Search This Blog

PENZI LANGU - 3

 





    Simulizi : Penzi Langu

    Sehemu Ya Tatu (3)



    baba yake Happy alipompeleka hospitali bintiye yake huyo aliyekuwa akisumbuliwa na moyo pamoja na kichwa chanzo kikiwa ni mapenzi ambacho mzazi wake hakujua . Hata hivyo , licha ya kumpeleka katika hospitali kadhaa hakupata nafuu . Je , kiliendelea nini? Tuwe pamoja ... Kutokana na kuumwa, baba aliamua kunihamishia shule ya karibu ili niwe karibu nao. Hata maendeleo yangu hayakuwa mazuri darasani kisa kikiwa mapenzi. Baada ya kumaliza miezi sita , mama alipoona sijakaa sawa kichwani alinipeleka kwa mtaalamu wa masuala ya saikoloji ambaye alizungumza nami kwa kirefu, nikamuelewa na tangu hapo nikapa nafuu. Kufuatia kuumizwa na mtu niliyempenda sana , niliamua kuacha kabisa kujihusisha na masuala ya mapenzi , kwa kiasi nilifanikiwa kwani niliweza kukaa bila kuwa na rafiki wa kiume kwa muda mrefu .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikiwa kidato cha sita nilikuwa bize na masomo na kuchati na marafiki mbalimbali kupitia faceboock. Marafiki zangu hao walikuwa kutoka nje ya nchi na hapa nchini . Miongoni mwa vijana niliokuwanachati nao alikuwepo mmoja aliyekuwa akisoma chuo kimoja kikuu kilichopo jijini Dar ambaye sitapenda kumtaja kwa jina . Kaka huyo, awali tulikuwa tukichati kama marafiki wa kawaida lakini kadiri siku zilivyosonga tukajikuta tumeanzisha uhusiano wa kimapenzi wa kwenye simu. Kilichonivutia zaidi alikuwa mtanashati na mara nyingi nilipenda kumwangalia kupitia picha alizokuwa akiziweka faceboock, pia namna alivyokuwa akinijali . Nasema kunijali ni kwamba ilikuwa siyo rahisi ipite saa moja asubuhi bila kunipigia simu na kujua hali yangu , kunitakia masomo mema , mchana pia tulipigiana simu kujuliana hali . Kukufafanulia hapo ni kwamba, kutokana na matatizo yangu ya moyo , kuumwa kichwa na mengine baba alininunulia simu na kuniombea ruhusa kwa walimu niwe na simu pale shuleni , wakamkubalia. Hata hivyo , baba alifanya hivyo bila kujua kama tayari nilikuwa namiliki simu kwa siri, aliponinunulia mpya yangu nilimpatia rafiki yangu Stella. Nikiwa nachati na mpenzi wangu huyo wa faceboock, alikuwa akiniomba kama tukifunga shule likizo ya muhula wa kwanza nikiwa kidato cha sita niende Dar nikaonane naye. Nilimfahamisha kwamba, licha ya kuwa na ndugu Dar wazazi wangu wasingeniruhusu kwenda huko ukizingatia nilitakiwa kujiandaa na mitihani ya kuhitimu kidato cha sita ambayo ilitakiwa niifanye vizuri. Kutokana na sababu niliyompatia alikubaliana nami na kuniambia atanisubiri hadi nitakapohitimu na kwamba hata yeye kama angepata nafasi angeweza kuja Musoma. Nilipomuuliza kama Musoma alikuwa na ndugu ambaye angefikia kwake, aliniambia kwamba hakuwa na ndugu angefikia hotelini na baada ya kukutana na mimi angerudi Dar . Kuhofia uhusiano wetu kugundulika na wazazi au watu waliokuwa wakinifahamu , nilimwambia anisubiri nikimaliza masomo ya kidato cha sita ningeenda Dar ambako ningekaa kwa muda mrefu wakati nikisubiri majibu. Mpenzi wangu huyo wa faceboock hakuwa na neno alikubaliana nami na kuniahidi kwamba siku tutakayokutana angefurahi, kila tulipokuwa tukichati alikuwa akinisifia kwamba mimi nilikuwa mzuri na aliamini nigekuwa mke wa maisha yake. Niliendelea na masomo hadi nilipohitimu masomo yangu , kwa kuwa sikubanwa na jambo lolote nilipomuomba ruhusa baba ya kwenda Dar kwa shangazi yangu alikataa . Kwa kuwa mzazi wangu alinizuia, sikuwa na jinsi na nilipomweleza mpenzi wangu alisikitika ambapo aliniambia tusubiri muda mwafaka ukifika tungekutana. Niliendelea kusubiri matokeo, bahati nzuri yalipotoka nilikuwa nimefaulu vizuri na kutakiwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu kwenye chuo chochote nilichohitaji . Baba , mama, ndugu na majirani wenye upendo walifurahishwa sana na matokeo yangu . Hata nilipomfahamisha mpenzi wangu naye alifurahi sana ! Kwa ajili ya maandalizi ya kujiunga na chuo kikuu , baba alimpigia simu mdogo wake anayeishi jijini Dar es Salaam na kumfahamisha kwamba ningeenda kwake kwa ajili ya kufanya mchakato wa kujiunga na chuo kikuu . Nilipomweleza mpenzi wangu kuhusu safari ya kwenda Dar , alifurahi sana ambapo aliniambia alikuwa akinisubiri kwa shauku , nikamwambia nami nitafurahi kumuona . Baada ya maandalizi ya safari kukamilika , niliondoka Musoma na njiani mtu niliyechati naye kwa muda mrefu alikuwa mpenzi wangu . Mpenzi wangu aliniambia licha ya kuja kupokelewa na baba mdogo aliyekuwa na usafiri wake , lazima angefika japo anione kwa mbali. Baada ya kuwasili stendi ya Ubungo , tuliwasiliana na mpenzi wangu ambaye alijongea hadi kwenye basi nililopanda , baba mdogo na dada yangu walikuwepo pale .



    Niliposhuka na kutupa macho mita kama nne hivi , nilimuona mpenzi wangu akiniangalia huku akitabasamu lakini kwa vile baba mdogo na ndugu zangu walikuwa wamenipokea nilijikausha . Baada ya kupandisha begi langu ndani ya gari, baba aliondoa gari nikawa namuangalia mpenzi wangu akiliangalia gari hadi lilipoishia, moyo uliniuma sana ! Gari likiwa limesimama kwenye taa za Ubungo, meseji iliingia kwenye simu yangu , nilipoifungua na kuisoma ilisomeka : “ Nimefurahi kukuona mpenzi wangu , nilitamani nikufuate , nikukumbatie na kukubusu lakini imeshindikana, pole kwa safari . ” Ujumbe huo uliniumiza lakini sikuwa na jinsi, nilimjibu Kwa kuwa ulipita muda mrefu bila kuonana na watoto wa baba mdogo , usiku nikiwa na binti yake mmoja tuliyekaribiana umri tukiwa chumbani tulipiga stori mbalimbali zikiwemo za marafiki zetu wa kiume . Nilimsimulia kisa cha kumfumania mpenzi wangu na rafiki yangu kipenzi na nilivyoumizwa na jambo hilo, Joyce alisikitika sana na kunieleza hata yeye aliachana na mpenzi wake wa mwanzo kisa kikiwa kutokuwa mwaminifu . Katika mazungumzo yetu , nilimweleza kila kitu kuhusu mpenzi wangu wa chuo niliyefahamiana naye kupitia facebook kisha nilimuonesha baadhi ya meseji tulizokuwa tukitumiana. “ Ni

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kweli alikuwepo pale stendi ya Ubungo kukupokea?” Happy anasema Joyce alimuuliza baada ya kusoma ile meseji iliyotumwa na mpenzi wa Happy . Nilimwambia alikuwepo isipokuwa mazingira hayakuruhusu

    tukaishia kuangaliana tu , akaniambia kijana huyo alionekana kunipenda . Kufuatia kauli hiyo , nilimwambia kwa jinsi tulivyokuwa tukiwasiliana naye , alionekana kunijali sana ndipo tulipanga kesho yake twende tukamtembelee chuoni. Kutokana na uchovu, nilipitiwa na usingizi hadi niliposhtushwa na adhana iliyopigwa kutokea msikiti ambao ulikuwa karibu na nyumba ya baba mdogo . Nilipoichukuwa simu yangu na kuiangalia nilikuta miss call sita kutoka kwa mpenzi wangu pamoja na meseji tatu, ya kwanza alikuwa akinipa pole ya safari pamoja na joto la Dar. Meseji ya pili aliniambia jinsi mwili ulivyomsisimka aliponiona na kuniambia kama ingewezekana muda ule tungekuwa wote akiniondoa uchovu kwa mabusu matamu . Ujumbe wa tatu, aliniambia iwe na isiwe kesho yake tuonane naye na kwamba alikuwa tayari kunifuata Kimara karibu na kwa baba yangu mdogo , kisha alinibusu kupitia simuni na kuniambia alikuwa akinipenda . Wakati nasoma meseji hizo , Joyce naye alikuwa ameamka nikamuonesha , alipozisoma aliniambia kweli yule mpenzi wangu alikuwa akinipenda. Nilipomuuliza kama ingewezekana kuonana naye siku hiyo , alisema uwezekano ulikuwa wa asilimia mia moja kwani tungejifanya tunakwenda mjini kununua vitu kisha kwenda kuonana na mpenzi wangu huyo wa kwenye facebook. Ingawa muda huo nilikuwa najua mpenzi wangu alikuwa amelala, nilimshukuru kwa meseji alizonitumia na kumwambia asiwe na wasiwasi tungeonana . Licha ya ujumbe huo kuonekana ulimfikia , hakunijibu kwa wakati jambo lililonifanya niamini bado alikuwa amelala, tukaendelea kupiga stori na Joyce . Stori zilinoga hadi tukapitiwa tena na usingizi, niliposhtuka ilikuwa saa mbili kasoro ambapo Joyce alikuwa ameamka kitambo na wakati huo alikuwa akindaa chai . Kama unavyoelewa kwamba mgeni siku ya kwanza hudekezwa, niliandaliwa maji ya kuoga , tukanywa chai , wakati huo baba mdogo na mama walikuwa wamekwenda kazini. “ Happy ikifika saa nne tunaenda ile safari yetu , tayari nimemfahamisha mama kwamba tutaenda mjini kakubali, ” Happy anasema aliambiwa na Joyce. Baada ya kujiandaa saa nne nilimpigia simu mpenzi wangu kwamba nilihitaji kuonana naye , akaniambia alikuwa na kipindi asubuhi mpaka saa sita angenifuata nitakapokuwa . Nilipomwambia Joyce alisema hakukuwa na shida , akashauri wakati tukisubiri saa sita ifike twende kwa rafiki yake aliyekuwa akiishi Mwenge, nikasema sawa . Tulikwenda Mwenge kwa rafiki yake, tulikaa huko hadi saa sita ndipo mpenzi wangu alinipigia simu na kuniuliza nilikuwa wapi nikamwambia Mwenge, hakuamini . “ Upo Mwenge kweli d? Mbona kama naota!” Happy anasema mpenzi wake alimwuliza . Nilipomhakikishia kwamba nilikuwa Mwenge tena na ndugu yangu ambaye ni mtoto wa baba mdogo , akasema nimpe dakika ishirini angewasili.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa kuwa bado tulikuwa nyumbani kwa rafiki yake Joyce aliomba atukute kwenye pub moja iliyopo maeneo ya Lufungila , nikamwambia sawa. Kama alivyokuwa ameahidi , nusu saa baadaye nilimuona kijana mtanashati aliyekuwa amevaa shati la cream, suruali nyeusi na miwani akija sehemu tuliyokuwepo , wote tukawa tunamwangalia. Alipokaribia, alinitambua ndipo niliinuka tukakumbatiana kwa furaha na bila kujali watu waliokuwa wakituona tulipigana mabusu kadhaa . Kumbe wakati tunafanya hivyo , Joyce ambaye ni mtundu alikuwa akitupiga picha kupitia simu yake lakini hakutuambia. Kwa kweli siku hiyo ilikuwa nzuri sana kwangu, nilifurahi kukutana na mpenzi wangu huyo ambaye kwenye faceboock alikuwa akitumia jina la Kikristo , wakati alikuwa Muislamu . Siku hiyo mpenzi wangu huyo alitumia zaidi ya shilingi 30 ,000 kwa vinywaji na chakula, tulizungumza mengi ndipo aliniomba kama sitajali kesho yake tuoanane tena pale ili aniambie kitu maalum . Kwa kuwa nilikuwa mtu mzima, nilijua alimaanisha nini. Kwa vile nami nilipitisha muda mrefu bila kuchangamsha damu nilimwambia asiwe na wasi tungekutana. Baada ya maongezi yetu alitupatia nauli tukaagana kwa kukumbatiana , hakika nilisisimka sana na kutamani kama ingewezekana niwe naye siku nzima . Tuliondoka na ndugu yangu kurudi nyumbani , tukiwa kwenye basi stori zilizotawala zilikuwa kuhusu mpenzi wangu , Joyce alimfagilia kwa kuwa handsome boy, mcheshi na mkarimu . ìMwenzangu umebahatika , kama hatabadilika naona aje awe shemeji yangu wa kudumu yaani mkimaliza masomo muoane kabisa! î Happy anasema Joyce alimwambia. Nilimwambia asijali kikubwa asibadilike tabia kwani sikuona kipingamizi kwa sababu alikuwa Mkristo kama mimi hivyo wazazi wasingepinga kama ningewaambia nimepata mchumba . Tulipofika nyumbani, nikiwa chumbani muda mwingi niliutimia kuangalia picha ya mpenzi wangu huyo kwenye ukurasa wake wa faceboock, kwa jinsi nilivyokolea kwake nikawa nazibusu . Usiku wa siku hiyo niliomba uende haraka ili nikakutane na mpenzi wangu, tayari Joyce aliyekuwa anajua mpango wangu alimuaga mama mdogo na kumwambia alitaka kunisindikiza chuo kikuu kujua taratibu za kuchukuwa fomu za kujiunga na chuo hicho. Mama mdogo hakuwa na neno alituruhusu bila kujua tulikuwa na mpango wetu , kulipokucha tulifanya usafi wa nyumba ikiwa ni pamoja na kuosha vyombo na kufua . Tulipomaliza kunywa chai, watoto wa kike tulijipala haswa tukabeba vipochi vyetu tukaondoka kuelekea Mwenge kukutana na mpenzi wangu ambaye alinipigia simu na kunieleza tayari alikuwa ananitusubiri. Kama ilivyokuwa jana yake, siku hiyo pia moyo wangu ulitawaliwa na furaha. Tulipofika Mwenge tulimkuta mpenzi wangu akitusubiri , kama kawaida tulikumbatiana na kupigana mabusu hadharani bila kuona soni . Baada ya salamu , tulikwenda kukaa sehemu ya vinywaji baridi, mimi nikaagiza juisi , Joyce soda na mpenzi wangu akaaiga maji . Tukiwa tunaendelea na stori alinitumia ujumbe kwamba alitaka tutafute sehemu japo tukapumzike kwa muda, akahoji tungemuagaje Joyce? Nilimtumia ujumbe kwamba Joyce alikuwa anajua kila kitu na kwamba alipanga kwenda kunisubiri kwa rafiki yake ili tukimaliza mambo yetu nimpigie. Nilipomfahamisha hivyo alisema sawa tusubiri tukimaliza vinywaji tuondoke , sijui ilikuwaje kwani aliponiambia hivyo mwili ulinisisimka na kuona tulichelewa kwenda hiyo sehemu ya kujidai. Kwa kihoro cha

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     kwenda kubilingishana na mpenzi wangu, nilimwandikia ujumbe Joyce kwamba akimaliza soda atuage kwamba kuna sehemu anakwenda angetupigia akitoka huko. Joyce alivyo mtoto wa mjini alimalizia soda yake chapuchapu , kisha alituaga ndipo mpenzi wangu alifungua pochi yake akamuongezea shilingi elfu kumi . Joyce alishukuru, akaondoka na kuniacha na ëbaby wanguí, haikupita hata dakika moja ujumbe kutoka kwa Joyce uliingia kwenye simu yangu , ulisema ; ìHaya mwenzangu kafurahi na handsome boy wakoí nimemkubali, analipa, anajua kujali na kamdekee utakavyo . Niliposoma ujumbe huo nilicheka ndipo mpenzi wangu aliniuliza kilinichekesha nini, nikamuonesha ile meseji , alipoisoma akacheka na kusema : Joyce ni mtundu sana , kwahiyo anajua kama tunakwenda chimbo ? Kufuatia kuniuliza hivyo , nilimwambia alikuwa akielewa kila kitu ndiyo maana aliamua kunitania , tukacheka.



    Tulipomaliza soda yetu tuliondoka huku akiniongoza mpaka nyuma ya Kanisa la Kakobe tukatokea kwenye nyumba moja ya kulala wageni , tukaingia na kwenda moja kwa moja mapokezi . Tukiwa hapo alilipia chumba cha shilingi 15, 000, mhudumu akatuongoza hadi sehemu yetu ya kujidai, kwa kuwa kila mtu alikuwa na hamu na mwenzake tulikumbatiana na kufanyiana michezo ya hapa na pale. Mpenzi wangu hakubandua mikono yake kifuani kwangu kwani alinisifia kwamba kilikuwa na viembe bolibo vizuri, akawa anavichezea na kuvibugia na kuvifumbata ni midomo yake. Hakika siku hiyo ilikuwa ya kipekee mno , tulifanyiana michezo hiyo na baadaye tulijikuta tupo kama tulivyokuja katika dunia hii iliyojaa karaha na raha za muda mfupi , tukajibwaga uwanjani tayari kwa kuiendea hatua ya mashamshamu. Nashindwa namna ya kuelezea jinsi nilivyoinjoi penzi lake, sijui ni kwa sababu nilikaa muda mrefu bila kufanya kitendo hicho au kwa vile nilitokea kumpenda sana mpenzi wangu huyo baada ya kusalitiwa. Kwa kifupi ni kwamba, niliinjoi nikajua nimempata mtu ambaye angenisahaulisha machungu niliyopitia huko nyuma baada ya kusalitiwa na mpenzi wangu wa kwanza aliyeniingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi . Niliwaza hivyo bila kujua kama penzi letu tamu lisingedumu kwa kukatishwa na jini , tukiwa tumejipumzisha mpenzi wangu aliniambia hakuamini kama tulikuwa pamoja. Nami nilimwambia nilikuwa kama naota ndoto za mchana , tukacheka na kukumbatiana tena , hakuna aliyetaka kumuacha mwenzake kwani ilikuwa ni burudani tupu ! Baada ya kila mmoja kukata kiu yake, tulioga kisha tulitoka nje ambapo nilimpigia simu Joyce akaniambia bado alikuwa kwa rafiki yake nikamwambia atatukuta kituo cha Mlimani City tunamsubiri. Joyce aliyenitania kwamba muda huo nilikuwa mwepesi hata kama ningeambiwa nikimbie hadi Kimara ningeweza , nikaishia kucheka. “ Kasema yupo wapi na mbona unacheka kwani kakuambiaje ?” Happy anasema mpenzi wake alimuuliza. Nilipomwambia kilichonifanya nicheke naye aliangua kicheko na kuniambia ndugu yangu Joyce alikuwa na vituko sana na kwamba ukikaa naye huwezi kuchoka. Tulipofika kituo cha daladala cha Mlimani City , alishauri tutafute sehemu tuketi huku tukimsubiri Joyce, nyuma yetu mita chache kulia kama unaenda Mwenge pana pub moja tukaenda kukaa hapo. Kutokana na kibarua tulichokuwanacho muda mfupi, nilihisi njaa ndipo mpenzi wangu aliniambia niagize chochote nilichohitaji , nikaagiza chipsi , mayai na mishkaki miwili. Kabla mhudumu hajaondoka , alimwita na kumwambia aongeze mishkaki miwili na ndizi moja. Aliagiza maji mimi nikaagiza soda tukawa tunakunywa huku kila mmoja akiwa na furaha. Katika maongezi yetu , mpenzi wangu aliniambia kwamba licha ya kuishi chuoni alikuwa amepanga chumba chake Tabata ambacho kilikuwa na kila kitu. Aliongeza kuwa mara nyingi siku za wikiendi hupenda kulala huko na kwamba aliamua kupanga ikiwa ni kujiandaa na maisha baada ya kuhitumu chuo kikuu . Taarifa hiyo ilinifurahisha sana , nilimpongeza kwa hatua hiyo ambapo alinishukuru. Kufuatia kuniambia hivyo , licha kutokiona chumba chake nilimuona ni kijana aliyependa maendeleo . “ Sasa utanipeleka lini nikapajue kwako ?” Nilimuuliza. Kufuatia swali langu alicheka na kuniambia siku yoyote nitakayokuwa na nanafasi nimwambie ili twende nikapaone , nikamwambia nitazungumza na Joyce aliyekuwa mratibu wa safari zetu , akacheka na kuniuliza; “ Inamaana bila kuwa na Joyce huwezi kutoka ?” Nilimfahamisha kwamba nitakapoanza chuo nitakuwa huru zaidi ila kwa kipindi kile kutoka nyumbani peke yangu ingekuwa vigumu kwa sababu sikuwa mwenyeji sana wa Jiji la Dar. Wakati tukiendelea kuzungumza tuliiona Bajaj ikipita kwenye barabara ya watembea kwa miguu na kwenda kuegeshwa kituo cha Mlimani City , mara simu yangu ikaanza kuita . Nilipoangalia mpigani, alikuwa Joyce nilipopokea aliniuliza tulikuwa wapi mbona hakutuona pale kituo cha Mlimani City , moja kwa moja nikajua alikuwa kwenye ile Bajaj . Nilipomuuliza kama alikuwa kwenye ile Bajaj akasema tena hata kushuka alikuwa bado nikamwelekeza tulipokuwa, akaletwa na alipotaka kumlipa dereva fedha yake, mpenzi wangu akamzuia na kulipa yeye. Tukiwa pamoja, mpenzi wangu alimwambia Joyce aagize alichohitaji kula lakini Joy alimwambia alikuwa ‘ jiwe ’ yaani alishiba mno kwani muda mfupi uliopita alikula kwa rafiki yake. Kufuatia kusema alikuwa jiwe , wote tulicheka ndipo mpenzi wangu alimwambia aagize japo maji , akamwita mhudumu na kuagiza soda ndogo ambazo wakati ule ndiyo zilikuwa zimeingia sokoni .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Baada ya kunywa na kufurahi, tuliagana na mpenzi wangu lakini kabla hajaondoka aliniambia angefurahi sana kama ningeenda Tabata kupajua alipokuwa amepanga yaani nyumbani kwangu . Kauli ya kwamba nikapujue nyumbani kwangu, ilinifurahisha sana kwani alionesha ni kwa jinsi gani alikuwa akinipenda , nikamwambia tungepanga na Joyce siku ya kwenda . Tulipoachana alielekea chuoni nasi tulipanda basi na kurudi nyumbani, kama ilivyokuwa wakati wa kwenda Mwenge, tukiwa tunarudi stori zilizotawala zilihusu uhusiano wangu na laazizi huyo niliyefahamiana naye kupitia facebook. Jioni ilipofika mama alituuliza kama tulipata fomu za kujiunga na chuo kikuu , kwa kuwa hatukwenda, Joyce alimdanganya kwamba tulienda lakini tuliambiwa twende baada ya siku tatu. Mama mdogo hakutuuliza sababu zaidi ya kusema sawa , akaendelea na shughuli za nyumbani nasi tukaendelea na yetu . Kufuatia penzi tamu alilonipa mpenzi wangu , ilikuwa siyo rahisi kupita saa mbili bila ya kuchati naye ambapo tulizungumza mengi kwa njia hiyo ya ujumbe . Baada ya kupita siku mbili bila kwenda kokote ndipo nilimwambia Joyce afanye mpango ili twende Tabata kwa mpenzi wangu , akaniambia safari hiyo tuifanye kesho yake ambapo tungeenda chuo kikuu kuchukua fomu . Kufuatia kuniambia hivyo , nilimfagilia sana kwa kuwa shap akasema kitendo cha kutoka nyumbani mara kwa mara kingemshtua mama mdogo . Kwa kuwa nilikuwa nina uhakika wa kutoka siku iliyofuata ambayo ilikuwa Ijumaa , nilimfahamisha mpenzi wangu ambaye aliniambia ilikuwa vizuri sana kwa sababu siku hiyo alikuwa na kipindi kimoja cha asubuhi hivyo tungeongozana. Kesho yake mishale ya saa nne tulikuwa tumeshajipodoa tukapanda gari la Mwenge, tukiwa njiani nilimfahamisha mpenzi wangu ambaye aliniambia yupo Makumbusho ila tungekutana Mwenge tukishatoka chuo kikuu . Bahati mbaya tulipofika chuoni , mhusika alituambia tulikuwa tumechelewa kwani idadi ya wanachuo waliohitajika ilikuwa imetosha, niliumia sana kwa sababu nilipenda sana kujiunga na chuo hicho. Nilipompigia simu baba na kumfahamisha alinishauri niende nikachukue fomu kwenye chuo kingine ambacho sitapenda kukitaja kwa jina . Nilipomaliza kuzungumza na baba , tulipanda gari hadi Mwenge tulipokutana na mpenzi wangu kisha tukapanda basi la kuelekea Temeke Mikoroshini. Tulipofika Tabata Dampo , tuliteremka tukapanda gari lingine hadi Tabata Bima tukashuka na kwenda kwenye nyumba aliyokuwa amepanga mpenzi wangu . Nyumba hiyo upande mmoja ambao alikuwa akiishi mpenzi wangu , walipanga wapangaji wawili vyumba viwiliviwili na upande mwingine walikuwepo pia wapangaji wawili . Alipofungua mlango na kutukaribisha ndani, tulishuhudia uzuri wa chumba hicho kilichokuwa na sofa seti moja, jokofu kubwa, radio kubwa ya kisasa na vitu vingine vya thamani. Kwa ujumla nilishangaa sana kuona mpenzi wangu aliyekuwa akisoma chuo kuwa na vitu vya thamani namna ile , nikapanga kumuuliza . Kilichonifanya niamue kumuuliza kwa sababu chumba chake kilikuwa sawa na cha mfanyakazi aliyekuwa akilipwa mshahara mnono . Tukiwa tumeketi sebuleni alitukaribisha kwa furaha na kutuambia pale ndipo alipokuwa akiishi hasa siku za mwisho wa juma au alipokuwa na nafasi. Kwa kuwa kwenye jokofu lake hakukuwa na vinywaji, alituuliza ni vinywaji gani tungependelea kunywa kila mmoja wetu akataja ndipo alikwenda kununua kwenye duka lililokuwa jirani. Akiwa ameenda huko, Joyce alimfagilia sana mchumba wangu kwa kuwa na akili na kuniambia alifaa sana kuwa mume wangu hivyo nisipoteze bahati . Nilimwambia hata mimi nilimkubali kwani kama angenioa tungekuja kuwa na maendeleo , tukiwa tunaendelea na mazungumo , mpenzi wangu alirejea na vinywaji . Tukiwa tunakunywa vinywaji, aliwasha runinga na kutuwekea CD ya filamu moja ya Kinigeria ambayo siikumbuki jina lake, tukawa tunaangalia. Baada ya muda alimuomba samahani Joyce kwamba alipenda anionyeshe chumbani kwangu, wote tukacheka. “ Hata mimi nisingekuelewa yaani mkeo afike hapa halafu asiingie chumbani kwako ?” Joyce alishadadia , tukacheka. Lakini kabla ya kwenda chumbani kwa mpenzi wangu, Joyce aliyekuwa anajua laaziz wangu alihitaji nini alituaga kwamba anaenda Segerea kumsalimia baby wake aliyenipa habari zake kwamba alikuwa akiishi huko . “ Mkiwa tayari utanipigia ili tusichelewe kurudi nyumbani, ” Joyce aliniambia nikamwambia sawa.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Happy akiwa amelala kitandani na mpenzi wake baada ya kuchoshana kwa walichofanyiana. Wakiwa wanatafakari penzi tamu walilopeana, Joyce ambaye naye alitoka kulishwa tende na mpenzi wake wa Segerea alimpigia simu Happy na kumfahamisha ndani ya dakika 35 angewasili.

    Joyce aliponieleza hivyo, tulikwenda kuoga tena kisha tulivaa na kwenda kukaa sebuleni tukaendelea kunywa vinywaji vyetu, wakati huo kila mmoja wetu alikuwa amechoka.Tukiwa tunaendelea na maongezi, mpenzi wangu aliniambia siku tukipata nafasi tutaenda katika chuo kikuu kimoja ambacho tawi lake lipo jijini Dar kwa ajili ya kuchukua fomu za kujiunga. Nilimshukuru kwa ushauri wake na moyoni nijiambia kwamba mpenzi wangu huyo ndiye angekuwa mume wangu bila kujua kama penzi letu lingetendwa na jini.Wakati tukimsubiri Joyce, mpenzi wangu aliyekuwa ameketi karibu, aliushika mkono wangu wa kulia akawa anachezea kiganja na kukisifia kwamba kilikuwa laini kama cha mtoto mchanga. Hakuishia hapo, akawa anachezea mapaja yangu na kuyasifia yalikuwa mazuri yaliyohamasisha yale mambo yetu, nikawa nacheka tu.Hakuishia hapo, aliniambia pia nilikuwa na midomo mizuri pamoja na macho ya kusinzia yaliyokuwa yanampagawisha mno, nikamshukuru kwa kunifagilia.Tukiwa tunapiga stori za hapa na pale, tulisikia mlango ukigongwa moja kwa moja tulijua Joyce alikuwa amefika, mpenzi wangu akaenda kufungua.Kama tulivyotarajia, mgeni huyo alikuwa Joyce na alipoingia ndani sebule yote ilinukia manukato mazuri. Kutokana na manukato hayo, nilimtania kwa kumueleza kwamba shemeji yangu alijua kumpetipeti, akacheka na kusema:“We acha tu, na alivyonimisi nimefurahije?” Baada ya Joyce kutoa kauli hiyo, wote tulicheka ndipo mpenzi wangu alimuuliza alipendelea kunywa kinywaji gani akasema apatiwe maji, akaletewa.Kwa kuwa muda ulikuwa umekwenda sana, mpenzi wangu ambaye siku hiyo aliamua kulala Tabata alitusindikiza hadi kituo cha daladala, akatupatia nauli na kabla hatujaagana  tulikumbatiana na kupigana mabusu.Kufuatia kumpenda sana, sikuona aibu kufanya hivyo hadharani kwani sikuvunja sheria ya nchi yetu. Tulipoagana naye tulipanda kwenye daladala ya Ubungo, tukiwa tumeketi siti ya tatu kutoka nyuma nilimsikia mama mmoja akimwambia mwenzake kwamba ‘mitandao imewaharibu watoto wetu’.Mwenzake alicheka na kusema enzi zao ilikuwa vigumu kumuona msichana na mvulana wakikumbatiana na kubusiana hadharani na kwamba mambo hayo yalifanywa na watu waliooana tena waliyafanyia chumbani.Wakati akina mama hao wakizungumza, Joyce aliniminya kwenye paja kisha aliniambia kwamba wale wamama walikuwa hawajui kama dunia ya leo ilikuwa imetengenezwa upya na siyo ya zamani, tukacheka.Hata hivyo, wale akina mama hawakuendelea na mada hiyo nasi tukaendelea na yetu ambapo Joyce alinifahamisha kuwa siku ile alijisikia raha sana.Nilipomuuliza sababu za kusema vile aliniambia alikuwa kammisi sana baby wake na kwamba alimfurahisha kwa kumpa alichokimisi, tukacheka.Tukiwa tunaendelea na safari nilimweleza kuhusu

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alivyoniahidi mpenzi wangu kwamba kesho yake angenipeleka kuchukuwa fomu za kujiunga na chuo kikuu kimoja cha nje ambacho tawi lake lipo jijini Dar. Joyce alimsifia sana mpenzi wangu kwa kunijali, tulipofika Ubungo tulipanda gari la kuelekea nyumbani, tukamkuta mama amesharudi.Mama alituuliza za tulikotoka tukamwambia nzuri na kumfahamisha kuhusu ushauri tuliopewa wa kwenda kuchukuwa fomu kwenye chuo tofauti na mlimani, akasema sawa bila kujua kama tulitoka kujirusha na wapenzi wetu.Kwa kuwa tulitoka mapema, tulifanya kazi za kupika na kuosha vyombo kisha tulizama chumbani kwetu ambako nilivua nguo na kumuonesha Joyce ‘Love bite’ yaani alama zilizotokana na mpenzi wangu kuning’ata meno wakati wa mashamshamu!Alama hizo zilikuwa shingoni na kwenye maziwa, Joyce alicheka kisha naye alivua na kunionyesha zake na kusema: “Yaani  hunifikii mimi, angalia zangu zilivyotapakaa.”  Joyce alinionyesha love bites zake zilizokuwa shingoni, na ule weupe aliokuwa nao zilikuwa kama damu ilivilia ndani, tukacheka sana.“Yaani leo ilikuwa kasheshe tupu na vile anavyoijua sanaa ya mapenzi we acha tu, tumekubaliana tukutane tena Ijumaa,” Happy anasema Joyce alimwambia.Kwa kuwa alama hizo zilikuwa zinaonekana, nilimwambia tuwe makini mama asije akatushtukia,  Joyce alinipongeza kwa kutoa ushauri huo, akainuka na kujongea kwenye kioo kilichokuwa kwenye mlango wa kabati la nguo akawa anajiangalia shingoni huku akicheka.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog