Simulizi : Nchi Ya Wachawi
Sehemu Ya Tatu (3)
“Mpaka hapo sasa nikawa nimeshajua kwanini niliwashtua watu kwa kauli yangu ile. Kumbe jina la Mungu kwenye makao makuu ya viumbe wale ni sumu kwao inayoweza kuwaangamiza mara moja. Kama mimi nilipolitamka mara moja tu kiongozi wao akatembea kwa kuchechemea huku akishindwa kuendelea na hotuba je, ningelirudia?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikiwa ndani, nilisimama mbele, yule Mkuu wa Nchi akaja, alinishika na kuniangalia kwa muda, kisha akasema:
“Unajua kuna mwananchi wangu ameshakufa?”
Nikamjibu: “Mimi sijui, kafaje?”
Mkuu: “Si kitendo chake cha kutokukupeleka kwenye chumba kile ulichokwenda sasa hivi. Hivi hapa kuna Msaidizi wangu Mkuu ameugua ghafla. Lakini ni salama kwako, kwani kama ingethibitika alikupeleka ungekufa wewe kifo kilekile.”
Nilitamani pia kumuuliza lile jina linawaathiri vipi, lakini kabla sijafikia huko, yeye mwenyewe alisema:
“Sisi huku hatutumii baadhi ya majina, kwani yana madhara na ndiyo maana tuko mstari wa mbele kuhakikisha tunawaumiza watu ili kumtesa aliyeumba nchi.”
Mara, mtu mmoja ambaye naye alikuwa mjumbe kama mimi, alikurupuka na kusema:
“Jina la Yesu je?”
Ghafla, ukumbini kulisikika mlio kama wa bomu zito huku moshi mkubwa na mzito ukifunika na kusababisha giza nene.
Vilio kutoka kila kona vilisikika, baadhi ya watu walisikika wakisema kwa kuomboleza kwamba, wanakufa huku mimi nikiwa nimesimama palepale.
Niliangalia pale aliposimama Mkuu wa Nchi, hakuwepo! Ilinishtua sana, nilijua niliyebaki mzima ni mimi peke yangu.
Lakini hali ilianza kutulia, ule moshi ukapungua, giza likaondoka, nilipoangalia wenzangu, wengi walikuwa hoi kama wamelewa, lakini waliokuwa wazima sana ni wajumbe tuliokwenda pale tu. Ina maana kwamba, kutajwa kwa jina la Yesu kuliwaathiri zaidi wale viumbe wa kule.
Sasa sisi tuliokuwa na afya zetu, tuliangaliana na kuulizana kwa mikono nini kifuate pale?
“Tunaomba utulivu kwa wote, tafadhali sana wageni wetu, tutulie kila mmoja pale alipo akae kwa matumaini kwani hali ni salama,”
sauti nyembamba, sauti ya mwanamke ilisikika bila kujua ilikotokea.
Kweli, wote tulijikuta tukitulia huku kila mmoja akiangalia pande zote za dunia. Ilikuwa hali ya kutisha sana, wengine walionekana kutulia lakini wakitetemeka sana.
“Baada ya muda, Mkuu wa Nchi atafika, kwa hiyo kila mjumbe aliyoko mahali hapa atatakiwa kutega sikio kumsikiliza atakachokisema.”
Ile sauti ikaendelea:
“Wewe uliyesimama mbele, tafadhali sana, tena sana rudi kwenye makao yako ya awali, kwa sasa tunaongelea zaidi dharura.”
Nilirejea kwenye kiti changu, nikakaa. Muda wote huo yule mjumbe aliyelitaja jina la Yesu alikuwa akilia, kichwa amekiinamisha kwa unyonge mkubwa. Alionekana kama anajutia alilolisema.
Sauti hiyo ilipokuwa kimya, tukasikia mlio wa viatu kutoka kusikojulikana ukitembea kuelekea tulikokuwa, ilifika mahali tukahisi mtu huyo anayetembea yuko mbele yetu na alibakiza hatua kadhaa amfikie aliyekuwa akimtaka au alipokuwa akipataka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara yule mtu aliyetaja jina la Yesu akalia mama nakufa! Akaanguka chini, damu zikawa zinamtoka kwa wingi kinywani, puani, masikioni na kwenye macho.
Wajumbe wote tulimzunguka na kumshangaa, wengine wakamwekea mikono mwilini kumpima hali yake lakini kusema ule ukweli mpaka muda huo mwenzetu alishakuwa marehemu.
Tukiwa tunashangaa shangaa, tukasikia mlio tena wa vile viatu ukitembea kutoka pale tulipomzunguka mwenzetu kuelekea ulikotoka.
Huu mlio, kwa kweli ulisikika katika tafsiri kwamba, aliyekuwa akitembea alikuwa akivuta hatua ndefu kidogo mpaka ulipopotea masikioni mwetu.
Mara, Mkuu wa Nchi akatokea akitembea kwa mwendo wa kusuasua. Alipofika mbele alisimama na kuachia tabasamu la aina fulani, kisha akasema:
“Lakini Mkutano wa mwaka huu vifo si vingi, wale waliokuwepo kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka jana wanyooshe mikono yao juu.”
Kisha akawa anaangalia huku na kule kama vile alitaka kuhesabu, akawa anatingisha kichwa.
Ilionesha ni nusu kwa nusu, kati yetu sisi wapya na wale waliokuwepo mwaka jana. Yule Mkuu akaendelea:
“Je, mwaka jana mpaka sasa humu wangekuwa wamepoteza maisha wangapi?”
“Wengi tu,” watu wa mwaka jana walijibu.
“Wengi tu,” alirudia kauli yule Mkuu. Akaendelea:
“Kusema kweli hapa tunakutana kibinadamu sana, kwani tukisema sisi wenyeweji tuwe kama tunavyotakiwa kuwa mtatukimbia, ndiyo maana tunajitahidi kujibadilisha ili tuonekane nasi ni binadamu kama wengine.”
Akaendelea kwa kuuliza swali:
“Au mnataka tuwe kama tunavyokuwa kwa asili?”
Mimi binafsi niliingiwa na shauku ya kutaka kujua viumbe wale huwa wanakuwaje?
Tukajikuta wote tukijibu:
“Ndiyooo.”
Ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua, yule Mkuu alirefuka huku tunamwona, masikio yake yakawa marefu kama ya mnyama, sura yake ilibadilika pia, jicho lake moja lilikaa juu ya paji la uso, halafu akaota mapembe mawili kwa kila upande moja.
Meno yake yalichomoza kwa mbele urefu wa wembe na kidevu kilishuka kwa urefu wa chupa ndogo ya chai. Tukiwa tunafikicha macho kwa kutoamini tulichokuwa tukikiona, mara akatokea yule dada MC, yeye alikuwa kituko zaidi, alikuwa mwembamba mfano wa katuni mbaya, kiuno chembamba sana, miguu nilidhani ni vidole vilivyopata uwezo wa kusimama.
“Mnaona hamuoni?” Alituuliza akionekana kuringia umbile lile.
Tulipiga makofi, lakini kwa kujikaza, maana kusema ule ukweli alitisha sana. Mimi mwenyewe nilijiuliza itakuwa vipi kama siku moja nitakutana na kiumbe kile, niliamini nitapoteza fahamu.
Lakini akaendelea kusema:
“Utaratibu wetu umeharibiwa na mtu mwenye kukiuka maadili na adhabu kali imeshachukuliwa. Sasa sina sababu ya kumwita yule aliyekuwa akiongea kwani karibu mambo yote ya msingi tumeshakubaliana nayo kinachotakiwa sasa ni utekelezaji wake tu, sawa jamani?”
“Sawa,” tuliitikia wote kwa pamoja huku tukipiga makofi kwa nguvu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sasa tutakwenda kwenye meza ya chakula, baada ya mlo kila mmoja atarudi kwake duniani, halafu utekelezaje wa yale yote niliyoyasema uanze mara moja. Mtasaidiwa na roho kutoka huku.”
Aliposema maneno hayo alisita kidogo, kisha akaendelea:
“Mnaonekana wengi mmeshtuka niliposema mtasaidiwa na roho kutoka huku, kweli?”
“Kweliii,” tulimjibu.
“Kwa hiyo mnataka kuwaona hao roho wa huku?”
“Ndiyooo.”
Pale pale alipiga au tuseme alipuliza winja wengine wanaita mbinja, wengine wanaita mluzi, kufumba na kufumbua, viumbe wa ajabu walijaa mbele yetu. Walikuwa wengi sana, wafupi kama paka, lakini wanasimama mfano wa binadamu, wakawa wanatembea kwa kurukaruka hapa na pale.
Walionekana hawana habari na sisi. Pia walionekana hawaogopi kitu na zaidi sana walionekana wamezoea kazi wanayoifanya.
Mkuu wa Nchi akasema kuwa, roho wale ndiyo wenye uwezo wa kujibadili na kuingia kwenye mwili wa binadamu na kumsaidia kuwaza au kuamua mambo ya kufanya, hasa yale mabaya.
Akasema: “Kuna roho wa kila aina hapa. Kuna roho anayeshughulika na maamuzi mabaya, ngoja asimame mbele.”
Kiumbe kimoja kilipita mbele ya wenzake na kusimama kwa pozi. Mkuu akasema anataka kuonesha mfano wa roho huyo anavyofanya kazi, akamwamuru akaingie kwa mzee mmoja aliyekuwa amevaa majani ya njano peke yake kama nguo za kwenye mkutano ule.
Kwanza, yule kiumbe pale mbele alipotea ghafla, kisha sekunde tano tu mbele, yule mzee akatoka alipokuwa na kufuata watu kisha kuanza kuwapiga huku akijisifia kuwa, yeye ni bondia wa ukweli hakuna wa kumuweza.
“Hata wewe Mkuu huniwezi mimi, eeeh! Mimi ndiyo Tyson wenu.”
Nilishangaa sana tena sana, nikawaza mambo mengi, kwamba, kumbe wale watu ninaowaona duniani wakiwa wakorofi, si wao. Kuna roho wamewaingia na ndiyo wanawaelekeza kufanya vile.
Kilichotokea sasa, Mkuu akasema anatuma roho mwingine anayeshughulika na maamuzi mabaya akaingie kwa mtu mwingine ili tuone kitakachotokea.
“Lengo langu mkitoka hapa mkajue ni jinsi gani sisi tulivyo na uwezo mkubwa,” alisema Mkuu huku akiwaangalia wale roho.
Roho mmoja akasimama mbele, akamwamuru akamwingie mzee mwingine aliyekuwa amevaa kaniki kukatiza kiuno, kichwani ana mvi tu.
Kufumba na kufumbua, yule mzee akaanza kumjia juu yule wa kwanza akimwambia hana lolote mbele yake, na anaweza kumuua kama ataendelea kutamba kwamba, yeye ni Tyson.
Mzozo mkubwa ulitokea, yule anayejiita Tyson akiendelea kutamba na sasa akawa anamfuata yule mzee wa mara ya pili ambapo alimrushia ngumi, yule mwingine akakwepa.
“Basi basi basi jamani. Naamini mmekubaliana na mimi.”
Wale wazee wakawa katika hali zao za kawaida na kurudi kwenye viti huku wakionekana kujishangaa wenyewe.
Mkuu: Basi sasa nendeni mkale chakula, kisha baada ya hapo mtawanyike, kila mmoja arudi kwenye nchi yake na kusubiri utekelezaji wa maagizo ya huku.
Mkuu alipotea pale pale akawa haijulikani alikoingilia wala kutokea. Viumbe wengine wale walitangulia kutokomea kabla ya Mkuu.
Kwenye foleni ya chakula sasa, meza ilikuwa kubwa, lakini si ya mbao, ilipambwa kwa ngozi ya mnyama mwenye manyoya mengi kama mbwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Chakula chenyewe kilikuwa ni mapande ya nyama ya kuchoma huku kwenye chupa ndogo za plastiki kukiwa na kinywaji chekundu. Harufu kali ilitawala mahali hapo kiasi kwamba nilitaka kuziba pua.
“Kwa kujikaza, niliendelea kuwa pamoja na wenzangu ambao wengine walikuwa kama mimi, lakini wengine walionekana kuwa wazoefu wa chakula kile.
Baada ya muda kidogo, Mkuu wa Nchi naye alitokea akaunga foleni na sisi huku akiwa na walinzi wake. Yupo mlinzi wake mmoja alikuwa nyuma yake kila mahali, akiwa amevaa mavazi kama ya kijeshi.
Kila aliyekuwa akikamilisha mlo wake, alitoka na kwenda kukaa sehemu flani ambayo kulikuwa na meza na viti vya dhahabu, tena za thamani kiasi kwamba, meza moja kama ingepata mtu wa duniani angekuwa bilionea kuliko mwingine yeyote yule.
Nilishangaa wakati fulani watu kuwa wachache na viti kuwa vyeupe tofauti na ilivyokuwa. Mimi nilikuwa nakula kile chakula huku naziba pua kwa siri ili nisijulikane.
Wakati wa mlo huo, akili nyingine ilikuwa ikiniambia ‘unajua kama unakula nyama za watu?’.
Hiyo iliniumiza na kunikera sana saikolojia yangu kwani nilihisi kutapika kile nilichokula.
Lakini moyoni nilijiuliza ni kwanini nilikubali kuishi maisha yale? Ni kwanini nimejikuta nakula chakula kama kile, maana hata kwa duniani, mtu anayeweza kula vile hayupo, hata kichaa hawezi, anajua kizuri na kibaya sasa kwanini mimi?
Alipita mtu mmoja ambaye ndani nilikaa naye jirani, nikamwita. Alipofika nikamuuliza:
“Mbona watu wanapungua kwa kasi, viti vimebaki vyeupe kama hivi?”
“Si tulishaambiwa baada ya kumaliza chakula unaondoka, kwa hiyo watu wengi wa duniani wameshaondoka zao, wewe bado?”
“Ndiyo namalizia,” nilisema huku nikimwangalia Mkuu wa Nchi.
“Mimi mwenzio nakwenda kunawa,” alisema yule mtu.
“Hicho chakula lazima kiishe,” kiumbe kimoja kilisema kikiwa kimekaa mbele yangu. Kilionekana kilikuwa kinachunguza ustaarabu wa pale.
Nilipomaliza kula nilisimama, nikashikwa mkono na kiumbe kimoja.
“Sasa unaweza kuondoka,” kilisema kikiniachia mkono.
Sikujua nielekee wapi, lakini nikiwa nawaza jinsi ya kuondoka, pale pale nilijikuta nimetua mahali pale pale nilipoondokea. Niliangalia huku na kule ili kuona kama ni kweli siko kule, ilikuwa kweli. Sikuwa kule kwenye Nchi ya Wachawi. Lakini nilijifunza kitu kikubwa sana, kwamba ile nchi ni kweli ya wachawi kwani tabia ya mazingira haikuwa ya kawaida.
Pia niligundua kuwa, wachawi wengi wa dunia hii huchukua mikoba na nguvu zao kule na ndiyo maana wanaisumbua sana dunia. Ni mahali ambapo hapahitaji nguvu za nishati kuendesha shughuli zake, mwanga upo, hali ya hewa inayokuwepo ni ile inayohitaji na wakazi wake kwa wakati ule.
Wakati tukiwa kwenye kikao kuna mtu aliniambia kuwa, ile ni nchi kubwa sana lakini kwa sababu sisi tulikwenda kwenye mkutano ndiyo maana hatukupewa nafasi ya kutembea mitaani kuona mazingira na tabia nchi.
***
Ilikuwa asubuhi ya siku iliyofuata, nilikuwa nyumbani kwangu, mlango uligongwa lakini nje nilisikia sauti za watu wengi wakiongea kama wanabishana vile.
“Inawezekana.”
“Hamna bwana, nyinyi mbona mnakuwa wabishi kiasi hiki?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndivyo wale watu nje walivyokuwa wakiongea, lakini huku mlango ukiendelea kugongwa.
“Nani?” Niliuliza kwa sauti nzito na ya juu.
Niliwasikia wale watu wakibishana kwamba, aliyehoji sikuwa mimi.
Nilitoka chumbani, nikavaa kitenge tu na kwenda kufungua mlango.
Nje nilikuta watu kama watano hivi, wote walionesha mshangao macho yetu yalipogongana.
“Upo?” Wawili kati yao walihoji.
“Nipo, kwani vipi?”
“Toka juzi hatujakuona, tukishika mlango unaonekana umefungwa kwa ndani, tukawa tunashangaa, hivi hapa leo tulitaka kuvunja mlango,” mmoja wao alisema huku wengine wakitingisha kichwa kwa ishara ya kukubaliana na mwenzao.
“Mimi nipo, nilikuwa nimelala tu,” nilisema kwa ukali kisha nikafunga mlango kwa nguvu mpaka ukalia puu!
Sikusikia tena kama wanasema nje, naamini waliondoka kimyakimya na kurudi makwao maana katika wale watu, kuna wazee wawili tulikuwa hatuna mawasiliano mazuri hata kidogo.
Nikiwa chumbani, nikasikia sauti kwa njia ya mwangwi ikisema:
“Ni wakati mzuri wa kuanza utekelezaji bila kuchelewa.”
Sauti hii ilikuwa ikijirudia kila baada ya dakika moja na mimi nilikuwa nikijibu sawa.
Basi, niliamua kutoka na kwenda kuzungukazunguka mtaani ili kuangalia mazingira na jinsi kazi nitakavyoifanya.
Nilitokea kwenye uchochoro mmoja, kisha nikaingia mwingine na kutokea kwenye nyumba ya mfanyabiashara mmoja maarufu, yeye mwenyewe alikuwa amekaa nje na wakeze wawili na binti zake watatu, lakini yeye alikuwa uchi wa mnyama.
“Nilichofanya, nilisimama mbele yao na kuwatumbulia macho huku nikiwa nimewanyooshea kidole.
Naweza sema kwamba, ilikuwa mara yangu ya kwanza kufanya vitendo vya kichawi tangu nitoke kwenye Nchi ya Wachawi.
Yule mwanaume alianza kujikuna huku akilalamika kwamba kuna joto sana siku hizi, lakini muda ulivyozidi kwenda na kujikuna kwake kuliongezeka kiasi cha kuwafanya wakeze kushikwa na wasiwasi.
“Mwenzetu mbona unatutisha sasa, hilo joto gani ambalo wewe linakusumbua kiasi hicho lakini sisi tuko imara?” Mkewe mmoja alimuuliza kwa sauti ya kumsuta.
Lakini yule mzee hakujibu, kujikuna kuliendelea mpaka ikafika mahali akasimama, akiendelea kujikuna mgongoni sasa.
Nilipenda sana kumwadhiri yule mzee kwa kuwafanya wake zake na mabinti zake wamwone yu uchi wa mnyama, lakini nikahisi naweza kufanya familia isiwe na amani tena, lakini moyoni nilisema kinachotakiwa ni kumfanya ajue kuwa mimi niko mbele yake nimesimama na ninamwona katika kila hatua.
Hivyo, nilimsogelea mpaka jirani kiasi cha kama hatua tatu tu, nikajijaza upepo na kuingia mwilini mwake kisha nikawa namwendesha mawazo, niliyaamuru mawazo yake yawe yanawaza ngono kwa mabinti zake, hasa mmoja ambaye ndiye mkubwa kuliko wote.
“Mwite,” nilisema, na yeye akamwita kweli huku akimtaka waingie ndani kuna kitu anataka kumwambia.
Waliingia ndani wote, na wale waliobaki nje walikuwa wakiongea mambo yao mengine.
Yule mzee aliingia mpaka chumbani kwake, binti yake alipofika mlangoni akasita, akasimama.
Mimi nikiwa bado upepo niliingia kwenye akili ya yule binti na kumwamuru aingine chumbani kwa baba yake licha ya mama zake kuwepo nje tu ya nyumba ile.
Binti aliingia chumbani kwa baba yake akiwa na ujasiri tofauti na alivyokuwa amesimama mlangoni.
Baba yake alimshika mabega akamvutia kitandani, kisha wakakaa wote.
“Lala na mimi,” alisema yule mzee.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Binti hakuonesha ubishi, alichofanya aliweka kiganja cha mkono kwenye uso, akawa amejiziba macho. Hii iliashiria aibu ya kibinadamu lakini si kukataa alichoambiwa na baba yake mzazi.
Baba alivua nguo kisha akamvua nguo binti yake na wakapanda kitandani wote na kuanza kufanya mapenzi haramu.
Wakiwa wanaendelea, mimi nilitoka nje na kuingia kwenye akili ya mke mkubwa wa mzee yule ambaye ndiye mwenye mtoto yule.
Nikamwamuru awaulize wenzake kuhusu wale waliongia ndani, yaani mumewe na binti yake mkubwa.
“Hivi hawa wameingia ndani kuongea nini cha siri mno?” Alihoji, kisha mimi nikaingia kwa mke wa pili ambaye anaitwa mama mdogo na yule binti aliyeingia ndani na baba ‘ake.
“Hivi kweli, kuna kitu gani cha siri kwa wao wawili, kama si unafiki na uongo ni nini? Ngoja mimi nikawasute,” alisema yule mke wa pili na kwenda ndani.
Nikiwa wote nimewaachia roho ya kuwaza na kuamua kwa jinsi nilivyotaka, yule mke wa pili au mke mdogo alisukuma mlango wa chumbani na kuwakuta wale wakiendelea na kuzini.
“Ha! Macho yangu au naota. Mama Hawa, we mama Hawa,” alihamaki kisha akaanza kuita yule mke mdogo huku amesimama katikati ya mlango.
Nilichofanya mimi, kwanza niliondoa ile roho kwa wote, kwa hiyo wakabaki na akili zao sasa, mume akataka kutoka mbio, lakini mkewe mkubwa, mama Hawa akawa amefika.
“Nini?” Aliuliza.
“Mwanao Hawa amelala na baba yake.”
Yule mke mkubwa, mama Hawa alipomkuta mumewe anang’ang’ania kutoka alimshika kumzuia kisha wakaingia wote chumbani na kumkuta Hawa bado hajavaa nguo, na mbaya zaidi nguo zake zilikuwa chini tu zinaonekana, kuanzia gauni, khanga, gagulo na nguo ya ndani.
“Hawa mwanangu, kweli unaweza kulala na baba yako mzazi?” Mama Hawa alianza kulia huku akianguka sakafuni.
Wale mabinti wengine nao walifika, nao wakaanza kulia baada ya kubaini nini kilichokuwa kikitendeka mle chumbani kati ya dada yao na baba mzazi.
“Kweli dada Hawa unaweza kufanya uchafu kama huu, na baba, tena baba mzazi,” mmoja wao alisema wakilia kwa sauti.
“Jamani ni shetani alinipitia, nisameheni sana,” yule mzee alisema huku na yeye akianza kulia na kujutia kile kitendo cha kulala na mwanae wa kumzaa.
Hapa nataka kuwafafanulia jambo kuhusu hali iliyotokea kwenye nyumba ile na jinsi mzee yule alivyoamua kujitetea kwa kusema ni shetani tu.
Karibu mara zote, binadamu anayejikuta akijutia sana kosa alilolitenda muda huo huo ni yule ambaye aliongozwa au alizidiwa nguvu za kishetani. Nguvu hizi humwingia mtu bila yeye kujua na kujikuta akifanya tendo ambalo kila anayelisikia au kuliona anakataa akili yake.
Ni nguvu tu ambayo imekuwa ikiwasumbua watu siku zote katika maisha, lakini kwa binadamu ambaye atapata bahati ya kubaini kuwa, analotaka kulitenda linatokana na nguvu au msukumo wa roho chafu ndiyo kinga au dawa yake na kulishinda tukio lenyewe.
Hata yule mzee, endapo angelibaini hilo asingelitenda, lakini kwa kuwa akili zake si za utafiti ndiyo maana alishindwa kujinusuru na kitendo kile cha kashfa.
Basi mgogoro mkubwa ulizuka kwenye ile nyumba, mama mzazi wa yule binti alisema anaondoka na ili kuonesha msisitizo wake, alianza kukusanya nguo zake kwenye begi kubwa huku akisema maneno yenye kiashirio cha laana kubwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Yule binti yake naye alikuwa akilia, wadogo zake pia walikuwa wakilia na kusema maneno mengi, baadhi ya watu majirani walianza kufika wakitaka kujua nini kilikuwa kikiendelea kwenye nyumba ile, lakini hawakupata ushirikiano wowote zaidi ya wao wenyewe kusikia kulichokuwa kikiongelewa:
“Hii ni laana kubwa sana, mwanao wa kumzaa kweli unalala naye, tena sisi tupo hapo hapo?” Alisema yule mke wa mzee.
“Tena hawa hawajaanza leo, ni mchezo wao wa kila siku,” yule mke mdogo alidakia.
Maneno yao hayo ndiyo yalifanya wale majirani wajue nini kilitokea. Wengi wa majirani hao walionekana kushika vinywa kwa mshangao wa habari waliyokuwa wakiisikia.
Kwa pale, mimi ndiyo nilikuwa kiboko, hata kama pangekuwa na mchawi wa vipi asingeniona na hata kama angeniona asingeweza kunifanya lolote maana uwezo wangu mpaka wakati huo ulikuwa wa juu kiasi cha kumudu kukaa au kuongea na viumbe wenyewe wale wa kuzimu na si wachawi wa hapa duniani.
Niliacha wale watu pale na kuendelea na safari yangu mpaka mtaa wa pili. Nilikuta akina mama wakiuza Mama Lishe. Lakini mmoja wao alikuwa akitumia vitu vya kichawi katika biashara yake.
Walikuwa wamekaa kwa mstari akina mama wanne, yule aliyekuwa akitumia mambo ya kichawi alikaa mwisho kabisa huku akitema mate kila sekunde.
Lakini wale waliokuwa naye sambamba au wateja walimwona akiimba na si kutema mate. Na wenzake walipenda sana kumtania kwa kumwambia alitakiwa kuwa mwanamuziki kwa sababu muda wote yeye anaimba, kumbe mwenzao alikuwa akitema mate ovyo kila wakati kulingana na masharti ya biashara yake.
Mbaya zaidi, kiti alichokaa kilikuwa ni sehemu ya makalio ya binadamu mweusi, tena mtu mzima, halafu alishika mwiko wa mkono wa mtoto ambapo kwa macho ya kawaida alionekana ameshika mwiko wa kupakulia chakula.
Sasa kutokana na hali hiyo ya kufanya biashara ya kichawi, wateja wake wengi walikuwa wakitokea upande wake wa kulia. Hata wale waliokuwa wakitokea kushoto, walijikuta wakikatiza upande wa pili na kwenda kutokea kulia kwa yule mwanamke.
Mimi nilifika hadi pale na kumsalimia, alipoinua uso tu alishtuka.
“Shikamoo Mkuu.”
“Marhaba. Kazi iko sawa?”
“Iko sawa Mkuu, lakini ushindani ni mkubwa sana maana kila mtaa siku hizi kuna watu kama mimi.”
Hapa nataka kufafanua kidogo, ni kwamba maneno yake yalikuwa yakisikiwa na wale wenzake, hapana! Ilikuwa yeye na mimi tu, na wale wengine walimwona akiwauliza maswali na walipojibu, yeye alionekana kama hajali kiasi cha wao kusema:
“Unatuulizia nini sasa kama hutusikilizi tunapokujibu, wewe vipi bwana!”
Mimi nilinyoosha mkono kumpa yule mwanamke, yeye naye akanyoosha kunipa. Hapo niligeuka ghafla na kuwa mteja. Alionekana akinipa moja ya biashara zake, nikaondoka.
Ule mkono wangu ulikuwa na ishara ya kumpatia kitu kikubwa sana katika biashara zake na hata yeye alijua hilo ndiyo maana alinipa mkono wake.
Nilipokuwa njiani naelekea mahali fulani, mbele yangu nilikutana na watu watatu wakiwa uchi wote na wamesimama pembeni ya daraja.
Mimi nilirudi nyumbani huku moyoni nikijisifia kwa jinsi nilivyomudu kumshikisha adabu yule mzee ambaye niliamini mpaka pale alikuwa amejua mimi ni nani kati ya watu anaowajua yeye.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikiwa ndani, nilisikia upepo ukivuma na kutikisa paa la nyumba yangu, nikaangalia juu, kisha nikasonya kwa hasira, mara upepo ukapoa kabisa.
Ghafla mlango ukagongwa.
“Nani?” Niliuliza kwa ukali.
“Mimi.”
“Wewe nani?”
“Si ufungue mlango utanijua tu.”
“Sifungui bila kujitambulisha, sawa?”
“Mimi naomba ufungue nina shida sana na nyumba hii.”
“Una shida na nyumba na mimi?”
“Na wewe na nyumba hii.”
Lengo la kuuliza maswali mengi vile ni kutaka kuisoma ile sauti, ilifanana kwa mbali na ya yule mzee, lakini yenyewe ilizidi unene kidogo.
Nikaenda mlangoni kufuangua, lakini ajabu sikuona mtu nje.
“Mshenzi sana,” nilitukana.
Mara nikasikia nyuma yangu kwa ndani sauti ikisema:
“Aa, mbona unatukana bwana, si umechelewa kufungua mlango ndiyo maana nikaamua kuingia mwenyewe.”
“Una uhakika upo salama kuingia ndani kwangu bila kibali changu?” Niliuliza uso wangu ukiwa bado nje bila kugeuka.
“Nina uhakika nipo salama.”
Jibu hilo lilinifanya nigeuke polepole na kumwangalia ni nani mchawi mwenye ubavu wa kupambana na mimi, tena mbaya zaidi nilishangaa kuona mapambano yangu baada ya kutoka kwenye nchi ya wachawi yamekuwa dhidi yangu, nikiwa na maana wachawi kwa wachawi badala ya sisi sote kuwashambulia watu wasiokuwa wachawi.
Nilikutana na sura ya binadamu ambaye simfahamu, alikuwa mzee kupita mimi, usoni alijipaka vitu kama chokaa, huku meno yake yakiwa ya kijani, sijui alipaka nini.
“Uko salama?” Nilimuuliza tena tukitazamana.
“Niko salama zaidi kuliko unavyofikiria.”
“Hata kwa mpambano?”
“Kati ya nani na nani?”
“Mimi na wewe?” Nilimjibu nikiwa na suo wa kujiamini.
“Nimekuja kwa ajili hiyo,” alisema.
Sijui hasira zangu zilitokea wapi, lakini nilijikuta nikimvamia ghafla na kumshika mkono wake wa kuume nikauminya huku nikimuuliza:
“Ni kweli umekuja kupambana na mimi?”
“Ndiyo, nimekuja kwa mpambano.”
“Kabisa kabisa?”
“Ndiyo. Na niko tayari hata kufa.”
Nilibadili aina ya adhabu, nikajibadili mbele yake na kuwa roho, nikaingia kwake na kumwamuru kwenda kujipiga ukutani mara kadhaa huku akipiga kelele.
Aliumia sana na alianza kupiga kelele, nikaamuru kelele zile zisimfikie jirani kama kelele, ikawa hivyo. Kelele zilipofika kwa jirani wakasikia muziki, kwamba nimefungulia redio kwa sauti ya juu zaidi, wakaja kwa nje na kuniomba nipunguze sauti ili na wao wapate fursa ya kupumzika baada ya majukumu ya mchana kutwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilimtoka yule mtu, nikawa kama nilivyokuwa wakati anakuja. Alikuwa hoi chini akigalagala huku akisemasema maneno kama vile alitaka kuwasiliana na mizimu yake au wakuu wake wa wachawi, lakini akashindwa maana mimi nilikuwa mkuu katika kanda yote ya nchi.
“Bado uko tayari kuendelea na mpambano?” Nilimuuliza, lakini wakati huo alikuwa akishindwa hata kufumbua macho, tena jicho moja lilikuwa likivuja damu.
Alikataa kwa kutingisha kichwa lakini akasema kwa tabu:
“Nilitumwa mimi, sijaja mwenyewe.”
“Na nani?” Nilimuuliza kwa hasira nikijua ni yule yule mzee.
Alilitaja jina la yule mzee niliyemfanyizia na binti yake mkubwa, akasema kuwa, hata alipokuwa anakubaliana aje kwangu alimuuliza uwezo wangu wa nguvu ya kichawi:
“Akasema nisikuogope, kwani huna lolote, na ni mgeni sana katika masuala ya kichawi. Lakini nilipokuona mambo yako nimekubali wewe ni mkongwe na tena uwezo wako ni mkubwa sana, nisamehe sana ndugu yangu.”
Huruma iliniingia kwani kama kweli alidanganywa ina maana yule alitaka kumuua mwenzake, kwani ni kweli ni mtu nisiyewahi kumwona katika maisha yangu.
Nilimpa pole sana na kumwomba siku nyingine asikubali kuingia kwenye mambo ambayo hana uhakika nayo, yanaweza kumtokea mambo kama yale.
“Mimi nilishaamua kukuua moja kwa moja, kwani sikuwa na sababu ya kukushindwa, una nini wewe mpaka ushindane na mimi. Kwanini huyo mtu asikwambie sababu ya kukutuma wewe? Kwanini asije mwenyewe?” Nilimuuliza.
“Alisema mnafahamiana.”
“Hata kama tunafahamiana, lakini si angekuja kwa sura nyingine, si inawezekana?”
“Ndiyo.”
“Sasa? Alikwambia kama alishakuja nikamfanyia mambo makubwa?”
“Hapana, ila alisema aliwahi kuja usiku akakuchezea kama mpira.”
“We uliamini?”
“Wakati anasema niliamini, lakini hali niliyoikuta hapa siamini hata kidogo.”
Nilimshika kichwani, nikasema maneno fulani ya kichawi, mwanga mkubwa ukammulika pale alipo, hali ikawa shwari, akasimama huku akijipukuta vumbi ingawa hakukuwa na vumbi.
“Naweza kwenda?”
“Unaweza, ila kuwa makini na maisha yako, hayana kitu cha kubadilishana nayo,” nilimwambia huku akifungua mlango na kutoka zake.
Huku nyuma nilibaki nimeduwaa, nilijiuliza maswali mengi, ni kwanini yule mzee aliamua kumtuma mtu dhaifu kuliko yeye ambaye kidogo ni mkongwe na anajua kupambana lakini bado nilimshinda.
Ile anaondoka tu na mimi nikiendelea kufikiria, mara upepo mkali ukavuma.
Niliinua uso wangu kuangalia juu ulikotokea upepo, nikahisi ni jaribio tena, lakini nililipuuza kwa kusimama, nikaingia chumbani na kubadili nguo. Nilivaa shuka ya kaniki nikasimama katikati ya chumba, nikanyoosha mikono nikapotea.
Nilikwenda kutua kwenye genge la kukutania ambapo kwa mara ya kwanza toka niende na kurudi kwenye Nchi ya Wachawi.
Ngoma za kichawi zilikuwa zikiendelea, kutua kwangu kukazisitisha na kuibua kelele za kunilaki.
Mpaka hapo nataka kusema, nilikuwa mkubwa katika ngazi ya wachawi kuliko mwingine yeyote katika ukanda wa nchi. Na si kwamba nilitakiwa kudumu kwenye kundi langu, la hasha!
Moja ya majukumu yangu ilikuwa ni kuendelea kutembelea makundi yote ya kichawi na kuyapa nguvu na njia ya kuzidisha mapambano dhidi ya utaratibu sahihi wa Mungu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walipotulia, nilisimama katikati ya kundi kusalimia na kuwaambia mawili matatu:
“Hii ni nchi ya Tanzania, lakini kumbe kuna nchi mbalimbali duniani. Mungu aliposema ameumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana ni kweli.
“Pia, kumbe utaratibu unaotumiwa na shughuli za duniani na huko kwa wenzetu pia upo. Kila kitu kinakwenda sawasawa na huko. Kuna masekretari, kuna makarani, walinzi na mambo mbalaimbali.”
Nikawaambia kuwa, mpambano uliopo sasa katika ya utawala bora wa Mungu duniani na ule wa chini ni kuhakikisha upotofu wa hali ya juu unafanyika katika maeneo mbalimbali ya haki.
Mfano, kuhamasisha viongozi wa dini kukubali matumizi ya kondom, kwa Mungu hata kama binadamu wote watakufa kwa Ukimwi kwa sababu hawakutumia kondom, ni sawa tu, yeye hana hasara.
Lakini pia uzazi, hakuna kitu kinachoshikiwa bango kwa Kiongozi Mkuu wa Nchi ya Wachawi kama kuvuruga uzazi, yaani wanawake wajawazito wasiwe wanazaa kwa usalama.
Haya niliyoyasema ukiyafuatilia kwa umakini utagundua ni kweli, kwani jamii sasa imekuwa ikikumbana na kauli ya baadhi ya viongozi wa dini au wanaharakati wanaotaka matumizi ya kondom ili kunusuru janga la Ukimwi au wengine wakisema mtu awe na mpenzi mmoja mwaminifu, hata kama hawako katika ndoa.
Lakini huko kwenye Nchi ya Wachawi wanajua na kuamini kuwa, uaminifu unaanzia kwenye ndoa tu na si nyuma ya hapo, yaani watu kama hawajaoana kwa ndoa uaminifu kwao wa nini, maana wanazini.
Hata wale wapenzi, anapotokea mmoja anamwomba mwenzake asimsaliti maana yake ni nini? Ni kwamba anaomba azini na yeye tu, asizini na mtu mwingine.
Wakati nawapa kwa ufupi kuhusu mambo ya duniani yanayojulikana kwenye nchi ile, walikuwa wametulia wakinisikiliza kwa umakini wa hali ya juu na mwisho wa yote, wachawi watatu walinyoosha vidole.
Nilimsimamisha mmoja ambaye aliuliza:
“Kwa maelezo yako, huko Nchi ya Wachawi wanajua usahihi wa jambo unaotakiwa kuwepo ni upi ila wao kazi yao kubwa ni kupotosha, si ndiyo?”
“Hawapotoshi, bali wanapambana na utaratibu sahihi wa Mungu.”
Nikamsimamisha mwingine ambaye aliuliza:
“Kumbe kama ni hivyo hakuna haja ya kuwa wachawi maana tunakubaliana kuwa, tunaunga mkono wale wanaompiga Mungu ambapo siku ya mwisho, tutakwenda motoni.”
Wakati huyu mchawi akiongea hivyo, upepo mkali ulitokea ukampaisha angani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment