Search This Blog

KWETU NI KUZIMU - 5

 







    Simulizi : Kwetu Ni Kuzimu

    Sehemu Ya Tano (5)





    Wale watu wawili waliokuwa wanang'aa kama jua,walizidi kunisogelea huku wakiwa wamenyanyua panga zao zilizokuwa zinawaka moto,nikaendelea kujaribu kupotea kimiujiza lakini ikashindikana,nikanasa palepale.

    "Hukumu yenu inakuja,jukumu letu,kuwalinda wale wamchao Bwana!",ni maneno hayo tu waliyasema,waliniangalia kwa macho yao,nikaungua sana na kuanza kupiga kelele.Gerrard ambaye alikuwa chini,alistaajabu sana kuona kelele hizo zinasababishwa na nini,huenda hakuwaona wale watu wawili waliokuwa wakimlinda.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Naondokaaaaa,sitarudi tenaaaaaa,niachieniiiiii",niliongea kwa sauti yangu ya kutisha kutokana na maumivu mazito niliyokuwa naendelea kuyapata.Baada ya kuteswa sana na kupewa somo ili nijue kuwa watu wanaomwabudu mtu yule sio wa kuchezea chezea,nikaachiwa,mwili wangu ulikuwa unatoka moshi tu.Nilikuwa nimeumia sana,nikapotea na kuondoka,sikujua ni kitu gani kiliendelea ila nilitua kuzimu na kwenda moja kwa moja kwa mfalme wetu Lusifa.

    "RUISOM KUL HEIL MEL DALIK"

    (Kazi uliyonituma nimeshindwa kuifanya)

    Nilimwambia hivyo mfalme wetu huku umbile langu likiendelea kutoa moshi.

    "WOFEJ SEIKOT NAMEI ZOIK?"

    (Umekubali kabisa ushindwe kirahisi?)

    Aliongea mfalme kwa ukali na hasira yake ikawa imepanda.

    Nilijaribu kumweleza kuwa Gerrard nisingeweza kupambana naye kwa sababu alikuwa akilindwa na watu wa mtu yule lakini Mfalme wetu Lusifa hakunielewa.Kwa cheo nilichokuwa nacho,sikutakiwa kutamka maneno ya kushindwa mbele zake,hakuangalia ni kwa namna gani nilikuwa nimeumizwa,alivua cheo changu na kuniambia sitakuwa tena mkuu wa majeshi ya majini huko kuzimu,akaninyang'anya hata nguvu zangu, akampatia Jini Makata ili aliyechukua nafasi yangu.Nikabakia na uwezo mdogo kama wa majini wa kawaida.

    Sikuona umuhimu wa kuendelea kukaa kuzimu baada ya kupata pigo hilo kubwa,niliamua kuanzisha rasmi maisha yangu katika bahari ya Hindi.Hapo ndipo chuki yangu dhidi ya Gerrard ikazidi kuongezeka,asingelikuwa yeye, ningeendelea kuwa mtu mwenye heshima kule kuzimu lakini kwa sababu ya kushindwa kumuangamiza,ndio nikapewa penati zilizoniumiza sana.Nikawachukia hata na wanadamu wengine,mawazo ya kwenda kulipiza kisasi kwa wanadamu,yakazid kunijaa lakini nguvu sikuwa nazo.Nilinyang'anywa zote.

    "Ili ufanikishe hilo,tafuta mwanamke yeyote huko duniani,mwekee mimba,akizaa mtoto,mtumie huyo kulipiza kisasi chako hata ikiwezekana aje amwendee huyo Gerrard aliyekusababishia matatizo hayo",liliniambia jini lenzangu ambalo lilinigawia nguvu kidogo.Nikaendelea kukusanya nguvu kwa majini menzangu kidogo kidogo,mwisho zikawa zimekuja nguvu za ajabu japo sio kama zile alizokuwa kaninyang'anya lusifa.

    Siku moja nilikaa kwenye pwani ya bahari hiyo,akatokea binti mmoja mzuri ambaye jina lake nilikuja kulijua baadaye,Gradness.Huyu yeye alikuwa amekuja kuogelea na wenzake ,nilitafuta mwanya, nikawa nimekaa kwenye kizazi chake.Nilifanya naye mapenzi usiku mmoja akiwa amelala bila yeye kujua japo asubuhi alihisi maumivu sehemu zake za siri,ndio akawa amepata ujauzito ambao hata hakujua kuwa anao.Niliuficha,hakuuona.

    Baadaye Gradness alikuja akaolewa na kijana mmoja aitwaye Andrew.Walianza maisha yao ya ndoa wakitarajia kuwa watapata mtoto na Gradness akawa anapata mimba,kila zikifikisha miezi nane,naua yule mtoto na kuiharibu mimba kwa sababu wewe ulikuwa kwenye lile tumbo.

    Kwa bahati nzuri hawakuwa watu wa kusali sana,hivyo niliwaonea sana bbila wao kujua.Mwaka wa kwanza ukakatika mpaka miaka mitatu,kila akibeba mimba na kufikisha miezi nane,nikaua na kuitoa.Nilizidi kufurahi,hata hakumshirikisha mtu yule akaaye kule juu,alichokifanya,akazunguka kwa wataalam wa afya,akaenda kwa madaktari tofauti lakini akaishia kuambiwa hana tatizo lolote.

    Taratibu mme wake,Andrew akawa ameanza kuyapunguza mapenzi ya dhati aliyomuoneshea katika miaka hiyo mitatu ya ndoa yao.Gradness akawa mtu wa mawazo kiasi cha kujikuta anapata vidonda vya tumbo.Hapo nikazidi kuppata mwanya wa kuweza kuiongoza akili yake.

    Ndipo siku moja alipoenda sokoni,nikaiongoza akili yake kununua kisu ambacho hakujua hata ana matumizi gani nacho ila nilikiandaa mahususi lengo likiwa wewe mwanangu upate damu ya kunywa.Alipofika nyumbani siku hiyo,akakuta mme wake anafanya mapenzi na msichana mwingine.Gradness akaumia sana,alikichukua kisu kwa uchungu wa hali ya juu na pale msichana yule alipotoka,Nilizikamata akili zake akawa amemuchoma kisu cha tumbo hadi utumbo ukawa umemwagika chini,yule msichana akafa.Nikazidi kuzikamata akili zake,akamuua hata mme wake.

    Baada ya kumaliza kufanya mauaji hayo,ndipo nikamtokea na kumweleza kwamba nataka anizalie mtoto ambaye atakuwa nusu jini,na nusu mwanadamu.Nilimnyoshea kidole changu cha shahada na kumgeuza katika umbilee lako wewe mwanangu.Sisi majini huwa tuko tofauti na binadamu,ulikuwa umeshakuwa na ulianza kuniambia kwamba una hamu ya kuja kulipiza kisasi.Nilishangilia niliposikia hayi,nikakwambia kuwa Gradness nilikuwa nimemtumia kuua bila kujua ili wewe unywe damu za watu wale.

    Nilinyosha tena kidole changu,Gradness akawa amerudia kwenye umbile lake la kibinadamu na akiwa na akili zake na sio zile za kuongozwa na mimi.

    "Nani kawaua hao?",alisema Gradness akiwa amejawa na mishangao isiyoelezeka.Ndipo alipokuja kujua kuwa mimi ndiye nilitumia akili zake na kusababisha aue bila ya yeye kujua.Moyo wa kuua haukuwa ndani yake japo mmewe alikuwa kamsaliti,alilia sana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku ya siku akawa amekuzaa wewe,manesi waliomzalisha walishangaa jinsi ulivyozaliwa.Kwanza ulianza kwa kutanguliza miguu badala ya kichwa,pili ukapiga chafya kama ya mttu mzima badala ya kulia kama watoto wengine wafanyavyo.Manesi waliogopa sana na siku ya kuzaliwa kwako nilikuwa pembeni nikishuhudia,Nilichokifanya ili kuhakikisha nazuia siri isijulikane,nikamuua Gradness punde baada ya kukuzaa,alirurusharusha miguu yake na kutokwa na mapovu mdomoni na huo ukawa mwisho wake.

    Wakati wanaosha maiti yake,walishangaa Gradness kafungua macho na anawatazama.Wale waoshaji wakakimbia maana kilikuwa kitendo cha ajabu.Huyo Gradness bado yupo na wale wawili aliowachoma visu bado wapo,siku zao za kufa hazikuwa tayari,wako hapahapa kuizmu.

    Mwanangu,nawachukia sana wanadamu.Natamani hata niuangamize ulimwengu wote na wanadamu wafe,asingekuwa mwanadamu,ningekuwa bado niko karibu ya mfalme wetu Lusifa,nikiendelea kuongoza majeshi ya majini huku kuzimu.Kazi bado ippo,mimi baba yako siwezi tena kufanya kazi hiyo,mpaka sasa nimekuwa wa kuombaomba nguvu kutoka kwa majini wenzangu.Siwapendi wanadamu na hicho ndio chanzo cha mimi kukutuma wewe ukalipize kisasi kwa niaba yangu.

    **********

    Johson aliposikia hadithi hiyo ambayo baba yake Subiani,alikuwa akimsimulia alihamaki zaidi.Na yeye alijihisi kuwa kama babaye,akawachukia wanadamu kama babaye.

    "Baba,huyo Gerrard bado anaishi!"

    "Ndiyo,ila kwa sasa ashakuwa mwinjilisti,ni mhubiri wa kimataifa,hutamuweza?"

    "Nitamuweza baba na je tukimwangamiza Mfalme wetu Lusifa anaweza akakusamehe na kukurudisha kazini tena?"

    " ndiyo mwanangu,saizi ndio atakuwa anamkela zaidi kwa sababu hafichui siri zake tu,bali anabadili mioyo ya watu,anawatoa watu kutoka kwenye ulimwengu wetu na kuwahamishia kwa mtu yule!"

    "Baba,nakuahidi kumwangamiza huyo Gerrard?"

    "Hutaweza mwanangu?"

    "Nitaweza baba,nakuahidi,hata kama sio leo ila lazima nimuangamize"

    Kilikuwa ni kiapo alichokitoa Johson kwa baba yake.Safari yake ya kulipiza kisasi ndio ilikuwa inaanza.

    "Safari hii baba nataka nikaanze na shule huko duniani,nitaendelea kumsaka Gerrard mpaka nijue aliko"

    "Sawa mwanangu,kama umeweza kumweka jela mch.Gregory Msigwa na kumchafua,hata kwa Gerrard utaweza"

    Babbaye Johnson,Jini Subiani alimfariji mwanaye.

    Johson alitoka kuzimu na kurudi tena duniani akiwa amevaa umbile lake lake la kibinadamu.Alifika usiku na kukaa barabarani na kuanza kulia kama mtoto ambaye alikuwa ameachwa,kwa vile alikuwa kakuakua,alikuwa anaweza kutembea na kukaa.Alikaa pale barabarani akilia.

    Kwa bahati mbaya ikapita gari moja,aliyekuwa akiiendesha alipoona mtoto mdogo analia pekee,akadhani atakuwa ameachwa na wazazi wake au ni mtoto wa mittaani.

    "Hujambo?",alisalimia mtoto yule.

    "Sijambo mjomba,shikamoo?",alisema mtoto yule huku akilia.

    "Marahaba,mbona uko mahari hapa usiku wote huu,huogopi?"

    "Mama yangu kaniacha huku,kaniambia atarudi kunichukua mpaka sasa hajarudi"

    "Unaitwa nani?"

    "Johnson"

    "Unakaa wapi hapa?"

    "Mii sijui hata kwetu ni wapi?,mama hakuniambia,leo ndio nimetoka hospitali baada ya kuumwa tangu nikiwa mtoto mchanga.Nipona tangu jana"

    "Pole sana!"

    "Asante"

    "Basi ngoja twende ukalale kwangu leo,sawa mtoto"

    "Ndiyo,mjomba"

    Alijibu Johson na kunyanyuliwa kwenda kwenye gari. Laiti mtu huyo angejua balaa alilolibeba,asingethubutu kujifanya msamalia mwema.Safari ikaanza‚kimoyomoyo Johson akasikika akisema maneno ya ambayo hupendelea kuyasema,

    "KWETU NI KUZIMU,DUNIANI NIMEKUJA KULIPA KISASI"



    Wakati gari linaendelea kuchoma mafuta,ulitokea mwanga mkali mbele ya kioo cha gari na haukujulikana ni wapi ulikokuwa umetokea.Dereva alisimamisha gari baada ya kushindwa kuona vizuri mbele.Aliyashikilia macho yake kwa mikono,taratibu yakawa yameanza kumuuma na ni kama alikuwa yuko kwenye moshi.Alipojaribu kuyafikicha,ngozi ya juu ya jicho(Choroid layer),ikatoka.Badala ya machozi kumtoka,akashangaa ute ute mzito unatoka na uko mikononi akayafumba macho na kuanza kulia kwa uchungu.

    "Aaaaaagh! Johson,Johson nisaidie kuchukua leso mfukoni!",aliongea dereva huyo bila kujibiwa.

    "Johnso,Johson,uko wapi?",alizidi kusema bila kupata jibu.Tayari Johson alikuwa kashapotea na alikuwa anajiandaa kufanya kazi iliyokuwa imemtoa kuzimu na kuja duniani.

    Dereva yule akabaki kayashikilia macho yake,yalikuwa yanamuwasha sana,alipojaribu kujikaza kwa kutokuyafikicha,ndivyo yalivyozidi kumuwasha zaidi.

    "Johson,umeenda wapi? Kwa nini hutaki kunijibu!",aliongea dereva yule kwa masikitiko makubwa sana.Kimbelembele chake cha kujifanya msamaria mwema ndicho kilichomsababishia hayo,huenda hakutambua kuwa dunia ya sasa,kabla hujamsaidia mtu,unatakiwa kuupa umakini nafasi ya kwanza.

    Uvumilivu ukamshinda,akayafikicha tena.Hapo ndipo aliharibu kabisa,ute mzito ukatoka na yeye akawa anauhisi mikononi.Macho yakazidi kumuwasha,na yeye akashindwa kujikaza,akayafikicha macho,damu zikaanza kumtoka.Akalia kwa uchungu na kuanza kupiga kelele akiita

    "Johnson nisaidieeeeee,nitakufa"

    Alipomaliza kusema hivyo,mbele ya gari lake,alitokea Johson akiwa katika umbile lake harisi la ujinini,maana yeye alikuwa nusu binadamu,nusu jini.Kama kawaida yake,alihitaji kumtesa kwanza dereva huyo aliyejitolea kumsaidia kabla hajamuua.Aliongea maneno ya ajabu,ukatokea upepo wa ajabu uliokuwa umegubikwa na sauti za kutisha.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dereva aliyekuwa ndani ya gari akiendelea kulia,alizisikia sauti zile za kutisha,hizo nazo zilianza kuumiza masikio yake.Akalia sana lakini kwa ujinga labda uliosababishwa na yeye kutokuwa karibu na mungu,hakusika hata akiomba mungu aje amwokoe kwenye maafa hayo mazito.Kelele zile zikamuumiza sana,taratibu akasinyaa,akawa ameangusha kichwa chake kwenye usukani wa gari na kupoteza maisha.

    Johson alipoona kashamaliza kazi yake,alihitaji kutumia uwezo wake kwenda kuidhuru hata familia ya dereva huyo.Furaha yake yeye ilikuwa ni kuona wanadamu wanakufa.Kwa uwezo wake wa ajabu,akawa ameuingia mwili wa dereva yuleyule ambaye alikuwa kamuua,aliliwasha gari na kwa kutumia nguvu zake za kishetani akaenda mpaka nyumbani kwa yule dereva.

    "Mme wangu,umeniweka macho mpaka sasa hivi,kitu gani kimekukuta?",aliongea mke wa dereva yule kwa kudhani kuwa aliyekuwa akisema naye ni mmewe kumbe sio ila jini lililouvaa mwili wake.

    "Mmmh!,ngoja nikaoge kwanza, nitakujibu nikimaliza!",liliongea jini lile na kwenda mpaka chumbani,likabadilisha nguo na kwenda kuoga.

    Lilipomaliza kuoga,likakaribishwa chakula

    "Mii bado sijala,watoto wetu ndio wamekula na wameshaenda kulala.Leo nimepika chakula vizuri"

    alizidi kuongea yule mwanamke bila kujua chochote.

    Johson alinawa,bila hata kuombea chakula,wakaanza kula.Walipomaliza wakawa wameenda kulala.

    "Mme wangu,kesho ni wikendi.Mwezi sasa umepita unanipa mzungu wa nne,leo nina hamu na wewe.Hata kama umechelewa ila mechi lazima tucheze";Aliongea mwanamke yule akijua yuko na mme wake wa siku zote.

    "Hata mimi nilikuwa na hamu na wewe,hebu soge hapa",alisema Johson .Ili aonekane kweli ni mme yule yule wa mwanamke huyo,Johson alihitaji kuonesha ufundi wake,akisha mfikisha kileleni tu,basi amwangamize.Hakutaka afanye mambo yake kwa pupa.

    Hatimaye,mama wa watu akapandishwa mpaka akalewa.

    "Kacha! Kacha! Kacha!",kilisikika kitanda kikilalamika kuttokana na watu hao kufanya mambo ya watu wazima, zoezi likaendelea,kama ni magoli yakafungwa mengi lakini ghafla yule mama alianza kubadilika usoni.

    Alianza kubadilika,uso wake ukawa kama kamwagiwa tindikali,damu nyingi zikaanza kumtoka kwenye kizazi.Akasikika naye akilia na kuita

    "Mme wangu,nisaidie"

    Hakusikia akijibiwa.Alipotazama vizuri na kumwona mtu ambaye alikuwa akimwita, "Mme wangu",zilisikika kelele za mtu akiita aliyemzaa badala ya mungu

    "Mamaaaaaaaaa"

    Tayari alikuwa kashauawa.Johson,alisogeza mdomo wake kwenye kizazi cha yule mwanamke na kunyonya damu.

    Baada ya kufanya ushenzi huo,hakutaka kuwaua wale watoto ila alichokifanya,aliongea vi maneno vyake vya ajabu ajabu,shoti ikatokea kwenye ile nyumba,moto ukawa umeanza kuwaka.Na yeye akaondoka ili kuendelea na kazi iliyomleta duniani.

    ************

    Mwimbishaji;

    Kama unampenda Yesu sema Amen.

    Watu;

    Amen

    Mwimbishaji;

    Kama unampenda Yesu sema ni Bwana

    Watu;

    Ni Bwana

    Mwimbishaji;

    Haleluya!

    Watu;

    Amen

    Mwimbishaji;

    Haleluya!

    Watu;

    Amen

    Mwimbishaji;Haaa....leeee....ruuuu....yaaaa

    Halelu,,,yaa!

    Alikuwa ni mwimbaji mmoja akiwachangamsha watu kwenye mkutano mkubwa wa injili punde baada ya kumaliza kuimba wimbo wake.

    Baada ya sifa kumalizika,ulikuwa ni mda wa kuabudu kwa ajili ya kuombea neno.Walipomaliza kuabudu,mhubiri akawa ameitwa madhabbahuni ili atoe neno la mungu.Hakuwa mwingine bali Gerrard Sanga,mwinjilisti wa kimataifa.Baada ya kuwa amehubiri mataifa mbalimbali kama Kenya,Nigeria,Afrika kusini,Zambia,Marekani na mataifa mengine na huko akiwa anatumiwa na mungu mtenda miujiza,leo alikuwa yuko viwanja vya jangwani,dar es salaam.

    Mamia ya watu walijazana pale,uwanja hata ulikuwa hautoshi.Waliokuwa na wagonjwa mahututi waliwaleta,viwete,viziwi na mabubu wakawaleta ili mungu akawafungue kupitia mtumishi wake.

    "Bwana Yesu asifiweeeeee!",aliongea Ev.Gerrard Sanga na umati wa watu ukamwitikia kwa kusema kwa sauti

    "Ameeeeeeeeeeen!"

    "Naona mbingu zimefunguka,nawaona malaika wa Bwana wakiwa mahari hapa.Uwepo wa mungu ulioko hapa ni mkubwa hebu tusimame sasa tukamwite akae katika mioyo yetu,tukalisikilize neno lake na yule adui shetani aliibaye tukamkee,tuombe",alisikika akisema Gerrard Sanga na kuanza kuomba.

    Ukiwa tu ndio mwanzo,hata hajaanza kuhubiri,walisikika watu waliokuwa na mappepo wakilipuka kwa sauti,na wengine walijaribu kukimbia huku wakisema uwanjani pale kuna moto unaowaunguza

    "Haleluya,Yesu yuko mahali hapa.Nimeshawaambia mahali hapa kuna uwepo wa Mungu usio wa kawaida",alisema Ev.Gerrard Sanga na kuanza rasmi kutoa neno la mungu.

    "Ufalme wa mbinguni sio lele mama,Biblia inatueleza kuwa tangu enzi za Yohana mbatizaji mpaka sasa,ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu,nao wenye nguvu wanauteka.Ole wako wewe unayeingia kanisani kila siku ili uonekane unasali sana ilihali huna mungu, ole wako.Siku mbaya zinakuja, ambazo neema ya wokovu itaondolewa,hata wahubiri unaowaona leo hutaweza kuwaona.Utatamani uokoke lakini itashindikana,Yesu ninaye mhubiri leo,bado anapatikana na yeye yuko tayari kukusamehe ukimpa maisha yako",alizidi kutwangwa injili kwa maneno hayo na kujifuta jasho kwa leso,akaendelea.

    "Watu wa siku hizi,mnapenda sana mahubiri ya kubarikiwa.Ndugu zangu,utafuteni kwanza ufalme wa mbinguni na haki yake,hayo mengine yote mtazidishiwa.Bora ukakosa vitamu vya dunia lakini moyoni ukawa na Yesu"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwinjilisti huyo akazidi kubamiza injili, mpaka watu walikouwa wakimsikiliza hasa wale ambao hawakuwa wamempa Yesu maisha yao,wakajikuta wanatoa machozi,mahubiri yaliwagusa sana, wakaona kutenda dhambi sio dili tena.Alipoita watu wa kwenda kuokoka,walienda wengi kuanzia watoto mpaka wazee na yeye akawa amewaongoza sara ya ttoba,baada ya hapo ulikuwa muda wa kuombea watu wenye shida mbalimbali.

    "Ukiamini,utauona mkono wa Bwana.Yasiyowezekana kwa wanadamu,kwa mungu wetu huwa yanawezekana,endapo utakuja hapa kuombewa na hauna imani,usitarajie kuwa utapona.Mimi simponyi mtu,ila Yesu wangu ndiye atawaponya,kumbukeni hata maandiko yanasema,pasipo imani,haiwezekani kumpendeza Mungu,hivyo basi kama utataka uponyaji,amini kwanza, usiangalie tatizo ulilo nalo ukalilinganisha na mungu.Yeye anaweza mambo yote",aliwaonya watu waliokuwa wameppita mbele kuombewa lakini kutokana na wingi,wale waliokuwa vipofu na viziwi,aliwaambia waliowaleta wawashike masikioni kama ni viziwi na machoni kama vipofu.Alianza kushusha maombi.

    Acha mapepo yaanze kizaazaa,kukawa na kizungu mkuti kwa mashetani.Uwanjani pale ikatendeka miujiza mikubwa iliyowaacha watu midomo wazi,viziwi walisikia,viwete wakatembea,vipofu wakaona na waliokuwa wamefungwa na nguvu za giza wakafunguliwa.

    Wakati maombezi yanaendelea,kuna gari lilikuja na kumshusha mama mmoja kwenye macchera.Huyu alikuwa anaumwa kansa ya titi la kulia.Lilikuwa limeanza kuoza na kutoa harufu mbaya sana,hospitali waliwashauri ndugu zake wampeleke India wakalikate,lakini waliposikia kuwa Ev.Gerrard Sanga yuko hapo Dar es Salaam,walimtoa Muhimbili na kumpeleka pale akaombewe.

    Yule mama akiwa kwenye machela,alipofikishwa karibu,kuna mtu mmoja alikuwa kashabadilika na kuwa nyoka kabisa.Alikuwa joka kubwa,liliinua kichwa chake na kumtazama Gerrard,lilionekana kama linataka kumtemea sumu machoni.





    "SANDARABOKURIA,RIBOROBOSIKA,ROBO...ROBO...In the might name of Jesus christ,I command you demon,go away.Fireeeeeeh! Fireeeeeh! Fireeeeeh!",Ev.Gerrard Sanga alizidi kulikemea joka lile kubwa kwa ujasiri.

    "Hsssss! Hsssss! Hssss!",ni sauti pekee iliyotolewa na joka lile kubwa lililokuwa limeinua kichwa chake na kutoa ulimi wake nje huku likimwangalia mwinjilisti Gerrard kwa jicho baya.Lilipojaribu limtee sumu,iligoma kutoka mdomoni.Wakati hilo likiendelea,watu waliohudhuria mkutano huo,walikuwa pembeni wakishuhudia maajabu hayo ya mtu aliyekuwa kageuka nyoka.

    "Nimepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge,na nguvu zote za yule mwovu wala hapana kitu kitakachonidhuru.Damu ya Yesu iliyomwagika pale Gorigota,naimwaga juu yako.Damu ya Yesu......Damu ya Yesu.....Damu ya Yesu.Haya sasa funga vilago vyako na uondoke...Ondoka...Ondokaaa,Naseme ondoka,ondoka kwa jina la Yesu"

    Mwinjilisti Gerrard aliendelea kulihamakia(Kulikemea) lile joka.

    Joka lile lilianza kuyumba,likaanguka chini na kuanza kugalagala.Wakati linajaribu kurudi nyuma,Gerrard aliliamuru kwa kusema;

    "Kwa mamlaka niliyopewa na Yesu kristo,nakuamuru ewe joka,simama hapo hapo"

    Na kwa vile ulimi wa imani una nguvu sana,joka lile lilisimama na Gerrard akasogea karibu zaidi.

    Aliporikaribia,joka lile likajirusha kwa nguvu likitaka kujiviringisha kwenye mwili wake ili limwangamize lakini mungu ambaye huwa karibu na wamchao kuliko nguo zao za mwilini,hakuruhusu hilo litokee.Joka lile lilianguka na kutulia kabisa baada ya kupigwa na nguvu za ajabu za mwenyezi mungu.kwa jinsi lilivyokuwa limekaa,ni kama lilikuwa limekufa.

    "Kila pando asilolipanda baba yangu wa mbinguni litaenda kung'olewa.Katika jina la Yesu,nakuamuru ewe jini,achia mwili wa mtu huyo.Nimesema achia kwa jina la Yesu",

    Gerrard aliposema hivyo,joka lile likajikunjurua na kuchomoza kichwa.Gerrard aliendelea kukemea bila ya kuchoka.

    Kilichoanza kutokea,kilimstaabisha hadi Gerrard.Kile kichwa cha nyoka kilianza kubadilika na kuwa kichwa cha mwanadamu.Mwili wa joka ukabaki vilevile isipokuwa kichwa ambacho kilikuwa cha mtoto mdogo(Johson).Watu walipoona hilo,walistaajabu sana,wakasika wakinong'ona

    "Dunia ya sasa imeharibika,ee mungu tusaidie"

    "Usiniangamize,KWETU NI KUZIMU,duniani nilikuja kulipa kisasi na leo nilitaka kukuangamiza na sitarudi kwetu kuzimu bila kukua,mshenzi mkubwa ulimsababisha baba yangu ashushwe cheo kule kuzimu baada ya kushindwa kukuua.Lazima nikuue"

    Alisikika akisema Johson huku akiwa anatikisa mkia wake.

    "Ni nani awezaye kupambana na mungu ninayemuabudu? Mtetezi wangu bado yu hai.Ewe shetani uliyekaa kwenye mwili wa mtoto huyo,nakuapisha kwa jina la Yesu,mwachilie.Nimepewa mamlaka ya kufunga wala hapana atakayefunga na kufungua wala hapana atakayefunga.Tokaaaaaaaaaaa!"

    Aliongea Gerrard, kwa kazi aliyokuwa nayo.Alivua koti lake la suti na kufungua tai maana mapepo yana tabia ya kukaba tai na yanaweza yakakuua yakiiikamata kwa kutumia mwili wa mtu ambaye yanakuwa yamemuingia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Johson alipitiwa na nguvu ya ajabu zaidi ya ile ya kwanza,akaanguka chini.Umbile lile la nyoka likaanza kupotea,kifua kikawa kinaonekana na baadaye miguu ikatoka.Katoto kadogo kakawa kako chini kamekaa tu huku kakiwa uchi wa mnyama.Kwa muda wote huo,Ev.Gerrard Sanga,alikuwa akikemea.

    Johson akiwa yuko chini,aliona majini menzake maelufu kwa maelfu yakiwa na baba yake Subiani,yakimpa mkono na kujaribu kumsaidia lakini haikuwezekana.Majini yale yakajitahidi kumsaidia Johson lakini bado yakagonga mwamba.Uwepo wa mungu uliokuwa mahali pale ulikuwa mkubwa na nguvu ya mungu ilikuwa imemzingira Johson.

    Tangu azaliwe na Gradness,Johson alikuwa nusu binadamu na nusu jini.Ila kwa maombi ya Gerrard na uwepo wa mungu uliokuwa umetanda mahali ppale,unusu jini uliondolewa na kumwacha Johson akiwa binadamu na sio jini tena.Hilo liliwezekana kwa sababu ya mungu alikuwa akitenda kazi pamoja na Gerrard.

    Majini yale yaliyokuwa yamekuja kumsaidia,yalishindwa kufanya chochote na tayari yakaona jinsi ambavyo Johson alikuwa kashavuliwa uasili wa kijini kwa kubakizwa kuwa mwanadamu wa kawaida.Jini subiani ambalo ndilo lilikuwa baba yake Johson,lilihamaki sana lakini uwezo wa kupambana na mungu,liliukosa.Lilibaki na maumivu yake.

    Johson akiwa yuko chini akiwa tayari kawekewa mikono na Gerrard,aliombewa na baada ya muda,Gerrard alisikia sauti ya roho mtakatifu ikimwambia

    "NIMESHAMFUNGUA"

    Aliposikia hivyo,alimwangalia Johson ambaye alikuwa akishangaa shangaa.

    "Hujambo?",Gerrard,alimsalimia lakini Johson hakumjibu aliendelea kushangaa.

    "Hujambo?",alirudia kumsalimu.

    "Sijambo,shikamoo?"Alisema Johson.

    "Marahaba,unajua uko wapi?"

    "Hapana,sijawahi kuishi eneo kama hili na hao walio mbele yangu ni akina nani?"

    Gerrard aliposikia hilo akashangaa lakini kwa vile katika utumishi wake,alipenda sana kumsikiliza roho mtakatifu,alisikia sauti ikimwambia

    "Huyo alizaliwa akiwa nusu jini,nusu binadamu ila sasa,nimemfungua.Kila anachokiona ni kigeni kwake isippokuwa,nimwemwacha ajue kuongea na hayo mengine mtamfunza"

    hapo ndipo Gerrard akajua ni kwa nini mttoto yule aliuliza swali lile.

    "Enhee! Hao wanaitwa binadamu!"

    "Binadamu!"

    Alisema Johson kwa kushangaa.Mara akaja mama mmoja akilia

    "Mtumishi,tumeleta hapa mgonjwa aliyekuwa anaumwa kansa ya titi,hebu njoo uone kinachoendelea"

    Alisema mama yule na Gerrard akamkabidhi Johson kwa watumishi na kwenda kuangalia mama huyo.

    Alimuona kawekwa chini na kalazwa kwenye machela,usaha mzito mzito ulikuwa unamtoka.

    "Msimamisheni"

    alisema Gerrard na mama yule akashikiliwa vizuri na kusimamishwa.Gerrard alimsogelea na kuanza kumwombea,usaha uliokuwa mzito kama makamasi ukazidi kutoka na baadaye ukawa unatoka mwingine ambao ulikuwa umeachanganyika na damu.

    "Tulieni,Yesu anamfanyia oparesheni.Yeye ni daktari wa madaktari,hakuna ugonjwa asioweza kuutibu ili mradi unaamini!"

    alisema Gerrard Sanga.

    Mama yule aliyekuwa ana kansa ya titi,akazidi kutokwa na usaha.Kiukweli ulikuwa unanuka sana,kwa jinsi ulivyokuwa ukizidi kumtoka,aliendelea kulia kwa uchungu.Kilichomliza sio maumivu aliyokuwa akiyapata,ila yalikuwa ni machozi yaliyosababishwa na maajabu hayo ya mungu.

    Bado uwanjani hapo vimbembembe havikwisha,kuna watu walizidi kupagawa,mapepo yalikuwa yamewapanda na mmoja alipelekwa kwa Gerrard akiwa anapiga makelele.

    "Niko makaburini nakula nyama za maiti,,,iiiiiii,,,,niachieni"

    Alipofikishwa karibu na Gerrard binti yule alirusha miguu kwa fujo na kutaka kumkimbia Gerrard aliyekuwa akimsogelea.Kilichomfanya amuogope Gerrard ni uwepo wa malaika wanne waliokuwa,mbele,nyuma,kushoto na kulia wakiwa na panga zinazowaka.Hicho ndicho kilimfanya binti yule atake kumkimbia Gerrard.

    gerrard alipomkaribia,alimkemea na kwa imani akasema kashafunguliwa.Akawaambia waombaji waendelee kumwombea.

    Hatimaye mkutano huo uliofanyika jangwani,ukawa umewaponya wengi.Vipofu watano walifunguliwa macho wakaona ila watatu tu ndio hawakuona labda kwa sababu hawakuwa na imani na huenda walidhani Gerrard ndiye anawaponya hivyo wakamwamini yeye.Viziwi wakapona,viwette wakawa wametembea.Hakika mungu alikuwa amejitukuza sana.Mama aliyeenda akiwa na kansa ya titi,Yesu alikuwa akiendelea kumfanyia oparesheni na zaidi ni kubadilika kwa kiumbe ambaye sikunza nyuma alikuwa nusu jini nusu binadamu,yaani Johson.Hakika mungu ni mkuu na ni mweza wa yote.

    "Makofi na vigelegele kwa Bwana!",alisema Ev.Gerrard na watu wakapigga makofi na hivyo vigelegele na wanaume japo hawakuambia,wakasikika wakipiga na miluzi.

    "Si niliwaambia,yasiyowezekana kwa wanadamu kwa mungu yanawezekana.Si niliwaambia ukiamini utauona utukufu wa mungu.Haleluuuuuuuuuuuuuuyaaaah!",alisema Gerrard na kuitikiwa na umati wa watu.

    "Ameeeeeeeen"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sasa nataka "Praise and worship team",ije hapa mbele tuimbe wote ule wimbo wa HAKUNA MUNGU KAMA WEWE.twende sasa

    Hakuna mungu kama weeewe,

    Hakuna mungu kama weeewe,

    Hakuna mungu kama weeewe,

    Hakuna na hata kuwepo imba hakuna

    Watu;

    Hakuna mungu kama weeewe,

    Hakuna mungu kama weeewe,

    Hakuna na hata kuwepo.

    Mwimbishaji;

    Oooo nimetembeaaa

    Watu;

    Nimetembea kote kote,

    Nimezunguka kote kote,

    Nimetafuta kote kote,

    Hakuna na hata kuwapoooooo!

    "Imetoshaaaa!",alisema Ev.Gerrard Sanga na kushuka madhabahuni.Watu walishangilia sana na kumtukuza mungu,walisikika wakisema

    "Yesu,Yesu,Yesu,Yesu,Yesu,Yesu!"

    ***************

    Johson alichukuliwa na Gerrard na kwenda naye nyumbani.Tukio lile la Johson kubadilika kuwa nyoka lilichukuliwa na waandishi wa habari na kurushwa kwenye taarifa ya habari.Watu walioona hilo,walishangaa sana na wengine walidiriki kusema moja kwa moja huku wakiwa wameshika vinywa vyao

    "Hakika kweli,MUNGU YUPO, YATUPASA TUMUABUDU KATIKA ROHO NA KWELI"

    Johson alikuwa akishangaa kila kitu alichokiona,hakuwa anajua gari,nyumba,sahani,chakula wala nini.Kila kitu kwake kilikuwa ni kigeni kwani ulimwengu aliokuwa akiishi hapo mwanzo ni tofauti na huu mpya ambao baada ya kufunguliwa alikuwa akiuona.

    Ev.Gerrard Sanga hakuacha kuwa anamwombea Johson kila siku na kumkabidhi mikononi mwa mungu ili aliyekuwa baba yake Subiani asije akamdhuru.David alikuwa kashakuwa mkubwa na mda mwingi aliutumia kuwa karibu na Johson akimfundisha vitu.

    "Hiki kinaitwa kiti,ile pale ni video,na ileee kule inaitwa meza"

    Alisema David.Alikuwa mwalimu wa Johson kwa kumfunza vitu vilivyokuwa duniani.Hata kanisani,Johson akawa anappelekwa,akawa anasali kama binadamu wengine.Wala mawazo ya kusema KWETU NI KUZIMU,DUNIANI NIMEKUJA KULIPA KISASI,hayakuwemo tena ndani yake.Kiboko wa viboko na mfalme wa wafalme alikuwa kamfanya kuwa binadamu na kwa jinsi alivyokuwa akiombewa hakuna nguvu ya shetani ingeweza kumdhuru.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    AMA KWELI HAKUNA NGUVU INAYOWEZA KUSHINDANA NA MUNGU NA KILA MWANADAMU ANAYEMWAMINI MUNGU,HAWEZI AKADHURIWA NA IBILISI.TUMCHE MUNGU WA KWELI NA TUMWABUDU KATIKA ROHO NA KWELI ILI TUUONE UKUU WAKE MAISHANI.

    ******Mwisho wa simulizi yetu*****

0 comments:

Post a Comment

Blog