Search This Blog

KWETU NI KUZIMU - 3

 







    Simulizi : Kwetu Ni Kuzimu

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Usiku huohuo ambao jini(Johnson) alikuwa kashamuua Salum na kuutuma mwili wake kuzimu kwa baba yake Subiani, bibiye salum(Bi.Fatma) alikuwa yuko makaburini na wachawi wenzake wakiendelea kula nyama za maiti waliokuwa wamezikwa siku hiyo kwa raha mstarehe .

    Bi.Fatma alikuwa mchawi tangu enzi za utoto wake hivyo hakuwa wa kuchezea hata kidogo,mzimu wa kikabila uitwao KWISUMBO ndio ambao ulikuwa ndani yake na yeye ndiye alikuwa malkia.Mrithi wake alikuwa bado hajawekwa wazi na mizimu.Roho ya huruma haikuweko ndani yake,majirani hata ndugu zake hawakumpenda,walimchukia na alishawahi kumuua mme wake miaka kumi na nane iliyokuwa imeshapita.

    Japokuwa kidunia alikuwa bibi kizee anayetembea kwa mkongojo kutokana na kula chumvi ya kutosha lakini ulipofika usiku,mambo yalibadilika,alirudi enzi zake za ujanani na mbio alizokuwanazo ni zaidi ya zile za mwanariadha Hussen Botti.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Paaaa!Paaaa!Paaaa!" Ilikuwa ni sauti ya radi iliyotoa mwanga mkali na kurudia kulia mara tatu.Wachawi wote waliokuwa makaburini hapo waliinua macho yao na kulitazama anga kwa kushangaa na miongoni mwao hakuna aliyetambua ishara hiyo zaidi ya Bi,Fatma aliyekuwa akiongozwa na mzimu wa kikabila wa KWISUMBO.Alijua kilichokuwa kimetokea japo alichelewa kupata taarifa hizo.

    Ndani ya sekunde hiyohiyo,alipotea na kutokea kwenye msitu mzito ambao mjukuu wake alikuwa ameenda kusfanya ibada ya kuita jini.Alitua mbele ya chumba kile kikubwa ambacho Salum alikimbizwa,aliponusa kwa kutumia pua yake,aligundua ni wapi jini lililokuwa limemuua mjukuu wake lilipokua,Alipotea na sekunde si nyingi wakakutana uso kwa uso na jini (Johnson):

    "SEIL NEZAMIK TAL MEL KALIKU?" Liliongea jini hilo likimaanisha "Hata wewe umefuata kifo kama mjukuu wako?"

    Bi.Fatna aliyeelewa vyema lugha za mashetani kutokana na kubobea katika fani ya uchawi tangu utoto wake alilijibu jini hilo,

    "SHIZOK KEIN ALMAL SUBIAN" AKIMAANISHA

    (Huniwezi ewe kitoto cha Subiani)

    "DAL BORIF KWISUMBO"

    (Unamtegemea KWISUMBO)

    "ZIMFOZ EILIB ALMAL SUBIAN"

    (Usiongee sana ewe kitoto cha Subiani)

    "ZIMFOZ EILIB! MIZOD NEZAMIK TAL MEL KALIKU"

    (Nisiongee sana! Ngoja nikuue kama mjukuu wako)

    "SHIZOK ,Ibosh NAL KWISUMBO)

    (Huwezi ukapambana na Kwisumbo)

    Alipoongea hivyo bibi kizee huyo alianza kutoa sauti ya ajabu,alianza kupiga kelele kwa sauti ya ajabu ambayo kwayo kama ungekuwa binadamu wa kawaida ngoma ya sikio ingeasuka kutokana na ukali wake.Hadi ardhi ilitetemeka, majani ya miti yakawa yanaanguka chini,miti ikawa inatikisika kana kwamba kuna upepo mkali unavuma.Alikinyoosha kidole chake cha shahada kwa jini(Johnson) na kuanza kuongea maneno ya ajabu kutoka kwenye kamusi ya kuzimu akisema kwa sauti yake ya utisho

    "JIFOK,JIFOK AL KAI MAIDU. SIDUN KAL BAL ZUU FEIB. VUSHIZOY KEIT TOKMOJ, ZASIF KWISUMBO"

    Jini(Johnson) nalo halikukaa kizembe, katika mapambano hayo,lilinyoosha kidole chake cha shahada kwa bibi kizee,na lenyewe lilikuwa likitamka maneno ya ajabu yaliyojaa misamiati migumu ya kuzimu ambayo hata kuiandika ni kazi kwelikweli.

    Wakati mapambano hayo yakiendelea na kila mmoja akiwa amemnyoshea kidole cha shahada mwenzake ili kumuangamiza huku wakitamka maneno ya ajabu,pambano lilionekana kutokuwa na mshindi lakini johnson alianza kuishiwa maneno kutokana na uchanga wake,kule kuzimu alikuwa ana miaka mia tatu tu,wakati kidunia katika mwili wake alikuwa bado ana miezi sita.Mengi ya kuzimu hakuyajua japo baba yake Subiani alikuwa kamuongezea nguvu,mzimu wa KWISUMBO uliokuwa ndani ya bibi yake Salum ulikuwa unajua mengi kutokana na kuwa zee la miaka elfu tatu,lilimuongoza bibi huyo kutamka maneno mazito ambayo yalianza kuzishusha nguvu za Jini (Johnson).

    Hatima ya hayo ni kwamba Johnson alijikuta akizidiwa nguvu,alibadilika kutoka kwenye umbile lake la kijini na kurudi katika mwili wa kibinadamu,akawa kitoto kichanga.Bi.Fatma alikuwa katika hatua za mwisho za kutaka kumkamata jini huyo.Kama ambavyo niliwaeleza hapo awali,bibi huyu alikuwa ni noma,majini kwake haikuwa shida, ni machache ya liyokuwa yanamzidi uwezo.

    "WUITOEK HAILUB DAL SIMIK"Aliongea bibi kizee huyo kwa kujitamba sana akimaanisah

    "Nilikwambia lakini hukunisikia".Alijiandaa kwenda kumuua jini (Johnson) ambaye alikuwa kashamzidi nguvu lakini ghafla upepo mkali wa kisulisuli ulikata miti ulisikika kwa mbali,mvua ikaanza kunyesha na radi zikapiga mara kumi mfululizo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "SUBIANI" alisikika bibi kizee huyo akisema,alishajua kuwa aliyekuwa akija hakuwa mwingine ila baba yake na jini hilo alilotaka kuliua.Hofu isiyo na kifani ilimwingia,akajua huo ndio utakuwa mwisho wake maana jini subiani lilikuwa na uwezo mkubwa kuliko wa mzimu wake.Alijitutumua kikike, akaizuia ile mvua isinyeshe,ndani ya dakika sifuri akaikata.Hakika kama ni uwezo alikuwa nao.

    Alipigiwa makofi na Subiani kwa kufanya hicho,jini hilo lilienda moja kwa moja hadi kwa mtoto wake aliyekuwa akija kazidiwa.Kama kawaida ya jini hilo,lilichomoa ulimi wake mrefu kama mita mia tatu hivi,likamvuta bibi kizee huyo na kwa uchungu lililokuwa nao na kwa kutumia uwezo wake mkubwa lilimuua ndani ya dakika sifuri.Huo ukawa mwisho wa Bi.Fatma,kama ni kuonea majini aliweza ila sio jini subiani na jini MakatalMajini haya mawili aliyaogopa kama nini kutokana na uwezo yaliyokuwa nayo.

    Baada ya hapo lilimwamsha mtoto wake na kumrudisha tena katika umbile lake huku likimpa mbinu moja ya kupambana na adui alipozinduka baadaye lilimwambia,

    "KISASI CHETU KWA WANADAMU KINAENDELEA,HAKUNA ATAKAYETUZUIA.MWANANGU,SIKU SI NYINGI NITAKWAMBIA KITU WALICHONIFANYIA WANADAMU HADI MIMI KUAMUA KULIPA KISASI.NENDA MJINI,KWA SASA UNAWEZA KUJIBADILI KATIKA UMBO LOLOTE LA JINSIA LA WANADAMU,KAMWAGE DAMU TENA"

    *******************

    Kesho yake asubuhi ulikuwa ni msiba wa kufiwa na Bi.Fatma,Haukuwa tena msiba bali kama sherehe,watu walifurahi sana kufa kwake maana aliwakosesha amani,si ndugu si majirani,hawakumpenda hata kidogo.walimchukia sana,siku tatu mbele ndio aliingizwa kwenye nyumba yake ya milele.

    Wiki mbili zilikatika ndugu na jamaa zake Salum wakiwa hawajui wapi alikuwa.Walimtafuta kila kona lakini hakuonekana.Polisi nao walishirikishwa kama wafanyavyo wanadamu wengi,huwategemea sana polisi kuliko kumwomba Mungu.Mambo mengine sio ya kuwaachia polisi bali Mungu aliyejuu ahusike.Hata yule mganga aliyemshauri Salum aende kuita jini msituni aliuawa siku mbili mbele baada ya kifo cha salum.Wanadamu hasa wale waliojiweka mbali na mungu,kisasi cha Subiani kilikuwa juu yao.

    ***********

    Petro alikuwa kijana mmoja mtanashati aliyewavutia warembo wengi,hakuwa mtulivu,kila mwanamke mzuri aliyemuona alitaka awe wake.Siku moja ikiwa ni saa moja jioni akiwa anatoka kazini na yuko ndani ya gari lake,aliona mttoto mmoja aliyekuwa kaumbika kweli.Kama kawaida,si yeye mara zote hujiita mzee wa saundi,alianza kutmtupia nyavu aliposimamisha gari,Yule msichana akakubali, akaingizwa kwenye gari.

    Vioo vya gari la Petro vilikuwa tinted,yeye ndiye aliona wa nje ila wa nje hakumuona wa ndani.Wakati gari analiondosha alivipandisha.Alianza kuongea na mrembo huyo ili akiwa kama walewale wa siku zote,akale mboga hiyo usiku huo huo.Lakini binti huyo alionekana kuwa mchangamfu.alichukua hoteli moja na kwenda kulala naye kwani alishatiki,Walipoingia kitandani na kuanza kufanya mambo ya watu wazima,kitu cha Petro kiligoma kutoka,kila akijaribu kutoa,akashindwa,zaidi kiliendelea kuzama kwenye mwili wa mrembo huyo.Taratibu,akaanza kuishiwa nguvu,alikokuwa kazama,kulikuwa hakuzamiki.



    Nguvu ziliendelea kumwishia Petro,akasinyaa na kuwa kama mlenda.Uso wake ukajawa na makunyanzi mithili ya babu kizee.Msichana aliyekuwa akifanya naye mapenzi alizidi kuuvuta uume wake ndani kimiujiza na kuanza kuubana taratibu.Badala ya raha ikawa ni karaha.Petro aliumia sana ,akajaribu kupiga kelele ili walau aite msaada lakini sauti ilikuwa imemkauka.

    Taratibu akaanza kupanda juu kimiujiza bila ya kuvutwa na mtu yeyote.Ngovi iliyoshikana na uume wake ikaanza kujivuta na kunyofoka kwa kadri alivyozidi kwenda juu.Maumivu ambayo alikuwa akiyapata hayakuwa na mfano wake.Mwisho uume wake ukaengana kabisa na ngozi yake,ukabakia kwenye uke wa yule msichana aliyekuwa akifanya naye mapenzi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ha!ha!ha!ha!ha!",alicheka msichana huyo kwa sauti ya ajabu iliyomfanya Petro awe na macho kama ya chura.Uume wa Petro ulizamishwa kwenye uke kimaajabu na hazikupita hata sekunde tano tayari yule msichana alibadilika na kuwa kitoto kidogo.Kitoto hicho kilimwangalia na baada ya muda kikawa kimepotea kimiujiza.Kwa muda wote huo,petro alikuwa bado yuko hewani akiwa ameganda kama kipepeo,hakushuka chini wala kupanda juu na hakuna aliyekuwa kamshikilia.Maumivu pekee ndiyo yalikuwa yamechukua nafasi yake.

    Ghafla ilitokea mikono miwili iliyokuwa na kamba na sura za watu hazikuonekana ila ilikuwa na kucha ndefu na vidole vyembamba nane na virefu kama sentimenta kumi.Mmoja ulishika mguu wake wa kulia na mwingine ule wa kushoto.Kamba zilifungwa na mikono hiyo ikapotea.Yote hayo Petro aliyashuhudia lakini hakuwa na namna ya kujisaidia.Zile kamba zilianza kujivuta na kumchana msamba,mwisha miguu ikanyofoka na damu zikaendelea kumwagika chini kama vile bomba limefunguliwa.Miguu nayo ilipotea kimiujiza.Hakika maumivu yalizidi kuongezeka,kwa jinsi alivyoyahisi hata kama angelikuwa ni komando lazima angalia tu.

    Chini yake kulikuwa na mdomo mkubwa uliokuwa umeachama na ulijaa kile chumba,ulikuwa kama plastiki na ulitanuka.Huo ndio ulioendelea kunywa zile damu zilizokuwa zikimiminika kutoka juu kwa petro ambaye alikuwa amebakia na kiwiliwili tu.

    Petro alijaribu kumwomba mungu ili aje kumwokoa japo hapo nyuma hata mlango wa kanisa hakuujua.Alitamani mauti imfike saa hiyo hiyo na kuzidi kusali kimoyomoyo,

    "Bwana Yesu ulikufa pale msalabani kwa ajili yetu.Nisamehe dhambi zangu zote,futa jina langu kwenye kitabu cha hukumu,andika jina langu kwenye kitabu cha uzima wa milele.Niue sasa na ipokee roho yangu maana nateseka",aliongea hivyo.

    "Ulikuwa wapi siku zote? Kwa nini hukunirudia kabla hujappatwa na adha hiyo? Unadhani mbingu ni rahisi kuingia kama ulivyokuwa ukiwaza kuwa ukikaribia kufa ndio utaokoka? Hiyo mbingu haipo na wewe sio mali yangu ila ya shetani",hiyo ilikuwa ni sauti aliyosikia ikinena moyoni mwake baada ya kutaka kuokoka kabla hajafa.

    Jehanam aliiona ile,moto wake ukamtisha sana zaidi alimuona kama vile malaika Israel anakuja kuichukua roho yake.Alijuta ni kwa nini siku za nyuma hakumpa Yesu maisha yake,alipenda sana anasa za dunia kuliko mungu.Hakujua kuwa dunia ya sasa haikaliwi na wanadamu tu bali hata majini nayo huishi na kuchangamana nao.Alijuta sana lakini neema ya wokovu hakuwa nayo.

    "TEIL FODIMOZ BAI KWEIJ",ilisikika sauti ya jitu kubwa(Johnson),likiongea.Petro hakuelewa hata maana yake akabaki anasubiria kifo tu."ATEIFAH!",liliongea jini hilo na petro akaanguka chini kwa kishindo kikubwa,ule mdomo ulikuwa umeshatoweka na jini(Johnson) akatokea na kuutoa ulimi wake mrefu na kuuburuza mwili wa Petro kinywani na kuutafuna kabisa,lilimaliza na kulamba chini maana wakati petro anaanguka alipasuka kichwa,ubongo ukawa nje nje .Hivyo ndivyo kisasi kilivyokuwa kinazidi kupamba moto.

    Maneno ya ajabu yalitoka kinywani mwa hilo jini,kitanda safi kikatokea tena kikiwa kimejitandika na shuka likiwa vilevile.Chumba kilibaki ni kisafi kiasi kwamba hakuna mtu angejua kuwa mle yalifanyika mauaji.Kama ni mtu aliyekuwa kauliwa hakujulikana alikokuwa kwani aliliwa,jini hilo lilipotea ili kwenda kufanya kazi nyingine.

    *************

    "Hizi ni siku za mwisho,wanadamu acheni kutenda dhambi,mrudieni mungu naye atawarehemu.Jehanamu iliwekwa kwa ajili ya shetani lakini kiumbe huyu hataki kwenda peke yake ndio maana anawadanganya kwa kuwashawishi mtende dhambi ili mwende wote.Shetani aliishi mbinguni na anajua raha iliyoko huko,mpe Yesu sasa maisha yako.Anasema njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo na mimi nitawapumzisha.Dhambi zako hizo,zinahitaji kuttoweshwa kwa kumwamini Yesu haleluya";

    alikuwa ni mch.Gregory Msigwa aliyekuwa akihubiri kanisani kwake "Mavuno christiani centre",TAG(Tanzania assamblies of God".CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ameeeeeeeeeeeen!",ilikuwa ni sauti ya waumini walioitikia na kuendelea kusikiliza mahubiri.

    **************

    Mch.Gregory Msigwa baada ya kuhubiri alienda ofisini kwake na kula chakula,baada ya hapo watu wenye mahitaji walianza kuingia ofisini kwake ,wengi walihitaji kuombewa na wengine walipewa ushauri wa kiroho.Dakika si nyingi aliingia binti mmoja aliyeonekana kuvaa kiheshima na mrembo.

    Akiwa amechuchumaa akamsalimu mchungaji,

    "Bwana Yesu asifiwe?"

    "Amina.Karibu,keti kwenye sofa hapo"

    "Asante sana baba"

    Aliongea binti huyo huku akivunja vunja vidole vyake.Alionekana kuwa kama ni mwenye aibu na mwenye heshima kwelikweli kiasi kwamba mchungaji akavutiwa kutaka kujua hitaji lake.

    "Binti yangu karibu,sema haraka maana kuna wengine wanasubiri waingie ukitoka"

    "Sawa baba.Mimi nina tatizo"

    "Tatizo gani hilo binti yangu? Yesu anaweza kukusaidia,usilifiche hebu liweke wazi?"

    "Tumbo langu limekuwa likininyonga chini ya kitovu"

    "Pole sana,sasa sogea hapa nikuombee"

    Binti huyo badala ya kusogea alianza kuvua nguo zake zote.Mchungaji akashangaa na kuuliza kulikoni lakini binti huyo akatoe zote mpaka kufuri akaitoa akabaki uchi.Alizishika chuchu zake zilizokuwa zimesimama kama papai na kuzifinya,akaung'ata mdomo wake na kuyalembua macho yake.Alianza kumsogelea mchungaji huku akitembea mwendo fulani.Kiukweli alikuwa ana ngozi nyororo na alikuwa ni mtotot kweli,kama ni chombo hakikuwa cha ovyovyo.

    Macho siku zote hayana pazia,mchungaji aliona kila kitu.

    "Kaa mbali nami usinisogelee ewe pepo mchafu"

    "Jamani,sogea hapa karibu nataka nikupe mambo"

    "Ushindwe kwa jina la Yesu, ushindwe"

    Hata mchungaji naye ni mwanadamu,ana hisia kama binadamu wenzake,mwili wake ulikuwa umeanza kusisimka na yule jamaa akaamka,alijikuta kasimama tu hasemi. Akaganda kama sanamu.

    "Haya sasa,sogea karibu nikupe vitu adimu",alisema binti huyo baada ya kuona kashampagawisha mchungaji.



    Msichana huyo alipomkaribia mchungaji ambaye alionekana tayari kulewa kimahaba,alianza kumvua koti kisha akafungua vishikizo vya shati la mchungaji ikifuatiwa na mkanda wa suruali.Ile anataka kuitelemsha chini,alijikuta yuko chini baada ya kusukumwa na mchungaji,alijibamiza ukutani na kupasuka kwenye sura yake na damu ikaanza kumtoka.

    "Ewe shetani ushindwe kwa jina la Yesu ",alisema mchungaji huyo na kufunga mkanda wake vizuri lakini wakati akiendelea kufunga vishikizo vya shati lake msichana huyo alipiga kelele kwa sauti huku akiwa ameshikilia nguo na kufunika uchi wake,

    "Ninabakwaaaaaaaaa,msaaada jamaniiiiii"

    Mchungaji alishangaa sana kusikia hilo."Paaaaaa",mlango ulifunguliwa kwa kishindo na wazee wa kanisa wakaingia.Walimkuta yule msichana yuko chini kafunika uchi wake huku akiwa analia,usoni alikuwa ameumia na walipomtazama mchungaji hakuwa amevaa koti na kishikizo kimoja kilikuwa hakijafungwa,zaidi ni pale walipotazama suruali yake na kuona haijachomekewa.

    "Baba mchuungaji, umeanza lini hii tabia?",alihoji mzee mmoja wa kanisa.Waumini hasa waimbaji waliokuwa wamebaki kanisani wakamiminika kwa wingi kwenye ofisi ya mchungaji ambako hata kuona mlango ilikuja ikawa kazi kwani watu walijazana tayari.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hallo! Ee polisi hapo,msaada jamani,tunaomba mfike kanisa la TAG(Mavuno Christian Centre) hapa tabata.......eee njoni msichelewe......mchungaji kabaka muumini wake,,,,sawa",alikuwa ni mumbeya mmoja aliyejitenga na wenzake na kuwafikishia taarifa polisi.Hatta hakuwa anajua kwa undani tukio lenyewe ila alisikia tu mtu akisema anabakwa.

    "Baba yetu,nini hii sasa,binti wa watu unathubutu kumbaka wakati unajua ni dhambi? Imani yako iko wapi? Huyo mungu unayetuhubiria kila siku ndio huyu?",alisikika akisema mama mwingine.

    Mama mchungaji alipoata taarifa hizo akawa amezilai,mtoto wake naye wa pekee alipojua akabaki analia.Hakuamini kama baba yake,ambaye amehubiri neno la mungu tangu yeye hajazaliwa kuwa leo hii alikuwa akijaribu kumbaka muumini wake.

    "Mungu pekee ndiye anayejua ukweli wa hili.Sijambaka mimi"

    "Hujambaka ee! Hebu angalia shati lako, ona ulivyomfanya binti wa watu,umemuumiza ,mchungaji gani wewe kama sio jina tu"

    Aliongea mama mwingine Kwa ukali.

    Yule msichana aliyekuwa bado akiliia akakazia,

    "Hafai kuitwa mchungaji,mbakaji huyo utadhani hana mke.Hakuna anachokifanya zaidi ya kutamani tu,mimi nakuja kuombewa......."

    "Funga kinywa chako ewe pepo mchafu"

    Aliongea mchungaji na hapohapo yule msichana akanyamaza.Watu hawakugundua kitu pale kutokana na maneno ya mchungaji aliyokuwa kayanena.

    "Hivi,kati yako wewe na huyo nani anastahili kuitwa pepo?"

    "Huyo sio mtu ni pepo?"

    "Pepo gani liwe hivi,mtu kabisa huyu,ana mifupa na nyama harafu una mwita pepo.Shetani mkubwa wewe"

    "Tena unaenda kunyea,kazi kutupotosha tu"

    "Imetosha"

    Aliongea mchungaji na kukaa kimya.Hakutaka kuongea na kujibizana nao sana maana ndio angemuasi mungu wake zaidi.Tayari alishajua yuko majaribuni kama Ayubu mtumishi wa mungu.

    "Pisha,,,pisha wewe,,,gari la polisi lile",walikuwa ni watu wakiambizana ili kuachia njia.

    Tayari polisi watatu walishafika na kwenda moja kwa moja ofisini kwa mchungaji ambapo walipewa njia na kuingia.Binti yule kama kithibitisho kwa polisi kuwa alitaka kubakwa alibakia vilevile japo uchi wake aliustiri kwa nguo,hakuacha kuendelea kulia.

    Polisi walipoingia ndani,hawakutaka maneno mengi,walimtia pingu mchungaji na kumpeleka kwenye gari lao.Wakiwa wako njiani, waandishi wa habari walikuwa wameshawasili na kuanza kumpiga picha mchungaji huku wengine wakimchukua video.Waumini hawakuamini kuwa mchungaji ndio alikuwa akiishia kama hivyo.Mijadala pekee ndiyo ilibakia.

    Siwema,kama ambavyo alijitambulisha kwa polisi kuwa ndio jina lake,naye aliambatana na polisi hao. Walipofika kituoni walimuweka mchungaji gerezani na siwema akapelekwa hospitalini ili akatibiwe usoni alikokuwa kaumia vibaya.

    "MCHUNGAJI ABAKA MUUMINI WAKE!",hicho ndicho kichwa kilichotawala kwenye vyombo mbalimbali vya habari.Kwenye mitandao ya kijamii watu walitengeneza na vikatuni kabisa huku wengine wakicheza hata tumaigizo.

    Viongozi wakubwa wa kanisa la TAG huko makao makuu akiwemo askofu mkuu wa kanisa hilo,Mch.Timotheo Sibonike,waliumia sana kupata taarifa hizo,zaidi ni kama aliliaibisha kanisa hata wenyewe kwa ujumla maana ilikuwa haijawahi kutokea.Hata huko jela hawakwenda kumwangalia,waumini nao hata hawakwenda.Walimzira na kanisa lake likawa limebadilishiwa mchungaji,akawa ameletwa mwingine.Kilichomuumiza mchungaji huyo ni kwamba hata familia yake hasa mkewe na mtoto wake hawakwenda hata kumjulia hali.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hatimaye kesi ilifunguliwa mahakamani na mchungaji akawa amehukumiwa jela miaka thelathini kwa kosa hilo la ubakaji.Hata hakulia alipopewa adhabu hiyo maana alijua hana hatia yoyote na ni jaribu lake licha ya wanadamu kumtenga.Alichokuwa akishikilia ni kwamba hata ulimwengu mzima umchukie lakini mungu akampeenda,hiyo ni faraja kubwa sana kwake.

    "Shikamoo kaka?"

    "Marahaba"

    "Pole sana"

    "Usiwe na shaka mdogo wangu?"

    "Kaka,hivi ni kweli ulibaka?"

    "Nimesingiziwa.Usilie sasa,hili ni jaribu langu"

    "Mungu atakusaidia utatoka"

    "Kabisa.vipi mke wangu anaendeleaje?"

    "Mh! Wifi kabadilika,shetani kashatawala maisha yake,kaolewa na mwanaume mwingine juzijuzi tena kwa ndoa ya kiserikali"

    "Na kijana wangu"

    "Kaka,yule mwanamke kumbe ni nyoka.Anakuzungumza vibaya mpaka yule mtoto hakujui wewe kama baba yake.Anakuchukia"

    "Ee mungu wangu nipe moyo wa uvumilivu"

    "Kaka,mimi bado niko pamoja na wewe japo ukoo wetu juzi ulikaa kikao na kukutenga"

    "Wala usijali,mungu akiwa upande wangu,ni nani aliye juu yangu?"

    Alikuwa ni mchungaji akiendelea kuongea na mdogo wake ambaye wakati akiwa mchungaji alikuwa anamsomesha shule ya wasichana ya St.Francis huko mbeya.

    Kila siku mchungaji alimwomba mungu rehema,roho ya tamaa iliyotaka kumfanya azini na yule msichana hakuacha kuikkemea.Hukohuko jela hakuacha kulitangaza neno la mungu kwa wafungwa wenzake.Wengi walibadilika kutokana na mahubiri yake,,wakaacha dhambi na kumrudia mungu.

    Usiku mmoja wakati akiwa amelala,aliota ndoto na kuona yule msichana aliyemsingizia kuwa kambaka akicheka sana karibia nusu saa.Baadaye binyi huyo alimuona akibadilika na kuwa kitoto kichanga na baadaye jitu kubwa la kutisha.

    "KWETU NI KUZIMU, duniani nimekuja kulipa kisasi",liliongea jitu hilo na hapohapo mch.Gregory Msigwa akashtuka kutoka kwenye njozi.Hapo ndipo alipoanza kuppata picha kamili ya tukio zima,ilibidi apige magoti na kuanza kumwomba mungu ili amtie nguvu katika jaribu hilo alilokuwa akipitishwa maana hata roho mtakatifu aliyekuwa akinena naye mara kwa mara hakuonesha kuwa tena karibu yake.Alikumbuka hata Yesu wakati yuko msalabani alisema

    "Eloi eloi,rama sabakithani",akimaanisha mungu wangu mungu wangu mbona umeniacha.kila siku alipasoma mahali hapo na kuzidi kujipa moyo.

    *********

    Johnson alippotinga kuzimu tena kwa baba yake,Subiani, alipokelewa kwa shangwe .Alipongezwa sana kwa kazi nzuri japo alishindwa kumuua mchungaji huyo lakini kkwa kumkomoa yeye na kumsababishia aende jela,hicho kilikuwa kisasi tosha kwake maana siku za nyuma alishawahi kumfukuza Johnson kwenye kituo cha watoto yatima.Jini subiani lilimkalisha kitako na kuanza kumweleza ni kwa nini ana kisasi na wanadamu.

    ***********

    Mwanangu ;binadamu wote ni adui zetu.Hivi unavyoniona baba yako,sivyo nilivyokuwa miaka ya nyuma.Miaka elfu saba iliyopita,hapa kuzimu nilikuwa kiongozi mkubwa sana,mfalme wetu Lusifa aliniteua kuwa gavana wa jimbo la VIYEG,niliifanya kazi hiyo kwa ufanisi wa hali ya juu,niliongoza majini wenzangu vizuri sana mpaka lusifa akanipa tuzo.Baadaye nilipandishwa cheo,nikatolewa kwenye ugavana na kuwa jenereli wa majeshi ya majini hapa kuzimu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mimi ndiye ambaye nilikuwa natoa kazi kwa majini kuja kufanya mashambulizi.Kuna ajali nyingi sana tukazitengeneza huko duniani ili kupata damu za watu.Kiukweli cheo hicho cha ujenerali kilionekana kunifaa zaidi ya ugavana.Nilidumu kwenye hicho cheo mpaka wewe unazaliwa.

    Moja kati ya vitu ambavyo nilivifanya na siwezi kuvisahau ni siku ambayo tuliwavamia wavuvi ziwani waliokuwa kwenye mashua.Ilikuwa huko ziwa Tanganyika miaka mia moja iliyopita,ilitokea meli kubwa ikawagonga wale wavuvi,kwa vilee ilikuwa ni ya kichawi,ilipotea nao wakawa wameletwa huku kuzimu.Binadamu hao walikuwa watatu na tulikuwa na shida nao sana.Kuna kazi niliyotaka wakanifanyie huko duniani,japokuwa hawakukubaliana nami lakini niliwalazimisha kufanya kile nilichowaamuru.Hao ndio ambao waliniletea matatizo makubwa sana mpaka nikajuta ni kwa nini niliwatuma wao.Sikuwa na namna nyingine,walipokamatwa na majini niliowatuma nikawaua.Kuna kitu walikifanya ambacho sikukipenda.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog