Simulizi : Nchi Ya Wachawi
Sehemu Ya Nne (4)
Tulibaki tumemtumbulia macho kule alikokuwa akielekea, lakini sekunde chache baadaye hatukuweza kumwona tena.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Jamani mwenzetu ametoweka!” Mzee mmoja alisema kwa sauti yenye mshtuko.
Wengine hawakusema lakini walibaki wameshika midomo kwa mshtuko uliowapata. Hakuna aliyejua nini kimetokea, ingawa ukweli ni kwamba, utowekaji wa yule mchawi mwenzetu ulitokana na maneno yake, hasa kuonesha mbele ya watu kwamba, anapingana na kitendo cha wachawi kumwabudu shetani wakati siku ya mwisho watakwenda motoni.
Kauli yake ilionesha kuwa, kumbe shetani hana nguvu kubwa kumpita Mungu, ingawa ukweli ni huo lakini siku zote mamlaka za kuzimu hutaka zionekane kuwa, zenyewe zina nguvu kubwa kuliko utawala wa Mungu juu ya ardhi.
Hili nalithibitisha hivi; Hata enzi za mapambano ya Mtawala wa Misri, Farao na Mtumishi wa Mungu, Musa, utawala wa kuzimu ulikuwa ukionesha nguvu zake hadharani, lakini Mamlaka ya Mungu ikawa inashinda kwa kishindo.
Basi, niliinua mkono wa kushoto juu ili kuwaweka sawa wachawi wote waliokuwa pale ambao walionekana kushtuka kwa tukio lile.
“Tulieni jamani,” nilisema kwa sauti yenye mamlaka.
Wote wakatulia na kuniangalia, lakini wapo baadhi ya wachawi waliendelea kugeukageuka kuangalia ule upande ambao mwenzao alitowokea.
“Naomba macho yote yawe kwangu,” nilisisitiza.
Nikaanza kwa kusema: “Kwanza napenda kusema lililotokea si tukio la kawaida wala la kupuuzia, kwani mpaka sasa mwenzetu si wetu tena.”
Watu wote wakashtuka kwa kusema: “Haaa! Jamani.”
“Ukweli ni huo. Na kwa uzoefu wangu yule amepelekwa mamlaka za kuzimu.
“Haaaa! Woyeee, tumekwisha sasa,” walisema kila mmoja kivyake na kusababisha hali fulani isiyo na utaratibu.
Mara sauti nzito, sauti yenye mtetemesho ilisikika ikisema:
“Kila aliye hapa amekula kiapo cha kutumika kwenye mamlaka ya kuzimu. Hivyo, kwenda kinyume na kiapo ni sawa na usaliti. Na sisi katika utawala wetu msaliti ana adhabu moja tu, ni kutangulia kwenye ziwa la moto.”
Wakati hayo yakisemwa, wachawi walianguka chini kwenye udongo kasoro mimi ambaye nilishatoka kushuhudia mazito zaidi ya yale.
Kufuatia tukio hilo la wachawi kulala chini, aliyekuwa akitoa ile sauti alijitokeza mbele yangu na kusimama sanjari na mimi.
Alikuwa mrefu wa wastani, mweusi tii. Pua yake ilichongokea mbele na kuwa kama ndizi, katikati ya paji la uso alikuwa na kipande cha pembe kikiwa kimekatika kwa mbele.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Na kila alipokuwa akinisemesha, kinywani alitoa cheche za moto huku zikianguka chini na kuzimika.
“Hakikisha hili lililotokea hapa leo halijitokezi tena. Sisi tuna uwezo wa kuwasikia wanadamu wanavyosema sehemu yoyote kwani dunia ni mali yetu.”
Niliitikia kwa kutingisha kichwa, halafu akakunja sura na kusema:
“Yule mzee uliyempa tama ya kulala na binti yake mkubwa hukumfanyia haki. Yule ni mwenzako, sasa tatizo lilikuwa wapi. Ulikingwa na cheo chako, lakini kama si hivyo na wewe ungerudi tena kule kule lakini safari hii si kwa mema.”
Nilishtuka kusikia maneno hayo, nikajikuta nikianguka ghafla na kupoteza fahamu.
Sikumbuki ni muda gani aliondoka, ila nilipokuja kuzinduka nilijikuta nimesimama haraka kama vile sikupenda wachawi wenzangu wajue kwamba nilianguka.
Na wao hakuna kati yao aliyekuwa anajitambua na walikuwa wamelala kule na huku kama watu waliokunywa sumu katika mlo wa pamoja.
“Inukeni,” nilisema kwa sauti ya juu, na yenye mamlaka.
Wote walisimama, karibu wote wakawa wanajipukuta vumbi kutokana na kulala chini.
“Leo nimeambiwa mambo makubwa sana hapa. Kwa hiyo nitakuwa mkali na makini. Kama mtu hataki kuwa mchawi ni kwanini aliapa kutumikia?” Nilihoji nikiwaangalia kama kuna mwenye hoja.
Mzee mmoja akanyoosha mkono.
“Ndiyo, unasemaje?”
“Ukifuatilia kwa undani tatizo lililompata mwenzetu lilisababishwa na maneno yako na wala si ufahamu wake.”
“Maneno yangu? Maneno gani hayo?”
“Kumbuka ulichokuwa unataumbia kuhusu huko ulikokwenda?”
Huyu naye wakati akisema hayo, upepo ule ule ulivuma tena kwa sekunde kadhaa huku wote tukimwangalia yule mzee ili kujua kama atatwaliwa au la.
“Jamani jamani jamani ee,” alipiga kelele.
Mzee mmoja akanyoosha mkono.
“Ndiyo, unasemaje?”
“Ukifuatilia kwa undani tatizo lililompata mwenzetu lilisababishwa na maneno yako na wala si ufahamu wake.”
“Maneno yangu? Maneno gani hayo?”
“Kumbuka ulichokuwa unatuambia kuhusu huko ulikokwenda?”
Huyu naye wakati akisema hayo, upepo ule ule ulivuma tena kwa sekunde kadhaa huku wote tukimwangalia ili kujua kama atatwaliwa au la.
“Jamani jamani jamani ee,” alipiga kelele.
ENDELEA MWENYEWE…
Kufumba na kufumbua, yule mzee akawa ametwaliwa juu kwa juu huku akiendelea kupiga kelele akisema anakufa:
“Nakufa jamani, maneno yangu yameniponza,” alisema yule mzee akipotelea hewani.
Hali ikawa tete pale kwenye mkutano, kwani sasa kila mmoja alikuwa ameshikwa na hofu kasoro mimi ambaye nilishajua nini kilikuwa kikiendelea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilifika mahali kutokana na hali ilivyokuwa, niliwaamuru wachawi wote wakalale ili kupumzisha akili lakini karibu wote walikataa wakisema lazima usiku huo watu waingie mtaani kuwangia wakazi wa mji huo.
“Hapana mkuu, hapana. Twendeni mtaani tukawange,” walisema kwa pamoja.
Ilibidi nikubaliane na matakwa yao, hivyo tulitoka katika vikosi vitatu vyenye mchanganyiko wa wake kwa waume.
Mimi niliongozana na wazee wa kiume wanne na wa kike watano ambao wote ni wakongwe sana katika uchawi. Kwa hiyo jumla yetu tulikuwa tisa.
Breki yetu ya kwanza ilikuwa kwenye kituo cha daladala cha Ubungo mwisho ambapo kulikuwa na watu wengi wakifanya biashara mbalimbali huku mabasi yakiendelea kupakia abiria na kuondoka.
Sisi tulisimama jirani kabisa na vijana waliokuwa wakiuza bidhaa ndogo ndogo kama vile sendozi, sabuni, vitana na kadhalika. Tulishikana mikono kisha mimi nikatoa nguvu zangu na kuwaingizia wale watu, nao wakawa tofauti, nikasema maneno kwa dakika tatu, palepale likatokea basi likiwa na abiria wachache ambao ni sisi wachawi.
“Mmoja kati yetu alikuwa dereva wa basi hilo, mmoja alisimama mlangoni na kuwa kondakta akiitia abiria kwa kelele kama makonda wengine wanavyofanya, wachawi wengine waliobaki walikaa kwenye viti.
“Tabata Relini, Tabata Bima, Mawenzi,” yule mchawi kondakta aliita.
Ilikuwa kufumba na kufumbua, basi lilijaa abiria waendao Tabata.
Dereva aliondoa basi kwa kasi kiasi kwamba, baadhi ya abiria walilalamika.
Kitu tulichokitengeza ni kuwa, basi lilipofika maeneo ya hoteli ya Landmark, Ubungo abiria waliokuwa wakishuka maeneo ya External waliamini wameshafika hivyo waliomba kushuka.
“Konda shusha External,” walisema abiria wawili, basi likasimama, wakashuka.
Kufika External, abiria wengine wakaomba kushuka.
“Konda acha Tabata Relini.”
Lakini tulipofika, Tabata Relini tulibadilisha aina ya ushukaji, sasa tukapitiliza kwenda Buguruni ambapo baadhi ya abiria wakaomba kushuka Bima wakati ni Buguruni.
Tulichokuwa tukikifanya, kila abiria tulimfuta uso kwa kutumia viganja vya mikono hivyo akawa anaona kinyume na hali halisi.
Dereva alikata kona pale na kuingia Barabara ya Uhuru kuelekea Ilala ambapo hakusimama hadi alipofika kituo cha Ilala-Boma ambapo abiria mmoja alisema anaomba kushuka Tabata Bima, dereva akaweka basi pembeni na yule abiria akashuka.
Hapa nataka kusema kuwa, naamini mara kadhaa kuna watu wamejikuta wameshuka kwenye daladala eneo ambalo silo walilolitarajia.
Wengine inapotokea hali hii hudhani walilala usingizi, wengine huamini wamepitiliza kwa bahati mbaya tu, lakini ukweli ni kwamba, unaweza ukawa umepanda basi la wachawi.
Na mabasi ya wachawi kwenye miji mikubwa ni mengi tu, mbaya zaidi hayana tofauti yoyote ile na mabasi mengine.
Makonda wake huvaa sare kama wengine, basi lina namba za kawaida, unaweza kuingia ndani ya basi ukakuta viti vingine vumechanika, vingine vimechafuka, yaani ili mradi kukupa uhalisia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Na hata wafanyakazi wa mabasi mengine wanaweza kujikuta wakiongea na wale wa mabasi ya kichawi kama vile wanafahamiana, lakini ni kiini macho tu kinachofanya kazi hapo.
Basi, konda alinifuata na kuniuliza mwelekeo kwa kuninong’oneza, nikamwambia Posta Mpya. Na yeye alipotoka kwangu, alimfuata dereva na kumwambia mwelekeo huo.
Tulipofika Shule ya Uhuru, abiria kadhaa walihoji kisa cha safari yetu kuwa ndefu siku hiyo tofauti na siku nyingine.
“Eti jamani! Yaani Mawenzi tu hapo lakini leo tumekuwa kama tunakwenda Chalinze?” Alihoji mzee mmoja akimuunga mkono mtoa hoja wa kwanza ambaye ni mwanamke.
Pale pale dereva alipiga honi mara mbili, kisha akawasha taa kwa full na kupunguza, kufumba na kufumbua, mbele yetu kukawa na foleni kubwa.
“Jamani abiria nyinyi hamuoni foleni hii?” Alisema dereva.
Abiria mmoja akaanza.
“Na huu mji bwana mimi naushangaa sana. Ukikuta hapa pako sawa, mbele foleni. Sijui hii foleni itakwisha lini?”
“Aa! Serikali yetu hii bwana ndiyo hivyo tena. Waliotengeneza ramani ya mji huu hawakuwa na ndoto za baadaye, walidhani magari yangeendelea kubaki kumi kama enzi za uhuru,” alisema kijana mmoja.
Wakati tunakaribia Posta, abiria wote walianza kusimama na kwenda mlangoni kwa lengo la kushuka, wao wakimaanisha ndiyo wanafika Tabata Mawenzi.
“Hii ndiyo Bongo bwana,” abiria mmoja alisema akiwa anatembea kuelekea mlangoni. Hakuna aliyejua kuwa, pale ni Posta.
“Naweza kusema kwamba, uchawi upo na asitokee mtu akabisha kwani anayebisha anamkosea hata Mungu kwani yeye ndiye Muumba na alisema uchawi upo, ila aliwaonya wanadamu wasiende kwa wachawi bali wamtumainie yeye.
“Haya Tabata Mawezi,” alisema kondakta wa kichawi huku akipiga bati la daladala.
Watu walishuka, wengine wakionekana kupoteza mwelekeo wa macho, kwani walikuwa wakishangaashangaa.
Sasa hapa nataka kutoa ufafanuzi, ni kwamba, kila binadamu aliyezaliwa na mwanamke ana malaika wake mlinzi, ambaye ndiye anayemwepushia na mabaya yote. Ukimwona mtu kanusurika na janga lolote watu wakasema mshukuru Mungu, jua ni malaika wake ambao wanatoka kwa Mungu.
Sasa, inategemea na usafi wa mtu. Binadamu msafi hata malaika wake anafanya kazi nzuri kwake ya kumlinda. Usafi ninaoongea hapa ni umbali wa matendo maovu, mfano, mtu hapendi kunywa pombe, hapendi kusengenya, hapendi kusema uongo, hapendi kuzini. Mtu wa aina hii malaika wake hufanya kazi nzuri ya kumlinda.
Sasa miongoni mwa watu walioshuka kule wapo waliokuwa na dhamira safi ndiyo maana macho yao yalianza kutambua mapema kwamba wamepotezwa njia kwa kushangaashangaa.
Nilichofanya mimi, nilikwenda kusimama katikati ya mlango nikainua mkono na kuwanyooshea wote kama vile nawaelekeza jambo, wale wote walioanza kushtuka wamepoteza ufahamu wa uelewa na kuwa kama wengine.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wapo walioanza kuvuka barabara wakiamini ndiyo wanaelekea majumbani mwao, wapo walioonekana wanataka kwenda baa kunywa pombe maana niliwasikia wakisema:
“Tukae hapa baa tupate bia mbili ndiyo twende nyumbani.”
Daladala letu likiwa limebaki tupu, tuliulizana, je tuendelee kupakia abiria wengine au tushuke na kufanya mambo mengine?
Mchawi mmoja akasema tutengeneze meli yetu tuipeleke Kigamboni.
Tulikubaliana kwa ajili ya hilo, tukalipoteza lile daladala na kupenya hadi kando kando ya bahari.
Tulisimama tukashikana mikono kisha tukaiinua juu, nilisema maneno yangu kwa muda pale pale pantoni kubwa ikasimama mbele yetu, tuliingia na kujipanga, nahodha alikaa kwake na kuanza kupiga honi.
Wakati huo kulikuwa na pantoni moja tu, ya kwenda na kurudi na ilikuwa ng’ambo ya pili ya Kigamboni ikipakia abiria.
Nahodha wetu alizidisha kupiga honi, kisha mmoja wetu alikwenda getini kufungua geti na kuruhusu abiria kuingia, lakini wafanyakazi wa pale wakawa hawana habari, wao waliona geti liko sawa na waliona pantoni iko Kigamboni ikapakia abiria kuja Magogoni.
Abiria waliingia kwa fujo wakilipa nauli kwa mchawi wetu lakini na wao wakawa wanapewa vipande vya vitambaa wakiamini ni tiketi.
Pantoni ilipojaa, iling’oa nanga huku ile iliyokuwa upande wa Kigamboni nayo ikikaribia katikati.
Tuliwapiga upofu abiria wetu na wale wa kwenye pantoni ile wasijitambue, hivyo ikawa rahisi pantoni yetu kufika salama, abiria wakashuka wote na kumalizikia mitaani kwao.
Hapa ina maana kwamba, wale abiria walipanda na kufika, lakini pesa zao hazikwenda serikalini, kwani tulizichukua sisi kwa ajili ya mambo yetu.
Baadaye tulipanda pantoni ileile ya halali na kurudi ng’ambo ambako tulikwenda kwenye kituo cha taksi na kukodi mbili tukawaambia maderava watupeleke Kigogo Mbuyuni. Tulikuwa na shida na majani ya mbuyu ndiyo maana ilitubidi tufike pale kwanza.
Wakati tunakodisha taksi zile, tulikuwa kama vijana kwa wasichana na tulionekana tunatoka Beach za Kigomboni.
“Kigogo Mbuyuni pale pale au?” Walituuliza.
“Pale pale,” nilijibu mimi.
“Ingieni, wengine kule, wengine huku,” alisema mmoja wao huku akiingia ndani ya gari lake.
Tulianza safari kwa kufuatana hadi maeneo ya Msimbazi Center, mimi nikajigeuza upepo na kutoka ndani ya gari, hatua kadhaa mbele, mchawi mwingine akafanya kama mimi, wakaendelea wengine na kwenye taksi nyingine mpaka wakaisha.
Tukiwa tumesimama tukiangalia kitakachofuatia, tuliyaona magari yote mawili yakiegesha pembeni mwa barabara kisha madereva wao wakashuka wakiwa na wasiwasi mkubwa.
“Ee bwana imekuwaje?”
“Najua basi, nashangaa sina abiria!”
“Mimi pia hivyo hivyo bwana,” alisema dereva mmoja.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walipogundua tukio lile liliwatokea wote, walikimbilia ndani ya magari yao na kuwasha, wakaondoka mbio na kuzunguka mduara wa Kigogo (Round About) na kurudi mjini kwa kasi kubwa.
Sisi tukaenda Mbuyuni ili kuanza kufanya mambo yetu.
Pale mbuyuni, tulikuta wachawi wengine wa makundi mbalimbali wakiutawazia ule mbuyu, tukaungana nao kwa tendo hilo.
Tuliingia kwenye mduara na kuutawazia mti wa mbuyu huku tukiimba na kucheza ngoma iliyokuwa inapigwa.
Hapa nataka kufafanua kuwa, unapoona mtaa au eneo fulani watoto wanaugua ghafla hasa magonjwa ya kukohoa au kutapika, tambua kwamba kuna wachawi waliotawazia mti mmoja uliopo maeneo hayo.
Na mara nyingi miti inayotumiwa na wachawi kutawaziwa huwa inadumu miaka mingi sana, hata kama ni barabara inapita eneo hilo, inapindishwa na kuukwepa mti.
Na ikitokea siku mti wa aina hiyo ukagongwa na gari hakuna anayetoka katika ajali hiyo, awemo mtu mmoja au zaidi.
Pili, lazima mti unaotumiwa kutawaziwa na wachawi utapata sifa ya kuitwa kwa jina la eneo. Mfano, mbuyuni, mfenesini, mwembeni, mzambarauni, mperani, michungwani au zaidi ya hapo.
Basi, tulipojiridhisha kwamba tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuutawazia ule mbuyu, tulitakiwa kumtwaa mtoto mmoja wa jirani na kumpandisha juu ya mti huo mnene.
Awali mimi nilimtuma mchawi mmoja akaingie kwenye nyumba yoyote na kututafutia mtoto mdogo, lakini nikaghairi na kwenda mwenyewe. Mpaka hapo wachawi wote walishajua mimi ndiye kiongozi mkuu, kwa hiyo nikawasimamia hata wale wachawi tuliowakuta.
Na alama kubwa kutoka kwangu ni kitambaa cheusi kilichokatisha kichwa toka upande mmoja kwenda mwingine, kwa wachawi wazoefu walijua ni nini.
Wakiwa wanaendelea kunisubiria pale pale mbuyuni, nilifutika na kupaa hewani huku nikizikodolea macho nyumba zote za eneo lile, ambapo niliweza kuona ipi ina mtoto au ina watoto.
Nilipoiona nyumba moja niliyoridhika nayo, nilishuka hapo na kuzama ndani kichawi huku nikiwaangalia wenye nyumba ambao wote walikuwa wamelala usingizi mzito.
Niliizunguka nyumba hiyo mara tatu na kisha nilipofika mlangoni nilisimama kuipa mgongo nikajibinua makalio na kugusa ukuta pembeni ya mlango.
Kufumba na kufumbua nilikuwa ndani ya nyumba, nilitembea kwa mwendo wa hatua za mbali mpaka kwenye mlango wa kuingia chumba cha watoto.
Pale mlangoni, nilisimama imara na kutanua miguu kwa kuacha nafasi yenye uwezo wa kuruhusu mtu kupita kwa kuinama na kutokea upande wa pili.
Niliinua mkono mmoja juu na kuuelekeza mlangoni huku nikiukazia macho mlango kwa umakini wa hali ya juu.
Kwa kuukazia macho mlango, nikawaona watoto watatu wamelala kitanda kimoja, yupo mdogo kuliko wote na mkubwa.
Nilimnyooshea kidole cha mkono yule mkubwa na kumfanyia ishara ya kumwita, baada ya sekunde tano alianza kuinuka taratibu kutoka kitandani mpaka kufikia hatua ya kukaa kitako.
Niliendelea, akaanza kushuka taratibu na kuanza kutembea kuelekea mlangoni niliposimama mimi. Alifanya hivyo mpaka akafika miguuni kwangu, nikamshika kichwa sehemu ya utosini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niligeuza na kutoka kwenye nyumba hiyo huku yule mtoto akinifuata kwa nyuma hadi nje ambako nilimshika mkono na kufutika ghafla mpaka juu ya mti wa mbuyu ambapo tulitua kwa kishindo kikuu.
Wachawi wote walipiga makofi kwa kufanikiwa kwangu kumfikisha mtoto yule kwenye mti. Nasema walipiga makofi kufurahia kwa sababu gani? Kwanza, nataka niseme kuwa, hakuna mahali ambapo wachawi wengi wanapata ajali na hata kufa kama kitendo cha kwenda kuingia kwenye nyumba ya mtu, hasa usiyemjua.
Maana walio wengi wamezitengeneza nyumba zao kiasi cha kuhatarisha maisha ya wachawi, kama mwanga ataingia kwenye nyumba ya mtu wa aina hii anaweza kuumia au kufa.
Basi, kule juu nilimwacha mtoto mimi nikashuka chini kuendelea na mizunguko miwili mitatu ya kuuzunguka mbuyu, baadaye nikampandia na kumchukua.
Nilikwenda naye hadi nje kwao na kumwacha mlangoni akiwa amelala. Hapa nataka kusema kitu cha muhimu ili watu wasio wachawi wakijue.
Naamini katika maisha kuna watu wameshajikuta wameamka wakiwa nje ya nyumba, mashambani au sehemu ambazo sizo walizolala usiku uliopita.
Kinachofanyika hapo ni kwamba, unachukuliwa na mchawi au wachawi na kukupeleka wanapotaka, lakini wengine badala ya kukurejesha kitandani, wanakutelekeza popote wanapotaka mpaka utakapoamka mwenyewe na kujishangaa.
Tuliondoka hadi njia panda ya kwenda Moroko na Manzese, pale Magomeni Mapipa. Kwa kawaida, katika barabara ya Morogoro, eneo lile karibu na kituo cha mafuta ndiyo pana wanga wengi.
Nataka kuwaambia watu kwamba, pale kona wanaposimama kusubiria daladala ni mahali hatari sana kwa wachawi, magari mengi yanayosimama pale si daladala halisi, pia hata watu wanaosimama pale muda wa usiku wakijifanya abiria si wa kawaida.
Na ukitaka kujua ukweli wa ninachoongea, ukifika maeneo yale saa sita usiku na kuendelea, kwanza utahisi kama nywele zinasisimka kwa muda.
Pili joto la mahali pale linaongezeka kuliko kawaida yake na hali ya uoga itakutawala tu hata kama mbele yako hakutakuwa na kitu.
Basi, pale ambapo tulipafikia kwa miguu ya kawaida kutoka Kigogo Mbuyuni, tulikwenda kusimama pembeni ya ukuta wa hoteli moja maarufu.
Basi la kwanza toka sisi kufika pale lilikuwa Hiace jeupe lenye lebo ya shule ya sekondari moja iliyopo Tegeta.
Lakini ukweli ni kwamba, lilikuwa ni gunia kubwa, lenye vikatuni ndani ambapo kwa macho ya kawaida walionekana ni abria ndani ya basi.
“wanaokwenda Ubungo…haya Ubungo Ubungo,” konda wa uongo alisema kwa sauti akiwa amesimama mlangoni.
Watu walilifuata kwa kugombea kiasi kwamba, katika akili za kawaida tu, ilikuwa rahisi kuhoji watu wote wale walikuwa wakitoka wapi kwenda wapi usiku ule?
Lilipojaa lilianza kuondoka taratibu huku konda wake wa uongo akituoneshea sisi dole gumba kwa sababu alishatuona kwa macho ya kichawi na kujua sisi kama wao.
Na mimi nilimuonesha dole gumba langu, akatingisha kichwa.
Sasa hapa unaweza au mtu anaweza kujiuliza kuna faida gani kwa wachawi kugeuza kitu chochote kuwa daladala na kupakiza abiria njiani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ukweli ni kwamba, hakuna kitu cha maana kinachopatikana katika hali ya macho ya kibinadamu, lakini sasa nje ya macho hayo kuna mambo makubwa.
Binadamu anaposema ana mkosi, au anahangaika na maisha, au watu wanaugua bila sababu, kwenye ndoa watu wanagombana hovyo, hii yote inatokana na tabia hizi.
Ninamanisha tabia ya kupanda kwenye usafiri wa daladala za kichawi. Na iko hivi, ogopa sana kuona uko ndani ya daladala lakini konda amesahau kukuchaji nauli, usidhani ni neema kwako kwamba umeachiwa mia mbili na hamsini, bali ni kusudi endapo konda huyo atakuwa wa daladala ya kichawi.
Sasa inapotokea ukamwona konda amejisahau, wewe mlipe nauli yake bila kujali au kuhoji ni wa daladala ya kawaida au ya kichawi.
Ndiyo maana watu wengi wameshasikika wakisema kuwa, walipata pesa jana yake lakini siku mbili mbele walipoteza.
Ndiyo mkosi wenyewe huo, wengi wanakutwa na mikasa hii baada ya kupanda mabasi ya wachawi toka sehemu moja kwenda nyingine.
Nataka nitoe mfano mmoja, kuna mwanamke mmoja alikuwa akiishi Manzese, Dar. Huyu mwanamke alishikwa na ugonjwa ambao madaktari walishindwa kuutibu, wakawaambia ndugu zake.
Jirani na mama huyo, kulikuwa na bibi kizee mmoja akamwambia mganga mwenye uwezo wa kutibu ugonjwa huo anaishi Mbagala.
Lakini ili atibiwe vizuri, anatakiwa kufika nyumbani kwa mganga, yaani Mbagala saa tisa usiku. Akapewa ramani ya kufika hadi mlangoni, yeye na nduguye mmoja ambaye alijitolea kumsindikiza.
Kutoka Manzese kwenda Mbagala kwa usiku ni tabu sana ya usafiri, lakini ilipofika saa saba wao waliondoka Manzese, wakapata daladala hadi Kariakoo.
Pale Kariakoo walikuta uhaba wa usafiri, lakini baada ya muda likafika daladala likiwa na abiria wengine, konda akatangaza linakwenda Mbagala, wale watu wakapanda.
Njiani hakuna abiria aliyeshuka mpaka kwenye kituo cha Mbagala, konda akawataka wale abiria wawili wanaokwenda kwa mganga washuke kwa vile wao wanakata kushoto kuingia ndani.
Kwa ramani waliopewa na wao wakaomba waendelee kuwemo garini kwani wanaelekea pande hizo hizo.
Daladala likaondoka, mbele konda akawaambia wao wanakata kushoto, wale watu nao wakasema hata sisi tunakwenda kushoto.
Mbele, konda akasema daladala linaishia kwenye nyumba ile ya mganga, kwa hiyo wale abiria washuke wandelee kwa miguu, lakini nao wao wakasema pia wamefika.
Wale watu wawili walitangulia kushuka na kuanza kuelekea mlangoni kwa mganga ili wabishe hodi, lakini kabla ya kitendo hicho, mganga alitoka na kuwauliza kama wanajua wamekuja na usafiri gani.
Kwa kuwa waliamini daladala ile nayo ilikuwa imefika waligeuka kuiangalia ili wamwambie mganga, lakini cha kushangaza hawakuona daladala wala dalili yake.
Hapa nataka kusema kuwa, usafiri wa aina hii Dar umejaa. Lakini unajua kwanini mganga alitoka haraka? Je, kulikuwa na uhusiano wowote kati ya mganga na wale wa daladala la kichawi au na yule bibi kizee aliyeelekeza kule Manzese?
Madhara mengine makubwa ambayo yanatokana na kupanda magari ya kichawi ni tabia za watu kupoteza poteza vitu mfano unakuwa hujui wapi umeweka fedha au wapi umeweka viatu lakini kumbukumbu zinakwambia ulikuwa umeshika.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Madhara mengine ni tabia za kujenga nyumba na kushindwa kuzimaliza. Mambo mengine yanayotokea na madhara ya mabasi haya ni mizozo inayotokea wakati wa sherehe mfano unakuta harusi inakwenda vizuri lakini ghafla kitu kidogo tu ugomvi unaibuka.
Ningependa kabla ya kuendelea mbele zaidi nitoe elimu fulani ambayo itawasaidia watu wasiokuwa wachawi.
Ni kwamba, hakuna dawa kubwa ya kuushinda uchawi kama kuupuuza, mfano, unaumwa sana, umekwenda hospitali madaktari wamesema hawaoni tatizo, umekwenda kwa mabingwa wa kutibu hospitali kubwa, lakini tatizo halionekani, ukapelekwa kwenye maombi makanisani, lakini wapi dawa ni kupuuza tu.
Hapa nina maana gani, uchawi ukiupuuza toka akilini unakosa nguvu ya kufanya kazi na ndiyo maana wapo binadamu ambao hawana kinga yoyote lakini uchawi haufanyi kazi kwenye miili yao.
Sasa hata kwa wale ambao watakuwa wamepanda daladala au basi la kichawi, ukihisi hivyo kutokana na jinsi nilivyoongea, unachotakiwa kufanya ni kupuuza tu, hakuna kingine.
Jamii imekuwa ikiangamia kwa uchawi kwa kukosa maarifa na ujasiri wa kuupuuza. Mfano, utakuta mtu anarudi nyumbani kwake, mlangoni anakuta hirizi, moyo unamshtuka na kuanza kufikiria kifo au matatizo mengine ya mwili.
Wapo ambao wanadiriki hata kuitunza hiziri hiyo isiguswe na mtu mpaka aende kwa mganga wa kienyeji akamuangalizie, hii
ni hatari kubwa.
Ukikuta hirizi mlangoni, ishike, ichome moto huku ukiwa na moyo uliojaa hasira, nawaambia hata kama iliwekwa kwa lengo la kumkomoa mtu au kumroga mtu haitafanya kazi. Kazi kubwa ya kichawi ni kuamini kwanza, baadaye damu ndiyo inapokea.
Mfano mwingine, inatokea katika kijiji au mtaa, kuna mtoto ameaga dunia, wengine wanasema kwa uchawi, wengine amri ya Mungu, ni rahisi sana kujua. Utajuaje? Ilivyo ni kwamba, kifo cha mtu aliyeaga dunia kwa mapenzi ya Mungu msiba unatawaliwa na watu kucheka, nikiwa na maana majonzi si sana, lakini msiba wa mtu aliyeuawa kwa uchawi, watu wanalia sana, tena sana.
Kingine ni kwamba, ukitaka kumjua mchawi mahali unapoishi au unapofanyia kazi, mara nyingi anakuwa na tabia isiyofanana na wengine. Mfano, asubuhi ukiamka, ukiwa unakwenda chooni, ukikutana na jirani yako ukamsalimia lakini akaitikia kwa sauti ya chini sana tena huku akiangalia ukutani, tambua huyo ni mchawi.
Au, unakwenda kazini, kufika unakutana na mfanyakazi mwenzako, unamsalimia kwa kumpa mkono yeye anaitikia salamu lakini hakupi mkono tambua huyo ni mchawi. hakuna mchawi asiyekuwa na dalili kwenye jamii, sema tu macho ya watu yamefungwa kuona yaliyo sirini kutokana na wingi wa dhambi zetu sisi wanadamu.
Mitaani tunapotembea, kuna viumbe vingi sana tunapishana navyo, vinatuona lakini sisi hatuvioni. Mbaya zaidi, viumbe hivi wakati mwingine vinaingia kulala kwenye majumba yetu baada ya kuchoka kwa shughuli zao za mchana kutwa.
Sema usiri wake ni kwamba, baadhi ya viumbe havina ubaya na binadamu, hata vikiingia ndani kwako vinataka hifadhi ya malazi tu asubuhi zinaondoka.
Umewahi kuwa peke yako usiku chumbani halafu ukajisikia hali ya kuogopa sana kiasi kwamba hutaki hata kulala na giza, unawasha taa mpaka kuna kucha? Basi tambua kwamba, kuna viumbe visivyoonekana vimeingia kulala chumbani kwako. Unaposhtuka na kuangalia dirishani vyenyewe vinakuona na kukucheka.
Kifupi kila unachofanya vinaona ila havina dhamira ya kukuzuru.
Sasa utajuaje kuwa ulilala na viumbe? Mara nyingi hivi viumbe humsababishia hali ya kwenda chooni mtu kila wakati. Unaweza kutoka chooni usiku mara nne, wakati si kawaida yako, jua ulilala na viumbe.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kikubwa, kama unahisi hatari hiyo, ukilala usifunge mlango, yaani ukae wazi. Viumbe hawa huwa hawana ubavu wa kuingia kwenye chumba au nyumba yenye mlango wazi.
Umewahi kutembea usiku peke yako ukafika mahali kwa mbele kama kuna watu au mtu lakini ukifika hakuna? Jua maeneo hayo kuna viumbe visivyoonekana. Na mara nyingi ukikutana na hali hii lazima itaambatana na hisia za nywele kusisimka kichwa kizima.
unaweza ukahisi nywele zinanyonyoka kwa jinsi zinavyosisimka, ujue ni maeneo yenye viumbe.
Tabia ya viumbe hivi ambavyo asili yake ni kutoka Nchi ya Wachawi, ni kupenda maeneo yenye watu wengi, mfano, sokoni, stendi ya mabasi na vituo vya daladala. Hakuna maeneo Dar es Salaam yana viumbe wa ajabu kwa wingi kama stendi ya mabasi, pale Ubungo na katikati ya mitaa ya Kariakoo.
Kwa Ubungo, unapoona watu wengi wakiingia na kutoka huku wamebeba mizigo, nyuma yao kuna viumbe hao, ndiyo maana huwa tunasema watu wengi, lakini ukweli ni kwamba tunawachanganya na viumbe.
Sasa ubaya wao hawa viumbe ni pale wanapoamua wakati mwingine kujitokeza na kuwa watu wanaoweza kuonekana kwa macho.
Hapo ndipo wanapoweza kuharibu eneo. Mfano, usidhani kilio cha mara kwa mara cha foleni jijini Dar es Salaam ni cha kweli, foleni nyingine tunaongezewa na hawa viumbe baada ya kujigeuza na kuwa binadamu.
Wana uwezo wa kufanya magari yao, wakatoka Kariakoo kwenda Kimara, kwenda Mwenge au Kibamba na wanapokuwa Magomeni na wao wanakuwa kwenye foleni wakati wana uwezo wa kufika wanakokwenda bila kuwepo kwenye foleni wala kuwa kwenye magari.
Tatizo ni kwamba, hata ukiliona gari la kiumbe kisichoonekana huwezi kulijua, lina namba za kawaida, kila kitu cha kawaida.
Ila, mara zote abiria wa magari haya hawazidi watatu ikiwa na pamoja na dereva. Na mara zote ndani ya gari kunakuwa na utulivu, hakuna anayeongea wala kucheka, mwanzo wa safari yao hadi mwisho.
Hatari iliyopo ni kwa wale wafanyabiashara wanaouza maji, juisi, sabuni au bidhaa nyingine kwa wenye magari.
Naamini hapa nimeeleweka, yaani ni kwamba, ukifika Magomeni Mapipa, si kuna foleni halafu kuna vijana wanauza vitu kwa watu waliomo ndani ya magari? Basi wale vijana wako hatarini zaidi.
Kwanini? Kwa sababu baadhi ya watu wanaowauzia ni wale viumbe wasioonekana ambao siku hiyo wanakuwa ndani ya gari.
Wana tabia ya kuchukua damu ya vijana kama hao na kwenda kuichafua, baada ya muda utakuta kijana anakuwa mdhaifu, hana maendeleo, mwili unakuwa umechoka, yaani anakuwa binadamu ilimradi anaishi lakini kwa upande mwingine si binadamu kamili.
Kifupi matukio yanayowakuta binadamu ni makubwa na mengi, yanatisha kama utasimuliwa kila siku.
Napenda kusema kuwa, mfano usiku. Hakuna siku iendayo kwa Mungu bila kuwepo kwa watu waliopata matatizo usiku, hasa ya kichawi ambayo kesho yake mtu anaweza kushindwa kusimulia hadi zipite siku nyingi.
Kinachowapata wanadamu wengi usiku, chanzo ni kutojua mwongozo wa kichawi, unaweza kugombana na mtu ukadhani ni wewe, kumbe wachawi wanasimamia kwa lengo la kuwapata mbele ya safari.
Nitoe mfano mmoja, mwaka jana kwenye Klabu ya usiku ya Swiss Pub, Tabata msichana mmoja, simtaji kwa jina, alitendewa uchawi bila mwenyewe kujijua.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Huyu msichana aliingia ukumbini akiwa na mpenzi wake kwa ajili ya kucheza disko. Walionekana wanapendana sana. Na ilionesha kazi ya wachawi usiku huo ilikuwa kuwagombanisha wanaopendana kwa kuwafanyia visa na vituko, hasa mambo ya ajabu-ajabu.
Ghafla ilitokea tafrani kati yao tena mbaya zaidi mbele za watu. Yule mwanaume alitoka nje kwa hasira akimwacha msichana wake ndani.
Alikwenda kuingia ndani ya gari na kuondoka, msichana akawa hana jinsi na alishindwa kumkimbilia kwa nyuma kwa sababu alivaa viatu virefu sana.
Lakini kwa vile mwanaume wake aliondoka, yule msichana naye aliondoka kumfuata kwake kwa kutembea kwa miguu usiku huo.
Akiwa peke yake njiani, aligeuka nyuma na kumwona mwanamke mmoja, mtu mzima akiwa amejitanda khanga juu na chini na kubakiza sehemu ya uso tu.
Yule msichana alishtuka kwa mambo mawili, kwanza ni muda wenyewe, haikuwa rahisi kwa mwanamke kama yule kuwa peke yake, lakini akajipa moyo kuwa, huenda kuna mahali anapeleka taarifa usiku huo na hakuwa na msindikizaji.
Lakini kilichomshangaza zaidi ni kitendo cha yule mwanamke kwenda sambamba na yeye, kwani alipotembea kwa kukazana, yule mama naye alifanya hivyo na alipotembea pole pole pia aliiga.
Lakini mwisho, yule mwanamke alimfikia akampisha. Wakiwa sanjari anapita, alimwangalia usoni na kubaini kuwa, alikuwa na macho meupe kupita kawaida kiasi kwamba, licha ya kwamba ilikuwa usiku lakini yalionekana yaking’aa.
Lakini ghafla yule mwanamke alipotea mbele ya msichana wakati hakukuwa na kona wala kichaka.
Msichana aliingiwa na woga wa ajabu, nywele kichwani zilimsisimka, aliamini ndiyo ilikuwa siku yake ya mwisho kuishi duniani.
Hata hivyo, kufumba na kufumbua mbele yake alimwona kijana akitembea mwendo wa kawaida kisha naye akapotea.
Msichana wa watu alitembea kwa mwendo wa haraka kuelekea nyumbani kwa yule mpenzi wake huku akitetemeka.
Alipofika, alichungulia kwenye upenyo na kulioga gari, lakini kikwazo kikawa jinsi ya kuingia kwani geti kubwa lilifungwa na hakuwa na simu ya kumpigia ili kumjulisha kwamba alikuwa nje.
Yeye lengo lake lilikuwa wakayaongee matatizo yaliyojitokeza na kuyamaliza waendelee kama mwanzo.
Akiwa anatafuta jinsi ya kuingia, ghafla alishikwa na hisia za kugeuka na kuangalia nyuma. Ndipo katika hali ya kushangaza akamwona yule kijana aliyemtokea muda mfupi nyuma, amesimama akiwa ameikunja mikono kwenye kifua.
Ilibidi ajipe ujasiri na kumwona yule kijana ni binadamu wa kawaida, akamuuliza kama ana simu amsaidie ili ampigie mpenzi wake amfungulie mlango.
Lakini yule kijana, badala ya kujibu kuhusu simu, alinyoosha mkono kuelekea kwenye geti la nyumba, kidole kimoja kikachomoza kwa kumaanisha anakoelekeza.
Mara, geti likafunguka lenyewe, akamwambia:
“Sikia we msichana, simu sina lakini siku nyingine usirudie tena. Alaa!”
Msichana aliingia ndani kwa kasi, akapitiliza hadi chumbani ambako alimkuta mpenzi wake amelala.
Kwa mwanaume sasa, lilikuwa tukio la ajabu kwani kuingia kwa mpenzi wake kulimtatiza, kama geti lilifungwa na uwezakano wa kuruka ni kwa mwanaume tena jasiri, sasa yule aliingiaje?
Alipomuuliza, msichana hakuweza kusema kwani alikasirika sana kwa kitendo alichomfanyia, kugombana na kumwacha ukumbini peke yake huku akijua ni usiku mwingi.
Lakini pia alikuwa haamini mambo aliyokutana nayo njiani. Alibaki kimya hadi asubuhi alipoamka na kuondoka zake bila kumwambia mpenzi wake nini kilimtokea usiku uliopita.
Sasa kilichopo kwenye tukio kama hili ni kwamba…
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment