Search This Blog

NYAYO ZA DAMU - 5







    Simulizi : Nyayo Za Damu

    Sehemu Ya Tano (5)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mama kama kufa kila kiumbe kitakufa na kila kiumbe hufa kwa ahadi kilichoumbwa nazo mbele ya Mungu, kuongopa kifo ni kijidanganya.”



    “Kwahi upo radhi tufe kwa ajili ya mapenzi yako.”



    -

    “Mama waliokufa wote hawakufa kwa ajili ya mapenzi.”

    “Sawa nimekuelewa.”



    Walikubaliana kumuongezea nguvu Nargis kupambana na mtaalam aliyepewa kazi ya kumrudisha Sakina katika umbile la ubinadamu. Taarifa ile ilimpa nguvu Nargis na kurudiwa na furaha, alimwaga mama yake na kurudi nchi kavu alipomuacha Sakina akilindwa na majoka makubwa ya kiini macho. Kabla ya kwenda kwa Sakina alirudi kwa mumewe Thabit.



    Baada ya Nargis kuondoka, malkia Zebeda alifanya kikao cha siri na mwanaye mkubwa ili kumdhibiti Nargis asilete balaa chini ya bahari. Vita aliyoiona mbele yao ilikuwa kubwa sana ambayo lazima itawashinda na kuwasambaratisha.

    “Abee, mama vipi, nilikuona na mwanao yupo wapi?”



    “Kaondoka.”

    “Hata bila kuniaga au kunisalimia?”

    ”Si wewe, amekuja hapa jicho limemtoka kama kakabwa shingo.”



    “Nini tatizo?”

    “Si mtu wake wa amri ya Mungu.”

    “Imekuwaje tena?”



    “Niliyomweleza sasa yanamtokea, leo kakutana na mtihani mdogo kachanganyikiwa. Nilikuwa nataka uifanye ile kazi mara moja.”

    “Ipi hiyo?”

    “Ya kummaliza Thabit.”



    “Mamaaa!!” Hailat alishtuka kwa mara ya pili.

    “Siyo ombi bali amri bila hiyo maisha yetu yapo mashakani, kibaya zaidi anataka kumleta mumewe chini ya bahari.”



    “Ili?”

    “Waishi huku.”

    “Mmh, sasa itakuwaje, akijua je?”



    “Hawezi kujua kuna kazi yake moja utaifanya ya kummaliza mganga mmoja aliyetaka kushindana na sisi. Tukimaliza ile kazi lazima Nargis atatuamini na hiyo ndiyo nafasi ya kummaliza Thabit bila kujua.”

    “Mmh sawa, lakini akigundua!”



    “Hawezi kugundua lolote.” Walikubalia kufanya mpango wa siri wa kumuua Thabit, kwa kuifanya kazi ya kwanza ya kummaliza mganga anayetaka kumrudisha Sakina katika umbile la kibinadamu toka umbile la mbwa.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kupewa kazi nzito na mama yake Hailat dada yake Nargis alijiandaa kwenda kuifanya kazi nzito ya kumuua mganga aliyetaka kuoneshana ubabe na Nargis na kisha kumuua Thabit mume wa mdogo wake Nargis. Aliondoka hadi nyumbani kwa mganga kisha aliingia katika chumba cha mganga na kujigeuza joka kubwa lililojaa chumba kizima na kumsubiri mganga.

    Mganga baada ya kukosa baadhi ya vitu alivyoagizwa alirudi kuwapa taarifa alivikosa. Ila alikuwa na uwezo wa kumrudisha Sakina alipofichwa na kisha kumrudisha katika umbile lake na kuwa tayari kupambana na jini Nargis ambaye alimuona nguvu zake ni ndogo hivyo angeweza kumkabili.



    “Kwa hiyo baba unatuambiaje?”Mama sakina aliuliza.

    “Kwa kweli nilivyouliza kuhusu ng’ombe mweupe asiye na doa wamenieleza kuwa mpaka wamtume mtu akamtafute bara. Sasa hatujui atapatikana lini na muda huo mtoto wenu ataendelea kuteseka na hatujui amepanga nini huenda anataka kumuua.

    Kwa sasa inaonesha kamficha kwenye pori moja bado hajampeleka chini ya bahari kwa kazi ya haraka tutafanikiwa kumrudisha. Tena tuna bahati moja kazi kubwa ni kumrudisha kwani kwa sasa hayupo katika umbile la mbwa.”

    “Sasa baba, si bado ataendelea kutufuata?”

    “Hiyo ni kazi ndogo nitawapeni dawa ambayo naamini itawasaidia sana hawezi kuwafuata tena.”



    “Na kuhusu kumpata Thabit?”

    “Kwa vile tumekosa dawa za kumpatia jini ambazo zingembembeleza na kumrudisha Sakina kwa hiyari yake huku tukiliahidi kutomfuata tena. Hatuna jinsi lazima tutumie nguvu, kutokana na uwezo wangu wa kukabiliana na majini sina budi kuingia kazini.

    Siku zote kuna mambo mawili jema likishindikana basi tumia la shari, kwa hiyo kazi nitaifanyia nyumbani kwa vile hapa sina dawa nyingi, nitakachokifanya nitamrudisha Sakina na kumpa dawa ya kinga kesho nikija nitakuja kamili na dawa ya kummaliza kabisa huyo jini.”



    Kauli ile ilimfanya Nargis aliyekuwa na Thabit chumbani kwao ahisi maumivu makali ya kichwa na kuanza kupiga kelele ambazo Thabit alikuwa ameisha zitambua.

    Nargis alijipiga ukutani mpaka akatoka damu kwa hasira, alishika mkono kwenye paji la uso na kutoweka. Ndani ya nyumba ya mama Sakina upepo mkali ulivuma kama wa mwanzo uliotupa vitu vyepesi nje ya nyumba. Mama Sakina na mwanae waliingia wasiwasi kwa kuamini jini Nargis amerudi.



    Vumbi lilikuwa kubwa kwa uchafu wa nje kuingia ndani pamoja na majani yaliyokatika kutokana na hasira za Nargis. Nargis alijipigiza kwenye ukuta wa nyumba mpaka nyumba ikatikisika, yote yale yaliwafanya mama Sakina na mwanae wazidi kuwa na hofu.

    Mganga alinyoosha mkono kushindana na upepo uliokuwa mkali kwa muda mrefu tofauti na mwanzo. Haikuwa rahisi kuuzuia kitu kilichomshtua mganga na kuamini anakazi kubwa kupambana na jini yule mwenye hasira. Kwa haraka alitoa kichupa chake kidogo na kuvuta dawa ya unga ambayo ilimfanya atoe chafya mfululizo.



    Ghafla naye macho yaligeuka rangi na kuwa mekundu huku mishipa ya kichwa ikimsimama hata sauti yake iligeuka na kuwa nzito. Mwili wake nao ulivimba kidogo kwenye mikono mishipa, ilimsimama naye alionekana kama kiumbe cha ajabu.

    Aliukemea ule upepo uliokuwa umejaza uchafu mwingi ndani toka nje ikiwemo miti makaratasi majani makopo nk. Mpaka upepo unatulia ndani ya nyumba kulikuwa kumegeuka kama dampo la muda mrefu. Mbele yao kulikuwa na Nargis aliyekuwa amesimama akivuja damu kichwani huku machozi yakimtoka.



    Mganga aliendelea kumkemea kitu kilichofanya Nargis apige kelele za maumivu kisha alitoweka, baada ya kutoweka mganga alitoa tena dawa kwenye kichupa chake na kuinusa, alipiga tena chafya mfululizo na kurudi katika umbile lake la asili.

    Wote walimshangaa kumuuliza walishindwa kwa vile midomo yao ilikuwa mizito kutamka kutokana na hofu nzito iliyokuwa mioyoni mwao. Mganga alichukua maji kwa shida kupita juu ya uchafu uliokuwa umejaa sebuleni, baada ya kuchukua maji yaliyokuwa kwenye beseni dogo alichukua unga wa dawa na kuuweka kisha aliingiza usinga na kuuchovya na kuanza kunyunyiza kila kona ya nyumba huku akimwita kwa jina Sakina.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliendelea kufanya vile kwa muda huku akizunguka ndani na kutoka nje ya nyumba. Alifanya vile kwa kuzunguka nje ya nyumba kisha alirudi ndani. Hakukoma kumwita Sakina kama mtu anamwita mtu aliyemuona mbali.

    Alirudi ndani na kuendelea kuita ghafla alishangaa kumuona Sakina akiingia ndani akiwa katika umbile la kibinadamu. Mganga aliendelea kumwita mpaka alipofika karibu yake alimshika kichwani na kuanza kunyunyiza maji ya dawa kwa muda, baada ya kufanya vile mengine alimnywesha.



    Baada ya kumnywesha maji ya dawa Sakina alirudiwa na fahamu kwa kujishangaa kuwepo nyumbani. Hali aliyoiona ilimshtua na kuhoji mbona ndani kumejaa uchafu. Walimueleza hali ilivyokuwa, hakusema kitu kila alivyokumbuka alivyokuwa na sehemu aliyokwenda kuwekwa na Nargis alikokuwa analindwa na nyoka wakubwa wasio na mfano, machozi yalimtoka.

    Mganga baada ya zoezi lile zito aliwaaga na kuwaahidi kurudi kesho yake ambako angefanya zoezi la kinga na kummaliza jini Nargis na wao kumpata Thabit. Aliwaaga na kuwaacha na zoezi zito la kutoa uchafu uliokuwa umejaa ndani.



    Nargis alipotoka nyumbani kwa mama Sakina alikwenda moja kwa moja porini alipomficha Sakina, lakini ajabu hakumkuta na aliporudi nyumbani kwao Sakina alimkuta akiwa na ndugu zake wakisomba uchafu kuutoa ndani.

    Alipojaribu kuisogelea ile nyumba moto mkubwa uliwaka na kumfanya asogee mbali. Kwa hasira alijipiga chini na kutoa kishindo kikubwa nilichowashtua wote. Walipoangalia sehemu iliyotokea kishindo kile, wote walishtuka kumuona Nargis akitoka kwenye vumbi.



    Ajabu vumbi lilipotulia alitoweka katika mazingira ya kutatanisha, hali ile iliwatia hofu na kuwafanya wakimbilie ndani na uchafu uliobakia wasiutoe tena. Waliomba Mungu siku ya pili ifike upesi ili mganga arudi na kuifanya kazi aliyowaahidi.



    NARGIS baada ya kumkosa Sakina porini alikomficha na kumkuta nyumbani kwao roho ilimuuma na kuamua kumfuatilia lakini alikutana na kizingiti kikubwa kuonesha wamejidhatiti kupambana naye. Aliamini kabisa ngoma ile ni nzito na maisha yake yapo hatarini.

    Wasiwasi wake mkubwa ulikuwa iwapo taarifa zile atazipeleka kwa mama yake lazima ataelezwa aachane na Thabit, kwake kuachana na Thabit ilikuwa sawa na kuondolewa moyo mwilini mwake. Lakini kwa mambo aliyoyaona kwa mtaalamu yule aliamini kabisa kwake ni maji mazito.



    Hakuwa na jinsi zaidi ya kwenda kuomba msaada wa haraka kwa mama yake Malkia Zebeda, kama kawaida mama yake baada ya kufika aliyaona yote, kwenye mboni za macho yake hakukuwa na haja ya kujieleza. Alipofika tu mbele ya mama yake mama yake alimkata kauli.



    “Unataka kusema nini, nimekueleza tokea mwanzo wanadamu ni viumbe wabaya sana hushikilia yasiyowahusu ili tu wawaharibie viumbe wengine, wao kwa wao hawapendani itakuwa sisi viumbe tusioonekana. Nimekueleza toka mwanzo kuwa tatizo kubwa ni mumeo lakini unaking’ang’ania kifo, lakini hatuna jinsi, tutahakikisha tunakulinda kwa nguvu zote.



    Kuhusu yule mganga dada yako nimemtuma anakwenda kuifanya ile kazi, kama atashindwa basi nitaongeza nguvu mimi, lakini namuamini anaweza kumaliza kazi ile.”

    “Na wale wabaya wangu?”

    “Nao pia hawawezi kufanya lolote wasikutie hofu.”



    “Mmh, sawa.”

    “Lakini kumbuka kuna vita nzito mbele yetu inakuja ambayo nina imani hatutaiweza.”

    “Mama tutapigana nayo mpaka tone la mwisho.”



    “Kama unajua hivyo mbona umechemsha.”

    “Ndiyo maana nikaja kwenu.”

    “Hivi Nargis hakuna wanaume wa kijijini walio wazuri?”

    “Wapo.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa kwa nini unamng’ang’ania mwanadamu ana uzuri gani kumshinda Zahal au Mehoob?”

    “Mama kila ndege hutua mti aupendao na si kila unachokipenda wewe mimi nakipenda au ninachokipenda mimi wewe utakipenda ndio maana tunatofautiana kwa Thabit. Kwangu Thabit ni mwanaume mwenye mapenzi ya dhati kwangu tena aliyejitoa mhanga kwa maisha yangu.”



    “Tunajua Thabit hana tatizo na kama wanadamu wote wangekuwa kama Thabit kwa kweli dunia nzima ingekuwa na amani.”



    “Sasa mtu huyo nikimpoteza nitampata wapi tena?”

    “Kwani hakuna majini walio na upendo kupita huyo mwanadamu?”



    “Wanaweza kuwepo, lakini niliapa sitaolewa na jini wala kumpoteza Thabit labda kwa mapenzi ya Mungu na si mkono wa kiumbe chochote.”



    “Basi hakuna tatizo tutakulinda.”

    “Nitashukuru.”



    Baada ya kutolewa hofu na mama yake Nargis aliamua kujipumzisha chini ya bahari kusubiri taarifa za dada yake aliyekwenda kwa mganga. Kwa upande wa pili Hailat dada yake Nargis aliendelea kumsubiri mganga aliyekuwa njiani akirudi nyumbani kwake kutengeneza dawa kwa ajili ya kupambana na Nargis.



    Hailat akiwa katika umbile la nyoka mkubwa akimsubiri mganga kwa hamu kubwa, mganga alipofika kwake hakuwa na wasiwasi wowote. Nje ya nyumba yake alikuwa na wagonjwa waliokuwa wakisubiri tiba yake. Aliwasalimia na kuingia ndani kwa kufunua pazia ya kitambaa chekundu.



    Alishtuka kumuona nyoka mkubwa aliyekuwa amejaa chumbani, alipotaka kurudi nyuma ili akimbie mkia ya yule nyoka wa ajabu ambaye hakuwahi kumuona wala kuhadithiwa maishani mwake ulimzunguka na kumkunja kiunoni na kumrudisha ndani.



    Alipotaka kukimbia hakuwez, kichwa cha nyoka yule aliyekuwa na ukubwa wa ajabu kilipungua na kuwa sawa na chatu kilianza kumsogelea taratibu usoni huku nyoka yule akitoa ulimi wake uliokuwa umegawanyika na kuonekana ana ndimi zaidi ya kumi.



    Nyoka alipomkaribia mganga alipiga kelele za kutaka kuomba msaada, alipofunua mdomo ili apige kelele nyoka yule aliingia mdomoni na kujivuta taratibu na kuingia mwilini mwa yule mganga. Joto la nyoka lilikuwa kubwa liligandisha damu ya mganga iliyomfanya aage dunia.



    Baada ya kumaliza kazi yake alijitoa mwilini kwa mganga na alijirudisha katika umbile la kibinadamu na kuuangalia mwili wa mganga kwa dharau, aliukanyaga kwa miguu huku akiugeuza. Moyoni alijisemea.

    “Kumbe nilijiandaa kwa nguvu nyingi kumbe mtu mwenyewe hata kiganjani hajai,” aliitemea mate maiti ya mganga kisha akacheka mfululizo kwa sauti ya juu sauti iliyosikika hata kwa wateja waliokuwa wakisubiri huduma za mganga yule.



    Kabla ya kuondoka alijikuta akiiwaza kazi nzito ya kumuua Thabit mume wa mdogo wake Nargis. Aliamini kazi ya kumuua Thabit si kubwa tena nyepesi kuliko ya mganga, lakini wasiwasi wake mkubwa Nargis akigundua kuwa yeye ndiye aliyemuua mume wake hali itakuwaje? Alijikuta akijisemea mwenyewe kwa sauti ya chini.

    “Kazi hii nimemaliza bado ya Thabit,” Hailat alicheka tena mfululizo kisha alishika kwenye paji la uso na kutoweka eneo lile kurudi nyumbani kupeleka taarifa ya kazi aliyoifanya.



    Sauti ya Hailat ya kucheka mfululizo iliwashtua wagonjwa ambao waliamua kuingia ndani ya kilinge kutaka kujua sauti ile kali ya kike ilikuwa ya nani. Wao waliamini mpaka muda ule hakukuwa na mtu ndani, lakini kicheko kile kiliwafanya waingie ndani kuona kuna nini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndani hakukuwa na mtu zaidi ya mwili wa mganga ukiwa amelala chini mdomo ukiwa wazi, ajabu ya Mungu sehemu zote zilizokuwa wazi katika mwili wa mganga zilitoa funzo kuonesha mtu yule amefariki wiki moja iliyopita. Wote walipata mshtuko kwa mtu kupita dakika tano akiingia ndani tena amewasalimia na kuwaeleza wangoje atengeneze mazingira mazuri ili awapatie tiba.



    Lakini ajabu ya karne, dakika tano tu mtu amekufa na kuoza na kutoa funza kila kona ya mwili kama mtu aliyekufa wiki nzima. Kila mmoja alitaharuki kufikia hatua ya watu kuondoka eneo la mganga bila kuaga huku kila mmoja akisema la kwake ilikuwa hali ya kutisha sana.





    Hailat dada yake Nargis baada ya kumuua mganga alirudi chini ya maji kurudisha taarifa kwa mama yake kuhusiana na kazi aliyotumwa. Alipofika mama yake kama kawaida alikwishayaona matukio yote kwenye mboni za macho za mwanaye.

    Kabla hajasema alimkumbatia kwa furaha huku akisema: “Asante sana mwanangu kazi nzuri umefanya.”



    Hailat hakusema kitu alitabasamu na kuinama kuonesha kupokea hongera za mama yake, lakini moyoni alikuwa na kazi nzito mbele yake ambayo kila alipoifikiria mapigo ya moyo yalimwenda mbio. Aliamini kabisa kitendo atakachokifanya kwa Thabit na mdogo wake agundue basi ingekuwa vita nzito ambayo mwisho wake ungekuwa mbaya sana.



    Alitamani kumueleza mama yake aachane na mpango ule wa hatari lakini aliogopa kama lingetokea tatizo basi yeye angebeba msalaba ule. Alikumbuka katika watu ambao walifanya makosa makubwa alikuwa yeye pale alipokaidi ushauri wa mama yake na mwisho wake ukawa majuto kwake.

    Wakati Hailat akiwa katika mawazo mazito juu ya kutekeleza amri ya kumuua shemeji yake, mama yake alimwita Nargis aliyekuwa amejilaza baada ya mshike mshike uliomtoa jasho.



    “Nargis... Nargis,” alimwita mwanaye aliyekuwa amepitiwa na usingizi.

    “ Abee mama.”

    “Kazi iliyokuwa ikikusumbua dada yako ameimaliza.”

    “Ipi hiyo mama?”

    ”Ya mganga.”

    “Mmemuua?”

    “Ndiyo.”



    “Ooh, asante sana dada, sasa nitaishi kwa amani na mume wangu.”

    Nargis alimkumbatia dada yake kwa furaha ya ajabu, kitendo cha Nargis kufurahi baada ya kuuawa mganga na kuamini mume wake atakuwa salama kilimuumiza sana Hailat na kujikuta akitokwa machozi ya uchungu ya kufikiria kama mdogo wake atajua aliyemuua ni dada yake nini kingefuata.



    Mdogo wake tukio lile aliliona na kushangazwa na kitendo cha dada yake kuangua machozi badala ya kufurahi.

    “Dada mbona unalia?”

    Sauti ya mdogo wake ilizidisha uchungu moyoni mwake na kumfanya ajitoe mikononi mwa mdogo wake na kukimbia nje kulia kilio cha kwikwi. Kitendo kile kilizidi kumchanganya Nargis kabla ya kufanya lolote alimuangalia mama yake ambaye hakuonekana kushtushwa na tukio lile, kitu kilichoongeza kumweka njia panda.

    Baada ya kuona mama yake akiona tukio lile la kawaida, aligeuka ili atoke nje kwenda kumuuliza dada yake nini kimemsibu. Lakini kabla hajanyanyua mguu mama yake alimwita.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nargis!”

    “Abee mama.”

    “Unataka kwenda wapi?”

    “Mama ina maana alichokifanya dada cha kawaida?”

    “Sasa cha ajabu nini?”

    “Mama, mtu mzima kulia kitu cha kawaida?”

    “Hebu ngoja.”

    Mama yake alitoka nje na kumuacha Nargis amesimama, Malkia Zebeda alitoka nje na kumkuta mwanaye akiwa ameinama huku akiendelea kulia. Alipofika alimshika mgongoni na kumuuliza.



    “Unalia nini?”

    “Mama umenipa mtihani mzito.”

    “Wa kawaida ni wasiwasi wako tu.”

    “Mama unafikiri Nargis akijua kutakuwa na usalama kweli?”

    “Hawezi kujua, kitendo cha kumuua mganga umemrudishia imani na kutuamini na kujua sasa hivi tupo upande wake. Kama utamuua Thabit lazima tuungane naye katika msiba mzito ili kuondoa wasiwasi upande wetu.”

    “Mama unajua jinsi gani tunavyompenda Nargis.”

    “Hilo najua ndiyo maana nafanya mpango huu ili kumuweka salama zaidi.”



    “Mama hakuna mpango mwingine zaidi wa huu wa kumuua Thabit?”

    “Huu ndiyo mpango utakaomuweka salama mdogo wako na sisi pia.”

    “Mh! Sina jinsi kuufanya lakini ni mpango wa kwanza kuufanya kwa shingo upande.”

    “Mwanangu siku zote kumponya mgonjwa wa jipu ni kumtumbua na si kumuonea huruma, maumivu ya kutumbuliwa ni mafupi kuliko maumivu ya jipu lenyewe.”

    “Mh! Sawa.”



    “Sasa mdanganye mdogo wako kilio chako kinatokana na maumivu aliyoyapata kupambana na mganga ili ajue kazi aliyoifanya ni kubwa kwa ajili yake nusra utoe roho.”

    “Sawa mama nitamwambia.”

    Walikubaliana na kurudi wote ndani.



    *****

    Baada ya kukaa ndani kwa siku nzima bila kutoka nje kwa ajili ya kumhofia jini Nargis, siku ya pili walisubiri bila mafanikio walipatwa na wasiwasi na kujiuliza kulikoni mganga mpaka muda ule hajaonekana. Siku ya pili nayo ilikatika wakiwa ndani na mganga hakuonekana.

    “Jamani mganga atakuwa wapi mbona hakuonekana kama alivyotuahidi baada ya kutuachia vita nzito na jini.”



    “Lakini mama mganga pamoja na kwamba haonekani lakini si alitueleza tunaweza kufanya mambo yetu bila jini kutufanya lolote,” mdogo wake Sakina alisema.

    “Tena kweli tumekaa ndani bure tulikuwa na uwezo wa kufanya shughuli zetu bila wasiwasi wowote.” mama Sakina alikumbuka kauli ya mganga.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    “Mnaonaje kesho tuende kwa mganga siamini kama tutapotea kwa vile amesema kuwa yeye ni maarufu sana maeneo yale,” Sakina aliongezea.

    “Basi kama hivyo uchafu huu ambao tuliuacha kumsubiri mganga tuuondoe usiku huu huu.”

    Walikubaliana wote kwa pamoja na kuanza kuutoa uchafu uliokuwa umebakia ndani baada ya mkwara wa jini Nargis. Waliutoa uchafu wote na kufanya usafi kisha walilala kusubiri siku ya pili waende kwa mganga.

    **********

    Siku ya pili walidamka mapema kuwahi kwa mganga ili wajue nini kilichomfanya asitokee siku ya pili. Kutokana na ramani waliyopewa hawakupotea walipomuulizia walielekezwa na kwenda moja kwa moja kwa mganga.

    Ajabu hapakuwa na mtu yeyote maeneo ya mganga, walisogea hadi kwenye nyumba na kupiga hodi.

    “Jamani wenyeji hodi!”



    Lakini hapakuwa na jibu, waliita kiasi cha kukata tamaa, Sakina aliamua kwenda chumba cha mganga akaangalie huenda kuna mtu yumo ndani ambaye angeweza kuwapa maelezo ya mganga. Sakina alifunua pazia na kuingia ndani.

    Alipotupa macho mbele alikutana na tukio la kutisha lililomfanya apige kelele za woga na kuanguka chini akapoteza fahamu.



    Sauti ya mshtuko iliwashtua mama Sakina na mwanaye waliokuwa nje wakisubiri majibu ya Sakina aliyeingia ndani. Pamoja na kupata mshtuko na hofu tele moyoni hawakuwa na jinsi zaidi ya kuingia ndani kuangalia Sakina amekutana na kitu gani cha kumtisha.



    Waliingia huku wakitetemeka kwa mwendo wa kunyata, Sada mdogo wake Sakina, ndiye aliyetangulia akifuatiwa na mama yake. Alifunua pazia taratibu na kutanguliza kichwa, macho yake yalitua kwenye mzoga wa mganga uliokuwa ukitoka funza kila kona na sehemu zake zingine zilionekana zimeliwa na funza. Maiti yake ilionesha kama mtu aliyekufa mwezi mmoja uliopita kwani sehemu za macho zilikuwa zimeliwa na funza, lakini ajabu alikuwa hanuki.



    Pembeni ya maiti ya mganga alikuwepo Sakina aliyekuwa amelala chali huku funza wakianza kumtambaa kwenye mikono na nguo, walikuwa wakitoka katika maiti ya mganga. Sada alishtuka kama dada yake na kupiga kelele za mshtuko na kuanguka juu ya mwili wa dada yake na kupoteza fahamu.



    Mama yao alitaharuki kuona watoto wake waliotangulia kuingia ndani wamepiga kelele za woga na kunyamaza. Alitamani akimbie lakini damu ilikuwa nzito kuliko maji, alipiga moyo konde na kuamua kuingia ndani huku akisema “Liwalo na liwe.”



    Alifungua pazia kwa nguvu na kuwa tayari kupambana na lolote lililokuwa mbele yake, mzoga wa mganga ulimshtua na kumtisha sana, lakini alijikaza kike kuhakikisha anakabiliana na lililokuwa mbele yake. Alimlaani shetani kimoyomoyo kisha alimuinamia Sakina aliyekuwa ameanza kutambaliwa na funza na kumnyanyua kumtoa nje kwa shida kutokana na umri wake na uzito wa mwanaye.



    Alimshika mikono na kumburuza hadi nje kisha alimrudia mdogo huku akiendelea kumuomba Mungu kimoyomoyo amuepushe na mtihani ule. Alifanikiwa kuwatoa wote nje na kuwapatia huduma ya kwanza kwa kuwamwagia maji yaliyokuwepo kwenye pipa nje ya nyumba ya mganga. Wote walirudiwa na fahamu, baada ya kurudiwa na fahamu hawakutaka waendelee kuwepo eneo lile kwani waliamini ni hatari kwa usalama wao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alirudi hadi kituoni ambako walipata gari kurudi kwao, njia nzima kila mmoja alikuwa kimya akitafakari kifo cha kutisha cha mganga. Mwili wake kuonekana kama mtu aliyekufa mwezi mmoja uliopita, hawakuamini kifo cha siku moja mtu aoze kiasi kile.



    Walipofika nyumbani Sakina na mdogo wake Sada waliangua kilio kutokana na kifo cha mganga pia hali aliyokuwa nayo iliyoufanya mwili uharibike huku baadhi ya sehemu ya mwili kuliwa na wadudu. Mama yao aliingia kazi ya kuwabembeleza wanae ambao hofu iliwajaa baada kuuona mwili wa mganga ulivyoharibika.

    “Mama lazima atakuwa yule mwanamke jini,” Sakina alitoa wazo baada ya kunyamaza kulia.



    “Mmh, kweli inawezekana,” mama aliunga mkono.

    “Mama kama kweli ni yeye hatuoni maisha yetu yapo hatarini?” Sada alihoji.



    “Ni kweli lazima maisha yetu yatakuwa mashakani,” mama yao aliongezea.

    “Sasa mama tufanye nini kabla mambo hayajaharibika?” Sakina aliuliza.

    “Ni kumtafuta mganga mwingine la sivyo tutaumia, Jini yule ni hata....”



    Kabla hajamalizia upepo ulianza kuingia ndani taratibu na kupeperusha mapazia. Kila dakika upepo uliongezeka huku milio wa kuvuma kwake ukisikika. Hali ya wasi wasi ilitanda na kuamini mbaya wao amefika, Sakina na Sada wote kwa woga walijisogeza kwa mama yao na kumkumbatia kwa nguvu.



    “Jamani wanangu tumuombe Mungu, lakini kama atatokea mimi sina ubavu wa kumzuia.”

    “Yaani mama najuta kujiingiza katika vita isiyonihusu,” Sakina alisema huku akizidi kumshikilia kwa nguvu.

    “Mama tukipona tuachane naye,” Sada naye alisema.



    Wakiwa wanajadili vile upepo ule ulipungua taratibu kisha ulitulia kabisa, baada ya upepo kutulia kilisika kicheko kama mtu amechekea mbali na sauti yake kusafirishwa na upepo. Baada kicheko kunyamaza hali ya utulivu wa awali ulijirudia.



    Kwa vile muda ulikuwa bado hawakutaka kupoteza muda, mama yao aliwaeleza waende kwa mganga mwingine aliyekuwa Kigamboni. Baada ya kukubaliana hata bila kuoga wala kubadili nguo, waliondoka kwenda kwa mganga Kigamboni.



    CHINI YA BAHARI

    Baada ya mpango wa kumziba macho Nargis kufanikiwa wa kumwua mganga, malkia Zebeda alimwita tena mwanaye mkubwa wa kike, Hailat, dada yake Nargis.



    “Hailat.”

    “Abee mama.”

    “Nafikiri sasa wakati muafaka umefika wa kummaliza shemeji yako.”



    “Ni kweli mama, lakini kwa nini moyo unaniuma kila nikifikiria kufanya kitendo hicho?”

    “Mwanangu umefanya mauaji mangapi hili likushtue.”

    “Mama si kunishtua bali uzito wa tukio lenyewe.”



    “Nikueleze mara ngapi kumtibu mgonjwa wa jipu ni kumtumbua na si kumuonea huruma. Litumbue jipu ili tuishi kwa amani, ningeweza kufanya hivyo mimi lakini Nargis akigundua kutakuwa hakuna wa kumtuliza.”

    “Mama kwa hiyo msalaba unanibebesha mimi?”

    “Kama itatokea, nitajua jinsi gani ya kumaliza tatizo hilo.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mmh, sawa lakini kuna kitu kizito kinakuja mbele ambacho huenda kikasambaratisha familia.”

    “Ni wasi wasi wako, kamwe hawezi kujua nani aliyemuua mume wake.”

    “Mama una uhakika na ukisemacho?”



    “Na siku hiyo atashinda huku, mpaka unamaliza kazi na kurudi nyumbani ndipo nitamruhusu. Kutokana na kuwa na vita na jirani yake lazima atawajua ni wale, nasi tutampa nguvu kuwafutilia mbali. Nakuhakikishia siku hiyo na mimi mama yenu nitashiriki nikumbuke enzi zangu.”





    Mama Sakina na wanae walipofika feri walipanda pantoni kuelekea Kigamboni, baada ya watu kujaa pantoni ilianza kutembea taratibu kuelekea upande wa pili wa bahari. Pantoni ilipofika katikati ya maji, ghafla upepo mkali ulizuka baharini na kuifanya pantoni kuyumba.



    Ilikuwa hali ya kutisha kwa kila mtu kulilia roho yake, upepo ambao haukuwahi kutokea baharini, uliendelea kuvuma kwa nguvu na kuifanya pantoni kuchota maji na baadhi ya watu kuangukia kwenye maji. Mmoja wa watu walioangukia kwenye maji alikuwa Sakina.



    Taarifa za pantoni kutaka kupinduka zilifika katika jeshi la majini ambalo lilichukua meli ya uokoaji na kuwahi eneo la tukio kuokoa watu walioangukia majini.

    Walifanikiwa kuwaokoa wote kasoro Sakina peke yake ndiye hakuonekana.



    Lilikuwa pigo jingine kwa mama Sakina na kuamini ule haukuwa upepo wa kawaida ila wa jini Nargis. Jeshi la uokoaji wa baharini lilifanya msako kwa kutumia vifaa vya kisasa kumtafuta Sakina akiwa hai au amekufa. Lakini kila kona chini ya maji hawakuona kitu.



    Baada ya kumkosa ikabakia kitendawili kwa watu waliokuwa wamefika salama Kigamboni. Kila mmoja aliamini siku ile ndiyo ilikuwa siku yao ya mwisho kutokana na ukubwa wa upepo ulioyumbisha pantoni ambayo ilionekana kuzama.



    Mama Sakina na mwanae Sada wote waliangua kilio kumlilia Sakina aliyepotelea ndani ya maji. Waokoaji walisema wamekata tamaa kwani wametumia vifaa vya kisasa kumtafuta Sakina bila mafanikio na kutoa taarifa kwa mtu yeyote atakayeuona mwili wake atoe taarifa.



    Baada ya watu wote kuondoka walibakia mama Sakina na mwanaye Sada kujipanga wafanye nini baada ya Sakina kupotelea majini.

    “Mama kwa nini tusiachane na yule jini?”

    “Mmh kweli, lakini kwa vile sisi tumebakia salama hatuwezi kurudi nyuma lazima twende kwa mganga tukajue dada yako yupo wapi.”



    “Mamaaa, lakini tunakuwa wabishi kama kenge mpaka tutoke damu masikioni!”

    “Sada kwa vile wewe ni mtoto hii imeishakuwa vita hatuna budi kupambana nayo.”

    “Mama utawezaje kushindana na kiumbe asiyeonekana?”

    “Ni kweli, lakini viumbe hawa ukiwaogopa sana wanaweza kukufanya wanavyotaka.”



    “Mamaaa, kwa nini tusirudi?”

    “Hapana maji tumeishayavulia nguo hatuna budi kuyaoga, na bila ya hivyo hatuwezi kumrudisha dada yako.”

    “Unataka kuniambia dada Sakina hajafa?”

    “Inawezekana kama kachukuliwa na jini, lakini kama kwa amri ya Mungu lazima atakuwa amekufa, lakini kupotea kwake nina imani hajafa.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mamaaa mbona kila siku dada Sakina?”

    “Unataka safari ijayo uchukuliwe wewe?”

    “Aku, jini nitazungumza nalo nini?”

    “Kwani dada yako alizungumza nalo nini?”

    “Mama vitu hivyo si vya kuomb....”



    Sada alinyamaza ghafla na kukishangaa kitu ambacho mama yake alipokiangalia hakukiona. Mama Sakina alikitazama kitu kilichomfanya Sada anyamaze lakini hakukiona ilibidi amuulize mwanaye ambaye alikuwa bado amekitumbulia macho kitu kisichoonekana.



    “Wee Sada,” alimshtua.

    “E...eh...eeh,” Sada alishtuka kama mtu aliyekuwa amepigwa na bumbuwazi.

    “Umeona nini mbona umenyamaza ghafla?”

    “Mmh,” aliguna bila kusema kitu.

    “Vipi kuna nini mbona unanitisha?”

    “Ina maana wewe mama huoni?”

    “Nini?”

    “Yule mwanamke jini.”



    “Mwanamke jini! Yuko wapi?”

    ”Mama si amepita mbele yetu na wewe nimekuona ukimtazama na kupotelea kwa watu.”

    “Hapana sijamuona huenda umemfananisha.”

    “Hapana mama mwenyewe namjua vizuri.”

    “Kwani aliku....”



    Mama Sakina naye alinyamaza ghafla na kukaza macho kuangalia mbele, safari hii ilikuwa kazi ya Sada kumshangaa mama yake anaangalia nini. Kila alivyoangalia mbele hakuona kitu lakini mama yake aliendelea kuangalia mbele kwa makini. Ilibidi Sada amshtue mama yake.

    “Mama vipi tena.”

    “Nimemuona.”



    “Nani?”

    “Mwanamke jini.”

    “Yupo wapi?”

    “Sada ina maana humuoni yule anaondoka karibia na lile gari linalokuja.”

    “Mama mbona mimi sioni kitu.”

    “Huo utani si yule,” alimuonesha kwa kidole.



    “Mamaa, sioni kitu chochote.”

    “Aah, basi tuachane naye.”

    “Mama turudi nyumbani, asije akatuua kama mganga.”

    “Acha woga kifo kimeumbwa, siwezi kurudi nyuma mpaka nijue hatima ya mwanangu.”

    Mama Sakina aligoma kurudi lakini moyoni alijawa na wasi wasi kwa vile jini Nargis alielekea mbele njia ya kuelekea kwa mganga. Lakini alipiga moyo konde na kuamua kwenda kwa mganga.



    *******

    Nargis baada ya kuipepesua pantoni kwa upepo mkali alifanikiwa kumnyakua Sakina kwenye kundi la watu na kwenda naye moja kwa moja kwenye gareza la chini ya miamba-maji.

    Nargis alionekana mwenye hasira kuliko siku zote, baada ya kumfikisha chini ya gereza alimfunga kamba na kuanza kumtandika kwa hasira.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sakina alipigwa mpaka akapoteza fahamu ndipo alipomuacha akamrudisha katika hali yake ya kawaida na kuanza kumhoji kwa nini amekuwa mbishi kutaka kufuatilia maisha yake.



    Sakina akiwa anavuja damu kila kona ya mwili, alifungwa kwenye mwamba kama anasurubiwa msalabani. Nargis alimsogelea Sakina aliyekuwa ameinamisha kichwa akiendelea kulia huku damu zikimtoka puani na mdomoni, alimshika chini ya kidevu na kuunyanyua uso wake.



    “Wee shetani wa kike nimekukoseeni nini mpaka kuamua kunifanya hivi?”

    “Naomba unisamehe,” Sakina aliomba kwa sauti ya kichovu kutokana na kipigo alichopata na mwili wake kumuuma kila kona.



    “Ninyi siyo watu wa kusameheni, nimekugeuza mbwa ili kukutisha lakini amekuja mtu na kuwatia kiburi, nafikiri mmeona nguvu zangu jinsi nilivyomfanya. Sikuwa na nia ya kukufanya hivi ila umenilazimisha. Kuanzia leo nitakugeuza nguruwe na kukuacha huku milele, sitaki kukuua kwa vile huna uwezo wa kuniua zaidi ya kutegemea msaada wa kiumbe kingine.



    Nakuhakikishia kukuletea mama na mdogo wako katika umbile nitakalokugeuza wewe, nina imani viumbe wapumbavu maisha yenu yanafaa huku.”

    “Tusamehe dada Nargis.”



    “Undugu wa jini na binadamu ulianza lini, wanadamu kwa wanadamu hamwelewani, itakuwa sisi majini. Mimi si dada yako, mimi ni jini adui yako,” Nargis alisema kwa hasira.

    “Hapana dada Nargis, ni mama ndiye aliyenilazimisha kuyafanya haya, naomba unisamehe.”

    “Ninyi wanadamu hamsikii upo kama kenge mpaka mtoke damu masikioni.”



    “Najua tumekukosea, tupo chini ya miguu yako.”

    “Unajua mama yako kwa sasa anafanya nini?”

    “Hata sijui.”



    “Mlikuwa mnakwenda wapi?”

    Swali lile lilikuwa zito kwa Sakina kwa kuamini Nargis alikuwa anajua walikuwa wanakwenda wapi, alibakia kimya bila kujibu swali. Nargis alimtazama kwa jicho kali lililomfanya aangalie pembeni kwa woga na aibu.



    “Nijibu la sivyo nitakufanya kitu kibaya kuliko nilichokufanya.”

    “Kwa mganga.”



    “Kufanya nini?”

    “Kukuzuia nimpate Thabit.”

    “Wanaume wote wamekwenda wapi mpaka mumng’ang’anie mume wangu?”



    “Hatukujua kama ameoa.”

    “Mganga alipowaeleza kuwa mimi ni mke wa mtu mlifanya nini?”

    “Kwa hilo tunaomba utusamehe“

    “Hujanijibu niwasamehe kwa lipi?”



    “La kutaka kukuachanisha na Thabit.”

    “Na mimi kunifanya nini?”

    “Dada Nargis tumekosa dada yangu, ni roho mbaya lakini tutajifunza kutokana na makosa.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hujanijibu, na mama yako sasa anakwenda wapi?”

    “Siwezi kujua dada Nargis.”

    “Ngoja nikuoneshe jinsi mlivyodhamiria vibaya juu yangu kisha mnaomba msamaha.”



    Nargis alinyoosha mkono mbele sehemu ya mwamba, ilikuwa kama sinema, mbele yake aliwaona mama yake na mdogo wake wakielekea kwa mganga.

    “Umewaona?”

    “Nimewaona.”



    “Pamoja na kuwatisha mama yako amekuwa mbishi, sasa nitamgeuza kiumbe cha ajabu.”

    Baada ya kusema vile alichota maji ya bahari kwa mkono na kuyanyunyizia kwa mama Sakina, ambaye alianza kujikuna mwili mzima kama aliyemwagiwa upupu huku akilia. Sakina alimshuhudia mama yake akivua nguo na kubakia mtupu kwa ajili ya kujikuna, ghafla alimwona mama yake mwili wote ukitoka mapele makubwa.



    Sakima alimsikia mama yake alivyokuwa akilia huku akiendelea kujikuna akiwa mtupu baada ya kuzitupa nguo zote. Mdogo wake Sada alionekana akijitahidi kumvalisha nguo mama yake lakini alishindwa kutokana na jinsi mama yake alivyokuwa akijitupa chini.



    Sakina roho ilimuuma na kutamani kumuombea mama yake msamaha, lakini bado hakujua hatima yake mbele ya Nargis aliyekuwa na hasira za ajabu.



    ***

    Wakati Nargis akiendeleza mateso mazito kwa mama Sakina na familia yake, ndani ya kasri ya Malkia Zebeda chini ya bahari, mpango ulipangwa na kupangika juu ya kifo cha Thabit mume wa Nargis. Malkia Zebeda alimwita mwanaye mkubwa Hailat kumweleza cha kufanya siku ile.

    “Nafikiri leo ndiyo siku mwafaka wa kutekeleza nililokutuma.”



    “Sawa mama, umeishamwita Nargis.”

    “Nitamwita tu, nimemtafuta sijamuona.”

    “Sasa mama tutafanyaje?”



    ”Kazi ile ni ya muda mfupi mpaka arudi atakuta mzoga wa mtu.”

    “Mama hatujui yupo wapi, huoni huo ni mtego tunaojiingiza wenyewe, kwa nini tusimtafute ili tujue kumndanganya na mimi nifanye kazi uliyonituma.”



    “Hesabu zangu zinaonesha kifo cha Thabit ndani ya saa moja lijalo zaidi ya hapo hatutamweza tena.”

    “Sasa mam..”



    “Hailat si muda wa mazungumzo sasa bado dakika hamsini inanionesha Thabit yupo nyumba sasa hivi.”

    Hailat alikubali shingo upande kwenda kumuua Thabit shemeji yake mume wa mdogo wake Nargis.





    Wakati mpango ule ukiwa umepamba moto, Sada mdogo wake Sakina aliyechanganyikiwa na hali ya mama yake aliyepagawa ghafla na kuanza kupiga kelele kuwa anawashwa mwili mzima kiasi cha kuvua nguo mbele za watu bila aibu.



    Wapita njia walijua yule mama ni mwendawazimu kutokana na kupiga kelele huku akijikuna na kuvua nguo zote. Sada alijitahidi kumvisha nguo lakini kila nguo ilipomgusa mwilini ilikuwa kama ina miba na kuziogopa kugusa mwilini mwake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kila alivyojikuna uchungu uliongezeka, ghafla mwili ulianza kutoka mapele makubwa kila kona huku mengine yakitoa usaha na kumfanya atoe harufu iliyowafanya watu wamkimbie na kubakia peke yake na mwanae ambaye alivumilia harufu mbaya iliyokuwa ikitoka mwilini kwa mama yake.



    “Mungu wangu nakufa nawashwa mimi, oooh nakufa jamani nisaidieni,” mama Sakina aliomba msaada kwa wapita njia lakini hakuna aliye shughulika naye.

    “Mama si uvae nguo,” Sada alimmbembeleza mama yake.



    “Siyo kwamba sitaki kuvaa nguo, kila ikigusa mwili wangu inakuwa kama ina miba, naumbuka mwanangu,” mama Sakina aliona dunia nzima ikimkimbia na kumwacha peke yake.

    “Mama nilikwambia unaona sasa.”

    “Mwanangu najuta, najuta kukubishia.”



    “Sasa tutafanyaje, hii hali inatisha.”

    “Sina jinsi mauti yananisubiri tu mwanangu, naumia jamani.”

    Kilio cha majuto kilisikika chini ya maji kwa Sakina kushuhudia mateso ya mama yake na kilio cha kukata tamaa. Alitamani kumpigia magoti kumuomba msamaha Nargis ili amsamehe mama yake na mateso yale mazito. Lakini bado aliamini makosa aliyofanya ni mazito na bado aliendelea kushindana naye.



    Nargis aliyekuwa amesimama ameshika mkono mmoja kiunoni, alimgeukia Sakina aliyekuwa akibubujikwa machozi ya uchungu wa mateso mazito ya mama yake. Alijikuta akisahau hata mateso yake na akili yote kuhamia kwa mama yake aliyekuwa akiteseka na kuadhirika kwa watu kumuona kama mwendawazimu.

    “Umemuona mama yako?”

    “Nimemuona,” Sakina alijibu kwa sauti ya kilio.



    “Unajua wanadamu ni viumbe wanafiki sana, siku zote hujificha nyuma ya machozi kwa kisingizio cha kuonewa kumbe dhamira yenu ilikuwa mbaya sana ya kuniua ili mumpate Thabit. Siamini nilichokifanya kinalingana na kosa mlilofanya.



    Nimekuwa nikiingia kwenye matatizo na wanadamu kila kukicha, hata leo hii nimuokote mwendawazimu na kumponya kisha awe mume wangu, mpo mtakaojitokeza na kumtaka huku mkitumia kila hila kuniondoa dunia.



    Sijamkosea mtu maisha yangu yananihusu mwenyewe na nilipoamua kumpenda Thabit nilijua hana mtu ndiyo maana nilimchagua lakini leo hii mmetokea watu mnaojifanya mnajua kupenda.



    Thabit kwani amezuka kama uyoga usio na mbegu, si alikuwepo sasa vipi leo aonekane mbele ya macho ya wanadamu. Nataka kukuuliza swali nakuomba unijibu bila hivyo adhabu ya mama yako itakugeukia wewe.”

    “Uliza tu dada yangu, nitakujibu bila kukudanganya.”

    “Jini na mwanadamu nani mbaya?”



    “Kwa kweli katika maisha yangu najua majini ni viumbe wabaya ambao hutumika kutoa roho za watu.”

    “Na mwanadamu anayemuua mwenzake ni jini?”

    “Hapana.”



    “Wewe umetoa mimba mbili na kutoa roho za viumbe visivyo na hatia na wewe ni jini?”

    “Hapana.”

    “Sasa kwa nini mmuone jini ndiye muuaji?”

    Sakina alikosa jibu na kuangalia chini kwa aibu, Nargis aliendelea kumuuliza maswali.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Na wanaoua Maalbino ni majini?”

    “Hapana.”

    “Kila kitu hapana, mbona hamuogopani ninyi wanadamu, viumbe wenye hila na roho mbaya. Na hata hao majini wanaoua watu hutumwa na ninyi wenyewe wanadamu, ndiyo maana angamizo kubwa katika karne zilizopita ni kwa wanadamu na si majini. Nafikiri mnaona jinsi gani wanadamu mlivyo wabaya kuliko majini mbele ya Mungu.



    Nimekuwa kiumbe mwenye huruma lakini huruma hiyo imenifanya nikose amani moyoni mwangu.

    Nilimuua mganga kwa sababu alikuwa akijua udhaifu wetu, tulimuwahi kabla hajafanya lolote. Lakini kiumbe anayemtegemea mtu huyo huwa hatusumbui sana, humtisha na akizidi humgeuza kiumbe wa ajabu. Hili litakuwa onyo la mwisho mkirudia tena nitafumba macho na kuutoa uhai wa kila kiumbe kitakacho taka kuingilia maisha yangu.



    Wakati Nargis akitaka kutoa msamaha kwa Sakina na mama yake dada yake Hailat alikuwa akiandaa kwenda kummaliza Thabit aliyekuwa nyumbani peke yake na vijakazi ambao walikuwa majini. Aliondoka hadi kwenye nyumba anayoishi mdogo wake na mumewe.



    Akiwa katika umbile la ndege, kwa vile kulikuwa na vijakazi majini wasio na uwezo mkubwa wa nguvu za kijini, alipofika aliitia nyumba ile kiza kizito na kufanikiwa kuwafungia chumba kimoja vijakazi wote kwa nguvu za kijini ambazo ziliwafanya washindwe kutoka.



    Baada ya kufanikiwa kuwafungia chumbani majini vijakazi, alirudi hadi sebuleni alipokuwa amekaa Thabit akisikiliza nyimbo zenye mahadhi ya kiarabu ambazo Nargis alikuwa akizipenda sana. Hailat alimpima Thabit na kumuona mwepesi sana.



    Lakini kabla ya kumvaa alijikuta akimuonea huruma shemeji yake huku akifikiria Nargis atapokea vipi kifo cha mumewe. Bila kutarajia machozi yalianza kumtoka kwa kumuonea huruma shemeji yake.



    Muda aliopewa na mama yake ulikuwa unazidi kuyoyoma zilikuwa zimebakia dakika ishirini, hakuwa na jinsi aliamua kumvaa Thabit, huku akisema liwalo na liwe.



    Hailat alimfuata Thabit aliyekuwa amejilaza kwenye kiti cha uvivu huku akibembelezwa na nyimbo laini za mahadhi ya Kiarabu. Upepo ulioingia ndani ulimshtua Thabit na kujua ule ni ujio wa majini ambao mara nyingi aliutumia Nargis kuingia ndani.



    Lakini ujio ule alikwishauacha na kuingia ndani katika hali ya utulivu ya mwanamke mwenye heshima kwa mumewe. Nargis pamoja na kuwa jini alikuwa na mapenzi mazito kwa mumewe kwa kumfanyia yote anayotakiwa kuyafanya mwanamke aliyeolewa kwa mume wake, vitu vilivyomteka Thabit kufikia hatua ya kutoona mwanamke yoyote duniani kama Nargis.



    Hakuna kiumbe yoyote angeweza kumbadilisha Thabit imani yake kwa majini viumbe wapole wenye upendo kuliko wanadamu ambao kutenda mabaya ni sehemu ya maisha yao. Thabit aliamini mkewe Nargis alikuwa anarudi, lakini upepo ulizidi kiasi cha kumtisha.



    Aliponyanyua macho juu alishangaa kuona joka kubwa likiingia dirishani na kumfuata alipokuwa amekaa. Thabit alishtuka alipotaka kupiga kelele joka lile lilimuingia mdomoni kwake, kwa vile alikuwa na nguvu ndogo za kijini alizoambukizwa na Nargis.



    Yule nyoka alipoingia kichwa na shingo alimshika ili asiingie wote, ikaanza vita nzito ambayo ilifanya vitu vyote ndani vipasukepasuke kutokana na Hailat kulazimisha kuingia ndani na Thabit alimshikilia asiingie ndani. Kila alipolazimisha alikuwa akimtoa upande mmoja kwenda mwingine na kumpigiza popote atakapoangukia na kusababisha vitu vyote ndani kuvunjikavunjika.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Thabit aliamini maisha yake yalikuwa mikononi mwake huku akiomba mkewe atokee. Muda ulizidi kukatika huku vita ikiwa kubwa. Wakati vita ikiendelea Nargis chini ya bahari hali ilimbadika ghafla na kujua kuna hatari iliyokuwa ikiendelea, lakini hakujua ipo wapi. Kwa haraka aliwachukua mdogo wake Sakina na mama yao aliyekuwa amerudiwa na akili na kuwaficha kwenye gereza la chini ya bahari ili aende akaangalie hatari inatoka wapi.



    Baada ya kumuacha mama Sakina na watoto wake chini ya mwamba bahari, alitoka moja kwa moja hadi kwao na kumkuta mama yake ambaye alishtuka kumuona Nargis.

    “Mama kuna usalama?”

    “Upo, kwani vipi?”



    Nargis hakusema kitu aligeuka na kutoka kasi kuwahi nyumbani kwake mama yake alijaribu kumwita, hakuitikia waka kugeuka alikimbilia nyumbani kwake. Mama yake alipoangalia muda zilikuwa zimepita dakika tano za ziada kwa muda aliompa mwanaye kumtoa roho Thabit.



    Alicheka kwa kuamini Hailat kishamaliza kazi kwa hiyo haraka ya mwanaye ilikuwa ya bure, kwani angekuta mzoga wa mtu. Hailat baada ya kuhangaika kuingia ndani na kushindwa alianza kukosa pumzi ndani ya Thabit hapo alianza kutapatapa kuokoa maisha yake, alifanikiwa kumpigiza sehemu Thabit akalegea na kumuachia. Muda ulikuwa umezidi dakika moja.



    Alikuwa akitweta akiwa na majeraha ya kujipigiza na mwili ulikosa nguvu kwa ajili ya kukosa pumzi kwa muda mrefu. Akiwa bado anajikongoja pembeni mwa mwili wa Thabit, kwa mbali alisikia kishindo cha mdogo wake kikija kwa kasi. Aliuacha mwili wa Thabit uliokuwa umelala chini ukitokwa na damu kila kona na kutimua mbio.



    Nargis aliingia ndani mwake kwa kasi, jicho lake lilitua kwenye mwili wa mumewe aliyekuwa amelala chini huku akitokwa damu kila kona ya mwili. Alipoangalia ndani ya nyumba vitu vyote vilikuwa vimevunjikavunjika kuonesha kulikuwa na mapigano mazito. Aliuinamia mwili wa mumewe ambaye alikuwa nusu mfu kwa jinsi alivyokuwa.



    Nargis alilia sana kumkuta mumewe nusu mfu huku akiwa hajui hatima ya kipenzi mumewe, mwanaume anayempenda kuliko kitu chochote duniani.



    Alipoangalia mdomoni alionekana ameumizwa sana, macho yake yalimuonesha shambulio lile halikuwa la kibinadamu wala ushirikina wa miti shamba ila nguvu za kijini. Mdomo wa Thabit ulikuwa umeishaanza kuoza na kutoa funza, Nargis kwa haraka alimkojolea Thabit mdomoni na kumpaka mkojo sehemu zote za majereha ili kuua sumu ya kijini ambayo ingeuozesha mwili wake.



    Baada ya kumsafisha Thabit ambaye alikuwa nusu mfu, alimlaza kitandani na kuwatoa wajakazi wake waliokuwa wamefungiwa chumba kimoja. Kabla ya kuondoka aliapa kwenye mwili wa Thabit ambao haukuwa na dalili za kurudiwa fahamu.



    “Naapa kupambana na yoyote hata akiwa mama yangu mzazi kama Thabit atakufa nami nitakufa kwa ajili ya kumpigania. Thabit mume wangu natoka nitapata jibu la tatizo lako.”



    Alimpiga busu shavuni na kuondoka kuelekea nyumbani kwao kupata ukweli wa tatizo la mumewe. Akiwa njiani kwenda kwao alijawa na mawazo juu ya tukio lile la kutaka kuutoa uhai wa mumewe, aliamini vita yake kubwa ilikuwa kwa wanadamu kumbe hata baadhi ya majini.

    Kilichomuumiza roho ni aliyetumwa alipania kumuua mumewe, alitembea kwa mwendo wa kasi huku akilia.



    *******

    Hailat baada ya kufanikiwa kutoroka kumkwepa mdogo wake, alirudi nyumbani akiwa hoi kutokana na kujipigiza sehemu mbalimbali akilazimisha kuingia mwilini kwa Thabit. Mwili ulijaa majeraha na kumfanya atembee kwa shida. Mama yake alipomuona alishtuka , lakini alitumbukia nyongo baada kuyaona matukio yote kwenye mboni za jicho la mwanaye.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    “Vipi imekuwaje tena?” alimuuliza macho yakiwa yamemtoka pima.

    “Mama hata siamini, yule mtu si bure bila kujitahidi kujiokoa angeweza kuniua; alinishika vibaya nikawa mbele siendi nyuma sirudi kila nilivyompigiza alining’ang’ania. Mama ilikuwa aibu nilikuwa nafia tumboni kwa Thabit, mpaka ananiachia nilifanya kazi.



    Mpaka analegea muda umekwisha hata nguvu za kufanya lolote sikuwanazo na muda huo mwanao alikuwa anakuja, sijui angenikuta bado nipo mdomoni kwa mumewe kutokana na jinsi nilivyochoka angeniuliza pale pale. Sasa sijui atajua ni mimi, mama kazi kwako la sivyo mpasuko unaokuja sijui nani atauzima, ila akichelewa kidogo atakuwa mumewe kaoza mwili.”



    “Namsikia anakuja tena kwa kishindo, fanya hivi; nenda chumbani kwangu ili asijue upo wapi.”

    Kabla hajanyanyua mguu Nargis alitua mbele yao kama jini la kutumwa akiwa amebadilika mwili na kuwa mweusi kwa hasira.



    Wote walishtuka kumuona Nargis amesimama mbele yao, alikuwa amebadilika na kuwa mweusi kama kisiki cha mpingo kwa hasira. Aliwatazama wote huku dada yake akiangalia pembeni kwa aibu. Mama yake hali ile aliiona na hali ya hatari ilikuwa imeisha jitangaza mbele yao.



    “Hailat nenda ndani,” Malkia Zebeda alimwambia mwanaye.

    Kabla hajapiga hatua kuelekea chumbani kwa mama yake Nargis aliruka na kusimama mbele ya dada yake.

    “Nataka mnieleze majeraha haya ameyapata wapi?”

    “Utajua tu, mwache akapumzike,” mama yao malkia Zebeda aliingilia kati kunusuru hasira za mwanaye mdogo.



    “Mama... mmetimiza mliyotaka kutimiza mmemuua mume wangu kwa nini?”

    “Nani kamuua?”

    “Ninyi, tena mmeumbuka majeraha ya dada bado mabichi.”

    Hailat moyoni alijuta kutimiza agizo la mama yake kwa kuamini duniani hakuna siri ya zaidi ya mtu mmoja. Aliamini mdogo wake kama atamkamata hataweza kushindana naye kwa vile alikuwa ameumia sana na kuchoka.



    “Nakuuliza kwa nini umemuua mume wangu?” Alimuuliza kwa sauti ya juu yenye ukali wa radi. Hailat hakuwa na jibu zaidi ya kumuangalia mama yake amtetee.

    Mama yao aliona kila dakika Nargis alipanda juu na dada yake alizidi kunywea, kabla hajasema kitu. Nargis alimvaa dada yake ambaye alikuwa ameathiriwa na majeraha na kuchoka kutokana na kukosa hewa kipindi kirefu mdomoni kwa Thabit.



    Akiwa na nguvu za ajabu alimpigiza mfululizo dada yake kwenye kuta za chini ya bahari kuzidi kumtia majeraha mwilini. Hakuwa na uwezo wa kujitetea, mama yao naye alizidiwa nguvu. Nargis alimbana dada yake chini kwa kumshika kwenye koromea, alipania kumuua kama alivyotaka kumuua Thabit.



    Japo aliamini Thabit bado hajafa lakini alikuwa na matumaini madogo ya kuendelea kuishi kutokana na sumu ya kijini kumwingia mwilini.

    Mama yake kuona hali imekuwa mbaya aliwaita walinzi wa chini ya bahari majini Kashi yenye ngozi nyeusi kama lami, yenye nguvu za ajabu za kuweza kupasua miamba. Walipofika walimuondoa Nargis juu ya dada yake huku vidole vikiwa vimeanza kupenya kwenye shingo vikutanie upande wa pili.



    Walimtoa kwa nguvu na kumuweka pembeni.

    Vidole vya Nargis vilianza kupata damu iliyoanza kutoka katika shingo ya dada yake, kama wangechelewa kidogo angemuuliza pale pale. Nargis hakukubali aliendeleza vita na majini Kashi ambayo hayakuwa na ruhusa ya kumpiga zaidi ya kumkamata.



    Kutokana na nguvu za hasira alizokuwa nazo Nargis ilikuwa vita kubwa ya kumtuliza. Aliweza kuwaua majini Kashi matatu. Hapo yaliona yanafanya utani kwani kumkata hivi hivi wasingeweza. Moja lilimpiga kofi zito lililomfanya apoteze fahamu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mama yake aliamuru achukuliwe apelekwe kwenye jela chini ya miamba bahari, walipofika kule chini waliwakuta wanadamu ambao hawakujua wamefikaje kule. Taarifa zilipomfikia malkia Zubeda aliyekuwa na hasira kwa kitendo cha mwanae kukosa adabu kwa ajili ya penzi la mwanadamu.



    Aliwaamuru watu waliokutwa kule chini ya miamba bahari wafikishwe mbele yake, Mama Sakina na wanae walifika mbele ya malkia Zebeda. Kabla ya kujieleza aliona mambo yote kwenye mboni za macho yao, baada kutambua kilichosababisha kuwa kule aliwaruhusu kurudi duniani na kuwaahidi kuwasaidia Sakina aolewe na Thabit.



    Alitumwa kijakazi mmoja kwenda nyumbani kwa Thabit kumpelekea dawa ya kumpaka, alipofika alikuta Thabit amelala kitandani nusu mfu. Alimpaka dawa ile na nyingine alimnywesha, baada ya muda Thabit alirudi katika hali yake ya kawaida.



    Malkia Zebeda alipanga kifungo cha mwanae kiwe miaka kumi chini ya bahari kwa utovu wa nidhamu, lakini adhabu ilipunguzwa miaka mitano huku akimuahidi kama atarudia basi atamfunga milele huku akiwa kipofu.



    Nargis aliumia chini ya miamba bahari huku akipanga siku akitoka atakacho kifanya hakitasahaulika na mauti yake yatakuwa siku ileile. Aliapa kuiteketeza familia nzima ya mama Sakina. Kilichomuuma zaidi kilikuwa ndoa ya Thabit na Sakina mwanamke aliyemsumbua na kumsamehe kwa makubaliano ya kutomfuatilia mume wake.



    Kila alilolifikiria roho ilimuuma, lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali yote hakuwa na uwezo wa kutoka kwenye kifungo muda wote alikuwa chini ya majini meusi Kashi. Nargis hakuamini kuona Thabit anaoa wakati walikubaliana hataoa mwanamke mwingine zaidi yake.



    Lakini maumivu yote yaliyeyuka moyoni na kuapa siku atakayotoka kifungoni ndiyo siku ambayo itakuwa safari yake ya kuzimu. Aliamini katika maisha yake Thabit ndiye mwanaume sahihi kwake ambaye alimpigania mpaka hatua ya mwisho.



    Thabit baada ya kuhakikishiwa Nargis hatamuona tena, alimuoa Sakina kwa msaada wa jini Zebeda Malkia wa bahari ambaye alikuwa chaguo la wote. Lakini kila usiku alimuota Nargis aliyekuwa kwenye mateso mazito chini ya miamba bahari kwa ajili yake. Hali ile ilimkosesha raha kufikia hatua ya kutaka kuachana na mkewe amfuate Nargis lakini hakujua atafikaje chini ya bahari.



    Siku zilikatika huku Thabit akiwa na mkewe Sakina na utajiri alioachiwa na Nargis ukizidi kushamiri. Siku moja usiku ulizuka moto ambao hawakujua umetoka wapi, Thabit na mkewe walichokumbuka ni shuka waliojifunika.

    Moto ule uliteketeza nyumba yote hakuna kilichopatikana.



    Siku ya pili Sakina alirudi kwao na huo ukawa mwanzo wa maisha ya taabu ya Thabit ambaye kila alichokifanya kilikuwa kibaya. Nguo za kuvaa na kula yake ilikuwa matatizo. Alitamani kujiua lakini kifo kilimkimbia, alimkumbuka mkewe Nargis na kuamini kumuoa Sakina ndiyo chanzo cha yote.



    Hakuwa na jinsi zaidi ya kuamua kila siku kushinda na kulala pembeni ya bahari kumsubiri Nargis. Thabit alikuwa mwenda wazimu kamili asiye kumbuka kuoga wala kuchagua chakula. Maisha yake yote duniani aliamua kuyamalizia baharini.



    Wapo waliomuona mwendawazimu lakini yeye alikuwa na akili timamu, aliapa hatatoka baharini mpaka Nargis amalize kifungo chake.Huu ni mwisho wa simulizi yetu, najua unataka kujua baada ya kifungo cha Nargis

    baada ya miaka 50 kizazi cha nargis kinakuja duniani kwa

    mtoto wa nargis aitwae balkees kuja dunian na mambo yalianzia hapa

    sasa endelea

    taratibu ili achukue simu ampigie baba yake amfuate eneo lile ambalo lilikuwa limemuweka katika hali ya hatari.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliponyanyua uso achukue simu iliyokuwa kwenye kwenye dash board, alishtushwa na mwanga mkali kama jua la saa saba mchana. Aliangalia katikati ya bahari palipokuwa kunatoka mwanga ule. Alituliza macho baada ya kumuona mwanamke aliyekuwa amevaa gauni jeupe lilikuwa liking’aa kutokana na mapambo yake.



    Hali ile ilimfanya asahau yalitomtokea muda mfupi na kutuliza macho kumuangalia yule mwanamke aliyekuwa akitembea juu ya maji huku nyuma akisindikizwa na wasichana walikuwa wamebeba vikapu vidogo vilivyokuwa na maua ambayo walimwagia kila hatua ilivyopigwa huku wakiimba nyimbo nzuri.



    Suzana alijikuta akipata ujasiri wa ajabu kwa kufungua dirisha kidogo ili aweze kusikia watu wale walikuwa wakiimba kitu gani. Zilikuwa sauti nzuri kama za kaswida zilizoibwa kwa lugha ya kiarabu. Nyimbo zile zilimvutia na kujikuta akiwa na hamu ya kuwaona watu wale waliokuwa wakitembea juu ya maji huku kwa mstari mbele akitangulia yule mwanamke ambaye usoni kwake kulikuwa kunawaka kama taa na kushindwa kuiona sura yake vizuri.



    Suzana alijikuta akisahau kama wale watu walikuwa wakitembea juu ya maji zaidi ya kushangazwa na sherehe ile ambayo toka azaliwe hajawahi kuona sherehe ya aina ile ya mtu mmoja kutangulia mbele wengine kumfuata nyuma huku wakimuwagia maua na kumwimbia nyimbo nzuri.



    Baada ya muda watu wote walikaa mstari mmoja, kisha yule mwanamke aliyekuwa amepeneza kuliko wote alipita katikati yao na kupigiwa vilegele huku akitupiwa maua. Manukato ya maua yalisambaa mpaka ndani ya gari la Suzana alilokuwa amefungua kioo kidogo kusikia nyimbo alizokuwa anaimbiwa yule mwanamke ambaye alionekana kama bibi harusi lakini muda wote hakumuona bwana harusi wala mwanaume kwenye kundi lile.



    Yule mwanamke alipita kwenye mstari mpaka mwisho alitembea peke yake bila kufuatwa na mtu kisha aligeuka na kuwapungia mkono wenzake ambao nao walimpungia huku wakimrushia maua. Baada ya kutembea kidogo Suzana alimshuhudia yule mwanamke alikunja gauni lake usawa na kifua na kushangaa kumuona akitembea ndani ya maji yaliyokuwa yamemfika tumboni.



    Suzana alijikuta akishtuka na kujiuliza yupo ndotoni au anaona kweli, kilichomshangaza ni umbali aliotoka yule mwanamke akitembea juu ya maji. Lakini cha kushangaza alipokaribia ufukweni alionekana yupo ndani ya maji yaliyomfikia tumboni.



    Aliendelea kumtazama amuone anakwenda wapi, yule mwanamke baada ya kutoka ndani ya maji alitembea juu ya mchanga kulifuata lile gari. Kila hatua ilivyokuwa akipiga ilizidi kumtisha Suzana, alijikuta akimshangaa kutaka kuijua sura yake. Alituliza macho yake kwenye uso wa yule mwanamke aliyekuwa akiisogelea gari huku manukato makali yakizidi kujaa ndani ya gari.



    Kilichomshangaza zaidi ni sura ya yule mwanamke alikuwa akifanana naye kwa kila kitu umbile na sura. Suzana alishtuka na kufunga kioo haraka ili mtu yule ambaye yeye alimuona wa muujiza asiingie kwenye gari. Yule mwanamke alisogea kwenye gari na kuligusa, ajabu baada ya kuligusa lile gari alitoweka ghafla.



    Suzana akiwa anatetemeka alijaribu kuwasha gari kwa mara nyingine, ajabu ya Mungu gari liliwaka aliondoka eneo lile kwa mwendo wa kasi. Alipofika nyumbani kulikuwa kumekucha, alikwenda kuoga haraka ili awahi kanisani kwani muda ulikuwa umekwenda.



    Baada ya kuoga alirudi ndani, lakini alishtushwa na harufu ya manukato ambayo aliyasikia muda mfupi darajani gari lake lilipozima na kuenea hadi ndani ya gari lake. Hakutaka kulifikiria sana lile kwa muda ulikuwa umekwenda, alikwenda kwenye kabati kubadili nguo ili awahi kanisani.



    Baada ya kumaliza kubadili nguo alijikuta akiingiwa na uvivu na kwenda kukaa kwenye kitanda haikupita muda. Usingizi mzito ulimshika na kulala bila kujielewa, aliposhtuka usingizini alishtuka kuiona familia yake yote imesimama mbele yake. Alijiuliza kuna nini, alipojiangalia alijiona alikuwa amevaa nguo za kuendea kanisani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Suzana upo sawa?” Mama yake alimuuliza.

    “Mbona unaniuliza hivyo? Halafu mbona kama wote mlikuwa mnalia kuna nini mbona mnanitisha?



    Nini kimemtokea Suzana mpaka familia yake ikusanyike mbele yake huku wakitokwa na machozi.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog