Search This Blog

NYAYO ZA DAMU - 4

 







    Simulizi : Nyayo Za Damu

    Sehemu Ya Nne (4)





    Nakuahidi kumkomesha Thabit kwa mkono wangu wewe najua si mama huruma, sasa niachie hiyo kazi na kwa vile umemleta mwenyewe humu ndani hatoki,” Hailat alisema kwa hasira baada ya kumuona mdogo wake akiteseka kwa ajili ya wanaume wa kibinadamu.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    “Dada wala Thabit hausiki hata kidogo,” Nargis alimtetea Thabit.

    “Sasa ni nani ninavyo kufahamu hakuna kiumbe kitakacho kutoa chozi zaidi ya Thabit kwa kuwa mapenzi nayajua, vile vile mapenzi upofu. Ona mwili wako ulivyopungua kwa wiki mbili hebu niambie ukweli ili nikusaidie.

    Na sasa hivi mimi na wewe tunaingia vitani kuwaua wanaume wote hatuangalii ameoa au hajaoa kila atakayetua anga zetu tunaye.”

    “Dada Thabit ananipenda na siri hii nimemficha, niliogopa nikimueleza anaweza kuniacha.”



    “Siri gani?”

    Nargis aliamua kumueleza dada yake jinsi mke wa Sule alivyomsumbua na kupania kumtoa dunia.

    “Mdogo wangu unaona jinsi wanadamu wasivyo na maana, sasa yeye lilikuwa linamuhusu nini heri angekuwa na uhusiano na Thabit. Lakini mdogo wangu njia ni ndogo kubali tummalize Thabit ili tujiepushe na wanadamu uishi maisha ya raha.”



    “Dada Thabit ndiye uhai wangu, bila Thabit labda ningechukua uamuzi mzito, kanitamkia toka moyoni mwake ananipenda na hataki kunipoteza.”

    “Mh! Sawa, lakini kumbuka kuna vita kubwa kuliko hii ya mke wa Sule pale tu maisha ya Thabit yatakapoanza kuwa mazuri lazima familia yake itamtaka aoe.”



    “Amesema atakataa.”

    “Na wakimlazimisha.”

    “Kila mwanamke atakayemuoa nitamuua.”

    “Hilo neno, haya ngoja nikamueleze mama yako.”

    Hailat alimuacha mdogo wake na kupeleka taarifa kwa mama yao mzazi sababu ya Nargis kuwa vile.



    HAILAT alimfikishia taarifa mama yake ambaye baada ya kusikia alikaa kimya kwa muda kisha alisema kwa sauti ya upole.



    “Hailat mdogo wako ana vita kubwa kuliko aliyopambana nayo, ya mtu mmoja imemtoa kamasi, ataweza ya familia na walimwengu waliomzunguka Thabit?”



    “Hilo mama nalijua kwani maisha na tabia za wanadamu nazijua vizuri, mama kupenda kubaya hata mimi kuna wakati nilipinga maelezo yetu kuhusu tabia za wanadamu ambao humgeuka kiumbe mwenzake kama kinyonga.”



    “Ni kweli Hailat kwa vile ndiyo ameanza kupenda na ugonjwa wa mapenzi ni mbaya kuliko ugonjwa wowote tuna kazi ya kumuelewesha.”



    “Hilo nalijua, Nargis anampenda sana Thabit haoni hasikii kwa ajili ya Thabit.”

    “Wanadamu ni viumbe wabaya sana kuliko hata nyoka, hebu angalia mateso aliyopata mwanangu kwa ajili ya mtu asiyehusika naye bali tu kiherehere na kufikia hatua ya kutaka kumtoa roho.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mama unajua mwanao kaniudhi sana, siku hizi sitapi chakula changu kwa ajili ya kumuacha mdogo wangu afurahie maisha ya mapenzi na kufanya mauaji ya wanaume wenye wake kupungua.



    Kitendo alichofanyiwa mama nitahakikisha sasa hivi sichagui yoyote nitakayekutana naye mbele yangu awe ameoa au hajaoa tena sasa hivi nguvu zote kwa wanawake wote nitampotezea mbali.”



    “Lakini kabla hujachukua uamuzi huo lazima tukae naye chini tupange naye, naamini vita iliyopo mbele huenda ikatupata hadi sisi.”

    “Kwa kusema hivyo unafikiri tutafanya nini ili kujikinga na balaa linalotaka kuja mbele yetu?” Hailat alimuuliza mama yake.



    “Dawa ni moja, kumuua Thabit.”

    “Etiii?” Hailat alishtushwa na kauli ya mama yake.



    “Najua unashtuka lakini ukweli ndio huo la sivyo kuendelea kwa Nargis kuwa na Thabit kutatuweka katika hali mbaya pengine kupoteza kizazi chetu chote.”

    “Mamaaa,” Hailat alibakia mdomo wazi.



    “Nataka nikuambie kitu, kwa tabia Thabit ni mpole tofauti na wanaume uliokutana nao wewe, tatizo waliomzunguka watataka kuzua chokochoko baada ya Nargis kumtengeneza kimaisha. Hapo itakuwa vita kubwa ambayo moyo unaniuma lazima tutampoteza Nargis na pengine na sisi wote.”



    “Mmh, mama hizi habari mbona nzito, kumbuka kumpoteza Thabit huenda nasi tukaingia katika vita nzito na Nargis kwani hawezi kukubali kumpoteza Thabit alinihakikishia kwa mdomo wake bora apotee yeye na sio Thabit.”



    “Sikiliza nataka tufanye siri moja ambayo Nargis asijue tujifanye tunampenda sana Thabit lakini akili kwenye kichwa. Siku moja nitakutuma ukamuue kwa mkono wako bila mdogo wako kujua.”



    “Mama ni mpango mzuri lakini Nargis lazima atagundua na vita kuhamia ndani.”

    “Wewe ulikuwa na wazo gani?”

    “Tumwite Nargis tumuulize mipango yake na Thabit na baadae tumueleze madhara ya yeye kuwa na Thabit na hatima ya maisha yake kama atang’ang’ania kuwa naye.”



    Walikubaliana kumwita Nargis ili wamueleze hatima ya maisha yake kama atakuwa na Thabit. Hailat alimfuata mdogo wake ambaye alikuwa chumbani kwake amekaa kitandani na Thabit alikuwa amepitiwa usingizi.

    Baada ya kufika kwenye sebule alikaa pembeni ya mama yake kusikiliza alichoitiwa.



    “Nargis,” mama yake alimwita.

    “Abee mama.”

    “Kwa nini unakuwa msiri kwa mambo mazito?”

    “Mama nilijua nitayamaliza mwenyewe kama yangenishinda ningeomba msaada wenu.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwa nini ulikuwa unalia?”

    “Ni hasira mama, wanadamu ni viumbe wabaya sana.”

    “Si tulikuambia?”



    “Ni kweli lakini nitapambana nao mpaka pumzi zangu za mwisho.”

    “Sasa raha ya mapenzi iko wapi, si heri ungeachana na Thabit ili ufurahie maisha.”

    “Mama sina raha ya maisha bila Thabit.”



    “Mmh! sawa, lakini kumbuka vita inayokuja mbele ni kubwa kuliko uliyoimaliza.”

    “Hilo nalijua ila nitaondoa huruma hiyo ndiyo dawa ya viumbe wabishi.”

    “Nargis mwanangu una kazi ya kumzuia Thabit asioe baada ya kumtengenezea maisha.”



    “Amenihakikishia haoi mwanamke mwingine zaidi yangu.”

    “Yeye anaweza kukataa lakini kiumbe chochote kilichokamilika lazima kitatakiwa kuoa ili familia yake ipate watoto wa kuongeza ukoo.”



    “Siyo siri siku zote sikuona mwanaume anayewafaa, dawa yenyewe ulimfanyia mwanaume anakuganda kama ruba.”

    “Mmh sawa, sasa nani?”



    “Utaanza wewe mkubwa ambaye umri unazidi kukimbia.”

    “Mmh, haya lini?”

    “Kesho.”



    Walikubaliana kuanza kampeni ya kumteka Thabit kimapenzi.

    Nargis aliyekuwa amekaa sebuleni alihisi maumivu makali ya kichwa na kupiga kelele za maumivu zilizomshtua Thabit na kutaka kujua kulikoni.



    Nargis aliendelea kupiga kelele huku akijipiga chini, Thabit alimuwahi mkewe na kumshika kabla hajajiumiza zaidi.

    “Vipi mke wangu? Mbona hivyo?”



    “Walimwengu bado hawajachoka kunisakama.”

    “Kuna nini tena mke wangu au bado mke wa Sule anakufuata?”

    “Jirani...Jirani mume wangu,” Nargis alisema kwa sauti ya uchungu.

    “Jirani gani tena?”



    “Mama Sakina na wanaye wanapanga kuniangamiza na kukuchukua wewe, sikubali nitaua mtu.”

    “Mke wangu usifanye hivyo, nitawadhibiti.”

    “Huwezi mume wangu, huwawezi wanadamu wana mbinu za hatari sana.”

    “Kama ni hivyo nitakwenda kuwaeleza kuwa sihitaji kuwa na mtu, nina mke wangu.”



    “Hawawezi kukuelewa Thabit, ninyi wanadamu ni wabishi na mna roho mbaya sana, kosa langu nini mpaka kila mwanadamu kuitaka roho yangu. Ina maana wanaume wameisha mpaka wakung’ang’anie wewe.... Mmh nimeamini aliyosema mama sasa yanajidhihirisha. Nitajua chakufanya.”

    Nargis alinyanyuka kusimama wima kisha alishika mkono kwenye paji la uso kabla ya kutoweka alimwambia Thabit.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Samahani mpenzi, nakuja sasa hivi, nafika kwa mama.”

    Baada ya kusema vile alipotea na kwenda moja kwa moja chini ya bahari, alipofika mama yake alimshangaa kumuona kwenye hali ile.



    “Vipi tena mwanangu?”

    ”Wanadamu mama.”

    “Wamefanya nini tena?”



    “Wanapanga kuninyang’anya Thabit wangu.”

    “Hili mbona nililijua mapema? Wanadamu kazi yao kusubiri utengeneze kisha wachukue. Ni viumbe wanaopenda kutumia nguvu kuny’ang’anya.”



    “Tena mama yao ndiyo kapanga kuwapeleka kwa mganga ili wamtengeneze mume wangu awapende wao na kuninyang’anya.”

    “Mmh, sasa unafikiri utafanya nini?”

    “Mama mimi sitakuwa na huruma nao nitawafutilia mbali.”



    Mama yake alimwangalia kwa muda mwanaye kisha alimvuta karibu na kumnong’oneza kwa muda kisha alimuuliza mwanaye;

    “Kufanya hivi unaonaje?”



    “Mmh, ngoja nijaribu, lakini..”

    “Hakuna cha lakini kama watataka kushindana tumia nguvu hizo kwa vile sasa hivi tupo karibu na wewe muda mwingi kuangalia maisha yako kwa vile tunajua vita na wanadamu ni nzito.”



    “Sawa mama, acha nimuwahi mume wangu maana nimemuacha yupo katika sintofahamu.”

    “Haya muwahi mumeo ila dada yako akijua patachimbika.”

    “Basi mama usimwambie.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Hakuna tatizo muwahi mumeo.”

    Nargis aliondoka huku akiwa na uso wa tabasamu tofauti na alivyokuja, alikuwa na siri aliyopewa na mama yake mzazi Malkia Zebeda.

    ***

    Siku ya pili mama Sakina aliwaamsha wanaye alfajiri ili kujiandaa kwenda kwa mganga kumfanyia dawa Thabit amuoe mmoja wa wale mabinti zake wawili. Binti mkubwa aliyeitwa Sakina alikuwa wa kwanza kuingia bafuni kuoga, bafuni kulikuwa na kioo kikubwa kilichoonesha mwili wa mtu kwa sehemu kubwa.



    Sakina baada ya kuingia bafuni alianza kuoga huku akiutaza mwili wake kwenye kioo, kila dakika aliutazama mwili wake na kuamini anafaa kuwa mke wa Thabit kijana tajiri. Kila dakika alipokuwa akioga alijitazama kwenye kioo na kuusifia mwili wake.



    Alipomaliza kuoga alisimama tena kwenye kioo na kujitazama huku akijifuta mwili, alipokuwa akijifuta alimuona Nargis kwenye kioo ikionesha yupo nyuma yake, alishtuka sana. Aligeuka kwa haraka ili amuone lakini ajabu hakuona kitu chochote nyuma yake.



    Alikwenda hadi mlangoni na kuuangalia labda mlango upo wazi kuna mtu kaingia na kutoka. Lakini mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani, alipuuza kuiona ile taswira ya Nargis kwenye kioo. Baada ya kuridhika mlango umefungwa na hakuna mtu mwenye uwezo wa kuingia ndani, alirudi na kusimama tena mbele ya kioo kujiangalia.



    Wakati akijifuta maji ili atoke baada ya kuitwa na mdogo wake aoge haraka ili nao waoge na kuwahi kwa mganga. Sakina alishtuka tena kuiona tena sura ya Nargis kwenye kioo, alitulia bila kugeuka na kumuona Nargis alikuwa na kitu kama unga mweusi aliokuwa ameshikilia kwa mikono miwili.



    Wasiwasi ulianza kumuingia na kuamini nyuma yake hakukuwa na kitu cha ndotoni bali ni kweli kuna mwanamke tena mwanamke wa Thabit waliopanga kumtoa ndani ya nyumba. Hakukubaliana na ile hali baada ya kumuona yule mwanamke kwenye kioo akimsogelea.



    Alipogeuka alikutana kweli na Nargis alipiga kelele za woga alizozisikia mama na mdogo wake.

    Lakini alikuwa amechelewa Nargis aliupuliza unga mweusi uliokuwa mkononi mwake ambao ulimpata Sakina mwilini. Dakika ile ile mwili wa Sakina ulianza kuota manyoya kama ya mbwa, Sakina alishtuka kuuona mwili wake umegeuka kama wa mnyama.



    Wakati huo Nargis alikuwa amepotea, hakuamini kama kweli mwili wake umeota manyoya kama mbwa. Ili kuhakikisha, aligeuka kwenye kioo kuangalia kama kweli anachokiona ni kweli au ni njozi za mchana. Alipojiangalia kwenye kioo alijiona amegeuka mbwa mwenye umbile la kibinadamu.



    Alishtuka na kupiga tena kelele ambazo kila mmoja tena alizisikia na wakati huo mama na mdogo wake walikimbilia bafuni kuangalia Sakina amepatwa na nini.



    “Najua kiasi gani unavyoteseka kwa ajili yangu, yote ni mapenzi ya dhati. Nargis mimi nipo tayari kwenda kuishi na wewe chini ya bahari au popote upendapo ili kuona furaha ya moyo wako inakuwepo kila siku huku tabasamu lako mwanana likirudi usoni kwako kama zamani. Nakupenda Nargis sipendi uumie kwa ajili yangu,” Thabit alisema huku akimnyanyua Nargis alipopiga magoti.

    “Asante mpenzi.”

    Nargis alimkumbatia Thabit kwa furaha baada ya kukubali ombi lake, alijiuliza Thabit amekubali mama yake ataupokea vipi uamuzi wake wa kwenda kuishi na mumewe chini ya maji huku akipambana na familia ya Thabit.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kupigwa na mfagio na viatu Sakina aliamua kutoka nje ya nyumba huku akiwa na majonzi mazito kutokana na hali iliyomkuta, alijisogeza mpaka upenuni wa ukuta na kujikunyata akiwa aamini ile hali ya yeye kugeuka mbwa.

    Alijikuta akilia kwa uchungu kwa sauti ya juu ambao ilikuwa ya mbwa, sauti yake ilikuwa karaha masikioni mwa watu. Aliamua kulia kimya kimya kwa kuhofia kugeuka karaha kwa mama na mdogo wake waliomuona ni mbwa.

    Mama na mdogo wake baada ya kumtoa nje yule mbwa bila kufahamu ndiye Sakina, walianza kumtafuta Sakina kila kona, lakini bila mafanikio.

    Kila kona waliyofika walimwita lakini hawakusikia sauti yake na kuzidi kuchanganyikiwa Sakina atakuwa wapi.

    Sakina aliwasikia wakimwita na kumpita alipokuwa amejilaza na kuzunguka nyuma ya nyumba huku wakimwita kwa sauti ya juu. Japo aliwasikia lakini alishindwa kuitikia kwani alipoitikia alitoa sauti ya mbwa kitu ambacho kingefanya afukuzwe kabisa eneo la pale.

    “Sasa atakuwa wapi Mungu wangu,” mama Sakina aliuliza akiwa amejishika mkono mmoja kiunoni.

    “Mama hata mimi nashangaa.”

    “Sasa atakuwa amekwenda wapi?”

    “Mama haya ni maajabu dada Sakina alikuwa akioga muda si mrefu, lakini cha ajabu aonekani, kingine kilichonishtua ni kutoka mbwa bafuni.”

    “Ile sauti ya dada yako ilitokea wapi?”

    “Mama, wote si tumesikia akipigia kelele bafuni.”

    “Sasa atakuwa wapi?”

    “Hapo ndipo nazidi kuchanganyikiwa.”

    “Sasa tutafanyaje, na muda unazidi kukatika, nilitaka tuwahi kwa mganga kisha turudi kuendelea na mambo mengine,”

    “Hii kali haijawahi kutokea dada alikuwa bafuni haonekani mbwa ambaye hakujulikana kapitia wapi tumemkuta bafuni.”

    “Mimi nafikiri hakuna haja na kupoteza muda tufanye twende kwa mtaalam, kama Sakina alikuwa hataki kwenda siangesema kuliko kutukimbia.”

    “Mama una uhakika gani kama ametukimbia, kapitia wapi?”

    “Hii siri unaijua wewe na dada yako, kwanza sioni umuhimu wa kwenda kwa mganga kama mnanichezea akili.”

    “Mama kilichotokea hata mimi sielewi wala hakuna ujanja wowote.”

    Wakati wakibishana wingu zito lilitanda na kuteremka mvua nzito, Sakina alijibanza pembezoni mwa nyumba yao kujikinga na mvua ile. Lakini mvua ilikuwa kubwa ya mawe yenye upepo mkali. Sakina alijikuta akilowa lakini alishindwa kuingia ndani kwani aliamini bado wanamwona mbwa.

    Yalikuwa mateso ambayo kwake hakujua sababu ya yeye kufanywa vile, mvua iliendelea kumpiga pamoja na baridi kali viliendelea. Kila mungurumo alijikunja kwa hofu katika maisha yake aliogopa mlio wa radi ya mvua.

    *******

    Baada ya mvua kukatika alipita mtu mmoja ambaye alikuwa mtaalam wa tiba za asili, macho yake yenye kuona mbali alipomwangalia Sakina mwanzo alimwona ni mbwa wa kawaida. Lakini tafsiri ya macho yake yalimuonesha yule si mbwa wa kawaida bali mwanadamu aliyegeuzwa mbwa.

    Alijiuliza nani aliyefanya vile, alitoa chumba yake ndogo yenye mavumba meupe na kuyanusa baada ya muda aliiona picha ya Sakina kugeuzwa mbwa ikijirudia.

    Baada ya kugundua hali ile alicheka mwenyewe kisha alijisongeza mpaka kwenye nyumba yao Sakina na kubisha hodi bila kumfanya lolote yule mbwa. Mdogo wake Sakina alifungua mlango na kumkaribisha ndani mgeni aliyekuwa mgeni machoni mwao.

    “Karibu.”

    “Asante,” mgeni aliitikia huku akiingia ndani.

    “Karibu mgeni,” mama Sakina alimkaribisha mgeni baada ya kuingia ndani.

    “Asante, najua mlikuwa na safari,” mgeni alisema baada ya kukaa kwenye kochi.

    “Umejuaje?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Na safari yenu mmeikatisha baada ya kupotea mtu mmoja.”

    “Jamani mbona makubwa umejuaje?”

    “Kibaya zaidi mmemkana mwenzenu na kumfukuzia nje bila huruma ambapo alinyeshewa na mvua yote.”

    “Baba mbona hatukuelewi,” mama Sakina alishindwa kumwelewa mgeni.

    “Ni vigumu kunielewa, kumbukeni safari yenu ndiyo iliyozua tafrani yote ya mwanao kugeuzwa mbwa.”

    “Mbwa, ina maana yule mbwa tuliyemkuta bafuni ndiye Sakina?”

    “Ndiye yeye.”

    “Mungu wangu, nini kilichomgeuzwa mbwa?”

    “Ji..ji....”

    Kabla hajaendelea upepo mkali ulivuma mule ndani na kusababisha vitu vyepesi kutupwa nje ya nyumba sauti ya mbwa ilikuwa juu ikionesha kuna kitu kinamtisha. Mtaalam alipotoka alishangaa kutomkuta yule mbwa. Wakati huo upepo mkali ulikuwa ukizidi kujaa ndani na kusababisha vumbi iliyofanya watu wasionane.

    Yule mgeni alinyoosha mkono na kuyasema maneno katika lugha ya kiarabu akiukemea, baada ya kunyoosha mkono upepo ulitulia, kilichowashtusha wote kilikuwa kumuona jini Nargis mbele yao akiwa ameshika mkono kiunoni kitu kilichowashtua wote waliokuwemo mule ndani.





    Nargis, baada ya kupata upinzani mkubwa kutoka kwa mtaalamu yule, aliamini kabisa upinzani alioambiwa na mama na dada yake juu ya ubaya wa wanadamu, yalikuwa yakitimia. Baada ya kumchukua Sakina katika umbile la mbwa na kumficha kwenye pori lililotisha lenye majoka na wanyama wakali.



    Sehemu aliyomficha walinzi wake walikuwa nyoka wakubwa waliokuwa wamemweka kati. Wakati huo alikuwa amemrudisha kwenye umbile la kibinadamu. Sakina akiwa katika umbile la kibinadamu, aliingiwa na hofu kutokana na nyoka wakubwa yaliyokuwa karibu yake lakini hakuna hata moja lililokuwa na habari naye.



    Nargis wakati akimpeleka kwenye pori lile aliokota kamba ambazo alizitawanya na kisha kumfanyia Sakina kiini macho ambacho aliamini kabisa wale ni nyoka. Lakini kama angekuwa na ujasiri angezipita zile kamba na kukimbia bila kufanywa lolote japo asingefika mbali lazima angeangukia mikononi mwa Nargis.



    Nargis baada ya kumuacha Sakina porini sehemu aliyoamini hakuna wa kumuona, aliondoka na kwenda kutafuta msaada kwa mama yake ambaye angesaidia kumpa ushauri kwani aliamini kwake ngoma ni nzito baada kuuona uwezo wa mtaalam ambaye alimtishia maisha.



    Nargis alikwenda chini ya maji kuonana na mama yake Malkia Zebeda kumweleza masahibu yaliyomkabili kuhusiana na ndoa yake kwa wanadamu kuiandama kila kukicha. Mama yake alipomuona alijua mtoto wake ana jambo ambalo lilimnyima raha.



    Kati ya vitu ambavyo malkia Zebeda vilivyo mkosesha raha ni pamoja na wanaye kuteswa na mapenzi ya wanadamu, ambao walikuwa wakiwapa mateso mazito kwa kulazimisha mahusiano nao. Ilikuwa ni vigumu kwa jini kukubali kuachana na mpenzi wake hasa anapoonja penzi la mwanadamu lenye joto ambalo huwachanganya majini.



    Malkia Zebeda mara nyingi huwakanya watoto wake ambao huwa wabishi na mwisho wa siku hupatwa na majuto. Hailat dada yake Nargis naye alikuwa mbishi lakini mwisho wake aliwachukia wanadamu mpaka kuanzisha kampeni ya kula nyeti za wanaume waliooa ambao walimdanganya na siku ya mwisho aliambulia maumivu.



    Alimuona Hailat ana afadhali kuliko mdogo wake ambaye aliamini kumficha mwanadamu chini ya maji ni vita kubwa. Aliwaogopa wanadamu ambao viumbe wenye hila mbaya ambayo inaweza kuupoteza ukoo mzima. Aliona tatizo la Nargis ni baya ambalo kwake alitafuta mbinu ya kukabiliana nalo.



    Malkia Zebeda alituliza akimtazama mtoto wake ambaye uso wake ulionesha yupo katika kipindi kigumu maishani mwake. Toka alipoanzisha uhusiano na Thabit na kwenda kulala kwa bwana yule, amekuwa mtu mwenye matatizo aliyekosa raha kwa ajili ya kulilinda penzi lake kwa mumewe. Mama yake aliona matukio yote yaliyomtokea mtoto wake kwenye mboni za macho ya mwanaye.



    Hakutaka kuyasema, aliyoyaona kwenye macho ya mwanaye, alimwuuliza kama hajui kitu ili apate ukweli wake.



    “Mmh, tatizo gani tena?”

    “Mama nilikuwa na mawili japo moja wakati najiandaa kuleta ujumbe wangu lilitokea ghafla, nilipotaka kupambana nalo maji yalikuwa mazito.”



    “Ni kweli yote yamejionesha kwenye macho yako nilitaka useme mwenyewe kwa mdomo wako.”

    “Mama utanisaidiaje?”

    “Mwanangu nilikueleza tokea mwanzo kuwa unachoking’ang’ania ni mauti yetu.”

    “Mama nahitaji msaada siyo malumbano.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Msaada wangu ni mmoja tu, kuokoa maisha yetu na ukoo wetu, ni wewe kuachana na Thabit.”

    “Mama suala la kuachana na Thabit, sahau, la muhimu ni kunieleza moja mtanisaidia kwenye vita hii au hamuwezi.”



    “Kwa vile kisu kimegusa mfupa, hatuna jinsi kuingia vitani, uwezo wa huyo mganga ni mdogo sana. Tutaweza kummaliza bila kutusumbua, lakini wavumao baharini mwanangu si papa tu, mtihani unaokuja mbele ambao nauona ni hatari kwa maisha yatu.”



    “Mama kama kufa kila kiumbe kitakufa na kila kiumbe hufa kwa ahadi kilichoumbwa nazo mbele ya Mungu, kuongopa kifo ni kijidanganya.”



    “Kwahi upo radhi tufe kwa ajili ya mapenzi yako.”



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog