Search This Blog

PENZI LANGU - 2

 







    Simulizi : Penzi Langu

    Sehemu Ya Pili (2)



    Happy akiwa sokoni alipoguswa mgongoni , alipogeuka alimuona mpenzi wake , katika hali ambayo hakuitegemea bila kujali watu alimkumbatia kisha kusabahiana . Je , kilifuatia nini kwa wawili hao? Tuwe pamoja . .. Baada ya kusabahiana mpenzi wangu aliniuliza alinifanyia nini kibaya kiasi cha kumfanyia vile, licha ya awali kuapa kukata kabisa mawasiliano naye nikacheka na kumuuliza ; “ Kwani wewe hujui ulichonifanyia?” Baada ya kumuuliza hivyo , aliniomba msamaha na kuniambia nisijali kwa kilichotokea siku ile kwani kila mwanamke anayeanza mapenzi lazima apitie hatua ile . Mpenzi wangu alizungumza nami kwa upole na kuongeza kuwa siku tutakapokutana tena ningefurahi kuwa naye na ningejua nini maana ya mapenzi . Maneno yake matamu yalifurahisha nikamuuliza kama alichonieleza kilikuwa na ukweli kwani nilikuwa na hamu ya kujua raha ya mapenzi , akaniambia alichonieleza alikimaanisha . Mpenzi wangu aliniuliza nilipanga kutumia muda gani hadi kurudi nyumbani, nikamwambia zisipungue dakika 45 kwa sababu nilitakiwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kwenda kupika chakula cha mchana . Nilipomweleza hivyo , akiwa ananiminyaminya vidole vyangu vya mkono wa kushoto aliniambia kama sikujali twende tukapige stori kidogo kwenye kile chumba cha rafiki yake ambacho alikuwa huru nacho . Sijui nisemaje kuhusu suala la mapenzi , licha ya kuapa kutomhitaji tena yule kijana kufuatia hisia nilizopata wakati akiniminyaminya vidole sikumbishia. Tuliongozana naye hadi kwenye geto la rafiki yake ambapo alifungua mlango tukaingia na kuketi sofani kisha akafungua muziki kwa sauti kubwa na kunifuata . Tukiwa tumekaa karibu, aliniambia jinsi nilivyompa wakati mgumu nilipokuwa sijibu meseji wala kupokea simu zake na wakati mwingine kumzimia . Alipotoa kauli hiyo , nilimwambia alikuwa na bahati kuamua kurudisha moyo nyuma kwani nilimchukia sana lakini ashukuru nilimsamahe , akacheka na kuniuliza : “ Jamani Happy ulinichukia kwa sababu gani . . . si uliniahidi kwa kinywa chako kwamba utanipa zawadi ?” “ Hata kama , ndiyo unifanyie vile yaani wewe sitakusahau maishani mwangu ,” Happy anasema alimwambia mpenzi wake . Nilipomwambia hivyo , aliushika mkono wangu wa kushoto

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akaanza kuviminyaminya tena vidole vyangu kisha akawa ananichezea maeneo mengine hususan nyonga

    zangu , mwili ukanisisimka . Hakuishia hapo , akawa ananichumu mashavuni na midomoni huku mikono yake ikileta fujo maeneo mengine ikiwa ni pamoja na kifuani kwenye ‘ viembe ’ vyangu bolibo. Hali iliyonikabili nashindwa namna ya kuielezea baadaye tulihamia kwenye uwanja wa fundi seremala ambapo tuliendelea na zoezi la kikubwa , kwa mara ya kwanza nilipata raha ya mapenzi badala ya karaha . Kila mmoja wetu alifurahi sana , sikujua kama mchezo niliouanza ungeniathiri siku za baadaye, baada ya kujiweka sawa alinisindikiza nikarejea nyumbani . Bahati nzuri mama hakuwepo, nilipika chakula cha mchana haraka kisha nilikwenda kujipumzisha chumbani na kuanza kutafakari raha ya mapenzi niliyopata . Tangu siku ile, kila nilipopata nafasi nilikuwa natoroka nyumbani nakwenda kukutana na mpenzi wangu ambaye alikuwa na upeo wa masuala ya uhusiano. Tukiwa tumebakisha siku kama tano kurudi shuleni , tulikutana na mpenzi wangu huyo kwenye chumba cha rafiki yake mwingine ambapo aliniuliza siku niliyoanza mzunguko wangu. Nilipomfahamisha aliniambia siku ile haikufaa kukutana kwa sababu ilikuwa ya hatari yaani kama tungefanya zoezi letu ningeweza kupata ujauzito , nikamuuliza alijuaje akacheka . Baadaye aliniambia kwamba alikuwa akielewa vizuri elimu ya uzazi kwa wanawake aliyoipata kupitia mwalimu wake wa sayansi , akanieleza siku gani zilikuwa salama na hatari . Kitendo cha mpenzi wangu kunipa darasa hilo, kilinifurahisha na kunifanya nimpende maradufu kwa sababu alionesha kunijali ili nifikie malengo yangu kimasomo. “ Wala usijali Happy , sisi bado tunasoma ni vizuri tukijihadhari na masuala ya mimba na magonjwa pia , nimefanya hivyo kwa sababu nakupenda ,” Happy alimnukuu mpenzi wake . Siku hiyo tulipiga stori mbalimbali ambapo nilimweleza kuhusu mkwara niliopigwa na baba kama ingetokea ningepata mimba au kufanya mambo ya kipuuzi . Mpenzi wangu aliniambia hata yeye mara kwa mara amekuwa akipewa risala hiyo na wazazi wake na kuwaahidi kwamba hatawaangusha huku nyuma ya pazia akiwa na mimi. Baada ya kurejea nyumbani, usiku tukiwa tunapiga stori na kaka yangu aliniasa kuhusu suala la kuzingatia masomo kama wazazi wetu walivyokuwa wakituambia . Kaka yangu huyo aliyekuwa tofauti na vijana wenzake waliokuwa bize na mambo ya kisharobaro , aliniambia kwamba tusome ili tusimuangushe baba aliyekuwa akitumia fedha nyingi kutusomesha shule za gharama . Maneno yake yaliingilia huku na kutokea kule kwani wakati huo penzi letu na mpenzi wangu lilipamba moto kweli , moyoni nilimwambia yeye asome kwa sababu alikuwa mtoto wa kiume . Siku moja kabla ya kuondoka kuelekea Mwanza nilikokuwa nasoma , wazazi wangu walinikalisha chini na kurudia onyo la kuzingatia shule na kuachana na mambo yasiyofaa bila kujua tayari nilikuwa nimeanza mapenzi . Baba alizungumza sana akafuatia mama , ambapo niliwaambia wasihofu nitazingatia waliyonieleza, moyoni niliwaambia mpaka namaliza nisingepa mimba. Nilijiamini hivyo kwa sababu mpenzi wangu alinipatia elimu ya namna ya kujikinga na mimba, baadaye nilipewa fedha za kwenda kutumia shuleni na kila kilichohitajika .</p><p> baba na mama yake Happy walipomuasa kwa mara nyingine binti yao huyo kuhusu kutojihusisha na masuala ya mapenzi ambapo moyoni alijisemea kwamba asingeweza kupata ujauzito kufuatia kupewa elimu ya namna ya kujizuia kutopata mimba na mpenzi wake . Je , kilifuatia nini? Songa mbele. .. Alfajiri, tuliondoka na baba , kaka na wadogo zangu tukaelekea stendi nilikopanda basi la kwenda Mwanza na kumuacha mpenzi wangu ambaye tulipishana wiki moja kufungua shule . Kama unavyofahamu wasichana wanapokutana shuleni baada ya kumaliza likizo wanavyopeana michapo ya makwao na wale mapepe stori za mapenzi , nilipokutana na rafiki yangu Rose nilimwambia nami nilianza masuala ya mapenzi . Rafiki yangu huyo ambaye tulielewana licha ya kwamba tayari alikuwa ameanza mapenzi mapema, alishangaa na kuniambia nisimtanie . Sikumficha, nilimhadithia kila kitu kuhusu mpenzi

    wangu ndipo aliniuliza niliona jinsi nilivyokuwa nakosa kitu muhimu katika maisha yangu , nikamwambia hakika mapenzi yalikuwa matamu ! Msichana huyo aliniuliza itakuwaje nikiwa nahitaji kuchangamsha damu wakati mpenzi wangu akiwa mbali, nilimwambia nitamsubiri hadi tutakapofunga shule . Rose alicheka na kuniambia jambo hilo lilikuwa gumu ndiyo maana yeye pale Mwanza alikuwa na mpenzi wake licha ya kwamba kwao alikuwa na mtu pia . Kwa kuwa nilikuwa nampenda sana mpenzi wangu, nilimwambia sikuhitaji kutoka na mwanaume mwingine zaidi yake na nilikuwa tayari kuvumilia mpaka tutakapokutana . Msichana huyo alicheka na kuniambia ataona kama ningeweza kuvumilia hasa kufuatia kusumbuliwa na wavulana kutokana na uzuri nilionao , nikamwambia sitamsaliti mtu wangu kamwe . Siku iliyofuata tulifungua shule ambapo kazi kubwa ilikuwa kuyaweka mazingira ya shule katika hali ya usafi, jioni wote tulikwenda kufanya mazoezi ya viungo uwanjani . Kwa kuwa wanafunzi hatukuruhusiwa kuwa na simu, niliificha kwenye mfuko mdogo wa begi kwani sheria ilikuwa mwanafunzi atakayekutwa na simu ni kutimuliwa . Niliendelea na masomo huku nikiwasiliana kwa siri na mpenzi wangu , nilipohitaji kuchati naye nilikuwa naingia msalani au sehemu ambayo haikuwa na watu. Kufuatia mazingira ya shule kuwa magumu kutumia simu , mpenzi wangu

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ambaye wazazi wake walikuwa na uwezo alikuwa akinitumia vocha tukawa tunawasiliana kwa siri. Jumapili ilipofika, rafiki yangu Rose akiwa na Mary na Zainabu waliniambia twende tukatembee mjini kwa sababu wakati wa wikiendi tuliruhusiwa kwenda mjini na kwa waliokuwa na ndugu walikwenda kuwasalimia. Niliwaambia nikitoka kanisani tutakwenda, kweli baada ya kurejea nyumbani kutoka kanisani, tulijiandaa na kwenda mjini kumsalimia dada yake Zainabu . Tukiwa hapo walikuja vijana wawili ambao walifahamiana na wenzangu, baada ya salamu waliendelea kupiga stori huku vijana hao wakiwaambia akina Mary kwamba waliwakumbuka sana . Kutokana na maongezi yao , nilibaini vijana wawili walikuwa wakitoka na Zainabu na Mary ila Rose mpenzi wake hakuwepo, kama nilivyohisi Mary alinitambulisha kwa mmoja wa wale vijana kwamba alikuwa mtu wake. Hakuishia hapo , Zainabu naye akanitambulisha kwa wake tukaendelea na habari za hapa na pale, kama saa moja baadaye lilifika gari dogo wakashuka vijana wawili ambao walikuwa wakifahamiana na waliokuwepo pale . Mmoja wa vijana hao mwenye asili ya kishombeshombe aliponiona akaachia tabasamu na kuja kunisabahi na kunipongeza kwa kuwa mzuri . Zainabu akaniambia yule kijana aliitwa Razaq kwao ni Tanga ila pale Mwanza alikuwa akiishi na wazazi wake ambao walikuwa wafanyabiashara, hakuishia hapo alimtambulisha nami kwamba niliitwa Happy tulikuwa tunasoma wote. Baada ya utambulisho, Razaq alituambia twende kwenye kibanda walichouza vinywaji baridi ambacho kilikuwa jirani, wote tukaongoza hapo ambapo alimtaka kila mmoja anywe kinywaji na kitafunwa alichohitaji . Wakati tukiendelea kupata vinywaji, yule kaka shombeshombe aliyekuwa yupo smati sana kuliko wenzake alikuwa akiniangalia lakini nilijifanya sikumuona. Kuna wakati macho yetu yalipogongana , alinikonyeza kijanja sana na kuachia tabasamu , nikajua alikuwa kavutiwa nami. Wenzangu waliendelea kupiga stori na wale vijana ambao walikuwa wakitoka nao ndipo nilimuona Zainabu na yule Razaq wakienda kando kidogo wakaanza kuzungumza. Baadaye Zainabu aliniita , nilipoenda alinitambulisha tena kwa yule kijana na kuniambia alihitaji kuzungumza na mimi hivyo kama sitajali nimsikilize , nikamuuliza azungumze kitu gani na mimi akasema nimsikilize tu . Moja kwa moja nilijua kijana huyo alitaka kuniambia kuhusu masuala ya mapenzi , nikamwambia kwa siku ile sikuwa tayari kuzungumza naye asubiri siku nitakayopata nafasi. “ Ni nafasi gani unayohitaji zaidi ya leo , usinifikirie vibaya tunazungumza mambo ya kawaida tu wala usihofu, ” yule kijana aliniambia. Licha ya Zainabu kunibembeleza sana nimsikilize yule kijana, nilisisitiza kwamba sikuwa tayari anisubiri mpaka nitakapopata nafasi kwa sababu siku ile sikujiandaa . Razaq hakuwa na la kufanya zaidi ya kukubaliana na matakwa yangu , ila aliniomba Jumapili iliyofuata tukutane tena ili azungumze nami , kwa kumridhisha nikamwambia sawa .



    Tulipokubaliana tulirudi kwa wenzetu ambapo Razaq aliyeonekana hakuwa na tatizo la fedha alituambia yeyote aliyehitaji kuongeza kinywaji afanye hivyo . Sikuelewa alifanya vile kuonesha uwezo aliokuwa nao ili iwe rahisi kunipata au laa , Zainabu , Mary na Rose na wale vijana wawili waliongeza vinywaji lakini mimi tumbo lilikuwa limejaa sikuongeza . Tulipomaliza kunywa soda Zainabu , Mary na wale wapenzi wao walisogea pembeni na kuniacha na Rose ambapo walizungumza kisha walirejea tulipokuwepo. Walipomaliza maongezi yao walirejea na baada ya kumaliza vinywaji wale vijana walituagaa lakini kabla ya kuondoka Razaq alifungua pochi na kumkabidhi Zainabu shilingi 12, 000 ambazo alisema tugawane. Baada ya wale vijana kuondoka nasi tulirudi nyumbani kwa dada yake Zainabu ambapo tulikuta katuandalia chakula tukala ndipo alituaga kwamba anatoka kidogo tusiondoke hadi atakaporudi . Tukiwa sebuleni tunazungumza , Zainabu aliniambia nitaendelea kukaa bila kuwa na rafiki wa kiume kama wao hadi lini , nikamwambia sikuhitaji kufanya hivyo kwa sababu nilikuwa na mpenzi wangu. Nilipotoa kauli hiyo , Zainabu alicheka na kuniambia hakukuwa na ubaya kuwa na mtu ambaye angechukua nafasi wakati mpenzi wangu akiwa mbali kwa sababu fimbo ya mbali haiui nyoka. Kwa kuwa nilisikia hakuna kitu kibaya kwenye mapenzi kama usaliti, nilimwambia sikuona haja ya kufanya hivyo na kwamba nitakuwa namsubiri ‘ mtu ’ wangu hadi tukifunga shule . Baada ya kusema hivyo , Mary alidakia na kuniambia kwamba nilipaswa kuchangamka kama wao ambao nyumbani kwao walikuwa na wapenzi na shuleni pia walikuwa nao. “ Si unaona wenzako , tumekutana na watu wetu tumepata kinywaji na kupewa shilingi 12, 000. . . sema leo Razaq inaonyesha hakuwa na hela siku nyingine huwa anatupa hadi shilingi ishirini elfu ,” Mary aliniambia . Mary alipotoa kauli hiyo , Zainabu alidakia na kunieleza kwamba Razaq alitokea kunipenda hivyo kama sitojali nimkubali ili kampani yetu itimie. Kwa hofu ya kutomsaliti mpenzi wangu, nilimkatalia lakini aliendelea kumsifia kijana huyo kwamba alikuwa poa sana na kwamba nikianza kutoka naye tatizo la fedha nitakuwa nalisikia kwa wenzangu. Marafiki zangu walipoona sijabadili msimamo wangu waliamua kuniacha , dada yake Zainabu alipofika tulimuaga tukarudi shuleni ambapo Mary aliniuliza kwa nini sikutaka kuwa na mpenzi kama wao .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilimwambia kwamba nilikuwa nampenda sana mpenzi wangu , pili nilimweleza kitendo cha kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja kingechangia kurudi nyuma kimasomo, akacheka na kuniambia : “ Kila kitu kina wakati wake , wakati wa kusoma utasoma na wakati wa mapenzi utajitegemea , we mkubali Razaq si umeona mambo yake?” Kuepusha usumbufu kuhusu huyo kijana nilimwambia aniache kwanza nifikirie , kufuatia kauli hiyo Mary alifurahi sana lakini hakujua kama sikuwa na mpango kabisa na huyo kijana. Baada ya mazungumzo ya muda mrefu , muda wa kwenda jikoni kuchukua chakula ulipofika tulikwenda kwenye bwalo la kulia tulikula kisha tulirudi bwenini. Wakati sikuwa na mpango kabisa wa kumkubalia Razaq , kumbe Mary na Zainabu walikuwa wakiwasiliana naye na kumwambia mambo yalikuwa yakienda vizuri yaani nilielekea kumkubali . Rose ndiye alikuwa akiniambia kila kitu kuhusu Mary na Zainabu kwa sababu wasichana hao watatu walikuwa marafiki na walifichiana siri zao . Kama nilivyokwambia kwamba licha ya shuleni kutoruhusiwa mwanafunzi kuwa na simu , niliendelea kutumia simu yangu kwa siri kuchati na mpenzi wangu ambapo alikuwa akinisisitiza sana nisije kumsaliti . Kwenye moja ya meseji yake aliniambia kwamba siku nikimsaliti atajua na huo utakuwa mwisho wa uhusiano wetu , kauli yake ilinifanya niwe muoga wa kumsaliti . Siku hiyo usiku nikiwa bwenini, Zainabu alinifuata na kunikabidhi shilingi 10, 000 na kuniambia kwamba alitumwa na Razaq aniletee zinisaidie kununua kitu chochote nilichopungukiwa. Kwa kuwa hata siku moja sikuwahi kupokea fedha kutoka kwa mwanaume ambaye sikuwa na undugu naye , nilimwambia asante na kumuomba amrudishie Razaq fedha zake. Zainabu ambaye baadaye alikuja kufukuzwa shule kwa kupewa mimba , alicheka na kuniambia niache ujinga napewa fedha halafu naringa kuzipokea. Msicha huyo alinishambulia na kwenda kuwaambia akina Mary ambao nao waliniona mtu wa ajabu , nakumbuka Zainabu aliniambia kwamba kweli kwenye miti hapakuwa na wajenzi. “ Yaani wewe Happy utafikiri unatoka kijijini, mtu anakupenda na kwa hiari yake kanipa fedha nikupatie unazikataa ? Sijapata kumuona msichana wa aina yako !” Zainabu aliniambia</p><p> Alipotoa kauli hiyo , Mary akadakia kwamba huyo mpenzi wangu kwanza alikuwa mwanafunzi kama mimi asingeweza kunisaidia chochote, nikawaambia acha waseme lakini nisingepokea zile fedha . Baadaye marafiki zangu waliamua kuniacha, kesho yake jioni baada ya kutoka shuleni walimtuma mlinzi akanunue chipsi tatu za mayai na samaki aina ya sato na soda . Mlinzi aliporejea aliwakabidhi mfuko uliokuwa na chipsi ndipo walizitoa, moja alichukua Mary, ya pili Zainabu na ya tatu walimpatia Happy pamoja na soda , Rose hakuwepo. Tukiwa tunakula Zainabu aliniambia kwamba ile shilingi elfu kumi niliyokataa kuipokea ndiyo waliamua kununua chipsi tulizokuwa tukila pamoja na soda na kuongeza kuwa siku zote kilichoenda kwa mganga akirudi . Alipotoa kauli hiyo nilijua wale rafiki zangu walikubuhu kwa masuala ya wanaume, nikamuuliza kama Razaq angewauliza kuhusu fedha yake angemwambia nini? “ Suala hilo niachie mimi , wewe si umekataa kupokea fedha hizo unajifanya huna shida lakini chipsi na soda unazifurahia ?” Zainabu alinichana live. Kauli yake ilinichoma lakini moyoni nilijisemea kwamba suala la kumsaliti mpenzi wangu lilikuwa halipo na sikumlazimisha aninunulie chipsi. Tuliendelea na stori huku tukila , tulipomaliza tulienda kujisomea hadi jioni ambapo tulikwenda kwenye mazoezi ambayo ilikuwa kawaida kuyafanya . Kama nilivyokuambia kwamba licha ya wanafunzi kutoruhusiwa kuwa na simu pale shuleni , usiku nilikwenda msalani na simu yangu nikachati na mpenzi wangu kwa dakika kadhaa. Kikubwa alisisitiza nisimsaliti, nilimhakikishia kwamba sitafanya hivyo kamwe kwa sababu nilikuwa nampenda. Tulipomaliza kuchati nilirudi bwenini, nikalala na kulipokucha tuliendelea na ratiba ya masomo kama kawaida . Ilipofika Jumapili ambayo wanafunzi tulikuwa tunaruhusiwa kwenda kutembea mjini na kwa wenyeji kwenda kuwasalimia ndugu zao , rafiki zangu waliniambia twende tukatembee mjini . Awali sikuona umuhimu wa kwenda huko ambapo nilitaka nibaki ili nifanye usafi kisha nijisomee lakini baada ya kubembelezwa sana na wenzangu nikaamua kwenda . Siku hiyo sikwenda kanisani, tulipokunywa chai tulitoka na kwenda mjini ambapo waliokuwa na fedha walinunua vitu walivyovihitaji , kwa upande wangu sikununua chochote. Sikufanya manunuzi kwa sababu karibu kila kitu nilikuwa nimenunuliwa nyumbani , tukiwa mjini Zainabu alituambia kabla hatujarudi shuleni twende tukamsalimie dada yake tuliyemtembea Jumapili iliyopita. Kutokana na ucheshi na ukarimu wa dada huyo, tulikubaliana tukashika njia kwenda huko ambapo alitupokea vizuri, alitupikia wali kwa samaki tukala tukashiba. Baadaye Zainabu alituambia twende tukapate vinywaji kwenye duka tulipokutana na wale wapenzi wao, moja kwa moja nilihisi wale vijana walikuwa pale. Sikutaka kuhoji tukaenda , kama nilivyohisi wakati tunakaribia kufika nililiona gari la Razaq na tulipofika nilimuona kijana huyo akiwa na wenzake watatu ambao tulikutana nao Jumapili iliyopita . Walipotuona walifurahi sana, Zainabu na Mary walikumbatiana na wapenzi wao ndipo Razaq akawa anataka kunikumbatia nikamkwepa . Kufuatia kitendo hicho aliniuliza mbona nilimkatili namna ile nikamwambia sikumkatili bali sikuzoea kufanya vile , akacheka na kuniambia ningezoeaje wakati sikutaka kujaribu! Razaq alipotoa kauli hiyo , akina Zainabu na wale vijana wengine walicheka ndipo Zai aliniambia mbona

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kukumbatiana hakukuwa na shida kwani ni kuoneshana upendo tu ! Licha ya kutoa kauli hiyo , niliwaambia sikuzoea kufanya hivyo , Razaq akiwa anacheka alituambia siku ile alitaka kutupeleka sehemu nyingine kwa ajili ya ofa ya chakula cha mchana . Ingawa muda mfupi uliopita tulikuwa tumekula, wenzangu hawakukataa ndipo nilijisemea moyoni kwamba tukifika huko sitakula chochote kwa sababu nilikuwa nimeshiba . Baada ya kukubaliana na Razaq , kijana huyo alituambia tupande kwenye gari lake ambapo aliwaambia Zainabu , Mary na Rose wakae siti ya nyuma na mimi nikae kiti cha mbele . Aliposema hivyo , nilimwambia mimi nitakaa nyuma na Mary na Rose ila Zainabu akae mbele lakini Razaq alipinga na kusema yeye alinichagua mimi nikae siti ya mbele . Kuondoa malumbano , niliingia na kukaa na wenzangu walikaa nyuma , kabla hajaondoa gari alitoa shilingi elfu tatu na kuwapatia rafiki zake ambao aliwaambia wakodi teksi watatukuta eneo alilowaelekeza .



    Kijana huyo aliendesha gari lake huku akiniangalia mara kwa mara lakini mimi sikuwa na habari naye , mawazo yangu yalikuwa kwa mpenzi wangu ambaye nilimuona ni kila kitu hapa duniani. Alipofika kwenye nyumba moja kubwa na nzuri iliyopo Nyakato alipiga hodi getini kijana mmoja akafungua mlango ndipo akaingiza gari ndani na kuliegesha . Baada ya kuegesha tulishuka ambapo alitufahamisha kwamba ile nyumba ilikuwa ya kaka yake ambaye wakati huo alikuwa amesafiri na familia yake kwenda Dar na kwamba alikuwa amebaki yeye, kijana wa kazi na msichana wa kazi. Alipotueleza hivyo , alitukaribisha ndani ambapo tulipita katika sebule ya kwanza iliyokuwa ina samani za bei mbaya , tukanyoosha kwenye korido na kwenda kutokea kwenye sebule nyingine ambayo haikuwa tofauti sana na ya kwanza. Tukiwa pale alitukaribisha tuketi kisha alituambia kwamba kwenye jokofu lililokuwa sehemu ya kulia chakula kulikuwa na vinywaji tofauti kasoro bia tu hivyo kila mmoja wetu aseme alihitaji kunywa nini. Mary alihitaji juisi ya embe, mimi nikasema ya nanasi na waliobaki walisema vinywaji walivyohitaji, Razaq alikwenda kwenye jokofu na kurejea na vinywaji hivyo . Wakati tumeanza kunywa , walifika rafiki zao tukajumuika pamoja ambapo mmoja aliinuka na kwenda kwenye jokofu akatoa soda mbili , tukawa tunakunywa. Razaq aliyekuwa akinywa kinywaji chake na kuniangalia alituambia kwamba tuwe huru kwa lolote hata kama tulihitaji kucheza muziki ilikuwa ruksa kisha alimwita Zainabu wakaelekea kwenye korido la kwenda vyumbani . Walikaa huko kama dakika tano hivi wakarejea, wakati huo wale vijana waliokuwa na uhusiano na Mary pamoja na Rose walikuwa wamekaa pea na wapenzi wao kasoro mimi . Baada ya dakika kama kumi hivi , Zainabu aliniomba nimfuate tukaongozana hadi kwenye mlango wa chumba kimoja lakini kabla hatujaingia nilimuuliza alitaka kufanya nini? Aliniambia nisiwe na wasiwasi alitaka tuzungumze jambo flani, moyo ulisita lakini baada ya kunibembeleza sana na kwa vile Razaq tulimuacha sebuleni nikaamua kuingia . Chumba hicho kilikuwa na kabati la nguo na kitanda kikubwa cha futi sita kwa sita kilichotandikwa mashuka ya pinki , kwa ujumla kilikuwa ni chumba cha ‘ ukweli ’ . Tukiwa mle ndani, Zainabu alianza kunishawishi nimkubalie Razaq ambapo aliniambia alitokea kunipenda sana na hata kufika kwetu pale ni kwa ajili yangu . Nilimwambia kwamba tayari nilikuwa na mpenzi wangu niliyekuwa nampenda hivyo nisingeweza kumsaliti , wakati tunazungumza Razaq aliingia mle chumbani, moyo ukapiga paa ! Kijana huyo aliyeonesha kunipenda , alipoingia aliketi kitandani akawa ananiangalia kisha akaniuliza kama nilifurahi kuwepo pale, nikamwambia nilifurahi. Nilipotoa kauli hiyo alifurahi kwani alihisi ningemkubalia ombi lake lakini ukweli ni kwamba sikuwa na wazo hilo kabisa na sikupendezwa na kitendo cha Zainabu kunishawishi niwe mpenzi wa Razaq . Baada ya kumwambia hivyo , Razaq alitoka nikabaki na Zainabu ambaye aliniambia kwamba kama ningemkubalia matatizo madogomadogo pale shuleni ningeyasikia kwa wenzangu. Kama waswahili walivyosema kwamba kila shetani na mbuyu wake , licha ya kijana huyo kuonekana fedha kwake kilikuwa kitu kidogo sikumpenda badala yake mawazo yangu yalikuwa kwa mpenzi wangu . Nilimwambia Zainabu kwamba sikuhitaji kuwa na Razaq , mosi kwa sababu nilikuwa na mpenzi wangu na pili , nilihofia kufanya vibaya katika masomo . Nilipotoa kauli hiyo , Zainabu alicheka na kuniuliza kwamba mbona wao walikuwa na wapenzi lakini darasani walifanya vizuri nikamwambia kama wasingekuwa wanajichanganya basi wangukuwa na akili nyingi zaidi . Alipoona nimeshikilia msimamo wangu, alichukia na kuniambia kuanzia siku hiyo wataacha kuongozana nami kwenye safari zao kwa sababu sikutaka kumuelewa nikamwambia sawa. Tuliposhindwa kuelewana , tulirudi sebuleni ambapo nilishangaa kutomuona Rose na Mary na wapenzi wao isipokuwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mmoja aliyekuwa na uhusiano na Zainabu . Moja kwa moja nikajua walikuwa wamekwenda kwenye vyumba vingine , nilipokaa yule kijana mpenzi wa Zainabu aligundua kama sikuwa sawa akaniuliza mbona nilikuwa katika hali ile , nikamwambia sikujisikia vizuri. Aliniuliza sikujisikia vizuri kwa sababu nilikuwa naumwa au kuna kitu sikufurahishwa nacho , nikamwambia aelewe tu kwamba sikujisikia vizuri, kufuatia jibu hilo aliguna akawa anaangalia runinga pamoja na Zainabu . Hakukaa muda mrefu aliinuka na kuelekea kwenye korido la vyumbani , ambapo dakika chache Zainabu naye alimfuata . Wakati huo sikumuona Razaq na wala sikujua alikuwa wapi. Nikiwa nimebaki peke yangu pale sebuleni , nilijua kilichokuwa kikiendelea kati ya wale wavulana na wenzangu, nikatamani kuondoka lakini nikaona kurudi shuleni peke yangu isingekuwa vizuri.



    Kwa kuwa nilikuwa naelewa kilichokuwa kikiendelea mle ndani, nikamkumbuka mpenzi wangu hasa jinsi alivyokuwa akinifanyia na kunisisimua lakini sikuwa na la kufanya zaidi ya kuvumilia mpaka tutakapoonana. Nikiwa natafakari, nilisikia muungurumo wa gari nje , awali sikufikiri kama Razaq alikuwa ametoka hadi alipoingia akiwa amebeba mifuko ya Rambo iliyojaa vitu akaniomba nimpokee . Sikuwa na kipingamizi , nilimpokea aliokuwa ameubana kwapani nikauweka kwenye meza nzuri ya mbao iliyokuwepo pale sebuleni, kisha aliniuliza wenzangu walikuwa wapi nikamwambia sikuelewa . Razaq alisema alikuwa anajua walipokuwa ndipo aliniacha kwa muda aliporudi , aliniambia wenzangu walikuwa wakipiga stori na rafiki zao na kunitaka nami niongozane naye tukazungumze kwenye chumba chake. Kuhofia kijana huyo kunifanyia fujo kwa sababu nilikuwa kwao , nilimwambia siku hiyo sikujiandaa kwa maongezi hivyo kama hatojali tupange siku nyingine ya kukutana naye. Baada ya kumwambia hivyo , Razaq aliachia tabasamu na kuniambia alifurahi sana kusikia kauli yangu akaongeza kuwa kabla ya wenzangu hawajarejea pale sebuleni angenipatia zawadi . Nilimwambia asijali na kwamba hiyo zawadi angenipatia siku tutakayokutana , akasema kwa vile nilimfurahisha alitaka kunipa muda uleule nikamwambia sawa . Kijana huyo alitoa pochi aliyoiweka kwenye mfuko wa suruali yake, akaifungua na kuchomoa noti mbili za shilingi 10 , 000 na kunikabidhi, ingawa nilikuwa nahofu nilizipokea . Alipoona nimezipokea aliniomba tukumbatiane kisha tubusiane kama ishara ya upendo, nikamwambia asiwe na haraka asuburi siku niliyomuahidi . Razaq aliniambia alitamani sana tukumbatiane siku ile japo kidogo huku tukisubiri siku rasmi lakini nilimwambia asiwe na shaka kwani siku ambayo tungekutana angefurahi na roho yake. Alipoona msimamo wangu alikubaliana nami lakini ukweli nilitaka nitoke salama mle ndani na niliahidi kutoambatana tena na akina Zainabu , tukiwa tumekaa tunatazamana na Razaq alifika Mary. Macho yangu na yake yalipogongana akaangalia chini kwa aibu , alikuwa katika hali hiyo kwa sababu ni kawaida ya wanawake kuwa hivyo wanapotoka kutenda ‘ dhambi ’ . Alipoketi alisema mambo vipi ? Nikamwambia poa tu kisha akamwambia Razaq niaje naye akamwambia ilikuwa poa tu! Tukiwa tunaangalia runinga , alirejea mpenzi wa Zainabu ambaye alikuwa akichekacheka , akamuuliza Razaq bado tulikuwa tukisikiliza muziki ? Kijana huyo alituomba samahani na kusema ngoja aweke filamu ya marehemu Kanumba iitwayo More Than Pain ambayo alikuwa akiipenda sana , hakuna aliyembishia . Wakati akitafuta DVD ya filamu hiyo , Rose alirudi huku akijibalaguza kwa kuimba, alipoketi akafuatiwa na mpenzi wake ambaye alikuja huku shati kalishika mkononi . “ Niaje waungwana . . . naona mumehamia kwa Kanumba sasa?” Yule kijana alituambia Razaq akamjibu filamu zake ni kali sana ndiyo maana tuliamua kuangalia. Tukiwa tunapiga stori Zainabu ambaye hakuwa na mshipa wa aibu alikuja huku kamkumbatia mpenzi wake , wakaenda kukaa kwenye sofa moja akawa anamchezea kidevu, wote tukawa tunacheka. Tukiwa tunaendelea na stori , Razaq aliniambia nifungue ile mifuko ya Rambo na kutoa chakula kilichokuwa kimefungwa kwenye maboksi maalum ya kubebea chakula ‘ Take away’ . Niliinuka nikatoa chakula na kumpelekea kila mmoja, ambapo waliinuka na kwenda sehemu ya kulia chakula palipokuwa na bomba wakanawa na kurejea ambapo kila mmoja alifungua boksi lake . Chakula kilichokuwemo ni kuku kwa chipsi, tulipomaliza kula tulimshukuru Razaq kwa kila kitu ndipo Zainabu aliaga kwamba muda wa kurudi shuleni uliwadia . Razaq aliyekuwa anaamini tungekutana kama nilivyomuahidi alitushukuru kisha tulitoka ndani ambapo wale rafiki zake walituaga na kuwasisitiza akina Zainabu wiki iliyofuata waonane . Zainabu alimwambia asijali kikubwa kama tungekuwa wazima tungeenda lakini kwa upande wangu siku ile ilikuwa mara yangu ya mwisho kutoka nje ya shule na akina Zainabu . Walipomaliza kuagana , tuliingia kwenye gari la Razaq aliyetupeleka kwa dada ya Zainabu ambaye hatukumkuta ndipo alitupeleka hadi karibu na shule , alitupatia shingili 10 ,000 na kutuambia tugawane lakini kabla hajaondoka alizungumza jambo na Zainabu aliyemjibu kwamba kila kitu kingeenda sawa . Moja kwa moja nilijua walinizungumzia na Zainabu ambaye alimhakikishia angefanikisha kunishawishi nimkubali Razaq , moyoni nilijisemea kwamba asingenipata ng’ o licha ya kunipatia shilingi 20 , 000.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Razaq ambaye alikuwa mcheshi , kabla ya kuondoka alituaga kwa kutushika mikono , alianza kwa Mary, Rose , Zainabu alipofika kwangu alikitekenya kiganja changu na kuniambia kwa kuninong’ oneza ; “ Kwaheri dada mzuri ila naomba Jumapili ijayo usiniangushe nitakusubiri pia nitakuandalia zawadi nzuri sana. ” Kufuatia kauli hiyo , nilimwambia asijali kama nitakuwa na afya njema tungeonana lakini niliapa kutotoka kabisa shuleni siku hiyo na nilipanga kujifanya mgonjwa . Nilipomweleza hivyo , Razaq alitabasamu akiwa na imani kwamba tayari alikuwa ameniweka sawa baada ya kunipatia shilingi 20, 000 ikiwa ni pamoja na mambo ya fedha aliyoyafanya nyumbani kwao . Kijana huyo kwa jinsi alivyokuwa handsome, kwa msichana yeyote ambaye hakuwa na msimamo ilikuwa rahisi kumkubalia kwa sababu ya kuwa na fedha na usafiri , alipotabasamu alinikonyeza kimtindo kisha aliingia kwenye gari lake akatupungia mkono na kuondoka . Wakati tunaelekea shuleni , Zainabu , Mary na Rose walimfagilia sana na kusema siku ile waliinjoi na kuniuliza kwa nini nilikuwa namzungusha Razaq wakati alikuwa akinipenda. Niliwaambia suala la mtu kumpenda mtu lipo juu yake mwenyewe na kwamba sikuwa tayari kumsaliti mpenzi wangu kwa sababu alikuwa mbali. Zainabu alicheka na kuniambia niache ushamba kwa sababu bado nilikuwa msichana mbichi ambaye kutokewa na wanaume wenye maisha yao kama Razaq lilikuwa jambo la kawaida, nikawaambia ninsingeweza kufanya hivyo . Licha ya kuwaeleza msimamo wangu, Zainabu aliniambia kwamba usiku tungeongea kwa kirefu na ningemuelewa , nikamweleza kama atakuja kwa ajili ya maongezi yaliyohusu masomo sawa lakini sikuhitaji kusikia habari za Razaq . Nilipomwambia hivyo , alicheka na kusema : “ Watu wengine kwa kujifanya wana misimamo!” Nilimjibu kwamba nilikuwa na msimamo kwa sababu nilikuwa najitambua, akacheka na kuniambia sikupaswa kuwa hivyo kwa sababu Razaq alitokea kunipenda sana. Tulipofika getini tuliacha maongezi hayo , tulimsalimia mlinzi kisha tulikwenda mabwenini lakini msimamo wangu ulikuwa ni kwamba nisingetoka tena kwenda matembezi na akina Zainabu . Usiku baada ya kula , Zainabu alinifuata na kuniuliza kama bado nilikuwa na msimamo wa kutokuwa na Razaq , nikamwambia asahau kabisa kuhusu suala hilo na akamwambie nilikuwa na mtu wangu . Alipobaini sikuwa na masihara, aliondoka na tangu siku hiyo uhusiano wetu haukuwa mzuri na hata siku ya Jumapili waliponiambia tutoke nilikataa. Tuliendelea na masomo lakini kabla ya kufunga shule kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka , Mary aligundulika alikuwa na mimba alipoulizwa mhusika alimtaja mmoja wa wale vijana tuliokuwa tukikutana kwa Razaq . Yule kijana alipogundua Mary kafukuzwa shuleni kwa sababu ya ujauzito aliompatia , alitoroka Mwanza na kwenda jijini Dar es Salaam ambapo hakupatikana kabisa. Kitendo cha Mary kupewa ujauzito kilinipa funzo kubwa sana na kujipongeza kwa kuwa na msimamo kuhusu kumkwepa Razaq ambaye nilijua lengo lake halikuwa zuri . Baada ya kufunga shule , nilirudi nyumbani tulikokutana na mpenzi wangu ambaye naye alikuja likizo, kila mmoja alifurahi kumuona mwenzake japo tulikuwa na muda mchache tulikuwa tukikutana mara kwa mara kwa ajili ya kupeana penzi . Kadiri siku zilivyosonga mbele na jinsi mpenzi wangu alivyokuwa akinifanyia utundu tunapokuwa faragha, nilitokea kumpenda mara dufu na kuapa nisingemsaliti . Tulifurahia penzi letu hadi muda wa kurudi shuleni ulipowadia , nakumbuka siku moja kabla ya kuondoka tulikutana kwenye nyumba moja ya kulala wageni . Siku hiyo ndiyo nilijua utamu wa mapenzi , yaani mpenzi wangu alinifanyia mambo mazuri ambayo yalinipa burudani ya aina yake, nikaapa nisingejihusisha na mwanaume mwingine. Usiku wa siku hiyo , kabla ya kulala baba na mama walituketisha na kaka yangu wakatuasa sana kuhusu kusoma na kuachana na masuala ya mapenzi na mambo mengine yasiyofaa .



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baba alisema zaidi niliyetakiwa kuwa makini ni mimi kwa sababu nilikuwa mwanamke niliyekutana na changamoto za wanaume, akasisitiza niwe makini na kwamba ikitokea nimepewa ujauzito nisirudi nyumbani kwake. Mama naye alinisisitiza sana kuhusu jambo hilo, maneno yao yalinichoma kwa sababu muda mfupi uliopita nilikuwa sehemu na mpenzi wangu tunafanya mambo waliyonikataza . Niliwashukuru baba na mama kwa kuniambia hivyo , mama alifanya maombi tukaenda kulala na kesho yake asubuhi nilielekea shuleni Mwanza . Kama kawaida niliendelea kuchati kwa meseji na kupigiana simu na mpenzi wangu kwa siri ambapo nilimwambia kila kitu walichonieleza baba na mama. Mpenzi wangu ambaye alikuwa akipenda sana utani, aliniambia kilichotakiwa ni umakini japo na wao enzi zao walijirusha hivyo lazima wawe wakali, tukacheka. Tuliendelea na masomo huku nikikwepa kwenda mjini kila Jumapili na akina Zainabu hadi tulipofanya mitihani ya kumaliza muhula wa kwanza , matokeo yalipotoka nilikuwa kwenye kumi bora ya waliofanya vizuri. Tulipofunga shule na kurudi nyumbani, baba , mama na shangazi zangu walinipongeza kwa kufanya vizuri nikashukuru, tangu siku hiyo wakawa na imani nami kwamba sikuwa mtukutu kumbe tayari nilianza mapenzi . Wakati huo wa likizo, mpenzi wangu naye alirudi nyumbani baada ya kufunga shule , kila nilipopata nafasi nilikuwa nikimpitia rafiki yangu kipenzi ambaye sitapenda kumtaja jina kwenda kukutana na mpenzi wangu. Kwa kuwa wote tulikuwa tunakaa eneo moja, mpenzi wangu alimfahamu vizuri rafiki yangu huyo aliyekuwa akisoma Arusha , kwa ujumla nilifurahia sana penzi lake tamu . Siku moja mama alinituma niende sokoni kununua mahitaji , kwa kuwa mpenzi wangu muda mwingi alikuwa akishinda kwenye chumba cha rafiki yake aliyekuwa anasafiri kikazi mara kwa mara , niliamua kwenda kwa kumsapraizi . Baada ya kununua mboga na vitu vingine nilishika njia kuelekea kwenye chumba cha rafiki yake mpenzi wangu ambacho tulikuwa tukikitumia kupeana malavidave . Nilipofika nilikuta mlango ukiwa umerudishiwa na kafungulia muziki kwa sauti ya juu , bila kubisha hodi niliingia na kumkuta akiwa na rafiki yangu kipenzi wakiwa kama walivyozaliwa wamelaliana. Kufuatia kitendo hicho moyo ulipiga paa , wakati huo nao waliacha walichokuwa wakifanya wakabaki wamenitumbulia macho, nakumbuka niliwaita kwa majina yao na kusema asante nikaanza kulia. Kwa hasira nilizokuwanazo, nilitoka mle ndani kama vile nilikuwa naota ndoto , nikashika njia kurudi nyumbani huku nikilia , kuhofia mama angeniuliza chanzo cha kulia kwangu nilijifuta machozi . Hata hivyo , haikusaidia kwani aligundua kwamba sikuwa katika hali ya kawaida kufuatia macho kuwa mekundu na nilivyokuwa nimepoteza uchangamfu . Nilimwambia nilikuwa nina tatizo ambalo ningemwambia baadaye na kumuomba kwa muda ule aniache kwanza, nikaenda chumbani kwangu nikalala kifudifudi na kuendelea kulia . Nililia sana na kumshangaa sana mpenzi niliyekuwa nampenda na kujiepusha na vishawishi vya wanaume walionitaka kimapenzi kwa ajili yake kuamua kunisaliti tena na rafiki yangu . Pia niliumia zaidi kufuatia rafiki yangu wa karibu kuamua kutoka na mpenzi wangu , tukio hilo liliniumiza kupita maelezo nikaishia kulia tu mle chumbani. Baada ya mama kuona nimetumia muda mwingi mle chumbani bila kutoka , alipata wasiwasi akanifuata lakini alikuta nimefunga mlango kwa ndani. Mama alinigongea na kuniambia nimfungulie, kabla sijafanya hivyo nilijifuta machozi kisha nikaenda kufungua, alipigwa butwaa kuona macho yakiwa yamenivimba na kuwa mekundu. Aliniuliza nilikuwa nasumbuliwa na nini, nikaishia kutikisa kichwa kama ishara ya kumkatalia kwamba sikusumbuliwa na chochote. Mama aliniambia kwa ukali nimweleze tatizo langu lakini nikakaa kimya ndipo aliniomba tuketi kitandani , kwa upole aliniomba nimweleze jambo lililonitatiza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    K wa kuwa mama alikuwa akinipenda, nilitaka kuweka wazi kila kitu lakini sauti moja ilinionya nisifanye hivyo kwani angemfahamisha baba halafu ingekuwa balaa . Kumtoa wasiwasi nilimwambia sikuwa na tatizo kubwa na kumuomba kama hakujali akaendelee na alichokuwa akikifanya , akasema asingetoka mpaka nimwambie jambo lililonifanya nilie mpaka kuvimba macho hata kama lilikuwa dogo . Kauli ya mama iliniweka katika wakati mgumu, ni kweli nilitamani kumweleza lakini nilihofia kama angemwambia baba pale nyumbani pangechimbika ukizingatia mara kwa mara alikuwa akinionya kuhusu masuala ya wanaume. “ Wewe una mimba nini?” Happy anasema mama yake alimwuliza kwa kumshtukiza . Kufuatia swali hilo, nilimwambia sikuwa na mimba ndipo aliniuliza au nilikuwa nimebakwa , nikamwambia hapana . Mama alipoona sitaki kumwambia kilichonifanya nilie na kukosa raha , alisimama na kuniambia baba atakapofika angemwambia ili aje aniulize nilikuwa ninatatizo gani , akaushika mlango kwa lengo la kuufungua ili atoke . Baada ya kugundua ambacho kingetokea kama angemwambia baba , nilimuomba asitoke mle chumbani ili nimwambie tatizo langu, niliamua kuweka wazi kwanza ikiwa njia ya kupunguza hasira , pili kuona angenisaidiaje. Nilijua angenisema sana lakini baadaye yangeisha, akiwa amekaa karibu yangu nilimuomba msamaha kwa ambacho ningemweleza, akasema nisiwe na hofu nimwambie. Nilimsimulia kisa kilichonipata, nilipomaliza alikunja sura na kuniuliza kwa hasira : “ Wewe umeanza mambo ya mapenzi ?” Kufuatia swali hilo nilijilaumu sana kumweleza, nikabaki ninamwangalia ndipo aliniuliza tena nilikuwa nimeanza mapenzi ? Kutokana na jinsi alivyokuwa, nilimuomba msamaha kwa kitendo nilichokifanya , akawa ananiangalia ndipo nikaanza kutiririkwa machozi . Mama aliniambia nimuondelee ujinga na kuhoji kwani sikuwasikia kufuatia kunionya sana kutojihusisha na masuala ya mapenzi , akasema jambo hilo lazima angelifikisha kwa baba . Mama aliponieleza hivyo aliniumiza sana, nilitoka pale kitandani na kwenda kujiangusha mbele yake na kuishika miguu na kumsihi anisamehe asithubutu kumwambia baba . Nilimwambia mama kilichonifanya niingie kwenye mapenzi zilikuwa hisia ukizingatia tayari nilikuwa nimevunja ungo na kwamba nilipanga kuwa na kijana huyo tu! Mama ambaye alikuwa akinipenda aliniinua, nilipomwangalia machoni naye alikuwa akitiririkwa machozi , akaniambia amenisamehe na kuongeza asingemwambia baba . Kauli ya mama kwa kiasi kikubwa ilinipunguzia maumivu ya kusalitiwa na mtu watu wangu wa karibu, nilimshukuru mama kwa kunielewa ndipo alinionya niache mambo ya mapenzi mpaka nitakapomaliza masomo na kuolewa . Nilimshukuru mama lakini nilimwambia kitendo cha kusalitiwa na mpenzi wangu kiliniumiza sana , akasema nijitahidi kukisahau na kuacha kuwasiliana naye . Mama aliyekuwa ameandaa chakula aliniambia niende nikaoge kisha nikale na kuahidi kuzungumza nami zaidi siku iliyofuata, nikamwambia sawa . Baada ya mama kuondoka , nilienda kuoga lakini nilipokumbuka tukio la kusalitiwa ambalo liliniumiza sana nilishindwa kuzuia machozi kunitoka . Nilipotoka bafuni nilikwenda chumbani kwangu ambapo nilibadili nguo na kuelekea sebuleni kujiunga na wenzangu kupata mlo . Kutokana na hali niliyokuwanayo, kaka yangu na mdogo wangu Dora waliniuliza kama nilikuwa mgonjwa na kuhoji sababu ya macho kunivimba , nikawadanganya nilikuwa naumwa. Kwa kuwa hawakujua kilichonisibu, walinipa pole na kumwambia mama anipeleke hospitali , mama akasema alinipatia dawa . Baada ya mama kuwaambia hivyo , alikwenda jikoni ambapo alipakuwa chakula na kukiandaa mezani na kutuita twende tukale . Ingawa nilikuwa mlaji mzuri wa chakula , nilipakua kiasi lakini kila nilipojaribu kula chakula kilikuwa hakipiti nikaamua kuacha ndipo kaka, Dora na mama wakaniambia nijilazimishe . Hata hivyo , nilishindwa nikainuka na kwenda chumbani kwangu ambapo nililala kifudifudi huku kichwa nimekilaza juu ya mto nikaanza kulia. Kitendo cha kumfuma mpenzi wangu na rafiki yangu kiliniumiza sana . Tangu siku hiyo kichwa changu kikiwa kimevurugika , nikapata tatizo la kuumwa moyo pamoja na kichwa sababu ya kuwaza sana, baba ambaye hakujua kilichonisibu alinipeleka hospitali kadhaa lakini sikupata nafuu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog