Search This Blog

NYUMBA YA MISUKULE - 4

 





    Simulizi : Nyumba Ya Misukule

    Sehemu Ya Nne (4)



    Walizidi kutetemeka kwa kuliona lile jeneza mbele yao tena likiwa na maiti ndani, hakuna aliyeweza kutamka kitu zaidi ya kutetemeka zaidi na zaidi, walitamani hata ingekuwa ni ndoto ili wakiamka mauzauza yale yawe yamepotea, ila ilikuwa ni kitu cha kweli kabisa kikiwatokea ndani ya nyumba yao wenyewe.

    Mara wakasikia kicheko toka kwenye ile maiti, Pendo aliona ni maajabu katika maisha yake ni machozi tu yalikuwa yakiwabubujika huku wakijaribu hata kuomba kimoyomoyo wakimsihi Mungu awahurumie. Hapo ndio utagundua kwamba mwanadamu anatambua uwepo wa Mungu kwenye matatizo.

    Walizidi kulia na kutetemeka, walionekana wakilia kama watoto wadogo na ile maiti kwenye jeneza ilizidi kucheka, halafu ikainua sura, Mungu wangu ni marehemu yuleyule aliyekufa kule kijijini, Pendo alijikuta mkojo ukimtoka pale kwenye kochi. Hakuna aliyepata ujasiri wa kuinuka tena, walitamani siku hiyo isingefika kwenye maisha yao.

    Mara lile jeneza likatoweka, wakazidi kutetemeka na kuogopa huku wakilia.

    Pale lilipotoka lile jeneza pakaonekana pameachwa ujumbe uliosomeka,

    "mbona hujawapa chakula tangu jana?"

    Pendo na mama yake wakabaki wanatazamana tu, kwa muda huo kila mmoja alikuwa ni tumaini kwa mwingine.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati wanaendelea kustaajabu na kulia, wakasikia mtu mwingine zaidi yao akilia wakazidi kutetemeka, wakatulia na kusikilizia vizuri ni kweli kabisa ile sauti ilitokea ndani ya nyumba yao.

    Mara huyo mtu aliyekuwa akilia akawasogelea kwa nyuma na wakamuhisi kabisa kwamba kuna mtu nyuma yao ila je ni nani mwenye ujasiri kati yao wa kugeuka na kumwangalia huyo mtu!! Hakukuwa na mwenye ujasiri huo hata kidogo,

    Mara yule mtu akamshika begani Pendo palepale alipokaa, Pendo alijikuta akitoa ukelele wa ajabu hadi akapoteza fahamu, bi.Marium naye alijikuta akizidi kumkumbatia Pendo kwani ndiye tumaini lake, naye aliogopa kugeuka alizidi kulia huku amemkumbatia mwanae aliyepoteza fahamu, alilia sana. Alijikuta akilia hadi nae akapoteza fahamu kabisa.

    Wakaja kushtuka kukiwa kumekucha kabisa, ilikuwa ni mida ya saa tano asubuhi ila kilichowashangaza ni kuwa walijikuta kitandani wamekumbatiana vilevile, wakakumbuka yaliyowapata usiku wake. Wote walibaki wanashangaa wakaanza kujiangalia na kujikuta wananuka mikojo waliyojikojolea kwa uoga, wote waliogopa kutoka mule chumbani.

    PENDO: Mama, ilikuwaje kwani?

    BI.MARIUM: Sijui kilichoendelea mwanangu, hata mimi nashangaa.

    PENDO: (Huku machozi yakimtoka), mama, kwanini sisi tufanyiwe hivi? Kwani tumekosa nini jamani?

    BI.MARIUM: (huku nae machozi yakimtoka), mwanangu sijui kitu kwakweli, sijui kwanini imekuwa hivi.

    PENDO: (Huku akizidi kulia), mama hivi tutapona kweli?

    BI.MARIUM: Mwanangu, Mungu ni mkubwa atatusaidia tu.

    PENDO: Mama, mie naogopa sana.

    BI.MARIUM: Hata mi mwenyewe naogopa mwanangu.

    Wakabaki wamejawa na uoga uliopitiliza, ikawa hata akipita mende mule chumbani wanashtuka.

    Wakiwa wanawaza, mara mlango wa mule chumbani ukafunguliwa hapo wakazidi kuogopa na kutetemeka huku wakiwaza ni mtu gani ataingia mule ndani ila baada ya muda ule mlango ukafungwa tena.

    PENDO: Mama, mbona kama huku chumbani kunatisha sana?

    BI.MARIUM: Mwanangu yani hapa naogopa hakuna mfano.

    PENDO: Twende sebleni basi.

    BI.MARIUM: Kheee!! Tutaendaje mwanangu?

    PENDO: Kwani humu chumbani tumekuja vipi?

    BI.MARIUM: Hata na mimi sijui ila nimejishangaa tu tupo huku chumbani.

    PENDO: Mmh mama naogopa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    BI.MARIUM: Hata mimi naogopa pia mwanangu.

    Mara ule mlango wa chumbani ukafunguliwa tena. Wakazidi kutetemeka, huku machozi na makamasi yakiwatoka, mara wakamuona panya akishuka toka darini ila yule panya alikuwa anaenda kwa kunyata uoga ukawashika zaidi baada ya kumuona panya anacheka maana ni tukio ambalo hawajawahi kukumbana nalo hata mara moja. Uoga uliwashika na kujikuta wamepoteza fahamu tena.

    Mara akaja mtu na kuwamwagia maji wakashtuka, kuangalia mbele wakaona panya watatu wakiwaangalia huku wanacheka, hapo wakapoteza fahamu tena.

    Ikiwa ni mida ya saa kumi na moja jioni, Yule mganga aliwasili na akafikia kwa mama Sarah moja kwa moja. Alikuwa na msaidizi wake.

    MAMA SARAH: Naomba mkamsaidie, maji yamemfika shingoni. Mambo magumu sana yamemfika.

    MGANGA: Nyumba yake inaonekana ni nzito sana.

    MAMA SARAH: Ndio mkamsaidie, maana tangu asubuhi nampigia simu hapokei sijui hata amekumbwa na nini mule ndani kwake.

    Ikabidi mama Sarah ampeleke yule mganga hadi nyumbani kwa bi.Marium.

    Walipofika pale ikaonekana geti limefungwa kwa ndani, mama Sarah akawaomba wale waganga waingie hata kwa kupanda ukuta. Ikabidi watafute ngazi, wapande na waingie ndani.

    Mama Sarah kwa uoga wake akagoma kuingia, yeye akarudi nyumbani kwake.

    Walipoingia pale ndani palikuwa ni kimya sana hawakuweza kusikia sauti ya mtu yeyote wala sauti ya kitu chochote.



    Wale waganga wakaanza kuizunguka ile nyumba kwa tahadhari ili waweze kuona uwepo wa watu, ila bado wakaona kimya kabisa.

    Ikawabidi waanze kuita kwani walishapewa majina ya watu waliomo mule ndani na mama Sarah.

    Safari hii bi.Marium na mwanae Pendo waliposhtuka wakasikia kuna mtu anawaita nje, bila kufikiri bi.Marium akabiga ukelele huku akihisi ni watu wamekuja kuwakomboa,

    "tupo huku chumbani jamani tusaidieni"

    yule mganga nae akawaambia watoke mule chumbani.

    Bi.Marium na mwanae huku wakisuasua na kuvutana wakaanza kutoka hadi wakafika sebleni ambako walikuta hali iko shwari kabisa kama hakuna chochote kilichotokea, ikawabidi waende kufungua ule mlango wa kuingilia ndani ili watu hao waingie, kwa muda huo wala hawakujali zile harufu za mikojo walizo nazo.

    Wakafungua mlango nao ukafunguka vizuri kabisa, wakawakuta wanaume wawili mlangoni, huku wakijawa na uoga na kushindwa jinsi ya kuongea nao, ikabidi wale watu wajitambulishe ili kuwatoa hofu Pendo na mama yake. Baada ya hapo ndipo wakawakaribisha ndani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wale watu wakajitambulisha tena kuwa mmoja ni mganga na mwingine ni msaidizi wa mganga.

    BI.MARIUM: Afadhari mmekuja jamani, hata siamini kama tumepona.

    MGANGA: Sawa mama usijari, ila je unatambua tatizo la nyumba yako?

    BI.MARIUM: Kiukweli sitambui baba naona miujiza tu ikinitokea.

    MGANGA: Mama, hii nyumba yako ina misukule.

    Pendo na bi.Mariumu walijikuta wakihamaki kwa pamoja, "misukule!!"

    MGANGA: Ndio ina misukule.

    PENDO: Misukule ndio nini?

    MGANGA: Misukule ni watu waliotolewa ufahamu kwahiyo akili zao si za kibinadamu, mara nyingi kwenye mazingira ya kawaida hujulikana wamepotea au wamekufa, kumbe wanatumiwa na wachawi.

    BI.MARIUM: Kivipi? Hata sielewi, na hiyo misukule imeingiaje wakati mi sio mchawi?

    MGANGA: Mama, nyumba yako kuwa na misukule haimaanishi kwamba wewe ni mchawi, ingawa mara nyingi nyumba za wachawi ndio huwa na misukule sababu wao huwafuga na kuwafanyisha kazi.

    BI.MARIUM: Sasa misukule hiyo kwangu imeingiaje?

    MGANGA: Hilo swali majibu yake utayapata tu ila cha muhimu kwa sasa tambua kwamba nyumba yako ina misukule.

    Wakajikuta wakitoa pumzi ndefu kwa kushangazwa na habari hizo za misukule.

    BI.MARIUM: Sasa tutafanyaje?

    MGANGA: Hakuna jinsi zaidi ya kuitoa tu.

    BI.MARIUM: Kumbe inawezekana kuitoa?

    MGANGA: Inawezekana ndio lakini si rahisi kama mnavyofikiria.

    Mganga akawaomba udhulu kidogo ili aende nje akaangalie baadhi ya mazingira ya pale na kuvaa mavazi ya kiganga.

    Wakiwa pale ndani Pendo na mama yake huku yule msaidizi akiwa kwa mbali kidogo, wakaanza kunong'onezana,

    PENDO: Hivi mama, wewe unaelewa habari za hiyo misukule?

    BI.MARIUM: Mmh hata sielewi mwanangu, mie nawasikiliza tu.

    PENDO: Mama, sijawahi kuona hiyo misukule hata mara moja. Bora aseme jingine ila swala la misukule sijamuamini kabisa.

    Mara yule mganga akawa amerudi mule ndani,

    MGANGA: Najua inakuwa vigumu sana kwa nyie kuamini ninachosema.

    BI.MARIUM: Hapana baba tunakuamini.

    MGANGA: Tatizo ni kuwa hamuoni kile nionacho mimi ila mkiona hata hii nyumba mtaiona chungu. Je mnataka kuona?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku zote wabishi huwa na tamaa ya kushuhudia ili wapate au wakose pa kubishia. Yule mganga akachukua dawa yenye asili ya unga unga na kuwapaka Pendo na mama yake.

    Baada ya hapo maongozi mengine yakaendelea, wakamweleza mganga waliyoyapata usiku uliopita na siku za nyuma.

    MGANGA: Yaani kwa yote hayo bado mnashindwa kuamini kama humu ndani ya nyumba yenu kuna misukule?

    BI.MARIUM: Kwanza leo hatutaki kabisa kulala kwenye nyumba hii. Bora hata tukalale barabarani.

    Basi mganga akawaambia watoke nje ili waizunguke nyumba hiyo nao waone, kutokana na jioni kuingia bi.Marium akaomba akachukue koti chumbani kwanza, kutokana na uoga walioupata ikabidi mwanae amsindikize na amngoje kwenye korido mama yake.

    Akaingia chumbani na kuchukua koti na kulivaa, wakati akitoka nje ya chumba lilishuka lijitu toka darini na kumkaba bi.Marium, Pendo kuona vile akapiga kelele na wale waganga wakasogea pale, mganga akatoa dawa na kumpulizia yule mtu mara akakosa nguvu wakamburuta hadi sebleni.

    Alikuwa ni mtu wa ajabu kwakweli, alikuwa na manywele mengi na marefu ambayo hayajawahi kuchanwa na pia alikuwa uchi kabisa na kucha ndefu, kwakweli Pendo na mama yake waliogopa sana.

    Mganga alipomuangalia yule msukule kwa makini akagundua kuwa anauwezo wa kusikia na kuongea ila alikuwa akiongea kama zezeta hivi.

    Yule msukule akasema kuwa yeye ndio mkubwa wa misukule mule ndani,

    MGANGA: Kwahiyo una wenzio?

    MSUKULE: Ndio tena wengi tu ila wao hawawezi kuongea.

    MGANGA: Nani kawaweka humu?

    MSUKULE: Alituambia kuwa huyu mama ni mchoyo na akatuweka humu tuwe tunakula vyakula vyote.

    MGANGA: Nani kawaweka humu?

    MSUKULE: Tuliambiwa huyo mama mchoyo ila tangu tumekuja tujajilia tu vyakula vizuri.

    MGANGA: Nani kawaweka?

    MSUKULE: Ila jana hajatupa chakula huyo mama.

    MGANGA: Mimi nataka muondoke humu.

    MSUKULE: Hatuwezi kuondoka humu tumepazoea.

    MGANGA: Mmepazoea kivipi?

    MSUKULE: Tupo wengi humu.

    MGANGA: Wewe ni nani?

    MSUKULE: Sijui

    MGANGA: Nani kawaweka?

    MSUKULE: Hatujala bado.

    Mganga akawageukia Pendo na mama yake na kuwaambia,

    "hapa inabidi ifanyike kazi ya ziada jamani"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pendo na mama yake walizidi kutetemeka kwani hawakuamini kama wamemuona msukule kweli kabisa kwa macho yao.

    MGANGA: Tuwafanyie nini ili mfurahi?

    MSUKULE: Tunataka damu.

    MGANGA: Damu ya aina gani?

    MSUKULE: Mtupatie damu mbichi debe tano.

    MGANGA: Mbona maswali mengine unayajibu kwa ufasaha na mengine unayakwepa?

    MSUKULE: Sijui.

    MGANGA: Basi tutawapatia hiyo damu ili muondoke.

    Yule msukule akayeyuka, bi.Marium na mwanaye Pendo hawakuwa na la kuzungumza zaidi ya kutetemeka tu.

    Mganga akawaambia kuwa watoke nje, na wote wakatoka pale nje ili kujadili namna ya kupata hiyo damu mbichi debe tano.

    Ilitakiwa pesa ili kukamilisha, bi.Marium alikuwa tayari kufanya chochote ili aweze kuondokana na hilo tatizo.

    Kwavile alikuwa na baadhi ya pesa ndani ikabidi aende na huyo mganga kuchukua pesa hiyo.

    Wakiwa pale nje, yule mganga akawaaga kuwa anaenda kuchukua hiyo damu, na akawaambia kutokana na yale mambo kuwa ya kichawi itabidi nae aenende kichawi, na hapo ndipo unapata sifa ya mganga kuwa naye ni zaidi ya mchawi sababu na yeye anafanya uchawi.

    Baada ya kuwaaga ikawa ni kufumba na kufumbua yule mganga nae katoweka, akawaacha pale bi.Marium, Pendo na yule msaidizi.

    Na huo ulikuwa ni msiku mji wote ukiwa umetulia, na watu wakiwa wamelala ila ikawa hakuna kulala kwa Pendo na mama yake.

    Kwenye mida ya saa tisa usiku yule mganga akawa amewasili ila kwa njia ya ajabu ile ile, akashusha pale debe tano za damu na zote zikiwa zimejaa damu kabisa.

    Wakaziingiza ndani, napo ikawa kitendo cha kufumba na kufumbua zile debe zilionekana tupu kabisa yaani damu yote wameimaliza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara likawatokea tena lile lijitu la mwanzo ila lilionekana likiwa na nguvu zaidi, kitendo hicho kiliwatetemesha wote.



    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog