Simulizi : Nchi Ya Wachawi
Sehemu Ya Tano (5)
“Napenda kusema kuwa, mpaka sasa dunia kama ilivyo, pamoja na watu wake wametawaliwa na nguvu za shetani. Japo kuna watumishi wa Mungu wamekuwa wakijitahidi kuomba usiku na mchana lakini nguvu za giza nazo zinafanya kazi usiku na mchana kama watumishi, lakini lengo ni kuhakikisha wanadamu wanapotoka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sasa kilichopo kwenye tukio kama hili ni kwamba, watu wengi hufanyiwa mambo hayo ili kuchezewa bila kujijua.
Ilikuwa usiku mmoja nikiwa nimelala baada ya kurudi kutoka kwenye mikutano yetu ambapo siku hiyo ilikuwa siku ya kujitolea nyama. Kila mchawi alitakiwa kutoa mtu wake wa karibu, ikibidi iwe damu yake, kama vile watoto, mkewe au mumewe ili kuwa chakula cha wenzake.
Tulipanga siku ya chakula hichi cha nyama za watu iwe wiki inayofuata, nikiwa kitandani niliamshwa na sauti yenye hasira.
“Unatakiwa kuamka haraka sana , unahitajika kwa Mkuu wa Nchi ya Wachawi, huu ni mwito wa dharura,” hiyo sauti ilisema.
Nikiwa najiweka uso vizuri maana nilikuwa uzingizini, nikasikia ikisisitiza.
“Si wewe tu uliyeitwa, hata wenzako ambao ni wakuu wa kanda zao wameitwa, wengine wameshafika, wengine bado ukiwemo wewe.”
“Sasa nitakwendaje?” Nilihoji kwa sauti ya uchovu wa kukosa usingizi.
“Ukitoka nje simama katikati ya uwanja wa nyumba yako, usafiri upo. Zingatia hili, mavazi yanayotakiwa kule leo ni shuka jeusi na jekundu.”
Nilichukua shuka langu jeusi maarufu kama kaniki, nikaondoka mpaka nje.
Nilisimama katikati ya uwanja na kutazama kulia na kushoto ili kujihadhari na majirani zangu ambao mpaka muda huo wengi walikuwa wakinong’ona kuhusu mimi.
Sikuona mtu, ila nikasikia sauti ikisema:
“Fumba macho.”
Nikafumba, kufumba na kufumbua nikajikuta nimesimama katikati ya ardhi ambayo siyo niliyoizoea, ila kwa kumbukumbu nikajua nipo kwenye nchi ya wachawi.
Nikiwa nashangaa mazingira, watu wengine kama kumi wakatua mbele yangu, pembeni yangu na kulia kwangu.
“Njooni huku haraka sana ,” sauti iliita kutokea mbele yetu umbali wa kama hatua hamsini.
Tulitembea kuelekea huko huku nikijisikia uchovu sana .
Mara, badala ya sauti kiumbe cha ajabu kilijitokeza mbele yetu.
“Hakuna cha ajabu sasa, nifuateni mimi,” kilisema huku kikiwa kimeanza kutembea.
Ilivyo ni kwamba, tulikotoka, nikiwa na maana dunia ya kawaida, ilikuwa usiku mnene, lakini kule kulikuwa na mwanga kama mchana. Ila kasoro yake ni kuwa, hakuna jua la kuonesha kweli ni mchana, sasa mwanga ulitoka wapi nitakwambia baadaye.
Tuliingizwa kwenye jumba kubwa ambalo kumbukumbu yangu inasema nilishaingia na ndiyo lile ambalo tulifanyia mkutano mkuu wa Nchi ya Wachawi chini ya uongozi wa Mkuu wa nchi hiyo.
“Sasa nataka kusema kitu, naamini wote mmeshakaa,” alisema Mkuu wa Nchi ambaye nilimtambua bila shaka yoyote. Alisimama mbele kabisa kwenye mimbari kama ya kanisani.
Uso wake ulionesha kujaa hasira tupu, kila kitu kwake kilionekana kama ukali.
“Karibu wote mlikuja kwenye ile semina, si ndiyo?” Aliuliza. Wote tulijibu ndiyo.
“Sasa mlijifunza nini, mbona kila kitu kwa binadamu kinakwenda vizuri, mbona wanadamu hawapotoki, wa kuzaa wanazaa salama, ndoa zinadumu. Wanafunzi wanafaulu mitihani, yaani wanadamu wanaishi maisha mazuri tu na wanamtukuza Mungu wao, inakuwaje na nyinyi mpo?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akaendelea:
“Nilishatoa maagizo na maelekezo kuwa, kazi yenu kubwa ni kuhakikisha maisha ya watu duniani yanakuwa mabaya na wanaanguka katika kila hatua.
“Sasa nataka kufundisha kitu. Kila mmoja wenu ahakikishe anashika kwa unyoofu kile nitakachokisema.
“Maana bila hivyo siku ya mwisho kutakuwa na sherehe kubwa kushindwa kwa utawala wangu na mimi sikubali kushindwa.
“Leo hii wanadamu wanamgeukia Mungu, wanatubu, na nyinyi mpo. Mnafanya kazi gani?”
Kusema ule ukweli mimi nilishindwa kumwelewa, nilichojifunza cha moja kwa moja pale ni kwamba, anatujulisha mapema kwamba kuna ukombozi ambao yeye na ufalme wake wanaupinga.
Hapa ana maana kwamba, sisi tukubaliane na utawala wake wenye uovu, lakini siku ya mwisho kwenye kuangamia, tutajijua wenyewe.
Akaendelea: “Nataka mhakikishe kwamba, kuanzia sasa, wachungaji wanaachana na mahubiri ya kumfanya binadamu amwelekee Mungu, bali wanapewa mahubiri ambayo yanahusu mambo yao ya duniani.
“Nasema tuwafanye wachungaji wahubiri, maana yangu ni kwamba, tukiwafanya wasihubiri haitawezekana, lazima wahubiri, ila mahubiri yao yapotoshe.
“Wengi wenu mtataka kujua watapotoshaje. Watapotosha hivi, wachungaji watakuwa wakiwaita watu kwenye makanisa ya kuwaambia wakienda huko wanabarikiwa na Bwana, kama hawana kazi watapata kazi, kama hawana fedha Bwana atawapa na kusaza.
“Pia, watawaambia kama msichana amehangaika hapati mume wa kumuoa, amekwenda hadi kwa waganga lakini wapi, wakienda kwa Bwana watapata wa kuwaoa, wale waliohangaika kutafuta watoto kwenye ndoa zao kiasi kwamba, waume zao wanakaribia kuwaacha kwa sababu wanawaita tasa, kwa Bwana watapata watoto na ndoa zao zitakuwa na furaha tena.
“Hii itawafanya wanadamu kuamini na kumiminika kwenye makanisa hayo wakiamini ni Mungu wao lakini kumbe ni sisi, na kule makanisani watakakokwenda watakuwa wao kama wao, hawataachana na mambo yao ya zamani.
“Hapa maana yangu ni kwamba, kama mtu ni mzinzi, kwa sababu atakwenda kwenye kanisa la kiroho kwa ajili ya kutaka kuzaa, basi uzinzi wake utabaki vile vile.
“Hii itatusaidia ndani ya makanisa haya ya kiroho wenyewe wanajiita walokole, kuwe na wasengenyaji, wezi, walevi, wenye husuda na mambo mengine yote yanayopatikana kwenye makanisa ya kimwili.”
Hapa nataka kusema kwamba, karibu yote aliyoyasema Mkuu wa Nchi ya Wachawi ndiyo yapo leo hii, kwamba mikutano yote wanayosema ya Mungu kinachohubiriwa ni mambo ya duniani, hilo hata wewe msomaji unalijua..
Utakuta mchungaji amesimama akisema: “Je, umeelemewa na madeni? Unatafuta kazi hupati? Msichana wachumba wanakuja kuleta posa kwenu lakini wanaingia mitini? Wewe mama huna furaha kwenye ndoa yako, huzai ndugu wa mume wanakuita tasa? Njoo kwa Bwana uombewe.”
Lakini ukweli ni kwamba, wakifika kwa huyo Bwana hawafundishwi jinsi ya kuutafuta ufalme wa Mungu kwani wakizisema njia hizo waumini wao wengi watakimbia.
Pia, kuzimu kwa sasa imekuwa ikitumia kila njia kuhakikisha viongozi wa dini wanajikita kwenye siasa, na wao wanakuwa waheshimiwa wabunge, wanakuwa wanasiasa kwa mtazamo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wanasimama kanisani wanakemea viongozi wa kisiasa na kuongea muda mrefu kwenye ibada habari za siasa lakini wanatumia muda mfupi sana kuongelea mapenzi ya Mungu.
Basi, Mkuu wa Nchi ya Wachawi akasema:
“Kwa hiyo nataka kusema kuwa, kuanzia sasa lazima tukaze nguvu ili kuzidisha uasi katika haya makanisa, sawa?”
“Sawa,” tuliitika wote.
“Nataka kuona dunia inachafuka.”
“Sawa.”
“Nataka kuona binadamu wanaishi kwa wasiwasi, sawa?”
“Sawa.”
“Nataka kuona watu hawafanikiwi katika maisha yao,sawa?”
“Sawa.”
“Pia, nataka kuona binadamu wanatutegemea sisi kwa kila jambo. Ikitokea tatizo kidogo waende kwa waganga, sawa?”
“Sawa.”
Hilo wote itabidi mlisimamie kikamilifu ili mambo yaende tunavyopanga. Kwani majira yaliyotajwa yamekaribia sana.”
Nilijiuliza sana ni majira gani yalikuwa yamekaribia kiasi hicho?
Pia, nilikuwa na maswali mengine, ni kwanini Mkuu alisema anataka wanadamu waishi kwa tabu wakati sisi anaotuambia ni sehemu ya binadamu. Nilimuona anatutakia mabaya, tuangamie kwa sababu yeye au wao walishaangamia siku nyingi sana.
“Kwa hiyo ni mategemeo yangu makubwa mnapotoka hapa mnakwenda kufanya maagizo yote, kwaherini sana,” alisema akapotea palepale bila kujua mwelekeo wake.
Na sisi tulianza kuondoka mmoja mmoja au wawili kwa kutembea kuelekea mwelekeo wa kuondokea nchi ile ya ajabu.
Nasema nchi ya ajabu kwa sababu, kama nilivyokwishasema awali, hakuna jua, lakini kuna mwanga.
Halafu huwezi kujua mwanga uliopo ni wa usiku au mchana. Watoto wapo wengi tu, wakiendelea na mambo yao kama ilivyo huku kwenye dunia hii.
Mara ya kwanza nilidhani ni nchi yenye mambo ya uchawi tu lakini kumbe kuna maduka makubwa na watu wanaendelea na shughuli za manunuzi huku wengine wakila na kunywa kwenye maduka kama ya Grosari ingawa sina uhakika kama kuna pombe.
Na Yule mkuu mwenyewe anapokuwa kwenye sura ya kawaida, anakuwa binadamu kama sisi. Kwa hiyo hata tunaposema sheteni mbaya,ana mapembe, ana meno makubwa huwa tunakosea sana.
Basi, mimi nilikuwa na mwenzangu mmoja ambaye nilivutika kumuuliza:
“Hivi aliposema majira yaliyotajwa yanakaribia sana alikuwa na maana gani?”
“Ah! Pale ana maana mwisho wa dunia umefika. Sasa anataka tuvune wanadamu wengi kwenda kuzimu badala ya mbinguni.”
“Unadhani inawezekana?”
“Inawezekana.”
“Kwa nini?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Unajua, ilitabiriwa kuwa, watu watakaokwenda mbinguni au peponi ni wachache sana, lakini atakaoingia motoni wapo wengi.”
“Mh!” Niliguna huku nikiwa nimeweka mikono nyuma kabisa.
“Sijawahi kusikia.”
“Imeandikwa mbona. Tena inadaiwa kwamba, vishawishi vya kuwafanya watu wapotee ni vingi sana kuliko vile vya kuwafanya watu waingie mbinguni.”
“Loo! Ina maana na sisi itakuwaje?”
Yule mwenzangu akashtuka na kusema:
“Huku wenzio huwa hatuhoji hivyo, hayo mambo mpaka duniani.”
Kufumba na kufumbua, mtu mmoja alisimama mbele yetu. Mrefu, mweusi tii. Meno makubwa, marefu akiongea kinywani anatoka mwanga.
“Inabidi mkubali upya kwamba mtaifanya kazi mlioagizwa, sawa?”
“Sawa,” mwenzangu aliitika.
“Wewe vipi?”Aliniangalia mimi.
“Sawa.”
“Haya, mseme wenyewe, mtaifanya kazi mliyoelekezwa?”
“Tutaifanya kazi tuliolekezwa kwa usahihi na ukamilifu wote kama alivyosema Mkuu wa Nchi.”
“Nchi gani?”
“Ya Wachawi.”
“Mkishindwa?”
“Tutendewe sawasawa na kushindwa kwetu.”
Pale pale Yule mtu akapotea machoni petu nasi tukaendelea kutembea:
“Unajua kwanini huyu mtu katutokea sisi tu?”
“Kwanini?”
“Matendo mabaya.”
“Yapi?”
“Ya kwako.”
“Yapi sasa?”
“Yale maswali yako si mazuri huku, hukunielewa?”
“Oo! Sasa tufanyeje?”
Kabla hajajibu mbele yetu sauti ikasema:
“Mlipo simameni.”
Tukasimama.
“Wekeni mikono sawa tayari kwa safari ya kurudi duniani.”
Tuliweka mikono sawa, kufumba na kufumbua mimi nilisimama nje ya nyumba yangu pale pale nilipoondokea usiku huo.
“Khaa!”Nilishangaa.
Kabla sijaingia ndani, upepo mkali ulivuma, ukifuatiwa na mlio wa majani makavu yanayoungua.
Hapa nataka kusema kuwa, mvua zina pande tatu za kunyesha kwake.
Kuna mvua zinanyesha kwa sababu ya nyakati na majira yake. Halafu nyingine zinanyesha kwa sababu ya matakwa ya Mungu. Kama vile ilivyokuwa kwenye gharika au sehemu nyingine.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Pia kuna mvua zinanyesha kwa sababu ya nguvu za giza. Hizi sasa ndiyo mbaya, kwani mara zote huacha ajali, magonjwa na uharibifu.
Unapoona mvua imenyesha kubwa na upepo mkali sana lakini baada ya muda tu ikakatika na jua kuwaka, tambua kuna mambo makuu mawili.
“Kwanza, kuna kazi za ulimwengu mwingine zinaendelea katika dunia hii tunayoishi. Au kuna mapambano makali kati ya jeshi la Mungu na shetani ambapo mara zote jeshi la Mungu huwa linaibuka na ushindi mkubwa.
Basi, katika kufanya kazi kwetu tuliendelea kufika maeneo ambayo tuliweza kusababisha mafuriko makubwa na kuua watu.
Tulichokuwa tunafanya ni kuwa, baada ya kumwaga maji ya baharini na mawingu mazito kutanda, mvua kubwa zikiambatana na radi kali zikashuka.
Tulichofanya, tulikuwa tunashuka hadi chini ardhini na kutengeneza njia za kuyafanya maji yatoke na kuleta mafuriko makubwa mitaani.
Mara nyingi mnapoona maji ya mafuriko yanaingia mitaani, si yenyewe tu, kuna kazi kubwa inayofanywa na roho chafu, lengo ni kuhakikisha jamii haiishi kwa amani wala maelewano, pia binadamu wanakufa sana.
Kwa mujibu wa habari za kule kwenye Nchi ya Wachawi, Mungu mwenyewe anasikitika sana kuona watu wake wanavyoangamia.
Labda unaweza kujiuliza, sasa kama Mungu huwa anaumia, ni kwa nini asizuie wakati ana uwezo mkubwa kuliko? Ni kweli lakini dhambi zetu wanadamu ndizo zinakinga nguvu ya Mungu kwetu.
Kabla sijaendelea mbele, nataka niseme. Kuna vitu vingi huwa vinasababishwa na roho wachafu, lengo ni kuangamiza watu.
Mfano, unaweza kuona mtu anavaa nguo haraka haraka, kisha anatoka anasema anakwenda mahali fulani wakati toka anaamka hiyo safari haikuwepo, mara mnasikia amegongwa na gari, hiyo ni moja ya kazi za roho wachafu.
Kinachotokea, roho ile inamwingia mtu na kumkumbusha kuhusu kitu au mtu fulani, anayekumbushwa ndiyo anapata wazo la kuondoka sehemu alipo.
Roho hiyo hiyo chafu ikitoka kwa huyu, inakwenda kuingia kwa mwenye gari wanayemtaka. Anaweza kumchelewesha au kusababisha tatizo lolote lile, ili mradi muda wa yule atakayegongwa, afike eneo la ajali.
Mfano, upo ndani ya daladala, dereva anaendesha, mara anafika kituoni kuteremsha abiria baada ya konda kumwambia ashushe na wengine mmesikia sauti ya huyo konda akitaka dereva asimame.
Lakini unaweza kushangaa, hakuna abiria anayeshuka na konda akiuliza sana hajibiwi. Lakini nyiye abiria mnakuwa kama mna kumbukumbu ya kusikia sauti ya mtu ikimwambia konda ashushe.
Mara nyingi inapotokea hali ya aina hii, tambua kuna kitu kikubwa mbele ya safari yenu, hususan ajali ambapo kuna ucheleweshaji ulifanywa makusudi ili tu yule mtu aliyekusudiwa kugongwa afike eneo husika.
Kingine, mko kwenye basi, kunatokea majibizano kati ya abiria na kondakta au dereva, labda abiria mmoja amejibizana vibaya na mmoja wao lakini ugomvi unakua hadi wengine wanaingilia na zogo kubwa linazuka. Mara nyingi ni kiashiria cha ajali kubwa mbele ya safari.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lakini sasa, endapo katika safari ya namna hii zogo likiwa kubwa halafu akatokea mtu mmoja na kusema:
“Jamani mpisheni shetani apite.” Au:
“Jamani ni shetani huyu, acheni mzozo.”
Mara nyingi kauli hiyo ndiyo inakuwa salama ya safari hiyo lakini kama hakuna mtu atakayekumbuka kusema hivyo, mbele lazima tatizo litokee.
Nataka kusema kuwa, kama ni zogo linatokea, watu wengine wakaingilia, hapo mawili, itakapotokea ajali, atakayekufa ni yule atakayekuwa kinara wa malumbano au atakayekuwa hachangii chochote kile katika vurugu.
Kingine, kuna watu wakipitwa na basi wanalalamika sana. Hilo ni tatizo, basi likikupita hata kama lina nafasi shukuru Mungu kwani ni malaika wako ndiyo wanaoingia kwenye ufahamu wa madereva na kuwaamuru wakupite ili wewe uwe salama.
Kingine tena, mnasafiri ndani ya basi, anatokea mtoto mdogo wa kuanzia miaka mitatu kurudi chini analia mpaka sauti inakauka hata baada ya kumbembeleza sana, hiyo pia ni dalili ya ajali mbaya mbele ya safari.
Na nataka kusema kwamba, utakuta baada ya ajali, kama usafiri mwingine utapatikana, mtoto huyo atakuwa amenyamaza bila sababu yoyote.
Kwa kawaida, basi linapokuwa kituoni, roho ya ajali inakuwepo pembeni ikilizunguka basi hilo. Na unaweza kushangaa siku hiyo tiketi zikaisha mapema sana kuliko jana yake au siku nyingine.
Kwa wale walioamka na kufanya sala kwa Mungu, mara nyingi huahirisha safari, hasa kama walishakata tiketi au kupanda magari mengine kama hawakukata tiketi.
Dalili nzuri za kuzuia ajali ni kusita kutembea na si kuwahi. Nasema hivi kwa maana kwamba, ukiwa unataka kutoka nyumbani kwenda mahali, halafu roho inasita, mara moja, mbili na tatu, basi acha kabisa hiyo safari.
Ingawa pia, unaweza kutaka kuondoka nyumbani kwenda mahali, hata matembezini, mtoto mdogo akakwambia hataki uondoke au akakufanyia mzaha wowote unaoashiria kukuzuia kutoka, basi tii.
Mizaha ya watoto ni kama vile unataka kutoka yeye anakupita na kusimama kwa mbele kisha anakuzuia usimpite, mara moja, mbili mpaka tatu, hapo lazima kuna kitu.
Ni mara chache sana unaposita kwenda mahali, ukapata tatizo pale pale ulipo. Ikitokea hivyo, utakuwa ulipata ishara ya kukutaka uende mahali lakini ukapuuza ukidhani umechoka, kumbe ajali.
Haya majanga ya moto, mafuriko na ajali nyingine mbaya zinafanyiwa kazi na roho wachafu kwa lengo la kuifanya dunia kuwa mahali pa kukosa amani.
Kingine, inawezekana ndani ya gari kukawa na mtu mmoja tu ambaye ndiye aliyelengwa kufa siku hiyo kwa ajali. Kinachotokea sasa ni hiki…
Hii roho ina mapana sana tofauti na roho ya uongo. Yenyewe inaingia kwa mtu na kumtengenezea mawazo kwenye akili. Haya mawazo hayahami kwa muda mrefu ndiyo maana, utakuta mwanaume amekaa mahali anaangalia wanawake wanavyopita na anapotokea mzuri anasonya au kusifia kwa sauti.
Kinachofanyika ndani ya ubongo wake pale ni kumchukua mwanamke huyo kiakili hadi kitandani. Kule anamlaza, anamvua nguo, anambusu na mambo kadha wa kadha kisha anafanya naye tendo la ndoa.
Baada ya kuwaza hayo sasa, ndipo unaweza kumwona mwanaume huyo anamwota mwanamke kwa sauti.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kazi nyingine ambayo inafanyika kwenye Nchi ya Wachawi ni kuhakikisha wafanyabiashara hawaendelei, labda wale wanaomtegemea Mungu au wanaokwenda kwa waganga wa kienyeji kusaka utajiri.
Tulichokuwa tunakifanya ni kuingiza viumbe wengi wa Nchi ya Wachawi kwenda duniani kuungana na binadamu halisi katika kufanya manunuzi mbalimbali.
Hapa nataka kusema kuwa, unapokwenda sokoni kununua bidhaa mbalimbali, wapo watu unakutana nao ukiamini ni kama wewe lakini ukweli ni kwamba, ni viumbe wa ajabu.
Kazi ya viumbe hawa ni kununua bidhaa lakini mara nyingi fedha wanazozitoa siyo halisi pia siyo bandia.
Fedha za viumbe ambao si binadamu zinaposhikwa na binadamu wa kawaida, hupotea dakika kumi baada ya kupokea kwani viumbe wale wale hufanya kazi ya kuzichukua.
Hapa nataka kusema kwamba, mara nyingi unapoona mtu amekuja dukani kwako au sehemu yako ya biashara akauliza bei ya kitu, akitaka kupokea kwanza bidhaa ndipo akulipe fedha muogope huyo.
Aidha, nataka kusema kwamba, duniani mpaka sasa kuna roho wa kupindisha upatikanaji wa fedha anafanya kazi kwa kasi ya ajabu.
Roho huyu huwaingia watu mbalimbali na kuharibu mipango yao ya kupata fedha, hasa ya kuendelezea maisha yao.
Natoa mfano, unakwenda kwa mtu kukosa fedha kwa ahadi ya kurejesha zaidi ya uliyokopa, kama milioni tano ukiahidi kurudisha milioni sita kamili.
Sasa anayekopesha anaweza kukwambia uweke dhamana ya gari, na wewe unakubali kisha mnapeana miezi mitatu tarehe f’lani ndiyo utalipa deni.
Kitakachotokea, ile roho ya kukwamisha fedha inamwandama yule mkopaji, kila anavyofanya ili kurejesha mkopo ule anafeli.
Wengi wao siku ikipita, wakopeshaji wanaongeza au wanatoza na faini, yaani ulipe deni lakini pia uongeze fedha ya usumbufu.
Hapa, kwa vyovyote vile itakwenda hadi itafika mahali mkopaji atashindwa kulipa deni na gari au mali aliyoweka kama dhamana itakwenda ‘na maji’ kwa mkopeshaji.
Hali hii si kwa wakopeshaji wa mitaani tu, hata wale wanaokopa kwenye mabenki makubwa. Tena utakuta mtu anakopa kwa ajili ya biashara, lakini wateja hawahatokei tu mpaka siku ya kulipa inafika, huna hata fedha inayoweza kulipwa, matokeo yake wengi hufuatwa na kupokonywa vitu vya nyumbani.
Hali hii imefika mahali wengi wanaamini wanaokopesha, au wale watu binafsi kwamba, wanatumia nguvu za giza kuzuia waliowakopesha kushindwa kupata madeni yanayowakabili baada ya kukopa.
Au, kuna roho nyingine kazi yake ni kushawishi. Inashawishi vipi? Inamwingia mtu aliyekopa na kufanya kazi kwenye akili yake.
Unakuta unatoka kukopa mkopo, lakini unaingiwa na wazo la kununua labda kabati la nguo, wakati lengo lako ni kufanyia biashara. Hapo ujue umeingiwa na roho ya kukufanya ushindwe kulipa mkopo.
Na mara nyingi mtu aliyetoka kuchukua fedha ya mkopo anajikuta akipitishwa kwenye njia ambazo atatokea kwenye ushawishi, hii ni lazima.
Ndiyo maana leo hii watu wanalia, wanaweka dhamana nyumba, magari, viwanja lakini wanashindwa kuvikomboa kwa sababu ya hilo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Leo hii wafanyabiashara wapo wengi lakini hawana kitu, hawaendelei. Wamekuwa wakilipa mikopo mpaka inafika mahali, anakopa NBC ili akalipe NMB, au anakopa CRDB ili akalipe ACB, hayo ndiyo maisha ya wafanyabiashara wengi wa sasa.
Hapa pia nataka kusema kwamba, mbali na roho hii ya vikwazo, kuna roho nyingine yenyewe kazi yake ni kuingiza matatizo makubwa kwa watu wa familia iliyochukua mkopo.
Unaweza kuchukua mkopo leo, au ile uko njiani kwenda kuchukua fedha yako ya mkopo, njiani unapigiwa simu baba, mama, shangazi, mjomba au mtu mwingine wa karibu yuko hoi au amefariki.
Kibinadamu, lazima utachota fedha kiasi kutoka kwenye kile ulichokopa ili kutatua matatizo. Wengine hupatwa na tatizo la watoto kufukuzwa shule, wakati mwingine wapo wawili au watatu, wanarudishwa wote nyumbani, ili mradi tu atumie fedha za mkopo.
Au kitu kingine cha ajabu, unaweza kuuza nyumba kwa lengo la kutunza fedha hiyo ili uchanganye na nyingine unazozisubiria kuzipata, lakini ukishazishika fedha hizo hata kama utaziweka benki, lazima utakuwa unazitoa kila siku kidogo kidogo mpaka zinakwisha.
Mbaya zaidi wale wanaohifadhi benki fedha za malengo kama hizo, huwa milango mingine inafungwa, huingizi hata shilingi elfu kumi.
Ukitaka kuchukua uzoefu mwingine ni pale zinapobaki siku tano kabla ya kupokea mshahara, lazima lijitokeze tatizo ambalo halivumiliki kwa wakati huo ili ukatumie kulitatua.
Mfano, una gari utashangaa kila ikikaribia siku ya mshahara, linaanza kugonga au kitu kingine chochote kinatokea ambacho si lazima gari lilale nyumbani, utajikuta unalikongoja hadi siku ikifika unaanza na gari badala ya kutatua matatizo mengine.
Na katika maisha yote, aminini kwamba ndani ya fedha yoyote ile, kuna roho ya kutibua akili, lazima.
Ndiyo maana watu wakasema kwenye fedha mipango si matumizi. Unaweza kusema kitu hiki na kile nitavifanya mwisho wa mwezi baada ya kupokea mshahara, lakini ukishaukamata zile akili za kumbukumbu zinatoweka kwa muda hadi utakapomaliza mshahara.
Hali hii haina mwenyewe, kila mtu humtokea, lakini yule unayemuona amefanikiwa lazima ana malaika wake, lakini si akili.
Kitu ambacho nilijufunza ni kwamba, kuna vita kubwa sana vya kiroho kati ya binadamu bila kujijua na utawala wa kishetani ukiwa unajua na kuweka mikakati.
Binadamu wanaishi tu, wengine wakimuomba Mungu kwa imani, wengine hawamuombi ingawa wanaamini yupo na ndiye anayewasaidia.
Lakini huko kwenye makao yao makuu kazi yao kubwa ni kujenga mikakati mikubwa ya kuuangamiza ulimwengu kwa njia yoyote ile ili kuhakikisha tabu na masumbufu.
Baada ya masumbufu wanatoa mwanga au wanawajazia akili watu kwamba, ufumbuzi wa matatizo yao ni kwenda kwa waganga wa kienyeji ambapo wanajua ni chukizo mbele ya Mungu.
Siku tuliporudi sisi tuliyokwenda kwa dharura kule Nchi ya Wachawi, mimi nilifikia kukutana na mgeni amesimama nje ya mlango wangu ingawa ulikuwa usiku mwingi.
Huyu mtu alikuwa mrefu kiasi, alivaa suti nyeusi au bluu iliyoiva. Alishika mkoba mkononi.
Nilishtuka nikiamini natakiwa kurudi tena kule nilikotoka.
“Nilikuwa nakusubiri wewe,” aliniambia kwa kujiamini huku akiacha kinywa wazi kwa tabasamu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Wewe ni nani?”
“Usitake kujua, lakini wewe si Bwana Israeli?”
“Ndiyo mimi.”
“Mchawi maarufu?”
“Nani kakwambia habari hizo?”
“Najua tu. Kweli si kweli?”
“Iwe kweli au siyo, we umejua kutoka kwa nani?”
“Kutoka kwa Muumba.”
“Muumba ndiyo nani?”
“Hujui Muumba ni nani?”
“Ndiyo maana nataka kujua.”?“Mungu!”
“ Wewe ni nani kwa Mungu?”
“Mtumishi wake.”
“Mtumishi wake!Una maana mchungaji au nani?”
“Mtume wake.”
“Yupi?”
“Si mimi.”
“Kwa hiyo ulikuwa unasemaje?” Nilimuuliza kijeuri sasa.
Na yeye bila jazba wala hasira akanijibu kwa amani na upendo mkubwa.
“Mungu amenituma, ameniambia nikuonye kuachana na hiyo njia unayopita. Tena ameniambia ikiwezekana iwe haraka sana.”
Nilishtuka kwanza. Niliamini mambo mawili yanaweza kutokea pale. Kwanza, kiumbe cha kule Nchi ya Wachawi kingeweza kutokea na kummaliza yule mtu akawa maiti pale pale, lakini pia yeye kama kweli alitumwa na Mungu anaweza kufanya tukio la ajabu.
“Nitahakikishaje kama kweli umetumwa na Mungu.”
Hakunijibu, pale pale akabadilika rangi, akawa mweupe kama mwanga wa taa kuzunguka mwili wake.
Akanyoosha mikono juu, ghafla hali ya mavazi yake ikabadilika, kutoka kwenye suti na kuwa kanzu kubwa nyeupe isiyo na hata alama ya kuwepo kwa doa.
“Unataka kuamini zaidi ya hapa?” Aliniuliza.
Nilishuka chini na kupiga magoti huku nikikunja mikono kwa unyenyekevu wa hali ya juu huku nikisema:
“Nisipokuamini wewe bwana nimwamini nani? Haya naomba mkono wako ili nipate kinga.”
Yule mtu, sasa akiwa hana mkoba, alinyoosha mkono na kuuweka juu ya kichwa changu.
“Pokea kukingwa na pia safishika na maovu yote, kamtumikie Bwana wako.”
Ghafla nilihisi mwili wote umekuwa mwepesi kama vile nilikuwa nimetua mzigo mkubwa uliokuwa kichwani kwa muda mrefu.
Nilishtuka kutomuona yule mtu, alikuwa amefutika. Hapo nikaingiwa na wasiwasi mkubwa, kwamba pengine ulikuwa wakati wa kujitokeza kwa kiumbe wa Nchi ya Wachawi.
Nilitembea kuelekea kwenye mlango wangu na kufungua huku kukiwa hakuna dalili yoyote ya tukio la ajabu.
Niliingia ndani na kuwasha taa, nikafanya ukaguzi wa hapa na pale hakukuwa nakitu kipya wala cha kutisha. Nilikaa kitandani na kuwaza:
“Lazima atakuwa ametoka kwa Mungu, kwani wa kutoka kule (Nchi ya Wachawi) asingeniambia vile. Tena angesemaje vile wakati na mimi nilitokea kule kule?”
Nilikwenda kuoga, nikarudi ndani na kujitupa kitandani bila kuwepo kwa jambo lolote la ajabu kwangu wala kwa nyumba yangu.
Asubuhi, niliamka nikatoka nje, hali ilikuwa shwari tu, majirani walinisabahi kwa heri na amani huku wakiniuliza habari ya safari, nikawajibu ilikuwa nzuri na salama kabisa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jumapili iliyofuata, siku nne baada ya kurejea, nilikwenda kwenye kanisa moja la kilokole, nikasali pale na kujikabidhi kwa Mungu nikimshukuru kwa kuninusuru kwa njia ambayo baada ya kuguswa na mjumbe wake ndiyo nikajijua nilikuwa upotevuni.
Nilianza maisha mapya ya kumtumikia Mungu kwa kusali sana na kuwaelekeza watu jinsi ya kuishi maisha ya kumpendeza Mungu aliyeumba ulimwengu huu, wengi kwao ilikuwa ni butwaa wakiwa hawaamini kwani nilishalichafua jina langu mbele ya jamii.
Kila nilipokuwa nakaa na kukumbuka mapitio ya nyuma nilikuwa natoa machozi kwani niliua wengine, nilitia vilema kwa magonjwa mbalimbali, wengine niliwaharibia maisha kwa kuwatia nuksi za maisha, hivyo kila walichokuwa wanakifanya hakikufanikiwa.
Nilimshukuru Mungu kwa kuniona na kumtuma mjumbe wake kuja kunionya. Lakini ukweli ni kwamba, katika uchawi hakuna mapenzi ya Mungu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
...Mwisho...
0 comments:
Post a Comment