Search This Blog

KWETU NI KUZIMU - 1

 





    IMEANDIKWA NA : ISRAEL BISELU



    *********************************************************************************



    Simulizi : Kwetu Ni Kuzimu

    Sehemu Ya Kwanza (1)





    Tangu Gradness aolewe na Andrew,ilipita miaka mitatu akiwa hajapata mtoto.Kila alipobeba ujauzito kwa miaka yote hiyo,ulikuwa unatoka.Hakujua ni kwa nini mimba zake zote ziliharibika kwani alishaenda vituo mbalimbali vya afya na kuzunguka kwa madaktari bingwa na tofauti wa uzazi akaambiwa kwamba vipimo vinaonesha hana tatizo lolote.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kitu gani huwa kinatoa na kuharibu mimba zangu ?Kila mimba ninayobeba ikifikisha miezi nane tu,inaharibika na kutoka.Kwa nini iwe miezi nane tu kwa mimba zangu zote? Hospitalini,nimepimwa mara nyingi na kuambiwa sina tatizo lolote,kuna kitu gani nyuma yangu jamani mbona sielewi!"Yalikuwa ni maneno aliyonena Gradness kichwani mwake wakati anawaza.



    Kwa jinsi alivyokuwa akiwaza,alijikuta akipoteza uzito wake akawa ni mwembamba.Wakati anaolewa kwa Andrew,Gradness alikuwa mnene lakini baada ya kuolewa na kugubikwa na wimbi zito la kuchomoka kwa mimba zake,unene wake ulianza kuyeyuka polepole akapungua sana. Hii ni kwa sababu,alikuwa na hali chakula vizuri kutokana na kukosa raha katika ndoa yake kwani utamu wa ndoa sio kufanya mapenzi tu bali ni kuwa na watoto pia.



    Andrew alikuwa akitamani sana siku moja aje kuitwa baba kama ambavyo marafiki zake aliooa pamoja nao walivyokuwa wakiitwa na watoto wao,aliumia sana hasa alipokuwa akiwatembelea au akiwaona wananunua nguo kwa ajili yao.Kuna wakati machozi yalimtoka.Katika miaka miwili ya mwanzo alionesha kuwa karibu na mkewe akimjali na kumfariji lakini alipoona mwaka wa tatu mambo yanazidi kuwa yaleyale,alijikuta akichoka na kukata tamaa.



    Taratibu,yale mapenzi ya dhati aliyokuwa akimuonyeshea mkewe hapo awali,yalianza kupungua.Nyumbani alianza kurudi usiku sana tena akiwa amelewa nyang'anyang'a.Mkewe alipojaribu kuuliza sababu za kuchelewa na wapi alikuwa,alijibiwa kwa jeuri huku akifokewa.Chakula akawa hali alichopikiwa na mkewa ingawa huko nyuma alimsifu sana kuwa anajua kupika ila kila akirudi alidai kuwa mkewe hajui kupika hivyo bora akale hotelini au kwa mamantiliye.Gradness aliumia sana ,zaidi mawazo ndio yakaongezeka.



    "Pole sana Gradness,majibu ya vipimo vyangu yanaonesha kwamba UNA VIDONDA VYA TUMBO. Hauruhusiwi kula maharage,pia nikuombe,usijaribu kujiweka katika mazingira ya kimawazo,utajiathiri endapo utafanya hivyo.Nenda pale dukani ukanunue dawa hizi nilizokuandikia,uhakikishe unazinywa"Alisema daktari.



    Hapohapo Gradness alihisi kuchoka,akaanza kuangua kilio kama cha mtoto mdogo;"Nimefanya nini mimi kwenye hii dunia,ina maana niliumbwa ili niteseke.Kwa nini nisife tu,nina faida gani mimi,bora nife"Aliongea Gradness huku akitililisha matone ya machozi kama mvua.



    "Usiseme hivyo Mama,hapa duniani tunapita na huwa tunakumbana na changamoto zilizojaa vikwazo vingi.Kulia sio suluhisho,mhusishe sana mungu kwenye matatizo yako ili akusaidie.Sawa mama,usilie,nyamaza basi" aliongea daktari huku akiwa anamfuta machozi Gradness kwa leso



    "Mungu,Mungu kitu gani? Mbona nimemlilia sana lakini hajanisikia,nahisi hayupo,kama angekuwepo angekuwa ameshanitoa kwenye dhiki zangu hizi"



    "Usiseme hivyo,unakufuru,Mungu anajibu kwa wakati wake.Yeye hachelewi wala hawahi,usichoke kumtegemea"



    "Sawa,asante kwa ushauri wako,acha mi niondoke"Alisema Gradness huku akijifuta machozi na kuanza kuondoka.Wakati anafungua mlango,daktari alimwangalia kwa jicho la huruma,akabaki anatikisa kichwa chake.

    ****************



    Gradness alihitaji kurudisha ndoa yake katika msitari,alipokuwa njiani kuelekea sokoni,kichwa kilianza kumuuma,akaanza kusikia sauti za ajabu ambazo hakujua hata zilikotokea,dakika tano mbele kichwa chake hakikumuuma tena wala zile sauti za ajabu na za kutisha,hakuzisikia,alibaki anashangaa.Alipofika sokoni alinunua nazi ,samaki aina ya migebuka na viungo vingine, alianza kuondoka,lakini kichwani likamjia wazo la kununua kisu kingine,badala ya kununua cha kawaida alijikuta akinunua kikubwa,tayari kulikuwa na kitu kilichokuwa kimeanza kuendesha akili yake.Hakutambua ni kwa nini kanunua kisu hicho.



    Bajaji ndiyo ilimbeba mpaka nyumbani kwake,aliposhuka tu na kugeuka kuiangalia bajaji hakuiona, ilikuwa imepotea ndani ya dakika sifuri.Tayari mauzauza yalikuwa yameanza kumtokea.



    Aliingia hadi ndani lakini mazingira alivyoyakuta,yalikuwa tofauti kidogo.Sebureni aliona pochi ya kike,aliingalia kwa muda akasikika akisema,"Hii pochi mbona kama naifahamu,si ni ya rafiki yangu Jeniffer,lakini mbona ghafla hivi,yaani kaja bila kunitaalifu.Hebu ngoja kwanza",alianza kuingiwa na wasiwasi na moyo wake ukaanza kwenda mbio.



    Kwa spidi kama ya mwanga,alielekea chumbani kwake ili akamuone mmewe kwani alikuwa hajaenda kazini kwa sababu ilikuwa ni wikendi.Alipoukaribia mlango,hakuamini kile kitu alichokisikia,alisikia sauti zilizoonesha wazi kwamba Jenniffer alikuwa akifanya mapenzi na mmewe.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Aaaasssss!"Ilikuwa ni sauti ya kimahaba aliyoitoa Jeniffer,aliisikiliza tena kwa umakini alipozidi kutoa sauti hizo za chumbani,hakuyaamini masikio yake kuwa kweli rafiki yake ambaye tangu utotoni waliendena kuwa leo kamsaliti kwa kuamua kutembea na mmewe.Kitendo hicho kilimuuma sana,alijikuta akishindwa kujizuia akaanza kulia kwa nguvu huku akiugonga mlango lakini waliendelea na mambo yao.



    Kwa asili Gradness alikuwa na wivu sana hasa wa kimapenzi,baada ya kulia sana mpaka machozi yakamkauka alijikuta akiwaza kufanya kitendo kibaya.



    "Haiwezekani,lazima niwaue wote,harafu na mimi nijimalize kwa kujiua,"Aliwaza Gradness na kuinuka kuelekea sebureni ambako alikuwa amekiweka kisu pamoja na mboga.



    Alipokichukua kile kisu ambacho wakati anakinunua alijikuta akikinunua bila kupenda.Majerha ya moyo hayatibiki,aliona akiendelea kuishi ndio atateseka zaidi,alikaa mlangoni na kuwangoja kwa hamu ili akaue.



    "Bebi baibai,love you"alisikika Jeniffer akimuaga Andrew.Kwa dharau Andrew akamwambia,"We nenda tu,usiogope hicho kitoi cha mchina".Jeniffer alipofungua mlango tu,alikutana na kisu cha tumboni,alipoangalia aliyemchoma alikuwa ni Gradness rafiki yake,"Grad!"Alisema Jeniffer lakini hakuitikiwa,Gradness alikizingusha kisu akakipeleka huku na kule mpaka tumbo la Jeniffer likawa wazi,utumbo ukamwagika nje.



    Andrew hakuyaamini macho yake alipoona hayo,Gradness akiwa ameshikilia kisu kilichokuwa kimetapakaa damu,alimwangalia mmewe kwa hasira,akakumbuka vitendo vyote alivyomfanyia hapo nyuma, akaanza kumsogelea ili amchinjechinje,mbele ya kifo Andrew alikuwa mpole kama kipolo cha juzi,mwanaume mzima na ndevu zake akajikojolea.Hilo halikumfanya Gradness amsamehe,huyo naye alimchoma kisu cha mbavuni,ukawa ndio mwisho wake.



    Gradness alipowaua wote ilibakia zamu yake,alikishika kile kisu lakini wakati anakipeleka tumboni kilipotea kimiujiza,akaanza kushangaa,ghafla likatokea jini likiwa limeshikilia kisu ambacho Gradness katumia kuulia,lilianza kusema"Nimekaa kwenye kizazi chako na kuharibu kila mimba uliyoibeba,sasa umefika wakati wa kunizalia mtoto ambaye atakuwa Jini mwenye sifa za kibinadamu,damu za hawa zitanywewa na mtoto wangu aliyeko tumboni mwako sasa"



    Hapohapo jini hilo lilinyosha kidole chake cha shahada kwa Gradness na kumgeuza kuwa kiumbe kingine.



    Gradness alianza kuongezeka kimo akawa mrefu,manyoya yalianza kumtoka huku meno yake yakibadilika na kuwa marefu kama ya ngiri.Muda huohuo kucha ndefu zilianza kuchomoza miguuni na mikonono,hali hiyo ilienda sambamba na kuongezeka kwa urefu wa vidole vyake. Alianza kukoroma na kutoa sauti nzito kama ya mtu aliye ndani ya maji.



    "Dunia itanitambua mimi ni nani,wanadamu watajuta na kujilaumu ni kwa nini walizaliwa,shida yangu kubwa ni kuleta shida.Sipendi kuona mwanadamu anafanikiwa,lazima niwaangushe tu.Nahitaji kuja duniani,nikamwage damu za watu kwa kutengeneza ajari.Nyama za wanadamu ni tamu sana,nawamezea mate wale wanaojifanya wanasali,naendakuwamaliza wote pamoja na wale wanaopenda ngono.Baba,mbona nachelewa,niruhusu japo sekunde chache"Aliongea Gradness kwa sauti ya kutisha ambayo kama ungelikuwa ni mwanadamu unayemsikiliza,usungeliweza kuistahimili.



    Aliyekuwa akiongea hivyo,hakuwa Gradness bali kile kitoto cha jini ambacho kilikuwa tumboni mwake,yeye alikuwa akitumika tu.



    "Hii dunia ni yetu,sisi ndio tunaoitawala na kuiongoza.Tuko wengi kila mahali lakini hawa vipofu wanadamu,hawatuoni.Subiri mwanangu,siku si nyingi utatoka huko uje huku kwao tena uishi nao na uwafanye kile utakachokitaka.Hebu kwanza kunywa hiyo damu ya hawa watu"Lilikuwa ni jibu la jini kwa mwanaye.



    Baada ya kuzungumza na mtoto wake,jini hilo lilinyoosha kidole chake cha shahada huku likimwangalia usoni Gradness,macho yake yalikuwa yakiwaka,liliongea maneno ya ujinini, hapo ndipo mwili wa awali wa Gradness uliporudi katika ukawaida wake.



    "Miaka kumi iliyopita,ulikuwa kando ya bahari ya hindi,wewe pamoja na mama yako mkipunga upepo.Nilipokuona tu,nilikupenda mpaka nikawaambia wenzangu.Kwa bahati nzuri uliingia kwenye maji na kuanza kuogelea,hapo ndipo nilipata mwanya wa kukaa kwenye kizazi chako.Mara nyingi umekuwa ukiota unavishwa pete ya dhahabu na mtu ambaye hukumfahamu,mtu huyo ni mimi.Sihitaji kukuoa ila nataka unizalie mtoto"yalikuwa ni maneno kutoka kinywani mwa jini ambalo lilikuwa likimwambia Gradness.



    Tayari akili za Gradness zilikuwa katika ukawaida wake,alipokuwa anaambiwa maneno hayo na jini,alikuwa akitetemeka.Alipoyatupa macho yake mbele aliona mme wake pamoja na rafiki yake wamekatwa katwa.Hakufahamu ni nani kawaua lakini alipojiangalia,alizona nguo zake zikiwa zimelowa damu.Alioangalia mbele tena,hakumuona yule jini,aliolitazama tumbo lake halikuonesha kama ana mimba.



    Alihisi kuchanganyikiwa kwa kitendo cha yeye kuua huku akiwa hajadhamilia.Wakati anafanya mauaji yale,haikuwa akili yake iliyomtuma bali jini ndilo lilizishika akili zake na kumlazimisha aue.Jini hilo lilitumia udhaifu wake wa wivu kwa kuuchochea na kumfanya aingiwe na pepo baya la kuua.Yote hayo yalienda vyema kutokana na kile kisu ambacho wakati anakinunua alijua ni cha kawaida kumbe ni cha jini na ndicho ambacho kiliukamata ubongo wake na kumfanya ajikute akiua.Ndiyo maana alijikuta akiwa na nguvu za ajabu,kama ni kusalitiwa tu kimapenzi,yeye kama wanawake wengine asingeweza kuchukua maamuzi hayo magumu ambayo mara nyingi,wanaume ndio huyafanya.



    Alianza kulia sana hasa akifikilia ni kwa namna gani angelimpata mwanaume mzuri ambaye alimpenda kwa dhati kama Andrew wake,aliumia sana lakini hakuwa na namna kwani kupitia kisu,tayari jini lilikuwa limeshamtumia kufanya mauaji.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Haiwezekani,hii mimba lazima niitoe kwa kutumia vidonge"aliwaza Gradness wakati akichukua simu yake na kuwapigia polisi ili waje eneo la tukio.Alikuwa kajitoa mhanga kwa lolote ambalo lingetokea kwani alijua fika kuwa angehisiwa kuwa yeye ndiye kawaua.Hakuwa na namna nyingine,polisi walipowasili walimtia pingu baada ya kuona nguo zake zimelowana kwa damu.



    Waandishi wa habari walifanikiwa kuzipata hizo taarifa,kwenye vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje,Gradness akatangazwa kuwa kahusika na mauaji ya watu wawili tena kinyama.Hiyo ndiyo ilikuwa habari ya kwanza kuzungumziwa na hapo ndipo watu walianza kumuita muuaji.Gradness aliendelea kukaa gerezani katika kpindi ambacho upelelezi ulikuwa unaendelea.

    ****************



    Ilikuwa ni usiku wa manane wakati Gradness amelala gerezani,jini lilimtembelea na kumchukua katika ulimwengu wa roho,kitu ambacho Gradness aliona kama ndoto,likaanza kuongea naye.



    "Pole sana,ndio dunia yenu ilivyo,sheria zenu hazina macho kwani zinahukumu kinyume.Wenye makosa hawaendi gerezani ila wasiokuwa na hatia,ndio huishia kunyea madebe"Lilisema jini hilo.



    "Hawajakosea,mimi ndiye niliyeua kwani nguo zangu zilikuwa na damu"



    "Hapana,haukua wewe uliyeua,ni mwingine aliyeua"



    "Umesemaje!"Aliongea Gradness kwa kushangaa.



    "Ila usijali,mimi naweza kujigeuza na kuwa mwanadamu,nitakuja nikutetee"Lilisema jini na kupotea.Hapohapo Gradness alishtuka katika njozi,alipoangalia huku na kule,hakumuona jini ambaye alikuwa akiongea naye kwenye ndoto.



    Kesho yake,jini kama ambavyo lilimwambia Gradness kwenye njozi,lilijigeuza likawa mwanadamu,likaenda mpaka gerezani kama mwanasheria,alipojitambulisha kuwa yeye ndiye anataka kuwa mwanasheria wa Gradness, mapolisi walimshangaa kwani ukweli ulikuwa wazi na tayari Gradness alikuwa ameshakili kuwa kahusika kuua.Wazazi na ndugu zake waliumia sana na kila mara walimtembelea,kama ni kumtenga wasingeweza.



    Barua iliandikwa na jini ambalo kwa wakati huo lilikuwa kama mwanadamu,likaituma mahakama ya hakimu mkazi ya kisutu na ombi lake lilikubaliwa kwani liliiambatanisha na ushahidi wa video.



    Hatimaye kesi ikaanza,Gradness alikuwa hajui kuwa hilo ndilo lile jini ambalo ana ujauzito wake kwani lilijigeuza na kuwa mwanadamu.Katika hii dunia kuna mambo mengi yanatendeka katika ulimwengu wa roho lakini sisi huwa hatujui,mwanasheria Ahmed Abeid alikuwa akisimama upande wa mshitaki akihitaji kupampana na mwanasheria Denis Tryphone kutoka upande wa mshitakiwa ambaye alikuwa jini aliyejigeuza mwanadamu ili kumtetea mwanamke ambaye alikuwa ana ujauzito wake.



    Kesi hiyo ilikuwa ni funika nikufunue kwani mwanasheria,Ahmed Abeid alikuwa maarufu sana nchini Tanzania akitumika katika serikali kwani hakuwahi kuweka rekodi ya kupoteza hata moja na alishhinda kwa asilimia mia.Leo hii alikuwa akipambana na mwanasheria jini ambaye kajigeuza mwanadamu.



    "Ushahidi unaohitajika hapa sio wa maneno tu,tunahitaji kuona video inayomuonesha dada huyu akiua,kama hiyo haipo basi aletwe mtu yeyote aliyrmuona Akiua"yalikuwa ni maneno ya jini Denis Tryphone. Hakimu ilibidi aipe mahakama mapumziko ya dakika tano kutokana na uzito wa hoja hiyo ambayo ilimtia kizaazaa Ahmed Abeid .



    "Mtuhumiwa ndiye alipiga simu polisi, akawapa taarfa lakini walipofika wakamkamata,hivi kweli angshindwaje kuushika mwili wa mmewe wakati kamuona kauawa.Mtoto wa watu hana hatia aachiwe huru"Lilisema jini hilo huku likimwangalia jaji .



    Kesi hiyo ilibidi ihailishwe na kutaka isikilizwe baada ya wiki mbili.



    Siku zote jini ni jini tu,hawezi kumsaidia mwanadamu kama afanyavyo mungu,siku tatu baada ya kesi,Gradness alishikwa na utungu,akakimbizwa hospitalini.



    "Sukuma,sukuma"Ilikuwa ni sauti ya wakunga wakimwambia Gradness,jini lilitua hospitalini hapo na lilikaa konani likisubiri kuona mtoto wake.



    Cha ajabu mtoto alitanguliza miguu badala ya kichwa,mara nyingi ikitokea hivyo mtoto anakuwa amefariki lakini huyo mtoto alikuwa mzima.Kitu kilichozidi kuwachanganya ni kwamba mtoto hakulia hata walipompiga ila aliachia chafya nzito kama ya mtu mzima hadi mkunga mmoja akakimbia kwa kuona maajabu hayo.



    Ghafla Gradness alianza kurusha miguu na kutokwa na mapovu baada ya kumzaa mtoto huyo.



    Punde baada ya kujifungua mtoto wa ajabu ambaye hakulia wakati amezaliwa bali kupiga chafya kama ya mtu mzima huku akiwa ametangulia kutoa miguu,Gradness alipoteza maisha.Jini lile ambalo lilimpa mimba hiyo ndilo ambalo lilimuua kwani halikutaka mtu mwingine ajue kuwa mtoto huyo alikuwa ni jini kama lenyewe.



    Gradness alikuwa tayari alishajenga dhana kuwa baadhi ya majini ni viumbe wazuri kitu ambacho hakikuwa na ukweli wowote.Aliamini kuwa hilo alipoona jini huyo akimtetea mahakamani kwamba hakuhusika na mauaji ya mmewe kwani lilikuwa limejigeuza mwanadamu.Hakujua kwambba majini ni viumbe ambao ni vigeugeu ambavyo vimejaa hila na roho mbaya.Matokeo ya kuliamini jini hilo ambalo alikuwa ana mimba yake,ndiyo hayo,akaishia kuuawa na jini hilo ambalo lilikuwa kama wakili wake katika kesi ambayo kama asingekufa ingeendelea.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku hiyohiyo aliyozaliwa mtoto huyo, alipotea na kutoonekana wodini alikokuwa kawekwa.Alitafutwa kila kona ya hospitali lakini hakuonekana,tayari kitoto hicho ambacho kilikuwa ni jini,kilianza kuonesha shughuli zake mapema tena katika uchanga wa masaa kadhaa baada ya kuzaliwa.



    Hospitalini,wakunga ambao ndio walikuwa wamemzalisha Gradness,walikamatwa na polisi baada ya kuhisiwa kuwa wao ndio ambao watakuwa wamehusika na kumficha mtofuto huyo.Wakunga walijaribu kujitetea kwa kueleza tena kwa machozi kwamba hawakujua aliko mtoto huyo lakini hawakusikilizwa zaidi ya kutupiwa Rumande wakati uchunguzi ukiendelea.



    Taarifa za kifo cha Gradness na za kupotea kwa mtoto wake muda amfupi baada ya kujifungua,ziliwaumiza sana wazazi na ndugu wengine wa wa Gradness. Japokuwa walikuwa wamempoteza binti yao,hawakutaka hata mjukuu wao wamkose.Hasira dhidi ya wakunga ambao hawakuwa na hatia zozote,zilizidi kuwawaka na kutamani wakunga hao wafungwe kwani waliwahisi kuwa wao ndio wanaweza wakawa wamehusika kumuua mtoto wao waliyempenda yaani Gradness.



    "Hawa wakunga,watakuwa wameuza mjukuu wangu!"

    "Kabisa,tena inawezekana walimuua mwanao ili watimize azma hiyo!"

    "Harafu kweli,sasa ama zangu ama zao,sitawaacha,lazima wafungwe"

    "Fanya hivyo"

    " Yaani inaniuma sana"

    "Pole sana!"

    "Asante,ila sisi binadamu hatufai,hivi unawezaje kununua mtoto wa mwenzako!"

    "Ndio ilivyo hasa kwa wale waliokaa kwenye ndoa bila kupata watoto"

    "Sikubali,wakunga hao,lazima nile sahani moja na wao"

    "Sasa usilie,nyamaza !"



    Yalikuwa ni maongezi kati ya mama yake Gradness na rafiki yake.Walichokuwa wakikizungumza,hawakukijua,laiti wangefahamu ukweli uliokuwa nyuma ya pazia,wangeendakule gerezani wawatoe wakunga wa watu ambao hawakuwa na hatia yoyote.



    Siku tatu mbele,mwili wa Gradness ulichukuliwa na kupelekwa nyumbani kwao kwa ajili ya mazishi.Kabla haujazikwa ilibidi uoshwe kwanza kwa kuogeshwa.Wakati wanaendelea kuuosha,Gradness alifungua macho yake na kuwatazama,akaanza kulia.Alionekana kutaka kuzungumza kitu lakini kulikuwa na kitu kilichokuwa kimemkaba kooni.



    Walipoona hilo,hakuna aliyebaki,walikimbia kama vile walikuwa wamevamiwa.Kitu ambacho walikuwa wamekiona,hakikuwa cha kawaida kwani mtu aliyekufa angewezaje kufumbua macho na kuanza kulia.Wote walikimbilia kwenye chumba ambacho walikuwa wakisubiriwa ili wakimaliza kuiosha maiti,waipeleke.



    "Jamani,hamuwezi kuamini,Gradness kafufuka!"

    "Umesemaje!"

    "Wakati tukimuosha,kafumbua macho,kaanza kulia!"

    "Acheni utani!"

    "Sio utani,nendeni mkajionee,ni mzima kabisa,hajafa!"

    "Hebu twende!"

    "Mh! Mii naogopa,sijui wenzangu!"

    "Twendeni bhana,umoja ni nguvu"

    "Haya!"



    Walianza kwenda kwenye chumba ambacho walikuwa wakiosha maiti ya Gradness. Walipoingia,walikuta Gradness akiwa amefumba macho yake kuonesha kwamba yuko kwenye usingizi wake wa milele.

    "Ndiyo huyu aliyefufuka sio!"

    "Maajabu!"

    "Maajabu gani? Acheni uoga,hivi ndio mara ya kwanza mnaosha maiti ee!"

    "Hapana ila tulichokisema ni kweli tupu"

    "Kweli hii! Endeleeni bhana"



    Kwa uoga wa hali ya juu,ilibidi wakubali kishingo upande japo moyoni amani ilikuwa imefutika na mioyo ilikuwa ikiwadunda huku wengine wakitetemeka kama wagonjwa waliokuwa wanaumwa homa kali.



    Walipomaliza kuuosha,waliupaka mafuta na kuungiza kwwenye sanda,tayari kwa ajili ya kwenda kuufanyia mazishi.

    ***************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwenye mlango wa nje wa geti la kulelea watoto yatima na waishio katika mazingira magumu,kulisikika sauti ya kitoto kichanga kikilia.mlinzi alipoisikia sauti alilifungua geti na kwenda kuangalia,hakuamini alichokiona,kulikuwa na kitoto kichanga kimetupwa nje karibu na geti hilo.Ilibidi akichukue haraka na kukimbiza ndani haraka kwa masista.

    "Wanawake wa bongo hawana uchungu kabisa na watoto,ni mashetani,yaani wanathubutu kutupa watoto kiasi hicho!"alisema mlinzi huyo kimoyomoyo na kuondoka.



    Laiti waangelimjua mtoto huyo wasingempokea,kilikuwandio kile kitoto ambacho kilipotea hospitali na kuwasababishia wakunga wakamatwe na polisi kwa kuhisiwa wamekificha kitu ambacho hakikuwa hicho.Kilikuwa ni kitoto cha jini na popote kilipokuwa,babayake alikuepo.Kituoni hapo kitoto hicho walikipa jina la Johnson.



    Hazikupita siku nyingi, wiki moja mbele baada ya Johnson kupokelewa kwenye kituo hicho,yalitokea mauaji ya sista mmoja.Mwili wake ulikutwa asubuhi ukiwa uchi huku akiwa amechomolewa macho,ulimi ukiwa umekatwa pamoja na matiti yake huku kizazi chake kikiwa kimenyofolewa.



    Hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye angeweza kuamini kuwa mtoto mdogo mwenye wiki moja na siku kadhaa kuwa yeye ndiye aliyehusika kumuua Sista tena kinyama kiasi kile.Mauaji hayo yalikuwa ya aina yake na ya kipekee kuwahi kutokea nchini Tanzania.Haikuwahi kutokea kwa mtu yeyote kuuawa na kuondolewa viungo vyake vya mwili kwa wakati mmoja kama ilivyokuwa imetokea.

    ***************

    Ilikuwa ni usiku uliokuwa umejawa na giza nene,nyota pekee angani ndizo ambazo zilionekana kuangaza,Sista mmoja alitoka ndani akiwa ameshikilia kitochi akielekea uwani kwani umeme ulikuwa umekatika.Akiwa anakaribia uwani,mwili wake ulianza kusisimka,nywele akahisi kama vile zinasimama huku joto la mwili wake likipanda ghafla,ilibidi asimame kwanza.

    Aligeuza shingo yake huku na kule akimlika na kitochi chake lakini hakuona chochote,alipuuzia ila ile ananyanyua mguu wake wa kulia,alisikia mtoto mdogo akilia karibu na bustani moja iliyokuwa karibu na choo hicho.Moyo ulianza kumdunda lakini akajipa roho ya simba na kuanza kusogea huko ambako alikuwa amesikia sauti ya kitoto kidogo kikilia.

    Hakuyaamini macho yake baada ya kukuta kile kitoto alichokuwa amekipokea wiki moja iliyopita kwa mlinzi,kwamba kilikuwa ndio chenyewe.Aliogopa sana,alipotaka kumsogelea nafsi ilimsuta na kumtaka aondoke haraka lakini yeye akawa mbishi.

    "Huyu mtoto kafikaje hapa usiku wote huu na nani kamleta hapa"Alijisemesha sista huyo bila kuwa na majibu yoyote.

    "Amefanana kwelikweli na Johnson,sijui atakuwwa yeye au pacha wake"Alizidi kujisemesha.Kwa muda wote huo,Katoto kalikuwa kakilia na kalionesha kuwa kanahitaji kubebwa.

    Sista huyo aliichukua tochi yake na kuiweka mdomoni,alipomshika tu mtoto yule,alipigwa na shotti ya ajabu,akaanguka chini kama gogo lakini hakuzirai.Alipotaka apige kelele za kuomba msaada ilishindikana kwani nguvu zilimwisha kabisa hata kutikisa mdomo ikawa shughuli nzito.

    Kwa macho yake mwenyewe, sista huyo aliona jinsi ambavyo kitoto kile kilianza kubalika.Kilirefuka ndani ya dakika sifuri,makucha yakakitoka huku mwili ukiwa umefunikwa kwa manyoya.Mtoto yule akabadilika kuwa jitu la kutisha,jicho moja tu lilionekana nalo lilikuwa kifuani,pua na mdomo vikiwa kichwani.Sista akiwa yuko chini,alijaribu kujitikisa lakini wapi,akashindwa,alipojitutumua kwa kutaka kuyafumba macho yake,napo alishindwa.Hata kufumba macho ilikuwa mtihani mgumu,hakuwa na namna akabaki kama ambavyo alikuwa.

    "HIKI NI KISASI TULICHONACHO KWENU WANADAMU,MLITUFANYIA KITU KIBAYA.MIMI NA BABA YANGU TUTASHIRIKIIANA KUHAKIKISHA TUNALIPIZA KISASI CHETU KWENU"Liliongea litoto lile ambalo wengi walilifahamu kama Johnson.Lilitoa sauti ya ajabu kama ya mtu ambaye alikuwa ndani ya maji,muungurumo lililoutoa wakati linapumua ulikuwa unatisha.Hapo hapo lilimvua sista nguo zote na kumbakiza uchi wa mnyama,lilianza kumshika shika ovyo katika maeneo yake.Ghafla liliyachomoa macho ya sista huyo na kuyatafuna,hiyo haikutosha kwa kucha zake kali kama kisu,liliyakata matiti ya sista huyo na kuanza kuyabugia.Halikuridhika likaongeza kwa kunyofoa kizazi chake nacho likakila.Maumivu aliyokuwa akiyapata sista huyo kwa wakati huo,hayakuwa ana mfano wake,alijiona kama vile kashatua jehanamu lakini hakutoa hata sauti wala hakujitikisha kwani shoti aliyopigwa ilinyonya nguvu zake zote na kumuacha kama bua.

    "KWETU NI KUZIMU,DUNIANI NIMEKUJA KULIPIZA KISASI"Liliongea jini hilo ,muda si mrefu lilianza kubadilika baada ya kufanya mauaji na kujirudi katika umbo la kitoto harafu lilipotea.

    Tayari sista huyo alikuwa ameshapoteza maisha,kiherehere chake cha kutoka usiku na kwenda kumchukua mtoto huyo bila ya kuwaza mara mbili na kumshirikisha mungu,kikawa kimeshamponza.

    **************

    Polisi waliendelea kufanya uchunguzi usiku na mchana kumsaka muuaji lakini bidii yao hiyo ilikuwa kama sifuri tu kwani haikuzaa matunda yoyote.Hawakujua kwamba aliyekuwa amehusika kuua ni mtoto mdogo ambaye umri wake haukuwa hata na wiki mbili tangu azaliwe.

    "Watoto wote ni wazima?"

    "Ndiyo!"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Vipi,kuna mtu mwingine kaathirika au kuna uvamizi wowote umetokea tena!"

    "Hapana,wote ni wazima!"

    "Kiukweli hata sisi polisi ni wanadamu,kuna mambo yanakuwa nje ya uwezo wetu.Inavoonekana baada ya mwili kufanyiwa vipimo,sio binadamu wa kawaida aliyehusika!"

    "Umesemaje! Si ninyi polisi hamuamini kuwa kuna uchawi"

    "Ni maneno tu ila mioyoni tunaamini sana!"

    "Sasa hao wachawi au mashetani watapataje njia ya kutuingilia wakatl huwa tunasari kila siku iendayo kwa mungu."

    "Sio hivyo,dunia imebadilika na sio wote unaowaona wanasali ukadhani kweli wanamcha mungu kwa mioyo yao wote,wengi ni wanafiki.Kama wewe unamaanisha,wengine wanafanya mizaha!"

    "Kwa maana hiyo?"

    "Ombeni sana mungu awatoe katika janga hili,mwanadamu hawezi kumaliza matatizo ya mwenzake isipokuwa mwenyezi mungu tu,hata kama tumeleta polisi wawalinde,kama mungu hayupo,ni kazi bure!"

    "Watawa kama sisi shetani atatuwezea wapi?"

    "Sawa ila nilichokuambia,kishike sana moyoni mwako.Langu neno ni moja tu,nalo ni OMBENI SANA.kwa heri"

    Aliongea kamanda wa jeshi la polisi,Abdul Mohammed na kuondoka.Yeye ndiye aliyekuwa kiongozi wa upelelezi kwenye hiyo kesi ya uhalifu,alishajua kwamba nyuma ya pazia kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea.

    "DONGE NONO LA SHILLINGI MILLIONI SABINI,LITATOLEWA KWA YEYOTE ATAKAYETUFICHULIA KUHUSU MUUAJI WA SISTA"Yalikuwa ni maneno kwenye vikaratasi vilivyokuwa vimebandikwa kila kona.Watu waliokuwa wamepigika ikawa dili yao kupepelelleza lakini hakuna walichogundua.

    Maneno ambayo aliyaongea Abdul Mohammed, yalimchoma sana mkuu wa kituo hicho aliyeitwa Mary na kujikuta akiwaza kitu fulani lakini roho ikawa inamsuta.Alichokifanya baada ya kutafakari ilikuwa ni kwenda kuwaita watumishi wa mungu ili wakakiombee kituo hicho.

    Johnson japo alikuwa mdogo kimwili,kiroho alikuwa mkubwa sana, aliweza kujua mipango iliyokuwa ikiendelea.Alipopima imani za watumishi wale,zilitosha kabisa kumuangusha na kumteketeza,ilibidi amjuze baba yake aliyekuwa kuzimu ili aje washirikiane kupambana na watu hao wa mungu tena ikiwezekana wawaue kabla hawajaenda kituoni pale.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog