Search This Blog

KWETU NI KUZIMU - 2

 







    Simulizi : Kwetu Ni Kuzimu

    Sehemu Ya Pili (2)



    Jeshi kubwa la majini maelfu kwa maelfu,lilikuwa limeshaandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha linawazuia watumishi wa mungu kwenda kuombea kituo cha watoto yatima.Jini makata ambalo kazi yake kubwa ni kusababisha ajali na kuua watu vibaya,nalo lilikuwemo kundini.Kituo chote kilikuwa kimezingirwa na majini,kwa vile wanadamu walio wengi hutua macho ya nyama kutazama kutokana na kuwa mbali sana na mungu,hakuna aliliona jeshi hilo kubwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jini makata na jini subiani ambalo ndilo lilikuwa baba yake Johnson,kutokana na kuwa na uwezo mkubwa sana,yenyewe yalijipanga kwa ajili ya kuhakikisha yanasababisha ajali na kuwaua wale watumishi wa mungu. Yalikuwa yamedhamiria kweli kuhakikisha yanafanya unyama huo,yalikuwa tayari kwa jambo lolote.Yalishajua hata barabara ambayo wangeipitia,yalikaa kwenye msitu mmoja ambao ilibidi wapitie yakiwangoja kwa hamu kwelikweli.



    "Kila mmoja wetu ahakikishe amejitakasa,maana mtu mmoja tu kati yetu akiwa mchafu kiroho,basi mungu hawezi kuyasikia maombi yetu hapa na huko tuendako na shetani anaweza atushinde.Amina watumishi wenzangu"Alisikika akisema mch.Gregory Msigwa kabla gari halijaanza kuondoka.



    Wote watano,walifumba macho yao na kuanza kujitakasa lakini kati yao kulikuwa na watumishi wawili ambao walikuwa wameficha makucha yao kwa kujifanya watakatifu na wacha mungu ilihali ni watenda dhambi wakubwa mbele za mungu hata kwa wanadamu wenzao.



    Mmoja wao alikuwa anaitwa padri.James Ezekiel,huyu yeye alikuwa msaliti mkubwa sana wa kanisa.Alikuwa malaya mkubwa sana na alikuwa ameshazaa watoto watatu na wanawake tofauti,wanawake hao walipomtishia kwamba watatangaza kuwa kazaa nao,alikuwa akiwapa pesa za kutosha.Hiyo ilikuwa ni siri yake mwenyewe na hakuka padri mwenzake aliyejua lakini aliendelea kufanya kazi ya mungu.Alikuwa akijua fika kuwa padri hatakiwi kuoa kutokana na kuapa kumtumikia mungu,ila yeye alikiapua kiapo chake kwa kufanya ushenzi huo na kuendeleza unafiki wake mbele ya maaskofu.



    Wa pili,alikuwa mch.Sospeter Ibrahim,huyu naye alikuwa simba hatari aliyekuwa akichunga kondoo wa Bwana.Hakufungua kanisa lake ili amtumikie Mungu,bali kutaka kula sadaka za waumini.Aliwadanganya wengi kwa miujiza ya kishetani aliyoionesha,Mkononi alikuwa na pete aliyokuwa ameifuata Nigeria na alipakaa mafuta fulani,aliponyoosha mkono wake watu walianguka kama mabua ya mahindi yaliyopulizwa na upepo.Wengi wakamuamini kuwa kweli yeye ni nabii wa mungu wakati ni feki.Hilo ni dhahiri katika maandiko matakatifu ambayo yanaweka wazi kwamba katika siku za mwisho watatokea manabii wa uongo ambao wataudanganya umati wa watu kuwa wametumwa na mungu. Watu waliomuamini mchungaji huyo walishindwa kutambua kwamba sio kila anayetaja jina la Yesu anamwamini kweli,wengi huwa wadanganyifu na wanapotosha watu wa mungu kwa kuwapandikiza mapepo na nguvu za giza.



    Mch.Gregory Msigwa alikuwa akimcha mungu katika roho na kweli,alikuwa mwombaji sana na alishawahi kutokewa na malaika wa bwana alipoenda mlimani kwenye maombi ya kufunga siku saba akiwa hanywi wala kula.Aliwaambia wenzake,



    "Jamani kazi ambayo tunaenda kuifanya ni ngumu,sio nyepesi kihivyo.Miaka miwili iliyopita nikiwa polini naomba,mapepo yalinijia,nilisikia sauti za vitu vikitembea.Niliinuka na kutazama na kuona majitu mawili yakinijia,yaliniambia nitoke pale eti ni kwao.Niliyaapisha kwa jina la Yesu yakawa yamenikimbia.Nilichotaka kukimaanisha ni hiki,shetani ni muongo sana,hatutakiwi kumsikiliza.



    Roho wa mungu amesema na mimi katika ulimwengu wa roho,kanionesha majeshi ya majini maelfu kwa maelfu,hivyo niwaambieni kuwa kama unajijua una hatia,tafadhari usiongozane na sisi.Shetani anaweza akatushinda kupitia mtu mmoja hata kama mia elfu wangekuwa watakatifu.Tuombe tena kwa kumaanisha,kama unajijua una dhambi nazidi kusisitiza bora ushuke usije ukatuponza"



    Padri James na mch.Sospeter waliguswa nafsi zao,wakajua kuwa roho wa mungu ananena nao kupitia kinywa cha mchungaji huyo lakini hawakumsikiliza,wakaendekeza viburi kwa kumchezea mungu kwa maombi yao ya kinafiki.Mungu sio wa kufanyia mizaha, hilo walilitambua lakini wakajificha.



    "Baba katika jina la Yesu, neno lako linatuambia kuwa vita vyetu sisi si juu ya damu na nyama bali ni vya rohoni.Ninayaapisha majeshi yote ya kuzimu kwa damu ya Yesu kristo,naenda kuisafisha njia yote mkono wak o ukapate kusimama katikati yetu.Katika kitabu cha mathayo,umesema litakalofungwa duniani na mbinguni litakuwa limefungwa.Naenda kufunga malango yote ya kuzimu,nashusha moto,ooo! Jitukuze mfalme sasa"Alikuwa mch.Sospeter akiomba kwa sauti ya juu iliyojaa unafiki mtupu.



    "Bwana Yesu ulikufa msalabani kwa ajili yetu,sisi sote tmepotoka,duniani hakuna atendaye mema.Tumeziasi njia zako,tunaomba uzisafishe dhambi zetu,ziwe nyeupe zaidi ya theruji.Usitiri uso wako usitazame dhambi zetu.Nashukuru baba kwa kutusamehe,safari hii naiweka mikononi mwako baba.AMINA"Alisema mch, Gregory Msigwa na kuyafumbua macho yake.Kutokana na kuzama rohoni,machozi yalimtoka,alianza kujifuta,safari ikawa imeanza.

    ************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "IBNIDU BAL KU,TERJU"Lilisema jini makata kwa sauti likimaanisha, wanakuja wale watu,jiandaeni.



    Kwa uharaka wa halinya juu majini yale yaliwavaa watoto wale na kuwakaa,ikatokea hali ya sintofahamu,fujo zikaanza kufanywa na watoto wadogo,wallianza kusambaratika na kukimbilia mitaani, walinzi walipojaribu kuwazuia walijikuta wakituppwa pembeni kwani walikuwa na nguvu za ajabu baada ya kuingiwa na mapepo wachafu.



    "Hivi,inakuwaje mpaka haya yanatokea,mbona tunaomba sana lakini mambo hayaendi.Kuna kitu gani kinachozuia maombi yetu kufika mbinguni"

    aliwaza Mary mkuu wa kituo hicho akiwa amebaki akishaanga kwa kile kilichokuwa kimewatokea watoto wake.



    ************



    Jini makata likiwa na jini subiani yaliendelea kufanya juhudi za kulipindua gari lile.Hayo yalifanyika katika ulimwengu wa roho,kama uko mwilini usingeweza kujua kilichokuwa kinaendelea.



    Ghafla, gari lilibinuka na kubiringika mara tano,likapinduka na kupondwa pondwa vibaya,kwa mwonekano ule ilitosha kabisa kusema kuwa hakuna aliyepona.Lakini cha kushangaza mch.Gregory Msigwa alitoka akiwa mzima tena akiwa hajaumia hata kidoga wala kuwa na jeraha lolote.Hakika mungu aliyemcha alimuokoa mikononi mwa ibilisi na kuyalinda maisha yake.



    Alipiga simu kuita ambulance,alipomaliza,mungu alimfumbua macho yake ya rohoni na kumwonesha mkanda na mchezo mzima ulivyokuwa.

    "Hapa kazi ipo"Alisikika akisema mch.Gregory Msigwa.



    Jini makata na jini subiani yalipokuwa yameshashirikiana kusababisha ajali ya gari walilopanda watumishi wa mungu kwa kufanikiwa kulipindua,yalijipongeza na kujisifu sana.Kitendo cha mch.Gregory Msigwa kutoka ndani ya gari lile akiwa mzima tena bila kuwa na jeraha lolote,kiliyakera sana majini hayo,yalijawa na hasira isiyokuwa na mfanp lakini yalipojaribu kwenda kumdhuru,ilitokea radi kutoka juu mbinguni ,ikayapiga yakaangukia mbali na kukimbia kabla hayajadhurika yenyewe.

    Mungu ambaye alikuwa akiabudiwa na mch.msigwa alikuwa mkuu kuliko yenyewe.Kama ni nguvu za kumdhuru mchungaji huyo,yalikuwa nazo lakini sio za kupambana na mungu aliuekuwa akimlinda mtumishi wake,hayakuwa na uwezo hata kidogo wa kupambana naye.Laiti mchungaji angelikuwa mtenda dhambi asiyejitakasa mara kwa mara mbele za mungu wake,hakika majini hayo yangemsambaratisha na kumuua.

    Uwepo wa waficha dhambi wawaili kwenye hilo gari,ndio uliofanya majini yale yapate mwanya wa kuweza kuipindua na kuisababishia ajali.Kama maandiko yanavyosema kwamba nawapenda wale wote wanipendao na wanitafutao kwa bidii wataniona,ndivyo ilivyokuwa kwa mch.Msigwa.Wale waficha dhambi wawili walikuwa tayari wameshapoteza maisha yao na wengine watatu ambao ni dererva,mchungaji na padri mmoja walikuwa bado hai japo walikuwa wameumia vibaya sana,walikimbizwa hospitalini dakika chache baada ya ambulance kufika eneo la tukio.

    "Baba mchungaji, hakika nimeamini kuwa una mungu,yaanj licha ya kupatwa na ajali lakini wewe hujaumia? Kweli wewe ni mtumishi wa mungu"

    "Sifa na utukufu vimrudie BWANA wangu,Niko ambaye Niko.Imeandikwa, BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yakokupigwa mbele yako,watakutokea kwa njia moja lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.Mungu wangu hawezi kukubali shetani ajitwalie utukufu kwa kuniangusha mimi harafu yeye akae na kutazama tu bila kunipigania! Najua kuwa mtetezi wangu, bado yuko hai"

    "Hakika baba!"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mara nyingi nimekuwa nikikuambia kuwa usije ukajaribu kumuacha mungu hata kama atakupitisha kwenye majaribu yaliyojaa mateso.Kila jaribu atakalokupa,atakufanyia na mlango wa kutokea"

    "Usemacho baba,kimejaa kweli tupu! Sasa, mimi nilikuja kukuchukua twende nyumbani ukapumzike"

    "Bado kuna kazi kubwa mbele yangu,mungu kanifumbua macho yangu ya rohoni na kanionesha jinsi ambavyo mambo yanafanyika,sina budi kwenda kituoni pale,hebu nipeleke haraka!"

    "Usijali,mimi nitakupeleka.Kuhusu hili gari, nimeshawapigia watu wa gereji waje kulichukua na kulifanyia matengenezo,gharama zote nitalipa mwenyewe!"

    "Mungu akuzidishie baraka uingiapo na utokapo,endelea kuwa na moyo huohuo kwani unapowatunza watumishi wa mungu,hata mungu naye hukulipa fadhira kwa kukutunza tena zaidi ya ulivyofanya wewe"

    Maongezi hayo yalikuwa kati ya mch.Msigwa a kijana wake mmoja aliyekuwa akimchunga .kijana huyu alikuwa anampenda sana mungu,kanisani alikuwa mtoaji mkubwa sana wa mafungu ya kumi na sadaka za kawaida.Kazi yake kubwa ilikuwa ni kumtunza mchungaji,alimnunulia suti nyingi za gharama na viatu vya kutosha.Kitendo hicho kilimbariki sana mchungaji na kujikuta akimuombelea baraka kwa mungu usiku na mchana.

    Mafanikio ya Samson yakawa nje nje kutokana na vitendo vyake hivyo,mungu alianza kum ffungulia milango ya baraka,kila alichokifanya kikawa kinafanikiwa,akwake nyota iling'ara mithili ya mbalamwezi na kujikuta vyeo vikijileta kwake vyenyewe bila hata kuvitaka.

    Samson alipopigiwa simu na mchungaji wake kuwa kappata ajali,aliondoka ofisini na kwenda eneo la tukio kwani halikuwa mbali na alikokuwa akifanyia kazi,baada ya kufika waliongea mengi sana ndipo akaambiwa ampleke kwenye kile kituo cha watoto yatima.

    ***************

    Saa moja na dakika ishirini mbele,waliwasili kwenye kituo hicho.Muda wa kupoteza haukuwepo,mch.Msigwa aliagiza waletwe watoto wote waliokuwa wamebaki,hao ni wale wasioweza kutembea ila wale waliokuwa wakitembea,majini yalikuwa yameshawavaa na kuwapeka mitaani ambako huko waliwatesa sana polisi, waliokuwa wakiwatafuta watoto hao.Karibia kila sista alibeba watoto wawili,mmoja mgongoni na mwingine mkononi isipokuwa mmoja tu ambaye alikuwa amemshikilia mtoto mkononi ambaye ni Johnson,huyu hakujua kuwa aliyekuwa kambeba mikononi ndiye jini hatari aliyekuwa katowesha amani ya pale kituoni.

    Mchungaji alianza kuongoza ibada hiyo fupi,aliwataka watu wajitakase kabla maombi hayajaanza,japo waroma wengi hawaimbi nyimbo za kilokole,aliwataka washirikiane kuimba wimbo kwa kumaanisha,walianza,

    Si kwa majeshi wala silaha,

    Ni kwa roho mtakatifu,

    Nguvu za giza zimeshindwa,

    Kwa jina la Bwana Yesu****2

    Walipokuwa wakiimba wimbo huo,mapepo yalilipuka kwa wakati mmoja kwa watoto wote,wakaanza kulia kwa sauti tena kilio chao kilikuwa kinafanana.Johnson alikuwa akiendelea kufanya kazi yake kwani yeye ndiye aliyekuwa kawarushia mapepo hayo hao watoto wenzake.Mchungaji aliposikia kilio hicho,alisikia sauti ya roho wa mungu ikimuongoza kufanya kitu fulani,walianza kuomba.

    "Baba katika jina la Yesu kristo,kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Luka kuwa tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule mwovu wala hapana kitu kitakachowadhuru.Ukazidi kusema katika kitabu cha nabii Yerermia sura ya 1 Mstari wa 10 Kwamba tazama leo nimekuweka juu ya mataifa na juu ya falme ili kung'oa na kuharibu,na kuangamiza ili kujenga na kupanda.Najua ee mungu kwamba unaliangalia neno lako ili upate kulitimiza.

    Enyi pepo wachafu mliokamata fahamu za watoto hawa wadogo,nawaapisha kwa jina la Yesu, tokeni.Nawang'oa na kuwateketeza.RIBOROBOSIKA SANDARABOKURIA,SIKARATIKABAKO NIKOMOKORORORO.ROBO,,,ROBO,,,ROBOSIKA.Tokeni kwa jina la Yesu."Alikuwa akiomba mch.Msigwa

    Ghafla watoto walinyamaza wote tena kwa wakati mmoja lakini mmoja tu ndiye aliyesikika kutoa sauti ya ajabu kama ya simba anayekoroma,ilibidi mchungaji aombe aletwe karibu yake,akamshika kichwani na kuanza kukemea,ghafla mtoto yule alibadilika na kuwa joka kubwa,mchungaji alitoa mkono wake lakini kwa bahati mbaya sista aliyekuwa kamshikilia Mtoto huyo alikuwa ameng'atwa na kuanguka chini,alionekana kama aliyekuwa kashapoteza maisha yake.

    Masista walipoona hilo,ilikuwa kila mmoja na miguu yake,walikimbia kama nini,waliogopa sana kuona maajabu ya kitotto kidogo kikibadilika na kuwa joka kubwa kama lile.Bado walitaka kuishi hivyo wakajihami mapema kwa kukimbia,walichungulia kwa mbali kuangalia yaliyokuwa yakiendelea.

    Mch.Msigwa aliendelea kulikemea joka lile mpaka likaonekana kuishiwa nguvu,likatulia tuli lakini halikukaa katika hali hiyo kwa muda mwingi,lilipotea kimiujiza.Hilo halikumfanya mchungaji ndio aogope,roho wa mungu aliyekuwwa ndani yake ndiye aliyemfanya yeye awe jasiri kiasi kile kwani hata Samson na Mary wakati akilikemea joka lile walikaa mbali kidogo.

    Mchungaji alienda kuungalia mwili wa sista aliyekuwa ameanguka na kukuta ameanza kukauka,uso wake ulionekana kama uliokuwa umeanikwa juani lakini mch.Msigwa kwa vile kila alichokuwa akikiffanya alimsikiliza sana roho,aliambiwa amuombee kwani kulikuwa na jini katupiwa.Alianza kumuombea huku akinena kwa lugha,ghafla lilitoka kwenye ule mwili wa sista jitu kubwa ambalo halikuwa na mikono huku likiwa na vichwa kumi vya nyoka kichwani,likaondoka.Kwa macho ya nyama halikuonekana. Hapo ndipo sista yule alirudi katika ubinadamu,akwa mzima mwenye afya kama ya awali,akamtukuza sana Mungu kwa kumuokoa na mauti.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hiyo ilikuwa ni moja,bado wale watoto waliokuwa mitaani,walihitaji kurjeshwa pale kituoni kwa njia ya maombi yaliyokuwa yamejaa imani,maana majini yaliyokuwa yamewaingia yangetolewa huko huko kwa nguvu ya imani.

    "Pasipo imani haiwezekani kumpendeza mungu,tukiitumia ngao ya imani vyema,tutaweza kuizima mishale yote ya moto kutoka kwa mwovu shetani,twende tukawaite wale watoto huko huko waliko waje hapa tulipo.Mungu anaweza kuwaleta hapa tukiamini"Alisema mch.Gregory Msigwa na hapohapo maombi yakaanza.

    Midomoni mwao zilitoka cheche nyingi za moto,laiti wangeliziona,wanfelibaki wanazishangaa badala ya kuendelea kuomba.Cheche hizo zilienda moja kwa moja mpaka kwa watoto waliokuwa wamefungwa akili na majini,ziliyachoma na kuyaunguza majini yale mpaka yakakimbia na kuwaacha huru.Kwa kuongozwa na roho wa Bwana watoto wale walirudi kituoni wakiwa salama salmini,roho wa mungu ndiye aliyewaongoza.Hakika maombi ya imani yana nguvu kuliko sumaku inayonyanyua vyuma vikubwa.Uwepo wa mungu huwa unasafiri kwa kasi isiyoelezeka kupitia maombi ya imani.

    Watoto wapatao mia mbili sabini,kimiujiza wakarejea wenyewe hakika mungu ni mkubwa sana ndio maana maandiko yananena waziwazi kuwa yasiyowezekana kwa wanadamu,kwa mungu huwa yanawezekana.

    Furaha iliyokuwa imepotea kituoni ppale ikawa imererjea.Hilo lilikuwa fundisho kubwa sana kwenye kituo kile,walianza kuwa na maombi ya kuwapeleka watoto mbele za mungu ili mapepo yasiwashinde,waliwanza watoto kuwa wansali kila wanapolala.Maombi ya kawaida na ya kufungwa yakawa yanafanyika kila baada ya wiki moja.Mapadri na wachungaji nao walishiriki.

    ***************

    Johnson baada ya kuumizwa vibaya sana kutokana na maombi,alirudi kwao kuzimu kujipanga tena upya maana mambo yalimuwia mazito baada ya kushindwa kupambana na mwenyezi Mungu hivyo kukimbia.Baba yake,jini subiani alikasirika sana kuona vile,ilibidi amuongezee nguvu mara nne zaidi ya zile za awali ili kwamba kisasi kile walichokuwa nacho kwa wanadamu wakitimilize.

    Mwezi mmoja baadaye Johnson alirejea duniani,safari hii alikuwa na kalenda kabisa ya kufanyia mauaji,alisika akisema maneno yaleyale apendayo kusema,"KWETU NI KUZIMU, DUNIANI NIMEKUJA KULIPIZA KISASI.HAWA WANADAMU WATANITAMBUA"



    Mwezi ulikuwa umeshaanza kuandama.Ilikuwa ni usiku wa saa tano ndani ya msitu mmoja,Salumu alipoingia kwenye chumba kimoja kikubwa na kufunga mlango.Alianza kuchoma udi,hazikupita dakika nyingi alisikika akitamka neno,"SALSAL",kwa kulirudia.Alikuwa akiita jini ili aongee nalo kwani alikuwa na shida ya kupata nyota nzuri.Mganga aliyemwendea alimwambia kwamba alitamke neno hilo mara elfu moja na jini lingemtokea na kumsaidia shida zake.

    "SALSAL",alizidi kulitamka huku mkononi akiwa ameshikilia mshumaa,alikuwa amevaa vazi lefu na jeusi.Salumu aliendelea kuliita jini kwa kuzidi kutamka neno hilo mpaka ifike mara elfu moja.Aliyafumba kabisa na macho yake.

    Ghafla taa alizowasha zilizimika,mishumaa nayo ikazimika jumlisha na udi.Ukuta mmoja wa chumba ulibomoka na kuanguka kwa nje,ulitokea upepo mkali wa kusulisuli uliokata hata miti.Anga likachafuka na mvua ikaanza kunyesha huku radi zikisikika kupiga kwa nje.

    Salumu alianza kutetemeka kwa hofu iliyokuwa imeshamuingia,moyo ukawa unamdunda kama unataka kutoka nje ya kifua.Alishajua kuwa jini ambalo alikuwa akiliita lilikuwa limekuja,kwa dalili hizo alishindwa hata afanyeje,akahisi kuchanganyikiwa.Alianguka chini na kulisujudia jini hilo kama mungu wake.

    "SWEI JOIK DAL KI" liliongea jini hilo kwa sauti ya kutisha ambayo ilitetemesha hadi chumba ambacho alikuwemo salumu.Lugha hiyo ilimshinda salumu,hakuielewa.

    "Sijakuelewa Mungu wangu,naomba unene nami kwa lugha yangu ya kiswahili"Alijibu Salumu huku akiwa bado kainamisha kichwa chake chini.

    "NIMESEMA,INUA SURA YAKO UNITAZAME"Lilikuwa ni jibu lililotoa jini hilo.

    "Siwezi kukuona ee mungu wangu,kuna giza mbele yangu"Alijibu Salumu

    "NIMEKWÀMBIA NITAZAME"Lilisema jini hilo kwa sauti ya juu iliyozidi kuyapandisha mapigo ya moyo ya Salumu.

    "Sawa mkuu"Alijibu Salumu na kuiinua sura yake kutazama jini hilo lilokuwa mbele yake.

    Alipoinua sura yake na kuangalia mbele,alijikuta akizidi kutetemeka na kupumua kwa kasi huku jasho jingi likianza kumtoka.Paka hakuwa paka wala ndege sio ndege.Lilikuwa jitu kubwa lililokuwa na vichwa viwili nyuma na mbele,mdomo wake ulikuwa kama wa ndege aina ya tai lakini mpana na wenye meno makubwa.Jicho lilikuwa moja tu,nalo lilikuwa kifuani,lilikuwa halitazamiki kwani hata masikio,halikuwa nayo.Salumu alizidi kutetemeka.

    "Usiogope chochote,nimekusikia ukiniita,Niambie unataka nini?"

    "Kwanza nakushukuru kwa kuja,miaka mingi imepita,nilikuwa natamani kukutana na jini lakini nikashindwa.Leo umekuja, naamini utanisaidia shida yangu ya kuwa na pesa"

    "Hilo tu"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hapana kuna lingine,naomba unipe nyota ya mvuto.Mimi ni mwanamziki,kila ninapotoa wimbo,watu huwa hawaupendi.Wengi wakisikiliza husema sikuimba bali nilikuwa nikipiga kelele"

    "Ongea kingine,naona umekificha hutaki kukisema"

    "Nakuomba ee mungu wangu,unisaidie niwe napendwa na wasichana.Nimetongoza warembo wengi ila kati yao hakuna aliyenikubali,sina nyota ya kupendwa,huwa naishia kuchezea za mbavuni na kulalia chaga"

    "Usijali,nyota yako itang'ara,Nimewapa wasanii wengi nyota.Hao wote unaowasikia wakitamba ndani na nje ya Tanzania,sisi ndio huwapa nyota"

    "Hata mimi,naomba mnisaidie nimpite nanihii,,,,"

    "Usiwe na pupa,hatutoi nguvu zetu burebure,mimi nina sharti moja tu"

    "Lipi hilo"

    "Uko radhi kulitimiliza"

    "Hata sasa hivi,nitalitekeleza"

    "Kweli ee!"

    "Ndiyo,ndiyo"

    "Hivi unajua kuwa KWETU NI KUZIMU"

    "Nafahamu hilo,hata mimi mbona nina mipango ya kujiunga na dini yenu ya huku duniani,nampenda sana LUSIFA kwa sababu mambo yake hacheleweshi,yako fasta sio hao mungu wanaoimbwa na waislamu wenzangu na wakristo"

    "Nyota yako itang'ara sio,Mimi sikuja duniani kusaidia watu,bali kulipiza kisasi kwenu wanadamu"

    "Mbona hivyo tena"

    "Si umesema utatekeleza"

    "Ndio"

    "Sasa nachokihitaji kwako ni damu,macho,ulimi na maeneo"

    "Yaani vya kwangu au mtu mwingine"

    "Wewe hapo"

    Liliongea jini hilo huku likiachama.

    Salumu alipoona hilo,alijua kuwa mambo yameshamwendea zigizaga,alisimama pekupeku na kuanza kukimbia.Hakujua mlango kaufunguaje,ila alijikuta kashatoka nje na anakimbia ili kujikomboa mikononi mwa jini hilo lililotaka kumuua.

    Hakufika hata mbali,alijikwaa kwenye kisiki na kidole chake gumba kikachanika na damu zikamtoka.Licha ya kuumia hivyo,mbele ya kifo maumivu hayo hakuyasikia,alikimbia kama nini vile.Alijigonga kwenye miti mara tano na kuanguka,lakinia alisimama na kuendelea kuuchapa mwendo.

    Wakati akiendelea kukimbia alijikuta akiwa amechoka sana na kuanza kujilaumu ni kwa nini alitamani kukutana na jini na kuamua kuliita.Wazazi wake walimsisitiza sana kuwa mtu wa kumwomba mungu lakini yeye akaona kama mungu anachelewa kumjibu na kwenda kwa mganga ambaye alimwambia aite jini ili limsaisdie.

    "Ee mungu uliye mbinguni,nimekukosea sana kwa kutokukuabudu wewe na kukimbilia kuita jini mungu.Baba alinisisitiza kuswali mara tano na mama akaniasa kuwa katika kila nifanyalo nikushirikishe wewe.Tamaa yangu ya kutafuta umaarufu ikaniweka mbali nawe na kumkimbilia shetani.Ona leo ndio najua,majini sio wa kuabudiwa,leo naenda kufa mimi"Alisema Salumu baada ya kuanguka tena alipokuwa kakimbia na kuchoka sana kiasi cha kushindwa kuendelea kukimbia.

    "Ha!ha!ha!ha"Lilisikika jini likicheka kwa sauti kubwa iliyotikisa hadi ardhi,miti ikaanguka chini lakini haikumwangukia Salumu."WANADAMU MLIMKOSEA SANA BABA YANGU,KANITUMA KULIPIZA KISASI.BABA,LEO NAUA MWINGINE"Liliongea jini hilo.

    Salumu alimkumbuka mungu aliyekuwa kamsahau siku za nyuma,leo alikuwa kwenye shida ndio akakazana kumuomba amsaidie,alikuwa wapi siku za nyuma.Kwa nini asubiri shida zimpate ndio amkumbuke mungu,je huyo mungu ni wa kuombwa wakati wa shida na angelimsikilizaje mtenda dhambi mkubwa kama yeye.Hayo yote hakujiuliza Salumu lakini shida ndizo zikamfanya akumbuke kuwa alikuwa ana mungu aliyekuwa akimuabudu siku za nyuma.

    "Wanadamu mnatushangaza sana,huyo mungu unayemuita akusaidiaje wakati ulisema unampenda Lusifa.Leo lazima ufe hata kama ungesali sara gani,huwezi kusikilizwa ewe msaliti mkubwa wa huyo mungu"Alisikika akisema jini huyo.

    Salumu akiwa yuko chini aliendelea kuomba huku akilia na kulia lakini mungu hakuwa tena naye.Kama alijiweka mbali naye siku za nyuma na kumkana ,hata leo kwenye msiba wake huo asingemsaidia kwani mungu huwapigania walio wa kwake na sio wale wamkanao kwa kuifuata dunia.

    Kwa muda huo,Salumu alikuwa akihema kwa kasi.Ghafla lile jini lilimtokea kwa mbele,salumu akalihisi, alipoinua macho yake aliliona lakini lilibadilika ndani ya dakika sifuri na kuwa kitoto kichanga.Salumu alipoona hilo akafurahi kwa kujua kuwa angeliua jini kitu ambacho mwanadamu wa kawaida hawezi.Alisogea polepole kwenye mwili wa kitoto hicho kichanga ambacho kilikuwa kikilia na kukikaba.Sekunde tatu mbele,alipigwa na kitu kama shoti ya umeme,akaanguka chini.Alipojaribu kujigeuza alishindwa.Hakika yale yaliyokuwa yamemtokea Sista,leo yalikuwwa yanaenda kumtokea Salum kijana aliyemuasi mungu kwa kutafuta umaarufu kwa njia za kishetani.

    Kama kawaida yake,jini hilo liliyanyofoa macho ya Salumu,liliukata ulimi wake,likanyofoa maeneo kwa kuyakata na viungo vyote hivyo lilivila.Hakika kisasi kilikuwa kimewaka moto,dunia nzima na wanadamu wote wangelijuta kuzaliwa kwenye hii dunia hasa wale wasiomjua mungu aliyewaomba.Hao ndio ambao wangeuawa na jini hilo.

    "KIUB BAL NIK BAA"Lilisema jini hilo likimaanisha,BABA,NIMEKULETEA NYAMA.hapo hapo mwili wa Salumu ambao ulikuwa umeshanyonywa damu na Jini hilo ukapotea na kwenda kuzimu.

    "GIl DELIJ AIK TEJIM"Liliongea jini hilo likimaanisha,KISASI CHETU NDIO KINAANZA.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog