Simulizi : Nyayo Za Damu
Sehemu Ya Tatu (3)
Alijilaumu kwa kushindwa kuwa msikivu na
matokeo yake kuishi kama nguruwe tena kwenye banda chafu lisilostahili mwanadamu
kuishi. Alijiuliza ataishi vile mpaka lini na kukumbuka kauli ya Nargis ya yeye
kuchinjwa mwishoni mwa wiki akichanganywa na nguruwe
wengine.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kufika
hapo alilia huku sauti yake ikiwa kero masikioni mwa watu kutokana na kusikika
zaidi kutokana na hali ya hewa ya usiku kuwa imetulia. Ubaridi wa usiku nao
uliendelea kumtesa kwa kumpiga bila huruma.
Njaa
na kiu baada ya kumshika sana na kumfanya aanze kuona kizunguzungu na kiza
kinene. Miguu haikuwa na nguvu alijilaza kwenye tope huku baridi likizidi
kumuingia mwilini. Kila dakika alimuomba Mungu amchukue kwani mateso yalikuwa
makubwa sana maishani mwake.
Sehemu chafu inanuka
asiyostahili mwanadamu kuwepo, njaa kali na kiu hakuna chakula zaidi ya chakula
kichafu cha nguruwe wale. Akiwa amejikatia tamaa alishtuka kujiona ametolewa nje
ya banda akiwa katika umbile lake halisi la
kibinadamu.
Alishangaa na kujiuliza nani aliyemtoa
na hali ile ni kweli au ni kiini macho, kabla hajapata jibu alimuona Nargis
amesimama mbele yake. Mke wa Sule alichanganyikiwa na kuamini ile ni nafasi
pekee ya kuomba msamaha, alipiga magoti mbele ya
Nargis.
“Nargis najua nimekosa naomba
unisamehe.”
“Mariamu sicho kilichonileta, nimekuletea chakula na maji
kwa kujua huwezi kula chakula na maji yake ya
nguruwe.”
“Ni kweli Nargis nateseka mwenzio naomba
unisamehe sirudii tena,” Mke wa Sule aliomba msamaha akiwa amepiga magoti huku
akilia kilio cha majuto.
“Mariamu kuwa muelewa,
sikufuata ujinga wako bali nimekuletea chakula usife na njaa na utakuwa ukila
mara moja kwa siku mpaka siku utakayochinjwa na nyama yako kuliwa na watu,”
Nargis alisema kwa sauti isiyo na mzaha hata
kidogo.
“Nargis najua kiasi gani nimekukosea, nipo
chini ya miguu yako sitarudia tena.”
“Mariamu wewe si wa kusamehewa na
ukizidi kuniudhi nitaongeza mateso ya kuutia madonda mwilini wako na kukufanya
utolewe kwenye banda na kukufanya utangetange kwa kupigwa mawe kila atakapo
kimbilia na kifo chato kitatokana na kipigo cha
wanadamu.”
“Usifanye hivyo Nargis, nakuahidi
siwezi kurudia na nikirudia nifanye lolote.”
“Kama uliweza kutaka
kuniangamiza na dawa ulibeba pamoja na kukutisha kila kona bado dhamila yako ya
kuniangamiza ilikuwa pale pale. Wewe ni kenge huwezi kusikia mpaka utoke damu
masikioni.”
“Basi niue kabisa kuliko kunitesa
hivi.”
“Sina uwezo huo ndio maana kifo chako
kitakuwa cha kupigwa na kuzilai kisha utachinjwa.”
“Na leo sikuachi
mpaka uniue nifanye lolote sikuachi,” mke wa Sule alijitutumua.
“Kabla
hujanigusa nitakutengeneza kiumbe wa ambabu afadhari nguruwe, kwanza
usinipotezee muda wangu kula chakula niondoke
zangu.”
Mke wa Sule kutokana na njaa aliyokuwa
nayo hakuona umuhimu wa kubishana zaidi ya kukishambulia kile chakula
kilichokuwa kitamu na maji matamu ambayo hakuwahi kula na kunywa maishani mwake.
Baada ya chakula hakujua Nargis amepanga kumfanya nini, baada ya kula
alimshukuru Nargis ambaye hakuihitahi shukurani ya kinafiki.
“Sina
haja ya shukurani zako mwanaume shetani usiye na huruma.”
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hapana Nargis ni
mawazi mabaya ya kuamini majini ni viumbe vibaya lakini wewe umeonesha kumbe ni
viumbe wapole na wenye huruma. Nimejifunza kupitia kwako nisamehe usinifanye
kitu chochote kibaya mateso ya muda mfupi nimetamani kufa lakini sikuwa na uwezo
huo.
Chonde Nargis usinitese tena inatosha Nargis
nateseka kumbuka mimi ni mwanadamu sifai kukaa na wanyama tena wachafu kama
nguruwe.”
“Nimekuleta huku na maana yangu, wewe si
ulikuwa ukitafuta maji na mifupa ya nguruwe ili uniangamize nimeamua nikulete
kabisa ukae nao ili uweze kuniteketeza vizuri”
“Nisamehe Nargis ni
shetani tu kanipitia nipo chini ya miguu
yako.”
“Nafikiri umeshiba,
rudi katika umbile lako la kinguruwe ili urudi kwa wenzako, naona unanipotezea
muda sicho kilichonileta. Nimekusamehe husameheki, nimekutisha hutishiki, bado
unaitaka roho yangu bado unaomba
nikusamehe.
Nargis baada ya kusema vile
alinyooshea kidole mke wa Sule ambaye kabla hajasema kitu alibadilika na kuwa
nguruwe na kurudishwa kwa nguruwe wenzake.
Mke wa
Sule alipojaribu kumuomba msamaha lakini alitoa mlio wa nguruwe, hakuwa na jinsi
zaidi ya kunyamaza kimya.
Sule alichanganyikiwa
baada ya mkewe kutoonekana kwa siku tano, wasi wasi wake mkubwa ulikuwa kwa
Nargis mpenzi wa Thabit lakini alishindwa kutibitisha kuwa Nargis ndiye chanzo
cha matatizo ya mkewe kwa vile hakuwa na ushahidi japo aliamini
hivyo.
Na aliogopa kumuuliza Thabit kwa kuwa ataulizwa ilianzaanzaje
mpaka kufikia hatua ile. Wazo la haraka lilikuwa kwenda kwa mtaalamu wa tiba za
asili mwenye uwezo wa kushindana na majini ili kujua mkewe siku tano alikuwa
wapi. Kama siku tatu alizopotea alikuwa Morogoro kwa kutembea kwa miguu baada ya
kukutana na Nargis.
Siku aliyopanga kwenda kwa
mganga ilikuwa ndiyo siku baadhi ya nguruwe kuchinjwa kwenye banda alilomo mke
wake. Mke wa Sule aliendelea kuteseka kuishi maisha magumu na nguruwe katika
banda moja na kula mara moja kwa siku.
Siku hiyo ilipofika aliingia
mtu bandani na kuhesabu nguruwe wa kwenda kuchinjwa na mke wa Sule alikuwa
katika idadi ile. Walipakiwa kwenye gari kupelekwa sehemu ya kuchinjia, mke wa
Sule alitamani atoe sauti kuwa yeye si nguruwe lakini kila alipotoa sauti
ilitoka ya nguruwe.
Sule naye alidamka asubuhi kuwahi kwa mtaalamu
ambaye hakuwa mbali alikuwa Mtoni kwa Azizi Ali. Kwa kuwa mganga huwa na watu
wengi alipandia gari Buguruni-Chama.
Ilikuwa ajabu
ya Mungu alipotelemka alijikuta yupo Kisarawe mkoa wa Pwani, hakuamini kwani
alipanda daladala iliyopigwa debe Buguruni Mtoni-Mtongani. Ilibidi apande
daladala nyingine iliyokuwa ikirudi mjini.
Baada ya kupanda daladala
alitulia kitini akiwa haamini kama kweli alipanda gari la kuelekea Kisarawe na
si Mtoni kwa Azizi Ali. Baada ya muda gari lilirudi mjini ili aelekee Buguruni
kwa mganga kuulizia habari za mkewe. Gari lilirudi hadi Buguruni ambako Sule
alipanda gari liendalo Mtoni kwa Azizi Ali.
Gari
lilipoanza kuondoka alipitiwa na usingizi mzito mpaka linafika mwisho wa safari
Mtoni Mtongani alikuwa bado amelala. Kutokana na ugumu wa usafiri gari
lilipofika abiria waliwahi kuingia na kukaa kwenye siti, hakuna aliyejua kama
Sule alitoka na daladala ile Buguruni.
Safari ilianza tena kuelekea
Buguruni, Sule alishtuliwa na konda kumdai pesa.
“Mzee acha kulala
nipe nauli.”
“Mara ngapi?”
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mzee sijadai nauli
kwa mtu yoyote toka abiria waingie.”
“Kaka si nimekupa mia tano
ukanirudishia mia mbili na hamsini muda mfupi uliopita?”
“Mzee wangu
sijachukua hata senti ya mtu.”
Mara konda alitoa shingo nje kuita
abiria baada ya daladala kusimama Vetenari kwa kupaza sauti.
“Buguruni
mia mbili,” kauli ile ilimshtua Sule na kuhoji.
“Konda tunatoka
Buguruni au tunarudi Buguruni?”
“Mzee tunatoka Mtoni tunakwenda
Buguruni.”
“Mungu wangu ina maana gari mpaka
linafika na kurudi mimi nilikuwa nimepitiwa na usingizi?”
“Kwani
ulikuwa unakwenda wapi?” abiria mwenzake aliyekuwa pembeni yake
alimuuliza.
“Mtoni kwa Azizi Ali na nilipandia Buguruni, ajabu
usingizi wa ajabu ulinipitia na kujikuta narudi nilipotoka.”
“Ooh,
pole unaweza kushukia hapa ili upande gari lingine.”
Sule alitelemkia
Vetenari kwa hasira ya kupotea na gari mara mbili aliamua kutembea kwa miguu
kwani aliamini kwa njia ya mkato ya kupitia Mwembe Yanga hawezi kuchelewa.
Alitembea kwa mwendo wa kasi kuokoa muda, lakini alijikuta akitembea mwendo
mrefu bila kufika. Kitu kilichomfanya achoke sana, kingine kilichomshangaza
mazingira aliyokutana nayo yalikuwa mageni
kwake.
Sule alitembea mpaka ikafikia hatua akawa
haoni anapokwenda kiu ya maji ya kunywa na njaa kali vilimshika na kiza kilianza
kuingia. Hakuamini kutoka Vetenari kwa miguu hadi Mtoni kwa Azizi Ali kunaweza
kuchukua masaa kumi.
Alitafuta mti wa mwembe uliokuwa mbele yake na
kujipumzisha.
Hayo yalikuwa kwa Sule, mkewe naye baada ya kuchanganywa
katika kundi la nguruwe wa kuchinjwa, walifikishwa kwenye machinjio na kupangwa
foleni kwa kuuawa mmoja mmoja. Mke wa Sule alikuwa wa tatu katika nguruwe kumi
waliokuwa wakichinjwa siku ile.
Alishuhudia nguruwe wa kwanza
akitandikwa nyundo nzito kichwani na kupoteza fahamu kisha alichinjwa, wa pili
ilikuwa vile vile alipokea kipigo kizito na
kuchinjwa.
Ikafuata zamu ya mke wa Sule ambaye
haja ndogo na kubwa vilimtoka pamoja na kulia kilio huku akiomba msamaha kuwa
yeye si nguruwe bali mwanadamu. Lakini kauli yake hakuna aliyeisikia zaidi ya
kutoa mlio wa nguruwe.
Alisogezwa kwenye sehemu ya shuruba kwa mtoa
ufahamu wa nguruwe, aliinua nyundo nzito juu tayari kuishusha kwenye kichwa cha
mke wa sule.
Mke wa Sule alifumba macho kusubiri kipigo kile, lakini
kabla nyundo haijashushwa mtu aliingia bila hodi na kusema.
“Samahani
ndugu usimuue huyo nguruwe.”
“Kwa sababu gani?” mpiga nguruwe
aliuliza.
“Nilikuwa namtaka huyo nguruwe.”
“Aah, bwana mbona
wapo wengi kumbe ni hilo usinipotezee muda.”
“Huyu ndiye niliyempenda,
na nitamnunua kwa kiasi chochote nimempenda kwa kuwa ni jike, kwani mimi ninaye
dume msumbufu nikimpelekea jike litapunguza usumbufu pia ninataka nguruwe
wengi.”
“Hakuna tatizo.”
Mke wa Sule
hakuamini kupona katika kifo kile japo aliamini yule atakayemchukua atampeleka
katika banda lingine la nguruwe na kumfuga. Kibaya zaidi ni kupandwa na nguruwe
dume ili azae watoto ambao yule bwana atatunza kwa ajili ya
biashara.
Mke wa Sule alisogezwa pembeni na kuchukuliwa nguruwe
mwingine ambaye alimuona akichukua kipigo kimoja na kutulia. Moyoni alijisemea
“Nilikuwa mimi nakutwa na yale, eeh Mungu niepushe na shari hii na nyingine
tena.”
Baada ya yule bwana kulipa pesa alitoka sehemu ya machinjio na
nguruwe wake, alimpandisha kwenye gari na kuondoka naye.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati akiwa ndani
ya gari usingizi mzito ulimpitia mke wa Sule, aliposhtuka alijikuta kwenye
umbile la kibinadamu, sehemu iliyokuwa ngeni kwake, ghala harufu ya manukato ya
Nargis ilisikika nyumba yake.
Alipogeuka alimuona akiwa amesimama
ameshika mikono yake kwa mbele kwa sauti ya upole
alisema.
“Mariamu.”
“Abee.”
“Nina
imani baadhi ya viumbe hawajui thamani ya maisha yao na mmoja wapo ni wewe,
nilikutoa kwa muda kwenye kifo kile cha kuchinjwa lakini baada ya mazungumzo
haya ukinijibu vizuri toka chini ya moyo wako nitakusamehe na kukurudisha kwa
mumeo ambaye kutwa nzima hajui anakwenda wapi.
La
utashindwa nitakurudisha kabla nguruwe wale hawajachinjwa na wewe uwe mmoja
wapo. Mariamu kipi kinachokukera mimi kuwa na
Thabit?”
“Hakuna basi tu
upumbavu.”
“Upumbavu, roho mbaya?”
“Roho
mbaya.”
“Shida yako nini
kwangu?”
“Nilikuwa na wasiwasi huenda wewe ni jini.”
“Baada
ya kujua mimi ni jini?”
“Najua majini ni viumbe
wabaya hivyo ungeweza kutudhuru.”
“Kwa hiyo ukaamua kunidhuru
mimi?”
“Ni kweli nilitaka kufanya
hivyo.”
“Kwa hatua hiyo mwanadamu na majini yupi
kiumbe mbaya?”
”Mwanadamu.”
“Mbona mimi
sijakudhuru?”
“Nisamehe Nargis, sirudii tena kumbe
ninyi ni viumbe wema sana sikujua.”
“Sasa sikiliza hili ni onyo la
mwisho, kama hutasikia nitajua cha kukufanya ila sitakuwa na simile wala kuuliza
zaidi ya kutenda.”
“Nimekuelewa dada yangu sirudii
tena tamu ya ukaidi wangu nimeiona kama nisiposikiliza sitakuwa mwanadamu mwenye
akili timamu.”
“Yangu yameisha rudi nyumbani
kwako.”
“Asante Nargis”
“Mariamu
sihitaji asante zako za kinafiki zaidi ya kuyatekeleza yote
niliyokwambia.”
“Niamini Nargis huyu ni Mariamu mpya msikivu na
nyenyekevu.”
“Mmh, haya tutaona.”
Baada
ya kauli ile Nargis alipotena na kumuacha mke wa Sule akishangaa yupo wapi na
atarudije nyumbani. Baada ya kutuliza akili alijishangaa kujiona yupo nyuma ya
nyumba wanayoishi. Alizunguka na kutokea upande wa mbele, alishangaa kukuta
mlango wa chumba chao umefungwa.
Kwa vile alijua
funguo wanapoweka alifungua mlango na kuingia ndani, kutokana na uchovu
alipitiwa usingizi mzito.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sule naye alishtuka
usingizini saa saba za usikukutokana na mvua kali ya upepo iliyokuwa ikinyesha,
alichanganyikiwa asijue pale alipokuwa ni wapi na wapi akimbilie kutokana na
kiza kinene na mvua kali.
Yalikuwa mateso mazito
kwa Sule ambayo hakuwahi kukumbana nayo katika maisha yake. Kingine kilichokuwa
kikimchanya ni kilio cha mtoto mdogo mwenye sauti kama ya mtoto wake aliyeonesha
naye ananyeshewa na mvua na kuomba msaada wa baba
yake.
Sule alijikuta akitapatapa kuifuata sauti ya
mtoto yule ambayo hakujua inatokea wapi. Alijikuta akisahau mateso yake na
kuanza kuifuatilia sauti ile kwa kuamini akifanya uzembe wowote mtoto wake
anaweza kupoteza maisha kwa mvua ile kali iliyoambatana na upepo
mkali.
Sauti ya mtoto ulizidi kutanda katika ngoma
za masikio ya Sule na kumfanya azidi kuifuata ili ajue mwisho wa sauti ile.
Alizidi kuifuata ile sauti huku akimuomba Mungu amsaidie amuone mtoto wake akiwa
hai.
Katika kumbukumbu zake alikumbuka aliamka
asubuhi kuwahi kwa mganga ili ajue sababu ya kupotea kwa mke wake. Lakini
alijikuta akitokewa na mambo ya ajabu ya kupotea kila alipotaka kwenda kwa
mganga kitu ambacho hakikuwahi kumtokea toka
azaliwe.
Sauti ya mtoto iliendelea kulia huku
akiendelea kuifuata na mvua nayo ilizidi kumpiga huku baridi la usiku nalo
likimuingia mpaka kwenye mifupa. Ajabu nyingine alijiona akitembea umbali mrefu
mpaka aliposhtuka kulikuwa kumepambazuka nakujishangaa kujiona yupo karibia na
nyumbani kwake miguu ikiwa amejaa tope kwa kutembea peku kwenye
mvua.
Ajabu alipofika nyumbani kwake sauti ile ya
mtoto wake ilisikika ikitoka ndani kuashilia mwanae ndani analia. Alipofika
aliingia ndani kwani mlango ulikuwa umefunguliwa, ndani alimkuta mtoto kitandani
peke yake. Mara aliingia mkewe aliyetoka
msalani.
“Vipi tena mwenzetu mbona hivyo?” Mkewe
alimuuliza baada ya kumuona mumewe alivyokuwa hoi nguo ilikuwa imebaki nusu
shati suruali nayo kama alivamia msitu wa chui na kumnyambua chini miguu ilikuwa
na tope kama alikuwa akilima jaruba.
“Mmh, weee
acha tu safari yako ya Morogoro leo ilinipata.”
Kauli ili ilimshtua
mke wa Sule na kuamini aliyefanya vile huenda ni Nargis ili asifike alipokuwa
amedhamilia kwenda.
“Mmh, kwani leo uliamka
kwenda wapi?”
“Si unajua mke wangu ulipotea katika mazingira ya
kutatanisha, jana alfajiri niliamka ili niende kwa mtaalamu kujua huenda yule
mt...”
Kabla hajamalizia sentesi yake mkewe
alimshika mkono mdomoni kumzuia aseseme na kusema.
“Mume wangu komea
hapo hapo.”
“Kwa nini au una ajenda
yako.”
“Nakuomba unisikilize mimi nipo chini ya miguu yako, kuanzia
leo tufanye kila linalotuhusu sisi wenyewe lisilotuhusu tuachane
nalo.”
“Mke wangu mbona sikuelewi hata la kupotea
kwako pia hata hili na mimi kupotea siwezi kukaa kipya.”
“Atiii,” Kopi
zito lilitua kwenye shavu la Sule.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Wee mwanamke
imeanza lini na leo iwe mara ya pili kunipiga.”
“We ni kiumbe gani
usiyesikia unajua mimi nilikuwa wapi, ungejua usingethubuti kunyanyua hata
unyayo wako kunitafuta.”
“Basi inawezekana
unanidanganya una mwanaume.”
“Mume wangu unaupungufu gani wa ufahamu
muda mfupi unasema yapi yamekukuta, kama mbishi fuatilia nyayo za damu utarudi
jina.”
“Wewe ni mwanamke tu huwezi kunishauri
upumbavu, lazima nijue sababu ya wewe kupotea na pili, itakuwaje mji niliozaliwa
nipotee sikubali hata kidogo.”
“Mume wangu ungejua
maisha niliyokuwa naishi usingethubutu kusema hayo, chonde chonde mume wangu
yote yaliyopita tuachane nayo.”
Mke wa Sule
alimpigia magoti mumewe kumuomba mumewe asitake vita na Nargis kwa kuamini
kupotea kote kule ni kwa Nargis na hakutaka kumzuru zaidi ya
kumtisha.
Lakini Sule bado
alionekana mbishi na kutaka kujua mwisho wa yote lazima aende kwa mtaalamu kwa
vile mateso aliyoyapata yalimtisha.
“Mke wangu
kwani tatizo nini?”
“Ubishi ndiyo ulionifikisha hapa sina hamu ya
kuvifuatilia visivyonihusu, naweza kusema sisi wanadamu ni wabishi pia tuna roho
mbaya pengine kuliko viumbe vyote.”
“Kwa nini unasema
hivyo?”
“Bila huruma ya yule niliyetaka kumtenda ningekuwa kiumbe wa
ajabu na maisha niliyoishi kwa wiki nzima yasikie si ya kuomba uishi,” mke wa
Sule alimsihi mumewe huku akitokwa na machozi.
“Basi nielezee
ilikuwaje ili nami nijue.”
Kabla hajasema kitu
alisikia sauti ya Nargis nje, hofu ilimtanda na kutoka nje ili kupata uhakika.
Alipotoka nje alimuona Nargis akiwa amesimama nje ya mlango wa Thabit, kwa hofu
alimsalimia.
‘Za saizi dada?”
“Mmh, nzuri tu shemu
hajambo?”
”Hajambo, e.e..ti,” mke wa Sule alipatwa na kigugumizi
alipotaka kuuliza kitu.
“Ulikuwa
unasemaje?”
“Mume wangu analazimisha nimueleze nilipokuwa,
nimweleze?”
“Mweleze tu.”
“Ni hayo tu dada.”
Mke
wa Sule alirudi ndani na kumueleza mume wake yote yaliyomtokea mpaka kufikia
siku ile kuwepo pale.
“Utani huo mke
wangu.”
“Kweli kabisa mume wangu, bila huruma yake
sijui ningekuwa katika hali gani. Ila nakuomba siri hii usimwambie mtu yeyote
zaidi yangu mimi na wewe, la sivyo atakacho tufanya Mungu
anajua.”
“Mh! Lakini kweli ulichokifanya kilikuwa hakikuhusu, bora
tuachane naye pia hapa tuhame.”
Wakiwa katikati ya mazungumzo mlango
uligongwa, alimruhusu aingie. Alikuwa Thabit.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ooh, best
karibu.”
“Asante.”
“Shemeji yupo?”
“Yupo ulikuwa
na shida naye?”
“Walaa, nilikuwa namuulizia tu.”
“Jamani mi
si mkaaji ila nimekuja kuwaaga leo ninahama.”
“Una hama, unahamia
wapi?”
“Nitawajulisha kwa kuwa bado mpo wala msihofu
nitawajulisha.”
Thabit baada ya kusema hayo aligeuka na kuondoka
akiwaacha mtu na mkewe
wakitazamana.
****
Nargis baada ya
kumkomesha mke wa Sule na mumewe aliamua kurudi chini ya bahari na mpenzi wake
Sule kupumzika kwani muda mwingi aliutumia kushindana na mke wa
Sule.
Hata wazazi wake hali ile waliiona ilikuwa ikijionesha katika
uso wake uliochoka na kukata tamaa.
“Vipi Nargis mbona upo hivyo
tumekuruhusu uwe na mwanadamu mbona unaonekana huna raha?” Mama yake
alimuuliza.
“Hakuna kitu mama nipo sawa.”
“Mh! Upo sawa
kweli mwanangu?”
“Nipo sawa mama.”
“Mh!
Sawa.”
Mama Nargis hakuridhika na majibu ya mtoto wake alimtuma mtoto
wake mkubwa wa kike ambaye ni shoga na mdogo wake Nargis ili kumchunguza mtoto
wao ana tatizo gani.
Hairat dada yake mkubwa Nargis alimfuata mdogo
wake ambaye alionekana mtu mwenye mawazo kila alivyofikiria kiburi cha mke wa
Sule kilimkosesha raha kwani hakuamini kama kweli vitisho vyote vile
ataogopa.
Alimkuta akiwa amezama kwenye dimbwi la
mawazo juu ya kitimtimu cha wiki mbili cha kumdhibiti mke wa Sule hata kushindwa
kulifaidi penzi lake kwa Thabit. Alipofika kutokana na mawazo hakuweza kumuona
dada yake mpaka alipomshtua.
Alishangaa kumuona mdogo wake
akibubujikwa na machozi tena akiwa sehemu ya peke yake kitu kilichouumiza moyo
wake.
“Nargis mdogo wangu unalia nini?”
Nargis alishtuka na
kumtazama dada yake huku akijitahidi kufuta machozi yaliyokuwa yakitoka bila
kizuizi.
“Hapana dada kawaida.”
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nargis kawaida
unalia, sijawahi kukuona ukilia haiwezekani wewe ni kipenzi changu tena ni
kipenzi cha familia. Tumekuruhusu uolewe na mwanadamu ili kuupa furaha moyo wako
lakini imekuwa kinyume.
Nargis mdogo wangu najua Thabit kakutenda,
hili nililijua mapema ndiyo maana nilikuonya na wazazi nao walikuonya lakini
umekuwa kichwa ngumu, matokeo yake kuikosesha furaha nafsi
yako.
Nakuahidi kumkomesha Thabit kwa mkono wangu wewe najua si mama
huruma, sasa niachie hiyo kazi na kwa vile umemleta mwenyewe humu ndani hatoki,”
Hailat alisema kwa hasira baada ya kumuona mdogo wake akiteseka kwa ajili ya
wanaume wa
kibinadamu.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment