Search This Blog

KWETU NI KUZIMU - 4

 







    Simulizi : Kwetu Ni Kuzimu

    Sehemu Ya Nne (4)



    Kazi niliyokuwa nimewatuma ya kumuua Gerrard Sanga,walikuwa wameishindwa.Mtu huyo alikuwa mtu anayemwabudu mfalme wetu Lusifa,alifanikiwa kufika mpaka daraja la nne na kuppewa kitabu kikubwa huku kuzimu kilichokuwa na sura elfu moja.Kwa kupitia kitabu hicho,kulikuwa na maandishi ambayo alipoyatamka tu,kila kitu alichokitaka alikipata.Lakini kitabu hicho hakufanikiwa kudumu nacho,alinyang'anywa na mfalme wetu kwani alipunguza ibada huku kuzimu,akawa anajiona yeye ni mungu mtu.

    Baada ya kupolwa kitabu hicho,Gerrard alikasirika sana kwani alishushwa pia daraja kutoka la nne mpaka la tisa.Taratibu akaanza harakati za kujitoa kwenye familia ya dini yetu,alienda kwa mganga mmoja huko kasulu kigoma,akamtengeneza mpaka akamtoa majini mia moja tuliyokuwa tumemwekea na ambayo ndiyo yalikuwa yakichunga biashara zake na kuzifanya ziwe zenye mafanikio.

    Siku zote Lusifa hapendi kusalitiwa,aliniagiza nitume majini mengi ili yakamuue yule mganga kisha yamkamate Gerrard na kumrudisha kuzimu ili aendelee kuteswa.Kama nilivyofanya siku zote,nikawa nimeandaa kikosi kikubwa cha majini yapatayo elfu tano.Mimi sikwenda,niliyaamuru yakamuue yule mganga na baadaye yakamteke Gerrard .Jeshi langu likawa limetoka na kuja moja kwa moja kigoma,njia yaliyotumia ilikuwa ya ziwa Tanganyika. Yalipofika kwa mganga yakaanza kupambana naye na majini elfu ishirini yakapigwa vibaya na kuumizwa na mganga yule maana alikuwa ana nguvu.Baadaye aliishiwa nguvu na yale majini yaliyobakia yakawa yamemvamia na kumuua kabisa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Majini hayo yalianza kunusa na kujua ni wapi Gerrard kaelekea,yalimtafuta mchana huo lakini yakiwa kama maili ishirini hivi ulitokea moto wa kutisha kutoka kwa mtu yule anayeishii huko juu ukawazuia.Yalipobisha na kutaka kusonga mbele yalipigwa na radi ikabidi yarudi,Jini moja nililoliteua kuwa kiongozi nililiambia nikiwa hukuhuku kuzimu kuwa Gerrard kaingia kanisani na ameshampa maisha yake mtu yule.

    Kanuni moja ya huku kuzimu ni kwamba ukitumwa kazi hautakiwi kurudi bila kuikamilisha,bora uumizwe hata ufe lakini ukiwa unafanya kile ambacho mfalme wetu anataka ukifanye.

    "Hata kama yuko kanisani na mmeshindwa kumfikia,akitoka tu,mshambulieni maana huyo hajabadilika kabisa,bado ana uwezo wa kimiujiza ndani yake.Ila muwe makini na miongoni mwenu asijaribu kurudi mtu huku kuzimu bila kumleta";

    Lilikuwa tamko nililomwambia kiongozi wa hayo majini.Kwa vile yaliijua kanuni ya mfalme lusifa,hakuna hata jini aliyebisha, yote yalirudi ziwani na kukaa huko mpaka usiku.

    Ilipofika saa tano usiku,Gerrard alikuwa ameshamaliza kuombewa na tayari alikuwa ameshajiunga na dini ya mtu yule na kuanza kutusema sisi vibaya.Alipoagana na wanamaombi ili akalale ndipo majini yale yaliipata harufu yake maana si alikuwa mwenzetu,yakaanza kumfuatilia mpaka kwenye hoteli aliyokuwa analala huko kigoma.Majini hayo yaliingia pale lakini yalipojaribu kuingia kwenye chumba alichokuwa kalala Gerrard,moto ulitokea ghafla na kuyalamba majini yote,hakuna lililotoka pale likiwa salama,mengine yaliunguzwa usoni,mengine mikononi na mengine miguuni.Hakuna lililorudi huku kuzimu likiwa halijajeruhiwa maana ule moto ulikuwa mkali.

    "Mkuu,tumeshindwa kumuua",hiyo ndiyo taarifa aliyonifikishia kiongozi wa majin yale.Sikuwaelewa japo walikuwa wameumizwa,niliwaua wote,sikuacha hata mmoja maana kazi niliyokuwa nimewatuma hawakuikamilisha.

    ***********

    Siku chache baada ya kuwaua wale,mfalme wetu Lusifa akawa ameniita tena na kunieleza kuwa yule Gerrard kaanza kuzifichua siri zake kwa wanadamu wenzake huko duniani,maana alirekodi hadi kanda na mikanda ya video kwa ajili ya shetani na mali zake zote alizokuwa kazipata kwa njia yetu alizitenekeza.Maduka aliyabomoa na kuyawasha moto,hata majumba yake na pesa zote alizoweka benki akaamua kufunga akaunti.Akabaki kama alivyo na kanisa likawa limemchangia,akanunua uwanja na pesa alizozipata kutokana na kuuza kanda zake za ushuhuda wa kufichua siri za shatani akazitumia kujenga nyumba yake.

    Mfalme wetu Lusifa alikasirika sana,akaniongezea mimi uwezo wa miujiza ili nihakikishe namuua Gerrard maana kufichua siri zake,kulikuwa ni kuwafanya wandamu wazidi kumchukia.

    Sikuyatuma majini tena maana yalionekana kuwa na uwezo mdogo sana wa kupambana na mtu huyo ambaye alikuwa analindwa na nguvu za mtu yule anayeishi huko mbinguni.

    Siku ya kwanza nilimuona akiwa na mkewe,kwa vile wanawake ni wepesi sana kuingiliwa na sisi na wana sehemu nyingi za kutufanya sisi tukakaa.Kweli nikafanikiwa kumuingia kwenye kifua chake,nikaanza kuzishikilia akili zake,nilifanikiwa kufanya hivyo kwa sababu huyo mwanamke alikuwa hana imani ndio maana nikamuingia.Hakuwa anamuomba mutu yule kuttoka rohoni ila ni kama alikuwa anamsindikiza mume wake kanisani.

    Mke wa Gerrard nikampa nguvu za ajabu kwenye miguu yake na kwa vile nilikuwa naziongoza akili zake,akatoka mbio pale kwa mmewe huku akilia.Gerrard alipoona mkewe anakimbia akajua kashakuwa kichaa,akaanza kumkimbiza na lakini akashindwa kutokana na nguvu nilizompa.Kwa kutumia uwezo wangu,nikampeleka mpaka barabarani ambapo nilipitisha lori kubwa likamgonga na kumsagasaga na kuwa kama chapati.Damu pekee ndizo zilizoonekana na hakuwa wa kutazamika tena.Lori hilo nililolileta kimiujiza likaenda kwa kasi hata hakuna aliyeliona lilipofika mbele.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hiyo ilikuwa ni kazi yangu ya kutaka kumfanya Gerrard apoteze matumaini na mtu yule na kuirudisha nyuma imani yake ili nipate wepesi wa kumwingilia na kumwangamiza.

    Gerrard alipofika barabarani na kukutana mkewe kagongwa na kusagwasagwa aliumia sana,akalia kama mtoto mdogo.Watu wengi walikusanyika na kushangaa tukio hilo,walililia sana.Ndipo na mimi nikajichanganya katikati yao kama binadamu wa kawaida nikawa namwangalia.

    Kwa kutumia roho nikajaribu kumwita maana si siku chache tu alikuwa mwenzetu.

    "Gerrard",niliita hivo na yeye akanisikia.Aliinua uso wake na kutazama mbele ambapo alikutanisha macho yake na mimi.Wanadamu wengine walikuwa wakiniona kama mtu mwenzao lakini yeye akanigundua kuwa mimi ni jini,akashituka na kugundua kuwa mimi ndo niliyesababisha.

    "Wewe mshenzi mkubwa umeniulia mke wangu!",alisema Gerrard kwa uchungu na kunifuata kundini huku akiwa amefula hasira na amekunja ngumi.Alipoirusha ngumi yake baada ya kunisogelea,niliikwepa ikampta binadamu mwenzake.Nilimcheka kisha nikapotea.Aliyekuwa kapigwa ngumi alitolewa jino moja,akahamaki,kwa kuwa alikuwa mwanaume akamsukuma na kumpiga Gerrard teke la tumboni.

    "Ndio maana umefilisika wee bwege",alisema mtu huyo aliympiga teke.Gerrard akaugulia maumivu,akataka arudi apigane naye lakini akshikwa mkono na mchungaji wake ambaye alikuwa amefika muda si mrefu baada mimi kuondoka.

    Nilifurahi sana kumfanyia hivyo nikijua kuwa imani yakee ingetindika na kmfanya azidi kukengeuka kisha mimi nipate wepesi wa kumshambulia na kumwangamiza maana ningeenda kichwa kichwa ningeishia kuwa kama wanajeshi wangu.

    Siku ya mazishi ya mke wake,nilienda makaburini na Gerrard akaniona,nikamcheka sana,aliponifuata huku akipiga kelele wanadamu wenzake hawakujua wakadhani atakuwa amechanganyikiwa,walimshika na kumtuliza.Alibaki analia tu na hiyo yote ni mbinu yangu niliyoitumia ili upenyo ukipatikana wa yeye kusahau kuomba na kuwaza sana kuhusu sisi nimuue.

    Usiku akiwa amelala chumbani kwake alikuwa mwenye mawazo sana,kitandani nilimwona akijigeuza upande huu na kwenda upande mwingine.Hakupata hata lepe la usingizi hata kitabu kile wanachosoma habari za mtu yule hakukisoma siku hiyo na hakuwa ameomba.Nikajua huo ndio muda wenyewe wa kumwangamiza.

    Sekunde sifuri nikatokea konani nikiwa nimeshikilia fimbo yangu ya miujiza.Gerrard alinihisi na aliponiangalia tu,nilinyoosha fimbo yangu,huwezi kuamini mwanangu(Johnson),lilitoka jini moja lililokuwa linawaka moto,likamshambulia Gerrard.Hapo ndipo nilipoanza kucheka kicheko cha ushindi,nikajua nimemuweza kumbe nilikuwa najidanganya.



    Jini nililomtumia Gerrard kutoka kwenye fimbo yangu likiwa linawaka moto likaanguka chini pale lilipomkaribia.Sikujua ni nani alilizuia,wakati nataka kumrushia kombola Gerrard wakatokea watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi meupe,nywele zao zilikuwa zinang'aa na walizifunga kwa kamba na kiunoni walivaa mikanda myekundu.Walipponiangalia tu,mwili wangu nikahisi unaungua,nikaumia na wakawa wamenyanyua panga zao,nilipotea haraka maana wangeniua na uwezo wa kupambana nao sikuwa nao kwa vile wao ni watumishi wa yule aliye juu na kazi yao kubwa huwa ni ya kuwalinda watu wanaomwabudu mtu yule wa huko juu.

    Nilikuwa nimeumizwa sana,maumivu niliyokuwa nimeyapata baada ya kutazamwa na wale watu wawili waliokuwa na macho ambayo yalitoa cheche za moto,niliungua sana.Kuumia kwangu huko kusingenifanya nirudi kuzimu, kama ambavyo nimekueleza,huku kuzimu ukitumwa hutakiwi urudi mpaka uhakikishe umekamilisha kazi.Nilikaa ziwa Tanganyika usiku huo nikiwa kwenye maumivu mazito sana,majini menzangu yaliyokuwa yanakaa hapo yakanihudumia ili nirudi kwenye hali yangu.

    "Gerrard,siwezi kumuua,analindwa na watumishi wa mtu yule wa juu.Kila nikipanga mashambulizi nashindwa,sijui nitafanyaje na kurudi kwa mfalme wetu Lusifa bila kumuua itakuwa hatari kwangu na anaweza akanishusha cheo changu hata kuniua kabisa",niliyaambia majini menzangu nikiwa chini ya ziwa Tanganyika.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa vile mimi huwa napenda kunywa damu za wanadamu,usiku mmoja nikiwa katika mapumziko na nikijiandaa kwa ajili yya kumuangamiza Gerrard,niliona kwa juu wavuvi wakiwa kwenye boti zao,walikuwa kundi japo walipanda kwenye boti tofauti.Sikutaka kuwaacha,nilihitaji kuwala na kwa vile ambavyo Gerrard aliniudhi,nikaona binadamu wote watakuwa kama yeye.

    Niliongea maneno yangu ya ajabu,ikatokea meli kubwa ya kichawi,nikaipanda kisha nikaanza kuiendesha kuelekea upande wao maana nilitaka vitoweo.

    "Ee bwana ee,cheki ile meli,kama ya Titanic vile,itakuwa imetoka wapi"

    "Sio wanga wa ziwa hili kweli?"

    niliwasikia wavuvi hao wakibishana,nilienda moja kwa moja na kuwagonga japo walijaribu kuikwepa,nikawazamisha chini na kuwaua kabisa.Nikawa nimepata mlo wangu kwa njia hiyo.

    **********

    Gerrard hakutishika na mashambulizi ambayo tulikuwa tunamfanyia,zaidi alizidi kusimama kanisani na kutuabisha,akawa anakili waziwazi kuwa sisi hatumuwezi eti kwa sababu yeye analindwa na mtu yule.Siri zetu za huku kuzimu akazidi kuzifichua kwenye haraiki ya watu.Nilizidi kuwa na hasira,uchungu ukawa umenivaa,nikatamani kumuua kila nilipomwona lakini nilishindwa kwa sababu wale watu wawili walioniangalia siku ile niliwaona wakimlinda japo yeye sijui kama aliwaona.Mmoja alikuwa mkono wake wa kuume na mwingine mkono wake wa kushoto.

    Bado nikaona kuwa nina kazi nzito sana ila kibarua nilichokuwa nacho kilikuwa cha kumtindisha imani ili mwanya upatikana wa kumwangamiza.Baada ya kumuua mke wake,nilidhani nitaitikisa imani kwa vile aliwaza sana kumbe sikujua aliyoyawaza.Njia pekee iliyobakia na ya mwisho kwangu kuijaribisha ilikuwa ni ya kumtupia mtoto wake pepo ambalo lingezivuruga akili zake na kumfanya awe kichaa.Hiyo nayo niliona ingeniwezesha kumfanya Gerrard akengeuke kiimani ili nimuue.

    Mtoto wake alipokuwa anatoka shhuleni,nikamwendea katika umbile la kibinadamu,kwa siku hizo niliweza kujibadilisha ila sio siku hizi.

    "Hujambo mtoto?"Nilimsalimia mtoto huyo

    "Sijambo uncle shikamoo?"

    "Marahaba,baba ni mzima"

    "Ndiyo"

    "Mmesoma nini leo?"

    "Hisabati,kiingereza na sayansi"

    "Haya,chukua pesa hii ukale ice cream"

    "Asante sana uncle"

    "Haya,umusalimie baba yako"

    "Sawa uncle,bai"

    "Bai"

    Nilikajibu katoto hako.Kalifurahia nilipokapa pesa,hakakujua kuwa kaliyekuwa kakiongea naye ni nani na pesa hizo alizompa zina siri gani.

    Pesa ile ilikuwa ina jini langu,katoto kale kalipoishika,jini lile lilikaingia na likakaongoza mpaka nyumbani.Kalimkuta baba yake anakasubiria,ile kanafungua mlango,kalianguka chini,kakaanza kurusha miguu,mapovu yakakatoka mdomoni na damo zikakatoka machoni,mwisho kakafa.

    Gerrard alichanganyikiwa,

    "David...David....Davidiiiiii usiniache baba yakoooooooo"

    Aliongea Gerrard kwa uchungu huku akitokwa na machozi.Aliposikiliza mapigo ya moyo kwenye kifua chake yalikuwa yamekata.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mama yako kafa juzijuzi na wewe tena unataka kuniacha.David,nakupenda sana mwanangu,fumbua mboni zako unitazame basi",alisema Gerrard, akili yake ilikuwa kama imechanganyikiwa.Damu aliziona zikimtoka mwanaye machoni lakini ni kama hakuziona zenyewe.

    "Hapana.David wangu hajafa,ngoja nimpeleke hospitali,atapona tu",aliongea Gerrard kwa kujipa matumaini.Kwa jinsi alivyompenda mwanaye,hakuamini kuwa kafa japo aliona mapigo ya moyo yamesimama.Alipomfikisha hospitalini jibu pekee alilopewa na daktari ni hilo,

    "Kazi ya mungu haina makosa,David kashatutoka"

    "It can't be doctor"

    (Haiwezi kuwa hivo daktari)

    "Let doctor be doctor and God be God,I'm human being like you,remember "

    (Mwache daktari awe daktari na mungu awe mungu,mimi ni binadamu kama wewe)

    Aliongea daktari huyo kwa kumaanisha kuwa asingeweza kumsaidia.

    "Mwanangu hajafa,kama huwezi kumtibu nipe nimpeleke kwa mchungaji wangu akamuombee maana hata, ,,,, ni daktari toshha",aliongea Gerrard na jina la huyo mtu sijakutajia mwanangu kwa sababu unamjua na sisi tunamwita mtu yule.

    Madaktari hata wanadamu wenzake wakamshangaa sana Gerrard hasa kwa kitendo chake cha kudai maiti ili aippeleke kwa mchungaji iombewe.Kwa muda huo,mimi nilikuwa nikishuhudia yote hayo kupitia uwezo uwezo wangu.

    Nilipoona Gerrard kawaza hilo,nikajua kashashtukia, ni kweli yule mtoto kwa wanadamu wenzao alikuwa amekufa ili kiroho bado alikuwa hai na niliyekuwa nimemuchukua ni mimi.Nikajua hapo nisipomzuia, basi mtoto yule aweza arudishwe lakini nikazizalau imani za wachungaji wa siku hizi ambao nao sio waaminifu kwa mtu yulel lakini nilitakiwa kumuzuia ili asifike kanisani huko.

    Gari la kwanza alilopanda ili limpeleke kanisani kwa mchungaji,nikalikalia kwenye injini.Kila dereva akiliwasha,halikuwaka,akajaribu tene na tena lakini bado likagoma.Akshuka na kukagua gari, akalikuta liko vizuri,akaliwasha tena,likawaka kidogo,likazimika tena.Akajaribu,ikagoma,akachoka na kumwambia Gerrard atafute gari lingine.

    Kweli Gerrard akatafuta taksi,hiyo akaipanda,nayo nikaiingia kwenye injini wakati iko kwenye mteremko.Ikazimika ghafla,breki zake nikazikata,teksi hiyo ikaanza kwenda kwa kasi, nikaigonganisha na gari lingine,dereva akajeruhiwa vibaya kichwani,Gerrard hakuumia sana zaidi ya kujeruhiwa mkononi kwenye hiyo ajali.Mtoto yule naye hakuumia alikuwa mzima.Nilihamaki,nikataka kumuua lakini ile najaribu,nikawaona wale watu wawili,nikawakimbia.

    "Poleni sana na ajali"

    "Asante"

    Aliongea mchungaji akimwambia Gerrard baada ya kufikisha mtoto wake nyumbani kwake.

    "Siamini kama mwanangu kafa,naomba umwombee"

    "Nitaombeaje maiti?"

    "Baba,hajafa huyu"

    "Sawa.unahisi kachukuliwa na mashetani uliokuwa ukiwaabudu"

    "Ndio baba mchungungaji"

    "Y.... anaweza na yeye ni njia ya kweli na uzima.Alifufua wafu na kama roho yake iko kwa mashetani itaenda kurejeshwa"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliwasikia na kuwaona wakizungumza.Hawa watu wanapoomba huwa wanatuumiza sana na kila wanalolisema huwa linafanyika,na maombi yao huwa kama bomu lililotegeshwa,nadhani hata wewe mwenyewe ulishajionea siku ile kwenye kituo cha watoto yatima.Kiliitwa kikundi cha wanamaombi,kwa kushirikiana na mchungaji,Wakaanza kumwombew yule mtoto niliyechukua roho yake ili afufuke.Kimbembembe kikawa kimeanza kunikuta.



    Niliendelea kuing'ang'ania roho ya David wakati wanaendelea kuombea maiti yake.

    "David nakuita huko roho yako ilikowekwa na mashetani,njoo kwa jina la ....",alikuwa akisema mchungaji.Ilikuja nguvu ya ajabu na yenye uwezo kuliko wa kwangu ikawa imeninyang'anya roho ya yule mtoto.Sikufanya chochote zaidi nikaachiwa majeraha mazito.

    "Ooh! Glory to God,thank you....."

    (Ooh! Utukufu kwa mungu,asante....)

    Alisema mchungaji yule baada ya kuona mtoto kafufuka kama ambavyo wanadamu husema.Waombaji wakashangaa kuona muujiza huo mkubwa,niliwasikia wakimshukuru mtu yule.

    "Kumbe yule.....aliyemfufua Lazaro bado yu hai,hakika hakuna kama yeye,anastahili kuabudiwa na kila goti lipigwe kwake!",alisikika akisema mwombaji mwingine.

    "David",alisikika akiita baba yake ,Gerrard lakini mtoto hakujibu.Jini nililokuwa nimemwekea kupitia ile pesa lilikuwa bado ndani yake japokuwa alikuwa kashafufuka na liliukamata ulimi na kifua,mtoto yule akashindwa kuongea,akawa kama bubu.

    "David,mimi ni baba yako",aliongea tena Gerrard huku akitokwa na machozi maana kufufuka kwa mtoto wake ambaye roho yake nilikuwa nayo mimi,kulimfurahisha sana.

    Mchungaji alipomwangalia yule mtoto,akagundua kuwa kuna roho ya kishetani bado iko ndani ya David.

    "David,niangalie usoni!",alisema mchungaji huyo kimakusudi na David hakumwangalia zaidi akalipuka kwa sauti akisema,

    "Wajinga wakubwa ninyi,mmenyang'anya roho yake kutoka mikononi mwangu wakati nilimuua.Leo sitoki humu mpaka niondoke na roho yake kuzimu,nasema sitoki na wewe Gerrard unayeendelea kutoa siri zetu kwa wanadamu wenzetu,utaona",maneno hayo hakuwa akiyasema David,bali jini lililokuwa ndani yake.

    Nikaendelea kusikiliza kilichoendelea nikiwa chini ya ziwa Tanganyika.Kitu ppekee kilichoanza kikawa ni maombi,walilikemea lile jini kwa muda mrefu likagoma kutoka,sio kwamba lilikuwa haliumii ila ni kwa sababu ya ile kanuni yetu ya huku kuzimu ya kutokurudi bila kukamilisha kazi ambayo unakuwa umetumwa.

    Saa la kwanza likaisha,jini hilo likawa libishi mpaka masaa matano yakaenda,jini hilo bado likagoma kwa kudai kuwa mpaka lirudi na roho ya David kuzimu.Walikemea mpaka sauti zikawakauka lakini halikutoka.

    "Mungu wetu aambaye ameweza kumfufua David kutoka mikononi mwa mashetani,anaweza pia kulitoa jini hili.Hebu tutumie mamlaka tuliyopewa na,.......akisema mtakanyaga nguvu zote za yule mwovu wala hapana kitu kitakachowadhuru, twende sasa tukalikemee kwa imani",nilimsikia mchungaji akiwaambia waombaji wenzake na kwa muda huo huo,giza lilikuwa limeshaanza kuingia.

    Wakaanza kukemea,wakakemea ila bado jini langu likabisha.Lilianza kuwavunja moyo,likawafyonya kisha likawaambiaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Heeee! Mnanitemea mate usoni,acheni kunyesha harafu ni kama hamjapiga miswaki,midomo yenu inanuka.Masaa saba sasa bado hamchoki tu,niacheni nichukue roho yake",lilizidi kuwakatisha tamaa.

    "Msimsikilize jini wala kumruhusu kunena sawa watumishi!",aliongea mchungaji huyo na kuendelea kukemea.Walikemea ila bado hata halikuppiga kelele japo lilikuwa limejeruhiwa vibaya,lilijikaza hivyohivyo ili wale watumishi waone kuwa maombi wanayoyafanya hayasikilizwi na mtu yule.

    Usiku ukaingia,hawakuchoka wakazidi kukemea,hata chakula hawakukiwaza,wakakeemea, ilipofika usiku wa manane,saa tisa usiku wakiwa wanakemea bila kuchoka,jini lile likawa hoi nyang'anyang'a,lilianza kupiga kelele.

    "Naungua,natokaaaaaaa"

    "Moto,tunashusha moto.Achia ewe jini,tunakuapisha kwa jina la.....",walizidi kuomba watu wale.Jini lile likaendelea kusumbua kwa kelele mpaka saa kumi na moja alfajiri.Maombi yakaendelea na ilipofika saa moja asubuhi baada ya kugangamala vya kutosha,jini langu likasalenda:

    "Haya chukua kila kilicho chako utoke",alisikika akisema mchungaji.Jini lile likaondoka huku likiwa hoi.Ile linatoka tu,mtoto alianza kutapika na kitu pekee kilichoonekana kwenye matapishi ni ile ppesa niliyokuwa nimempatia wakati anatoka shuleni ya shilingi elfu moja.

    Mchungaji alipoiona,hakuruhusu mtu yeyote aiguse, wakaanza kuomba na ile noti ikaungua na yale matapishi yakakauka.Walijipigia makofi na kumtukuza mtu yule japo waliomba kwa muda mrefu.

    "Mungu wetu hawahi wala hachelewi,anajibu kwa wakati wake.Hongereni kwa maombi ya kishujaa pia poleni kwa njaa na usingizi kwani miongoni mwetu hakuna aliyelala",alisema mchungajinhuyo na kunikera sana kwa maneno hayo.Tayari nilikuwa nimeshindwa kumwangusha Gerrard kwa mara nyingine.Mara nikasikia sauti ya Gerrard akiongea na mwanaye.

    "David?"

    "Yees daddy! "

    (Ndiyo baba)

    "Pole

    "Baba sijui nilikuwa wapi,eneo nililokuwa kulikuwa na giza sana na nilimuona mama yangu"

    "Umesemaje"

    "Nimemuona mama,yuko huko kwenye kuna giza na analia tu"

    "Wewe,mimi nani kwanza"

    "Baba"

    "Yule pale"

    "Mchungaji"

    "Umemuona mama yako akifanya nini?"

    "Alikuwa analia tu,kule aliko anaseka na bado ni mzima ila hawezi kuongea,walimkata ulimi na nilipokuwa nataka niwe naye,kuna majitu ya ajabu yalinishikilia na kunizuia"

    "Usilie sasa"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Baba twende tukamsaidie anateseka"

    "Sawa mwanangu"

    Nilisikia akiongea hivy Gerrard.Katoto hako kalikuwa kamepeleka kitu kingine,mke wa Gerrard nilimuua mwenyewe kwa kumsababisha agongwe na lori na kwa vile muda wake wa kufa haukuwa bado nikakaa naye huku kuzimu na kale katoto wakati nimeshikilia roho yake kalimuona na kakawa kameenda kuwaambia.

    "Kumbe mke wangu naye aliuliwa na mashetani na wanamtesa",nilimsikia Gerrard akiongea kwa uchungu huku akilia.

    "Tulishamzika,hatuwezi tukalifukua kaburi lake",alijibu mchungaji huyo.

    Gerrard akabaki analia tu .

    *********

    Mbinu nyingi sana nilikuwa nimezitumia ili kuhakikisha ninamnasa Gerrard lakini kati ya hizo hakuna iliyofanikiwa.

    "SUIDAL KAL BEIL JOIR EIL SUBIAN"

    (Kazi niliyokutuma mbona huikamilishi ewe Subiani)

    Aliniuliza mfalme wetu Lusifa nikiwa huko ziwani kwani alinifuata.

    "VESOH YUILIB DUJIK ANEI SHEZIK,SIUF NIL KWEIKOJ"

    (Nimetumia kila mbinu mfalme ikashindikana,nipe nafasi nyingine)

    "OSOKOMOK HASOD EIL SUBIAN"

    (Umepewa ya mwisho tu ewe subiani)

    "BUIBAL"

    (Asante)

    Tulimaliza mazungumzo yetu kwa namna hiyo.Nafasi niliyokuwa nimepewa ya kuhakikisha namwangamiza Gerrard ilikuwa ya mwisho,na endapo nisingefanikisha basi huo ndio ungekuwa mwisho wangu wa kuwa jenerari wa majeshi ya majini huku kuzimu.

    Maandalizi nikaanza kuyafanya,nilisoma nakala za vitabu vya huku kuzimu vingi sana ili niwe na uwanja mpana wa kuhakikisha namwangamiza Gerrard. Pia nikashika dua zile kubwa za kuniongezea uwezo pindi nitakapomvamia Gerrard.

    Ulikuwa mtihani mzito sana ambao sikuwa na uhakika kama ningeushinda.Nilijua fika kuwa kama Gerrard akiwa uraiani siwezi kumuua,hivyo niliandaa mazingira ya kuhakikisha namppeleka jera,huko nikaweke pepo kubwa la kukataliwa na kila mtu amchukie, kisha nipate mwanya wa kumwangamiza maana ningesema niende kichwakichwa ningeishia kuambulia patupu.

    Siku moja nilienda mpaka nyumbani kwa Gerrard,ilikuwa ni usiku wakati wako mezani wanaendelea kula chakula cha usiku.Nilikata umeme nyumba nzima,Gerrard akatoka na simu yake, akaiwasha tochi na kwenda kwenye swichi kuu kuangalia kama kweli umeme ulikata au ilikuwa shoti.Alipofika na kuangalia kwa kumurika akaona ni kama shoti imetokea,aliponyoosha mkono wake ili apeweke vizuri alipigwa na shoti yangu ya kishetani akaanguka chini.Umeme nikaurejesha,na siku ya leo sikuwaona wale watu wawili waliokuwa wakimlinda na sijui ni kwa nini,labda alikuwa kamkosea mungu wake,nilirusha kombola langu la nguvu,likampata Gerrard,nikaongeza na lingine,akawa hoi.Kitoto chake kikatokea,kiliponiona tu kikasema

    "Usimuue baba yangu tafadhari"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikaangalia kwa uchungu wa hasira zetu za kishetani,,nilirusha kombola lakini likazuiliwa,hapo hapo wakatokea wale watu wawili wakiwa wanang'aa sana,nywele zao walikuwa wamezibana na kiunoni walikuwa wamevaa mikanda miyekundu.Sikuwaangalia kwa sababu macho yao yalikuwa yanawaka,nilipojaribu kutaka kukimbia nikashindwa,Nikanata palepale na wale watu wakanijia huku wameshikilia panga ambazo zilikuwa zinawaka.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog