Search This Blog

NILIOLEWA NA MGANGA KWA TAMAA YA CHEO KAZINI - 5

 







    Simulizi : Niliolewa Na Mganga Kwa Tamaa Ya Cheo Kazini

    Sehemu Ya Tano (5)





    ILIPOISHIA:

    “Mmh! Temea chini babu umekamilika.”

    “Basi mjukuu, kama babu hakufikishi kuna dawa nitakupa utamwekea kwenye chai, nakuhakikishia tabu zote zitaisha nawe utafaidi kama wenzako.”

    “Nitashukuru babu, lakini baada ya kurudi safari yangu, naogopa nikimwekea sasa hivi na mimi kuondoka nitakuwa nawatengenezea wengine huenda nikirudi asiwe wangu.”

    SASA ENDELEA...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Basi ukirudi nitakupa.”



    “Nitashukuru, ila bado nilikuwa na ombi moja.”

    “Ombi gani mjukuu?”

    “Ila babu usinielewe vibaya.”

    Kwa kweli lazima niseme ukweli penzi alilonipa babu liliniridhisha akili na kutamani angalau nimpate kwa siku moja sehemu nzuri ili nikisafiri basi niwe mwepesi. Ilibidi nitengeneze mpango wa kumpeleka mjini kwa siku moja au mbili ili niweze kulifaidi penzi lake kwa kina. Niliamua mtoto wa kike kumvaa mzimamzima.



    “Sema tu mjukuu wangu mimi na wewe!” babu alinitoa hofu.

    “Babu najua mimi na wewe si wageni tena katika uhusiano?”

    “Ndiyo najua, vipi unataka uwe mke wa tano?”

    “Hapana babu.”



    “Unatakaje?”

    “Na...na...taka,” nilijikuta nikiingiwa na aibu ya kike kuishia kuuma kucha.

    “Mjukuu sema tu yaani hujui wewe ni zaidi ya wake zangu sema chochote nitakusikiliza.”

    “Nilikuwa nataka kama safari yangu itakuwepo uje tukae siku mbili kwangu.”

    “Kuhusu safari yako ipo kama nilivyokueleza baada ya kesho kuikamilisha kazi iliyobaki. Jumatatu jioni kuna taarifa zitakufikia juu ya safari yako ila Jumanne utapata uhakika kamili.”



    “Nitashukuru babu, kwa vile safari itakuwa Jumapili au Jumatatu najua nitapewa mapumziko ya kujiandaa na safari nataka nitafute hoteli nzuri nikae na wewe kwa siku mbili ili unimalize haja zangu kisha niondoke mwepesi mtoto wa kike.”



    “Hakuna tatizo wewe tu.”

    Kwa vile mazungumzo yetu tulikuwa tukitembea tulijikuta tukiingia maeneo ya nyumbani bila kujua.

    “Basi babu usiniangushe nakutegemea wewe, penzi la kwenye majani limekuwa tamu vile vipi la hotelini tena kwenye kitanda kipana si ndiyo nitasahau safari?”



    “Walaa, najua una kutu kwa siku mbili nitaitoa yote. Dozi nitakayokupa itakufanya usiwaze mapenzi mpaka unarudi.”

    “Unaona babu, hiyo ndiyo naitaka au tufanye siku tatu?”

    “Hizo mbili zinatosha si unajua hali aliyonayo shoga yako hapendi niwe mbali kwa kipindi hiki.”

    “Sawa, lakini usipozimaliza sikuruhusu uondoke.”



    Tulikuwa tumekaribia nyumbani, tulibadili mazungumzo, kwa vile ulikuwa usiku sana nilikwenda kwenye chumba nilichoandaliwa na kulala kuitafuta siku ya pili. Usiku ulikuwa mrefu kwangu niliwaza mengi juu ya uwezo wa kimapenzi wa babu yule ambaye ukimwangalia vibaya utasema atakufia kifuani.



    Nilifurahi kukubali ombi langu la kuja mjini kunipa raha kwa siku mbili kabla ya safari japo bado sikuamini kama safari kwa upande wangu ilikuwepo. Usingizi ulivyonichukua sikujua nilishtushwa na sauti ya Rose aliyeniamsha. Macho yangu yalikutana na mwanga mkali kuonesha kumekucha muda mrefu.

    “Vipi shoga mpaka asubuhi unakoroma jana ulichoka sana?”



    “Kiasi sema tumerudi muda mbaya.”

    “Kwa hiyo unaondoka saa ngapi?”

    “Siondoki leo.”

    “Kwa nini?”

    “Shughuli tulidhania ndogo kumbe nzito, jana hatukumaliza tunamalizia leo.”

    “Pole shoga ndiyo kutafuta huko usikate tamaa.”



    “Nashukuru shoga kwa moyo wako,” nilimshukuru Rose bila kujua kwenye kibuyu chao cha asali nami nimetia mkono.

    Niliamka kuoga na kukuta kifungua kinywa kimeshaandaliwa, niliungana na wenzangu kupata kifungua kinywa. Baada ya kufungua kinywa nilijumuika na wenzangu kuzungumza mawili matatu. Mzee Sionjwi alituaga anakwenda porini kufuata dawa ya kazi ya usiku.



    Ajabu wakati babu anaondoka nilimsindikiza kwa macho huku hali yangu ikibadilika na kutamani kitu kutoka kwake. Lakini nilijizuia kama asingekuwa ana wake ningemuomba nifuatane naye ili akanipe raha tena.



    angalau cha majanini ili usiku kwenye kazi tusiingie majaribuni na kuharibu tena tiba.

    ***

    Usiku kama kawaida baada ya chakula cha usiku na kupumzika kidogo safari ya mzimuni ilianza. Nilibeba vitu kama nilivyobeba jana yake ila tuliongeza na kuku mwekundu ambaye tulikwenda naye kwa ajili ya kuuomba mzimu msamaha kutokana na uchafu wetu wa jana yake.



    Tulipofika, nilivua nguo zangu zote na kujifunga upande wa kanga na yeye alijifunga kipande cha shuka nyeupe. Alimchukua kuku na kusogea karibu ya mti ule mkubwa na kusema kwa sauti ya juu.

    “Mzimu najua jana uliondoka kwa hasira, leo nimekuleta zawadi nzuuuuri, naomba uje uchukue.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alimweka kuku juu ya jiwe lililokuwa mbele ya mti mkubwa, mara ghafla nilisikia mtikisiko ukifuatiwa na upepo mwanana. Ghafla niliona majani yakizunguka kama kimbunga na kuelekea kwenye lile jiwe na kuzunguka kwa muda kisha ulipanda juu kuelekea juu ya mti ule mkubwa.



    Ajabu ya Mungu kuku yule hakuwepo kuonesha mzimu ulikuja kama kimbunga na kuondoka na yule kuku. Baada ya muda hali ilitulia na kutokea mguno mzito kisha pakawa kimya.



    Mganga alichukua usinga wake na maji ya dawa na kuanza kunyasia kila kona na kusema:

    “Asante mzimu, asante kwa kukubali ombi letu na kutuhakikishia kazi iliyofanyika imekwenda vizuri.”

    Baada ya kusema vile aliweka dawa kwenye maji yaliyokuwa kwenye beseni pamoja na majani ya kujisugulia. Alinieleza nijimwagie maji na kujisugua na majani kisha nijimwagie tena maji kuondoa uchafu na baada ya zoezi hilo aliniwekea kipande cha shuka nyeupe pembeni ili nijifunge.



    Ajabu ya Musa baada ya kunitayarishia kila kitu aliondoka na kuniacha peke yangu na yeye kwenda kuendelea na mambo mengine na kuniomba nikimaliza nimjulishe ili tuendelee na zoezi lingine. Sikutaka kuhoji ya jana yake na ya siku ile.



    Nilifanya kama nilivyoelekezwa kwa kujimwagia maji na kujisugua mwili mzima ilikuwa tofauti na jana yake kujisugua kiungo kimojakimoja na kujimwagia maji na kuhamia kingine lakini siku ile baada ya kujimwagia maji mwili mzima nilitakiwa kujisugua na majani yale mwili mzima kisha kujimwagia maji tena baada ya hapo zoezi lile linakuwa limekwisha.



    Baada ya kumaliza zoezi nilivua kanga iliyokuwa imetota kwa maji na kujifunga kipande cha shuka nyeupe kisha nilimwita babu kuwa nimemaliza.



    Baada ya kumaliza zoezi  nilivua kanga iliyokuwa imetota kwa maji na kujifunga kipande cha shuka nyeupe kisha nilimwita  babu na kumweleza nimemaliza kuoga maji ya dawa. Babu alikuja na kunieleza nizunguke mti ule mkubwa mbele yake kulikuwa na kichuguu na kunieleza nipande juu ya kichuguu ili anipandishe nyota.



    Kabla ya kupanda alinivisha hirizi mbili moja nyeusi na nyeupe na shanga za rangi ileile ya hirizi zile mbili. Baada ya kunivisha hirizi na shanga alinipa kibuyu kidogo kilichokuwa na shanga mchanganyiko shingoni na kunieleza nipande nacho juu ya kichuguu huku nimekibeba kichwani.



    Nilifanya vile kisha babu naye alipanda na kuanza kunichanja baadhi ya sehemu alizozichagua.  Baada ya kumaliza kunichanja alinieleza nitoe kibuyu kichwani na kunyoosha mikono kisha niombe mambo ninayoyataka kimoyomoyo. Nami niliomba niipate ile nafasi ya kwenda kusoma ulaya pia niipate nafasi ya juu katika kazi yangu na mshahara mnono.



    Wakati nikiomba vitu ninavyovitaka ilishuka mvua ya nguvu ya dakika mbili na kunifanya nihofie kazi yetu kuharibika kwa mara ya pili, lakini babu alisema:



    “Mjukuu una bahati kila kitu chako kinaonekana kina baraka toka kwa mizimu. Hakika kila ulichokiomba kitakubaliwa.”



    Baada ya zoezi lile alinieleza niteremke chini huku nimenyoosha mikono kwa mbele nikiwa nimekishika kibuyu. Baada ya kuteremka alikichukua kibuyu chake huku akionesha tabasamu kwa kazi yake kwenda vizuri sana.



    “Mjukuu una nyota kali sana katika watu waliowahi kuja mzimuni wewe umekuwa na bahati kubwa.”



    “Usiniambie!”



    “Kweli mjukuu, kila kitu kimekwenda kama ulivyotaka.”



    Zoezi la siku ile halikuchukua muda mrefu kama jana yake, tulibadili nguo na kurudi nyumbani kupumzika ili kesho nifanye safari ya kurudi mjini na kuusubiri muujiza wa babu. Pamoja na kupewa matumaini makubwa lakini bado kwangu ilikuwa kama njozi ya mchana.



    Sikutakiwa  kuhoji kitu kwani nilionekana kama naingilia kazi pia simuamini. Baada ya kufika nyumbani nililala mpaka siku ya pili, niliamshwa alfajiri na kuogeshwa maji ya fukuto kisha sikutakiwa kurudi ndani nilitakiwa niondoke.



    “Mjukuu wangu kazi imekwisha unatakiwa kwenda kwenye gari na kuondoka.”



    “Sawa babu.”



    Niliondoka bila kuwaaga wenyeji wangu hasa shoga yangu Rose, sikuwa na jinsi yalikuwa ndiyo masharti ya babu. Katika wake wa mzee Sionjwi niliagwa na mkewe mdogo aliyeamka kunipashia maji moto wengine niliwaacha wamelala, nilijiuliza Rose atanilaumu vipi kuondoka bila kumuaga, haikuwa amri yangu bali masharti ya mganga.



    Nikiwa kwenye gari langu tayari kurudi mjini nilijiuliza itakuwaje kama nikimuhitaji babu. Ajabu babu hakushughulika tena na mimi baada ya kuniaga alirudi ndani. Niliwasha gari na kuondoka huku nikijawa na mawazo juu ya babu kuja mjini kama nitaipata nafasi ya kwenda kusoma.



    Wasiwasi wangu huenda babu kaona ngoma nzito hivyo katafuta sababu ya kutokutaka kuniaga kwa kujua lazima tungeagana aje mjini hivyo asingekuja kutokana na kazi aliyoifanya kwenda kinyume japo yeye mwenyewe alijinadi  hashindwi na kitu  kisicho amri ya Mungu.



    Kwa vile ilikuwa alfajili niliendesha gari kwa uhuru mkubwa kutokana na hakukuwa na magari njiani mpaka nilipoanza kuingia mjini ndipo nilikutana na magari machache mpaka naingia nyumbani kwangu sikupata usumbufu wowote.



    Kwa vile siku ile  ilikuwa ni Jumapili sikutaka kufanya kitu chochote nilijipumzisha kutokana na kushindwa kulala vizuri kwa siku mbili nilizokuwa kijijini. Kutokana na uchovu mkubwa nililala kama mfu, nilishtuka jioni ikiwa njaa inaniuma sana.



     Nilikwenda kwenye bar ya jirani na kuchukua chipsi na kuku na kuja kula.



    Baada ya chakula niliandaa nguo zangu za kuvaa siku ya pili kazini kisha nilipanda  tena kitandani kulala. Ajabu nilipopanda kitandani mara ya pili nilijikuta nikilikumbuka penzi la babu na kutamani siku ile kama angekuwa karibu yangu ingekuwa nzuri kwangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kingine kilichonichanganya ni jinsi tulivyoagana na babu bila kupeana miadi ya kukutana, moyoni mwangu nilipanga hata kama nitakwenda kusoma lazima nimlete mjini ili anikate kiu. Usingizi hata ulivyonichukua sikujua mpaka nilipoamshwa na alam ya alfajiri ili nijiandae kwenda kazini.



    Niliamka kama kawaida na kwenda kuoga na kuvaa nguo zangu na kuwahi kazini huku nikiwa bado najiuliza alichokisema mzee Sionjwi kitawezekana japo hapo nyuma alinifanyia mambo makubwa lakini lile nililiona zito kutokana na mchakato  na hatua aliyofikia.



    Kama kawaida niliwasili ofisini na kujipangia majukumu ya siku ile, kabla ya kuanza kazi nilimpigia simu shoga yangu Safia. Baada ya kusalimiana nilianza kazi kama kawaida huku nikisubiri kupata taarifa yoyote kuhusiana na Happy Kinono msichana aliyechaguliwa kwa hila kwenda kusoma nje.



    Japo nilikuwa kazini lakini akili yangu yote ilikuwa kusubiri tukio nililoelezwa na babu.  Ajabu muda uliendelea kukatika bila kupata taarifa zozote, niliangalia saa ya mkononi ilionesha bado kama dakika kumi muda wa kutoka kazini ufike. Sikuiamini saa yangu niliangalia ya ukutani nayo ilinionesha muda uleule nilioangalia kwenye saa ya mkononi.



    Kutokana na kuchanganyikiwa hata hiyo sikuiamini niliangalia saa ya kwenye kompyuta haikupishana sana na saa zote nilizoangalia. Nilijikuta nikikata tamaa kuona tulichokifanya kwa babu kilikuwa kazi bure. Niliingiwa wasiwasi huenda tukio la kufanya uchafu mzimuni ulisababisha mambo yaharibike.



    Muda ulipotimu nilianza kufungasha vitu vyangu ili niondoke kuwahi nyumbani. Mara simu yangu iliita nilipoangalia ilikuwa inatoka kwa Safia, nilijua tu alitaka kujua kama naondoka kwa vile aliniomba lifti kutokana na mumewe kuwa na udhuru.



    Niliipokea kwa kumwambia:



    “Shoga nisubiri kwenye gari ndo nafungasha.”



    “Shoga nilitaka nikuombe unisubiri hata robo saa kwa vile kuna kazi naimalizia ili tuondoke wote.”



    “Hakuna tatizo, basi nitakusibiri ofisini kwangu.”



    “Tena shoga nina ubuyu (umbeya) mpya hata sokoni haujaingia,” Safia alinirusha roho.



    “He! Wa nini tena?” nilishtuka.



    “Shoga kwa vile tunaondoka pamoja basi nitakupakulia wa haja.”



    “Mmh! Haya.”



    Kwa vile nilikuwa nimesimama niliweka mkoba wangu juu ya meza na kuketi kwenye kiti changu kumsubiri Safia huku nikiwa na shauku kubwa ya kuusikia huo ubuyu ambao haujaingia hata sokoni. Nilijikuta nikiwaza huenda ni taarifa niliyoambiwa na babu Sionjwi ya kusikia taarifa ya kushtua.



    Lakini nilikuwa mpole kuusubiri huo ubuyu ili nijue unahusu nini pia yaliyosemwa na mzee Sionjwi yana ubashiri gani. Baada ya dakika ishirini Safia alinifuata ofisini akiwa na tabasamu pana kitu kilichonishtua.



    “Vipi shoga unaonekana leo una furaha kulikoni?”



    “Mmh! Mbona makubwa madogo yana nafuu.”



    “Yepi tena hayo shoga?”



    “Kwa vile tunakwenda pamoja nisikuonjeshe ukakinahi mapema.”



    Sikutaka kuongeza neno, nilibeba begi langu na kuongozana na Safai kuelekea kwenye gari langu.



    Baada ya kuingia ndani ya gari tuliondoka eneo la kazini huku nikiwa na hamu ya kujua ubuyu huo una ladha ya aina gani.



    Tulipotoka kidogo  Safia alianza kunipa ubuyu nami nilitega masikio huku mapigo ya moyo ukinienda mbio.



    “Basi dada kuna bonge la gogoro.”



    “Lipi tena hilo?”



    “Aliyeteuliwa kagoma kwenda mpaka aipate ndoa.”



    “Mteuliwa nani?”



    “Si Happy.”



    “Happy yupi?”



    “Aliyewaengua na kuchaguliwa kwenda kusoma ili akirudi awe juu yenu.”



    “M’hu.”



    “Basi ndiyo kagoma kasema haendi mpaka wafunge ndoa anataka aondoke kama mke wa mtu na si mchumba.”



    “Sasa kuna tatizo gani bado muda upo wa kufunga ndoa na kwenda kusoma.”



    “Kweli walikuwa na mpango wa kufunga ndoa lakini safari ya kwenda kusoma ilivuruga kila kitu.”



    “Kama walikuwa wameisha jipanga wanaweza kwenda kufunga ndoa tu, sherehe akirudi.”



    “Inavyosemekana walikubaliana kufunga ndoa baada ya kurudi, lakini kuna taarifa kazipata kuwa mchumba wake ana mwanamke mwingine, kitendo cha kwenda kusoma huku nyuma wanafunga ndoa na akirudi akute kila kitu kimekwisha.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mmh! Makubwa, sasa yeye taarifa hizo kazitoa wapi?”



    “Hata najua.”



    “Wewe nani kakuambia?”



    “Mkurugenzi.”



    “Ilikuwaje mpaka akakuteleza habari hizo?”



    “Huwezi kuamini leo meneja alikuja mapema na kuingia kwa mkurugenzi, wamekaa ndani zaidi ya saa nne. Alipotoka alionekana kachanganyikiwa, si ndiyo mama usipitwe nikamfuata mkurugenzi kutaka kujua kuna kitu gani kimemtokea meneja.



    “Ndipo aliponipa ubuyu huu, kuna kitu alinieleza kuwa kama itashindikana wangemteua mtu mwingine haraka kabla ya Jumatano si ndiyo na mimi nikapiga chapuo uende wewe.”



    “Ehe! Akasemaje?”



    “Akasema anasubiri jibu la meneja atakalompa jioni kuwa mchumba wake anakwenda au haendi. Kama haendi kesho asubuhi waanze mchakato wa kumtafutia viza mtu watakayemteua.”



    “Mmh!” nilijikuta nikiguna tu.



    “Tena huwezi kuamini maombi yangu yule msichana akatae kwenda ili uende shoga yangu.”



    “Bado muda huenda wakakubaliana.”



    “Aah, wapi mwanamke yule ameapa hatakwenda bila ndoa.”



    “Mmh! Ngoja tuone.”



    “Ukweli wa mbivu na mbichi utazijua kesho asubuhi.”



    Nilimpeleka Safia mpaka kwake kisha mimi nilirudi nyumbani kupumzika nilijiuliza yaliyozungumzwa na Safia yana ukweli gani. Nilijikuta nikitabasamu mwenyewe baada ya kuiona kauli ya babu inakaribia kuwa kweli. Niliamini jibu la kesho ndilo litanipa picha kamili kama nitakwenda mimi au la.



    Wasiwasi wangu ilikuwa kama kitaitishwa kikao cha bodi ya uteuzi ningeweza kupoteza nafasi ile. Lakini majina niliyopeleka kwa babu niliamini yakafanya kazi japokuwa sikuwa na uhakika kama watakuwa ni walewale.



    Siku ya pili nilikwenda kazini kama kawaida nikiwa na shauku kutaka kujua kuna jipya gani kutokana na kauli ya mchumba wa meneja kama bado ana msimamo uleule wa kutaka ndoa kabla ya kwenda au kuna mabadiliko yoyote. Kama kawaida kabla ya kazi nilimpigia simu Safia kumjulia hali lakini nikiwa nataka kujua kuna habari gani mpya juu ya taarifa alizonipa jana yake.



    Baada ya salamu hakuna kilichoendelea zaidi ya kunitakia kazi njema, nilijiuliza ina maana hakukuwa na kipya kutokana na taarifa zake za jana yake.



    “Safia bosi amefika?” nilijifanya kumuulizia bosi ili nisikie Safia ana taarifa gani.



    “Muda tu.”



    “Vipi kuna jipya?”



    “Mpaka sasa sijasikia kitu ndiyo maana sijakueleza chochote.”



    “Kwani meneja leo hajaja?”



    “Sijamuona.”



    “Labda wamemalizana.”



    “Kina nani?”



    “Meneja na mchumba wake.”



    “Mh! Kwa kweli nami bado nipo njia panda maana jana alinieleza jibu la kusafiri au kutosafiri ningelipata asubuhi lakini imekuwa kimya.”



    “Kwani mkurugenzi anaonekanaje?”



    “Yupo kawaida.”



    “Mh! Sawa, hukumuuliza?”



    “Nitaanzia wapi, siku zote mimi mtekelezaji kuuliza ni kiherehere labda alianzishe yeye ndipo nimchimbe.”



    “Mh! Sawa.”



    “Shoga usikate tamaa hata kama hutaenda bado thamani yako ni kubwa sana.”



    “Basi baadaye.”



    “Poa.”



    Nilikata simu ili niendelee na kazi lakini hamu yote ilikatika hasa nilipokumbuka kauli ya Safia kuwa hata nikikosa sitapungukiwa na kitu bila kujua jinsi gani nilivyoitafuta nafasi hiyo kwa udi na uvumba kufikia hatua ya kujidhalilisha kwa kiasi kikubwa. Kwa kauli ile ilionesha wazi hakukuwa na safari.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilijiuliza ile taarifa ya kushtua niliyoambiwa nitaisikia jana yake ambayo niliamini ilikuwa ni ile ya mchumba wa meneja kugoma kusafiri lakini imekwenda kinyume. Matumaini yalikatika ghafla ya kujiona kama nimetwanga maji kwenye kinu na kupewa matumaini yasiyo na ukweli.



    Niliwasha kompyuta ili nianze kazi, lakini moyo ulitumbukia nyongo, niliangalia kioo cha kompyuta lakini hamu sikuwa nayo kabisa, wazo lilikuwa niombe ruhusa kuwa naumwa ili nirudi kwa babu kumuuliza. Sikutaka kufanya kitu, niliamua kuizima kabisa.



    Nilipitia mkoba wangu ili niende kuomba ruhusa niondoke zangu kwani mambo yalikwenda ndivyo sivyo. Nilipofika mlangoni simu ya mezani iliita, nilijiuliza niipokee au niachane nayo. Lakini niliona si busara kuiacha simu iite huenda ni mkurugenzi.



    Nilirudi kwenye meza na kuchukua mkonga wa simu na kupokea.”



    “Haloo.”



    “Ooh! Eflazia upo?”



    “Ni…ni…nipo bosi,” ilikuwa sauti ya mkurugenzi iliyonifanya nipate kigagaziko cha ghafla.



    “Njoo mara moja ofisini.”



    “Sawa nakuja.”



    Kwa vile ndiyo nilikuwa nataka kutoka niliweka mkoba juu ya meza na kwenda kumsikiliza bosi. Nilipofika kwa katibu wake muhtasi, ambaye alikuwa shoga yangu Safia aliponiona alishtuka.



    “Vipi shoga kwetu asubuhi asubuhi?”



    “Mkuu kaniita.”



    “Pita hakuna mtu.”



    Niligonga mlango na kulakiwa na sauti nzito ya bosi.



    “Pita ndani.”



    Nilifungua mlango na kuingia, bila kukaa niliitikia na kusimama kusubiri kuelezwa nilichoitiwa.



    “Eflazia kaa kwenye kiti.”



    Nilifanya nilivyoelekezwa na kusubiri maelekezo, bosi alionekana yupo bize na kusoma moja za karatasi zilizokuwa mbele yake. Nilikaa dakika kumi bila kuelezwa kitu chochote, baada ya kumaliza kusoma aliniita jina langu:



    “Eflazia.”



    “Naam bosi.”



    “Kweli riziki ya mtu huwezi kuizuia bali utaichelewesha.”



    “Ni kweli, unamaanisha nini?”



    “Unajua nafasi ya wewe kwenda kusoma nje nilipendekeza mimi, lakini kikao cha bodi kilinishinda kwa hoja.”



    “Sasa tatizo nini?”



    “ Ndiyo maana nikasema riziki haizuiliki bali huchelewa.”



    “Bado sijakuelewa.”



    “Nafasi uliyoitaka umeipata.”



    “Nafasi ipi?”



    “Ya kwenda kusoma nje.”



    “Na aliyechaguliwa?”



    “Anawaza mapenzi zaidi kuliko kazi.”



    “Una maanisha?”



    “Namaanisha kuwa yule msichana tuliyemchagua amegoma kwenda kusoma, baada ya taarifa ile niliweza kuwasiliana na wenzangu tukutane leo ili tuteue mtu mwingine. Mmoja alitoa wazo tukuchague wewe nami niliunga mkono basi umepita hivyo mama jiandae na safari.”



    “Etii?” nilimsikia lakini sikumwelewa nilikuwa kama nipo ndotoni.



    “Umechaguliwa.”



    “Ooh! Asante Mungu.”



    Nilipiga magoti kumshukuru Mungu huku nafsi ikinisuta nikiamini haikuwa amri ya Mungu bali kazi ya mzee Sionjwi ndiyo iliyobadili matokeo yale. Nilijua kabisa haikuwa hiyari yake Happy kuikataa safari adhimu kama ile bali kugeuzwa mawazo na nguvu za kiza.



    Nilikubaliana na mzee Sionjwi kuwa hashindwi na kitu kilicho nje ya kudra za Mungu. Nilishika mikono kifuani huku machozi yakinitoka kwa furaha, mkurugenzi alizunguka meza yake na kuja kuninyanyua na kunipigapiga mgongoni kunipongeza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hongera kwa kuipata nafasi adhimu kama hii, nakuamini katika kazi yako na nidhamu yako nina imani utafanikiwa na Mungu akutangulie kwa kila jambo.”



    “Amen, asante bosi.”



    “Basi nikuache ukaendelee na kazi, kesho utamkabidhi msaidizi wako aendelee na kazi zako zote, ili kuanzia kesho kutwa uwe na mapumziko na kujiandaa na safari.”



    “Asante sana bosi,” nilijibu huku nikifuta machozi ya furaha.



    “Basi kamalizie kazi.”



    “Sawa bosi,” nilitoka ofisini kwa bosi nikiwa nimechangangikiwa kwa furaha.



    Nilijikuta nikimpita Safia bila kujua mpaka aliponishtua.



    “He! Shoga kulikoni kunipita kama gogo kuna nini tena?”



    Niligeuka kumtazama Safia aliyekutana na machozi kitu kilichozidi kumshtua na kutoka kwenye kiti chake na kuja haraka kunikumbatia akiamini nina matatizo.



    “Jamani shoga yangu kuna nini tena?” Safia aliniuliza kwa sauti ya huruma.



    “Hamna kitu.”



    “Hapana niambie mpenzi.”



    “Kweli, haya ni machozi ya furaha.”



    “He! Furaha ya nini mpenzi?” aliniuliza huku akinishika mabegani na kunitazama usoni. Nilikutana na michirizi ya machozi mashavuni kwake kuonesha jinsi gani matatizo yangu yanavyo ugusa moyo wake.



    “Ile nafasi nimeipata.”



    “Nafasi! Nafasi ipi?”



    “Na kwenda kusoma.”



    “Wewee! Kweli?”



    “Kweli kabisa, nashukuru shoga Mungu amesikia maombi yetu.”



    Tukijikuta tukikumbatiana tena kwa furaha, Safia aliacha ofisi yake na kunisindikiza mpaka ofisini kwangu. Niliamini naye alikuwa na furaha kama yangu, nilimuomba akaendelee na kazi ili jioni tupate muda wa kuzungumza kwa kirefu.





    Siku ile nilifanya kazi kwa furaha huku nikiufikiria uwezo wa babu Sionjwi, kwangu ulikuwa muujiza ambao kwa akili yangu ya kawaida ilikuwa vigumu kuamini. Nilijiuliza babu Sionjwi nimpatie zawadi gani itakayolingana na kazi nzito aliyonifanyia.

    Kwa vile nilijua nikiondoka sitarudi tena pale nilimalizia kazi zangu zote na kuandaa mambo ya kumkabidhi msaidizi wangu ambaye niliamini ndiye atakayeshika nafasi yangu. Kutokana na ubize na furaha ya safari hata muda ulivyokwenda sikujua.

    Safia aliponipitia twende tukale nilimweleza siwezi kutoka kwa vile nilitaka kumaliza kazi zote. Nilimuomba aninunulie soda na keki, huwezi amini kwa furaha ya safari hata njaa sikuisikia kabisa.

    “Shoga soda na keki tu kwa nini nisikuletee chipsi kuku.”

    “Shoga hata hiyo soda keki nakunywa tu basi kwa vile mchana usipite.”

    “Mmh! Au umeshiba safari?”

    “Shoga wee acha tu kwangu naona muujiza.”

    “Shoga ilikuwa riziki yako na siku zote riziki ya mtu haipotei.”

    “Basi shoga baada ya kupata ujumbe ule furaha niliyoipata hata njaa nasikia?”

    “Basi nitakuletea keki na soda.”

    “Hapo umecheza hata hivyo naweza kuvibakiza.”

    “Mmh! Sasa hiyo sifa hata soda na keki ubakize?”

    “Safia we wahi acha nikimbizane na kazi leo siondoki mpaka nimalize kila kitu ili kesho nikifika nakabidhi kazi kwa muda mfupi na kwenda kupumzika kujiandaa na safari.”

    “Sasa shoga siyo uende ukirudi unisahau.”

    “Safia wewe ni zaidi ya kila kitu, hata kabla ya kuondoka kuna zawadi nitakupatia.”

    “Usiniambie!”

    “Tena itakufurahisha sana, basi wahi,” nilimuharakisha aondoke maana Safia porojo zilikuwa haziishi.

    Safia aliondoka na kunipa nafasi ya kuchakarika kumalizia viporo vyote pia kuandaa mipango mipya ambayo nilikubaliana na mkurugenzi niifanye siku inayofuata. Mtoto wa kike nilichakarika kama sina akili nzuri huku nikihakikisha mahesabu yote yanakaa vizuri ili nikiondoka pasiwepo na maswali.

    Kutokana na wingi wa kazi muda wa kutoka ulipofika ilibidi nimwambie Safia atangulie, aliondoka na kuniacha. Siku ile nilitoka kazini majira ya saa nne usiku nikiwa nimechoka sana. Lakini kutokana na furaha ya safari uchovu haukuwa mkubwa sana.

    Kama kazi ile ningepewa na kampuni lazima siku ya pili ningelala nyumbani au kuingia kazini mchana. Baada ya kumaliza mambo yote muhimu niliondoka huku mlinzi akifunga mlango na mimi kurudi nyumbani. Nilipofika nyumbani nilioga na kupata chakula na kupanda kitandani. Kwa vile siku ya pili sikutakiwa kuwahi sana kutokana na sikuwa na kazi kubwa zaidi ya kukabidhi majukumu. Lakini kwa upande wangu nilitaka kumaliza mambo yangu mapema ilinilazimu kuwahi asubuhi.

    Kwa vile nilimjulisha msaidizi wangu awahi ili tukabidhiane na kuelekezana mambo muhimu. Nashukuru nilimkuta kama tulivyokubaliana, kwa vile kazi kubwa nilimaliza jana yake hakukuwa na kazi kubwa kumwelewesha ilichukua saa tatu kumaliza kila kitu.

    Baada ya kukamilisha kila kitu, nilipeleka paspoti kwa mkurugenzi kwa ajili ya viza, nilirudi kwa Safia ili kumpatia zawadi ya mkufu ambao niliununua kwa gharama bila kuuvaa. Kwa thamani ya ule mkufu nilijua angeupenda sana. Nilipofika mbele ya meza yake alisimama kabla hajasema neno nilimuomba afumbe macho naye alifanya hivyo.

    Kwa vile nilikuwa nimeshaufungua mkufu nilimvisha na kumfunga kisha nilimweleza afumbue macho. Safia hakuamini alipouona mkufu wa thamani shingoni mwake. Alinikumbatia kwa furaha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Waaaooo! Asante mpenzi wangu, Mungu akuzidishie uende salama, urudi salama pia akutangulie kwa kila jambo lako,” Safia alisema akiwa amenikumbatia kwa nguvu.

    “Amen ndugu yangu, kizawadi changu ni hicho kidogo Mungu akijalia nikirudi salama nitakuletea kikubwa.”



    “Kingine majaliwa lakini leo umenifanyia bonge la sapraizi, nashukuru sana shoga yangu Mungu akulipe mara mia.”



    “Amen, basi shoga kuna mambo nataka niwahi nyumbani ili nijiandae kwa safari, muda wa kuwa nje na nyumbani ni mrefu kidogo.”

    “Sawa dada, lakini usiache kuniaga kabla ya kuondoka.”

    “Wewe tena? Lazima nikuage.”



    Niliagana na Safia huku akili yangu yote ikiwa kwa babu Sionjwi kwenda kumchukua na kumpa zawadi yake. Nilipitia mjini kununua vitu kwa ajili ya familia yake. Kwa vile sikuwa na kitu chochote cha kunirudisha nyumbani kwa wakati ule nilikwenda kijijini kumchukua babu ili aje anipe raha kwa siku mbili nikiondoka niondoke nikiwa mwepesiii.



    Kwa vile ilikuwa mapema, sikutembea mwendo wa kasi, nilikwenda kawaida na kutumia saa nne na nusu badala ya saa tatu nilizokuwa nikitumia njiani. Moyoni kila dakika moyo wangu ulichanua kwa furaha, nilijiuliza nitamtazamaje babu Sionjwi kwa muujiza alionifanyia.



    Nikiwa nakaribia kwa babu na nyumba yake kuiona kwa mbali nilijiuliza nitamchukuaje babu ili aje mjini kulala nami kwa siku mbili. Kama nilivyokuwa nimepanga kulala naye nyumba ya wageni, nilikuwa nimeshachagua ambayo ipo nje kidogo ya mji.



    Wazo la wasiwasi wa kushindwa kutoka sikulipa nafasi kwa kuamini babu tiba zake zote hakuzifanyia nyumbani, kuna muda alikuwa anatoka hata mwezi na kuwa nje ya nyumbani kwake hilo lilinipa faraja.



    Gari lilisogea hadi kwenye uzio wa nyumba ya babu Sionjwi, nje kulikuwa na wakeze na watoto wakati ule babu alikuwa na watoto sita na kijacho wa shoga yangu Rose angekuwa wa saba. Walipoliona gari langu niliwaona sura zao zikitawaliwa na tabasamu kwa kujua mkombozi wao nimefika.



    Nilisogeza gari sehemu ninayoliegesha kila nilipokwenda pale huku wenyeji wangu wakisogea kunipokea. Nilimuona shoga yangu Rose akijilazimisha kunyanyuka huku tumbo likitangulia mbele. Pamoja na kulakiwa na wake wa babu lakini shauku yangu kubwa ilikuwa kumuona babu, kiumbe mwenye maajabu chini ya jua anayeweza kugeuza nyeusi kuwa nyeupe.



    Baada ya kuegesha gari na kulizima, nilifungua mlango ili nitoke, kwa mbali nilimuona babu Sionjwi akirejea na kapu la dawa. Bila kujitambua kuna watu wamekuja kunipokea nilifungua mlango na kutimua mbio kwenda kumlaki babu kwa kumkumbatia kwa vile nilikwenda mbio na nguvu tulijikuta wote tukienda chini.



    “Waaaooo babuuu!”

    “Mjukuu utaniua bure mwenyewe nimejiishia.”

    “Babu unatisha.”



    “Kwa nini mjukuu?” aliniuliza huku akinyanyuka nilipomuangushia nami nilinyanyuka na kuliokota kapu la dawa lililokuwa limeanguka pembeni.

    “Nimeipata… nimeipata nafasi babu, mwisho wa wiki ninaondoka.”



    “Hongera, mi mbona nilijua kila kitu mapema, sema wasiwasi wako tu.”

    “Dah! Sasa itakuwaje?” ilibidi nimuulize kabla hatujafika kwa wakeze.

    “Kuhusu nini?”



    “Safari ya mjini maana nina muda wa siku mbili tu kabla ya kuondoka.”

    “Wewe tu.”

    “Kwa hiyo babu tunaondoka?”

    “Kila nilichokuahidi ndicho kitakachokuwa.”



    “Waaaooo.”



    “Si tunaondoka jioni ya leo?”

    “Ndiyo babu.”

    Tulirudi hadi nyumbani nikiwa nimebeba kikapu cha dawa na kumfanya Rose atanie:

    “Umependeza sana kama mke na mume, babu mjukuu anafaa kuwa mke wa tano.”

    “Ati eeh,” Babu aliitikia kwa utani.



    “Sasa, yaani kwa jinsi alivyo akija hapa wewe ndiye utakuwa mke mkubwa.”

    “Rose, wake wanne wanamtosha babu,” nilisema huku nikimuacha akipokewa na watoto wake.



    Kwa vile nilikuwa mwenyeji nilikipeleka kikapu cha dawa sehemu anayoweka dawa. Baada ya kuweka dawa sehemu yake nilikwenda kwenye gari kushusha mizigo. Kwa vile nilijua hatutaonana kwa muda mrefu nilikuwa nimewanunulia vitu vingi.



    Baada ya zoezi lile nilipata muda wa kuzungumza na babu kwa kituo kumpa taarifa ya kufanikiwa mpango alioutengeneza ambao kila hatua uliyabadili maisha yangu. Kabla ya mazungumzo nilimpatia bahasha iliyokuwa na kiasi cha pesa shilingi milioni moja.

    “Babu zawadi yako.”



    “Nini tena mjukuu? Leo naona mzigo kwenye bahasha.”

    “Pesa babu.”

    “Kiasi gani?”

    “Milioni moja.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Acha utani?” Babu hakuamini.

    “Kazi uliyofanya ni kubwa sana hata hicho kiasi kwangu nakiona kidogo niombee kwa Mungu niende salama nirudi salama ili ule matunda ya kazi yako.”

    “Usiwe na wasi kila kitu naamini kitakwenda kama kilivyopangwa, acha cheo utakachokipata, nakuhakikishia hata ukiutaka ukurugenzi utaupata.”



    “Usiniambie?” nilishtuka kusikia maneno yale japokuwa hayakuwa mageni mdomoni mwa babu, lakini muujiza alionifanyia kubadili matokeo nilimuamini kwa asilimia mia moja.



    Jamani tamaa mbaya nilijikuta nikiutamani na ukurugenzi, lakini niliamini ule haukuwa muda muafaka. Kwa vile nilikuwa nakwenda kusoma na kuongeza elimu na cheo sikuona sababu ya kuutaka ukurugenzi kwa muda ule.

    “Mjukuu kila kitu kwangu kinawezekana.”

    ‘Basi babu nikirudi tu tunaanza zoezi hilo.”



    “Wewe tu mjukuu wangu, nyota yako inang’aa hainisumbui kukutengenezea mambo yako.”

    “Sawa, babu basi jiandae tuondoke zetu.”



    “Mjukuu kuna dawa nitakutengenezea pia kuna kihirizi cha kukuongezea mvuto na bahati pia nitakupa dawa ya kuoga na kujifukiza.”



    “Ha! Babu nitawezaje kujifukiza wakati huko hakuna moto wa mkaa?”

    “Chumba utakachokuwamo nitaipaka dawa ambayo itachanganywa na mafuta mazito kwenye mshumaa na kuuwasha usiuzime mpaka uishe.”

    “Hapo sawa.”



    “Basi ngoja nikuandalie sawa, nataka ukirudi usichukue hata miezi sita uwe mkurugenzi.”

    “Babuu, sijui nitakupa zawadi gani?”

    “Labda unizalie mtoto.”



    “Babu watoto unao wengi.”

    “Mbona ninao wachache baba yangu alikuwa na watoto ishirini na tano nataka mmoja toka kwako.”



    “Basi yote hayo tutapanga nikirudi.”

    “Hakuna tatizo mjukuu.”

    Babu alinyanyuka na kuelekea kuandaa dawa zangu, nilibakia nikimtazama bila kummaliza kwani kwa umri wake hakutakiwa kuongeza watoto. Nilijua nikirudi hatakumbuka suala la kuzaa na mimi tena japo raha zake sikutaka kuzipa kisogo.



    Nilijumuika na wakeze kwa mazungumzo huku nikiwaaga safari yangu ya kwenda nje ya nchi kimasomo. Kila mmoja aliniombea kwa Mungu niende salama na nirudi salama. Niliwashukuru kwa dua zao na kuwaahidi kuwafanyia mambo mazuri pindi nikirudi.



    Pia nilitumia muda ule kuzungumza mengi na shoga yangu Rose huku nikimsihi asibebe mimba ovyo kwa vile maisha ya kule kijijini si mazuri. Aliniahidi kuwa makini kuhakikisha kuchukua muda mrefu kupata mtoto wa pili.



    Kutokana na ukaribu wetu nilimpatia vitu vingi kwa ajili ya mtoto wake atakayezaliwa na baadhi ya pesa za matumizi yake binafsi. Shoga naye aliniombea kwa Mungu safari yangu iwe ya heri na baraka, tulizungumza mengi kwa muda ule nikimsubiri babu Sionjwi.



    Tukiwa katikati ya mazungumzo babu aliwaita wake zake wote, nilibaki na watoto waliokuwa wakicheza. Baada ya muda walirudi, nilimdodosa shoga yangu Rose waliitiwa nini na babu!



    “Vipi mbona mmeitwa wote?”

    “Mmh! Tuliitwa kuagwa kuwa mnaondoka wote kwenda mjini kuna kazi anatakiwa kukufanyia siku mbili kabla ya wewe kuondoka.”

    “Ni kweli, kwa vile kazi yangu ilikuwa ina vikwazo vingi ameona kabla ya kuondoka basi afanye mambo yake.”



    “Hakuna tatizo, ungekuwa hujaniletea mambo yangu ningekuagiza kwa vile kila kitu umeniletea ukiondoka usafiri salama.”

    “Asante shoga, nina imani kwa uwezo wa Mungu kila kitu kitakwenda alivyopanga niende salama nirudi salama ili tuonane.”

    “Mjukuu nipo tayari,” ilikuwa kauli ya babu.



    Nilipogeuka kumwangalia huku pua yangu ikilakiwa na manukato ya bei mbaya, sikuamini kumuona babu akiwa katika suti ya bei mbaya. Nilibakia mdomo wazi. Babu alikuwa amebadilika hakuwa yule mzee wa kijijini mwenye mavazi yasiyo na hadhi.

    Babu alikuwa amebadilika kwa kiasi kikubwa, alivaa suti nyeupe juu alivaa kofia ya pama rangi ya ugoro na miwani ndogo. Chini alivaa viatu vya ngozi vya rangi ya ugoro iliyofanana na kofia. Mkononi alikuwa na bakora yenye nakshi ya dhahabu.



    Kwa jinsi babu alivyobadilika ukikutana naye utajua ni profesa na wala si mganga wa jadi. Nilibakia nimepigwa na bumbuwazi na kujiuliza vitu vya gharama babu kavitoa wapi na alivinunua kwa ajili gani ikiwa kila siku yeye na shamba, shamba na yeye.



    “Mjukuu nipo tayari,” babu alinishtua baada ya kuniona nimepigwa bumbuwazi.

    “Babu ni wewe?” nilimuuliza mkono mdomoni.



    ”Heh! Shoga usijirahisi kwa mume wetu bure, kafanyeni kazi iliyowapeleka la sivyo patakuwa hapatoshi,” Rose yalimtoka makavu bila kujua safari ile haikuwa na kingine zaidi ya kwenda kuchuma ndizi kwenye mkungu wao.



    “Jamani siwezi kufanya lolote baya, ila leo lazima niseme babu kanifanyia sapraizi, kumbe handsome babu.”



    Nilinyanyuka na kuongozana na babu hadi kwenye gari, kwa vile wakeze na watoto wake walikuwa wamesogea karibu na gari tuliwaaga na kuondoka. Ndani ya gari ulinukia uturi wa babu uliokuwa ukipendeza ndani ya pua zangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa jinsi alivyokuwa sikuwa na wasiwasi kuingia naye hoteli yoyote tena tukiwa tumeshikana mikono.Tukiwa safarini nilimtupia jicho la wizi babu aliyekuwa ametulia macho yake yakiwa mbele.

    “Babu,” nilimwita.



    “Mjukuu,” aliitikia huku akinitazama.

    “Babu vitu vizuri hivi umevitoa wapi?” nilimtupia swali la kizushi.

    “Mjukuu wangu unaniangalia vibaya, nina suti kama hizi ishirini, pea za viatu kumi na nguo za kawaida sanduku tatu.”



    “Ha! Sasa hizo nguo zote unazivaa wapi?”

    “Historia yangu ni ndefu haitoshi kwa muda huu ipo siku nitakueleza naamini utaandika kitabu jinsi nilivyoingia kwenye uganga, nilikuwa bonge la bishoo.”

    “Ha! Sasa uliingiaje kwenye uganga?”



    “Ndiyo maana nimekueleza nina historia ndefu na ya ajabu, kwa kifupi kazi yangu si ya kijijini tu, mjini huwa nakuja mara nyingi hivyo siwezi kwenda katika mavazi ya kiganga kila mtu ajue mimi ni nani. Pia nimesha safiri nchi zaidi ya kumi kwa hii kazi yangu.



    “Hivi unaweza kusafiri na tunguri mkononi? Lazima ulingane nao kwa kuvaa suti kali inayolingana na wapanda ndege. Pia dawa zangu naweka kwenye Brif case mkononi. Kama hivi nilivyotoka nani atajua mimi mganga? Kama siyo profesa,” kauli ya babu ilinifanya niangue kicheko.



    “Mmh! Huko unatumia lugha gani?”

    “Kwani wewe unatumia lugha gani unapotoka nje ya nchi?”

    “Kiingereza na Kifaransa kidogo.”



    “Basi mimi zote hizo nazizungumza kwa ufasaha zaidi.”

    “Babu umesoma hadi kidato cha ngapi?”

    “Chuo kikuu.”

    “Uongo!”



    “Ndiyo maana nikakuambia historia yangu ni ndefu bila kurithishwa uganga na babu yangu na shinikizo la majini nami ningekuwa nakula bata kama ninyi.”

    “Kwani ilikuwaje?”



    “Mjukuu ni historia ndefu ina siku yake.”

    “Unajua kuendesha gari?”

    “Acha kuendesha, nilikuwa namiliki magari.”

    “Nikikuachia utaendesha?”

    “Bila shaka.”



    Nilisimamisha gari ili nipate uhakika na kauli ya babu kuwa anajua vitu vingi pia aliwahi kumiliki magari. Tulipishana babu alikaa kulia na mimi kushoto, mwanaume alikanyaga mafuta kama hana akili nzuri. Babu alikuwa mahiri wa kuendesha gari kama kazaliwa nalo.

    Tuliwahi kuingia mjini tofauti na mwendo wangu, nikamuuliza alipenda tufikie hoteli gani.



    Niliingia ndani na kujitupa kitandani, pamoja ilikuwa burudani lakini iliniacha hoi. Niliamka saa sita za usiku nikiwa na njaa kali. Nilipata chakula kisha nilioga na kurudi kitandani, kutokana na uchovu nilipogusa kitandani usingizi mzito ulinichukua.

    Huwezi kuamini usiku mzima njozi zote zilikuwa kwa babu Sionjwi mpaka kunakucha.



    Niliposhtuka kitandani na kujikuta peke yangu nilijikuta nikiingia unyonge na kujilaumu kumrudisha mapema heri ningeachana naye jioni ya siku ile.

    Nilitakiwa nitumie siku ile kujiandaa kwa kukaa na familia kwa ajili ya kupanga na kuagana. Siku zote safari kama ile ilitakiwa upate baraka za wazazi.



    Lakini nilijikuta nikimuwaza sana babu na kutamani niwe naye karibu, niliona kuna haja ya kumfuata kisha awe mjini na kufanya akili yangu itulie na kuweza kupata utulivu wa moyo ambao niliuona kama ukipepea kutaka niwe karibu ya babu muda wote.



    Kwa vile jioni ya siku ile nilikuwa na miadi ya kukutana na familia kwa ajili ya sherehe fupi ya kuniaga. Niliona asubuhi ile kuna haja ya kukimbilia kijijini kumfuata mzee Sionjwi ili niwahi kurudi kujiandaa na sherehe iliyokuwa ya kifamilia, sikutaka kubwa zaidi ya familia yangu tu.



    Kumbukumbu zangu zilinionesha baada ya kupata kifungua kinywa, niliwaaga wadogo zangu huku nikiwaelekeza wanipangie nguo na vitu nitakavyoondoka navyo kwenye sanduku na begi. Kwa vile kulikuwa na dawa zilizotakiwa kuondoka nazo, niliziweka mwenyewe kwenye begi dogo ambalo ningeingia nalo kwenye ndege.



    Baada ya kuacha kila kitu kipo sawa huku moyo ukinisukasuka kama mtu aliye na kiu kikali aliyeelezwa sehemu yalipo maji. Kila dakika iliyokuwa ikija mbele yangu niliona nachelewa kumuona babu kiumbe aliyeuteka moyo wangu kwa mapenzi mazito ambayo sikuwahi kuyapata katika maisha yangu.



    Mwanzo nilimuona kama kiumbe wa ajabu asiye na hadhi kwangu lakini safari yetu ya mjini na jinsi alivyobadilika na kuonekana mzee wa kisasa na penzi alilonipa lilinichanganya akili mtoto wa kike.



    Baada ya kila kitu kwenda kama nilivyopanga niliondoka kumfuata babu ambaye nilipanga kulala naye nyumbani kwangu na kushinda naye mpaka jioni ya kesho yake ambayo ningemkodia gari mpaka kijijini huku mimi nikielekea uwanja wa ndege kwa safari.



    Niliwasha gari kuelekea kijijini kumfuata babu tustarehe kwa mara ya mwisho kabla ya kuondoka jioni ya siku ya pili. Njia nzima mawazo yangu yote yalikuwa kwa babu nilimuona kama kijana wa miaka kumi na nane kwa jinsi alivyouteka moyo wangu kwa kasi ya ajabu na kujuta kuchelewa kumfahamu.



    Nilijilaumu kuchelewa kumjua babu mapema kwani mpaka naondoka moyoni mwangu ningemuona wa kawaida japokuwa ningekuwa nampenda lakini si kwa kiasi kile cha kuhisi kuchanganyikiwa vile kila nilipomuwaza.



    Katika kumbukumbu zangu za mwisho, nakumbuka nilifika mpaka kwa babu na kupokelewa, lakini kilichoendelea kuanzia hapo sikuelewa chochote mpaka siku tulipofumwa na mama Sabuni.



    Mama Sabuni ndiye aliyenielekeza kwa mzee Sionjwi kwa msaada wa shoga yangu Rose baada ya kusumbuliwa na mhasibu wangu Mbwana, aliyekuwa akishikilia ofisi kishirikina wakati elimu yake ilikuwa ndogo tofauti na cheo alichokuwanacho baada ya waganga wengi kugonga mwamba kumng’oa.



    Alikuwa amemleta mtu aliyekuwa na matatizo ya muda mrefu hivyo alimkumbuka babu Sionjwi na kwenda kubahatisha kama yupo kwa vile ulikuwa muda mrefu tangu aende kupata huduma mara ya mwisho.



    Alipofika alimfahamu shoga yangu Rose ambaye aliwahi kufanya naye kazi kabla mimi sijafika. Kwanza alimfananisha alipomwita jina lake kama ni yeye kweli.

    “Rose.”



    “Abee,” Rose aliitikia bila kumfahamu aliyemwita.

    “Unafanya nini huku?”

    “Kwani we nani?”

    “Mimi mama Sabuni.”

    “Mama Sabuni yupi?’



    “Rose si tulikuwa tunafanya ofisi moja siku za nyuma na wewe ndiye uliyemleta shoga yako kuomba msaada nikawaelekeza huku.”

    “Ooh! Za siku?” Rose alimkumbuka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nzuri, Rose unafanya nini huku?” “Kwani unaniona nafanya nini?” Rose alimjibu kwa mkato huku akimtengeneza mtoto aliyekuwa mgongoni.



    “Na…na…na huyu si…si…si shoga yako nani kweli?”



    “Eflazia,” nilimjibu nikiwa nambembeleza mwanangu aliyekuwa anataka kulala.



    “Jamani hii si kawaida kuna kitu, watoto wazuri kama ninyi kuja kwa kibabu hiki si bure lazima kuna kitu,” mama Sabuni alilalamika kwa sauti ya huzuni nilimsikia lakini sikumuelewa.



    “Bibi eeh fuata kilichokuleta ya huku mengine  hayakuhusu,” Rose alikuwa mkali baada ya kuona kama tunaingiliwa maisha yetu.



    Kwa vile mama Sabuni alimleta mtu, alionana na mzee Sionjwi kisha alirudi mjini akiwa na kitu moyoni mwake. Hakukubali kuliacha lipite, alikwenda hadi ofisini kuulizia tunapoishi. Kwanza walishangaa kusikia mimi nipo japo kuna watu waliamini nilikwenda kusoma lakini sikurudi kazini na Rose aliacha kazi kwa hiyari yake.



    Alipoelekezwa alikwenda kwenye familia zetu na kuwaeleza habari zetu walizoziona mpya masikio mwao baada ya kutoweka kwetu ghafla. Baada ya kutoweka akili zao zilipumbazwa na dawa za babu hakuna hata mmoja aliyetukumbuka.



    Baada ya sisi kutoweka wengi hawakutuwaza na kuona jambo la kawaida na kulipuuzia na kuendelea na mambo yao mengine. Baada ya kupewa taarifa mama Sabuni aliongozana na familia zetu pamoja na polisi mpaka kijijini ambako tulichukuliwa mpaka kituo cha polisi.



    Ilikuwa kama wana kijiji kwa jinsi tulivyokuwa watoto wetu walikuwa jumla ishirini na tano, wake tuliowakuta wote walikuwa na watoto kumi na nne na mimi na Rose tulikuwa na watoto kumi na moja. Wote jumla tulikuwa thelathini pamoja na mume wetu.



    Babu mzee Sionjwi ambaye alikuwa mume wetu wakati huo alikuwa amechoka kwa umri alifunguliwa mashtaka ya kututorosha. Lakini sisi wote wake zake watano tulipinga kuwa hatukutoroshwa bali tulikwenda kwa hiyari yetu kwa vile tulikuwa tumevuka umri wa miaka kumi na nane tulikuwa na maamuzi yetu.



    Maelezo yetu yalifanya babu kuachiwa kwa vile hakukuwa na ushahidi wa kututorosha watu wazima kama sisi. Wakati huo ilikuwa imepita miaka tisa na nusu nikiwa na watoto sita ambapo uzao wa kwanza mapacha wawili, wa pili mtoto mmoja, wa tatu mapacha wawili wa nne mtoto ambaye alifariki akiwa na umri wa miezi minne na wa mwisho mtoto mmoja.



    Mapacha wa kwanza muda huo walikuwa na umri wa miaka minane aliyewafuata  alikuwa na miaka sita, mapacha wengine walikuwa na miaka mitano na wa mwisho mwaka mmoja na nusu ambaye walinikutana nambebembeleza.



    Familia zetu zilipotuchukua kwa nguvu lakini wote tulitoroka na kurudi kwa mume wetu. Ilibidi nao wahangaike kwa waganga baada ya kuonekana tulichezewa mchezo na babu wa kupumbazwa akili kutufanya tumuwaze yeye tu muda wote.



    Kitendo cha babu kukamatwa na misukosuko ya polisi kisha kuswekwa ndani kwa siku mbili, kilifanya apate mshtuko hata alipoachiwa huru hali yake haikuwa nzuri kwa presha kuwa juu sana.



    Kutokana na kupatwa shinikizo la damu ilibidi akimbizwe hospitali ambako alikaa siku mbili na kufariki dunia. Kifo cha babu kilituchanganya sana wake zake, tulichanganyikiwa tulijiuliza duniani bila babu tutaishije kwani tuliamini yeye ni kila kitu kwetu chini ya jua.



    Lakini kila jambo lilikuwa na makusudio yake baada ya mazishi, familia zetu zilipata urahisi kutuchukua japokuwa wake wenzatu mwanzo hawakujulikana wanatoka wapi kwa vile kila mke wa babu hakuwahi kutembelewa na ndugu yake.



    Baada ya kutolewa kijijini tulipelekwa kwa mtaalamu ambaye aliweza kutuzindua na kuzirejesha akili zetu za kawaida. Kila mmoja akukubaliana na hali aliyojikuta nayo. Tulikuwa watu tulioishi kama misukule tusiojielewa baada ya kutekwa akili na babu.



    Sikuamini kujikuta nikiwa nimechoka huku nikiwa na watoto sita mwenye afya dhaifu na shoga yangu Rose akiwa na watoto watano kwa kuzaa mara tano. Kiafya nilionekana kama mwanamke wa miaka sitini wakati nilikuwa nina miaka 37 na Rose 39, hata wake wenzatu nao pia walikuwa wamechoka kwa maisha ya kijijini.



    Baada ya kuzinduliwa na akili yangu ya kawaida kukaa sawa, kila mmoja alikumbuka alipotoka na kwa msaada wa polisi tulifikishwa makwetu. Niliporudisha kumbukumbu zangu nilikumbuka muda ule nilitakiwa niwe wapi na pale nipo wapi. Kwa kweli nililia sana badala ya kwenda kusoma Ulaya nilikwenda kuolewa na mganga wa jadi huku elimu yangu ikipotea bure kwa tamaa ya cheo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Katika miaka tisa ambayo niliondoka nyumbani nilishukuru Mungu familia yangu niliikuta ipo katika hali nzuri japokuwa nilikuwa nimempoteza baba yangu kipenzi miaka mitatu iliyopita. Nyumba yangu aliyokuwa akiisimamia mama ilikuwa imeisha wakati huo ilikuwa  imepangishwa kwa kampuni moja ya nje.



    Kwa kweli kila nilivyofikiria dhamira yangu na sehemu niliyoangukia nilikuwa nikilia huku nikiwaangalia watoto wangu wadogo wasio na baba tena wenye afya dhaifu.



    Lakini namshukuru mama yangu kipenzi alisimama nami muda wote kunitia moyo na kunieleza nisahau yote kwani ni mapito. Baada ya misukosuko mingi niliamua kuokoka kujikabidhi mikononi mwa Bwana. Namshukuru Mungu niliweza kujengeka kiimani na kusahau yote yaliyopita.



    Kutokana na elimu niliyokuwa nayo niliweza kupata kazi katika mradi wa kanisa kama mhasibu mkuu. Japokuwa mshahara haukulingana na elimu yangu lakini namshukuru Mungu maisha yanaenda kama alivyotaka yeye, haikuwa sawa na kukaa bure pia hata umri ulikuwa umekwenda.



    Mpaka napata nafasi ya kusimulia mkasa huu ni miaka kumi imepita, wanangu mapacha wakubwa wana miaka kumi na nane, wa kiume yupo kidato cha tatu baada ya kuchelewa kuanza shule, wa kike ameacha shule akiwa kidato cha kwanza baada ya kupata ujauzito, hivi sasa mimi ni bibi nalea mjukuu.



    Anayefuata ambaye ni msichana pia ana miaka kumi na sita naye yupo kidato cha tatu kama kaka yake. Wengine wapo darasa la saba na tano, mmoja wa kiume alikataa kuendelea na shule baada ya kujiingiza kwenye mabangi.



    Kwa sasa nipo na mwanaume mwingine ambaye nimezaa naye mtoto mmoja kwa hiyo nina watoto saba. Baada ya kufanya kazi ya kuajiriwa kwa muda mfupi na kupata ujauzito nikiwa kazini, nilipopata likizo ya uzazi sikurudi tena kazini niliamua kuacha kazi na kuwa mjasiriamali baada ya kuhudhuria mafunzo kadhaa.



    Kwa sasa nafuga kuku wa mayai na nyama na ng’ombe wa maziwa. Maisha yangu namshukuru Mungu yanakwenda vizuri japo nilipata pigo zito la kumpoteza mama yangu kipenzi, iliniuma sana na kuwa vigumu kumtoa akilini, lakini Mungu alinisimamia kunipa ujasiri. Siku zote sitaacha kuwaombea wazazi wangu kwa vile hiyo ni njia yetu sote.

    Mkasa huu kila nikiufikiria niliishia kucheka tu, kama kulia nililia sana mpaka nikataka kumkufuru Mungu. Nakumbuka nilifikia wakati wa kutaka kujiua kwa kuiogopa aibu ya wanadamu, msomi kama mimi kuolewa na mganga wa jadi, heri angekuwa kijana lakini kizee kama kile.



    Lakini sina budi kumheshimu babu Sionjwi kama mzazi mwenzangu, sikutaka kumlaumu kwa vile niliamini mimi mwenyewe kushindwa kujiamini na kukimbilia nguvu za giza ndizo zilizosababisha safari ya Ulaya kuishia kuwa mke wa mganga.



    Kwa vile babu alikuwa na eneo kubwa, mifugo na mashamba vyote viliuzwa na pesa yake tuligawiwa wakeze na kusaidia watoto wake. Kiasi kile kilinisaidia kutanua miradi yangu ili kupunguza ukali wa malezi ya watoto wangu sita.



    Bado najiuliza kama mama Sabini asingekuja kijijini maisha yangu yote yangekuwaje? Mwisho napenda kuwaasa wote wanaoamini jitihada hushinda kudra za mwenyezi Mungu. Bidii pekee na baraka za Mungu ndizo zitakazokunyanyua na wala si kitu kingine, si mizizi wala tunguri. Siku zote tumtangulize Mungu mbele kwa kila kitu kwa vile ndiye ajuaye kesho yetu na siyo sisi wanadamu.



    Siku zote tamaa mbele mauti nyuma, tuache tamaa ya maisha kwa vile kila mwanadamu ana riziki yake na riziki ya mtu huwa haipotei bali hucheleweshwa. Tumtegemee Mungu kwa kila kitu ili atuongozee maisha yetu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Asante kwa kupoteza muda wako kunisoma, naomba uchukue mazuri yote na mabaya yawe funzo kwenu.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog