Search This Blog

NYUMBA YA MISUKULE - 3

 





    Simulizi : Nyumba Ya Misukule

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Walipoangalia pale mezani chips hazipo zote zimeliwa, wakabaki wanatazamana.

    PENDO: Mama, mbona sielewi!!

    BI.MARIUM: Yaani mi ndo sielewi chochote mwanangu.

    PENDO: Mama, sasa chips zimeliwa na nani?

    BI.MARIUM: Sijui maana humu ndani tumebaki wawili tu mimi na wewe na wote tulikuwa jikoni.

    PENDO: Mama ila haya sio mauzauza yetu, hii kitu ni kweli kabisa.

    Wakiwa hawaamini vizuri kuwa chips zimeliwa, wakaenda kuangalia vizuri kwenye sahani na kujaribu hata kuinama chini kuangalia labda zimemwagika.

    PENDO: Mama inamaana humu ndani kuna panya wanaoweza kula namna hii?

    BI.MARIUM: Labda mwanangu, pengine panya hao ndio walioliza masufuria jikoni.

    Wakaanza kujipa moyo ili tu imani ya kishirikina isiwatawale.

    PENDO: Ila njaa inaniuma, itakuwaje sasa?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    BI.MARIUM: Mwanangu, mimi na wewe wote tupo kwenye kiulizo hapa. Cha msingi twende tukalale tu.

    Wakaamua kwenda kulala.

    Kesho yake wakawahi kuamka na kujiandaa halafu wote wakatoka na kufunga geti, hakuna aliyekuwa na imani ya kubaki ndani peke yake.

    BI.MARIUM: Ukirudi utanikuta kwa mama Sarah halafu tutarudi wote nyumbani.

    PENDO: Sawa mama.

    Kila mmoja akaenda kwenye mizunguko yake ila wote wakiwa na mawazo na nyumba yao hata bila kuelewa kinachoendelea.

    Baada ya mizunguko ya hapa na pale, bi.Marium akaenda nyumbani kwa mama Sarah kuongea nae mawili matatu huku akimngoja mwanae.

    MAMA SARAH: Ila vipi mauzauza nyumbani kwako bado yanaendelea?

    BI.MARIUM: Sio kuendelea tu, yani saivi ndio kuzidi.

    MAMA SARAH: Kwahiyo una mpango gani?

    BI.MARIUM: Hata sijui, mara nyingine natamani hata kuikimbia nyumba yangu.

    MAMA SARAH: Nilikwambia kama ukiona vipi tumwambie yule mganga wa Sumbawanga aje akusaidie.

    BI.MARIUM: Mmh! Mwanangu hataki kabisa hayo maswala ya ushirikina.

    MAMA SARAH: Sio ushirikina mama Amina, hata Mungu alisema jisaidie nami nikusaidie.

    BI.MARIUM: Mmh mama Sarah na wewe, unahusudu kweli mambo ya waganga.

    MAMA SARAH: Sio kwamba nayahusudu, yaani kwa vile vifo vilivyotoa nyumbani kwako ule ni ushirikina tosha umefanyika. Fungua macho mama Amina, usije poteza watoto wako wote.

    BI.MARIUM: Sasa na wewe mama Sarah unanitisha kwakweli.

    MAMA SARAH: Sio kukutisha ila nahitaji ufunguke upeo wako, uchawi upo, ulikuwepo na utaendelea kuwepo kwahiyo hayo mambo yapo ulimwenguni mama Amina.

    BI.MARIUM: Loh waniogopesha.

    MAMA SARAH: Huwa sisahau kamwe lile tukio lililotokea makaburini wakati wa kumzika mwanao, mama Amina jaribu kutazama nyuma ya pazia.

    BI.MARIUM: Nitajuaje sasa?

    MAMA SARAH: Huwezi kuyajua bila kumpata mtaalam, siku zote uchawi ukikupata ndio utaamini na kukubali kama upo. Yaani ipo hivi kama vile movie inavyofanyika kunakuwa na behind the scene, bila kuelewa unaweza kuhisi ile movie ni kweli hadi utakapoambiwa mambo ya nyuma ya pazia. Mama Amina, fungua macho yako uone matukio. Usikae bure, dunia hii ina watu na viatu shauri yako.

    BI.MARIUM: Haya nimekuelewa mama Sarah, nitafanyia kazi mawazo yako.

    MAMA SARAH: Sawa kama umenielewa, ila kuwa makini. Ningekuwa mimi nisingerudi kwangu hadi kutengemae.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    BI.MARIUM: Usijari mama Sarah, mambo yote yatakuwa sawa tu.

    Mara Pendo akampitia mama yake ili warudi wote nyumbani.

    Wakati wa kurudi wakaamua kupita kwenye kibanda cha chips ili wale kabisa ndio warudi.

    Wakaenda kwenye mgahawa, wakala kabisa na kuanza safari ya kurudi.

    Wakiwa njiani,

    BI.MARIUM: Yaani mama Sarah anapenda mambo ya kishirikina huyo.

    PENDO: Yule mama ana mambo ya kiswahili sana ndiomana anahusudu ushirikina.

    BI.MARIUM: Eti ananishauri nitafute mganga.

    PENDO: Mama, achana na yule mmama atatupotosha tu na usikute ni mchawi.

    BI.MARIUM: Vipi mwanangu kwani unadhani kuna uchawi duniani?

    PENDO: Hakuna mama ni imani za watu tu.

    BI.MARIUM: Kweli kabisa mwanangu.

    Wakafika nyumbani, na siku hiyo wakalala salama kabisa bila kusumbuliwa na chochote.

    Kesho yake kama kawaida wakatoka wote, na wakati wa kurudi wakafanya kama jana yake, wakapita mgahawani wakala na kurudi.

    Usiku wa siku hiyo sasa, wakiwa sebleni wanatazama luninga, mara ikazimwa wakabaki wanatazamana,

    BI.MARIUM: (Huku akimwangalia Pendo), vipi umezima Tv?

    PENDO: Hapana mama, remote hizo hapo mezani.

    BI.MARIUM: Sasa nani kazima?

    Kabla Pendo hajajibu, ile Tv ikawashwa tena.

    Wote wakashtuka, mara ikaanza kujiongeza sauti, wakawa wanaogopa wote wawili.

    Baada ya muda ile hali ikatulia, Pendo akaamua kuchukua remote na kuizima kabisa ile luninga yao akaenda kuizima hadi kwenye (switch).

    Mara wakasikia kama sufuria zinagongana jikoni, wakajikuta wote wawili wakiinuka na kwenda kutazama ila hawakukuta kitu, kurudi sebleni wakakuta Tv inawaka tena, wakaanza kuogopa huku wameshikana.

    Mara ikazimwa tena,

    PENDO: Mama sielewi kabisa.

    BI.MARIUM: Hata mimi sielewi mwanangu.

    PENDO: Kwakweli mama uoga umenishika sitaweza kulala humu ndani leo.

    BI.MARIUM: Kwahiyo unataka kwenda wapi?

    PENDO: Bora niende kwa dada Amina.

    BI.MARIUM: Na mimi je?

    PENDO: Twende wote mama, hii hali ni mbaya.

    Walipokuwa wakitafakari hayo mara wakasikia kuna mtu anafungua maji kwenye choo chao cha ndani, wakazidi kuogopa na kutetemeka. Mara kidogo wakasikia mvua ikianza kunyesha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakasikia mvua imeanza kunyesha nje, hofu zikazidi kuwatanda kuwa watatokaje. Yale maji waliyokuwa wamesikia yakifunguliwa chooni nayo yalizidi kutoka yaani ni kama kuna mtu aliyekuwepo humo.

    Bi.Marium akamshika mwanae mkono hadi kwenye makochi, wakakaa hapo

    BI.MARIUM: Mwanangu hakuna jinsi, hapa tufanye maombi tu.

    PENDO: Kweli kabisa mama tufanye maombi.

    Wakiwa wanaanza maombi yao, mara kilisikika kitu kikianguka kwenye paa, wote wakashtuka na kujikuta wakitetemeka na kuacha yale maombi.

    PENDO: (Huku akinyanyuka pale alipokaa), mama cha msingi tuondoke tu humu ndani hata kama mvua inanyesha.

    BI.MARIUM: Mwanangu ni usiku kumbuka, hata huko nje kutakuwa kunatisha pia.

    PENDO: Mama, unadhani tutafanyaje?

    BI.MARIUM: Sijui mwanangu, hivi na mbwa wangu yupo nje kweli na mvua hii?

    PENDO: Mama, mbwa toka jana hayupo hata sijamsikia kabisa.

    BI.MARIUM: Mmh atakuwa wapi jamani?

    PENDO: Sijui, ila mimi nataka kuondoka humu ndani mama.

    BI.MARIUM: Mwanangu tuvumilie tu hakuna jinsi.

    PENDO: Sawa mama, ila ngoja nikaangalie na nje nione nako vipi, kama vipi tukalale kwenye kijumba cha mlinzi mama.

    Pendo akainuka hadi jikoni, kufungua mlango ukagoma kufunguka. Alipoulazimisha ule mlango ukamgonga Pendo kwenye paji la uso, Pendo akapiga kelele, mama yake kufika pale akamuona Pendo akiugulia kwenye paji la uso, kwakweli bi.Marium hakuelewa ila naye akashindwa kushika kile kitasa afungue mlango.

    Bi.Marium akaamua aende dirishani ili achungulie nje, ile kuchungulia akaona pale nje pametapakaa damu, bi.Marium uoga zaidi ukamshika, akamwita na mwanae Pendo naye ashuhudie ile kuangalia tu hofu ikazidi kutanda, wakarudi na kukaa.

    Mara kidogo wakahisi kama kuna mtu anatembea mule ndani ya nyumba yao tena wakisikia milango ya vyumbani ikifungwa na kufunguliwa, wakazidi kutetemeka pale ndani.

    Ikabidi bi.Marium ampigie simu mama Sarah ili kuomba msaada,

    BI.MARIUM: Maji yametufika shingoni tupo kwenye wakati mgumu tunaomba msaada.

    MAMA SARAH: Ngoja basi nijaribu kumpigia simu yule mtaalam.

    BI.MARIUM: Fanya hivyo tafadhari, tuna wakati mgumu sasa.

    MAMA SARAH: Sawa usijari.

    BI.MARIUM: Hivi mvua inayonyesha ni kubwa sana eeh!!

    MAMA SARAH: Mvua? Mvua gani?

    BI.MARIUM: Kwani hakuna mvua huko?

    MAMA SARAH: Hakuna mvua kabisa na hata dalili hakuna.

    BI.MARIUM: Mmh basi kwangu mvua yanyesha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MAMA SARAH: Dah hayo majanga mama Amina, ngoja nimpigie simu sasa hivi nimpe na namba yako.

    Kile kitendo cha kuambiwa kuwa mvua inanyesha kwao tu, kiliwafanya wazidi kujawa na hofu na uoga.

    PENDO: Haya ni maajabu kwakweli.

    BI.MARIUM: Kweli ni maajabu mwanangu.

    Wakiwa bado wanatetemeka, bi.Marium akapigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa yeye ni mganga.

    BI.MARIUM: Tuna matatizo sana, tusaidie tafadhari.

    MGANGA: Sawa, ila jitahidini mvumilie tu na msitoke nje hadi nitakapofika mimi hapo kesho.

    BI.MARIUM: Maisha yetu yapo hatarini.

    MGANGA: Naelewa hilo ila vumilieni kwanza.

    Wakabaki wakitetemeka na hakuna aliyetamani kwenda kulala, walijihisi kama wapo ndotoni.

    Wakiwa hapo, mara taa za pale sebleni zikazimwa, walizidi kutetemeka wakaona usiku huo ni usiku mrefu kuliko yote.

    Ikawa wamekumbatiana tu muda wote, ila kila muda waliona mende wakipishana pishana pale sebleni hakuna aliyeelewa kwakweli, ufahamu uliwatoka na uoga ulizidi kuwatanda.

    PENDO: Mama, haya mambo ni ya ajabu jamani.

    BI.MARIUM: Mwanangu, yaani nimekumbuka hadi maneno ya mama Sarah, maana alisema angekuwa yeye asingerudi hadi nyumba itengemae.

    Mara kidogo wakasikia watu wakipiga makofi, wakazidi kutetemeka kwa hofu.

    PENDO: (Huku akizidi kumkumbatia mama yake), mama naogopa.

    BI.MARIUM: Hata mimi naogopa mwanangu, naona kama miujiza kwakweli.

    Kabla hawajaendelea kuongea wakaona kama mtu anawamwagia maji na baada ya muda wakawa wote wameloa chapachapa.

    Lile tukio liliwafanya watetemeke zaidi, Pendo alizidi kumkumbatia mama yake, wakahisi kama kuna watu wanatembea juu ya dari, hakuna aliyeweza kuangalia ni nani aliyewamwagia maji au ni nani aliyetembea, wote walijikuta wakitetemeka kwa uoga tu.

    Mara wakasikia mtu akicheka, wakashindwa kugeuka na kuangalia sauti ilipotokea, wakahisi yule mtu anayecheka akiwafata kwa nyuma tena akiwafata kwa kunyata, waliogopa sana, hakukuwa mwenye ujasiri hata mmoja wa kuongea chochote.

    Mara mbele yao wakawekewa jeneza lile lile aliloliona Pendo ile siku kabla ya msiba tena jeneza hilo likiwa na maiti ndani yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog