia mapigo ya moyo wa mwenzake kisha waliachiana na kusindikizana nje. Alipofika mapokezi Shehna alimuaga Sara.

    "Shoga nikukimbieni."

    "Jamani, lini utakuja kwangu tuongee?"

    "Tutapanga."

    "Haya shoga sisi tunaendelea na kazi."

    "Ila zingatia yote tuliyozungumza ili uishi kwa amani."

    "Nitafanya hivyo."

    "Haya kwa heri."

    "Haya shoga."

    Mustafa alitoka na Shehna hadi nje, alishangaa kutoona usafiri wowote nje uliomleta, alijiuliza ataondokaje.

    "Shehna unatumia usafiri gani?"

    "Utanisindikiza mpaka njia panda kuna gari la nyumbani litanipitia."

    "Sawa." Waliingia kwenye gari la Mustafa na kumpeleka mpaka sehemu aliyotaka na kumwambia.

    "Niache hapa kuna gari litanipitia sasa hivi."

    "Sawa."

    Mustafa alisimamisha pembeni ya barabara kwenye mti wenye kivuli na kumwambia:

    "Haya mpenzi nenda salama daima nitakukumbuka."

    "Jamani Mustafa si mwezi tu."

    "Kwa umpendaye siku moja mwaka."

    "Najua, hata mimi nilipenda ujauzito huu niulee na wewe, lakini mila lazima nifanye tambiko bila hivyo naweza kupoteza wanangu."

    "Haya mama naheshimu kwa vile ni kwa ajili yetu."

    Waliagana kwa kukumbatia kwa muda kisha Shehna aliteremka kwenye gari na kwenda kusimama chini ya mti, Mustafa aliondoa gari kurudi ofisini. Siku ile Shehna hakutaka kuondoka kwa mtindo wake wa kutoweka ghafla, alihofia baada ya utata uliojitokeza kwa Mustafa ilibidi afanye vile ili wajue ni kiumbe cha kawaida wala si kama wanavyomdhania. Baada ya kumuona Mustafa ametoweka naye alitoweka ghafla na kurudi chini ya bahari.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***

    Sara baada ya kumaliza kazi aliondoka kuelekea kwa mganga wake ili apate ukweli wa kitu kilichomsumbua. Ili kukwepa foleni alichukua bodaboda kuelekea kwa mganga Vingunguti kwa vile walitumia usafiri ule waliweza kukwepa foleni za barabarani na kutumia nusu saa kufika kwa mganga.

    Kwa vile hakutaka dereva wa bodaboda ajue anakwenda wapi, aliteremka mbali kidogo na nyumba ya mganga ambayo ilikuwa vigumu mtu kujua mpaka aelekezwe. Alitembea hatua kama hamsini na kutokea uani kwa mganga, alikuta wateja zaidi ya nane waliokuwa chini ya mti, wanawake sita pamoja na yeye jumla wakawa saba na mwanaume mmoja alikaa kwenye benchi palipokuwa na nafasi.

    Kwenye mkeka kulikuwa na wanawake watatu walikuwa wamejionyoosha na kuchukua nafasi kubwa. Baada ya kuketi na kuwasalimia kwa vile alikuwa mzoefu alitoa simu yake kwenye mkoba na kumtumia ujumbe mganga kumjulisha alikuwa nje.




    Baada ya muda alitoka kijana mmoja mwenye umri isiozidi miaka 30 akiwa amevaa suruali ya jinsi na tisheti, ukimuangalia harakaharaka utajua brazameni.

    Hakusema neno lolote, alimwita Sara kwa ishara ya mkono na kumwelekeza apite ndani.

    Baada ya kuingia alikutana naye nje ya chumba cha uganga.

    "Karibu."

    "Asante, za siku?"

    "Nzuri, umeadimika sana."

    "Mambo mengi ustaadh wangu."

    "Karibu ndani, maana nimefanya upendeleo."

    "Najua ndiyo maana nikatuma ujumbe, niliogopa kupiga," Sara alisema huku akiingia ndani ya chumba cha mganga na kuketi kwenye mkeka.

    "Mmh! Lete habari," mganga alisema.

    "Habari nzuri, ile kazi ilikwenda vizuri yule bwana alirudi na alifanya kama ulivyosema, kwa sasa amekwenda nje kikazi, akirudi anakamilisha kila kitu."

    "Sasa mbona hukurudi tumalize kazi?"

    "Ndugu yangu kuna mambo yalinitokea ambayo sijawahi kutokewa toka nizaliwe."

    "Mambo gani?"'


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sara alianza kumueleza mauzauza yaliyokuwa yakimtokea kuanzia kupotea njia mpaka kuona nguruwe na sauti alizokuwa akisikia, pia wasiwasi wake kwa Shehna.

    Mganga baada ya kumsikiliza alichukua kitabu cha uganga, karatasi na kalamu na kuandika vitu kwenye karatasi nyeupe kisha alifungua kitabu kuangalia alichoandika kilimaanisha nini kutokana na maelezo ya Sara.

    Baada ya kusoma kwa muda alimuangalia Sara na kumuuliza swali;

    "Unasema sauti ilisemaje?"

    "Ilisema nisifuatilie mambo yasiyonihusu la sivyo nitageuzwa nguruwe kabisa."

    "Kwa nini unafuatilia?"

    "Kuna mambo yananitatiza."

    "Ndiyo kuna kitu nimekiona hapa, inavyoonekana hakuna tatizo lolote zaidi ya kufuata maelekezo uliyopewa na ile sauti. Hutakiwi kupewa dawa yoyote zaidi ya kuisikiliza ile sauti. Kinyume cha vile mganga yoyote atakayejifanya anajua, moto utamuwakia."

    "Kwa nini?"

    "Hapana hakuna, tatizo unalo wewe kutaka kuingilia visivyo kuhusu achana nayo uwe salama, zaidi ya hapo utajuta kuzaliwa."

    "Sasa utanisaidia vipi?"

    "Msaada ni kuacha kufuatilia visivyokuhusu."

    "Una maana ile hali haitatokea tena?"

    "Ikutokee vipi nawe umeacha kufuata mambo yasiyokuhusu."

    "Nitamjuaje anayenifanyia mchezo huo?"

    "Sara kuwa muelewa, achana na mambo yasiyokuhusu, umjue ili iweje? Zaidi ya hapo sina msaada wowote wa kukusaidia."

    "Hakuna kinga yoyote?"

    "Kinga ya nini?"

    "Inaweza kunitokea tena."

    "Kama utayapuuza yale maneno na kujifanya unajua utageuzwa nguruwe na hakuna wa kukurudisha."

    "Mmh! Sawa."

    "Una lingine?"

    "Kwa leo sina ila mwisho wa wiki nitakuja kwa ajili ya mambo yangu."

    "Karibu sana."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sara aliagana na mganga wake na kutokea mlango mwingine na kutoa nafasi kwa wateja wengine kupata huduma. Alitembea taratibu hadi kwenye kituo cha bodaboda na kukodi mpaka nyumbani kwake. Baada ya kufika kwake alikuwa mtu mwenye mawazo mengi kutokana na majibu ya mganga.

    Alijiuliza kwa nini mganga alikataa kumsaidia, bado hakukata tamaa. Alipanga kwenda kwa mganga mwingine ili kupata ukweli aliamini kabisa mganga yule wa awali uwezo wake mdogo.

    Kwa vile ilikuwa bado mapema, alichukua simu yake na kumpigia shoga yake anayeishi Kigogo.

    Baada ya simu kuita kwa muda, ilipokelewa upande wa pili.

    "Haloo Sara."

    "Eeh! Mwaju za sahizi?"

    "Nzuri, vipi shoga?"

    "Eti mzee Gogo yupo?"

    "Yupo, kwani vipi?'

    "Nilikuwa nina shida naye."

    "Kwa lini?"

    "Leo hii."

    "Mbona usiku?"

    "Siwezi kulala mpaka nimuone kuna mambo yananitatiza."

    "Mambo gani hayo ambayo lazima uende usiku huu."

    Sara alimweleza sababu ya kutaka kuonana na mzee Gogo, baada ya kumsikiliza, alishusha pumzi na kusema:

    "Mmh! Shoga una haki ya kwenda muda huu kwa mzee Gogo."

    "Sasa tunafanyaje?"

    "Nakusikiliza wewe."




    “Basi kodi Bajaj nipitie nitalipa.”

    “Nipe dakika ishirini nitakuwa hapo jiandae nikifika tunaondoka.”

    “Wala sina shida ya kujiandaa utanikuta nje nakusubiri.”

    Sara hakutaka kuoga alichukua pochi yenye pesa na kutoka kumsubiri shoga yake, baada ya muda Mwajuma alifika na Bajaj ambapo Sara aliingia na kuelekea Tandale kwa mzee Gogo. Kwa vile walipitia njia za nyuma walikwepa foleni na kufanikiwa kufika kwa mzee huyo mapema.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walikuta watu bado hawajaondoka, walikaa kwenye benchi kusuburi muda wa kuingia ndani. Wakiwa wamekaa kwenye benchi alitoka mzee wa makamo kichwa chote kilikuwa kimejaa mvi aliyekuwa amevaa fulana ya mikanda chini alijifunga kaniki. Kwa vile alikuwa amezoeana na Mwaju alipomuona alishtuka na kumuuliza.

    “Vipi tena mama, mbona usiku?”

    “Shida tu mzee wangu.”

    “Karibu hapa ndiyo kwa mzee Gogo asiyeshindwa na kitu.”

    “Asante, vipi tutapata upendeleo?”

    “Nipe dakika kumi nitakuiteni.”

    Mzee Gogo alikwenda kwenye mti uliokuwa pale uani na kuchukua vitu kisha alirudi ndani kuendelea na kazi. Baada ya muda alitumwa mtu kwenda kuwaita, waliingia ndani na kukaa kwenye mkeka.

    “Karibuni.”

    “Asante.”

    Mzee Gogo alitulia kwa muda akipanga vizuri dawa zake kisha alinyanyua macho na kusema:

    “Mmh! Mabinti mna tatizo gani?”

    “Shoga yangu ndiye mwenye tatizo.”

    “Eti mama una tatizo gani?” alimgeukia Sara.

    Sara alimueleza mikasa iliyomkuta na jinsi mganga aliyekwenda jioni ile kukataa kumtibu. Baada ya kumsikiliza alichukua kikopo kilichokuwa na unga mweupe ambapo alichota kidogo na kuumwaga mbele yake na kutulia kama anatazama kitu. Alitulia akikaza macho kwenye unga ule kisha alisema:

    “Ni kweli kabisa ni jini.”

    “Nani?”

    “Huyu mpenzi wa bosi wako.”

    “Mungu wangu una maanisha Shehna?”

    “Ndiyo.”

    “Sasa tutafanyaje?”

    “Wewe unataka tumfanyeje?”

    “Tumpoteze kabisa.”

    “Kumpoteza itakuwa vigumu kwa vile tayari amekuwa mpenzi wa bosi wako.”

    “Na ndiye aliyenitesa vile?”

    “Ndiyo.”


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tumfanyeje ili kuvunja penzi na bosi wangu pia asinifuatefuate?”

    “Kuvunja urafiki ni vigumu kwa vile tayari ana ujauzito wa bosi wako.”

    “Sasa tutafanya nini?”

    “Labda kumuua tu.”

    “Sawa.”

    Baada ya kusema vile alichukua chupa ndogo na bakuli dogo na kumimina maji yake kisha alizungumza maneno ambayo hawakuyaelewa. Ghafla mganga alinyamaza na kuanza kung’ata maneno mara mtetemeko mkubwa ulitokea ndani ya chumba cha uganga lakini nje hakuna aliyejua nini kinaendelea.

    Wakiwa wameingiwa na wasiwasi walishtuka kumuona mganga akijishika mikono shingoni kama anamzuia mtu asimkabe na kuliacha bakuli likianguka chini na kumwaga maji.

    Sara na shoga yake walishtuka kumuona mganga akihangaika kama anapigana na mtu aliyeonekana kumkaba shingoni ambaye hawakumuona. Mara walimuona akianguka kama mzigo huku mikono yake ikiwa bado shingoni na kuanza kurusha miguu na kufanya dawa zilizokuwa pembeni yake kutawanyika ovyo.

    Walinyanyuka walipokuwa wamekaa kwa woga, mganga aliendelea kurusha miguu kama kuku aliyekatwa kichwa kisha alitulia. Baada ya kutulia waliogopa kumsogelea na kutoka nje kumwita msaidizi wake. Aliingia na kwenda alipokuwa amelala mzee Gogo. Walimkuta macho na ulimi vimemtoka nje akiwa amekufa.

    Sara na shoga yake waliona msala utawageukia walitoka taratibu bila kuaga na kurudi nyumbani. Njia nzima Sara alijiuliza maswali na kukumbuka maneno ya mganga wa Vingunguti aliyemweleza kuwa mganga yeyote atakayetaka kuingilia kesi ile lazima moto umuwakie. Alipofika kwake aliteremka na kumuacha shoga yake akirudi nyumbani kwake Kigogo.









    Alipofika alijikuta akizidi kukosa amani moyoni mwake na kujiuliza nini hatima yake baada ya kukaidi amri ya sauti ya kuacha kufuatilia mambo yasiyo muhusu Kilishomshtua zaidi kujua Shehna ni jini na ndiye aliyekuwa akimfanyia mauzauza yale.

    Alijiuliza atamtazamaje hasa baada ya kumuasa aache kufuatilia mambo yasiyo muhusu. Alipofika nyumbani hakuwa hata na hamu ya kula, alinunua soda na keti, alikula kisha alioga na kupanda kitandani.

    Usiku wa manane akiwa amelala alishtushwa na sauti kali ya vicheko mfululizo, alifumbua macho kutazama na kukutana na kiza kizito. Vicheko viliendelea mpaka kikawa kero masikioni mwake, mapigo ya moyo yalimwenda mbio kwa hofu.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipapasa pembeni ya kitanda na kushika swichi ya kitandani na kuwasha taa.

    Ilipowaka alishtuka kuona viumbe wa ajabu mbele yake wakiwa wamesimama sambamba na ukuta. Walikuwa watu weusi sana wanne wenye mikia mifupi kama ya mbuzi na pembe ndogo kichwani. Sara alishtuka na kutetemeka kwa hofu huku haja ndogo ikimtoka bila kujijua.



    Alijiuliza wale ni kina nani na wamefuata nini, wazo lake lilielekea moja kwa moja kwa wachawi. Akiwa bado hajajua nini kinaendelea aliiona ardhi ikipasuka na kuingia mwanamke aliyekuwa amekaa kwenye kiti cha dhahabu cha kifalme kilichokuwa kimebebwa mabegani na wanaume wengine wanne weusi wenye miili mikubwa na mikia kama wenzao lakini hao walikuwa na pembe moja katikati ya kichwa tofauti na wale wengine waliokuwa na pembe mbili.

    Wale viumbe wa ajabu waliendelea kukibeba juu kiti kilichokaliwa na mwanamke mrembo mpaka ardhi iliyopasuka kujifunga ndipo walipomtua chini. Sara aliendelea kutetemeka huku akiwa amejikunyata upenuni mwa kitanda akiwa umesogea ukutani kabisa.

    Yule mwanamke alikuwa amempa mgongo, alipopiga kofi aligeuzwa kumtazama, Sara hakuamini macho yake kumuona aliyekuwa mbele yake ni Shehna rafiki wa bosi wake. Baada ya kutulia alipiga makofi, viumbe vile vya ajabu vilitoweka na kubakia peke yake akiwa bado amekaa kwenye kiti chake cha dhahabu.

    Baada ya kubaki wawili, Shehna aliteremsha pumzi nzito na kunyanyuka kwenye kiti na kusimama. Alimtazama Sara aliyekuwa bado amejikunja pembeni ya ukuta kwa woga. Alitembea taratibu kukizunguka chumba, alipompa mgongo alishtuka kumuona Shehna ana mkia mkubwa kama wa kangaroo lakini ule ulikuwa umenenepa sana.

    Alipofika mwisho wa ukuta aligeuka akiwa amegeuka sura yake na kuwa ya kutisha meno yake yaligeuka kama ya ngiri juu ya paji la uso kulikuwa na pembe mbili kama za faru. Macho yake yalikuwa yakiwaka moyo, alicheka kicheko kizito kilichofanya Sara atokwe damu masikioni.

    Shehna alikuwa kiumbe cha kutisha ambacho Sara hakuwahi kukiona maishani mwake, kwa sauti kali Shehna alisema huku moto ukitoka mdomoni.

    “Sara umenichimba sana, sasa umenijua haya niambie shida yako?”

    “Ni..ni ..samehe She..she...”

    “Sara sitakusameha lazima utajua faida ya kiburi chako, nilikuonya kwa sauti hukusikia nikaja mwenyewe hukunielewa, nina imani ulitaka uone nini kitatokea baada ya wewe kufuatilia mambo yasiyokuhusu. Nimekutisha ninavyojua lakini kichwa chako kimejaa kiburi nami nataka nikuonesha jeuri yangu.

    “Sitakuua bali nitakupa adhabu ya kipindi chote nitakapokuwa sipo chagua adhabu moja, nikugeuze Nguruwe, Chura, Funza maisha yako yote yawe kwenye kinyesi, bundi au mbwa?” 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sara hakujibu, alijitahidi kumsogelea Shehna ili amuombe msamaha.

    “Shehna nisamehe shoga yangu.”

    “Wewe si shoga yangu, mlitaka kuniua na mganga wako bila kosa, nimekukosea nini Sara?” Shehna alirudi katika umbile la kibinaadamu na kuanza kulia machozi ya damu.

    “Ni sa..samehe sirudii tena.”

    “Sitaki kusikia sauti yako, umetaka kunijua leo umenijua mimi ni jini, ujini wangu umekuathiri nini katika maisha yako?”

    “Najua nimekukosea naomba unisamehe sirudii tena.”

    “Sara sitakusamehe ukichelewa kuchagua adhabu yako nitakugeuza kiumbe cha ajabu kisicho na mfano.”



    Itaendelea wiki ijayo, siku ya Jumatano katika gazeti la Risasi Mchanganyiko.



    Sara alijikuta kwenye wakati mgumu wa kuamua ageuzwe kiumbe gani, kabla hajapata jibu Shehna alipiga makofi mara walitokea viumbe wawili vya ajabu vinavyotisha sana tofauti na vyote vilivyotangulia.

    “Naam binti wa mfalme wa bahari ya dhahabu una shida gani?”

    “Enyi watwana wenye roho chafu nataka mumtafutia adhabu yoyote kali huyu mwanadamu mnataka nimepa adhabu gani?”

    “Kwa nini tusimbanike kama mbuzi karibu na jua?” mmoja alipendekeza adhabu.

    “Hapana adhabu hiyo kali sana, nataka ya kumtesa ili atambue siri aliyoitaka kuijua faida yake ni nini.”

    “Sisi hatuwezi kuchagua adhabu ndogo binti wa mfalme, tunaomba wewe uchague adhabu yoyote kwake tunajua amekuudhi sana. Adhabu yetu kwake ni kifo tena cha maumivu makali zaidi ya hapo hatuna adhabu.”

    “Basi mnaweza kunipisha nitoe adhabu yangu.”

    Baada ya kusema vile viumbe wa ajabu alitoweka na kubakia Shehna katika umbile la kawaida la mwanamke nzuri katika vazi pana kutokana na ujauzito wake na Sara ambaye alikuwa akitetemeka mpaka utumbo. Alimuangalia kwa muda Sara aliyekuwa amejikunyata kwa woga upenuni mwa kitanda kwa sauti ya upole alimwita.

    “Sara.”

    “A..a..bee.”


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Unaniweka katika wakati mgumu katika maisha yangu wa kukufanya kitu kibaya. Sikupenda kukufanyia chochote kibaya, narudia nimejitahidi kukuelekeza lakini umekuwa na masikio ya kenge mpaka utoke damu. Kwa vile umekataa kuchagua adhabu mimi nitakuchagulia adhabu, nilifikilia nikugeuze nguruwe lakini hiyo kwangu ni adhabu kubwa, nimejifikilia kukugeuza funza maisha yako yake kwenye kinyesi nayo hiyo nimeona ni adhabu kubwa.

    “Adhabu ndogo kuliko zote nimeonelea nikugeuze uwe mbwa ambaye atakuwa unazurura mitaani na kupigwa nawe na lakini sitaruhusu wakuue. Chakula chako nitakijua mimi utakula mara moja kwa siku. Nina imani utajua thamani ya kiburi chako.”

    “Nitakuwa mbwa mpaka lini?” Sara alijitahidi kuuliza.

    “Mpaka nitakapojifungua.”

    “Shehna shoga yangu hakuna adhabu nyingine zaidi ya hiyo?”

    “Sara mimi huwa sitoi adhabu bali umewaona watoa adhabu na adhabu zao, kama ningewaachia sijui ungekuwa kwenye hali gani?”

    “Nipunguzie shoga yangu.”

    “Sara unanichelewesha muda wangu umekwisha.”

    Baada ya kusema vile alinyoosha kidole ghafla Sara aligeuka mbwa, kisha Shehna alipiga makofi na viumbe wa ajabu walitokea. Aliwaonesha ishara ya macho huku akipanda kwenye kiti chake. Walikibeba juu ghafla ardhi ilipasuka na wao kuzama ndani yake kisha alijifunga na kuwa kama mwanzo.

    Sara alibakia juu ya kitanda huku akiamini yeye ni mtu wala siyo mbwa, lakini bado hakuamini kilichotokea ni kweli zaidi ya kuota ndotoni. Siku ya pili aliamka asubuhi kama kawaida na kutoka nje kwenda kuoga ili awahi kazini lakini watoto wa jirani walipiga kelele kumuona mbwa.

    Kitendo kile kilimfanya Sara arudi ndani lakini alishangaa kusikia.

    “Amekimbilia ndani kwa ma’ mdogo Sara,” alisema mtoto mmoja.

    “Kwani Sara yupo wapi?” alimsikia jirani yake mama Saidi akiuliza.

    “Sara..Sara,” Happy alimwita kwa sauti.

    Sara aliyekuwa chumbani kwake aliitika kwa sauti.

    “Abee nimo ndani,” lakini ilitoka sauti ya mbwa kufoka.

    “Jamani mbwa huyu katokea wapi na Sara kaenda wapi asubuhi yote na kuacha mlango wazi,” jirani mwingine alisikika akisema.

    “Jamani tufanyeni msaada wa kumtoa huyo mbwa ndani,” mtu mwingine alitoa wazo huku majirani wakizidi kukusanyika.

    “Na kweli labda kichaa anaweza kutuuma pia hata watoto wetu.”

    Jirani mmoja alishika fimbo na kuingia chumbani kwa Sara na kushtuka kumuona mbwa juu ya kitanda. Alimtishia kumpiga ili atoke nje lakini Sara alitaka kujitetea kwa kuwaeleza kuwa yeye si mbwa ni mtu kama watu wengine lakini aliishia kumfokea kitu kilichoonesha anataka kumuuma. Ilibidi jirani amtandike fimbo iliyomfanya Sara atoe ukelele wa maumivu na kutoka nje ili kuokoa kipigo kile na kutokomea mitaani.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kila mtaa alipopita watoto walimpiga mawe kitu kilichozidi kumweka kwenye wakati mgumu yeye alijifahamu ni mwanadamu na si mbwa lakini kila kona alipopita aliitwa mbwa. Alitafuta jumba bovu na kuingia humu kujificha japokuwa kulikuwa na kinyesi ambacho kilimnukia harufu mbaya. Lakini aliamini ile ni sehemu salama kwake kuliko kuzurula mitaani na kupugwa mawe na watoto.  




    Sara alijikuta kwenye wakati mgumu wa kuamua ageuzwe kiumbe gani, kabla hajapata jibu Shehna alipiga makofi wakatokea viumbe wawili wa ajabu wanaotisha sana tofauti na waliotangulia.

    "Naam binti wa mfalme wa bahari ya dhahabu una shida gani?"

    "Enyi watwana wenye roho chafu nataka mumtafutie adhabu yoyote kali huyu mwanadamu, mnataka nimpe adhabu gani?"

    "Kwa nini tusimbanike kama mbuzi karibu na jua?" mmoja alipendekeza adhabu.

    "Hapana adhabu hiyo kali sana, nataka ya kumtesa ili atambue siri aliyoitaka kuijua faida yake ni nini."

    "Sisi hatuwezi kuchagua adhabu ndogo binti wa mfalme, tunaomba wewe uchague adhabu yoyote kwake tunajua amekuudhi sana. Adhabu yetu kwake ni kifo tena cha maumivu makali zaidi ya hapo hatuna adhabu nyingine."

    "Basi mnaweza kunipisha nitoe adhabu yangu."

    Baada ya kusema vile wale viumbe wa ajabu walitoweka na kubakia Shehna katika umbile la kawaida la mwanamke mrembo katika vazi pana kutokana na ujauzito wake na Sara ambaye alikuwa akitetemeka mpaka utumbo. Alimuangalia kwa muda Sara aliyekuwa amejikunyata kwa woga ubavuni mwa kitanda, kwa sauti ya upole alimwita.

    "Sara."

    "A...a...bee."

    "Unaniweka kwenye wakati mgumu katika maisha yangu wa kukufanya kitu kibaya. Sikupenda kukufanyia chochote kibaya, narudia nimejitahidi kukuelekeza lakini umekuwa na masikio ya kenge mpaka utoke damu. Kwa vile umekataa kuchagua adhabu mimi nitakuchagulia adhabu. Nilifikiria nikugeuze nguruwe lakini hiyo kwangu ni adhabu kubwa, nimejifikiria kukugeuza funza wa kwenye kinyesi maisha yako nayo nimeona ni adhabu kubwa.

    "Adhabu ndogo kuliko zote nimeonelea nikugeuze uwe mbwa ambaye atakuwa unazurura mitaani na kupigwa mawe lakini sitaruhusu wakuue. Chakula chako nitakijua mimi, utakula mara moja kwa siku. Nina imani utajua thamani ya kiburi chako."

    "Nitakuwa mbwa mpaka lini?" Sara alijitahidi kuuliza.

    "Mpaka nitakapojifungua."

    "Shehna shoga yangu hakuna adhabu nyingine zaidi ya hiyo?"

    "Sara mimi huwa sitoi adhabu bali umewaona watoa adhabu na adhabu zao, kama ningewaachia sijui ungekuwa kwenye hali gani?"

    "Nipunguzie shoga yangu.".


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sara unanichelewesha muda wangu umekwisha."

    Baada ya kusema vile alinyoosha kidole ghafla Sara aligeuka mbwa, kisha Shehna alipiga makofi na viumbe wa ajabu walitokea. Aliwaonesha ishara ya macho huku akipanda kwenye kiti chake. Walikibeba juu ghafla ardhi ilipasuka na wao kuzama ndani yake kisha alijifunga na kuwa kama mwanzo.

    Sara alibakia juu ya kitanda huku akiamini yeye ni mtu wala siyo mbwa, lakini bado hakuamini kilichotokea ni kweli zaidi ya kuota ndotoni. Siku ya pili aliamka asubuhi kama kawaida na kutoka nje kwenda kuoga ili awahi kazini lakini watoto wa jirani walipiga kelele kumuona mbwa.

    Kitendo kile kilimfanya Sara arudi ndani lakini alishangaa kusikia.

    "Amekimbilia ndani kwa ma' mdogo Sara," alisema mtoto mmoja.

    "Kwani Sara yupo wapi?" alimsikia jirani yake mama Saidi akiuliza.

    "Sara...Sara," Happy alimwita kwa sauti.

    Sara aliyekuwa chumbani kwake aliitika kwa sauti.

    "Abee nimo ndani," lakini ilitoka sauti ya mbwa kufoka.

    "Jamani mbwa huyu katokea wapi na Sara kaenda wapi asubuhi yote na kuacha mlango wazi," jirani mwingine alisikika akisema.

    "Jamani tufanyeni msaada wa kumtoa huyo mbwa ndani," mtu mwingine alitoa wazo huku majirani wakizidi kukusanyika.

    "Kweli labda kichaa anaweza kutuuma pia hata watoto wetu."

    Jirani mmoja alishika fimbo na kuingia chumbani kwa Sara na kushtuka kumuona mbwa juu ya kitanda .















    Alimtishia kumpiga ili atoke nje lakini Sara alitaka kujitetea kwa kuwaeleza kuwa yeye si mbwa ni mtu kama watu wengine lakini aliishia kumfokea kitu kilichoonesha anataka kumuuma.

    Ilibidi jirani amtandike fimbo iliyomfanya Sara apige kelele kwa maumivu na kutoka nje ili kujiokoa na kipigo kile na kutokomea mitaani.

    Kila mtaa alipopita watoto walimpiga mawe kitu kilichozidi kumweka kwenye wakati mgumu, yeye alijifahamu ni mwanadamu na si mbwa lakini kila kona alipopita aliitwa mbwa.

    Alitafuta jumba bovu na kuingia humo kujificha japokuwa kulikuwa na kinyesi ambacho kilikuwa na harufu mbaya, lakini aliamini ile ni sehemu salama kwake kuliko kuzurura mitaani na kupigwa mawe na watoto.

    ***


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Shehna baada kumtia adabu Sara japokuwa moyo wake haukupenda kutoa adhabu yoyote, alirudi nyumbani kwao na kuingia chumbani kwake na kuanza kulia sana, kitu kilichomshtua mama yake Bi Zaldau, mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu aliyempenda sana mwanaye Shehna kama mboni ya jicho lake, hakupenda hata siku moja kumuona akiumizwa na kitu.

    Akiwa amejipumzisha chumbani kwake, alishtuka kuona machozi yamemdondokea kifuani, ile ilimjulisha mwanaye ana tatizo na muda ule alikuwa akilia.

    Alijiuliza kipenzi chake Shehna kipi kimempata mpaka kulia machozi mengi yaliyomfikia yeye, alikwenda moja kwa moja chumbani kwa mwanaye na kumkuta akiendelea kulia.

    “Shehna,” alimwita na kumfanya mwanaye ashtuke na kujifuta machozi haraka kisha alimgeukia mama yake.

    “Shehna mwanangu una tatizo gani mama?”

    “Hapana mama sina tatizo bali nimemkumbuka mpenzi wangu Mustafa.”

    “Shehna nilikueleza mapema kuwa kama unamtaka mwanadamu, mtafute asiye na mke ungeweza kuja naye huku.”

    “Mama, Mustafa nilimpenda muda mrefu sana lakini ninyi ndiye mliyenichelewesha kuonana naye mpaka akaoa mwanamke mwingine.”

    “Ulikuwa bado hujatimiza umri wa kukutana na mwanaume.”

    “Hata kama bado, nilitakiwa nionane naye mapema ili asioe mwanamke mwingine anisubiri mimi.”

    “Hilo kweli tulifanya kosa, lakini mbona linawezekana kurekebishika.”

    “Utalirekebisha vipi wakati ana mke tayari?”

    “Si tunampoteza mkewe.”

    “Hapana mama siwezi kufanya hivyo, kosa la mkewe lipi mpaka apotezwe?” Shehna alimkatalia mama yake kumuua mke wa Mustafa.

    “Basi tumfanye asiwe na hamu na mumewe.”

    “Vilevile sioni kosa lake.”

    “Halafu mbona inaonesha kinachokuliza sicho unachonieleza, ulitoka na Kubash, mlikwenda wapi halafu juzi nilimuona Shush akiwa na damu mikononi, kuna nini ambacho sikijui?” mama Shehna mke wa mfalme wa bahari ya dhahabu Malkia Bi Zaldau alihoji.

    “Mama ndicho kinachoniliza, kuna msaidizi wa Mustafa ananifuatilia sana, nimejaribu kumtisha lakini hasikii. Jana usiku alikwenda kwa waganga wawili, mmoja alikataa kumtaka kumfanyia kazi yake lakini wa pili alikubali na kutaka kuniua. Wakati nimejilaza, nilianza kupoteza nguvu na kumwita Shush haraka awahi kumzima yule mganga kwani angechelewa ningekufa mimi.”

    “Sasa umempa adhabu gani?”

    “Nimemgeuza mbwa.”


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Shehna mtu anataka kukuua, unamgeuza mbwa adhabu gani hiyo isiyolingana na dhamira yake mbaya?” mama yake alikasirika.

    “Mama hata kumgeuza mbwa kwangu nimeona ni adhabu kubwa sana, nilitaka kumuacha lakini imebidi nifanye hivyo.”

    “Mwanangu huruma gani hiyo ya kujiumiza?”

    “Mama, kosa lake kwenda kwa mganga bila hivyo wala asingenisumbua, nimemuua mganga kwa vile alitaka kuniua, zaidi ya hapo nisingesumbuka naye.”

    “Mmh! Sasa kinakuliza nini?”

    “Sipendi kuingia katika dhambi ya kulazimishwa.”

    “Basi kama umempa hiyo adhabu inatosha, usilie mwanangu.”

    “Sawa mama nimekuelewa.”

    Shehna alijilaza kifuani kwa mama yake kuonesha amekubaliana naye.”

    ***

    Mustafa alishtuka, siku ya pili alishtuka kufika kazini na kukuta ofisi bado imefungwa, alifungua na kuingia ndani. Ofisi ilikuwa chafu, hata hali ya hewa ilikuwa mbaya. Alijiuliza Sara atakuwa wapi mpaka muda ule, kitendo cha kuchelewa kazini kilizidi kumfanya amchukie Sara na kupanga akifika lazima amfukuze kazi.

    Alishindwa kukaa ndani kutokana na hali aliyokuwemo na kutoka nje, alikwenda hadi kwa mlinzi ili akamwambie afanye usafi. Kabla hajafika kwa mlinzi, simu yake iliita. Alipoangalia ilikuwa inatoka kwa mpenzi wake Shehna.

    Aliipokea na kuzungumza.

    “Haloo mpenzi.”

    “Haloo laaziz, vipi mpenzi wangu?”

    “Safi tu.”





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog