Search This Blog

PENZI LANGU - 1

 

    .



    IMEANDIKWA NA : SHIWAWA BINSALAAN AL JABRY



    *********************************************************************************



    Simulizi : Penzi Langu

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Kabla sijaanza kuwasimulia kisa changu, napenda kuwaambia watu ambao kwa namna moja ama nyingine huwa hawaamini kama majini wapo na wanaishi katika jamii yetu kwamba viumbe hao wapo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Nasema hivyo kwa sababu hapo awali nilikuwa nasikia tu watu wakisema majini walikuwepo na wakimpenda mtu huweza kumfanyia mambo mazuri kama kumpa utajiri, nk, wakimchukia huweza kumtesa kwa maradhi au kwa shida mbalimbali na kumpoteza juu ya uso wa dunia.

    Katika shule niliyokuwa nasoma jijini Mwanza, alikuwepo rafiki yangu kutoka Kigoma aliyekuwa na jini ambaye alikuwa akimuongoza kwa mambo mbalimbali.

    Nakumbuka siku niliyoona muujiza wa jini huyo, mimi, msichana huyo na wasichana wengine wawili tulikwenda kutembea sehemu moja maarufu sana jijini Mwanza inayoitwa Salma Cone.



    Baada ya kuburudika kwa vinywaji na chakula, tulitoka na kuanza kurudi shuleni lakini tulipofika kwenye makutano ya Barabara ya Posta na Nyerere ghafla mbele yetu alitokea dada mmoja mrefu sana wa Kiarabu macho yake yalikuwa yakizunguka kama gololi na alivaa baibui lililofunika kabisa miguu yake.



    Jambo la kushangaza mimi na wale wasichana wengine tulishtuka isipokuwa yule rafiki yetu wa Kigoma ambaye alitabasamu na kutuambia tusiogope kwani alifuatwa na rafiki yake.



    Yule dada wa Kiarabu alimsalimia rafiki yetu na kumuuliza alitoka wapi akamwambia tulitokea Salma Cone, yule jini akatusalimia kisha alituambia alifurahishwa na urafiki wetu.

    Aliongeza kwamba wakati anatoka kwao kama angejua angekutana nasi angetuletea zawadi lakini kwa wakati ule hakuwa na zawadi yoyote.



    Dada huyo, alitusihi tuishi kwa upendo na kutuahidi kutuletea zawadi siku nyingine kisha alituaga lakini kitendo cha kutoweka ghafla mbele yetu kilitushtua sana!



    Rafiki yetu alituwahi kwa kutuambia tusiogope kwani yule Mwarabu alikuwa jini wake aliyeanza kuwa naye tangu akiwa binti mdogo, akatuomba tusimwambie mtu siri hiyo.



    Alituambia kwamba akiwa darasa la pili ndipo jini huyo alijitokeza wakati anaumwa na kumwambia alimpenda na kwamba atakuwa naye katika maisha yake yote akimwezesha kwa kila jambo.



    Nilipomuuliza kwa nini hakumkataa alituambia, jini huyo hakuwa mbaya ni wa ukoo wao na kwamba baada ya bibi yake aliyekuwa akimmiliki kufariki dunia ndipo alihamia kwake kwa sababu alikuwa akipendwa sana na marehemu bibi yake.



    Tangu siku hiyo ndipo niliamini majini walikuwepo na walikuwa wakiishi na watu bila kujua kama nami siku moja ningekuja kufundishwa mambo mengi na jini wa mpenzi wangu ambaye alikuja kututenganisha.



    Kwa kuwa nimeamua kuelezea kisa cha jini huyo aitwaye Mariamu, naanza kwa kuelezea historia ya maisha yangu hadi nilipofahamiana na mpenzi wangu aliyekuwa akiishi na jini na kuja kugundua baadaye sana.

    Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 25 ninayetokea mkoani Mara, familia yetu ina watoto wanne, wawili wa kiume na tuliobaki ni wa kike.



    Kutokana na malezi tuliyolelewa, nilikaa muda mrefu kabla ya kuanza uhusiano wa kimapenzi kama wanavyofanya baadhi ya wasichana kwani nilikuwa nahofia sana kupoteza usichana wangu.

    Hata hivyo, hisia za mapenzi hazina kizuizi kwani nikiwa darasa la sita katika Shule ya Msingi Mukendo tukatokea kupendana na kijana mmoja tuliyekuwa tukisoma pamoja ila yeye alikuwa mbele yangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliendelea kuwa karibu na kijana huyo bila kufanya mapenzi hadi nilipohitimu darasa la saba na kufaulu kujiunga na sekondari ya serikali, wakati huo yule kijana alikuwa amehamia Dar es Salaam kwa ajili ya masomo ya sekondari.

    Licha ya kufaulu, sikujiunga na sekondari ya serikali badala yake nilikwenda kujiunga na shule moja ya binafsi iliyopo jijini Mwanza.



    Nikiwa huko tulikuwa tunawasiliana na mpenzi wangu, shule zilipofungwa tulirudi nyumbani Musoma kwa ajili ya likizo ambapo tulikutana na kufurahi.

    Licha ya mara kwa mara kijana huyo kunishawishi tufanye mapenzi, nilimkatalia kwani niliogopa kufanya kitendo hicho kuhofia kupoteza usichana wangu.



    Nakumbuka siku moja aliniomba twende tukatembee mjini kwa ajili ya kupata vinywaji na chakula, kwa kuwa nilijiamini sana nilikubali bila kujua lengo lake lilikuwa nini.

    Kwa kuwa kutoka nyumbani bila sababu ilikuwa kazi, nilimdanganya mama kwamba nakwenda kwa mjomba wangu aliyekuwa askari polisi aliyeishi kwenye kota za polisi, akakubali.



    Kutoshtukiwa, tulipokutana na mpenzi wangu sehemu tuliyokubaliana nilimwambia lazima kwanza niende kwa mjomba na baada ya kuonekana nitaaga ndipo twende mjini.

    Mpenzi wangu alifurahi sana, tuliongozana hadi karibu na kota za polisi za Mabatini akakaa sehemu kunisubiri, nikaenda kwa mjomba ambapo niliwasalimia.



    Kwa kuwa nilikuwa nina safari yangu, nilipofika kwa mjomba moyo wangu ulikuwa juujuu kwani nilikuwa naona nachelewa kwenda mjini na laazizi wangu.



    Tulizungumza mawawili matatu na mke wa mjomba nikamwambia sikuwa mkaaji sana, kwa kuwa haikuwa kawaida yangu kufika na kuondoka aliniuliza mbona niliondoka mapema nikamwambia naenda kuchukua vitabu kwa rafiki.

    “Hapo sawa, soma shangazi yangu maana maisha ya leo bila kusoma huwezi kufanya chochote halafu kuwa mwangalifu na wanaume, sawa shangazi yangu?” Happy anasema shangazi yake alimwambia.



    Nilimshukuru kwa ushauri wake na kumuahidi nisingefanya hivyo ambapo alifurahi na kuniambia nikikaribia kurudi shuleni niende nikachukue zawadi yangu, kisha nilimuaga.

    Nikiwa naelekea sehemu aliyokaa mpenzi wangu, nikawa nayatafakari maneno ya shangazi lakini nikajiambia moyoni kwamba hakuna mwanaume atakayeugusa mwili wangu mpaka nitakapoolewa.



    Nilifikiria hivyo bila kujua kama wanaume ni wajanja na wana mbinu za kila aina wanapomtaka msichana na ndivyo ilivyokuja kutokea kwangu.

    Nilipofika eneo alilokuwepo mpenzi wangu, tulitamani kukumbatiana na kupigana mabusu lakini tukashindwa sababu ya watu waliokuwepo, tukaishia kushikana mikono.



    Tukiwa katika hali hiyo, tuliongozana hadi kituo cha daladala tukapanda basi na kuelekea Mtaa wa Uhuru, tulipoteremka tulikwenda kukaa kwenye baa ambayo ilikuwa na gesti.

    Siku hiyo mpenzi wangu alikuwa na furaha mpaka nikamuuliza kulikoni alikuwa vile, akaniambia ni kwa sababu tulikuwa pamoja halafu tulipendeza sana.



    Hakusema uongo, siku hiyo tulikuwa tumependeza kwa sababu yeye alivaa suruali ya jinzi, fulana nyeupe na jaketi jepesi la jinzi na viatu vyeusi na miwani, nami nilivaa sketi ya jinzi iliyoishia chini ya mapaja na kuzifanya hipsi zangu kuonekana kimtindo, fulana nyekundu na sendozi nyeusi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa ujumla tulipendeza na kila aliyetuona alikuwa akituangalia, tukiwa tunaendelea kupata vinywaji, mpenzi wangu aliniambia siku hiyo alitaka kunisapraizi lakini kitendo hicho kilihitaji tuwe sehemu ya faragha.

    Nilipomuuliza ni sapraizi ya aina gani, akaniambia nitaiona tukiwa sehemu ya peke yetu. Alipotoa kauli hiyo, nilitazama upande wa kushoto nikamwambia tuhamie sehemu ile ambayo haikuwa na mtu na ilitulia kwa ajili ya sapraizi aliyoniambia.



    Mpenzi wangu alicheka na kuniambia eneo alilolizungumzia ni zaidi ya sehemu niliyomuonesha, yaani alimaanisha chumbani.

    “Chumbani?” nilimuuliza.

    Kwa jinsi nilivyomuuliza kwa kuhamaki alinijibu ndiyo, nikamwambia isingewezekana kufanya hivyo kwa sababu muda ulikuwa bado, akacheka.



    “Muda gani kwani unajua mimi nataka kufanya nini?” mpenzi wangu aliniuliza.

    “Najua unataka tukafanye mapenzi!” nilimwambia.

    Kufuatia kutoa kauli hiyo, mpenzi wangu huyo kama kawaida yake ya kupenda kucheka, alicheka na kuniambia mawazo yangu niliyapeleka mbali sana kwani hakuhitaji kabisa kufanya kitendo hicho.



    “Mh! Kama huhitaji kitendo hicho sasa kwa nini twende chumbani kwani ni sapraizi gani unayotaka kunifanyia?” nilimuuliza.

    “Happy mpenzi wangu, wewe niamini kwamba sihitaji kufanya mapenzi na wewe...wewe twende tu ndani utaenda kuona hukohuko!” Happy anasema mpenzi wake alimwambia kwa sauti nyororo ya kubembeleza.



    Licha ya kuniambia hivyo, moyo wangu ulikuwa mzito lakini baadaye nikaamua kumpa sharti kwamba tukiingia chumbani asithubutu kunishika sehemu yoyote ya mwili wangu na akishanifanyia hiyo sapraizi yake tutoke mle chumbani.

    Nilipomweleza hivyo, alinishukuru kwa kukubali ombi lake na kusisitiza kwamba tukiingia chumbani suala la mapenzi halitakuwepo ndipo alinyanyuka na kuelekea upande wa gesti.



    Dakika kama tano hivi, alikuja kijana mmoja aliyekuwa mhudumu wa ile gesti akaniambia mpenzi wangu alimwambia anifuate, yule mhudumu akabeba vinywaji vyetu na kuniongoza lakini kabla hatujafika alinitania kwa kusema;

    “Naona leo unaenda kuchangamsha damu na mwenzako?”



    Kwa kuwa sikuwa na mpango huo , maneno ya

    yule kaka yalinikera sana nikamwambia

    kuingia chumbani hakukumainisha tunakwenda

    kufanya mapenzi na nikamuonya aache

    kuchunguza mambo ya watu .

    Yule mhudumu aliniambia alikuwa akinitania tu

    na kama sikupenda nimsamehe , sikumjibu na

    wakati huo tulikuwa tumefika kwenye mlango

    wa chumba alichokuwemo mpenzi wangu .

    Tulipofika mhudumu alibisha hodi ,

    alipokaribishwa tuliingia akaweka vinywaji

    kwenye meza na kutuuliza kama tulihitaji

    huduma nyingine , mpenzi wangu akamwambia

    hatukuhitaji .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tukiwa mle chumbani sikukaa kitandani

    alipokuwa amekaa mpenzi wangu bali nilikaa

    kwenye kochi dogo , ingawa tulipokuwa nje

    tulikuwa tunazungumza lakini kwa dakika

    kadhaa kila mmoja alikaa kimya .

    Binafsi nilikuwa nasubiri kuona sapraizi

    ambayo mpenzi wangu aliniambia alihitaji

    kunifanyia tukiwa sehemu ya peke yetu lakini

    upande mwingine mapigo ya moyo yalinienda

    kasi kuhofia kufanya mapenzi bila kupenda .

    Nilipojiwa na mawazo hayo nilijilaumu kwa

    nini nilikubali kuingia mle chumbani kwani

    hata kama mpenzi wangu angeamua

    kunilazimisha tufanye mapenzi ningeonekana

    niliafikiana naye.

    Wakati natafakari hivyo , mpenzi wangu

    alinishtua kwa kuniuliza nilikuwa nawaza nini

    nikajibalaguza kwa kumwambia sikuwaza

    chochote.

    Kufuatia kumweleza hivyo , alinipinga na

    kusema baada ya kuingia mle chumbani

    nilibadilika ghafla kisha aliniuliza kama

    sikupenda kuingia mle ndani.

    Kwa sababu ya kumpenda sana sikutaka

    kumkwaza, nilimwambia nilikuwa kawaida,

    akaniambia kama nilikuwa kawaida nisimame

    pale kwenye kochi nimfuate kitandani

    alipokuwa amekaa.

    Alipotoa kauli hiyo moyo ulipiga pa nilijua

    siku hiyo ndiyo usichana wangu ulifikia

    mwisho. . . yaani ndiyo siku ningekutana kwa

    mara ya kwanza na mwanaume .

    Wakati nawaza hivyo , mpenzi wangu aliniita

    kwa sauti ya utulivu wa hali ya juu, nilipoitika

    akaniomba niinuke pale kwenye kiti na

    kumfuata kitandani alipokuwa amekaa.

    Nikiwa namwangalia na kufikiria ni namna gani

    nitafanya ili nisifanyenaye mapenzi , aliinuka

    akanifuata pale kwenye kiti kisha akanishika

    mikono na kuniinua tukawa tumesimama

    tunatazamana .

    Tukiwa katika hali hiyo , alinikonyeza nikajikuta

    nacheka mwenyewe naye akaporomosha

    tabasamu zito ambalo kwa mara ya kwanza

    nililiona siku ile .

    Kitendo hicho kiliyafanya mapigo ya moyo

    wangu yaende kasi nikawa namtazama mpenzi

    wangu, ambaye aliniomba tukae kitandani

    nikamwambia asubiri kwanza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa kuhisi kwamba siku hiyo sikuwa na

    ujanja lazima angemla ‘ kuku ’ wangu

    alikubaliana nami, aliponiachia nikarudi kuketi

    kwenye kiti yeye akakaa pale kitandani .

    Nikiwa kwenye kiti , nilimuuliza kuhusu sapraizi

    aliyotaka kunifanyia akaniambia nihamie pale

    kitandani ndipo atanionyesha, nikabisha na

    kumuomba anifanyie pale kwenye kiti

    vinginevyo ningeondoka.

    Baada ya kumwambia hivyo , aliniinuka na

    akavua shati na kuniambia alihisi joto

    akalitundika juu ya enga iliyokuwa kwenye

    mlango kisha akanifuata pale kwenye kiti

    akachuchumaa mbele yangu .

    “ Mpenzi wangu unapokaa hapa kwenye kiti

    nitashindwa kukufanyia sapraizi

    niliyokuandalia kwa kuanzia hebu fumba

    macho nikikwambia fumbua fanya hivyo . . . haya

    fumba!” mpenzi wangu aliniambia.

    Nilifumba macho kama alivyoniambia hadi

    aliponiambia nifumbue ambapo nilikuta akiwa

    kavua suruali yake na kubaki na nguo ya

    ndani iliyokuwa na michirizi, nilishtuka na

    kuhoji ndiyo sapraizi aliyotaka kuniambia !

    Mpenzi wangu alitabasamu na kuniambia

    aliamua kunisaparaizi kwa kunivulia nguo kwa

    sababu alikuwa akinipenda na lengo lake

    alitaka nimuone akiwa vile .

    Aliniomba nami kama sitajali nivue ili kila

    mmoja ayajue maumbo ya ndani ya

    mwenzake, moja kwa moja nikabaini alikuwa

    akitaka tufanye mapenzi , nikakataa .

    Baada ya kukataa alinibembeleza sana

    kwamba tusingefanya mapenzi bali alitaka

    tuonyeshane sehemu zetu za mwili za ndani,

    kuna wakati nikawa nataka kukubali lakini

    sauti nyingine ilinikataza nisithubutu .

    Mpenzi wangu alipobaini kwamba huenda

    angenikosa kufuatia msimamo wangu,

    alinifuata kama alivyofanya mwanzo akanishika

    mikono na kuniinua .

    Tukiwa tumesimama tunatazamana , nilitupia

    macho sehemu yake ya mbele nikaiona

    haikuwa na utulivu halafu mpenzi wangu

    alikuwa akihema nikajua kama ningemlegezea

    angemtafuna ‘ kuku ’ wangu .



    Kwa haraka nilimwambia mama alisisitiza niwahi kurudi nyumbani na muda ulikuwa umekwenda sana, mpenzi wangu alinibembeleza japo nivue nguo za juu akione kifua changu nikamwambia asubiri kidogo.

    Nilipomweleza hivyo, hakunielewa alinibembeleza sana lakini sikubadili msimamo wangu nikamwambia kwa kuwa tulikuwa tunapendana asijali kabla hatujarudi shuleni ningempatia penzi.

    “Hivi mpenzi wangu maneno yako yana ukweli?” kijana huyo aliniuliza.

    Kwa kuwa nilihofia sana kufanya kitendo hicho, nilimhakikishia kwamba asiwe na wasiwasi tungefanya hivyo siku yoyote lakini siyo siku ile.

    Kufuatia kumweleza hivyo, mpenzi wangu alikubaliana nami na kunieleza kuwa alinielewa lakini aliniomba kama sitajali basi anibusu tu shavuni na kunishika kidogo kifuani kwangu.

    Alipotoa kauli hiyo, nilimweleza asubiri siku tutakayokutana tena ambayo nitamuachia mwili wangu wote auchezee atakavyopenda, akatabasamu na kuniuliza;

    “Happy unamaanisha ulichosema?”

    Nilimhakikishia asiwe na wasiwasi na kwa kuwa nilikuwa nampenda, yeye ndiye atakayemla ‘kuku’ wangu kwa mara ya kwanza, akafurahi sana!

    Baada ya kumuweka sawa, alivaa kisha tulitoka mle chumbani tukiwa tumeongozana bila wasiwasi kwamba tulikuwa wanafunzi.

    Ukiwa unatoka upande wa gesti ilikuwa ni lazima upite kwenye sehemu ambayo watu hukaa kwa ajili ya kupata vinywaji ambapo tulikaa awali.

    Kwa kuwa hatukufanya mapenzi, wote hatukuwa na aibu tulipita eneo hilo huku watu wachache waliokuwepo pale wakituangalia, tukatoka na kuelekea kituo cha daladala.

    Njiani mpenzi wangu alinilaumu kwa kutompa nafasi ya kunishika kifua changu na maeneo mengine, nikamwambia asijali asubiri siku nyingine.

    Nilimweleza hivyo kwa kumdanganya kwani nilipanga kutoingia naye tena gesti kwani tayari nilijua lengo lake lilikuwa ni kutaka tufanye mapenzi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikutaka kufanya kitendo hicho wakati nikiwa shuleni kwa sababu nilikwisha washuhudia wasichana kadhaa waliopata mimba wakiwa shuleni jinsi walivyoharibikiwa maisha na yupo mmoja aliyeitwa Boke alifariki wakati wa kujifungua.

    Kila nilipokumbuka kifo cha Boke tuliyekuwa tunaishi mtaa mmoja niliogopa sana, hata wakati nakwenda kuanza shule Mwanza mama alinikalisha chini na kunionya nisithubutu kufanya mapenzi.

    Tulipofika kituo cha daladala tulipanda basi tukarudi nyumbani, tulipoteremka kijana huyo alinisindikiza na kuniambia kama usiku angepata nafasi angekuja mitaa ya nyumbani.

    Kwa kuwa mama alikuwa hapendi tutoke nje usiku nilimzuia asije tungeonana kesho yake, akasema atakuja tu hata asiponiona akiiona nyumba yetu atafurahi, nikacheka.

    Aliniambia nisimcheke alifanya vile kwa sababu alikuwa akinipenda, kuonesha nami nilimpenda nilimwambia aje lakini iwe kabla ya saa mbili angenikuta nje.

    Baada ya kumwambia vile alifurahi sana, akasema ikifika saa moja kasoro atafika, nilikubaliana naye huku moyoni nikiapa kwamba nisingefanyanaye mapenzi kabisa.

    Ukweli ni kwamba nilikuwa sijui kama wanaume walikuwa wajanja sana na washawishi, baada ya kumaliza kupika nilioga nikatoka ndani na kwenda kukaa kibarazani.

    Lengo la kufanya vile ni kutaka kuonana na mpenzi wangu ambaye licha ya kutopenda kutoka naye kimapenzi nilikuwa nampenda kwani alikuwa ni ‘handsome boy’ na alinipenda sana.

    Sikukaa sana nilimuona akija na baiskeli ndogo, aliponifikia alinisalimia nilipoitikia salamu yake tulikwenda kusimama mwisho wa ukuta wa nyumba yetu sehemu iliyokuwa na bustani.

    Yule kijana aliegesha baiskeli yake ukutani tukawa tunapiga stori kwa sauti ya chini ili waliondani wasitusikie, maongezi yaliponoga alinisogelea akanishika mkono na kuanza kuchezea kiganja changu.

    Wakati akifanya hivyo nikawa napata hisia fulani na kujisikia vizuri ndipo aliniomba tusogee tukasimame sehemu iliyokuwa na miti na maua mengi ili tusionekane.

    Ingawa mimi ni yuleyule niliyemkatalia tukiwa kule gesti, nilijikuta nakubali, tukasogea na kuzama kwenye maua marefu ambako hakukuwa na mwanga.

    Tukiwa pale yule kijana ambaye sitamsahau maishani mwangu alinivutia maungoni mwake na kuanza kunishika hapa na pale zaidi kifuani na kunipiga mabusu, nikahisi kuchanganyikiwa.

    Alipoona nimetulia, akafungua blauzi niliyovaa nami nikawa namkodolea macho yaani nikawa nipo tayari kwa lolote na kusahau onyo nililopewa na mama kuhusu kufanya mapenzi.

    Yule kijana alikivamia kifua changu ambacho kipindi hicho kilikuwa kibichi kabisa, ninaposema kibichi najua unaelewa namaanisha nini.

    Wakati anaendelea na alichokuwa akinifanyia mama akaniita, nikafunga vifungo fasta na kutoka mbio.

    Nilipofika kibarazani niliitikia wito wa mama ambaye aliniuliza nilikuwa nafanya nini nje wakati nilitakiwa kuandaa chakula, nikamwambia nilikuwa nimesimama tu kibarazani.

    Mama alinifokea na kuniambia niache ujinga kwani muda ule mtoto wa kike sikutakiwa kukaa nje hivyo niingie ndani nikaandae chakula kwani wadogo zangu walitaka kula.

    Wakati mama ananiita alikuwa amekaa sebuleni, nikahisi kama ningepita pale kwa jinsi nilivyokuwa nimebadilika usoni kufuatia kupagawaishwa na mpenzi wangu angegundua.

    Kuhofia kugundulika, nilizunguka nikapitia mlango wa jikoni na kuingia ndani ili niende chumbani kwangu kabla ya kuelekea jikoni kupakua chakula.

    Ile kuingia tu jikoni nilipotaka kuelekea kwenye korido la kuelekea vyumbani tukakutana na mama, akaniuliza nilitoka wapi mbona kichwani kulikuwa na maua, moyo ukapiga pa!

    Kukwepa maswali zaidi nilimwambia nilikuwa kwenye bustani ya maua, akanifokea sana na kunionya nisipende kwenda bustanini usiku na kunikumbusha tukio la kugongwa na nyoka mfanyakazi wetu wa kiume.

    Wakati nazungumza na mama nilikwepesha macho yasigongane na yake kwani kwa jinsi nilivyokuwa kwa mtu mzima kama yeye angehisi kitu flani.

    “Tena kesho mwambie John aende akamwambia mzee Bakari aje apunguze maua maana naona umekuwa msitu,” Happy anasema mama yake alimwambia.

    Baada ya kuniambia hivyo nilijua soo limekwisha, nilizuga kwa kwenda chumbani kwangu na kurudi jikoni nikawa napakua chakula huku nikimfikiria mpenzi.

    Nikawa nawaza mambo aliyokuwa akinifanyia hasa alipokuwa akinichezea kifua changu na alivyonibusu, mwili ukanisisimka na kutamani kama vile tungeendelea.

    Wakati nawaza hivyo, kuna sauti ilikuwa ikiniuliza nilikuwa nimefanya nini na kwa nini nilitaka kujiingiza kwenye mapenzi wakati bado nilikuwa nasoma!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kufuatia raha niliyoipata kwa muda mfupi, nilihisi nilikuwa naidhulumu nafsi yangu na kukumbuka rafiki zangu Mary, Zainabu, Rose walioanza kutoka na wanaume walivyokuwa wakinieleza kuhusu raha ya mapenzi.

    “Wewe Happy nawe utajifanya mdogo mpaka lini, asikudanganye mtu mapenzi matamu bwana, eti mama yako kakukataza wakati yeye anayafurahia!”

    Happy anasema alikumbuka siku moja aliambiwa maneno hayo na Rose aliyekubuhu kwa masuala ya mapenzi licha ya umri mdogo aliokuwanao.

    Nilipokumbuka kauli ya Rose, sauti moja iliniambia nami nianze lakini nyingine ilinikataza, basi nikawa navutana na mawazo huku nikiandaa chakula.

    Baada ya kuandaa, niliwaita wadogo zangu na kujumuika nao mezani tukawa tunakula lakini mawazo yangu yalikuwa kwa mpenzi wangu na kuwaza vile alivyonifanyia kule bustanini.

    “Kama mama asingeniita leo ningefanya mapenzi kwa mara ya kwanza tena bustanini maana tulikokuwa tukielekea ilikuwa balaa,” niliwaza.

    Wakati nawaza hivyo kumbe nilipozi kula ndipo mdogo wangu Caro akanishtua na kuniuliza nilikuwa nawaza nini, nikajibalaguza kwa kumwambia nilihisi chumvi ilikuwa kidogo kwenye mboga.

    Baada ya kutoa kauli hiyo, Caro alidakia na kusema ni kweli chumvi ilikuwa kidogo akainuka kuifuata ndipo niliendelea kula hadi nilipotosheka nikawaacha wadogo zangu wanamalizia.

    Nikiwa najifuta maji kwa taulo, nilisikia muungurumo wa gari la baba nikatoka kwenda kufungua geti. Alipoegesha aliniambia nifungue buti nichukue mizigo, nikafanya hivyo.

    Baada ya kupeleka jikoni mkungu wa ndizi, nyanya na vitu vingine niliingia sebuleni ambako nilimshukuru baba kwa vitu alivyonunua akasema asante ndipo nilitaka kuelekea chumbani kwangu, akaniita.

    Nikiwa nimeketi baba aliniambia kuna jambo alitaka kuzungumza nami tatizo alikuwa bize na kazi na kuniambia kabla ya kulala tuonane, nikamwambia sawa.

    Kama alivyopanga baada ya kumaliza kula, baba alimwita mama pamoja nami tukakaa lakini kabla ya kuanza mazungumzo aliwauliza wadogo zangu kama walikuwa wanajisomea!

    Kwa kuwa muda mwingi walipenda kuangalia

    runinga, walisita kujibu ndipo aliwajia juu na

    kuwaambia kuanzia siku ile akirejea kutoka

    kazini na kumkuta mtu yupo kwenye runinga

    atakula viboko .

    Alipowaeleza hivyo , aliwaamuru waende

    wakalale tukabaki mimi, baba na mama ndipo

    akaniuliza nilikuwa ninaendeleaje na

    masomo !



    Tukiwa sebuleni baba aliniuliza niliendeleaje na masomo yangu, nikamjibu kwamba niliendelea vizuri.

    Baada ya kumpa jibu hilo, alikaa sawa na kuniuliza kama nilikuwa namfahamu binti wa rafiki yake mmoja aliyekuwa akifanya kazi TRA aliyeitwa Joyce.



    Kwa kuwa najua alikuwa anajua namfahamu nikahisi kulikuwa na kitu nikamuuliza; “Si yule anayesoma Uganda?”

    “Kumbe unamfahamu, ni huyo huyo!” Baba alinijibu huku akiniangalia kwa makini.

    Baba aliniambia kwamba Joyce alisababisha baba yake kulazwa hospitali kufuatia kupata presha alipoambiwa alikuwa na mimba na alikuwa Kenya kwa kijana aliyempa ujauzito.

    Baba alipotoa kauli hiyo, alibadilika na kuanza kuzungumza kwa ukali na kuniambia kanipeleka shuleni hataki ujinga wa aina yoyote na siku nikipata mimba nisirudi nyumbani kwake.

    “Nimeamua kuzungumza nawe mbele ya mama yako ili anisaidie kuzungumza na wewe, siku ukibeba mimba naye ajiandae kuondoka na wewe... kwa suala hilo sitakuwa na msamaha kwa yeyote,” baba aliniambia.

    Baba ambaye siku hiyo alinipania sana, aliendelea kuniambia kwamba alikuwa akijinyima ili mimi na wadogo zangu tusome tuje tuwasaidie baadaye hivyo asingependa kusikia nimefanya uzembe wowote kwenye masomo.

    Aliongeza kuwa, heri kama nitakuwa nina shida yoyote niwafahamishe kuliko kurubuniwa na wanaume ambao wakishawapatia mimba wasichana huwatelekeza na jukumu hilo hubaki kwa wazazi wao.

    Baada ya baba kuzungumza mengi, aliniita na kuniuliza kama nilimuelewa nikamwambia nilimuelewa ndipo alimpa nafasi mama ya kuzungumza nami.

    Mama naye aliniasa kama alivyosema baba yangu na kusisitiza kwamba alikuwa akijinyima sana ili ahakikishe tunasoma ndipo aliniuliza kama nilikuwa najua baba alikuwa na jozi ngapi za viatu, nikashindwa kumjibu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Na suruali unajua anazo ngapi?” mama akaniuliza tena.

    “Sijui!” nilimjibu.

    Baada ya kumjibu hivyo, mama aliniambia kwamba baba yetu alikuwa na jozi moja ya viatu na suruali nne pamoja na mashati sita na kuongeza kuwa siyo kwamba alikuwa anapenda kuwa na nguo chache namna ile isipokuwa alitaka tusome.

    Mama alipotoa kauli hiyo, baba alirudia kuniambia kwamba nizingatie alichoniambia ili siku nikibeba mimba nisije kumlaumu pia alisema kama nitafaulu atanipatia zawadi nzuri sana.

    Alipotoa kauli hiyo aliinuka na kuelekea chumbani kwake na kutuacha na mama, mama alirudia kunisisitiza nisijihusishe na masuala ya mapenzi na kusisitiza sana nizingatie onyo la baba.

    Nilimwambia mama sitajihusisha na mapenzi kama walivyonionya, akafurahi na kuniambia alitegemea nisingemuangusha ndipo aliniacha nikiangalia runinga, akaenda kulala.

    Nikiwa pale sebuleni nikawa natafakari maneno niliyoambiwa na wazazi wangu pamoja na raha niliyoipata wakati mpenzi wangu alipokuwa akinishika hapa na pale hususan maziwa yangu.

    “Walichoniambia baba na mama ni jambo zuri lakini hata mapenzi nayo ni matamu yaani kama kushikwa tu nilipata raha ile, je nikifanya kabisa si ndiyo itakuwa balaa...ndiyo maana wenzangu wananicheka!” Nikawaza.

    Baada ya kuangalia runinga kama dakika 35 hivi niliizima nikaenda chumbani kwangu, nikiwa nimelala mawazo yote yakawa kwa mpenzi wangu, kwa kuwa nilikuwa na simu niliyonunuliwa na mjomba wangu baada ya kufaulu, nikafungua sehemu ya picha nikawa namuangalia mpenzi wangu.

    Sielewi ni kwa sababu nilikuwa mwanafunzi wa mapenzi, nilijikuta naibusu picha yake na kumwambia nilikuwa nampenda na kumuahidi kwamba siku tutakayokutana tena ningempa ‘kuku’ wangu awe wa kwanza kumla.

    Japo onyo la kutofanya mapenzi nililopewa na wazazi wangu lilikuwa likijirudia mara kwa mara kichwani, nililipuuza na kujisemea moyoni mbona rafiki zangu akina Rose, Zainabu na Mary walianza kufanya mapenzi muda mrefu lakini hawakupata mimba!

    “Nikirudi shuleni nitawauliza walikuwa wanafanyaje kujizuia kupata mimba ili nami nianze mapenzi kwani sikuona tofauti iliyokuwepo kati yao na yangu kama umri tulikuwa sawa,” niliwaza.

    Baada ya kuwaza nikaamua kumtumia ujumbe wa mapenzi mpenzi nikamueleza jinsi nilivyojisikia alipokuwa akinishika kifuani, nilipomtumia hakuchelewa kunijibu.

    “Kwa upande wangu mpaka muda huu nakuwaza wewe mpenzi wangu...yaani Happy una kifua kitamu sana, nilitamani kuendelea kuwa nawe sema mama yako katukatili!”

    Baada ya kusoma ujumbe huo, nilisisimkwa sana, nikamtumia ujumbe nikimfahamisha kwamba kabla ya kurudi shuleni lazima tukutane ili nimpe penzi tena nilimwambia siku hiyo iwe Jumamosi ambayo nilikuwa napata nafasi kufuatia baba na mama kwenda Sabato.

    Kufuatia hali ya mashamushamu niliyoipata siku ile pale bustanini, niliamua acha niiingie kwenye ulimwengu wa mapenzi bila kujua kama mapenzi yalikuwa na mateso makubwa!

    Nilipomtumia ujumbe huo mpenzi wangu, alifurahi sana na kuniambia angenitafutia zawadi nzuri kwa kuwa yeye angekuwa mwanaume wa kwanza kumla ‘kuku’ wangu.

    Kwa kuwa mdogo wangu Dora alipenda sana kupekua simu yangu, kabla sijalala nilifuta meseji zote zilizoingia na kutoka kisha nililala na kupitiwa na usingizi.

    Jambo la ajabu ni kwamba, siku hiyo niliota nipo hoteli na mpenzi wangu tunapeana raha ambayo nashindwa namna ya kuielezea, eti baada ya kutoka pale alinirudisha nyumbani kwetu ambapo alikutana na baba na mama waliompokea vizuri.

    Nikiwa katikati ya ndoto hiyo nilishtuka, nikajiuliza ilikuwa na maana gani, sikupata jibu nikaangalia saa ambayo ilionesha ilikuwa saa 9.30, nilikwenda msalani, kisha nikalala tena.

    Kulipokucha nilikuta baba amekwishaenda kazini, nilitoa vyombo vichafu kwenye karo nikaanza kuviosha huku wadogo zangu wakifanya usafi wa mazingira.

    Wakati naosha vyombo, mama alikuja kunijulia hali nami nikamuamkia ndipo aliniambia aliota ndoto kwamba nilipewa mimba na mwanafunzi mwenzangu, nikamwambia mama ndiyo ndoto gani hiyo!

    Mama aliniambia hata yeye alishangazwa na ndoto hiyo, akaongeza kwamba baada ya baba kugundua nilikuwa na ujauzito alitutimua na mama pale nyumbani tukaenda Shinyanga kwa mjomba.

    Kwa kweli mama aliponiambia kuhusu ndoto hiyo nilifedheheka kwani yote aliyonieleza baba yalijirudia kwenye ndoto, nikaogopa sana. Mama aliniambia niwe makini kwa sababu ndoto yake haikuwa nzuri!

    Baada ya kuzungumza na mama, aliingia ndani na kuniacha nikiendelea kuosha vyombo huku nikitafakari juu ya ndoto aliyoota mama na niliyoota nilikuwa hoteli na mpenzi wangu.

    Hata hivyo, nilikumbuka mwalimu wangu mmoja wa sayansi aliwahi kutuambia kwamba ndoto mara nyingi huwa ni marudio ya maongezi na vitendo vinavyofanywa mchana au kabla ya kulala na binadamu, nikatabasamu!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kweli kabisa ndoto yangu na ya mama ni marudio ya maongezi tuliyozungumza usiku na nilivyokuwa nawaza mchana siku ile tulipokwenda kule gesti mjini na mpenzi wangu,” nikajiambia.

    Baada ya hapo sikuwa na wasiwasi tena wala kufikiria kama ndoto niliyoota huenda ingekuja kuwa kweli baadaye, nilipomaliza kuosha vyombo niliwasha moto nikachoma chapati na kuandaa chai.

    Siku hiyo mawazo yangu yalikuwa juu ya mapenzi na nilitamani kama ingewezekana jioni tukutane tena pale bustanini na mpenzi wangu ili anifanyie kama jana yake.

    Baada ya kuoga, kunywa chai na kuosha vyombo, niliingia chumbani kwangu ambako nilijilaza kitandani nikaanza kuchati na mpenzi wangu mambo ya mapenzi.

    Tulichati hadi nikasisimka na kutamani kama angekuwa karibu yangu, kwa ujumla tangu siku ile mpenzi wangu aliponifanyia fujo zake pale bustanini nikawa nimechanganyikiwa kabisa.

    Niliacha kuchati baada ya mdogo wangu kunifuata na kuniambia mama alikuwa akiniita ili niende sokoni kununua mboga na vitu vingine, nikafuta meseji zote nikaenda kumsikiliza mama.

    Kufuatia kuwa chumbani kwangu muda mrefu wakati haikuwa kawaida yangu, mama aliniuliza kama nilikuwa naumwa nikamwambia nilikuwa najisomea, akaniomba samahani kwa kunikatisha kusoma.

    Nilimwambia asijali ningeendelea kusoma baada ya kutoka sokoni bila kujua kama nilimdanganya, alinipatia fedha na kunipa maelezo ya vitu nilivyotakiwa kwenda kuvinunua.

    Wakati nataka kuondoka kuelekea sokoni, mdogo wangu Dora ambae alikuwa akinipenda sana alitaka tuongozane lakini nilimzuia na kumwambia akanifulie nguo zangu.

    Dora alikubali bila kujua nilipanga kumtumia ujumbe mpenzi wangu ili tukutane sokoni japo nimuone tu, kama nilivyopanga nikiwa njiani nilimpigia simu mpenzi wangu na kumuomba kama anaweza aje sokoni.

    Kijana huyo aliniuliza anikute wapi, nikamwelekeza ambapo alisema nimpe dakika kumi tu angekuwa hapo kwa sababu muda ule alikuwa mbali kidogo.

    Nilipofika sokoni, nilinunua fasta vitu ambavyo nilielekezwa nikarejea sehemu ambayo nilimwelekeza mpenzi wangu angenikuta nikakaa ambapo sikumaliza dakika tatu aliwasili.

    Kwa kweli nilijisikia raha sana nikatamani kumkumbatia lakini nilihofia kuonwa na watu waliokuwa wakinifahamu ambao wangeenda kumwambia mama, tulisalimiana na mpenzi wangu akaniomba twende tukakae sehemu japo tuzungumze kidogo.

    Awali nilikataa kuhofia kuchelewa kurudi nyumbani lakini aliponibembeleza sana nikakubali ambapo tulikwenda mtaa wa nyuma ya soko kwa rafiki yake aliyekuwa amepanga chumba kimoja.

    Kwa kuwa rafiki yake huyo alikuwa amekwenda kazini na kumuachia funguo, alifungua tukaingia ndani akanikaribisha niketi kwenye sofa, mtoto wa kike bila kujali kama ningechelewa nyumbani nikajibwaga pwaaa!



    “Happy mpenzi wangu, mpaka muda huu bado nimejilaza kitandani nikitafakari ulivyojaliwa kuwa na kifua kizuri chenye vichuchulee bomba.”

    Baada ya kuusoma, nilivuta pumzi na kuufuta fasta ndipo mdogo wangu Dora akaniuliza mbona nilivuta pumzi na kuzishuka kama mtu aliyepatwa na jambo fulani.

    Kufuatia swali hilo nilimwambia kulikuwa na jambo ambalo hakupaswa kulijua lakini aling’ang’ania nimwambie, nikamfokea na kumwambia asiingilie mambo ya wakubwa akanyamaza.

    Baada ya kumwambia hivyo, Dora aliondoka na kwenda nje ndipo niliinuka na kwenda kumuangalia mama alikuwa wapi ili niweze kuchati na mpenzi wangu bila hofu.

    Nikiwa kwenye mlango wa uani, nilimsikia mama akizungumza na jirani yetu mama Jesca kuhusu msiba wa bibi mmoja wa mtaa wa pili aliyekuwa akiugua kwa muda mrefu.

    Mama na mama Jesca walipanga kwenda kumpa pole rafiki yao mama John aliyefiwa na mama yake, nilimsikia mama akimwambia mama Jesca kwamba amsubiri akachukue khanga ndipo nilirudi jikoni na kujifanya nipo bize na mapishi.

    Mama alikuja jikoni na kunipatia taarifa ya msiba wa bibi John nami nikajifanya kusikitika ndipo aliniambia wanakwenda kuwapa pole hivyo niendelee na zoezi la kupika, nikamwambia sawa.

    Mzazi wangu alipoondoka nilichukua simu na kuandika meseji isemayo; “D, hunifikii mimi, mwenzio mpaka muda huu mwili unaninyevua, sema mama katuharibia ila nitafanya kila njia jioni nije ili nikupe haki yako mpenzi wangu!”

    Baada ya kumtumia ujumbe huo naye akanitumia huu; “Kwa jinsi ninavyoteseka hapa nilipojilaza jioni naiona kama wiki nzima, hivi huwezi kufanya ujanja wowote uje mara moja hata kwa bodaboda Happy wangu?”

    Nilipousoma ujumbe huo nikakumbuka jinsi mpenzi wangu alivyokuwa akikitendea haki kifua changu chenye embe bolibo za ukweli na alivyokuwa akizishika hipsi na alivyokuwa akinibusu, nikawa hoi.

    “Hivi nikienda mara moja kutakuwa na ubaya gani, kwa nini najitesa namna hii...cha msingi ngoja niweke maji ya kutosha kwenye mboga kisha niende maana hapa nimeharibikiwa mtoto wa kike!” Nilijisemea moyoni.

    “D, nimeamua kuja cha msingi tusitumie muda mrefu kwani mama amekwenda msibani mtaa wa pili na anaweza kurudi muda wowote,” niliandika ujumbe huo nikamtumia.

    “Ndiyo maana nakumpenda Happy, wewe ni mwanamke unayejiamini nakusubiri kwa hamu mpenzi wangu na utanikuta nimelala chali naugulia maumivu ya mapenzi,” mpenzi wangu alinitumia ujumbe huu.

    Baada ya kuusoma, nilikwenda jikoni nikafunua sufuria na kukuta maji bado yalikuwa mengi, hata hivyo niliongeza na kumwita Dora ambapo nilimwambia nakwenda mara moja kwa rafiki yangu aitwaye Johari nilikuwa nina shida.

    Dora akaniambi nisichelewe kwa sababu mama aliniachia jukumu la kupika, nikamwambia sitachelewa na kumsisitiza awe makini kuangalia mboga isiungue, akasema sawa.

    Nilipompa maagizo hayo nilikwenda chumbani ambako nilibadili nguo yangu ya mwisho kabisa ambayo wakati huo haikufaa, kwa kuwa wewe msomaji wangu ni mtu mzima najua umenipata sawia ile nataka kutoka nikasikia mama anazungumza nje, moyo ukapiga pa!

    Siyo siri siku hiyo nilimchukia mama kwa kuniharibia ishu yangu, niliishia kusonya na kuketi kitandani huku nimeshika simu katika mkono wa kushoto.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa kuwa nilibaini kama nisingemtumia ujumbe mpenzi wangu wa kumfahamisha kwamba sitakwenda kufuatia mama kurudi ningeshindwa kufanya hivyo kwa wakati, niliandika ujumbe huu.

    “D, nasikitika kukuambia kwamba siwezi kufika kwani limama limerudi, pole mpenzi wangu lakini naahidi hazitapita siku mbili lazima tutakutana...nimeumia sana.” Nikamtumia.

    Kwa kuwa nilisahau kumwambia asijibu ujumbe huo nikaandika mwingine fasta na kumwambia aanze kuchati nami mara nitakapomuanza kwani mazingira yalikuwa tata.

    Nikiwa chumbani nilimsikia mama akimuuliza Dora nilikuwa wapi, mdogo wangu huyo akamwambia nilikwenda kwa akina Johari.

    Baada ya mama kuambiwa hivyo alianza kufoka na kuhoji kwa akina Johari kufanya nini wakati aliniachia kazi ya kupika, Dora akamwambia hakujua kilichonipeleka huko.

    “Huyu mtoto ananitafuta ubaya, kwanza kachelewa kutoka sokoni kwa madai aliporwa simu saa hizi tena kaacha kupika kaenda kwa akina Johari, leo atanitambua,” mama aliongea kwa hasira.

    BAADA ya kubaini kizaazaa ambacho kingeibuka, nilibadili nguo fasta nikajifunga kanga kwa mtindo wa kuikatisha kifuani juu nikavaa blauzi nikatoka chumbani, ile nafungua mlango wa jikoni nikakutana uso kwa uso na mama.

    Mama aliyekuwa akifoka aliponiona alipoa kidogo na kuniuliza nilikuwa wapi, nikamwambia chumbani akaniuliza mbona Dora alimwambia nilikwenda kwa akina Johari!

    Nilimfahamisha kwamba Johari alinipigia simu na kuniomba nikipata muda niende kwao alikuwa na shida na mimi, nafikiri Dora hakunielewa alidhani nilitaka kwenda muda ule.

    Baada ya kumweleza hivyo, mama alipoa na kuniambia nilikuwa nina bahati sana kama ningekwenda kwa akina Johari na kuacha kupika ningemtambua.

    Ingawa moyoni nilikuwa nina hasira kufuatia kuniharibia ishu ya kwenda kwa mpenzi wangu, upande mwingine nilishukuru aliporudi na kunikuta maana angenikosa lingekuwa bonge la msala.

    Kwa vyovyote vile angemwambia baba na balaa lake lingekuwa kubwa kwa sababu ni siku chache zilipita tangu aliponionya kuhusu mambo ya kipuuzi na kusisitiza nizingatie masomo.

    Baada ya kumaliza kuzungumza na mama, niliendelea kupika na baada ya kula nilikwenda kupumzika chumbani kwangu ambako nilifunga mlango kwa ndani ili mtu yeyote aliyetaka kuingia anigongee.

    Ukweli ni kwamba siku hiyo kichwani nilikuwa nikiwaza masuala ya mapenzi kufuatia msisimko nilioupata kila mpenzi wangu alipokuwa akinishika sehemu mbalimbali za mwili wangu.

    Nikiwa nimejilaza nilichukua simu na kumtumia meseji mpenzi wangu, ambapo nilimhakikishia kwamba zisingepita siku mbili lazima tungekutana ili tukate kiu ya mapenzi tuliyokuwanayo.

    Alipopata ujumbe huo aliniuliza nilikuwa wapi, nikamjibu nyumbani, akaniuliza nilikuwa nafanya nini nikamwambia nilijilaza kitandani chumbani kwangu.

    Mpenzi wangu aliniuliza mama alikuwa wapi, nikamwambia alikuwepo akasema alitaka kuniambia kitu lakini kwa kuwa mama alikuwepo haitasaidia, nilimuuliza kitu gani akasema alitaka niende pale kwenye chumba cha rafiki yake.

    “Kwa mazingira yaliyopo itakuwa vigumu, kwanza nitamwambia nakwenda wapi?” nilimtumia ujumbe huo.

    Nilipomtumia meseji hiyo nikakumbuka nilimfahamisha mama kuhusu Johari kunihitaji nyumbani kwao, nikajua hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya kumuaga.

    Baada ya kujua mama asingeweza kunizuia kwa sababu nilikwishapika mboga ya kula usiku, nilimwandikia ujumbe huu mpenzi wangu ambaye nilikuwa nimeamua kumzawadia ‘kuku’ wangu kabla sijarudi shuleni.

    “D, nilimdanganya mama kwamba Johari alinipigia simu ili niende kwao, ngoja nikamwambie nataka kwenda huko, akiniruhusu tu nakuja.”

    “Utakuwa umefanya vizuri sana d, ukifika nitakufanyia zaidi ya nilivyokufanyia asubuhi,” mpenzi wangu alinitumia ujumbe huo.

    Ujumbe wake ulinisisimua sana kwani ulinikumbusha jinsi alivyokuwa akikitendea haki kifua changu na alivyokuwa akinishika maeneo mengi yenye msisimko.

    Nilitoka chumbani kwangu na kwenda sebuleni nilikomkuta mama akinywa juisi nikamuomba ruhusa ya kwenda kwa akina Johari, kwa kuwa muda huo sikuwa na kazi aliniambia si nisubiri jua lipoe.

    Aliponieleza hivyo, nilimwambia nilitaka kwenda mapema kwa sababu nilihitaji kurudi mapema kwa ajili ya kuosha vyombo na kupika chakula cha usiku, mama hakuwa na kipingamizi akaniruhusu.

    Hata hivyo, aliniambia kwamba yeye anakwenda msibani na kusisitiza nisichelewe kurudi, nikamwambia sitachelewa.

    Baada ya kupewa ruhusa, nilikwenda chumbani kwangu, nikavaa sketi nyeusi iliyokuwa inanibana kimtindo na kufanya hipsi zangu zitokeze na blauzi nyekundu nikatoka kama naelekea kwa akina Johari.

    Nilipofika mtaa wa nyuma, nilimuona mwendesha bodaboda nikapanda na kumwelekeza nilikokuwa nakwenda akasema alikuwa anapafahamu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikuchukua muda mrefu tulifika kwenye nyumba aliyokuwa amepanga rafiki wa mpenzi wangu, nilikwenda moja kwa moja kwenye chumba husika na kubisha hodi.

    Mpenzi wangu alipofungua mlango na kuniona alinikumbatia kwa furaha kisha alinibeba juu na kwenda kunilaza kitandani akaanza kunipiga mabusu mfululizo na kusema hakuamini kama nilifika.

    Hakuishia hapo aliendelea kunishika kila sehemu tamu ya mwili wangu, akanivua nguo zote. Tangu nilipozaliwa sikuwahi kuvuliwa nguo na kubaki kama nilivyokuja duniani, mpenzi wangu akawa wa kwanza.

    Kufuatia mushawasha wa mapenzi nilioupata, sikufikiria kama kitendo hicho kilikuwa kibaya kufanywa na mwanafunzi na kwamba kingekuja kunigharimu baadaye na kujuta.

    Si unajua fisi mwenye njaa anapoukuta mzoga wa mnyama anavyoushambulia, mpenzi wangu aliendelea kunipagawisha kwani alicheza na kifua changu na maeneo mengine mpanga nikawa hoi.

    Alipoona mtoto wa kike nimekolea, hakuona sababu ya kuchelewa aliuondoa usichana wangu ambapo nilipata maumivu ambayo sitayasahau.

    Kufuatia maumivu niliyopata nililia sana ndipo mpenzi wangu akawa ananipa pole huku akinifanyia huduma ya kwanza, siku hiyo niliyachukia mapenzi kwa sababu sikuona raha badala yake ilikuwa karaha.

    Kwa kuwa muda ulikuwa umekwenda, mpenzi wangu alinitoa mle chumbani na kunisindikiza mpaka karibu na nyumbani, licha ya njiani kunisemesha na kunipa pole sikumjibu.

    Kwa kifupi nilimchukia na kujilaumu kwa kitendo nilichokifanya, kutokana na maumivu niliyopata nilipofika nyumbani nilikwenda chumbani kwangu, nikafunga mlango na kuanza kulia tena.

    Baada ya kugundua kilio changu kingemshitua Dora ambaye angetaka kujua nilipatwa na nini kisha kumwambia mama, nilinyamaza, nikaenda kuchemsha maji ya moto na kujichua kwa lengo la kupunguza maumivu.

    Baada ya kujichua nilikwenda kwenye karo na kuanza kuosha vyombo lakini muda mwingi niliutumia kujutia kitendo nilichokifanya, nilimchukia sana mpenzi wangu.

    Kufuatia kupoteza uchangamfu kufuatia maumivu niliyopa, mdogo wangu Dora aliniuliza nilikuwa nasumbuliwa na nini nikamwambia tumbo akanipa pole.

    Jioni hiyo kaka yangu aliyekuwa anasoma Dodoma alifika lakini aligundua kama sikuwa katika hali ya kawaida akaniuliza kulikoni nikamwambia tumbo lilikuwa likinisumbua.

    Aliniuliza kama nilikunywa dawa, nikamwambia nilikunywa akasema kama litaendelea angenipeleka hospitali, nikamwambia sawa ndipo tukaendelea na stori za hapa na pale.

    Japo nilipotembea nilipata maumivu, nilijikaza lakini mama aliporejea aligundua sikuwa sawa, aliponiuliza nilimwambia tumbo la wakubwa lilikuwa likinisumbua ndipo akaniambia nimwachie kazi ya kupika nikapumzike.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mama aliniambia hivyo kwa sababu alikuwa akielewa nilivyokuwa nasumbuliwa na tumbo nilipokuwa katika kipindi cha hedhi, lakini ukweli wa maumivu niliyopata niliujua mwenyewe.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog